Na. Dokta Mungwa Kabili……0744 000 473.
Kuna watu huwa wanaota ndoto kinyume. Ndoto za kinyume ni pale unapoota kuhusu jambo Fulani halafu unakuja kutokewa na jambo ambalo lipo kinyume na ndoto uliyo iota.
Mara nyingi huwa inakuwa mtu anaota jambo zuri lakini anakuja kutokewa na jambo baya ambalo lipo kinyume na lile alilo liona ndotoni.
Mfano unaweza ukawa umelala usiku ukaota nyumbani kwenu kuna sherehe kubwa sana dada yako au binti yako ameolewa.
Lakini baada ya siku kadhaa dada yako uliye muota ameolewa anakufa na msiba wake unahudhuriwa na watu wengi sana.
Bibi harusi wa kwenye ndoto anageuka kuwa marehemu katika uhalisia na sherehe inageuka kuwa msiba na wale watu wengi ulio waona kwenye harusi hiyo ya kwenye ndoto wanageuka kuwa waombolezaji.
NDOTO ZINAPASWA KUWAJE ?
Kikawaida kabisa katika masuala ya elimu ya nyota na ndoto anazo ota mwanadamu, kuna uhusiano mkubwa sana kati ya mambo ambayo mtu anayaona kwenye ndoto na mambo yatakayo mtokea katika maisha yake.
Na hii ni kwa sababu kabla mambo hayatokea kwanza katika ulimwengu wa nyama huwa yanatokea kwanza katika ulimwengu wa rohoni na ndoto ni masuala ya rohoni.
Nafsi ya mwanadamu imepewa upendeleo wa kuyaona katika ndoto mambo yatakayo tokea mwilini kabla hayajatokea.
KAMA NDIO HIVYO SASA KWANINI WATU HUOTA NDOTO KINYUME.
Unapoota ndoto za kinyume tafsiri yake ni kwamba kuna mtu au watu ambao wanayaona mambo unayo yaona kwenye ndoto .
Yaani mambo yote unayo yaona kwenye ndoto wao pia huyaona kama ulivyo yaona wewe.
WATU HAWA WAKISHAYAONA MAMBO MAZURI AMBAYO UMEYAOTA, WANACHO KIFANYA NI KUYANENEA AU KUYATAMKIA KINYUME.
Suala la kuyatamkia kinyume mambo uliyo yaona ndotoni hufanyika kama ibada na hufanyika kwa umakini mkubwa sana. Matokeo yake wewe uliye ota jambo zuri unatokewa na jambo ambalo lipo kinyume na kile ulicho kiota.
Kuna watu mpaka wameshafikia hatua ya kuikubali hali hii na kuiona kama haki yao. Utamsikia mtu anasema “ Aisee mimi huwa nikiota jambo zuri limetokea basi huwa linatokea jambo baya ambalo lipo kinyume na lile nililo liona kwenye ndoto”.
JE WATU WANAWEZA KUYAONA MAMBO AMBAYO MTU MWINGINE AMEYAONA KWENYE NDOTO ?
Kwa kutumia maarifa makubwa sana ya kichawi, wachawi wanaweza kuyaona mambo ambayo watu wengine huyaona katika ndoto. Wachawi wana uwezo wa kuyaona mambo hayo kabla hujayaona wewe, au katika wakati huo huo ambao unayaona wewe au baada ya kuwa umeyaona wewe.
Haya ni maarifa ambayo hata watu wanao fanya ibada sawa sawa wanaweza kuwa nayo kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu. Kama wewe ni msomi vizuri wa vitabu vya dini nadhani utakuwa umewahi kusoma kisa cha Mfalme Nebukadnezar na Daniel. Mfalme Nebukadneza aliota ndoto ya ajabu ambayo hakuweza kuikumbuka .
Mfalme alitaka apate mtu ambae atasaidia kumkubusha ndoto aliyo iota na pili kumpa tafsiri ya ndoto hiyo. Kukatisha maelezo Danieli aliweza kuonyeshwa na Mwenyezi Mungu ndoto hiyo na kupewa tafsiri yake na mwisho wa siku akamjulisha mfalme kuhusu ndoto hiyo na kumpa tafsiri yake.
Kwa mfano huo hapo utakubaliana na mimi kuwa watu wanaweza kuyaona mambo ambayo umeyaota na wanaweza kuyaona kabla hujayaona wewe, au katika wakati ule ule ambao unayaona wewe au hata baada ya kuwa umeyaona wewe kama ilivyo kuwa kwa Danieli.
