Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Sumaye Aipa Serikali Mambo Matatu Muhimu Kuepuka Machafuko Uchaguzi wa Marudio

$
0
0
Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye ameeleza mambo matatu muhimu ya kuzingatia wakati nchi ikielekea kwenye uchaguzi mdogo utakaofanyika Septemba 16.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jana, Sumaye alisema mambo hayo ni utawala bora, matumizi sahihi ya vyombo vya dola na kutambua umuhimu wa uchaguzi.

Alisema mambo hayo kama yasipozingatiwa katika uchaguzi huo, huenda yakaibuka machafuko.

Sumaye ambaye pia ni mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Pwani alitoa kauli hiyo wakati akieleza mwenendo wa kampeni za uchaguzi zinazoendelea jimbo la Ukonga.

Alisema uchaguzi huo unapaswa kuwa wa haki na uwazi na ushindani wa halali.

Kuhusu utawala bora, Sumaye alieleza kuwa Tume ya Taifa ua Uchaguzi (Nec) inapaswa kuwa huru kwa kuwa ndiyo mhimili kwenye uchaguzi.

Pia, Sumaye aliiomba tume hiyo kuweka ratiba mapema ya yakiwamo majina ya wapiga kura, siku saba kabla ya uchaguzi ili kuondoa usumbufu.

Alivitaka vyombo vya dola kutofuata maagizo ambayo yanalenga kupendelea upande mmoja.

Sumaye alisema jukumu la mhimili huo ni kuhakikisha kuwa uchaguzi unafanyika kwa amani bila vurugu ambazo zilijitokeza katika uchaguzi uliopita.

“Siyo kuwapiga watu au kuwakamata bila makosa, hii inasababisha chuki kwa wananchi kwa hiyo wao wahakikishe amani inakuwapo na siyo kutumika vibaya,” alisema.

Kuhusu kutambua umuhimu wa uchaguzi, Sumaye alisema hakuna jambo linaloweza kuingiza nchi katika machafuko kama uchaguzi, hivyo kuwataka wananchi waachwe wachague kiongozi wanayemtaka, si kinyume chake.

“Tunashuhudia mara kwa mara nchi nyingi duniani zinaingia kwenye machafuko kwa ajili ya uchaguzi ambao haufuati sheria, haki na usawa hivyo tunaamini amani tuliyonayo haitaingia mashakani kwa ajili ya uchaguzi tutendee haki,” alisema na kubainisha kuwa wapo tayari kupokea matokeo ya haki.

Waraka wa Hamisa Mobetto wagusa Hisia za wengi

$
0
0
Mwanamitindo Hamisa Mobetto ameelezea kile anachokabiliana nacho kwenye maisha yake kwa sasa.

Hii ni baada ya maneno kuwa mengi mtandaoni kuhusu yeye, sasa ameamua kuvunja ukimya kwa kuandika waraka mrefu kiasi. 

==>>Hapa chini tumekuwekea kile alichoandika Hamisa kupitia ukurasa wake wa Instagram;

"Pengine hufahamu alipotoka Hamisa Mobetto... Wacha nikufahamishe, nilianza kutambulika rasmi kwenye tasnia ya urembo mwaka 2010 baada ya kuibuka mshindi wa Miss XXL After School Bash. Njia ya mafanikio ilifunguka hapo na hatimae nilishiriki Miss Tanzania na Also Miss New World Tanzania Na Kua first Runner Up 2012.

"Lakini Pia Nilifanikiwa Kushriki Miss UniAfrica na kuingia Top Ten... Safari ikaendelea na kwa kuwa urembo ni kipande cha sanaa niliingia kwa pia kwenye Bongo Movie na kucheza filamu kadhaa na huku pia nikiwa Video Vixen kwa baadhi ya nyimbo za Bongo Fleva.

"Nisieleweke vibaya kwa hili, kitanda hakizai haramu... nilipata mtoto wangu wa kwanza miaka michache iliyopita na ninashukuru katika mahusiano yale nilipendwa mimi na mwanangu na kuhudumiwa kwa kila kilichohitajika baadae tena nikapata mtoto mwengine katika mahusiano mengine ambayo pia yalikuwa mazuri na huduma zote kama kawaida zilikuwepo na zinaendelea kuwepo mpaka sasa, Shukrani kwa baba wote wa watoto wangu...

"Huyo ni mimi Hamisa Mobetto, safari hiyo imenifundisha mengi sana mpaka sasa na nafikiri nimekomaa kwa kiasi fulani... Nashukuru Hamisa Mobetto imekuwa Brand kubwa mpaka kufikia kunipa 'Deals' mbalimbali zinazoendelea kuja (Alhamdullilah). Sio tu 'Deals' pekee bali hata fanbase imekuwa kubwa mno kitu ambacho ninakifurahia kwani ni Support kubwa sana ninaipata.

"Wapo walioamua kutengeneza page za Social Media mbalimbali kwa ajili ya kuonyesha support na wengine pia kutumia fursa hiyo kutengeneza ajira kupitia matangazo n.k nasemaje Yote Heri!.

"Dunia inaenda mbele na watu wanabadilika, pengine lifestyle ya zamani haikuwa nzuri na mpaka kusababisha 'mambo flani flani' kutokea katika maisha yangu lakini umri unapozidi kusonga mbele akili inatanuka na kujifunza mambo mengi kwenye maisha.

"Hamisa wa sasa sio kama yule wa zamani, nimezidi kuwa na akili yenye kupambanua mabaya na mazuri na kuchukua hatua ili kuenda na kasi ya ukuaji wa akili yangu. Namshukuru Mungu ananiongoza vyema na naona baraka anazonipatia.

"Nimeingia katika migogoro ya hapa na pale kama kutukanana na watu kwenye mitandao na yote hayo ni aidha kwa kufahamu au kutofahamu lakini kwa kuwa yamepita basi niyaache tu na niendelee na safari ya maisha nikiwa mpya kabisa. Fanbase nayo haikuniacha ilikuwa na mimi wakati wote huo kama ugomvi basi walipigana kwa ajili yangu.

