Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Diwani Mwingine CHADEMA Atimkia CCM

$
0
0
Diwani wa kata ya Kianyari wilayani Butiama, Mugingi Muhochi (Chadema) amejiuzulu wadhifa wake na kujiunga na CCM.

Akizungumza leo Septemba 11 Muhochi amesema amechukua uamuzi huo baada ya kuridhishwa na utekelezaji wa ilani ya CCM chini ya Mwenyekiti wa CCM, Taifa, John Magufuli.

Muhochi ambaye katika Uchaguzi Mkuu uliopita aligombea udiwani kupitia CCM lakini alishindwa katika kura za maoni za chama hicho na kuamua kujiunga na Chadema. Baada ya kujiunga na Chadema, alishinda udiwani kata ya Kianyari.

Muchochi amesema ameamua kurudi CCM kwa hiari yake mwenyewe na bila kushawishiwa na mtu yeyote.

Amesema katika kata yake yenye vitongoji 20 ambavyo vyote viko chini ya CCM amekuwa akipata ushirikiano wa kutosha licha ya tofauti ya vyama.

Akizungumza mara baada ya kumpokea diwani huyo, Katibu wa CCM wilaya ya Butiama, Ashura Suleman amempongeza diwani huyo kwa uamuzi alioufanya.

Dr. Kigwangalla Aruhusiwa Kutoka Hospitali

$
0
0
Dar es Salaam, 11/09/2018. Jopo la Madaktari Bingwa wa MOI linalomhudumia Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla limemruhusu kutoka wodini baada ya kujiridhisha kwamba afya yake imetengamaa na anaweza kurejea nyumbani ili kuja hospitali kama mgonjwa wa nje.

Jopo hilo la madaktari bingwa 5 wa kada za Mifupa, Usingizi na magonjwa ya ndani limefikia maamuzi hayo baada ya kumhudumia Dkt. Kigwangalla toka tarehe 12/08/2018 alipohamishiwa katika taasisi ya tiba ya Mifupa MOI kwaajili ya matibabu ya kibingwa ya mkono wake wa kushoto baada ya kupata matibabu mengine katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt.Respicious Boniface amemtakia kila kheri Dkt Kigwangalla katika kutekeleza majukumu yake ya kitaifa kwani ni muda muafaka wa kwenda kuwatumikia wananchi.

"Kwaniaba ya jumuiya ya Taasisi ya Mifupa MOI, tunakutakia kila la kheri katika kutekeleza majukumu yako ya ujenzi wa Taifa, ilikuwa heshima kubwa kuwa nawe hapa kwa kipindi cha takribani mwezi mmoja, tunaamini umeridhishwa na huduma zetu na kama kuna mahali umeona mapungufu ni vyema ukatujulisha ili turekebishe" Alisema Dkt Boniface.

Dkt. Boniface amemueleza Dkt. Kigwangalla kwamba kwa kuwa yeye ni daktari itakua rahisi kubaini mabadiliko yoyote ambayo sio ya kawaida na hivyo kushauriana na madaktari wa MOI ili kupata ufumbuzi.

Kwa upande wake Dkt. Kigwangalla ameushukuru uongozi wa Taasisi ya MOI, madaktari na wauguzi ambao wamekuwa wakimhudumia katika kipindi chote alipokuwa wodini.

"Nichukue fursa hii ya kipekee kuwashukuru watoa huduma, watanzania wote ambao mmekua mkiniombea na kunitembelea hapa hospitali baada ya kupata ajali, namshukuru Mungu afya yangu inaendelea vizuri sasa na nimeruhusiwa kwenda  nyumbani" alisema Dkt Kigwangalla.

Dkt. Kigwangalla alipata ajali ya b gari tarehe  4/08/2018 na kupata matibabu ya awali mkoni Manyara kabla ya kuhamishiwa  katika hospitali ya Taifa Muhimbili na baadae katika Taasisi ya Mifupa MOI.
Mwisho

CHADEMA Wamkaribisha Maalim Seif Kugombea Urais

$
0
0
Baraza la Wazee wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, kupitia kwa Mwenyekiti wake Hashim Issa Juma, limesema watamkaribisha Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi,  CUF Maalim Seif endapo chama chake kitakufa.

Akiongea na wanahabari leo, Hashim Issa amesema wao kama CHADEMA hawafurahishwi na kinachoendelea ndani ya  CUF na endapo kitakufa wao watajiimarisha zaidi Zanzibar na kumpa nafasi Maalim kugombea Urais visiwani humo kupitia CHADEMA.

''CHADEMA na CUF ni kitu kimoja, kwa hiyo CUF ikitetereka  sisi tutaimarika zaidi na kushika nguvu Zanzibar na sisi tutawakaribisha wagombea wote Zanzibar wachukue fomu na kugombea kupitia CHADEMA na hiyo ndio mipango yetu kama Baraza la Wazee'', amesema.

Aidha amesisitiza kuwa sababu kuu ya msingi ya CHADEMA na CUF kuungana ilikuwa ni kukubalika kwa CUF kwa zaidi ya asilimia 80 katika visiwa vya Zanzibar lakini kwasasa CCM wakifanikiwa kuipangua CUF Zanzibar CHADEMA haitashindwa kuchukua hatamu huko.

