Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Serikali Yamnyima Kibali cha Kazi Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Vodacom

$
0
0
Serikali imetangaza rasmi kumnyima kibali cha kazi Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Kampuni ya Simu za mikononi ya Vodacom, raia wa Kenya, Sylvia Mulinge.

Kampuni ya Vodacom ilisambaza ujumbe jana ikisema sasa ni rasmi kuwa mkurugenzi huyo hawezi kupewa kibali cha kufanya kazi nchini.

"Vodacom Tanzania inathibitisha kuwa serikali ya Tanzania imekataa kutoa kibali cha kazi kwa Sylvia Mulinge na sasa itaanza mchakato wa kumpata mkurugenzi mpya," ilisema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo ambayo ilitolewa na Mwenyekiti wa Vodacom Tanzania, Ali Mufuruki, ilisema wamekatishwa tamaa na kusikitishwa na uamuzi wa Kamshina wa Kazi na wamejipanga kuwasiliana na mamlaka.

"Tunauhakika kwamba Vodacom ina timu imara ya usimamizi ambayo itaiongoza kampuni vyema mpaka pale suala la kutafuta kiongozi mwingine anayefaa litakapomalizika," ilieleza taarifa hiyo.

Mulinge ambaye anaongoza idara ya biashara kwa wateja katika kampuni ya simu ya Safaricom ya Kenya, aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Aprili, mwaka huu.

Hata hivyo, alishindwa kuanza kazi katika kipindi alichoteuliwa kutokana na kusubiri kupata kibali cha kufanya kazi Tanzania.

Wakati akisubiri kibali hicho, Vodocom imetoa taarifa ikieleza kunyimwa kibali cha kazi kwa mkurugenzi mpya ambaye alitakiwa kuanza rasmi majukumu yake tangu Juni mwaka huu.

Aidha, Kampuni ya Vodacom Tanzania ilimteua Hisham Hendi, kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji kuanzia Septemba 1, mwaka huu, mpaka mchakato wa kumpata mkurugenzi mtendaji mpya utakapokamilika.

Hendi amekuwa na kampuni ya Vodacom Tanzania tangu mwaka 2016 akiwa Mkurugenzi wa Biashara. Pia ana uzoefu wa miaka 15 katika sekta ya mawasiliano na amewahi kushika nafasi mbalimbali katika kampuni ya Vodafone na kampuni mama ya Vodacom Group.

Uteuzi huo wa Hendi umefanyika ikiwa imepita miezi minne tangu Mulinge alipotakiwa kuchukua nafasi ya aliyekuwa akishika nafasi hiyo, Ian Ferrao, ambaye pia alikosa kibali cha kufanya kazi nchini.


Tisa Wakamatwa Pwani Kwa Makosa Ya Kiuhalifu

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
JESHI la Polisi mkoani  Pwani  linawashikilia watu Tisa kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya uvunjaji, wizi na vitendo vingine vya kihalifu.
 
Ikumbukwe kwamba,  septemba 18 majira ya saa 21:15 usiku katika kitongoji cha Kibosho ,Mapinga Wilaya ya Bagamoyo, watuhumiwa 15 wakiwa na gobore, mapanga, nondo na visu walivamia makazi ya  Jaji mstaafu Salum Masati (69) na Flora Timoth (59) muuguzi hospitali ya Mwananyamala-Dar es salaam. 
 
Aidha baadhi ya nyumba za wananchi wa eneo hilo, waliwajeruhi na kuiba pesa taslim, simu wa mkononi aina mbalimbali, laptop, televisheni, ipad, saa za mkononi, spika za music system na vitu vingine vyenye thamani mbalimbali na kutokomea navyo. 
 
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani humo, Wankyo Nyigesa, alisema kufuatia matukio hayo jeshi hilo kwa kushirikiana na raia wema lilipokea taarifa za watuhumiwa wanaojihusisha na matukio hayo.
 
“Septemba  28 kati ya saa 6-8 usiku na tulifanikiwa kuwakamata watuhumiwa tisa (majina yamehifadhiwa) “
 
“Baada ya kufanyiwa upekuzi tuliwakamata na gobore, televisheni 4,deki za video 5, amplifaya 3, ving’amuzi 4, redio za subwoofer 3, spika 5,simu za mkononi za aina mbalimbali 15, bangi ambayo haijasokotwa kifurushi kimoja ,misokoto/kete 169 na pakiti moja ya karatasi za kusokotea iitwayo lizla”alieleza Wankyo. 
 
Aliwataka ,wananchi  wa Mapinga na maeneo ya jirani waliowahi kuvamiwa, kujeruhiwa na kuporwa kufika katika kituo cha polisi cha Mapinga wilaya ya Bagamoyo kwa ajili ya kutambua mali zilizokamatwa .
 
