Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Mchungaji Msigwa asema kuhamia Dodoma si kipaumbele cha Taifa

$
0
0
Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema) Mchungaji Peter Msigwa amesema uamuzi wa Serikali kuhamia Dodoma haukuwa sahihi kwasababu si kipaumbele cha Taifa.

Amesema pia jambo hilo halimo katika mpango wa Taifa wa Maendeleo wa miaka mitano.

Akizungumza bungeni leo Jumanne Septemba 4, 2018 katika mjadala wa muswada wa sheria ya kulitangaza Jiji la Dodoma kwa Makao Makuu ya nchi mwaka 2018, Mchungaji Msigwa amesema kuifanya Dodoma kuwa makao makuu ni dhana nzuri lakini kuna tofauti kubwa ya kufanya jambo zuri na sahihi.

“Inaweza kuwa jambo zuri lakini lisiwe sahihi sisi kama wabunge ni wajibu wetu kusimamia kodi za serikali,” amesema.

“Kwa hiyo masuala mengi tunayoletewa na Serikali ni wajibu wetu kutafakari kwa pamoja kama Taifa kwamba hili suala tunalokwenda kulifanya is it economical.”

Amesema kuwa wengi wa wabunge wanasema Mwalimu Julius Nyerere alishawahi kusema kuhusu Dodoma kuwa makao makuu lakini ukweli ni kwamba amesema mambo mengi.

“Ameshawahi kusema kuwa chama kinachofuata kutawala baada ya CCM ni Chadema mbona na hili nalo hamlitekelezi? Hatuwezi kusema mambo yote aliyosema mwalimu Nyerere tuyatekeleze,”amesema.

Amesema Tanzania ina matatizo mengi na kuhoji kwa kupima mizani suala la kuhamia Dodoma ni kipaumbele cha Taifa na kwamba suala hilo halikuwa katika mpango wa maendeleo wa Taifa wa miaka mitano wala wa mwaka mmoja.

Serikali Yawasilisha Muswada wa Kulitangaza Jiji la Dodoma Makao Makuu ya Nchi

$
0
0
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo leo amwewasilisha Muswada wa Sheria ya Kulitangaza Jiji la Dodoma kuwa Makao Makuu ya Nchi katika mkutano wa kumi na mbili wa kikao cha kwanza cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 


Waziri Jafo amesema dhumuni la muswada huo ni kupendekeza kutungwa kwa sheria ambayo italitangaza rasmi Jiji la Dodoma kuwa makao makuu ya nchi na makao makuu ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Waziri Jafo amesem chimbuko la hoja ya kutunga sheria hiyo ni kukosekana kwa sheria inayotambua na kuweka misingi ya uendelezaji wa makao makuu ya nchi, hivyo hatua ya kulitambua jiji la Dodoma kama  makao makuu ya nchi itachochea ukuaji wa mji wa Dodoma na maeneo yanayozunguka moka wa Dodoma kiuchumi na kijamii.

“Kukosekana kwa sheria inayotambua Dodoma kuwa makao makuu ya nchi kulisababisha uendelezaji wa makao makuu ya nchi kutofikia malengo, hivyo msingi wa kutunga sheria hii ni kutambua kisheria jiji la Dodoma kuwa makao makuu ya nchi” alisema Waziri Jafo.

Akifafanua kuhusu muswada aliowasilisha mbele ya Spika Job Ndugai, waziri Jafo amesema muswada huo utakuwa na vifungu sita vikiwemo vya utangulizi, matumizi, tafsiri ya maneno yaliyotumika, kulitangaza  Jiji la Dodoma kama makao makuu ya nchi na mwisho ni kifungu ambacho kimeweka masharti ya kubadilisha makao makuu ya nchi.

Uamuzi wa kuwasilisha muswada wa kulitanganza jiji la Dodoma kuwa makao makuu ya nchi na serikali, ni mwendelezo wa hatua za kimageuzi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Pombe  Joseph  Magufuli.

TADB Yawanufaisha Wakulima 527,291

$
0
0
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO
Hadi kufikia Julai, 2018 Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) imewanufaisha jumla ya wakulima 527,291 kwa kuwapa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 48.67.

Takwimu hizo zimetolewa leo na Naibu Waziri wa Kilimo, Dkt. Mary Mwanjelwa alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Magomeni, Mhe. Jamal Kassim Ali lililohoji juu ya mikakati ya Serikali ya kuwasaidia wakulima kupitia Benki ya Maendeleo ya Kilimo.

