Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Kamanda Senga Awataja Waliofarikia Kwenye Ajali ya Basi la Arusha Express Iliyotokea Leo

$
0
0
Na John Walter-Babati.
Watu wanne wamefariki dunia na 11 kujeruhiwa baada ya kupata ajali mbaya ya gari la abiria  walilokuwa wakisafiria kutoka Arusha kuelekea Mbeya mara baada ya dereva kushindwa kulimudu wakati akikata kona kwenye eneo la Mlima Haraa wenye kona kali kata ya Bonga mjini  Babati.

Kamanda wa polisi mkoa wa Manyara Agustino Senga amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa 3:15 asubuhi ya leo Oktoba 8-2018 katika Bara bara ya Babati-Dodoma ambapo gari la Abiria kampuni ya Arusha Express lenye namba za Usajili T 750- BYQ Scania likitokea Arusha kuelekea mkoani Mbeya lilimshinda dereva huyo aliefahamika kwa  jina Kennedy Shayo  kurudi upande wa pili wa kulia baada ya kukata kona ya haraka katika eneo lenye mlima na kona nyingi kisha kupinduka na kusababisha vifo na majeruhi kumi.

Waliofariki ni kondakta wa gari hilo Nassibu Ramadhani  (43) mkazi wa Morogoro, Salvatory Thomas mkazi wa Haraa Babati,Laurent Mwanyabala mkazi wa Mbeya (46)Janefredy Mushi,ni mwanafunzi (21) mkazi wa Galapo Babati.

Kamanda wa polisi mkoa wa Manyara, Agustino Senga  amefika katika eneo la tukio na kuthibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba dereva wa gari hilo lililokuwa limebeba abiria 56 alikimbia kusikojulikana baada ya ajali.

“Tutamtafuta dereva popote alipo kamahatojisalimisha, jitihada za kumtafuta dereva zinafanyika na chanzo cha ajali ni kushindwa kulimudu gari kwenye kona.” alisema Kamanda Senga.

Miili ya marehemu wote imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Babati Mrara kwa ajili ya maandalizi ya mazishi.

Shahidi Akwamisha Kesi ya Lugha Chafu Kwa Rais Inayomkabili Halima Mdee

$
0
0
Mahakama  ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Oktoba 8 mwaka 2018 imeshindwa kuendelea kusikiliza kesi ya kutoa lugha chafu ya matusi dhidi ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli inayomkabili Mbunge wa Kawe, Halima Mdee  kwa sababu shahidi wa upande wa mashtaka aliyetarajiwa kutoa ushahidi hakufika.

Wakili wa Serikali Mwandamizi Mwita amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa kesi hiyo ilipangwa kwa ajili ya kusikilizwa lakini shahidi hajafika leo.

Alidai shahidi waliyemtarajia kutoa ushahidi katika kesi hiyo, walimtumia wito lakini kwa bahati mbaya yupo nje ya Mkoa wa Dar es Salaam, aliiomba mahakama kuipangia tarehe nyingine kesi hiyo.

Hakimu Simba ameiahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 22, mwaka huu kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka.

Katika kesi hiyo tayari mashahidi watatu wa upande wa mashtaka wamekwishatoa ushahidi katika kesi hiyo akiwamo  mkuu wa Kituo cha Polisi cha Urafiki, Mrakibu wa Polisi (SP) Batseba Kasanga.

Mdee anadaiwa,  Julai 3,2017  katika ofisi za Chadema alitamka maneno dhidi ya  Rais John Magufuli kuwa  “anaongea hovyohovyo , anatakiwa  afungwe breki”  na kwamba kitendo ambacho kingeweza  kusababisha uvunjifu wa amani.

Waraka wa Tundu Lissu Akipangua Hoja ya Katibu Mwenezi CCM, Humphrey Polepole

$
0
0
Hoja ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole ya kwamba wapinzani watakaoshindwa kujiunga na chama hicho mwaka huu wasubiri hadi uchaguzi mkuu ujao, imemuibua mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) Tundu Lissu akihoji uhalali wa hamahama hiyo.

Jana Polepole aliandika katika ukurasa wake wa Twitter “Tumezingatia na tunaweka jitihada zetu zote katika kushughulika na utatuzi wa shida za watu wetu wa Tanzania. Mwaka 2018 ndio mwisho kwetu kufanya chaguzi ndogo za ubunge kwa wale wanaohama vyama vyao na kujiunga na CCM. Watakaoikosa round hii mbaki hukohuko tutakutana 2020,”.

Wakati Polepole akisema hayo, aliyekuwa mbunge wa Simanjiro (Chadema) James Ole Millya alitangaza kukihama Chadema na kujiunga na CCM akiwa mbunge wa saba wa upinzani kujiunga na chama tawala.

Kauli hiyo imewaibua wanasiasa mbalimbali wakipinga kile kilichosemwa na Polepole akiwamo Lissu ambaye yupo nchini Ubelgiji akiendelea na matibabu.

