Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Godbless Lema: Wananchi Wamejaa Hofu, Mawaziri Nao Wanahofu na Wamekosa Ubunifu

$
0
0
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), amesema kwa sasa viongozi wa umma wakiwamo mawaziri, hawana ubunifu kwa sababu ya hofu waliyo nayo.

Lema aliyasema hayo bungeni jana wakati akichangia Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo ya Taifa wa mwaka 2019/20.

“Sasa taifa lina hofu kubwa, wafanyabiashara wana hofu, Takukuru (Taasisi ya kuzui na Kupambana na Rushwa), TRA (Mamlaka ya Mapato Tanzania) si rafiki, kwa sasa mtaji mkubwa sana unahamishwa nchini.

“Dk. Mpango (Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango), Serikali haiwezi kuendelea bila wafanyabiashara kuwa na amani, mbia namba moja wa kodi ni mfanyabiashara.

“Leo hii ukienda kila mahali wafanyabiashara wana hofu. Ukienda kwenye taasisi kuna hofu, mawaziri wana hofu, makatibu wakuu wana hofu, maendeleo yanaletwa na vitu vingi bila viongozi kujiamini hawawezi kuwa waaminifu,” alisema Lema.

Alisema katika maeneo mengine wakuu wa mikoa wanaonekana kuwa na nguvu kuliko hata mawaziri.

Lema pia alizungumzia suala  la kutekwa kwa mfanyabiashara Mohamed Dewji na kusema polisi wamekuwa wakilifanya jambo hilo kama sinema.

Mizizi 29 Power Ni Dawa Ya Nguvu Za Kiume Ambayo Imechanganywa Na Mizizi 29

$
0
0
Kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa wanaume wazee hata na vijana kupungukiwa au kutokuwa kabisa na nguvu za kiume nanimekuwa nikipigiwa simu na wanawake wakilalamika ndoa zao zipo mashakani maana hawaridhishwi na Waume au wapenzi wao pale wanapoaza kushiriki tendo la ndoa 

Kwa Nini Ujione Mpweke Pale Ukutanapo Na Mpenzi Au Mke Wako Kisa Eti Hauna Nguvu Za Kiume? ;Tumia MIZIZI 29 POWER, hii ndio tiba itakayorudisha heshima ya ndoa yako . 

Dawa hii itakufanya;
 1 Uchelewe kufika kileleni mda wa dakika 15-25 kwa tendo la kwanza 
2 Dawa hii itakupa uwezo wa kurudia tendo zaidi ya Mara tatu 
3  Dawa hii uhimalisha misuri iliyolegea na kusinyaa?dawa hizi hazina madhara kwa mtumiaji nani tofauti na ulizowai kutumia ata wazee wenye umri mkubwa wanapona 

NSONSOMA; Dawa hii itakufanya umridhishe  mke au mpenzi wako kwani uboresha uume saizi upendayo urfu wa nchi 5,6,7 na 8 na unene wa sentimita 2,3,4 na 5 dawa  hii ipo ya kupaka na kunywa 

NSHOLA; NI dawa ya uzazi kwa waliongaika mda mrefu bila kupata mtoto 

MWITA; Dawa hii humvuta meme, mke,au mpenzi mliyetengana pia umrudisha mtu kazini haliyefukuzwa, kumpatanisha mwajiliwa na bosi wake 

Tunatibu presha kisukari, busha ,vidonda vya tumbo tumbo kuunguruma kujaa gesi na kukosa choo 

MAHALI ILIPO OFISI; PANDA DALADALA SHUKA BUGURUNI MALAPA AU ROZANA NA MWANZA YUPO WAKALA PIGA SIMU 0752348593 DR NYAROBI .Kama hauna nafasi ya kuja ofisini utaletewa popote ulipo huduma hizi

Serikali yapiga marufuku Walimu kutoa adhabu ya viboko kwa wanafunzi

$
0
0
Serikali kupitia kwa Naibu Waziri wa Elimu William Ole Nasha imepiga marufuku Walimu kutoa adhabu ya viboko kwa mwanafunzi bila kibali maalum na pia amepiga marufuku Walimu kutembea na viboko.

