Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

DAWASCO Yavunjwa Rasmi ......Yaunganishwa Na DAWASA

0
0
Shirika la majisafi na Majitaka Dar es Salaam(DAWASCO) limevunjwa rasmi na kuunganishwa katika Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam(DAWASA).

Akizungumza katika sherehe za kuunganishwa kwa DAWASA na DASAWCO leo Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema kuunganishwa huko kutaokoa Sh Bilioni 2.9 kila mwaka zilizokuwa zikipotea katika uendeshaji wa Dawasa na Dawasco.

Amesema fedha hizo zitakwenda kusaidia upatikanaji wa huduma ya maji katika Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.

“Serikali iliamua kuunganisha Dawasa na Dawasco ili kupunguza matumizi na fedha hizi zitaimarisha miundombinu na kuboresha huduma za maji katika eneo la huduma,” alisema Profesa Mkumbo.

Profesa Mkumbo amewaonya wafanyakazi wa Dawasa mpya kuacha tabia ya ya dharau, nyodo,kukumbatia matatizo, na kuomba rushwa kwa wateja.

“Baadhi yenu mmekuwa na nyodo, kikola,rushwa na kuridhika na mafanikio kidogo tabia hizi zikome kuanzia sasa,” alisema Profesa Mkumbo.

Ametaka Dawasa mpya kujiendesha kama kampuni binafsi inayolipwa na wananchi wa Dar es Salaam na si Idara ya serikali ili kuongeza makusanyo ya fedha.

“Niwaombe mpunguze upotevu wa maji ambao kwa sasa asilimia 47 ya maji yanayozalishwa na Dawasa yanapotea,” alisema Profesa Mkumbo.

Aidha alisema serikali imeamua kuwapa Dawasa jengo la ghorofa lililopo Ubungo njiapanda ya kwenda chuo kikuu ili walimalizie na kuhamia humo.

Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa, Cyprian Luhemeja ameahidi kuteteleza baakukamilisha miradi mitatu na kutoa muendelezo wa miradi mingine ndani ya siku 100.

“Zawadi yetu kwa Rais Dk John Magufuli hadi kufikia Disemba 9, mwaka huu tutakamilisha mradi wa maji wa Chalinze, usambazaji wa maji upande wa Goba tegeta na maeneo mengine yaliyokaribu,” alisema Luhemeja.

Amesema  ndani ya siku 100 hizo watafunga mita za malipo ya kabla nyingi na kuwahakikishia wanaanza ujenzi wa matenki ya Pugu na kusanifu upya mradi wa visima vya Mpera.

“Ndani ya siku hizo pia tutaongeza mapato kutoka Sh Bilioni tisa hadi kufikia Sh Bilioni 12 na pia tutahakikisha tunapunguza upotevu wa maji,” alisema Luhemeja.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya Septemba 9

Ujio Mpya wa Wema Sepetu

0
0
Malkia wa filamu Wema Sepetu aka Tz sweetheart ametangaza ujio wake mpya baada ya ukimya wa muda mrefu.

Mrembo huyo atafanya matukio mawili kwa pamoja, uzinduzi wa filamu yake mpya ‘Dad’ alioshirikiana na Van Vicker kutoka Nigeria pamoja na kusherekea birthday yake ambayo ameiita Bithday Gala.

“The Moment tuliokuwa tukisubiria saaaaanaaa sio,  I hope you are Ready,” aliandika Wema Sepetu kupitia picha ya matangazo ya show hiyo.

Hili litakuwa ni tukio la kwanza la mrembo huyo toka ahukumiwe na Mahakama ya Kisutu baada ya kukutwa na hatia ya kutumia dawa za kulevya aina ya bangi.

Wengi wanadai umaarufu wa Wema umeshuka tofauti na kipindi cha nyumba ambacho inadaiwa alionekana kukubalika zaidi.

Muonekano mpya wa Ommy Dimpoz Baada ya Kupata Nafuu

0
0
Msanii wa muziki Bongo, Ommy Dimpoz amekuwa akipatiwa matibabu Afrika Kusini mara dada ya kufanyiwa upasuaji wa koo. Hizi ni picha za mwanzo kabisa za muimbaji huyo tangu alivyopata nafuu.
Picha zote Na George Dufanda

Rais Magufuli: Kama Mnaona Hii Sheria Haifai Nendeni Bungeni Mkaifute ili Watu Wavue Tu Samaki Watakavyo

0
0
Rais Dkt. John Magufuli ameonyesha kukerwa na uvuvi haramu na kuwataka wanasiasa nchini kuliangalia kwa upana suala hilo na kama wanao halina tija kwa upande wao, amewaomba waende Bungeni wakaifute sheria ya uvuvi namba 22 ya mwaka 2005.