Wankyo alitoa rai kwa wananchi  kuliamini Jeshi la Polisi na kuendelea kuwapatia taarifa za uhalifu na wahalifu pasipo kusita waweze kukamatwa na sheria ichukue mkondo wake.

Kwanini Baadhi ya Wanaume Wana Maumbile Mafupi na Upungufu wa Nguvu za Kiume? Suluhisho Hili Hapa

$
0
0
KWANINI BAADHI YA WANAUME WANA MAUMBILE MAFUPI NA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME... DR SITTA NDO SULULISHO LAKO

Tatiza, hili limekuwa likiwaathiri watu wengi sana kisaikolojia hasa baadhi yao kujiona wako tofauti na wanaume wengine. Kwa kawaida, mwanaume anatakiwa awe na uume, usiopungua nchi 6-7au-8 ,vinginevyo mtu huyo anamatatizo.

Zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo hilo... baadhi ni  upungufu wa vichocheo vya, HORMONES ZA CETROGEN .

SUPER MIZIZI, ni dawa inayozalisha HORMONES ZA CETROGEN,na kufanya, uume kukuwa na kuongzeka sazi utakayo na kuzibua mrija iliyosinyaa,

NSHOLA; ni dawa bora, ya kurudisha nguvu za kiume kwa kutibu kabisa  tatizo hilo na kukupa  hamu ya  kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara nne 4 bila kuchoka 

Pia  kuna dawa za kutibu presha ya kupanda na kushuka, kisukari , kuondoa mafuta  mwilini na maumivu ya mgogo kiuno, matazo, ya hedhi kwa wanawake, hedhi zisizokuwa na mpangilio.

NKANYA; ni dawa ya mvuto wa kimapenzi ,mchumba mpenzi aliyekuacha, mke, mme atakurudia .

NKOMA; Ni dawa kuongeza HIPS na mguu wa bia kwa wadada ,

NGAKAMA ,ni dawa ya kutibu miguu kufa ganzi na kuwaka moto, huduma zetu ,zipo ,vizuri, popote pale dawa utaletewa! 

DR SITTA, amebobea kwa tiba asili

SONGEA BOMBAMBILI, SHINYANGA- KAHAMA MJINI, 

KWA MAELEZO ZAIDI  PIGA SIMU; 0763172670/ 0715172670,/

WOTE  MNAKARIBISHWA... KAMA, UTAKUWA NA TATIZO, UTAHUDUMIWA,

Mtendaji Mkuu TIC , Balozi Wa Denmark Nchini Tanzania Wafanya Mazungumzo Kuhusu Uwekezaji

$
0
0
Na Grace  Semfuko-MAELEZO
MTENDAJI Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Geophrey Mwambe amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Einar Jensen.

Miongoni mwa mambo ambayo wamezungumza ni pamoja na wawekezaji wa nchini Denmark kuja kuwekeza kwa kudai Tanzania  kuna mazingira mazuri ya uwekezaji.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mtendaji Mkuu wa TIC amesema Balozi Jensen amekuwa mdau mkubwa katika kuhakikisha kunakuwa na mazingira mazuri ya uwekezaji na pande hizo mbili kufanyabiashara.

“Balozi Jensen ni rafiki mkubwa wa biashara na amekuwa akishiriki kikamilifu katika kuandaa mazingira mazuri ya kiabiashara.Tumekuwa tukishirikiana na Balozi Jensen kuratibu za kuwezesha wafanyabiashara,” amesema Mwambe.

Pia amesema Balozi Jensen katika kutafuta masoko ya bidhaa za kilimo kwa kuhakikisha wakulima wanakuwa na soko la uhakika huku akieleza kwamba Balozi amekuwa akihamasisha wawekezaji wa Denmark kuwekeza nchini Tanzania.

Mwambe amesema siku za karibuni amefanya mazungumzo na Balozi huyo na moja ya mambo waliyoyazungumza ni namna ya kusaidia katika mabadiliko ya kimfumo yanayoendelea kufanywa na TIC.

“Balozi amekubali kuisaidia TIC katika mabadiliko ya kimfumo kiutendaji…kama nchi, tumedhamiria kushindana kidunia, tunakuza uwezo wa kuongeza ajira kwa Watanzania,” amesema

Pia wamekubaliana na Balozi Jensen katika kuandaa maeneo ya yaliyopimwa kwa ajili ya uwekezaji.”Nchini kwetu hatuna tatizo la ardhi kwani ipo ya kutosha ila changamoto ipo kupata eneo ambalo limepimwa.

“Hivyo moja ya mipango yetu ni kuhakikisha maeneo ya uwekezaji yanapimwa na mwekezaji anapohitaji eneo inakuwa rahisi kupata.Bolozi amekubali kusaidia katika upimaji wa maeneo,” amefafanua.

