Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Mkuu wa Mkoa Ataka Wahamiaji Haramu Wakamatwe Haraka na Kufungwa

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanuel Maganga ameiagiza Idara ya Uhamiaji kuanza msako wa kuwakamata wahamiaji haramu waliojificha kwenye mashamba na majumbani.

Alitoa agizo hilo jana Jumatatu Agosti 6, 2018 wakati akiwaapisha wakuu wa wilaya ya Kasulu na Buhigwe ambapo alisema wahamiaji haramu mkoani humo wanatakiwa kukamatwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria ili wahukumiwe kifungo.

Kaitka hatua nyingine RC Maganga alioomba mahakama kuhakikisha kesi zote za wahamiaji haramu zinapewa kipaumbele ili kupunguza msongamano wa mahabusu magerezani, ambao wanakula chakula bila kuzalisha.

Alisema kuna wahamiaji haramu na wakimbizi waliotoroka kambini wanaishi mitaani na kwenye nyumba za wananchi kinyume cha sheria, jambo ambalo halikubaliki.

Multichoice (Dstv) na Zuku hatarini kunyang'anywa leseni za kurusha matangazo Tanzania kwa kukaidi Agizo la TCRA la kutoonyesha televisheni za ndani

$
0
0
Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) inakusudia kusitisha leseni ya kampuni ya Multichoice Tanzania Limited, wamiliki wa king’amzi cha DSTV na Simbanet Tanzania Limited inayomiliki Zuku kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kukiuka masharti ya leseni.

Taarifa iliyowekwa kwenye vyombo vya habari na mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo, leo Agosti 7 inaeleza kuwa kampuni hizo zimejumuisha katika vifurushi vyao chaneli za ndani ambazo hazitakiwi kulipiwa.

 “Simbanet Tanzania Limited, Multichoice Tanzania Limited, hairuhusiwi kuonyesha chaneli za televisheni zenye leseni za kutazamwa bila malipo kupitia ving’amuzi vyao isipokuwa TBC1 peke yake,” limeeleza tangazo hilo.

Tangazo hizo linasema TCRA imewahi kuziamuru kampuni hizo kuacha kubeba na kuonyesha chaneli hizo kwa kuwa ni kinyume na matakwa ya sheria na leseni walizopewa lakini zimekaidi onyo hilo na kuendelea kuonyesha chaneli hizo.

Limeongeza kuwa TCRA inakusudia kusimamisha kabisa leseni zote zilizotolewa na mamlaka hiyo kwa kampuni hizo kwa sababu zimeshindwa kutekeleza amri halali na masharti ya leseni zao.

DC Jokate Mwegelo Atoa Maagizo kwa Wataalamu wa Afya

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo amewataka wataalamu wa afya wilayani humo kutoa elimu ya njia sahihi za kunyonyesha watoto.

Amesema elimu hiyo itawawezesha kinamama kupata kizazi chenye afya bora na kushiriki vyema masuala ya uchumi na kijamii kwa siku zijazo.

Ameyasema hayo leo Agosti 7 muda mfupi mara baada ya kufunga maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji watoto duniani yaliyofanyika mjini humo kwa ngazi ya wilaya ya Kisarawe.

Hii ni kazi ya kwanza kwa Jokate tangu ateuliwe na kuapishwa kuwa mkuu wa wilaya ya Kisarawe.

"Uongozi wa Serikali kwa ngazi zote mnapaswa kuweka misingi imara na kuhamasisha jamii yetu ili itilie maanani kunyonyesha watoto kikamilifu."

Jokate amewakumbusha waajiri kuzingatia sheria za ajira zinazowataka kuwapa likizo ya uzazi ya siku 84 ili waweze kunyonyesha watoto wao kikamilifu.

"Hii si kwa upande wa kinamama pekee bali hata kinababa nao wanapaswa kupewa likizo ya uzazi ya siku tatu pindi wake zao wanapojifungua na hizo siku wanapaswa wazitumie kuwapa misaada mbalimbali wake zao ili waweze kunyonyesha watoto wao kikamilifu," alisema Jokate.

Rais Wa Uganda, Yoweri Museveni Kufanya Ziara Nchini Agosti 9, 2018

$
0
0
 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUHUSU ZIARA YA RAIS WA UGANDA NCHINI
Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni atafanya ziara ya kikazi ya siku moja hapa nchini tarehe 09 Agosti 2018.

Lengo la ziara hiyo ni kuimarisha ushirikiano na ujirani mwema uliopo kati ya Tanzania na Uganda.

Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Mheshimiwa Rais Museveni atapokelewa na mwenyeji wake Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akiwa nchini, Mheshimiwa Rais Museveni atakutana kwa mazungumzo ya faragha na Mheshimiwa Rais Magufuli yatakayofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Mazungumzo hayo yatafuatiwa na Chakula cha Mchana kilichoandaliwa na Mheshimiwa Rais Magufuli kwa heshima ya Mheshimiwa Rais Museveni.

