Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Amber Lulu apata ajali akielekea kwa Mesen Selekta

0
0
Msanii wa Bongo Fleva na video vixen, Amber Lulu amenusurika kwenye ajali ya gari.

Hitmaker huyo wa ngoma Jini Kisirani amepata ajali akiwa anaelekea kwenye birthday producer Mesen Selekta.

"Wiki hii imekuwa ina misuko sukosana kwangu na Shukuru Mungu kwa yote ilikuwa siku ya jana saa 7 usiku tulikuwa tukielekea kwenye birthday ya Messen tulipata ajali mbaya sana na Shukuru tulitoka salama japo mimi nilibanwa mkono lakini nipo salama," ameeleza Amber Lulu.

Kwa sasa Amber Lulu anafanya vizuri na wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Vuruga.

Zari The Bosslady: Sio lazima kumnga’anga’nia mtu

0
0
Mrembo Zari The Bosslady amezidi kutoa ushauri kwa wale wanaomfutialia kwenye mitandao ya kijamii.

Zari kwa sasa ameshauri kuwa hakuna ulazima wa kuendelea kuwa na watu ambao wanaondoa furaha yake kwenye mitandao ya kijamii. 

Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika;

"Sio lazima kunga’anga’nia mtu anaesumbua na kuondoa amani yako katika mitandao ya kijamii na hata maisha kwa ujumla futilia mbali watu kama hao."-Zari

Zari The Bosslady ambaye anaishi Afrika Kusini na familia yake ni miongoni mwa warembo wenye ushawishi mkubwa kwenye mitandao ya kijamii akiwa na followers zaidi ya Milioni 4 kwenye ukurasa wake Instagram.

Video Mpya ya Nandy - AIBU

0
0
Msanii wa muziki Bongo, Nandy anakukariisha kutazame video ya wimbo wake mpya uitwao Aibu. Itazame hapa.

Zitto Kabwe Aitupia Lawama Serikali Kushuka Kwa Bei Ya Korosho Mwaka Huu

0
0
Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema Serikali haipaswi kukwepa lawama kwenye suala la uuzaji wa korosho na ikubali kuwa imefanya makosa.

Zitto ametoa kauli hiyo leo Oktoba 28, 2018  zikiwa ni siku chache baada ya Serikali kusitisha minada ya zao hilo mpaka Oktoba 30 itakapotoa maelekezo mapya baada ya wakulima kugoma kuuza korosho zao kutokana na bei ndogo waliyotaka wanunuzi.

"Badala ya Serikali kulichukulia zao la korosho kama la kimkakati imekuwa haisikii, haielewi, na sasa imeharibu kuku anayetaga mayai ya dhahabu katika nchi yetu," amesema.

Amesema korosho ndio zao pekee la kuiokoa nchi kwamba Serikali ilieleza kuwa imepata wanunuzi wa korosho kutoka Marekani watakaonunua kilo moja kwa Sh5,000 jambo ambalo si kweli.

Pamoja na ahadi hiyo ya Serikali, Zitto amesema kufuatia taarifa alizonazo kutoka Bodi ya Korosho Tanzania (CBT) na wanunuzi, uzalishaji wa zao hilo utashuka kwa asilimia 40.

"Mnaweza kuona fedha za kigeni tunazoenda kupoteza kwa uamuzi wa Serikali kuchukua fedha zote za export levy (ushuru wa forodha) badala ya kupeleka zinakostahili," amesema Zitto.

Kuhusu kushuka kwa uzalishaji na bei, amesema kutaathiri  mapato ya wakulima na Serikali pia.

Msimu wa mwaka jana, wakulima waliuza kilo moja kwa Sh4,000 hivyo kuiwezesha Serikali kuingiza Dola 209 milioni za Marekani.

Minada mitatu ya kwanza iliyoandaliwa na Chama cha Ushirika Tandahimba na Newala (Tanecu), Masasi na Mtwara (Mamcu) na Ruangwa, Nachingwea na Liwale (Runali) haikufanikisha mauzo ya tani 5,100 kutokana na kushuka kwa bei.

Bei kubwa zaidi kwa kilo moja kwenye mnada wa Tanecu uliohudhuriwa na kampuni 15 ilikuwa Sh2,717 na Sh2,520 kwa Mamcu kulikokuwa na kampuni nane wakati ni kampuni tano pekee zilijitokeza mnada wa Runali ambako bei ilikuwa Sh2,657.
 
Kutokana na mwenendo usioridhisha wa mauzo ya korosho mwaka huu, wiki iliyopita, Rais John Magufuli aliagiza kuondolewa kwa kaimu mkurugenzi wa CBT, Profesa Wakuru Magigi.

Waziri Mwijage: Reli ya kisasa ya (SGR) haitaathiri biashara ya kusafirisha mizigo

0
0
Waziri  wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, amesema reli ya kisasa ya (SGR) haiwezi kuathiri biashara ya usafirishaji wa mizigo kwa njia ya barabara na amewataka wamiliki wa malori kutokuwa na hofu.

Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam jana wakati akifungua mkutano wa Chama cha Wasafirisaji (TAT).

Alisema Serikali inatambua mchango mkubwa wa wasafirishaji nchini kwa kuwa wanachangia kwa kiasi kikubwa kuingizia mapato, hasa ya kigeni.

“Tutajenga reli ya standard gauge lakini malori bado yanaendelea kuhitajika, Uingereza na Marekani yapo licha ya nchi hizo zina reli za kisasa,” alisema.

Mwijage alisema sekta ya barabara inachangamsha uchumi wa nchi na inaajiri watu wengi kupitia nyanja mbalimbali.

Alisema mwelekeo wa Serikali ni kujenga viwanda vya kati na vikubwa ili kuchochea maendeleo ya nchi.