Naibu Waziri Dkt. Mwanjelwa amesema serikali inatambua changamoto za upatikanaji wa mitaji kwa ajili ya shughuli za kilimo zinazotokana na taasisi nyingi za fedha kuweka masharti magumu hususan kwa waombaji kutoka sekta ya kilimo ndio maana Benki hiyo inajitahidi kutafuta vyanzo vipya vya mtaji ili kuimarisha uwezo wa benki kuwahudumia wakulima.

“Ili kuwaendeleza wakulima, Serikali itaendelea kuiongezea mtaji Benki ya TADB na kuhamasisha uanzishwaji na usimamizi wa Vyama vya Ushirika ili kuwezesha upatikanaji wa mikopo nafuu kwa wakulima, hadi kufikia Julai 2018 jumla ya wakulima 527,291 katika mikoa ya Iringa, Njombe, Mbeya, Songwe, Morogoro, Tanga, Manyara, Kagera, Arusha, Zanzibar na mikoa ya Kanda ya Ziwa walipatiwa mikopo,” alisema Dkt. Mwanjelwa.

Ameongeza kuwa Serikali imeweka mikakati mbalimbali ikiwemo ya kuipatia benki ya kilimo mkopo wa gharama nafuu kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika wa shilingi bilioni 103, kufadhili miradi ya ubunifu vijijini pamoja na kuratibu utoaji wa dhamana kwa mikopo itakayotolewa  na mabenki na taasisi nyingine za fedha.

Aidha, Naibu Waziri wa Kilimo amefafanua juu ya uongezaji wa matawi ya benki hiyo nchini ambapo katika Mwaka wa Fedha 2018/19, Serikali imepanga kuanzisha Ofisi sita za kanda zikiwemo za Nyanda za Juu Kusini na Kanda ya Magharibi lakini Kanda za Kusini, Kaskazini na Zanzibar zitafunguliwa baadae.

Serikali Kuendelea Kutoa Ruzuku Kwa Halmashauri Nchini

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
Serikali imesema kuwa itaendelea kupeleka fedha za ruzuku katika Halmashauri zote nchini kutokana na makusanyo halisi kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato.

Hayo yameelezwa Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alipokuwa akijibu maswali ya Mbunge wa viti maalum, Mhe. Leah Jeremiah Komanya aliyetaka kujua ni lini Serikali itaanza kupeleka fedha za ruzuku katika Halmashauri za wilaya kama zilivyopitishwa na Bunge.

Akijibu swali hilo Dkt. Kijaji alieleza kuwa kinachoidhinishwa na Bunge ni makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka husika na utekelezaji wake kwa sasa unafanyika kwa mfumo wa kutumia kile kinachopatikana ‘cash budget’.

Dkt. Kijaji alisema kuwa ruzuku kutoka Serikali Kuu hupelekwa kwenye Halmashauri za wilaya kulingana na makusanyo halisi ya mapato ya mwezi husika.

Serikali Yaelezea Mbinu Za Kukabiliana Na Umaskini

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
Serikali imeeleza kuwa inazingatia Dira ya Taifa ya Maendeleo, Ilani ya Uchaguzi ya Chama Tawala (ccm), Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano na mwaka mmoja, pamoja na Mwongozo wa Bajeti kugawa rasilimali fedha na watu katika kukabiliana na changamoto za umaskini nchini.

Hayo yameelezwa Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alipokuwa akijibu maswali ya Mbunge wa Kasulu Mjini Mhe. Daniel Nicodemus Nsanzugwanko (CCM), aliyetaka kujua mbinu za Serikali katika kuhakikisha mikoa maskini nchini inapata rasilimali fedha na watu ili iweze kuondokana na hali hiyo ya umaskini.

Dkt. Kijaji alisema kuwa mgawanyo wa rasilimali fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo huenda sambamba na mgawanyo wa rasilimali watu kwa ajili ya utekelezaji, usimamizi, uperembaji na kutoa huduma kulingana na aina ya miradi.

Aidha Mhe. Nsanzugwanko alihoji hatua zilizochukuliwa na Serikali katika Mkoa wa Kigoma ili kujenga ulinganifu katika maendeleo.

Akijibu swali hilo Dkt. Kijaji alisema Serikali imebainisha  maeneo na miradi ya kimkakati kwa ajili ya utekelezaji ili kufungua fursa za kiuchumi  mkoani huo.