Mwambe amesema ushirikiano kati ya Tanzania na Denmark kuna kampuni kubwa za nchi hiyo ambazo zimejenga viwanda.

Pia amesema kupitia Balozi huyo Denmark kwa sasa kuna mchakato wa  mradi wa umeme wa upepo unaoendelea mkoani Dodoma.

Kwa upande wake Balozi Jensen amesema nchi hizo mbili zimekuwa kwenye ushirikiano mkubwa kwa miaka 50 na kwamba nchi ya Denmark imekuwa ikisaidia katika mambo mbalimbali yanayohusu uwekezaji.

Zoezi la Kuinasua MV Nyerere Lakamilika....Rais Magufuli Atoa Maagizo Haya

$
0
0
Rais Dk. John Magufuli amemuagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe, kuzitumia fedha za rambirambi zilizobaki zaidi ya Sh milioni 689.99 kati ya Sh milioni 949.6 kujenga majengo matatu ya wodi katika Kituo cha Afya cha Bwisya kilichopo Ukara wilayani Ukerewe, Mwanza.

Kauli hiyo ilitolewa mjini hapa jana na Kamwelwe wakati akihutubia wananchi, viongozi na wataalamu walioshiriki shughuli ya uokoaji na uopoaji baada ya Kivuko cha MV Nyerere kuzama Alhamisi wiki iliyopita saa nane mchana katika Ziwa Victoria wakati kikitokea Kisiwa cha Bugolora kuelekea Kisiwa cha Ukara kilichopo Ukerewe mkoani Mwanza huku kikidaiwa kubeba idadi kubwa ya abiria na mizigo mingi kuliko uwezo wake.

Pia alisema shughuli ya uokoaji na uopoaji imefungwa rasmi kutokana na kazi ya kukivuta kivuko hicho kukamilika kwa asilimia 100 jana jioni.

Alisema shughuli hiyo imefanikishwa na watu 588 kutoka taasisi mbalimbali za umma na binafsi katika shughuli za uokoaji, uopoaji miili 228 iliyopatikana na watu 41 waliookolewa wakiwa hai hadi inakamilika na kufungwa rasmi.

“Tumeanza jana asubuhi saa 5:21 kuanza kukivuta lakini tukasitisha kutokana na maboya yaliyokuwa yamejazwa upepo ndani ya kivuko na maji yaliyokuwa yamejaa katika ghamla la kivuko na vyumbani hadi saa 10 jioni tulipoanza na kukamilika saa 11: 15 jioni,” alisema.

Pia alisema Magufuli amewapatia motisha watu wote 588 na Sh milioni 240 zitatumika kuwapa posho ya Sh 400,000 kila mmoja na Sh milioni 266 zilitumika kulipa manusura 41 wa ajali hiyo na waliopoteza ndugu na jamaa zao katika ajali hiyo.

Alisema fedha hizo pia zitatumika kujenga uzio katika makaburi na kuwekwa mnara wa kumbukumbu ili kuweka alama ya kumbukumbu ya tukio hilo.

“Gari aina ya canter lenye namba za usajili T 554 DBA liliopolewa na winchi ya gari la Mwauwasa la Mwanza lililokuwa ndani ya Kivuko cha Orion II la Kampuni ya Kamanga Ferry hadi ufukweni kutolewa ndani ya maji,” alisema.

Pia alisema upokeaji wa michango ya ajali hiyo ulihitimishwa jana saa saba mchana na wasiochangia waelekeze maeneo mengine kunako jielekeza kuna matatizo.

Jipatie Tiba ya Asili ya Ngiri, Vidonda vya Tumbo,Kisukari na Nguvu za Kiume

$
0
0
Super nzoka IKEMEKO TRDITONAL clinic Ni dawa ya Asili ya vidonge iliyotengenezwa kwa techknojia ya kisasa na ubora wa hali ya juu 

Huongeza nguvu za kiume maradufu hata kwa wale wasiojiweza kabisa kufanya tendo la ndoa na wapo abao hata wakifanya hushindwa kutoa maji maji maji ambayo ndani yake kuna mbegu za kiume zinazotakitakiwa kurutubisha yai

Dawa hii huboresha na tunatibu nakumaliza matatizo haya kwa muda mfupi tu na haina madhara kwa mtumiaji yeyote hata wa umri wa miaka 80 na kuendelea.... inaongeza hamu, urijali kwa wanaoshindwa kuendelea na tendo la ndoa.

