Na. Dokta Mungwa Kabili…….0744 000 473. Misukule Huogeshwa na Mungu ni kitabu changu kingine ambacho kinaelezea kuhusu maisha ya misukule usukuleni.
Kitabu hiki kinaelezea A mpaka Z kuhusu masuala yote yanayo husu misukule kuanzia jinsi wanavyo chukuliwa na wachawi, jinsi wanavyo tumikishwa na wachawi, maisha halisi ya misukuleni kuanzia asubuhi wanapo amka hadi usiku wanapo enda kulala, vyakula wanavyo lishwa, madawa wanayo lishwa, kazi wanazo tumikishwa na kadhalika.
Lakini kikubwa kuliko vyote kitabu hiki kinaelezea kuhusu namna gani wewe mwenyewe unaweza kujikinga wewe pamoja na familia yako dhidi ya kuchukuliwa msukule na wachawi.
Maelezo yaliyomo ndani ya kitabu hiki yanatisha na kuogofya sana na kama wewe una moyo mwepesi ninakushauri usijaribu kusoma kitabu hiki.
Hata hivyo lengo la mtunzi wa kitabu hiki sio kumtisha au kumuogofya msomaji, ila ni kumuonyesha msomaji uhalisia uliopo katika ulimwengu usio onekana.
Kitabu hiki kitamsaidia msomaji kuujua kwa mapana yake ulimwengu usi onekana pamoja na kuiona nafasi yake katika ulimwengu usio onekana.
Maana Ya Jina La Kitabu : Jina la kitabu hiki linasadifu mambo yaliyomo ndani ya kitabu hiki.
Mtu anapo chukuliwa msukule hupelekwa usukuleni kwa ajili ya kutumikishwa kazi mbalimbali na wachawi.
Anapokuwa usukuleni huunganishwa na misukule wengine na kufungwa kwenye banda ambalo ndani yake kunakuwa misukule wengi.
Misukule hawa ni binadamu kama walivyo binadamu wengine. Binadamu hula,hunywa, hulala na hujisaidia haja kubwa na haja ndogo.
Misukule hufanya vyote kama binadamu wengine ingawa kwa namna tofauti kidogo. Hula vyakula kama binadamu wengine lakini hula mizoga na vyakula vichafu katika mazingira machafu.
Hujisaidia haja kubwa na ndogo lakini hawajisaidii vyooni kama binadamu wa kawaida. Wao hujisaidia katika sehemu yoyote ile iwe ni porini au katika mabanda yao na wanapo jisaidia huwa hawaogi wala kuogeshwa wala kusafishwa. Hayo ndio huwa maisha yao ya kila siku.
Misukule huoga tu pale wanapo pata ‘ bahati’ ya kunyeshewa na mvua.
Msukule unaponyeshewa na mvua ndio unakuwa umepata bahati ya kuoga. Ndio maana tunasema “ Misukule huogeshwa na Mungu “ kwa sababu ni mvua tu ya Mwenyezi Mungu ndo kitu pekee kinacho weza kuwafanya misukule waoge, lakini vinginevyo hakuna anae weza kuwaogesha.
Uhalisia wa kitabu hiki katika maisha : Kitabu hiki kimebeba uhalisia katika maisha kwenye jamii zetu. Wachawi wapo wanawachukua watu misukule kwa lengo la kuwatumikisha na wakiwa wanatumikishwa huwa hawaogeshwi wala kusafishwa hata wakienda haja kubwa.
Ndio maana vijiji vyote vinavyo daiwa kuwa na misukule wengi huwa vinatoa harufu mbaya sana kwa sababu ya misukule hao. Na kama ulikuwa haujui binadamu ndio kiumbe mwenye kutoa harufu mbaya sana kuliko kiumbe mwingine yoyote Yule wa Mwenyezi Mungu.
Ukitaka kuthibitisha fanya tathmini kati ya harufu ya maiti ya kiumbe yoyote Yule aliye kufa na mwanadamu aliye kufa.
Au fanya tathmini kati ya kiumbe yoyote Yule ambae amekaa mjuda mrefu bila kuoga na binadamu aliye kaa muda mrefu bila kuoga.
