Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Shilole Ampa Neno Diamond....."Ndo Maana Wanawake Wanakuroga"

$
0
0
Bado kile kinachodaiwa kuwa Hamisa Mobetto alitaka kumloga Diamond Platnumz na familia yake kinazidi kuchukua nafasi kwenye mitandao ya kijami.

Mjadala umekuwa mpana hasa kwa kauli aliyoitoa jana Diamond kupitia Wasafi TV ingawa upande wa Hamisa amekuwa kimya kwenye suala hilo.

Sasa muimbaji Shilole hajawa nyuma kwenye hilo ameposti picha ya Diamond Platnumz (ipo chini) na kuisindikizia na caption iliyosema; 'Ndio maana wanakuroga, medamshi sana kaka yangu Diamond Platnumz,'.
Mwanamitindo Hamisa Mobetto amezaa mtoto mmoja na Diamond Platnumz na utakumbuka hadi muimbaji huyo anakiri kuwa amezaa na Hamisa ilikuwa ni baada ya mvutano mrefu na hii ni kutokana kipindi hicho Diamond bado alikuwa na mahusiano na Zari.

Polisi yaua Majambazi Matatu kwenye majibizano ya risasi....Yakamata Silaha 2

$
0
0
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limekamata bastola moja aina ya Browing namba A 183847 ikiwa na risasi tatu ndani ya magazine pamoja na Shotgun iliyotengenezwa kienyeji.

Akithibitisha tukio hilo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari leo, Kamanda wa Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa, amesema tukio hilo lilitokea mnamo Agosti 29, mwaka huu majira ya saa moja jioni katika Bar ya Big Brother iliyopo Mbagala kiburugwa.

” Agosti 29 2018 saa moja jioni huko maeneo ya Baa ya Big Brother iliyopo Mbagala kiburugwa Jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam liliwakurupusha wahalifu katika baa hiyo wanaodhaniwa kuwa walikuwa wanapanga njama za kufanya uhalifu.

“Baada ya wahalifu hao kuwaona askari walianza kujihami kwa kurusha risasi kuwashambulia, askari walijibu mapigo na kufanikiwa kuwajeruhi wahalifu watatu wanaume wanaokadiriwa kuwa na miaka (30-38) na wawili kufanikiwa kukimbia kusikojulikana,  walipopekuliwa walikutwa na silaha mbili,”amesema.

Majeruhi walifariki dunia wakati wakipelekwa hospitali, na miili yao imehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa  Muhimbili(MNH), Jeshi la Polisi linaendelea na msako mkali kuwasaka wahalifu wengine waliokimbia.

Aidha katika tukio jingine Mambosasa amesema Jeshi hilo limefanikiwa kukusanya kodi za tozo za makosa mbalimbali ya usalama barabarani kufikia kiasi cha zaidi ya bilioni 2.3, kiasi hiki kimekusanywa kuanzia Agosti 1 hadi Agosti 30 mwaka huu na kukamata magari 57,716 na Pikipiki 1872.

Dogo Janja afunguka kuhusu kuachana na Irene Uwoya

$
0
0
Msanii wa muziki Bongo, Dogo Janja amejibu kuhusu taarifa zinazodai kuwa ameachana na mkewe, Irene Uwoya.

Hitmaker huyo wa ngoma kama Kidebe, My Life na nyinginezo amesema kuwa hilo halina ukweli wowote kwa sasa.

"Hatujaachana ni sisi tumeamua kutoweka sana mambo yetu wazi na ndiyo maana unakuta hatuna picha nyingi tulizopiga wote" Dogo Janja ameiambia XXL ya Clouds FM.

Hivi karibuni kumekuwa na minong'ono ya chini kwa chini huwenda wawili hao wameachana mara baada ya Irene Uwoya kuoenekana akila bata pekee yake nchini Dubai.

Ploisi Kanda Maalumu Dar Yawaonya Mgambo Kupiga Raia

$
0
0
Jeshi la Polisi Kanda maalum limeonya mamlaka mbalimbali kuacha kujichukulia sheria mkononi kwa kupiga watu kwa sababu yoyote ile kwani kufanya hivyo ni jinai.

