Hatimaye Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limetoa
taarifa ya wizi uliotokea katika Benki ya Barclays, Tawi la Kinondoni
Aprili 15, mwaka huu, likisema tukio hilo lilipangwa ndani ya benki
hiyo.
Katika taarifa yake jana, Kamanda wa Kanda hiyo,
Suleiman Kova alisema watu 13 akiwamo meneja wa tawi hilo na meneja wake
wa uendeshaji wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za
Wizi wa milioni 500 Benki ya Barclays: Mameneja wa benki hiyo watiwa mbaroni.....Uchunguzi wabaini kuwa tukio hilo lilipangwa na robo tatu ya fedha iliibiwa siku moja kabla ya tukio
↧
↧
Trafiki afia ndani ya daladala aliyoikamata mkoani Kilimanjaro..."wakiwa njiani kuelekea kituoni ghafla yule trafiki akawa haongei",anasema shuhuda wa tukio hilo
Ofisa wa polisi mwenye cheo cha Koplo, Wilson Mwakipesile wa
Kikosi cha Usalama Barabarani mkoani Kilimanjaro amefariki dunia ghafla
akiwa ndani ya daladala alilokuwa amelikamata.
Hata hivyo, haikujulikana mara moja iwapo trafiki
huyo alifariki dunia akiwa njiani kulipeleka gari hilo kituo cha polisi,
alifariki muda mfupi baada ya kufika kituoni au wakati anapelekwa
hospitali.
↧
Wapinzani watoa sababu za kususa na kutoshiriki sherehe za miaka 50 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani wametoa sababu
zilizowafanya wasihudhurie sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Katika sherehe hizo zilizofanyika Jumamosi katika
Uwanja wa Uhuru, viongozi wa vyama vikuu vya upinzani, Chadema, CUF na
NCCR-Mageuzi hawakuonekana.
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alisema
kutokuonekana kwao
↧
Askari 6 wa kikosi cha usalama barabarani ( Trafiki) wafukuzwa kazi kwa tuhuma za kuomba,kushawishi na kupokea rushwa
Jeshi la
Polisi Mkoani Mbeya limewafukuza kazi Askari 6 wa kikosi cha Usalama
barabarani Wilaya za Rungwe na
Mbeya kwa tuhuma za kuomba,kushawishi na kupokea rushwa.
Kamanda wa
Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi amewatataja Askari hao kuwa
ni pamoja na waliokuwa wakifanya kazi wilaya ya Mbeya barabara ya Mbeya/Tunduma
eneo la Songwe ambao ni Copro Jonson,PC Rymond na PC Simon.
Msangi
↧
Wanafunzi watatu wapoteza maisha wakiogelea kwenye ‘Swimming Pool’ jijini Dar
Simanzi na vilio jana vilitawala katika Mtaa wa Kijitonyama
Mpakani A, baada ya watoto watatu wa familia jirani kufariki dunia baada
ya kuzama katika bwawa la kuogelea walipokuwa wakisherehekea siku ya
kuzaliwa mtoto mwenzao aliyetimiza mwaka mmoja.
Tukio hilo lilitokea juzi jioni katika Hoteli ya Landmark, Kunduchi Beach Dar es Salaam.
Waliofariki katika ajali hiyo ni Ndimbumi
↧
↧
Basi la Hood ( Mbeya - Arusha ) lateketea kwa moto eneo la Wami, Pwani
↧
Husna Iddi Kisoma, mkazi wa mkoa wa Pwani atiwa mbaroni na jeshi la polisi kwa tuhuma za kuzinyofoa sehemu za siri za mumewe katika ugomvi wa wivu wa mapenzi
Jeshi la polisi mkoa wa Pwani linamshikilia Husna Iddi Kisoma (19) ,
mkazi wa Kisemvule Mkuranga mkoa wa Pwani kwa tuhuma za kumuua mumewe
Jumane Mwalami (21) baada ya kumvuta sehemu za siri na kuzinyofoa
kutokana na ugomvi uliosababishwa na wivu wa mapenzi.
Akizungumza na kipindi cha Maskani cha 100.5 Times Fm, kamanda wa
Polisi mkoa wa Pwani, Ulrich Matei ameeleza kuwa tukio hilo
↧
Picha za ajali ya basi la Sumry: Waliofariki dunia ni watu 19 wakiwemo askari wanne wa jeshi la polisi.
Baadhi ya miili ya wakazi wa
kijiji cha Utaho wilaya ya Ikungi, waliogongwa na basi la Summry ikiwa
katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa wa Singida
mjini humo.
************
ASKARI Polisi wanne wa
kituo cha Polisi Singida mjini na wakazi 15 wa kijiji cha Utaho tarafa
ya Ihanja wilaya ya Ikungi mkoani Singida,wamefariki dunia baada ya
kugongwa na basi la kampuni ya
↧
Airtel yazindua Whatsapp,Facebook na twitter BURE kupitia vifurushi vya yatosha....Ukijiunga na kifurushi chochote, bando lako halitakatwa kwa hii mitandao ya kijamii
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayoongoza kwa kutoa huduma
bora imezindua huduma ya kibunifu itakayowawezesha wateja wake kupata na
kuunganishwa kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook, Whatsapp na
twitter BURE kupitia huduma ya Airtel yatosha.