Katika waraka wake uliotolewa leo, Oktoba 8, Tundu Lissu amesema hamahama ya viongozi wa  Chadema haiwezi kukiua chama hicho kwa sababu wanaohama Chadema ni wageni na hawajashiriki katika kukijenga chama hicho kikuu cha upinzani nchini.

“Katibu Mwenezi wa CCM, Polepole, amesema kwamba mwisho wa 'kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli za kuwaletea wananchi maendeleo' ni Desemba 2018. Kwa nini zuio hilo la CCM linalingana ama kukaribiana na zuio la kikatiba na kisheria kwa chaguzi za marudio?" Ameandika Lissu

“Je, hii ni bahati mbaya tu au kuna njama iliyofichwa kwenye hii ratiba ya CCM na ratiba iliyowekwa na Katiba na Sheria za Uchaguzi?,”Amesema.

Amesema licha ya wabunge hao kuhama, Chadema itabaki kuwa imara huku akiwataka Watanzania kufikiria kwa undani juu ya kwanini viongozi hao wanahama hasa kipindi hiki.

“Huu mjadala wa hama hama ya wabunge wa Chadema ni muhimu sana. Unahitaji kujadiliwa kwa tahadhari na kwa umakini, vitu ambavyo ni adimu katikati ya kelele na vumbi kubwa vilivyotokana na hama hama hii,” amesema.

Amesema wabunge wote wanaokihama Chadema hivi sasa ni wapya na wengi wao walijiunga na Chadema kutokana na vuguvugu la Lowassa kuhamia Chadema mwaka 2015.

“Baadhi, kama Dk Mollel wa Siha na Ole Kalanga wa Monduli, waliingia  Chadema na bungeni kutokana na wimbi la Lowassa la '15. Baadhi, kama Waitara, Ryoba na Ole Millya, wana muda mrefu Chadema lakini ni wabunge wapya,” ameandika Lissu.

Amehoji “Kwani kujiuzulu ubunge au udiwani wa Chadema na baadaye kugombea nafasi zile zile kwa CCM ni njia pekee ya kumuunga mkono Magufuli? Kumbuka, John Shibuda wa Chadema na John Cheyo wa UDP walikuwa wakiunga mkono jitihada za Rais Kikwete (Jakaya) lakini hawakuwahi kujiuzulu ubunge au uanachama wa vyama vyao.”

Amesema sababu inayotolewa na wabunge hao ya kuwapo kwa migogoro ndani ya vyama pinzani si ngeni lakini ameshangazwa na wimbi la wabunge hao kuhamia CCM.

Wabunge sita waliohamia CCM ni Maulid Mtulia (Kinondoni-Cuf),Dk Godwin Mollel (Siha-Chadema) Julius Kalanga (Monduli-Chadema), Mwita Waitara (Ukonga-Chadema), Zuberi Kuchauka (Liwale-CUF),  Marwa Chacha (Serengeti-Chadema) huku  Lazaro Nyalandu (Singida Kaskazini) akitoka CCM kwenda Chadema.

Ahadi ya Rais Magufuli kwa Bibi aliyedhulumiwa kiwanja yatimizwa na Waziri Mabula

$
0
0
 Na Munir Shemweta,  Mara
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angeline Mabula amemkabidhi Bibi Nyasasi Masige  Hati za viwanja viwili vilivyopo eneo la Bunda mkoa wa Mara na kutoa onyo kwa wataalamu wa ardhi kutotoa ushauri potofu kwa viongozi wa serikali  wakati wa utekelezaji wa majukumu ya sekta ya ardhi.


Utoaji wa hati kwa bibi Masige unafuatia bibi huyo kuwasilisha malalamiko kwa mhe Rais John Pombe Magufuli  wakati wa ziara yake katika wilaya ya Bunda mkoa wa Mara kutaka kudhulumiwa viwanja vyake. Hati za viwanja  alivyokabidhiwa bibi Masige ni za viwanja  Na 92 na  93/ Kitalu S/ Nyasula C vilivyopo katika wilaya ya Bunda mkoa wa Mara.

Mabula alikabidhi hati hizo pamoja na hati nyingine 92 kwa wananchi wa Bunda leo akiwa katika ziara ya siku tano katika mkoa wa Mara  kufuatilia utekelezaji wa maagizo aliyatoa katika ziara yake ya februari mwaka huu 2018 katika mkoa wa Mara.

Alisema serikali inategemea wataalamu katika kuendesha shughuli zake na kitendo cha wataalamu kutoa ushauri potofu ikiwemo suala la viwanja vya bibi Masige siyo tu kunawapoteza viongozi katika kutekeleza majukumu yao  bali kunachangia kuwepo migogoro katika sekta ya ardhi.

"haiwezekani kupima viwanja na kuchanganya viwanja vidogo, vikubwa na vya kati na kama mtaalamu ukienda kinyume utachukuliwa hatua kwa kutozingatia taaluma."" Alisema Mabula.