Dkt. Magufuli ametoa kauli hiyo jana akiwa wilayani Busega mkoani Simiyu katika muendeleo wa ziara yake ya kikazi aliyoanza Septemba 03, 2018 na kusisitizia kuwa anahitaji kuiona nchi ikizingatia sheria ambazo zimetungwa na watanzania wenyewe.

"Kama mnaona wanasiasa hili suala la mifugo na samaki halifai muende mkaifute hiyo sheria namba 22 ya mwaka 2005 ili watu wavue tu halafu muone baada ya miaka miwili kama mtakuwa na samaki hapa Busega. Ni lazima tuweke utaratibu na utaratibu ndio utakao ujenga hii nchi katika hali ya uchumi", alisema Rais Magufuli na kuongeza;

"Uvuvi haramu ni ugonjwa, siku za nyuma tulikuwa na samaki wengi sana hapa Busega lakini leo wote hawapo, mjue tumewamaliza sisi wenyewe. Madhara ya kuwamaliza samaki tumeyafanya sisi wenyewe"

Aidha, Dkt. Magufuli amewahakikishia wananchi wa Busega pamoja na watanzania kiujumla kuwa zoezi la kupambana na uvuvi haramu halitoweza kuisha kwa haraka kama baadhi yao wanavyofikiria na kuwataka wafahamu kuwa zoezi hilo ni endelevu.

"Nilipokuwa Waziri nilienda Magu na kuchoma nyavu sasa nimemuachia hii kazi Waziri Luhaga Mpina msimchukie anafanya kazi ya serikali, kwa niaba ya serikali kwa mujibu wa sheria ya namba 22 ya mwaka 2005. Na niwaombe ndugu zangu msinunue wala kuvua samaki wachanga", alisisitiza Rais Magufuli.

Mbali na hilo, Rais Magufuli amemuagiza Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina kuwachukulia hatua stahiki maofisa uvuvi endapo atabaini uvuvi haramu katika eneo analosimamia.

"Maofisa Uvuvi hawa ndio walioendeleza uvuvi huu haramu, na mimi nikuombe Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina anza kuwashughulikia maofisa uvuvi wako. Ukikuta mahali kuna uvuvi haramu na kuna ofisa uvuvi shika huyo muweke ndani, kwasababu wanalipwa pesa za serikali na uvuvi haramu unaendelea kwao",alisema Dkt. Magufuli.

Kabla ya agizo hilo la Rais Magufuli, itakumbukwa mnamo mwezi Februari mwaka 2018, Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina alianzisha operesheni yake ya siku 40 katika mikoa ya kanda ya ziwa kwa lengo la kupinga uvuvi haramu, ambao unakosesha fedha serikali kwa namna moja ama nyingine.

Flaviana Matata Akutana LIVE na Nicki Minaj

0
0
Mwanamitindo maarufu Bongo, Flaviana Matata amekutana na rapper Nicki Minaj kutokea Marekani.

Wawili hao walikutana mara baada ya kumalizika kwa zoezi la utoaji wa tuzo FMAS kwa mwaka 2018. Hii si mara ya kwanza kwa Flaviana Matata kukutana na mastaa wakubwa wa Marekani. 
 
Utakumbuka September 2017 Flaviana alishare video kwenye ukurasa wake wa mtandao wa twitter akionyesha pindi alipokutana na Jay Z pamoja na Beyonce.

Shindano la Miss Tanzania 2018 Lilifanyika Usiku wa Kuamkia Leo na Huyu Ndo Mshindi

0
0
Usiku wa kuamkia leo September 9, 2018 kumefanyika shindano la Miss Tanzania kwa mwaka 2018. Mrembo Queen Elizabeth ndiye aliyeshinda taji hilo.

Queen Elizabeth kutoka Zone ya Dar es salaam alifanikiwa kuondoka na taji hilo huku akiwamwaga wenzake 19 baada ya kuingia tano bora.

Warembo hao waliulizwa  maswali na aliyejibu vizuri alijichukulia maksi nyingi kutoka kwa majaji,kati ya warembo hao kuna wengine walijibu vizuri huku mmoja wao akipata kigugumizi wakati wa kujibu swali husika.