Alieleza kuwa miongoni mwa maeneo ya kimkakati yaliyobainishwa na kuanza kutekelezwa kwenye Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17-2020/21 ni pamoja na mradi wa upanuzi na ujenzi wa Uwanja wa Ndege Kigoma.

“Miradi mingine ni mradi wa uzalishaji wa umeme wa maji katika maporomoko ya mto Malagarasi MW 44.7, kuanzisha na kuendeleza eneo huru la uwekezaji Kigoma, mradi wa gridi ya Kaskazini Magharibi kv400 na ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha kimataifa”, alisema Dkt. Kijaji.

Katika swali jingine, Mhe. Nswanzugwanko alitaka kujua kwa nini Serikali isitenge shilingi bilioni 5 kila mwaka kwa kila mkoa ili kuondoa tishio la mikoa hiyo kuachwa nyuma kimaendeleo.

Mhe. Dkt. Kijaji alieleza kuwa kwa sasa Serikali haina sera wala mwongozo wa kutenga shilingi bilioni 5 kila mwaka kwa kila mkoa ili kukabiliana na changamoto za umasikini.

Alifafanua kuwa hoja ya kutenga shilingi bilioni 5 kwa kila mkoa kila mwaka ni lazima ifungamanishwe na Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano na Ilani ya Uchaguzi ya Chama Tawala.

Halima Mdee: “Sijawahi kuona Bunge linapelekwa na Serikali kama hili”

$
0
0
September 4, 2018 Wabunge walikuwa wakijadili Muswada wa sheria ya kulitangaza jiji la Dodoma kuwa makao makuu ya nchi wa mwaka 2018 (The Dodoma capital city Declaration Bill 2018) ambapo miongoni mwa waliopata nafasi ya kuchangia ni pamoja na Mbunge wa Kawe Halima Mdee ambaye amekosoa taratibu zilizotumika na Serikali katika kutekeleza mapendekezo hayo.

Amesema hakuna anayepinga Dodoma kuwa jiji wala Serikali kuhamia lakini hoja ni utaratibu wa kisheria umekiukwa na pia mipango ya Taifa haijatekelezwa kama Katiba inavyotaka.

“Isije ikajengwa propaganda kwamba kuna mtu anapinga Dodoma kuwa makao makuu maana sasa hivi siasa zetu zimetoka katika hoja na kwenda katika vihoja,”amesema.

Mdee ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la wanawake wa Chadema (Bawacha) amesema Serikali imechomeka suala la makao makuu na hivyo kuhalalisha Bunge kupokonywa mamlaka yake kisheria.

“Mimi nimekuwa mbunge kwa awamu tatu, mara ya kwanza nikiwa mbunge wa viti maalum na kisha mbunge wa jimbo kwa mara mbili, sijawahi kuona Bunge linalopelekwa pelekwa kama hili,” amesema Mdee.

Amesema anasheria ya mipango miji ya mwaka 2008 ambayo inaonyesha vigezo vya jiji ni pamoja na mamlaka ya kutangazwa kwa eneo kuwa jiji ni ya Bunge.

“Sasa mtuambie ni lini Bunge hili lililetewa muswada wa sheria ambao uliinyanyua Dodoma kuwa jiji,” amesema.

Amesema Rais John Magufuli hana mamlaka ya kulitangaza Dodoma na kwamba Rais anaweza kusema lakini ni mamlaka ya Bunge kulipa uhalali ya kuwa jiji lazima itekelezwe.

Amesema alitarajia waziri kusema wanaitambua Dodoma kuwa makao makuu lakini ndani yake wamechomekea kuhusu jiji kuna vigezo kadhaa vimefikiwa.

Amesema ni wajibu wa Spika Job Ndugai kulinda heshima na hadhi ya Bunge hilo.

Akijibu hoja hiyo Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk Adelardus Kilangi amesema wabunge wengi waliosema kuwa Rais alikosea kulitangaza Dodoma kuwa jiji walitumia Sheria ya Mipango Miji.

Amesema si sahihi kutumia sheria hiyo na kwamba sheria hiyo ilikusudiwa kwa ajili ya kuweka mipango mizuri ya matumizi ya ardhi katika maeneo ya mijini.

Amesema sheria sahihi ambayo Rais Magufuli aliitumia ni Sheria ya Mamlaka ya Serikali za Mitaa ambayo inasema mamlaka ya kutangaza jiji yako kwa Rais.



Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya Septemba 5

Instagram Kumechafuka....Tazama hapa Diamond Akijibu Tuhuma za Kutaka Kulogwa na Hamissa Mobetto

$
0
0
Msanii Diamond Platnumz amejibu kuhusu voice note inayosambaa mtandaoni ambayo inadaiwa kuwa ni ya Hamisa Mobetto akipanga njama za kumloga muimbaji huyo pamoja na mama yake mzazi.

Sasa Diamond amesema kuwa anauhakika sauti hiyo ni ya Hamisa na kueleza kushangazwa kwake na kitendo hicho.

“Unapotaka kwenda kwa mganga uniroge mimi na mama yangu, unaonekana wewe haushindwi hata kumuua mama yangu, kama unawaza sijui nikupe nyumba. Voice notes zinasambaa sambaa hata mimi nilitumiwa, ninazo unasikia kitu halafu unajua huyu ni yeye, halafu nikamwambia huyu ni wewe,” alisema Diamond kupitia Refresh ya Wasafi TV.

Aliongeza,”Watu kuna vitu wanaongea ongea halafu wanajaribu kuvipindisha aonekane Mama yangu na dada yangu wana matatizo, mama yangu na dada yangu hawawezi kuwa na matatizo. Halafu hao watu wako unaowatuma wakatukane nimeshakuona ukiwatuma wakatukane kwa watu wengine kwa sababu pia uliwatuma pia wamtukane na Zamaradi,”

Wiki hii dada wa Diamond Platnumz, Esma aliandika ujumbe mrefu kukanusha taarifa ambazo zilikuwa zinasambaa kwenye mitandao kwamba wameandaa voice note kwaajili ya kumchafua Hamisa Mobetto.

==>>Msikilize Diamond Hapo chini Akitema Cheche

==>.Cheki na hii

Rais Magufuli Akutana na Kufanya Mazungumzo na Spika mstaafu wa Bunge la Tanzania Pius Msekwa

$
0
0
Rais Magufuli asubuhi hii ya Septemba 5, 2018 amekutana na Spika mstaafu wa Bunge la Tanzania Pius Msekwa na mkewe Mama Anna Abdallah Ikulu ndogo mjini Nansio katika kisiwa cha Ukerewe Mkoani Mwanza na wamezungumza mengi ikiwemo Msekwa kupongeza jitihada za Rais Magufuli

Waziri Lugola Atembelea Eneo La Ajali Ya Magari Manne Yaliyogongana Yakiwa Katika Msafara Kuelekea Mkutano Wa Rais Magufuli,

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akiliangalia gari la CCM Mkoa wa Mwanza lenye namba ya usajili T223 CHN Toyota Land Cruiser, lililopata ajali Kijiji cha Kasuguti Jimbo la Mwibara, wilayani Bunda Mkoa wa Mara, leo. Magari manne likiwemo moja walilopanda waandishi wa habari, yalikua katika msafara yakielekea katika Mkutano wa Rais Dkt John Pombe Magufuli, wa uzinduzi wa barabara ya kiwacho cha lami katika Kijiji cha Kisorya, wilayani humo.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akizungumza na baadhi ya majeruhi wa ajali iliyojumuisha magari manne yaliyokuwa yanaenda katika Mkutano wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kwa ajili ya uzinduzi wa barabara ya kiwacho cha lami katika Kijiji cha Kisorya, Jimbo la Mwibara, wilayani Bunda, Mkoa wa Mara.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli (wapili kulia), akimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto) alipokua anampongeza kwa kuja jimboni kwake Mwibara, pamoja na kumpa changamoto wanazokabiliwa nazo jimboni humo, Wilaya ya Bunda, Mkoani wa Mara, jana. Rais Magufuli alizindua barabara yenye kiwango cha lami inayojengwa kutoka Kisorya mpaka Mramba katika jimbo hilo.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli (wapili kushoto), akikata utepe kuashiria barabara ya kiwango cha lami iliyoanza kujengwa kutoka Kijiji cha Kisorya mpaka Mramba yenye kilomita 51kuzinduliwa. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola akishuhudia tukio hilo lililofanyika katika Kijiji cha Kisorya, Wilaya ya Bunda, Mkoani wa Mara, jana. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Serikali Yasema Hakuna Madini Yoyote Yaliyogunduliwa Ruangwa

$
0
0
Serikali imesema hakuna uthibitisho wa uwepo wa madini aina ya Coltan yaliyogunduliwa katika wilaya za Ruangwa, Masasi na Newala.

Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amesema hayo bungeni leo Jumatano Septemba 5, wakati akijibu swali la Mbunge wa Newala Vijijini, utaratibu uliotumika katika kuweka alama za mpaka katika wilaya nyingine.

