Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Mbunge wa CCM Aliyenaswa kwa Rushwa AAchiwa kwa Dhamana

0
0
Mbunge wa Kishapu (CCM) Suleiman Nchambi na wenzake 10 wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera wakishtakiwa kwa kosa la kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Wakizungumza mahakamani  leo Jumatatu Agosti 6, 2018 waendesha mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru),  Dismas Muganyizi na Joseph Mulebya wamesema watuhumiwa hao walifanya  miamala ya rushwa kinyume na  kifungu cha 15 cha sheria namba 11 cha mwaka 2007 ya taasisi hiyo.

Amesema watuhumiwa hao kwa nyakati tofauti katika mgodi wa Stamigold ulioko wilayani Biharamulo kati ya Septemba 2015 hadi Oktoba 2016 walitenda kosa la kufanya miamala ya rushwa na kuvunja kifungu cha 15(1) (a&b) cha sheria namba 11 ya mwaka 2007 ya kupambana na kuzuia rushwa.

Mbele ya hakimu wa mahakama hiyo, Flora Ndale, Muganyizi  amewataja washtakiwa hao kuwa ni Clara Mwaikambo, Chacha Wambura, Christopher Mwinuka,  Sadick Kaswia, Fortunatus Rulemeja, Reginald Haule, Yasini  Mohammed, Fabian Ngelela , Felician Edward, Braithony Luchagula  na Nchambi.

Amesema Nchambi na Mohammed, Oktoba 2016 walifanya muamala wa rushwa na kumpatia Sh5 milioni mhasibu wa Stamigold co. Ltd ambaye ni Clara kama zawadi ya kupatikana malipo yao ya dola 170,945 za Marekani walizokuwa wakidai katika machimbo ya mgodi huo.

Washtakiwa hao wamekana mashtaka hayo na kuachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili wenye hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya Sh10milioni, huku mmoja akiwa mtumishi wa umma.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 3, 2018 itakapotajwa tena.

Serikali Yatarajia Kudahili Wanafunzi 380 Wa Kada Za Afya

0
0
Na WAMJW – TANGA
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, inatarajia kufanya udahili wa wanafunzi kwa asilimia 100 kutoka wanafunzi Mia moja na Hamsini (150) hadi Mia tatu themanini wa kada za Afya nchini.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Mhe. Ummy Mwalimu (Mb) wakati wa hafla ya makabidhiano ya majengo ya chuo cha Uuguzi Tanga, yaliyojengwa kupitia ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kupambana na UKIMWI, KIFUA KIKUU (TB) na MALARIA (Global fund).

Waziri ummy aliendelea kusema kuwa majengo yaliyokabidhiwa ni juhudi za Serikali kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo katika kuhakikisha wanazalisha wataalamu wa kada za Afya, hususani Wauguzi na Wakunga jambo litalowawezesha kuwa Wataalamu bora.

“Udahili wa wanafunzi umeongezeka kutoka 190 hadi 260, Huwa tunapata shida sana, wanafunzi wengi wanafaulu na tunakuwa hatuna nafasi ya wapi pakuwapeleka, kwahiyo tunawashukuru Global fund , tunaweza kudahili hadi wanafunzi 368” Alisema Waziri Ummy Mwalimu.

Aidha, amemwagiza Mkurugenzi wa Mafunzo na Rasilimali watu kutoka Wizara ya Afya kushirikiana na NACTE kuwachukua wanafunzi wote waliosoma na kufaulu vizuri masomo nya Sayansi na wenye vigezo na wenye vigezo katika kada ya Afya.

Waziri Ummy aliongeza kuwa, kutokana na jitihada hizo kumekuwepo na ongezeko la wahitimu ngazi ya astashahada na Stashahada kwa mafunzo kutoka wahitimu 4473 mwaka 2012/2013 hadi 7561 kwa mwaka 2016/2017 , ongezeko hili ni sawa na Asilimia 69.

Wakati huo huo Kaimu katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Otilia Gowelle amesema kwa mwaka huu wa fedha , Wizara imetenga shilingi Bilion 8 kwaajili ya ukarabati wa majengo chakavu katika chuo hicho.

Aliendelea kuwa Wakufunzi 143 wamepangiwa kufanya kazi katika vyuo vya Afya nchini, vikiwemo vyuo vya Wauguzi na Wakunga ambao ndio msingi wa kupunguza athari ya uzazi pamoja na vifo vya wakina mama wajawazito wakati wa kujifungua.

Nae Mwakilishi wa Global Fund Dkt. Hiltruda Temba amesema kuwa, Global fund imeboresha miundombinu yakufundishia katika vyuo 14 na kuwezesha kufadhili zaidi ya wanafunzi 1500 wa kada za Uuguzi na Ukunga wa Technolojia dawa, Technolojia maabara na Tabibu katika kipindi cha Mwaka 2015/2016 hadi 2017/2018, pamoja na kutenga shilingi Billion 1.1 kwaajili yakuboresha mifumo ya Afya.