Akiongelea kuhusu huduma hiyo Mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa
Airtel Bi Beatrice Singano Mallya alisema” sasa ni bure kabisa kwa
↧
↧
Lundenga akiri kuwepo wasichana wanaotoa rushwa ya ngono kupata taji la Miss Tanzania
Mkurugenzi wa Kampuni ya Lino International Agency, ambao ni waandaji
wa Miss Tanzania, Hashim Lundenga amedai kuwa wasichana wengi
wanaoingia kwenye mashindano ya Miss Tanzania hufanya mbinu za
kuwalaghai baadhi ya watu kwenye kamati kwa kuwapa rushwa ya ngono ili
washinde taji la miss Tanzania.
Akizungumza na Global TV, Lundenga amedai kuwa kuna wasichana wanaoingia kwenye
↧
VIDEO ya Basi la Hood kutoka Mbeya - kwenda Arusha likiteketea kwa moto eneo la Wami, Pwani
↧
UKAWA waruhusiwa kufanya mkutano wa hadhara Zanzibar leo
Hatimaye mkutano wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa),
uliokuwa umezuiwa kupisha sherehe za Muungano utafanyika leo katika
Viwanja vya Kibandamaiti, Unguja baada ya kupata baraka za polisi.
Mkutano huo awali ulikuwa ufanyike Aprili 19,
mwaka huu lakini ukazuiwa na polisi kwa maelezo kuwa intelijensia yao
ilionyesha kuwa kungekuwa na tishio la maisha ya watu. Hivyo
walishauriwa
↧
Magazeti ya leo Jumatano ya tarehe 30 April 2014
↧
↧
Binti aliyepigwa na Chid Benz yuko Mahututi....Kwa siku anazimia mara 5, Mama Chid atimuliwa nyumbani
MREMBO Mwanaisha Kiboye, mkazi wa Ilala, Dar anayedaiwa kupigwa na
mwanamuziki wa Kizazi Kipya Bongo, Rashid Makwilo ‘Chid Benz’, hali
imekuwa mbaya kwani yu mahututi.
Juzi Jumatatu, wakati staa huyo akipandishwa kizimbani katika
Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar kwa kesi hiyo, Mwanaisha alikuwa
akipumua kwa tabu kwenye chumba maalum katika Hospitali iitwayo Aviation
iliyopo maeneo
↧
Majambazi yaua polisi wawili mkoani Tabora....Yalivamia nyumbani kwa mfanyabiashara, Polisi walipofika walifyatuliwa risasi na kufariki papo hapo
Jeshi la Polisi limepata pigo kutokana na askari wake wawili kuuawa kwa
kupigwa risasi na majambazi...
Askari wawili wa jeshi hilo waliuawa kwa kupigwa risasi na majambazi katika Tarafa ya Usoke wilayani Urambo mkoani Tabora.
Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Suzan Kaganda, alisema jana kuwa tukio
hilo lilitokea juzi saa 2:30 usiku katika kijiji cha Usoke.
Kamanda Kaganda aliwataja
↧
Mgomo wa wafanyakazi wa kampuni ya ujenzi wa barabara ya magari yaendayo kasi ‘STRABAG’ waingia siku ya tatu leo....
Hali bado
si shwari katika kampuni ya ujenzi wa barabara ya magari yaendayo kasi
‘STRABAG’ iliyopo maeneo ya Ubungo jijini Dar, ambapo asubuhi hii Askari
wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wametanda eneo la ofisi hizo na
hakuna mfanyakazi yeyote wa kawaida anayeruhusiwa kuingia ndani.
Mgomo huo
ulioanza Jumatatu, Aprili 28 mwaka huu leo ulikuwa unaingia siku ya tatu
ambapo
↧
Sudani Kusini kujua hatima ya ombi lake la kujiunga na jumuiya ya Afrika Mashariki leo
Mkutano wa kumi na mbili wa viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unaaanza rasmi hii leo mjini Arusha nchini Tanzania.
Miongoni mwa maswala muhimu yatakayojadiliwa ni ombi la Sudan Kusini kutaka kujiunga na jumuiya hiyo.
Mkutano wa mwisho kama huu uliofanyika
mjini Kampala Uganda mwezi Novemba mwaka jana, uliweka bayana kwamba ni
katika mkutano huu wa Arusha, ambapo tarehe ya
↧
↧
Basi la AM Coarch lapata ajali Ipuli na kusababisha kifo cha mwanafunzi mmoja
↧
Rais Kikwete ahudhuria mkutano wa Afrika Mashariki jijini Arusha leo
Rais
Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya
katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Arusha(AICC) kwenye mkutano wa
12 wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika mjini
Arusha.Rais Kenyatta ndiye mwenyekiti wa jumuiya hiyo ya wananachama
watano.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Rais Yoweri
Kaguta
↧
Majambazi yajitangazia Serikali.....Wajiundia Jeshi la Ukombozi la Wana Sonjo , Wabuni bendera, mahakama na polisi yao ...Vijiji vyawatii, waendesha ujangili na ujambazi
Watu wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 500 wanaodhaniwa kuwa ni majambazi na
majangili, wamejiundia serikali ndani ya Msitu wa Igombe mkoani Tabora, JAMHURI inathibitisha.
Wamejiundia uongozi madhubuti pamoja na jeshi walilolipa jina la Jeshi la Ukombozi la Wana Sonjo.
Uchunguzi uliofanywa na JAMHURI
umebaini kuwa huenda idadi ya watu hao ikawa kubwa kuliko
inavyodhaniwa, kwani wanadaiwa
↧
More Pages to Explore .....