Huanza kufanya kazi baada ya dakika 60 tu na kufanya uchelewe kufika kileleni dakika 20 kwa tendo la kwanza itakuwa unauhakika wa kurudia tendo la ndoa zaidi ya Mara tatu bila kuhisi kuchoka 

SILYA; inakuza uume uliosinyaa kurefusha umbile dogo urefu inchi (6-9)na unene wa cm 4 za upenyo kwa wenye kasoro za kimaumbile na walioathiriwa na kupiga punyeto pamoja na matatizo ya kiafya

Tiba hii ni ya kudumu.Pia tunatibu ngiri ya kupanda na kushuka,tumbo kuuguruma chini ya kitovu ,kaswende kisukari ,maumivu ya mgongo, kiuno, kutopata choo vizuri na uvimbe kupitia njia ya mkojo, presha, vidonda vya tumbo

Wasiliana Nasi kwa namba;  0716343218,0789289945. TUNAPATIKANA MBAGALA ZAKIEM STENDI ya musanga

Video Mpya : Mimi Mars - Kodoo

$
0
0
Msanii wa muziki Bongo, Mimi Mars ameachia video ya wimbo wake mpya uitwao Kodoo. Itazame hapa.

Video Mpya: Professor Jay Ft. Ruby - Vunja Mifupa

$
0
0
Msanii  nguli wa muziki Bongo, Professor Jay ameachia video ya wimbo wake mpya uitwao Vunja Mifupa ambapo kamshirikisha msanii Rubby. Itazame hapa.


Chadema yataka Takukuru ichunguze wabunge wake Kuhamia CCM

$
0
0
Uamuzi wa aliyekuwa Mbunge Serengeti, Ryoba Chacha kutangaza kujiuzulu ubunge na kuhamia CCM, umekifanya chama chake cha zamani cha Chadema kuitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuchunguza kuona kama kuna aina mpya ya rushwa ya madaraka ambayo inawavuta wabunge wengi wa chama hicho kukimbilia chama tawala.

Ombi hilo limetolewa na Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema.

“Wabunge wamekuwa wakiahidiwa kupewa ubunge wao baada ya kuhamia CCM, hiyo ni aina nyingine ya rushwa, Takukuru waingilie kati suala hilo na kuchukua hatua,” amesema.

Mrema alidai suala la wabunge na madiwani wa Chadema kutimukia CCM haliwapi shida kwa sababu wanajua mazingira yalivyo sasa.

Alidai Mbunge huyo (Ryoba) amefanya kile alichokisema wakati wa mkutano wa Rais Magufuli huko Serengeti na kwamba hawashangazwi na uamuzi wake kwa sababu yeye siyo wa kwanza kuhama.

Makanga 3 Power; Dawa Bora Nguvu Za Kiume

$
0
0
Kutibu nguvu za kiume dakika(10) na kupona muda wa siku tatu tuu. Kuimarisha misuli ya uume uliolegea, pia ipo Dawa ya kurefusha uume mfupi inchi NNE hadi saba na kunenepesha uume mfupi sentimita NNE.

Tiba ya kudumu kutibu maumivu ya mgongo,kiuno, tumbo kuunguruma na kujaa gesi, kupata choo vizuri, na kutibu uzazi, kutibu busha bila operesheni, kisukari, presha ,miguu kuuma, uzazi, fangas sugu, vidonda vya tumbo.

Ni docta bingwa wa kutibu magonjwa sugu, kutoa ndagu za utajiri kwa kutumia Pete, kazi ,cheni, mikufu maalumu ya bahati, una kesi umedhulumiwa Mali au pesa? Zitarudi muda wa Masaa matatu tuu.

Onana na Dr shilindes shida zako zote zitakwisha, anatoa Dawa za utajiri kwa wafanyakazi, wakulima, na wafugaji, wafanyabiashara na wachimba madini kwa kutumia pete, kazi kwa yeyote anaetaka kuwa na pesa nyingi.

Pia anaboresha akili kwa wanafunzi darasani, masomo na kufaulu mitihani pia kushinda bahati nasibu yeyote.

Pia tunatoa Dawa kumrudisha Mume, mke, mpenzi, hawara, kwa muda wa SAA moja tuu, na kuomba msamaha kwa kukupigia magoti na yeyote yule, unaemtaka kimapenzi au kuoana, utampata na kumfunga asitoke nje ya ndoa daima na kutekeleza shida zako zote. Kupunguza unene, kupunguza matiti makubwa, tumbo na nyama uzembe muda wa siku sita unapata saizi uipendayo.

Kutoa makovu mwilini, chunusi, upele na mabaka, pia tunayo Dawa ya kuongeza hipsi, makalio, mguu wa bia na kupata shepu safi kwa muda wa siku saba tuu.

Wa mikoani mtapata huduma popote mlipo.
Tupo dar es salam mbagala rangi tatu.

Mawasiliano simu namba: 0784 460 348.