Hayo yalisemwa leo na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, Lazaro Mambosasa wakati akiongea na waandishi wa habari.

Agosti 31 ilisambaa video kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha mgambo wakimpiga raia kwa marungu akidaiwa  kukataa kulipa faini ya kuzoa takataka ambayo ni sh. 50,000.

Mambosasa amesema kama waliofanya kitendo hicho ni mgambo walipaswa kumkamata mhalifu na kumfikisha katika vyombo vinavyotakiwa badala ya kujichukulia sheria mkononi.

“Nchi hii inafuata misingi ya sheria kilichofanyika ni uhalifu na kimeifedhehesha nchi, hivyo kitendo kilichofanyika hakikubaliki hata kidogo,”amesema Mambosasa.

Amesema mgambo hao tayari walikamatwa na kufunguliwa mashtaka hivyo wanastahili kufikishwa mahakamani kwa kitendo walichokifanya.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Kijazi Aiagiza Bodi ya Usajili ya Wahandisi nchini (ERB) Ipitie Upya Sheria ya Manunuzi ya Mwaka 2016

$
0
0
Na. Immaculate Makilika- MAELEZO
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi ameitaka Bodi ya Usajili ya Wahandisi nchini (ERB) kuipitia upya Sheria ya manunuzi ya mwaka 2016 ili kuweza kubaini changamoto zilizopo katika sheria hiyo kuhusu fursa  za wakandarasi wazawa kushiriki kikamilifu  katika ujenzi wa miradi mikubwa ya Serikali.

Akizungumza na  waandishi wa habari leo jijini Da es salaam, wakati akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika  ufunguzi wa  Kongamano la Maadhimisho ya miaka 50 ya Bodi ya Wahandisi sambamba na Siku ya Wahandisi nchini linalofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi aliitaka Bodi ya Wahandishi (ERB)  kuhakikisha kwamba   inaisoma upya Sheria ya Manunuzi ya mwaka 2016 ili kubaini changamoto zilizopo badala ya kulalamika kuwa Serikali haiwashirikishi kikamilifu wakandarasi wazawa.

“Nawaomba ERB  mkaisome upya Sheria ya Manunuzi ya mwaka 2016, ambayo ilifanyiwa marekebisho  hasa vifungu  vya 55A, 55B, 55C na 55D ili kufahamu kwa kina jinsi sheria hiyo ilivyoainisha utaratibu wa kampuni za ndani katika miradi ya ujenzi, ili kubaini mapungufu yaliyopo na kuleta mapendekezo yatakayosaidia kuboresha zaidi badala ya kulalamika kuwa Serikali haiwashirikishi kikamilifu katika miradi ya mikubwa ya nchi”

Balozi Kijazi, alisisitiza kuwa Serikali iko tayari kupokea mapendekezo hayo na  itarekebisha sheria hiyo kulingana na maoni yatakayotolewa.

Aidha, Katibu Mkuu Kiongozi amepongeza mafanikio yaliyopatikana katika kazi za kihandisi, hasa ukilinganisha kuwa kabla ya Uhuru nchi hii ilikuwa na wahandisi wawili tu, lakini hadi sasa ERB imesajili jumla ya Wahandisi 22,226 kati yao wakiwemo wahandisi wanawake 22,235 sawa na asilimia 10.

Naye, Rais wa Shirikisho la Wakandarasi Afrika, Julius Riunga alizitaka Serikali za nchi za kiafrika kuwaunga mkono wakandarasi ili waweze kuendeleza ujenzi wa miundombinu mbalimbali kwa ajili ya kuleta maendelo kwa wananchi. Ambapo pia alisisitiza  kuwa Afrika itajengwa na wandarasi  wa kutoka Afrika.

Aidha, amewataka wakandarasi kutumia rasilimali zilizopo kwa ajili ya kutatua changamoto zilizopo katika nchi zao, ikiwa ni pamoja na kuliletea maendeleo bara la Afrika kwa ujumla.

