Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Takukuru yamburuza Askofu kortini tuhuma wizi wa mahindi ya yatima

$
0
0
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imemfikisha Askofu wa kanisa la Gospel Ministry, Christopher Madole, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma kwa kukabiliwa na mashtaka mawili, likiwamo la uchepushaji wa mahindi ya watoto yatima.

Katika shtaka lingine anakabiliwa na kosa la kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu.

Akisoma hati ya mashtaka mbele ya hakimu Mary Senapee, Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Biswaro Biswaro, alisema kati ya Januari na Machi 2016, Askofu Madole, alichepusha mahindi tani 360 kutoka katika Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), aliyochukua kwa ajili ya kupeleka kwa familia maskini za Wilaya za Bahi na Chamwino na badala yake akayauza kwa mtu mwingine na hivyo kujipatia fedha kwa udanganyifu.

Aidha, taarifa kutoka kwa Kamanda wa Takukuru, Mkoa wa Dodoma, Sosthenes Kibwengo, ilisema taasisi hiyo wilayani Kondoa imewafikisha mahakamani askari wanyamapori watatu wa pori la akiba la Mkungunero kwa kosa la kuomba rushwa ya Shilingi milioni nne.

Washtakiwa hao Steer Waliya, David Kayila na Nginanu Olepesa, walifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kondoa wakituhumiwa kukamata ng'ombe 88 walioingia kwenye hifadhi na kupokea rushwa kutoka kwa wamiliki wa mifugo hiyo ili waiachie.

Wilayani Mpwapwa, Takukuru imemfikisha katika mahakama ya wilaya hiyo Lazaro Masimami, ambaye ni Ofisa Ardhi Msaidizi wa halmashauri ya wilaya kwa kosa la kuomba rushwa ya Sh. 300,000 kwa mwananchi mmoja, ili amsaidie kupata hati ya kiwanja chake.

Wakati huo huo, Takukuru hivi karibuni imeshinda kesi ilizokuwa inaendesha wilayani Kondoa na Mpwapwa kwa mshtakiwa Saidi Abdalah, kuhukumiwa kifungo cha mwaka mmoja na kulipa faini ya Sh. 500,000 baada ya kutiwa hatiani kwenye shtaka la ubadhirifu na ufujaji na pia alitakiwa kurejesha Sh. 2,859,050 alizofuja wakati akiwa katibu wa kamati ya maji wa Kijiji cha Mwaikisabe, wilayani humo.

Aidha, Mahakama ya Wilaya ya Mpwapwa imewatia hatiani na kuwahukumu kwenda jela mwaka mmoja au kulipa faini, walimu wawili wa Shule ya Msingi Idilo, Henry Kindole na Peter Joctan, waliokuwa wanakabiliwa na shtaka la ufujaji na ubadhirifu wa fedha za mradi wa ujenzi wa shule hiyo.


Kama Dalili Hizi Unazo Upo Kwenye Hatari Ya Kuishiwa Nguvu Za Kiume Kabisa

$
0
0
Una dalili zifuatazo?
1: Kushindwa kurudia tendo la ndoa
2: Kutojisikia hamu ya tendo la ndoa
3: Maumivu ya kiuno mgongo
4: Tumbo kuunguruma na kujaa gesi
5: Uume kusinyaa, kuingia ndani na kuwa mdogo au mfupi
6: Korodani moja kuvimba

KAMA DALILI HIZI UNAZO UPO KWENYE HATARI YA KUISHIWA NGUVU ZA KIUME KABISA

Kwa matibabu tumia OZYMIX POWER-dawa bora ya nguvu za kiume ya miti shamba ambayo haina kemikali ambayo itakuwezesha kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara tatu bila hamu kuisha.
Pia tunatoa huduma hizi:>

1.Dawa ya Kuondoa michirizi
2.Kumrudisha mwanaume aliyekuacha 
 
Tunapatikana KAWE UKWAMANI karibu na kituo cha mabasi.
KWA MAWASILIANO ZAIDI ; 0716096205 /0756726865 FIKA OFISIN AU PIGA SIMU NA UTALETEWA DAWA POPOTE ULIPO DAR ES SAALAM NA KWA MIKOANI TUNATUMA KWA NJIA YA MABASI.

TEMBELEA KATIKA BLOG YETU HAPA>>>;

Makonda: Ninalaani tukio la kushambuliwa raia kisa 50,000 ya usafi

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ameagiza mgambo waliopiga raia katika eneo la Bunju A kuchukuliwa hatua kali kwani walichokifanya haukuwa mpango wa mkoa.

Makonda amekemea vikali kitendo hicho amabacho kimefanyika kwenye Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Bunju ambapo Mgambo hao wamepiga raia na kuwajeruhi akiwemo mfanyabiashara, Robson Orotho mkazi wa Bunju kutokana na kushindwa kulipa Sh. 50,000 ya taka.

”Nimeshtuka sana baada ya kuona video hiyo sio kitendo cha kufanywa na watendaji kwani lengo letu ni kusimamia usafi na si kupiga raia, nalaani kitendo hicho na naagiza hatua kali zichukuliwe dhidi yao,” amesema Makonda.