Kauli hiyo ya Mabula inafuatia Kauli ya Mkuu wa wilaya ya Bunda Lydia Mpilipili kueleza kuwa tatizo la viwanja vya bibi Masige lisingefikia hatua hiyo kama wataalam wa ardhi wangetoa ushauri sahihi kwa viongozi wa wilaya katika kushugulikia mgogoro wa bibi huyo.

Aidha,  Naibu Waziri wa ardhi,  Nyumba na Maendeleo ya Makazi alitoa rai kwa wananchi wakati akikabidhi hati kupeleka kero zao za migogoro ya ardhi kwa viongozi ili ziweze kushughulikiwa sambamba na kutaka watendaji wa sekta ya ardhi kutekeleza maagizo yanayotolewa na viongozi na kuyafanyia kazi .

Bibi Masige alitoa malalamiko ya kudhulimiwa viwanja vyake kwa mhe Raisi wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli wakati wa ziara yake 05 septemba 2018 wilayani Bunda mkoa wa Mara ambapo mhe Raisi aliagiza kusimamishwa kazi kwa Kamishna Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Ziwa  Joseph Shewiyo  Kwa kushindwa kusimamia agizo la Waziri wa ardhi William Lukuvi kuhusiana na viwanja vya bibi huyo.

Vile. Vile,  katika kutekeleza agizo la Rais Waziri wa ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi  naye alifanya ziara katika wilaya Bunda mkoa wa Mara wa lengo la kushughulikia tatizo la bibi huyo tarehe 18 Septemba 2018.

Rais Magufuli Kakutana na Viongozi Mbalimbali Ikulu Leo Na Kukubali Kuteuliwa kuwa makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC)

$
0
0
Rais John Magufuli, amepokea rasmi taarifa ya uteuzi wa kuwa makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC),  kwa mwaka mmoja kuanzia Agosti 2018 - Agosti 2019.

Taarifa hiyo imekabidhiwa kwa Rais Magufuli leo Oktoba 8, 2018 na Katibu mtendaji wa Jumuiya hiyo Dkt. Stergomena Tax, ambaye amesema amekutana na Rais Magufuli ili kumpa taarifa ya uteuzi uliofanyika kupitia mkutano mkuu wa 38 wa SADC ambao ulifanya Agosti 17-18, 2018 mjini Windhoek nchini Namibia.

Taarifa ya Ikulu imeeleza kuwa kufuatia uteuzi huo sasa Rais Magufuli atakuwa ndiye Mwenyekiti wa SADC ajaye katika kipindi cha mwaka 2019/2020 ambapo atahudumu kwa mwaka mmoja kama ilivyokawaida.

Kwa upande wake Rais Magufuli ameeleza kuwa ameupokea kwa heshima kubwa uteuzi huo na yupo tayari kufanya kazi hiyo kwa kushirikiana na wenzake kwa manufaa ya nchi zilizopo kwenye jumuiya hiyo.

Waziri Mkuu: Mhasibu Wa Mapori Arejeshwe Kwenye Nafasi Yake

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Meneja wa Mapori ya akiba ya Buligi, Biharamulo na Kimisi Bw. Bigilamungu Kagoma amrudishe Mhasibu wa mapori hayo Bw. Adam Kajembe katika nafasi yake.

Ametoa agizo hilo baada ya Meneja wa Mapori hayo Bw. Kagoma kumuondoa mhasibu huyo  na kumteua Bibi Ruth Philemon ambaye ni Mhifadhi wa Wanyamapori kuwa mhasibu wa mapori hayo.

Ameyasema hayo leo (Jumatatu, Oktoba 8, 2018) wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Biharamulo kwenye ukumbi wa JWTZ na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Biharamulo.

Waziri Mkuu amesema Meneja wa Mapori hayo hana mamlaka ya kuteua watumishi wa mapori hayo hivyo amemuagiza amuondoe haraka Bibi Ruth katika nafasi aliyompa na kumrudisha Bw. Adam kwenye nafasi yake.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amepiga marufuku wananchi kuingiza mifugo katika mapori ya akiba ya Biharamulo, Buligi na Kimisi.

Amesema mapori hayo kwa sasa yapo katika hatua za mwisho kutangazwa kuwa mbuga za wanyama, hivyo kuifanya wilaya hiyo kuwa miongoni mwa wilaya za kitalii nchini.

Waziri Mkuu amemuagiza Meneja anayesimamia mapori hayo, Bw. Kagoma ahakikishe mapori hayo yanalindwa na hakuna mifugo inayoingizwa.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, OKTOBA 8, 2018.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne Ya Septemba 9

Sakata la Kawaha ....Rais Magufuli Kaagiza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, OCD, Mkuu wa Upelelezi, Mkuu wa Kituo Kyerwa Wasimamishwe Kazi

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  ameagiza kusimamishwa kazi mara moja kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera Augustine Ollomi, Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Kyerwa Justine Joseph, Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Kyerwa Everist Kivuyo na Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Kyerwa Robert Marwa.

