Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 102 na 103 )

0
0
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA  

“GAIDI AMBAYE TUNAMTAFUTA ANAJULIKANA KWA JINA LA DANY, PICHA ZAKE TUTAANZA KUZISAMBAZA MUDA MFUPI KUANZIA HIVI SASA KWENYE VYOMBO VYA HABARI. ILA NINACHO TAKA KUMUELEZA DANY, POPOTE ULIPO NAJUA BADO UPO TANGA NITAHAJIKISHA SAA SITA USIKU HAIFIKI NITAKUWA NIMEKUKAMATA NA SHERIA ITACHUKUA SHERIA YAKE.”
Maeno ya Babyanka yakanifanya nichukue rimoti ya Tv na kuizima, Cajoli akabaki akiwa amenitumbulia macho na kukosa cha kuzungumza.
   
ENDELEA   
Nikazima tv na kuirudisha rimoti juu ya meza. Nikaka kwenye sofa huku kichwa changu kikiwa kimejawa na mawazo mengi sana.
“Dany si wanaweza kuja hadi hapa?”   
“Sidhani, ila ninahitaji kuondoka hapa”
“Uondoke hapa!!?”
“Natambua utapata sana shida wakifahamu kwamba mimi nipo hapa”
“Dany no, siwezi kuruhusu hilo swala kuweza kutokea kwako, ni bora hata ufikiria mbinu nyingine ya kufanya ila si kuondoka hapa Dany”
“Cajoli ila hii unaona hii ni hatari kwenye maisha yako”
“Vyovyote Dany ila sitaki uondoke kwanguu”
Cajoli alizungumza huku akimwagikwa na machozi mfululizo. Nikakaa kimya huku nikiendelea kufikiria ni mbinu gani nyingine ambayo ninaweza kuifanya”
“Ok nimefikiria mbinu nyingine”
“Mbinu gani?”
“Nahitaji kukua”
“Kukua?”
“Ndio”
 
Nikanyanyuka kwenye sofa na kueleka katika chumba ambacho kina silaha ambazo tulizihifadhi.
“Dany ila maneno yako kusema kweli sijayaelewa”
“Najua kwa sasa hivi huto weza kuielewa”
“Naomba unifafanulie kwa maana mimi ndio mtu wako wa karibu ambaye unaweza kunieleza kila kitu kinacho kusumbua”
“Cajoli nimeishia kwa miaka minne sasa, nikiwa ninaonekana kwamba mimi ni gaidi, ila kusema la ukweli mimi sio gaidi, nilikuwa ni mpelelezi katika kikosi cha NSS”
“Imekuwaje ukaonekana wewe ni gaidi?”
 
“Ni mambomengi ambao yametokea, kwenye maisha yangu, nikianza kukusimulia ninaamini leo hii itaishia nikiwa ninakusimulia”
“Niambie kwa kifupi tu Dany, au huniamini?”
Nikamtazama Cajoli usoni mwake, taratibu nikaanza kumsimulia historia ya maisha yangu kwa ufupi. Kitu nilicho kiepuka ni kumsimulia kuhusiana na maswala ya mahusiano ambayo niliyapitia hapo nyuma.
“Kwa sasa sihitaji kuwa mtu mwema”   
Nilizungumza huku nikiwa nimeyakaza meno yangu kwa hasira kwa maana maisha yangu yameharibika kutokana na mambo ya ajabu ajabu kwenye hii nchini. Watu wachache wananifanya nishindwe kuishi kwa amani, nishindwe kufanya mambo yangu kwa uhuru kama mwananchi wa kawaida ambaye ninahitaji kuyafurahia haya maisha kama wananchi wengine.
 
“Dany”
“Mmmmm”
“Nipo tayari kuhakikisha kwamba unakuwa mtu yoyote. Nimeumbwa kwa ajili yako, nipo kwa ajili ya kukusaidia, hukustahili kupitia magumu yote hayo ambayo umeyapitia. Bado kijana mdogo, laiti leo hii usinge kuwa umepitia matatizo hayo uliyo nieleza, ninaamini leo hii ungekuwa mbali sana”
“Yaa”
“Sasa unataka kuwa nani?”
“Gaidi, gaidi kama wanaye msema wao”
“Hata mimi nipo tayari kwa hilo”
“Real”
 
“Ndio Dany”
Tukajikuta tukikumbatiana kwa nguvu huku kila mmoja akilia kwa uchungu, ninamshukuru Mungu kwa kunipatia Cajoli, japo nimepitia mambo mengi, ila Cajoli amekuwa ni msichana anaye jitoa maisha yake kwangu mimi, japo wapo wengi ambao walijitoa maisha yao kwa ajili yangu ila kila mmoja alikuwa na malengo yake kwenye haya maisha.
“Nakupenda sana Dany”
“Ninakupenda pia honey”
Taratibu tukajiuta tukianza kunyonyana midomo yetu, hisia za mapenzi zikaitawala miili yetu. Tukaanza kupeana raha ambayo inastahili kwenye mahusiano yetu, baada ya kuhakikisha kwamba tumeridhika na kila mmoja amepata haki kwa mwenzake, tukaingia bafuni na kuoga.
“Nahitaji umpigie shem Cajoli”   
“Nimueleze nini?”
 
“Nahitaji kuitingisha serikali kwa huu mpango ninao uhitaji kuufanya. Nahitaji viongozi wote walio ingia madarakani kwa njia za short cut, nilazima watoke”
“Sawa”
Cajoli akachukua simu yake na  kumpigia Cajoli.
“Unaweza kuja kwangu”
“Nakuomba ufanye hivyo”
“Poa best”
Cajoli akakata simu na kurudi kitandani nilipo kaa.
“Anakuja ndani ya dakika kumi atakuwa hapa”
“Yupo hapa hapa town?”
“Sijamuuliza, ila huwa Cajol akisema dakika kumi, basi ni kumi kweli”
“Unaweza ukaniletea zile nguo nyeusi nilizo zichukua kwa Cajoli”
“Yaa zipo humu kabatini”
 
Cajol akanitolea nguo hizo ambazo zipo kwa ajili ya mapambano tu. Nikazivaa, na kujitazama kwenye kioo vizuri.
“Hapa kazi inakwenda kuanza leo hii”
Ndani ya dakika kumi, Cajoli akafika nyumbani kwetu.
“Shem wewe ndio umesababisha varangati lile?”
“Yaani wee acha tu”
“Mmmm ni shida aiseee kumbe una mtiti yaani huko njiani magari full kukaguliwa. Tanga sijawahi kuona foleni ila leo foleni ipo”
“Watanisaka sana, ila nahitaji kuwakomesha kwa aina nyingine”
“Kiaina gani”
“Nahitaji kutega bomu la nyuklia na ninahitaji raisi atoke madarakani”
Cajoli wote wakaka kimya huku kila mmoja akitafakari ni nini cha kunishauri kwa maana swala la bumu tena la nyuklia ni swala jengine sana kwenye maisha haya ya Watanzania.
“Dany”
 
“Ndio shem”
“Unajua uzito wa bomu la nyuklia?”
“Ndio ninafahamu”
“Unajua madhara yake yanakuwaje?”
“Cajoli hadi kuzungumza hivyo ujue ninatambua kila kitu. Mimi nilikuwa ni agent wa NSS, hao unao waona sasa hivi barabarani wakinitafuta, mimi nilikuwa ni miongoni mwao”
“Dany mume wangu, ila hili swala tulitazame kwa jicho jengine, kuna mamilioni ya watu ambao hawana hatia kwenye kisasi chako, sasa kwa nini unataka hao nao wahusike kwenye vifo vya bomu hilo”
“Hamjanielewa maana yangu. Nilikuwa nina maanisha kwamba kwa kutumia bomu hilo nitaji raisi kuweza kuachia madaraka”
 
“Asipo achia na bomu unalo inakuwaje hapo shem?”
“Nina lilipua”
Taratibu nikamuona Cajoli akikaa kwenye sofa huku akionekana kuchoka, ninahisi moyoni mwake anajutia sana kuwa katika mahusiano na mimi.
“Shem”
“Naam”
“Hili swala ni kubwa sana, ninakuomba tufikirie mbinu nyingine”
“Munahitaji kunisaidia au laa?”
Nilizungumza kwa ukali hadi wote wakastuka.
“Tupo tayari kukusaidia”
“Shukrani shem, kuanzia sasa sihitaji muwasiliane na watu wengine zaidi yangu mimi”
“Sawa”
“Natambua NSS akili zao, kwa sasa wananitafuta kwenye barabara, viwanja vya ndege, baharini. Huku kwenye majumba hawatoweza  kunitafuta. Kama itawezekana nalihitaji lile bomu”
 