Chukua n’gombe au mbuzi au kondoo, mfungie miezi mitatu bila kumuogesha halafu na wewe ukae siku saba bila kuoga wala kufua halafu linganisha harufu zenu.
YALIYOMO NDANI YA KITABU HIKI
Kama hutopata fursa ya kusoma kitabu hiki basi hutoweza kufahamu chochote kuhusu misukule. Na hii kwa sababu ni katika kitabu hiki pekee ndio unaweza kufahamu undani wa hawa viumbe wajulikanao kama misukule.
Mwenyezi Mungu akikupa uhai hadi siku kitakapo ingia mtaani kitabu hiki basi hakuna mchawi yoyote yule chini ya jua hili ambae ataweza kukuchukua msukule kwa sababu ndani ya kitabu hiki yamewekwa wazi maarifa yatakayo kusaidia kujikinga wewe mwenyewe pamoja na familia yako dhidi ya kuchukuliwa msukule.
Hiki ni kitabu ambacho kitawatoa machozi watu wengi sana kwani ndani yake yameandikwa maisha ya misukule usukuleni ambayo kusema ukweli ni maisha yenye mateso mazito sana na yasiyo mithilika.
Hivi unajua wachawi wanaweza kumchukua mtu msukule kwa sababu ya kijinga kabisa ? Kwa mfano unaweza kuwa umegombana na mchawi na akaamua akuchukue msukule ili akutumikishe kazi kwa lengo la kukukomoa.
Mchawi anaweza kumtaka mapenzi mwanamke na mwanamke akimkataa basi mchawi huyo anamchukua mwanamke huyo msukule na kumfanya mke wake.
Wachawi wanaweza kumchukua mtu msukule kwa lengo la kutumia nyota yake tu jambo ambalo wangeweza kulifanya hata bila kumchukua mtu huyo msukule.
Hivi unajua tofauti iliyopo kati ya msukule na kikoa ? Kikoa ni msukule kama walivyo misukule wengine isipokuwa huyu kikoa anakuwa amechukuliwa na mchawi kwa ajili ya sadaka ya kuongeza nguvu zake za kichawi na kupandishwa cheo kaika uchawi.
Msukule wa kawaida anaweza kuwa mtu mwingine yoyote Yule lakini kikoa huyu ni msukule ambae anakuwa ametolewa na ndugu yake wa damu ambae ni mchawi kwa ajili ya sadaka.
Je unajua kuwa mbali na kufanyishwa kazi nyingine kama kulima , kuvua, kuita wateja dukani nakadhalika, misukule hutumiwa pia kwa ajili ya kuchimba na kutwanga dawa za kichawi pamoja na kutafuta vizimba vizito vya kichawi.
Kazi nyingine ya misukule ni pamoja na kutumiwa na wachawi katika kutafuta na kukamata viumbe hatarishi kama vile nyoka wenye sumu kali au vizimba ambavyo huonekana kwa nadra au ambavyo havionekani kwa macho ya kawaida.
Misukule wana uwezo wa kuviona kwa sababu hulishwa madawa yenye uwezo wa kuwafanya kuona yasiyo onekana.
Kwa mfano porini kuna nyoka mmoja ana vichwa viwili ( Sio Ndumilakuwili ).
Makaazi ya nyoka huyu huwa ni ndani ya misitu minene.
Nyoka huyu ana sifa moja ya kipekee. Anapotaka kuhama msitu, huruka juu kama ndege na hutembea na mwanga mkali kama kimondo au nyota.
Anapokuwa msituni huwa anazungusha fimbo za mti mmoja wa porini ambazo zimekaa kama kamba kuzunguka eneo lake .
Miti hii inayo zunguka eneo la nyoka huyu ikiguswa, kuvunjika au kukatika nyoka huyo husimama wima kwa mkia wake kuona adui aliyeko eneo lake ana dhumuni gani.
Miti hiyo ndio mali inayo tafutwa kwa udi na uvumba na wachawi. Miti hiyo hutokana na mti mmoja wa porini ambao hukaliwa na majini au mizimu wa nyoka huyu.