“Serikali imepokea na itaendelea kuzifanyia kazi changamoto zilizopo katika sekta ya usafirishaji nchini,” alisema.

Awali, Rais wa TAT, Zacharia Hanspope, alisema sekta ya usafirishaji inakumbwa na changamoto mbalimbali zikiwamo vizuizi vingi visivyo vya kodi na visivyo vya lazima katika baadhi ya barabara wanazotumia.

Alitaja changamoto nyingine ni kuwapo kwa sheria na kanuni mbalimbali za vyombo vya Serikali zinazokinzana kwa kutoa maelekezo yanayotofautiana.

Alisema changamoto nyingine ni utaratibu unaotaka wasafirishaji kutembea na risiti za malipo za kieletroniki (EFDs) katika magari yaliyobeba mizigo wakati wahusika bado hawajalipa.

Pia alisema wasafirishaji hawaridhishwi na utaratibu uliowekwa wa kuadhibu wamiliki wa magari ya kusafirisha mizigo kwa makosa yaliyofanywa na madereva.

“Ni matumaini yetu kuwa Serikali itazingatia changamoto hizi kwa undani na kuangalia namna ya kuzitatua ili tuweze kufanya biashara vizuri na kwa ufanisi zaidi jambo litakalotufanya kuchangia kwa ukamilifu juhudi za Serikali za kukuza uchumi,” alisema Hanspope.

Katika mkutano huo, wajumbe walipokea taarifa za utendaji wa chama hicho kwa mwaka mzima. Pia wamefanya uchaguzi wa viongozi wa juu baada ya waliokuwapo kumaliza muda wao.

Ofisa Mtendaji, Ofisa Tarafa Kortini Kwa Rushwa Ya Sh. Milioni Moja

0
0
Taasisi  ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Morogoro imewafikisha Ofisa Tarafa ya Kimamba, Ayubu Mvurungu na Ofisa Mtendaji wa Kata ya Rudewa, Thomas Mbwilo, katika Mahakama ya Kilosa kwa kosa la kupokea rushwa ya Sh milioni moja.

Taarifa hiyo ilitolewa mjini hapa juzi na Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Morogoro, Janeth Machulya.

Alisema watuhumiwa hao walifunguliwa kesi ya jinai namba 365/2018 mbele ya Hakimu Timoth Lyon na kusomewa shtaka la kupokea rushwa chini ya kifungu namba 15 (1) (a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007.

Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Sarah Martin, alidai mahakamani hapo kuwa Septemba 26, mwaka huu washtakiwa hao walipokea fedha hiyo ili waandae muhtasari   utakaoonesha kwamba hati ya kimila namba 19 KLS/2238 ya umiliki wa shamba la mlalamikaji ilitolewa baada ya mkutano wa Halmashauri ya Kijiji cha Rudewa Mbuyuni kuridhia.

Washtakiwa hao walipokea fedha hizo huku wakijua wanachofanya ni kinyume na maadili yao ya kazi.

Hata hivyo, washtakiwa walikana mashtaka hayo na wapo nje kwa dhamana ya Sh milioni moja na kesi hiyo itatajwa tena Novemba 9, mwaka huu.

Muuza gongo kortini kwa kumhonga polisi

0
0
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Arusha, imempandisha kizimbani mkazi wa Kijiji cha Kikatiti, Warieli Mungure, anayeuza pombe haramu aina ya gongo kwa tuhuma za kutaka kumhonga Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Kikatiti, Marco Magere.

Katika shauri hilo namba 318 la mwaka huu lililopo Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha, mtuhumiwa huyo alisomewa shtaka la kutoa hongo ya Sh 100,000 kwa Marco ili asimchukulie hatua za kisheria baada ya kuhusishwa na vitendo hivyo vya uuzaji pombe hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Arusha, Frida Wikesi, mtuhumiwa huyo alifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Gwanta Mwankuga, Oktoba 10, mwaka huu.

“Mtuhumiwa alikana kutenda kosa hilo ambalo ni kinyume na kifungu cha 15(1) (b) na (2) cha sheria namba 11 ya mwaka 2007 ya kuzuia na kupambana na rushwa,” alidai.

Pia alisema walipata taarifa kutoka kwa Marco kuwa Mungure alimuahidi kuwa atakuwa akimpatia fedha hizo kila mwezi ili asifuatiliwe katika biashara yake.

Alisema baada ya kupata taarifa hiyo, walianzisha uchunguzi wa awali na baada ya kuthibitisha tuhuma waliandaa mtego Oktoba 9, mwaka huu uliofanikisha kumkamata Mungure katika eneo la Enspall Lodge, Kikatiti.

“Takukuru inawataka viongozi na watu wengine kuiga mfano wa Marco ambaye hakuwa tayari kuhongwa kwa sababu ni watu wachache wenye tabia hiyo ya kizalendo na tunawahakikishia taarifa zinazopokelewa zitafanyiwa kazi kwa haraka,” alisema.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 8, mwaka huu itakapotajwa tena na mtuhumiwa huyo yuko nje kwa dhamana.

Kangi Lugola asema serikali bado inawasaka waliomteka Mo Dewji

0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema Serikali inaendelea kuwatafuta watu waliomteka mfanyabiashara Mohammed Dewji ‘Mo’.

Mfanyabiashara huyo alitekwa Oktoba 11 mwaka huu katika Hoteli ya Colessium iliyopo Masaki jijini Dar es salaam na kupatikana Oktoba 20 mwaka huu kwenye viwanja vya Gymkhana Jijini humo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa, Dodoma leo Jumapili Oktoba 28, Waziri Lugola, amesema bado msako unaendelea kuwatafuta wale wote waliomteka mfanyabiashara huyo.

