Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Hatima ya Nondo Kujulikana leo Mahakamani

$
0
0
Mahakama ya Wilaya ya Iringa  leo inatarajia kusoma hukumu ya kesi ya Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo.

Nondo anakabiliwa na mashtaka mawili likiwamo la kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni Machi 7, mwaka huu akiwa eneo la Ubungo, Dar es Salaam na kuzisambaza kupitia mtandao wa kijamii wa Whatsapp kwamba yupo hatarini.

Katika shtaka la pili, anadaiwa kutoa taarifa za uongo kwa mtumishi wa umma Mafinga alipokuwa anatoa taarifa kwa askari kwenye Kituo cha Polisi Mafinga kwa kusema kuwa alitekwa na watu wasiojulikana Dar es Salaam na kupelekwa Kiwanda cha Pareto Mafinga.

Katika kesi hiyo Nondo anatetewa na mawakili wawili wakiongozwa na Jebra Kambole chini ya mtandao wa watetezi wa haki za binadamu nchini (THRDC).

Kauli ya Kwanza ya Ommy Dimpoz Baada ya Kurudishwa Tena Hospitalini Afrika Kusini

$
0
0
Baada ya dua nyingi kutoka kwa wasanii ndugu jamaa na marafiki wa Msanii Omary Nyembo alimaarufu Ommy Dimpoz,ambaye yuko nchini Afrika ya kusini kwa ajili ya matibabu, jana jumapili  ametoa taarifa juu ya hali yake ya kiafya.

Msanii huyo ameamua kutoa taarifa kupitia Insta story yake kwa kile kilichopelekea mashabiki na watu wote kutaka kujua maendeleo ya kipenzi chao Ommy Dimpoz kwani zilisambaa taarifa kuwa yuko mahututi na yupo kwenye chumba maalumu cha (ICU).

Diamond, Mbosso wakimbiza Chart za iTunes Nchini Kenya

$
0
0
Wasanii kutokea lebo ya WCB wanaonyesha kufanya vizuri katika chart za iTunes nchini Kenya.

Wasanii hao ni Mbosso na Diamond Platnumz ambapo wapo katika nafasi tano za juu wakishindana na wasanii wengine kama Drake na Sauti Sol.

Wimbo wa Diamond Platnumz (WCB Wasafi) uitwao Jibebe ambao amewashirikishwa Mbosso na Lava Lava unashika nafasi ya kwanza kwenye chart hiyo.

Huku Mbosso akiingiza nyimbo mbili katika ile top five, wimbo wake Nadekezwa upo nafasi ya nne na ngoma Nipepe nafasi ya tano.
 
Diamond Platnumz, Mbosso na Lava Lava kwa sasa wanafanya vizuri na wimbo wao Jibebe ambapo hapo jana ndipo walitoa video ya wimbo huo ambayo imefanyika nchini Afrika Kusini na Director Justin Campos.

Huna Sababu Ya Kuaibikatena............ Jipatie Dawa Bora Ya Nguvu Za Kiume, Maumbile Madogo Na Mvuto Wa Mapenz

$
0
0
Usikate tamaa ondoa maradhi yako, maana matatizo haya yamekua yakiasili watuwengi kisaikolojia hasa baada ya kujiona wako tofauti sana na wengine kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia (6-8) vinginevyo mtuhuyo anamapunguvu katika mwiliwake.

Kunasababu nyingi sana zinazosababisha matatizo haya, chango hushambulia never ambayo huasili misuli ya uume, Ngili :- hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kufanya tumbo kuunguluma na kujaa gesi, kolodani moja kuvimba au kuingia ndani pamoja na kutopata choo vizuli. Sababuhizi na nyingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba na marakwamara husababisha kukosa hamu ya kuludia tendo la ndoa na baadae kushindwa kabisa

MASISA 3POWER :- nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa mfumo wa vidonge, huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka 15-90 , inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii) inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa, itakufanya uludie tendo la ndoa zaidi ya mara nne (4) birahamu kuisha wara kuhisi kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya dk (20-30 )

YONINANI:- hurefusha na kunenepesha maumbile madogo ya uume uliosinyaa inchi 6-8 na unene wa sm 3-4 kwa mda mfupi sana,

SUPER MORINA :- nidawa inayotibu ama kutatua tatizo la kisukali kwawaliohangaika bila mafanikio, huondoa tatizo la kisukali na kupona kabisa, vilevile ninadawa ya magonjwa sugu km vile presha, vidondo vya tumbo, miguu kuwakamoto, muwasho mwilin, kaswende,uzazi nk.

LUGIMBA :- nidawa ya mvuto wa mapenzi, humtuliza mke, mme, mchumba, hawara au mtu yoyote umpendae na kumfanya akutimizie chochotekile unachokitaka kutoka kwake na kumfunga asiwe na mtu yoyote zaidi yako.

WASILIANA NA DR CHIPUPA NAPATIKANA DAR ES SALAAM KUMBUKA HUDUMAHII ITAKUFIKIA POPOTE ULIPO  0759208637 / 0622344969

Mahakama Yasema Nondo Anakesi ya Kujibu

$
0
0
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi (TSNP), Abdul Nondo anayekabiliwa na mashtaka ya kusambaza taarifa za uongo akidai kutekwa amekutwa na kesi ya kujibu.

Uamuzi huo umetolewa leo Jumatatu Agosti 27, na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Iringa,  Liad Chamshama baada kupitia ushahidi wa upande wa mashtaka.

Hakimu Chamshama amesema kutokana na uamuzi huo, Nondo anatakiwa kujitetea dhidi ya mashtaka yanayomkabili ambapo anatakiwa kujitetea.