Taarifa Kwa Umma Kuhusu Ufafanuzi Raia Kuzuiliwa Kuondoka Nchini

Waziri Mkuu Afungua Michezo Ya Majeshi Ya Polisi.....Awasisitiza wayatumie kwa kubadilishana taarifa za kiintelejensia

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka askari wanaoshiriki katika michezo ya Shirikisho la Majeshi ya Polisi Ukanda wa Afrika Mashariki watumie mashindano hayo kama fursa ya kubadilishana taarifa za kiintelijensia, kujadili namna ya kufanya operesheni za pamoja na kwa wakati mmoja.

Pia namna ya kushirikiana katika masuala ya kisheria ambayo mara nyingi yamekuwa vikwazo katika utendaji wao hasa katika shughuli za upelelezi ili kuendelea kuwatia hatiani wahalifu wanaovuka mipaka.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatatu, Agosti 6, 2018) wakati akifungua michezo ya Shirikisho la Majeshi ya Polisi Ukanda wa Afrika Mashariki yanayofanyika katika Uwanja wa Uhuru, Jijini Dar es Salaam.

“Wote tunaelewa kuwa makosa yanayovuka mipaka kama vile vitendo vya ugaidi, ujangili, usafirishaji haramu wa binadamu, biashara haramu ya silaha ndogo ndogo, bidhaa bandia, utakatishaji wa fedha haramu, biashara ya dawa za kulevya na mienendo ya wahalifu wanaovuka mipaka huathiri amani, usalama na maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika kanda yetu,” amesema.

Amesema uhalifu huo hauwezi kuzuiwa pasipo jitihada za makusudi na mikakati ya pamoja ya kupambana nayo, hivyo anatarajia kuwa michezo hiyo itatoa fursa ya kipekee kwa nchi wanachama kubuni mikakati mbalimbali ya kupambana na kuzuia uhalifu hasa ule unaovuka mipaka ya nchi zao.

Waziri Mkuu amesema kwa kufanya hivyo watakuwa wametimiza lengo la Shirikisho la Wakuu wa Polisi la Ukanda wa Afrika Mashariki. “Hivyo tutakuwa kwenye nafasi nzuri ya kuendeleza maendeleo ya kiuchumi na kijamii ambayo yameanza kuonekana katika Nchi zetu,”.

Kadhalika, Waziri Mkuu amewataka askari hao waendeleze ushirikiano huo kwa usalama wa ukanda wa Afrika Mashariki kwa sababu michezo ni moja ya nyenzo za kuleta na kuimarisha usalama na amani kwenye jamii.

Amesema kaulimbi ya mwaka huu ambayo ni ‘Michezo katika Kukuza Ushirikiano wa Kikanda wa Polisi, Amani na Usalama”. (“Sports for Promoting Police Regional Cooperation, Integration, Peace and Security”). inajieleza yenyewe kuhusu umuhimu wa kushirikiana katika kuleta amani na usalama.

Ufunguzi wa mashindano hayo yanayoshirikisha nchi saba kati 14 za Ukanda wa Afrika Mashiriki ambazo ni mwenyeji Tanzania, Uganda, Kenya, Sudani, Sudani Kusini, Burundi na Rwanda yameanza leo na yanatarajia kukamilika Agosti 12, 2018.

Rais Magufuli apokea barua kutoka kwa Rais wa China na kwa Nkurunziza

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na Balozi wa China hapa nchini Wang Ke ambaye pamoja na kufanya nae mazungumzo amewasilisha barua kutoka kwa Rais wa China Xi Jinping.

Katika mazungumzo hayo Wang Ke amemueleza Rais Magufuli kuwa uhusiano na ushirikiano wa Tanzania na China umeendelea kukua kwa kasi kubwa hususani katika masuala ya kiuchumi, ambapo miradi mbalimbali ya maendeleo imetekelezwa na inaendelea kutekelezwa na kwamba katika kipindi cha miaka 6 iliyopita uwekezaji wa China nchini Tanzania umekuwa mara kumi kutoka Shilingi Trilioni 1.58 hadi kufikia Shilingi Trilioni 15.82.

Wang Ke amemhakikishia Rais Magufuli kuwa China itaendelea kuwa mshirika muhimu wa maendeleo ya Tanzania.

Kuhusu ombi alilolitoa Rais Magufuli wakati meli ya matibabu ya China ilipokuja hapa nchini mwezi Novemba 2017, Wang Ke amesema Rais Xi Jinping ameshafanyia kazi ombi hilo kwa kutoa udhamini wa masomo kwa madaktari 20 watakaosomea ngazi ya uzamili na uzamivu katika matibabu ya ini na uboho (bone marrow) katika Chuo Kikuu cha Shandong cha China, na pia nafasi 30 za wataalamu watakaohudhuria semina ya mafunzo ya usimamizi wa hospitali.

Rais Magufuli amemshukuru Rais Xi Jinping kwa kutoa nafasi hizo za masomo na kwa mchango mkubwa wa China katika maendeleo ya Tanzania, na amemuomba Wang Ke kufikisha ujumbe wake kwa Rais Xi Jinping kuwa Tanzania itaendeleza na kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano wake wa kidugu na kihistoria na China.

Rais Magufuli ametoa wito kwa Wang Ke kuendelea kuwahimiza wawekezaji zaidi kuja kushirikiana na Tanzania katika uwekezaji kwenye maeneo mbalimbali kwa manufaa ya pande zote mbili na kwamba Serikali ya Tanzania itakuwa tayari kujenga mazingira mazuri ya uwekezaji na biashara.

