Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Waziri Mkuu: Ukosefu Wa Uadilifu Uliitia Doa Sekta Binafsi

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ukosefu wa uadilifu ni moja ya eneo ambalo lilitia doa utendaji wa sekta binafsi hususan pale ambapo ilishirikiana na Serikali.

Ameyasema hayo jana (Jumanne, Agosti 28 ,2018) wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 18 wa mwaka wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) kwa niaba ya Rais Dkt. John Magufuli.

Katika mkutano huo uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena, jijini Dar Es Salaam, Waziri Mkuu amesema uadilifu ni changamoto kubwa inayopaswa kufanyiwa kazi na Serikali na TPSF.

“Katika kusisitiza suala la uadilifu, nitoe rai kwamba muwe na mfumo wa kujitathmini,kupeana alama chanya na kuhimizanakuenenda katika misingi bora ya uendeshaji wa shughuli zenu.”

Kadhalika, Waziri Mkuu ameitaka TPSF ijifunze kwa wenzao walioendelea kwa kutokuwa na vitendo vya rushwa, kutoa adhabu kwa wanaoenda kinyume na misingi ya uadilifu walijiwekea.

Amesema kwa kufanya hivyo watakuwa wamejiongezea nguvu yao kama taasisi lakini pia kupeleka ujumbe kwa wanachama wao kuwa wanathamini haki na kuchukia rushwa.

Waziri Mkuu ameongeza kuwa shughuli za sekta binafsi zimeendelea kuongoza katika kuchangia pato la Taifa na ukuaji wa uchumi kwa ujumla.

Amesema kwa mujibu wa takwimu sekta ya utalii inachangia asilimia tisa, huduma asilimia 35, kilimo asilimia 26.6, madini asilimia 3.3 na sekta ya viwanda inachangia takribani asilimia 10.

“Jukumu letu sote ni kuchochea uzalishaji na kufanya wepesi  kwa wajasiriamali wetu watoke nje ya mipaka yetu na kwenda kuuza bidhaa zetu nchi jirani. TPSF mtusaidie katika hili.”

Waziri Mkuu amesema Serikali kwa upande wake itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa kuboresha miundombinu, kutoa vivutio kwenye kodi, kanuni na sheria ili kukuza sekta binafsi.

Hivyo, Waziri Mkuu amesema sekta binafsi nchini nayo haina budi kutumia vema fursa hiyo ya uwepo wa mazingira wezeshi na rafiki kwa kuwekeza kwenye uchumi wa nchi.

Amesema ni vema wakatambua kwamba wana jukumu kuliletea Taifa maendeleo, hivyo wafanye kazi kwa ukaribu na ubia baina yao ili kuhakikisha nchi inanufaika na fursa zilizopo.

Pia amewasihi waendelee kuwekeza zaidi kwenye uzalishaji wa bidhaa za viwandani na wahakikishe kuwa wanajali maisha ya Watanzania ambao ndio soko na wateja wa bidhaa zao.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,


Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Kijazi Amjulia Hali Dkt.kigwangalla MOI

0
0
Na Andrew Chale
Katibu Mkuu Kiongozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Mhandisi John  Kijazi jana tarehe 28/08/2018 amemtembelea na kumjulia hali Dkt Hamisi Kigwangalla ambaye anapata matibabu katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI akiuguza majeraha ya mkono aliyopata katika ajali iliyotokea Agosti 4, mwaka huu Mkoani Manyara.

Balozi Kijazi amempa pole Mh Dkt. Kigwangalla na kumtakia heri na apone haraka ili aweze kurejea kwenye majukumu yake ya kila siku  kwani Taifa linauhitaji mchango wake.

“Pole sana.  Mungu atajalia utapona na utarejea nyumbani mapema, na kwa kuwa wewe ni daktari ukiona hali si nzuri utawafahamisha wenzio mapema ili mjadiliane namna ya kuikabili hali itakayojitokeza” Alisema Balozi Kijazi wakati wa kumjulia pole Hospitalini hapo.

Aidha, Balozi Kijazi amemueleza Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt. Respicious Boniface kwamba kwa sasa wananchi wanaridhishwa na huduma zinazotolewa na MOI na Muhimbili kwa ujumla na hii ni faraja kubwa kwa Serikali na hivyo kuelekeza ari hiyo iendelezwe.

“Pamoja na Jitihada kubwa za Mh Rais Dkt John Pombe Magufuli za kuboresha huduma za Afya hapa nchini, nanyi pia kwa upande wenu mnajitahidi sana na wananchi wanaridhishwa na huduma mnazotoa. Nafahamu kuna changamoto chache lakini bado mmeendelea kufanya kazi nzuri” Alisema Balozi Kijazi.

Kwa upande wake, Dkt Hamis Kigwangalla amemshukuru Balozi Kijazi kwa kumtembelea na kumjulia hali na amemueleza kwamba afya yake imeendelea kuimarika na anaamini katika kipindi kifupi kijacho madaktari watakapojiridhisha wanaweza kumpa ruhusa ya kutoka hospitalini.

“Ninaendelea vizuri, afya yangu inaimarika siku hadi siku, na pia naendelea na mazoezi na kila siku najiona imara zaidi na hii ni ishara tosha kwamba ninaweza kuruhusiwa kurejea nyumbani”  Alisema Dkt. Kigwangalla.

