Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya leo Jumapili ya Agosti 5


Lugola atoa siku 15 kwa kampuni zilizofanya ufisadi NIDA

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola ametoa siku 15 kwa kampuni saba zilizobainika kufanya ufisadi katika mradi wa mfumo wa utambuzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), kurejesha Sh28.5bilioni walizolipwa, ili kuepuka kuwa wateja wa mahakama ya mafisadi.

Ametoa kauli hiyo  jana Jumamosi Agosti 4, mjini Dodoma ikiwa ni siku moja  baada ya kukutana na wamiliki wa kampuni hizo kuomba wawasilishe vielelezo vya malipo hayo, ambapo amezitaja kampuni hizo kuwa ni Gotham International Ltd (Sh2.8 bilioni), Iris Corporation Berhard (Sh22.9 bilioni), Gwiholoto impex Ltd (Sh 946.4 milioni), Skyes Travel Agent (Sh6 milioni), Dk Shija Paulo Rimoy (Sh27 milioni), Aste Insurance (Sh1.2 bilioni) na BMTL (Sh 569.1 milioni) ambayo imekubali kurejesha fedha hizo.

“Takwimu nilizonazo mahakama ile ya mafisadi bado ina uhaba wa mafisadi, mimi nina dhamana ya kuitafutia wateja. Nyinyi tuliohojiana muombe msiwe miongoni mwa wateja ninaoitafutia mahakama hiyo, na msilete mchezo na serikali hii ya awamu ya tano”, alisema Lugola

Kuhusu hatima ya aliyekuwa mkurugenzi wa Nida, Dickson Maimu na kampuni ya Iris Corporation Berhard ya nchini Malasia ambayo ililipwa Shilingi bilioni 32 na Nida kwa ajili ya kuleta mtambo wa kutengenezea kadi ghafi nchini, amesema itajulikana Agosti 17, 2018.

“Maimu ametusaidia kupata maelezo ya ziada kuhusu ile kampuni,baada ya siku 14 watakavyokuja ndio tutajua hatima yake, tutajua kama suala litaisha ama la,” alisema Lugola.

Julai 25, 2018 Lugola aliipa wiki mbili kampuni ya Iris na Ghotham kwenda ofisini kwake kujadiliana jinsi ya kumaliza suala hilo, ambapo jana Maimu na mmiliki wa kampuni ya Jack Ghotham waliitika wito wake na kutoa maelezo ya ziada ambayo yatawasaidia katika kutafuta ufumbuzi wa suala hilo.

Ufisadi huo katika mradi wa mfumo wa utambuzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), uligundulika katika ukaguzi uliofanywa na Mamlaka ya  Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA), Februari, 2016.

BASATA wafunguka ishu ya kumtaka Diamond alipie kibali cha kuhudhuria birthday ya Tiffah Afrika Kusini

$
0
0
Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) limekanusha taarifa zilizosambaa mtandaoni kwamba wamemtaka Diamond kwenda kulipia kibali cha kusafiri kwenda Afrika Kusini kwenye birthday ya mtoto wake Tiffah.

Hatua hiyo imekuja baada ya wiki moja iliyopita baraza hilo kutangaza sheria mpya zinazowakata wasanii kuomba vibali wanapotaka kwenda nje ya nchi kwaajili ya show zao.

Basata wamesema sio kweli kwamba wamemtaka Diamond kuchukua kibali cha kwenda kuhudhuria birthday ya mtoto wake kama inavyoadiwa katika mitandao ya kijamii.

“Tunapenda kuutarifu umma kuwa taarifa inayosambaa kwamba Msanii Diamond anatakiwa kuchukua kibali BASATA kwenda kuhudhuria sherehe ya kuzaliwa mwanaye si ya kweli,” wameandika Basata kupitia mtandao wao.

Waliongeza “Vibali vya wasanii kwenda nje havihusiani na safari binafsi. Tunazidi kuwakumbusha wasanii kufuata taratibu zote wanapoenda kufanya maonesho nje ya nchi.,”

Wiki moja iliyopita muimbaji huyo alizuiwa na Basata kwenda kufanya show nje kwa kuwa hakuchukua kibali cha kwenda kufanya show nje ya nchi lakini baadae aliweza kufuata taratibu za kuchukua na kusafiri.

Timbulo: Siwezi Kuvaa Kikuku, tena sahau kabisa

$
0
0
Msanii wa muziki Bongo, Timbulo amejibu iwapo anaweza kuvaa kikuku. Muimbaji huyo anayetamba na ngoma yake mpya 'Sangoma' amesema hawezi kufanya hivyo kabisa.