“Dany kusema kweli bomu kulileta  mjini hapa kwa njia ya gari ni ngumu sana. Labda cha kukushauri hapa twende Kange kule tunaweza kupanga kila kitu”
“Wazo zuri, honey nikuombe kitu?”
“Ndio”
“Nakupenda sana mke wangu, ninakuomba hili swala niweze kulifanya mimi na shem”
“Cajoli ni mtu muhimu kwetu ana uwezo mkubwa sana katika maswala ya computer na ugunduzi. Best au bado hukumueleza mumeo juu ya kipaji chako”
“Nilihitaji kumfanyia suprize, ili nitahakikisha kwamba kila jambo linakwenda vizuri”
 
“Basi nyinyi mutakwenda pamoja mimi nitajua wapi kwa kupitia”
“Sawa, ila itahitajika pikipiki kuhakikisha kwamba unafika kwa wakati”
“Pikipiki itapatikana wapi?”
“Ngoja niwasiliane na Hassani”
Shem Cajoli alizungumza, sikutaka kumzuia kwa maana ili niweze kufika kange kwa nja rahisi ni kuhakikisha kwamba ninapata pikipiki.
“Niletee pikipiki hapa kwa wajina”   
“Nahitaji mpya yenye uwezo mkubwa. Iwe full tank”
“Acha kunihoji mswali mengi wakati maelekozo nimekupatia”
Cajoli akakata simu na kututazama.
“Pikipiki italetwa baada ya muda mchache kuanzia sasa”
“Sawa, jiandaeni kwenda Kange. Hivi sasa ni saa mbili kasoro usiku”
 
Cajoli na mwenzake hawakupinga chochote, wakaanza kujianda. Haukupita muda mwingi Hassani akaleta pikipiki aina ya boksa, akamkabidhi shem Cajoli, kisha jamaa akaondoka pasipo kielewa kitu kinacho endelea.
“Mlinzi weko hivi anatambua uwepo wangu?”
“Sidhani honey”
“Kwa shem, mlizi hakuwahi kukuona?”
“Nikirudi nipo ndani ya gari, nikishuka ninaingia ndani. Hajawahi kuniona kabisa”
“Ngoja nimpe likizo”   
Cajoli akatoka na kuniacha na shemeji. Kwa kupitia dirishani nikamuona akizungumza na mlinzi. Kisha akarudi ndani, akachukua kiasi cha pesa na kwenda kumkabidhi mlinzi huyu ambaye hakuonekana kurishishwa na maamuzi haya ya muda mfupi.
 
“Sisi utatukuta Kange”   
“Sawa kuweni makini”
“Poa”
Cajoli na rafiki yake wakaondoka hapa nyumbani huku kila mtu akitumia gari lake. Nikakaa kwenye sofa huku nikisubiria masaa yazidi kusonga mbele ili hata nikuondoka basi asinione mtu yoyote. Nikawasha tv na kukuta habari yangu ikiwa ndio inatawala kwa wakati huu. Picha zangu zinarushwa kwenye kila kituo cha televishion huku mtu ambaye atafanikisha kukamatwa kwangu atazawadia shilingi bilioni moja ya Kitanzania.
 
“Wenda wazimu nyinyi”
Nilijikuta nikizungumza huku nikielekea ndani ya chumba chenye begi lenye silaha. Nikachukua begi na kurudi nalo sebleni. Nikaanza kukiko bastola moja baada ya nyingine huku nikizichomeka sehemu mbali mbali katika mwili wangu, nikianzia kiunoni hadi miguuni, na uzuri wa suruali niliyo ivaa ina sehemu nyingi ya kufichia silaha.
 
Ilipo timu saa tano kamili usiku nikatoka nje na begi langu. Nikaliweka kwenye pikipiki vizuri. Nikaufunga mlango wa kuingilia ndani kwa Cajoli kisha funguo nikaificha kwenye kopo la maua lililopo karibu na mlango. Nikapanda pikipiki, taratibu nikatoka getini huku nikiwa nimevaa kofia maalumu la pikipiki, kwenye viganja nimevaa glovos ngumu na zenye rangi nyeusi kuhakikisha kwamba mikono haitelezi. Safari yangu nikainza huku nikiwa makini sana kila ninapo pita. Nikiwa katika maeno ya msikiti wa Madina, gari mbili za polisi nikaziona zikija nyuma yangu kwa kasi huku zikiwasha ving’ora, jambo lililo nifanya nizidi kuongenza mwendo kasi wa piki piki yangu aina ya Boxer, ambazo husifika kwa mwendo kasi barabarani.
                                                                           
AISIIIII……….U KILL ME 103                                                                                               

Kadri nilivyo zidi kwenda kasi ndivyo jinsi nilivyozidi kuwaacha askari hawa umbali mkubwa na wala sifahamu kama wananifwata mimi au laa. Nikapita barabara za mkato hadi nikafanikiwa kufika nyumbani kwa Cajoli.
“Vipi hawajakustukia?”
“Hapana, japo kuna gari mbili za polisi zilikuwa zikinifukuzia, ila sijajua kama ni mimi ndio waliokuwa wakinifukuzia au mtu mwengine”
“Karibu tena nyumbani kwangu”
“Usijali”
Shem Cajoli akachukua pikipiki yangu na kuiweka kwenye moja ya chumba, cha nje kisha tukaingia ndani pamoja.
“Wife yupo wapi?”
“Yupo huku chini”
 
Tukashuka kwenye ngazi za kuelekea katika chumba ambacho kipo chini ya ardhi. Nikamkuta Cajoli akimunya minya batani ya computer iliyomo humu chumbani.
“Karibu honey”
“Asante”
Nilimjibu huku nikimbusu shavuni mwake.
“Ndio tunaanza kazi hapa na nimepata wazo jipya ambalo tulilizungumza na wajina hapa, tukaona ni vyema kukushirikisha”
“Ehee ninawasikiliza makamanda wangu”
Nilizungumza huku nivuta kiti kilichopo pembeni na mpenzi wangu Cajoli.
“Dany hii tunayo kwenda kuifanya ni biashara, ambayo kwanza italitingisha taifa, pili tutahakikisha kwamba tunaingiza pesa nyingi sana. Unatambua kwamba ukiwa na pesa unaweza kufanya kila kitu hata kumtoa raisi madarakani inawezekana kwa kutumia pesa”
“Eheee niambie mama maana ninaona hilo unalo kwenda kulizungumza lina udabwidambwi ndani yake”
“Hahaa shem kumbe una maneno ya Kiswahili namna hiyo”
“Kawaida tu shemeji yangu. Baby endelea”
 
“Hapa nipo katika hatua ya kutengeneza virus, ambavyo tutaviweka kwenye maji ambayo watu wakinywa. Hawato kufa ila wataugua ugonjwa wa kutoka mapunye mwili mzima”
“Mapunye!!?”
“Yaa mapunye haya yatawatoka mwili mzima. Na yatapelekea mtu kuoza mwili wake. Ila sisi tunaweza kutengeneza dawa, itakayo waponya mapunye hayo. Kwa njia hiyo tutaingiza bilioni of shillings”
Cajoli alizungumza kwa kujiamini sana.
“Shem hilo wazo ni zuri sana. Kutokana wewe unapambana na watu ambao wapo serikalini na unataka kuwaangusha kirahisi, hakuna haja ya kutumia nguvu nyingi sana. Hapa cha kutumia ni akili, maarifa na utalipiza kisasi chako taratibu na ninakuhakikishia kwamba utajikuta ukifika mbali sana”
Nikakaa kimya kwa sekunde kadhaa huku nikitafakari mpango mpya ambao wasichana hawa wameuweka mezani.
“Hao virus watakuwa kwa njia ya maji maji au?”
 