Viongozi hao wa Polisi wanasimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za kuhusika katika magendo ya zao la kahawa katika Wilaya ya Kyerwa pamoja na tuhuma nyingine.

Aidha,Rais Magufuli amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Mej. Jen Jacob Kingu na Inspekta Generali wa Polisi Simon Sirro kuhakikisha uchunguzi wa kina unafanyika na hatua stahiki zinachukuliwa endapo watabainika kuhusika katika magendo ya kahawa na makosa mengine kwa mujibu wa sheria.

Tuhuma dhidi ya viongozi wa polisi katika Wilaya ya Kyerwa zimebainika  wakati wa ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa.

Tanzania Kushiriki Mazoezi Ya Kikosi Cha Dharura Cha Ulinzi Wa Amani Cha Sadc Nchini Malawi

$
0
0
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) zimejipanga kuzuia na kudhibiti madhara yanayosababishwa na machafuko ya kisiasa katika jumuiya hiyo na Bara la Afrika kwa ujumla. 

Wawakilishi wa nchi hizo wamekusanyika nchini Malawi kuanzia tarehe 1 Oktoba hadi 17 Oktoba 2018 kwa ajili ya kufanya mazoezi ya namna ya kutuliza ghasia pamoja na kutoa misaada ya kibinadamu kwa waathirika katika kipindi cha machafuko

Wawakilishi wa Tanzania kutoka Jeshi la Wananchi, Magereza na taasisi za kiraia ikiwemo Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ni miongoni mwa watu 600 wanaoshiriki zoezi hilo lililopewa jina la EX UMODZI CPX 2018 na kaulimbiu ya Afrika ni Amani na Maendeleo (Africa for peace and prosperity).

Katika hafla ya ufunguzi wa mazoezi hayo iliyofanyika leo tarehe 08 Oktoba, 2018 katika Chuo cha Kijeshi cha Malawi kilichopo mji wa Salima takriban kilomita 120 kutoka Lilongwe, Naibu Waziri wa Ulinzi wa Malawi, Mhe. Evaton Chemulirenji alisema mazoezi hayo ni utekelezaji wa maazimio ya SADC na Umoja wa Afrika (AU) wa kuandaa kikosi cha kukabiliana na machafuko barani Afrika (Standby Force-SF) ambacho kinatakiwa kiwe kimekamilika ifikapo Januari 2019.

Alisema madhumuni ya mazoezi hayo ni kuhakikisha kuwa kikosi cha SF kinapewa mafunzo ya vitendo ya kutosha ili kiwe na ujuzi na mbinu za kushiriki operesheni za kulinda amani na/au kuingilia kati na kuzuia machafuko (peace keeping and enforcement) pale yanapotokea barani Afrika. Aidha, alisema mazoezi hayo ni muhimu kwa kuwa yatasaidia kuimarisha ushirikiano na kuaminiana baina ya nchi wanachama wa SADC.

Mazoezi hayo yanajumuisha makundi mbalimbali ikiwa ni pamoja na majeshi  ya ulinzi,  askari polisi, askari magereza na raia wa fani tofauti kama vile za Utawala wa Sheria, siasa, mawasiliano, Utawala, haki za binadamu na jinsia ambao wana mchango mkubwa katila masuala ya operesheni za kulinda amani.

Wanajeshi watafanya zoezi la namna ya kutuliza machafuko na raia watajifunza namna ya kusaidia jamii punde tu machafuko yanapodhibitiwa na vikosi vya usalama.
 
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki,
Salima,Malawi

Video Mpya: Amber Lulu X Mr LG - Vuruga

$
0
0
Msanii wa muziki Bongo, Amber Lulu anakukaribisha kusikiliza wimbo wake mpya uitwao Vuruga. Isikilize hapa.

Alikiba, Diamond, Harmonize, Vanessa Mdee Waambulia Patupu AFRIMMA 2018

$
0
0
Usiku wa kuamkia jana kulitolewa tuzo za African Muzik Magazine Awards (AFRIMMA) 2018 nchini Marekani.

Wasanii wote kutoka Tanzania waliotangazwa kuwania tuzo hizo wametoka mikono mitupu, huku wasanii kutoka Kenya na Uganda wakifanya vizuri.

Wasanii wa Bongo wa Fleva waliokuwa wakiwania ni pamoja na Jux, Diamond Platnumz, Ommy Dimpoz, Navy Kenzo, Alikiba, Harmonize, Vanessa Mdee na Nandy.

Rapper kutokea nchini Kenya, Khaligraph Jones ameshinda kwenye kipengele cha Best Rap Act, huku Eddy Kenzo kutoka Uganda kwenye kingele cha The East African Artist of the Year.