Mheshimiwa Rais Museveni na Ujumbe wake wataondoka nchini siku hiyo hiyo kurejea Uganda.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma. 07 Agosti 2018

Matapeli 13 wa ile pesa Itume kwa Namba Hii wafikishwa Mahakamani

$
0
0

Watu 13 wamefikishwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu  wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi ikiwemo utakatishaji fedha wa Shilingi Milioni 154.

Akiwasomea mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Kelvin Mhina wakili wa serikali mkuu, Nassoro Katuga amedai kuwa washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka 5 ambayo wameyatenda katika mikoa tofauti.

Katika kosa la kwanza la kula njama ya kutenda kosa linawakabili washtakiwa wote ambapo wanadaiwa wamelitenda kati ya March 2018 na June 2018 katika jiji la Dar es Salaam na mkoa wa Rukwa na katika maeneo mengine ya Jamhuri ya Tanzania.

Pia kosa jingine ni kusambaza taarifa za uongo kupitia mfumo wa kompyuta ambapo wanadaiwa wamelitenda March na June 2018 wakiwa Dar es Salaam na Rukwa ambapo walichapisha taarifa fupi za jumbe (Message) ili kujipatia kitu.

Wakili Katuga amedai kosa jingine ni kusambaza jumbe (message) kwa njia ya Elektroniki kati ya March na June, 2018 kwa nia ya kudanganya na kushawishi kati ya Dar es Salaam na Rukwa walisambaza kwenda kwa watu tofauti tofauti ili kuonyesha wana mamlaka hayo.

Pia katika kosa jingine la kusambaza jumbe fupi za Kielektroniki, wanadaiwa walilitenda March na June, 2018 kati ya Dar es Salaam na Rukwa walisambaza jumbe zisizotakiwa kwa njia ya Kielektroniki.

Katika kosa la mwisho wanadaiwa ni utakatishaji fedha ambapo wanadaiwa wamelitenda kati ya March na June 2018 katika maeneo ya Dar es Salaam na Rukwa.

Inadaiwa kwa pamoja walijihusisha katika ufanyaji wa muamala wa Sh.Mil 154,032,830 ikiwa ni zao la kosa la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Wakili Katuga amedai upelelezi haujakamilika ambapo Hakimu Mhina amesema kesi hiyo haina dhamana kwa sababu ni ya uhujumu uchumi, hivyo wataenda rumande ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi August 21,2018.

Wanachama wa CCM Monduli waandamana kumkataa Mbunge aliyetoka CHADEMA ( Julius Kalanga)

$
0
0
Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Monduli wameandamana kwenye ofisi za chama hicho wakitaka aliyekuwa Mbunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA), Julius Kalanga aliyejiunga na chama hicho kufuata utaratibu ikiwemo hatua za uteuzi wa nafasi ya kugombania ubunge.

Aidha, Wakizungumza katika Ofisi hizo wamesema kuwa wamesikia taarifa za kuteuliwa kwake bila kufuata utaratibu ikiwemo kukaa vikao na wazee wa kimila Malaigwanani ili waweze kumpitisha.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Monduli amesema kuwa hajashiriki kwenye vikao na wazee wa kimila kama inavyodaiwa na baadhi ya wanachama hao na kwamba utaratibu utatumika katika kuwapata wagombea

“Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinataratibu zake, kina katiba, sheria ambazo zote zitafuatwa katika mchakato huu wa kumpata mgombea ubunge wa jimbo hili la Monduli,”amesema mwenyekiti wa chama wilaya ya Monduli, Wilson Lengima

Mizizi 29 Power ,ndio Dawa Bora Na Imara Kwa Sasa Kwa Kutibu Na Kuponesha Tataizo La Nguvu Za Kiume Kwa Dakika 30 Tu

$
0
0
Tatizo la upungufu wa nguvu za kiume limekuwa ni janga kubwa sana kwa sasa sio vijana au wazee wanalalamiki kukimbiwa na wa wapenzi wao au ndoa kuvunjika kutokana na mwanaume kulala na mwanamke kitanda kimoja hata wiki mbili bila kushiriki tendo la ndoa na hii ndio inachangia wanawake wengi kutoka nje ya ndoa kwa nini huteseke na wakati dawa zipo ambazo zitarudisha heshima yako ya ndoa 

MIZIZI 29 POWER; ni ambayo hutibu na kurudisha virutubisho mwilini ambavyo humfanya mwanaume awe na matatizo yafatayo 1 kuwahi kukojoa kabla mke au mpenzi wake

 2. kushindwa kurudia tendo dawa, hii itakufanya kurudia tendo zaidi ya Mara tatu 

3... dawa hii inatibu uume uliolegea na kusinyaa 

4. dawa hii inatoa miungurumo ya tumbo na uchovu wakati wa kumaliza tendo 

NINI KINASABABISHA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME 1 kupiga punyeto kwa mda mrefu 
2 upungufu wa vichochoe mwilini 
3 magonjwa ya moyo, kisukari, presha, vidonda vya tumbo kiuno na mgongo 
4 utumiaji ovyo wa madawa ya kizungu 
4 usongo wa mawazo, hasira, tumbo kujaa gesi na kutopata choo.