MAKUNDI YA WATU AMBAO WANAWEZA KUYAONA MAMBO AMBAYO UNAYAONA NDOTONI.
Watu ambao wana weza kuyaona mambo ambayo unayaona ndotoni wapo katika makundi yafuatayo :
1. WACHAWI AMBAO WAMEIBA SIRI ZAKO
Katika makala yangu yaliyo pita nilieleza kuhusu jinsi ya kutafsiri chale za kichawi. Nikaeleza kuwa wachawi wakitaka kumchanja mtu chale huwa wanamchanja kwa kutumia kucha na sio kwa kutumia uwembe au kifaa kingine chochote.
Nikaeleza zaidi kuwa katika kutafsiri chale za kichawi huwa yanaangaliwa mambo mbalimbali na moja kati ya mambo yanayo angaliwa ni pamoja eneo katika mwili wa mwanadamu ambalo chale hizo zimechanjwa .
Nikasema kuwa wachawi wakitaka kujua siri za mtu huwa wanamchanja chale kwenye kifua. Mtu akishachanjwa chale kwenye kifua hupakwa dawa maalumu za kichawi kwa dhumuni la kuunganisha nafsi ya aliye chanjwa chale na nafsi ya alie mchanja huku lengo likiwa ni kujua siri za rohoni za mtu alie chanjwa.
Mchawi akikuchanja chale hizi basi anakuwa anaona kila kitu unacho kiona. Hapa ieleweke wazi kwamba mchawi huyu aliye kuchanja haja kuchanja chale hizo kwa lengo la kukuibia nyota yako, isipokuwa amekuchanja ili kujua siri zako . Siri ambazo zimeandikwa kwenye nyota yako. Siri za maisha ya kila mwanadamu zimeandikwa kwenye nyota yake.
Yeye nyota yako haihitaji. Anacho hitaji yeye ni kukuharibia wewe usiweze kuyapata yale ambayo unastahili kuyapata.
Wachawi wanapo ota ndoto nzuri ambayo na wewe unakuwa umeiota pia wanacho kifanya huwa ni kufanya ibada maalumu ya kichawi kwa ajili ya kuinenea kinyume ndoto hiyo.
Ibada hii hufanyika kwa usirias mkubwa sana na hufanyika kana kwamba wanaweza kupoteza uhai wao endapo hawatafanya ibada hiyo ya kunenea au kutamkia kinyume ndoto yako hiyo.
Tamko la kwanza kunenea kinyume ndoto uliyo iota hufanywa na mchawi husika mara tu baada ya kushtuka usingizini na baada ya hapo suala hilo hupelekwa kwenye vilinge vya wachawi huku agenda kuu ikiwa ni ndoto yako hiyo.
Vilinge vya wachawi huwa vinakuwa kwenye miti mikubwa mikubwa ambayo hupatikana karibu katika kila eneo. Na mara nyingi vilinge hivi huwa vinabeba majina ya maeneo kama vile Mbuyuni, Mkuyuni, Mkoroshini nakadhalika.
Wachwai wakisha nenea kinyume ndoto yako basi kitakacho tokea ni wewe kupatwa na jambo ambalo lipo kinyume na kile ulicho kiona kwenye ndoto.
2. WATU WAKO WAKARIBU AMBAO UMEUNGANISHWA NAO KWA DAMU.
Watu wako wa karibu kabisa hasa ambao umeunganishwa nao kwa damu wana uwezo wa kuyaona mambo ambayo unayaona ndotoni.
Ninaposema watu wako wa karibu nawajumuisha na mke au mume wako au mpenzi wako kwa sababu mke na mume au mtu na mpenzi wake huunganishwa kwa damu kupitia tendo la ndoa.
Hata marafiki zako wa karibu sana wanaweza pia kuyaona mambo ambayo unayaona katika ndoto.
Hii ni kwa sababu watu wanapo kuwa na ukaribu kwa muda mrefu nafsi zao hukamatana na nafsi zinapo kamatana nafsi moja inaweza kuona mambo ambayo nafsi nyingine inayaona katika ndoto.
Huu si uchawi isipokuwa ni uwezo kutoka kwa Mwenyezi Mungu mwenyewe.
