Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Dr. Reginald Mengi Aguswa Na Mkakati Wa Rc Makonda Kusaidia Walemavu, Amuahidi Bilioni 5 Kwaajili Ya Ujenzi Kiwanda Cha Kuajiri Walemavu Dar

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda katika mkakati wake wa kuwapa tumaini jipya watu wenye ulemavu leo ameahidiwa Kiasi cha Shilingi Billion 5 na Mwenyekiti wa makampuni ya IPP Dr. Reginald Mengi kwaajili ya ujenzi wa kiwanda kitakachowaajiri watu wenye ulemavu ambao wana ujuzi wa aina mbalimbali ili wajikwamue kiuchumi.

Hatua hiyo imekuja baada ya RC Makonda kueleza mpango wa kuwasiliana na wizara ya ardhi ombi la kupatiwa eneo la kujenga kiwanda cha kuajiri watu wenye ulemavu jambo lililomgusa Dr. Mengi na kuahidi kutoa shilingi billion 5 kuunga mkono mpango huo.

Hayo yote yamejiri leo wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya kusaidia walemavu ya Dr. Reginald Mengi persons with disabilities Foundation iliyozinduliwa na Waziri mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ambae pia amemsifu RC Makonda kwa agizo alilotoa kwa wenye viwanda kuwapa ajira walemavu kwa mujibu wa sheria na pia kampeni ya miguu bandia inayoendelea kuwasaidia walemavu.

Aidha RC Makonda pia ameeleza Mkakati wa kukutana na wamiliki wa shule binafsi kwaajili ya kuwaomba kusomesha watoto wawili wenye ulemavu bure kwa kila shule kuanzia ngazi ya msingi hadi sekondari ili kuwawezesha walemavu kupata elimu bora.

Kwa upande wake Naibu waziri Wizara ya Ajira, Wazee, watoto na watu wenye ulemavu Mhe. Anton Mavunde, Mbunge wa viti maalumu Mhe. Amina Molel na Shirikisho la Vyama vya Watu wenye Ulemavu wamemshukuru RC Makonda kwa namna anavyopambana kuwakwamua watu wenye ulemavu.

Watu Zaidi Ya 1,500 Watakiwa Kuhakiki Silaha Zao Dodoma

0
0
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma amewataka wamiliki zaidi ya 1,500 kuhakiki uhalali wa umiliki wa Silaha zao na kutakiwa kujisalimisha polisi kabla ya masoko dhidi yao kuanza

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto, amesema kuwa  msako mkali kwa watako kaidi agizo hilo utafanyika katika wilaya zote na vitongozi vyake

“Kuna zaidi ya watu 1500 wanaomiliki silaha zikiwemo bastola, shotgun na rifle. Waje kwenye vituo vya polisi mkoani au wilayani kuhakiki uhalali wa umiliki wa silaha zao na kusema kuwa Majina yao tunayo. Tunataka kujiridhisha uhalali wa umiliki wao pamoja na kutakiwa kulipa tozo halali ya serikali.

Aidha Kamanda huyo ametangaza kuuawa kwa majambazi wanne waliomvamia mfanyabiashara mkazi wa kijiji cha Maziwa, Tarafa ya Farkwa na kumuibia sh. milioni moja ya mauzo ya duka.

Katika tukio hilo wananchi walianza msako dhidi ya majambazi hao na walipofika kwenye kijiji cha Kitalalo, wilayani Manyoni mkoani Singida, walibaini majambazi watatu kati ya wanne wamejificha porini majira ya saa sita usiku.

“Jambazi aliyekuwa na bunduki iliyotengenezwa kienyeji alijaribu kuwafyatulia risasi lakini iligoma ndipo wananchi walipoanza kuwashambulia majambazi hayo hadi kuwaua,” alieleza.

SACP Muroto alibainisha kuwa baada ya polisi kufika eneo la tukio walikuta silaha moja aina ya shotgun na fedha taslimu sh. laki moja.

Katika tukio lingine, kamanda huyo wa polisi alieleza polisi imewakamata vijana wanne wakiwa wamechapisha noti bandia 3,181 za dola ya Kimarekani zikiwa kwenye sanduku na  pia walikamata kompyuta zilizowekwa program ya kudurufu noti bandia kwa kikundi cha vijana ambao wanaunda kikundi cha kisanii

“Kumezuka mtindo  wasanii pamoja na watu kutengeneza fedha bandia na kuzitumia kiholela mitaani na wengine kusingizia ni wasanii wanafanya sanaa.

