Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Rais Magufuli ampa pole Rais wa Kenya, Uhuru Kenyata

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Joh Pombe Magufuli amemtumia salamu za Pole Rais wa Jamhuri ya Kenya Uhuru Kenya kufuatia tukio la ajali ya basi iliyotokea nchini humo, ambalo zaidi ya abiria 50 wameripotiwa kufariki dunia.

Rais Magufuli ametoa salamu hizo za rambirambi kupitia ukurasa wake wa rasmi wa twitter ambapo ameandika;

 “Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya ajali ya basi iliyotokea Kericho nchini Kenya na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 50. Nakupa pole Rais Uhuru Kenyatta, familia za marehemu na Wakenya wote. Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema na majeruhi wapone haraka.”

Mapema wiki hii Rais Magufuli alipokea Shilingi millioni 125 kutoka kwa serikali ya Kenya kufuatia ajali ya MV Nyerere iliyotokea mwishoni mwa mwezi Septemba katika kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 200.

Makonda Aingilia Kati Sakala la Mabasi ya Mwendokasi..."Viongozi wa Mwendokasi Niwakute Kimara Stand"

$
0
0
Mkuu  wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema hafurahishwi na namna mradi wa mabasi yaendayo haraka jijini humo unavyoendeshwa na kugeuka kuwa kero kwa wananchi badala ya kuwa msaaba kama yalivyokuwa matarajio ya Serikali na wananchi wake.

Makonda amesema hayo leo kupitia ukurasa wake wa Instagram na kuwataka viongozi wanaosimamia mradi huo akutane nao kesho asubuhi katika stendi ya mabasi ya Mwendokasi eneo la Kimara.

“Sifurahishwi na namna mradi wa mwendokasi unavyoendeshwa kwani matarajio ya Mh. Rais Magufuli ni kuona changamoto ya muda mrefu ya usafiri kwa wananchi wa Jiji la Dar es Salaam ikigeuzwa historia kupitia mradi huu.

“Kwa sababu hizo nimeagiza watendaji wote wanaosimamia mwendokasi niwakute Kimara Stand ya mwendokasi kesho saa 12:30 asubuhi wanieleze kwanini hakuna hatua madhubuti walizochukua huku wakishuhudia kero wanazopitia wananchi.

“Nitumie pia fursa hii kuwaomba radhi wananchi kwa kero hii na niwaahidi kuwa jambo hili litapatiwa ufumbuzi hivi karibuni. Tukutane mapema asubuhi mwendokasi kimara.” ameandika Makonda.

Mapema leo Oktoba 10 katika kituo cha mabasi hayo Kimara kimeonekana kuwa mlundikanao wa abiria wengi hadi kusababisha baadhi ya0 kuzirai kwa kukosa hewa ya kutosha huku wengine wakigombania kwa kupita dirishani mara yanapotokea.

Serikali Yampa ONYO Kali Mtendaji Mkuu Mabasi ya Mwendo Kasi Dar

$
0
0
Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo, ametoa onyo kwa Mtendaji Mkuu wa wakala wa usafiri wa mabasi yaendayo kasi jijini Dar es saalam Dart Mhandisi Ronald Lwakatare, kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake na kumtaka kujieleza ni kwanini ameshidwa kumsimamia mtoa huduma UDART.

Pia Mhe. Jafo amemwagiza Naibu Waziri wake Joseph Kakunda leo kufanya kikao kitakacho jumuisha mtendaji mkuu wa Dart pamoja na mtoa huduma UDART   ili kuweza kubaini matatizo makubwa ambayo yamekuwa yakichangia huduma hiyo kudorola kwa siku za hivi karibuni.

“Usafiri huu ulikuwa ni neema sana kwa wakazi wa Dar es salaam ambao wengine walikuwa wanatumia zaidi ya masaa matau kutoka Kimara kwenda Posta lakini leo hii kupitia usafiri huu wanatumia takribani dakika 40 hadi 45 hivyo hatuwezi kuacha huduma ziendele kudorola kwa kiasi hiki”amesema Jafo

Pamoja na kumwagiza naibu Waziri pia Jafo amemtaka katibu mkuu Tamisemi Mussa Iyombe, kufanya uchunguzi katika ofisi ya Dart ili kuweza kuona kama wapo watendaji ambao wanakwamisha huduma hiyo ili kuweza kuwaondoa na kutoa nafasi kwa wengine watakao fanya kwa ufanisi.