"Hapana hiyo, sahau kabisa; siwezi kwa sababu mimi hata hereni tu sijawahi kuvaa," Timbulo ameiambia The Playlist ya Times Fm.

Utakumbuka hivi karibuni msanii Diamond Platnumz aliposti picha katika ukurasa wake wa Instagram ikimuonyesha amevalia kikuku mguuni kitu kilichoibua mjadala mpana katika mitandao.

Polepole Amkataa Joshua Nassari

$
0
0
Chama cha Mapinduzi (CCM), kimemtaka mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari kutofikiria kuomba kujiunga nacho kwa madai kuwa hana viwango vinavyoendana na CCM.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole alitoa kauli hiyo jana asubuhi wakati akihojiwa na kituo kimoja cha redio.

Kauli hiyo ya Polepole ilitokana na watangazaji wa kipindi hichokutaka kujua ukweli wa tuhuma zilizowahi kutolewa na Nassari juu ya CCM kushiriki mchezo mchafu wa kuwanunua madiwani kutoka Chadema.

Watangazaji hao walitaka kufahamu upi msimamo wa CCM kuhusu tuhuma hizo na kauli aliyowahi kuitoa aliyekuwa mkuu wa Wilaya wa Arumeru, Alexander Mnyeti kuwa Nassari naye kama anataka ‘kununuliwa’ aende dau lake ni kubwa.

Mtangazaji aliuliza, “kama unachosema ni kweli kwamba CCM hainunui wapinzani ni ipi kauli yenu kuhusu madai ya Nassari na kauli aliyoitoa Mnyeti kuwa fedha zipo wanaotaka kununuliwa waende na dau la Nassari ni kubwa?”

Akijibu swali hilo, Polepole alisema, “kwanza huyo Nassari asifikirie kuja CCM maana hana viwango vyetu na kule Arumeru Mashariki asubiri 2020 kuna mtu wetu tumemuandaa anaenda kulichukua lile jimbo.”

Nassari alipotafutwa  kuzungumzia kauli hiyo alijibu kwa kifupi, “ukiwa safarini kama nilivyo mimi nikiwahudumia watu wa Meru halafu akatokea mbwa anabweka ukimrushia mawe utapoteza muda kufika safari yako, hivyo huyo nampuuza maana hajui anachokifanya.”

Kuhusu hamahama ya wabunge na madiwani wanaotoka upinzani kwenda CCM, alisema hilo ni suala la utawala bora na si kweli kwamba marudio ya uchaguzi yanaharibu bajeti nyingine.

“Pesa ya uongozi bora ipo, si kweli kwamba tunapofanya uchaguzi pesa ya elimu inapunguzwa, hapana. Ndiyo sababu Tume ya Uchaguzi ina bajeti yake ila tatizo linakuja hapa ikiwa upande wa CCM, ila wakifanya vyama vingine inaonekana ni sawa,” alisema.

“Juzi Chadema imewafukuza madiwani wake kule Mbeya, lakini hilo halionekani kuwa tatizo wala kuleta hasara maana lazima uchaguzi utafanyika ila ikifanya CCM inaonekana nongwa, hizi ni siasa za double standard.”

Polepole pia alizungumzia suala la wapinzani wanaohamia CCM kusimamishwa kwenye uchaguzi na kueleza kuwa msingi wa chama hicho unasisitiza usawa kwa wote, hivyo hata wanaohamia wana haki ya kuchagua au kuchaguliwa.

Alisema wagombea wote wanaosimamishwa kanuni na taratibu za chama hicho zinazingatiwa na anashangazwa na watu wanaoonekana kuguswa na mambo yanavyokwenda ndani ya CCM.

Lugola awageukia viongozi wenzake.....Ataka Madereva Wa Serikali Wanaovunja Sheria Wakamatwe

$
0
0
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola, ameliagiza Jeshi la Polisi nchini kuwachukulia hatua kali viongozi wa serikali pamoja na madereva wao wanapovunja sheria za usalama barabarani.

Amesema madereva wa viongozi wa serikali wamekuwa vinara kwa uvunjaji Sheria za Usalama barabarani na kulitaka Jeshi hilo liwashughulikie bila kuangalia vyeo walivyo navyo.

Alitoa agizo hilo jana wakati akizindua rasmi Baraza jipya la Taifa la Usalama Barabarani jijini hapa.