“Niendelee kuwasihi ndugu zangu, mmekuwa mkitaka sana kujua tunaendeleaje kuwatafuta watekaji wa Mo, mimi nimeendelea kuwaambia kwamba Jeshi la Polisi linashughulika na matukio yote ambayo yametokea na kama kuna matukio yametokea ya mtu kupotea haonekani wote hao kwa ujumla wao tutayashughulikia.

“Wale ambao hatujawapata bado Jeshi la Polisi tunaendelea kuwatafuta hadi yule wa mwisho atakapotiwa mbaroni kwa hiyo ninyi msidhani kwamba hatuwatafuti kila mkiuliza mnaulizia Mo tu tunaomba muwe waangalifu,” amesema.

Kugola pia amesema hatua hiyo italeta dhana kwamba watu wa kawaida wanapopata matatizo hawana thamani au pengine serikali haiwatafuti wale waliofanya uhalifu, na kuongeza kuwa kama Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi hawezi kuacha hilo likaendelea.

Habari Njema: Tunatibu Busha, Korodani Kuvimba,Ngiri, Miguu Kufa Ganzi Pamoja na Matatizo ya Nguvu za Kiume

0
0
Ni dawa pekee iliyotibu watu wengi nchini na nje ya nchini kwa kufanya kazi Mara 3 kwa wakati mmoja 1 ...kurefusha uume na kunenepesha saizi upendayo, kuogeza nguvu za kiume na inatibu matatizo , ikisha tibu aina madhara inaimalisha mishipa ilio regea na uzalishaji wa mbegu za kiume. TAHADHARI HAKIKISHA UNA MKE AU    MPENZI. 

NINI HUCHANGIA MATAZO HAYA . Ngiri ni chanzo Kikubwa cha matatizo,haya kujua kwamba una ngiri dalili zake ni 1.kufika haraka kileleni wakati  watendo la ndoa 
2.Kushindwa kulundia tendo la ndoa 
3.Kutoa choo kama cha mbuzi 
4. Tumbo kujaa gesi na kuunguruma 
5 kukosa choo kabisa 
6 Maumbile kuingia ndani na kuwa mafupi 
7 korondani moja kuvimba 
8 kutosikia hamu ya tendo la ndoa
 9 maumivu ya kiuno na mgongo  

Pia tunatibu busha bila kufanyiwa opresheni .Umeachwa na umpendae na bado unamwitaji?

WASILIANA  NA MTALAM  CHALLO 0714 006521. YUPO MBAGALA.

Tromex Power : Dawa Bora Na Imara Ya Nguvu Za Kiume

0
0
TROMEX POWER DAWA BORA NA IMARA ya   NGUVU ZA KIUME; Baada ya kufanyiwa utafiti na majaribio sasa imeingia sokoni 

Habari njema kwa tanzania pamoja na africa nzima mkombozi wa ndoa yako ni dawa anbayoitwa TROMEX. 

Dawa hii imeonyesha uwezo wa hali ya juu katka kutibu tatizo la upungufu wa nguvu za kiume ,dawa hii ni mpya na inapatikana katika clinic yetu 

Dawa hii ni dawa ya asilia ya mitishamba,mwaka juzi tuliipeleka nchini Ghana kwa ajili ya utafiti  katika utafiti ilishindanishwa na dawa zingine 4 kutoka nchi kenya, Uganda, msumbiji, pamoja na kongo, na imeonyesha asilimia 92 imeonyesha inauwezo mkubwa wa kutibu tatizo kwa mda mfupi sana 

Katika utafiti huo watu 1839 ambao walikuwa legelege walipewa dawa hii kwa ajili ya majaribio,baada ya kuitumia watu 1792 walipona kabisa na sasa wanaweza kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara 3 kwa wakati mmoja na watu 38 hawakupona kabisa pia watu 9 hawakurudi kuleta majibu 

Dawa hii ukiitumia itakufanya uwe na uwezo wa kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara 3 bila hamu kuisha

Dalili za upungufu wa nguvu za kiume ni kushindwa kurudia tendo la ndoa...Kutojisikia hamu ya tendo la ndoa....Korodani moja kuvimba,tumbo kuunguluma na kujaa gesi, pia inazalisha homons za uzazi kwa mwanaume ambaye mbegu zake za uzazi ni nyepesi ambazo hazina virutubisho vya kuweza kumzalisha mwanamke 

Pia inauwezo wa kufanya maumbile yawe marefu kama yameingia ndani na kuwa mafupi sana, pia inatibu magonjwa zaidi ya 6 

Itumie sasa dawa hii inapatikana katika Clinic yetu iliyopo Kawe DAR mikoani tunatuma kwa njia ya mabasi 

Ukiwa nje ya nchi tunatuma kwa njia ya EMS ..maelezo zaidi 0756726865/ 0716096205 au tembelea    www.kihembehebalist.blogspot.com

Rais Dkt. Magufuli Akutana Na Kuzungumza Na Wanunuzi Wa Korosho Jijini Dar Es Salaam Na Kutoa Msimamo Wa Serikali Kuhusu Bei Ya Korosho

0
0
Rais John Magufuli ametoa msimamo wa Serikali kuwa bei ya korosho isipungue Sh3000 kwa kilo moja.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Jumapili Oktoba 28, 2018 alipokutana na wadau na wanunuzi wa korosho katika kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.


Hayo yamejiri baada ya wakulima wa zao hilo katika mikoa ya Lindi na Mtwara kuingia kwenye mgomo wa kuuza zao hilo la Korosho kwa kile walichokidai kushuka kwa bei ya zao hilo ukilinganisha na miaka miwili iliyopita huku gharama za uzalishaji zikiwa zimepanda.