Waziri Jafo amesema kuwa onyo hilo kwa mtendaji mkuu wa DART linakuja kutoka na yeye kushindwa kumsimamia mtoa huduma wa mradi huo UDART ambaye ameshindwa  kufanya kazi zake kwa ufanisi.

Aidha amesema kutokana na kushindwa kusimamia kumekuwepo na malalamiko mengi kwa watendaji wa mradi huo wakiwemo madereva pamoja na wakatisha tiketi hali ambayo imesabaisha watu kukosa huduma.

Jafo pia amemwagiza Mtendaji mkuu huyo kuhakikisha mchakato wa kumpata mtoa huduma wa kudumu unafanyika haraka ili kuweza kufanya kazi katika ubora ulio tarajiwa na wananchi.

“Usafiri huu wa mabasi yaendayo kasi ulishalipatia heshima Jiji la Dar es Salaam  hadi kupata cheti cha kuwa na usafiri uliobora na watu kutoka mataifa mbalimbali wamekuwa wakija kujifunza kwetu juu ya mradi huu hivyo hatuwezi kuendelea kuwafumbia macho watendaji ambao hawatimizi majukumu yao”amesema Jafo.

Vijana watakiwa kuwa wabunifu katika kujiajiri

$
0
0
Vijana wametakiwa kuwa wabunifu kwa kuonyesha uthubutu katika kujiajiri kwa kuzithamini kazi wazofanya.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa  Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi na Ajira, Anthony Mavunde, wakati wa ufunguzi wa wiki ya vijana kitaifa inayofanyika katika viwanja vya Tangamano, Jijini Tanga.

Amesema vijana wanatakiwa kuzithamini shughuli wanazofanya kwa kuzipa kipaumbele ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuondokana na dhana ya kuajiriwa.

“Vijana muondokane na mawazo mgando kutegemea kuajiriwa badala yake wajikite katika kujiajiri na Serikali itawapa mikopo kwa ajili ya kukuza mitaji na kuboresha mazingira ya shughuli mnazofanya,” amesema Mavunde.

Katika hatua nyingine  Waziri mavunde amewataka vijana kujitokeza kwa wingi katika sherehe za kilele cha mbio za mwenge zitakazofanyika Oktoba 14, katika viwanja vya Mkwakwani, mjini hapa.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi ya October 11

Waziri Mkuu Atoa Siku 10 Kwa Mkurugenzi Wa Mpwapwa Awe ameshatoa fedha za mikopo kwa vijana, wanawake na walemavu

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim ametoa siku 10 kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa, Bw. Peter Swea awe ametoa fedha za mikopo kwa ajili ya vijana, wanawake na walemavu.

"Leo (jana) ni tarahe 10 nataka hadi ikifika tarehe 20 ya mwezi huu uwe umeshatoa fedha za mikopo kwa wanawake, vijana na walemavu. Habari za mpaka kikao kiridhie hayo ni mambo ya zamani na ndio maana ikatungwa sheria kwa ajili ya jambo hilo. "

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana (Jumatano, Oktoba 10, 2018) wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Kibakwe wilayani Mpwapwa mara baada ya kukagua ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kibakwe, akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Dodoma.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo baada ya Mkurugenzi huyo kumueleza kuwa bado hajatoa fedha kwa ajili ya mikopo hiyo ambazo alipaswa kuzitoa kila robo mwaka, akidai bado kikao cha kuidhinisha hakijakaa.

Amesema fedha hizo ambazo ni asilimia 10 ya mapato ya ndani yanayokusanywa kwenye halmashauri, ambapo anatakiwa kutumia asilimia nne kwa ajili ya mikopo ya wanawake, asilimia mikopo kwa ajili ya vijana na asilimia mbili zitolewe kwa walemavu.

Kadhalika,Waziri Mkuu amewaagiza watendaji wote wa vijiji kuainisha maeneo yote yenye misitu na vyanzo vya maji pamoja na kuwachukulia hatua kali watu wote watakaobainika kukata miti bila kibali.