Avril Ampa mkono Khaligraph Jones kwa kupeperusha Bendera ya Kenya Marekani

$
0
0
Staa wa muziki na Muigizaji kutoka nchini Kenya, Judith Nyambura Mwangi a.k.a Avril amempa pongezi ya ushindi wa tuzo ya AFRIMMA 2018 rapa Khaligraph Jones.

Mrembo Avril alimpongeza Khagraph kwa tuzo ya ushindi ya kipengele cha ‘Best Rap Act’ cha tuzo zilizofanyika usiku wa kuamkia jana  huko Dallas Texas Marekani.

Avril alindika ujumbe huu kwenye ukurasa wake wa Instagram ulioambatana na Picha ya Khaligraph Jones.

“Waking up to great news .. congratulations @khaligraph_jones 🙌🏼 #BestRapAct 🇰🇪 #Afrimma 🇰🇪 #KenyaToTheWorld #KeepYourOwnPace ”

Khaligraph Jones aliwapiga chini wakali wenzake kibao kwenye kipengele hicho cha tuzo .Pia Khaligraph alipata nafasi ya kutoa burudani kwenye jukwaa la Tuzo hizo zilizowakutanisha mastaa mbalimbali kutoka Afrika.

Naibu Waziri Mabula Akagua Majalada Ya Ardhi Serengeti Na Kuwapigia Simu Waliocheleweshewa Hati

$
0
0
Na Munir Shemweta,  WANMM Serengeti
Katika kile kinachoonekana kútekeleza kauli mbiu ya serikali ya awamu ya tano ya hapa kazi tu,  Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Angeline Mabula amekagua majalada ya ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Serengeti mkoa wa Mara na kuwapigia simu wananchi ambao majalada yao yana muda mrefu bila ya kupatiwa hati za ardhi.

Akiwa katika oisi ya kutunzia majalada katika halmashauri ya Serengeti  Mabula alikagua jalada moja hadi jingine na kubaini badhi ya majalada yakiwa na muda mrefu huku wananchi wakiwa hawajapatiwa hati ambapo baadhi yake ni za  tangu mwaka 2017 na kumhoji afisa ardhi mteule suala la kuchelewa kuwapatia hati za ardhi pamoja na wahusika kujaza fomu za maombi.

Mabula alielezwa kuwa baadhi ya wananchi wameshindwa kupatiwa hati kwa wakati kutokana na kushindwa kukamilisha baadhi ya taratibu pamoja na jitihada mbalimbali zilizofanywa na maafisa ardhi wa halmashauri kuwakumbusha jambo lillilomshtua Naibu Waziri kwa kuwa wananchi wengi wamekuwa na  shauku kubwa ya kupatiwa hati.

Katika kujiridhisha na maelezo ya afisa ardhi mteule wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti,  Mhe.  Mabula aliamua kumpigia mwananchi aliyejitambulisha kwa jina la Stanslaus na kumuuliza kwa nini hajapatiwa hati katika kiwanja Na 619 kitalu B Chamoto wakati aliwasilisha maombi ya kupatiwa hati.

Mwananchi huyo alipopokea simu na kuelezwa kuwa aliyekuwa akiongea naye ni Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na alikuwa akihoji maombi yake ya hati ya ardhi aliyoyawasilisha  ofisi za halmshauri ya wilaya ya Serengeti,  alishangaa kwa kuwa  muda aliopigiwa simu majira ya saa kumi na mbili jioni  haukuwa muda wa kazi.

Mwanachi huyo mkazi wa Mugumu wilaya ya Serengeti alimueleza Mabula kuwa  alielezwa kuwa hati yake haijafika na yeye hakuelewa kama kuna taratibu hajazikamilisha ili apatiwe hati ingawa alishapatiwa hati za viwanja vingine viwili alizoomba katika halmshauri hiyo.

Kufuatia hali hiyo Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi  aliwataka watendaji wa sekta ya ardhi katika halmshauri ya Wilaya ya Serengeti kuhakikisha inawafuatilia waombaji wote wa ardhi na kuwasaidia kuwaelekeza taratibu  zitakazowawezesha kupata   hati zao bila usumbufu wowote.

Alisema,  serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuli haitaki kuona wananchi wanasumbuka katika kupatiwe hati za ardhi kwa kuwa hati hizo ni haki yao na zitawasaidia katika shughuli zao za kiuchumi hivyo alitaka wahusika wafahamishwe kwa njia ya simu pamoja na barua kwa lengo la kuweka kumbukumbu sawa.

Aakikagua  majalada ya ardhi katika halmshauri ya Serengeti, Mabula alibaini utunzaji wa majalada usiofuta taratibu na kuamuru watendaji wa sekta ya ardhi kuhakikisha taratibu zote katika kushughulikia  majalada ya ardhi ikiwemo maelekezo kutoka afisa mmoja kwenda kwa mwingine yanazingatiwa ili kuepuka ujanja unaoweza kufanywa katika majalada hayo na kuleta usumbufu kwa waombaji hati.