Ole Nasha ametoa agizo hilo wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalum CCM Rose Tweve aliyetaka kujua kauli ya Serikali kwa Walimu wanaokiuka sheria za adhabu kwa Wanafunzi

“Haitakiwi vizidi viboko vinne, hairuhusiwi kwa mwalimu yeyote yule kuchapa viboko, bali ni mwalimu mkuu tu, na lazima kiombwe kibali cha kufanya hivyo, ni marufuku mwalimu yeyote kumchapa mwanafunzi kinyume na taratibu na sheria, lakini vile vile na marufuku mwalimu yoyote kutembea na viboko kwa lengo la kumchapa mwanafunzi, kwa kufanya hivyo ni kuvunja sheria na hatua zitachukuliwa”, alisikika Naibu Waziri wa Elimu William Tate Ole Nasha.

Hivi karibuni kulikuwa na mjadala wa kuchapwa viboko wanafunzi baada ya mwanafunzi mmoja kufariki dunia baada ya kuchapwa viboko na mwalimu wake, akimtuhumu kuiba pochi yake ambayo baadaye aliletewa na dereva boda boda baada ya kuisahau.

Marekani Yatoa Onyo Kuhusu Kuzorotoa Kwa Haki Za Kiraia Na Haki Za Binadamu Tanzania

$
0
0
Serikali ya Marekani imetoa tamko la kusikitishwa kwa kile ilichoeleza kuwa ni kushamili  kwa matukio ya mashambulizi. 

==>>Soma taarifa hiyo zaidi iliyotolewa na Ubalozi wa Marekani Tanzania

Serikali ya Marekani imesikitishwa sana na matukio ya mashambulizi yanayoshamiri na hatua za kisheria zinazochukuliwa na serikali ya Tanzania, ambazo zinakiuka uhuru wa raia na haki za binadamu, na zinazojenga mazingira ya vurugu, vitisho na ubaguzi. 

Tunahuzunishwa na hatua za ukamataji watu unaoendelea na unyanyasaji wa makundi maalum, wakiwemo mashoga, na wengine wanaotaka kutumia haki zao za uhuru wa kujieleza, kushiriki na kukusanyika. Vyombo vya kisheria vinatumika kudhibiti uhuru wa raia kwa wote.

Kuzorota kwa hali ya haki za binadamu na utawala wa sheria nchini Tanzania kunakwamisha maendeleo, ustawi wa uchumi,  amani na usalama. 

Tunatoa wito kwa mamlaka nchini Tanzania kuchukua hatua za makusudi kulinda haki za asasi za kiraia, watetezi wa haki za binadamu, waandishi wa habari, wafanyakazi wa afya, wanaharakati wa kisiasa na watu wote kwa mujibu wa katiba ya Tanzania, mkataba wa Afrika wa haki za binadamu na watu, na makubaliano ambayo  nchi imeridhia kikanda na kimataifa.

Haji Manara Amkingia Kifua Diamond Sakata la Wimbo Wao Kufungiwa na BASATA

$
0
0
Msemaji wa Simba SC, Haji Manara amefunguka mwanzo mwisho kuhusiana na kufungiwa kwa nyimbo ya Rayvanny aliyomshirikisha Diamond ya Mwanza.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Manara amesema; ”Sanaa kwa maana ya Art na hasa ya Mziki ni fumbo ni kitu kinachorandama na kuimba kwa njia za mafumbo,.
 
Siku za nyuma kuna bendi iliimba nyimbo ikiitwa Makumbele,hebu itafsiri moyoni hilo neno MAKUMBELE,lazma utaona ile bendi ilitukana ila kwao wao na kiuhalisia c tusi ni jina tu kama Yale ya kijapan.
 
Basata endeleeni kusimamia maudhui kiweledi ili hata anaefungiwa nyimbo yake au film yake asipate hata pakutokea,.
 
Hv Issa Matona leo angekuwa hai na zile nyimbo zake zenye maudhui mazuri zingepona kweli?
 
Kama sheria inaruhusu kuapeal maamuzi ya Basata ningeshauri kwa hili la nyimbo ya Nyegezi,Wasafi do that!!
 
Hv mtu siku akiimba neno linataja kitongoji cha Mchamba wima au Dole nyimbo yake itapona kweli? Mm nilipanga kutoa featuring na Chibu @diamondplatnumz inakisifia kitongoji cha Kunduchi na hoteli zake,sijui kama Basata watairuhusu!! Ahhh nimeikumbuka lile songi la Nyama ya Bata!!
 