Amesema mtu yeyote atakayebainika kukata miti bila kibali achukuliwe hatua kali kwa sababu wamekuwa wakisababisha ukosefu wa maji, ambapo wakandarasi wa maji kwenye wilaya hiyo wanapata changamoto ya kukosa maji kwenye maeneo mengo wakati awali  Mpwapwa awali ilikuwa na ardhi ya chepechepe.

"Nimepata habari, hapa Kibakwe watu wanakata miti ili kushindana ubavu wao wa kuishi. Nawaagiza watendaji wote wa vijiji kuainisha maeneo yenye vyanzo vya maji na misitu na muyalinde. Madiwani pia mnatakiwa kushiriki kukemea ukataji miti.”

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Bw. Jabir Shekimweli ameishukuru Serikali kwa kutenga sh. bilioni 1.4 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa vituo vitatu vya afya ambavyo ni Kibakwe, Mima na Pwaga.

Amesema miradi hiyo imesimamiwa vizuri na kamati za ujenzi kwenye kata na vijiji husika kama ambavyo muongozo ulivyoelekeza.

NayeMbunge wa Jimbo la Kibakwe, Bw. George Simbachawene amesema utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) umefanyika kwa mafanikio makubwa kwenye sekta ya afya, umeme na elimu.

Mbunge huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, ameomba ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kutoka Kongwa, Mpwapwa hadi Kibakwe, uharakishwe ili kuondoa adha ya miundombinu inayowakabili wananchi.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU

Waziri Mkuu Abaini Ubadhilifu Halmashauri Ya Mpwapwa

$
0
0
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema atatuma timu maalum kuchunguza wizi unaofanyika kupitia ukusanyaji wa mapato katika halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa na kwamba hakuna atakayethubutu kuharibu ushahidi kwa kuwa nyaraka zote za ukusanyaji anazo.

Ameyasema hayo jana (Jumatano, Oktoba 10, 2018) wakati akizungumza na wafanyakazi wa halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Dodoma.

Amesema hayo baada ya kubaini ubadhirifu kwenye makadirio na ukusanyaji wa mapato unaofanywa na baadhi ya watendaji wa Idara ya Fedha na Mipango kwenye Halmashauri hiyo.
 
Waziri Mkuu amesema maeneo ya ubadhirifu ambayo ambayo ameyabaini ni katika ukusanyaji wa ushuru wa samaki kwenye bwawa la Mtera, Kituo Kikuu cha Mabasi Mpwapwa na kwenye ushuru wa mabango na majengo.

Amesema katika halmashauri hiyo kuna genge la wabadhirifu, ambalo ndilo lililosababisha kufukuzwa kazi kwa Mkurugenzi wa awali wa halmashauri hiyo, ambapo sasa  hawatoi ushirikiano kwa Mkurugenzi aliyekuwepo Bw. Peter Swea kwa kuwa amedhibiti mianya ya ubadhirifu.

Waziri Mkuu akiwa kwenye mkutano huo alimtaka Afisa Mipango wa halmashauri hiyo kusimama na kueleza namna anavyokadiria na kukusanya mapato. "Afisa Mipango hebu tueleze namna unavyopanga katika kukadiria na kukusanya mapato, je unakwenda field "eneo la kazi" au unabandika tu makadirio kwenye makaratasi," amehoji.

Afisa Mipango huyo alieleza kuwa huwa anakwenda kwenye eneo la tukio kabla ya kuandaa makadirio ya mapato na baada ya kutoa maelezo hayo Waziri Mkuu akaeleza namna makadirio na ukusanyaji mapato yaliyofanyika kwenye ushuru wa samaki.

“Katika mwaka wa fedha 2016/2017 ilikadiriwa kukusanywa sh. milioni 80 lakini fedha zilizokusanywa ni sh. milioni 32 na kwenye mwaka wa fedha uliofuata makadirio uliyashusha kwa asilimia 50 lakini fedha zilizokusanya ni sh. milioni 109.”