Dkt. Kigwangalla alihamishiwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI tarehe 12/08/2018 baada ya kupata matibabu ya awali katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kwa sasa bado anaendelea na tiba kuuguza mkono wake wa kushoto.

Mtoto Wa Jinsia Mbili Ya Kike Na Kiume Azaliwa Muleba Mkoani Kagera

0
0
Na Dotto Mwaibale, Kagera
Mtoto wa Jinsia mbili ya kike na kiume amezaliwa katika Hospitali Teule ya Rubya iliyopo wilayani Muleba mkoani Kagera.

Kuzaliwa kwa mtoto huyo kumethibitishwa na Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dkt.Geore Kasibante (pichani),  ambaye alisema hali ya mtoto huyo inaendelea vizuri na kuwa wakati wowote atapelekwa hospitali kubwa kwa ajili ya uchunguzi ili afanyiwe upasuaji kwa vile katika hospitali  hiyo hawana madaktari bingwa wa kuweza kufanya upasuaji huo.

Songwe,Kigoma, Mwanza yajipanga kudhibiti Ebola

0
0
Uongozi  wa Viwanja vya Ndege vya Songwe na Kigoma, umejiandaa kwa kushirikiana na maafisa afya, kuhakikisha hakuna mgonjwa mwenye dalili za Ebola anaingia nchini, akitokea maeneo ya Tunduma na nchini Burundi.

Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Songwe, Bw. Pius Kazeze alimwambia Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bi.Bahati Mollel kwa njia ya simu kuwa, tayari Maafisa wa Afya wameshafunga mashine maalum (thermo scanners) inayotambua joto la mwili la abiria ambaye anasafiri kwa kupitia kiwanja hicho, na likizidi 38 anatakiwa kutoa taarifa za afya yake.

Bw. Kazeze amesema Kiwanja cha Songwe ni tofauti kidogo na Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), ambapo zaidi wanakagua abiria wanaoondoka kwa kuwa wengi wanatoka mpakani maeneo ya Tunduma na kwenda maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi.

“Tayari maafisa Afya wamefunga mashine ya ukaguzi wa afya eneo la nje la kuondokea abiria kwani kwetu huku tunapata abiria wengi wanaotoka nchi jirani wanaopitia mpakani Tunduma, hivyo wengi wao wanatoka nchi zinazopakana na Kongo, ambayo inasadikika ugonjwa wa Ebola umeibuka kwa kasi kubwa,” alisema Bw. Kazeze.

Hatahivyo, amesema mbali na mashine hiyo kubwa iliyowekwa sehemu maalum, pia wanamashine mbili ndogo zinazotumiwa kwa kushikwa mkononi na maafisa Afya, lakini wanakabiliwa na changamoto ya uhaba wa Watumishi wa afya, ambao tayari wameshaomba kuongezewa mmoja ili kufanikisha kazi hiyo kuwa rahisi.

Naye Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Kigoma, Bw. Theophan Bileha amesema wapo mbioni kiweka kifaa hicho kwa kuwa wanatarajia abiria kutoka Burundi watakaowasili kwa ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), itakayoanza safari zake kuanzia Agosti 30, 2018.

“Tumeshafanya kikao na wenzetu wa Afya, na wameahidi kuleta mashine mojawapo, tunatarajia abiria wanaotoka Bujumbura, kwani tumeambiwa ATCL itaanza kwenda huko kuanzia tarehe 30, na hawa wapo watakaoshuka hapa na wengine wanakwenda kwenye viwanja vingine kulingana na ratiba ya ndege hii,” alisema Bw. Bileha.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kigoma, Dk. Peter Nsanya amesema mashine hiyo itawekwa kiwanjani hapo kwa kipindi, ambacho ndege zinatua na baada ya ratiba za ndege kumalizika, wanahamishia eneo la Bandarini kwa kuwa pia kuna abiria wanaotoka maeneo mbalimbali.

“Sisi tumejipanga kukabiliana na maradhi haya ikiwa na kuhakikisha hatutaruhusu uingie nchini, na ndio maana tunaratiba za ndege, ambapo tutakuwa tunakwenda kutoa huduma, na baadaye kuhamia bandarini,” amesema.

Meneja wa Kiwanja cha Ndege cha Mwanza, Mohamed Maulid amesema wamejiandaa kwa kushirikiana na Maafisa Afya wamekuwa wakitumia mashine ya mkono kwa ukaguzi wa abiria wanaotoka nchi za Uganda, Nairobi na Kongo.

Ugonjwa wa Ebola unaosambazwa kwa virusi vya Ebola, husababisha homa kali inayoweza kuambatana na kutokwa damu mdomoni, puani, masikioni, machoni na sehemu nyingine za wazi na unaenea kwa haraka. Hivi karibuni  umetangazwa kutokea nchini Kongo na kusababisha vifo.

Dalili za Ebola ni pamoja na homa kali, maumivu ya kichwa na misuli, mwili kulegea, kutapika, kuharisha, vipele na kutokwa damu.

Juzi Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) kilitangaza kuchukua hatua kali za kuweka zuio kwa abiria wanaongia nchini kupitia Kiwanja hicho, ambapo kumefungwa vifaa ambavyo vinabaini joto la abiria na endapo litazidi nyuzi joto 38, atatakiwa kutoa maelezo zaidi ya maisha yake.

