Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Updates: Miili Mingine Mitano Yaopolewa Ajali MV Nyerere.....Waliofariki Dunia Wafika 157

$
0
0
Idadi ya watu waliofariki dunia katika ajali ya kivuko cha MV Nyerere kilichozama juzi mchana Septemba 20, 2018 imefikia 157  huku uokoaji ukiendelea.

Akizungumza akiwa katika eneo la tukio, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amesema miili mingine imeopolewa leo asubuhi Septemba 22, 2018.

“Leo miili mingine imeopolewa lakini bado uopoaji unaendelea,” amesema.

Amesema vikosi vya uokoaji vinaendelea na shughuli ya uokoaji na ikitarajiwa shughuli hiyo kufanyika hadi kesho Jumapili.

“Vikosi vya uokoaji vinafanya kazi yake vizuri na tunaendelea na tunatarajia Mungu akijalia hadi kesho tutakuwa tumekamilisha,” alibainisha mkuu huyo wa mkoa.

Mongella amesema kuwa baadhi ya miili imeshatambuliwa huku kazi ya utambuzi akisema inaendelea.

“Hadi jana (Ijumaa Septemba 21, 2018) miili 116 imeshapata ndugu na tunaamini miili mingine itatambulika maana wananchi wanaendelea kuwasili kuja kuitambua,” amesema Mongella.

BREAKING: Mhandisi Wa Mv Nyerere Aokolewa Akiwa Hai ....Lakini hawezi kuongea

$
0
0
Mmoja wa Mainjinia wa Kivuko cha Mv.Nyerere kilichopata ajali ya kuzama ziwa Victoria ameokolewa muda mfupi uliopita akiwa hai japo hali yake ni mbaya lakini anapatiwa huduma.

Imeelezwa fundi huyo alikuwa amekwama kwenye moja ya vyumba vya manahodha na alikuwa akigongagonga vitu ili waokoaji wamsikie jambo ambalo limetimia.

Lakini hawezi kuongea kutokana na hali yake kuwa mbaya baada ya kukaa ndani ya maji kwa takribani siku tatu.

Katibu Mkuu wa CCM Dk Bashiru Ally atuma salamu za rambirambi ajali ya MV Nyerere

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM Dk Bashiru Ally ametuma salamu za rambirambi kwa Rais John Magufuli na Watanzania kutokana na ajali ya kivuko cha MV Nyerere kilichozama juzi Septemba 20, 2018 Kisiwa cha Ukara, wilayani Ukerewe Mkoa wa Mwanza.

Ametuma salamu hizo leo Jumamosi Septemba 22, 2018 akiwa mkoani Mtwara kwa ajili ya ziara ya kikazi, kulazimika kubadili ratiba ya ziara hiyo.

“Taifa letu lipo kwenye msiba na kama mnavyojua bendera zinapepea nusu mlingoti. Tuendelee kuwaombea na tutafakari namna tunavyoweza kukabiliana na majanga yanayotokea,”amesema Dk Bashiru.

“Tupate fursa ya kutafakari na kujadiliana namna nzuri ya kusimamia vyombo vyetu vya usafiri na shughuli zote zinazohusu huduma kwa Watanzania.”

Amesema kutokana na ajali hiyo amelazimika kubadili ratiba ya ziara yake na kuungana na Watanzania wengine katika maombolezo.

 “Sijasitisha  ziara yangu lakini itabidi baadhi ya ratiba zirekebishwe ziendane na maombolezo,” amesema.

“Nimewatuma wajumbe wawili Humphrey Polepole (Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM) na  Kanali Lubinga (Ngemela-Katibu wa Siasa na Uhuasiano wa Kimataifa wa CCM) kwenda kule wafuatilie  namna shughuli zinavyoedelea.”

Updates: Waliofariki Dunia Ajali ya MV Nyerere Wafika 166....Serikali Kutoa 500,000 kwa Mwili Utakaotambuliwa

$
0
0
Miili 116 kati ya yote iliyoopolewa baada ya kuzama kwa Kivuko cha MV Nyerere juzi Septemba 20, 2018 imetambuliwa na ndugu.

Ndugu, jamaa na wananchi wamepiga kambi eneo la bandari ya Bwisya kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe tangu kazi ya uokoaji ilipoanza.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 22, mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amesema Serikali itatoa ubani wa Sh500, 000 kwa familia, kwa kila maiti itakayotambuliwa na kuchukuliwa kwa ajili ya maziko.