Wakati huo huo, Rais Magufuli ameagana na Balozi wa Canada hapa nchini Ian Myles na Balozi wa Ubelgiji hapa nchini Paul Cartier baada ya Mabalozi hao kumaliza muda wao.

Baada ya mazungumzo hayo Mabalozi hao wameelezea kufurahishwa kwao na uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na nchi zao na wamempongeza Rais Magufuli na Serikali anayoiongoza kwa hatua kubwa za kuleta mageuzi ya kiuchumi, kuboresha utendaji kazi wa watumishi wa umma, kupambana na rushwa na kuboresha huduma za kijamii.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi Ezechiel Nibigira ambaye amewasilisha barua kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Burundi Pierre Nkurunziza.

Aidha, Rais Magufuli amefanya mazungumzo na Nibigira, mazungumzo ambayo yamehudhuriwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Susan Kolimba na Balozi wa Burundi hapa nchini Gervais Abayeho.

Kocha mpya wa Taifa Stars katangazwa leo, aliichezea Barcelona

0
0
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amemtambulisha winga wa zamani wa kimataifa wa Nigeria, Emmanuel Amunike kuwa kocha mpya wa timu ya taifa, Taifa Stars.

Karia amemtambulisha Amunike mwenye umri wa miaka 47 katika mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika hoteli ya New Africa mjini Dar es Salaam jioni hii baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili.
 
Amunike aliyeng’ara na Super Eagles katika fainali za Kombe la Dunia mwaka 1994 nchini Marekani akicheza wingi ya kushoto, mtihani wake wa kwanza utakuwa ni mchezo dhidi ya Uganda Septemba 8, mwaka huu mjini Kampala, kabla ya kuwafuata Cape Verde Oktoba 10 kukamilisha mechi zake za mzunguko wa kwanza kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).

Taifa Stars inakuwa timu ya kwanza ya taifa ya wakubwa Amunike kufundisha, baada ya awali kuwa kocha wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya kwao, Nigeria kuanzia mwaka 2014 hadi 2017.

Zaidi ya hapo, Amunike mwenye umri wa miaka 47 amefundisha klabu za Al Hazm ya Saudi Arabia, kama Kocha Msaidizi mwaka 2008 kabla ya kuhamia Julius Berger hadi mwaka 2011 alipojiunga na Ocean Boys, zote za Nigeria.
 
Alipoachana na U-17 ya Nigeria akaenda kufundisha Al Khartoum SC ya Sudan kuanzia mwaka 2017 hadi 2018 na sasa anakuja kuujaribu ‘mfupa’ uliowashinda wengi, Taifa Stars.  
 
Kisoka, Amunike aliibukia klabu ya Concord mwaka 1990 kabla ya kwenda kuchezea Julius Berger 1991, zote za kwao, Nigeria baadaye Zamalek ya Misiri mwaka 1991 hadi 1994 ndipo akahamia Ulaya.
 
Alianza na klabu ya Sporting CP ya Ureno kuanzia 1994 hadi 1996 kabla ya kuhamia Barcelona ambako alicheza hadi mwaka 2000 alipohamia Albacete zote za Hispania na mwaka 2003 alijiunga na Busan I’Cons ya Korea Kusini alikocheza hadi 2004 akahamia Al-Wehdat ya Jordan kumalizia soka yake.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya Agosti 7

Kigwangala amlilia Hamza Temba......Asherehekea Miaka 43 Akiwa Hospitalini

0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamis Kigwangala leo anaadhimisha siku yake ya kuzaliwa akiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili anakotibiwa.

Dk Kigwangala, leo Agosti 7, anatimiza miaka 43 ya kuzaliwa kwake. Waziri huyo alipata ajali ya gari Agosti 4 mwaka huu eneo la Magugu, Manyara.

Ameandika katika ukurasa wake wa twitter akimshukuru Mungu kwa kufikisha umri huyo.

“Leo ninatimiza miaka 43 toka nizaliwe. Ahimidiwe Allah aliye Mkuu kuwa bado nipo hai mpaka sasa. Najua ni kwa utashi na kusudio lake. Namshukuru na nazidi kuomba kwake shufaa, siha na mafanikio tele. Ninawashukuruni nyote kwa dua zenu. Tudumu kwenye sala ndugu zangu.” Ameandika.

Pia, ameutumia mtandao huo, kumkumbuka Ofisa Habari wa Wizara yake, Hamza Temba aliyefariki  dunia katika ajali hiyo.
 
“Sijui hata Kwa nini usiku huu nimegusa simu? 😭😭😭 Only to look at my phone and come across chats and pics za ziara yetu ya #PoriKwaPori and rise to the reality that mdogo wangu, bwashee wangu, this hard working, smart, handsome and very hopeful young man sintomuona tena na kumtania. What more can I say?! Alhamdulillah. Qaalu inna lillah wainna ilayhir rajiuun. 🙏🏿 #AllahAkbar“ 


Mkuu Mpya wa mkoa wa Mbeya ajiapiza kumng'oa Sugu jimboni 2020......Awataka wanaCCM Wavunje Makundi

0
0
Mkuu  wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila amekabidhiwa ofisi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo, Amos Makalla huku akijiapiza kuwa yuko tayari kutumbuliwa na Rais kama viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani humo, hawatakubali kuondoa makundi na kupoteza tena Jimbo la Mbeya Mjini.