Kwa upande wake, Balozi wa Norway nchini Tanzania Trygve Bendiksby alisema kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana na Tanzania katika  miradi mbalimbali ikiwemo  ufadhili wa mafunzo kwa wakandarasi wanawake  463 hadi sasa, kutika wakandarasi 96 waliokuwa mwaka 2010.

Balozi  Bendiksby, alisisitiza kuwa “Norway ni mshirika mzuri wa maendeleo na tutaendelea kufanya hivyo, tunaona mabadiliko makubwa na watu wanafaidika na juhudi za kupambana na rushwa zinazofanywa na Rais John Pombe Magufuli”

Aidha, katika Maadhimisho hayo ya miaka 50 ya ERB, zimefanyika shughuli mbalimbali ikiwemo kutoa tuzo kwa kutambua michango ya watu mbalimbali walioshiriki katika shughuli za kihandisi kwa kipindi cha miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Bodi hiyo.

Kati ya waliotunukiwa tuzo hizo ni pamoja na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere ambaye aliyetunukiwa tuzo maalumu iliyopokelewa na Milton Nyerere kwa niaba ya familia yake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi ambao walitunukiwa tuzo za heshima kwa michango yao ya taaluma katika sekta ya ujenzi nchini.

Kongamano hilo la Maadhimisho ya miaka 50 ya Bodi ya Wahandisi na Siku ya Wahandisi mwaka huu inaadhimishwa  kwa mara ya 16, likiwa na  mada inayosema “miaka 50 ya mchango wa wahandisi  kwenye Taifa, mafanikio, changamoto na mikakati ya baadae, ambapo kongamano hilo litarajiwa kumalizika keshokutwa, huku ikihusisha majadiliano na mada kutoka kwa watu mbalimbali.

Katika maadhimisho hayo ya siku tatu yanatarajiwa kuhudhuriwa na  viongozi mbalimbali wa Serikali, mashirika ya umma, na binafsi, na wageni kutoka nchi za Zambia, Nigeria, Ghana, Uganda, Ethiopia, Rwanda, Misri, Malawi na Kenya.

Rais Magufuli Atembelea Shule Aliyosoma Nyerere, Atoa Mili. 20

$
0
0
Leo Septemba 5, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli amefanya ziara na kutembelea shule ya msingi Mwisenge aliyosoma Hayati Mwalimu Julias Kambarage Nyerere na kuwaahidi kuwapatia kiasi cha fedha Milioni 2o ndani ya wiki mbili na kutaka fedha hizo zitumike kukarabati shule hiyo.

Mbali na ahadi hiyo Rais Magufuli ametoa papo kwa papo kiasi cha fedha Shilingi Milioni Moja kwa wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi pamoja na macho ili washerekee fedha hiyo na walimu wao.

Aidha Rais amewataka wanafunzi hao wasome kwa bidii kwani Serikali inawawependa na kuwajali.

Hayati Mwalimu Nyerere alisoma shule hapo elimu ya Msingi tarehe 20/4/ 1934 hadi 1/10/1936. 

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya Septemba 6

Katibu Mkuu CCM: Hakuna Dar Es Salaam Ya Makonda

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM, Dk. Bashiru Ally Katika mwendelezo wa mahojiano aliyoyafanya na Raia Mwema, amemnyooshea kidole, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa namna anavyotekeleza majukumu yake ya ukuu wa Mkoa na kudai kuwa kulikuwepo udhaifu katika kushughulikia makontena kutokana na kufanya kazi bila kushirikishana.

Alieleza kuwa, Mkuu wa Mkoa alipaswa kuwashirikisha wenzake tangu hatua za awali, kwa kuwa Serikali ni moja, hakuna cha Waziri wala Mkuu wa Mkoa – wote ni Wateule wa Rais.

Bashiru alimnyooshea kidole Makonda kwa ubinafsi na kukumbushia jinsi ambavyo Mkoa wa Dar es Salaam ni mmojawapo ya Mikoa aliyoitaja hivi karibuni kwa kutotekeleza vyema Ilani ya CCM kutokana kufanya kazi bila ushirikiano.