Ni jambo la kawaida kabisa kwa ndugu au watu wa karibu wa mtu Fulani kuyaona katika ndoto mambo ambayo mtu huyo huyaona katika ndoto.
Sasa basi kama una umezungukwa na watu wenye wivu na mafanikio yako, halafu ikatokea bahati mbaya wameyaona mambo mazuri ambayo umeyaota ndotoni, wanaweza kwenda kwa wachawi kuyabatilisha ama kuyanenea kinyume yasitokee.
Watu wako wa karibu hawana uwezo wa kuyaona mambo unayo yaota pekee bali hata mambo ambayo unayafanya ambayo pengine sio ya kawaida.
Kwa mfano kama wewe unajihusisha na tabia ya ushoga kwa siri basi jua wazi kabisa, moja kati ya ndugu zako au watu wako wa karibu watakuwa wameisha onyeshwa katika ndoto na watakuwa wanafuatilia nyendo zako.
Au kama wewe umejiingiza kwenye chama cha wachawi, basi tambua wazi kabisa moja kati ya ndugu zako wa karibu watakuwa wamepata taarifa katika ndoto.
Au pengine labda upo mkoa wa mbali na nyumbani kwenu au nchi ya mbali halafu umepatwa na tatizo kubwa, usiwe na wasiwasi kuhusu ndugu zako kujua kuhusu matatizo yako. Amini nakwambia moja kati ya ndugu au watu wako wa karibu lazima ataonyeshwa kuhusu hali yako katika ndoto.
Au kama unajihusisha na tabia ambazo ni hatarishi katika maisha yako, basi jua pia moja kati ya ndugu au watu wako wa karibu watakuwa wameonyeshwa katika ndoto.
Ninao mfano mmoja mzuri hapa kutoka kwa mteja wangu mmoja. Anasema “ Nilitoka kwetu mkoani mwaka 2007 na kwenda kusoma chuo kwenye taasisi moja ya elimu ya juu iliyopo jijini Dar Es Salaam. Ilikuwa ndio mara yangu ya kwanza kufika Dar Es Salaam. Nilifika dar siku mbili kabla ya siku ya kuripoti chuo.
Kwa kuwa sikuwa na ndugu Dar nilifikia kwenye gesti moja ambayo hapohapo kuna bar. Nikiwa hapo nilimuona muhudumu mmoja wa kike katika bar hiyo nikamtongoza na usiku wa siku hiyo akaja kulala na mimi chumbani kwangu kwa malipo.
Kusema ukweli nilinogewa sana na penzi la mwanamke huyo. Hata nilipo anza chuo na kuanza kupewa bumu langu nilikuwa kila wiki naenda kulala na mwanamke huyo.
Kibaya zaidi mwanamke huyo nilikuwa nafanya nae mapenzi bila kutumia kondomu.
Siku moja ambayo ilikuwa ni kama mara ya kumi kulala na mwanamke huyo tangu nianzishe nae mahusiano nilienda kufanya mapenzi na mwanamke huyo bila kutumia kondomu kama ilivyo kuwa kawaida yetu.
Usiku wa siku hiyo nikiwa nimelala nilijiwa na ndoto ya ajabu sana . Mama angu mzazi ambae alikuwa Kigoma kipindi hicho alinitokea katika ndoto na kunisihi kwa unyenyekevu wa hali ya juu sana kwa maneno yafuatayo “ MWANANGU UWE UNATUMIA KONDOMU” nikastuka usingizini na kuitafakari sana ndoto hiyo.
Ndoto ilinistua sana na sikuelewa maana yake ni nini. Baadae nilipata usingizi tena lakini cha ajabu sasa hata baada ya kupitiwa na usingizi nilijiwa na ndoto ile ile mama yangu mzazi akinisisitizia “ MWANANGU UWE UNATUMIA KONDOMU “
Mama alikuwa ananiambia kwa unyenyekevu mkubwa sana huku akiwa amelengwa na machozi. Ndoto hii ilinifikirisha sana . Nili tafakari vitu vingi sana na kujiuliza kwanini ndoto hii ije kipindi hiki , kipindi ambacho nipo katika mahusiano na baamedi na ninafanya nae mapenzi bila kutumia kinga ?
Katika hali ya kawaida kwa mila na desturi zetu na jinsi mama yangu alivyo kuwa mpole hajawahi kabisa kuniambia au kunishauri kuhusu masuala ya kujiepusha na ngono zembe yani hata kwa kutumia lugha ya kuzunguka.