Chalamila alitoa kauli hiyo wakati wa makabidhiano hayo jana na kudai kuwa kwa mtazamo wake anaona jimbo hilo kwa sasa lipo wazi na linaweza kurejea katika himaya ya CCM katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2020.

CCM ililipoteza kwa mara ya kwanza jimbo hilo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 1995, Polisya Mwaiseje (NCCR-Mageuzi) alipomshinda Bruno Mpangala, lakini ikalirejesha mwaka 2000 kupitia kwa Benson Mpesya.

Mwaka 2010, Mpesya aliangushwa na Joseph Mbilinyi 'Sugu' (Chadema) anayeendelea kuliongoza hadi sasa.

Katika makabidhiano hayo, Chalamila alisema kuwa pamoja na mtazamo wake huo wa uwezekano mkubwa wa kulirejesha CCM jimbo hilo, wanachama wa CCM wasishangae kushindwa tena ikiwa wataendelea na makundi makubwa yaliyo ndani ya chama hicho.

Alisema amekuwa akifuatilia migogoro ya CCM Mbeya tangu alipokuwa Iringa na amebaini kuna makundi makubwa ambayo yanaweza kukigharimu chama hicho.

“Endapo nitaondolewa kwa sababu ya CCM kupoteza jimbo hili, nitarudi kulima, nitamshukuru Rais na nitamwambia kuwa sijasikitika," Chalamila alisema na kuongeza:

"Kama mtataka ushirikiano wa kujenga, mimi kama kamisaa wa chama, nitawapa lakini kama ni ushirikiano wa kuvurugana sitawapa."

Aliongeza kuwa msimamo wake ni kufanya kazi bila kuingiliwa na kiongozi yeyote na yeyote atakayetaka kuingilia majukumu yake atamtaka kusoma katiba na miongozo ya chama.

Chalamila alimshauri Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya, Jacob Mwakasole na timu yake kuhakikisha wanapambana na kuyaondoa mapema makundi yaliyokivuruga chama hicho.

Alisema kuwa atakuwa tayari kutoa ushauri na kama wataona ushauri wake haufai, atawaacha na hatawaingilia katika uamuzi wao.

Kiongozi huyo wa serikali aliongeza kuwa kwa muda mrefu wananchi wa Mkoa Mbeya wamefarakanishwa kwa itikadi za kisiasa zilizokuwa zinasababishwa na baadhi ya viongozi.

Alimpongeza Makalla kwa jitihada alizozionyesha kwenye utatuzi wa migogoro ya ardhi katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo, hasa Mbarali na Rungwe.

Awali, Makalla ambaye amehamishiwa Mkoa wa Katavi, alimweleza Chalamila kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja na miezi minne, alikuwa anapambana na migogoro ya ardhi ambayo ndiyo ilikuwa changamoto kubwa mkoani humo.

Alisema baadhi ya migogoro alishaimaliza ikiwamo ya wananchi waliohamishwa wakati wa upanuzi wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha. Wananchi hao walikuwa wanalalamika kupunjwa malipo ya fidia.

“Nakuhakikishia kuwa tumeshirikiana na wakuu wa wilaya pamoja na viongozi wengine wakiwamo wa dini kumaliza baadhi ya changamoto, lakini nitakukabidhi baadhi ya migogoro ya ardhi kwa maandishi ili uendelee kuitatua,” alisema.

Makalla aliwataka wananchi na viongozi wa Mbeya kumpa ushirikiano Chalamila kama walivyofanya kwake wakati akiuongoza mkoa huo unaosifika kwa uzalishaji wa nafaka.

CHADEMA: Wabunge na Madiwani Mnaorubuniwa na CCM Ondokeni Haraka Mtupishe Tujenge Chama Chetu

0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Zanzibar), Salum Mwalimu, amesema milango ipo wazi kwa wabunge na madiwani wa chama hicho wanaokubali kurubuniwa na kukikimbia chama.

Alisema wabunge na madiwani hao hawana dhamira ya dhati ya kuwatumikia wananchi, hivyo wanaweza kwenda wanakorubuniwa.

Alisema hayo mwishoni mwa wiki mjini hapa wakati akiwahutubia mamia ya wananchi katika mkutano wa hadhara wa kumnadi mgombea udiwani wa Kata ya Bagara, Mathias Zebedayo.

"Kwa wale wenye njaa watakwenda, kwa wale wasio na hofu ya Mungu watakwenda na kwa wale ambao walikuwa hawana dhamira ya kweli watakwenda kwa kuwa walihitaji udiwani na ubunge, lakini wanaohitaji mapinduzi ya kweli watabaki,'' alisema.

Aidha, alidai Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilizoea kutumia nguvu za dola kuwaibia kura wapinzani wakaona mbinu hiyo haitoshi, sasa wameamua kuanza kuwanunua wabunge na madiwani.