Nondo anatarajia kuleta mahakamani mashahidi wasiopungua watano kutoa ushahidi katika kesi yake hiyo ambayo imepangwa kusikilizwa kati ya Septemba 18 na 19, mwaka huu.

Nondo ambaye pia alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kabla hajasimamishwa masomo kutokan ana kesi hii, anadaiwa kusambaza taarifa za uongo akiwa jijini Dar es Salaam kuwa ametekwa na shtaka la pili anadaiwa kutoa taarifa za uongo kwa polisi katika Kituo cha Mafinga mjini Iringa.

BREAKING: Lugola Amsweka Ndani Mkuu Wa Kituo Kikuu Polisi Mtwara Kwa Kushindwa Kuwaweka Watuhumiwa Mahabusu

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amemweka ndani Mkuu wa Kituo Kikuu cha Polisi mjini Mtwara (OCS), Ibrahim Mhando  kwa kushindwa kuwaweka mahabusu watuhumiwa wanne.

Miongoni mwa watuhumiwa hao ni mhandisi mshauri wa kampuni ya Y&P Architects, Benjamin Kasiga ambaye anadaiwa kutoa taarifa ya uongo kwa waziri huyo kuhusu ujenzi wa ofisi ya Uhamiaji mkoani humo.

Tukio hilo limetokea leo asubuhi Agosti 27, 2018 wakati Lugola na katibu mkuu wa wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu walipofika katika kituo hicho kwa kushtukiza.

Lugola alipokuwa anakwenda uwanja wa ndege kwa ajili ya kurudi jijini Dar es Salaam, alitaka kuthibitisha kama mtuhumiwa ambaye alielekeza jana usiku akamatwe awekwe mahabusu kama polisi walitekeleza agizo lake.

Hata hivyo, Lugola alimkuta mtuhumiwa huyo akiwa chumba cha upelelezi badala ya kuwekwa mahabusu ya polisi, hivyo akamuuliza kamanda wa polisi wa mkoa huo, Lucas Mkondya  sababu za kutotekelezwa agizo lake.

“Hivi ndivyo polisi mnafanya hivi, haya ndiyo madudu mnayoyafanya? Tabia hii siku zote tunaipinga ikichafua Polisi na hii ndiyo tabia yenu. Najua ndiyo mana nimekuja ghafla, mnafahamu maadili ya Jeshi,” alihoji Lugola.

“RPC hawa polisi wako wanafanya nini? OCS njoo hapa, kwa nini umeweka hawa watuhumiwa chumba cha upepelezi badala ya mahabusu, nawe unaingia ndani kwa kushindwa kuwaweka ndani hawa watuhumiwa, RPC muweke ndani sasa hivi huyu,” aliamuru Lugola.

Hata hivyo, Mkondya alimweleza  Lugola kuwa polisi wake walifanya makosa kwa kutowaweka mahabusu watuhumiwa hao.

Naye mkuu wa kituo hicho, Mhando kabla ya kuwekwa mahabusu pamoja na wale watuhumiwa ambao alishindwa kuwaweka mahabusu, amesema sababu kubwa ya kutowaweka mahabusu ni kwamba chumba kilijaa na wanafanya hivyo mara chache inapotokea.

Lugola aliipinga kauli hiyo kuhusu mahabusu hiyo kujaa wakati nafasi ya kukaa watuhumiwa hao ilikuwapo ndani ya mahabusu hiyo.

“Mbona nafasi ipo pale mahabusu, ile pale nafasi naiona, siwezi kukubaliana na uzembe huu na hii ni tabia yenu huwa mnakamata watuhumiwa lakini baadhi hamuwaweki mahabusu, unanidanganya kuwa mahabusu imejaa, hii haikubaliki!” amesema Lugola.

Mkurugenzi Wa Kituo Cha Uwekezaji TIC Akemea Tabia Ya Baadhi Ya Viongozi Wa Serikali Kutoa Matamko Na Kuwakamata Hovyo Wawekezaji Nchini

$
0
0
Mkurugenzi  Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) Godfrey Mwambe amewataka viongozi wa ngazi mbalimbali wakiwamo wakuu wa wilaya,wakuu wa mikoa na mawaziri kuacha kutoa matamko na maagizo kwa wawekezaji nchini.

Amesema ni vema kila mamlaka ikatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria na kufafania iwapo kuna tatizo lolote likiwemo la kodi,vibali au bora wa bidhaa kwa muwekezaji yoyote haja ya kufuata taratibu za kutafuta ufumbuzi kupitia mamlaka husika badala ya kutolewa maagizo ambayo hazingatii sheria.

Mwambe amesema hayo leo jijini Dar es Saalam wakati anazungumzia ziara ambayo TIC pamoja na wadau wanaohusika na sekta ya dawa na vifaa tiba nchini ambayo waliifanya Korea Kusini na China, tuzo waliyoipata ya kushika nafasi ya pili katika Maonesho ya Nanenane pamoja na kueleza majukumu yao ya kuelimisha umma na kumasisha uwekezaji.

Hivyo ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa kuna wimbi la viongozi kutoa maagizo na matamko na hasa yanayohusiana na masuala ya kikodi,vibali na mambo mengine.

Amesema kwamba TIC wanafanya kazi kubwa na ngumu ya kuhamasisha wawekezaji na mitaji kuja nchini na wanatumia gharama katika kufanikisha

“Kama kuna muwekezaji yoyote ana tatizo lolote wa kufahamishwa na ni kituo cha wawekezaji.Ni jambo la kushangaza Mkuu wa Wilaya anatoa makadirio ya kodi, anatoa siku mbili kodi ilipwe wakati sheria haiko hivyo.

” Unapozungumzia suala la kodi kuna utaratibu wake na sheria zake,hivyo iwapo kuna tatizo la kikodi kwa muwekezaji kiongozi wasiliana na mamlaka husika watatafuta ufumbuzi wake.