“Yaa watakuwepo kwenye maji machache tu. Na kwadakika moja virus hao ninao watengeneza watakuwa wakiongezeka kwa zaidi ya virusi milioni mia moja. Sasa piga picha lisaa moja lina lina dakika ngapi, siku moja nayo ina dakika ngapi. Ni watanzania wangapi kwa siku wanakunywa maji?”
“Ni wengi, sasa kwa mfano wale wanao chemsha maji inakuwaje kwao?”
“Honey hawa virusi ninao watengeneza hata akichemshwa, awekewe sijui water gurd hafi yaani hii ni taaluma ambayo ninayo mimi mwenyewe duniani kwa kutengeneza hawa virusi, mtu mwengine ni mama yangu ambaye kwa sasa ni marehemu”
 
“Hao virusi katika maji wanaweza kuishi kwa kipindi gani?”
“Zaidi ya mwaka mmoja na nusu”
“Waoooo”
Katika maisha yangu sikuwahi kufikiria wazo kama hili. Japo ni watanza wengi ndio wanakwenda kuathirika na huu ugonjwa, ambao hakuna mtu atakaye kufa, basi kwangu ni furaha kwani kisasi changu kinakwenda kukamilika taratibu taratibu
“Na mtu atakapo kunywa maji ni baada ya muda gani anaweza kuathirika”
“Lisaa, ninataka wachukue lisaa kuutawala mwili wa binadamu, ili isije kugundulika mapema kwamba tatizo kubwa lipo kwenye maji”
“Hapo safi, na utachukua muda gani hadi kukamilisha kuwatengeneza”
“Nina dakika kumi na tano mbele, nikisha watengeneza kuna kemikali nitazichanya baada ya hapo virusi watakuwa tayari kuanza kazi”
 
“Shemeji mke wako yupo vizuri, nikuibie siri?”
“Niibie tu”
“Yeye ndio aliye tengeneza hili bomu la nyuklia”
“Weeee!!”
“Ohoo nakuambia hapo mukipata mtoto basi atakuwa genius”
Kwa furaha nikajikuta nikimkumbatia Cajoli wangu.
“Hii kazi ikikamilika, ninawahakikishia mutaishi maisha ya furaha na yakijiri”
“Mungu abariki katika hili”
“Samahani injinia, sasa hivi mke wangu nitakuwa ninakuita injinia”
“Bila sahamani mume wangu”
“Hao virusi tukiwaweka kwenye maji, watasambaa kwenye maji Tanzanzima kwa kasi ya kiasi gani?”
“Yaani hawa virusi tukiwamwaga, kwa mfano kwenye chanzo cha maji ya dawasko hapa Tanga watasambaa kwa kasi ya yaa naweza kufananisha na kasi ya nini?”
“Ferrari?”
 
“Aghaa hilo ni gari mume wangu, ninaweza kuchukulia kasi ya sauti au hewa”
“Duu ni kasi kibwa sana”
“Yaa nahitaji hadi asubuhi kuna pambazuka tuna amka na habari hii”
“Kazi nzuri mke wangu, ngoja tusikuchanganye tukuachie nafasi ya kufanya kazi”
“Ahaa munaweza kubaki humu humu tu, mukaangalia jinsi ninavyo waunda”
Ikatubidi mimi na shem Cajoli tubaki kuwa watazamaji wa kitu anacho kifanya Cajoli kwenye hii computer, jambo ambalo kusema kweli hadi sasa hivi sielewi kitu ambacho anakifanya kwa maana sisi wawili hatuna utaalamu wa mambohayo. Baada ya dakika kumi na tano, akatugeukia na kututazama.
 
“Virusi wetu wapo tayari, hapa kazi iliyo baki ni kuanza kuinda hiyo fumula niliyo iweka kwenye computer”
“Hapo kumbe ulikuwa una unda fumula?”
“Yaa, baada ya hapo ninachukua kemikali ambazo zinahitaji, kirusi chetu tunamuunda ndani ya dakika mbili atakuwa hai”
“Sawa”
“Wajina naomba zile kemikali nilizo undia bomu la nyuklia”
“Poa”
Shem Cajoli akatembea hadi kwenye moja ya ukuta katika hichi chumba. Kuna kijimlango cha chumba, akaingiza namba za siri kisha akakifungua. Akatoa chupa kadhaa alizo zishika kwa umakini, Cajoli akachukua glove pamoja na miwani kubwa, akazivaa na kuisogelea meza ambayo shem Cajoli ameweka chupa hizi za kemikali. Cajoli akawasha taa kubwa iliyopo kwenye meza yenye kemikali
 
“Nawaomba mukae mbali kidogo, kwa maana hizi kemikali sio nzuri pake zitakapo mdondokea mtu”
“Sawa injinia”
Tukasimama umbali kidogo kutoka katika sehemu alipo Camila, akaanza kuchanganya changanya kemikali zake haraka haraka. Alipo hakikisha zimekamilika akachukua kibakuli alicho changanyia kemikali hizo na kukiweka kwenye darubini(Microscope) na kuanza kupima.
“Njooni muone”       
Cajoli alizungumza huku akitabasamu sana. Tukakimbilia hadi sehemu alipo, akaanza kuchungulia shem Cajoli, kisha akanipisha mimi kuchungulia kitu anacho kiona kwenye hii darubini ya kidaktari.
 
Kitu ninacho kiona ni vijidudu dudu, vidogo sana na kila baada ya dakika moja vinaongezeka.
“Hivi ndio virusi?”
“Yaa hivyo ndio virusi ambavyo nilikuwa nikiviunda, hapo ni lazima watu wataisoma namba”
“Kazi nzuri mke wangu, sasa si tuanze na majaribio kwanza?”
“Hakuna haja ya majaribio shem, hapa tunalibwaga bomu, alafu tukaa pembeni kusikilizia majibu”
“Ila watu si hawato  kufa mke wangu?”
“Nakuhakikishia mume wangu hakuna mtu ambaye  atakufa kwa maana hichi tunacho kifanya, ni kuiforce serikali hii ambayo leo hii wewe inakuita gaidi ila kesho au kesho kutwa watakuita daktari”
“Kama ni hivyo ninakuomba virusi hawa tuanze kuwaachia kuanzi sasa”
“Itabidi hapa tugawane kazi, vyanzo vyote vya maji yanayo tumiwa kwa watanzania tumwage hawa virusi”
“Ila nimepata wazo jengine?”
“Wazo gani?”
 
“Tukisema tutumie njia ya kupeleka kwenye vyanzo vya maji, inaweza kuwa ngumu sana. Nilicho fikiria kwamba hao virusi niwabadilishe kuwa katika hali ya hewa, nikiwaachia hewani. Wakimbilie sehemu yoyote ya maji ambayo hayajafunikwa”
“Inawezekana kubadilishwa?”
“Ndio inawezekana”
“Basi tufaje hivyo”
“Ila itachukua lisaa kufanya hivyo”
“Hakuna tabu mke wangu”
Cajoli kwa haraka akavuta kiti alicho kuwa amekalia. Akaanza kuminya minya batani za computer akatengeneza alicho kitengeneza kisha akarudi kwenye meza ya kemikali. Tukaa umbali kidogo, alipo hakikisha amemaliza kutengenza virusi hawa wawe kwenye njia ya hewa, akachukua kichupa kidogo na kuweka maji maji hayo kisha akakifunga.
“Hichi kichupa, wajina nitahitaji ukiweke juu ya nyumba yako ukifungue, maji maji hayo yatapungua kadri jinsi virusi watakavyokuwa akisafiri kwa hewa”
“Sawa, sasa na sisi maji ya humu ndani?”
“Tuanzeni kufunika, tuhakikishe kwamba maji tunayo kunywa yawe katika usalama”
“Unaonaje ukatengeneza kinga yake”
“Ni rahisi kuitengeneza na tutakuwa tunaitumia sisi wenyewe.”
“Sawa, shem twende ukanisaidie”
“Twendeni wote”
Tukatoka katika chumba hichi kilichopo chini ya ardhi. Tukaanza kazi ya kufunika vyombo vyote vyenye maji. Tulipo hakikisha kwamba tumemaliza. Tukatoka nje, Cajol akanipa kichupa hicho, tukaweka ngazi sehemu ambayo ninaweza kupanda kwenda juu kirahisi. Kazi ya kupanda juu haikuniwia ugumu kabisa. 
 
‘Mungu tusamehe katika hili’
Nilizungumza huku taratibu nikifungua kichupa hichi. Nikaanza kushuhudi jinsi kinavyo pungua maji yake taratibu. Nikashuka na kuwakuta Cajoli wakinisubiri,
“Kinapungua kweli aisee”       
“Yaa hiyo itakuwa ni kazi, hapa virusi hao wanakimbilia sehemu yenye maji. Na hewa hii itasambaa  nzima”
“Vipi kwa wale wa Kenya, kwa maana hii hewa haina mipaka?”
Ukimya ukatawala kati yetu huku kila mmoja akifikiria jambo hilo.
“Ngoja tuangalie itakuwaje, ikionekana vipi nao wacha waje tu. Ni moja ya biashara, unacho kihitaji wewe Dany ni pesa na nguvu”
Cajoli alizungumza kwa kujiamini na kuzidi kunifanya nijione mshindi katika kisasi changu ambacho kwa sasa sihitaji kutumia nguvu sana kulipiza, ila ninatumia akili kuhakikisha maadui zangu wanaisoma namba.

==>>ITAENDELEA KESHO

Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 08

0
0
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA  

“Angalia mlangoni”
Nikatazama mlangoni, sikuona kitu chochote, nikageuka kumtazama katika sehemu ambayo alikuwa amekaa, ila sikumuona, nikastukia mlango ukifunguliwa, akaingia mzee mmoja aliye valia suti nzuri huku akiwa ameongozana na walinzi huku mkono wake wa kulia akiwa ameshika Camila ambaye usoni mwake ana mwagikwa na machozi. Nikanyanyuka kwa haraka kitandani na nikamsalimia mzee huyu kwa heshima sana, ila sura yake ikaonyesha kukasirika sana, na kwa haraka nikaweza kumtambua kwamba huyu ndio raisi wa hapa Ujerumani kwa maana picha yake ipo katika ofisi ya mkuu wa shule na waalimu wengine.

