Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Waziri Mkuu Majaliwa Arejea Nchini Akitoka Nchini China

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam akitoka nchini China, Septemba 9, 2018 alikomwakilisha Rais John Magufuli kwenye Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) uliofanyika Beijing hivi karibuni. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Lukuvi Na Waziri Hasunga Wazidi Kusisitiza Wananchi Kuheshimu Mipaka Ya Msitu Wa Kazimzumbwi ....Ni Baada ya Kushindwa Kesi Mahakamani

$
0
0
Serikali imewataka wananchi wanaoishi kuzunguka Hifadhi ya Msitu wa Kazimzumbwi waliokuwa wamefungua kesi na baadaye kushindwa waendelee kuheshimu mipaka ya Msitu huo huku  Chama cha Mapinduzi kikiangangalia namna bora ya kuwasaidia.

Hatua hiyo inakuja kufuatia Wananchi hao waliokuwa na mgogoro wa Ardhi ndani ya Msitu huo kufungua kesi mwaka 2017,  kwenye Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi na maamuzi ya shauri la madai hayo yaliipa serikali ushindi, baada ya wananchi hao  kushindwa kuonyesha ushahidi wa umiliki wa ardhi ikiwa ni ushahidi wa manunuzi na urithi wa ardhi hiyo katika  Msitu wa Hifadhi ya Kazimzumbwi,

Akizungumza kwenye mkutano na wananchi hao katika eneo la Zingiziwa wilayani Ilala mkoani Dar es Salaam, Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Wiliam Lukuvi amewaambia wananchi hao kuwa  hawana  haki kwenye ardhi hiyo kwa mujibu wa hukumu iliyotoka,

Aliongeza kuwa mipaka ya msitu huo ipo sahihi na si  vinginevyo hali iliyopelekea wananchi hao kushindwa  kukata rufaa.

 Hata hivyo  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi  amejipa siku 30 kuangalia namna ya kuwasaidia wakazi hao walioshindwa kesi.

 Ameongeza kuwa  tayari ameshaunda kamati iliyopewa muda wa miezi miwili na tayari imeshamaliza mwezi mmoja na hivyo itatoa majibu ndani ya siku 30 lengo likiwa ni kuwasaidia wananchi hao ambao kisheria walishindwa kesi.

"Mgogoro huu ulishafika mahakamani na uamuzi ukatolewa kuwa mmevamia hilo lipo wazi na sisi hatupingani na uamuzi wa mahakama.

"Ila kwa kuwa nyie ni wananchi wetu, CCM imeamua kununua kesi, sio kwa maana ya kupinga mahakama Bali ni kwa kuangalia tunawasaidia vipi," alisema Mhe. Lukuvi

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Japhet Hasunga amesema wizara yake haina tatizo na wakazi hao zaidi ya kuhakikisha msitu huo uko salama.

Amesema katika kipindi ambacho msitu huo ulivamiwa athari kubwa zilijitokeza.

"Msitu huu tunaweza kusema ndio mapafu ya Dar, sasa ukivamiwa kwa kuwekwa Makazi au shughuli za kibinadamu mambo yanakuwa mabaya,”

Tunategemea tupate hewa nzuri kutoka huku lakini wao walivamia na kutengeneza hewa chafu. Sisi tunachosimamia ni kuhakikisha msitu unatunzwa na kubaki kuwa msitu,"amesema.

Baadhi ya wawakilishi wa kundi hilo la wananchi  waliokuwa wamevamia msitu huo  wameeleza kuwa wanachotaka ni kuonyeshwa mipaka ya kitaalam ya unapoanzia msitu huo.

"Hatupingani na mahakama wala wizara sisi tunataka wataalam wa wizara ya ardhi waje wafanye vipimo na kutuonyesha kitaalam ilipo mipaka," amesema Jackson Rwehumbiza.

Akizungumza kuhusu msitu huo Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo alisema, Mwaka 1954 serikali ilianzisha Msitu wa Hifadhi wa Kazimzumbwi wenye ukubwa wa hekta 4,860, kwa Tangazo la Serikali Na. 306 la mwaka 1954 na ramani Jb 196 ya mwaka 1954 kwa kutambua umuhimu wake.

Profesa Silayo anasema licha ya umuhimu wake Msitu wa Hifadhi wa Kazimzumbwi umekuwa ukivamiwa mara kwa mara na wananchi wanaoishi kuzunguka msitu huo na serikali ilifanya zoezi la kuwaondoa mwaka 1998,2003,3007,2011 na 2014.

Msitu huu upo katika Wilaya ya Kisarawe na upande wa mashariki ndiyo mpaka kati ya wilaya ya Kisarawe mkoa wa Pwani na wilaya ya Ilala mkoa wa Dar es Salaam.
                                MWISHO

Makanga 3 Power; Dawa Bora Nguvu Za Kiume

$
0
0
Kutibu nguvu za kiume dakika(10) na kupona muda wa siku tatu tuu. Kuimarisha misuli ya uume uliolegea, pia ipo Dawa ya kurefusha uume mfupi inchi NNE hadi saba na kunenepesha uume mfupi sentimita NNE.

Tiba ya kudumu kutibu maumivu ya mgongo,kiuno, tumbo kuunguruma na kujaa gesi, kupata choo vizuri, na kutibu uzazi, kutibu busha bila operesheni, kisukari, presha ,miguu kuuma, uzazi, fangas sugu, vidonda vya tumbo.