Ndoto hiyo ilinipa tafsiri moja kwamba inawezekana kuwa hiki ninacho kifanya mama yangu anakiona kwenye ndoto na kinamuhuzunisha sana na pengine labda anamuomba Mungu awatume malaika wake waje waniambie niachane na zinaa lakini anashindwa kufanya hivyo.
Pia ndoto hii nili itafsiri kuwa pengine Yule mwanamke niliekuwa katika uhusiano nae ana maambukizi ya ukimwi au yupo mbioni kupata maambukizi hayo kwa hiyo malaika wa Mungu wananistua niachane na mwanamke huyo.
Asubuhi kulipo kucha nilimpigia simu mama yangu na kumuuliza anaendeleaje akaniambia anaendelea vizuri, ilikuwa Jumapili siku hiyo akaniuliza mwanangu umeenda kanisani leo, nikamdanganya kuwa nimeenda ili kumfurahisha ingawa kiukweli sikuwa nimeenda. Akaniambia mshikilie sana Mungu na jiepushe na vibaka kwa sababu vibaka hadi chuo kikuu wapo mwanangu kwa hiyo uwe makini sana baba. ( Kwa vibaka hapa alikuwa anamaanisha wasichana ambao hawajatulia ama w asichana mapepe )
Nilimtoa wasiwasi mama yangu kwa kumwambia mimi ninacho kifikiria ni kusoma tu na sio kitu kingine.
Nilifanya maamuzi ya kuachana kabisa na Yule mwanamke na kubadilisha laini yangu ya simu. Nikaenda kupima damu bahati nzuri nikakutwa nipo Negative nikaambiwa njoo baada ya miezi mitatu nikakutwa Negative tena.
Nilimshukuru sana Mungu na kuanza kuwa makini.
Mwaka ulio fuata yani mwaka 2008 sikurudi nyumbani likizo. Nilibaki chuo. Mwaka 2009 nilipigiwa simu kutoka nyumbani na kuambiwa dada ako amefariki.
Mara ya mwisho kuonana na dada angu huyu ilikuwa mwaka 2006 mwishoni. Afya yake haikuwa nzuri sana lakini sikuweza kuhisi chochote kwa sababu nilihisi tu labda maisha ya ndoa yamekuwa machungu kwake. Alikuwa amekonda sana. Alikuwa ameolewa toka mwaka 2004.
Nilipokuwa msibani sasa ndio nikagundua kwamba kumbe dada angu alikuwa muathirika wa ukimwi ambao alipewa na mume aliye muoa mwaka 2004.
Taarifa hizo mama yangu alizipata tangu mwaka 2006 katikati kwa sababu dada angu alibeba ujauzito ambao ulitoka kabla ya muda wake jambo lililo fanya dada angu adhoofike sana.
Jambo hili mama angu alinificha.
Katika kipindi chote cha mwaka 2007 mwanzoni hadi narudi chuo sikupata nafasi ya kuonana na dada angu kwa sababu nilivyo maliza Form Six nilipata kazi ya kufundisha kwenye shule moja ya sekondari ambayo ilikuwa katika mkoa jirani na nilio kuwa ninaishi. Tulikuwa tunawasiliana kwa simu tu.
Hata nilivyo pata nafasi ya kwenda kusoma Dar nilirudi nyumbani kumuaga mama na kuondoka Dar dada angu niliongea kwa simu tu sikupata nafasi ya kuonana nae.
Wakati nipo Dar sasa hali ya dada ikazidi kuwa mbaya mama akamtoa kwa mumewe na kumleta nyumbani ili amuuguze nyumbani.
Dada yangu huyo alichelewa kuanza kula vidonge ndio maana ugonjwa huo ulimsumbua sana.
Dada alimtesa sana mama. Ni katika kipindi hicho hicho cha mwaka 2007 mwezi wa tisa ambacho dada ailetwa nyumbani kuuguzwa ndio kipindi hicho hicho ambacho mimi nilikuwa nafanya mapenzi bila kutumia kinga na Yule na baamedi nan i katika kipindi hicho hicho ndio mama yangu alikuwa ananitokea ndotoni akiniambia nitumie kondomu.