ENDELEA
“Wewe ndio kijana unaye itatiza akili ya mjukuu wangu?”
Mzee huyu alizungumza kwa ukali sana hadi mimi mwenyewe nikaanza kutetemeka huku machozi yakianza kunilenge lenga.
“Ninakuonya mtoto, kaa mbali na mjukuu wangu la sivyo hii nchi utaiona mbaya, na wewe umekuja shule kusoma na si kuingia ingia kwenye mabweni ya wanaume umenielewa?”
Camila akatingisha kichwa huku akiendelea kumwagikwa na machozi usoni mwake. Mzee huyu akanitazama kwa muda kidogo kisha wakatoka ndani humu na walinzi wake. Mwalimu wangu wa darasa akaingia huku akiwa amejawa na sura ya huzuni. 
 
“Ethan”
“Naam”
Niliitikia kwa sauti ya unyonge sana huku nikimtazama mwalimu wangu huyu ambaye ana nipenda kutokana na kipaji changu cha mpira uwanjani.
“Una mahusiano na huyu binti?”
Mwalimu aliniuliza kwa sauti ya upole sana huku akiwa amekaa kitandani, kwa uoga nilio nao nikajikuta nikishindwa hata kuzungumza zaidi ya kuanza kulia. Taratibu mwalimu akanivuta jaribu yangu na kunikumbatia na kuanza kunibembelea kwani habari hii ikifika kwa bibi Jane Klopp na mume wake sijui watanichukuliaje.
“Usiwe karibu na yule binti sawa”
“Sawa mwalimu, ila ni rafiki yangu tu wa kawaida?”
“Ndio nina litambua kwa umri wako huwezi kuwa na mahusiano ila muheshimiwa alikuhisi tu vibaya, ila nakuomba usipende kuwa naye karibu sihitaji kukupoteza kwenye darasa langu”
 
“Sawa mwalimu”
Mwalimu akaniachia huku akinitazama usoni mwangu. Akaniomba niweze kujipumzisha na nisitoke ndani humu hadi kesho. Mwalimu alipo ondoka rafiki zangu wakingia ndani ya chumba hichi huku nao wakiwa wanahitaji kufahamu ni kitu gani ambacho kimetokea hadi raisi kunifwata humu bwenini. Kwa mtazamo wa haraka haraka wengi wao wanahisi kwamba raisi amekuja kunipongeza kwa kufanya vizuri kwenye mechi yangu ya kwanza tu.
“Ethan unazidi kuwa maarufu”
Wezangu walizidi kunipongeza huku wakiwa wamejawa na fur asana, ila laiti kama wangefahamu kwamba nimetoka kufokewa tena na mkuu wa nchi yao wala wasinge zungumza lolote juu yangu.
                                                                                                                      ***
    Umaarufu wangu katika shule hii ukazidi kupanda siku hadi siku. Michuano ya mpira madarasa ya shule hii ya msingi yakazidi ninifanya nizidi kuwa kipenzi cha wanafunzi na waalimu wengi. Kwani nikiwa kama kapten wa timu yangu, ya darasa la kwanza, niliweza kuingoza timu yangu katika kila ushindi tulio upata katika mechi za madarasa tulizo kutano nayo. Katika safu ya ufungaji, niliongoza kwa magoli ishirini na sita huku anaye nifwatia akiwa na magoli kumi. Katika kipindi chote sikuhitaji kukaa karibu na Camila na kila nilipo muona ana kuja nilipo kwa ajili yangu, nilifanya kila ina ya mbinu kuhakisha kwamba nina mkwepa.
“Ethan”
Niliitwa na msichana mmoja tukiwa uwanjani tunajiandaa na mechi ya kucheza na darasa la sita.
 
“Ndio”
“Kuna ujumbe wako hapa”
“Kutoka kwa nani?”
“Wewe chukua”
Msichana huyu alinipa ujumbe huu, nikataka kuusoma ila mchezaji mwenzangu aka nizuia kwa maana tumebakisha dakika chache sana kabla ya kuingia uwanjani. Ujumbe huu nikauingiza kwenye soksi zangu za mpira kisha nikaingia uwanjani. Mwalimu akaniita kwa ajili ya kunipa maelekezo yake kama kocha.
“Una muona yule mwenye macho ya blue kiasi?”
Mwalimu alizungumza huku akinionyesha mchezaji wa darasa la sita.
“Ndio”
“Yule ni beki wao, na anacheza rafu anaweza hata kukuvunja. Hakikisha kwamba unakuwa makini naye sawa”
“Sawa mwalimu”
 
“Ushindi ni muhimu, kumbuka tuna mechi moja mbeleni, tukishinda hii ya robo fainal, najua tutakao kutana nao nusu nilazima tutawafunga na tutaingia fainali”
“Sawa kocha”
Nilizungumza huku nikiangaza angaza macho yangu katika kumuangalia ni wapi alipo Camila, ila nikashindwa kabisa kumuona jambo lililo nipa wasiwasi mwingi sana, japo ninamkwepa ila moyo wangu una niuma sana. Nikamuona mlinzi mmoja wa Camila akifika katika eneo hili kwa kasi sana, akamnong’oneza mwalimu jambo amalo hata mwalimu mwenyewe akaonekana kustuka kidogo. Mwalimu akanitazama kwa sekunde kadhaa kisha aka ninong’oneza.
“Nakuomba uongozane na huyu mlinzi kuna jambo la muhimu sana limetokea, ila hakikisha kwamba unatumia kila mbinu unalitatua na unarudi hapa kiwanjani sawa”
“Sawa”
 
Nikavua kitambaa cha muongozaji wa timu(capten) na nikanza kukimbia na mlinzi huyu, jambo ambalo kidogo likawastua mashabiki walio weza kuliona tukio hilo. Tukakimbilia hadi kwenye mabweni ya wasichana na nikawakuta baadhi ya waalimu na wazazi wa Camila wakiwa chini ya gorofa hili huku juu kabisa akiwepo Camila mwenyewe akihiyaji kujirusha kutoka gorofani hapo ili afe. Hapa ndipo nikawazia juu ya ujumbe ambao nilipatiwa na sikuusoma.
“Wewe ndio Ethan?”
Mama Camila aliniuliza huku machozi yakimwagika usoni mwake.
“Ndio ni mimi”
“Ninakuomba umsaidie mwanangu, nakuomba mwanangu ana kuhitaji wewe tafadhali nakuomba sana kijana”
Nikasimama katika sehemua mbayo Camila ambayo anaweza kuniona, nikamtazama.
“Camila……Camil”
 
Niliita kwa sauti ya kuu na Camila akanitazama.
“Panda juu ukazungumze naye tafadhali”
Baba Camila alizungumza huku naye akionyesha dhairi kwamba ana wasiwasi mkubwa sana. Nikaanza kupandisha ngazi za gorofa hili huku nikikimbia, nikafika gorofa ya nane na nikapanda juu kabisa alipo Camila, nikamakuta akiwa amesimama kwenye ukingo wa gorofa hili na endapo atafanya mchezo kidogo basi anaanguka chini na kufa.
“Camila, kwa nini unataka kufanya hivyo mpenzi wangu”
“Ethan kaa mbali na mimi, hunipendi”
Camila alizungumza kwa ukali sana.
“Ninakupenda Camila, nina kuhitaji mpenzi wangu”
“Kwa nini ushindwa kupigania penzi letu. Ninakufwata ila unanikimbia kimbia, ni maisha gani ambayo unanifanyia lakini eheee?”
 
Camilia alizungumza huku akilia sana, kwa umri ambao tunao hakika haistahili kwa sisi kuwa na mapenzi ya namna hii, kusema kweli Camila ana nipenda hadi anaamua kutaka kujiua kwa ajili yangu.
“Hapana Camila, nina ogopa. Baba yako anaweza kunidhuru, je unataka nife ehee?”
“Acha nife mimi kama unaogopa kufa”
“Hapana Camila, sihitaji ufe. Nina kuapia kwa mwenyezi Mungu kuanzia leo wewe ni wangu, hakuna ambaye atatutenganisha, nife mimi au ufe wewe, ila wewe ni wangu Camila”
Nilizungumza huku machozi yakinimwagika usoni mwangu, nikaanza kutembea taratibu huku nikimfwata Camila alipo simama.
“Camila na kuomba usifanye hivyo mpenzi wangu, nakuomba sana.”
 