Hakuna mtu alie katika hali ya kawaida ambae anaweza kuichukua miti hiyo kwa sababu kwa kufanya hivyo atakuwa ana jihatarishia kifo.
Kwa sababu hiyo basi wachawi huwatumia misukule kuchukua miti hiyo.
Nyoka huyu huonekana kwa nadra sana na hapa kwetu amewahi kuripotiwa kuonekana kwenye msitu mmoja uliopo huko katika wilaya ya Mlele mkoani Katavi na mwingine amewahi kuripotiwa kuonekana huko mkoani Morogoro.
Kwa kifupi nyoka huyu ni nyoka mwenye maajabu mengi sana na katika uganga na utabibu nyoka huyu hujulikana kama Fimbo ya Mussa kwa sababu miti anayo tumia kuzungusha eneo lake ina uwezo wa kutenganisha maji katika mito na bahari.
Miti hiyo hiyo hutumiwa na wachawi kuleta ama kuzuia mvua. Hutumika pia katika kutibu baadhi ya maradhi ya kisheitwani.
Kwa ufupi miti ya nyoka huyu ina mambo mazito mengi sana. Mambo yote hayo utayajua ndani ya kitabu hiki.
Kama hiyo haitoshi, wachawi pia hutumia vitu vya misukule kama vile nywele, kucha, nguo, mate, nyewele za siri nakadhalika kama vizimba.
Msukule ni binadamu ambae thamani yake imeshushwa chini sana na kuwa kama mnyama.
Ndio maana wachawi huwatumia misukule katika kazi zao mbalimbali kama ambavyo mganga anaweza kutumia mnyama kama kuku au kondoo.
Katika ulimwengu wa misukule hakuna kitu cha msukule kisicho kuwa na thamani. Kuanzia mate, nywele, kucha, nywele za siri nakadhalika vyote hutumika kama vizimba kwa ajili ya kutengeneza madawa makali ya kichawi.
Mfano kucha za misukule hutumika kama nyembe za kuwachanja watu chale za kichawi.
Wala hakuna msukule usio na thamani kuanzia msukule kijana wenye afya hadi msukule mzee usio na afya ambao unaweza kufa wakati wowote. Vyote vina thamani na matumizi makubwa katika uchawi.
Wakati misukule vijana wenye afya wakitumikishwa kufanya kazi mbalimbali kama vile kulima, kuvua samaki, kuchimba migodi, kuita wateja madukani nakadhalika, misukule wazee hutumiwa na wachawi kubadilishana na msukule mpya na mara nyingi misukule wanao tumika hapa ni misukule wazee wenye maradhi mazito
Kwa mfano kama wachawi wanataka kumchukua mtu Fulani msukule kwa staili hii ya kubadilishana na msukule wao mzee ambae ni mgonjwa mgonjwa na ambae wanaona amekaribia kufa baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Kitu cha kwanza watakacho kifanya wachawi hao ni kwanza kumtupia maradhi ya kisheitwani mtu huyo alie kusudiwa ambayo yatamfanya ajihisi homa kali sana au malaria.
Maradhi haya yatamfanya mtu huyo ashindwe kufanya shughuli zake na kushinda amelala siku hiyo. Lakini sura ya maradhi ya mtu huyu itakuwa ni ya kawaida tu. Yani atakuwa kama mtu anae ugua maradhi mengine ya kawaida.
Usiku wa siku hiyo wachawi watakuja na msukule wao mzee ambao umeugua kwa muda mrefu na unakaribia kufa hadi katika nyumba anayo ishi mtu huyu ambae wamekusudia kumchukua msukule.
Wakishafika nyumbani hapo watamchukua huyo mgonjwa aliye lala kitandani hapo na kuondoka nae halafu kwenye kitanda hicho watamlaza msukule wao ambae ni mzee na mgonjwa sana ambae ameugua kwa muda mrefu na kukaribia kufa.
Msukule huyo atavalishwa sura ya Yule mgonjwa alie kuwa amelala kitandani.