 PATA TIBA YANGU NA NI TOFAUTI NA ULIZO WAHI KUTUMIA: 

Je una uume mfupi na mwembamba? MASHESHA MIX ni dawa ya kuboresha uume saiz upendayo asa kwa wale waliofanyiwa tohara wakiwa wadogo.. chagua saizi upendayo inch 5,6,7, adi 8 iyo ni kwa urefu na unene sentimita 2,3,4, adi 5 .dawa hizi zipo za kupaka na kunywa na hazina madhara yoyote kwa mtumiaji ,

Tunatibu kisukari,vidonda vya tumbo,ngiri, korodani iliyovimba, kupnguza kitambi, maziwa makubwa NK 

KWA TIBA NA USHAULI FIKA OFISINI KWANGU DARE S SALAAMU MBAGALA ZAKHEMU NA MIKOA YA KANDA YA ZIWA YUPO WAKALA WETU HAPO MWANZA NA KWA AMBAO HAWANA NAFASI YA KUJA OFISINI HUDUMA YETU UTALETEWA POPOTE ULIPO PIGA SIMU 0783185060 DR MAKOYE

PICHA: Rais Magufuli Akutana Na Viongozi Wa Jumuiya Ya Kikristo Tanzania (CCT) Ikulu Jijini Dar Es Salaam Leo

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT)  ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Moravian Tanzania Jimbo la Kusini Magharibi  Alinikisya Cheyo, aliyeongoza ujumbe wa viongozi wapya wa Jumuiya hiyo kumtembelea na kujitambulisha kwake Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 7, 2018.

Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Makamu wa Kwanza wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT)  Dkt. Frederick Shoo wakati ujumbe wa viongozi wakuu  wa Jumuiya hiyo  ulipomtembelea na kujitambulisha kwake Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 7, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Makamu wa Kwanza wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT)  Dkt. Frederick Shayowakati ujumbe wa viongozi wakuu  wa Jumuiya hiyo  ulipomtembelea na kujitambulisha kwake Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 7, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa watika mazungumzo  na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT)  ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Moravian Tanzania,  Alinikisya Cheyo, Makamu Mwenyekiti wa Kwanza wa Jumuiya hiyo Dkt. Frederick Shoo, Makamu wa Pili wa Mwenyekiti  Dkt Jacob Chimeleje na Katibu Mkuu wa CCT  Canon Moses Matonya ujumbe huo viongozi wapya wa jumuiya hiyo ulipomtembelea na kujitambulisha kwake Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 7, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT)  ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Moravian Tanzania,  Alinikisya Cheyo, Makamu Mwenyekiti wa Kwanza wa Jumuiya hiyo Dkt. Frederick Shoo, Makamu wa Pili wa Mwenyekiti  Dkt Jacob Chimeleje na Katibu Mkuu wa CCT  Canon Moses Matonya baada ya ujumbe wa viongozi  hao kumtembelea na kujitambulisha kwake Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 7, 2018.

PICHA: Rais Magufuli Akutana Na Viongozi Wa Baraza La Maaskofu Wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC) Ikulu Jijini Dar Es Salaam

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akifanya sala na Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC) Askofu Gervas John Nyaisonga, Makamu wa Rais wa Baraza lhilo Dkt. Flavian Kasalla na  Katibu Mkuu wa TEC  Dkt. Charles Kitima viongozi hao wapya wa kanisa walipomtembelea na kujitambulisha kwake Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 7, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na  Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC) Askofu Gervas John Nyaisonga, Makamu wa Rais wa Baraza lhilo Dkt. Flavian Kasalla  wakiwa na  Katibu Mkuu wa TEC  Dkt. Charles Kitima viongozi hao wapya wa kanisa walipomtembelea na kujitambulisha kwake Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 7, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono na Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC) Askofu Gervas John Nyaisonga na  Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC) Dkt. Flavian Kasalla  wakiwa na  Katibu Mkuu wa Baraza hilo Dkt. Charles Kitima baada ya viongozi hao wapya wa kanisa kumtembelea na kujitambulisha kwake Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 7, 2018.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC)   Dkt. Charles Kitima akiwa na Rais wa Baraza hilo Askofu Gervas John Nyaisonga na Makamu wa Rais wa Baraza hilo Dkt. Flavian Kasalla viongozi hao wapya wa kanisa walipomtembelea na kujitambulisha kwake Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 7, 2018.
Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC) huku Makamu wa Rais wa Baraza hilo Dkt. Flavian Kasalla  wakiwa na Katibu Mkuu wa Baraza hilo Dkt. Charles Kitima
ambaye anaongea na wanahabari mara baada ya viongozi hao wapya wa kanisa kumtembelea na kujitambulisha kwake Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 7, 2018