“Ethan wewe hunipendi una nidanganya”
“Nakuapia haki ya Mungu nipo tayari kwa lolote, nina kupenda sana Camila wangu”
Niliendelea kuzungumza huku nikipiga hatua za taratibu hadi nikafanikiwa kufika sehemu alipo simama Camila, taratibu nikampatua mkono wangu wa kulia huku nikiendelea kumtazama usoni mwake.
“Camila, nipo tayari tukue pamoja, tuje kuishi pamoja na kuzaa watoto pamoja. Nitakuepeleka kwetu Tanzania, ukaona mazingira mazuri ya nchi yetu nakuomba sana Camila wangu tafadhali.
Camila akanitazama kwa macho yake mazuri, akashusha pumzi taratibu.
“Una niahidi nini?”
“Tayari nimesha kuahidi mengi mpenzi wangu”
“Nataka kusikia upya”
“Nakuahidi kuwa na wewe, nakuahidi kuishi nawe, nakuahidi kukupeleka kwetu Tanzania, nakuahidi kupigania penzi letu, nina kupenda sana mpenzi wangu”
“Upo tayari kusimama mbele ya babu yangu na kumuambia kwamba una nipenda?”
“Ndio nipo tayari”
 
Nilijibu ili maradi kumridhisha, ila kusema kweli sina ujarisi wa kusimama mbele ya mzee huyu mkali sana, na nimuambie kwamba nina mpenda mjukuu wake. Camila akanivuta mkono wangu na kuanza kushuka kwenye ukingo huu wa gorofa. Tukakumbatiana kwa nguvu, Camila akaanza kunibusu mdomoni mwangu bila ya kujali kwamba tupo katika eneo la shule.
“Nisikilieze mpenzi wangu, uwanjani mechi imesha anza, ninakuomba twende ukanishangilie mume wako”
“Kweli mpenzi wangu?”
“Ndio”
“Na leo nataka ufunge magoli matano mpenzi wangu”
“Sawa, kwa ajili yako nitafunga”
“Nakupenda sana Ethan”
“Nakupenda pia Camila wangu”
Mlango wa eneo la huku juu ukafunguliwa, akaingia baba mama Camila kisha akafwatia mke wake pamoja na walinzi wao. Wote wakashangaa ni ushawishi gani ambao nimeufanya kwa binti yao hadi kugairi kujiua.
 
Camila akaniachiana kukumbatiana na wazazi wake.
“Tunashukuru sana kijana”
Alizungumza baba Camila huku akinitazama usoni mwake.
“Sawa sawa mzee”
“Wazazi wangu, naomba mumuambie babu, nina mpenda Ethan, ninataka awe ndio mwanaume wa maisha yangu, sijali ni muafrika au ni mweusi na wala sijali utoto wetu, ila ninampenda, naomba musikilize hisia zangu wanazai wangu”
Camila alizungumza huku machozi yakiendelea kumwagika. Walimu nao wakafika katika eneo.
“Tutamueleza na sisi ndio wazazi wako, sisi ndio wenye maamuzi juu yako na si baabu yako. Tupo tayari uwe na huyo kijana kwa maana hatujaona ubaya wowote kwake kwanza ni handsome boy”
Mama Camila alizungumza huku akinikonyeza. Nikatabasamu huku nami nikiwa nimejawa na furaha.
“Kweli mama?”
 
“Asilimia mia moja”
“Asante mama na baba nina wapenda sana”
“Tuahidi hauto fanya hili jambo tena?”
Baba Camila alizungumza huku akimtazama mwanaye usoni
“Sinto lifanya nina waahidi wazazi wangu ila mukinitenganisha na Ethan kwa namna yoyote basi nitajiua”
Camila alizungumza kwa msisitozo na wazazi wake wakaka kimya.
“Mpenzi wangu ni mchezaji mpira, na timu yake ipo uwanjani, twendeni tukamshangilie”
“Sawa twendeni”
Tukaondoka juu ya gorofa hili na kuelekea uwanjani. Tukiwa karibu ya uwanjani tukasikia shangwe kubwa ambazo zikanifanya nikimbilie uwanjani. Nikatazama ubao wa magoli, nikaona timu yangu ikiwa imefungwa goli mbili bila na goli hili la pili ndio limetoka kuingia muda si mchache. Mwalimu alipo niona akatanasamu sana kwani timu inacheza kwa kuto kujiamini na nina amini kwamba wachezaji wezangu watakuwa wakijiuliza ni wapi nilipo elekea na ni kitu gani ambacho kilinipata hadi nikaondoka kabla ya mechi kuanza.
“Umefanikiwa?”
 
“Ndio mwalimu yule pale na wazazi wake”
Nilizungumza huku nikimuonyesha alipo Camila na wazazi wake.
“Sawa anza kupasha”
Nikaanza kukimbia kimbia pembezoni mwa uwanja na kuwafanya mashabiki wa darasa langu kuanza kushangilia, wachezaji wezangu walipo ndani ya uwanja walipo niona nao wakaanza kupata hamasa ya kucheza kwa juhudi. Nikawatazama wakwe zangu, nao nikawaona wakiwa wamkini sana wakifwatilia mpira huu huku wakiwa wamekaa kwenye jukwaa maalumu la wageni rasmi, kocha akaniita.
“Kiungo kimepwaya, na hata ngome yao ni ngumu sana kuipita yule beki niliye kuonyesha ana cheza namba tano, hakikisha kwamba unakuwa naye makini”
“Sawa mwalimu, zimebaki dakika ngapi kabla ya kipindi cha kwanza kuisha?”
“Dakika kumi”
“Sawa”
 
Yakafanyika mabadiliko, akatoka mshambuliaji mmoja kisha nikaingizwa mimi. Uwanja mzima ukarindima kwa shangwe, kila mtu akafurahi uwepo wangu uwanjani. Hofu ikaanza kuwapata wachezaji wa darasa la sita, mimi na rafiki yangu Rafael ambaye huwa tunaendana sana kwenye swala la uchezaji na ushambuliaji, tukaanza kupeleka mashambulizi ya kasi sana kwa darasa la sita. Ndani ya dakika nne, Rafael akafanikiwa kufunga goli la kwanza huku pasi ya goli hilo ikitokea kwangu. Nikamuona jinsi Camila anavyo shangili huku akinipungia mkono.
“Tunaweza kurudisha?”
 
Niliwahimiza wachazaji wezangu huku nikipotea kitambaa cha kuongoza timu kutoka kwa golikipa. Mpira ukaanza kwa kasi ya ajabu huku wachezaji wezangu wakijitahidi kwa hali mali kuhakikisha kwamba tunakomboa hili goli moja lililo sali, nikafanikiwa kupata mpira huku mbele yangu kukiwa kumebakia mabeki wawili, mmoja ndio yule ambaye kocha aliniambia niwe naye makini. Mabeki hawa wawili wakanifwata kwa kasi sana, nikiwa katika harakati za kuwapita, kutokana na uwefu wa vimo vyao, nikahisi kisi kitu kizito kikinipiga kichwani mwangu na mzima mzima nikaanguka chini na giza nene taratibu likaanza kupoteza nuru ninayo iona kwenye mboni za macho yangu na baada ya sekunde kadhaa nikapoteza kumbukumbu.

==>>ITAENDELEA KESHO

Alichokisema Rais Magufuli Leo Baada ya Kukutana na Wakimbiza Mwenge IKULU

Serikali kuliweka kwenye kumbukumbu gari la Nyerere lililokarabatiwa na Veta

0
0
Serikali imesema italichukua na kulihifadhi kama kumbukumbu ya vitu alivyokuwa anatumia hayati baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere, gari alilokuwa akitembelea mwaka 1968 na kuundwa upya na Chuo cha Ufundi Stadi (Veta), mkoani Kilimanjaro.

Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk. Ally Mohamed Shein, amesema hayo jana katika sherehe za  kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru baada ya kutembelea banda la Veta na kujionea gari alilokuwa akitumia mwalimu wakati wa harakati zake za kutafuta uhuru ambapo pia aliwapongeza vijana hao kwa umahiri wa kutengeneza gari hilo.

“Vijana hao wameonyesha kwamba wamefuzu vizuri na wameonyesha uzalendo, Serikali inatambua mchango huo.

“Serikali itaongeza vyuo vya ufundi Tanzania Bara na Visiwani kwa lengo la kuhakikisha vijana wanapata fursa ya kujiunga na vyuo hivyo ili waweze kujiajiri,” alisema Dk. Shein.

Chadema wakanusha kuwepo mgogoro ndani ya chama kati ya Katibu Mkuu na Mwenyekiti Mbowe

0
0
Chadema kimekanusha taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu Dk Vincent Mashinji wametofautiana kwenye kikao cha Kamati Kuu.