Aliyekuwa Akiongoza MV Nyerere Hakuwa na Sifa ya Kuendesha Chombo Hicho

$
0
0
Wakati Tume maalumu iliyoundwa na Serikali ikiendelea na uchunguzi juu ya ajali ya Mv Nyerere, taarifa zinaeleza kuwa aliekuwa akiongoza chombo hicho siku hiyo hakuwa na sifa za kufanya hivyo bila uangalizi wa karibu wa nahodha.

Wakati anayetakiwa kuongoza kivuko au meli yenye hadhi ya Mv Nyerere akitakiwa kuwa na kiwango cha elimu ya masuala ya unahodha na ubaharia kuanzia Master Near Coast Deck Officer Class 4, marehemu Alan Mahatane anayedaiwa ndiye alikuwa akiongoza Mv Nyerere, alikuwa elimu ya Deck Ratings (Rating Forming Part of a Navigation Watch). Alipata elimu hiyo mwaka 2014 kutoka Chuo cha Ubaharia cha Dar es Salaam Maritime Institute (DMI).

Mmoja wa watu aliosoma nao, Salum Adam alisema licha ya kuongoza chombo hicho, kiwango chake cha elimu na majukumu ya wenye elimu hiyo haviruhusu kufanya hivyo bila usimamizi wa nahodha.

Adam ambaye ni baharia katika meli ya Mv Nyehunge inayosafirisha abiria na mizigo kati ya Nansio na Mwanza, alisema mwenye alimu kama yake anayetaka kuongoza chombo kama hicho, lazima ajiendeleze.

VIDEO: Msikilize Rais Magufuli akitoa maagizo kwa Naibu Waziri aliyemuapisha LEO

$
0
0
Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemuapisha Dkt. Damas Ndumbaro kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ikulu Jijini Dar es salaam leo Septemba 29, 2018.

==>>Msikilize hapo chini akitoa maagizo mazito

Serikali Kuendelea Kuwezesha Wananchi Wanyonge Kumiliki Ardhi

$
0
0
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO Dodoma.
Serikali ya Awamu ya Tano itahakikisha wananchi hasa waishio vijijini wanapata haki za msingi za umiliki wa ardhi na makazi nchini.

Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Mheshimiwa Angelina Mabula wakati wa uzinduzi wa Matokeo ya Utafiti wa Haki na Usalama wa Umiliki wa Rasilimali Ardhi na Makazi Tanzania  mwaka 2017/2018.

“Tunafahamu Watanzania walio wengi na ambao ni masikini wanaishi vijijini na wizara yangu inadhamana ya kusimamia eneo hili, kama Waziri mwenye dhamana nitajitahidi kadri ya uwezo wangu na kuendelea kushirikiana na viongozi wenzangu na wananchi wote kuhakikisha nyaraka rasmi za umiliki ardhi na makazi zinatolewa” ameongeza Dkt. Mabula.

Aidha, akizungumzia kuhusu utoaji wa hati, Dkt. Mabula amesema kuwa kwa sasa utoaji wa hati umeongezeka kwa mujibu wa taarifa kutoka katika Kanda nane nchini.

“Jumla ya Hati 25,463 zimeandaliwa katika Halmashauri mbalimbali nchini, Hati 17,680 zimewasilishwa ofisi za Kanda kwa ajili ya usajili na Hati 9,739 zimeshakamilika” amefafanua Dkt. Mabula.

hata hivyo Dkt. Mabula amesema kuwa, kwa mwaka 2018/2019 Wizara yake imejipanga kuandaa hati za hakimiliki za kimila 120,000 mpango wa matumizi bora ya ardhi katika vijiji 30 na mpango kina wa vijiji na kupima viwanja 20,000 ikiwa ni kumuwezesha mwananchi kuwa na uhakika na salama ya miliki yake na kuepusha mgogoro.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa amesema kuwa utafiti huo umelenga kutoa viashiria mbalimbali kuhusu rasilimali ardhi, nyumba na makazi nchini na kutumika katika kufuatilia malengo yaliyopo katika Mpango kazi wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano ijayo, Malengo endelevu ya Maendeleo na Afrika Ajenda 2063.

“Utafiti huu ulifanyika Tanzania Bara na Zanzibar na sampuli ilichaguliwa kwa utaalamu na ilitumika kwa watu wazima wenye umri wa miaka 18 na kuendelea” ameongeza Dkt. Chuwa.

Utafiti wa Haki na Usalama wa Umiliki wa Rasilimali Ardhi na Makazi Tanzania  kwa mara ya kwanza ulifanyika mwaka 2016/2017 na wa pili mwaka 2017/2018 na watatu mwaka 2018/2019 unaendelea na ukusanyaji wa taarifa za kitakwimu ambao matokeo yake yatazinduliwa mwaka 2019.

