Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Polisi waonyesha nyumba aliyohifadhiwa ‘Mo’ Dewji Baada ya Kutekwa

$
0
0
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa ameonyesha nyumba anayodaiwa kuhifadhiwa mfanyabiashara Mohammed Dewji ‘Mo’ baada ya kutekwa na watu ambao mpaka sasa hawajajulikana.

Mo Dewji (43), alitekwa Oktoba 11,2018 alfajiri katika Hoteli ya Colosseum jijini Dar es Salaam nchini Tanzania alikokwenda kufanya mazoezi lakini alipatikana Oktoba 20 katika viwanja vya Gymkhana baada ya kutelekezwa na watekaji.

Leo  Jumapili Novemba 11, 2018 mbele ya wanahabari, Kamanda Mambosasa ameonyesha nyumba hiyo yenye ghorofa moja iliyopo Mtaa wa Mwansasu Mbezi Beach jinini hapa.

Amesema baada ya mfanyabiashara huyo kupatikana  polisi waliendeleza msako na kufanikiwa kuipata nyumba hiyo iliyopo umbali kilomita moja toka barabara ya Old Bagamoyo.

"Nyumba hii ndipo alipokuwa akihifadhiwa Mo baada ya kutekwa, Nyumba hii ni ya marehemu Mwansasu lakini sasa hivi inamilikiwa na binti zake,” amesema Mambosasa.

"Katika nyumba hii walitokea watu waliojitambulisha kuwa ni wafanyabiashara wa madini kutoka Afrika Kusini walipanga lakini walipitia kwa Twalib Mussa," amesema.

Kamanda Mambosasa amesema makubaliano yaliyokuwapo ni wafanyabiashara hao kulipa Dola za Marekani 1,500 (Sh3.4 milioni) kwa mwezi huku wahusika wa nyumba wakipata dola 1,300 huku Mussa aliyefanikisha wafanyabiashara kupata nyumba hiyo akiambulia dola 200.

Kwa upande wake, Twalibu ambaye ni dereva wa teksi anayefanya shughuli zake Hotel ya Whitesands amesema yeye ndio aliyefanikisha wafanyabiashara hao kupata nyumba hiyo baada ya kuwaunganisha na madalali.

Naibu Waziri wa Ujenzi anusurika kifo ajalini

$
0
0
Naibu Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye leo Jumapili Novemba 11, amenusurika kifo baada kupata ajali eneo la Iguguno Kata ya Mkalama mkoani Singida.

Naibu waziri huyo amesema alikuwa katika ziara ya kikazi lakini anamshukuru Mungu yeye na alioambatana nao katika msafara huo wametoka salama.

“Ni kweli tumepata ajali, ilikuwa kilomita 25 kabla ya kuingia Singida nilikuwa natokea Nzega kikazi lakini namshukuru Mungu tumetoka salama wote,” amesema.

Yusuf Manji athibitisha kurudi rasmi Yanga

$
0
0
Baada ya Baraza la Michezo Tanzania (BMT) na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuitaka Yanga kuitisha uchaguzi wake kwa ajili ya kujaza nafasi zilizo wazi ikiwemo ya Manji aliyeandika barua ya kujiuzulu Mei 2017 baraza la wadhamini limetoa tamko.
 
Mwenyekiti wa Baraza la wadhamini wa Yanga ambaye ni Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika amesema kuwa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuphu Manji amerejea rasmi.

"Kwenye mkutano mkuu ule wa wanachama, ilipigwa kura nani wanamtaka Manji arudi, wajumbe wote 4500 walisema tunamtaka Manji arudi na sisi katika baraza la wadhamini tukasema Manji aandikiwe barua ", amesema.

"Tukamuandikia barua na mimi mwenyekiti wa baraza ndiye niliyetia saini, amejibu Manji kwa kifupi anasema, Nimepokea maamuzi ya wanachama wa Yanga, lakini bahati mbaya kipindi nimepokea nipo kwenye matibabu, tarehe 15 Disemba madaktari wanasema nitakuwa nimekamilika, nitaanza kuhudhuria ofisini mara kwa mara kuanzia 15, Januari," ameongeza Mkuchika.