Asubuhi mgonjwa wenu ataamka akiwa amezidiwa na hali yake ikiwa imebadilika.
Nyinyi mkiamka mtaona hali ya mgonjwa wenu imebadilika na kuwa sirias.
Mtaanza kumuuguza eidha hapo hapo nyumbani au kwa kumpeleka hospitalini. Lakini hali yake haitobadilika kwa sababu anakuwa sio yeye bali ni huo msukule.
Mtahangaika nae na mwisho wa siku msukule huo utakufa na ninyi mtaamini aliye kufa ni ndugu yenu ilihali ndugu yenu bado yupo hai amechukuliwa msukule ila alie kufa hapo ni msukule.
( ANGALIZO : Hapo juu nimesema wachawi wakitaka kumchukua mtu kwa staili hii huwa wanaanza kwa kumtupia maradhi ya kisheitwani. Lakini sio mara zote. Wakati mwingine mtu anaweza kuwa na maradhi halali kabisa na wachawi wakayatumia kama mlango wa kuingilia… Ndio maana watu wanashauriwa kuwa wasiri pale wanapo kuwa wanauguza wagonjwa wao. Si kila mtu anatakiwa kujua Fulani anaumwa au amelazwa. Wengine ni wachawi kama hao ambao wanaweza kumchukua msukule na wengine wanaweza wasimchukue msukule lakini wanaweza wakamfunga asipone maradhi yake. Yani kila dawa anayo tumia inakuwa haifanyi kazi mwilini )
Kama nilivyo sema hapo juu wachawi wanawatumia misukule katika mambo mengi sana.
Mbali na mambo niliyo yataja hapo juu, wachawi huwatumia pia misukule katika mambo mengineyo kama ifuatavyo :
·-Kuchinja wanyama mbalimbali wa kafara kama vile n’gombe nakadhalika.
·-Kutumwa safari ndefu: Wachawi huwatuma misukule safari ndefu sana ambazo misukule huenda kwa miguu. Hii huwa kazi rahisi kwa misukule kwa sababu huwa wanalishwa madawa ya kuwafanya wawe na nguvu za ziada ambazo huwezi kuzikuta kwa binadamu wa kawaida.
·-Hutumwa kwenda kuiba vitu kwa watu mbalimbali kwa ajili ya matumizi ya kichawi. Kwa mfano kama wachawi wanataka kuchukua nguo za mtu Fulani kwa ajili ya kumroga wanaweza kuwatumia misukule kuja na kuchukua nguo hizo. Hili linawezekana kwa sababu misukule huwa wanachanjiwa madawa yanayo wafanya wasiweze kuonekana na watu wa kawaida.
·-Pia hutumiwa kwenda kuchukua vitu mbalimbali kutoka kwa watu ambao wachawi wamekusudia kuwafanyia ubaya kama vile kucha pamoja na kutumika kuwachanja watu chale na kuwapaka madawa ya kichawi. Mara nyingi unapo amka ukiwa umechanjwa chale za kichawi basi ni asilimia nyingi kuwa chale unakuwa umechanjwa na misukule walio tumwa kuja kwako kwa ajili ya kazi hiyo na chale hizo hawakuchanji kwa kutumia wembe bali wanakuchanja kwa kutumia kucha.
·-Misukule hutumwa kwenda kuweka sumu za kichawi kwenye vyakula au vinywaji vya watu walio kusudiwa kwa lengo la kuwasababishia maradhi ya kichawi.
·-Misukule hutumiwa na wachawi kutafuta vizimba vinginevyo vya kichawi visivyo weza kuchukulika kwa njia rahisi kama vile mayai ya bundi nakadhalika
·-Misukule hutumika pia katika chuma ulete
Wachawi huweza kutumia njia mbalimbali kuwachukua watu misukule. Mbali na kuwachukua watu misukule kwa njia ya kubadilisha na msukule mgonjwa kama nilivyo onyesha hapo juu, wachawi wanaweza kumchukua msukule pia kwa njia ya ajali, kufa maji, kupotea nakadhalika.