Pia abiria wote wanaowasili kwa ndege zinazotoka nchi jirani na Kongo wanatakiwa kupitia eneo maalum ambalo hutakiwa kunawa mikono yao kwa dawa maalum ili kuua vijidudu mbalimbali.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO CHA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA (TAA)

Sugu Alivyomwaga Machozi Akisoma Wasifu wa Mama Yake....."Afya ya Mama Ilibadilika Baada ya Mimi Kufungwa"

0
0
MBUNGE wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu), alishindwa kujizuia na kujikuta akiangua kilio na kumwaga machozi alipokuwa akisoma wasifu wa marehemu mama yake, Bi. Desderia Lungu Mbilinyi wakati wa ibada ya kuaga mwili wa mama huyo.

Bi. Desderia Mbilinyi alifariki dunia Jumapili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa kwenye wodi ya wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) akipatiwa matibabu.

Hilo lilijiri  jana Agosti 28, katika Kanisa Katoliki lililopo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.

Akisoma wasifu wa Desderia aliyezaliwa Desemba 25, 1956, Sugu alisema maisha ya mama yake kwa sehemu kubwa alikuwa mkulima mdogo na alikuwa mjane toka mwaka 1992.

“Mama alikataa kuolewa tena na kujikita kanisani akiwa ni mwana Karistimatiki Katoliki.

“Februari (2018) wiki moja baada ya mimi (Sugu) kufungwa, mama yangu bado aliendelea kuamini kuwa nilifungwa kwa kuonewa,” alisema Sugu.

Alisema baada ya hapo, afya ya mama yake ilibadilika na alianza kuugua shinikizo la damu lililozidisha tatizo alilokuwa nalo awali la figo.

Alisema mama yake alianza kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Mbeya, Julai alihamishiwa Muhimbili kwa matibabu zaidi hadi Agosti 26, alipofariki dunia.

Sugu akitumia Biblia, alisoma Waraka wa Timotheo 4:7 na kusema “Mama yangu amevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo ameumaliza, Imani ameilinda."

Baada ya kusema hivyo alishindwa kuendelea kuusoma wasifu huo na kububujikwa machozi, hali iliyosababisha waombolezaji wengine nao kuanza kutokwa na machozi.

Desderia ameacha watoto wa kuzaa watano na wa mumewe watatu.

"Natoa shukrani kwa madaktari wa Rufaa Mbeya, Taasisi ya Jakaya Kikwete na Kitengo cha Figo hapa Muhimbili," alisema Sugu.

Baadhi ya viongozi waliohudhuria misa hiyo ya maziko ni pamoja na Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye, Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita, Meya wa Ubungo, Boniface Jacob na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema-Zanzibar,  Salum Mwalimu.

Desderia anatarajiwa kuzikwa nyumbani kwake jijini Mbeya leo .

Kuanzia Septemba 5 Visimbuzi ( Ving'amuzi) Kuonesha channeli za ndani BURE

0
0
Na. Immaculate Makilika na Bushiri Matenda- MAELEZO
Serikali imesema kuanzia septemba 5, mwaka huu visimbuzi vitaanza kuonesha channeli zote za ndani bila kutoza gharama yoyote kwa mtazamaji.

Akiwaeleza waandishi wa habari jana jijini Dar es salaam, kuhusu yaliyozungumzwa katika  kikao kati ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe na wadau na wamiliki wa televisheni nchini, Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi amesema kuwa serikali imefikia uamuzi huo baada ya visimbuzi vya AZAM, ZUKU na DSTV kutoonesha channeli za ndani, kulingana na aina ya leseni zao.

“Ningependa watanzania wafahamu kwamba kuanzia septemba 5 mwaka huu, visimbuzi vya Ting, Starmedia, Continental na Digtek vitaonesha takribani channeli  34 za ndani bure, ili kutoa fursa ya kila mwananchi kuwa na  haki ya kupata taarifa” alisema Dkt. Abbasi

Aidha, alielezea kuwa wadau hao na wamiliki wa televisheni wameonesha kuridhishwa na hatua hiyo  kwa vile Serikali imetengeneza miundombinu itayoruhusu channeli zao kuonekana nchi nzima.

Dkt. Abbasi, alisisitiza kuwa “nchi imeandaa mfumo, ambao unaweza kufanyakazi bila kutegemea kampuni kutoka nje ya nchi kwa ajili ya kuonesha channeli za ndani au matangazo, kwa hivyo wadau au wamiliki wa vyombo vya habari wasihofu kuhusu hilo”

Kikao kati ya Waziri Mwakyembe na wadau  na wamiliki wa televisheni  nchini, kimefanyika kwa lengo la kuwa na majadiliano ya pamoja baina serikali na wadau hao ili kupata muafaka kuhusu kutooneshwa kwa chaneli za ndani katika visimbuzi vilivyokiuka masharti ya leseni zao.

Aidha, kikao hicho pia kilihudhuriwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Injinia James Kilaba, pamoja na wataalamu wake.

Je ni Kweli Mr. Nice Kakwama Uganda baada ya kutoswa na Promota?