Aliwataja waliokamatwa ni Amri Mtaki (21), Salim Hamis (19) Salmin Mohammed (22) na Asajile Mwakalinga (22) na kusema kuwa mtindo wa watu kutumia fedha kwa kuzidhalilisha haikubaliki na wahusika wote watakamatwa na kupandishwa mahakamani

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya Septemba 27

Manusura FEKI waibuka mgawo wa milioni moja za Ajali MV Nyerere

0
0
Baada ya serikali kutangaza nyongeza ya Sh. milioni moja kwa kila ndugu aliyefiwa na ndugu yake katika ajali ya kivuko cha MV. Nyerere, wameanza kujitokeza watu wakidai na wao walikuwa kwenye kivuko hicho.

Hata hivyo, serikali imeushtukia utapeli huo na kuweka wazi kuwa hakuna mtu yeyote wa aina hiyo atakayepewa fedha hizo.

Akizungumzia suala la watu kujitokeza kudai fidia, Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa ambaye ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe, alisema hawatatoa fedha zozote kwa mtu ambaye hayumo katika orodha ya waliofariki na manusura.

Waziri Kamwelwe alisema kuwa idadi inayotambuliwa na serikali ni watu waliofariki ambao ni 228 na waliookolewa ni 41 tu.

“Yule anayejidanganya kujitokeza eti alikuwa katika kivuko ili alipwe huyo asahau, alikuwa wapi kujitokeza siku ile au kesho yake ambapo serikali ilikuwa hapa inafanya uhakiki,” alisema Waziri Kamwelwe jana na kuongeza:

“Idadi ikiongezeka ni ya wale marehemu watakaopatikana na tukajiridhisha ndugu waliojitokeza ni halali watapatiwa fedha zao na si vinginevyo.”

Aidha, Kamwelwe alisema idadi ya miili imefikia 228, ingawa kulikuwapo na taarifa ya kuonekana kwa miili miwili katika kijiji jirani.

Hata hivyo, alieleza kuwa ulikutwa mwili mmoja, hivyo idadi kufikia 229 si sahihi.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kumsomesha msichana aliyepooza

0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, ameahidi kumsomesha Wakonta Kapunda (26) ambaye alipata ulemavu unaosababisha aandike kwa kutumia ulimi.

Wakonta ambaye ameishia kidato cha sita alipata ajali mwaka 2012 mkoani Tanga alipokuwa akienda katika sherehe za mahafali yake.

Akizungumza jana  wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya Dk. Reginald Mengi inayojihusisha na watu wenye ulemavu (DRMF), alisema atawasiliana na familia ya binti huyo ili kumwezesha kutimiza ndoto zake.

“Serikali inaheshimu na kulinda utu wa jamii mbalimbali wakiwamo watu wenye ulemavu, tutaendelea kusimamia ulinzi imara kwa watu wenye ulemavu na kuchukua hatua kali kwa yeyote atakaye wanyanyapaa na kuwaficha,” alisema Majaliwa.

Pia ametoa wito kwa wafanyabiashara nchini kutenga sehemu ya faida wanazopata kusaidia watu wenye ulemavu kwa sababu suala la kuwahudumia watu wenye ulemavu si la Serikali pekee bali jamii nzima.

Alisema taasisi hiyo ni kielelezo muhimu cha mchango wa Dk. Mengi kwa watu wenye ulemavu hapa nchini na kuwataka watu wengine waige mfano huo.

Naye Dk. Mengi ameahidi kutoa Sh bilioni 5 kuwezesha ujenzi wa kiwanda kwa ajili ya watu wenye ulemavu kitakachojengwa jijini Dar es Salaam.

“Usilalamike huna miguu au mikono bali tumia kikamilifu kile kilichobaki,” alisema Dk. Mengi.