Ni docta bingwa wa kutibu magonjwa sugu, kutoa ndagu za utajiri kwa kutumia Pete, kazi ,cheni, mikufu maalumu ya bahati, una kesi umedhulumiwa Mali au pesa? Zitarudi muda wa Masaa matatu tuu.

Onana na Dr shilindes shida zako zote zitakwisha, anatoa Dawa za utajiri kwa wafanyakazi, wakulima, na wafugaji, wafanyabiashara na wachimba madini kwa kutumia pete, kazi kwa yeyote anaetaka kuwa na pesa nyingi.

Pia anaboresha akili kwa wanafunzi darasani, masomo na kufaulu mitihani pia kushinda bahati nasibu yeyote.

Pia tunatoa Dawa kumrudisha Mume, mke, mpenzi, hawara, kwa muda wa SAA moja tuu, na kuomba msamaha kwa kukupigia magoti na yeyote yule, unaemtaka kimapenzi au kuoana, utampata na kumfunga asitoke nje ya ndoa daima na kutekeleza shida zako zote. Kupunguza unene, kupunguza matiti makubwa, tumbo na nyama uzembe muda wa siku sita unapata saizi uipendayo.

Kutoa makovu mwilini, chunusi, upele na mabaka, pia tunayo Dawa ya kuongeza hipsi, makalio, mguu wa bia na kupata shepu safi kwa muda wa siku saba tuu.

Wa mikoani mtapata huduma popote mlipo.
Tupo dar es salam mbagala rangi tatu.

Mawasiliano simu namba: 0784 460 348. Au 0659 103 360.

Makamu wa Rais Awataka Viongozi wa Dini Wahubiri Amani, Wajiepushe na Migogoro na Wasichanganye Dini na Siasa

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali inatambua mchango wa madhehebu ya dini katika kuwaletea wananchi maendeleo endelevu.

Makamu wa Rais ameyasema haya jana wakati wa sherehe za kusimikwa wakfu wa Askofu Mkuu Msaidizi pamoja na Maaskofu wanne wa majimbo wa Kanisa la Pentekoste Motomoto, Mwanga mkoani Kigoma.

“Serikali imeweka mazingira rafiki kwa madhehebu ya dini nchini kuweza kutoa huduma za kijamii hususan elimu na afya” alisema Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais amesisitiza umuhimu wa kanisa kujiepusha na migogoro ya kiutawala ndani ya Kanisa na pia liepuke kuchanganya dini na siasa

“Kazi kubwa ya Kanisa iwe kuhubiri Amani kwa waumini wake na wananchi kwa jumla” alisema Makamu wa Rais huku akinukuu neno la Mungu katika Waebrania 12:14, ambalo linasema “tafuteni kwa bidii kuwa na Amani na watu wote”.

Aidha, Eneo jingine ambalo Serikali inalitegemea Kanisa ni katika kujenga maadaili mema ya jamii, hivyo Makamu wa Rais alilitaka Kanisa kusaidiana na Serikali katika kupiga vita tamaduni mbaya za nje ili kujenga Taifa lenye maadili ya Kitanzania, pia Serikali inalitegemea Kanisa katika kupiga vita rushwa na ufisadi ambavyo ni adui wa maendeleo ya nchi.

Kwa upande wake Askofu Mkuu wa Kanisa hilo Baba Askofu Ezra Enock Mtamya ameupongeza Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano kwa juhudi zake za kuijenga Tanzania yenye maendeleo ambapo pia alisema kama Kanisa wamekuwa mstari wa mbele katika maendeleo ya jamii na utunzaji wa mazingira ambapo wameiomba Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais kuwapa wataalam wa mazingira pamoja na ufugaji nyuki.

Akizungumza kabla ya kumkaribisha Makamu wa Rais, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma amewata Wanaume wawe mstari wa mbele katika kupima afya zao na kuzingatia lishe bora kwa watoto.

Maaskofu waliosimikwa jana ni Askofu Mkuu Msaidizi Bwami J. Mathias, Askofu Shemu A. Mwenda (Jimbo la Kati), Askofu Simon S. Bikatago  wa Jimbo la Magharibi, Askofu Jackson Maneno  wa Jimbo la Tanganyika na Askofu Eliasaph  Mathayo wa Jimbo la Mashariki.

Waziri Wa Kilimo Dkt Charles Tizeba Arejea Nchini Baada Ya Kumalizika Kongamano La Afrika La Mapinduzi Ya Kijani (AGRF 2018) Nchini Rwanda

$
0
0
Na Mathias Canal (WK), Dodoma
Kumalizika kwa Mkutano wa Mapinduzi ya kijani Barani Afrika (AGRF 2018) mjini Kigali nchini Rwanda kumeongeza tija na ufanisi kifikra kwa washiriki ikiwemo Tanzania kwa kuhakikisha kwamba wananchi wanakuwa na mafanikio chanya kiuchumi kulingana na rasilimali zake nyingi za asili ikiwemo ardhi yenye rutuba katika kilimo.