Mtu anaweza kwenda kisimani kuchota maji akapotelea huko huko kumbe kachukuliwa msukule, au mtu anaweza kwenda porini kusenya kuni akapotelea huko huko kumbe kachukuliwa msukule, mwingine anaweza kutoka usiku nje kujisaidia na asirudi tena ninyi mkadhani labda ametoroka kumbe amechukuliwa msukule.
Misukule wanao chukuliwaga ghafla bila kuugua huwa wanakuwaga wakorofi sana. Wachawi wanapo ona msukule amekuwa mkorofi sana huwa hawamuui isipokuwa wanamtoa akili na kumpeleka mkoa wa mbali au nchi ya mbali.
Mfano kama mtu huyo kachukuliwa labda Lindi anaweza kupelekwa Shinyanga. Au mtu aliye tolewa Rufiji anaweza kupelekwa Goma , Kongo au kinyume chake.
Msukule kutoka Kongo unaweza kupelekwa Senegali na ule wa Senegeli ukaletwa Tanzania.
Mtu huyo akipelekwa katika sehemu ambayo wachawi wamechagua huanza maisha mapya kama mwendawazimu asiye ongea.
Na hii ndio sababu wapo wendawazimu hawajulikani wanakoishi au wanapotoka. Hawajulikani majina yao wala makabila yao na wala hawana uwezo wa kuongea.
Unaweza ukadhani ndugu zake wamemtelekeza lakini sivyo ndivyo. Mtu huyo anakuwa msukule aliye tupwa kutoka nchi ya mbali au mkoa wa mbali.
Katika hali ya kawaida watu wenye kuugua maradhi ya uwenda wazimu yawe ni ya kawaida ama ya kisheitwani huwa wanapiganiwa na ndugu zao.
Ndugu wa watu wenye maradhi ya uwendawzimu huwa wanawaletaga vilingeni wagonjwa wao kwa ajili ya kuwatafutia tiba.
Ni nadra sana kwa misukule kuugua maradhi ya kawaida hasahasa msukule ambae yupo usukuleni kwa muda mrefu. Hali ya kuugua hutokea kwa misukule wageni kwa sababu miili yao inakuwa haijazoea vyakula vya kisukule na maradhi yao hutokana na vyakula wanavyo kula pamoja na mazingira wanayo ishi ambayo ni sawa sawa na mazingira wanayo ishi wendawazimu na inapotokea msukule umeugua huwa wanalishwa madawa maalumu ya kichawi.
Misukule wanapo ugua hawana uwezo wa kusema “ naumwa” kwa sababu hawana uwezo wa kuzungumza. Ni jukumu la mchawi mwenyewe kujua hapa msukule wangu anaumwa au la yaani kama mtu anae fuga n’gombe, mbuzi au kondoo. Atajua kondoo wake anaumwa kwa kumtazama hali yake.
Misukule hulishwa vyakula vichafu sana kama vile mizoga iliyo okotwa majalalani au iliyo gongwa na magari na mchawi anapokosa vyakula vya kuwalisha misukule wake huwa amuru waende kula kuiba vyakula majumbani kwa watu au kama nyumbani kwenu hamuhifadhi vyakula ambavyo havijapikwa basi misukule hao huamuriwa kuwa wanaenda kula pamoja na watu kwenye nyumba au mji Fulani.
Kwa mfano ataawaambia ninyi mtakuwa mnaenda kula kwa Fulani na ninyi wengine mtakuwa mnaenda kula kwa Fulani.
Ikifika muda wa kula chakula misukule hufika kwenye meza na mnapo pakuwa na kula chakula nao hula nanyi. Ndio maana mnaweza kuwa mmepika chakula kingi lakini mnakula kidogo tu kinaisha na ninyi mnakuwa bado na njaa kali. Hapo jueni mnakula na misukule.
Hii hutokea kwenye familia nyingi sana na kama nilivyo sema hapo juu mkitaka kujua kama huwa mnakula na misukule basi dalili ya kwanza ni chakula kingi kuisha haraka bila walaji kushiba na dalili nyingine unaweza kuwa ulikuwa umekaa vizuri kwenye kiti au ghafla ukajikuta umekalia kalio moja hapo maana yake ni kwamba umempisha msukule akae.