Kwa upande mwingine Mwenyekiti huyo amesema wao kama Baraza la Wazee wataendelea kuhakikisha CHADEMA inaendelea kuimarika nchini kote hususani Zanzibar kwasababu wameona CUF inaweza kuvunjika kutokana na hali ilivyo sasa.

Kamati Ya Maadili Ya Taifa Yaitaka Chadema Kutekeleza Maamuzi Yaliyotolewa Na Kamati Ya Maadili Jimbo La Ukonga.

$
0
0
Kamati ya Maadili ya Uchaguzi Ngazi ya Taifa, imekitaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kiendelee kutekeleza maamuzi ya Kamati ya Maadili ngazi ya Jimbo la Ukonga yaliyokitaka chama hicho kusahihisha makosa yaliyotendeka na kuomba msamaha hadharani kwa kosa la kimaadili walilotenda.

Uamuzi huo umetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Jaji Mst. Mary Longway baada ya kikao cha kamati hiyo kupitia na kujadili rufaa dhidi ya uamuzi wa Kamati ya Maadili Jimbo la Uchaguzi Ukonga, iliyowasilisha na Chadema Septemba 5, 2018 ikiitaka kamati hiyo itengue uamuzi wa Kamati ya Maadili ya Jimbo.

Alisema kwa mujibu wa vielelezo vilivyoambatishwa katika Rufaa hiyo, Kamati ya rufaa imefikia maamuzi ya kuwa rufaa hiyo imewasilishwa nje ya muda wa saa 48 kinyume na maelekezo ya  kipengele cha 5.7 (b) cha Maadili tajwa.

“Rufaa iliyowasilishwa yenye Kumb. Na. CDM/ILALA/MAADILI/2018/28 ya tarehe 5 Septemba, 2018 iliyopokelewa Tume tarehe 7 Septemba..Imewasilishwa nje ya muda wa saa 48 kinyume na maelekezo ya  kipengele cha 5.7 (b) cha Maadili tajwa. Hivyo, Kamati inaelekeza kuwa mrufani aendelee kutekeleza maamuzi ya Kamati ya Maadili ngazi ya Jimbo.”, alisema Jaji Mst. Longway.

Kwa mujibu wa uamuzi wa Kamati ya Maadili ngazi ya Jimbo la Ukonga, Chadema kimeonywa kuhakikisha kuwa kinafuata Kanuni na Taratibu za Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015 na kutekeleza maamuzi hayo ndani ya saa 48 tangu kutolewa na adhabu hiyo.

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ukonga Jumanne Shauri mnamo Agosti 27, 2018 alipokea malalamiko na kupitia utetezi wa Chadema na kujiridhisha kuwa Chadema kilitumia kiongozi wa dini kumpigia kampeni mgombea wa chama hicho kinyume na kifungu cha 2.2 (k) cha Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015.

Msimamizi huyo wa Uchaguzi aliongeza kuwa “Dr. Makongora Mahanga akiwa kiongozi wa Chadema, siku ya kampeni tarehe 25/8/2018 alitumia lugha ya matusi, kashfa, kejeli na udhalilishaji dhidi ya mgombea wa CCM, ikiwa pia ni kinyume na kifungu cha 2.2 (k) cha Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015” aliongeza taarifa ya Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Ukonga ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Jimbo hilo”

Mbali na uamuzi juu ya rufaa hiyo, Kamati hiyo pia imepitia barua ya tarehe 5 Septemba, 2018 iliyowasilishwa Tume tarehe 7 Septemba, 2018 kupinga maelekezo ya Kamati ya Maadili Jimbo la Ukonga yaliyokiagiza Chadema kuwasilisha ndani ya Saa 48 kuanzia tarehe 4 Septemba, 2018 vielelezo vilivyothibitishwa na Mamlaka ya Mawasiliano na wataalamu wa lugha ya Kikurya ili kutoa maamuzi ya shauri husika.

Akizungumzia barua hiyo, Jaji Mst. Longway alisema baada ya kupitia vielelezo na kujadili barua husika, imeamuliwa kuwa rufaa hiyo imekosa sifa kwa kuwa hakuna maamuzi yaliyofanywa na Kamati ya Maadili Jimbo la Ukonga.

Kutokana na jambo hilo, Kamati ya Maadili ya Uchaguzi ya Taifa imekielekeza Chadema kuwasilisha vielelezo Kamati ya Maadili ya Jimbo la Ukonga kwa uamuzi kama ilivyoelekezwa na Kamati husika.

Mwisho

Makamu wa Rais Alitaka Jeshi la Polisi Kumkamata Anayetumia Jina Lake Kuwatapeli Wananchi

$
0
0
Makamu wa Rais, Samia Hassan Suluhu ameagiza kukamatwa mara moja baadhi ya watu wanaotumia jina lake na kuwadanganya wananchi kwa kuwachangisha fedha ili wapate Sh50 milioni zilizoahidiwa katika kampeni za uchaguzi Mkuu 2015.

Kauli hiyo imekuja siku moja mara baada ya makamu huyo wa Rais kusema fedha hizo zitatumika katika miradi mbalimbali ya maendeleo na sio kupewa wananchi moja kwa moja kama walivyoahidi awali.