Pia, Mkuchika amesema kuwa klabu hiyo sasa ina mwenyekiti wake ambaye ni Yussuph Manji na suala hilo liko kihalali kwakuwa ni maamuzi ya mkutano mkuu.

"Mwenyekiti karudi, Manji amerudi ametuma barua yake sasa kama amerudi yeye ndiye kiongozi wetu amesharudi na Lingalangala yeye ni kaimu Mwenyekiti," alisema.

Uchaguzi wa Yanga ulipangwa kufanyika tarehe 13 januari mwakani na fomu zilitangazwa kutolewa TFF na Ofisi ya Yanga.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu Ya Novemba 12

Lulu Diva: Hata Kutulia na Mpenzi Mmoja ni Usafi

$
0
0
Muimbaji wa Bongo Fleva, Lulu Diva ameeleza mtazama wake kuhusu mapenzi.

Lulu Diva  anayefanya vizuri na wimbo wake uitwao Alewa ameeleza kuwa hata mtu kutulia na mpenzi mmoja ni usafi. Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika; "Usafi sio kuoga, kufagia, wala kufua tuu, hata kutulia na mpenzi mmoja pia ni usafi,"

Ni mara kadha Lulu Diva amekuwa akiripotiwa kuwa kwenye mahusiano na Rich Mavoko lakini wote wamekuwa wakikanusha hilo.

Aslay alivyoanguka kwenye jukwaa Kenya -VIDEO

$
0
0
Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania Aslay amepata  ajali kazini baada ya kudondoka jukwaani akipafomu katika moja ya tour ya anayoifanya nchini Kenya.

Aslay wakati anaperform katika mji wa kisumu alidondoka jukwaani kutokana na jukwaa hili kuonekana halikuwa imara na baada ya hapo alibebwa kwa ajili ya kupumzishwa lakini baadaye alirudi tena jukwaani.

Kupitian ukurasa wake wa Instagram Aslay alisema;” It’s normal for celebrities and performers to encounter some challenging moments while on stage and mine came through yesterday, I slipped on stage but miraculously I wasn’t hurt, I came back on stage and gave one of the most electrifying performance, #Kisumu you guys are AMAZING the Energy was insane. 

"Mwenyezi Mungu Awabariki !!! …….. Ni Kawaida kwa Wasanii kupatana na changamoto jukwani, na Jana ilikuwa zamu yangu, yalitokea Haya punde tu nilipopanda jukwani kwa bahati nzuri sikuumia ,nilirejea jukwani na kuburudisha Mashabiki wangu wa Kisumu waliyojitokeza kwa wingi. Asanteni sana nyote Mwenyezi Mungu Awabariki!!!”

Jipatie Dawa ya Asili ya Kupunguza Maziwa, Kupunguza Tumbo,Kuongeza Unene, Kuongeza Maumbile ya Kiume na Kuondoa Chunusi

$
0
0
NATURAL BEAUTY PROD. Tumeingiza mzigo mpya ni bidhaa zilizothibitishwa kiafya na kupewa kibali original cha kuuzwa hadharani.  Bidhaa hizi zimetengenezwa kwa mimea na matunda hazina chemical wala madhara yoyote kwa mtumiaji. Ukinunua bidhaa kuanzia mbili utapatiwa offer ya bidhaaa nyingine yoyote uipendayo wewe.