“Hapa sina maana kwamba ni Mkuu wa Mkoa tu hapana, ni uongozi mzima chini ya Mkuu wa Mkoa na uongozi mzima chini ya Mwenyekiti wa Chama. Rais hawezi kwenda kuwafundisha uhusiano mwema, wao wenyewe ndio wanatakiwa kujua kwamba uhusiano mwema kikazi unamjenga zaidi kiongozi yeyote…”

Vilevile, Katibu Mkuu alimuonya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam juu ya tabia yake ya kuwaita wakazi wa Dar es Salaam, wananchi (Mkoa) wangu. “Na hii habari ya Dar es Salaam ya Makonda, hakuna Dar es Salaam ya Makonda, ni Dar es Salaam chini ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Makonda.”

Bashiru aliongezea kuwa: “Kuna wakati namsikia anasema wananchi wangu, nani kamwambia anao wananchi wake? Hakuna wananchi wako. Hakuna kiongozi anamiliki wananchi, ni wananchi wenzangu.”

Aidha, Dk. Bashiru alikumbushia jinsi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alivyowahi kuonya juu ya ubinafsi: …. mkianza kusema mimi – wewe au wao – sisi, hamfiki.

Hivyo, aliwaasa vijana wanaopewa uongozi wawe wanyenyekevu na kuacha papara kwani watapotea kama ambavyo vijana wengi waliowahi kuwa juu walipotea kwa kukosa unyenyekevu.

BREAKING: Rais Magufuli Kateua Mkurugenzi Mpya wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Kamishna wa Polisi Diwani Athumani kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Uteuzi wa Kamishna Diwani Athumani unaanza leo tarehe 06 Septemba, 2018. Kabla ya uteuzi huo Kamishna Diwani Athumani alikuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera.

Kamishna Diwani Athumani anachukua nafasi ya Kamishna wa Polisi Valentino Mlowola ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.

Kuwa Wakwanza Kupokea Habari Zetu....Download App Yetu Kwa Kubonyeza Hapa, Huhitaji tena kuwa na Computer

$
0
0
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa urahisi kabisa kupitia simu yako ya mkononi muda wowote hata usiku wa manane au ukiwa kazini...

Pata kurasa za mbele Magazetini, habari za kitaifa, matukio yote ya kisiasa, burudani na udaku   kupitia simu yako ya mkononi.

Huhitaji tena kuwa na Computer. Ingia Play Store, pakua App yetu  tukuhabarishe masaa 24.

VIDEO: Mkuu wa Wilaya Jerry Murro Akimfokea Hadharan Mkurugenzi wake...."Huu ni UPUUZI, Sitauvumilia"

$
0
0
Uvumilivu ulimshinda Mkuu wa Wilaya Jerry Muro na kujikuta akimfokea hadharani Mkurugenzi kwa kuchelewa kwa dakika 10 katika ziara iliyowahusisha viongozi wote akiwemo mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo

"...Dakika 10 nzima tunakusubiri kwenye msafara, huu ni UPUUZI na sitauvumilia, usicheke mkurugenzi, usinidharau" -Ni baadhi ya Maneno ya DC Jerry Muro

==>>Msikilize hapo chini

Waziri Mkuu Ampongeza Rais Wa China.....Ni kutokana na mikakati aliyoitangaza ya kuendeleza Afrika

$
0
0
WAZIRI MKUUKassim Majaliwa amempongeza Rais wa China Xi Jinping kwa mikakati mbalimbali kuimarisha ushirikiano na nchi za Afrika aliyotangaza kwenye Mkutano wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC).

Waziri Mkuu ameyasema hayo jana  (Jumatano, Serptemba 05, 2018) alipokutana na Meya wa Manispaa ya Shenzhen na Katibu wa Chama cha Kikomunisti cha China wa Jimbo hilo Wang Wanzhong  katika hoteli ya Wu Zehou  iliyoko  Shenzhen.

Alisema anampongeza Rais Xi kwa kutangaza mkakati wa kuimarisha ushirkiano na nchi za Afrika kwa sababu Tanzania nayo itaendelea kunufaika zaidi kupitia mipango na mikakati hiyo.