Afrika ina hekta milioni 600 za ardhi isiyozalishwa ambayo ni sawa na asilimia 60 ya jumla ya kimataifa. Waziri wa kilimo Tanzania-Mhe Dkt Charles Tizeba anaamini kwamba mafanikio katika kukuza na kuimarisha uchumi Barani Afrika ni kupitia kilimo hivyo msisitizo mkubwa ni kusimamia kiufasaha mikakati inayowekwa kwenye sekta hiyo kuliko mijadala pekee.

Anasema Afrika inakadiriwa kuwa na idadi kubwa kufikia bilioni mbili mwaka wa 2030 hivyo mapinduzi ya kilimo yanapaswa kuimarisha mahusiano ya serikali na wananchi kwa kuwatunza wakulima kama wateja na kuwapatia ujuzi na huduma bora ili kuongeza uzalishaji wa Mazao yao.

Kurejea kwa waziri wa kilimo Mhe Tizeba jana tarehe 9 Septemba 2018 kunamfanya kuendelea na majukumu nchini mwake akiwa na fikra chanya kupitia tukio la kila mwaka la kongamano la Mapinduzi ya kijani (AGRF) linalowaweka pamoja wakuu wa nchi, wajasiriamali, wataalamu wa sekta na wakulima kwa mazungumzo muhimu juu ya hali ya kilimo barani Afrika.

Waziri huyo wa kilimo nchini Tanzania alipochangia mjadala kuhusu upotevu wa chakula baada ya uvunaji alisema jambo hilo limeendelea kuwa tatizo kubwa siyo tu katika chakula lakini pia katika malighafi kwa maendeleo ya viwanda huku akizitaja juhudi zilizofanywa na serikali ya Tanzania kupunguza upotevu wa chakula.

Dkt Tizeba, alielezea juhudi hizo kuwa ni pamoja na kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo, taasisi za kimataifa kama vile Bill and Melinda Gates foundation, HELVETAS Swiss Inter Cooperation Agency, Rockefeller foundation, AGRA, shirika la chakula Duniani, mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo yameboresha kwa kiasi kikubwa teknolojia ya uhifadhi kama vile mifuko ya plastiki ya kuhifadhia nafaka ambayo imeonesha kuwa na mafanikio makubwa sana kwa kuzuia wadudu waharibifu kupenya na kushambulia nafaka.

Sambamba na hilo alisema juhudi za kupambana na upotevu wa chakula kumeifanya Tanzania kuanzisha mfumo wa kubadilishana bdhaa. Kuweka mazao katika masoko yaonekanayo ili kurahisisha uuzaji na kupunguza upoteaji wa bidhaa za kilimo. Chini ya mradi huu mazao yatatunzwa chini ya mfumo wa vikundi vya wakulima na kuuzwa moja kwa moja  katika mfumo wa kupitia soko la bidhaa.

Kongamano hilo limefika ukomo hapo jana tarehe 8 Septemba 2018 baada ya kujadili maswala ya kilimo kwa siku nne mfululizo, lilihudhuriwa pia na viongozi wengine wa Afrika akiwemo Rais wa Ghana Mhe Nana Addo Dankwa Akufo Addo, Makamu wa Rais wa Kenya Mhe William Ruto, Waziri Mkuu wa Gabon Mhe Emmanuel Issoze-Ngondet sambamba na Waziri Mkuu mstaafu wa Uingereza Mhe Tony Blair.

MWISHO.

Huna Sababu Ya Kuaibikatena............ Jipatie Dawa Bora Ya Nguvu Za Kiume, Maumbile Madogo Na Mvuto Wa Mapenz

$
0
0
Usikate tamaa ondoa maradhi yako, maana matatizo haya yamekua yakiasili watuwengi kisaikolojia hasa baada ya kujiona wako tofauti sana na wengine kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia (6-8) vinginevyo mtuhuyo anamapunguvu katika mwiliwake.

Kunasababu nyingi sana zinazosababisha matatizo haya, chango hushambulia never ambayo huasili misuli ya uume, Ngili :- hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kufanya tumbo kuunguluma na kujaa gesi, kolodani moja kuvimba au kuingia ndani pamoja na kutopata choo vizuli. Sababuhizi na nyingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba na marakwamara husababisha kukosa hamu ya kuludia tendo la ndoa na baadae kushindwa kabisa

MASISA 3POWER :- nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa mfumo wa vidonge, huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka 15-90 , inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii) inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa, itakufanya uludie tendo la ndoa zaidi ya mara nne (4) birahamu kuisha wara kuhisi kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya dk (20-30 )

YONINANI:- hurefusha na kunenepesha maumbile madogo ya uume uliosinyaa inchi 6-8 na unene wa sm 3-4 kwa mda mfupi sana,

SUPER MORINA :- nidawa inayotibu ama kutatua tatizo la kisukali kwawaliohangaika bila mafanikio, huondoa tatizo la kisukali na kupona kabisa, vilevile ninadawa ya magonjwa sugu km vile presha, vidondo vya tumbo, miguu kuwakamoto, muwasho mwilin, kaswende,uzazi nk.

LUGIMBA :- nidawa ya mvuto wa mapenzi, humtuliza mke, mme, mchumba, hawara au mtu yoyote umpendae na kumfanya akutimizie chochotekile unachokitaka kutoka kwake na kumfunga asiwe na mtu yoyote zaidi yako.