0
0
Kuna taarifa kuwa msanii Mkongwe wa Bongo Fleva, Mr. Nice amekwama Kampala Uganda baaada ya  promota Abtex wa Abtex Promotion kushindwa kumlipa fedha msanii huyo ambaye walikubaliana kuwa angetumbuiza kwenye tamasha la  Ekyeppukulu, June 24, 2018 kwenye uwanja wa Namboole

Kutoka wakati huo (mwezi Juni) kumekuwa na uvumi kuwa Mr. Nice amekwama Kampala baada ya Abtex kushindwa kumlipa fedha zake.

Taarifa zinaeleza kuwa Mr. Nice alifikia kwenye hotel Sport View ndani ya Kirenga ambapo alikaa hapo kwa siku kadhaa kwa ajili ya tamasha hilo, hata hivyo taarifa nyingine zinadai kuwa muimbaji huyo kabaki Kampala kwa ajili ya shughuli zake za kimuziki.

Hata hivyo pia katika video iliyowafikia Mseto East Africa, Mr. Nice alijibu yote yanayozungumzwa kuhusu yeye kukwama Kampala.

"Kuna  uvumi kwamba Mr. Nice amekwama Kampala, ninaweza kukwama kwenye eneo langu?  Abtex hakunilipa hata asilimia moja. Huyu jamaa alipotea kabisa na nilipata mateso lakini Mr. Nice ni jina kubwa hivyo nikajitenga kwenye hali hiyo mwenyewe, haikuwa vizuri kwa wao kunifanyia hivi" amesema.

Ili kuthibitisha zaidi kwamba wanaomkosoa/kumbeza kuhusu hilo hawapo sahihi, Mr. Nice alionyesha gari aina Range Rover 2018 ambayo anaendesha kila siku akifurahia maisha Uganda huku bado akiendelea kuishi kwenye Hotel.

Dr Kanengo: Bingwa Wa Tiba Asili Hutibu Matatizo Yafuatayo

0
0
NKURURU:-ni dawa inayotibu miguu kuwaka moto, kiuno tumbo kupooza kupoteza fahamu 

MALABALA; hutibu kisukari , uti wa mgogo, Change, pumu, busha, kaswende, kifua kikuu, muwasho sehemu ya siri 

NKURUNGU,: Ni dawa kutibu  N, B, G, POWER :-ni dawa ya kuongeza nguvu za kiume ni vidonge 20 

MPERAMPERA:- ni dawa ya kurudisha Mke, mme, mpenzi,mchumba aliyekuacha /kuteseka, ni kwa mda wa siku 2 tu kusafisha , pia kuna dawa za kupunguza vitambi(nyama uzembe), maziwa makubwa,michirizi, mikovu makubwa, chunusi sugu. 

NR SIX POWER:-inatibu upungufu wa nguvu za kiume kwa wasio weza kumudu tendo la ndoa itakufanya uwe na hamu ya kurudia tendo la ndoa zaidi ya Mara 4 bila hamu Kuisha, inaboresha maumbile madogo na inaimarisha misuri iliyo legea na kusinyaa una pona kabisa, ndani ya siku 4 tu 

GASELA:-ni dawa ya maajabu (9) yaliyoshindikana. (1)-Kisukari, vidonda vya tumbo, tezi dume,walioshindikanika kupata watoto(ugumba),busha bila oparesheni, (2)zindiko Kali Katika biashara yako (chuma ulete) ndo kiboko yao kumkamata mwizi aliye kuibia vitu vyako pikipiki, gari, n, k( 2)zindiko la nyumba, mashamba, viwanja,.(4)kukutolea sumu uliyo ikanyaga (Mtego) (5)ujiamini kutumia dawa ya maajabu Saba (6)kutoa mikafara mfano ugomvi ndani ya nyumba kufukuzwa kazini bila sababu (7)kutabiri nyota na kung'arisha (8)kurudisha Mali iliyo potea mazingira ya kutatanisha, kushinda kesi uliyo sumbuka nayo mda mrefu. (9)kufukuza majini wachafu ndani ya mji,.

Haya yote yanawezekana kwa DR KANENGO popote ulipo . Muone  DR KANENGO,anatibu nguvu za kiume anarefusha na kunenepesha uume kwa saizi uipendayo kwa muda mfupi sana, pamoja na kuwa na hamu ya kurudia tendo la ndoa mara 4 bila hamu kuisha Na utachelewa kufika kileleni kwa muda wa dakika 40 bila kuchoka .

Angalizo usitume meseji wala kubipu..
 
You can get it in all East African countries,,our service is fast and easy... contact Whatsapp 0784,47,59,46.Dar es salaam Tanzania. ,..Dr. KANENGO 0744,92,29,82...You are welcome. Yuko pia Khahama Mjini, Bunda kwa sasa

Tatizo La Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Na Maumbile Madogo

0
0
Tatizo La Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Na Maumbile Madogo Ya Uume Limekuwa Kubwa Kwa Lika Zote Hapa Kwetu Na Duniani Kote. Tatizo Si Tatizo Bali Ni Iletiba Sahihi Ya Matatizo Haya Chanzo Chake Na Visababisho Vyake.

DALILI;mwili kuchoka, maumivu ya mgongo na kiuno, kutopata choo vizuri hata ukipata choo kinakuwa kigumu au gololi kama mavi ya mbuzi. misuli ya uume kulegea na kusinyaa hata uume kulegea na kushindwa kufika kileleni. miguu kuuma na kuwaka moto.

 TIBA YAKE;LUKUBA 4mix ni dawa pekee inayoweza kutibu matatizo hayo inarudisha nguvu za kiume mara dufu na kufanya urudie tendo la mara tatu bila kuchoka. 