Kufuatia mgomo wa minada ya siku mbili, Oktoba 26, Rais Magufuli, alimuagiza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuwaeleza kuwa anaunga mkono hatua ya maamuzi hayo ya wakulima na kusema yuko nao bega kwa bega.

Miongoni mwa viongozi walioshiriki katika kikao hicho ni pamoja na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Waziri wa Kilimo, Dkt. Charles Tizeba na watendaji wengine wa serikali.


"Nawataka wafanyabiashara muelewe kuwa, hakuna korosho itakayouzwa chini ya shilingi 3,000. Kama hamtanunua, mniambie.

"Serikali tunaunga mkono wakulima kukataa bei za korosho. Ndio maana kiongozi wa Bodi ya Korosho alipowatisha wakulima kuwa lazima wakubali, tumemuondoa, na hatorudi huko."Amesema Rais Magufuli


Chegeni, Lawrence Masha Na Vijana Wengine 10 Watiwa Mbaroni Jijini Mbeya

0
0
Jeshi la Polisi mkoani Mbeya limethibitisha kuwakamata, kuwahoji na kuwaachia kwa dhamana mbunge wa Busega (CCM), Dk Raphael Chegeni na Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha kwa madai ya kuharibu mali za mwekezaji raia wa Ujerumani.
 

Kamanda wa Polisi wa mkoani humo, Ulrich Matei amesema wawili hao walikamatwa jana, kuhojiwa na kuachiwa kwa dhamana.

Amesema polisi walipata taarifa kutoka katika ubalozi wa Ujerumani kwamba kuna mabaunsa 20 wamevamia nyumba ya mwekezaji huyo mwenye mashamba ya parachichi.

“Masha na Chegeni walikuwa wanatimiza wajibu wao kwa mujibu wa Mahakama ya kumuondoa mwekezaji huyo katika eneo lile,” amesema Matei.

“Hata hivyo hawakufuata utaratibu ikiwemo kumpa taarifa mhusika na haikuwa siku ya kazi. Kama yule Chegeni ni mbunge angetumia utaratibu hata kupitia kwa mkuu wa mkoa kuliko kufanya kama vile.

Amebainisha kuwa walipopata taarifa kutoka ubalozi wa Ujerumani ziliwashtua kwa sababu Tanzania ni nchi ya amani.

Kwa mujibu wa Kamanda Matei, polisi walipofika eneo hilo walikuta baadhi ya vitu vimeharibiwa huku mwekezaji huyo ambaye ni mwanamke akijeruhiwa sehemu mbalimbali mwilini.

Lady Jaydee Afunguka Tetesi Za Kuachana Na Mpenzi Wake

0
0
Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambaye ni mkongwe kwenye game Lady Jaydee amefunguka juu ya tuhuma za kuachana na mpenzi wake Spice, ambaye ni msanii kutoka Nigeria Spice.

Akizungumza na kituo cha EATV  amesema kwamba hajaachana na Spice, isipokuwa wawili hao wanafanya kazi ambayo inawalazimu kuwa mbali mbali kwa muda mrefu, ikichangiwa na kuwa raia wa nchi mbili tofauti.

Jaydee ameendelea kwa kusema kwamba licha ya Spice kuwa mbali, amechangia kwa kiasi kikubwa kuweza kufanikisha tamasha la #VocalsNight2018, kwa kuweza kumuunganisha na UTI ambaye  alikuwa MC wa siku ile.

“Unajua sisi ni wanamuziki, na wanamuziki ni watu wa kusafiri, na hatuishi nchi moja, kwa hiyo yeye yuko kwenye kazi zake na mimi nipo kwenye kazi zangu, ni sawa na mume na mke, mume anaenda kazini na mke anaenda kazini kwake, haimaanishi kila siku muwe mnafuatana, leo hayuko hapa lakini ni mtu ambaye nashirikiana naye kwenye mambo mengi, kama kunisaidia kumpata UTI na kuhakikisha amefika hapa Tanzania”, amesema Lady Jaydee.

Hivi karibuni kulikuwa na tetesi za wawili hao kuachana baada ya kuwepo ukimya kati yao na kutoonakana pamoja kwa muda mrefu.

Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 20

0
0
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA  
         
“Nchi ya kuwa nazo makini sana hapo ni Uingereza na Italy, tukifanya makosa hatuto songa mbele na wezetu wamejiandaa kisawa sawa, kwani wachezaji wao wana vipaji na wana uwezo mkubwa. Ethan wewe ni jicho langu, Frenando wewe ni kifua changu na mulio salia nyinyi ni mikono yangu. Nawaomba musiniangushe, nawaomba mufanye kile munacho paswa kufanya kwa miaka yote ya nyuma kwenye mashindano mengine. Haya ni mashindano mapya kabisa kwa timu za sekondari, hapa ndipo kwa kujiuza nyinyi wewenyewe kwani mameneja na makocha kutoka timu kubwa duniani watakuwa wakifwatilia mashindano hayo ambayo yatarushwa moja kwa moja kwenye televishion. Tulinde heshima ya nchi, na heshima na shule pia. Kwa pamoja tutakiwa kishinda sawa”
 
Wachezaji wote tukamuitikia kocha wetu kwani amezungumza maneno hayo hadi machozi yanamwagika usoni mwake, ikiashiria kwamba ana uchu na hamu sana ya kutuona vijana wake tunashinda na kuwa timu bora katika bara zima la Ulaya.