Kadhalika, Waziri Mkuu amesema kwenye ushuru wa mabango kwa mwaka wa fedha 2016/2017 walikadiria kukusanya sh. milioni tisa lakini fedha zilizokusanywa ni sh. milioni moja sawa na asilimia 17. Pia kwenye mwaka wa fedha 2018/2019 makusanyo yaliyokadiriwa ni sh. milioni saba lakini hadi sasa hakuna fedha zozote zilizokusanywa.

"Kwenye ushuru wa majengo mwaka 2017/2018 makadirio yalikuwa kukusanya sh. milioni 5.5 lakini makusanyo yalikuwa sh.milioni 20 zaidi ya asilimia 360. Hapa tunaweza kusema ulifanya vizuri. Hata hivyo kwenye mwaka huu wa fedha licha ya makusanyo hayo makadirio yaliyowekwa ni kukusanya sh. milioni 5.5 lakini hadi jana hakuna fedha iliyokusanywa.”

Waziri Mkuu amesema kwenye ushuru wa kituo cha mabasi katika mwaka wa fedha 2016/2017 fedha ziliokadiriwa kukusanywa zilikuwa sh. milioni 7.2 na makusanyo yalikuwa sh. milioni 10.6 sawa na asilimia 148 na katika mwaka huu wa fedha makadirio yalikuwa sh. milioni 18 lakini hadi jana hakuna kiasi chochote cha fedha kilichokusanywa.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU

Tanzania Kutunukiwa Tuzo Ya Kimataifa Kwa Kuimarika Katika Udhibiti Wa Usalama Wa Anga


Video Mpya: Vichou ft. Lady Jaydee - KUGATUMBA

$
0
0
Msanii wa muziki, Vichou anakukaribisha kutazama video ya wimbo wake mpya uitwao KUGATUMBA ambao amemshirikisha Lady Jaydee. Itazame hapa.

VIDEO Mpya | Lizzy - Fall In Love

Kesi Ya Walimu Wanaotuhumiwa Kuiba Mitihani Darasa la 7 Yapigwa Kalenda Hadi Octoba 24

$
0
0
Upelelezi wa kesi ya kupata mitihani ya taifa ya darasa la saba inayowakabili walimu watano wa shule ya msingi ya kimataifa ya Hazina iliyopo Magomeni katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu bado haujakamilika.

Wakili wa Serikali, Mwanaamina Kombakono aliyaeleza hayo jana Oktoba 10, 2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Kombakono alidai mahakamani hapo kesi ilipangwa kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wake bado haujakamilika na akaomba ipangiwe tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Baada ya kutolewa maelezo hayo, Hakimu Shaidi aliiahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 24, 2018.

Washtakiwa hao watano wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo ya Hazina, Patrick Cheche (43), mkazi wa Mapinga Bagamoyo na walimu wake Laurence Ochien (30), Justus James (32), Nasri Mohamed (32) na Mambo Idd (32).

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama ya kuingilia mitihani ya Taifa, kupata na kuwaonyesha watahiniwa maudhui ya mtihani na kufanya mawasiliano na watahimiwa.

Breaking News: Mo Dewji Adaiwa Kutekwa Na Watu Wasiojulikana....Zitto Kabwe, January Makamba Wafunguka

$
0
0
Mfanyabiashara maarufu , Mohammed Dewji, anadaiwa kutekwa na watu wasiojulikana waliokuwa na silaha za moto leo saa 11 Alfajiri wakati akiingia kufanya mazoezi Gym ya Colosseum, Oysterbay Dar es salaam.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, inasemekana watu hao wamefyatua risasi hewani kuwatishia watu walikuwa karibu na eneo hilo kabla ya kuondoka naye.

Kamanda wa Polisi Kinondoni, Jumanne Muliro amethibitisha.

Zitto Kabwe na January Makamba ni miongoni mwa viuongozwi walioguswa na taarifa hizi na kuandika yafuatayo

Breaking News: Mbunge wa Ukerewe, Joseph Michael Mkundi Kajiuzulu Ubunge CHADEMA...Katangaza Kuhamia CCM

$
0
0
Mbunge wa Ukerewe, Joseph Michael Mkundi ametangaza kujiuzulu uanachama na nyadhifa zake zote ndani ya CHADEMA, na kuomba kujiunga CCM.

Miongoni mwa sababu alizotoa, ni kutopata ushirikiano kutoka kwa viongozi wenzake (CHADEMA) wakati wa ajali ya MV Nyerere.