Baada ya mazishi nilikaa na mama angu akaniambia baba dada ako ndio hivyo tena ameondoka na maradhi hayo . Jitahidi mwanangu uwe makini sana hali sasa hivi ni mbaya sana. Akaniambia ulivyo ondoka kwenda chuo niliota ndoto nakuona upo unafanya tendo la ndoa na kahaba. Ndoto hii ilikuwa inajirudia rudia sana. Nikapiga magoti na kumuomba Mwenyezi Mungu akuepushe na janga hilo. Kwa hiyo mwanangu kuwa makini, Dada ako amenitesa sana.
Hapo ndio nilipo amini kwamba kweli ukiwa unafanya jambo baya au la hatari watu wako wa karibu wanaweza kuliona katika ndoto na kumuomba Mungu aepushe lisije kukutokea.
MAZINGIRA YANAYO WEZA KUWAFANYA WATU WAKO WA KARIBU KUINENEA KINYUME NDOTO YAKO AMBAYO WAMEIONA.
Mfano mume amemuoa mke wake lakini hataki mke wake afanye shughuli wala kazi yoyote ile kwa kuhofia kwamba kazi hiyo inaweza kumfanya mwanamke huyo kupata bwana mwingine.
Mume huyu atafanya kila njia kumzuia mkewe asipate kazi. Lakini mke kwa sababu anataka kufanya kazi ili aongeze kipato cha familia nae atafanya kila ujanja ili apate kazi.
Atasoma tangazo la kazi linalo muhusu, atatuma maombi kwa siri bila kumshirikisha mumewe. Ataiwa kwenye intavyuu na ataifanya vizuri sana.
Wiki moja baadae mwanamke huyu ataota ndoto kuwa ameshinda intavyuu na ameitwa kwenye kazi. Bahati mbaya kwa mwanamke huyo , mume wake pia anaweza kuota ndoto hiyo hiyo. Atakacho kifanya mume huyu ni kwanza yeye kama yeye kuinenea ndoto kinyume kasha baada ya hapo ataenda kwa wachawi kuwaomba wa tamkie kinyume ndoto hiyo. Matokeo yake majibu ya intavyuu yanatoka dada huyu jina lake linakuwa halimo miongoni mwa walio itwa kazini.
Mfano mwingine mwanamke anawachumba wawili ambao wote hawajuani. Wote wana nia ya kumuoa na kila mmoja anapambana kuweka mambo yake sawa ili aweze kumuoa mwanamke huyo.
Mmoja kati ya wachumba hao mambo yake yanamnyookea na anafuata mwanamke huyo kumwambia sasa yupo tayari kwenda kujitambulisha.
Siku kadhaa baadae mwanamke huyo anaota ameolewa na mwanaume huyo. Bahati mbaya kwa mwanamke huyo ndoto hiyo inaonwa pia na mchumba wake mwingine ambae ataitamkia kinyume na anaweza kwenda mbali zaidi kwa kuwashirikisha wachawi.
Mwisho wa siku mchumba huyo anakuja kufunga ndoa na mwanamke mwingine.
Hizo ndio sababu kuu kwanini baadhi ya watu hutoa ndoto kinyume. Hata hivyo ni muhimu kujua masuala yafuatayo kuhusu ndoto,
KUNA WATU WAO HUWA HAWAO TAGI NDOTO NZURI, BALI HUOTA NDOTO MBAYA TU KILA SIKU. SIKU ASIPO OTA NDOTO MBAYA BASI ATAYAOTA MAMBO YA KAWAIDA KABISA AMBAYO ALIKUWA ANAYAFANYA MCHANA AU MAMBO ALIYO KUWA ANAYAWAZA.
JE HII MAANA YAKE NI NINI KITABIBU ?
Hii maana yake ni kwamba kuna watu wmeiba nyota yako ambayo ndio inaibeba nafsi yako. Watu wakiiba nyota ya mtu huwa wanachuja na kuyachukua mambo mazuri tu na mambo mabaya wanayaachia kwa mmiliki halali wa nyota hiyo.
Mambo yote mazuri ambayo ulitakiwa kuyaona kwenye ndoto unazo ota wewe wanayaona wao na yanatokea katika maisha yao na wewe unabaki na mambo mabaya pekee.
KUNA WATU HUWA WANA OTA MAMBO MAZURI HALAFU HAYATOKEI. JE HII MAANA YAKE NI NINI ?
Ukiota mambo mazuri halafu yasitokee tafsiri yake ni kama ifuatavyo :
Kwanza maana yake kuna watu wanayaona mambo hayo na badala ya kunenea kinyume basi wao wanayabatilisha tu ili usifaidike nayo. Ndio maana unaishia kuyaota tu lakini hayatokei katika maisha yako.