Tafsiri ni ww mwenyew ila Maudhui anayo Msanii ( sheria zifuatwe bila shuruti)”

Rais Magufuli Kuwa Mgeni RasimSherehe za Baraza la Maulid -Tanga

$
0
0
Rais John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Baraza la Maulid litakalofanyika wilayani Korogwe mkoani Tanga.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Jumanne Novemba 13, 2018, Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zuberi amesema baraza hilo limeandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata).

Amesema Maulid hayo ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) yatafanyika Novemba 19.

Amewataka wananchi wa Tanga na mikoa jirani kuhakikisha wanafika kwenye maulidi hayo yanayofanyika mara moja kwa mwaka, huku akisema kuchaguliwa mkoa huo ni bahati hivyo wajitokeze kwa wingi.

Kiongozi huyo wa kiroho, amekemea vitendo vya mmomonyoko wa maadili nchini akisema hatua hiyo ndiyo chanzo cha vijana wengi  kupiga picha za utupu bila aibu na kuziweka kwenye mitandao ya kijamii.

Amesema vitendo hivyo vinavunja hadhi ya nchi na kuomba waliofanya hivyo wakadhibitika sheria kali zichukuliwe dhidi yao ili angalau kukomesha hali hiyo inayotia doa taifa kwa ujumla.

''Hii inasababishwa na malezi mabaya nyumbani kwani mtu mwenye akili timamu hawezi kuvunja heshima yake kwa kuweka picha  chafu za kwenye mitandao ya kijamii huo ni uvunjifu wa maadili kwa kiasi kikubwa,'' amesema

Alisema mengi yanayohusu kukemea tabia hiyo yataongelewa na watu maalum kwenye maadhimisho ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa baraza hilo hapa nchini ambalo lilianzishwa mwaka 1968 mpaka sasa.

Bungeni: Serikali inafuatilia stahiki za Mtanzania aliyetunga wimbo wa

$
0
0
Serikali imesema bado inafuatilia malipo ya John Joseph aliyetunga wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dk Damas Ndumbalo amesema tayari Serikali imeshawasilisha ombi la madai kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki na wanasubiri majibu.

"Tulipokea barua kutoka wizara ya habari kuhusu Mtanzania aliyetunga wimbo huo akidai stahiki zake, tayari tumepeleka kwenye jumuiya na wenzetu wanapitia kuona kama kulikuwa na makubaliano yoyote ili waweze kuyafuata," amesema Dk Ndumbaro

Amlitoa kauli hiyo bungeni leo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Martha Mlata aliyetaka kujua stahiki za Mtanzania huyo kutoka mkoani Kagera.

Katika swali la msingi, Mlata alihoji Tanzania ilishiriki namna gani katika mchakato wa kuupata wimbo maalum wa Afrika Mashariki.

Naibu waziri huyo alisema Tanzania ilikuwa miongoni mwa nchi tatu waanzilishi wa EAC ikiwamo Uganda na Kenya na ndizo zilianzisha mchakato wa kuupata wimbo wa jumuiya.

Alizitaja hatua mbalimbali zilizopitiwa katika kuupata wimbo huo hadi kuupata mmoja uliokubaliwa na kuruhusiwa.

Hakimu akubali kesi ya Kaburu kusikilizwa mfululizo

$
0
0
Makamu wa Rais wa Klabu ya Simba, Geofrey Nyange maarufu Kaburu ameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusikiliza mfululizo kesi inayomkabili yeye na waliokuwa viongozi wenzake wawili sababu ya kuchukua muda mrefu.

Kaburu na wenzake wanakabiliwa na kesi ya utakatishaji fedha na kughushi, kesi yao ilikwama jana kuendelea mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba.

Kesi hiyo ilikwama kuendelea na ushahidi baada ya upande wa utetezi kupinga kupokelewa kwa kielelezo mahakamani.

Kielelezo kilichokataliwa kilitolewa na shahidi wa kwanza, Boaz Mbupila ambaye ni msimamizi wa Benki ya CRDB anayeangalia kama benki inakidhi taratibu za kibenki.

Boaz alitoa kielelezo cha taarifa ya benki ya fedha na taarifa nyingine ya kuhamisha fedha kutoka benki moja kwenda nyingine.