Ameyabainisha hayo leo Septemba 11, wakati akizungumza na wananchi, viwanja vya Soweto katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Munzeze wilayani hapa mkoani Kigoma mara baada ya kumaliza kuzindua zoezi la kupanda miti.

"Kuna wanjanja wanapita katika vijijini wakitumia jina langu na kuwadanganya wananchi huku wakiwachangisha fedha  kuwaambia watakaowahi kutoa watakuwa wakwanza kupata Sh. 50 Milioni zilizotengwa, huu ni uongo na hao ni matapeli wakamatwe mara moja,"amesema Mama Samia.

Amesema kuna baadhi ya watu wamekuwa wakipita vijijini na kuwachangisha fedha ili wapate Sh50milioni na kuwaambia wametumwa na makamu wa Rais jambo ambalo si kweli lazima watu hao wachukuliwe hatua mara moja.

Amesema fedha iliyopo serikali kwa sasa yote ni ya kufanya maendeleo kwa wananchi na kuwaasa wananchi waepuke matapeli.

“Mtu yeyote anayekuja kwenu na kukusanya fedha kwa ajili hiyo mkamateni na muitieni polisi mara moja hii pesa bado kutoka, kwasasa tunashugulikia mambo mengine," amesema Makamu wa Rais.

Awali akizungumza katika mkutano huo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amewataka wazazi kushirikiana na serikali kwa kutokomeza utoro mashuleni kwa kuwahimiza watoto wao kwenda shule.

Amesema kwa sasa serikali inatumia kiasi kikubwa cha fedha katika kuwekeza kwenye sekta ya elimu ambapo kila mwezi inatoa zaidi ya Sh20 bilioni.

Akizungumza mara baada ya uzinduzi wa zoezi la upandaji miti, Meneja wa Wakala wa Huduma za Misitu wilaya ya Buhigwe(TFS), William Samweli amesema changamoto iliyopo wilayani hapo ni ukosefu wa ardhi ya kutosha kupanda miti.

Benki Zinazotoa Mikopo Ya Kilimo Tanzania Bara Na Zanzibar Zatakiwa Kufuata Vigezo Vya Ukopeshaji

$
0
0
Na. WFM
Serikali imezitaka Benki zote zinazotoa mikopo ya kilimo Tanzania Bara na Zanzibar kuhakikisha zinatoa mikopo kwa kuzingatia vigezo vya ukopeshaji vikiwemo kuangalia historia ya mkopaji ili kuondoa mikopo Chechefu (NPL).

Hayo yameelezwa Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Bububu Mhe. Mwantakaje Haji Juma, aliyetaka kujua utaratibu unaotumika kutoa mikopo kwa wakulima wa Zanzibar kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB).

Dkt. Kijaji alieleza kuwa kabla ya kutoa mkopo ni lazima Benki ijiridhishe na aina ya mradi wa mkopaji ikiwa utaleta faida itakayomuwezesha mkopaji kurejesha mkopo huo kwa wakati ili kuzuia ukuaji wa Mikopo Chechefu.

Akijibu swali la msingi la Mbunge huyo aliyetaka kujua ni wananchi wangapi wanaonufaika na mikopo ya Kilimo kwa upande wa Zanzibar, Dkt. Kijaji alisema kuwa jumla ya wananchi 3,000 wamenufaika na mikopo ya Benki ya TADB hadi kufikia Julai 31, 2018.

“Kati ya wanufaika hao 3000, idadi ya wanaume walionufaika ni 1800, wanawake 900 na vijana wa kike na kiume ni 300”, alieleza Dkt. Kijaji.

Alisema kuwa jumla ya mikopo ya shillingi bilioni 6.50, imetolewa kwa wananchi hao wa Zanzibar hadi kufikia Julai 31, 2018.

Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango.

Mahakama ya uhalifu ya kivita ICC kuwekewa vikwazo na Marekani endapo itaendelea kuwashtaki raia wake

$
0
0
Marekani imetishia vikwazo dhidi ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC ikiwa itaendelea na mikakati yake ya kuwashtaki raia wa Marekani.Mahakama hiyo kwa sasa inatathmini kuwafungulia mashtaka wanajeshi wa Marekani kwa madai ya kuwatesa wafungwa nchini Afghanistan.

Mshauri wa masuala ya usalama ya kitaifa John Bolton alisema mahakama hiyo sio halali na kuapa kuwa Marekani itafanya kila iwezalo kuwalinda raia wake.

Baada ya tamko hilo kutoka marekani ikumbukwe kuwa wakati fulani mwaka uliopita nchi tatu za Afrika – Burundi, Gambia na Afrika Kusini ziliashiria nia yao ya kujitoa kutoka mahakama hiyo ya kimatafa ya uhalifu wa kivita ICC. Kulikuwa na hofu kuwa nchi zaidi zingefuata.

Mwezi Oktoba mwaka 2016, Burundi na Afrika Kusini waliandika kwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kuelezea uamuzi wao wa kuondoka kutoka ICC.

Wakati huo, nchi ya Gambia ambayo ni nchi ndogo ambayo sehemu yake kubw iko ndani ya Senegal magharibi mwa Afrika ilitangaza kuwa ingejitoa. Lakini hatua hiyo ilifutwa mara wakati serikali mpya iliingia madarakani.