“Kama ni suala la vibali wapo wanaohusika na vibali kwa ajili ya wawekezaji,hivyo fuata utaratibu badala ya kutoa maagizo wakati huna mamlaka ya kufanya hivyo,” amesema.

Ameongeza kwamba viongozi wote jukumu lao ni kutoa taarifa kwa mamlaka husika na si kutoa maagizo na miongozo bila kufuata taratibu.

Amefafanua kuwa TRA wapo vizuri katika kufanya shughuli zao na wanacho kitengo cha uchunguzi hivyo kama mkuu wa wilaya au waziri unahisi kodi inayolipwa na muwekezaji ni ndogo au hajalipa muda mrefu lazima utaratibu ufuatwe.

Ametoa mwito kwa viongozi wote kushirikiana na TIC katika kuhakikisha wanaendelea kuweka uaminifu kwa wawekezaji ili kifikia uchumi wakati.

Pia ameomba ngazi zote za kimamlaka kila mmoja kusimama katika mipaka yake kwani kila mmoja yupo kisheria na sababu za kueleza hayo ni kukumbusha wajibu wa kila taasisi kutekeleza majukumu yake bila kuingia mipaka ya mwingine.

Mwambe ameeleza pia atamuandikia barua Kamisha wa TRA kumueleza umuhimu wa maofisa wake wa kodi kukusanya kodi kwa wawekezaji badala ya kumuacha muwekezaji anakaa miaka saba bila kulipa kodi.

“Kuna taarifa ya hivi karibuni muwekezaji amekaa miaka saba hakudaiwa kodi,anakuja mwingine mpya ndio anadaiwa na ile kodi ya miaka ya nyuma.Huu ni uzembe.

“Kwanini miaka yote ofisa wa TRA hawezi kwenda kukusanya kodi?Huo ni uzembe, nitahakikisha nasimamia hili kwa kuzungumza na Kamishna wa kodi,” amefafanua.Mwambe na kusisitiza lazima TRA wakusanye kodi.

Kuhusu ziara ya Korea Kusini na China,amesema Agosti 10 had I 18 mwaka hui aliongoza ujumbe wa wadau wanaohusika na dawa na vifaa tiba wakiwamo Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA)pamoja na Chama cha wenye viwanda vya dawa za binadamu na vifaa tiba.
 
Mwambe amesema Agosti 13 wakiwa Korea Kusini walifanya kongamano ambalo lilihusisha zaidi ya kampuni 100 wanaohusika kwenye eneo na pia wanafanya kongamano China.

Amesema matokeo ya ziara hiyo kuna kampuni tano ambazo zinahusika na uzalishaji dawa na vifaa tiba watakuja nchini Septemba mwaka huu kwa ajili ya mazungumzo kwani wanataka kuwekeza hapa nchini.

“Kampuni zote ambazo zilishiriki wanatambuliwa na HWO na kwamba ushawishi mkubwa ulikuwa kuwahamasisha waje kufanya uzalishaji dawa na vifaa tiba nchini,” amesema.

Amesema kikubwa ambacho TIC inatamani kuona ni uwekezaji wenye tija ambazo utatoa fursa Watanzania kunufaika na kuchangamkia fursa zilizopo.

Akizungumzia ushiriki wa maonesho ya Nane nane na kwamba wanazokanda saba katika kuboresha utoaji huduma kwa wadau na lengo lao Kubwa ni kutoa elimu kwa watanzania.

Amesema wamefanikiwa kushika nafasi ya pili katika ubora wa utoaji huduma na hasa katika kuwafikia wananchi na katika maonesho hayo waliwatembelea wajasiriamali waliokuwa kwenye mabanda mbalimbali kutoa elimu.

Kuhusu utendaji kazi wa pamoja ambapo TIC kuna kitengo maalum ambacho kinahusisha taasisi mbalimbali kwa lengo la kurahisisha utoaji huduma kwa wawekezaji kwa haraka.

Amesema kutokana na uwepo wa kitengo hicho wamekubaliana na NIDA nao wawepo ndani ya kituo hicho na tayari maofisa wawili wa NIDA wamewasili hapo.

Hivyo amesema wawekezaji wote wanaohitaji vibali vya NIDA watavipata TIC.Pia ameelezea umuhimu wa kuwawezesha wajasiriamali waliopo nchini kwani ndio muhimili wa maendeleo ya nchi.

Amesema nchi nyingi ambazo zimefanikiwa ni kwasababu ya wajasiriamali na kwamba TIC wanataka kuona wajasiriamali wanashiriki katika shughuli mbalimbali baada ya wawekezaji kuingia.

Amefafanua kwa mtazamo wake haoni sababu ya Dangote kuingiza magari 600 kwa ajili ya kubeba saruji, kwani hilo lilipaswa kufanywa na watanzania.

Ameongeza haiwezekani Dangote ahangaike kuzalisha saruji na wakati huo huo anahangaika na kusafirisha saruji.

Amesema jukumu muwekezaji baada ya kuzalisha kazi inayofuata ni watanzania kuchangia fursa hizo.

“Watanzania waamke na waone kuna fursa nyingi ambazo wakizitumia vizuri zitasaidia kuendeleza shughuli za kiuchumi,” amesema.

Pia amesema jukumu lao TIC ni kuendelea kutoa elimu kwa wajasiriamali ikiwa pamoja na kuwajengea uwezo na kuwaunganisha na na lengo ni kuwaunganisha na kampuni kubwa.

“Malengo ya Rais ni kuona Watanzania wanafanikiwa na ndicho ambacho hata TIC nasi tunakisimamia,” amesema.