==>>Hapo chini ni taarifa ya CHADEMA
Ndugu waandishi, Zipo taarifa potofu zinasambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Mwenyekiti wa Chama Mhe.Freeman Aikaeli Mbowe na Katibu Mkuu Dr.Vincent Mashinji wametofautiana kwenye kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika nyumbani kwa Mwenyekiti mwishoni mwa juma hili.

Napenda kutoa ufafanuzi kama ifuatavyo;

1. Hakuna kikao chochote cha Kamati Kuu ambacho kimefanyika mwishoni mwa wiki hii, sio tu nyumbani kwa Mwenyekiti Mbowe bali Popote pale.

2. Hakuna Popote ambako viongozi hao waandamizi wametofautiana kuhusu yanayoendelea kwenye mitandao ya kijamii.

3. Haijawahi kutokea wakati wowote Vikao vya kamati kuu vikafanyika nyumbani kwa Mwenyekiti wa Taifa

4. Tunaomba watanzania na Wanachama wetu wapuuze taarifa hiyo potofu inayosambazwa kwenye mitandao.

John Mrema
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje.
15 Oktoba, 2018
 

Godbless Lema Kesho Atazungumza na Waandishi wa Habari Kuhusu Sakata La Mo Dewji Kutekwa

0
0
Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amesema amekamilisha uchunguzi wa sakata la kutekwa kwa mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji ‘Mo’ na kesho atazungumza.

Lema ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani, amesema mkutano huo na waandishi utafanyika makao makuu ya Chadema mtaa wa Ufipa, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Familia ya mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji ‘Mo’ leo imezungumza na waandishi wa habari kuhusu kutekwa kwa bilionea huyo na kutangaza dau la Sh1 bilioni kwa mtu yeyote atakayewezesha kupatikana kwake.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne Ya October 16

RC Makonda Aagiza Kukamatwa Kwa Vigogo Waliohujumu Soko La Kariakoo Na Kusababisha Hasara ya Bilioni 1.3

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ameagiza kukamatwa kwa waliokuwa viongozi wa Soko la Kimataifa Kariakoo kwa kusababishia serikali hasara ya zaidi ya Shilingi Bilioni 1.3.

Vigogo walioagizwa kukamatwa ni aliekuwa Mkuu wa idara ya fedha, Mkuu idara ya utumishi, mkuu idara ya manunuzi na aliekuwa mkuu idara ya mipango na biashara ambao wameagizwa kufikishwa mahakamani Mara moja.

RC Makonda ametoa maagizo hayo wakati wa mkutano wa utatuzi wa kero za wafanyabiashara Soko la Kariakoo ambapo pia ametoa siku tano kwa watendaji kupitia upya sheria zote za ushuru mdogomdogo baada ya kubaini uwepo wa ushuru mkubwa unaoumiza na kuwarudisha Nyuma wafanyabiashara.

“Hatuwezi kuwa na shirika linaloongeza kero kwa wafanyabiashara na kuwarudisha Nyuma, haiwezekani mtu alipie kodi ya pango, ushuru wa kuingiza mzigo 600, ushuru wa Siku 1,700, muuza kahawa alipe 1,000 na bado mtu huyohuyo analipa ushuru wa Choo na Bafu 500, hili haliwezekani” Alisema RC Makonda.

Aidha RC Makonda ameagiza kuvunjwa kwa mkataba wa makusanyo ya ushuru baina ya mbia na soko na badala yake ameagiza kazi ya ukusanyaji wa ushuru ifanywe na uongozi wa soko.

Pamoja na hayo RC Makonda ameagiza soko kuu la kariakoo kurejeshwa kwenye hadhi ya kimataifa na sio kuendeshwa kiholela Kama ilivyo sasa ambapo linapokea bidhaa za rejareja kutoka mitaani badala ya kuwa soko la kuuza bidhaa za jumla.

Miongoni mwa kero zilizolalamikiwa na wafanyabiashara ni uhusiano mbovu baina ya viongozi na wafanyabiashara, kodi ya pango, vyanzo vingi vya ushuru, mikataba, mikopo, soko kupoteza mwelekeo, mkanganyiko kwenye viwango vya vipimo, kadi ya kizimba na ukamataji ambapo RC Makonda ameahidi kuzifanyia kazi.

Mkongo Wa Taifa Wa Mawasiliano Waongeza Mapato Ya Serikali

0
0
Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano umeongeza makusanyo ya mapato ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye maeneo ya mipakani mwa Tanzania na nchi jirani za Rwanda, Uganda, Burundi na DRC Congo

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye wakati wa ziara yake ya kukagua Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwenye kituo cha mpakani cha Mtukula ambacho kinawezesha usafirishaji wa taarifa na data za wateja na bidhaa kutoka Tanzania kwenda nchi jirani ya Uganda.

Nditiye amesema kuwa, “maeneo ya mipakani ndi lango la kuongeza mapato na kukuza uchumi wan chi yetu, niwatake muendelee na kasi hii ya ukusanyaji wa mapato ya Serikali kwa kutumia Kituo cha Pamoja cha Huduma ambapo tayari kwa kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo wa mwaka wa fedha wa 2018/2019, mwezi Julai hadi Septemba, 2018 mapato yameongezeka zaidi ya asilimia 100 kwa mwezi na kufikia asilimia 150”.

Naye Afisa Mfawidhi wa Forodha wa Kituo cha Huduma cha Pamoja cha Mtukula, Bwana Mohammed Shamte amesema kuwa katika mwaka wa fedha wa 2018/2019, malengo yao ni kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 15.9 kwa mwaka ambapo tayari imeonekana kiwango hicho kitafikiwa kwa kuwa tayari kwa mwezi wanakusanya shilingi bilioni 1.3 ambazo ni wastani wa asilimia 110 hadi 150 ya makusanyo kwa mwezi ambayo yanavuka malengo. 

“Baada ya Serikali kuweka Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, umeongeza spidi na uhakika wa kusafirisha taarifa na data tofauti na hapo awali tulipokuwa tunatumia satelaiti, hivyo Mkongo umewezesha ongezeko la mapato”, amesema Shamte.

Nditiye ameongeza kuwa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano umebadilisha sekta ya mawasiliano nchini na kwenye nchi za jirani zilizounganishwa na Mkongo huo za Uganda, Rwanda, Burundi, Kenya na DRC Congo ambapo wanafurahia huduma za mawasiliano. 

“Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano lazima ulindwe, ni kama reli au barabara, na mawasiliano ni uchumi na maendeleo ambapo unaingiza mapato kwa Serikali yetu,” amesema Nditiye

Pia, amewataka wafanyakazi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation) waendelee kuutunza na kuendesha Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwa kuwa ni watu sahihi, wana utaalamu na ujuzi wa kutosha kufanya kazi na Serikali imewaamini na kuwapa jukumu hilo kwa kuwa mawasiliano ni uchumi na ni usalama hivyo ukicheza na mawasiliano nchi inasambaratika.

Wakiwasilisha changamoto za mawasiliano kwa Nditiye, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misenyi Bi. Thabitha Solomoni amesema kuwa wakati mwingine mtandao unakwenda taratibu au kukosekana hivyo kuathiri usafirishaji wa taarifa na data za watumishi kwa Serikali wa malipo na masuala ya watumishi

Naye Meneja wa TTCL Mkoa wa Kagera Bi. Irene Shayo amejibu changamoto hio kwa kusema kuwa inategemea aina ya kifurushi ambacho Halmashauri husika imenunua na wanachotumia. 

Ametoa rai kwa Halamshauri kutumia wataalamu wao kufahamu uwezo wa mtandao wa intaneti wanaotumia ili uweze kuendana na mahitaji na ukubwa wa taarifa au data wanazotuma au kupokea, hivyo Ofisi za Serikali zizingatie ubora wa huduma kuendana na mahitaji yao na TTCL ina ofisi zake nchi nzima, wako tayari kuwahudumia.

Nditiye amepokea changamoto hiyo kuhusu spidi ya intaneti kwenye ofisi zao na amewataka wataalamu wa TEHAMA  kupeleka mahitaji sahihi ya mtandao wa intaneti kwa Wakurugenzi wa Halmashauri zao na TTCL wako tayari kushauri ili mahitaji yanayotakiwa yaweze kutolewa na TTCL kuendana na mahitaji stahiki

Naye Mkurugenzi wa TEHAMA, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Bwana Mulembwa Munaku amewataka maafisa TEHAMA wote kufungia mitandao ya kijamii muda wa saa za kazi ili mtandao wa intaneti uweze kutumika vizuri kwa matumiz ya Serikali

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti amemweleza Nditiye kuwa bado hakuna mawasiliano ya kuridhisha kwenye maeneo mbali mbali ya mkoa huo licha ya kwamba makampuni yote ya mawasiliano yapo ila bado kuna changamoto ya upatikanaji wa mawasiliano ya uhakika kwenye mkoa huo

Akitoa ufafanuzi kuhusu changamoto hiyo, Nditiye amesema kuwa tayari Serikali imechukua hatua kuhusu jambo hilo kwa kuongeza minara ya mawasiliano kwenye maeneo ya mipakani ambapo mawasiliano ni hafifu kwa kuwaelekeza wataalamu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote kufika kwenye maeneo hayo, kufanya tathmini na kupeleka mawasiliano kwa kuwa hadi sasa watanzania wanapata mawasiliano kwa kiwango cha asilimia 94 isipokuwa maeneo machache. 