-----------MWISHO------------

Dawa za Asili ya Kuzuia Mimba kutoka, Mtu Aliyepata Ajali, Degedege, Busha, Kuota Nyama Sehemu za Siri

$
0
0
Mbepe; ni dawa ya nguvu za kiume,kurefusha na kunenepesha maumbile madogo kwa muda mfupi.

MHOLA; ni dawa inayotibu kisukari,presha,degedege,kifafa,mwili kupooza, Kipanda uso,kiuno,mgongo,kuzuia mimba isotoke, Kuuma tumbo chini ya kitovu.

NDAGULA; ni dawa ya kuunga mifupa kwa mda mfupi kwa aliye pata ajali na kuvunjika,ataanza kupata nafuu ndani ya siku 14 na kufanya mazoezi

Inhondi; ni kwa wale wenye busha,kuota nyama sehemu ya Siri, Miguu kuwaka moto.

Lukomolo;  Ni dawa ya mvuto wa mapenzi Kumvuta mme, Mke, Mchumba hawala atakutafuta mwenyewe

Tupo mbagala rangi 3, kwa dar huduma utaletewa popote ulipo kwa tiba na ushauli piga no. 0742215230/0787131395/0712757594 dr MASELE

Makanga 3 Power; Dawa Bora Nguvu Za Kiume

$
0
0
Kutibu nguvu za kiume dakika(10) na kupona muda wa siku tatu tuu. Kuimarisha misuli ya uume uliolegea, pia ipo Dawa ya kurefusha uume mfupi inchi NNE hadi saba na kunenepesha uume mfupi sentimita NNE.

Tiba ya kudumu kutibu maumivu ya mgongo,kiuno, tumbo kuunguruma na kujaa gesi, kupata choo vizuri, na kutibu uzazi, kutibu busha bila operesheni, kisukari, presha ,miguu kuuma, uzazi, fangas sugu, vidonda vya tumbo.

Ni docta bingwa wa kutibu magonjwa sugu, kutoa ndagu za utajiri kwa kutumia Pete, kazi ,cheni, mikufu maalumu ya bahati, una kesi umedhulumiwa Mali au pesa? Zitarudi muda wa Masaa matatu tuu.

Onana na Dr shilindes shida zako zote zitakwisha, anatoa Dawa za utajiri kwa wafanyakazi, wakulima, na wafugaji, wafanyabiashara na wachimba madini kwa kutumia pete, kazi kwa yeyote anaetaka kuwa na pesa nyingi.

Pia anaboresha akili kwa wanafunzi darasani, masomo na kufaulu mitihani pia kushinda bahati nasibu yeyote.

Pia tunatoa Dawa kumrudisha Mume, mke, mpenzi, hawara, kwa muda wa SAA moja tuu, na kuomba msamaha kwa kukupigia magoti na yeyote yule, unaemtaka kimapenzi au kuoana, utampata na kumfunga asitoke nje ya ndoa daima na kutekeleza shida zako zote. Kupunguza unene, kupunguza matiti makubwa, tumbo na nyama uzembe muda wa siku sita unapata saizi uipendayo.

Kutoa makovu mwilini, chunusi, upele na mabaka, pia tunayo Dawa ya kuongeza hipsi, makalio, mguu wa bia na kupata shepu safi kwa muda wa siku saba tuu.

Wa mikoani mtapata huduma popote mlipo.
Tupo dar es salam mbagala rangi tatu.

Mawasiliano simu namba: 0784 460 348.

Waziri Mkuu Atoa Siku Mbili Kwa Afisa Elimu Muleba

$
0
0
* Ifikapo Jumatano awe amepeleka walimu shule ya msingi Rwenzige
*Ina wanafunzi 216 wa darasa la awali hadi la nne bila mwalimu


 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa siku mbili kwa Kaimu Afisa Elimu (Msingi) wa wilaya ya Muleba, mkoani Kagera Bw. Bukuru Malembo awe amepeleka walimu wawili katika shule ya msingi iliyoko kwenye kitongoji cha Rwenzige kwa kuwa haina mwalimu hata mmoja.

Shule hiyo yenye madarasa wawili na ofisi moja ya mwalimu ina jumla wanafunzi 216 wa darasa la awali hadi la nne, ilijengwa na wananchi ambapo wanafunzi wake wanafundishwa na mwananchi mmoja aliyemua kujitolea ili kuwapunguzia watoto kutembea umbali wa kilomita 16 kwenda kusoma katika shule ya kijiji cha Kiteme.

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana (Jumatatu, Oktoba 8, 2018) baada ya wanafunzi wa shule hiyo kuwasilisha malalamiko yao kwa njia ya bango wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kiwanja cha kituo cha afya Kimeya, baada ya kukagua majengo ya kituo hicho.