Na kati ya warembo hao warembo watatu walijibu maswali kwa lugha ya Kiingereza huku warembo wawili yaani aliyeshika nafasi ya tano na ya nne hao waliweza kujibu maswali kwa kutumia lugha ya taifa ya kiswahili huku mshindi namba tatu mpaka namba moja wakijibu kwa lugha ya kiingereza.

==Tazama baadhi ya picha hapo chini
Warembo waliofanikiwa kufika hatua ya tano bora
Miss Tanzania mwaka 2016/18, Diana Flave akijiandaa kukabidhi taji
Katikati ni Mshindi wa Miss Tanzania  mwaka 2018, Queen Elizabeth
Msanii Ruby akitumbuiza

Kalulumila:Dawa Bora ya Nguvu za Kiume na Maumbile Madogo

0
0
 BORA YA NGUVU ZA KIUME NA MAUMBILE MADOGO KALULUMILA.
----------------------------------------
Ni dawa pekee iliyojipatia umaarufu nchini na nje ya nchi kwa kufanya kazi mara 3, kwa wakati mmoja 1, kurefusha uume na kunenepesha saizi uipendayo kuongeza nguvu za kiume na inatibu matatizo na gerentii miaka 30. Na kuendelea haina madhara, inaimarisha mishipa ya uume iliyoregea na udhalishaji wa mbegu za kiume. 


---------NINI HUCHANGIA MATATIZO HAYA--Ngiri ni chanzo kikubwa cha matatizo haya ili kujua kwamba una ngiri ni chanzo kikubwa cha matatizo haya, ili kujua kama unangiri dalili zake ni kufika haraka kileleni wakati wa tendo la ndoa, 2)kushindwa kurudia tendo la ndoa. 3)kutoa choo kama cha mbuzi. 4)tumbo kujaa gesi na kuunguruma. 5)kukosa choo kabisa. 6)maumbile kuingia ndani na kuwa mafupi. 7) korodani moja kuvimba 8)kutosikia hamu ya tendo la ndoa na maumivu ya kiuno wakati wa tendo la ndoa. 9)maumivu ya kiuno na mgongo pia tunatibu kisukari kwa siku7, presha, busha, bila kupasuliwa na magonjwa mbalimbali. 

---------------------------------------
TUPO TEGETA KWA NDEVU KARIBU NA MACHINJIO YA NGOMBE UTAONA OFSI IMEANDIKWA KALULUMILA HERBALIST CLINIC HOSPITAL SIMU .
----------------------------------------
-0655-557-182.
-0755-557182.
-0784-557-182.
PIA UTAWEZA KULETEWA POPOTE ULIPO.
---------------------------------------
KARIBUNI SANA.
----------------------------------------

Makanga 3 Power; Dawa Bora Nguvu Za Kiume

0
0
Kutibu nguvu za kiume dakika(10) na kupona muda wa siku tatu tuu. Kuimarisha misuli ya uume uliolegea, pia ipo Dawa ya kurefusha uume mfupi inchi NNE hadi saba na kunenepesha uume mfupi sentimita NNE.

Tiba ya kudumu kutibu maumivu ya mgongo,kiuno, tumbo kuunguruma na kujaa gesi, kupata choo vizuri, na kutibu uzazi, kutibu busha bila operesheni, kisukari, presha ,miguu kuuma, uzazi, fangas sugu, vidonda vya tumbo.

Ni docta bingwa wa kutibu magonjwa sugu, kutoa ndagu za utajiri kwa kutumia Pete, kazi ,cheni, mikufu maalumu ya bahati, una kesi umedhulumiwa Mali au pesa? Zitarudi muda wa Masaa matatu tuu.

Onana na Dr shilindes shida zako zote zitakwisha, anatoa Dawa za utajiri kwa wafanyakazi, wakulima, na wafugaji, wafanyabiashara na wachimba madini kwa kutumia pete, kazi kwa yeyote anaetaka kuwa na pesa nyingi.

Pia anaboresha akili kwa wanafunzi darasani, masomo na kufaulu mitihani pia kushinda bahati nasibu yeyote.

Pia tunatoa Dawa kumrudisha Mume, mke, mpenzi, hawara, kwa muda wa SAA moja tuu, na kuomba msamaha kwa kukupigia magoti na yeyote yule, unaemtaka kimapenzi au kuoana, utampata na kumfunga asitoke nje ya ndoa daima na kutekeleza shida zako zote. Kupunguza unene, kupunguza matiti makubwa, tumbo na nyama uzembe muda wa siku sita unapata saizi uipendayo.