"Lakini pia inawezekana niliwahi kuwakwaza watu kwa mambo yangu, nichukue fursa hii KUWAOMBA SAMAHANI na kuwaahidi kuwa haitokuja kutokea tena kwa sababu Hamisa wa sasa nimebadilika na ndio maana sitahitaji tena kuingia kwenye ugomvi wa aina yoyote na mtu yeyote yule katika maisha yangu.

"Pia niwaombe mashabiki zangu na Fanbase kwa ujumla iwe kwenye groups za whatsapp au pages za kwenye social media kutojihusisha na ugomvi au matusi na mtu yeyote atakaetaka ugomvi na mimi na badala yake nguvu kubwa iwe kwenye kuendelea kuni'support kwa nguvu kubwa. Nia yangu ni kutowaingiza wale wanaonipenda katika matatizo kwa sababu hawastahili hata kidogo kupata shida kwa sababu yangu. Ninawapenda mno Namalizia kwa kurudia tena 'Dunia inaenda mbele na watu wanabadilika'"-

Utakumbuka kuwa Hamisa Mobetto ni mama wa watoto wawili kwa sasa aliozaa na Majay pamoja na muimbaji Diamond Platnumz.

Kama Dalili Hizi Unazo Upo Kwenye Hatari Ya Kuishiwa Nguvu Za Kiume Kabisa

$
0
0
Una dalili zifuatazo?
1: Kushindwa kurudia tendo la ndoa
2: Kutojisikia hamu ya tendo la ndoa
3: Maumivu ya kiuno mgongo
4: Tumbo kuunguruma na kujaa gesi
5: Uume kusinyaa, kuingia ndani na kuwa mdogo au mfupi
6: Korodani moja kuvimba

KAMA DALILI HIZI UNAZO UPO KWENYE HATARI YA KUISHIWA NGUVU ZA KIUME KABISA

Kwa matibabu tumia OZYMIX POWER-dawa bora ya nguvu za kiume ya miti shamba ambayo haina kemikali ambayo itakuwezesha kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara tatu bila hamu kuisha.
Pia tunatoa huduma hizi:>

1.Dawa ya Kuondoa michirizi
2.Kumrudisha mwanaume aliyekuacha 
 
Tunapatikana KAWE UKWAMANI karibu na kituo cha mabasi.
KWA MAWASILIANO ZAIDI ; 0716096205 /0756726865 FIKA OFISIN AU PIGA SIMU NA UTALETEWA DAWA POPOTE ULIPO DAR ES SAALAM NA KWA MIKOANI TUNATUMA KWA NJIA YA MABASI.

TEMBELEA KATIKA BLOG YETU HAPA>>>;

Makanga 3 Power; Dawa Bora Nguvu Za Kiume

$
0
0
Kutibu nguvu za kiume dakika(10) na kupona muda wa siku tatu tuu. Kuimarisha misuli ya uume uliolegea, pia ipo Dawa ya kurefusha uume mfupi inchi NNE hadi saba na kunenepesha uume mfupi sentimita NNE.

Tiba ya kudumu kutibu maumivu ya mgongo,kiuno, tumbo kuunguruma na kujaa gesi, kupata choo vizuri, na kutibu uzazi, kutibu busha bila operesheni, kisukari, presha ,miguu kuuma, uzazi, fangas sugu, vidonda vya tumbo.

Ni docta bingwa wa kutibu magonjwa sugu, kutoa ndagu za utajiri kwa kutumia Pete, kazi ,cheni, mikufu maalumu ya bahati, una kesi umedhulumiwa Mali au pesa? Zitarudi muda wa Masaa matatu tuu.

Onana na Dr shilindes shida zako zote zitakwisha, anatoa Dawa za utajiri kwa wafanyakazi, wakulima, na wafugaji, wafanyabiashara na wachimba madini kwa kutumia pete, kazi kwa yeyote anaetaka kuwa na pesa nyingi.

Pia anaboresha akili kwa wanafunzi darasani, masomo na kufaulu mitihani pia kushinda bahati nasibu yeyote.

Pia tunatoa Dawa kumrudisha Mume, mke, mpenzi, hawara, kwa muda wa SAA moja tuu, na kuomba msamaha kwa kukupigia magoti na yeyote yule, unaemtaka kimapenzi au kuoana, utampata na kumfunga asitoke nje ya ndoa daima na kutekeleza shida zako zote. Kupunguza unene, kupunguza matiti makubwa, tumbo na nyama uzembe muda wa siku sita unapata saizi uipendayo.

Kutoa makovu mwilini, chunusi, upele na mabaka, pia tunayo Dawa ya kuongeza hipsi, makalio, mguu wa bia na kupata shepu safi kwa muda wa siku saba tuu.

Wa mikoani mtapata huduma popote mlipo.
Tupo dar es salam mbagala rangi tatu.

Mawasiliano simu namba: 0784 460 348. Au 0659 103 360.

Askofu ashambuliwa baada ya kushika titi la Msanii Mbele ya Waumini

$
0
0
Huko nchini Marekani Askofu aliyekuwa akiongoza ibada ya mazishi ya gwiji wa muziki nchini humo, Aretha Franklin amejikuta akishambuliwa mtandaoni baada ya kuonekana akishika titi la msanii Ariana Grande wakati ibada ya mazishi ikiendelea.

Picha na video zinamuonyesha Askofu Charles H Ellis wakimshika Ariana juu ya kiuno chake huku vidole vyake vikiwa vimeshikilia upande mmoja wa kifua chake.

“Sio lengo langu kumshika mwanamke matiti”, aliambia shirika la habari la AP.

Aliongeza, “Pengine nilivuka mpaka, pengine nilijihisi kuwa karibu naye sana kama rafiki. Lakini tena naomba msamaha. Muhubiri huyo balisema kuwa aliwakumbatia wasanii wote waume kwa wake wakati wa shrehe hiyo ya kumuaga malkia wa muziki wa soul.