Alisema Chadema inawaacha wabunge na madiwani wanaokubali kununuliwa ili waende kushirikiana na watu waliozoea wizi na ufisadi katika majimbo yao na halmashauri zao na kusababisha huduma za kijamii kukosekana.

Aliwaomba wakazi hao kumchagua mgombea udiwani wa Chadema ili waendelee kuleta maendeleo katika halmashauri hiyo kwa kuwa wameshaonyesha njia.

Alisema kwa mfano, wakati wanaichukua halmashauri walikuta makusanyo kwa mwezi ni Sh. milioni 700, lakini kwa sasa halmashauri chini ya Chadema inakusanya Shilingi bilioni mbili ambazo zinasaidia kuwaletea maendeleo.

Akimwombea kura za ndiyo mgombea wa Chadema, Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini, Pauline Gekul, aliwataka wananchi kujipanga kulinda kura zao.

"Wale ambao wamezoea kutuonea kwenye uchaguzi na kutuibia kura zetu awamu hii tumeandaa wazee wa kimila, ili wakituhujumu kwa njia yoyote wafe mtaona watakavyolaliana hapa wakifa mmoja baada ya mwingine,'' alisema.

Mgombea udiwani wa Kata ya Bagara, Mathias Zebedayo, aliwaomba kumchagua ili aweze kuyaendeleza yale yote aliyoshindwa mtangulizi wake kwa miaka mitatu iliyopita na kutimkia CCM.

Roma awatolea uvivu BASATA ....."Mnaua sanaa, ubunifu na vipaji."

0
0
Rapa Roma Mkatoliki ameamua kuwachana Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) huku akidai kuwa taasisi hiyo inaua sanaa, ubunifu na vipaji vya Watanzania.

Roma kupitia ukurasa wake wa Twitter amefunguka hayo na kuwaomba Watanzania waeleze makosa yanayopatikana kwenye wimbo wao mpya na Stamina wa Parapanda.

“BASATA You Are Killing 1. An Art 2. Creativity 3.Talent I don’t Hate The Industry I hate The System!! Hivi Wimbo Wa PARAPANDA Una Matatizo Gani??? Hebu Nisaidie Wewe Mtanzania Mwenzangu!!!!”ameeleza Roma Mkatoliki.

Jana  Agosti 6, 2018 Roma na Stamina waliitwa BASATA ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa BASATA alisema waliwatembelea tu kujua Sheria na kanuni mpya za baraza hilo.

Je Umepungukiwa Nguvu Za Kiume Na Umetumia Dawa Nyingi Bila Mafanikio?

0
0
Hakika nawashukuru wote mliotumia hii dawa na kunipa pongezi nyingi Sana sasa offa imeisha maana nilitoa ya wiki 2 tu     na watu wengi walioitumia wamepona kabisa 

Dawa hii ni dawa ya maajabu kabisa na huwezi kuamini ila wengi walioitumia wameiamini maana kati ya watu 89 walioitumia ndani ya wiki 2 watu76 wamepona kabisa na watu 9 hawajapona na watu 4 hawajatoa majibu! 

Dawa hii ni dawa inayotibu tatizo la upungufu wa nguvu za kiume na unapona kabisa, dawa hii ni dawa ya asili,(mitishamba) utaitumia mara moja tu na hautatumia dawa ya nguvu za kiume tena 

Dawa hii inawafaa watu kuanzia miaka 18 mpaka miaka 70, zaidi ya miaka hyo haitakusaidia ....watafiti wa dawa asilia pamoja na waganga  wameikubali pia dawa hii inawafaa hata wanawake wasiopata hisia za mapenzi 

Ukitumia hii dawa unakuwa na uwezo wa kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara 3 bila hamu kuisha, inauwezo wa ajabu na tiba bora kabisa

 SOMA DALILI HIZI;  kutokuwa na hamu ya tendo la ndoa 2 .kushindwa kurudia tendo la ndoa 3. kuwahi kufika kileleni 

Dawa hii imesaidia watu wengi sana dawa hii imegunduliwa na dr kiboko mganga wa tiba za jadi kutoka mafia pia tunatibu matatizo mbalimbali kama mambo ya biashara, nyota, kesi, mapenzi, nk, pia tunahitaji WAKALA wa kupokea dawa zetu katka nchi ya KENYA, ZAMBIA, UGANDA, mikoani tunatuma kwanjia ya mabasi au fika ofisini kwangu  Mafia kisiwani  

maelezo zaidi wasiliana na DR KIBOKO 0679923297

Kalulumila:Dawa Bora ya Nguvu za Kiume na Maumbile Madogo

0
0
 BORA YA NGUVU ZA KIUME NA MAUMBILE MADOGO KALULUMILA.
----------------------------------------
Ni dawa pekee iliyojipatia umaarufu nchini na nje ya nchi kwa kufanya kazi mara 3, kwa wakati mmoja 1, kurefusha uume na kunenepesha saizi uipendayo kuongeza nguvu za kiume na inatibu matatizo na gerentii miaka 30. Na kuendelea haina madhara, inaimarisha mishipa ya uume iliyoregea na udhalishaji wa mbegu za kiume. 