WASILIANA NA DR CHIPUPA NAPATIKANA DAR ES SALAAM KUMBUKA HUDUMAHII ITAKUFIKIA POPOTE ULIPO  0759208637 / 0622344969

Rais Magufuli: Sitatoa Chakula Cha BURE....Tufanye kazi kwa Bidii

$
0
0
Rais John Magufulia amewaambia wakazi wa Itilima mkoani Simiyu wachape kazi, huku akisisitiza kuwa Serikali haitatoa chakula cha bure.

Rais Magufuli ameyasema hayo jana Septemba 9, ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake mkoani Simiyu akitokea Mara. Amewataka wananchi hao kutafuta maendeleo ya kweli hasa kwenye kilimo ambacho ndiyo shughuli kuu ya uchumi wao.

“Endeleeni kuchapa kazi, chakula cha bure hakitakuja. Hili lazima niwaambie ukweli, Serikali haina shamba,”  alisema Rais Magufuli aliposimama na kuzungumza na wakazi hao.

Rais Magufuli amewataka pia kuachana na imani za kishirikina badala yake wapeleke watoto wao shule kwa sababu Serikali inatoa elimu bure.

“Kila mwezi tunatoa Sh23.85 bilioni kwa ajili ya elimu bure. Pelekeni watoto shule,” alisema Magufuli huku akishangiliwa na wananchi hao.

Rais Magufuli Awaambia Watanzania Wazae tu.....Asema Kama Mtu Unachapa Kazi, Uzazi wa Mpango wa Nini?

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amesema yeye sio muumini sana wa sera ya uzazi wa mpango kutokana na sera hiyo kusababisha upungufu wa nguvu kazi kwa taifa.

Rais Magufuli ameyasema hayo jana, kwenye mkutano wa hadhara aliofanya wilayani Meatu mkoani Simiyu ikiwa ni sehemu ya ziara yake katika mikoa ya kanda ya ziwa ambapo amesisitiza watanzania waendelee kuzaa lakini wachape kazi ili kuwatimizia mahitaji muhimu watoto wao.

''Najua Waziri wa Afya Ummy Mwalimu hapa angependa kuongelea mambo ya uzazi wa mpango lakini mimi mengine huwa sikubaliani nayo sana, utapangiwaje kuzaa'' ? alihoji Rais katika mkutano huo.

Rais Magufuli alisema amezunguka mataifa mengi duniani na amejionea jinsi yanavyotafuta nguvu kazi kutokana na mambo ya uzazi wa mpango hivyo kuwashauri wananchi kusikiliza na kuchuja baadhi ya mambo.

''Kwahiyo katika kushauriwa mengine tukubali na mengine tukatae tutumie msemo wa mzee Jakaya Kikwete (Ukiwambiwa changanya na za kwako) kuzaa ni muhimu'', amesema.

Aidha alisisitiza kuwa anajua watapinga sana lakini ukweli ndio huo watu wamejazwa mawazo ya ajabu na kwamba huwezi kuwa mwanaume kisha ukubali kufungiwa kizazi.

Dr Kanengo: Bingwa Wa Tiba Asili Hutibu Matatizo Yafuatayo

$
0
0
NKURURU:-ni dawa inayotibu miguu kuwaka moto, kiuno tumbo kupooza kupoteza fahamu 

MALABALA; hutibu kisukari , uti wa mgogo, Change, pumu, busha, kaswende, kifua kikuu, muwasho sehemu ya siri 

NKURUNGU,: Ni dawa kutibu  N, B, G, POWER :-ni dawa ya kuongeza nguvu za kiume ni vidonge 20 

MPERAMPERA:- ni dawa ya kurudisha Mke, mme, mpenzi,mchumba aliyekuacha /kuteseka, ni kwa mda wa siku 2 tu kusafisha , pia kuna dawa za kupunguza vitambi(nyama uzembe), maziwa makubwa,michirizi, mikovu makubwa, chunusi sugu. 

NR SIX POWER:-inatibu upungufu wa nguvu za kiume kwa wasio weza kumudu tendo la ndoa itakufanya uwe na hamu ya kurudia tendo la ndoa zaidi ya Mara 4 bila hamu Kuisha, inaboresha maumbile madogo na inaimarisha misuri iliyo legea na kusinyaa una pona kabisa, ndani ya siku 4 tu 

GASELA:-ni dawa ya maajabu (9) yaliyoshindikana. (1)-Kisukari, vidonda vya tumbo, tezi dume,walioshindikanika kupata watoto(ugumba),busha bila oparesheni, (2)zindiko Kali Katika biashara yako (chuma ulete) ndo kiboko yao kumkamata mwizi aliye kuibia vitu vyako pikipiki, gari, n, k( 2)zindiko la nyumba, mashamba, viwanja,.(4)kukutolea sumu uliyo ikanyaga (Mtego) (5)ujiamini kutumia dawa ya maajabu Saba (6)kutoa mikafara mfano ugomvi ndani ya nyumba kufukuzwa kazini bila sababu (7)kutabiri nyota na kung'arisha (8)kurudisha Mali iliyo potea mazingira ya kutatanisha, kushinda kesi uliyo sumbuka nayo mda mrefu. (9)kufukuza majini wachafu ndani ya mji,.

Haya yote yanawezekana kwa DR KANENGO popote ulipo . Muone  DR KANENGO,anatibu nguvu za kiume anarefusha na kunenepesha uume kwa saizi uipendayo kwa muda mfupi sana, pamoja na kuwa na hamu ya kurudia tendo la ndoa mara 4 bila hamu kuisha Na utachelewa kufika kileleni kwa muda wa dakika 40 bila kuchoka .