Vielelezo hivyo vilipingwa kwa sababu upande wa Jamhuri hawakuonyesha msingi kabla ya kuomba kutoa vielelezo hivyo.

Hakimu Simba baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili aliahirisha kesi na kupanga Novemba 26 kwa ajili ya kutolew uamuzi.

Hata hivyo Hakimu huyo amekubali maombi ya Kaburu na kuipanga kesi hiyo kusikilizwa mfululizo kuanza Novemba 26, Desemba 4 na 5 mwaka huu.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni aliyekuwa Rais wa Klabu ya Simba,  Evans Aveva,  Makamu wake,  Geofrey Nyange na Mwenyekiti wa  Kamati ya Usajili wa Klabu hiyo, Zacharia Hans Poppe.

VIDEO:Rais Magufuli akutana na Rostam Aziz, Ikulu Jijini Dar es Salaam

$
0
0
Mfanyabiashara maarufu Tanzania Rostam Aziz ametinga IKULU kuonana, kuzungumza na Rais Magufuli ambapo baada ya mazungumzo yao Rostam ameongea yafuatayo.

==>>Tazama hapo chini

Habari Njema Kwa Wenye Matatizo Ya Nguvu za Kiume, vitambi, nyama uzembe

$
0
0
(1).Fikiria ulianzia wapi? Je,ulifanikiwa au bado?

(2).Upo tayari kupona kwa haraka?

TIBA ZITOLEWAZO NI,

NGORO 4 POWER; Huongeza nguvu za kiume yenye mfumo wa unga na vidonge dozi siku(6).

MELAMELA; Hurefusha na kunenepesha uume ipo katika mfumo wa unga dozi siku (4).

KASELA; Hurudisha mke,mme,mchumba na hawara ndani ya siku mbili tu,atatimiza mahitaji yote hata Kama yupo mbali na kumfunga asiwe na mtu mwingine.

IKUMBUJA; Humfanya mtu  kupandishwa cheo kazini na kulipwa madeni au mafao yako pia na kumaliza kesi kabisa.

DUDUMA; Huongeza hips,makalio na mguu wa bia.

SWASWA: Hupunguza maziwa makubwa, kitambi, nyama uzembe, michirizi na muwasho sehem za Siri,na harufu mdomoni.

KOOLA;Hutibu magonjwa sugu ya zinaa, tumbo kujaa gesi,kuuma chini ya kitovu, kiuno ,fangasi za miguu, na kuvimba miguu au miguu kuwaka Moto.

Kwa hayo na mengineyo mfatilie DR.HINDU kwani ana uwezo wa kuhudumia ndani na nje ya TANZANIA.Kwa Dar es salaam anapatikana BUGURUNI MALAPA pia KAHAMA anapatikana MARUNGA.

Kwa wasio na mda wa kufika ofisini kwangu Nina vijana wa kukuletea mpaka ulipo kazini ama nyumbani kwako.

OFISI ZINAFUNGULIWA SAA 07 :00 ASUBUHI.

CONTACTS 0744 922 982(WhatsApp), 0716608959.

  "WOTE MNAKARIBISHWA".DR   HINDU NI SULUHISHO LAKO.

Taarifa Toka IKULU: Rais Magufuli akutana na Rostam Aziz, James Mbatia, John Cheyo na John Shibuda, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Wananchi wa Tanzania (JWTZ) akamatwa na mirungi

$
0
0
Jeshi la Polisi mkoani Manyara, linamshikilia Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wa Monduli mkoani Arusha kwa kukutwa na dawa za kulevya aina ya mirungi kilo 20.

Akithibitisha kukamatwa kwa askari huyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Augustino Senga amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa jana saa 16:50 jioni maeneo ya Minjingu Kata ya Nkaiti, Wilaya ya Babati wakati askari wakiwa katika upekuzi wa magari na ufuatiliaji wa taarifa fiche.

“Wakati wanaisimamisha gari lenye namba T543DHJ, aina ya Alteza ikitokea Makuyuni, Arusha katika kizuizi cha mabasi Minjingu, ghafla gari hilo lilibadilisha mwelekeo kurudi nyuma kuelekea Arusha na ndipo askari hao walipotilia shaka na kuanza kuifukuza kwa nyuma na kufanikiwa kuikamata maeneo ya Nanja Wilaya ya Monduli ikiwa inaendeshwa na dereva mwanajeshi mwenye namba  MT. 12014 Abdul Bashiri Ally miaka 25 Askari wa JWTZ Monduli Arusha,”amesema Kamanda Senga.