ENDELEA               
Siku iliyo fwata tukaingia kambini rasmi huku kila mmoja akiwa amesha jiandaa vizuri kwa ajili ya mashindano haya.
“Frenando hembu fanya mpango wa kupata simu ni wasiliane na Camil”
“Poa kaka, ila namba yake unayo?”
“Nitawapigia shuleni kwao, ili waweze kunipatia namba wanayo itumia nchini huko”
 
“Ingekuwa vizuri ukatumia hiyo simu ya chumbani kwetu kuwasiliana nao?”
“Hizi si zimeunganishwa na hapa hapa hotelini, au zinaweza kutoka nje ya hii hoteli?”
“Sijajua ila ngoja tujaribishe tuone itakavyo”
Frenando, akaingiza namba ya mama yake iliyopo nchini Mexco kwenye simu hii, akaisikilizia kwa muda kisha akatingisha akimaanisha kwamba hii simu haina uwezo wa kutoa simu nje ya hoteli hii.
“Badae tutoroke tuende tukatafute simu mjini”
“Hapana hakuna haja ya kutoroka, tumuombe kocha ruhusa kisha tutoke”
“Tatizo lako Ethan wewe ni muoga”
“Sio uwoga Frenando”
“Ila?”
 
“Sura yangu kila sehemu inajulikana, umaarufu muda mwengine ni shida”
“Mmmm, ngoja nina mpango”
“Mpango gani?”
“Nina kuja”
Frenando akatoka chumbani humu na kuniacha mimi peke yangu.
‘Mutakwenda kushinda michezo yote ila fainali sijajua’
Niliisikia sauti ya Ethan mwenzangu huku akiwa amekaa kwenye moja ya sofa humu ndani, nikanyanyuka kitandani na kukaa sofa la mbele yake huku tukitazamana.
“Ina maana fainiali hatushindi?”   
“Sijajua kwa maana timu ambazo mutaingia fainali zote ni ngumu na kuna hati hati ya nyinyi kuto shinda”
Nikakaa kimya kwa muda huku nikimtazama Ethan kwa maana ni jini ambaye ana nitabiria vitu vingi sana vya mbeleni.
 
“Tuachane na maswala ya mpira, vipi mpenzi wangu Camila yupo sehemu salama?”
“Ndio, ukizungumza naye leo usiku hakikisha kwamba unamsisitizia haendi nchini Somali”
“Kwa nini?”
“Somali sio nchi salama kwa wao kwenda, kuna matukio ya kila aina ambayo yanaweza kumkuta. Ukiachilia mbali na matatizo hayo, baba yake anagombania kiti cha uraisi, zinaweza kutumiwa njama za kutekwa kwake, kisha baba yake akashinikizwa kuendelea kugombania uraisi na kama unavyo jua siasa za hapa Ujerumani, watu wana misimamo na niwaelewa wa mambo. Mzuie mpenzi wako kwenda huko na hata ikiwezekana apande ndege mara tu ya kumaliza ziara yao nchi Tanzania.”
Nikashusha pumzi taraibu huku nikimtazama Ethan usoni mwake.
“Naamini huto hitaji kukiona kifo cha mpenzi wako, fanya hivyo nilivyo kuambia”
“Nimekuelewa na ninashukuru sana Ethan”
“Karibu”
“Asante”
“Rafiki yako ana kuja ngoja niondoke”
Ethan akapotea kwenye uepo wa macho yangu. Frenando akaingia huku akiwa ameshika mfuko mweusi.
 
“Ume beba nini?”
“Haya ni makofia ambayo tutavaa tukitoroka”
“Frenando akili yako ipo wapi rafiki yangu. Ninacho taka mimi ni simu na sio makofia”
Nilizungumza kwa kufoka kidogo hadi Frenando mwenyewe akanishangaa kwa maana katika kipindi chote cha urafiki wetu hakunishuhudia siku hata moja nikiwa nimekasirika.
“Ethan kuna jambo lolote baya nililo kufanyia”
“Samahani rafiki yangu. Akili yangu haipo sawa nina hisia mbaya kuhusiana na Camila”
“Hisia mbaya? Hisia gani?”
“Wana ziara ya kwenda nchi Somali wakitoka nchini Tanzania hivyo nahitaji asiende Somali”
“Somali si ndio kule kwenye kundi la Al-Shubabu sijui Al-Shabibi?”
 
“Ndio huko huko”
“Mmmmm hili swala ni muhimu Ethan, sio la kimapenzi tena ni kweli unatakiwa kumzuia kwenda”
“Ndio hivyo nahitaji simu”
“Twende tukamuombe kocha simu yake, kwa maana sisi si wametuzia kuwa na simu”
Nikamtazama Frenando usoni mwake kwa muda kidogo kisha nikaanza kutembea kuelekea nje, akanifwata kwa nyuma na tukaingia kwenye chumba cha kocha bila hata ya kubisha hodi. Tukamkuta kocha akifanya mapenzi na mmoja wa wahudumu wa hoteli hii ambaye alitopokea kwa bashasha sana.
“Ohoo Mungu. Ethan ndio nini hicho”
Kocha alizunguzma huku akijifunika shuka na muhudumu huyo.
 
“Waoooo!!”
Frenando alizungumza huku akijawa na tabasamu pana usoni mwake.
“Simu”
Nilizungumza kwa ufupi tu huku nikimtazma kocha usoni mwake.
“Nini?”
“Nataka simu yako”
Nilimfokea kocha kana kwamba ni kijana mwenzangu. Kocha kwa ishara akanionyesha simu yake ilipo ni ndani ya koti la suti yake aliyo kuwa ameivaa. Nikaingiza kiganja kwenye mfuko wa kushoto, ila sikuikuta, ila katika mfuko wa upande wa kulai nikaikuta. Nikaitoa simu hiyo aina ya Samsung S8.
“Mke wako anapiga”
 