Akionyesha kukerwa na ajali hizo, alisema takwimu za Jeshi la Polisi nchini zinaonyesha kuwa madereva wa viongozi wa serikali wamekuwa wakiongoza katika matukio ya uvunjaji wa Sheria za Usalama Barabarani kwa kiwango cha juu.

Pia madereva hao wamekuwa wakilalamikiwa kwa kuendesha mwendo kasi kinyume na sheria huku viongozi wao wakikaa kimyaa bila kuwaonya.

"Kiongozi ambaye dereva wake atabainika kuendesha kinyume cha sheria zetu za nchi achukuliwe hatua stahiki kama ilivyo kwa madereva wengine bila kujali anamwendesha bosi gani," alionya Lugola.

Aidha, aliwataka viongozi mbalimbali wa serikali kuwa mfano katika kusimamia sheria za nchi kwa kuendesha kwa tahadhari ili kupunguza ajali ambazo zimekuwa zikitokea kutokana na mwendo kasi.

"Sheria imewekwa ili kumlinda kila raia na ndiyo maana leo hii mtu akinywa sumu na akanusurika kufa anashtakiwa, hivyo basi kama wewe kiongozi upo na dereva wako anasababisha ajali kizembe atachukuliwa hatua kali kama ilivyo kwa watu wengine bila kumwonea huruma," alisema.

Alisema Sheria ya Usalama Barabarani inatakiwa kufanyiwa marekebisho ili kutoa adhabu kali ambayo madereva wengi watawajibishwa na kupunguza ajali za kizembe.

"Hivi sasa mtu anaposababisha ajali anakuwa na shauku sana ya kufikishwa mahakamani. Hii yote ni kwasababu ya kile ambacho atakikuta huko, akifikishwa mahakamani na akakiri kosa anapewa faini ambayo ni ndogo ukilinganisha na ajali aliyosababisha," alisema Lugola.

Aidha, alisema Jeshi la Polisi kupitia kitengo cha usalama barabarani wapo katika operesheni ya ukaguzi wa leseni kwa watu ambao walipatiwa bila ya kwenda shule na watakao bainika watafutiwa umiliki.

"Kuna watu walipatia leseni mezani sasa ni muda mwafaka wa kufanya ukaguzi kama ambavyo Rais Magufuli alivyokagua watumishi wasio na vyeti na sisi tunakagua walio na leseni bila vyeti na watakao bainika tutazifungia leseni zao," alisema.

Hata hivyo, alilitaka Jeshi la Polisi nchini kuongeza umakini katika kusimamia Sheria za Usalama Barabarani ili kukomesha ajali zinazotokea mara kwa mara nchini.

Naye Mjumbe wa Baraza hilo la Usalama Barabarani, Hamza Kasongo, alisema kwa kushirikiana na wadau mbalimbali watahakikisha wanaanza kumaliza tatizo la ajali za barabarani hasa kwa magari ya serikali.

"Madereva wetu wakiwa wanaendesha STK au STL huwa wananajiona wao ni watu maalumu sana na kuvunja sheria za usalama barabarani kwa kuendesha ovyo na kupita kwa mwendo kasi hata maeneo wasiyo ruhusiwa kufanya hivyo, sasa ndiyo tutaanza nao kwa kuwashughulikia," alisema Kasongo.

Waziri Mkuu Aupongeza Uongozi Wa Makumbusho

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameupongeza uongozi wa Makumbusho ya Taifa kwa kuchora ramani ya Tanzania katika Kijiji cha Makumbusho ambayo itatumika kwenye ujenzi wa nyumba za utamaduni wa makabila mbalimbali nchini.

Amesema uamuzi huo utarahisisha watu kufika kwa urahisi katika nyumza za tamaduni za mikoa yao kwa kuwa watakuwa wanatumia ramani Tanzania.

Waziri Mkuu aliyasema hayo jana Jumamosi, Agosti 4, 2018 wakati akizungumza na wakazi wa mkoa wa Lindi kwenye kikao cha kujadili maandalizi ya Tamasha la Utamaduni wa Mtanzania katika Kijiji cha Makumbusho, jijini Dar es Salaam.

“Kwa kutumia ramani hii kila mkoa utaweza kufika kwenye eneo lake kwa kutumia ramani ya Tanzania na mkoa wa Lindi tayari umeshaoneshwa eneo lake kwa ajili ya ujenzi wa nyumba inayozingatia utamaduni wetu,” alisema.