“Madini aina ya Coltan, yamegunduliwa katika wilaya za Masasi, Newala na Ruangwa, lakini serikali imeweka alama za mpaka katika kijiji cha Namndimba Kata ya Chilangala, je serikali haioni kupora rasilimali ya wilaya nyingine kunaweza kusababisha mgogoro, ni lini serikali itamaliza mgogoro huu?” amehoji mbunge huyo.

Akijibu swali hilo, Nyongo amesema madini yaliyogunduliwa katika wilaya hizo ni ya Graphite ambapo baadhi ya kampuni zimepewa leseni za utafiti na uchimbaji wa madini hayo.
“Kwa mujibu wa Sheria ya Madini ya Mwaka 2010 na marekebisho yake ya mwaka 2017 na kanuni zake, mmiliki wa leseni anatakiwa kuweka alama zinazoonyesha mipaka ya leseni yake ili jamii inayozunguka maeneo hayo ijue mwisho wa leseni husika.

“Lakini pia alama za Kijiji cha Namdimba, ziliwekwa na Kampuni ya Nachi Resources Limited wakati wa ukusanyaji wa taarifa muhimu, hata hivyo, serikali haina mpango wa kupora rasilimali za wilaya nyingine bali lengo lake ni kuhakikisha rasilimali za madini zinazopatikana katika eneo husika zinawanufaisha wananchi kwa ujumla,” amesema.

Kalulumila:Dawa Bora ya Nguvu za Kiume na Maumbile Madogo

$
0
0
 BORA YA NGUVU ZA KIUME NA MAUMBILE MADOGO KALULUMILA.
----------------------------------------
Ni dawa pekee iliyojipatia umaarufu nchini na nje ya nchi kwa kufanya kazi mara 3, kwa wakati mmoja 1, kurefusha uume na kunenepesha saizi uipendayo kuongeza nguvu za kiume na inatibu matatizo na gerentii miaka 30. Na kuendelea haina madhara, inaimarisha mishipa ya uume iliyoregea na udhalishaji wa mbegu za kiume. 


---------NINI HUCHANGIA MATATIZO HAYA--Ngiri ni chanzo kikubwa cha matatizo haya ili kujua kwamba una ngiri ni chanzo kikubwa cha matatizo haya, ili kujua kama unangiri dalili zake ni kufika haraka kileleni wakati wa tendo la ndoa, 2)kushindwa kurudia tendo la ndoa. 3)kutoa choo kama cha mbuzi. 4)tumbo kujaa gesi na kuunguruma. 5)kukosa choo kabisa. 6)maumbile kuingia ndani na kuwa mafupi. 7) korodani moja kuvimba 8)kutosikia hamu ya tendo la ndoa na maumivu ya kiuno wakati wa tendo la ndoa. 9)maumivu ya kiuno na mgongo pia tunatibu kisukari kwa siku7, presha, busha, bila kupasuliwa na magonjwa mbalimbali. 

---------------------------------------
TUPO TEGETA KWA NDEVU KARIBU NA MACHINJIO YA NGOMBE UTAONA OFSI IMEANDIKWA KALULUMILA HERBALIST CLINIC HOSPITAL SIMU .
----------------------------------------
-0655-557-182.
-0755-557182.
-0784-557-182.
PIA UTAWEZA KULETEWA POPOTE ULIPO.
---------------------------------------
KARIBUNI SANA.
----------------------------------------

Serikali Yasema Itaanza Kuandika Sheria zote na Miswada Kwa Kiswahili

$
0
0
Serikali imesema itaanza kuandika sheria zote pamoja miswada na inayowasilishwa bungeni kwa lugha ya Kiswahili.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk. Adelardus Kilangi amesema hayo bungeni jijini Dodoma leo Jumatano Septemba 5, wakati akitoa ufafanuzi kuhusu swali la nyongeza lililoulizwa na Mbunge wa Viti Maalumu, Faida Bakari aliyetaka mahakama ziendeshe kesi na kutoa hukumu kwa lugha ya Kiswahili sanjari na miswada na sheria mbalimbali zinazowasilishwa bungeni.

“Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa Rais wetu anakienzi Kiswahili na lugha hiyo ndiyo lugha yetu rasmi, lakini miswada inayowasilishwa hapa inawasilishwa kwa Kiingereza si wote tunafahamu lughha hiyo, je serikali haion i umuhimu wa kutumia lugha hiyo,” amehoji.