1. SHARK POWER--Hii ni dawa ya kupaka ya kuongeza uume urefu na upana mpaka nchi 7.5 inapatikana kwa @170,000/=

2. VIGA 84000---Hii dawa ya kuspray yenye uwezo mkubwa wa kuchelewesha wakati wa tendo la ndoa @160,000/=

3. HANDSOME UP ORIGINAL-- Hichi ni kifaa cha kuongeza maumbile kwa size uipendayo pamoja na kuimalisha misuli kifaa hichi kinapatikana kwa @230,000/=

4. MAXMAN CAPSULE--- Hii ni dawa ya vidonge ya kuongeza uume urefu na upana pamoja na kuongeza nguvu za kiume kwa wiki mbili tu bei yake ni @200,000/=

5. VIG RX---- Hii ni dawa ya kupaka ya kuongeza uume urefu na upana mpaka nchi 10 inapatikana kwa @190,000/=

6. BODY BOOSTER---Hii ni dawa ya kunywa ya kuongeza mwili pamoja na hamu ya kula vizuri @150,000/=

7. BOTCHO MULT PLUS-- Hii ni dawa ya kunywa ya kuongeza (hips mapaja na makalio) kwa size uipendayo unaipata kwa @200,000/=

8. WHITE COLLECTION---- Ni vidonge vya kuwa mweupe mwili mzima pamoja na kuwa soft @150,000/= N.K  Wasiliana nasi kwa simu

NO:. +255 759029968  AU +255 659618585

Popote ulipo utapata huduma zetu.

Pia hakikisha unapatiwa risiti yenye muhuri halisi wa NATURAL BEAUTY PROD ununuapo bidhaa kampuni hii.  WELCOME ALL

Tatizo La Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Na Maumbile Madogo

$
0
0
Tatizo La Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Na Maumbile Madogo Ya Uume Limekuwa Kubwa Kwa Lika Zote Hapa Kwetu Na Duniani Kote. Tatizo Si Tatizo Bali Ni Iletiba Sahihi Ya Matatizo Haya Chanzo Chake Na Visababisho Vyake.

DALILI;mwili kuchoka, maumivu ya mgongo na kiuno, kutopata choo vizuri hata ukipata choo kinakuwa kigumu au gololi kama mavi ya mbuzi. misuli ya uume kulegea na kusinyaa hata uume kulegea na kushindwa kufika kileleni. miguu kuuma na kuwaka moto.

 TIBA YAKE;LUKUBA 4mix ni dawa pekee inayoweza kutibu matatizo hayo inarudisha nguvu za kiume mara dufu na kufanya urudie tendo la mara tatu bila kuchoka. 

LUKUBA 3 pump; ni dawa inayorefusha na kunenepesha uume hadi inchi 7 hadi 9 na kunenepesha kwa CM 2 na kukupa umbile la uhakika. ITUMIE TIBA HII KUOKOA NDOA YAKO NA KUOKOA KUKIMBIWA NA UMPENDAYE,

 ISABILO; Ni dawa itoayo mafanikio na utajili kwa watu walioshindwa kufanikiwa kimaisha, 

MWITE; Ni dawa ya mvuto kumvuta umpendaye na kumrudisha aliyembali na atakutimizia ahadi zote awe mwanamke au mwanaume. 

LUTA CD; Ni dawa inayotibu magonywa nyemelezi yanayopunguza kinga za mwili na kusababisha mwili kuzoofu na inaondoa miwasho na kuondoa kemikali na taka zinazozagaa mwilini. 

KISUKARI; Tunayo dawa ya DAYON inayotibu na kuzalisha insulin kwa wingi na kumfanya mwenye tatizo hili kupona kabisa ugonjwa wa kisukari, kwani husababisha misuli ya mwili kutokufanya kazi vizuri

MPIGIE DR DAGOTIMAN NDIYE SULUHISHO LA MATATIZO YAKO   0658920640/ 0754372325 / 0620806813
 
HUDUMA HII INAWEZA KULETWA POPOTE ULIPO OFISI ZETU ZIPO MBAGALA ZAKHEM DAR ES SALAAM.

Msemaji wa Jeshi la Magereza: Lulu Michael Bado Ni Mfungwa

$
0
0
Msemaji wa Jeshi la Magereza, Amina Kavirondo, ametoa ufafanuzi juu ya kuachiwa huru kwa muigizaji Elizabeth Michael 'Lulu' ambaye inasemekana amemaliza hukumu ya kifungo chake, akisema kwamba Lulu bado ni mfungwa.