Kwa upande wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni limethibitisha kuwashikilia mgambo watatu wa Manispaa hiyo ambao wamehusika katika tukio hilo na taratibu za kisheria zinaendelea na upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani.

Aidha, Kamanda Murilo amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Goodluck Festo, Rehema Nyange na Kelvin Edson, ambao wote ni Mgambo wa Manispaa hiyo huku akibainisha kuwa mfanyabiashara huyo anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Mwananyamala.

Siku za hivi karibuni zimesambaa picha za video katika mitandao ya kijamii zikionyesha mgambo wakitoa kipigo kwa watu na kuzua taharuki, wengi wakiwa ni wafanyabiashara ndogo ndogo

Waziri Mbarawa Amteua Mhandisi Luhemeja Kukaimu Nafasi Ya Afisa Mtendaji Mkuu Dawasa

Makanga 3 Power; Dawa Bora Nguvu Za Kiume

$
0
0
Kutibu nguvu za kiume dakika(10) na kupona muda wa siku tatu tuu. Kuimarisha misuli ya uume uliolegea, pia ipo Dawa ya kurefusha uume mfupi inchi NNE hadi saba na kunenepesha uume mfupi sentimita NNE.

Tiba ya kudumu kutibu maumivu ya mgongo,kiuno, tumbo kuunguruma na kujaa gesi, kupata choo vizuri, na kutibu uzazi, kutibu busha bila operesheni, kisukari, presha ,miguu kuuma, uzazi, fangas sugu, vidonda vya tumbo.

Ni docta bingwa wa kutibu magonjwa sugu, kutoa ndagu za utajiri kwa kutumia Pete, kazi ,cheni, mikufu maalumu ya bahati, una kesi umedhulumiwa Mali au pesa? Zitarudi muda wa Masaa matatu tuu.

Onana na Dr shilindes shida zako zote zitakwisha, anatoa Dawa za utajiri kwa wafanyakazi, wakulima, na wafugaji, wafanyabiashara na wachimba madini kwa kutumia pete, kazi kwa yeyote anaetaka kuwa na pesa nyingi.

Pia anaboresha akili kwa wanafunzi darasani, masomo na kufaulu mitihani pia kushinda bahati nasibu yeyote.

Pia tunatoa Dawa kumrudisha Mume, mke, mpenzi, hawara, kwa muda wa SAA moja tuu, na kuomba msamaha kwa kukupigia magoti na yeyote yule, unaemtaka kimapenzi au kuoana, utampata na kumfunga asitoke nje ya ndoa daima na kutekeleza shida zako zote. Kupunguza unene, kupunguza matiti makubwa, tumbo na nyama uzembe muda wa siku sita unapata saizi uipendayo.

Kutoa makovu mwilini, chunusi, upele na mabaka, pia tunayo Dawa ya kuongeza hipsi, makalio, mguu wa bia na kupata shepu safi kwa muda wa siku saba tuu.

Wa mikoani mtapata huduma popote mlipo.
Tupo dar es salam mbagala rangi tatu.

Mawasiliano simu namba: 0784 460 348. Au 0659 103 360.

Mkuu wa Mkoa Ataka Mwalimu Atakamchapa Viboko Vingi Mwanafunzi Kinyume cha Sheria na Yeye Apigwe Bakora

$
0
0
Katika kuhakikisha kitendo kilichotokea mkoani Kagera cha mwanafunzi kupigwa na kusababishiwa kifo hakitokei mkoani Tanga, mkuu wa mkoa huo Martine Shigela amewaagiza viongozi wa mkoa huo kusimamia sheria za adhabu mashuleni.

Akiongea jana kwenye kikao cha robo ya tatu ya mwaka cha kamati ya ushauri ya mkoa (RCC), Mh. Shigela alisema mwalimu atakayebainika kutoa adhabu kinyume na utaratibu naye aweze kuadhibiwa kama ilivyokuwa kwa mwanafunzi.

''Mwalimu akienda kinyume na sheria ya adhabu mashuleni maana yake kajitengenezea sheria yake ambayo haijatungwa na bunge hivyo kwa kosa hilo lazima iwepo adhabu kwa mwalimu aliyevunja sheria na kwasababu anakuwa ametoa adhabu ya viboko ni vyema na yeye akapata viboko kama alivyo mchapa mwanafunzi'', alisema.

Kwa upande wake afisa elimu mkoa wa Tanga Mayasa Hashim amewaasa walimu kufuata utaratibu wa aina ya adhabu anazopaswa kupewa mwanafunzi huku akiongeza kuwa sio kila kosa linahitaji adhabu bali makosa mengine yanatakiwa kuishiwa kwa mwalimu kumshauri mtoto ili asirudie.

Makamu wa Rais Kuzindua Jengo la Kitega Uchumi la Ghorofa 16 Jijini Arusha

$
0
0
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuwaongoza maelfu ya wananchi wa Mkoa wa Arusha katika hafla ya uzinduzi wa jengo la kitega uchumi la Jakaya Kikwete Ngorongoro Tower (JKNT).

Jengo hilo la ghorofa 16, ambalo ni mali ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), linatarajiwa kuzinduliwa rasmi na Makamu wa Rais, Septemba 16, mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati walipotembelewa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Arusha, kukagua jengo hilo, Mwenyekiti wa Bodi ya NCAA, Profesa Abiud Kaswamila, alisema Makamu wa Rais amethibitisha kuhudhuria katika hafla ya uzinduzi wa jengo hilo.