"Chama cha Siasa kama Taasisi ya Umma na inayotoa maelekezo Kwetu wawakilishi wa Wananchi, yenyewe inapokuwa msingi wa Kujenga Chuki, uhasama, ubaguzi na Ukinzani na serikali. Taasisi hii inapoteza Uhalali wa Kiuongozi (leadership Legitimacy).

"Kwa Msingi Huo Leo Siku ya Jumatano tarehe 10 Oktoba 2018 natangaza kujivua uanachama wa Chadema na hii ikiwa kwa Mujibu wa Katiba ya Chadema ibara ya 5.4.1,chama ambacho kwa Tiketi yake nilikuwa Diwani wa Kata ya Bukiko na Mbunge wa Jimbo la Ukerewe

"Natangaza kuomba Kujiunga na CCM, Chama ambacho kwa hakika nimeona wakidhihirisha kwa Vitendo Itikadi yao ambayo imejengwa katika misingi ya Utu, Undugu, Mshikamano, Haki na Umoja wa watu wa Tanzania" -Joseph Michael Mkundi 

UPDATES: RPC Lazaro Mambosasa Asema waliomteka mfanya biashara Mohamed Dewji (Mo) ni wazungu wawili

$
0
0
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Lazaro Mambosasa amesema msako mkubwa unafanywa kwa raia wa kigeni wote waliopo nchini kufuatia kutekwa kwa mfanyabiashara Mohammed Dewji

Mambosasa amesema kwamba wameweka vizuizi  kila sehemu kuhakikisha hakuna mtu anayetoka, ili watekaji wasitoke nje ya nchi, na kwamba waliohusika kwenye tukio la kumteka  ni raia wawili wa kigeni.  

Mohammed Dewji, anadaiwa kutekwa na watu wasiojulikana waliokuwa na silaha za moto leo saa 11 Alfajiri wakati akiingia kufanya mazoezi Gym ya Colosseum, Oysterbay Dar es salaam.

Makanga 3 Power; Dawa Bora Nguvu Za Kiume

$
0
0
Kutibu nguvu za kiume dakika(10) na kupona muda wa siku tatu tuu. Kuimarisha misuli ya uume uliolegea, pia ipo Dawa ya kurefusha uume mfupi inchi NNE hadi saba na kunenepesha uume mfupi sentimita NNE.

Tiba ya kudumu kutibu maumivu ya mgongo,kiuno, tumbo kuunguruma na kujaa gesi, kupata choo vizuri, na kutibu uzazi, kutibu busha bila operesheni, kisukari, presha ,miguu kuuma, uzazi, fangas sugu, vidonda vya tumbo.

Ni docta bingwa wa kutibu magonjwa sugu, kutoa ndagu za utajiri kwa kutumia Pete, kazi ,cheni, mikufu maalumu ya bahati, una kesi umedhulumiwa Mali au pesa? Zitarudi muda wa Masaa matatu tuu.

Onana na Dr shilindes shida zako zote zitakwisha, anatoa Dawa za utajiri kwa wafanyakazi, wakulima, na wafugaji, wafanyabiashara na wachimba madini kwa kutumia pete, kazi kwa yeyote anaetaka kuwa na pesa nyingi.

Pia anaboresha akili kwa wanafunzi darasani, masomo na kufaulu mitihani pia kushinda bahati nasibu yeyote.

Pia tunatoa Dawa kumrudisha Mume, mke, mpenzi, hawara, kwa muda wa SAA moja tuu, na kuomba msamaha kwa kukupigia magoti na yeyote yule, unaemtaka kimapenzi au kuoana, utampata na kumfunga asitoke nje ya ndoa daima na kutekeleza shida zako zote. Kupunguza unene, kupunguza matiti makubwa, tumbo na nyama uzembe muda wa siku sita unapata saizi uipendayo.

Kutoa makovu mwilini, chunusi, upele na mabaka, pia tunayo Dawa ya kuongeza hipsi, makalio, mguu wa bia na kupata shepu safi kwa muda wa siku saba tuu.

Wa mikoani mtapata huduma popote mlipo.
Tupo dar es salam mbagala rangi tatu.