Msemaji huyo amesema kwamba utaratibu wa mfungwa yeyote anayemaliza kifungo chake lazima ufuatwe kwanza, ndipo aachiwe rasmi na Jeshi la Magereza, na ndipo anaweza kuwa huru na maisha yake.

“Taratibu nafikiri zinaeleweka, anakuwa bado ni mfungwa, na anapokuwa na kifungo hicho cha nje kuna taratibu zake, akimaliza basi kuna taratibu kama mfungwa yeyote, hata kama ni maarufu. Kile ambacho Lulu atafanyiwa ndicho atakachofanyiwa mfungwa mwingine yeyote, 'treatment' yetu ni sawa na wafungwa wengine," amesema.

"Kama hatukutangaza wakati wafungwa wengine wanatoka hata yeye hatutatangaza, na hakutakuwa na upendeleo, na mwenyewe anajua anatakiwa afanye nini, yule ni mfungwa kama wengine, hawezi kumaliza akaondokea kule kule”, ameongeza Amina Kavirondo.

Muigizaji huyo anatarajiwa kumaliza kifungo chake mwezi huu, baada ya kubadilishiwa hukumu kutokana na msamaha wa Rais na kupewa kifungo cha nje, kwa kesi ya mauji bila kukusudia iliyokuwa ikimkabili hapo awali, ambapo alihukumiwa miaka miwili jela.

BASATA Yaufungia Wimbo Mpya wa Diamond na Rayvanny- Mwanza (Nyegezi)

$
0
0

Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) limetangaza kuufungia wimbo mpya wa mwanamuziki Rayvanny kwa maelezo kuwa unahamasisha masuala yasiyokubalika katika jamii.

Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza amesema  kuwa wameufungia wimbo huo ambao amemshirikisha Diamond Platnumz na kupiga marufuku kuchezwa mahali popote.

Ameongeza kuwa wanawasiliana na mamlaka nyingine ili kuchukua hatua zaidi kwa kuwa tayari wimbo umeenea mitandaoni.

Kuhusu kupigwa katika tamasha lao la Wasafi linalotarajiwa kuanza kutimua vumbi Novemba 24 mwaka huu amesema nalo watalifungia iwapo watautumia.

Ameainisha kuwa maneno yaliyotumika katika wimbo huo yanahamasisha ngono kinyume na maumbile na matusi mengine yanayobomoa maadili.

Kiboko Ya Matatizo Ya Nguvu Za Kiume,maumbile Madogo, Mvuto Wa Mapenzi ,magonjwa Sugu

$
0
0
Matatizo ya nguvu za kiume  yamekua yakiathiri watu wengi sana kisaikologia hasa baada ya kujiona wakotofauti sana na wengine, kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia nchi (6-8) vinginevyo mtuhuyo anamatatizo.

Zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo hili, chango :- hushambulia never ambayo huasili misuli ya uume, Ngiri :- hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kufanya tumbo kuunguluma na kujaa gesi, kolodani moja kuvimba au kuingia ndani pamoja na kutopata choo vizuli Sababuhizi na nyingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba namarakwamara husababisha kukosa hamu ya kuludia tendo la ndoa na baadae kukosa kabisa

MIHINI:- Nidawa ya vidonge iliyotengenezwa kwa mitishamba, huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka (15-80) inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii) ,inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa, itakufanya uwe na hamu ya kuludia tendo la ndoa zaidi ya maratatu bilahamu kuisha wara kuhisi kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kilelen Kwa mda wa dk (18-25).

SUNUPER :- hurefusha na kunenepesha maumbile madogo ya uume uliosinyaa inchi 6-8 na unene wa sm 3-4 kwamda mfupi sana , ni Dr GALIMU mtatuzi wa matatizo yako kunadawa ya kupunguza unene, kitambi (nyamazembe),matiti makubwa kuwa madogo, uzazi, kuludisha mali iliyopotea, kuuzavitu bila kununuliwa, biashara, wachimba madini kusafisha nyota, kuludishwa kazini mvuto wa mapenzi nk.