---------NINI HUCHANGIA MATATIZO HAYA--Ngiri ni chanzo kikubwa cha matatizo haya ili kujua kwamba una ngiri ni chanzo kikubwa cha matatizo haya, ili kujua kama unangiri dalili zake ni kufika haraka kileleni wakati wa tendo la ndoa, 2)kushindwa kurudia tendo la ndoa. 3)kutoa choo kama cha mbuzi. 4)tumbo kujaa gesi na kuunguruma. 5)kukosa choo kabisa. 6)maumbile kuingia ndani na kuwa mafupi. 7) korodani moja kuvimba 8)kutosikia hamu ya tendo la ndoa na maumivu ya kiuno wakati wa tendo la ndoa. 9)maumivu ya kiuno na mgongo pia tunatibu kisukari kwa siku7, presha, busha, bila kupasuliwa na magonjwa mbalimbali. 

---------------------------------------
TUPO TEGETA KWA NDEVU KARIBU NA MACHINJIO YA NGOMBE UTAONA OFSI IMEANDIKWA KALULUMILA HERBALIST CLINIC HOSPITAL SIMU .
----------------------------------------
-0655-557-182.
-0755-557182.
-0784-557-182.
PIA UTAWEZA KULETEWA POPOTE ULIPO.
---------------------------------------
KARIBUNI SANA.
----------------------------------------

Dr Kanengo: Bingwa Wa Tiba Asili Hutibu Matatizo Yafuatayo

0
0
NKURURU:-ni dawa inayotibu miguu kuwaka moto, kiuno tumbo kupooza kupoteza fahamu 

MALABALA; hutibu kisukari , uti wa mgogo, Change, pumu, busha, kaswende, kifua kikuu, muwasho sehemu ya siri 

NKURUNGU,: Ni dawa kutibu  N, B, G, POWER :-ni dawa ya kuongeza nguvu za kiume ni vidonge 20 

MPERAMPERA:- ni dawa ya kurudisha Mke, mme, mpenzi,mchumba aliyekuacha /kuteseka, ni kwa mda wa siku 2 tu kusafisha , pia kuna dawa za kupunguza vitambi(nyama uzembe), maziwa makubwa,michirizi, mikovu makubwa, chunusi sugu. 

NR SIX POWER:-inatibu upungufu wa nguvu za kiume kwa wasio weza kumudu tendo la ndoa itakufanya uwe na hamu ya kurudia tendo la ndoa zaidi ya Mara 4 bila hamu Kuisha, inaboresha maumbile madogo na inaimarisha misuri iliyo legea na kusinyaa una pona kabisa, ndani ya siku 4 tu 

GASELA:-ni dawa ya maajabu (9) yaliyoshindikana. (1)-Kisukari, vidonda vya tumbo, tezi dume,walioshindikanika kupata watoto(ugumba),busha bila oparesheni, (2)zindiko Kali Katika biashara yako (chuma ulete) ndo kiboko yao kumkamata mwizi aliye kuibia vitu vyako pikipiki, gari, n, k( 2)zindiko la nyumba, mashamba, viwanja,.(4)kukutolea sumu uliyo ikanyaga (Mtego) (5)ujiamini kutumia dawa ya maajabu Saba (6)kutoa mikafara mfano ugomvi ndani ya nyumba kufukuzwa kazini bila sababu (7)kutabiri nyota na kung'arisha (8)kurudisha Mali iliyo potea mazingira ya kutatanisha, kushinda kesi uliyo sumbuka nayo mda mrefu. (9)kufukuza majini wachafu ndani ya mji,.

Haya yote yanawezekana kwa DR KANENGO popote ulipo . Muone  DR KANENGO,anatibu nguvu za kiume anarefusha na kunenepesha uume kwa saizi uipendayo kwa muda mfupi sana, pamoja na kuwa na hamu ya kurudia tendo la ndoa mara 4 bila hamu kuisha Na utachelewa kufika kileleni kwa muda wa dakika 40 bila kuchoka .

Angalizo usitume meseji wala kubipu..
 
You can get it in all East African countries,,our service is fast and easy... contact Whatsapp 0784,47,59,46.Dar es salaam Tanzania. ,..Dr. KANENGO 0744,92,29,82...You are welcome.

Jux na Vanessa Wamewapa Changamoto Diamond na Wasafi Festival

0
0
Wasanii wa muziki wa Bongo fleva Juma Jux na Mpenzi wake Vanessa Mdee wamewapa changamoto kubwa Diamond na timu nzima ya WCB.

Jux na Vanessa ambao wamemaliza tour yao ya ‘In Love and Money’ ambayo imefanya vizuri sana kuliko ilivyotegemewa wameonekana kuwapa changamoto WCB ambao nao wametangaza kuja na Tour yao ya Wasafi Festival.

Babu Tale ambaye ni Meneja wa Diamond na mratibu wa Wasafi Festival amesema , kwamba mafanikio makubwa na tamasha hilo ni changamoto kwa tamasha la Wasafi Festival ambayo litaanza kutimua vumbi miezi michache ijayo.
 Katika Show ya Aug 4, 2018 Dar es salaam, kila msanii aliuwa kwa show kali na stage na mashabiki walijitokeza kuenjoy, show ilikua na mizuka ya hali ya juu na surprise za kutosha kutoka kwa Mirror, Lady Jaydee na Chid Benz.