Tangu asubuhi leo, miili 30 imeopolewa na kufanya idadi ya miili iliyoopolewa hadi sasa kufikia 166 baada ya mili mingine 136 kuopolewa hadi jana jioni.

Miili yote iliyoopolewa imehifadhiwa katika Kituo cha afya cha Bwisya.

PICHA: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Atembelea Eneo La Ajali Ya Kivuko cha MV Nyerere

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela  (katikati) na Mkuu wa Mjeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo kuelekea katika eneo kilipozama Kivuko cha MV Nyerere katika kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe, Septemba 21, 2018. Kivuko hicho kinatoa huduma kati ya Kisiwa  cha Ukara ba JKisiwa cha Bugorola. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama eneo kilipozama   Kivuko cha Mv Nyerere kinachotoa huduma kati ya kisiwa cha Ukara na Bugorola  wilayani Ukerewe wakati alipowasili kwenye kisiwa cha Ukara kujionea shughuli za uokoaji Septemba 21, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Jipatie Tiba ya Asili ya Ngiri, Vidonda vya Tumbo,Kisukari na Nguvu za Kiume

$
0
0
Super nzoka IKEMEKO TRDITONAL clinic Ni dawa ya Asili ya vidonge iliyotengenezwa kwa techknojia ya kisasa na ubora wa hali ya juu 

Huongeza nguvu za kiume maradufu hata kwa wale wasiojiweza kabisa kufanya tendo la ndoa na wapo abao hata wakifanya hushindwa kutoa maji maji maji ambayo ndani yake kuna mbegu za kiume zinazotakitakiwa kurutubisha yai

Dawa hii huboresha na tunatibu nakumaliza matatizo haya kwa muda mfupi tu na haina madhara kwa mtumiaji yeyote hata wa umri wa miaka 80 na kuendelea.... inaongeza hamu, urijali kwa wanaoshindwa kuendelea na tendo la ndoa.

Huanza kufanya kazi baada ya dakika 60 tu na kufanya uchelewe kufika kileleni dakika 20 kwa tendo la kwanza itakuwa unauhakika wa kurudia tendo la ndoa zaidi ya Mara tatu bila kuhisi kuchoka 

SILYA; inakuza uume uliosinyaa kurefusha umbile dogo urefu inchi (6-9)na unene wa cm 4 za upenyo kwa wenye kasoro za kimaumbile na walioathiriwa na kupiga punyeto pamoja na matatizo ya kiafya

Tiba hii ni ya kudumu.Pia tunatibu ngiri ya kupanda na kushuka,tumbo kuuguruma chini ya kitovu ,kaswende kisukari ,maumivu ya mgongo, kiuno, kutopata choo vizuri na uvimbe kupitia njia ya mkojo, presha, vidonda vya tumbo

Wasiliana Nasi kwa namba;  0716343218,0789289945. TUNAPATIKANA MBAGALA ZAKIEM STENDI ya musanga

Dawa Za Nguvu Za Kiume Na Kukosa Hamu Ya Tendo La Ndoa

$
0
0
Asilimia 45-80 ya wanaume wapo tofauti na wengine kwa kutowatimizia vyema wake au wapenz wao na kuwasababishia kutoka nje ya mahusiano yao. 

NINI CHANZO CHA HAYO? Kupiga punyeto,Ngiri, Vidonda vya tumbo, Korodani moja kuvimba, Msongo wa mawazo, Presha, Magonjwa ya zinaa, Kufanyiwa tohara ukiwa na umri mkubwa, Kisukari. 

DR. LUTAJA Sasa anakuletea tiba sahihi ya tatizo la Nguvu za kiume. 

NTOMBO :Hii hutibu na kuponya kabisa tatizo la Nguvu za kiume, utakuwa na uwezo wa kufanya tendo la ndoa zaidi ya mara tatu bila kuchoka na itakufanya uchelewe kafika kileleni kwa mda wa dk 20-45. Dawa hii imechanganywa na miti 18,Hata wazee wenye umri mkubwa wa zaidi ya miaka 85 wanapona kabisa okoa mahusiano yako, ndoa yako sasa. 