Misukule wakisha maliza kula chakula kwenye miji ya watu huwa wanarudi kwenye makazi yao na kufungiwa kwenye mabanda yao.
Maisha ya misukule hayana tofauti na wanyama wa kufugwa kama mbuzi, kondoo, ng’ombe nakadhalika kwani licha ya kutumikishwa na kupigwa mijeledi kila kukicha lakini hata wanapo achiwa na kwenda kula kwenye majumba ya watu wanarudi tena kwenye makazi yao na kufungiwa bandani.
Wachawi wakisha mchukua mtu msukule kabla hawajamkata ulimi huwa wanamlisha dawa moja ya kichawi. Dawa hii hufuta kumbukumbu zake zote za miaka ya nyuma na kuanza maisha mapya. Yani kwake anakuwa kama hajawahi kuishi kabisa hapo awali. Dawa hiyo ya kichawi hutumika pia kuwafarakanisha mke na mume. Mke au mume akilishwa dawa hii kwa manuizi haya, husahau kabisa kama aliwahi kuwa katika mahusiano au ndoa na mume au mke wake.
Na kama atanuiziwa na watoto pia, basi atasahau kabisa kama aliwahi kuwa na watoto. Atakuja kukumbuka siku atakayo ingia kaburini. Hapa ndio unakuta mwanamke amezaa watoto watatu na mwanaume, mtoto wa mwisho hana hata mwaka mmoja, mwanamke huyo ataondoka na kwenda kuishi na mwanaume mwingine na hatorudi tena kwa mumewe . Ataonekana kama mtu mwenye roho mbaya lakini kiukweli inakuwa sio akili yake. Mume pia anaweza kuondoka na kutelekeza familia na watoto wake bila kuwakumbuka.
Kama mtu alie chukuliwa msukule alikuwa ana nyonyesha wachawi huwa wanamleta kila siku jioni aje kumnonyesha mwanae mpaka mtoto huyo atakapo timiza miaka miwili huku lengo likiwa ni kuandaa mazingira ya kuja kumchukua na mtoto huyo kwa sababu mwanamke huyo huwa anapakwa pia madawa ya kichawi kwenye manyonyo yake na mtoto wake anapo nyonya madawa hayo ya kichawi yanakuwa yanamuingia na kumuandaa kuja kuchukuliwa pia hapo baadae.
Zoezi la kumleta mwanamke huyu msukule kumnyonyesha mtoto wake huwa linafanyika kila giza linapo ingia.
Kuhusu kuoga misukule huwa hawaogi wala hawaogeshwi. Na hii ni kwa sababu uchafu wao una thamani kubwa sana kwa wachawi kuliko usafi wao.
Kwa hiyo hata kama atajisaidia hakuna kujisafisha wala kusafishwa. Kuoga kwa msukule ni mpaka mvua inyeshe. Huu ni msemo maarufu sana miongoni mwa wachawi. “ Kuoga kwa msukule ni mpaka mvua inyeshe. Yani mpaka mvua inyeshe ndio msukule anaweza kuoga lakini vinginevyo msukule hubaki katika mazingira ya uchafu usio mithilika.
Kwa ufupi haya ni baadhi ya mambo yameelezewa kwa undani sana ndani ya kitabu “ KUOGA KWA MSUKULE MPAKA MVUA INYESHE “ kitabu hiki kitakuwa mitaani siku ya tarehe 5 DESEMBA 2018 na kitatoka pamoja na kitabu kingine kiitwacho “ MAARIFA YA JADI “.
Maelezo kuhusu yaliyomo ndani ya kitabu “ MAARIFA YA JADI “ yatakujia siku ya Jumatatu ya tarehe 12 NOVEMBA 2018.
Vitabu vyote hivi vimeandikwa na DOKTA. MUNGWA KABILI. Dokta. Mungwa Kabili anapatikana kwa SIMU NAMBA : 0744 000 473.