Rais Mstaafu Mkapa Mgeni Rasmi Kilele Cha Nanenane Kitaifa 2018 Simiyu

$
0
0
Na Stella Kalinga, Simiyu
RAIS mstaafu Mhe. Benjamini Mkapa kesho Agosti 08, atakuwa Mgen Rasmi katika Kilele cha  Maonesho ya Sherehe ya wakulima Nanenane Kitaifa mwaka 2018, ambayo yanafanyika katika Uwanja wa Nyakabindi Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu.

Akizungumza na vyombo vya habari , Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.  Anthony Mtaka amesema  Mkapa atakuwa mgeni rasmi katika madhimisho hayo akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. 

Amesema pia katika kilele cha Maadhimisho ya maonesho hayo  viongozi mbalimbali wa Chama na  Serikali watashiriki wakiwemo Katibu Mkuu wa CCM , Dkt. Bashiru Ally Sambamba na Mawaziri, Manaibu Waziri na Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Mkuu wa wizara mbalimbali.

“Watakuwepo viongozi mbalimbali wa Chama na  Serikali pamoja na viongozi wa Taasisi mbalimbali za Fedha wakiwemo  Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania(BOT) Prof. Florens Luoga na Mkurugenzi wa Benki ya NBC, Theobald Sabi”

“Wageni wengine ni Wakurugenzi wa Benki ya NBC na NMB pamoja Viongozi waandamizi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, hivyo napenda kuwakaribisha wananchi wote wa Mikoa ya Mara, Shinyanga na kwa msisitizo wananchi wa Simiyu ambao ndiyo mkoa mwenyeji kujitokeza kwa wingi kushuhudia maadhimisho ya maonesho haya ambayo ni mara ya kwanza kufanyika Mkoani kwetu” alisema.

Katika hatua nyingine Mtaka amewahakikishia wananchi kuwa usafiri wa kufika katika Uwanja wa Nanenane utakuwa wa uhakika kwa kuwa mabasi ya kwenda huko yapo ya kutosha na nauli zimepunguzwa  kutoka Lamadi mpaka Nyakabindi na kutoka Mjini Bariadi kwenda Nyakabindi.

MWISHO

Mkuu Mpya wa Mkoa wea Songwe Brigedia Jenerali Mwangela Awasili ofisini.....Gawala Awabeza Wanafurahia Kustaafu Kwake

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brigedia Jenerali Nicodemas Elias Mwangela amewasili katika ofisi yake mapema leo asubuhi kufuatia kuteuliwa kwake kuuongoza Mkoa wa Songwe na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe John Pombe Magufuli Julai 28, 2018.

Brigedia Jenerali Mwangela amepokelewa na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa, Wakuu wa Wilaya nne za Mkoa wa Songwe, wakurugenzi wa halmashauri tano za Mkoa huu, wakuu wa idara pamoja na watumishi wote wa ofisi yake.

Mara baada ya mapokezi hayo Brigedia Jenerali Mwangela amepokea taarifa ya makabidhiano kutoka kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe Luteni Mstaafu Chiku Gallawa katika kikao cha pamoja na wakuu wa wilaya, wakurugenzi, wakuu wa idara na wajumbe wa kamati ya ulinzi na Usalama.

Gallawa amesema kuwa anayo furaha kumkaribisha Brigedia Jenerali Mwangela na anamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe John Pombe Magufuli kwa kumteua Brigedia Jenerali Mwangela, na kuwa wale waliokuwa wakifurahia kuondoka kwake wakijua sasa wataanza kufanya kazi ndivyo sivyo wajue wamepata kiongozi ambaye ni makini zaidi

Ameongeza kwa kuwataka watendaji na wanasiasa waendelee kuchapa kazi kwa bidii wakiwa na lengo la kumkomboa mwananchi wa Songwe kutoka katika umasikini na kuongeza pato la mkoa na taifa.

Naye Brigedia Jenerali Mwangela amemshukuru Gallawa kwa kuweka misingi mizuri ambayo imelenga kuuinua Mkoa wa Songwe kiuchumi na kuahidi kuwa atahakikisha mazuri yote atayaendeleza hasa pale alipoishia.