Pia ameipa TTCL mwezi mmoja kuhakikisha vocha na laini za TTCL zinapatikana nchi nzima ili kuwawezesha watanzania kuwasiliana kwa kuwa mawasiliano ni uchumi na ni usalama

Nditiye amefanya ziara hiyo ya kukagua miundombinu ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kwenye vituo vya mpakani vya Kabanga, Rusumo Mtukula na Biharamulo

Lowassa Afunguka na Kutoa Ushauri Mzito Kwa Timu Yetu ya Taifa Stars

0
0
Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa amewataka wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, kucheza kama morani wa kimasai katika mechi yao ya  leo Jumanne October 16  dhidi ya Cape Verd uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
 
Katika Taarifa yake kwa vyombo vya habari Lowassa ambaye pia ni mjumbe wa kamati Kuu ya CHADEMA, amewataka wachezaji hao wa Stars kucharuka na kutokuwa legelege uwanjani ili kulipambania Taifa lao.
 
“Kule kwetu masaini tuna vijana shupavu wanaitwa Morani..morani wale wanaua Simba na ni wakali kweli kweli sasa hawa wachezaji wetu wageuke kuwa Morani pale uwanjani..kipigo walichokipata kule kwao(Cape Verde) iwe kama Simba amevamia zizi letu la ng’ombe..wamtoe na kumuua hapana kuwa legelege”Amesema  Lowassa.
 
Aidha Lowassa amelitaka shirikisho la soka nchini TFF kuweka kiingilio cha chini;

 “Nasikia wameweka kiingilio cha shilingi 2000 kule kwa kawaida..mimi ningependa iwe 1000 ili watu waujaze uwanja ule kuwapa moyo Morani wetu”

IGP Simon Sirro, Makamanda wa polisi wapewa maagizo mazito

0
0
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro na Makamanda wote Nchini wameagizwa kuchukua hatua za kuwadhibiti baadhi ya maafisa wanaojihusisha na vitendo vya kupokea rushwa, ubambikizaji wa kesi kwa Wananchi, kutumia nguvu kupita kiasi pamoja na kutoa huduma hafifu kwa Wananchi.

Tazama Video Kamili Hapo Chini

Credit:Azam Tv

Kubenea, Halima Mdee,Mkurugenzi washambuliana ....Uchaguzi Waahirishgwa

0
0
Uchaguzi wa Naibu Meya wa jiji la Dar es salaam jana ulilazimika kuahirishwa kutokana na wajumbe wa mkutano huo kutoafikiana kwa baadhi ya vipengele, ikiwemo kutokukubaliwa kwa hati ya mgombea wa nafasi hiyo aliyetokea (UKAWA) kupitia Chama Cha Wananchi CUF.

Katika mkutano huo ilishuhudiwa baadhi ya wajumbe akiwemo Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea wakiingia kwenye malumbano ya maneno na Mkurugenzi wa Jiji, Sipora Riama juu ya hati ya mgombea huyo.

"Tunaomba hoja iliyotolewa na mjumbe Ndugulile aipokee Mkurugenzi na aseme ameikubali ili twende mbele, mheshimiwa ndugulile  tumuulize Mkurugenzi amekubali kuja na utaratibu mpya kwenye kikao kijacho", alisema Kubenea.

"Kwanini unaingilia majukumu yangu, huyu naye ni (Meya wa jiji) ana maslahi hawezi kutoa miongozo, mimi nina wanasheria hapa, maafisa utumishi ili kusimamia uchaguzi na miongozo mimi ndo natoa", alisema Sipora wakati akizungumza kwa sauti kwenye kikao hicho.

"Nimshukuru Mheshimiwa Ndugulile, kwa kuwa tumekubaliana kuhairisha kikao, naomba UKAWA kupitia chama cha wananchi CUF kipate haki yake ya kupata mgombea wake, tunaomba kikao kinachokuja ajenda moja wapo iwe ni uchaguzi", alisema Mdee kwa kumalizia.

Awali Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia na Wazee na Watoto, Dkt Faustine Ndugulile alitoa ushauri wa kuhairishwa kwa ajenda ya uchaguzi kwenye kikao hicho, hoja ambayo ilikuja kukubaliwa mwishoni mwa kikao.

"Kikao chetu kimedumu kwa zaidi ya saa 4 kitu ambacho nakiona hapa, mjadala huu hautafika mwisho, naomba tuhairishe ajenda ya uchaguzi mpaka siku nyingine"

Jishindie Gari la Bure Toka Japan.....Kushiriki Ni Bure Kabisa

0
0
Kampuni ya Car From Japan huendesha mashindano ya magari ya Bure kabisa  kila mwezi. shindano hili ni Bure na huhitaji kutoa chochote kushiriki.

Mshindi ataletewa gari lake alitakalo hadi nchini mwake 

Zimebaki siku chache tu uibuke mshindi. Mshindi atatangazwa tarehe 31 Mwezi huu. Changamkia dili la bure fasta

Hatimaye TAKUKURU Yamtia Mbaroni Zacharia Hanspoppe

0
0
Baada ya kumsaka kwa muda mrefu, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imemkamata mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu ya Simba, Zacharia Hanspoppe.

Takukuru imemkamata Hanspoppe baada ya kumtangaza katika vyombo vya habari na kumtaka aripoti katika ofisi zake ili kujibu tuhuma zinazomkabili.

Hanspoppe alikamatwa juzi baada ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), saa 8.59 mchana akitokea Dubai.

Akizungumzia kukamatwa kwa mfanyabiashara huyo maarufu, naibu mkurugenzi mkuu wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo alisema, “Ni kweli amekamatwa, alikamatiwa uwanja wa ndege mara tu alipowasili.”

Alisema walipata taarifa kwamba Hanspoppe anakuja nchini na wakawasiliana na watendaji wa Idara ya Uhamiaji.

“Na vijana wetu wakawepo pale wanamsubiri na alipofika tu wakamkamata. Hanspoppe ataunganishwa moja kwa moja mahakamani kesho (leo).”

Pamoja na Hanspoppe mwingine aliyekuwa anatafutwa na Takukuru ni Franklin Lauwo ambaye naibu mkurugenzi huyo wa Takukuru alisema kuwa amekwishawasiliana nao na kudai atajisalimisha mwenyewe mara baada ya kurejea nchini akitokea Pakistan.

Waziri Ndalichako: Elimu Ya Msingi Itaendelea Kuwa Miaka 7 na Si Vinginevyo

0
0
Waziri  wa Elimu, Sayansi na Teknologia Profesa Joyce Ndalichako amesema kwamba wanafunzi wanaosoma kupitia mtaala mpya watasoma kwa kipindi cha miaka saba kama ilivyokuwa awali.

Profesa Ndalichako aliyasema hayo  mjini Pangani wakati wa Kongamano la Elimu wilayani Pangani lililoenda sambamba na harambee ya kuchangia ujenzi wa mabweni ya wanafunzoi shule ya sekondari Mwera mbapo alisema suala la muda wa elimu msingi lipo kwa mujibu wa sheria ya elimu ya mwaka 1982.

Alisema sheria hiyo imeweka bayana kwamba muda wa elimu ya msingi ni miaka saba na bado sheria hiyo haijafanyiwa marekebisho hivyo wanafunzi wanaosoma kupitia mtaala mpya watasoma miaka saba.

Akitolea ufafanuzi suala hilo alisema ikifika mahali kama kutakuwa na ulazima wa kubadilisha miaka ya kwenda shule kitakachotanguliwa ni kufanya marekebisho ya sheria kwa sababu jambo linalokuwa ndani ya sheria huwezi kulifanyia mabadiliko bila kuanza kufanya marekebishi ya sheria husika.

“Niwatoe hofu watanzania kwamba suala la kisheria huwezi kubadilika kwa tamko wala waraka wa kamishna wa elimu au kubadilika kwa maelekezo mengine yoyote bali linaweza kubadilika pale sheria ya elimu 1982 kwenye kipengine kinachoeleza muda wa elimu ya msingi miaka 7 kitakapofanyiwa marekebisho”Alisema Waziri Profesa Ndalichako

Alisema baada ya kufanyiwa marekebisho ndio inaweza kubadilika na haitakuwa kinyumenyume na itaweka bayana kwa sababu badiliko kama hilo ni kubwa la sera na kisheria hivyo watu watafahamu mapema.