Lakini waliohudhuria walianza kutuma picha kutoka katika ibada hiyo wakati Ariana aliposimama na kuanza kuimba wimbo wa Aretha Franklin ‘You Make Me Feel a natural Woman’

Watu wengi walihisi kwamba mkono wa Askofu Ellis ulikuwa juu zaidi ya mwili wa mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 25 alipokuwa akizungumza naye na kusema kuwa hakupendelea kushikwa hivyo

Esma akana kwamba yeye na mama yake walikuwa wanaandaa Mpango wa Kumchafua Hamissa Mobetto

$
0
0
Dada wa Diamond Platnumz, Esma Platnumz ameibuka mtandaoni kukanusha madai ya kwamba yeye na mama yake walikuwa wanafanya audition kwaajili ya kumpata mtu mwenye sauti kama ya Hamisa Mobetto.

Kwa mujibu wa shabiki huyo wa Hamisa amedai wawili hao walifanya mpango huo kwaajili ya kuandaa sauti ambayo itatumika kumchafua mrembo huyo ambaye ni mzazi mwenza na Diamond Platnumz.

Esma ameona azijibu tuhuma hizo huku akidai kwamba yeye pamoja na mama yake hawawezi fanya kitu kama hicho kwa Mobetto.

“Dada bora ukae kimya halafu unapata zambi kumshilikisha Mwenyezi Mungu ktk swala km hili kuongopa vitu mbona sie wenyewe tupo Kimya au ndio mnatapatapa embu mjitulize jamani hata MUNGU HAPENDI kwani ye ndio Muamuzi plz naomba msinitungie uongo wa kijinga jinga mlichokifanya wenyewe mnakijua na nafsi zinawasuta sipendi kuniingiza ktk uongo wa kijinga msijisafishe kutaka kuchafua watu. Huyo huyo mama mnaotaka awapende kutwa mnachamba na kumtungia uongo naombeni mkitaka kuweka uongo wenu bora mniweke mimi sio mamaangu. MLICHOFANYA MNAKIJUA
#temporarypost🙌#mfaMajiHamuishiKutapatapa,” aliandika Esma kupitia Instagram.

Aliongeza, “Katika maisha ni vema kukaa kimya pindi ukikosea na hasa ukijua wazi kuwa nimekosea ila ukijaribu kufuta au kusawazisha kosa kupitia njia za wasiogusa maisha yako ujue kosa linazaa kosa…Ungetulia maana watu wameshiba vielelezo na ushahidi 100%,”

Mwanafunzi Aliyezirai Kwa Kipigo Cha Mwalimu Atoka Hospitali

$
0
0
Mwanafunzi wa sekondari ya Kalangalala mkoani Geita, Jonathan Mkono anayedaiwa kupigwa na mwalimu wake na kulazwa hospitalini, ameruhusiwa jana mchana Septemba Mosi, 2018.

Mkono alikuwa amelazwa hospitali tangu Agosti 30 baada ya kuchapwa na kupoteza fahamu na mwalimu wa nidhamu, Lawson Lechipya kwa kosa la kukutwa bwenini wakati wa vipindi jambo lililosababisha maumivu makali mwilini.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya Mkoa wa Geita, Dk Moses Simon alisema mwanafunzi huyo ameruhusiwa baada ya afya yake kuimarika.

Alisema alifikishwa hospitalini hapo akiwana maumivu baada ya kuchapwa fimbo mgongoni na kwamba hakuna eneo ambalo amevunjika.

"Daktari aliyempokea anasema alifika hapa akiwa na maumivu na alikuwa ana alama za kuchapwa mgongoni, alihudumiwa anaendelea vyema na sasa ameruhusiwa kurejea shuleni,” alisema.

Mwanafunzi huyo hakuweza kueleza hali yake kwa sasa baada ya walimu kumchukua na kumzuia kuzungumza na waandishi wa habari.

Gari ya watalii yapata ajali mbaya Jijini Arusha

$
0
0
Gari ya watalii imepata ajali mbaya  Jijini Arusha.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha (SACP) Ramadhani Ng’anzi, amethibitisha kutokea kwa ajali ya gari  iliyohusisha Lori na gari ya kubeba watalii.

Ajali hiyo imetokea eneo la Mti mmoja Wilayani Monduli.

Kamanda Ng’anzi amesema gari aina ya Land Cruiser iliyokuwa imebeba watalii imegongana uso kwa uso na Lori la mizigo takribani Kilometa 10 kutoka njia panda ya Monduli.

”Nipo eneo la ajali hapa muda huu, tunaendelea na vipimo hapa, nitawajulisha kwa undani lakini vifo vipo ila bado hatujajua ni idadi gani”, amesema.

Taarifa za awali zinaeleza takribani watu watano wamefariki katika ajali hiyo.


Waziri Mkuu: Tanzania Inaongoza Kwa Uwekezaji Ukanda Wa Afrika Mashariki

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Tanzania inaongoza kwa kupokea uwekezaji wa kigeni  wa moja kwa moja katika Ukanda wa Afrika ya Mashariki.

“Mtiririko wa uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja nchini umeongezeka kwa zaidi ya miaka 10 iliyopita na sasa wawekezaji wameipa kipaumbele Tanzania kama kitovu cha uwekezaji barani Afrika.”

Ameyasema hayo leo (Jumapili, Septemba 02 ,2018) wakati akihutubia Kongamano la Biashara kati ya Tabnzania na China kwenye Hoteli ya  Winstin jijini Beijing nchini China.

Waziri Mkuu amesema Tanzania imethibitika kuwa ni Taifa lililodhamiria  kwa dhati  kujenga uchumi wa viwanda , pamoja na kulinda na kudumisha amani na utulivu.

Amesema ripoti ya uwekezaji duniani iliyotolewa mwaka 2018, inaonesha kuwa Tanzania  inaongoza kwa kupokea  uwekezaji  katika ukanda wa Afrika ya Mashariki na imepokea kiasi cha Dola za Marekani bilioni 1.2 mwaka 2017.

Waziri Mkuu amesema Tanzania inafanya juhudi kubwa  ili iweze kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo  mwaka 2025, hivyo imeweka mkazo  mkubwa katika  kujenga msingi imara wa viwanda.

“Ili kufanikisha hilo tumeandaa Ukanda wa Kuzalisha kwa ajili ya mauzo ya Nje na Ukanda maalum wa Kiuchumi tukilenga kutimiza  mkakakati wetu wa kukuza  uchumi wa viwanda na biashara.”