Ameongeza kwa kuwasihi watendaji kufanya kazi kwa kufuata sheria, taratibu na maadili ya utumishi wa umma na kwa kushirikiana kwa kuwa anaamini katika ushirikiano kazi zinafanyika kwa ufanisi.

"Tufanye kazi tuwatumikie wananchi wa Songwe, milango ya ofisi yangu itakuwa wazi kwenu kwakuwa napenda kufanya kazi kwa ushirikiano, nami pia ninaomba ushirikiano wenu kama mliokuwa mnapa Gallawa ikiwezekana hata Zaidi,” amesema Brigedia Jenerali Mwongela.

Amewataka watumishi kuzingatia muda katika kila jambo wanalotekeleza wasiopoteze muda huku akiwasisitiza kufanya kazi kama timu moja.

“Nawapa mfano wa silaha ya mzinga ambao ili iweze kufanya kazi vizuri wanahitajika watu sita ambao kila mmoja ana jukumu lake la kufanya ili mzinga huo ufanye kazi kwa ufanisi, hii ni timu na akikosekana mmoja mzinga hautaweza kufanya kazi sawasawa, nasisi tuige ushirikiano kama huu kila mmoja atekeleze jukumu lake ili tufikie lengo moja”, amefafanua Brigedia Jenerali Mwangela

NEC Yatangaza Uchaguzi Mdogo Wa Udiwani Katika Kata 21

$
0
0
Hussein Makame, NEC
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza Uchaguzi Mdogo wa Udiwani katika kata 21 za mikoa 10 ya Tanzania Bara utakaofanyika tarehe 16 Septemba mwaka huu.

Akitoa taarifa ya uchaguzi huo jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Dkt. Athumani Kihamia, alisema fomu za uteuzi wa wagombea wa uchaguzi huo zitatolewa kati ya tarehe 17 hadi 23 Agosti mwaka huu.

Aliongeza kuwa uteuzi wa wagombea utafanyika tarehe 23 Agosti wakati kampeni za Uchaguzi zitafanyika kati ya tarehe 24 Agosti hadi tarehe 15 Septemba mwaka huu.

Dkt. Kihamia alisema kuwa Tume imetangaza uchaguzi huo baada ya kupokea taarifa ya uwepo nafasi wazi za udiwani katika kata hizo 21 zilizopo katika Halmashauri 15 kutoka kwa Waziri mwenye dhamana na Serikali za Mitaa.

“Nafasi wazi za udiwani katika Kata hizo zimetokana na sababu mbalimbali zikiwepo kifo, kujiuzulu, kutohudhuria vikao na kufutwa uanachama” alisema Dkt. Kihamia na kuongeza kuwa;

“Baada ya kupokea taarifa hiyo na kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13(3) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa; Tume ina utaarifu Umma kuhusu kuwepo kwa Uchaguzi mdogo katika Kata hizo 21.”

Kufuatia taarifa hiyo, Dkt. Kihamia alitoa mwaliko wa Tume kwa vyama vya siasa, wadau wote wa Uchaguzi na wananchi kwa ujumla kushiriki katika Uchaguzi huo.

“Tume inachukua fursa hii kuviasa vyama vya siasa na wadau wote wa Uchaguzi kuzingatia matakwa ya Katiba, Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa (Madiwani) za mwaka 2015” alisema Dkt. Kihamia.

Aidha alivitaka vyama vya siasa na wadau wa uchaguzi kuzingatia Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2015 pamoja na maelekezo yote yaliyotolewa au yatakayotolewa na Tume wakati wote wa Uchaguzi mdogo.

Uchaguzi huu mdogo wa udiwani katika kata 21 unatarajiwa kufanyika sanjari na uchaguzi mdogo wa ubunge katika majimbo ya Korogwe Vijijini, Ukonga na Monduli na kata za Tindabuligi na Kisesa katika Halmashauri ya Wilayani Meatu, uliotangazwa juzi ambao utakaofanyika siku ya Jumapili tarehe 16 Septemba mwaka huu.

Rais Magufuli Azawadia Kitabu Cha Mwongozo Wa Sala Na Rais Wa Baraza La Maaskofu Wa Kanista Katoliki (TEC ) Askofu Gervas John Nyaisonga

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea kitabu cha Muongozo wa Sala toka kwa  Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC) Askofu Gervas John Nyaisonga. Kulia ni Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki (TEC) Dkt. Flavian Kasalla na kushoto ni Katibu Mkuu wa Baraza hilo Dkt. Charles Kitima baada ya viongozi hao wapya TEC kumtembelea Rais Magufuli ili kujitambulisha kwake Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 7, 2018 