LUKUBA 3 pump; ni dawa inayorefusha na kunenepesha uume hadi inchi 7 hadi 9 na kunenepesha kwa CM 2 na kukupa umbile la uhakika. ITUMIE TIBA HII KUOKOA NDOA YAKO NA KUOKOA KUKIMBIWA NA UMPENDAYE,

 ISABILO; Ni dawa itoayo mafanikio na utajili kwa watu walioshindwa kufanikiwa kimaisha, 

MWITE; Ni dawa ya mvuto kumvuta umpendaye na kumrudisha aliyembali na atakutimizia ahadi zote awe mwanamke au mwanaume. 

LUTA CD; Ni dawa inayotibu magonywa nyemelezi yanayopunguza kinga za mwili na kusababisha mwili kuzoofu na inaondoa miwasho na kuondoa kemikali na taka zinazozagaa mwilini. 

KISUKARI; Tunayo dawa ya DAYON inayotibu na kuzalisha insulin kwa wingi na kumfanya mwenye tatizo hili kupona kabisa ugonjwa wa kisukari, kwani husababisha misuli ya mwili kutokufanya kazi vizuri

MPIGIE DR DAGOTIMAN NDIYE SULUHISHO LA MATATIZO YAKO   0658920640/ 0754372325 / 0620806813
 
HUDUMA HII INAWEZA KULETWA POPOTE ULIPO OFISI ZETU ZIPO MBAGALA ZAKHEM DAR ES SALAAM.

Huna Sababu Ya Kuaibikatena............ Jipatie Dawa Bora Ya Nguvu Za Kiume, Maumbile Madogo Na Mvuto Wa Mapenz

0
0
Usikate tamaa ondoa maradhi yako, maana matatizo haya yamekua yakiasili watuwengi kisaikolojia hasa baada ya kujiona wako tofauti sana na wengine kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia (6-8) vinginevyo mtuhuyo anamapunguvu katika mwiliwake.

Kunasababu nyingi sana zinazosababisha matatizo haya, chango hushambulia never ambayo huasili misuli ya uume, Ngili :- hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kufanya tumbo kuunguluma na kujaa gesi, kolodani moja kuvimba au kuingia ndani pamoja na kutopata choo vizuli. Sababuhizi na nyingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba na marakwamara husababisha kukosa hamu ya kuludia tendo la ndoa na baadae kushindwa kabisa

MASISA 3POWER :- nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa mfumo wa vidonge, huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka 15-90 , inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii) inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa, itakufanya uludie tendo la ndoa zaidi ya mara nne (4) birahamu kuisha wara kuhisi kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya dk (20-30 )

YONINANI:- hurefusha na kunenepesha maumbile madogo ya uume uliosinyaa inchi 6-8 na unene wa sm 3-4 kwa mda mfupi sana,

SUPER MORINA :- nidawa inayotibu ama kutatua tatizo la kisukali kwawaliohangaika bila mafanikio, huondoa tatizo la kisukali na kupona kabisa, vilevile ninadawa ya magonjwa sugu km vile presha, vidondo vya tumbo, miguu kuwakamoto, muwasho mwilin, kaswende,uzazi nk.

LUGIMBA :- nidawa ya mvuto wa mapenzi, humtuliza mke, mme, mchumba, hawara au mtu yoyote umpendae na kumfanya akutimizie chochotekile unachokitaka kutoka kwake na kumfunga asiwe na mtu yoyote zaidi yako.

WASILIANA NA DR CHIPUPA NAPATIKANA DAR ES SALAAM KUMBUKA HUDUMAHII ITAKUFIKIA POPOTE ULIPO  0759208637 / 0622344969

Kama Dalili Hizi Unazo Upo Kwenye Hatari Ya Kuishiwa Nguvu Za Kiume Kabisa

0
0
Una dalili zifuatazo?
1: Kushindwa kurudia tendo la ndoa
2: Kutojisikia hamu ya tendo la ndoa
3: Maumivu ya kiuno mgongo
4: Tumbo kuunguruma na kujaa gesi
5: Uume kusinyaa, kuingia ndani na kuwa mdogo au mfupi
6: Korodani moja kuvimba

KAMA DALILI HIZI UNAZO UPO KWENYE HATARI YA KUISHIWA NGUVU ZA KIUME KABISA

Kwa matibabu tumia OZYMIX POWER-dawa bora ya nguvu za kiume ya miti shamba ambayo haina kemikali ambayo itakuwezesha kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara tatu bila hamu kuisha.
Pia tunatoa huduma hizi:>

1.Dawa ya Kuondoa michirizi
2.Kumrudisha mwanaume aliyekuacha 
 
Tunapatikana KAWE UKWAMANI karibu na kituo cha mabasi.
KWA MAWASILIANO ZAIDI ; 0716096205 /0756726865 FIKA OFISIN AU PIGA SIMU NA UTALETEWA DAWA POPOTE ULIPO DAR ES SAALAM NA KWA MIKOANI TUNATUMA KWA NJIA YA MABASI.