Alisema jengo hilo ni kati ya majengo ya kisasa zaidi kujengwa mkoani hapa na litatumika maalum kama kituo kimoja cha kukuza na kurahisisha biashara ya utalii nchini.

Maneja wa mradi wa ujenzi wa jengo hilo, Profesa Camillius Lekule, ambaye ndiye aliyebuni mchoro wa jengo hilo, alisema kiasi cha fedha zilizotumika hadi sasa ni Sh. bilioni 39.9 kati ya Sh. bilioni 45 zilizokadiriwa awali.

Alisema matarajio ya NCAA baada ya kuwekeza fedha nyingi katika ujenzi wa mradi huo gharama za ujenzi zitarudi baada ya miaka 20.

Alisema jengo hilo lina uwezo wa kudumu kwa miaka 100 ijayo bila ya kupoteza ubora wake na uhalisia kutokana na ujenzi wa kitaalam uliotumia vifaaa vya kisasa na vyenye ubora zaidi.

Lekule alisema usanifu wa jengo hilo ulianza Januari 2011 na ujenzi ulianza Novemba 7, mwaka 2013 na sasa upo katika hatua za mwisho kukamilika.

Naye Meneja Uwekezaji wa NCAA, Needpeace Wambuge, alisema jengo hilo ni maalum kwa ajili ya kitega uchumi cha biashara ya utalii ili kuendeleza utalii baada ya kutokea kwa mtikisiko kwenye sekta hiyo, ulioathiri shughuli za utalii sehemu mbalimbali nchini.

Aidha alisema hadi sasa asilimia 45 ya jengo hilo limeshapangishwa na wadau mbalimbali na gharama za ukusanyaji wa mapato kwa mwezi zitafikia kiasi cha Sh. milioni 350, na kwa mwaka mzima kodi inayotarajiwa kukusanywa ni Sh. bilioni 4.3.

Huna Sababu Ya Kuaibikatena............ Jipatie Dawa Bora Ya Nguvu Za Kiume, Maumbile Madogo Na Mvuto Wa Mapenz

$
0
0
Usikate tamaa ondoa maradhi yako, maana matatizo haya yamekua yakiasili watuwengi kisaikolojia hasa baada ya kujiona wako tofauti sana na wengine kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia (6-8) vinginevyo mtuhuyo anamapunguvu katika mwiliwake.

Kunasababu nyingi sana zinazosababisha matatizo haya, chango hushambulia never ambayo huasili misuli ya uume, Ngili :- hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kufanya tumbo kuunguluma na kujaa gesi, kolodani moja kuvimba au kuingia ndani pamoja na kutopata choo vizuli. Sababuhizi na nyingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba na marakwamara husababisha kukosa hamu ya kuludia tendo la ndoa na baadae kushindwa kabisa

MASISA 3POWER :- nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa mfumo wa vidonge, huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka 15-90 , inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii) inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa, itakufanya uludie tendo la ndoa zaidi ya mara nne (4) birahamu kuisha wara kuhisi kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya dk (20-30 )

YONINANI:- hurefusha na kunenepesha maumbile madogo ya uume uliosinyaa inchi 6-8 na unene wa sm 3-4 kwa mda mfupi sana,

SUPER MORINA :- nidawa inayotibu ama kutatua tatizo la kisukali kwawaliohangaika bila mafanikio, huondoa tatizo la kisukali na kupona kabisa, vilevile ninadawa ya magonjwa sugu km vile presha, vidondo vya tumbo, miguu kuwakamoto, muwasho mwilin, kaswende,uzazi nk.

LUGIMBA :- nidawa ya mvuto wa mapenzi, humtuliza mke, mme, mchumba, hawara au mtu yoyote umpendae na kumfanya akutimizie chochotekile unachokitaka kutoka kwake na kumfunga asiwe na mtu yoyote zaidi yako.

WASILIANA NA DR CHIPUPA NAPATIKANA DAR ES SALAAM KUMBUKA HUDUMAHII ITAKUFIKIA POPOTE ULIPO  0759208637 / 0622344969

Gari la Waziri wa Afya Nusura Liue Mwendesha Baiskeli

$
0
0
Mkazi wa Kata ya Ngogwa, Kahama mkoani Shinyanga, Marco Charles (48), amenusurika kifo baada ya kugongwa na gari lenye namba za usajili STL 2777 lililokuwa limembeba Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.

Waziri Ummy alikuwa akitokea mkoani Kagera kutekeleza majukumu yake ya kikazi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Simon Haule, alisema tukio hilo lilitokea Agosti 27 majira ya saa 10.30 jioni, eneo la Ngogwa barabara ya Masumbwe kuelekea Kahama.

Kamanda Haule alisema gari hilo lililokuwa likiendeshwa na Jumanne Ally (45), dereva wa Waziri Ummy Mwalimu, lilikuwa likitokea Ngara mkoani Kagera kwenda Dodoma ndipo lilimgonga mwendesha baiskeli, Marco Charles (48) na kumsababishia majeraha kichwani, mkono wa kulia na shingoni.