PICHA: Makamu Wa Rais, Mama Samia Amjulia Hali Waziri Kigwangalla

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 7, Agosti 2018 amemtembelea Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kingwangalla aliyelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam ambapo alimjulia hali na kumpa pole kufuatia ajali ya gari aliyoipata Agosti 4,2018 huko Manyara.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 7, Agosti 2018 amemtembelea Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kingwangalla aliyelazwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam ambapo alimjulia hali na kumpa pole kufuatia ajali ya gari aliyoipata Agosti 4,2018 huko Manyara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimjulia hali na kumpa pole Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla aliyelazwa  katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam, baada ya kupata ajali ya gari Agosti 5, 2018. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya Agosti 8


Serikali: Nane Nane Isingoje Mwezi Wa Nane

$
0
0
Na. Atley Kuni- Simiyu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo, amewataka Maafisa Kilimo kuhakikisha kuwa wanaendelea kutoa utaalamu wa kilimo katika mabanda ya Nanenane hata baada ya maonesho hayo kukamilika ili wananchi waweze kufaidi utaalamu wao

Aliongeza kuwa ipo haja kwa kila kanda kunapofanyikia maonesho ya Nanenane kuandaa wataalamu wa kilimo ambao watakuwa wakiendelea kutoa huduma hizo hata baada ya maonesho hayo kumalizika

Waziri Jafo alitoa kauli hiyo jana kwenye maonesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa mkoani Simiyu, kabla ya kuzindua mwongozo wa namna ya kuandaa mipango ya kilimo ya wilaya (District Agricultural Development Plans Guideline- DADPs Guideline).

Alisema kuwa mwaka jana akiwa jijini Dodoma aliagiza kuwa wataalamu wa kilimo hawana budi kuwa na watumishi wa kudumu katika vibanda vya maonesho ili waweze kutoa utaalamu wao kwa wananchi wanaohitaji huduma hiyo.

“Wakulima wetu hawapaswi kungoja msimu wa Nane Nane ndio waje kujifunza mbinu na maarifa ya ukulima bora ambao utakuwa na manufaa kwao bali inatakiwa kila mkulima anapotaka kujifunza ajue lipo eneo ambapo anaweza kwenda na kupata ushauri nasaha juu ya jambo linalo mtatiza katika Mifugo, Kilimo au Uvuvi” alisema Jafo.

Mhe. Jafo alisema asilimia 65 ya malighafi za viwanda hutokana na mazao ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi hivyo suala la wananchi wanaofanya shughuli hizo kuwa endelevu halina budi kuzingatiwa na kupewa kipaumbele.

“Tunapoendelea na Kampeni ya Kiwanda changu mkoa wangu ambapo tumeonekana kufanya vizuri katika robo ya kwanza na kufikia asilimia 49 ya malengo ya kuwa na viwanda 100 kwa kila mkoa lazima tujidhatiti katika kutoa utaalam wa kutosha kwa wakulima wetu,” alisema Jafo.

Mbali na uzinduzi wa mwongozo wa kilimo wa wilaya, Mhe. Jafo pia alikagua na kujionea shughuli mbali mbali zinazoendelea katika kanda hiyo inayounganisha mikoa ya Simiyu, Mara na Shinyanga na kujionea Vipando kutoka Halmashuri za Mikoa hiyo, Mabanda ya Biashara sambamba na kujionea shughuli ndogo ndogo za wajasiriamali zikiwepo shughuli za usindikaji.

Waziri huyo mwenye dhamana na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa alifanikiwa pia kutembelea Banda la Wizara yake pamoja na taasisi zilizo chini ya Wizara yake kisha kuwapongeza kwa namna wanavyo toa huduma kwa wananchi.

“Niwape pongezi kwa kweli kwa kazi kubwa mnayofanya, wingi wa watu wanaowafikia kutaka ufafanuzi wa masuala mtambuka ni ishara kwamba wananufaika na elimu mnayowapa hivyo endeleeni kutoa huduma,” alisema Waziri Jafo.

Mapema kabla ya kuzindua mwongozo huo, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Kisekta kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa bwana Leo Martin Mavika alieleza kuwa mwongozo huo unalenga kuelezea hatua kwa hatua namna ya kushirikisha wananchi na wadau mbalimbali katika kuandaa mpango wa maendeleo ya kilimo wa kijiji.

Aliongeza kuwa mwongozo huo pia unalenga kuunganisha mipango ya vijiji katika kata na hatimaye kupata mpango wa  wilaya.

Bwana Mavika alisema kuwa mwongozo huo utatumika katika kuandaa mipango ya kilimo kuanzia mwaka wa fedha 2019/20. Kabla ya kufikia kipindi hicho timu ya uwezeshaji wa taifa itatoa mafunzo ya namna ya kutumia mwongozo huo kwa mikoa na halmashauri zote Tanzania

Maonesho ya Nane Nane ya 2018 yanafanyika mkoani Simiyu na yanabebwa na kaulimbiu “Wekeza katika Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa Maendeleo ya Viwanda. 