Jipatie Tiba ya Asili ya Ngiri, Vidonda vya Tumbo,Kisukari na Nguvu za Kiume

0
0
Super nzoka IKEMEKO TRDITONAL clinic Ni dawa ya Asili ya vidonge iliyotengenezwa kwa techknojia ya kisasa na ubora wa hali ya juu 

Huongeza nguvu za kiume maradufu hata kwa wale wasiojiweza kabisa kufanya tendo la ndoa na wapo abao hata wakifanya hushindwa kutoa maji maji maji ambayo ndani yake kuna mbegu za kiume zinazotakitakiwa kurutubisha yai

Dawa hii huboresha na tunatibu nakumaliza matatizo haya kwa muda mfupi tu na haina madhara kwa mtumiaji yeyote hata wa umri wa miaka 80 na kuendelea.... inaongeza hamu, urijali kwa wanaoshindwa kuendelea na tendo la ndoa.

Huanza kufanya kazi baada ya dakika 60 tu na kufanya uchelewe kufika kileleni dakika 20 kwa tendo la kwanza itakuwa unauhakika wa kurudia tendo la ndoa zaidi ya Mara tatu bila kuhisi kuchoka 

SILYA; inakuza uume uliosinyaa kurefusha umbile dogo urefu inchi (6-9)na unene wa cm 4 za upenyo kwa wenye kasoro za kimaumbile na walioathiriwa na kupiga punyeto pamoja na matatizo ya kiafya

Tiba hii ni ya kudumu.Pia tunatibu ngiri ya kupanda na kushuka,tumbo kuuguruma chini ya kitovu ,kaswende kisukari ,maumivu ya mgongo, kiuno, kutopata choo vizuri na uvimbe kupitia njia ya mkojo, presha, vidonda vya tumbo

Wasiliana Nasi kwa namba;  0716343218,0789289945. TUNAPATIKANA MBAGALA ZAKIEM STENDI ya musanga

Historia Mpya: Muhimbili Yatenganisha Watoto Walioungana Tumbo, Kifua

0
0
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imefanya upasuaji mkubwa wa watoto pacha walioungana sehemu ya tumboni na  kufanikiwa kuwatenganisha watoto hao wenye jinsia ya kiume.

Upasuaji huo ambao ulitumia saa tano ulifanywa na  wataalamu wa upasuaji wa Muhimbili kwa kushirikiana na watalaamu kutoka Ireland.

Akizungumza na waandishi wa habari jan, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru amesema hospitali imefanikiwa kufanya upasuaji kwa mafanikio na kwamba upasuaji huo umewezekana baada ya  kuboreshwa kwa miundombinu ya utoaji huduma katika vyumba vya upasuaji ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa wataalamu.

Prof. Museru amesema kuongezwa kwa vyumba hivyo kumesaidia kupunguza msongamano wa huduma ya upasuaji na hivyo kurahisisha utoaji huduma kwa watoto kutoka mara 4 hadi mara 10 kwa wiki.

Amesema awali baada ya watoto hao kufikishwa Muhimbili walilazwa katika chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu (ICU) ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kufanyiwa upasuaji wa kuwatenganisha.

Naye Daktari Bingwa Upasuaji wa Watoto, Dkt. Petronila Ngiloi amesema walishirikiana vyema na wataalamu wa upasuaji kutoka Ireland katika kuhakikisha watoto hao wanatenganishwa na kwamba lengo kubwa lilikuwa ni kupunguza hatari yoyote inayoweza kutokea kwa watoto hao wakati wa upasuaji.

Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto, Dkt. Zaituni Bokhary amesema upasuaji huo ulihusisha timu ya wataalamu 10 wa upasuaji wa watoto, wauguzi na wataalamu wa tiba ya usingizi.

“Nashauri watoto pacha walioungana au wenye matatizo ya kiafya waletwe Muhimbili ili wafanyiwe uchunguzi wa kina na baada ya kujiridhisha tutawapatia huduma stahiki,” amesema Dkt. Bokhary.
Watoto pacha wakiwa wamelazwa wodini katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kabla ya kufanyiwa upasuaji na wataalamu wa hospitali hiyo kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Ireland.
Madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kutoka kulia, Dkt. Zaitun Bokhary,  Dkt. Petronila Ngiloi na Dkt. Victor Ngotta wakiwafanyia upasuaji wa kuwatenganisha watoto pacha waliokuwa wameungana kwa kushirikiana na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Watoto kutoka Ireland, Prof. Martin Carbally.
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu upasuaji wa kuwatenganisha watoto pacha waliokuwa wameungana sehemu ya tumboni. Watoto hao hivi sasa wanaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji.