Haule aliongeza kuwa, kutokana na ajali hiyo, majeruhi huyo alipelekwa Hospitali ya Wilaya ya Kahama na anaendelea na matibabu.

Wakati huohuo, Kamanada Haule alisema tarehe 26 majira ya saa 9.53 usiku mtaa wa Nyasubi katika baa ya Chillar Kahama mjini, Emmanuel Philimon (39), mlinzi wa baa hiyo, alijeruhiwa kwa kupigwa na risasi katika mapaja yote mawili na George Nyamhanga (41), ambaye ni mhasibu wa baa hiyo.

Ilielezwa kuwa, alifanya hivyo wakati akisaidia kuwazuia watuhumiwa watatu waliokuwa wamekamatwa kwa tuhuma za kumjeruhi mlinzi mwingine wa baa hiyo, Baharia Athumani (25), mkazi wa Nyasubi aliyepigwa na chupa.

Kamanda alisema chanzo cha tukio hilo ni uzembe wa mtumiaji wa bastola hiyo yenye namba za usajili 785819 CAR Na. 00104206 aina ya Browning, kutochukua tahadhari za kutosha wakati akifyatua risasi hewani ili kuwatuliza watuhumiwa watatu wasitoroke.

Watuhumiwa hao walikuwa wamekamatwa kwa kumpiga chupa mlinzi huyo.

Kamanda alisema mtuhumiwa alikamatwa na silaha hiyo kwa uchunguzi zaidi na kwamba majeruhi wamelazwa katika hospitali ya mji wa Kahama na hali zao zinaendelea vizuri.

Muna Love kutoa kitabu cha Maisha ya Patrick

$
0
0
Msanii wa Filamu Bongo, Muna Love amesema kuwa ana mpango wa kutoa kitabu cha maisha ya mwanae Patrick aliyefariki.

Muna amesema hayo jana akiongea na waandishi wa habari kwenye hafla ya uzinduzi wa kitabu cha William Malecela a.k.a Lemutuz kiitwacho My American Experience.

"Unajua ukishakuwa kwenye wokovu msiba pia ni furaha, hakuna mtu ambaye ataishi milele. Nahitaji kutoa kitabu changu cha mimi na Patrick," alisema Muna.

Mtoto Patrick alifariki July 03, 2018 akipatiwa matibabu Nairobi nchini Kenya na alizikwa July 07, 2018 Dar es Salaam, Tanzania.

Lulu Diva Azungumzia nyimbo Mbili Mpya za Rich Mavoko

$
0
0
Msanii wa muziki Bongo, Lulu Diva amefunguka kuhusu nyimbo mbili mpya za Rich Mavoko, Happy na Ndegele.

Muimbaji huyo akipiga stori na SnS Tanzania (Simulizi na Sauti) amesema kuwa anaona nyimbo hizo zinafanya vizuri tu mtaani.
 
"Ngoma bado zinazidi kwenda na bado muda, ngoma zinazidi kusikilizwa sio kwamba hazijafanya vizuri, mimi napita mtaani nazisikia," amesema Lulu Diva.

Alipoulizwa anahisi kwanini Rich Mavoko hajazifanyia nyimbo hizo promotion kwenye media, alijibu, 'Lakini nafikiria na yeye mwenyewe ametoa kama bonus, unaona hajafanya interview yoyote, hajaongelea popote, ametoa tu,'.

Wimbo wa mwisho kwa Lulu Diva kutoa amemshirikisha Rich Mavoko unaokwenda kwa jina la Ona ambao hadi sasa una views zaidi ya Milioni 1 katika mtandao wa YouTube na ndio wimbo wa kwanza kwa msanii huyo kufanya hivyo.

LIVE | Tazama Hapa Makontena ya Makonda Yakipigwa Mnada

$
0
0
Mnada wa mali zilizomo ndani ya makontena 20 ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, unaendelea na tayari wateja wameshakagua bidhaa na wanashindana kununua.

Bidhaa zilizomo kwenye makontena hayo ni samani za ofisini kama vile viti, meza na makabati.

Mkurugenzi wa kampuni ya Yono Auction Mart, Scholastica Kevela amewataka wanunuzi kuwa na vitambulisho, leseni ya gari na pasi ya kusafiria.

Hata hivyo, bado wateja wengi hawajafikia bei zinazotakiwa. Bei zinazotajwa ni kati ya Sh6 milioni hadi 15 milioni.

Awali Mkurugenzi Mwenza wa kampuni hiyo, Yono Kevela aliwaambia waandishi wa habari kuwa kuna matumaini ya bidhaa zote kununuliwa tofauti na mnada wa awali uliokosa wateja.

==>>Tazama Hapa Makontena Hayo  Yakipigwa Mnada

Bobi Wine aruhusiwa kuondoka Uganda

$
0
0
Mbunge wa Uganda ambaye inadaiwa aliteswa na maafisa wa usalama, Robert Kyagulanyi  maarufu kwa jina la Bob Wine ameruhusiwa kusafiri kuelekea Marekani kwaajili ya matibabu.

Alhamisi usiku Polisi walimkamata Kyagulanyi na mbunge mwenzake wa upinzani Francis Zaake uwanja wa ndege wa Kampala wakati wakijiandaa kwenda nje ya nchi kupatiwa matibabu.