Waziri Mkuu liesema licha ya asilimia 70 ya Watanzania kutegemea kilimo katika kuendeshaji wa maisha yao, Serikali imeamua kuboresha uchumi wa nchi kupitia  sekta ya viwanda  hususani vya kuchakata mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi. Hivyo, inahitaji washirika wengi kwa ajili ya kubadilishana uzoefu.

“Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imeamua kuboresha uchumi kupitia viwanda. Mkakati wa kuwekeza katika viwanda unatoa fursa kwa Watanzania na watu kutoka nje ya nchi ikiwemo China kuja kuwekeza.”

Kadhalika, Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wakezaji kutoka Manispaa ya Shenzhen  waje wawekeze kwenye maeneo mbalimbali nchini kama uchimbaji na uchakataji wa madini hususani ya Tanzaniteili kuiwezesha nchi kunufaika na madini hayo yanayopatikana  Tanzania tu.

Waziri Mkuu alisema anaamini kuwa miji mbalimbali Tanzania inaweza kufikia maendeleo ya viwanda yaliyofikiwa na mji wa Shenzhen katika  kipindi cha miaka 38 tangu kuanzishwa kwa mji huo kama eneo la kwanza la kiuchumi.

“Nawakaribisha wawekeze kwenye sekta ya teknolijia ya habari na mawasiliano nao waje nchini kama ilivyofanya kampuni ya HUAWEI ya Shenzhen  ambayo inafanya kazi nzuri na kutoa mchango mkubwa kwa sekta hiyo nchini kwetu.”

Kwa upande wake, Meya wa Manispaa hiyo, Bw. Wang  amemshukuru Waziri Mkuu kwa kutenga muda wake na kutembelea Shezhen na kwamba  Shenzhen itaitikia wito wa Rais Xi  wa kushirikiana na Tanzania kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo sekta ya uchakataji mazao ya kilimo.

Kuhusu uwekezaji wa viwanda, kiongozi huyo aliahidi kuwasiliana na EPZA kuona namna bora ya kushirikiana na Tanzania . Aidha aliahidi kutuma ujumbe nchini kutoka Shirikisho la Wasanifu na Watengenezaji Vito vya Madini waje waangalie namna ya kushirikiana na Tanzania hususani katika madini ya Tanzanite.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu ametembelea Kampuni ya Huawei Technologies, Kituo cha Sanaa na Makumbusho cha Sea World na Kampuni ya China Merchant ambayo ina mpango wa kuwekeza kwenye mradi wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo na eneo la viwanda.

Makanga 3 Power; Dawa Bora Nguvu Za Kiume

$
0
0
Kutibu nguvu za kiume dakika(10) na kupona muda wa siku tatu tuu. Kuimarisha misuli ya uume uliolegea, pia ipo Dawa ya kurefusha uume mfupi inchi NNE hadi saba na kunenepesha uume mfupi sentimita NNE.

Tiba ya kudumu kutibu maumivu ya mgongo,kiuno, tumbo kuunguruma na kujaa gesi, kupata choo vizuri, na kutibu uzazi, kutibu busha bila operesheni, kisukari, presha ,miguu kuuma, uzazi, fangas sugu, vidonda vya tumbo.

Ni docta bingwa wa kutibu magonjwa sugu, kutoa ndagu za utajiri kwa kutumia Pete, kazi ,cheni, mikufu maalumu ya bahati, una kesi umedhulumiwa Mali au pesa? Zitarudi muda wa Masaa matatu tuu.

Onana na Dr shilindes shida zako zote zitakwisha, anatoa Dawa za utajiri kwa wafanyakazi, wakulima, na wafugaji, wafanyabiashara na wachimba madini kwa kutumia pete, kazi kwa yeyote anaetaka kuwa na pesa nyingi.

Pia anaboresha akili kwa wanafunzi darasani, masomo na kufaulu mitihani pia kushinda bahati nasibu yeyote.

Pia tunatoa Dawa kumrudisha Mume, mke, mpenzi, hawara, kwa muda wa SAA moja tuu, na kuomba msamaha kwa kukupigia magoti na yeyote yule, unaemtaka kimapenzi au kuoana, utampata na kumfunga asitoke nje ya ndoa daima na kutekeleza shida zako zote. Kupunguza unene, kupunguza matiti makubwa, tumbo na nyama uzembe muda wa siku sita unapata saizi uipendayo.