IGP Mstaafu Pundugu Afariki Dunia


Tatizo La Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Na Maumbile Madogo

0
0
Tatizo La Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Na Maumbile Madogo Ya Uume Limekuwa Kubwa Kwa Lika Zote Hapa Kwetu Na Duniani Kote. Tatizo Si Tatizo Bali Ni Iletiba Sahihi Ya Matatizo Haya Chanzo Chake Na Visababisho Vyake.

DALILI;mwili kuchoka, maumivu ya mgongo na kiuno, kutopata choo vizuri hata ukipata choo kinakuwa kigumu au gololi kama mavi ya mbuzi. misuli ya uume kulegea na kusinyaa hata uume kulegea na kushindwa kufika kileleni. miguu kuuma na kuwaka moto.

 TIBA YAKE;LUKUBA 4mix ni dawa pekee inayoweza kutibu matatizo hayo inarudisha nguvu za kiume mara dufu na kufanya urudie tendo la mara tatu bila kuchoka. 

LUKUBA 3 pump; ni dawa inayorefusha na kunenepesha uume hadi inchi 7 hadi 9 na kunenepesha kwa CM 2 na kukupa umbile la uhakika. ITUMIE TIBA HII KUOKOA NDOA YAKO NA KUOKOA KUKIMBIWA NA UMPENDAYE,

 ISABILO; Ni dawa itoayo mafanikio na utajili kwa watu walioshindwa kufanikiwa kimaisha, 

MWITE; Ni dawa ya mvuto kumvuta umpendaye na kumrudisha aliyembali na atakutimizia ahadi zote awe mwanamke au mwanaume. 

LUTA CD; Ni dawa inayotibu magonywa nyemelezi yanayopunguza kinga za mwili na kusababisha mwili kuzoofu na inaondoa miwasho na kuondoa kemikali na taka zinazozagaa mwilini. 

KISUKARI; Tunayo dawa ya DAYON inayotibu na kuzalisha insulin kwa wingi na kumfanya mwenye tatizo hili kupona kabisa ugonjwa wa kisukari, kwani husababisha misuli ya mwili kutokufanya kazi vizuri

MPIGIE DR DAGOTIMAN NDIYE SULUHISHO LA MATATIZO YAKO   0658920640/ 0754372325 / 0620806813
 
HUDUMA HII INAWEZA KULETWA POPOTE ULIPO OFISI ZETU ZIPO MBAGALA ZAKHEM DAR ES SALAAM.

TMA Yatahadharisha Ujio Wa Mvua Kubwa Katika Mikoa Ya Dar, Pwani Na Zanzibar

0
0
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari katika baadhi ya maeneo ya nchi kuwepo na vipindi vya mvua kubwa kwa saa 24 zijazo.
 
Taarifa iliyotolewa  Septemba 26 na TMA imeeleza kuwa vipindi vya mvua kubwa vinatarajiwa katika baadhi ya maeneo ya mkoa wa Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.

“Mawimbi makubwa yanayozidi mita mbili yanatarajiwa katika maeneo ya ukanda wote wa Pwani, huku upepo wa pwani ukitarajiwa kuvuma kwa kasi ya kilomiya 30 kwa saa kutoka Kusini – Mashariki kwa Pwani ya Kaskazini na kutoka Mashariki kwa Pwani ya Kusini,” ilisema taarifa hiyo.

Hali ya bahari inatarajiwa kuwa na mawimbi makubwa kiasi na matazamio kwa siku ya Ijumaa Septemba 28 ni kuendelea kwa mvua katika maeneo ya ukanda wa Pwani ya Kaskazini.

“Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua katika maeneo machache na vipindi vya jua, huku mikoa ya Kagera na Geita ikitarajiwa hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua,” ilieleza taarifa hiyo.

Wizara ya Afya yawatahadharisha wananchi kuhusu akaunti feki inayotumia jina la Waziri wa Afya Kutapeli Watu

0
0
WAZIRI  wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amekanusha vikali kuhusika na tangazo na umiliki wa ukurasa wa mtandao wa Facebook wenye chapisho la matapeli wa mtandaoni linalotangaza ajira za Shirika la Msalaba Mwekundu kwa watu 100 kila wilaya nchi nzima lilioandikwa TANZANIA RED CROSS JOB APPLICATION FORM.