Mzee Mwinyi kuwa Mgeni rasmi Maadhimisho siku ya Wazee Kitaifa jijini Arusha

$
0
0
Rais Mstaafu, Ally Hassan Mwinyi, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya wazee duniani ambayo kitaifa yatafanyika jijini Arusha Oktoba Mosi, mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Arusha Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Naftali Ng’ondi, amesema maadhimisho hayo yatafanyika katika Uwanja wa Kumbukumbu wa Sheikh Amri Abeid.

“Kabla ya maadhimisho hayo yenye kauli mbiu isemayo ‘Wazee ni hazina ya Taifa, tuenzi juhudi za kutetea haki na ustawi wao’, shughuli mbalimbali zitafanyika ikiwamo uzinduzi wa maadhimisho hayo ambapo wazee watapata huduma za kupima afya, ushauri wa kitabibu yakifuatiwa na kongamano la wataalamu na wadau wa masuala ya wazee.

“Natoa rai kwa jamii kutambua wajibu wa kuwaondolea vikwazo wazee katika kupata huduma za kijamii ikiwa ni pamoja na afya, matunzo na ulinzi, kama ambavyo imekuwa ikisisitizwa na Sera ya wazee ya mwaka 2003 inavyohimiza kuwatambua wazee kama rasilimali muhimu katika maendeleo ya taifa,” amesema.

Akizungumzia upatikanaji wa matibabu bure kwa wazee, Dk. Ng’ondi amesema idadi ya wazee waliotambuliwa na kustahili kupatiwa matibabu bure ni zaidi ya milioni 1.9 kwa mujibu wa takwimu hadi za Machi mwaka huu na kuwa licha ya changamoto ya matibabu kwa wazee, huduma za afya kwa kundi hilo zimeendelea kuboreka.

“Tuliwaagiza maafisa ustawi wafanye tathmini na kuhakikisha wazee waliopitishwa na wanaopaswa kupatiwa matibabu bure wanapatiwa, tumejiridhisha hilo linatekelezeka na tuna mfumo wa ufuatiliaji,” amesema.

Huna Sababu Ya Kuaibikatena............ Jipatie Dawa Bora Ya Nguvu Za Kiume, Maumbile Madogo Na Mvuto Wa Mapenz

$
0
0
Usikate tamaa ondoa maradhi yako, maana matatizo haya yamekua yakiasili watuwengi kisaikolojia hasa baada ya kujiona wako tofauti sana na wengine kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia (6-8) vinginevyo mtuhuyo anamapunguvu katika mwiliwake.

Kunasababu nyingi sana zinazosababisha matatizo haya, chango hushambulia never ambayo huasili misuli ya uume, Ngili :- hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kufanya tumbo kuunguluma na kujaa gesi, kolodani moja kuvimba au kuingia ndani pamoja na kutopata choo vizuli. Sababuhizi na nyingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba na marakwamara husababisha kukosa hamu ya kuludia tendo la ndoa na baadae kushindwa kabisa

MASISA 3POWER :- nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa mfumo wa vidonge, huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka 15-90 , inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii) inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa, itakufanya uludie tendo la ndoa zaidi ya mara nne (4) birahamu kuisha wara kuhisi kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya dk (20-30 )

YONINANI:- hurefusha na kunenepesha maumbile madogo ya uume uliosinyaa inchi 6-8 na unene wa sm 3-4 kwa mda mfupi sana,

SUPER MORINA :- nidawa inayotibu ama kutatua tatizo la kisukali kwawaliohangaika bila mafanikio, huondoa tatizo la kisukali na kupona kabisa, vilevile ninadawa ya magonjwa sugu km vile presha, vidondo vya tumbo, miguu kuwakamoto, muwasho mwilin, kaswende,uzazi nk.

LUGIMBA :- nidawa ya mvuto wa mapenzi, humtuliza mke, mme, mchumba, hawara au mtu yoyote umpendae na kumfanya akutimizie chochotekile unachokitaka kutoka kwake na kumfunga asiwe na mtu yoyote zaidi yako.

WASILIANA NA DR CHIPUPA NAPATIKANA DAR ES SALAAM KUMBUKA HUDUMAHII ITAKUFIKIA POPOTE ULIPO  0759208637 / 0622344969

Okoa Ndoa Yako Mke,Mume Na Afya Yako Sasa Kwa Kutumia Dawa Za Asili

$
0
0
Asilimia kubwa ya binadamu wanasumbuliwa na magonjwa mbalimbali na wengi wamejaribu kutumia tiba sehemu tofauti bila mafanikio na  kukata tamaa hasa kina baba ambao ndoa zao au mahusiano yao na wapenzi wao yapo hatarini kuvunjika kwa sababu Mume hana uwezo wa kumridhisha mpenzi wake 

KWA NINI UJIONE MPWEKE PALE UKUTANAPO NA MKE AU MPENZI WAKO SABABU ETI UNAUPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME AU UUME MDOGO: tumia dawa ya NSENWA POWER ;dawa hii hutibu na kuponesha tatizo la  nguvu za kiume .