Kutoa makovu mwilini, chunusi, upele na mabaka, pia tunayo Dawa ya kuongeza hipsi, makalio, mguu wa bia na kupata shepu safi kwa muda wa siku saba tuu.

Wa mikoani mtapata huduma popote mlipo.
Tupo dar es salam mbagala rangi tatu.

Mawasiliano simu namba: 0784 460 348. Au 0659 103 360.

Rais Magufuli: Sitapeleka Maji Chato Hadi Wajifunze

0
0
Rais John Magufuli amesema hatapeleka mradi wa maji Wilaya ya Chato kwa sababu wakazi hao waliharibu mradi wa maji waliopelekewa 1970.

Rais Magufuli ameyasema hayo jana Septemba 8 wakati akizungumza na wananchi wa mji wa Lamadi mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa maji wa Lamadi, Simiyu.

Alisema   miradi mingi ya maji  haidumu kutokana na wananchi na viongozi kushindwa kutunza na kuisimamia ipasavyo.

Alitolea mfano katika kijiji cha Chato kilichopelekewa mradi wa maji mwaka 1970 lakini walishindwa kuutunza na mpaka sasa hawana maji. Alisema kamwe hawatapelekewa mpaka wajifunze.

Alisema kuwa yeye hashindwi kupeleka miradi ya maji Chato kama ilivyo kwa maeneo mengine  ya Mwanza,Simiyu na Musoma lakini anafanya hivyo ili wajute na kujifunza umuhimu wa kutunza miundombinu.

"Siwezi kukubali kuona miradi ya maji haidumukwa sababu eti wananchi na viongozi wanashindwa kutambua thamani ya utunzaji wa miradi ya maji na endapo mtashindwa kulinda na kutunza kamwe sitawaletea miradi mingine,”alisema Rais Magufuli

Rais amewataka Viongozi wa Wilaya ya Busega kushirikiana na wananchi ili kutunza mradi wa maji wa Lamadi  wenye thamani ya Sh 12.8 bilioni.

 Amesema endapo watashindwa kufanya hivyo kamwe hawatapelekewa miradi mingine.

Mbunge CCM Amvaa Lowassa Sakata la Richmond

0
0
Mbunge wa Ulanga (CCM),Goodluck Mlinga amewataka wakazi wa Monduli mkoani Arusha kumuuliza waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa sababu za kujiuzulu baada ya kuibuka kwa sakata la  Richmond.

Mlinga alitoa kauli hiyo jana Jumamosi Septemba 8, 2018 katika mkutano wa kampeni jimbo la Monduli uliofanyika eneo la Mukuyuni.

Alisema Lowassa anamshambulia mgombea wa CCM katika jimbo hilo, Julius Kalanga kuwa amejiuzulu uanachama wa Chadema na kuhamia chama tawala kwa sababu alikuwa na deni la Sh. milioni 600, wakati yeye alijiuzulu uwaziri mkuu kwa kuchukua fedha za Richmond.

Waziri huyo mkuu wa kwanza wa Serikali ya Awamu ya Nne, amekuwa hazungumzii sakata hilo la Richmond na inapotokea kulizungumzia amekuwa akieleza kuwa alijiuzulu kisiasa kuilinda Serikali ya CCM na kwamba ushiriki wake ulitokana na maagizo kutoka juu.

Kampuni ya Richmond Development Company ya Marekani ilipewa zabuni ya kufua umeme wa dharura wakati nchi ilipokuwa na tatizo kubwa la ukosefu wa nishati hiyo mwaka 2006.

“Jamani kati ya anayedaiwa na ambaye amejiuzulu kwa tuhuma za kuchukua fedha za umma nani bora,” alihoji Mlinga.

Mlinga alisema watu wengi wamekopa na kudaiwa lakini sio tatizo kwa kuwa anayekopa hulipa, deni halifungi mtu.

Aliwataka wakazi wa Monduli kupuuza tuhuma kuwa Kalanga alijiuzulu ili kulipiwa deni kwani kauli hizo ni za kisiasa.

Rais Magufuli Amtumbua Profesa Mwandosya...Nafasi Yake Kapewa Wasira

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli amemteua Steven Wasira kuwa mwenyekiti wa bodi ya chuo cha mwalimu Nyerere nafasi iliyokuwa inashikiliwa na Mark Mwandosya.

Aidha, wakati huo huo Rais Dkt. Magufuli amemteua Dkt. Festus Bulugu kuwa mwenyekiti wa baraza la uwekezaji la wananchi kiuchumi.