Ummy Mwalimu kupitia akaunti yake ya Twitter ameandika: “Huu ni UTAPELI, Sihusiki na Sijui lolote kuhusu Kazi za Red Cross, na nimewaomba TCRA kufuatilia na kuwachukulia hatua wahusika/matapeli hawa.”

Katika tangazo hilo, muombaji wa ajira anatakiwa kutuma pesa kiasi cha Tsh. 10,000/= wanazodai kuwa ni za uanachama na kuzituma kupitia M-pesa namba 0767291550 (yenye jina la Mr. Shabu Lifumike, Ofisa Muajiri Mkuu).

Makanga 3 Power; Dawa Bora Nguvu Za Kiume

0
0
Kutibu nguvu za kiume dakika(10) na kupona muda wa siku tatu tuu. Kuimarisha misuli ya uume uliolegea, pia ipo Dawa ya kurefusha uume mfupi inchi NNE hadi saba na kunenepesha uume mfupi sentimita NNE.

Tiba ya kudumu kutibu maumivu ya mgongo,kiuno, tumbo kuunguruma na kujaa gesi, kupata choo vizuri, na kutibu uzazi, kutibu busha bila operesheni, kisukari, presha ,miguu kuuma, uzazi, fangas sugu, vidonda vya tumbo.

Ni docta bingwa wa kutibu magonjwa sugu, kutoa ndagu za utajiri kwa kutumia Pete, kazi ,cheni, mikufu maalumu ya bahati, una kesi umedhulumiwa Mali au pesa? Zitarudi muda wa Masaa matatu tuu.

Onana na Dr shilindes shida zako zote zitakwisha, anatoa Dawa za utajiri kwa wafanyakazi, wakulima, na wafugaji, wafanyabiashara na wachimba madini kwa kutumia pete, kazi kwa yeyote anaetaka kuwa na pesa nyingi.

Pia anaboresha akili kwa wanafunzi darasani, masomo na kufaulu mitihani pia kushinda bahati nasibu yeyote.

Pia tunatoa Dawa kumrudisha Mume, mke, mpenzi, hawara, kwa muda wa SAA moja tuu, na kuomba msamaha kwa kukupigia magoti na yeyote yule, unaemtaka kimapenzi au kuoana, utampata na kumfunga asitoke nje ya ndoa daima na kutekeleza shida zako zote. Kupunguza unene, kupunguza matiti makubwa, tumbo na nyama uzembe muda wa siku sita unapata saizi uipendayo.

Kutoa makovu mwilini, chunusi, upele na mabaka, pia tunayo Dawa ya kuongeza hipsi, makalio, mguu wa bia na kupata shepu safi kwa muda wa siku saba tuu.

Wa mikoani mtapata huduma popote mlipo.
Tupo dar es salam mbagala rangi tatu.

Mawasiliano simu namba: 0784 460 348.

Mwanafunzi Kortini Kwa Kumpa Mimba Mwanafunzi Mwenzie

0
0
Mwanafunzi wa kidato cha tano shule ya Sekondari ya Mbezi (19), Juma Idd  jana Jumatano Septemba 26, 2018 amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya wilaya ya Kinondoni kwa tuhuma za kumpa ujauzito mwanafunzi wa darasa la tano mwenye miaka 14.

Mwanafunzi aliyepewa ujauzito wenye miezi mitano sasa anasoma shule ya msingi Kunduchi na tayari ameshaanza kliniki katika zahanati ya Tegeta.

Akisoma shtaka hilo jana mbele ya hakimu Joyce Mushi, wakili wa Serikali Daisy Makakala amedai tarehe tofauti kuanzia Aprili hadi Septemba mshtakiwa alimwingilia kimwili mwanafunzi huyo huku ukijua ni kosa kisheria.

Baada ya kusomewa shtaka hilo mshtakiwa alikana kosa na wakili Makakala aliieleza mahakama kuwa upelelezi haujakamilika, kumuomba hakimu apange tarehe nyingine.

Hakimu Mushi alimweleza mshtakiwa huyo kuwa dhamana yake iko wazi kwa kuwa shtaka hilo linalomkabili linadhaminika.

Hivyo Hakimu Mushi alimtaka mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wenye barua ya mwenyekiti wa serikali ya mtaa na kila mmoja atasaini bondi ya Sh1 milioni, masharti ambayo mshtakiwa huyo aliyatimiza na kuachiwa huru kwa dhamana.