Tangu wakati huo hatua hatua za nchi za Afrika kujitoa kutoka ICC huzijafua dafu, hata baada ta Muunganoa wa Afrika kutoa kauli ya pamoja na kujitoa kutoka mahaka hiyo.

“Kundi la watu wasio na maaana,” rais wa Uganda Yoweri Museveni wakati mmoja aliielezea ICC, huku rais wa Rwanda Paul Kagame akisema kuwa mahakama haikuwa kwa minajili ya haki bali siasa zinazotajwa kuwa haki ya kimataifa.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ambaye wakati mmoja alikabiliwa na kesi katika mahakama hiyo alisrma makahama hiyo ni chombo ya siasa za dunia lakina sio kuhusu haki ilizotakiwa kuteleleza.

Kurodhika na mahakama hiyo kumetokana na hisia kuwa ICC ilikuwa inawalenga waafrika na haieshimu siasa na uhuru wa nchi za Afrika. Keshi kumi kati ya tisa zilizo, kwenye mahakama hiyo zinahusu nchi za Afrika.

Mahakama hiyoi inachunguza na kuwaleta hukumuni wale wanaohusika kwenye uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu, ikiingilia kati wakati mahakama za nchi haziwezi kuwahukumu.

ICC ilibuniwa chini ya mkataba wa Roma wa mwaka 2002 na imeungwa mkono na nchi 123 ikiwemo Uingereza.

Baadhi ya nchi za Afrika zimataja kuondoka kutoka mahakam hiyo zikisema kuwa inazionea nchi za Afrika.

Chanzo BBC.

Petit afunguka kuhusu kuchepuka na kumpachika Mnyarwanda mimba

$
0
0
Baada ya mwanadada maarufu mtandaoni, Mange Kimambi kuvujisha sauti zinazodaiwa kuwa za Petit Man akisikika akizungumza na mwanadada anayedaiwa kuwa mpenzi wake Mnyarwanda, mume huyo wa Esma mdogo wake Diamond, amefunguka.

Akiongea na U Heard, Petit alidai yeye anashinda na watoto kwahiyo kama kuna mwanamke ambaye anadai anamtoto wake basi ajitokeze.

“Azae tu sisi hatukataagi watoto,” alisema Petit baada ya kuambiwa kuna mwanamke Mnyarwanda ana mimba yake.

Aliongeza,”Watoto kwangu ni baraka kweli kweli, kwa sasa nina mtoto mmoja tu, nahitaji waongezeke familia iwe kubwa zaidi, kwahiyo yeye kama ana kibendi changu azae huu sio muda wa maneno,”

Mapema leo asubuhi Mange alikuwa kwenye malumbano na mke wa Petit, Esma na ndipo mwanadada huyo ambaye anaishi Marekani akaamua kuvujisha sauti hizo ambazo anasikika Petit akimbembeleza Mnyarwanda huyo.

Kamishna Wa TRA Apata Ajali Dodoma

$
0
0
Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Charles Kichere amepata ajali leo Jumanne, Septemba 11, 2018 baada ya gari lake aina ya Toyota Land Cruiser V8 namba STL 5199 kugongana na gari dogo la mtu binafsi lenye namba za usajili T 416 BTH, eneo la Nanenane, jijini Dodoma.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Polisi  Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto, amesema, ajali hiyo imetokea na kwamba hakuna madhara kwa binadamu bali ni uharibifu wa magari ndio umetokea.

Gari la Mamlaka ya Mapato lilikuwa likitokea Morogoro kuelekea Dodoma ndipo lilipogongana na gari lililokuwa likielekea chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) ambalo lilichomoza wakati gari la Kamishna likipita gari jingine.

Amesema gari la Kamishna lilikuwa likiendeshwa na Peter (35) kabila ni Msukuma ambaye ni mkazi wa Kurasini Dar es salaam huku lile jingine lilikuwa linaendeshwa na Paul (39) kabila ni Masai ambaye ni mhadhili wa Chuo Kikuu cha UDOM.

Ameweka wazi kuwa wamejiridhisha mpaka sasa kiafya wahusika wote wako salama.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya Septemba 12

Taarifa Kwa Umma Kuhusu Takwimu Za Deni La Serikali Kwa Benki Kuu Ya Tanzania

$
0
0
Benki kuu ya Tanzania (BoT) inakanusha taarifa potofu zinazozosambazwa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii zikidai kuwa Benki Kuu imechapisha noti zenye thamani ya shilingi trilioni 1.5 kwa ajili ya matumizi ya serikali.

Benki Kuu inauarifu Umma kuwa, taarifa hiyo sio sahihi na inalenga kuathiri imani ya Wananchi na wadau wa kimataifa kuhusu uthabiti wa fedha ya Tanzania. 

Aidha, Benki Kuu inawaasa Wananchi kuwa utoaji wa taarifa potofu kuhusu sekta ya fedha unaweza kuleta athari kubwa kwa mwenendo wa uchumi. 