Akizungumzia kuhusu sekta ya fedha, Waziri Mkuu amesema Tanzania inawakaribisha wawekezaji  kuanzisha Taasisi za Kifedha kama vile benki kwa ajili ya kutoa mikopo midogo midogo, benki za uwekezaji, benki za kilimo na benki za biashara.

Kuhusu uwekezaji kutoka China uliosajiliwa na Kituio cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kati ya Novemba 2015 hadi Oktoba 2017,  Waziri Mkuu amesema  umefikia thamani ya Dola za Marekani bilioni 1.077 na umejikita katika meneo ya kilimo, majengo ya biashara, rasilimali watu, viwanda na utalii.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesemakuna fursa nyingi kwenye sekta ya huduma hususan katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ambayo ni miongoni mwa sekta ndogo zinazokuwa kwa haraka nchini Tanzania.

Pia kumekuwa na ukuaji na mageuzi ya haraka katika soko la TEHAMA nchini kwa miaka 10 iliyopita. “Soko la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano limekuwa kwa ongezeko la watumiaji, aina ya huduma zinazotolewa pamoja na kupanuka kwa eneo ambalo huduma hizo hutolewa.”

Waziri Mkuu ameongeza kuwa, “Tanzania kuna fursa zisizo na ukomo katika eneo hili huku kukiwa na matarajio ya kukuwa kwa soko la kikanda.”

“Maeneo ya kuwekeza ni pamoja na utoaji wa huduma za simu hususan katika maeneo ya vijijini, utoaji na uendeshaji wa huduma za mtandao pamoja na ukarabati na matengenezo ya vifaa vya mawasiliano. Tunawakaribisha wawekezaji kuwekeza katika maeneo haya.”

Amesema kwa wale ambao nia yao ni kuwekeza katika kilimo, Tanzania ina hekta milioni 44 za ardhi inayofaa kwa kilimo na takribani hekta milioni 29.4 kwa ajili ya umwagiliaji.

 “Ninawakalibisha wawekezaji kuja kuwekeza katika kilimo cha biashara kwa mazao kama miwa, mpunga, ngano, kahawa, chai na mahindi. Tuna fursa kubwa ya kuwekeza katika kilimo cha miwa na uzalishaji wa sukari.”

Madiwani Wengine Wawili CHADEMA Watimkia CCM

$
0
0
Kimbunga cha madiwani na wabunge kuhama hasa vyama vya upinzani na kuhamia CCM kimeendelea kutimka, ambapo jana usiku madiwani wengine wawili wa jiji la Arusha walifuata mkondo.

Madiwani hao walioshinda uchaguzi wa mwaka 2015 kwa tiketi ya Chadema, jana usiku walitangaza kujiuzulu nafasi zao na kujiunga na CCM hivyo kufanya idadi ya madiwani wa Arusha waliochukua hatua hiyo kufikia wanane.

Wakizungumzia sababu za kujiuzulu, Alex Marti wa kata ya Olasitin na Amani Liwadi wa kata ya Engutoto, wamesea lengo ni kumuunga mkono Rais John Magufuli.

“Nimeamua kwa ridhaa yangu mwenyewe kujiuzulu udiwani. Nimeandika barua kwa viongozi wa Chadema kueleza uamuzi wangu, kikubwa kilichofanya niamue hivi ni kazi nzuri inayofanywa na Rais John Magufuli,” alisema Marti.

Liwadi pia alitoa sababu sawa na za Marti na kwamba tayari ameandika barua kwenda Chadema.

Uamuzi huo wa madiwani hao unaifanya Chadema kubaki na madiwani 25, huku madiwani wa CCM wakiwa saba kutoka idadi ya madiwani wawili waliochaguliwa mwaka 2015.

Arusha inatajwa kuwa ni moja kati ya ngome kubwa zaidi za Chadema.

Shirika la Posta Kununua Ndege Yake

$
0
0
Shirika  la Posta Nchini lipo katika mchakato wa kununua ndege kwa ajili ya kusambaza vifurushi na huduma nyingine ili kurahisisha huduma kwa wateja wao.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam juzi, Postamasta Mkuu wa Shirika hilo, Hassan Mwang’ombe, alisema ununuzi wa ndege hiyo unatokana na mafanikio yaliyopatikana tangu bodi iteuliwe mwaka 2016.

Alisema mchakato wa ukamilishwaji wa ndege hiyo unaendelea na kwamba utawapunguzia muda wateja kupata mizigo yao pindi inapotumwa kupitia shirika hilo.

Katika hatua nyingine, alisema kutokana na kukua kwa teknolojia, shirika hilo limeanzisha duka la mtandaoni, ambalo tayari lina wateja kutoka duniani kote.

Alisema tayari wameunganisha ofisi 125 za posta kwenye mfumo wa kutolea huduma kielektroniki unaojulikana kama Postglobal netsmart na mpango wa kuunganisha nyingine 27 utakamilika mwishoni mwa Septemba, mwaka huu.

“Maboresho na mifumo hiyo ya mawasiliano inalenga kuboresha huduma ya biashara mtandao nchini na nje ya nchi na kuwafanya wateja wa shirika hilo kufurahia huduma zetu’’.

Aliongeza kuwa, wamefanikiwa kuboresha huduma za kisasa katika ukanda wa Afrika kwenye kufikisha huduma kwa wateja,  hasa maeneo korofi kwa kutumia ndege zisizo na dereva zijulikanazo kama ‘drones’.

Naye Mwenyekiti wa bodi wa Shirika hilo, Dk. Haroun Kondo, alisema tangu bodi yake iteuliwe wameweza kuzalisha faida.

Dk. Kondo alisema kutokana na hilo, kwa mwaka wa fedha wa 2016/2017 walitoa gawio la Sh milioni 250 kwa Serikali, huku mwaka huo wa fedha 2017/2018 wanatarajia kutoa gawio la zaidi Sh bilioni moja.

Dk. Kondo alisema hilo limetokana na jitihada za Bodi na Menejimenti ya Shirika katika kulifanya lijiendeshe kwa faida tofauti na ilivyokuwa huko nyuma, ambapo lilikuwa likizalisha hasara tu.