Kutoa makovu mwilini, chunusi, upele na mabaka, pia tunayo Dawa ya kuongeza hipsi, makalio, mguu wa bia na kupata shepu safi kwa muda wa siku saba tuu.

Wa mikoani mtapata huduma popote mlipo.
Tupo dar es salam mbagala rangi tatu.

Mawasiliano simu namba: 0784 460 348. Au 0659 103 360.

Waziri wa Afya: Dawa za minyoo, kichocho kwa wanafunzi ni salama

$
0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema dawa za kingatiba ya kichocho na minyoo ya tumbo zilizotolewa kwa watoto wa miaka 5 hadi 14 ni salama. 

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Waziri Ummy alisema kumekuwa na upotoshwaji kuwa dawa hizo zina madhara.

Alisema upotoshaji huo una lengo la kufifisha juhudi za serikali katika kumkinga mtoto wa kitanzania na magonjwa yasiyopewa kipaumbele. 

“Kingatiba ya kichocho na minyoo iliyokuwa inatolewa kwa watoto haina madhara yoyote na ni salama na imetolewa kwa watoto katika halmashauri zote na Mkoa wa Dar es Salaam ndio ulikuwa wa mwisho kutoka dawa hizo kwa mwaka huu,” alisema. 

Aliongeza; “ Hizi ni dawa hata kwenye vituo vya afya mtoto akikutwa na magonjwa haya anaandikiwa na kupewa, na si huduma ngeni kutolewa mashuleni, tulianza mwaka 20 0 5 kwenye mikoa ambayo watoto walikuwa wameathirika zaidi na mwaka 2015 serikali ikaamua kutoa kwa halmashauri zote 184.

“Taarifa za upotoshaji zinazosambazwa kwenye mitandano ya kijamii hazina ukweli wowote, dawa hizi ni salama, na Serikali kabla ya kuanza kutoa kingatiba kama hizi dawa zinathibitishwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na Shirika la Afya la Dunia (WHO)” alisema. 

Hata hivyo, Ummy alisema wamebaini kuwapo kwa baadhi ya changamoto katika utekelezaji wa utoaji huo wa dawa ikiwa ni baadhi ya shule kutoa dawa bila kuwataarifu wazazi na pia watoto kupewa dawa bila kula.

“Ni kweli kuna baadhi ya shule hawakutoa taarifa kwa wazazi, na shule zingine zimetoa dawa kwa watoto wakiwa hawajala jambo ambalo limewafanya kupata madhira yasiyo na madhara kama ya kutapika, lakini hili linaisha pale mtoto anapopewa maji,” alisema na kuongeza kuwa changamoto hizi wataziondoa wakati wa utekelezaji wa hapo baadaye.

 Alisema utaratibu wa utoaji wa dawa hizo, unaendana na uzito wa mtoto na anatakiwa kumeza masaa mawili baada ya kula. 

Mwalimu alisema lengo la serikali ni kuhakikisha magonjwa ya minyoo na kichocho, ambayo yanawakumba watoto, yanapungua hadi kufikia angalau asilimia 1 au kuyatokomeza.

 “Mwaka 2005 magonjwa ya kichocho na minyoo kwa watoto ilikuwa ni asilimia 84 na baada ya kuanza kwa programu ya kutoa kingatiba imepungua hadi kufikia asilimia 30 ,” alisema.

Mwanafunzi Ajinyonga Baada ya Kutuhumiwa Kumpa Mimba Mwanafunzi Mwenzake

$
0
0
Mwanafunzi  wa Kidato cha nne, Emmanuel Tarimo (18) wa Shule ya Sekondari Rau iliyopo  wilayani Moshi, mkoani Kilimanjaro amejinyonga hadi kufa baada ya kulazishimishwa na mwalimu wake kukiri kumpa ujauzito wanafunzi wa kidato cha kwanza ujauzito.