TEMBELEA KATIKA BLOG YETU HAPA>>>;

Viwanja Vikubwa, Vimepimwa Na Vinauzwa: Bunju Na Mapinga (Baobab Sec)

0
0
Kwa upande wa Bunju, viko viwanja 2 vya ukubwa wa sqm 1700 kila kimoja na ukiviunganisha utapata kiwanja kimoja kikubwa zaidi cha sqm 3400 kwa bei ya sh 45 milion kwa kimoja  sawa na 90 milion kwa viwanja vyote viwili. Viwanja hivi vimegusa barabara kuu (Bagamoyo road) na tayari viko fenced.

Kwa upande wa Mapinga (Baobab secondary, Kimele na Vikawe), viko viwanja vingi, vya size tofauti kama ifuatavyo: sqm 3018 kwa tsh 39m, sqm 2386 kwa tsh 31m, sqm 1985 kwa tsh 25m, sqm 1573 kwa tsh 20m, sqm 1400 kwa tsh 20m, Kiharaka beach sqm 1000 kwa tsh 18m, sqm 800 kwa tsh 8m, sqm 400 kwa tsh 4m.

Ruksa kulipa kwa awamu 2 ndani ya miezi 3. Kianzio ni 50%

Viwanja vyote vimepimwa na hati ziko Halmashauri, unapatiwa ndani ya mwezi mmoja tu. Viwanja viko umbali wa km 3 kutoka Main road. Barabara, maji na umeme vipo sawa.

Hakuna dalali, mpigie mhusika: call 0758603077, whatsap 0757489709

Kamanda wa Polisi Mwanza afunguka kisa cha mtawa kujirusha ghorofa ya tano

0
0
Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, Jonathan Shanna amezungumza na kutaja chanzo cha kifo cha marehemu, Mtawa Bartholomew aliyekuwa Mkurugenzi wa Fedha na Mipango katika hospitali ya Rufaa Bugando (BMC), kilichotokea jana asubuhii mara baada ya mtawa huyo kujirusha kutoka ghorofani ya tano.

Mtawa huyo aliamua kujiuua kutokana na kesi inayomkabili ya upotevu wa fedha kiasi cha shilingi milioni 380 zilizobainika kupotea.

“Hadi sasa tunaweza kusema kifo chake kimetokana na tukio la upotevu wa fedha katika ofisi yake, akiwa kama mkuu wa kitengo cha fedha tulimkamata na kumhoji kwa siku kadhaa kuhusiana na upotevu huo wa fedha na kumuachia kwa dhamana, hivyo wakati akijirusha kujiua alikuwa nje kwa dhamana,” amefafanua.

Kamanda Shana amesema siku chache kabla ya kifo chake mtawa huyo alikamatwa na kuhojiwa pamoja na watumishi wengine nane ambao walikuwa wakikabiliwa na tuhuma za ubadhirifu wa fedha zaidi ya Sh milioni 380 za hospitali hiyo.

Mwalimu Anayedaiwa Kuua Mwanafunzi kwa Kipigo Atiwa Mbaroni

0
0
Polisi mkoani Kagera inamshikilia mwalimu Respicius Patrick wa shule ya msingi Kibeta akituhumiwa kusababisha kifo cha mwanafunzi wa darasa la tano, Siperius Eradius.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augustino Ollomi alisema kifo cha mwanafunzi huyo kilitokea jana akipelekwa hospitali.

Alisema Patrick (50), ambaye ni mwalimu wa nidhamu anadaiwa kumpiga mwanafunzi huyo akihusishwa na upotevu wa mkoba wa mwalimu Herieth Gerard (46) uliokuwa na Sh75,000 na vitambulisho vyake. 

Hata hivyo taarifa kutoka eneo la tukio na kwa baadhi wa wanafunzi wa shule hiyo, wakati mwanafunzi huyo akiendelea kuadhibiwa, pochi ikiyodaiwa kuibwa ilipelekwa shuleni hapo na mwendesha pikipiki aliyemsafirisha mwalimu Herieth wakati akienda kazini, akidai aliisahau. 

Baba wa mwanafunzi huyo, Justus Balilemwa alisema alimchukua mtoto huyo kituo cha watoto yatima cha Ntoma baada ya mama yake kufariki dunia akijifungua.

Mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa Mkoa wa Kagera, Dk John Mwombeki alisema uchunguzi wa awali wa mwili wa mwanafunzi huyo unaonyesha alama zinazohusishwa na kupigwa.

Kauli ya Simbachawene baada ya kuchaguliwa kumrithi Ghasia Aliyejiuzulu Jana

0
0
Mbunge wa Kibakwe(CCM), George Simbachawene amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti huku akiahidi kuongoza kamati hiyo kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizopo kwa maslahi ya Taifa.

Simbachawene amechaguliwa jana kushika nafasi hiyo baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa kamati hiyo Hawa Ghasia kujiuzulu.

Aidha Mbunge wa Maswa Mashariki (CCM)Mashimba Ndaki naye amechukua nafasi ya Makamu Mwenyekiti iliyoachwa na Jitu Son ambaye pia alijiuzulu.

Akizungumzia kuchaguliwa kwake, Simbachawene amesema jana aliteuliwa na Spika wa Bunge Job Ndugai kuwa mjumbe wa kamati hiyo baada ya kuhamishwa kutoka Kamati ya Katiba na Sheria.

“Nilipofika kamati ya Bajeti nikaambiwa Mwenyekiti na Makamu wake wamejiuzulu  basi nikapata Interest ngoja nigombee na wajumbe wamenipitisha kwa kauli moja nataka niseme tu kwamba kamati ile nafahamu ni kamati muhimu katika mhimili wa bunge na serikali,”amesema.