Hivyo ni vyema Wananchi wajue yafuatayo kuhusu utoaji wa fedha kwa matumizi ya Serikali:

1.Mapato ya serikali hayawiani moja kwa moja na matumizi yake mwezi-hadi-mwezi. Kuna wakati mapato yanakuwa makubwa mfano miezi ya mwisho wa robo mwaka na wakati mwingine yanakuwa madogo. Kwa sababu ya kupishana kwa mapato na matumizi ya serikali, sheria imeruhusu serikali kuchukua mkopo wa muda mfupi kutoka Benki Kuu ili kuziba pengo pale linapotokea na kurejesha baadaye. Utaratibu huu unatumika duniani pote na hapa Tanzania sheria inairuhusu Serikali kukopa kutoka Benki Kuu kwa vipindi vifupi hadi ukomo wa asilimia 12.5 ya mapato ya ndani ya serikali ya mwaka uliotangulia.

2.Ili kupata picha halisi ya utekelezaji wa bajeti ya serikali na hali ya deni la Taifa, ni vyema kuangalia mwenendo mzima katika kipindi cha miezi kumi na mbili ya mwaka wa fedha husika, badala ya kuangalia mwezi mmoja mmoja, ambapo kuna mabadiliko ya kimsimu. Mtazamo wa mwaka mzima hutoa uhalisia wa mapato na matumizi, na ongezeko la deni lililohitajika kuwezesha utekelezaji wa bajeti ya serikali katika kipindi hicho. Taarifa ya kila mwezi ya uchumi ya Benki Kuu toleo la mwezi Julai inaonesha kwamba mkopo wa muda mfupi (overdraft) wa Benki Kuu kwa serikali uliongezeka kutoka shilingi bilioni 610.0 mwezi Mei 2018 hadi shilingi bilioni 1,937.4 mwezi Juni 2018, sawa na ongezeko la shilingi bilioni 1,327.4. Ongezeko hili halipaswi kuangaliwa kama tukio la mwezi Juni 2018 pekee kwani taarifa hiyohiyo inaonesha kuwa kati ya mwezi Juni 2017 na mwezi Mei 2018 overdraft ya Benki Kuu ya Tanzania kwa serikali ilipungua kwa shilingi bilioni 936.6, kutoka shilingi bilioni 1,546.6 hadi shilingi bilioni 610.0.  Kupungua huku kulichangiwa na mapato ya kawaida ya serikali pamoja na mikopo kutoka nje ya nchi.

3.Aidha, Benki Kuu haijachapisha noti mpya katika kipindi hiki, hata hivyo noti mpya, hazichapishwi kiholela ili kutoa pesa kwa serikali, bali huchapishwa kulingana na taratibu za kisheria. Kwa kawaida utengenezaji wa noti na sarafu huanza baada ya kukamilika kwa mchakato wa usanifu wa michoro, aina ya karatasi itakayotumika, alama za utambulisho wa nchi pamoja na alama za usalama. Na mara baada ya kukamilika kwa mchakato huo, Benki Kuu huandaa kiasi gani kitakachoweza kutosheleza mahitaji ya nchi kwa kipindi maalum kwa kuzingatia ukuaji wa pato la Taifa, Mfumuko wa bei na pia kufidia fedha zilizochakaa ambazo hazipaswi kurudi katika mzunguko na kiasi kilichobaki (buffer stock) ili kutosheleza kipindi chote cha mchakato wa uchapishaji.

Benki kuu inawaasa Wananchi kutotoa taarifa zisizo za kweli zenye lengo la kuupotosha Umma na kusababisha hofu na kupoteza imani juu ya uthabiti wa fedha ya Tanzania na badala yake wawe wanaomba kupewa taarifa kutoka Taasisi husika.

BENKI KUU YA TANZANIA
Idara ya Uhusiano wa Umma na Itifaki
11 Septemba, 2018

Rais Dkt. John Magufuli Atimiza Ahadi Aliyoitoa Jwtz Kwa Ajili Ya Ufugaji Wa Samaki Mkoani Mara

$
0
0
Katibu wa Rais Ndg. Ngusa Samike akikabidhi fedha kiasi cha shilingi Milioni 40 kwa Mkuu wa kikosi cha 27KJ Luteni Kanali Js Mshashi kilichopo Makoko mkoani Mara. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliahidi kutoa fedha hizo Septemba 6,2018 alipokuwa ziara Mkoani humo kw aajili ya kuongeza Vizimba 10 vya kufugia Samaki.

Makabidhiano hayo yalifanyika Jijini Dodoma mbele ya Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo Septemba 11,2018.

Kikwete, Mkapa na Mwinyi Walivyosherehekea miaka 20 ya Balozi wa Marekani

$
0
0
Balozi mstaafu wa Marekani nchini Tanzania wakati wa utawala wa Serikali ya awamu ya tatu chini ya Benjamin Mkapa, Balozi Charles Stith amesema anajisikia faraja kusherehekea miaka 20 ya ubalozi nchini kutokana na mapenzi mema na nchi ya Tanzania.

Balozi Charles amesema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wa sherehe ya kuadhimisha miaka 20 ya ubalozi ambapo maraisi wastafu mzee Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Dk.Jakaya Kikwete walishiriki kwenye sherehe hiyo.

Mbali ya marais wastaafu, wakati wa sherehe hiyo viongozi wengine wa ngazi mbalimbali pamoja na wageni waalikwa wakiwemo baadhi ya madaktari bingwa kutoka Marekani pia  walishiriki.
 