“Haiwezekani watoto wadogo wenye umri wa kuanzia miaka mitano wakatembea umbali wa kilomita 16 kwenda shule wakati katika kitongoji chao kuna shule yenye madarasa mawili na chumba kimoja cha ofisi ya mwalimu na Afisa Elimu hadi sasa hajapeleka walimu na kumuachia mwalimu Benson (kijana ambaye si mwalimu ila anajitolea kufundisha) akifundisha wanafunzi hao peke yake.”

Waziri Mkuu alimuagiza Afisa Elimu huyo ahakikishe ifikapo Jumatano (Oktoba 10, 2018) saa nne asubuhi awe ameshawapeleka walimu hao katika shule hiyo ya msingi ili waweze kuwafundisha wanafunzi hao na kisha Mkuu wa wilaya hiyo, Mhandisi Richard Ruyango awasilishe taarifa ya utekelezaji wa agizo hilo ofisini kwake. “Walimu wengi mmewaacha katika shule za barabarani huku za vijijini zikiwa hazina walimu.”

Kwa upande wake, Bw. Benson Bukerebe (29) maarufu mwalimu Benson alisema yeye kitaaluma si mwalimu bali ni mhitimu wa kidato cha nne, alimua kuanzisha darasa kwa ajili ya kuwafundisha wanafunzi hao kwani alikuwa akiwahurumia kwa sababu baadhi yao hawakuwa na uwezo wa kutembea umbali wa kilomita 16 hadi iliko shule ya msingi ya Kiteme.

Kijana huyo alisema kwa muda wote huo ameweza kumudu kuwafundisha wanafunzi hao kwa kutumia vitabu vya kuazima kutoka shule mbalimbali za msingi, lengo ni kuhakikisha watoto wenye umri wa kuanza shule katika kitongoji chao wanapata fursa ya elimu ambayo ni haki yao ya msingi.

Katika hatua nyingine,Waziri Mkuualisema Serikali imeweka sheria kali ili kuwalinda watoto wa kike na wanatakiwa kuheshimiwa katika jamii kwa kuachwa waendelee na masomo yao bila ya usumbufu wa aina yoyote na atakayebainika kukatisha masomo yao atachukulia hatua kali za kisheria.

Alisema Serikali  itatoa adhabu kali ya kifungo cha miaka 30 jela kwa mtu atakayekatisha elimu ya mtoto wa kike iwe kwa kumuoa, kumpa ujauzo na hata ukikutwa naye nyumbani kwako na katika nyumba ya wageni.

“Tukikukuta na binti wa shule katika kona isiyoeleweka tunakukamata na kukuchukulia hatua za kisheria. Ole wenuvijana, mkibainika mmewapa mimba mabinti wanaosoma, adhabu yake ni miaka 30 jela.”

Waziri Mkuu alisema kwa wazazi au walezi watakaowaozesha watoto kike ambao bado ni wanafunzi na kwa upande wa wazazi watakaomsindikiza mtoto wao wa kiume kwenda kuoa mwanafunzi wote watachukuliwa hatua za kisheria.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, OKTOBA 9, 2018.

Aliwa na Mamba Akiogelea Ziwa Tanganyika

$
0
0
Mkazi  wa Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa, Msema Msafiri maarufu kwa jina la Giriki (35), ameliwa na mamba, alipokwenda katika mwambao wa Ziwa Tanganyika kuogelea.

Imeelezwa kuwa Msafiri, mkazi wa Kitongoji cha Lyela kilichopo mwambao wa Ziwa Tanganyika katika Kijiji cha Izinga Kata ya Wampembe, alikwenda kuogelea kutokana na joto kali alilokuwa akilihisi.

Alikumbwa na mkasa huo Ijumaa majira ya mchana, baada ya kuingia ziwani na kuanza kuogelea.

Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa Kijiji cha Izinga, George Fataki, alisema kuwa kijana huyo alikuwa ni mgeni katika kitongoji hicho na alikuwa ametokea mkoani Kigoma katika Kijiji cha Kalago na kwenda katika katika kitongoji hicho ambacho ni makazi ya wavuvi mwezi mmoja uliopita, kwa lengo la kufanya shughuli hizo.

Alisema kwa kuwa mazingira aliyotoka yalikuwa na baridi, hivyo mazingira ya ziwani yalikuwa yakimsumbua kutokana na joto kali, kitendo kilichosababisha ajenge mazoea ya kwenda kuogelea ziwani.

Kwa mujibu wa Fataki, siku ya tukio hilo majira ya saa 8 mchana aliwaaga wavuvi wenzake kuwa anakwenda kuupoza mwili kwa kuogelea ziwani na alipofika aliingia ndani ya maji na kuanza kuogelea, ghafla aliibuka mamba na kumvutia katika kina kirefu cha maji na kuanza kumla kisha kuondoka naye.

Mwenyekiti wa kijiji hicho alisema kuwa baadhi ya wavuvi walikuwa wanashuhudia tukio hilo kwa mbali, lakini walishindwa kutoa msaada, hivyo mamba huyo kuondoka na Msafiri na mpaka sasa jitihada za kuutafuta mwili wake zinaendelea.