Polisi walidai kuwa viongozi hao wa upinzani, ambao wote wanakabiliwa na tuhuma za uhaini walikuwa katika harakati za kukimbia nchi.

Hata hivyo, wabunge hao wawili wamesema kuwa waliteswa baada ya kukamatwa huko nyuma na hospitali ya Kampala ilitoa pendekezo kwamba wapatiwe matibabu nje ya nchi.

Marekani yasitisha kutoa misaada kwa Palestina

$
0
0
Marekani imesema kuwa imesitisha ufadhili kwa Shirika la Umoja wa Mataifa linalotoa misaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA, hatua inayotishia kuzidisha mzozo kati ya Palestina na utawala wa Rais wa Marekani Donald Trump.

Msemaji wa Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas amelaani uamuzi huo wa Marekani ambao ameutaja kama hatua ya kuwadunisha Wapalestina na inayoendana kinyume na maazimio ya Umoja wa Mataifa.

Aidha, kwa upande wake msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani, Heather Nauert amesema kuwa operesheni na muundo wa shirika hilo la UNRWA una mapungufu makubwa na baada ya tathmini ya kina, Marekani imeamua kusitisha ufadhili.

Marekani huchangia karibu asilimia 30 ya bajeti ya shirika hilo ambalo husaidia kutoa huduma ya afya, elimu na huduma nyingine kwa wapalestina takriban milioni 5 katika ukanda wa Gaza, ukingo wa Magharibi mwa Jordan, Syria na Lebanon.

Wengi wa wakimbizi hao ni watu waliokimbia vita vya mwaka 1948 ambavyo vilipelekea kuundwa kwa taifa la Israel ambalo limekuwa katika mgogoro na nchi za mashariki ya kati.

Hata hivyo, Rais wa Marekani, Donald Trump na maafisa wa utawala wake wamesema kuwa wanataka kuboresha maisha ya Wapalestina na pia kuyafufua mazungumzo ya kutafuta amani kati ya Israel na Palestina.

Makontena ya Makonda Yakosa Wateja Kwa Mara ya Pili

$
0
0
Mnada wa mali zilizomo ndani ya makontena 20 ya yaliyoandikishwa kwa jina la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, umeendeshwa na tayari wateja baadhi wamekagua bidhaa kwa ajili ya kununua lakini wameshindwa kufika bei iliyotakiwa na mamlaka ya mapato nchini (TRA).

Mkurugenzi Mtendaji  wa kampuni inayohusika na kuendesha minada ya Yono Auction Mart, Scholastica Kevela Yono, amewaambia waandishi wa habari kuwa kuna matumaini ya bidhaa zote kununuliwa tofauti na mnada wa awali uliokosa wateja kabisa lakini leo baadhi wameweza kununua na mnada mwingine utaendeshwa Jumamosi ijayo Septemba 8.

Akiendesha mnada huo Kevela amezitaja bidhaa zilizomo kwenye makontena hayo ni samani za ofisini kama vile viti, meza na makabati, huku bei zilizotajwa ni kati ya Shilingi milioni 6 hadi milioni 15 huku akibainisha kuwa mnada huo umehusisha sio makontena ya Mhe. Makonda pekee yake bali na makontena mengine ambayo yameshindwa kulipiwa ikiwemo vifaa vya kilimo pamoja na magari.

Mnada huo umefanyika katika bandari kavu ya Malawi Cargo na wanunuzi wametakiwa kuwa na vitambulisho, leseni ya gari na hati ya kusafiria.

Makontena hayo yanapigwa mnada baada ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, kuagiza makontena 20 ya samani yaliyoingizwa nchini na Makonda, yapigwe mnada ikiwa ni sehemu ya kusimamia sheria na kanuni za kodi zilizopo nchini.

Mbali na Makonda mwenyewe kutoridhia uamuzi huo wa serikali, tayari Rais Dkt. Magufuli amesema sheria za nchi zinasema wazi kuwa ni mtu mmoja tu katika nchi mwenye dhamana ya kutolipa kodi kwa mujibu wa sheria ya fedha, sheria ya madeni, sheria ya dhamana na ya misaada.

Rais Magufuli amesema kuwa hakuna mtu mwingine zaidi ya aliyeruhusiwa kwa mamlaka aliyopewa, “Sasa ukichukua makontena kule, umezungumza na watu wengine labda na wafanyabiashara, unasema ni makontena yako, halafu ukasema tena labda ni ya walimu, wala hata shule hazitajwi, Maana yake nini?”.

Hawa ndio Wajumbe tisa waliopitishwa na UVCCM

$
0
0
Umoja wa Vijana wa CCM unapenda kuujulisha umma wa Watanzania na wanachama wote kwa ujumla kuwa kikao cha Baraza kuu la UVCCM Taifa kilichokutana jana tarehe 31 Agosti, 2018 Jijini Dodoma chini ya Mwenyekiti wake Ndugu Kheri Denice James (MCC) kilifanya Uchaguzi ili kuwapata wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la UVCCM Taifa ambapo wafuatao walichaguliwa:-

Tanzania Bara:-
1.Ndg. Saitoti Zelothe Steven
2. Ndg. Joanfaith John Kataraiya

Tanzania Zanzibar
1.Ndg. Abdulghafar Idrissa Juma
2.Ndg. Mariam Ally Juma

Aidha kilipokea na kuwathibitisha Wakuu wa Idara Tano za Umoja wa Vijana wa CCM Taifa kama ifuatavyo:-

1.Ndg. Peter Kasera-Katibu wa Idara ya Organaizesheni, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.