Amesema misingi ya uendeshaji wake ipo kwa mujibu wa kanuni, taratibu na sheria hivyo atasimamia sheria zote zinazosimamia sheria.

“Pia tutafanya majukumu yetu kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizopo lakini pia kwa maslahi ya Taifa,”amesema.

Mwenyekiti huyo amesema haoni kama ni mzigo mkubwa sana kwake kwa kuwa anachojua kazi yake ni kukusanya mawazo ya wajumbe ili kutoa ushauri kwa sababu kazi ya Bunge ni kutoa ushauri kwa serikali.

Lowassa, Mangula Kuwasha Moto Monduli Leo

0
0
Vyama vya CCM na Chadema, leo vitapimana ubavu katika uzinduzi wa kampeni za ubunge wa Monduli jijini Arusha katika mikutano miwili tofauti ya kampeni.

Kampeni za ubunge wa jimbo hilo ambalo lilikuwa CCM tangu uhuru, hadi mwaka 2015 lilipochukuliwa na Chadema zinatarajiwa kuwa za aina yake.

Julai 30, aliyekuwa mbunge wa Monduli (Chadema), Julius Kalanga alijiuzulu na kujiunga na CCM na chama hicho tawala kikampitisha kuwania tena ubunge wa jimbo hilo na sasa atachuana na Yonas Laiser wa Chadema.

Katika uzinduzi wa leo, Chadema watakuwa katika mji wa Mto wa Mbu, na kampeni zao zitazinduliwa na waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa ambaye ndiye mwenyekiti wa kamati ya kampeni za Chadema katika jimbo hilo akiwa na wabunge na viongozi wengine wa chama hicho.

Upande wa CCM, kampeni zitazinduliwa na makamu mwenyekiti wa CCM-Bara, Philip Mangula, Monduli mjini.
 
Katika uchaguzi huo, wagombea wengine katika jimbo hilo ni Omar Kawanga (DP), Feruzi Juma (NRA), Simon Ngilisho (Demokrasia Makini), Francis Ringo (ADA-Tadea) Elizabeth Salewa(AAFP) na Wilfred Mlay (ACT-Wazalendo).

Mwalimu Kizimbani Kwa Kumbaka Mwanafunzi

0
0
Mwalimu wa Shule ya Sekondari Engusero wilayani Kiteto, mkoani Manyara, Henry Michael (30), amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kiteto kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wa Kidato cha pili (16).

Mwendesha mashtaka wa polisi, Inspekta Mbaruku Makame, amedai mahakamani hapo leo Jumatano Agosti 29, kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 26, mwaka huu saa mbili usiku shuleni hapo baada ya mwanafunzi huyo kutumwa baadhi ya vifaa nyumbani kwa mtuhumiwa huyo.

Amedai mwanafunzi huyo alikuwa anaishi bweni na wenzake ambapo usiku wa siku hiyo mtuhumiwa huyo alimtuma aende nyumbani kwake kuchukua vifaa vya shule ndipo akamfuata nyuma na kumbaka  kichakani.

Baada ya kusomewa shitaka hilo mshtakiwa amekana na kurejeshwa rumande kwa kushindwa kutimiza msharti ya dhamana yaliyotaka kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya Sh milioni mbili na kesi imeahirishwa hadi Septemba 5, mwaka huu.

Ommy Dimpoz Kafunguka Kila Kitu Kuhusu Ugonjwa Wake....Anasema Alilishwa Sumu Bila Kujua

0
0
Vipimo  vya afya alivyofanyiwa msanii wa Bongofleva, Omary Nyembo maarufu kama Ommy Dimpoz ambaye yupo nchini Afrika Kusini kwa matibabu, vimeonyesha aliwekewa sumu kwenye chakula.

Ommy Dimpoz alianza kuugua mapema Mei mwaka huu na kwenda kutibiwa mjini Mombasa kabla ya kupelekwa Afrika Kusini ambako aligundulika kuwa na tatizo katika njia ya chakula ambako alifanyiwa upasuaji.

Akizungumza na Kituo cha Redio cha Clouds, Dimpoz, alisema vipimo vya madaktari vimeonyesha tatizo lake linatokana na kuwekewa sumu kwenye chakula ama kinywaji.

“Awali nilifanyiwa vipimo katika moja ya hospitali jijini Dar es Salaam na kugundulika nina kansa, lakini baada ya vipimo vikubwa huku Afrika Kusini, imeonekana nimekula sumu,”  alisema Ommy Dimpoz.

Alisema anashukuru kuona hali yake imeanza kuimarika baada ya awali kushindwa kuzungumza kabisa na anaamini sala za Watanzania wenzake na watu ambao wamekuwa karibu naye zitamsaidia na kuweza kurejea kwenye hali yake.