SUNGURURU MIX:Ndio tiba sahihi kwa wale wenye maumbile madogo hurefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo nchi 3-8 na unene cm 2-5,dawa hii ipo katika mfumo wakupaka nakunywa na haina madhara yoyote kwa mtumiaji :Hii ni tiba tofauti kabisa nazile ambazo umekwisha wahi kutumia. 

Pia tunadawa za Kupandisha nyota , Uzazi, Pumu, Malaria sugu, miguu kuwaka moto, Kaswende, Kisonono pamoja na mvuto wa mpenzi.

 DR. LUTAJA ANAPATIKANA DAR-ES-SAALAM Simu 0713-821823 kwa wale wa mikoani huduma hii utaipata popote ulipo.

Ufafanuzi: Serikali Yasema Jumatatu ni Siku ya Kazi Kama Kawaida.... Rais Alitangaza Maombolezo, Sio Mapumziko

$
0
0
Serikali kupitia kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa imetoa ufafanuzi kuwa Jumatatu  Septemba 24, 2018  ni siku ya kazi kama kawaida.

Baada ya Rais Magufuli kutangaza siku 4 za maombolezo kufuatia ajali ya MV Nyerere iliyoua watu 166, kumekuwa na mkanganyiko kidogo  kwa baadhi ya watu kudhani Jumatatu itakuwa ni mapumziko.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Msigwa amesema Rais Magufuli alitangaza siku 4 za maombolezo  na sio siku za Mapumziko.

Msigwa ameandika;"Napenda kutoa ufafanuzi kuwa Jumatatu tarehe 24 Septemba, 2018 ambayo ni siku ya mwisho ya maombolezo ya Kitaifa, itakuwa ni siku ya kazi kama kawaida. Mhe. Rais Magufuli ametangaza siku 4 za MAOMBOLEZO na sio MAPUMZIKO."

Waziri Wa Afya Atoa ONYO Kwa Wanaosambaza Picha za Waliofariki Ajali ya MV Nyerere

$
0
0
Waziri wa Afya maendeleo ya Jamii jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu ameonya usambazaji wa picha miili ya ajali ya Mv-Nyerere iliyotokea juzi Mkoani Mwanza kisiwa cha Ukala.

Kwa mujibu Waziri Mwalimu usambazaji wa picha hizo zinaongeza majonzi kwa ndugu na waathirika wa tukio la ajali ya Mv-Nyerere badala yake amewataka watanzania kutumia nafasi hiyo kuwaombea.

Ummy Mwalimu ameeleza hayo kupitia ukurasa wa Twitter.

"Ndugu zangu Watanzania, ninawaomba sana TUACHE KUSAMBAZA NA KUPOSTI PICHA ZA MAREHEMU WA AJALI YA MV NYERERE. 

"Tuheshimu Utu na Ubinadamu wao. Lakini pia watu wapo kwenye majonzi makubwa ya kupoteza wapendwa wao, hivi kuna faida gani kwa baadhi yetu sisi kuposti picha hizi za marehemu?. 

"Tafadhali tuwapunguzie maumivu familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu kwa kuto-posti picha hizi. Muhimu tuendelee kuwaombea familia za marehemu Mwenyezi Mungu awape subra na ustahamilivu ktk kipindi hiki kigumu. Aidha tuwaombee rehema wenzetu waliotangulia mbele ya haki. #MbeleYaoNyumaYetu "
aliimalizia Waziri Mwalimu.

Updates: Waliofariki Ajali MV Nyerere Wafika 196

$
0
0
Idadi ya watu waliofariki dunia katika ajali ya kivuko cha MV Nyerere kilichozama juzi mchana Septemba 20, 2018 imefikia 196, miili 60 imeopolewa kwa leo hadi muda huu na uokoaji bado unaendelea.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amesema miili mingine imeopolewa leo asubuhi Septemba 22, 2018 na kwamba vikosi vya uokoaji vinaendelea na shughuli ya uokoaji na inatarajiwa shughuli hiyo kufanyika hadi kesho Jumapili.

“Hadi jana (Ijumaa Septemba 21, 2018) miili 116 imeshapata ndugu na tunaamini miili mingine itatambulika maana wananchi wanaendelea kuwasili kuja kuitambua,” amesema Mongella.

Kangi Lugola Asema Wote Wanaotumia Ajali ya MV Nyerere Kama Mtaji wa Kisiasa Watakamatwa

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola, amewasili katika eneo la tukio kilipozama kivuko cha Mv Nyerere huko Ukara Ukerewe mkoani Mwanza. 