Mwanafunzi huyo inadaiwa kabla ya kujinyonga alihojiwa na timu ya walimu wa shule hiyo kwa zaidi ya saa 12 huku wakimtaka akiri kwamba alimpa mimba mwanafunzi mwezake.

Inadaiwa mwanafunzi huyo kabla ya kifo chache aliwekwa kikaangoni na walimu wake waliomshikiniza kukiri kutenda kosa hilo lakini baadaye ilibainika msichana aliyedaiwa kuwa na mimba hakuwa nayo.

Dada wa marehemu, Tedy Maro alisema ni jambo lisiloingia akilini mdogo wake kuchukua uamuzi mgumu wa kujinyonga kama asingetishiwa maisha na walimu.

“Ndugu yetu alipewa vitisho na walimu ndiyo maana alichukua hatua ya kujiua, tunaomba serikali ichunguze hili tukio kwa sababu limetupa fedheha kubwa sana familia.

“Hata kama alifanya kosa ilitakiwa wazazi wapewe taarifa ili watafute namna ya kulishughulikia tatizo hilo,” alisema Maro.

Babu wa Mwanafunzi huyo, Jerome Maro aliiomba serikali ifuatilie madai ya vitisho vilivyotolewa na walimu.

Akijibu tuhuma hizo, Mkuu wa shule hiyo, Nyoni Njinjinji alikiri kuhojiwa kwa wanafunzi huyo baada ya kudaiwa kujihusisha kimapenzi  na mwanafunzi mwenzake wa kidato cha kwanza.

“Marehemu alidaiwa kujihusisha kimapenzi na mwanafunzi wa kidato cha kwanza na baada ya tuhuma hizo walihojiwa na walimu wa nidhamu,” alisema Njinjinji.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Hamis Issah alithibitisha kutokea kwa kifo cha mwanafunzi huyo kwa maelezo kuwa alijinyonga akiwa sebuleni kwao kwa kutumia mkanda wa suruali yake.

Kamanda Issah alisema tukio hilo limetokea Septemba 4, mwaka huu majira ya saa tano usiku baada ya mwanafunzi huyo kukutwa akiwa amejiningiza nyumbani kwao akiwa amekwishakufa.

“Baada ya kufuatilia walibaini kwamba kijana huyo siku tatu kabla ya kifo chake alituhumiwa kujihusisha kimapenzi na wasichana zaidi ya mmoja na kwamba kitendo hicho cha kuitwa na walimu na kumhoji kilimfedhehesha, mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro, Mawenzi,” alisema.

VIDEO: Bei ya Petroli na Dizeli zashuka kwa baadhi ya mikoa, ufafanuzi watolewa

$
0
0
Mamlaka ya udhibiti wa huduma za maji na nishati (EWURA) imetangaza kushuka kwa bei ya mafuta katika baadhi ya mikoa huku mikoa mingine bei ikisalia kuwa juu. 

Kwanini hali iko hivyo?...Sikiliza hapo chini

Serikali Yakanusha....Yasema Hakuna Tishio Lolote la Sunami Katika Bahari ya Hindi

$
0
0
Serikali kupitia Idara ya Maafa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu imesema hakuna tishio lolote la Sunami katika Bahari ya Hindi.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jioni Septemba 5,2018, Mkurugenzi wa idara hiyo, Kanali Jimmy Said alisema, Taarifa ya Sunami inayosambaa mitandaoni si ya kweli.

Alisema walikuwa wanafanya mazoezi ya utayari kwa magari ya zimamoto na watu wa hatua mbalimbali wakichukua.

“Taarifa za Sunami zinapotolewa wananchi hawachukulii uzito hivyo leo tulikuwa tunaangalia kama wananchi watalichukuliaje hili jambo,” alisema Kanali Said.

Alisema wamejipima mambo mengi na kwamba kama kungekuwa na tishio hilo kituo cha mawasiliano na dharura kilichopo chini ya Waziri Mkuu idara ya maafa ndiyo inaratibu kutoa taarifa ya Sunami.