Amesema lengo lao kuanzia sasa ni kuchangia pato la taifa kwa kutoka gawio la kuanzia Sh bilioni na kuendelea, kwa madai kuwa shirika lina uwezo huo kupitia rasilimali ilizo nazo, ikiwamo majengo na viwanja wanavyovimiliki.

Alisema katika mafanikio hayo alipitia changamoto mbalimbali, kama Mwenyekiti, ikiwamo kulalamikiwa kuwa mbabe kwa kuwaondoa baadhi ya wafanyakazi waliokuwa wakifanya kazi kwa mazoea na kulisababishia shirika hasara na kufikishwa katika vyombo mbalimbali, lakini hakujali.

Emmanuel Mbasha Ampa Makavu Shilole...Amtaka afanye kazi Badala ya Kujiliza Kwea Rais Kuomba Msaada

$
0
0
Muimbaji wa nyimbo za Injili nchini Tanzania, Emmanuel Mbasha ameamua kuwatolea uvivu watu wote maarufu wanaomuandama Rais Magufuli kwa kutaka msaada wa mali ile hali wana uwezo kifedha, akiwemo msanii wa muziki nchini Tanzania, Shilole.

Mbasaha amesema kuwa Slogan ya Rais Magufuli ni ‘Hapa Kazi Tu’ huku akimshangaa msanii mkubwa kama Shilole kubitaji msaada wa ada ya kumsomesha mtoto wake ile hali anafanya kazi na ni mjasiriamali.

“Habari za mda huu . Naandika kwa masikitiko makubwa sana juu ya watu wanaopenda kutumia vibaya huruma ya raisi wetu, haswa wasanii wa bongo movie. Jamani sera ya raisi wetu ni kila mtu afanye kazi na ndiyo maana slogan yake inasema “HAPA KAZI TU” Ukifanya kazi na kujituma kama sisi mbona maisha ni mazuri tu hapa Tanzania jamani, ila ukipenda mteremko ndiyo inaweza kuku cost 😁😁😁😁. Dada yangu Shilole, yaani juzi tu umepost bonge la jumba hapa kila mtu akafurahia na kukupongeza hadi mie nilikupongeza, japokuwa wiki moja kabla ya hapo kuna kijana alikuwa anadai pesa zake za pili pili😭.😭😭😭. Leo nileshangaa kuona clip inasambaa ukilia na kuomba raisi akusaidie kukusomeshea mtoto, sitaki kukupinga ila nakuuliza na kukushauri. 

"Jambo ambalo nakuuliza ni kwamba, Je ! Umesahau kuwa elimu ni bure kuanzia chekechea hadi form four ? Je ! Huyo unaetaka asomeshwe yuko darasa la ngapi dada yangu? Mimi nadhani vitu vingine tungevipima kabla ya kuamua kuchukua hatua. 

"Hebu jiulize, leo raisi akikulipia ada ya mwanao unadhania hawa watoto wa maskini kabisa ambao hawana hata makazi watajisikiaje kama sio kutaka kubebeshana lawama ??,“ameandika Emmanuel Mbasha kwenye ukurasa wa Instagram na kutoa ushauri kwa wasanii.

“Mimi nadhani wasanii tutumie majina yetu kusaidia jamii isiyojiweza na sio kutafuta mteremko. Kweli marafiki zako wote umeshindwa hata kuwakopa kimya kimya hiyo pesa ya ada kisha uwarejeshee kidogo kidogo pale biashara inapokwenda sawa ? Mimi nadhani hichi ulichokifanya ulistahili kukifanya kwa niaba ya mtu ambaye hana jina wala connection kama zako ili utumie jina lako kumuombea msaada kwa raisi, na siyo mwanamke mpambanaji kama wewe.mie nadhani ungeandika andiko ambalo ungempelekea raisi na ukaomba akudhamini ili upate pesa Bank 400 Ml au Zaidi ukakopeshwa na ukafungua hotel kubwa na pia utakua umetengeneza ajira kwa vijana wenzetu kuliko hilo wazo,

"Pia kumbuka juzi tu tulikuwa na msiba kule Chato nadhani badala ya kuibuka leo na kutaka msaada angarau ungejitokeza na rambirambi kidogo ili ikuwekee mazingira mazuri ya kuja kukiwakilisha hichi kilio chako hapo baadaye. Haya ni maoni yangu kama Mtanzania huru, sitaki povu hapa jamani. Kamati yangu ya kublock kaeni mkao wa kura.kama unaweza kuzunguka na Ttcl nchi nzima.kajifunze kwa @munalove100 basi,“ameeleza Mbasha.

Kwa upande mwingine Shilole amemjibu kwa kusema “Nakuheshimu sana kaka yangu please tulinde heshima yetu”.

Wiki mbili zilizopita Shilole alikaririwa kwenye vyombo vya habari akiomba msaada kwa Rais Magufuli wa kumsomesha mtoto wake mmoja wa kike ambae amedai kuwa baba yake mzazi amefariki dunia.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya Septemba 3

Kamati Za Bunge Zaishauri Serikali Kutekeleza Miradi Ya Maendeleo Kwa Ubia Na Sekta Binafsi

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
WAJUMBE wa Kamati za Kudumu za Bunge za Miundombinu, Bajeti na Kamati ya Uwekezaji na Mitaji, wameishauri Serikali kutekeleza kwa vitendo miradi mikubwa na yenye tija kwa Umma kwa kutumia njia ya Ubia kati ya Umma na Sekta binafsi ili kuchochea haraka maendeleo ya nchi.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mhe. Mashimba Ndaki amesema kuwa  wabunge wameridhishwa na na hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha kuwa mpango wa ubia kati ya Serikali na sekta binafsi unafanikiwa na unachochea maendeleo ya wananchi.

“Kama wabunge tungependa kuona mpango unaingizwa katika mipango ya Serikali ili kuharakisha miradi ya maendeleo na pia tunapongeza hatua zilizochukuliwa na Serikali ikiwemo kumteua Kamishna anayeshughulikia miradi ya ubia kati ya sekta binafsi na ile ya umma, “ Alisisitiza Mboya

Alibainisha kuwa jukumu la Serikali ni kuhakikisha kuwa inaweka mazingira wezeshi kwa wawekezaji wote watakaojitokeza kushirikiana na Serikali katika kutekeleza miradi ya maendeleo hapa nchini.