Kamanda Senga amesema baada ya kuipekua gari hiyo ilikutwa ba bunda 60 za mirungi sawa na kilo 20 ikiwa imehifadhiwa kwenye buti la gari hilo.

“Mtuhumiwa amekamtwa kwa mahojiano kubaini mahali alikoitoa na kubaini mtandao wake kwani wakati anakamatwa mwenzake alishuka kwenye gari na kutoroka.

Rayvanny, Diamond na Lebo ya WCB wapigwa faini ya Tsh mil. 9 na BASATA

$
0
0
Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) limewatoza Sh9 milioni wanamuziki Rayvanny na Diamond Platnumz , kwa kutoa wimbo Mwanza ikieleza kuwa una mashairi yanayokiuka maadili.

Hatua hiyo imekuja baada ya leo Novemba 13 kufanyika kikao kati Rayvanny ambaye ndiye mwenye wimbo huo, kilichoketi kwa takribani saa tatu katika ofisi za Baraza hilo zilizopo Ilala Bungoni, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu wa Baraza hilo, Godfrey Mngereza amesema kiasi hicho cha fedha kimetozwa kwa wasanii Rayvany na Diamond kila mmoja  Sh3 milioni na kwa lebo ya Wasafi ambayo nayo imesajiliwa Basata.

Sambamba na hilo, Mngereza amesema wametakiwa kupeleka mashairi ya wimbo huo na kusisitiza kuwa hakuna mahala utakaporuhusiwa kupigwa hapa nchini Tanzania iwe usiku au mchana kwa kuwa hauifai.

“Huu wimbo haufai kabisa. Hata kwenye kikao tumemuuliza Rayvanny je, unaweza kuuimba mbele ya wazazi wako akajibu hapana, inaonyesha namna gani hata yeye anaona hauna maadili, na kwa nini tupige marufuku usipigwe halafu turuhusu ifanywe hivyo usiku?" Alihoji Mngereza.

Kwa upande wake Meneja wa lebo ya Wasafi, Hamis Taletale 'Babu Tale'  amesema katika kikao yameamuliwa mambo mawili ikiwamo kupeleka mashairi ya wimbo huo yakahaririwe na kutoendelea kuusambaza.

Akizungumza mara baada ya kikao hicho kilichodumu kwa takribani saa tatu, Babu Tale amesema barua ya kuitwa kikaoni waliipata jana jioni na kati ya mambo waliokubaliana ni kupeleka mashairi ya wimbo huo.

Kuhusu kuufuta kwenye mitandao amesema hilo wataenda kulijibu kwa barua.

Suala la wasanii wao kujitetea kupitia Instagram, amesema wameona mambo yatakayozungumzwa kikaoni huenda yakabaki humo, hivyo wameamua kutumia majukwaa ya mitandao kueleza utetezi wao.

Maandalizi Ya Mpango Na Bajeti Kwa Mwaka 2019/20 Kuzingatia Maoni Ya Wabunge

$
0
0
Na Saidina Msangi na Farida Ramadhani-WFM
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) amesema kuwa Serikali itazingatia maoni na ushauri wa wabunge wote katika Maandalizi ya Mpango na Bajeti kwa Mwaka 2019/2020.

Waziri Mpango alitoa kauli hiyo Bungeni wakati akiahirisha mjadala wa Mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa na Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2019/2020.

Akitoa ufafanuzi wa baadhi ya  maoni ya wabunge kuhusu kuboresha sekta ya kilimo  ikiwemo kuongeza bajeti ya kilimo, Dkt. Mpango alisema kuwa uongezaji wa bajeti ya kilimo ni muhimu lakini lazima ufanyike kwa ulinganifu wa mahitaji ya kibajeti ya sekta nyingine muhimu.

“Ni muhimu kukumbuka kuwa sekta ya kilimo ina mwingiliano mkubwa na sekta nyingine. Mwenendo bora wa kilimo unategemea sana uwekezaji wa sekta saidizi hasa miundombinu ya umwagiliaji, barabara vijijini, umeme kwa ajili ya kuendesha viwanda vya kuongeza thamani ya mazao, uzalishaji wa zana za kilimo, dawa, elimu na afya kwa wakulima” alisema Waziri Mpango.