Angalizo usitume meseji wala kubipu..
 
You can get it in all East African countries,,our service is fast and easy... contact Whatsapp 0784,47,59,46.Dar es salaam Tanzania. ,..Dr. KANENGO 0744,92,29,82...You are welcome. Yuko pia Khahama Mjini, Bunda kwa sasa

Hospitali Ya Taifa Ya Muhimbili (NHC ) Yaokoa Tzs 3.96 Bilioni

$
0
0
 Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 

*Wagonjwa 45 wahudumiwa, wagharimu Tshs. 360 Mil. badala ya Tshs. 4.320 Bil kama wangeenda nje ya nchi

*Mmoja agharimu Tshs. 8 Mil. badala ya Tshs. 96 Mil. nje ya nchi 


Hospitali ya Taifa Muhimbili imeanzisha kwa mara ya kwanza hapa nchini utoaji wa huduma za tiba radiolojia (Interventional Radiology) ambapo kabla ya uanzishwaji wake wagonjwa waliokuwa wanahitaji huduma hizi walikuwa wakienda nje ya nchi.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam wakati akielezea kuanzishwa wa huduma hiyo, Mkurugenzi wa wa huduma za Tiba Shirikishi Dkt. Praxeda Agweyo amesema kuwa tiba hiyo inahusisha utalaam wa kutumia vifaa vya radiolojia kama X-Ray, MRI, CT-Scan na Ultra-Sound kutibu moja kwa moja ugonjwa au kuchukua sampuli kwa ajili ya uchunguzi.

Amesema kuwa huduma ambazo zimeanza kutolewa kupitia njia hiyo kwa sasa ni kuondoa uvimbe kwenye sehemu ya kinywa, uso na shingoni (sclerotherapy for haemangioma and lymphangioma), kuweka mirija kwenye figo ambazo mirija ya kutoa mkojo imeziba (nephrostomy tube placement), kuzibua mirija ya nyongo iliyoziba (percutaneous trans hepatic biliary drainage) na kuzibua mirija ya uzazi iliyoziba (fallopian tube recanalization).

Tiba nyingine ni kunyonya usaha ndani ya tumbo (abscesses drainage). Ameongeza kuwa wastani wa mgonjwa mmoja kutibiwa uvimbe kwenye sehemu ya kinywa (sclerotherapy for haemangioma) inagharimu kiasi cha Tshs. 2 mil. ambapo kutokana na ugonjwa huo mgonjwa anahitaji kutibiwa hatua nne ili kukamilisha mzunguko wa tiba hiyo sawa na Tshs. 8 mil.

"Mgonjwa kama huyo alipokuwa akienda nje ya nchi ilikuwa inagharimu kiasi cha Tshs. 24 mil. kwa kila hatua moja sawa na Tshs. 96 mil. kwa hatua zote nne," amesema Dkt. Ongweyo. Tangu kuanzishwa kwa huduma hizi Novemba 2017, jumla ya wagonjwa 45 wamenufaika kwa gharama ya Tshs. 360 mil. sawa na Tshs. 8 mil. kwa kila mgonjwa. Kama wangeenda nje ya nchi ingeigharimu Serikali kiasi cha Tshs. 4.320 Bil. sawa na Tshs. 96 mil. kwa kila mgonjwa.

"Tunamshukuru Mungu mpaka sasa Hospitali ya Taifa Muhimbili imeokoa kiasi cha Tshs. 3.96 Bil. kwa kutoa huduma hiyo hapa nchini. Uwepo wa huduma hii hapa nchini utasaidia wananchi wengi kunufaika na hatimaye kupunguza mzigo wa kulipa fedha nyingi kwa matibabu huko nje," amesema Dkt. Ogweyo.

Kabla ya uanzishwaji wa huduma hizi hapa nchini, vifaa vilivyopo katika Idara ya Radiolojia kama vile X-Ray, MRI, CT-Scan na Ultra-Sound vilikuwa vinatumika kufanya uchunguzi tu wa magonjwa lakini sasa vinatumika kutibu pia.

"Tunashukuru uongozi mzima wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kuweza kuwapa madaktari wao mafunzo zaidi na kuweza kuwa wa kisasa zaidi, tulipopata mafunzo kwa madaktari wa hospitali ua Kenyatta walitufungua mengi na sasa nasi tunaweza na tunaokoa fedha za serkali," amesema Dkt. Ogweyo.

Mbunge Ataka Wilaya Ya Tunduru Igawanywe, Serikali Yagoma

$
0
0
Serikali imesema imesitisha uanzishwaji wa maeneo mapya ya utawala hadi yaliyopo yaimarishwe kikamilifu.

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Josephat Kakunda, amesema hayo bungeni jijini Dodoma leo Jumatatu Septemba 10, wakati akijibu swali la Mbunge wa Tunduru Kusini, Daimu Mpakate ambaye alihoji mpango wa serikali kuigawa Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru, mkoani Mtwara ambayo ina wilaya sita.