“Kumekuwa na mchanganyika kwa sababu sera ya elimu ya mwaka 2014 imeonyesha serikali itakuja kuweka utaratibu lakini haikusema itaweka lini kwamba elimu ya msingi iwe lazima mpaka sekondari”Alisema.

Alisema bado hatujawa tayari kuwa elimu ya msingi na sekondari kwa wanafunzi wote hivyo tunaendelea kuboresha elimu ya msingi na sekondari kuhakikisha mazingira mazuri ya kufundisha na walimu wa kutosha.

Alisema watakapoona wamefika mahali na kuona haja ya kufanya hayo watu wamekuwa wakiulizia serikali itawashirikisha wadau wote kwamba tunakwendaje huku akieleza mkakati ni serikali kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia.

LIVE: Godbless Lema akizungumzia tukio la MO DEWJI kutekwa

0
0
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema anazungumza na Waandishi wa Habari kuhusu tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara maarufu nchini Tanzania Mohamed Dewj na watu wasiojulikana wiki iliyopita ya october 11 2018  katika hotel ya Collesiums.

Msikilize hapo chini

Sakata la Mo Dewji Kutekwa: Watu 19 Akiwemo Haji Manara Waachiwa kwa Dhamana.

0
0
Watu 19 kati ya 26 waliokuwa wakishikiliwa na Polisi kufuatia tukio la kutekwa mfanyabiashara Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’ wameachiwa kwa dhamana jana usiku Oktoba 15, 2018 akiwemo Afisa Habari wa Simba, Haji Manara.
 
Akithibitisha kuachiwa kwa watu hao leo Jumanne, Oktoba 16,  Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa amesema kufuatia kuachiwa kwa watu hao, polisi inaendelea kuwashikilia wengine saba ili kuendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

Manara alishikiliwa na Jeshi la Polisi tangu 12, Oktoba kwa kosa la kusambaza taarifa hizo kwenye mitandao ya kijamii kwa madai ya kutumwa na familia jambo ambalo polisi imesema si za kweli.

Mapema Oktoba 11, baada ya kuenea kwa taarifa za kutekwa kwa mfanyabiashara huyo, Manara alisema kuwa taarifa hiyo ilimshtua kila mmoja na kwamba bado wanawaachia mamlaka husika kufanya kazi yake kumpata mwekezaji wao.

“Wanasimba wawe watulivu wakiliachia Jeshi la Polisi kufanya kazi yake na tunaamini MO atapatikana akiwa hai,” alisema Manara.

Mpaka jana Oktoba 15, walikuwa wameshikiliwa watu 26 kwa mujibu wa Kamanda Mambosasa, ambapo baadaye mchana familia ya mfanyabishara hiyo ilizungumza na vyombo vya habari na kutangaza dau la shilingi bilioni moja kwa mtu yeyote atayefanikisha kupatikana kwa Mohammed Dewji 'Mo Dewji'.

Hanspope afikishwa Mahakamani Leo

0
0
Mwenyekiti wa kamati ya Usajili ya klabu ya Simba, Zacharia Hans Poppe na mfanyabiashara Franklin Lauwo wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Jumanne Oktoba 16, 2018 .

Hans Poppe na Lauwo baada ya kufikishwa mahakamani hapo wamepelekwa moja kwa moja katika chumba cha mahabusu wakisubiri kupandishwa kizimbani.


Mwenyekiti huyo wa usajili wa Simba amefikishwa mahakamani hapo siku moja baada ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kukiri kumkamata Airport akitokea Dubai.


April 2018, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ilitangaza dau nono la Shilingi Milioni 10 kwa yeyote atakayefanikisha kukamatwa kwa mfanyabiashara huyo na mwenzake Frank Lauwo.

Ofa ya Hadithi Tamu za Kusisimua

0
0
OFA YA HADITHI TAMU NA ZA KUSISIMUA
Je umesha soma hadithi hizi mwanzo wake na ukakosa muendelezo.

SORRY MADAM SEASON TWO, TANGA RAHA SEASON ONE na AIISSII YOU KILL ME SEASON ONE
Sasa ni wakati wa kusoma muendelezo wa hadithi hizo zilizo andaliwa kwa utaalamu wa hali ya juu na muandishi wako Eddazaria G.Msulwa. Sasa una weza kupata muendelezo wa hadithi hizo kwa bei  nafuu kabisa.

-SORRY MADAM SEASON THREE(PRESIDENT WIFE) ni sh 8000/= TU
-TANGA RAHA SEASON TWO(RETURN OF OLVIA HITLER) episode moja utaitapa kwa sh 250 UKINUNUA EPISODE 20+20=5000/=
EPISODE 40=40=10000/=
AIISSII YOU KILL ME SEASON TWO(AIISSII YOU KILL ME LEGACY) ni sh 10000/= TU
Pia una weza kupata ofa ya hadithi MPYA KABISA MJINI iitwayo SIN. Episode moja ni sh 250 Tu. UKINUNUA
EPISODE 20+20=5000/=
EPISODE 40=40=10000/=

HADITHI HIZI ZINA PATIKANA KWA WATUMIAJI WA WHATSAPP NA EMAIL TU. WASILIANA NAMI WHATSAPP KWA NAMBA 0657072588 au 0742334453. EMAIL NI eddazariaM@gmail.com 

Una weza kunipigia  simu kwa mamba 0657072588 AU 0768516188
MALIPO NI KUPITIA
 MPESA 0768516188 JOYCE MBWAMBO
TIGOPESA 0657072588 AZARIA MSULWA
NOTE   
UNAPO FANYA MALIPO AU  KABLA YA KUFANYA MALIPO HAKIKISHA UNA WASILIANA NAMI KWENYE NAMBA MOJA WAPO HAPO ILI IWE RAHISI KUKUPATIA HUDUMA KWA UHARAKA SANA. KARIBUBI SANA HADITHI HIZI ZITA KUBURUDISHA NA KUKUPA AFYA NZURI YA UBONGO WAKO.
BY
EDDAZARIA G.MSULWA

Godbless Lema Afunguka sakata la Mo Dewji Kutekwa.....Aitaka Serikali Iruhusu Vyombo vya nje Visaidie Kufanya Uchunguzi

0
0
Waziri Kivuli wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni mbunge wa CHADEMA, Godbless Lema amesema njia pekee ya Serikali kujiondoa katika lawama tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara Mohammed Dewji ‘Mo Dewji’ ni kuruhusu vyombo vya nje kufanya uchunguzi.

Lema ametoa kauli hiyo leo Jumanne Oktoba 16, 2018 katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika makao makuu ya Chadema Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
 
Amesema haitakuwa aibu kwa Serikali kuhusisha vyombo vya nje kwa kuwa hata mataifa yaliyoendelea huwa yanaomba msaada inapobidi.
 
"Kama Serikali inaweza kuomba msaada wa Chandarua kwa ajili ya Malaria kwanini tunashindwa kuomba wasaidizi wa wa nje waje kutusaidia kuchunguza haya matukio ya kiharifu ili wananchi wawe na imani na Serikali .

"Kama serikali inataka kujiondoa katika lawama hizi za kutekwa kwa Mohamed Dewji basi tunaitaka iruhusu wachunguzi wa kimataifa kuja kufanya kazi ya kumtafuta Mohamed Dewji."Amesema Lema

Amesema kwa mazingira ya eneo ambalo Mo Dewji ametekwa kuna ulinzi wa hali ya juu, kushangazwa na mfanyabiashara huyo kutopatikana hadi sasa.

Lema pia amemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola kutozuia watu kujadili tukio hilo.


"Baada ya tukio la kutekwa kwa Mo Dewji Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe Kangi Lugola akatoka hadharani na kuwazuia watu kuongea habari za MO, kuzuia watu kuongea habari za kutekwa na kupotea ni kuzuia watu kulia wakiwa msibani, huu ni msiba.

"Kwa wajibu nilionao Mimi yale maneno ya Kangi kwamba wanasiasa tusitafute umaarufu kwenye tukio la MO Dewji ni ya kupuuza, niko tayari wanikamate lakini siwezi kukaa kimya.


"Hata kama nisingekuwa waziri kivuli nisingeogopa kuongelea swala la MO Dewji kwa sababu ya vitisho, ni bora kupiga kelele ili watu wengine wapone, siwezi kumuogopa Waziri wakati napigania maisha ya wanadamu wenzangu."Amesisitiza Lema


Jana,  familia ya Dewji ilitangaza dau la Sh1bilioni kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa zitakazosaidia kupatikana kwake.

Dewji alitekwa na watu wasiojulikana Alhamisi Oktoba 11, 2018 saa 11:30 alfajiri wakati akiwa Hoteli ya Colosseum.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images