1 itakupa uwezo wa kurudia tendo zaidi ya Mara tatu 
2 itakupa uwezo kuchelewa kukojoa mda wa dakika 15-20 na kumfanya mpenzi wako naye aridhike 
3 huimalisha misuri iliyo legea na kusinyaa 

JE UNA UUME MFUPI NA MWEMBAMBA : tumia dawa ya MASHESHE NO 2; hii huboresha uume saizi upendayo kuazia urefu wa inch 5,6,7,8 na unene  wa sentumita 2,3,4,5, dawa hizi hazina madhara yeyote kwa mtumiaji hata wazee hutumia na kupona 

MASANZA ni dawa ya vidonda vya tumbo zipo dawa za mvuto wa biashara ,mpenzi,uzazi ngiri,korodani kuvimba miguu. mgongo,kiuno kuuma nk 

MAHALI ILIPO OFISI UNAWEZA UKASHUKIA BUGURUNI MALAPA AU BUGURUNI ROZANA na MWANZA YUPO WAKALA pia unaweza ukaletewa popote ulipo wasiliana nami 0783185060  0752348593 DR AGU

Rais Magufuli Ataja Sababu Za Kumtumbua Naibu Waziri, Katibu Mkuu Wizara Ya Mambo Ya Nje

$
0
0
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Dkt. John Magufuli ametaja sababu za kutengua uteuzi wa aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Susan Kolimba na kumhamisha aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Adolf Mkenda.

Akizungumza katika hafla ya kumuapisha Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk.Damas Ndumbaro  iliyofanyika leo tarehe 29 Septemba 2018 Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli amesema baadhi ya watendaji wa wizara hiyo hasa wakurugenzi wamekuwa wanafanya kazi kwa mazoea.

“Na hili nalirudia, mambo yake pale hayaendi vizuri kama inavyotakiwa kufanya, inawezekana wakurugenzi pale wengi wako weak (dhaifu) sana  au wamezoea, wanajua wanafanya kazi kwa mazoea,” amesema Rais Magufuli .

“Ninasema hivi kwa makusudi ili (Dk Ndumbaro) ukienda huko  usipojua la kufanya halafu likatokea hilo la kutumbua usije kulaumu kwamba sikusema.”

Amesema wizara hiyo imekuwa haitoi ushirikiano hata katika baadhi ya mataifa yanayotuma barua, huku akitolea mfano wa Balozi wa China kutuma barua 24.

“Balozi wa China aliwahi kuandika barua 24 pale (Wizara ya Mambo ya Nje) lakini zikajibiwa mbili, Balozi Kairuki kule China hawajibu.”

Dk Ndumbaro ambaye ni mbunge wa Songea Mjini ameteuliwa kuchukua nafasi ya aliyekuwa naibu waziri wa wizara hiyo, Dk Dk Suzan Kolimba.

Katika maelezo yake, Rais Magufuli amesema viongozi wa wizara hiyo husafiri nje ya nchi hususani waziri (Dk Augustine Mahiga) ambaye hivi karibuni amemtuma kumwakilisha katika mkutano wa kimataifa ulioandaliwa na Umoja wa Mataifa (UN).

“Tunategemea anapobaki naibu waziri ofisini ndio anakuwa mkuu wa shughuli zote za wizara, anakuwa msimamizi wa mambo yote siyo naibu anayekuwa anaendeshwa  na wakurugenzi,”

Rais Magufuli Atoa Onyo Kwa Mabalozi Wanaoenda Nje 'Kunywa Wine'

$
0
0
Rais John Magufuli, amewataka mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nchi za nje, kufanya kazi waliyotumwa au wajiandae.

Akizungumza baada ya kumwapisha Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Damas Ndumbaro aliyemteua wiki hii baada ya kutengua uteuzi wa Dk. Susan Kolimba, amesema hatamvumilia balozi asiyefanya kazi.

“Kama kuna balozi atakwenda kule kunywa ‘wine’ miezi sita yote bila kufanya kazi ajiandae… wizara hii ina mambo ya ajabu sana Balozi wetu kule China, ameandika barua zaidi ya 24 zilizojibiwa ni mbili ndiyo maana nikaamua kutoa Naibu Waziri na Katibu Mkuu wake,” amesema.

Kwa upande wake Dk. Ndumbaro amesema atakwenda kutekeleza kufanya kazi kwa mujibu wa maelekezo  aliyopewa.

“Nikuahidi rais nitakwenda kutekeleza maagizo hayo kwa mujibu wa maelekezo uliyotoa, nitatekeleza majukumu ya Katiba na kufuata Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ukurasa 110 hadi 111 inayoongelea masuala ya kimataifa,” amesema Dk. Ndumbaro.