Mwenyekiti wa Bunge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi Mhe. Endrew Chenge amesema kuwa nchi nyingi Duniani zimefanikiwa kuwaletea wananchi wake maendeleo kupitia utaratibu huo ambapo jambo la muhimu ni kufanywa kwa maandalizi ya kina na kuwepo kwa utashi kutasaidia kufanikiwa kwa miradi husika .

Aliongeza kuwa mwaka huu Serikali imeleta Bungeni Mswada wa Marekebisho ya Sheria ya PPP utakaojadiliwa na wabunge katika Bunge linaloanza Septemba 4 mwaka huu, pamoja na mambno mengine Muswada huo unapendekeza kuanzishwa kwa Kituo cha PPP chini ya Wizara ya Fedha na Mipango, ambacho kitakuwa na jukumu la kuishauri Serikali kuhusu masuala yanayo husu miradi mbalimbali itakayowasilishwa kwa mfumo wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi

Akizungumza katika Semina hiyo, Kamishna  wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. John Mboya amesema kuwa Dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa inaweka mazingira wezeshi katika kutekeleza miradi ya ubia na Sekta binafsi ili kuleta mageuzi katika maisha ya wananchi.

“Lengo la kuwa na miradi ya ubia kati ya Serikali na sekta binafsi ni kutekelezaIilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kutekeleza mpango wa maendeleo na hatimaye kutoa huduma bora kwa wananchi,” Alisisitiza Mboya

Akifafanua Mboya amesema kuwa moja ya hatua za maboresho zilizochukuliwa na Serikali ni kuhamisha Kituo cha kusimamia miradi ya ubia katika ya Umma na Sekta binafsi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kuja Wizara ya Fedha.

Akizungumzia majukumu ya chombo cha kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo Dkt. Mboya  amesema kuwa chombo hicho kimepewa jukumu la kufanya uchambuzi wa kina kuhusu miradi yenye sifa na kusimamia mchakato wa uteklezaji wa mpango huo kwa kufuata ngazi zote zilizopo hadi utekelezaji wa mradi husika.

Aliongeza kuwa ili kufanikisha mpango huo Serikali inasisistiza uwazi, uwajibikaji na utayari hali itakayo sababisha  kufikiwa kwa malengo ya miradi ya ubia kati ya sekta hizo mbili ambapo alitaja baadhi ya miradi itakayotekelezwa ambayo upembuzi yakinifu umekamilika kuwa ni ile ya ujenzi wa Viwanda vya dawa, usambazaji wa gesi majumbani katika Jiji la Dar es Salaam, Mtwara , Lindi na ule wa uendeshaji wa mabasi ya mwendo kasi Jijini Dar es Salaam ambao umeanza na uko katika hatua mbalimbali za uendelezwaji.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD) Bw. Laurean Bwanakunu amesema kuwa tayari Bohari hiyo imekamilisha upembuzi yakinifu wa mradi wa ujenzi wa viwanda vya dawa na vifaa tiba vinavyotokana na malighafi zinazozalishwa hapa nchini ikiwemo pamba na kufikia machi mwakani zabuni ya mradi huo itatangazwa ili kuwapata wabia.

Katika kutekeleza mradi huo kiwanda cha kuzalisha maji ya dripu yanayotumika kwa wagonjwa mahosipitalini pia kitajengwa ambapo kwa sasa maji hayo yanaagizwa kutoka nchini Uganda na kwamba hatua hiyo itapunguza gharama za Serikali za kuagiza dawa na vifaa hivyo kutoka nje ya nchi ambapo zaidi ya shilingi trilioni 1.8  hutumika kuagiza bidhaa hizo kila mwaka.

Kwa upande wake. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) Mhandisi  Kapuulya  Musomba amesema kuwa mradi wa kusambaza gesi majumbani katika Jiji la Dar es Salaam, Mtwara na Lindi unaotarajiwa kuhgaribu zaidi ya shilingi bilioni 300, utaleta mageuzi kwa wananchi wa mikoa hiyo ambapo wananchi zaidi ya 120,000 katika Jiji la Dar es Salaam watafikiwa.

Aliongeza  kuwa katika mikoa ya Lindi na Mtwara wananchi zaidi ya 5,000 wataunganishiwa gesi majumbani mwao huku viwanda zaidi 30 katika maeneo ya mradi vitaunganishiwa huduma hiyo pamoja na vituo vya kujaza gesi kwenye magari yanayotumia nishati hiyo.

Semina kwa wabunge wa Kamati za Bajeti, Miundombinu na ile ya Uwekezaji Mitaji imefanyika Jijini Dodoma ikiwashirikisha wajumbe wa Kamati hizo ili kuwajengea uwezo wa namna dhana hiyo inavyoweza kuleta maendeleo hapa nchini.

……….Mwisho…….

Serikali Yawataka Wananchi Kutonunua Sukari Inayouzwa Kwa Magendo maana ni Hatari kwa Afya Zao

$
0
0
Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba amewataka watanzania kuwa waangalifu na kuacha mara moja kununua sukari kutoka kwa wafanyabiashara na vifungashio holela, kwani hali hiyo ina hatarisha maisha yao pamoja na kuathiri uchumi wa nchi.
 
Dkt. Tizeba ametoa kauli hiyo baada ya bodi ya sukari kubaini uwepo wa kiasi kikubwa cha sukari kinachoingizwa nchini kimagendo, ikiwemo sukari nyeupe kwa ajili ya matumizi ya viwandani maarufu kama 'white sugar'.

"Sukari iliyokuwa kwenye vifungashio vya plastiki ambavyo havijulikani vimetoka wapi licha ya kwa muonekano wa macho ni sukari. Kifungashio kinapaswa kiwe na 'information' yote ya nani kafungasha, kilichomo humo ni kitu gani", amesema Dkt. Tizeba.

Pamoja na hayo, Dkt. Tizeba ameendelea kwa kusema "kwa kweli wananchi nawaomba muepukane na jambo kama hili la kununua sukari bila ya kusoma maelezo ya kwenye mifuko inayoelezea bidhaa husika kwasababu mnaweza kutumia sumu bila ya kujijua".

Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Sukari nchini Bw. Miraji Kipande amesema katika operesheni hiyo wanayoendesha hadi sasa wameshakamata zaidi ya mifuko elfu nne na kufanikiwa kumkamata mfanyabiashara mmoja eneo la Tandika Jijini Dar es Salaam kwa kutengeneza vifunganishio 'fake'.

Katika miezi ya hivi karibuni hii ni mara ya pili kwa Waziri wa Kilimo Dkt. Tizeba kubaini uingizwaji wa bidhaa hiyo kimagendo na kutoa agizo kwa Jeshi la Polisi kuwakamata wahusika kwa kuwa vitendo hivyo ni kinyume za sheria za nchi.

Lugola Akerwa na Mgambo Kuwapiga Kikatili Wananchi.....Atoa Onyo Kwa Walimu Wanaotumia Nguvu Nyingi Kuwapiga Wanafunzi

$
0
0
Na Felix Mwagara, MOHA
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amelaani tukio lililofanywa na Mgambo wa Jiji la Dar es salaam akisema ni la kihuni, kishenzi na kinyama na halipaswi kufumbiwa macho na wapenda amani, watetezi wa haki za binadamu na wananchi wote kwa ujumla.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza, Lugola alisema Serikali inalaani vikali tukio hilo ambalo lililotokea wiki iliyopita jijini humo, na kutokana na unyama huo tayari hatua za kisheria zimeanza kuchukuliwa.

“Jeshi la Polisi tayari limewakamata wahusika kama Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni tarehe 31 Agosti, 2018 ilivyoeleza. Natumia fursa hii kuwakumbusha tena Mgambo wote kuwa makini katika utekelezaji wa maagizo wanayopewa na kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu,” alisema Lugola.

Pia kutokana na tukio hilo, Lugola alisema anazitaka Mamlaka za Majiji, Manispaa na Halmashauri kufikiria kuanzisha Huduma ya Polisi Wasaidizi (Auxiliary Police) katika maeneo yao kwa mujibu wa Sheria ya Polisi na Polisi Wasaidizi Sura ya 322 ili kuepuka matukio ya uvunjifu wa haki za Binadamu kama tukio la Mgambo watatu  jinsi lilivyo tokea.

Aidha, Lugola pia alizungumzia kuhusu baadhi ya matukio mengine ambayo watu  wanajichukulia Sheria mkononi na kuwaadhibu kwa kuwapiga watu wengine kwa sababu mbalimbali.

Aliyataja matukio hayo ni pamoja na ugomvi wa kifamilia ndani ya ndoa ambao huhusisha Wanaume kuwapiga wake zao au wake kuwapiga waume zao, pia  wananchi kuwapiga watu wanaowatuhumu kwa makosa mbalimbali, pamoja na walimu kuwapiga wanafunzi kinyume cha sheria.

Pia Lugola aliwaonya baadhi ya Askari Polisi ambao wanatumia nguvu isiyo ya kadiri kulingana na mazingira halisi wanapowadhibiti watuhumiwa.

“Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Mambo ya Ndani ya Nchi inalaani vikali matukio ya kujichukulia Sheria mkononi na kupitia kwenu Wanahabari nawataka Watanzania kufuata sheria za nchi kwa kuacha vitendo vya kujichukulia Sheria mkononi. Vitendo hivi pamoja na kusababisha uvunjifu wa amani vinaweza kuleta madhara kwa watu ambao hawana makosa na kuichonganisha Serikali na wananchi wake,” alisema Lugola.

Kutokana na matukio hayo, Lugola aliwataka wanandoa wanakumbushwa kutumia Dawati la Jinsia katika Vituo vya Polisi kote nchini ili kuwasilisha malalamiko yao ya unyanyasaji wa kijinsia ndani ya ndoa ili hatua stahiki zichukuliwe.

Pia aliwataka wananchi waendelee kuheshimu sheria za nchi na kuepuka kujichukulia unakuta mtu anapigwa hata haulizi anayepigwa amekosa nini nae anajiunga nao na kumpiga hali ambayo imesababisha majeraha, vilema vya kudumu na vifo kwa watu wasio na hatia.

Hata hivyo, Lugola aliwaonya walimu kwa kufanya matukio kujirudia kwa kuwaadhibu wanafunzi kwa kuwachapa na kuwapiga hovyo kiasi cha kusababisha maumivu makali, ulemavu na vifo.
 
“Natumia fursa hii kuwakumbusha Walimu kote nchini kuzingatia Sheria, Kanuni na Miongozo ya Adhabu kwa wanafunzi ambayo imetolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ili kuepuka madhara yake, kuondoa hofu kwa wazazi na kufanya shule zetu kuwa mahali salama kwa watoto wetu,” alisema Lugola.

VIDEO: Ajali yaua watalii wanne Arusha, yajeruhi wawili

$
0
0
Watu Sita wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa kwenye ajali ya barabarani iliyotokea eneo la Nanja Wilayani Monduli Mkoani Arusha baada ya gari la Watalii aina ya Toyota land cruiser kugongana uso kwa uso na gari la mizigo aina ya Semi trela lililokuwa likitokea Mkoani Kigoma kuelekea Nchini Kenya. 

Katika ajali hiyo iliyotokea jana Septemba 02,2018 majira ya saa tatu asubuhi waliopoteza maisha ni Watalii Wanne, Dereva moja na mpishi waliokuwa kwenye gari ya Watalii yenye namba za usajili T 418 AHX mali ya kampuni ya Tabia Safari iliyokuwa ikitokea Mjini Arusha kuelekea hifadhi ya Wanyama ya Tarangire.