PICHA: Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo azindua Operesheni Jokate yenye lengo la kuwaondoa wavamizi Wote Misitu ya Ruvu

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo amezindua "Operesheni Jokate" yenye lengo la kuwaondoa wavamizi wote wanaoendesha shughuli za kilimo na ufugaji katika misitu ya Ruvu Kusini na Kazimzumbwi wilayani humo. 

Jokate alizindua oparesheni hiyo   jana Agosti 7 akiwa kwenye msitu wa Ruvu Kusini ambako alienda na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya na maofisa wa Wakala wa Misitu ( TFS) kwa ajili ya kuwaondoa wavamizi waliopo humo.

Alisema lengo lake ni kuwasaka na kuwaondoa wavamizi ambao hawataki kufuata sheria na utaratibu wa hifadhi ya misitu katika msitu wa Ruvu Kusini uliopo wilayani humo.

Jokate alisema operesheni hiyo ni ya siku sita na imeanza  Agosti 7 ambapo katika siku ya kwanza ng'ombe zaidi ya 150 walikamatwa ndani ya msitu huo na zoezi la kuwakamata wamiliki wake linaendelea.


Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) Yanza zoezi la kuwapima umri wachezaji watakaoshiriki kwenye michuano ya CECAFA

$
0
0
Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) imeanza zoezi la kuwapima umri wachezaji watakaoshiriki kwenye michuano ya CECAFA Kanda ya 5 itakayofanyika hapa nchini kuanzia tarehe 11/08/2018.



Jinsi Punyeto Inavyo Sababisha Kusinyaa Na Kudumaa Kwa Maumbile Ya Kiume

$
0
0
Wanaume  wanao  jihusisha  na  upigaji  wa  punyeto  kwa  muda  mrefu  husalia  kuwa  na  maumbile  ya  kiume  yaliyo  sinyaa  na  kudumaa.

Kwa mujibu  wa  tafiti  mbalimbali  za  kitaalamu, kufanya  punyeto  kwa  muda  mrefu  huathiri  na  kuharibu  mishipa  na  misuli  ya  uume na  hivyo kusababisha  kujengeka  kwa  mafuta na  tishu  zisizo vutika  kwenye  mishipa  ya  ateri na  hivyo  kuzuia  mishipa ya  ateri  kupanuka na  kuongezeka  pamoja  na  damu  kutiririka  kwenda  kwenye  misuli  ya  uume.

Mambo  hayo  mawili yanapotokea  huathiri  uzalishaji  wa homoni muhimu  zinazo  husika  na ukuaji wa misuli ya  uume, na hatimaye  hufanya  uume  wa  mhusika  kudumaa, kusinyaa, kunywea  na  kurudi ndani  kiasi  cha  kuufanya  uonekane  kama wa  mtoto.

 Homoni  hizo hujulikana   kitaalamu kama  HGH  na  huzalishwa  kwenye  ini.

Sababu nyingine   inayo  tajwa  na  wataalamu  ni kwamba, mtu  anaye fanya punyeto   hutumia  akili,  nguvu na  nishati  nyingi sana, jambo ambalo  huathiri utendaji  wa  ogani  nyingine  muhimu  katika  mwili , likiwemo  ini.

Na kwamba  ini  linapo kosa  nishati   ya kutosha  hushindwa  kufanya kazi  zake  vizuri  na  moja  kati  ya  kazi kubwa  za  ini  ni  pamoja  na  uzalishaji  wa  homoni  zijulikanazo  kitaalamu kama  HGH  ambazo  kama  ilivyo andikwa  hapo juu, zinahusika na  kuchochea  ukuaji  wa  sehemu mbalimbali  katika  mwili  wa  mwanadamu  ikiwemo   misuli  ya  uume.

Mbali na  kuathiri  utendaji  wa  ogani  nyingine  mwilini, upigaji  punyeto  husababisha  athari nyingine  kwenye  mwili wa  mwanadamu  kama  vile uchovu  sugu  wa mwili  pamoja na kunyonyoka kwa  nywele.

Athari nyingine  za  upigaji punyeto  ni  pamoja  na  kupoteza  kumbukumbu, kuwahi  kufika  kileleni  ambako  husababishwa  na  kulegea  kwa  mishipa  ya  ateri, kushindwa  kurudia  tendo  la  ndoa, kukosa  hamu  ya  tendo  la  ndoa, uume  kusimama  katika  hali  ya  ulegelege,   maumivu  wakati  wa  tendo  la  ndoa  husuani  wakati  wa  kurudia  tendo  la pili na    mara  baada  ya  tendo  la  ndoa  la  kwanza.