Aidha, waziri Mpango aliongeza kuwa ni muhimu kuvutia sekta binafsi kuwekeza katika sekta za kilimo na uvuvi, kuimarisha upatikanaji wa mikopo kwa wakulima, wafugaji na wavuvi pamoja na kutafuta masoko ya kikanda na kimataifa.

Akizungumzia miradi mikubwa inayotajwa kukwama Waziri Mpango alifafafanua kuwa miradi iliyokwama imetokana na masharti hasi ya wawekezaji ambayo hayana maslahi kwa Taifa.

“Serikali ina nia ya kuona nchi inaendelea haraka hata hivyo inayo dhamana ya kuhakikisha kuwa rasilimali hizo zinatumika vizuri kwa kulinda maslahi mapana ya Taifa” alisema Dkt. Mpango

Kuhusu kupungua kwa ukwasi katika uchumi waziri ameeleza kuwa madai hayo yanahusishwa na kupungua kwa fedha mifukoni kwa wananchi na kwa benki za biashara kwani upatikanaji wa fedha kwa mianya isiyo halali umedhibitiwa, ukwepaji kodi, madai hewa , ufisadi, rushwa, wizi, ubadhilifu wa mali ya umma vimekomeshwa.

Ametoa wito kwa wananchi kujishughulisha katika shughuli halali  na kufanya kazi kwa bidii na ufanisi ili kujenga Taifa na kufikia azma ya ujenzi wa uchumi wa viwanda.

Pia, Waziri Mpango ametoa rai kwa wabunge kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano katika kuwaletea wananchi maendeleo. 

Mwisho

 

Waziri Mkuu Asikitishwa Na Wizi Kwenye Mradi Wa NSSF Dege.

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea mradi wa nyumba unaojengwa kwa ubia kati Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na kampuni ya Azimio Housing Estate Limited katika eneo la Dege Beach Kigamboni na kutamka kuwa amesikitishwa na uharibifu wa mali na wizi unaendelea kwenye eneo hilo.

Amewaagiza Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, William Erio na Mkurugenzi wa Mkuu kampuni ya Azimio Housing Estate Limited, Mohammed Iqbal  wakutane na Kamishna Mkuu wa  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere ili wajadiliane namna ya kudhibiti wizi na kuimarisha ulinzi.

Waziri Mkuu alitembelea eneo la mradi huo jana jioni (Jumatatu, Novemba 12, 2018) ambapo baada ya kufika katika eneo ambalo linajengwa nyumba zaidi ya  7,000 alionesha kusikitishwa na uharibifu wa mali na wizi unaoendelea na kutoa maagizo kwa wahusika.

“Kuna mpango gani wa ulinzi wa mali hapa, mali zinaendelea kuibiwa, tutakuja kuanza ujenzi hapa na kukuta hakuna mali hata moja. Ulinzi lazima uimarishwe pande zote mbili za mradi huu eneo la ujenzi na eneo la kuhifadhia vifaa vya ujenzi.”

Kwa upande wakeMkurugenzi Mkuu wa NSSF, Erio alimuahidi Waziri Mkuu kwamba atahakikisha wanakutana na Kamishna wa TRA na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya AZIMIO ili kujadiliana na namna ya kuimarisha ulinzi na kutatua changamoto ya wizi wa mali unaoendelea katika eneo hilo.

Mkataba kati ya NSSF na Azimio Housing Estate Limited (AHEL) ulisainiwa mwaka 2012 na kuanzisha kampuni ya hodhi ya “Hifadhi Builders” ambapo AHEL ilikuwa na asilimia 55 na NSSF asilimia 45. Katika asilimia 55 za AHEL, asilimia 20 ni ardhi iliyotoa kwenye mradi na asilimia 35 angetakiwa kuweka fedha taslimu.

Mradi ulihusisha ujenzi wa nyumba 7,460 ambapo jumla ya gharama za mradi zilikadiriwa kuwa Dola za Marekani 653,436,675 ambazo kati yake ujenzi ungegharimu Dola 544,530,562 wakati gharama za ardhi zingekuwa Dola 108,906,113. Kwa fedha za Tanzania mradi pamoja na ardhi ungegharimu sh. trilioni 1.5.