Nilimuambia kocha huku nikimtazama usoni mwake, kwani ni kweli mke wake anapiga simu na ameizima mlio wake ili isisikike pale anapo pigiwa. Kocha akabaki akiwa amenitumbulia macho huku akiwa amejawa na wasiwasi mwingi sana. Nikaipoke simu hiyo na kuiweka sikioni mwake.
“Ndio mama Philipes”
“Nani mwenzangu”
“Ethan mmoja wa wachezaji wa mume wako”
“Ethan Klopp?”
“Ndio”
“Ohoo nafurahi kusikia hivyo mwanangu habari yako”
“Salama tu mama Philipes”
 
Nilizungumza huku nikiwa nimekazia macho kocha pamoja na muhudumu huyu wa hoteli huko wote wakiwa wamekaa kimya huku miili ikiwatetemeka.
“Yupo wapi kocha wako?”
“Nimetoka na simu yake mara moja na nipo mjini nikirudi nitakufahamisha uzungumze naye”
“Ohoo sawa sawa Ethan, ninafurahi kuzungumza nawe”
“Hata mimi mama nina furahi kuzungumza nawe”
“Sawa nikutakie mchana mwenma”
“Nawe pia”
Nikakata simu na kumtazama kocha na nikamuona jinsia navyo shusha pumzi nyingi. Sikumsemesha kitu chochote zaidi ya kutoka chumbani humu na kurudi chumbani kwetu.
“Ethan umemuachia mzee wa watu hali mbaya”
“Kwa nini?”
 
“Si tazama jinsi vile alivyo pata wasiwasi mwingi jamani.”
“Hahaaa…..umalaya unamsumbua na anatusisitiza sisi tusiwe na wapenzi sijui anatuona sisi sio watu”
“Anatamatatizo”
Nikaingiza namba ya shuleni kwa kina Camila, nikaipiga simu hiyo. Ikaanza kuita na baada ya sekunde kadhaa ikapolewa.
“St Lilian High school. Mery ninazungumza nani mwenzangu”
“Unazungumza na Ethan Klopp”
“Ohoo habari yako”
“Salama, ninaweza kupata mawasiliano ya mpenzi wangu kwa nchi waliyo kwenda?”
“Tanzania?”
“Ndio”
 
“Sawa ngoja nikutumie kwa njia ya meseji”
“Nashukuru sana, je wamefika salama?”
“Ndio wamefika salama”
“Naomba msaada wako Mery”
“Usijali  Ethan”
Nikakata simu kwani sio mara yangu ya kwanza kuzungumza na sekretari wa shule hii. Haikuisha hata dakika moja meseji ikaingia ikiwa na maelezo ya namba ambayo inatumiwa na uongozi walio ongozana nao kwenye safari hiyo nchini Tanzania.
“Duu kumbe nchi ya Tanzania code namba yake ni +225”
Nilizunugmza huku nikimuonyesha Frenando namba hiyo
“Wemechelewa sana kupata huduma za simu”
“Yaaa”
Nikaingiza namba hiyo, ila nikapewa taarifa kwamba simu hii haina salio la kutosha, niongeze tena kisha nipige tena.
“Kocha mzima hana salio kwenye simu yake”
 
“Mmmm sasa tunafanyeje?”
“Inabidi tutoke tukanunue”
“Umeona sasa”
Frenando akanikabidhi moja ya kofia aliyo nunua. Tukatoka chumbani kwetu na kufunga mlango wetu na kuondoka. Tukaanza kuzunguka mitaani huku ni baadhi ya watu wachache sana ambao waliweza kutugundua na wengine walituomba waweze kupiga picha nasi. Tukaingia kwenye moja ya duka la kununu simu, nikatia kadi yangu ya malipo ambayo ina kiasi cha kutosha na sehemu yoyote katika nchi hii ya Ujerumani, nina weza kuitumia kununua kitu cha ina yoyote ile na katika duka lolote.
 
“Tununue simu zetu na tumrudishie yule mwehu simu yake”
Nilizungumza huku tukizunguka katika duka hili ambalo simu zote zilizomo humu ndani ni simu za garama sana. Kila mtu akanunua simu yake, tukasajiliwa laini zetu kama kanunu na taratibu za nchi hii. Tulipo maliza maunuzi yetu tukaingia kwenye moja ya mgahawa, tukanunua vyakula na vinywaji kisha tukarudi hotelini.
“Shika mrudishie simu yake”
Frenando akachukua simu ya kocha na kumpelekea chumbani kwake, nikaipiga namba niliyo kabidhiwa na sekretari. Namba hiyo ikaanza kuita na baada ya muda kidogo ikapokelewa.
 
“Habari yako?”
“Salama, ninaitwa Ethan Klopp ninahitaji kuzungumza na Camila Marco”
“Ohoo hivi sasa ni usiku sana, labda kukipambazuka atakutafuta”
“Sawa sawa mwalimu, ila ana endeleaje?”
“Anaendelea vizuri tu ni jambo la kumshukuru Mungu kwa kweli”
“Asante basi kukipambazuka utanifahamisha”
“Sawa Ethan”
Nikakata simu huku nikiwa na faraja kuba sana moyoni mwangu, kwani mwalimu huyo aliye pokea simu ni mlenzi wao kwa upande wa wanawake.
 
“Vipi umesha zungumza naye?”
Frenando alizungumza huku akiingia ndani ya chumba hichi
“Ndio ila kule ni usiku amepokea matron wao”
“Ahaa, hivi sasa na huko masaa huwa yana pishana sana ehee?”
“Ndio ila sijajua yanapishana kwa masaa mangapi mangapi”
Tukapata chakula cha mchana. Jioni tukaelekea katika viwanja vya karibu kabisa na hoteli hii kwa ajili ya mazoezi ya hapa na pale.
“Ethan na Frenando nina waomba”
Kocha alituita mara baada ya kumaliza mazoezi, tukasimama mbali kidogo na basi letu la timu.
“Naamini mumeona kilicho tokea mule chumbani”
“Ndio”
“Ninawaomba iwe siri yenu. Ninaomba musiweze kuitoa siri hiyo kwa mtu yoyote”
Kocha alizungumza kwa msisitizo huku akitutazama kwenye nyuso zetu.
 