Mawasiliano simu namba: 0784 460 348.

Jinsi Punyeto Inavyo Sababisha Kusinyaa Na Kudumaa Kwa Maumbile Ya Kiume

$
0
0
Wanaume  wanao  jihusisha  na  upigaji  wa  punyeto  kwa  muda  mrefu  husalia  kuwa  na  maumbile  ya  kiume  yaliyo  sinyaa  na  kudumaa.

Kwa mujibu  wa  tafiti  mbalimbali  za  kitaalamu, kufanya  punyeto  kwa  muda  mrefu  huathiri  na  kuharibu  mishipa  na  misuli  ya  uume na  hivyo kusababisha  kujengeka  kwa  mafuta na  tishu  zisizo vutika  kwenye  mishipa  ya  ateri na  hivyo  kuzuia  mishipa ya  ateri  kupanuka na  kuongezeka  pamoja  na  damu  kutiririka  kwenda  kwenye  misuli  ya  uume.

Mambo  hayo  mawili yanapotokea  huathiri  uzalishaji  wa homoni muhimu  zinazo  husika  na ukuaji wa misuli ya  uume, na hatimaye  hufanya  uume  wa  mhusika  kudumaa, kusinyaa, kunywea  na  kurudi ndani  kiasi  cha  kuufanya  uonekane  kama wa  mtoto.

 Homoni  hizo hujulikana   kitaalamu kama  HGH  na  huzalishwa  kwenye  ini.

Sababu nyingine   inayo  tajwa  na  wataalamu  ni kwamba, mtu  anaye fanya punyeto   hutumia  akili,  nguvu na  nishati  nyingi sana, jambo ambalo  huathiri utendaji  wa  ogani  nyingine  muhimu  katika  mwili , likiwemo  ini.

Na kwamba  ini  linapo kosa  nishati   ya kutosha  hushindwa  kufanya kazi  zake  vizuri  na  moja  kati  ya  kazi kubwa  za  ini  ni  pamoja  na  uzalishaji  wa  homoni  zijulikanazo  kitaalamu kama  HGH  ambazo  kama  ilivyo andikwa  hapo juu, zinahusika na  kuchochea  ukuaji  wa  sehemu mbalimbali  katika  mwili  wa  mwanadamu  ikiwemo   misuli  ya  uume.

Mbali na  kuathiri  utendaji  wa  ogani  nyingine  mwilini, upigaji  punyeto  husababisha  athari nyingine  kwenye  mwili wa  mwanadamu  kama  vile uchovu  sugu  wa mwili  pamoja na kunyonyoka kwa  nywele.

Athari nyingine  za  upigaji punyeto  ni  pamoja  na  kupoteza  kumbukumbu, kuwahi  kufika  kileleni  ambako  husababishwa  na  kulegea  kwa  mishipa  ya  ateri, kushindwa  kurudia  tendo  la  ndoa, kukosa  hamu  ya  tendo  la  ndoa, uume  kusimama  katika  hali  ya  ulegelege,   maumivu  wakati  wa  tendo  la  ndoa  husuani  wakati  wa  kurudia  tendo  la pili na    mara  baada  ya  tendo  la  ndoa  la  kwanza.

KWANINI   WATU WENGI  WANAO  JIHUSISHA  NA  UPIGAJI  PUNYETO  WANA  MAUMBILE  MADOGO  YA  KIUME YALIYO  DUMAA, SINYAA  NA  KURUDI NDANI.

Uzeofu  unaonyesha  kuwa,  asilimia  kubwa  ya  wanaume  ambao  wamewahi  kufanya  punyeto  kwa  muda  mrefu, wanakabiliwa  na  tatizo  la kuwa  na  maumbile  ya  kiume yaliyo dumaa, sinyaa  na  kurudi ndani.

SABABU  KUBWA   NI  HII  HAPA
Sababu  kubwa  ni kwamba   vijana wengi  wa  kiume, huanza  kujihusisha  na  punyeto   wakiwa  na  miaka  kumi  na sita , kumi na  saba  au  chini  ya  hapo.

Hiki ni  kipindi  ambacho  vijana  hawa  ndio  wanakuwa  wamebalehe.