Mama Amchoma Moto Mwanae Akimtuhumu Kuiba Laki 2

$
0
0
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni Muliro Jumanne Muliro amethibitisha kukamatwa kwa mwanamke anayetuhumiwa kumuunguza mtoto wake wa kumzaa kwa mafuta ya taa kwa madai ya kuiba kiasi cha shilingi laki mbili zilizokuwa zimehifadhiwa ndani.

 Kamanda Muliro amesema mtoto aliyefanyiwa ukatili huo ni wa kike ambaye anasoma kidato cha kwanza shule ya Sekondari Magomeni na alifanyiwa hivyo usiku wa kuamkia Septemba 1, 2018 maeneo ya Boko Magereza.

''Hili ni kosa la jinai na alikusudia huwezi kusema ni bahati mbaya wakati mtu amenunua mafuta na amefanya maandalizi kabisa, kwahiyo sisi kama chombo cha dola kazi yetu ni kuhakikisha tunamfikisha katika mkono wa sheria kwa ukatili aliomfanyia mtoto wake mwenyewe'', amesema.

Kamanda Muliro ameweka wazi kuwa mtuhumiwa atafikishwa mahakamani muda wowote kuanzia sasa kwakua taratibu za kipolisi zimekamilika.

Kalulumila:Dawa Bora ya Nguvu za Kiume na Maumbile Madogo

$
0
0
 BORA YA NGUVU ZA KIUME NA MAUMBILE MADOGO KALULUMILA.
----------------------------------------
Ni dawa pekee iliyojipatia umaarufu nchini na nje ya nchi kwa kufanya kazi mara 3, kwa wakati mmoja 1, kurefusha uume na kunenepesha saizi uipendayo kuongeza nguvu za kiume na inatibu matatizo na gerentii miaka 30. Na kuendelea haina madhara, inaimarisha mishipa ya uume iliyoregea na udhalishaji wa mbegu za kiume. 


---------NINI HUCHANGIA MATATIZO HAYA--Ngiri ni chanzo kikubwa cha matatizo haya ili kujua kwamba una ngiri ni chanzo kikubwa cha matatizo haya, ili kujua kama unangiri dalili zake ni kufika haraka kileleni wakati wa tendo la ndoa, 2)kushindwa kurudia tendo la ndoa. 3)kutoa choo kama cha mbuzi. 4)tumbo kujaa gesi na kuunguruma. 5)kukosa choo kabisa. 6)maumbile kuingia ndani na kuwa mafupi. 7) korodani moja kuvimba 8)kutosikia hamu ya tendo la ndoa na maumivu ya kiuno wakati wa tendo la ndoa. 9)maumivu ya kiuno na mgongo pia tunatibu kisukari kwa siku7, presha, busha, bila kupasuliwa na magonjwa mbalimbali. 

---------------------------------------
TUPO TEGETA KWA NDEVU KARIBU NA MACHINJIO YA NGOMBE UTAONA OFSI IMEANDIKWA KALULUMILA HERBALIST CLINIC HOSPITAL SIMU .
----------------------------------------
-0655-557-182.
-0755-557182.
-0784-557-182.
PIA UTAWEZA KULETEWA POPOTE ULIPO.
---------------------------------------
KARIBUNI SANA.
----------------------------------------

Gigy Money: Lazima Nitembee na Mtoto wa Zari na Ntazaa Nae

$
0
0
Msanii wa muziki Bongo, Gigy Money amefunguka na kudai kuwa ana mpango wa kuzaa na mtoto wa kwanza wa Zari The Bosslady.

Muimbaji huyo akipiga stori na SnS Tanzania (Simulizi na Sauti) amesema atafanya hivyo ili Zari aweze kumuheshimu kama mkwe wake.

"Sasa Zari, mimi ninachokuaidi kitu kimoja, lazima nizae na mtoto wako wa kwanza halafu wewe utakuwa bibi wa mwanangu ndio utaniheshimu. Atakuwa mama Mkwe wangu na hatoamini, mimi nitapita na mwanae wa kwanza na nitazaa naye," amesema Gigy Money.

Kauli ya muimbaji huyo inakuja ikiwa ni muendelezo wa beef kati ya warembo hawa, Gigy na Zari
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images