“Mke wako ana kasoro gani?”
Nilimuuliza kocha kwa upole sana huku nikimtazama usoni mwake.
“Ethan”
“Usiseme Ethan kocha. Tambua nimebeba dhambi kubwa sana ya kumdanganya mke wako. Je dhambi hiyo mimi nina ilipaje eheee?”
“Ethan natambua nyinyi bado ni wadogo, ila muikingia kwenye ndoa mutaweza kujua ni nini kinacho tokea hadi wanaume tunaamua kuwa na wake wa nje”
“Wacha weeee”
Frenando alizungumza kwa kejeli huku akimtazama kocha usoni mwake. Gafla simu yangu ikaanza kuita ikiwa ndani ya kibegi changu mgongoni. Kocha akatoka na macho ya hasira kwani moja ya sheria tukiwa kambini ama shuleni haturuhusiwi kuwa na simu.
“Ethan kwa nini una simu?”
Kocha aliniulza kwa kunifoke sana.
“Acha upuuzi wewe mzee. Muache apokee simu la sivyo tunakwenda kuzungumza uchafu wote kwa mke wako na ushahidi wapicha ninao”
Frenando alizungumza kwa kujiamini na kumfanya kocha kukodolea macho na kukosa jambo la kuzungumza kwa muda huu.

==>>ITAENDELEA KESHO

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu Ya October 29


Israel yatishia kuipiga Iran, yadai ni Kisasi cha Kushambuliwa Ijumaa

0
0
Israel imesema kuwa Iran inahusika na mashumbulizi ya makombora yaliyorushwa kwenye ardhi yake kutoka ukanda wa Gaza mwishoni mwa wiki.

Akizungumza jana kuhusu mashambulizi hayo yaliyoshuhudiwa tangu Ijumaa, msemaji wa jeshi la Israel, Luteni Kanali Jonathan Conricus alidai kuwa yamefanywa na makundi yenye msimamo mkali kwa maelekezo na kusaidiwa na Iran.

Jeshi hilo limeeleza kuwa makombora 30 yalirushwa kwenye ardhi ya Israel na kwamba mfumo wao wa kijeshi ulifanikiwa kuzuia ziadi ya makombora 12.

Alisema kuwa makundi mawili yenye itikadi kali yanayosaidiwa kifedha na Iran, yalitekeleza mashambulizi hayo yakisaidiwa pia moja kwa moja na jeshi la Iran ambalo lina vikosi nchini Syria.

Aidha, Israel imetishia kuishambulia kijeshi Iran kwa kupiga vikosi vyake vilivyoko nchini Syria kama sehemu ya hatua za kulipa kisasi.

“Usiku wa jana tulipeleka ujumbe huu kwa pande husika, na ninasisitiza kuwa majibu yetu hayatakuwa na mipaka ya kijografia,” alisema Conricus.

Kwa mujibu wa CNN, mashambulizi ya Ijumaa yalianza kushuhudiwa majira ya jioni na kusababisha muonekano mwekundu kwenye eneo la ukanda wa Gaza.

Jeshi la Israel limeeleza kuwa kwa majibu ya awali, ndege zake za kivita zilishambulia takribani maeneo 100 ya adui zao ikilenga maeneo ya kutengenezea silaha pamoja na vifaa vya kijeshi vinavyomilikiwa na makundi yenye itikadi kali pamoja na jeshi la Hamas ambalo linaidhibiti Gaza.

Video Mpya: Sultan Wa Pwani - NIMEJIGONGA

0
0
Video Mpya: Sultan Wa Pwani - NIMEJIGONGA 

Itazame hapa.

Diamond na Rayvanny wafunga mitaa Posta Dar es Salaam

0
0
Wasanii kutokea WCB, Rayvanny na Diamond Platnumz  jana Jumapili October 28, walifunga baadhi ya mitaa Posta Dar es Salaam kutokana na utengenezaji wa video ya wimbo wao mpya.

Tukio hilo lilivuta umati mkubwa wa watu licha ya jana kutokuwa ni siku ya kazi kitu kilichopelekea baadhi ya shughuli kusimama kwa muda.

Bila shaka wimbo huo utakuwa wa tatu kwa Diamond Platnumz kumshirikisha Rayvanny baada ya nyimbo kama Salome na Iyena.

Waziri Mwijage: Serikali Inaendelea Kujenga Uchumi Imara Na Shindani

0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu
Waziri wa viwanda,biashara na uwekezaji Mhe. Charles Mwijage amesema serikali  inaendelea kujenga uchumi wa Kitaifa(jumuishi) ulio imara na wenye ushindani  kuelekea uchumi wa kati ifikapo 2025  kwa kuanzia uzalishaji mashambani hadi sokoni.

Hayo ameyasema wakati akihitimisha Maonesho ya (SIDO) Kitaifa yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu, yakiwa na Kauli Mbiu: “PAMOJA TUJENGE VIWANDA KUFIKIA UCHUMI WA KATI”

Mhe. Mwijage amezitaja baadhi ya sifa za uchumi wa Kitaifa (Jumuishi) kuwa ni pamoja na Kipato cha wastani kwa Mtanzania kufikia dola 3000 kwa mwaka ifikapo mwaka 2025, Watanzania kuwa na maisha mazuri, watu kuwa na elimu na wepewi kwa kujifunza, pamoja na kuwa na uchumi imara ulio shindani.