Alisema kwa tamaduni za makabila ya mkoa wa Lindi nyumba zote hujengwa kwa udongo na kuezekwa kwa makuti upande wa maeneo ya pwani ya upande mwingine huezeka kwa nyasi, ambapo aina zote zitajengwa ili kuwakilisha tamaduni za wakazi wa mkoa huo.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewaasa wananchi wa mkoa wa Lindi ambao kwa mwaka huu ndio waandaaji wa tamasha hilo wadumishe mshikamano wao ili waweze kutimiza malengo waliyojiwekea katika kuboresha maendeleo.

Alisema katika tamasha hilo ambalo linatarajiwa kuanza Agosti 26 hadi 29 wahakikishe wanapeleka kila kitu ambacho kinahusiana na utamaduni wa mkoa huo ili kuwawezesha Watanzania wengine wajue kama vyakula na mavazi .

Pia alishauri wawepo wazee wenye kujua historia ambao watasimulia utamaduni wa wananchi wa Lindi pamoja na kutambulisha ngoma zao za utamaduni. “Halmashauri zote za mkoa wa Lindi zitumie fursa hii kutangaza vivuti vya utalii vilivyopo na Kilwa walete mtu atakayeelezea kuhusu magofu,”.

Waziri Mkuu alisema tamasha hilo ni muhumu kwa sababu utamaduni ulianza kufifia nchini kutokana  na mabadiliko ya kiteknolojia jambo ambalo lingeweza kuuondoa katika kumbukumbu, hivyo aliwashauri siku ya tamasha hilo wavae nguo za kitamaduni kulingana na kabila husika.

Kadhalika, Waziri Mkuu aliwapongeza viongozi wa mkoa wa Lindi wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa Bw. Godfrey Zambi kwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo ikiwa ni pamoja na kusimamia vizuri mwenendo wa zao la korosho.

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Profesa Audax Mabulla alisema mwaka huu Tamasha la Utamaduni wa Mtanzania linawakilishwa na jamii kutoka mkoa wa Lindi na kwamba anatumaini watafanya vizuri kwa kuwa uwezo na nia wanayo.

Profesa Mabula alisema mwaka 1994 Bodi ya Makumbusho ya Taifa ilianzisha siku ya utamaduni ili kutoa fursa kwa jamii mbalimbali nchini kuonesha utajiri walionao katika tamaduni zao na ufanisi wa siku hiyo unatokana ushirikishwaji wa wanajamii husika.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, AGOSTI 5, 2018.

Ajali yaua wanafunzi 9.....Kenyatta Aomboleza

$
0
0
Wanafunzi tisa wa Shule ya msingi ya St. Gabriel huko Mwingi, Kaunti ya  Kitui nchini Kenya, wamefariki huku  wengine 32 wakiwa wamejeruhiwa katika ajali iliyohusisha basi ya shule na lori usiku wa Jumamosi kuamkia leo.

Wanafunzi nane wametajwa kufariki katika eneo la ajali hiyo huku mmoja ambaye anaongeza idadi ya kufika tisa amefariki akiwa hospitali ya taifa wakati anapatiwa matibabu.

Wanafunzi hao walikuwa wakitokea Mombasa kwenda katika safari ya kimasomo ambapo basi lao liligongana uso kwa uso na Lori katika daraja la Kanginga, Kilomita moja kutoka mji wa Mwingi kwenye barabara ya Thika-Garissa usiku wa manane.

Aidha kati ya majeruhi 32 ya wanafunzi ya waliofikishwa katika Hospitali ya Mwingi, wanafunzi Sita wanadaiwa kuwa katika hali mbaya (mmoja amefariki na kubaki watano)  ambapo wameshahamishwa katika hospitali ya Taifa ya Kenya, (Kenyatta National Hospital).

Wanafunzi nane waliofariki ni kati ya abiria 50 waliokuwa kwenye basi hilo pamoja na walimu.

Katika ujumbe wake kwa wazazi na walezi wa wanafunzi, Rais Kenyatta amesema ni bahati mbaya kwamba maisha ya wanafunzi wasio na hatia yamekatisshwa na kwamba  "Tumewapoteza wale ambao tulitegemea kujenga nao taifa siku za usoni".

Aidha Dereva wa lori hilo tayari amekwishakamatwa na Jumatatu atafikishwa mahakamani.



Waziri Mkuu Amjulia Hali Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla Muhimbili

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasili katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH)  kumjulia hali Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla aliyepata ajali ya gari jana Jumamosi Agosti 4, 2018.