KWAHUDUMA NA MSAADA WASILIANA NA DR GALIMBO ATAKUSAIDIA SM NO :- 0744391089  au  0653182109

Nape Alianzisha Bungeni Kuhusu Korosho....Naibu Waziri Amtuliza

$
0
0
Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye ameitaka Serikali kutoa majibu ni wapi zitapatikana fedha za kuchangia elimu mkoani Lindi ikiwa korosho hazijauzwa.

Nape ameuliza swali hilo bungeni leo Jumatatu Novemba 12, 2018 akisema yaliyotokea kwenye korosho yanajulikana.

"Mheshimiwa mwenyekiti, sisi mkoa wa Lindi tukikubaliana kukata Sh30 kwa kilo ya korosho ili kuchangia elimu na mwaka jana katika jimbo langu pekee zilipatikana zaidi Sh 400 milioni lakini yaliyotokea sote tunajua, je nini mkakati wa serikali katika hilo," amehoji Nape

Akijibu swali hilo ni vizuri Naibu Waziri TAMISEMI, Josephat Kandege amesema; "Nape tusubiri, najua unatamani korosho zinunuliwe, lakini vile ambavyo tulipanga viende kwenye maendeleo lazima viendelee"

LIVE: Rais Magufuli Akiwaapisha Mawaziri Wapya Aliowateua....Fuatilia Hapa

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo anawaapisha Mawaziri na Makatibu ambao amewateua Jumamosi ya Novemba 10, 2018. 

==>>Tazama hapo chini

Breaking News: Makampuni 13 Yajitokeza Kununua Korosho...Kampuni Moja Linataka Korosho Tani Laki 2

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kwamba kuna makampuni 13 yamejitokeza kutaka kununua korosho kwa bei elekezi ya serikali.

Majaliwa ametoa kauli hii leo Jumatatu November 12 wakati wa zoezi la kuwaapisha mawaziri wapya walioteuliwa na Rais Magufuli.

Amesema, makampuni matano yalipeleka barua ofisi ya Waziri Mkuu Dar es Salaam huku makampuni 8 yakipeleka Dodoma.

Waziri Mkuu ameyataja makampuni hayo kuwa  ni Mega movers  ambayo inataka tani laki 2, kampuni ya Kitanzania Mkeme Agri inataka tani elfu 5, na makampuni matatu yatachukua tani elfu 5, makampuni manne, tani elfu moja moja.

Amber Rutty Na Mpenzi Wake Wakosa Dhamana Tena na Kurudishwa Gerezani

$
0
0
Msanii Rutyfiya Abubakary maarufu 'Amber Ruth' na mpenzi wake Said Kitomali wamekosa dhamana tena baada ya wadhamini wao kutofika kwenye kesi inayowakabili katika Mahakama ya Kisutu Dar  ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile. 

Wadhamini hao, wanatakiwa wawe na vitambulisho vya Taifa na washtakiwa hao wasalimishe hati zao za kusafiria mahakamani na wasitoke nje ya Dar es Salaam bila ruksa.

Kwa upande wa mshtakiwa mwenzao, James Delicious yeye alifanikiwa kutimiza masharti hayo ya dhamana Novemba 2, 2018 walipofikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza.

Wakili wa Serikali Mwanaamina Kombakono leo Novemba 12 katika Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizile amedai kuwa kesi ilipangwa kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wake bado haujakamilika.

Hata hivyo, baada ya Kombakono kueleza hayo, Amber Ruty amenyoosha mkono akiwa kizimbani katika ukumbi namba 2 wa Mahakama ya wazi na kuomba dhamana.

Baada ya kutoa ombi hilo, Hakimu Rwizile ameita mahakamani hapo wadhamini wake mara kadhaa na wakili wa Serikali Kombakono naye amewaita wadhamini hao lakini hakuwepo hata mmoja.