Na kwa mujibu  wa  tafiti  za kisayansi, katika  kipindi  hiki cha  balehe  ndio  kipindi  ambacho  homoni za  HGH  ambazo huhusika  na  ukuaji  wa  sehemu  mbalimbali  za  mwili  ikiwemo  maumbile ya  kiume, huzalishwa  kwa wingi.

Kama  tulivyo ona  hapo  juu, upigaji  punyeto  huathiri  uzalishwaji  wa   homoni  hizo.

Mwisho wa  siku  maumbile  ya  kiume  ya  wahusika, hushindwa  kukua  na  kuishia  kudumaa na  kusinyaa.

Na  hii ndio  sababu  kubwa  wanaume  wanao  kabiliwa  na  tatizo  hili  husalia  kuwa  na  maumbile yenye  ukubwa  ule  ule  walio kuwa  nao wakati wa  kubalehe

NINI  TIBA  ASILIA  YA  TATIZO  LA  KUDUMAA, KUSINYAA  NA  KURUDI NDANI KWA  MAUMBILE  YA  KIUME.
Kama uume wako  umedumaa, sinyaa, legea, nywea  na  kurudi ndani  kwa  sababu  ulifanya  punyeto  kwa  muda  mrefu  na  unataka  kuondokana  na  hali  hiyo. HII  NI HABARI NJEMA  SANA  KWAKO! 
 
Ipo dawa  ya ASILI   ambayo  HUTIBU  na  KUPONYESHA  KABISA  tatizo la  KUDUMAA, KUSINYAA, KUNYWEA  NA  KURUDI NDANI  KWA MAUMBILE  YA  KIUME kunako  tokana  na  ufanyaji  punyeto  wa  muda  mrefu.
 
Ni  dawa  ya  asili  kabisa ambayo  hutibu  na  kuponyesha  kabisa  tatizo  la kudumaa  na  kusinyaa  kwa  uume  ndani ya siku thelathini.

JINSI YA  KUPATA  TIBA  HII : Kupata  tiba  hii  fika  ka6ika  duka  la  kuuza  dawa  za  aslili  la  NEEMA  HERBALIST.  Tunapatikana  UBUNGO  jijini  DAR  ES  SALAAM  jirani  na  SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING  nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA.

Kwa wateja  waliopo  jijini  Dar  Es  Salaam  ambao  hawana  nafasi  ya  kufika  ofisini  kwetu  watapelekewa  dawa  mahali  walipo  ( HOME & OFFICE  DELIVERY )  na kwa  wateja  waliopo  nje  ya  mkoa  wa  Dar  Es  Salaam  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  usafiri  wa  mabus  au  boti  kwa  waliopo  Zanzibar.

Wasiliana  nasi  kwa  simu  namba  :    0693  005 189.

Makonda Apiga Marufuku Mabasi ya Mwendo Kasi Kuacha Abiria Vituoni....Pia Kawaruhusu Abiria Kupiga Picha

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema ni marufuku kwa dereva yeyote wa mabasi yaendayo kasi kuacha abiria vituoni. Mabasi hayo ni yale ya ‘Express’ ambayo husimama vituo maalumu pekee.

Makonda ametoa kauli hiyo leo alipotembelea kituo cha mabasi cha Kimara na kusikiliza kero za wananchi.

Baada ya kusikiliza kero za abiria katika kituo cha Kimara-Mwisho, Makonda amesema haoni sababu ya madereva kuacha kuchukua abiria vituoni kwa sababu ni Express.

"Nimeshaongea na viongozi, hakuna haja ya gari kupita kwenye kituo na kuacha abiria. Kuanzia sasa hivi wanaotoa huduma za usafiri hakuna abiria kuachwa njiani," amesema.

Makonda amesema usafiri huo ulianzishwa kwa lengo la kurahisisha shughuli kwa wananchi na si kuwachelewesha kama hali ilivyo hivi sasa.

Katika hatua nyingine, RC  Makonda amesema ni  ‘ruksa’ kwa abiria wa mabasi yaendayo kasi kupiga picha kwenye vituo vya mabasi hayo.

Licha ya katazo la kupiga picha kwenye vituo vya mabasi hayo, Makonda amewataka abiria kuwa huru.