Tido Mhando akutwa na kesi ya kujibu

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemkuta na kesi ya kujibu aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa (TBC) Tido Mhando katika kesi yake ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya Sh.Mil 887.1 ambapo ataanza kujitetea September 20 2018.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shaidi baada ya Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Leornad Swai kufunga ushahidi wa mashahidi 5 wa upande wa mashtaka.

Hakimu Shaidi amesema amepitia ushahidi wote wa mashahidi watano ulioletwa na upande wa mashtaka na kuona mshtakiwa ana kesi ya kujibu, ambapo ameahirisha kesi hadi September 20 2018 ili Tido aanze kujitetea.

Katika kesi hiyo Tido anakabiliwa na mashtaka manne ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh.Milioni 887.1 na miongoni mwa mashahidi  wa upande wa mashtaka waliotoa ushahidi ni Ofisa uchunguzi wa Takukuru Victor Lesuya Mwanasheria wa TBC  Gwakisa Mlawa na Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa TBC Clement Mshana.

Katika kesi hiyo inadaiwa kuwa June 16, 2008 Mbando akiwa Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Tido ambaye alikuwa mkurugenzi wa TBC  kwa makusudi alitumia madaraka yake vibaya kwa kusaini mkataba wa kuendesha na utangazaji wa vipindi vya televisheni kati ya TBC na Channel 2 Group Corporation (BV1) bila ya kupitisha zabuni, kitu ambacho ni kinyume na Sheria ya Manunuzi na kuinufaisha BVl.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Kafunga Mjadala.....Mgombea Ubunge CCM huko Korogwe Kapita Bila Kupingwa

$
0
0
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewataka Wasimamizi wa Uchaguzi mdogo wa Ubunge na Udiwani utakaofanyika Septemba 16 mwaka huu katika Majimbo ya Ukonga na Monduli na kwenye Kata 13 za Tanzania Bara kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia matakwa ya Katiba, Sheria na Kanuni zinazosimamia uchaguzi huo.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji (Rufaa), Semistocles Kaijage ameyasema hayo leo jijini Dodoma wakati akifungua mafunzo kwa Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi wa Kata na Majimbo hayo.

Jaji Kaijage amewataka Wasimamizi hao kuzingatia weledi na kuepuka kufanya kazi kwa mazoea ili wapunguze na kuondoa malalamiko yanayojitokeza wakati wa uchaguzi.

Amesema  Uchaguzi ni mchakato unaojumuisha hatua na taratibu mbalimbali zinazopaswa kufuatwa na kuzingatiwa akisisitiza kwamba hatua na taratibu hizo ndiyo msingi wa uchaguzi mzuri wenye ufanisi usio na malalamiko au vurugu.


“ Tunakutana hapa kwa muda wa siku tatu (3) ili kwa pamoja tubadilishane uzoefu, tujadili namna ya kufanikisha zoezi la uchaguzi lakini pia namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoweza kujitokeza katika hatua zote za uchaguzi,” Amesema Jaji Kaijage.


Aidha, amewataka Wasimamizi hoa waepuke madhara yanayotokana na ukiukaji wa Sheria, Kanuni na taratibu za Uchaguzi  na akisisitiza kwamba katika kipindi hiki chaguzi  zinafanyika katika mazingira ambayo yana hamasa kubwa ya Kisiasa, kutoaminiana na wakati mwingine hutawaliwa na mihemko ambayo imekuwa chanzo cha ufunjivu wa amani.

Jaji Kaijage amewaeleza Wasimamizi hao kwamba wameaminiwa na kuteuliwa katika nafasi hizo za usimamizi wa Uchaguzi kwa kuwa wana uwezo wa kufanya kazi hiyo hivyo wajiamini na kujitambua.

Amaetoa wito kwa Wasimamizi hao kuhakikisha kuwa wanayaelewa vema maeneo yao ya kazi na kuhakikisha kwamba wanawatumia vizuri wasaidizi walio nao katika maeneo yao kwa matokeo bora.

“Mjue mna jukumu la kuimarisha imani ya wananchi pamoja na wadau wote wa uchaguzi kwa Tume. Hivyo mfanye kazi kwa ufanisi wa hali ya juu, bila kuegemea upande wowote. Kufanya kazi kwa uhuru na kwa uwazi kutasaidia kudumisha amani katika maeneo yenu ya Uchaguzi” Amesisitiza.

Kuhusu kufanyika kwa Uchaguzi huo mdogo Septemba 16 mwaka huu,  Jaji Kaijage amesema kwa kuzingatia matakwa ya kifungu cha 37 (1) (b) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura 343 kikisomwa pamoja na kifungu cha 13(3) cha Sheria ya Serikali za Mitaa, Sura 292, ni jukumu la Tume kusimamia, kuendesha na kuratibu uchaguzi wa kujaza nafasi zilizo wazi.

Amesema kwa nyakati tofauti Tume imepokea taarifa kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye kwa kuzingatia Kifungu cha 37 (3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura 343 aliitaarifu Tume uwepo wa nafasi wazi za Ubunge katika Majimbo ya Ukonga, Korogwe Vijijini na Monduli.

Pia amefafanua kuwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa, ambaye kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali ya Mitaa, Sura, 292 alitoa taarifa ya uwepo wa nafasi wazi za Madiwani katika Kata 23 kutoka katika Halmashauri 15 zilizopo katika Mikoa 10 ya Tanzania Bara.

Aidha, katika uchaguzi huu mdogo wa Ubunge na Udiwani utakaofanyika Septemba 16 mwaka huu Mgombea Ubunge katika Jimbo la Korogwe Vijijini amepita Bila Kupingwa na jumla ya wa wagombea 10 wa Udiwani katika Kata 10 wamepita bila Kupingwa, hivyo jumla ya Kata zilizobaki zitakazoingia kwenye uchaguzi mdogo ni 13 na Majimbo 2 ya Monduli, Arusha na Ukonga jijini Dar es salaam.