Hivyo ameiahirisha kesi hiyo hadi Novemba 26, 2018 na kuwaeleza washtakiwa hao iwapo wadhamini wao watafika ndani ya muda wa mahakama watadhaminiwa.

Breaking News: Rais Magufuli Kasema Korosho Zote Zitanunuliwa Na Serikali kwa sh 3,300....Kagoma Kuyaruhusu Makampuni Yanunue

$
0
0
Rais Dkt. John Pombe Magufuli  amegoma kuyauzia makampuni Korosho kwa madai kwamba ni wababaishaji na wanataka kuwaibia wananchi.
 
Badala yake amesema kwamba serikali itanunua korosho  yote kwa bei ya shilingi 3,300 kwa kilo.
 
Awali, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema kwamba kuna makampuni 13 yamejitokeza kutaka kununua korosho kwa bei elekezi ya tsh. 3000

Aliyataja makampuni hayo kuwa  ni Mega movers  ambayo inataka tani laki 2, kampuni ya Kitanzania Mkeme Agri inataka tani elfu 5, na makampuni matatu yatachukua tani elfu 5, makampuni manne, tani elfu moja moja. 


Ombi hilo limekataliwa na Rais Magufuli kwa madai kwamba  wafanyabiashara hao  ni wababaishaji, hivyo korosho yote itanunuliwa na serikali kwa sh 3,300 kwa kilo isiyobanguliwa.

“Hawa wanaokuja leo hawa ni ujajnja tuu kwanini hawakuja mwezi uliopita? watakuja Na macondition ya ajabu. Sisi hatuwezi kukaa kimya wakulima wetu wananyanyaswa. TANTrade muanze kutafuta masoko ya mazao mengine kama cocoa Na mengine”.  Amesema Rais Magufuli

Habari Njema Kwa Wenye Matatizo Ya Nguvu za Kiume, vitambi, nyama uzembe

$
0
0
(1).Fikiria ulianzia wapi? Je,ulifanikiwa au bado?

(2).Upo tayari kupona kwa haraka?

TIBA ZITOLEWAZO NI,

NGORO 4 POWER; Huongeza nguvu za kiume yenye mfumo wa unga na vidonge dozi siku(6).

MELAMELA; Hurefusha na kunenepesha uume ipo katika mfumo wa unga dozi siku (4).

KASELA; Hurudisha mke,mme,mchumba na hawara ndani ya siku mbili tu,atatimiza mahitaji yote hata Kama yupo mbali na kumfunga asiwe na mtu mwingine.

IKUMBUJA; Humfanya mtu  kupandishwa cheo kazini na kulipwa madeni au mafao yako pia na kumaliza kesi kabisa.

DUDUMA; Huongeza hips,makalio na mguu wa bia.

SWASWA: Hupunguza maziwa makubwa, kitambi, nyama uzembe, michirizi na muwasho sehem za Siri,na harufu mdomoni.

KOOLA;Hutibu magonjwa sugu ya zinaa, tumbo kujaa gesi,kuuma chini ya kitovu, kiuno ,fangasi za miguu, na kuvimba miguu au miguu kuwaka Moto.

Kwa hayo na mengineyo mfatilie DR.HINDU kwani ana uwezo wa kuhudumia ndani na nje ya TANZANIA.Kwa Dar es salaam anapatikana BUGURUNI MALAPA pia KAHAMA anapatikana MARUNGA.

Kwa wasio na mda wa kufika ofisini kwangu Nina vijana wa kukuletea mpaka ulipo kazini ama nyumbani kwako.

OFISI ZINAFUNGULIWA SAA 07 :00 ASUBUHI.

CONTACTS 0744 922 982(WhatsApp), 0716608959.

  "WOTE MNAKARIBISHWA".DR   HINDU NI SULUHISHO LAKO.

Upelelezi Kesi Ya Uhujumu Uchumi Inayomkabili Mdogo Wake Rostam Azizi Haujakamilika

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa upelelezi dhidi ya kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mfanyabiashara Akram Azizi ambaye ni mdogo wa mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Azizi bado haujakamilika.