Dk Kigwangalla alipata ajali eneo la Magugu mkoani Manyara na kupata majeraha sehemu mbalimbali mwilini. Katika ajali hiyo ofisa habari wa wizara hiyo, Hamza Temba alifariki dunia.

Majaliwa alifika hospitalini hapa saa 4 asubuhi akiwa ameambatana  na mkewe na kupokewa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Waziri huyo aliyepata ajali hiyo, Babati mkoani Manyara, amelazwa wodi ya Mwaisela akiendelea na matibabu.

Awali, Kigwangalla alipatiwa matibabu katika kituo cha afya cha Magugu na kuhamishiwa hospitali ya Arusha Lutheran Medical Center kwa helkopta na kisha kuletwa Muhimbili jana jioni.

Rais Maduro wa Venezeula Anusurika Kuuawa

$
0
0
RAIS wa Venezuela,  Nicolas Maduro,  ameapa kuhakikisha kuwa sheria inachukua mkondo wake baada ya jaribio linalodaiwa kufanyika dhidi ya maisha yake ambalo anasema limepangwa na rais wa Colombia Juan Manuel Santos.

Ndege zisizokuwa na rubani zikiwa na milipuko zililipuka karibu na rais huyo katika jaribio la kutaka kumuua ambalo lilitokea wakati akitoa hotuba kwa maelfu ya wanajeshi ambayo ilikuwa inatangazwa moja kwa moja katika televisheni.

“Hili lilikuwa jaribio la kutaka kuniua,” alisema baadaye alipolielezea tukio hilo. “Leo walijaribu kuniua.”

Waziri wa Habari,  Jorge Rodriguez,  alisema tukio hilo lilitokea muda mfupi baada ya saa 11.30 jioni saa za Venezuela  wakati Maduro alikuwa akisherehekea siku ya jeshi la taifa. 

Kiongozi huyo ambaye alionekana dhahiri kuingiwa woga alisema aliona “kitu kinaruka angani ” ambacho kililipuka mbele ya macho yake. Alidhani huenda ni kitu kilichokuwa kimelengwa kwa ajili ya maonyesho kwa heshima ya sherehe hiyo.

Katika muda wa sekunde kadhaa, Maduro alisema alisikia mlipuko wa pili na mtafaruku ulifuatia. Walinzi wake walimuondoa Maduro kutoka katika mahali hapo na picha za televisheni zilionyesha wanajeshi waliokuwa katika sare za jeshi walioikuwa wamesimama katika utaratibu fulani haraka wakitawanyika kutoka katika eneo hilo.

Alisema , “kundi la mrengo wa kulia” likifanya kazi kwa uratibu na wapinzani mjini Bogota na Miami, ikiwa ni pamoja na Rais wa Colombia, Juan Mnuel Santos, wanahusika. 


Baadhi ya “wale waliotoa baadhi ya vifaa ” vilivyotumika katika shambulio hilo tayari wameshakamatwa akiongoza  uhunguzi utafanyika kubaini kiini cha shambulio hilo bila kujali nani atahusika

Kundi lisilojulikana la waasi ambalo linaundwa na raia wa Venezuela na wanajeshi lilidai kuhusika na shambulio hilo la kutaka kumuua Maduro, hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyowekwa katika mtandao wa kijamii.

“Ni kinyume na hadhi ya jeshi kuwalinda watu katika serikali ambao hawakusahau tu katiba , lakini pia ambao wamefanya ofisi za umma kuwa ni fursa ya kujitajirisha,” kundi hilo limesema.

Kwanini Baadhi ya Wanaume Wana Maumbile Mafupi na Upungufu wa Nguvu za Kiume? Suluhisho Hili Hapa

$
0
0
KWANINI BAADHI YA WANAUME WANA MAUMBILE MAFUPI NA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME... DR SITTA NDO SULULISHO LAKO

Tatiza, hili limekuwa likiwaathiri watu wengi sana kisaikolojia hasa baadhi yao kujiona wako tofauti na wanaume wengine. Kwa kawaida, mwanaume anatakiwa awe na uume, usiopungua nchi 6-7au-8 ,vinginevyo mtu huyo anamatatizo.

Zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo hilo... baadhi ni  upungufu wa vichocheo vya, HORMONES ZA CETROGEN .