Akiuliza swali hilo bungeni jijini Dodoma jana, mbunge huyo amesema; “Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru iliomba kuigawa wilaya hiyo ambayo ni kubwa zaidi mkoani humo ikiwa na wilaya sita, kata 39 na vijiji 167, je serikali ina mpango gani wa kuigawa ili iwe rahisi katika kutoa huduma karibu zaidi na wananchi.”

Kajibu swali hilo, Kakunda amesema suala hilo lina changamoto ya kuimarisha kwanza miundombinu kama majengo ya ofisi, nyumba za watumishi na mahitaji mengine kama vifaa, watumishi wa kutosha na vyombo vya usafiri kwenye maeneo mapya ya utawala tangu mwaka 2010 na 2012.

“Maombi ya kugawa Wilaya ya Tunduru na kuanzisha Halmashauri ya Wilaya ya Busanda, yaliwasilishwa Tamisemi yakiwa na ombi la kuanzisha Mkoa mpya wa Selous. Serikali imetafakari maombi hayo na kuyaona ni ya msingi lakini yana changamoto nilizoainisha awali,” amesema Kakunda.

Rais Magufuli Amgomea Waziri Wake Hadharani

$
0
0
Rais  Magufuli amekataa ombi la Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina ambaye pia ni Mbunge wa Kisesa mkoani Simiyu la kutaka jimbo lake liwe halmashauri.

Rais Dk.Magufuli alisema kuanzisha maeneo mapya ya utawala kumekuwa kukiongeza gharama za uendeshaji.

Alisema ni bora fedha hizo akazitumia kuwaletea wananchi maenedeleo kuliko kuongeza halmashauri.

Rais Magufuli alitoa kauli hiyo jana katika mji wa Mwandoya wilayani Meatu aliposimama kusalimia wananchi, wakati wa ziara ya kukagua shughuli za maendeleo.

Awali Mpina alimwomba Rais Dk. Magufuli kuwapatia halmashauri wananchi wa Kisesa kutokana na kutembea umbali mrefu kufuata huduma za kiutawala.

“Wananchi wa Kisesa wamekuwa wakipata wakati mgumu kwenda mji wa Mwanhunzi  ambapo kuna ofisi za halmashuari.

“Wilaya ya Meatu kuna majimbo mawili na yote yanategemea halmashauri moja. Hawa wananchi mheshimiwa Rais, wanatembea umbali wa kilomita zaidi ya 100 kwenda makao makuu ya mkoa, kilomita 60 kwenda makao makuu ya halmashauri.

“Mheshimiwa Rais umbali huo wote ni mrefu, sisi hatuombi wilaya, tunaomba utupatie halmashauri ya kwetu sisi wenyewe,” alisema waziri huyo.

Mpina alisema uwezo wa kujiendesha kama halmashauri upo, kutokana na kuwapo kwa idadi kubwa ya watu zaidi ya 170,000.

Alisema mbali na idadi ya watu, Jimbo la Kisesa lina uwezo wa mapato, kwani limekuwa likikusanya zaidi ya Sh bilioni 2 kwa mwaka pamoja na kuwapo kwa miundombinu mingine ya kutosha kuwa halmashauri.

Huku akishangiliwa na umati mkubwa wa wananchi, Waziri Mpina alisema kupatikana kwa halmashauri kutasababisha wananchi wa jimbo hilo kupata maendeleo kwa haraka.

Akizungumzia ombi hilo, Rais Magufuli alisema kwa sasa hawezi kuanzisha maeneo mapya wakati wananchi wengi bado ni maskini na badala yake atahakikisha anawaletea maendeleo na si kuwaletea halmashauri.

Rais Magufuli alilazimika kutoa mifano mbalimbali ya majimbo yenye maeneo makubwa, lakini kuna halmashauri moja, ambapo alitolea mfano wa halmashauri ya Chato ambayo alieleza kuwa idadi ya watu ni zaidi ya 400,000.

“Kuna majimbo mengi tena makubwa zaidi ya hili na yana idadi kubwa ya watu kuliko hapa Kisesa, kuna halmashauri moja, siwezi kuleta halmashauri wakati najua itaongeza gharama za uendeshaji,” alisema Rais Magufuli.

“Kupanga ni kuchagua, niache nishughulikie masuala ya barabara, umeme, maji na afya, siyo kuwaletea halmashauri, haya maombi yenu yatakuwa baadaye lakini siyo sasa hivi, siwezi kuleta halmashauri, nitaleta maendeleo,”alisema Rais Maguli.

Alisema hawezi kuwadanganya kuwa atawapatia  halmashauri wakati jambo hilo hawezi kulifanya kwa sasa.

Picha ya Irene Uwoya Yazua Balaa Mtandaoni

$
0
0
Msanii wa Filamu Bongo, Irene Uwoya amejikuta akiibua mjadala mkubwa mara baada ya kuachia picha ambayo inaonyesha eneo la kifuani likiwa wazi kwa asilimia kubwa.

Mremmbo huyo ametumia ukurasa wake wa Instagram kuweka picha hiyo ambapo mashabiki wake wamejikuta wakichagia kwa wingi kuliko ilivyo kawaida kuhusu picha hiyo 

==>>Picha iliyozua gumzo

VIDEO: Serikali Yagoma Kuwalipa Watumishi Waliofukuzwa Kazini Kwa Kuwa na Vyeti FEKI

$
0
0
Serikali imesema haitawalipa watumishi waliofukuzwa kazi kwa kuwa na vyeti feki kutokana na udanganyifu huo.

Akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu, Aida Khenani bungeni jijini Dodoma leo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, George Mkuchika amesema serikali haijapanga kumlipa mtumishi yeyote ambaye mkataba wake ni feki.

Akiuliza swali hilo, Aida amesema kabla ya kupunguzwa kwa watumishi hao waliodaiwa kuwa na vyeti feki, serikali ilikuwa na vyeti feki na hadi sasa kuna upungufu wa watumishi wa kiasi gani.

“Serikali ya Tanzania inathamini zaid vyeti kuliko taaluma, kuna wengine walikuwa wamebakisha mwaka mmoja tu ili wastaafu, je, serikali ina mpango gani wa kuwalipa watumishi hao,” amesema.

Mkuchika akijibu hilo amesema; “Mwajiri alikuajiri akijua vyeti ulivyompelekea ni sahihi, kitendo cha kumdanganya kinafuta mkataba wenu na serikali haijapanga kuwalipa watumishi wa aina hiyo,” 
 
Katika swali lake la msingi, Aida alitaka kujua mkakati wa serikali kuziba nafasi zilizoachwa wazi na watumishi waliokumbwa na sakata la vyeti feki ambapo Waziri Mkuchika alijibu serikali imeshatoa kibali cha kuajiri watumishi wapya 15,000 ili kuziba pengo la lililosababishwa na kuondolewa kwenye orodha ya malipo ya mishahara watumishi wa umma waliobainika kughushi vyeti.

==>>Tazama video hapo chini

Spika wa Bunge Job Ndugai Awapiga Marufuku Wabunge Kuingia Bungeni na Kucha Bandia au Kope Bandia

$
0
0
Spika wa Bunge, Job Ndugai, leo septemba 10, 2018  amepiga marufuku wabunge waliobandika kucha na kope bandia kuingia katika Ukumbi wa Bunge.

Spika Ndugai amesema hayo wakati wa kipindi cha maswali na majibu, baada ya Mbunge wa Viti Maalumu, Fatma Tawfiq kuhoji idadi ya wanawake walioathirika macho kutokana na matumizi ya kope bandia kwani baadhi ya wanawake wameathirika na vipodozi vikiwamo kucha za na kope za kubandika.

Swali hilo lilijibiwa na Naibu Waziri wa Afya Mhe. Faustine Ndugulile  ambapo amesemaTakribani wagonjwa 700 kwa mwaka hupokelewa katika hospitali ya Taifa Muhimbili (MHN), wakiwa na matatizo ya ngozi yanayaotokana na kumeza vidonge vinavyobadili rangi ya mwili mzima, pamoja na vipodozi vyenye kemikali. 
 
Dk. Ndungulile amesema kwa sasa wizara kupitia Mamlaka Chakula, Dawa na Vipodozi (TFDA) haina utaratibu wa kudhibiti kope wala kucha za kubandika kwa sababu hakuna sheria inayoipa ya kudhibiti bidhaa hizo.


Pamoja na mambo mengine, Dk. Ndungulile alisema anaomba kuwapa somo wabunge akisema; “tunapozichubua ngozi zetu tunaondoa kinga, mtu anayejichubua ngozi anaingia katika hatari ya kupata saratani, magonjwa ya ngozi, rangi ya asili ni nzuri ilitengenezwa kwa ajili ya kujikinga na magonjwa mbalimbali hivyo nawaomba msiharibu ngozi zenu kwa vipodozi.”

Baada ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndungulile kujibu swali hilo, Spika Ndugai alisema; “Kutokana na elimu hiyo, na mimi leo napiga marufuku kwa wabunge wote kuingia bungeni wakiwa na kucha na kope bandia, lakini kwa wale wanaojichubua naendelea kuchukua maoni,” amesema Spika Ndugai huku baadhi ya wabunge wanaume wakipaza sauti kwa kusema “na nywele bandia huku Dk. Ndunglile akimshukuru kwa kuungana na serikali kupiga marufuku matumizi ya kope na kucha bandia.”



Serikali Kuajiri Watendaji Kata 1000

$
0
0
Serikali ina mpango wa kuajiri watendaji kata 1,000 ili kupunguza pengo kubwa la ukosefu wa watendaji hao katika maeneo mengi nchini.

Kauli hiyo imetolewa leo bungeni na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi, Joseph Kandege.

Kandege alitoa kauli hiyo wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Tundulu Kusini (CCM), Daim Mpakate ambaye alitaka kujua ni lini Serikali itaajiri watendaji kata kwani maeneo mengi yako wazi.

Naibu Waziri huyo alikiri watendaji ni watu muhimu katika shughuli za maendeleo hivyo Serikali imeona umuhimu wa kuwaajiri ili kusukuma mbele kurudumu la maendeleo.

"Tumeomba kibali na tumepewa kuajiri watendaji kata 1,000, hivyo tuna amini tukishaajiri hao tutakuwa tumepunguza pengo hilo kwa kiasi kikubwa," alisema Kandege.

Naibu Waziri huyo alisema mpango huo utafanyika mapema kwa kuwa uhitaji wao ni mkubwa.

Yanayojiri Bungeni: Spika Ndugai Kaamua Kulifuta Swali la Sugu...Kwa nini? Tazama Hapa

$
0
0
Spika Ndugai amelifuta swali la Mbumbe wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi, maarufu kama Sugu, lililokuwa likihoji juu ya madai ya CCM kupora mali za wananchi. 