Balozi Stith alisema akiwa balozi kati ya mwaka 1998 hadi mwaka 2001 amepata ushirikiano mkubwa kwa Rais mstaafu Mkapa huku Rais mstaafu Dk.Kikwete wakati huo akiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Amemshukuru Mkapa na Kikwete kwa ushirikiano ambao walikuwa wakimpatia katika kuhakikisha uhusiano wa nchi hizo unaendelea na kwamba akiwa nchini Tanzania amefanikisha kuingiwa kwa makubaliano mbalimbali yenye tija kwa nchi za Afrika na hasa Tanzania.
 
“Nimefurahi kuja Tanzania kukutana na kusheherekea miaka 20 ya Ubalozi.Nimefurahi kumuona Rais mstaafu Mwinyi,Rais mstaafu Mkapa na Rais mstaafu Kikwete.Tulishirikiana na tunaendelea kushirikiana,” Alisema Balozi Stith.

Waziri Mkuu: Ulaji Usiofaa Unaongeza Magonjwa Yasiyoambukiza

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesemalishe duni pamoja na ulaji usiofaa na mitindo ya maisha vinachangia kwa kiasi kikubwa katika ongezeko la magonjwa yasiyo ya kuambukiza hususan kwa vijana na watu wazima, ambao ndiyo nguvu kazi kwa Taifa.

“Ni jambo lisilopingika kuwa hatua za kukabiliana na magonjwa ya kusendeka (mfano matatizo ya moyo, saratani, kisukari na shinikizo kubwa la damu) zinachangia kwa kiasi kikubwa katika kupunguza kasi ya maendeleo yetu kwani gharama za matibabu yake ni kubwa mno; si kwa kaya zinazoathirika tu bali kwa Taifa zima.”

Waziri Mkuu  ametoa kauli hiyo leo (Jumanne, Septemba 11, 2018),  wakati akifungua mkutano wa tano wa wadau wa masuala ya lishe, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kambarage, Hazina jijini Dodoma. 

Waziri Mkuu amesema lishe iliyozidi inadhihirishwa na ongezeko kubwa la magonjwa yasiyoambukizwa yanayotokana na mabadiliko ya mitindo ya maisha na ulaji usiofaa kama vile uzito uliozidi, viriba tumbo, shinikizo la damu pamoja na kisukari.

Amesema kasi ya ongezeko la magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza inapaswa kudhibitiwa kwa kuzingatia ulaji unaofaa na mtindo bora wa maisha. “Huu ni wakati wa kuangalia kwa pamoja kama jitihada zetu zinaleta matunda tunayotarajia.”

Waziri Mkuu amesema Serikali inatambua kuwa lishe bora ni msingi wa maendeleo ya Taifa letu hivyo, uwepo wao katika mkutano huo unaonesha umuhimu wa kuimarisha ushiriki wa kila sekta, kila mdau ikiwemo sekta binafsi kwa nafasi yake katika kupambana na aina zote za utapiamlo. 

Amesema ushiriki wa kila sekta ni wa muhimu kwa sababu hakuna sekta moja pekee inayoweza kuondoa tatizo la utapiamlo, pia ni vema kwa wadau hao wakajitathmini mmoja mmoja katika sekta zao kuona kama wanaelekea katika muelekeo sawa na mipango ya Serikali.

“Kwa kuzingatia hilo, ofisi yangu imeweka utaratibu maalum wa kuratibu utekelezaji wa kazi za lishe nchini, ambapo kamati ya Kitaifa ya Usimamizi na Ushauri kuhusu masula ya lishe nchini yaani High Level Steering Committee on Nutrition imeundwa ili kusimamia utekelezaji wa azma hiyo.” 

Waziri Mkuu amesema kwamba watu wote wanatambua jitihada kubwa zilizowekwa na Serikali kwa kushirikiana na wadau katika kupambana na matatizo ya lishe nchini, ambapo taarifa za wataalamu zinasema kuwa kwa sasa nchi inakabiliwa na aina mbili za utapiamlo yaani lishe duni na lishe iliyozidi au iliyokithiri. 

Amesema walengwa wakubwa wa lishe duni ni pamoja na watoto chini ya miaka mitano, wanawake walio katika umri wa kuzaa hususani wajawazito na wanaonyonyesha pamoja na vijana balehe (hususan wa kike). “Hii ni kwa sababu mahitaji ya virutubishi kwa ajili ya miili yao ni makubwa, ukilinganisha na ule unaohitajika na makundi mengine.” 

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Gigy Money Afunguka Baada ya Video Kusambaa Wakipapasana Gizani na Msani Lavalava

$
0
0
Msanii wa muziki Bongo, Gigy Money amefunguka kuhusu ukaribu wake na Lava Lava kutokea WCB.

Hii ni baada ya hivi karibuni kuwepo kwa video inayowaonyesha wawili hao wakishikana sehemu ambayo ilkuwa na giza kiasi. Hata hivyo Gigy Money ameeleza kuwa hapo walikuwa club na hakuna chochote kati yao.

"Mshikaji tu kwani kulambana ni nini, ni club pale na inategemea na mlivyozoeana," amesema Gigy Money.