Tafsiri ya pili ni kwamba kuna watu wanayaona mambo yako kabla hujayaona wewe. Wanacho kifanya ni kuyachukua halafu wanakutumia kivuli cha mambo yanayo fanana na mambo yako ambayo waliyaona katika ndoto.
KOSA KUBWA LINALO FANYWA KATIKA KUTAFSIRI NDOTO.
Kuna kosa moja kubwa sana huwa linafanywa na baadhi ya watu katika kutafsiri ndoto. Kosa hilo ni KUKARIRI TAFSIRI ZA NDOTO.
Yaani kuna watu wamekariri kabisa kwamba ukiota ndoto Fulani basi ujue maana yake ni hivi. Ni makosa makubwa sana kutafsiri ndoto kwa kutumia muktadha huo.
Hii ni kwa sababu ndoto zingine hutoka kwa maadui ( wachawi na mapepo wa kisheitwani ). Maadui wakishajua umezijua mbinu zao watakacho kifanya ni kubadilisha mbinu zao. Mwisho wa siku utakuwa unaota ndoto yenye kutoa ishara Fulani halafu kitu ulicho kiona hakitokei ).
Unapo taka kutafsiri ndoto unatakiwa kuzingatia mambo mengi sana. Baadhi ya mambo hayo ni pamoja na je umeiota ndoto hiyo ukiwa katika kipindi cha maisha yako ? Ulikuwa kwenye msiba?kwenye harusi ? safarini ? ugenini ? nakadhalika nakadhalika.
Je kabla ya kuota ndoto hiyo kuna dawa yoyote ya asili ambayo ulikuwa umeitumia ? Kuna dawa yoyote ulikuwa umeichoma ? kuna dawa yoyote ulikuwa umeoga, umechanjwa au kujipaka ?
Kwa mfano kuna ndoto moja ambayo imekuwa maarufu sana katika siku za hivi karibuni nayo ni “ KUOTA UPO SHULENI AU KUOTA UPO UTOTONI “
Watu wengi huwa wanatafisiri ndoto hii kwamba muotaji mambo yake yanarudishwa nyuma na wachawi.
Unaweza kuwa sahihi ukiamini hivyo lakini unaweza usiwe sahihi kabisa ukizingatia baadhi ya mambo niliyo yataja hapo juu.
Kwa mfano kuna dawa moja ya asili. Dawa hii inatumika kutibu maradhi ya nguvu za kiume ya kichawi. Mara nyingi watu wanao tumiaga dawa hii katika siku za mwanzo huwa wanaotaga ndoto wapo shuleni wanasoma na mara nyingi huwa inakuwaga darasa sa sita, la saba au fomu wani.
Kama ukiwa umetumia dawa hiyo halafu ukaota umerudi utotoni au shuleni maana yake ni kwamba nguvu zako za kiume zilichukuliwa wakati upo katika darasa hilo ambalo umeliona katika ndoto na kwamba nguvu zako zilizo chukuliwa kichawi zimerejeshwa.
Sasa basi kwa kuwa nguvu za kiume za mwanadamu huwa zinachukuliwa kichawi kwa kuiba nafsi ama nyota yake na nyota hii hupewa mtu mwingine kwa ajili ya kuitumikisha.
Nyota hii ikirejeshwa kwako kitu cha kwanza kabisa inachokikumbuka ni mwaka na mahali ambapo iliibwa.
Kama nyota yako iliibwa wakati unasoma shule ya msingi darasa la sita, nyota yako itakapo rejeshwa kwako itarejea na mambo yako yote muhimu ambayo yaliibiwa na wachawi kuanzia kipindi nyota yako ilipoibwa hadi muda huu.
Kwa sababu hiyo sasa utaanza kuwa unayaona katika ndoto matukio ambayo ulikuwa unafanya utotoni kama vile kuwa shuleni nakadhalika.
Pia dawa nyingi zinazo tumika kusafisha nyota na kurejesha nyota iliyo ibiwa na wachawi akizitumia mwanamke ambae labda Alisha zaa , ataota ndoto amerudi utotoni, labda yupo shuleni darasa la tatu au hata la kwanza nakadhalika.
Hii maana yake ni kwamba mwanamke nyota yake imerudishwa upya. Amerejea kwenye ubikira wa rohoni. Kwa hivyo hapaswi kuwa na wasiwasi kwa kudhani kwamba wachawi wanamrudisha nyuma.