Kama Dalili Hizi Unazo Upo Kwenye Hatari Ya Kuishiwa Nguvu Za Kiume Kabisa

$
0
0
Una dalili zifuatazo?
1: Kushindwa kurudia tendo la ndoa
2: Kutojisikia hamu ya tendo la ndoa
3: Maumivu ya kiuno mgongo
4: Tumbo kuunguruma na kujaa gesi
5: Uume kusinyaa, kuingia ndani na kuwa mdogo au mfupi
6: Korodani moja kuvimba

KAMA DALILI HIZI UNAZO UPO KWENYE HATARI YA KUISHIWA NGUVU ZA KIUME KABISA

Kwa matibabu tumia OZYMIX POWER-dawa bora ya nguvu za kiume ya miti shamba ambayo haina kemikali ambayo itakuwezesha kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara tatu bila hamu kuisha.
Pia tunatoa huduma hizi:>

1.Dawa ya Kuondoa michirizi
2.Kumrudisha mwanaume aliyekuacha 
 
Tunapatikana KAWE UKWAMANI karibu na kituo cha mabasi.
KWA MAWASILIANO ZAIDI ; 0716096205 /0756726865 FIKA OFISIN AU PIGA SIMU NA UTALETEWA DAWA POPOTE ULIPO DAR ES SAALAM NA KWA MIKOANI TUNATUMA KWA NJIA YA MABASI.

TEMBELEA KATIKA BLOG YETU HAPA>>>;

Makanga 3 Power; Dawa Bora Nguvu Za Kiume

$
0
0
Kutibu nguvu za kiume dakika(10) na kupona muda wa siku tatu tuu. Kuimarisha misuli ya uume uliolegea, pia ipo Dawa ya kurefusha uume mfupi inchi NNE hadi saba na kunenepesha uume mfupi sentimita NNE.

Tiba ya kudumu kutibu maumivu ya mgongo,kiuno, tumbo kuunguruma na kujaa gesi, kupata choo vizuri, na kutibu uzazi, kutibu busha bila operesheni, kisukari, presha ,miguu kuuma, uzazi, fangas sugu, vidonda vya tumbo.

Ni docta bingwa wa kutibu magonjwa sugu, kutoa ndagu za utajiri kwa kutumia Pete, kazi ,cheni, mikufu maalumu ya bahati, una kesi umedhulumiwa Mali au pesa? Zitarudi muda wa Masaa matatu tuu.

Onana na Dr shilindes shida zako zote zitakwisha, anatoa Dawa za utajiri kwa wafanyakazi, wakulima, na wafugaji, wafanyabiashara na wachimba madini kwa kutumia pete, kazi kwa yeyote anaetaka kuwa na pesa nyingi.

Pia anaboresha akili kwa wanafunzi darasani, masomo na kufaulu mitihani pia kushinda bahati nasibu yeyote.

Pia tunatoa Dawa kumrudisha Mume, mke, mpenzi, hawara, kwa muda wa SAA moja tuu, na kuomba msamaha kwa kukupigia magoti na yeyote yule, unaemtaka kimapenzi au kuoana, utampata na kumfunga asitoke nje ya ndoa daima na kutekeleza shida zako zote. Kupunguza unene, kupunguza matiti makubwa, tumbo na nyama uzembe muda wa siku sita unapata saizi uipendayo.

Kutoa makovu mwilini, chunusi, upele na mabaka, pia tunayo Dawa ya kuongeza hipsi, makalio, mguu wa bia na kupata shepu safi kwa muda wa siku saba tuu.

Wa mikoani mtapata huduma popote mlipo.
Tupo dar es salam mbagala rangi tatu.

Mawasiliano simu namba: 0784 460 348. Au 0659 103 360.

Waitara Apiga Kampeni Ukonga....Asena Yeye Sio Msaliti, Ataja Sababu za Kuikimbia CHADEMA na Kurudi CCM

$
0
0
Mgombe Ubunge wa jimbo la Ukonga kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mwita Waitara  amesema yeye sio Msaliti bali amechagua CCM  ili aweze kumalizia alipoishia hususani swala la barabara , Umeme na Maji katika jimbo  hilo. 

Waitara aliyasema hayo jana Jumapili Septemba 2  katika Mkutano wake wa Kampuni uliofanyika katika Kata ya kitunda.

Alisema kuhamia kwake CCM ameona imefika mahali kero zinazowasumbua wananchi hataweza kuzitekeleza kwani kuna baadhi ya vikao ukienda ukirudi kwenye vikao vya chama unaambulia matusi.

"Naomba muelewe kwamba mimi nimekulia Kitunda, nimesomea shule Kitunda na nimeoa hapa hivyo najua kero zote zinazowahusu wanakitunda ikiwemo barabara, elimu pamoja na huduma za kijamii kama maji na umeme," alisema.

Hata hivyo, Waitara amesema alipokuwa Chadema ameweza kwenda maeneo yote ikiwemo mitaa 70 kutembelea kina mama vijana wa bodaboda, vikoba hivyo hakuna anayeweza kusimama na kusema kuwa Waitara hajafanya chochote alipokuwa mbunge wa Chadema.

Pia, aliongeza kwa kipindi chote akiwa Chadema ameshindwa kutekeleza baadhi ya changamoto, kwani viongozi wa chama walikuwa wakimwambia afanye hivyo kwa kuwatuakana viongozi wakiwemo mawaziri ambao wengine ni wakubwa kwake jambo ambalo hawezi.

Waitara alisema ilifika mahali kutokana na yaliyokuwa yanaendelea ndani ya Chadema ikiwemo kutoruhusiwa kuhoji mapato na matumizi ya chama.

Kutokana na hilo amesema alikuwa kashafikia hatua ya kuwa mbunge bubu ndani ya Bunge na hivyo hakuona faida ya kuwa mbunge kupitia chama hicho ambacho huruhusiwi hata kuhoji.

Alisema kwa CCM anaona kina faida kwani wabunge wana nafasi katika vikao vyao kukaa na mawaziri wa nchi hii na kuwa na nafasi ya kupenyeza kero za wananchi ili zishughulikiwe.

Mwita amewaahidi wananchi hao kama watamchagua, atazidi kuwaletea maendeleo, kwani aliyafanya hayo akiwa mtoto wa kambo na sasa amerudi nyumbani.

Kwa upande wake Mjumbe wa Halmashauri Juu ya CCM  Livingstone Lusinde aliwataka watu wa ukonga wasifanye makosa kwani sasa wanachagua Mbunge wa  jimbo atakayefanya kazi na serikali na sio uchaguzi Mkuu.

Alisema CCM peke yake ndio inatekeleza ilani Kwa kupewa dhamana ya kuongoza dola hivyo wakichagua mgombea kutoka vyama vingine watakuwa wamejitafutia matatizo wenyewe
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images