Akizungumzia kuhusu namna upasuaji wake ulivyofanyika na kusababisha kukaa Chumba cha Uangalizi Maalumu ICU kwa muda wa wiki tatu baada ya mapafu yake kuleta shida, Dimpoz amesema;

“Baada ya kufanyiwa upasuaji kulikuwa kuna matatizo, mapafu yakawa hayafanyi kazi vizuri, kwahiyo baada ya kutoka kwenye upasuaji nikapelekwa ICU (chumba cha wangojwa mahututi) hali ilibadilika kwa sababu upasuaji walisema ni masaa 4 lakini yakaenda mpaka masaa 11. Kwa hiyo nikaa ICU kwa wiki tatu baada ya pale nikahamishiwa wodi ya wangonjwa ya kawaida muda ukafika wakaniruhusu bwana unaweza kwenda lakini unatakiwa kurudi baada miezi 3,”

Kuhusu sauti kubadilika alisema, “Side effect ya upasuaji huu sauti inaweza kwenda na kurudi, kwahiyo hivyo vitu tayari nilishaambiwa. Sometime nakuwa nipo fresh some time ndio inakuwa hivyo lakini wakati nipo mapumzikoni Kenya nilijaribu kuingia studio. Mabadiliko mengine tumbo langu sasa hivi limeamishwa limevutwa juu, kwahiyo hata nikila nashiba haraka nikila kidogo,”

Muimbaji huyo amesema bado hajajua ni sumu ya aina gani ambayo ametumia au amelishwa.

Katika hatua nyingine amesema baada ya kufika hospitali nchini Afrika Kusini safari hii aliwaeleza madaktari jinsi anavyojisikia na kufanyiwa vipimo.

“Walivyonipima wakakuta ndani kuna usaha mwingi sana, akaseama inabidi tukutoboe pembeni ya tumbo tuunyonye, kwahiyo kuutoa siku ya kwanza wakatoa lita moja, wakaendelea mpaka mambo yakakaa sawa,” alisema Ommy.

Makanga 3 Power; Dawa Bora Nguvu Za Kiume

0
0
Kutibu nguvu za kiume dakika(10) na kupona muda wa siku tatu tuu. Kuimarisha misuli ya uume uliolegea, pia ipo Dawa ya kurefusha uume mfupi inchi NNE hadi saba na kunenepesha uume mfupi sentimita NNE.

Tiba ya kudumu kutibu maumivu ya mgongo,kiuno, tumbo kuunguruma na kujaa gesi, kupata choo vizuri, na kutibu uzazi, kutibu busha bila operesheni, kisukari, presha ,miguu kuuma, uzazi, fangas sugu, vidonda vya tumbo.

Ni docta bingwa wa kutibu magonjwa sugu, kutoa ndagu za utajiri kwa kutumia Pete, kazi ,cheni, mikufu maalumu ya bahati, una kesi umedhulumiwa Mali au pesa? Zitarudi muda wa Masaa matatu tuu.

Onana na Dr shilindes shida zako zote zitakwisha, anatoa Dawa za utajiri kwa wafanyakazi, wakulima, na wafugaji, wafanyabiashara na wachimba madini kwa kutumia pete, kazi kwa yeyote anaetaka kuwa na pesa nyingi.

Pia anaboresha akili kwa wanafunzi darasani, masomo na kufaulu mitihani pia kushinda bahati nasibu yeyote.

Pia tunatoa Dawa kumrudisha Mume, mke, mpenzi, hawara, kwa muda wa SAA moja tuu, na kuomba msamaha kwa kukupigia magoti na yeyote yule, unaemtaka kimapenzi au kuoana, utampata na kumfunga asitoke nje ya ndoa daima na kutekeleza shida zako zote. Kupunguza unene, kupunguza matiti makubwa, tumbo na nyama uzembe muda wa siku sita unapata saizi uipendayo.

Kutoa makovu mwilini, chunusi, upele na mabaka, pia tunayo Dawa ya kuongeza hipsi, makalio, mguu wa bia na kupata shepu safi kwa muda wa siku saba tuu.

Wa mikoani mtapata huduma popote mlipo.
Tupo dar es salam mbagala rangi tatu.

Mawasiliano simu namba: 0784 460 348. Au 0659 103 360.

Kauli ya Serikali kuhusu mwanafunzi aliyefariki kwa kipigo cha Mwalimu

0
0

Waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako amezungumzia tukio la kuuawa kwa mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi Kibeta, mkoani Kagera Siperius Eradius akitaka vyombo vya usalama kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mwalimu anayetuhumiwa.

Akizungumza leo Agosti 29 wakati wa Kongamano la Kimataifa la Hisabati linalofanyika Chuo Kikuu cha Aga Khan, Profesa Ndalichako amedai kusikitishwa na tukio hilo na kwamba Serikali haitamfumbia macho yeyote atakayebainika kuhatarisha usalama wa wanafunzi shuleni, wakiwamo walimu wao.

Amesema mwalimu aliyesababisha mauaji hayo hakutumwa na mtu isipokuwa utashi wake.

Profesa amewaomba wananchi kuwa watulivu wakati vyombo vya usalama vinapofanya kazi yake na kwamba tukio hilo lisitoe tafsiri kuwa shule  siyo mahali salama kwa watoto.
 
 Shule ni sehemu ambayo ni salama kwa hiyo asitokee mtu akafanya vitendo ambavyo hata wazazi wajiulize harugusu mtoto kwenda shule au asiende lakini serikali itachukua hatua kwa mtu yeyote atakayefanya shule ionekane si mahali salama‘-Waziri Ndalichako

Siperius (13) anadaiwa kuuawa kwa kupigwa na mwalimu akituhumiwa kuiba pochi ya mwalimu.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images