MWISHO

TRA Yataja Walengwa Wanaostahili Msamaha Wa Riba Na Adhabu Ya Malimbikizo Ya Kodi

$
0
0
Na Veronica Kazimoto
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewataja walengwa wanaostahili kuomba msamaha maalum wa riba na adhabu ya malimbikizo ya madeni ya kodi kwa asilimia 100 ambapo mwisho wa kutuma maombi ya msamaha huo ni tarehe 30 Novemba, 2018.

Akizungumza wakati wa mkutano wa washauri wa walipakodi (Tax consultants)  mkoani Tabora, Afisa Elimu Mkuu kwa Mlipakodi wa mamlaka hiyo Rose Mahendeka amesema Walengwa wa msamaha huu ni makampuni, taasisi na watu binafsi ambao wamewasilisha ritani za kodi lakini bado wanadaiwa kodi yote au sehemu ya kodi zitokanazo na ritani hizo.

"Walengwa wengine ni wale wote ambao hawajawasilisha ritani za kodi, hawajasajiliwa na kupatiwa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) au Namba ya Usajili wa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na wale walio wasilisha pingamizi au rufaa za kodi ambazo bado zinashughulikiwa katika ofisi za TRA, Bodi ya Rufaa na Mahakama ya Rufani za kodi", alisema Mahendeka.

Aidha, amewataja wasiohusika na msamaha huu kuwa ni pamoja na wale ambao wangestahili kupata msamaha lakini tayari wameshalipa madeni yao, ambao masuala yao ya kikodi yapo katika hatua ya ukaguzi au uchunguzi, wana madeni ya nyuma ya kodi ambayo yanatokana na kesi za jinai za kodi, utakatishaji fedha, usafirishaji wa binadamu au shughuli nyingine haramu kama ilivyothibitika kisheria.

"Wengine ambao hawahusiki na msamaha huu ni taasisi, makampuni na watu binafsi ambao wana madeni ya nyuma ya kodi yanayotokana na adhabu zilizoamuliwa tayari au adhabu za makosa yatokanayo na uzembe wa kukusudia uliobainika kisheria pamoja na wenye riba au faini zilizotokana na kutoa au kutumia risiti za kielektroniki za kughushi," alibainisha Mahendeka.

Kwa upande wake Afisa Elimu kwa Mlipakodi wa TRA Chama Siriwa ametoa wito kwa washauri wa walipakodi mkoani hapa kuendelea kuwaelimisha wafanyabiashara na wale wote wenye taasisi na makampuni mbalimbali yenye malimbikizo ya madeni ya kodi kuwahi kutuma maombi ya msamaha huo kabla muda uliopangwa haujamalizika.

"Mimi napenda tu kusisistiza kuwa mwisho wa kutuma maombi ya msamaha huu ni tarehe 30 Novemba, 2018. Hivyo, natoa wito kwenu washauri wa walipakodi muendelee kuwaelimisha wafanyabiashara na wote wenye taasisi na makampuni kutuma maombi mapema ili waweze kunufaika na msamaha huu," alieleza Siriwa.

Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania ilitangaza msamaha wa riba na adhabu ya malimbikizo ya madeni ya kodi mwezi Julai, 2018 kwa lengo la kutoa unafuu kwa walipakodi wenye malimbikizo ya madeni ya riba na adhabu kwa kusamehe madeni yao na kuwapa fursa ya kulipa malimbikizo ya madeni ya msingi ya kodi - principal tax mara moja au kwa awamu ndani ya mwaka wa fedha wa 2018/19.

Mwisho.

 

Breaking News: Waziri Mpango Kaagiza Makontena ya Paul Makonda Yapigwe Mnada.....Kasema Kamwe Haogopi Vitisho Vyake

$
0
0
Benny Mwaipaja, WFM, Dar es Salaam
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amefanya ziara ya kushitukiza katika eneo la kuhifadhia makontena-Bandari Kavu Dar es Salaam (DICD), na kukagua makontena 20 yaliyoingizwa nchini na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na kuiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania -TRA kuendelea na mnada wa makontena hayo ili kupata kodi ya Serikali inayokadiriwa kufikia shilingi bilioni 1.2.

Dkt. Mpango amesema kuwa kodi hiyo inadaiwa kwa mujibu wa sheria za nchi baada ya mwenye mali kushindwa kulipa kodi na kwamba amesikitishwa na vitisho vinavyotolewa na Mkuu huyo wa Mkoa na vilivyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini  akitumia vifungu vya Biblia kwamba yeyote atakaye nunua mzigo huo atalaaniwa.

"Sheria za nchi hazichagua sura wala cheo cha mtu, na mimi ndicho nilicho apa, kutekeleza sheria za nchi, sheria za kodi, ndiyo dhamana niliyo pewa kwahiyo Kamishna, simamia sheria za kodi bila kuyumba" alisisitiza Dkt. Mpango akitoa maelekezo kwa Kamisha wa Forodha Bw. Ben Usaje.

Alifafanua kuwa mzigo wa Samani ulioagizwa kutoka nje ya nchi hauna msamaha wa kodi na kwamba huyo aliye agiza (RC Paul Makonda) alipe kodi stahidi na asipo lipa kodi hiyo mchakato unaoendelea wa kuyapiga mnada makontena hayo uendelee.

"Napenda niwaombe viongozi wenzangu Serikalini, ni muhimu tukachuja maneno! unasema mtu anayekuja kununua samani atapata laana, tena laana ya Mungu, kwa nini tunamhusisha Mungu kwenye vitu vya namna hii" alieleza kwa masikitiko Dkt. Mpango

Dkt. Mpango alitoa wito kwa watanzania wanaotaka kununua bidhaa hizo ambazo nyingi ni vifaa vinavyoweza kutumika shuleni ama maofisini kama vile viti meza na makabati, kujitokeza bila hofu kununua mali hizo.