Kamanda wa Polisi mkoani Rukwa, George Kyando, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwatahadharisha wananchi wanaoishi maeneo ya mwambao mwa ziwa na mito kuacha tabia ya kwenda kuogelea, kwa kuwa ni hatari kwa usalama wao.

Naibu Waziri Apiga Marufuku Waliomaliza Darasa La Saba Kufanya Kazi Za Ndani

$
0
0
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha amewataka viongozi kuanzia ngazi ya mkoa hadi vijiji nchini kuhakikisha wanafunzi wanaomaliza darasa la saba hawaondoki katika maeneo yao kwenda kufanya kazi za ndani wakati wakisubiri matokeo ya kuhitimu darasa la saba.

Ole Nasha ametoa agizo hilo mkoani Manyara wakati akizungumza na viongozi hao kuhusu hali ya Elimu mkoani humo ambapo amewataka kusimamia kwa ukaribu suala hilo ili kutokatisha ndoto za watoto hao na kwamba wale wanaofanya hivyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

“Hakikisheni watoto wanaposubiri matokeo hawasafirishwi kwani wanapofika huko wanarubuniwa na waajiri hivyo hata matokeo yakitoka na kuonesha kuwa wamefaulu hawarejei kuendelea na masomo “ alisisitiza Naibu waziri Ole Nasha.

Kiongozi huyo ameendelea kuwasisitiza wazazi kuwa fursa za Elimu katika nchi yetu ni kubwa, ikizingatiwa kuwa Elimu msingi ni bure hivyo hakuna kisingizio tena kuwa mtoto hawezi kusoma.

“Wazazi msiwe sehemu ya kuchangia watoto wenu kwenda mjini kwa kuwa tu wanawatumia fedha kwa ajili ya matumizi bali hakikisheni mnawasimamia vyema watoto hao katika kipindi chote cha kusubiri matokeo na kuwapeleka shule pindi matokeo yanapotoka na kuonekana wamefaulu,” alisisitiza Naibu waziri Ole Nasha.

RPC Manyara Agundua Mbinu Mpya Za Kusafirisha Madawa Ya Kulevya

$
0
0
Na John Walter-Babati
Watu wawili wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Manyara  baada ya kukamatwa na madawa ya kulevya aina ya Mirungi  kilo tano sawa na mabunda 14 yakisafirishwa kutoka mkoani Arusha kwenda Babati.

Kamanda wa polisi mkoa wa Manyara  Agustino Senga  amesema watuhumiwa hao wamekamatwa Oktoba 6-2018 Majira ya saa 12 Jioni katika kituo cha ukaguzi wa magari  eneo la Minjingu kata ya Nkaiti wilaya ya Babati  wakiwa wameficha madawa hayo ya kulevya kwenye miili yao maeneo ya tumboni hadi mgongoni.
 
Amewataja waliokamatwa ni Aisha Mohamedi  [38] mkazi wa Endasaki, Amani Hassan [30] mkazi wa Sakina Arusha ambao walikuwa wakisafirisha Mirungi kilo hiyo iliyokuwa imefungwa kwenye  magazeti na kuwekwa  gundi ya karatasi na kisha kuifunika kwenye nguo walizokuwa wamevaa.

 Senga amesema Watu hao walikamatwa wakiwa katika gari  kampuni ya Makara yenye namba za Usajili T 128 -PDC  Fuso wakiwa wamejifunga madawa hayo kwa mabunda madogo madogo 14 wakiwa wamejizungushia tumboni ili kuonekane ni mtu mwenye vitambi au mwenye ujauzito na muda wowote watapandishwa kizimbani.

Ikumbukwe kwamba Matumizi ya madawa ya kulevya yameathiri vijana wengi kiafya kutokana na baadhi yao kushindwa kufanya kazi , hivyo kulazimika kujihusisha na matukio ya wizi katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Kamanda amewatahadharisha wakazi wa mkoa wa Manyara na wanaoingia katika mkoa huo kwamba Mkoa wake sio mlango wa kupitisha madawa ya kulevya.

Lori la Oil Com lakutwa na pombe kali na Vipodozi Vilivyopigwa Marufuku

$
0
0
Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya, linalishikilia lori la mafuta mali ya Kampuni ya Oil Com, baada ya kukutwa limebeba vipodozi na pombe  vilivyopigwa marufuku kuingia nchini.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei, amesema gari hilo lenye namba za usajili T 233 CXL limekamatwa eneo la Mbarali jijini hapa, jana saa nane mchana, likitokea nchini Zambia.

Kamanda Matei amesema katoni 15 za vipodozi na katoni mbili za pombe kali zimekutwa ndani ya gari hilo.

Amesema dereva wa gari hilo anatafutwa na polisi kwani baada ya gari hilo kukamatwa alifanikiwa kukimbia.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images