Lugola ametokea mkoani Kigoma ambapo amesitisha ziara yake ya kikazi  na kulazimika kuelekea Jijini mwanza kufuatilia ajali ya MV Nyerere.

Amesema  zoezi la uokoaji na uopoaji litaendelea mpaka hatua ya kivuko kuondolewa majini. 

Pia amesema wote wanaotumia ajali ya Kivuko cha MV Nyerere kama mtaji wa kisiasa watakamatwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria. 

“Hatuko tayari kupitia tukio hili kuchonganisha serikali na wananchi wake, tutakaowabaini tutawakamata”   Amesema Lugola

Breaking News: Waliofariki Ajali ya MV Nyerere Wafikia 209....Waliookolewa Wakiwa Hai ni 41

$
0
0
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Ujenzi Mhandisi Isaack Kamwele hadi sasa miili 209, imeopolewa na watu 41 wameokolewa wakiwa hai katika ajali ya kivuko cha Mv Nyerere kilichozama katika ziwa Victoria eneo la Ukara Ukerewe.

Waziri Kamwele amesema Miili 172 imetambuliwa, 37 haijatambuliwa, 112 imeshachukuliwa na ndugu kwa ajili ya mazishi na uokoaji bado unaendelea .

Maandalizi ya mazishi ya pamoja ya waliofariki ajali ya MV Nyerere Yameanza

$
0
0
Jeshi la polisi wakishirikiana na wananchi tayari wameshaanza kuchimba makaburi kwa ajili ya kuwapumzisha Marehemu waliofariki ktk ajali ya MV Nyerere. 

Hadi kufikia sasa takribani Miili 172 imetambuliwa, 37 haijatambuliwa, 112 imeshachukuliwa na ndugu kwa ajili ya mazishi

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumapili ya Septemba 23

Waliofariki dunia ajali ya kivuko cha MV Nyere wafikia 218....Mazishi Kufanyika Leo

$
0
0
Miili 171 kati ya 218 iliyoopolewa baada ya kuzama kwa Kivuko cha MV Nyerere juzi Septemba 20, 2018 imetambuliwa na ndugu.
 
Akizungumza na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) jana  Jumamosi Septemba 22, 2018 saa 2 usiku Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella alisema wapo baadhi ya ndugu wanaotaka kuwazika wapendwa wao kisiwani humo.

Alisema kwa sasa taratibu mbalimbali zinafanyika, ikiwa ni pamoja na jitihada za kukinyanyua kivuko hicho kazi ambayo itafanywa na timu ya waokoaji.

“Kesho ( leo)  kuanzia saa 2 asubuhi kamati itafanya maziko ya miili 47,” alisema Mongella.

Miili iliyoopolewa imehifadhiwa katika Kituo cha afya cha Bwisya.


Waziri Mkuu kuongoza mazishi waliofariki dunia kwenye kivuko cha MV Nyerere....Hadi Sasa Idadi Imefika 225

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwasili katika kijiji cha Bwisya Kisiwa cha Ukara kuongoza ibada ya mazishi ya baadhi ya watu waliopoteza maisha katika ajali ya Kivuko cha MV Nyerere iliyozama Septemba 20, 2018.

Akizungumza leo Jumapili Septemba 23, 2018 mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella amesema kiongozi huyo atajumuika na viongozi wengine ambao wapo kisiwani hapa kushiriki mazishi  ya miili ambayo haijatambulika na ambayo ndugu wameomba izikwe kwa utaratibu ulioandaliwa na Serikali.

Zaidi ya miili 225 imeopolewa, miili 172 kutambuliwa na 112 imechukuliwa na ndugu kwa ajili ya mazishi huku 37 ikiwa haijatambuliwa hadi leo asubuhi.

Mkebe Spesho Wa Dawa Ya Mitishamba Yenye Uwezo Mkubwa Wa Kumsaidia Mtu Aliyeathirika Na Upungufu Wa Nguvu Za Kiume

$
0
0
Je, Unamatatizo haya na yamekusumbua kwa muda mrefu bila kupata tiba?

Wanaume wengi wanaupungufu wa nguvu za kiume. na kuwa na maumbile madogo ya kiume. 