Lugola Atangaza Operesheni Kuwaondoa Wahamiaji Haramu Mkoani Kigoma

$
0
0
Na Felix Mwagara, MOHA-Buhigwe
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, ameitaka Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Kigoma ishirikiane na Jeshi la Polisi kufanya operesheni maalum ya kuwaondoa wahamiaji haramu mkoani humo.

Akizungumza na mamia ya wananchi katika uwanja wa Mnanila mjini Manyovu wilayani Buhigwe, leo, Lugola alisema anataarifa za kutosha kuhusu wahamiaji haramu kutoka nchi za jirani wapo mkoani humo, hivyo lazima waondolewe kwa mujibu wa sheria.

Lugola ambaye alikua akishangiliwa na wananchi baada ya kutoa agizo hilo, pia alikemea tabia ya baadhi ya watu wanaohifadhi raia hao wa kigeni ambao wameingia nchini kinyume cha sheria.

“Sasa natoa agizo hili na litekelezwe, Uhamiaji mkoa washirikiane na polisi kuwaondoa raia hawa wa kigeni ambao wameingia nchini kwa njia zisizo halali, nataka operesheni hii ianze mara moja,” alisema Lugola.

Lugola pia aliirudia kauli hiyo ya kuondolewa kwa wahamiaji hao haramu alipokua anazungumza na wananchi wa Kijiji cha Kalinzi, Wilaya ya Kigoma Vijijini, na kuongeza kuwa anashangaa wahamiaji hao wanaendelea kuwepo mitaani huku maafisa uhamiaji wakiwepo mkoani humo.

“Hivi inakuaje, wananchi wanalalamika hapa kuhusu uwepo wa wahamiaji haramu, lakini Uhamiaji mpo, mnakaa kimya tu, mnataka mpaka mimi nije ndio nitoe maelekezo haya? Hii sitaki kusikia tena, nataka operesheni hii ianza mara moja na iwe endelevu,” alisema Lugola.

Hata hivyo, Lugola alisema katika operesheni hiyo lazima maafisa wa uhamiaji wawe makini wakati wanawaondoa wahamiaji haramu pekee na sio kuwasumbua wananchi wa Kigoma ambao ni raia halali wa nchi hiyo.

Lugola alifafanua kuwa operesheni hiyo itasaidia kupunguza matukio ya uhalifu katika maeneo mbalimbali mkoani humo ambapo kwa kiasi kikubwa hutekelezwa na wahamiaji hao haramu.

Aidha, Waziri Lugola akiwa wilayani Buhigwe, pia ametembelea kituo cha Polisi cha Manyovu kilichopo mpakani na nchi ya Burundi na kukagua utendaji kazi wa askari Polisi wa kituo hicho pamoja na kuiwahoji watuhumiwa waliopo mahabusu kujua makosa yaliyowafanya wawepo ndani ya kituo hicho.

Mwenyekiti Wa CCM Rais Magufuli Aongoza Kikao Cha Kamati Kuu Maalum Ya Halmshauri Kuu Ya Chama Cha Mapinduzi.

$
0
0
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Rais Dkt.John Magufuli akipiga makofi na wajumbe wengine kabla ya kuanza kikao cha kamati kuu Maalum ya Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi, Lumumba Jijini Dar es salaam.Septemba 29,2018.

Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Rais Dkt.John Magufuli pamoja na wajumbe wengine wakiwa wamesimama kwa dakika moja ili kuwakumbuka na kuwaombea Majeruhi na waliopoteza maisha katika ajali ya kivuko cha Mv Nyerere iliyotokea Septemba 20,2018 katika ziwa Victoria  kabla ya kuanza kikao cha kamati kuu Maalum ya Halimashauri kuu ya chama cha mapinduzi, Lumumba Jijini Dar es salaam.Septemba 29,2018.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Rais Dkt.John Magufuli akiongoza kikao cha kamati kuu Maalum ya Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi, Lumumba Jijini Dar es salaam.Septemba 29,2018.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Rais Dkt.John Magufuli akizungumza jambo na Makamu mweyekiti wa CCm na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ally Mohammed Shein mara baada  ya kikao cha kamati kuu Maalum ya Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi, Lumumba Jijini Dar es salaam.Septemba 29,2018.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Rais Dkt.John Magufuli akizungumza jambo na Makamu mweyekiti wa CCm na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ally Mohammed Shein mara baada  ya kikao cha kamati kuu Maalum ya Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi, Lumumba Jijini Dar es salaam.Septemba 29,2018.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Rais Dkt.John Magufuli akizungumza jambo na Makamu mweyekiti wa CCm na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ally Mohammed Shein mara baada  ya kikao cha kamati kuu Maalum ya Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi, Lumumba Jijini Dar es salaam.Septemba 29,2018.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images