Pia ameongeza kuwa, 'Sina mume wala sina mpango wa kuolewa, am single, i mean i have no boy friend'.

Dr Kanengo: Bingwa Wa Tiba Asili Hutibu Matatizo Yafuatayo

$
0
0
NKURURU:-ni dawa inayotibu miguu kuwaka moto, kiuno tumbo kupooza kupoteza fahamu 

MALABALA; hutibu kisukari , uti wa mgogo, Change, pumu, busha, kaswende, kifua kikuu, muwasho sehemu ya siri 

NKURUNGU,: Ni dawa kutibu  N, B, G, POWER :-ni dawa ya kuongeza nguvu za kiume ni vidonge 20 

MPERAMPERA:- ni dawa ya kurudisha Mke, mme, mpenzi,mchumba aliyekuacha /kuteseka, ni kwa mda wa siku 2 tu kusafisha , pia kuna dawa za kupunguza vitambi(nyama uzembe), maziwa makubwa,michirizi, mikovu makubwa, chunusi sugu. 

NR SIX POWER:-inatibu upungufu wa nguvu za kiume kwa wasio weza kumudu tendo la ndoa itakufanya uwe na hamu ya kurudia tendo la ndoa zaidi ya Mara 4 bila hamu Kuisha, inaboresha maumbile madogo na inaimarisha misuri iliyo legea na kusinyaa una pona kabisa, ndani ya siku 4 tu 

GASELA:-ni dawa ya maajabu (9) yaliyoshindikana. (1)-Kisukari, vidonda vya tumbo, tezi dume,walioshindikanika kupata watoto(ugumba),busha bila oparesheni, (2)zindiko Kali Katika biashara yako (chuma ulete) ndo kiboko yao kumkamata mwizi aliye kuibia vitu vyako pikipiki, gari, n, k( 2)zindiko la nyumba, mashamba, viwanja,.(4)kukutolea sumu uliyo ikanyaga (Mtego) (5)ujiamini kutumia dawa ya maajabu Saba (6)kutoa mikafara mfano ugomvi ndani ya nyumba kufukuzwa kazini bila sababu (7)kutabiri nyota na kung'arisha (8)kurudisha Mali iliyo potea mazingira ya kutatanisha, kushinda kesi uliyo sumbuka nayo mda mrefu. (9)kufukuza majini wachafu ndani ya mji,.

Haya yote yanawezekana kwa DR KANENGO popote ulipo . Muone  DR KANENGO,anatibu nguvu za kiume anarefusha na kunenepesha uume kwa saizi uipendayo kwa muda mfupi sana, pamoja na kuwa na hamu ya kurudia tendo la ndoa mara 4 bila hamu kuisha Na utachelewa kufika kileleni kwa muda wa dakika 40 bila kuchoka .

Angalizo usitume meseji wala kubipu..
 
You can get it in all East African countries,,our service is fast and easy... contact Whatsapp 0784,47,59,46.Dar es salaam Tanzania. ,..Dr. KANENGO 0744,92,29,82...You are welcome. Yuko pia Khahama Mjini, Bunda kwa sasa

Makanga 3 Power; Dawa Bora Nguvu Za Kiume

$
0
0
Kutibu nguvu za kiume dakika(10) na kupona muda wa siku tatu tuu. Kuimarisha misuli ya uume uliolegea, pia ipo Dawa ya kurefusha uume mfupi inchi NNE hadi saba na kunenepesha uume mfupi sentimita NNE.

Tiba ya kudumu kutibu maumivu ya mgongo,kiuno, tumbo kuunguruma na kujaa gesi, kupata choo vizuri, na kutibu uzazi, kutibu busha bila operesheni, kisukari, presha ,miguu kuuma, uzazi, fangas sugu, vidonda vya tumbo.

Ni docta bingwa wa kutibu magonjwa sugu, kutoa ndagu za utajiri kwa kutumia Pete, kazi ,cheni, mikufu maalumu ya bahati, una kesi umedhulumiwa Mali au pesa? Zitarudi muda wa Masaa matatu tuu.

Onana na Dr shilindes shida zako zote zitakwisha, anatoa Dawa za utajiri kwa wafanyakazi, wakulima, na wafugaji, wafanyabiashara na wachimba madini kwa kutumia pete, kazi kwa yeyote anaetaka kuwa na pesa nyingi.

Pia anaboresha akili kwa wanafunzi darasani, masomo na kufaulu mitihani pia kushinda bahati nasibu yeyote.

Pia tunatoa Dawa kumrudisha Mume, mke, mpenzi, hawara, kwa muda wa SAA moja tuu, na kuomba msamaha kwa kukupigia magoti na yeyote yule, unaemtaka kimapenzi au kuoana, utampata na kumfunga asitoke nje ya ndoa daima na kutekeleza shida zako zote. Kupunguza unene, kupunguza matiti makubwa, tumbo na nyama uzembe muda wa siku sita unapata saizi uipendayo.

Kutoa makovu mwilini, chunusi, upele na mabaka, pia tunayo Dawa ya kuongeza hipsi, makalio, mguu wa bia na kupata shepu safi kwa muda wa siku saba tuu.

Wa mikoani mtapata huduma popote mlipo.
Tupo dar es salam mbagala rangi tatu.