Magonjwa kama. kisukari. presha, ngiri, kolodani kuvimba busha tumbo kuunguruma kujaa ngesi na kutopata choo vizuri , punyeto nk huchangia kwa kiasi kikubwa upotevu wa nguvu za kiume 

Tumia dawa nzuri ya mitishamba ambayo haina madhara kwa mtumiaji ata uwe na miaka 80 ,    inatibu na kuponyesha matatizo haya yote         

 SUPER SHAFT;  ni dawa yenye uwezo mkubwa wa kuogeza nguvu za kiume mara dufu na maumbile madogo ya uume                                    
 (1) itakufanya uwe na nguvu za ajabu ukiwa unafanya tendo la ndoa                                        
 (2) inaongeza hamu ya kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara tatu bila kuchoka.                           
 (3) itakufanya uchelewe kufika kileleni ndani ya dk 30 na kuimalika uume zaidi                                  
(4) pia itakupa nguvu za kusimamisha uume wako barabara kama msumari wakati wa tendo la ndoa 
    
NYATI POWER; inarefusha na kunenepesha uume saizi utakavyo kuazia 1_8 unene  sm 2_4 
(1) inaimalisha mirija ya uume iliyo legea ama kusinyaa                                                                       
(2) inasaidia kusafisha mirija ya kwenye uume na hivyo kusaidia kuongeza kasi ya msukumo wa damu kwenye mishipa ya uume                        
(3) Husaidi kuurudisha nje uume uliyoigia ndani      
(4) inasaidia kuongeza manii nyingi ambazo zina viini vya uzazi                                                              
(5) Husaidia kutibu madhara ya punyeto matumizi makari ya madawa ya kizungu mirungi bangi na sigara

Tunatibu Magonjwa Yote Sugu Ngiri Kolodani Kuvimba Busha Bila Kufanyiwa Opresheni Tezi Dume Kisukari Presha Aina Zote Ugonjwa Wa Moyo Kwikwi Kichomi Miguu Kufa Ngazi Nk

Tunapatikana Magomeni Mikumi Karibu Na Kanisa Katoriki La Roma

Tumaini Tradition Clinc Ndiyo Sululisho La Matatizo Tote 

PIGA SIMU 0745_495181 AU  0682_ 644040                               
WOTE MNAKARIBISHWA TUMAINI TRADITION CLINC 
 

Diamond Ammwagia SIFA Kibao Zari..."Umenizalia watoto wazuri, ndio maana sikuongelei hovyo kwenye interview "

$
0
0
Diamond Platnumz amevunja ukimya kuhusu Zari The Bosslady kwa kumshukuru kuwa mama mzuri kwa watoto wake wawili.

Ujumbe huu unakuja mara baada ya takribani miezi nane tangu walivyoachana na kila mmoja kuendelea na maisha yake. Hiyo ni katika kumtakia Kheri ya siku yake ya kuzaliwa.

Diamond amemueleza Zari siku zote amekuwa akimuheshimu ndio maana hakuna siku amefanya interview kuzungumzia ni kitu gani kilitokea kati yao hadi kuachana. 

Kupitia ukurasa wake Instagram ameandika;

"A very special Birthday to the Mother of my Beloved kids...Thank you for blessing me with 2 amazing & cute Kids and thank you for continue being a good Mother to my Kids....Trust me, no matter how crazy & a proud man you think i might be, but am always grateful and i do respect you for that.

"That why, you've never heard or saw me on any interview talking anything about you....not even talking about my side point of what happened to us!!...coz the kids you blessed me with, means a lot to me.....and that is what made Love, respect and take you more than a blood sister / Brother for Life....May God bless you with long life, Happiness, and More Winning!!!"

Kauli ya Diamond unakuja ikiwa ni siku mmoja imepita tangu Hamisa Mobetto ambaye ni mzazi mwenzie na muimbaji huyu pia, kufanya Mahojiano na kipindi cha The Playlist cha Times FM na kueleza yote yalitokea kati yao hadi kuachana, ugomvi wa kifamilia na shutuma za kulogana.

Oparesheni Tokomeza ZERO Ya DC Jokate Mwegelo Yapata Milioni 125

$
0
0
Jana September 22, 2018 ndio ilikuwa harambee ya kuchangia Programu iliyoanzishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo kwa ajili ya kutokomeza Zero.