 Aliwaomba walimu na wanafunzi wasiwe na wasiwasi na kwamba Serikali ya Awamu ya Tano imejipambanua na kuwekeza kwenye elimu kwa kutenga zaidi ya shilingi bilioni 20 kila mwezi kulipa ada ya wanafunzi ili wasome bila kulipa ada na ina mpango madhubuti wa kuboresha miundombinu ya elimu nchi nzima ikiwemo ujenzi wa madarasa na ofisi za walimu.

"Tunawapenda na kuwathamini sana walimu wetu, asitokee mtu yeyote  akaanza kuwaambia hadithi kama vile Serikali hii inawapuuza! si kweli hata kidogo" Aliongeza Dkt. Mpango

Kwa upande wake, Kamishna wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, Ben Usaje, alimweleza Dkt. Philip Mpango kwamba Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Paul Makonda, aliwasilisha maombi ya kutaka kupewa msamaha wa kodi wa makontena 36 yenye samani kutoka Diapora nchini Marekani.

Alisema kuwa kati ya makontena hayo, yaliyoingia nchini ni makontena 20 ambayo yanadaiwa kodi ya shilingi bilioni 1.2 na kwamba utaratibu kwa kumtaka Paul Makonda alipe kodi hiyo ili aruhusiwe kuyachukua makontena hayo ulifanyika kwa mujibu wa sheria na kwamba mpaka sasa hajayachukua ndio maana yanapigwa mnada.

Naye aliwatahadharisha watu wanao tumia masuala ya siasa na uongozi Serikalini kutaka kukwepa kulipa kodi a kwamba suala la kodi za samani zinaonekana ziko juu kwa sababu Bunge lilitunga sheria hiyo ili kulinda soko la ndani la samani na kuweka sheria ya kutokuwepo kwa msamaha wowote wa kodi kwenye bidhaa kama hizo.

Mwisho.

Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa Aiomba Mahakama Impe Wiki 3 Atafute Wakili Mwingine

$
0
0
Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa ameiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu impatie muda wa wiki 3 ili atafute wakili mwingine kwa kuwa Wakili wake Jeremiah Mtobesya amejitoa.

Msigwa pamoja na vongozi wenzake 8 wa (CHADEMA) akiwamo Freeman Mbowe wanakabiliwa na mashtaka 13 ikiwemo uchochezi na kufanya mkusanyiko usiohalali.

Kwa pamoja viongozi hao walipaswa kusomewa maelezo ya awali (Ph) mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri lakini imeshindikana kwa sababu mshtakiwa wa tano Esther Matiko ambaye ni Mbunge wa Tarime Mjini anaumwa.

Naye Wakili wa utetezi Peter Kibatala aliieleza mahakama kuwa mshtakiwa Msigwa kwa sasa hana wakili kwani awali alikuwa akitetewa na wakili Jeremiah Mtobesya ambaye amejitoa na baada ya kueleza hayo Kibatala, Msigwa alinyoosha mkono na kuieleza mahakama kuwa impatie muda wa wiki 3 ili aweze kutafuta wakili mwingine.

Kutokana na maombi hayo Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi September 27 2018 ili washtakiwa wasomewe maelezo ya awali.

Washtakiwa wengine ni Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu, Naibu katibu Mkuu bara na Mbunge wa kibamba John Mnyika, Mbunge wa Tarime Vijijini John Heche, Mbunge wa Kawe Halima Mdee na Mbunge wa Bunda Esther Bulaya na Katibu Mkuu wa Chama hicho Dk .Vincent Mashinji.

Washtakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 13, ikiwemo kula njama,  kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendajia jinai kati ya February 1 na 16, 2018, Dar es Salaam.

Thamani ya taji la Miss Tanzania ni Milioni 6

$
0
0
Kamati ya Miss Tanzania imeweka wazi taji atakalovaa Miss Tanzania mwaka huu linathamani ya Sh6 milioni.

Mkurugenzi wa kampuni ya Look inayoendesha mashindano hayo Basila Mwanukuzi ameonyesha taji hilo litakalovaliwa na mshindi atakayepatikana Septemba 8.

Amesema sanjari na taji hilo mrembo atakayeibuka kidedea katika shindano hilo atapewa zawadi ya gari.

Mwanukuzi ameeleza kuwa kamati yake imeendelea kusimamia na kuhakikisha mrembo anapata zawadi bora na yenye viwango.

Amesema kulingana na maandalizi ya kamati hiyo mshindi atapewa gari zuri ambalo hata hivyo hakuweka wazi ni aina gani.

Kando na hilo alielezea utaratibu wa kupata tiketi ambazo mwaka huu zitauzwa kwa mfumo wa kielektroniki.

Meneja Masoko wa kampuni ya Otapp inayohusikan na uuzaji wa tiketi hizo Joachim Ferdinand amesema tayari tiketi timeshaanza kuuzwa.

Bobi Wine aachiwa kwa dhamana

$
0
0
Mahakama Kuu ya Gulu nchini Uganda imempatia dhamana Mbunge wa Kyadondo Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine katika kesi yake inayomkabili ya uhaini.

Dhamana hiyo ni baada ya Mbunge huyo na wenzake 34 waliofika  mahakamani mjini Gulu kuomba mahakama iwaachilie kwa dhamana leo asubuhi wakiwa na mawakili wao.

Jaji wa mahakama ya Gulu Stephen Mubiru alikubali maombi ya dhamana hiyo, baadhi ya watu walioshtakiwa pamoja na mbunge huyo ni Mbunge wa kuteuliwa Kassino Wadri, Mbunge wa Jinja Magharibi,Paul Mwiru,Mbunge wa Ntungamo Gerald Karuhanga, na aliyekuwa mstaafu wa Makindye Mike Mabikke.