2.Ndg. Lusekelo Nelson-Katibu wa Idara ya Uchumi, Uwezeshaji na Fedha

3.Ndg. Kamana Juma Simba-Katibu wa Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu.

4.Ndg. Hassan Bomboko
Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi.

5.Ndg.Mohamed Abdalla
Katibu wa Idara ya Usalama na Maadili.

Pamoja na mambo mengine, Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM Taifa liliazimia yafuatayo:-

1.Pongezi kwa Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein kwa kuendelea kuwaamini Vijana katika Serikali zao na kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa mafanikio makubwa.

2.Pongezi kwa Katibu Mkuu wa CCM Taifa Dkt. Bashiru Ally Kakurwa kwa kuaminiwa na kuteuliwa na NEC kushika nafasi hiyo, pamoja na utendaji unaokirejesha Chama chetu katika misingi ya kuasisiwa kwake na maelekezo yake kwenda kutekelezwa kuanzia ngazi ya Tawi.

3.Hotuba ya Katibu Mkuu wa CCM Taifa kupokelewa kama maelekezo kwa Jumuiya yetu, na kufanyiwa utekelezaji kuanzia ngazi ya Tawi.

4.Kupitisha Mpango Mkakati wa Jumuiya unalenga Kujitegemea Kiuchumi na kuimarisha Jumuiya nchi nzima ili kwenda sambamba na dhana ya Siasa ni Uchumi.

5.Tunaitaka Serikali kuendelea kuweka mazingira rafiki kwa Vijanawenzetu waliojiajiri katika sekta isiyo rasmi kama vile Bajaji, Bodaboda, wajasiriamali, wachimbaji wadogo, wavuvi,wapagazi, wakulima, wafanyabiashara wadogo, wasanii, MamaLishe n.k. pamoja na kuweka mazingira rafiki kwa Vijana walioajiriwa viwandani, migodini n.k.

6. Kuitaka Serikali kuweka mazingira rafiki kwa vijana wenzetu wanaohitimu Vyuo Vikuu kupata nafasi za kujitolea katika Taasisi, Idara, Mashirika na Mamlaka ya Serikali pamoja na sekta binafsi ili kupata uzoefu. Pamoja na kutazama masharti ya taasisi za kifedha ya upatikanaji wa mikopo ili waweze kujiajiri.

7. Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM limeazimia kwa Kauli moja kumlinda Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein dhidi ya uharamia wowote Kutoka ndani au nje ya Tanzania.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Mwl. Raymond S. Mwangwala (MNEC)
KATIBU MKUU
01/09/2018

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya Septemba 2

Serikali Kutekeleza Miradi Kwa Kushirikiana Na Sekta Binafsi Yenye Thamani Ya Mabilioni Ya Shilingi

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
Serikali ya Tanzania imepiga hatua kubwa katika kuanzisha na kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo kwa ubia kati ya Sekta ya Umma na  Binafsi (PPP) ambapo miradi  zaidi ya 11 iko katika hatua mbalimbali za utekelezaji lengo likiwa ni  kufanikisha azma ya kuwa na uchumi wa viwanda.

Hayo yamesemwa na Kamishna wa Idara ya  Ubia Sekta ya Umma na Binafsi (PPP),  Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. John Mboya  wakati akiwasilisha mada ya utekelezaji wa dhana ya ushirikishwaji wa sekta binafsi katika miradi ya maendeleo nchini kwenye semina iliyowashirikisha mawaziri, naibu mawaziri na baadhi ya watendaji wa serikali iliyofanyika kwenye ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango jijini Dodoma.

Akiwasilisha mada hiyo, Dkt. John Mboya amesisitiza umuhimu wa kuwepo kwa  umakini mkubwa katika uandaaji na utekelezaji wa dhana hiyo ya ubia Sekta ya Umma na Binafsi kwa kuzingatia sheria, sera, miongozo, kanuni na taratibu mbalimbali zilizopo.

Aidha alizitaka taasisi na wadau wa utekelezaji kuwa tayari kujifunza kutoka katika nchi zilizoendelea kupitia dhana hii ya ushirikikishwaji wa sekta binafsi katika kuchochea ukuaji wa viwanda na uchumi wa nchi kwa ujumla.

Dkt. Mboya aliitaja baadhi ya miradi iliyoko katika hatua mbalimbali ya utekelezwaji kwa Ubia kati  ya Sekta ya Umma na Binafsi kuwa ni  mradi wa mabasi yaendayo haraka (DART), Ujenzi wa Viwanda vya dawa, mradi wa VETA utakaohusisha ujenzi wa vyuo 10 ambavyo vinatarajiwa kutoa ujuzi mbalimbali kwa wanafunzi wapatao 90,000 ili kukidhi mahitaji ya wataalamu watakao saidia kufanikisha uchumi wa viwanda.