Lugola Awapa Wiki Mbili Polisi Kigoma Kusambaratisha Ujambazi Wilayani Kibondo

0
0
Na Felix Mwagara, MOHA-Kibondo
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola ametoa wiki mbili kwa Jeshi Polisi Mkoa wa Kigoma, kuhakikisha linakomesha matukio ya ujambazi yaliyokithiri katika Wilaya ya Kibondo pamoja na sehemu zingine mkoani humo.

Lugola aliongeza kua, katika kupambana na majambazi hao ambao wanasumbua wananchi  wilaya hiyo ya Kibondo na kukosa amani katika maeneo yao, polisi ifanye operesheni maalumu kuwatia mbaroni watuhumiwa hao.  

Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Community Centre mjini Kibondo, leo, Lugola alisema katika operesheni hiyo pia itambatana na utoaji onyo kwa watu wasio waaminifu wanaowahifadhi raia wa kigeni ambao wengi wao ni wahalifu.

‘’Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, natoa wiki mbili tu, kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya fanyeni operesheni ya kuwasaka majambazi hawa usiku na mchana mpaka jambazi wa mwisho awe amekamatwa,’’ alisema Lugola.

Lugola alisema haiwezekani tukasalimu amri kwa majambazi, haiwezekani kunyoosha mikono kwa jambazi  waliopo katika maeneo mbalimbali wa wilaya hiyo pamoja na mkoa kwa ujumla.

Waziri Lugola pia aliwataka wananchi wilayani humo kutoa taarifa polisi za wahalifu hao ili kuwezesha operesheni hiyo ifanikiwe zaidi na wananchi waweze kuishi kwa amani na kufanya shughuli zao za kuijenga nchi.

Waziri huyo pia licha ya kusema anajua changamoto mbalimbali zinazowakibili polisi ikwemo ukosefu wa magari lakini aliwataka aliwataka wawahi katika  matukio ya uhalifu yanapotokea, wanaweza kutumia pikipiki ili kuwahi kwa wakati katika matukio hayo.

Waziri Lugola yupo katika ziara ya kikazi Mkoa wa Kigoma ambapo anatembelea Wilaya zote mkoani humo kwa kufanya kikao na watumishi walio chini ya wizara yake pamoja na kuzungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara kwa ajili ya kusikiliza kero zao pamoja na kuzitatua.

RC Makonda Atuma Ombi Kwa Rais Magufuli

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Joh Pombe Magufuli kufanya ziara ya mara kwa mara kwa Mkoa wa Dar es salaam ili kuwawezesha wananchi wa mkoa huo kumuona kiongozi huyo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa matumizi ya barabara ya juu Flyover Tazara jijini Dar es salaam Mkuu wa Mkoa Paul Makonda amemuomba Rais Magufuli kuiongeza Dar es salaam kwenye ziara zake ili aweze kukutana na wananchi wa jiji hilo.

“Mheshimiwa Rais sina mengi ya kuomba kwako zaidi ya kukuomba unapofanya ziara zako mkoani uwe unakuja na Dar es salaam walau uwe unakutana na wananchi wa Mbagala, Yombo, pamoja na maeneo mengine maana hawa huwa wanakukumbuka sana, pia huwa tunaona wivu unapofanya ziara mikoani lakini kwetu hatukuoni.” Amesema Makonda

Aidha mkuu wa huyo mkoa ameeleza Daraja la Nyerere lililopo Kigamboni linaingiza shilingi milioni 800 kwa mwezi kupitia tozo zinazotolewa na watumiaji wa daraja hilo pamoja na kueleza changomoto ya utapeliunaofanywa na baadhi ya madalali Dar es salaam kwa kushirikiana na taasisi za kifedha.

Jishindie Gari la Bure Toka Japan.....Kushiriki Ni Bure Kabisa

Kauli ya kwanza ya Msanii Maua Sama baada ya kutolewa mahabusu kwa Dhamana

0
0
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Maua Sama ameweza kufunguka na kueleza jinsi alivyopitia katika kipindi kigumu akiwa mahabusu. 

Maua Sama alikamatwa na Polisi wiki mbili zilizopita kwa tuhuma za kuidhihaki pesa ya Tanzania kwa kupost video inayoonesha watu wakizichezea pesa za kitanzania.