Mawasiliano simu namba: 0784 460 348. Au 0659 103 360.

Dawa Za Nguvu Za Kiume Na Kukosa Hamu Ya Tendo La Ndoa

$
0
0
Asilimia 45-80 ya wanaume wapo tofauti na wengine kwa kutowatimizia vyema wake au wapenz wao na kuwasababishia kutoka nje ya mahusiano yao. 

NINI CHANZO CHA HAYO? Kupiga punyeto,Ngiri, Vidonda vya tumbo, Korodani moja kuvimba, Msongo wa mawazo, Presha, Magonjwa ya zinaa, Kufanyiwa tohara ukiwa na umri mkubwa, Kisukari. 

DR. LUTAJA Sasa anakuletea tiba sahihi ya tatizo la Nguvu za kiume. 

NTOMBO :Hii hutibu na kuponya kabisa tatizo la Nguvu za kiume, utakuwa na uwezo wa kufanya tendo la ndoa zaidi ya mara tatu bila kuchoka na itakufanya uchelewe kafika kileleni kwa mda wa dk 20-45. Dawa hii imechanganywa na miti 18,Hata wazee wenye umri mkubwa wa zaidi ya miaka 85 wanapona kabisa okoa mahusiano yako, ndoa yako sasa. 

SUNGURURU MIX:Ndio tiba sahihi kwa wale wenye maumbile madogo hurefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo nchi 3-8 na unene cm 2-5,dawa hii ipo katika mfumo wakupaka nakunywa na haina madhara yoyote kwa mtumiaji :Hii ni tiba tofauti kabisa nazile ambazo umekwisha wahi kutumia. 

Pia tunadawa za Kupandisha nyota , Uzazi, Pumu, Malaria sugu, miguu kuwaka moto, Kaswende, Kisonono pamoja na mvuto wa mpenzi.

 DR. LUTAJA ANAPATIKANA DAR-ES-SAALAM Simu 0713-821823 kwa wale wa mikoani huduma hii utaipata popote ulipo.

Muhimbili Yatumia Mil 600 Kwa Mwezi Kuhudumia Wasiojiweza

$
0
0
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), inatumia kati ya Sh. milioni 450 hadi Sh. milioni 600 kila mwezi kugharamia wagonjwa wanaoshindwa kulipia matibabu yao.

Hayo yalielezwa Dar es Salaam jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru alipokuwa akimkabidhi msaada wa baiskeli ya matairi matatu, Said Mtonga ambaye amekatwa miguu yote miwili kutokana na maradhi yanayomsumbua.

“Jukumu letu ni kutibu lakini inapobidi huwa tunaenda zaidi ya hapo na kutoa msaada ‘rehabilitation’, kwa mgonjwa kama huyu, ili anapotoka hapa aweze kwenda kuendelea na majukumu yake, ajenge uchumi wa nchi na wake pia.

“Hivyo, hospitali imegharamia matibabu yake yote kwa kuwa hakuwa na uwezo wa kulipia na kwa mwezi huwa tunatumia kiasi cha kati ya Sh. milioni 450 hadi Sh. milioni 600,” alisema.

Ofisa Ustawi wa Jamii Muhimbili, Wodi ya Kibasila, John Mwakyusa alisema matibabu ya Said yamegharimu Sh. 935,000 tangu alipofika hospitalini hapo Mei, mwaka huu. .

“Alikukuja miguu yake ikiwa imevimba na ina vidonda, alichunguzwa na kuonekana haikuwa saratani, madaktari wakamfanyia upasuaji kukata mguu wake mmoja lakini baadae mguu uliobaki nao ulionyesha tatizo, nao ukakatwa.

“Ndugu zake hawakuwahi kujitokeza, tukawatafuta lakini tulipowapata walitueleza hawakuwa na uwezo wa kumsaidia, hata marafiki zake pia hawakuja,” alisema.

Alisema waliendelea kumtibia hadi alipopona kabisa wakaona ni vema kumtafutia baiskeli ili aweze kutembelea.

“Tunamshuruku mkurugenzi alitupatia Sh. 500,000 tukaenda SIDO kutafuta Sh. 80,000 tukampa mtaji,” alisema.

Mkuu wa Idara ya Ustawi wa Jamii Muhimbili, Emmanuel Mwasota alisema ugonjwa uliokuwa ukimsumbua Said kitaalam unaitwa Septic Wound with Gangrene.

Uteuzi Uliofanywa na Rais Magufuli Muda Mfupi Kabla ya Kuwaapisha

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanazania John Pombe Magufuli amefanya uteuzi mwingine na kumteua Balozi Dkt.  Aziz Ponary Mlima kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uganda.

Kufuatia uteuzi huo Balozi Mlima anatarajia kuapishwa leo Septemba 12, 2018 Ikulu Chamwino, Jijini Dodoma.

Pia Septemba 3, 2018 Rais Magufuli alifanya uteuzi wa Dkt. John Antony Kiang’u Jingu kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ambapo kabla ya uteuzi huo Kingu alikuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambaye naye atakula kiapo leo.

Aidha, naye Kamishna wa Polisi Diwani Athumani aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU anatarajia kuapishwa leo Chamwino Jijini Dodoma.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images