Makonda amesema abiria wapige picha ili kuwafichua watoa huduma wavivu na wanyanyasaji.

Amesema ndani ya siku tatu ufumbuzi wa kudumu juu ya kero za usafiri utapatikana.

Kwanini Ushindwe Kumkizi Mwenzi Wako Kwa Tatizo La Nguvu Za Kiume Na Maumbile Madogo Suluhisho La Matatizo Hayo Muone Dr Masele Atamaliza Matatizo Yako

$
0
0
Mbepe; ni dawa ya nguvu za kiume,kurefusha na kunenepesha maumbile madogo kwa muda mfupi.

MHOLA; ni dawa inayotibu kisukari,presha,degedege,kifafa,mwili kupooza, Kipanda uso,kiuno,mgongo,kuzuia mimba isotoke, Kuuma tumbo chini ya kitovu.

NDAGULA; ni dawa ya kuunga mifupa kwa mda mfupi kwa aliye pata ajali na kuvunjika,ataanza kupata nafuu ndani ya siku 14 na kufanya mazoezi

Inhondi; ni kwa wale wenye busha,kuota nyama sehemu ya Siri, Miguu kuwaka moto.

Lukomolo;  Ni dawa ya mvuto wa mapenzi Kumvuta mme, Mke, Mchumba hawala atakutafuta mwenyewe

Tupo mbagala rangi 3, kwa dar huduma utaletewa popote ulipo kwa tiba na ushauli piga no. 0742215230/0787131395/0712757594 dr MASELE

RC Makonda Afunguka Tukio la kutekwa Mo Dewji

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa DSM Paul Makonda amezungumza akiwa eneo la tukio ambalo leo October 11, 2018 Mfanyabiashara maarufu nchini MO Dewji ametekwa akiwa anaingia Gym alfajiri.

Amesema tayari upekuzi umeshaanza katika maeneo yote muhimu hasa kwenye hoteli, nyumba za wageni, mipakani na kwenye viwanja vya ndege kuhakikisha jeshi  linanasa mtandao wa watuhumiwa waliohusika na utekaji huo

RC Makonda amefafanua kuwa miongoni mwa watekaji nyara, wapo wazungu wawili, hali inayoonyesha  kuwa tukio hili limefanywa na wenyeji kwa kushirikisha na  raia hao  wa kigeni.

Amesema  baadhi ya walinzi na wahudumu wa Gym ya Colosseum wamekamatwa ili kulisaidia jeshi la polisi maana wao ndo wanajua ni gari gani ilifika pale, ilikuwa na watu gani na walikaa muda gani

RC Makonda Akanusha Taarifa za Mo Dewj Kupatikana, Atoa Onyo kwa Wanaosambaza uongo

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amekanusha taarifa za kupatikana kwa mfanyabishara Mohammed Dewji, na kwamba taarifa zilizosambaa kuwa amepatikana sio sahihi.

RC Makonda ametoa onyo kali kwa yeyote atakayeibuka na kuanza kusambaza taarifa za uongo kuhusiana na tukio hili au kuligeuza na kulifanya mtaji wa kisiasa.

Amesema msemaji wa tukio hili kwa upande wa polisi ni  Kamanda wa Kanda Maalum Dar Lazaro Mambosasa na kwa upande wa Serikali ni yeye.

Katika hatua nyingine,Makonda, amependekeza  kufungwa kwa kamera katika maeneo yote jijini Dar es salam, ili kupata msaada mkubwa yanapotokea matukio ya kiuhalifu kama hili.

Amesema iwapo Dar es salaam itafungwa kamera, itakuwa msaada mkubwa kwa vyombo vya usalama kufuatilia matukio ya kiuhalifu kama la kutekwa kwa Mo Dewji.

“Tuna mpango mkubwa zaidi nafikiri umefika wakati sasa wa mkoa wa Dar es salaam wote kufungwa camera, leo hii tungekuwa na camera, tungeongezea hata weledi wa jeshi letu la Polisi kufuatilia gari iko wapi, ifike hatua Dar es salaam iwe na camera tukamate wahalifu kwa haraka zaidi, kuliko kutumia nguvu kubwa kumfuatilia mtu ambaye hujui amepita wapi”, amesema Paul Makonda.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images