Juzi tarehe 25 Maua Sama na mtangazaji wa CloudsFm Soudy Brown waliachiwa majira ya saa moja usiku kwa dhmana.

Na hii ndio kauli yake:-

LIVE: Rais Magufuli akizindua Flyover ya TAZARA

0
0
Mamia ya wananchi wamejitokeza kwenye sherehe za uzinduzi wa daraja la juu ‘flyover’ la Mfugale lililopo katika eneo la Tazara jijini Dar es Salaam.

Daraja hilo linazinduliwa rasmi leo Septemba 27, 2018 na Rais John Magufuli 

==>>Fuatilia tukio hilo hapo chini

Kwanini Baadhi ya Wanaume Wana Maumbile Mafupi na Upungufu wa Nguvu za Kiume? Suluhisho Hili Hapa

0
0
KWANINI BAADHI YA WANAUME WANA MAUMBILE MAFUPI NA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME... DR SITTA NDO SULULISHO LAKO

Tatiza, hili limekuwa likiwaathiri watu wengi sana kisaikolojia hasa baadhi yao kujiona wako tofauti na wanaume wengine. Kwa kawaida, mwanaume anatakiwa awe na uume, usiopungua nchi 6-7au-8 ,vinginevyo mtu huyo anamatatizo.

Zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo hilo... baadhi ni  upungufu wa vichocheo vya, HORMONES ZA CETROGEN .

SUPER MIZIZI, ni dawa inayozalisha HORMONES ZA CETROGEN,na kufanya, uume kukuwa na kuongzeka sazi utakayo na kuzibua mrija iliyosinyaa,

NSHOLA; ni dawa bora, ya kurudisha nguvu za kiume kwa kutibu kabisa  tatizo hilo na kukupa  hamu ya  kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara nne 4 bila kuchoka 

Pia  kuna dawa za kutibu presha ya kupanda na kushuka, kisukari , kuondoa mafuta  mwilini na maumivu ya mgogo kiuno, matazo, ya hedhi kwa wanawake, hedhi zisizokuwa na mpangilio.

NKANYA; ni dawa ya mvuto wa kimapenzi ,mchumba mpenzi aliyekuacha, mke, mme atakurudia .

NKOMA; Ni dawa kuongeza HIPS na mguu wa bia kwa wadada ,

NGAKAMA ,ni dawa ya kutibu miguu kufa ganzi na kuwaka moto, huduma zetu ,zipo ,vizuri, popote pale dawa utaletewa! 

DR SITTA, amebobea kwa tiba asili

SONGEA BOMBAMBILI, SHINYANGA- KAHAMA MJINI, 

KWA MAELEZO ZAIDI  PIGA SIMU; 0763172670/ 0715172670,/

WOTE  MNAKARIBISHWA... KAMA, UTAKUWA NA TATIZO, UTAHUDUMIWA,

Rais Magufuli Ataka FlyOver ya TAZARA Ifungwe Kamera

0
0
Rais John Magufuli ameagiza kufungwa kamera katika daraja la juu ‘flyover’ la Mfugale  lililopo eneo la Tazara  lifungwe kamera ili kuwabaini watu watakaokiuka  taratibu za usalama barabarani.

Mbali na daraja hilo, pia ameagiza madaraja mengine makubwa yanayojengwa nchini kufungwa kamera.

Ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Septemba 27, 2018 wakati akizindua  daraja hilo.

“Ili hata pale anapokuja mtu amelewa na kusababisha ajali tumjue ni nani hata kama atatelekeza gari lake hapo,” amesema.

“Tutengeneze vitu vizuri vitusaidie na si kutuletea matatizo mengine ambayo yanaweza kuzuilika.”

Kiongozi mkuu huyo wa nchi ametaka miradi yote ya ujenzi inayosimamiwa na DMDP iwekwe chini ya Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (Tarura).

“Tarura ilipitishwa na Bunge hatuwezi kuwa na chombo kingine kinachojitegemea wakati tulishakubaliana. Hivyo barabara, madaraja, mifereji inayojengwa yote iwe chini ya Tarura,” amesema.

“Na lengo la kufanya hivi ni kutaka kuhakikisha fedha zote zinazoelekezwa katika miradi zinatumika ipasvyo.”
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images