SUPER MIZIZI, ni dawa inayozalisha HORMONES ZA CETROGEN,na kufanya, uume kukuwa na kuongzeka sazi utakayo na kuzibua mrija iliyosinyaa,

NSHOLA; ni dawa bora, ya kurudisha nguvu za kiume kwa kutibu kabisa  tatizo hilo na kukupa  hamu ya  kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara nne 4 bila kuchoka 

Pia  kuna dawa za kutibu presha ya kupanda na kushuka, kisukari , kuondoa mafuta  mwilini na maumivu ya mgogo kiuno, matazo, ya hedhi kwa wanawake, hedhi zisizokuwa na mpangilio.

NKANYA; ni dawa ya mvuto wa kimapenzi ,mchumba mpenzi aliyekuacha, mke, mme atakurudia .

NKOMA; Ni dawa kuongeza HIPS na mguu wa bia kwa wadada ,

NGAKAMA ,ni dawa ya kutibu miguu kufa ganzi na kuwaka moto, huduma zetu ,zipo ,vizuri, popote pale dawa utaletewa! 

DR SITTA, amebobea kwa tiba asilia 

Kwa DAR ANAPATIKANA MBAGALA ZAKHEM, SONGEA BOMBAMBILI, SHINYANGA- KAHAMA MJINI, 

KWA MAELEZO ZAIDI  PIGA SIMU; 0763172670/ 0715172670,/

WOTE  MNAKARIBISHWA... KAMA, UTAKUWA NA TATIZO, UTAHUDUMIWA,

Dr Kanengo: Bingwa Wa Tiba Asili Hutibu Matatizo Yafuatayo

$
0
0
NKURURU:-ni dawa inayotibu miguu kuwaka moto, kiuno tumbo kupooza kupoteza fahamu 

MALABALA; hutibu kisukari , uti wa mgogo, Change, pumu, busha, kaswende, kifua kikuu, muwasho sehemu ya siri 

NKURUNGU,: Ni dawa kutibu  N, B, G, POWER :-ni dawa ya kuongeza nguvu za kiume ni vidonge 20 

MPERAMPERA:- ni dawa ya kurudisha Mke, mme, mpenzi,mchumba aliyekuacha /kuteseka, ni kwa mda wa siku 2 tu kusafisha , pia kuna dawa za kupunguza vitambi(nyama uzembe), maziwa makubwa,michirizi, mikovu makubwa, chunusi sugu. 

NR SIX POWER:-inatibu upungufu wa nguvu za kiume kwa wasio weza kumudu tendo la ndoa itakufanya uwe na hamu ya kurudia tendo la ndoa zaidi ya Mara 4 bila hamu Kuisha, inaboresha maumbile madogo na inaimarisha misuri iliyo legea na kusinyaa una pona kabisa, ndani ya siku 4 tu 

GASELA:-ni dawa ya maajabu (9) yaliyoshindikana. (1)-Kisukari, vidonda vya tumbo, tezi dume,walioshindikanika kupata watoto(ugumba),busha bila oparesheni, (2)zindiko Kali Katika biashara yako (chuma ulete) ndo kiboko yao kumkamata mwizi aliye kuibia vitu vyako pikipiki, gari, n, k( 2)zindiko la nyumba, mashamba, viwanja,.(4)kukutolea sumu uliyo ikanyaga (Mtego) (5)ujiamini kutumia dawa ya maajabu Saba (6)kutoa mikafara mfano ugomvi ndani ya nyumba kufukuzwa kazini bila sababu (7)kutabiri nyota na kung'arisha (8)kurudisha Mali iliyo potea mazingira ya kutatanisha, kushinda kesi uliyo sumbuka nayo mda mrefu. (9)kufukuza majini wachafu ndani ya mji,.

Haya yote yanawezekana kwa DR KANENGO popote ulipo . Muone  DR KANENGO,anatibu nguvu za kiume anarefusha na kunenepesha uume kwa saizi uipendayo kwa muda mfupi sana, pamoja na kuwa na hamu ya kurudia tendo la ndoa mara 4 bila hamu kuisha Na utachelewa kufika kileleni kwa muda wa dakika 40 bila kuchoka .

Angalizo usitume meseji wala kubipu..
 
You can get it in all East African countries,,our service is fast and easy... contact Whatsapp 0784,47,59,46.Dar es salaam Tanzania. ,..Dr. KANENGO 0744,92,29,82...You are welcome.