Akitoa ufafanuzi wa kisheria, Dk. Kilangi amesema nafasi ipo kwamba mashtaka kama mashtaka yanaendeshwa kwa Hakimu au Jaji anaweza kuruhusu yaendelee kwa Kiswahili au Kiingereza.

“Lakini kuhusu miswada na sheria kuandikwa kwa lugha ya Kiswahili, hilo liko katika mpango wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kuanza na kutafsiri karibu sheria zote ziwe na zisomeke kwa lugha ya Kiswahili kwa sababu ndiyo lugha inayozungumzwa na kueleweka na watu wote.

“Lakini suala hili linahitaji rasilimali na tuna changamoto kidogo za rasilimali na wataalamu wa kutosha kwa sababu kuna hatari maana sheria ina lugha yake ukitafsiri tu moja kwa moja kwenda Kiswahili kuna changamoto pia ya kupoteza mantiki iliyokusudiwa.

“Kwa hiyo tuna changamoto pia ya kuwa na wataalamu wanaoweza kutufanyia kazi hii kwa usahihi walau ni kati ya mambo ambayo tumeyawekea mipango tuanze kuyafanyia kazi kwamba sheria zote ziandikwe kwa lugha ya Kiswahili,” amsema Dk. Kilangi.

Mbunge Chadema ahoji uhuru wa tume ya uchaguzi Tanzania

$
0
0
Mbunge wa Serengeti (Chadema) Chacha Marwa amesema Tume ya Uchaguzi (NEC) haiwezi kuwa huru kwa kuwa wakurugenzi ambao kimsingi ndio wasimamizi wa uchaguzi, waligombea ubunge na kushindwa, hawajawahi kujiuzulu uanachama katika vyama vyao.

Ametoa kauli hiyo jana  Jumanne Septemba 4, 2018 wakati akiuliza swali ya nyongeza bungeni.

Alisema kwa mujibu wa Katiba ofisa wa NEC hapaswi kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa.

“Lakini wakurugenzi wengi ni wanachama wa CCM, wengi waligombea ubunge. Walioshindwa wameteuliwa lakini hawajajiuzulu ubunge. Matokeo yake wananyimwa fomu ama wanajificha wakati wa kurudisha fomu, “ alisema.

Alisema walinzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) maarufu green guard wamekuwa wakiwateka wapinzani wakati wa mikutano ya kampeni, hata yeye amewahi kukumbwa na jambo hilo.

“Hivi ndio tume huru ya uchaguzi? Huku tunapoenda mnataka hadi damu imwagike?” Alihoji Marwa na kukatizwa na Spika wa Bunge Job Ndugai.

Ndugai alimueleza mbunge huyo kuwa maswali yake mawili yanatosha, anakoelekea anaweza kuzungumza kauli za kichochezi.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Antony Mavunde alisema NEC inapimwa kutokana na majukumu yake kikatiba yalivyoainishwa katika ibara ya 74 ya Katiba.

“Ibara ya 74 ya Katiba imeainisha majukumu ya tume yakiingiliwa ndio tume inakosa uhuru. Sitaki kuamini kuwa tume sio huru,”alisema.

Kuhusu kutekwa, Mavunde alisema suala la kutekwa si la NEC bali ni kosa la kijinai na kwamba anatakiwa kuripoti polisi.

Mbunge Ahoji Kiingereza Kutumika Mahakamani

$
0
0
Mbunge wa Viti Maalumu, Faida Bakari amehoji ni kwanini baadhi ya mahakama nchini zinaendesha kesi zake kwa lugha ya kiingereza wakati wa mijadala yake na kutoa hukumu.

Akiuliza swali hilo bungeni jijini Dodoma leo, mbunge huyo pia amesema Kiswahili ndiyo lugha rasmi ya taifa na kinapaswa kutumika katika nyanja zote ili kukipa hadhi yake.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Mavunde amesema matumizi ya lugha katika mahakama yamewekwa kwa mujibu wa sheria, Kifungu cha 13 (1) na (2) cha Sheria ya Mahakama za Mahakimu Sura ya 11, lugha inayotumika kuendeshea kesi katika mahakama za mwanzo ni Kiswahili lakini pia lugha inayotumika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi na Mahakama ya Wilaya ni Kiswahili na Kiingereza.

“Hata hivyo, shauri linaweza kuendeshwa kwa lugha yoyote kwa maelekezo ya Hakimu anayeendesha kesi katika mahakama hizo japokuwa kumbukumbu za shauri na maamuzi zinapaswa kuandikwa katika lugha ya Kiingereza.