List ya Wasanii walioperform ilikuwa ya kizazi sana, Weusi, MOCO, Navykenzo, Mimi Mars, Kreest wa Gabon, Jojo wa Gabon, Marioo, Ben Pol, Maua Sama, Brian Simba, na wengine kibao na HOST wa Show nzima alikuwa Presenter mkali kutoka show ya The Playlist, Times FM - Lil Ommy, THE MVP, Halfman, Half Amazing.




Hakikisheni Taarifa Mnazozitoa Wakati Wa Kusajili Kadi Zenu Za Simu Ni Sahihi, Vinginevyo Sheria Itafuata Mkondo Wake

0
0
Na. Vero Ignatus Arusha.
Mamlaka ya mawasiliano nchini TCRA imewataka wananchi kufahamu wajibu na haki zao wanazostahili  kupata kutoka kwenye mitandao inayotoa  huduma za mawasiliano sambamba na kutambua wajibu walionao kama watumiaji wa huduma za mawasiliano

Kaimu mkuu wa Kanda ya kaskazini Francis  Msungu amesema kuwa mamlaka inatoa elimu kwa wananchi kuzijua haki zao kutokana na mabadiliko yanayotokea ni mengi ya sayansi na teknolojia pamoja na maendeleo ya matumizi ya vifaa vya mawasiliano katika mitandao ya simu.

Amesema kwa sasa kumezuka wimbi la utapeli kupitia simu za mikononi,  hivyo wananchi  wametakiwa kuwa na tahadhari kubwa, wasikubali kurubuniwa katika vitu ambavyowanafahamuhawajashiriki Usitekeleze maagizo yeyote yahusuyo fedha kwa ujumbe wa maandishi,

"Mfano unatumiwa ujumbe kuwa umeshinda bahati na sibu katika
Mashindano ambayo hujashiriki, ukipokea ujumbe umetumiwa pesa na mtu usiyemfahamu usizitoe fedha hizo, hadi uthibitishe ya kwamba zimetumwa kwa nia nzuri"

Amewataka wananchi mara waonapo fedha imetumwa kwenye mitandao yao  na aliyezituma bado hajafahamika, ni vyema wakawa na subira hadi watakapo hakikisha zimetumwa kwa nia njema ili wasiingie kwenye matatizo.

"Watu huwa wanakosea pia yamkini zilitumwa kwa bahati mbaya, ukiwahi kuzitoa nawe unahesabika unaiba. "alisema

Amewataka watumiaji wa simu za mkononi kufahamu kuwa zipo tahadhari za kuchukuliwa ikiwepo kusajili namba kwa majina kamili  ya muhusika kwani ni takwa la kisheria, bila kusahau kwamba kila taarifa zinazoyolewa wakati wa usajili ziwe za sahihi.

Taarifa zako zikiwa za uongo hilo nikosa kisheria utapata adhabu ya kifungo au kulipa shilingi milioni 3 au vyote kwa pamoja.

Ameshauri kwamba yeyote akipoteza simu au kadi atoe taarifa kwa jeshi la polisi na kwa mtoa huduma, samba na kuchukua tahadhari mara uokotapo simu au kadi ya simu utoe taarifa kwa usalama wako zaidi

Wananchi wote wanaotembelea maonyesho  25 ya kilimo na sherehe za nanenane kanda ya kaskazini mwaka 2018 wanashauriwa kutembelea banda la TCRA ili waweze kupata elimu zaidi ya mawasiliano.

Kwanini Baadhi ya Wanaume Wana Maumbile Mafupi na Upungufu wa Nguvu za Kiume? Suluhisho Hili Hapa

0
0
KWANINI BAADHI YA WANAUME WANA MAUMBILE MAFUPI NA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME... DR SITTA NDO SULULISHO LAKO

Tatiza, hili limekuwa likiwaathiri watu wengi sana kisaikolojia hasa baadhi yao kujiona wako tofauti na wanaume wengine. Kwa kawaida, mwanaume anatakiwa awe na uume, usiopungua nchi 6-7au-8 ,vinginevyo mtu huyo anamatatizo.

Zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo hilo... baadhi ni  upungufu wa vichocheo vya, HORMONES ZA CETROGEN .

SUPER MIZIZI, ni dawa inayozalisha HORMONES ZA CETROGEN,na kufanya, uume kukuwa na kuongzeka sazi utakayo na kuzibua mrija iliyosinyaa,

NSHOLA; ni dawa bora, ya kurudisha nguvu za kiume kwa kutibu kabisa  tatizo hilo na kukupa  hamu ya  kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara nne 4 bila kuchoka 

Pia  kuna dawa za kutibu presha ya kupanda na kushuka, kisukari , kuondoa mafuta  mwilini na maumivu ya mgogo kiuno, matazo, ya hedhi kwa wanawake, hedhi zisizokuwa na mpangilio.

NKANYA; ni dawa ya mvuto wa kimapenzi ,mchumba mpenzi aliyekuacha, mke, mme atakurudia .

NKOMA; Ni dawa kuongeza HIPS na mguu wa bia kwa wadada ,

NGAKAMA ,ni dawa ya kutibu miguu kufa ganzi na kuwaka moto, huduma zetu ,zipo ,vizuri, popote pale dawa utaletewa! 