Dkt. Limbu anachukua nafasi ya Dkt. John Jungu ambaye amekuwa Katibu Mkuu wizara ya Afya, Jinsia Wazee na Watoto.

Itakumbukwa Dkt. Festus Burugu Limbu alikuwa mbunge wa Jimbo la Magu mkoani Mwanza, kwa awamu tatu tofauti akianza mwaka 2000 hadi 2015 na Stephen Masato Wasira  alihudumu kama Mbunge wa jimbo la Bunda Mjini kutoka mwaka 2005 hadi 2015 ambapo aliangushwa na Mbunge wa sasa Easter Bulaya.

Wizara Ya Mambo Ya Ndani Yatuma Rambirambi Kwa Wafiwa Wa Ajali Iliyotokea Jijini Mbeya

0
0
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, inatoa pole kwa familia zote ambazo zimepoteza ndugu na jamaa zao na wengine kujeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyohusisha magari matano, iliyotokea katika eneo la Igawilo Mjini Mbeya siku ya tarehe 7 Septemba, 2018 na kusababisha vifo vya watu 15 na kujeruhi wengine.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Kangi Alphaxard Lugola, (MB), kwa masikitiko makubwa anatoa pole kwa familia zote zilizopoteza wapendwa wao na kuwatakia majeruhi wote ahueni ya haraka ili warejee katika hali zao za kawaida na kuendelea na shughuli zao za kujenga nchi.

“Natoa pole nyingi kwa Watanzania wenzangu waliowapoteza wapendwa wao katika ajali hii na nawatakia majeruhi wote afya njema na wapate ahueni haraka ili waweze kurejea katika hali zao za kawaida”.

“Ni wakati muafaka kwa Watanzania wenzangu, Wasimamizi wa Sheria za Usalama Barabarani na Madereva kutokatishwa tamaa na ajali hii na badala yake changamoto hii iwafanye waongeze umakini barabarani, kuongeza umadhubuti katika usimamizi wa Sheria ya Usalama barabarani kwa kuchukua hatua kali zaidi kwa madereva wazembe na askari wasiotimiza wajibu wako wa kuhakikisha magari mabovu hayaruhusiwi kutembea barabarani”.

Mwenyezi Mungu azipe roho za ndugu zetu pumziko la amani. Amina

Imetolewa na:
Meja Jenerali Jacob G. Kingu, ndc
KATIBU MKUU

Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi ( WCF) Kuhakiki Michango Kwa Njia Ya Mtandao

Huna Sababu Ya Kuaibikatena............ Jipatie Dawa Bora Ya Nguvu Za Kiume, Maumbile Madogo Na Mvuto Wa Mapenz

0
0
Usikate tamaa ondoa maradhi yako, maana matatizo haya yamekua yakiasili watuwengi kisaikolojia hasa baada ya kujiona wako tofauti sana na wengine kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia (6-8) vinginevyo mtuhuyo anamapunguvu katika mwiliwake.

Kunasababu nyingi sana zinazosababisha matatizo haya, chango hushambulia never ambayo huasili misuli ya uume, Ngili :- hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kufanya tumbo kuunguluma na kujaa gesi, kolodani moja kuvimba au kuingia ndani pamoja na kutopata choo vizuli. Sababuhizi na nyingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba na marakwamara husababisha kukosa hamu ya kuludia tendo la ndoa na baadae kushindwa kabisa

MASISA 3POWER :- nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa mfumo wa vidonge, huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka 15-90 , inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii) inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa, itakufanya uludie tendo la ndoa zaidi ya mara nne (4) birahamu kuisha wara kuhisi kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya dk (20-30 )

YONINANI:- hurefusha na kunenepesha maumbile madogo ya uume uliosinyaa inchi 6-8 na unene wa sm 3-4 kwa mda mfupi sana,

SUPER MORINA :- nidawa inayotibu ama kutatua tatizo la kisukali kwawaliohangaika bila mafanikio, huondoa tatizo la kisukali na kupona kabisa, vilevile ninadawa ya magonjwa sugu km vile presha, vidondo vya tumbo, miguu kuwakamoto, muwasho mwilin, kaswende,uzazi nk.

LUGIMBA :- nidawa ya mvuto wa mapenzi, humtuliza mke, mme, mchumba, hawara au mtu yoyote umpendae na kumfanya akutimizie chochotekile unachokitaka kutoka kwake na kumfunga asiwe na mtu yoyote zaidi yako.