KWANINI   WATU WENGI  WANAO  JIHUSISHA  NA  UPIGAJI  PUNYETO  WANA  MAUMBILE  MADOGO  YA  KIUME YALIYO  DUMAA, SINYAA  NA  KURUDI NDANI.

Uzeofu  unaonyesha  kuwa,  asilimia  kubwa  ya  wanaume  ambao  wamewahi  kufanya  punyeto  kwa  muda  mrefu, wanakabiliwa  na  tatizo  la kuwa  na  maumbile  ya  kiume yaliyo dumaa, sinyaa  na  kurudi ndani.

SABABU  KUBWA   NI  HII  HAPA
Sababu  kubwa  ni kwamba   vijana wengi  wa  kiume, huanza  kujihusisha  na  punyeto   wakiwa  na  miaka  kumi  na sita , kumi na  saba  au  chini  ya  hapo.

Hiki ni  kipindi  ambacho  vijana  hawa  ndio  wanakuwa  wamebalehe.

Na kwa mujibu  wa  tafiti  za kisayansi, katika  kipindi  hiki cha  balehe  ndio  kipindi  ambacho  homoni za  HGH  ambazo huhusika  na  ukuaji  wa  sehemu  mbalimbali  za  mwili  ikiwemo  maumbile ya  kiume, huzalishwa  kwa wingi.

Kama  tulivyo ona  hapo  juu, upigaji  punyeto  huathiri  uzalishwaji  wa   homoni  hizo.

Mwisho wa  siku  maumbile  ya  kiume  ya  wahusika, hushindwa  kukua  na  kuishia  kudumaa na  kusinyaa.

Na  hii ndio  sababu  kubwa  wanaume  wanao  kabiliwa  na  tatizo  hili  husalia  kuwa  na  maumbile yenye  ukubwa  ule  ule  walio kuwa  nao wakati wa  kubalehe

NINI  TIBA  ASILIA  YA  TATIZO  LA  KUDUMAA, KUSINYAA  NA  KURUDI NDANI KWA  MAUMBILE  YA  KIUME.
Kama uume wako  umedumaa, sinyaa, legea, nywea  na  kurudi ndani  kwa  sababu  ulifanya  punyeto  kwa  muda  mrefu  na  unataka  kuondokana  na  hali  hiyo. HII  NI HABARI NJEMA  SANA  KWAKO! 
 
Ipo dawa  ya ASILI   ambayo  HUTIBU  na  KUPONYESHA  KABISA  tatizo la  KUDUMAA, KUSINYAA, KUNYWEA  NA  KURUDI NDANI  KWA MAUMBILE  YA  KIUME kunako  tokana  na  ufanyaji  punyeto  wa  muda  mrefu.
 
Ni  dawa  ya  asili  kabisa ambayo  hutibu  na  kuponyesha  kabisa  tatizo  la kudumaa  na  kusinyaa  kwa  uume  ndani ya siku thelathini.

JINSI YA  KUPATA  TIBA  HII : Kupata  tiba  hii  fika  ka6ika  duka  la  kuuza  dawa  za  aslili  la  NEEMA  HERBALIST.  Tunapatikana  UBUNGO  jijini  DAR  ES  SALAAM  jirani  na  SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING  nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA.

Kwa wateja  waliopo  jijini  Dar  Es  Salaam  ambao  hawana  nafasi  ya  kufika  ofisini  kwetu  watapelekewa  dawa  mahali  walipo  ( HOME & OFFICE  DELIVERY )  na kwa  wateja  waliopo  nje  ya  mkoa  wa  Dar  Es  Salaam  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  usafiri  wa  mabus  au  boti  kwa  waliopo  Zanzibar.

Wasiliana  nasi  kwa  simu  namba  :    0693  005 189.

Kigwangalla kuhamishiwa Taasisi ya Mifupa (MoI)

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla anatarajiwa kuhamishiwa katika Taasisi ya Mifupa (MoI) pindi atakapokamilisha matibabu yake katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, alikolazwa tangu mwishoni mwa wiki.

Jana akijibu swali la mwandishi wa habari aliyetaka kujua maendeleo ya waziri huyo aliyepata ajali ya gari wiki iliyopita akiwa katika ziara ya kikazi, Mkurugenzi Mtendaji wa Moi, Dk Respicious Boniface alisema kuwa waziri huyo atahamishiwa kwenye taasisi hiyo wakati wowote. Alisema lengo la kumhamishia kwenye taasisi hiyo ni kuendelea na matibabu ya viungo vilivyovunjika.

Dk Boniface alikuwa akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu programu inayoendeshwa na taasisi hiyo ya uchunguzi wa umri kwa wachezaji wa timu ya taifa ya vijana walio chini ya miaka 17 ambao watashiriki michuano ya Cecafa itakayoanza jijini mwishoni mwa wiki.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images