“MIradi Mingine ni Ujenzi wa Bandari ya Mwambani, barabara ya Dar es salaam hadi Chalinze, Ujenzi wa Reli kwenye miradi ya Mchuchuma hadi Mbambabay mikoa ya Kusini ya Lindi na Mtwara, Ujenzi wa Reli kuanzia Tanga, Arusha hadi Musoma, na  mradi wa umeme wa Chuo Kikuu cha Dodoma.

Akijibu swali la Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,   Josesph Kakunda, aliyetaka kujua kuhusu kuondolewa kwa sheria ya utekelezwaji  wa miradi kwa Ushirikishwaji wa Pamoja kati ya serikali na sekta binafsi (Joint Venture) ambayo haikufanikiwa kama ilivyokusudiwa hapo awali, Dkt. Mboya alisema kuwa sheria hiyo haijaondolewa bali  miradi hiyo itatekelezwa kupitia sheria ya Kampuni.

Akichangia katika mjadala wa semina hiyo, Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya, alisema ni vema wakati wa kuchagua miradi wahusika wawe makini ili kuepuka kuanzisha miradi inayofanana na ambayo inaweza kuwa chanzo cha kufa kwa miradi iliyotangulia.

“Ninashauri kuwepo kwa fursa ya ushirikishwaji katika miradi midogo ambayo ina manufaa kwa wananchi ikiwemo ya ujenzi wa nyumba za waalimu” Alisema Mhandisi Manyanya

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, alizitaka taasisi ambazo zinatekeleza miradi kwa ubia na sekta binafsi zielezee umma wa watanzania mafanikio yaliyopatikana ili kuhamasisha wadau wengine kufuata nyayo hizo huku  akitolea mfano Shirika la Maendeleo ya Petroli  nchini (TPDC) ambalo nalo liko katika utekelezaji wa dhana hiyo.

Mwenyekiti wa semina hiyo  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, alisema kuwa Serikali imepeleka Muswada Bungeni unaohusu PPP, ambao ukipitishwa na Bunge linalotarajiwa kuanza Septemba 4, 2018, utekelezaji wa ubia huo utakwenda kwa kasi zaidi ili kuiwezesha nchi kufikia malengo yake ya kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya wananchi.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge , Kazi,Vijana, Ajira na Walemavu, Jenister Mhagama, akiahirisha mafunzo hayo, aliwataka wadau wa semina hiyo kuendelea kukutana na kuelimishana hadi hapo marekebisho ya sheria hiyo ya Ubia Sekta ya Umma na Binafsi (PPP) yatakapofanyika.

“Utekelezwaji wa dhana hii ya Ubia Sekta ya Umma na Binafsi ndio njia rahisi itakayosaidia kukamilisha miradi mingi ambayo imeainishwa katika ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapainduzi (CCM) na kwenye Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano, bila ushirikiano huu na sekta binafsi hatuwezi kufikia uchumi wa viwanda kwa kasi inayotakiwa’’ Alisema Waziri Mhagama.

Semina hiyo ya siku moja imeendeshwa na wataalamu wa masuala ya Ubia Sekta ya Umma na Binafsi kutoka Benki ya Dunia, ambapo Jumapili, kamati tatu za Bunge zitapatiwa elimu na kujengewa uwezo kuhusu dhana hiyo ya PPP.

Mizengo Pinda Asema Wapinzani Watapata Tabu sana Wasipojitafakari Upya

$
0
0
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mizengo Pinda ametoa ushauri kwa vyama vya upinzani vijitafakari kwa nini viongozi wao wanawakimbia, vinginevyo watapata taabu sana.

Pinda ametoa ushauri huo aliouita ni wa bure kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Kivule Kata ya Kivule, alipozindua kampeni za Uchaguzi Mdogo wa ubunge Jimbo la Ukonga wilayani Ilala mkoani Dar es Salaam.

Alikuwa akimnadi mgombea wa CCM, Mwita Waitara ambaye alikuwa Mbunge wa jimbo hilo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kabla hajakihama na kurudi CCM hivi karibuni.

“Ajenda yao kuu upinzani ni kunung’unika pekee, watapata tabu sana, sio ile wa wapigwe tu, hii ni watapata tabu sana, wakae chini wajitafakari huu ni ushauri wa bure,” amesema Pinda ambaye ni Waziri Mkuu mstaafu.

Pinda amesema kama wapinzani wataendelea kutoa majibu mepesi katika maswali magumu, wataona linalokuja mbele.

Amemuombea kura Waitara awe Mbunge wa jimbo hilo, huku akimtaka apuuze hoja dhaifu zinazodai kuwa amenunuliwa.

Amesema CCM haikukosea kumteua Waitara, kugombea kupitia chama hicho katika uchaguzi utakaofanyika Septemba 16, mwaka huu.

“CCM haiendeshi mambo yake kiholela, mpeni kura Waitara kwani CCM ilifanya maamuzi ya busara kwa kuzingatia mazingira na kuamua kumrudisha,” amesema.

Aidha, aliwataka wananchi kumuunga mkono Rais John Magufuli kwa kazi yake nzuri ya kupaisha uchumi pamoja na kuendelea kutatua kero za wananchi kila kukicha.