Huna Sababu Ya Kuaibikatena............ Jipatie Dawa Bora Ya Nguvu Za Kiume, Maumbile Madogo Na Mvuto Wa Mapenz

$
0
0
Usikate tamaa ondoa maradhi yako, maana matatizo haya yamekua yakiasili watuwengi kisaikolojia hasa baada ya kujiona wako tofauti sana na wengine kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia (6-8) vinginevyo mtuhuyo anamapunguvu katika mwiliwake.

Kunasababu nyingi sana zinazosababisha matatizo haya, chango hushambulia never ambayo huasili misuli ya uume, Ngili :- hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kufanya tumbo kuunguluma na kujaa gesi, kolodani moja kuvimba au kuingia ndani pamoja na kutopata choo vizuli. Sababuhizi na nyingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba na marakwamara husababisha kukosa hamu ya kuludia tendo la ndoa na baadae kushindwa kabisa

MASISA 3POWER :- nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa mfumo wa vidonge, huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka 15-90 , inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii) inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa, itakufanya uludie tendo la ndoa zaidi ya mara nne (4) birahamu kuisha wara kuhisi kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya dk (20-30 )

YONINANI:- hurefusha na kunenepesha maumbile madogo ya uume uliosinyaa inchi 6-8 na unene wa sm 3-4 kwa mda mfupi sana,

SUPER MORINA :- nidawa inayotibu ama kutatua tatizo la kisukali kwawaliohangaika bila mafanikio, huondoa tatizo la kisukali na kupona kabisa, vilevile ninadawa ya magonjwa sugu km vile presha, vidondo vya tumbo, miguu kuwakamoto, muwasho mwilin, kaswende,uzazi nk.

LUGIMBA :- nidawa ya mvuto wa mapenzi, humtuliza mke, mme, mchumba, hawara au mtu yoyote umpendae na kumfanya akutimizie chochotekile unachokitaka kutoka kwake na kumfunga asiwe na mtu yoyote zaidi yako.

WASILIANA NA DR CHIPUPA NAPATIKANA DAR ES SALAAM KUMBUKA HUDUMAHII ITAKUFIKIA POPOTE ULIPO  0759208637 / 0622344969

Nape: CHADEMA Mnapoteza Muda tu

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitaibuka na ushindi katika Jimbo la Buyungu lililopo mkoani Kigoma, hivyo wapinzani wasipoteze muda wao bure.

Amesema kuwa takwimu za tathmini ya maendeleo ya kampeni jimboni Buyungu zinaonyesha kuwa CCM inaongoza kwa mvuto miongoni kwa wapiga kura na kwamba huenda chama hicho kikashinda kwa zaidi ya asilimia 70.

Aidha, Nape amewataka viongozi wa vyama vya upinzani na wagombea wao kuzungumza kwa takwimu wanapoeleza mafanikio ya mambo yaliyofanywa na wabunge wao badala ya kupiga makelele na kuwadanganya wananchi na kwamba wakati wa wapinzani kupiga kelele na kudanganya wananchi umekwisha.

PICHA: Waziri Mkuu Akimjulia Hali Waziri Kigwangala Na Msanii Majuto

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na Mkewe Mary wakimpa pole Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamisi Kigwangalla, ambaye amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, jijini Dar es salaam Agosti 5, 2018, akipewa matibabu baada ya kupata ajali.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamisi Kigwangalla, ambaye amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, jijini Dar es salaam akipatiwa matibabu baada ya kupata ajali Agosti 5, 2018,
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa na Mkewe Mary wakimpa pole Msanii Amri Athumani (Mzee Majuto), ambaye amelazwa katika hospitali ya Muhimbili, jijini Dar es salaam Agosti 4, 2018, kushoto ni Mke wa Meze Majuto, Aisha Mbwa
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimjulia hali mama wa Mthamini Mkuu wa Serikali, Evelyne Mugasha wa kwanza kulia, ambaye amelazwa katika Taasisi ya Jakaya Kikwete, Muhimbili jijini Dar es salaam Agosti 4, 2018, kutoka kushoto ni Dk. Tulizo Sanga, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda,

Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Serikali Yafanya Uteuzi Wa Baadhi Ya Makatibu Tawala Wa Wilaya

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya Agosti 6

Waziri Aagiza Wafanyakazi wa Benki Nchini Waanze Kuchunguzwa

$
0
0
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk. Philipo Mipango, amezitaka benki zote nchini kuanza kuwachunguza wafanyakazi wao na wasiowaadilifu ili wachukuliwe hatua. Waziri Mpango amesema lengo la agizo hilo ni kuzijengea benki imani kwa wateja wao.