Mbunge huyo mpaka kukamatwa kwake na kushikiliwa kwenye gereza la jeshi la Makindye nchini humo alidaiwa kukamatwa akiwa na risasi na kuushambulia msafara wa Rais Yoweri Museveni kwa mawe. Lakini Bobi Wine ameonekana akitembea kwa magongo na kuzua masikitiko kwa wafuasi wake mahakamani hapo.

Sababu 2 za Jackline Wolper kutoswa shindano la Miss Tanzania

$
0
0
Hatimaye imebanika sababu ya Jackiline kutoswa kwenye kamati ya Majaji ya Miss Tanzania kwenye fainali ya mashindano yaliyofanyika Kanda ya Ziwa hivi karibuni.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo August 27, 2018 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya The Look inayosimamia Mashindano hayo, Basilla Mwanukuzi ameleza sababu za Wolper kutolewa.

"Katika ngazi ya kanda Majaji ni kamati ya Miss Tanzania au watu ambao kamati itapendekeza, sasa Wolper sio kamati ya Miss Tanzania," amesema.

"Lakini pia Majaji wanapewa semina, Wolper alichelewa kufika kwenye semina, ataingiaje kujaji hajaongozwa?. Sio tu uwe super star  uje kujaji, hapana! kuna miongozo maalumu alitakiwa awahi ahudhurie semina ambayo wale Majaji wengine walipewa, yeye kafika semina imeshaisha," amesema  

Harmonize aeleza namna Kwangwaru inavyotikisa Kenya

$
0
0
Msanii wa muziki Bongo, Harmonize ameeleza jinsi wimbo wake, Kwangwaru ulivyomkubwa nchini Kenya.

Muimbaji huyo kutokea WCB kwa sasa anafanya tour nchini humo. Katika show  anazofanya inaonyesha kuwa na muitikio mkubwa sana wa watu kuhudhuria.

Harmonize ameeleza katika show yake ulipofika wakati wa kuimba Kwangwaru mashabiki hawakutaka aimbe hata kidogo badala yake wao ndio waimbe.

Ameongeza kuwa hata baadhi ya watu nchini humu wamemueleza kuwa Kwangwaru ndio wimbo wa mwaka, yaani uliofanya vizuri zaidi. 

Wimbo Kwangwaru ambao Harmonize amemshirikisha Diamond Platnumz hadi sasa una views Milioni 23 katika mtandao wa YouTube ukiwa na miezi minne tangu ulipotoka na kuwa wimbo wa kwanza wa msanii huyo kufikisha idadi hiyo ya views.

CAF yarodhishwa na maandalizi ya AFCON

$
0
0
RAIS wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), Bw. Ahamd Ahmadamesema ameridhishwa na maandalizi ya michuano ya Afrika ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (AFCON).

Mashindano ya mpira wa miguu kwa Vijana wenye umri wa chini ya  miaka 17 AFCON yanayotarajiwa kufanyika mwaka 2019 nchini Tanzania.

Ameyasema hayo jana (Jumatatu, Agosti 27, 2018) wakati akizungumza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
 
Pia ameihakikishia Serikali kwamba hakuna mabadiliyo yoyote ya ratiba yatakayofanyika kuhusu wenyeji wa mashindano na kwamba CAF itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kufanikisha michuano hiyo.

Rais wa CAF yupo nchini kwa ajili ya kuongoza mkutano maalum wa mabadiliko ya katiba ya Baraza la Vyama vya Soka katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
 
Mkutano huo unaofanyika jijini Dar es Salaam, umehudhuriwa na viongozi wa juu wa nchi wanachama wote 12 wa CECAFA wakiwemo marais.
 
Kwa upande wake,Waziri Mkuu WAZIRI amesema mechi zoteza michuano ya Afrika ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (AFCON) zitafanyika jijini Dar es Salaam.mashindano

“Tupo katika hatua za mwisho za maandalijzi ya michuano hiyo itakayofanyika jijini Dar Es Salaam katika viwanja vya Taifa, Uhuru, Chamanzi na JK Park utatumika kwa mazoezi.”

Waziri Mkuu amesema ni muhimu kwa nchi kushiriki katika mashindano makubwa kama hayo kwa kuwa yanasaidia kwenye ukuzaji wa vipaji kwa vijana ambao wengi wao ni wanafunzi.

 (mwisho)

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, AGOSTI 27, 2018.

Kigogo wa TFF afungiwa maisha kwa kosa la kuiba na kughushi

$
0
0
Kamati ya Maadili iliyokutana Jumamosi Agosti 25,2018 Makao Makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) imemfungia kutojishughulisha na soka Mbasha Matutu.

Matutu ambaye ni Msimamizi wa kituo cha Shinyanga na Mjumbe wa Kamati kuu TFF, amefungiwa kwa makosa matatu ya kushindwa kutekeleza majukumu yake, ubadhirifu, kughushi na kuiba kinyume na kanuni za Maadili na Ligi Kuu.

Kiongozi huyo kwa sasa amefutwa rasmi wadhifa wake ndani ya Shirikisho hilo akiwa kama Mjumbe wa Kamati Kuu na sasa hatohusika tena na masuala ya soka nchini.

Maamuzi hayo yametolewa na TFF  kupitia Makao yake yake yaliyopo Ilala, Karume baada ya kuitisha kikao na Waandishi wa Habari.

CHADEMA Washinda unaibu Meya Arusha

$
0
0
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (chadema) jijini Arusha kimeshinda nafasi ya naibu meya wa Jiji baada ya mgombea wake Paulo Matthysen kumbwaga mgombea wa CCM, Prosper Msofe.