Amewashauri kuwa karibu na mabalozi, ambao ndio watakaosaidia kuomba kura kwa wananchi na pia kuendelea kubaini changamoto za wananchi na kuzitafutia majibu.

Waitara amesema upinzani wana hoja dhaifu kuwa amesaliti wananchi wa Ukonga, wakati wanajua kuwa mambo ndani ya chama hicho yalikuwa hayaendi, jambo ambalo lilimfanya ashindwe kufanya kazi vizuri ya kutatua kero za wananchi.

“Mliponipigia kura nilipata tabu sana, kulikuwa na kero nyingi, lakini mizigo ndani ya Chadema ilikuwa ni mingi wananchi wakiniletea kero zao lazima niongee na viongozi wa serikali ambao wanatoka CCM ili wanisaidie, lakini nikionekana tu na viongozi natakiwa kujieleza,” alisema Waitara.

Amesema ukiwa Chadema, hawataki mtu kusema ukweli hasa kwenye mambo mazuri ambayo yanafanywa na Serikali ya CCM, badala yake wanataka utukane CCM bungeni.

Waitara aliyewahi kuwa Katibu wa UVCCM Mkoa, alisema mpaka sasa katika jimbo hilo lenye kata 13, hakuna hata kata moja ambayo haina miradi inayoendelea kutekelezwa na alipongeza jitihada hizo za serikali.

Amewaomba wananchi wa kata hiyo ya Kivule, ambako aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kivule kumpa kura ili arudi bungeni kuwatumikia na kuwa mtatuzi wa kero zao, kwani sasa atakuwa karibu na serikali kuliko alikokuwa (Chadema).

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Tanzania Bara, Rodrick Mpogolo amesema chama hicho kinakubalika kwa kiwango kikubwa nchini kwa sasa, hivyo wananchi wa kata hiyo na jimbo hilo kiujumla wasipoteze nafasi yao kwa kumchagua mgombea wa chama kingine.

“Na niwaambie tu hii ni awamu ya sita ya Uchaguzi Mdogo toka Uchaguzi Mkuu mwaka 2015, kati chaguzi zote hizo kila ikitokea uchaguzi tunashinda kwa kishindo nawashauri Ukonga msipoteze fursa hii mumchague Mwita Waitara,” amesema Mpogolo.

Mjumbe mwingine wa Kamati Kuu, Makongoro Nyerere amesema hoja ya upinzani kuhusu CCM kuwa na mafisadi na wala rushwa, sasa imepotea na kwamba sasa wala rushwa wakuu ni wao.

Watalii 64 Wawasili Dar Kupitia Reli Ya TAZARA

$
0
0
Na Fatma Salum- MAELEZO
Watalii 64 kutoka nchini Ujerumani wamewasili Jijini Dar es Salaam leo kupitia reli ya TAZARA wakitokea nchini Afrika ya Kusini kwa kutumia treni maarufu ya kitalii ijulikanayo kama ROVOS ya nchini humo.

Watalii hao wamekuja Tanzania kwa ajili ya kutembelea maeneo mbalimbali yenye vivutio vya utalii hapa nchini ikiwemo mbuga za wanyama na visiwa vya Zanzibar.

Akizungumza katika hafla fupi ya kuwapokea watalii hao iliyofanyika stesheni ya TAZARA Dar es Salaam, Meneja Mkuu wa TAZARA Tanzania, Fuad Abdallah alieleza kuwa treni hiyo iliondoka mji wa Cape Town nchini Afrika ya Kusini Agosti 18, mwaka huu.

“Watalii mbalimbali huja nchini mara tano kwa mwaka kwa kutumia ROVOS kupitia reli ya TAZARA na nchi yetu hunufaika na ujio huu hasa faida za kiuchumi,” alisema Fuad.

Aidha alibainisha kuwa treni ya ROVOS ni miongoni mwa treni tatu bora duniani, hivyo ujio wa treni hiyo na watalii unatokana na vivutio bora vya utalii na miundombinu mizuri ya reli ya TAZARA.

“Treni hii inatumia reli ya TAZARA kuleta watalii kwa sababu nchi yetu imekidhi vigezo vya utalii na reli yetu imekidhi vigezo vya usalama na mawasiliano ya uhakika,” aliongeza Fuad.

Alisema kuwa katika safari hiyo ya treni watalii hao pia walipata fursa ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Selous iliyopo kusini mwa Tanzania na kuona wanyama mbalimbali wanaopatikana kwenye hifadhi hiyo.

Wakizungumza kwa furaha ya kuwasili Tanzania, watalii hao wa kijerumani walisema kuwa wamefurahia sana safari hiyo na mapokezi mazuri ya watanzania na kuahidi kurudi kwa mara nyingine.

Kwa upande wake mfanyakazi wa treni ya ROVOS, Monica Rieder mwenye asili ya Ujerumani alisema kuwa amewahi kufika Tanzania mara 14 na anavutiwa na mabadiliko makubwa ya kimaendeleo yanayofanyika hapa nchini siku hadi siku.

TAZARA ni shirika la reli ya pamoja ya Tanzania na Zambia iliyoanza mwaka 1976 na inamilikiwa kwa asilimia 50 kila upande.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images