Hadi kufikia Juni 2018 NSSF walishailipa kampuni ya Hifadhi Builders Dola 133,838,662.2 kama mchango wake kwenye ujenzi wa mradi huo ambazo ni sawa na sh. bilioni 305.8 wakati kampuni ya Azimio ikitoa Dola 5,500,000 sawa na sh. Bilioni 12.6 tu.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, NOVEMBA 13, 2018.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano ya Novemba 14

Tanzania yatoa sababu ya kutosaini mkataba wa Afrika kuhusu demokrasia, chaguzi na utawala bora

$
0
0
Tanzania imetaja sababu za kutotia saini mkataba wa Afrika kuhusu demokrasia, chaguzi na utawala bora ikisema ni kutokana na baadhi ya vifungu kukinzana na ibara za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dk Damasi Ndumbaro ameliambia Bunge hayo jana wakati akijibu swali bungeni.

Katika swali la msingi, Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Neema Mgaya alisema miaka sita iliyopita Tanzania ilishiriki nakupitisha azimio kuhusu masuala ya demokrasia, chaguzi na utawala bora na kutaka kujua hadi sasa Serikali imefikia wapi.

"Je Serikali inaweza kueleza ni kwa nini hadi leo azimio hilo halijaridhiwa na kusainiwa rasmi na Serikali ina mkakati gani kuhakikisha linaridhiwa?," alihoji Mgaya.

Akijibu, naibu waziri huyo alisema hadi sasa ni nchi 35 tu ndizo zimeridhia mkataba huo wakati nchi 19 hazijaridhia ikiwamo Tanzania.

Alisema wakuu wa nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika walikutana Januari 30, 2007 na kuzitaka nchi kuzingatia na kutekeleza utawala bora, utawala wa sheria na haki za binadamu kama ilivyo katika ibara ya 3 na 4 ya mkataba.

Watalii 10,000 kutoka China kuja kuitembelea Tanzania mwakani

$
0
0
Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imesaini makubaliano na kampuni ya Touchroad International Group ya China kwa ajili ya kusafirisha watalii 10,000 kutoka jiji la Shanghai kutembelea Tanzania mwaka 2019 kwa kutumia ndege Maalum (chartered flights).

Makubaliano hayo yalisainiwa sambamba na mikutano ya kutangaza utalii katika soko la China- Tourism Roadshow katika miji mitano ya China iliyoanza katika jiji la Shanghai tarehe 12 Novemba 2018.

Mikutano hiyo ni matokeo ya jitihada za Ubalozi wa Tanzania nchini China kwa kushirikiana na TTB ambapo katika mkutano wa kwanza uliofunguliwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki, washiriki mbalimbali zaidi ya 200 walijitokeza wakiwemo makampuni ya utalii (tour operators), mawakala wa usafirishaji (travel agents), mashirika ya ndege (airlines), na vyombo vya habari.

Katika mkutano huo, Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii, Bi. Devotha Mdachi alitoa mada maalum kuhusu vivutio vya utalii vilivyopo nchini Tanzania pamoja na fursa za uwekezaji katika sekta ya utalii. Aidha, makampuni ya utalii kutoka Tanzania yalipata fursa ya kuelezea packages zao za utalii mahsusi kwa soko la China. Kadhalika, Shirika la Ndege la Tanzania lilitumia fursa hiyo kutangaza juu ya mpango wake wa kuanza safari za moja kwa moja kutoka Tanzania hadi China katika mji wa Guangzhou mwezi Februari 2019.

Mikutano ya kutangaza utalii itaendelea kufanyika katika miji mingine ikiwa ni pamoja na Guangzhou tarehe 14 Novemba 2018, Hong Kong tarehe 16 Novemba 2018, Chengdu tarehe 19 Novemba 2018 na Beijing tarehe 20 Novemba 2018.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma, 13 Novemba 2018

Video Mpya: Fid Q Ft. Chin Bees – Maselabration

$
0
0
Msanii Fid Q anakukaribisha kutazama video ya wimbo wake mpya uitwao Maselabration ambao amemshirikisha Chin Bees. Itazame hapa.

Video Mpya: Kassim Mganga Ft. Nandy X Fid Q - InBobo

$
0
0
Video Mpya: Kassim Mganga Ft. Nandy X Fid Q - InBobo. Itazame hapo chini
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images