WASILIANA NA DR CHIPUPA NAPATIKANA DAR ES SALAAM KUMBUKA HUDUMAHII ITAKUFIKIA POPOTE ULIPO  0759208637 / 0622344969

Jokate Mwegelo Aipiga Faini Kampuni Kwa Kukiuka Agizo la Naibu Waziri

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya hiyo, Jokate Mwegelo, ameichukulia hatua kampuni ya Rak Kaolin, ambayo imekuwa ikijihusisha na uchimbaji wa madini ya Kaolin licha ya kuzuiliwa na Naibu Waziri wa Madini Madini Stanslaus Nyongo.

Jokate na Kamati yake walibaini kitendo hicho cha mwekezaji kuendelea kuchimba madini hayo kwenye zoezi la ukaguzi lililofanyika Septemba 06-07 mwaka huu katika maeneo mbalimbali ya shughuli za uchimbaji wilayani humo.

Taarifa ya wilaya hiyo imeeleza kuwa ukaguzi huo ulifanikiwa kukamata malori matatu yenye jumla ya tani 100 za madini hayo ambayo yana thamani ya shilingi za Tanzania 2,100,000.

Serikali ya wilaya ya Kisarawe katika kikao cha pamoja na Kamishna wa Madini Ukanda wa Mashariki Mhandisi Ally Maganga kimeamuru Kampuni hiyo kulipa adhabu ya kukiuka maagizo ya Naibu Waziri, Sheria ya Madini ya mwaka 2010 na marekebisho yake ya 2017.

Kampuni hiyo ya Rak Kaolin pia imetakiwa kulipa mapato yote ya Serikali ambayo imekwepa huku Jokate akitoa rai kwa wawekezaji wote wilayani humo kuhakikisha wanafuata sheria na kanuni zilizowekwa zikiwemo za kulipa kodi bila shuruti.

Msafara wa Rais Magufuli Wapata Ajali Simiyu....Waandishi wajeruhiwa

0
0
Gari lililokuwa limebeba waandishi wa habari wa Mkoa wa Simiyu limepata ajali kwenye msafara wa Rais John Magufuli wilayani Meatu ambapo liligongwa na magari mengine kwa nyuma.

Waandishi wa habari watatu, Adan Mhando wa Channel Ten, Faustine Fabian wa Mwananchi, Rehema Evansi wa Azam TV, na Mpiga picha wa ITV, wamepata majeraha madogomadogo na wamekimbizwa hospitali ya wilaya Meatu.

Wengine waliokuwemo katika  ajali hiyo na kunusurika ni Berensi China,Samwel Mwanga,Derick Milton,Costantine Mathias na Rehema Evance.

Lulu Michael Kavunja Ukimya Kwa Kumwandikia Maneno Matamu Mpenzi Wake💕💕💕

0
0
Baada ya kimya cha muda mrefu cha takribani siku 324 mitandaoni, hatimaye Muigizaji wa filamu nchini Tanzania, Elizabeth Michael almaarufu Lulu amerudi rasmi kwa kumuandikia ujumbe mahsusi mpenzi wake Majizzo ambaye pia ni Mkurugenzi wa EFM na TV-E .

Lulu ameandika ujumbe huo kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuandika; Lover,Best Friend,Business Partner,Ride Or Die And A Shoulder To Always Cry On...!! .

Asante Kwa Kunionyesha Maana Halisi Ya Upendo Wa Agape(KIUNGU)❤️❤️❤️
Baraka Zikufuate Siku Zote Za Maisha Yako.

Happy Birthday Baba G....I Love You💕💕💕
@majizzo @majizzo
 
Lulu hajawahi kuposti kitu chochote kile mtandaoni tangu mwaka jana ahukumiwe jela na baadae kutolewa jela kwa msamaha wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ujumbe huo pia ameutoa leo ikiwa ni siku ya kumbu kumbu ya kuzaliwa kwa Majizzo. Mashabiki wake wameoneshwa kufurahishwa zaidi na kitendo hicho

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya Septemba 10

Naibu Waziri Masauni aagiza mmiliki wa lori lililoua 15 Mbeya akamatwe

0
0
Naibu Waziri Masauni ambaye pia ni mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani Taifa ameamuru kukamatwa kwa mmiliki wa lori la Azania lililosababisha ajali ya gari iliyoua watu 15 mkoani Mbeya wiki hii

==>>Msikilize Naibu waziri hapo chini
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images