“Aidha, kuendelea kutumika kwa Kiswahili katika mahakama zetu na hukumu kuandikwa kwa lugha ya Kiingereza kunatokana na kwamba Tanzania ni Mwanachama wa Jumuiya ya Madola na inafuata mfumo wa ‘Common Law’,” amesema.

Waziri, Mbunge CHADEMA Wavutana Bungeni

$
0
0
Mbunge wa Ndanda, Cecil Mwambe (Chadema),  jana alilazimika kufuta kauli yake ya kwamba watumishi wa serikali waliohamishiwa Dodoma, hawajalipwa stahili zao.

Mwambe alikuwa akichangia mjadala wa Muswada wa Sheria ya Kulitangaza Jiji la Dodoma kuwa Makao Makuu ya Nchi ya mwaka 2018 jana Septemba 4, bungeni uliowasilishwa na Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo.

Akiendelea kuchangia mjadala huo, Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera, Uratibu, Ajira, Kazi na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama alisimama kumpa taarifa mbunge huyo ambapo alisema anazo taarifa za uhakika zenye uthibitisho kuwa wote wameshalipwa stahili zao kwa kuhamia Dodoma.

“Mheshjimiwa Mwenyekiti, naomba kumpa taarifa mbunge kuwa taarifa anazochukua huko anakopata si za kweli wote wameshalipwa,” alisema Jenista.

Hata hivyo, Mwambe baada ya kupewa nafasi ya kuzungumza tena alisema hapokei hiyo taarifa kwa sababu watu hao wanakutana nao mitaani na wanasema hayo.

Majibu hayo yalimuibua tena Waziri Jenista, ambaye alisema kwa kutumia Kanuni ya 64 (1), Kanuni ndogo b, mbunge hatatoa taarifa ambazo hazina ukweli.

“Mwenyekiti ninasoma pamoja na kanuni ya 63, ambayo inataka nitoe uthibitisho wa jambo ninalosema, mimi kama waziri ninao ushahidi wa kuhamia Dodoma kwa awamu zote nne watumishi wamelipwa, namuomba mbunge ama atoe uthibitisho au afute kauli yake,” alisema.

Hatua hiyo ilimfanya Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge kusimama na kusema; “Mambo mengine huwa tunayakuza tu, waziri amelithibitishia bunge yeye ni kweli lazima atoe ukweli ambao yanalifanya bunge liamini, mimi ningelikuwa wewe ningeenda moja kwa moja kwamba watumishi wamelipwa stahiki zao, hiyo ndiyo njia nzuri ya kwenda mbele.”

Akijibu taarifa hiyo, Mwambe alisema: “nimefundishwa kusema ndiyo na hapana lakini anayetakiwa kuthibitisha ni yule ambaye anasema mimi nimesema uongo.”

Baada ya kauli hiyo, Chenge alisema; “nimejieleza nilikuwa namuongoza waziri atufikishe kwenye kanuni ya 63, si kwamba ajielezee, hatua inayofuata tutaangalia uthibitisho wa wafanyakazi waliokuja Dodoma, sasa tuambie unafuta kauli au utaleta uthibitisho?” alihoji Chenge.

Hata hivyo, Mwambe alisema anafuta kauli na kuongeza kuwa ukweli huu utaendelea kuishi.

Rais Magufuli Alivyompigia Simu Waziri Lukuvi Live na Kuagiza Kamishina wa Kanda Asimamishwe Kazi LEO

$
0
0
Tazama hapo chini Rais  Alivyompigia Simu Waziri Lukuvi Live  na kumtaka amsimamishe kazi Kamishina wa Ardhi

Wabunge walia na mishahara ya Suma JKT, wataka ipandishwe

$
0
0
Serikali imekiri kuwa mishahara wanayolipwa vijana wanaofanya kazi kampuni ya Suma JKT ni midogo na haikidhi mahitaji. 

Waziri wa Ulinzi, Dkt. Hussein Mwinyi amesema mazungumzo yanafanywa na uongozi wa kampuni hiyo ili kuboresha viwango.

==>.Sikiliza hapo chni

Baraka Da Prince Amwangukia Mange Kimambi

$
0
0
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo mwenye 'hit song' ya 'sina', Baraka The Prince amemuomba msamaha mwanadada mkosoaji wa mtandaoni, Mange Kimambi asimuhusishe katika 'vichambo' anavyovitoa, kwa madai ana hofia kuharibiwa kipaji chake.