Uchaguzi huo uliofanyika jana baada ya kuapishwa kwa madiwani wanne wa CCM, ambao awali wote walikuwa ni wanacahama wa Chadema ni pamoja na Matthysen ambaye ni diwani wa Mushono amepata kura 27 za madiwani wote wa chadema  na Msofe ambaye ni diwani wa Daraja mbili amepata kura saba za madiwani wote wa CCM katika baraza hilo.

Akitangaza  matokeo hayo, Mwanasheria wa jiji, Grayson Orcado alisema wapigakura halali katika uchaguzi huo walikuwa  34 na hakuna kura  iliyoharibika.

Akizungumza baada ya kutangazwa kwa matokeo, Meya wa Jiji la Arusha, Kalist Lazaro alisema ushindi huo umedhihirisha kuwa madiwani wa chama hicho bado wako imara jijini humo.

“Ushindi huu unaonyesha bado tupo imara, lakini pia leo tumempokea mkurugenzi mpya, Dk Maulid Madeni aliyeteuliwa na Rais John Magufuli, tunaahidi kumpa ushirikiano wa kutosha,” alisema meya huyo.

Alisema kikao hicho ambacho ni cha robo ya nne ya mwaka, kimewachaguwa pia wenyeviti wa kamati wote kutoka chadema.

Meya Lazaro amesema Diwani wa Sombetini, Ally Benanga alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya mipango miji na diwani wa Ngarenaro, Isaya Doita alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya elimu, afya na uchumi.

Wakati huo huo, kabla ya uchaguzi huo, madiwani wanne wa CCM walioshinda katika uchaguzi wa Agosti 12 waliapishwa jana. Madiwani hao ni Msofe wa Daraja mbili, Emmanuel Kessy wa Kaloleni, Obedi Meng'oriki wa Terati na Elirehema Nnko  wa Kata ya Osunyai .

Serikali yathibitisha kuwepo kwa saruji ya kutosha nchini........Wanaopandisha Bei Kiholela Kunyang’anywa Leseni

$
0
0
Serikali imethibitisha kuna saruji ya kutosha nchini baada ya kuwepo kwa hifadhi ya Tani 16,000 kwa jana pekee ambapo uzalishaji ukiendelea vizuri utafikia Tani Milioni 5.8 kwa mwaka wakati mahitaji ya mwaka ni tani Milioni 4.8.

Kutokana na hali kuwa hivyo, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amewaagiza watengenezaji saruji kuwafutia leseni mawakala ambao watabainika kupandisha bei huku pia akitumia fursa hiyo kuwakaribisha wageni kutoka nje kuja kununua saruji nchini.

Mwijage ametoa kauli hiyo jana Agosti 27, 2018 jijini Dar es Salaam wakati alipotembelea kiwanda Tanzania Portland Cement (Twiga)  kilichopo Wazo na Camel Cement Company kilichopo Mbagala.

Akizungumza na uongozi wa kiwanda kinachozalisha saruji ya Twiga, Mwijage alisema lazima baadhi ya mawakala watolewe kafara ili kudhibiti hali hiyo.

Pia ameuagiza uongozi wa kiwanda hicho kumpatia orodha ya mawakala wote wanaosambaza bidhaa hiyo pia waagizwe kushusha bei ya saruji  ambayo sasa imepaa hadi Sh 18,000 katika baadhi ya maeneo.

“Mimi nimefanya kazi hapa miaka 18, nafahamu mchezo wote wa vijana wako wanaoufanya, ndio maana nakuagiza uniletee orodha ya mawakala wote wanaosambaza saruji ili niwabaini na kuwafutia leseni.

“Kwa sababu sasa Dangote anazalisha tani 4,500 kutoka tani 2000 kwa siku, Twiga anazalisha tani 6,000 kutoka tani 3,500 kwa siku, Tembo tani 1,100, Nyati tani 2,000 hivyo hakuna uhaba wa saruji sasa. Tayari hali imetangamaa ila kwanini bei iendelee kubaki juu.

“Kiujumla kwa siku tunazalisha tani 16,000 na sasa tunatumia tani milioni 5.8 kutoka tani milioni 4.8 kwa mwaka na viwanda vyote vilivyosimikwa sasa vina uwezo wa kuzalisha tani milioni 10.5 kwa mwaka,” alisema.

Aidha, alisema ili kuendelea kuhimili soko la ndani na la nje, tayari kuna viwanda vitatu ambavyo ni cha Mamba,  Nyati namba 2 na kiwanda cha wachina cha Engian ambacho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha malighafi inayotumika kuzalisha saruji (clinker) zaidi ya tani milioni saba kwa mwaka.

“Suala hili la saruji kupanda, naomba watu wanivumilie, dawa ya kupanda naijua, saruji imejaa sokoni, bei inashuka yenyewe, ila wale wanaopandisha inaitwa ‘profiteering’ siku ya kiama inshallah basi hukumu ni yao kama wanataka kuishi duniani shauri yao hukumu ni yao.

Aidha, Meneja Undelezaji Biashara wa Kampuni ya Saruji ya Twiga (TPCC), Mhandisi Danford Semwenda  ni kazi ngumu kuwadhibiti mawakala wa uuzaji wa saruji hiyo hivyo wanaomba ushirikiano kutoka serikali ili kudhibiti hali hiyo.

Kwa upande wake Meneja Mkuu Msaidizi wa Kiwanda cha Camel, Ghalib Hassan Ghalib  alisema kutokuwapo kwa umeme wa uhakika nao umekuwa kikwazo kwa kiwanda hicho kufikia malengo ya kuzalisha tani 600 kwa siku na hivyo kuzalisha tani 400.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images