Spika amesema analifuta swali hilo kwa sababu halina ukweli na wala halihusiani   kwa namna yoyote ile na Waziri  wa Habari  aliyeulizwa swali hilo

==>>Tazama hapo chini

VIDEO: Lugola aja na staili mpya ya kichungaji kumsifia Rais Magufuli

$
0
0
Waziri  wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola amekuja  na staili mpya ya kichungaji kumsifia Rais Magufuli kwa utendaji uliotukuka huku akimhakikishia ataendelea kupambana na mafisadi yote yanayokula fedha za umma.

Lugola amefunguka hayo Leo Septemba 10, 2018 wakati Rais Magufuli akizindua ujenzi wa Daraja la  mto Sibiti linalounganisha mkoa wa Simiyu na Singida.

==>>Msikilize hapo chini

Wafanyabiashara Watakiwa Kutumia Mawakala Waliothibitishwa Na Tra Kupata Karatasi Za Risiti

$
0
0
Serikali imetatua tatizo la kuwepo kwa karatasi za risiti  zinazofutika maandishi zinazotolewa na Mashine za Kielektroniki za kutolea Risiti (EFDs)  kwa kuwataka wafanyabiashara wote kununua karatasi hizo kwa mawakala waliothibitishwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Hayo yameelezwa Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Tanga Mjini Mhe. Mussa Bakari Mbarouk, aliyetaka kujua kauli ya Serikali kuhusu risiti zinazotolewa na Mashine za EFDs kufutika maandishi kwa muda mfupi na muda ambao utatolewa kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kurekebisha hali hiyo.

Akijibu swali hilo Dkt. Kijaji alieleza kuwa Serikali inatambua kuwa kuna karatasi feki, lakini tatizo la kufutika kwa risiti halihitaji kutoa muda kwa TRA wa kufanya marekebisho kwa kuwa Serikali ililifanyia kazi, hivyo ni jukumu la wafanyabiashara kufuata maelekezo ya ununuzi wa karatasi hizo kwa wakala waliothibitishwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania.

Naibu Waziri Kijaji, akijibu maswali ya  Msingi ya Mbunge huyo aliyetaka kujua bei halisi za Mashine ya EFDs na kwa nini Serikali isitoe Mashine hizo bure kwa wafanyabiashara, alisema kuwa kuna aina tano za Mashine ambazo mfanyabiashara anaweza kununua kulingana na mahitaji yake.

“Mashine za EFDs ni kama Rejista za kielektroniki za kodi (ETR) ambayo bei yake ni Sh. 590,000 na hutumiwa na wafanyabiashara wasiotumia mifumo ya Kompyuta na kihasibu na Mashine za kielektroniki zinazoweka alama/saini (Electronic Signature Devices) ambazo hutumiwa na walipa kodi wanaotumia mifumo ya kompyuta na kihasibu, bei yake ikiwa ni kati ya Sh. 1,000,000 hadi 1,200,000”, alieleza Dkt. Kijaji.

Alisema kuwa Mashine nyingine ni Printa za kielektroniki za kodi (Electronic fiscal printers) ambazo hutumia mfumo maalum wa kompyuta, bei yake ikiwa ni kati ya Sh. 1,500,000 hadi Sh. 1,700,000, pia zipo mashine ya Printa za Pampu za Mafuta ya Petroli au Dizel (EFPP) ambazo hutumiwa na wafanyabiashara wa mafuta, bei yake ikiwa ni Sh. 6,000,000 ikijumuisha gharama za ufungaji na uunganishwaji kwenye pampu za mafuta.

Aidha kuna Mashine ya Printa za Maduka ya kubadilisha Fedha za Kigeni, bei ya mashine hizo ni Sh. 2,150,000 ikiwa ni pamoja na program ya mfumo wa software.

“Ubora wa Mashine hizo ni lazima uthibitishwe na Mamlaka ya Mapato Tanzania- TRA kabla mashine hizo hazijaingizwa sokoni na kuanza kutumika”, alifafanua Dkt. Kijaji.

Dkt. Kijaji alisema kuwa wafanyabiashara wasiosajiliwa kwenye Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) wanaponunua mashine za EFDs hulipa gharama za ununuzi wa mashine hizo na baadae Serikali hurejesha gharama kwa kumruhusu mlipakodi kujirejeshea fedha zake kwa utaratibu wa Input- Output tax kwenye mauzo ya mwezi husika.

Vilevile kwa wafanyabiashara wasiosajiliwa kwenye VAT na wanaoandaa hesabu za mizania, hujirejeshea gharama za ununuzi wa mashine kwa kuingiza gharama husika kama gharama za kuendesha biashara kwa mujibu wa sheria ya Kodi ya Mapato.

Naibu Waziri huyo amebainisha kuwa, kwa wafanyabiashara wasioandaa hesabu za mizania wanajirejeshea gharama za mashine kwenye kiasi cha kodi walichokadiriwa kwa mwaka husika na iwapo hawatakuwa wamejirejeshea kwa asilimia miamoja, kiasi kilichobakia kitasogezwa mwaka unaofuata.

Imetolewa na ;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Fedha na Mipango.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya Septemba 11

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images