Baraka ametoa kauli hiyo leo asubuhi kupitia ukurasa wake wa Instagram Septemba 05, 2018, baada ya kupita saa chache tokea Mange Kimambi kuuaminisha umma kuwa Wema Sepetu alishawahi kutoka kimapenzi na kijana huyo lakini suala hilo amekuwa akilificha

Mange ametoa madai hayo wakati alipokuwa anaendelea 'kuchambana' na Wema Sepetu, katika ugomvi uliozunguka mitandaoni unahusisha imani za kishirikina ambapo mrimbwende huyo anadaiwa kuwa kinara wa matukio hayo pamoja na kuongoza idadi kubwa ya kulala na wanaume waliokuwa maarufu na wasiokuwa na majina makubwa ndani na nje ya nchi.

"Kwanza niseme samahanini sana kwa kinachoendelea katika 'page' ya Mange kimambi, ningeomba nisemehe kitu kimoja na kikufike dada yangu Mange kuwa najenga 'brand' yangu katika mazingira magumu sana, natukanwa, nadharaulika, nakatishwa tamaa. Lakini 'stil' naamini katika ubora wa kile nachokifanya ndio kitanifanya niendelee kutetea nafasi hii niliyonayo", ameandika Baraka.

Pamoja na hayo, Baraka ameendelea kwa kufafanua baadhi ya mambo kuwa "nimeshatengenezewa stori nyingi mbaya ili kusudi nishuke na kupotea kabisa, basi naomba na wewe Mange usiwe miongoni mwa wanaotaka kuiporomosha 'career' yangu na kama niliwahi kukukosea sehemu yeyote tafadhali nikuombe msamaha na hilo suala lako unalotaka kupotosha jamii kuhusu mimi uachane nalo".

Aidha, Baraka amedai hajawahi kuwa na ukaribu wa kupitiliza na Wema kwani ana mheshimu kama dada yake ambaye aliyeweza kumfahamu kupitia kazi zao za sanaa huku akimsisitiza Mange aachane na yeye juu ya jambo hilo alilo muhusisha.

"Naomba sana dada yangu nisamehe kwa hilo mimi sio mtu wa hizo 'trend' muziki na mashabiki ndio maisha yangu 'please', kama kuna mtu amekutuma mtalaaniwa wote", amesisitiza Baraka.

Mwanadada Mange Kimambi ambaye anaishi mjini Los Angels nchini Marekani amejipatia umaarufu mkubwa kwa harakati za kukosoa watu mbalimbali bila ya kuwa na hofu juu ya jambo lolote.

Muswada wa Bodi ya Walimu Wawasilishwa Bungeni Leo

$
0
0
Serikali imewasilisha bungeni Muswada wa Sheria ya Bodi ya Kitaalamu ya Walimu Tanzania ya Mwaka 2018 itakayokuwa na majukumu mbalimbali yakiwamo ya kuweka viwango vya utaalamu wa ualimu.

Akiwasilisha muswada huo bungeni leo Jumatano Septemba 5, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amesema madhumuni ya muswada huo ni kuweka muundo wa kisheria wa usimamizi na uendeshaji wa Bodi ya Kitaalamu ya Walimu ambayo pamoja na mambo mengine itakuwa na jukumu la kuinua kiwango cha utaalamu wa ualimu kwa lengo la kuhakikisha walimu wanakuwa na viwango stahiki kitaaluma.

“Serikali inatarajia kwamba baada ya sheria hii kupita na kutekelezwa, matokeo yatakuwa kuinua hadhi ya taaluma ya ualimu na walimu kwa kusajili walimu wote kulingana na viwango vyao vya weledi na kuwapa leseni ya kufundisha katika ngazi stahiki, kulindwa kwa hadhi ya taaluma na utaalamu wa ualimu kwa kuzuia watu wasiokidhi vigezo na viwango stahiki kufanya kazi ya ualimu na mengineyo,” amesema Profesa Ndalichako.

Aidha, amesema hali ilivyo sasa kutokana na idadi kubwa ya walimu, kumekuwapo na changamoto zinazohitaji kuwa na mfumo thabiti wa usimamizi wa ubora wa walimu na taaluma ya ualimu.

“Vile vile, kwa kuzingatia Itifaki ya Soko la Pamoja la Afrika Mashariki, wananchi wa nchi wanachama wana uhuru wa kufanya kazi katika nchi za Jumuiya,” amesema.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images