Mifano ipo mingi sana.
JE KUNA DAWA ZINAZO WEZA KUMFANYA MTU AWE ANAYAONA MAMBO YAKE KATIKA NDOTO KABLA HAYAJATOKEA ?
Ni kweli kabisa zipo dawa ambazo huwapa watu uwezo wa kuyaona mambo yao katika ndoto kabla hayajatokea.
Dawa hizo zimegawanyika katika makundi makuu mawili. Zile zinazo tumiwa na wachawi tu na zile ambazo zinaweza kutumia na watu wasio wachawi lakini pia zipo dawa ambazo zinaweza kutumiwa hata na watu ambao si wachawi lakini wanataka kuwa na uwezo wa kuwa wanayaona kabla hayajatokea mambo yanayo wahusu wao wenyewe na watu wao wa karibu.
Zipo za aina nyingi sana ila leo nitazingumzia za aina mbili, moja ya kichawi na nyingine ya kawaida.
Hii ya kichawi hutumiwa na wachawi tu na mhusika huchanjwa kwa lengo la kumpa uwezo wa kuwa anayaona mambo yake kabla hayajatokea ili aweze kuchukua hatua stahiki za kiroho.
Ndumba hii ya kichawi hutengenezwa kwa miti kadhaa ya porini, ubongo wa mnyama wa porini ambae chakula chake kikuu ni mizoga pamoja na ubongo wa ndege mmoja wa porini aitwae mbesi ambae hujulikana kwa waganga na wachawi kama mtaalamu wa kuvumbua mizoga.
Ni hivi huyu ndege anapokuwa amelala usiku porini huwa ana ota mahali mzoga ulipo. Na anapo amka asubuhi basi huwa anapaa hadi mahali palepale ulipo mzoga ambao aliuona kwenye ndoto.
Tuchukulie mkoa mzima wa Dar Es Salaam ni pori. Huyu mbesi yupo Msasani amelala. Anaweza akaota mzoga ambao upo Mbagala na asubuhi atakwenda hadi Mbagala katika sehemu ile ile ambayo aliiona katika ndoto.
Dawa hii hutumiwa na wachawi tu kuona mambo yatakayo tokea sikuza usoni. Dawa hiyo wachawi huitumia katika mambo mengine mengi sana kama vile mapenzi kumtega mtu dawa. Kwa mfano A anamtaka B na wote wanaishi jijini Dar Es Salaam. A anaishi Mbagala na B anaishi Chanika . A atachanjiwa ama kufukizwa kwa dawa hiyo halafu usiku akiwa amelala atamuona A akiwa anapita katika eneo ambalo huyu B analifahamu. Inaweza kuwa Kariakoo. Ilala, Manzese au sehemu yoyote ile. Basi kesho yake asubuhi huyu A ataenda kutega dawa mahali alipo paona ndotoni na B akishapita tu mahali hapo ataruka dawa hiyo ambayo itamvaa na kumuingia.
Wachawi huitumia pia dawa hiyo kuwadhuru watu kama vile kuwatega watu ajali au kuwatega wajawazito wasipate mimba nakadhalika.
Dawa ya pili ni dawa ambayo inaweza kutumiwa na mtu yoyote Yule hata ambae si mchawi. Hii inatokana na mti mmoja wa porini ambao kwa hapa Tanzania upo Morogoro tu. Inatumika kunywa. Mtu akichemsha na kunywa dawa hii basi wakati wa usiku akiwa amelala nafsi yake inarudi duniani na kuona na kufanya kila kitu kana kwamba hajalala.
Dawa za ndoto zipo nyingi sana, nimezielezea kwa kina sana kupitia kitabu changu. “ MAMBO TISA YANAYO UNDA NYOTA YA MWANADAMU: UHUSIANO KATI YA NYOTA YA MTU NA MAFANIKIO YAKE KATIKA MAISHA “
Toleo la pili la kitabu hiki litatoka mwezi Novemba 2018. Ndani ya kitabu hiki pia pamoja na mambo menginhe mengi utapata kujua zaidi kuhusu aina mbalimbali za ndoto .
Kufahamu kuhusu yaliyomo ndani ya kitabu hicho tembelea : http://mungwakabhili.blogspot.com/2018/06/mambo-tisa-yanayo-unda-nyota-ya.html