Program hiyo imelenga kuinua kiwango cha ufaulu wilayani humo kwa kuhakika wanafunzi wanakuwa na madarasa mazuri ya kusomea, vifaa na chakula. 

==>.Soma taarifa kamili ya Jokate Mwegelo hapo chini;

Kutokana Na Maombolezo Ya Msiba Ukerewe, Serikali ya Wilaya ya Kisarawe kwa pamoja tuliamua kuhairisha shamrashamra za programu yetu ya Tokomeza Zero Harambee Pale Minaki Sekondari, tukasimama na kuombea ndugu zetu waliopoteza maisha lakini pia kutoa faraja kwa kuchangia Milioni Moja kama rambirambi kutoka Wilaya ya Kisarawe. .

Lakini tuliruhusu waliofika kuchangia na baada ya kupiga mahesabu leo tumeweza kuchangisha Milioni 125.062 katika awamu hii ya kwanza. Hii ahadi ya michango ya pesa taslimu imevuka lengo letu la awali ambalo lililuwa ni Milioni 100 ilituweze kuhudumia makambi ya wanafunzi mpaka mwezi wa kumi na moja ambapo wataanza mitihani yao ya mwisho ya taifa. .

Napenda kuchukua fursa hii kuwashukuru sana wananchi wenyeji wa Kisarawe kwa kuitikia wito kwa wingi sana ila pia na wadau wetu kutoka nje ya Kisarawe. Tunawashukuru sana. Mungu awaongezee pale mlipopunguza. .

Kwa kipekee nimshukuru Ndg. Masanja Kadogosa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika La Reli Tanzania (TRC) na Wakandarasi Yepi Merkezi kwa kuahidi kujenga madarasa wenyewe na kuchangia chakula kwenye makambi yetu. Reli ya Kisasa inayojengwa inapita Kisarawe na tunawezesha ujenzi huu kwa ku-supply malighafi za ujenzi. Kwahiyo Kisarawe ni wadau wakubwa wa TRC. .

Naendelea kuwakaribisha wadau mbalimbali kutuunga mkono kwenye Programu hii ya Tokomeza Zero awamu zinazofuata ni kuboresha mazingira ya kusoma na kufundisha ikiwa ni kuhakikisha miundombinu mbalimbali ya Elimu inapatikana. Na pia tutakuwa na Tokomeza Zero Inspirational Talks - kufuata wanafunzi na jamii walipo na kuongea nao juu ya umuhimu wa Elimu.

Jipatie Tiba ya Asili ya Ngiri, Vidonda vya Tumbo,Kisukari na Nguvu za Kiume

$
0
0
Super nzoka IKEMEKO TRDITONAL clinic Ni dawa ya Asili ya vidonge iliyotengenezwa kwa techknojia ya kisasa na ubora wa hali ya juu 

Huongeza nguvu za kiume maradufu hata kwa wale wasiojiweza kabisa kufanya tendo la ndoa na wapo abao hata wakifanya hushindwa kutoa maji maji maji ambayo ndani yake kuna mbegu za kiume zinazotakitakiwa kurutubisha yai

Dawa hii huboresha na tunatibu nakumaliza matatizo haya kwa muda mfupi tu na haina madhara kwa mtumiaji yeyote hata wa umri wa miaka 80 na kuendelea.... inaongeza hamu, urijali kwa wanaoshindwa kuendelea na tendo la ndoa.

Huanza kufanya kazi baada ya dakika 60 tu na kufanya uchelewe kufika kileleni dakika 20 kwa tendo la kwanza itakuwa unauhakika wa kurudia tendo la ndoa zaidi ya Mara tatu bila kuhisi kuchoka 

SILYA; inakuza uume uliosinyaa kurefusha umbile dogo urefu inchi (6-9)na unene wa cm 4 za upenyo kwa wenye kasoro za kimaumbile na walioathiriwa na kupiga punyeto pamoja na matatizo ya kiafya

Tiba hii ni ya kudumu.Pia tunatibu ngiri ya kupanda na kushuka,tumbo kuuguruma chini ya kitovu ,kaswende kisukari ,maumivu ya mgongo, kiuno, kutopata choo vizuri na uvimbe kupitia njia ya mkojo, presha, vidonda vya tumbo

Wasiliana Nasi kwa namba;  0716343218,0789289945. TUNAPATIKANA MBAGALA ZAKIEM STENDI ya musanga
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live


Latest Images