“Tunataka mwaka 2025 tuwe na uchumi imara na shindani lakini tuendelee kudumisha amani na msihikamano; njia rahisi ya kufikia mahali mbapo kipato cha wastani cha Mtanzania kuwa dola 3000 kwa mwaka ni kupitia uchumi wa viwanda na uchumi wa viwanda ni zaidi ya viwanda, uchumi wa viwanda unaanzia shambani hadi sokoni” alisema.

Katika hatua nyingine alitoa wito kwa Watanzania kulinda viwanda vya ndani hapa nchini kwa kununua bidhaa zinazozalishwa hapa nchini.

Mkuu wa Mkoa wa Mhe. Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema  Mapinduzi ya viwanda yanatokana na Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO), hivyo ni vema  wizara ya viwanda ,biashara na uwekezaji ikaliwezesha shirika la kuhudumia  viwanda vidogo ili kutekeleza azma ya Tanzania ya viwanda.

Akizungumzia maonesho ya Viwanda vidogo Mkurugenzi Mkuu wa SIDO Prof. Silvester Mpanduji, amesema jumla ya wajasiriamali 515 kutoka mikoa 23 nchini na nchi jirani za Uganda na Burundi, wameshiriki manesho haya na kupata fursa ya kuonesha bidhaa wanazozalisha na kubadilisha uzoefu katika masuala mbalimbali.

Aidha, amesema kupitia maonesho hayo mashine za kuongeza thamani katika mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi na misitu zenye thamani ya zaidi ya shilingi 800 zimenunuliwa na nyingine kuwekewa ahadi ya kununuliwa.

Naye Mkurugenzi Msaidizi wa UNDP anayeshughulikia miradi Amoni Manyama ameahidi kuwa Shirika hilo liko tayari kushirikiana na Serikali hapa nchini katika Ujenzi wa Uchumi wa Viwanda kwa kutoa msaada wa kifedha na utaalam wa kuchambua miradi ya viwanda katika Mkoa wa Simiyu na mikoa mingine pia.

Maonesho ya Viwanda Vidogo SIDO Kitaifa yaliyofanyika kwa muda wa siku sita katika Viwanja vya Nyakabindi Mkoani Simiyu yalifunguliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Oktoba 23, 2018, pamoja na wajasirimali 515 kushiriki takribani taasisi za Umma na Binafsi 24 zimeshiriki maonesho haya.

Waziri Lukuvi Alitaka Shirika La Nyumba Nhc Kuwa Mfano Katika Kusimamia Na Kutunza Nyumba Zake

0
0
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi amelitaka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuwa mfano katika, kuhifadhi, kutunza na kujenga nyumba bora za gharama nafuu kwa ajili ya kuziuza au kuzipangisha kwa wananchi wakiwemo watumishi wa umma.

Aidha, amelitaka shirika la NHC kuwa mfano kwa taasisi nyingine zinazojishughulisha na ujenzi  kwa kujenga nyumba bora na wakati huo kuwapangisha wananchi kwa malipo ya kodi ya  mwezi mmoja mmoja badala ya utaratibu uliozoeleka wa kupangisha kwa malipo ya kipindi cha miezi sita au mwaka mzima na kuepuka kutumia ‘vishoka’ wakati wa kupangisha nyumba zake.

Lukuvi aliyasema hayo jana alipolitembelea Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) katika mkoa wa Kilimanjaro wakati wa mwisho wa ziara yake ya kushughulikia migogoro ya ardhi katika wilaya za Hai, Moshi na Same mkoani Kilimanjaro.

Alisema, Shirika la Nyumba la nyumba NHC lazima liwe na mkakati mzuri wa ukarabati nyumba zake na kubainisha kuwa haiwezekani Shirika kubwa kama hilo kuwa na nyumba nyingi katika maeneo ya vitovu vya miji huku nyingi ya nyumba hizo zikiwa zimechoka na kusisitiza kuwa hataki kusikia NHC inakuwa na nyumba za aina hiyo.

Amelitaka Shirika kujipanga vizuri na kuhakikisha linashirikiana vizuri na ofisi za Mikoa na Halmashauri kwa lengo la kujenga nyumba za gharama nafuu kwa ajili ya watumishi na wakati huo kutangaza shughuli zake kwa kuwa NHC ina Kampuni yake ya ujenzi iliyosheheni wataalamu wa fani mbalimbali sambamba na kuwa na uwezo wa kujenga majengo mbalimbali kama vile Shule, Hospitali, Vituo vya Afya na Vyuo.

Aidha, Lukuvi amelitaka Shirika la NHC kuimarisha kitengo chake cha huduma kwa wateja na kujiwekea utaratibu wa kuwatembelea wapangaji wake kwa lengo la kufahamu changamoto zinazowakabili katika nyumba na kuzitafutia ufumbuzi changamoto hizo.

Kwa upande wake Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa mkoa wa Kilimanjaro Juma Kiaramba alimueleza Lukuvi kuwa Shirika la NHC katika mkoa huo liko kwenye mazungumzo na halmashauri ya Manispaa ya Moshi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba 25 za gharama nafuu na mradi huo utagharimu jumla ya shilingi bilioni 1.4 na utachukua miezi kumi na nane mpaka kukamilika.

Kwa mujibu wa Kiaramba, NHC mkoa wa Kilimanjaro pamoja na kufanya ukarabati wa majengo yake katika mkoa huo, kwa sasa Shirika iko kwenye  mazungumzo na taasisi mbalimbali mkoani humo ikiwemo halmashauri ya Same kwa ajili ya kujenga nyumba za gharama nafuu ingawa kumekuwa na chanagamoto kubwa ya uhaba wa ardhi katika maeneo kadhaa ya mkoa huo.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images