Wakili wa Serikali Elia Athanas ameeleza hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustine Rwizile kesi hiyo ilipoitwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa.

"Mheshimiwa kesi hii leo imekuja kwa ajili ya kutajwa, upelelezi bado haujakamilika, tunaiomba ipangiwe tarehe nyingine ya kutajwa" amedai wakili Athanas.

Kufuatia malezo hayo, Hakimu Rwizile ameahirisha kesi hiyo hadi Novemba 26 itakapokuja kwa ajili ya kutajwa.

Katika kesi hiyo, Mshtakiwa Azizi anakabiliwa na mashtaka 75 yakiwemo mashtaka 71 ya kukutwa na Silaha za aina mbali mbali mbali, utakatishaji wa fedha kiasi cha USD 9018.

Pia anakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na nyara za serikali zenye thamani ya sh milioni 108, risasi 6496 na pia anakabiliwa na kosa la kukutwa na nyama ya Nyati, Kilogramu 65 yenye thamani ya Shilingi Mil 4.35 bila kuwa na kibali, ambalo anadaiwa kulitenda Oktoba 30,2018 huko Oysterbay Kinondoni Dar es Salaam.

Rais Magufuli: Mimi Sio Mkorofi, Ninyi Ndo Wakorofi

$
0
0
Rais John Magufuli amewataka mawaziri kuwa makini na kushirikian ana vyombo vyote kuhakikisha hata korosho moja haipotei.

Aidha, amewataka kufanya maamuzi bila kuamriwa na rais au Waziri Mkuu kwa lengo la kukuza maendeleo ya nchi.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Jumatatu Novemba 12, Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akiwaapisha mawaziri na naibu waziri aliowateua Jumamosi wiki iliyopita.

“Mawaziri muwe mnafanya maamuzi sio kila kitu Waziri Mkuu au rais wawasaidie kufanya na mimi ninapenda mawaziri wanaofanya maamuzi wenyewe.

“Mnasema mimi mkorofi lakini si kweli ninyi ndiyo wakorofi kwa kuwa hamfanyi yale wananchi wanayotaka mfanye.

“Ni lazima kila mmoja awajibike, mimi sitojali kubaki na mmoja mbona kila siku nabadilisha ni kitu cha kawaida na ninafanya hivyo ili nipate matokeo mazuri, kwanza wabunge wako 365 hata nikiwateua kwa miezi mitano mitano ni sawa tu,” amesema Magufuli.

Waziri wa Nishati avunja Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini

$
0
0
Waziri wa Nishati Dk Medard Kalemani leo (Novemba 12.2018) amevunja Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa Nishati Vijiji REA kutokana na kutoridhishwa na utendaji kazi wake.

Waziri Kalemani amewaambia waandishi wa habari leo jijini Dodoma  kuwa bodi hiyo iliundwa mwaka 2017 kwa mujibu wa sheria ya wakala vijijini No.8 ya mwaka 2005.

“Kwa mujibu wa mamlaka niliyopewa chini ya kifungu 9 (3)(b) cha sheria No. 8 ya nishati vijijini ya 2005 nimeamua kuivunja bodi kwa kutengua uteuzi wa mwenyejuti pamoja na wajumbe wa bodi ya wakurugenzi ya wakala wa nishati vijijini kuanzia leo tarehe 12 novemba 2018″amesema Kalemani.

Aidha amesema kuwa bodi nyingine itaundwa baadae kwa mujibu wa sheria ya nishati vijijini ya mwaka 2005. Bodi hiyo iliyokuwa ikiongozwa na mwenyekiti wake Gigion Kaunda imedumu kwa muda wa mwaka mmoja.

Wajumbe wa Bodi ambao wametenguliwa ni pamoja na Mhandisi Innoceent Lwogwa,Happiness Mhina,Stella Mandago, Scholastica Jullu,Amina Chinja,Teobard Sabi na Michael Nyagoga.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images