DR SITTA, amebobea kwa tiba asilia 

Kwa DAR ANAPATIKANA MBAGALA ZAKHEM, SONGEA BOMBAMBILI, SHINYANGA- KAHAMA MJINI, 

KWA MAELEZO ZAIDI  PIGA SIMU; 0763172670/ 0715172670,/

WOTE  MNAKARIBISHWA... KAMA, UTAKUWA NA TATIZO, UTAHUDUMIWA,

Watoto Wawili Wafariki Dunia Baada ya Nyumba Kuwaka Moto

0
0
Watoto wawili wa kike, mmoja wa mika miwili na mwingine wa miezi 6  wamefariki  dunia baada ya nyumba walimokuwa wamelala kuungua moto. Ajali hiyo imetokea usiku wa kuamkia leo Agosti 7 katika katika kijiji cha Rwazi kata ya Kikuku, Kagera.

Chanzo cha moto huo kinaelezwa kuwa ni  kibatari kilichokuwa kikiwaka, kuangukia godoro na chandarua.

Taarifa zinaarifu kuwa  wakati moto huo unaanza, mama wa watoto hao  alikuwa  amekwenda kwa jirani kuomba chumvi.

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Kagera Agustino Ollomi amesema amepokea taarifa hizo na akatoa  rai kwa wazazi na jamii kwa ujumla kuchukua tahadhari.

Kikwete Ataka Teknolojia Mpya Ya Kilimo, Ufugaji Iwafikie Wananchi.

0
0
Rais mstaafu, Jakaya Kikwete, ametaka teknolojia mpya ya kilimo, ufugaji na uvuvi inayoonyeshwa wakati wa maonyesho ya wakulima na wafugaji maarufu kama Nanenane, iwafikie wananchi ili kuwakwamua katika umasikini.

Kauli hiyo aliitoa juzi baada ya kutembelea vipando na mabanda katika maonesho hayo Kanda ya Mashariki yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. J. K. Nyerere mjini Morogoro.

Alisema pamoja na wataalamu wa sekta ya kilimo, ufugaji na uvuvi kujitahidi kuvumbua teknolojia mpya katika sekta hiyo, bado haiwafikii wananchi wa vijijini.

Hivyo amewataka watalaamu hao pamoja na kuongeza jitihada za kuvumbua, elimu hiyo waipeleke kwa wananchi ili kuondoa umasikini miongoni mwao.

“Kazi kubwa imefanyika ya utafiti, viwango vimeongezeka sana vya ubora, suala kubwa ni namna gani uvumbuzi unaofanywa na maabara kwenye vituo vyetu utawafikia wakulima,” alisema Kikwete.

Alisema ili kuondokana na umasikini kwa haraka, wataalamu wanatakiwa kutoa elimu kwa wakulima na wafugaji namna ya kulima na kufuga kibiashara na kuondokana na dhana ya kufanya kazi hizo kwa kujikimu peke yake.

Huna Sababu Ya Kuaibikatena............ Jipatie Dawa Bora Ya Nguvu Za Kiume, Maumbile Madogo Na Mvuto Wa Mapenz

0
0
Usikate tamaa ondoa maradhi yako, maana matatizo haya yamekua yakiasili watuwengi kisaikolojia hasa baada ya kujiona wako tofauti sana na wengine kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia (6-8) vinginevyo mtuhuyo anamapunguvu katika mwiliwake.

Kunasababu nyingi sana zinazosababisha matatizo haya, chango hushambulia never ambayo huasili misuli ya uume, Ngili :- hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kufanya tumbo kuunguluma na kujaa gesi, kolodani moja kuvimba au kuingia ndani pamoja na kutopata choo vizuli. Sababuhizi na nyingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba na marakwamara husababisha kukosa hamu ya kuludia tendo la ndoa na baadae kushindwa kabisa

MASISA 3POWER :- nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa mfumo wa vidonge, huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka 15-90 , inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii) inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa, itakufanya uludie tendo la ndoa zaidi ya mara nne (4) birahamu kuisha wara kuhisi kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya dk (20-30 )

YONINANI:- hurefusha na kunenepesha maumbile madogo ya uume uliosinyaa inchi 6-8 na unene wa sm 3-4 kwa mda mfupi sana,

SUPER MORINA :- nidawa inayotibu ama kutatua tatizo la kisukali kwawaliohangaika bila mafanikio, huondoa tatizo la kisukali na kupona kabisa, vilevile ninadawa ya magonjwa sugu km vile presha, vidondo vya tumbo, miguu kuwakamoto, muwasho mwilin, kaswende,uzazi nk.

LUGIMBA :- nidawa ya mvuto wa mapenzi, humtuliza mke, mme, mchumba, hawara au mtu yoyote umpendae na kumfanya akutimizie chochotekile unachokitaka kutoka kwake na kumfunga asiwe na mtu yoyote zaidi yako.

WASILIANA NA DR CHIPUPA NAPATIKANA DAR ES SALAAM KUMBUKA HUDUMAHII ITAKUFIKIA POPOTE ULIPO  0759208637 / 0622344969
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images