Aliziagiza benki zote kufanya uhakiki na kuwachunguza wafanyakazi wao wote ili kutambua ambao sio waaminifu.

Aidha, ameliagiza Jeshi la Polisi na vyombo vya ulinzi na usalama kuchunguza matukio ya uhalifu yanapotokea kwenye benki na kwamba endapo wafanyakazi watabainika kupanga njama, uongozi wa benki husika uwachukulie hatua za kisheria.

Waziri Mipango alisema hayo wakati wa ufunguzi wa tawi la Benki ya Amana jijini hapa kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Aidha, alilitaka Jeshi la Polisi na vyombo vya ulinzi na usalama kuchukua hatua kwa benki zitakazobainika wafanyakazi wake kuhusika katika tukio lolote la wizi wa fedha za wateja.

Dk. Mpango pia alizungumzia matukio ya watu kuvamiwa na kuporwa baada ya kutoka kwenye benki.

Alieleza kuwa matukio ya wateja kuporwa fedha wanapotoka benki ni ya kutisha na kwamba yanatokana na baadhi ya wafanyakazi ambao siyowaadilifu na waaminifu kushirikiana na wahalifu hao.

Alitaka matukio hayo yafike mwisho kwa wafanyakazi kuchunguzwa na kwamba benki ambayo haitafanya uchunguzi kwa wafanyakazi wake na likatokea tukio kama hilo, viongozi wake wawajibike.

Alisema lengo la zoezi hilo ni kujenga imani kwa wateja kwa kuwa matukio hayo yanawafanya kuona benki siyo mahala pa siri na si salama tena kwa usalama wao na mali zao.

Ujumbe wa Diamond katika Birthday ya mwanae Tiffah

$
0
0
Leo August 06, 2018 mtoto wa Diamond Platnumz, Tiffah anasherekea siku yake ya kuzaliwa.

Mtoto huyu maarufu kama ilivyo kwa wazazi wake anatimiza umri wa miaka mitatu. Huu ni jumbe wa Diamond kwenda kwa Tiffah katika siku hiyo muhimu kwake;

"I do love you, not because you are my Daughter...Nah! I love you because you love me more than aything in the World.... sometimes i even wonder why you Love me so....and that is the reason why i can't sleep without praying for you..

"I can't sleep without thinking about you... and most of the time when you come to my mind i feel like i owe you more than a life...Inshaallah, Mwenyez Mungu akukuze vyema, Akupe akili, Afya, Adabu, Umri mrefu wenye Furaha na Future nzuri baadae.....

"Nakupenda sana Mwanangu, Nakupenda sana Tiffah angu.... Happy 3 Birthday mama🙏🏻 @princess_tiffah 💖💖💖💞💝💞."

Waziri Lugola Atoa Onyo Kali Kwa Makampuni Binafsi Ya Ulinzi, Asema Yanaajiri Vikongwe, Atoa Mwezi Mmoja Kujirekebisha

$
0
0
Na Felix Mwagara, MOHA
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, ametoa mwezi mmoja kwa Makapuni binafsi ya Ulinzi kuhakikisha yanarekebisha mfumo wao wa kuajiri pamoja na utoaji wa mishahara kabla ya Wizara yake haijaanza kuyahakiki makampuni hayo.

Lugola amesema baadhi ya Makampuni hayo yameajiri wazee wasiojiweza ambao muda wote wanalala na wanasabaisha uhalifu kuendelea kwa kasi, wakati vijana wapo wengi wenye nguvu zao wanaweza wakazifanya kazi hizo kwa umakini zaidi, na pia tatizo lingine wanalipwa mishahara midogo hali hiyo inawafanya pia wajiingize katika uhalifu.

Akizungumza na mamia ya wananchi mjini Bunda, mkoani Mara katika mkutano wa hadhara uliofanyika Stendi ya zamani mjini hapo, Waziri Lugola alisema, Serikali ya awamu ya tano kamwe haitataka uzembe, hivyo makampuni hayo yanayovunja utaratibu huo siku zao zinahesabika.

Lugola aliongeza kua, licha makampuni hayo yamekua yakiwekeza nchini na pia yanasaidia kufanya doria katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo ya miji, lakini yapo maeneo machache baadhi ya makampuni yanavunja sheria ya nchi kwa kufanya mambo kinyume na sheria inavyowaelekeza.

“La kwanza kabisa makampuni haya yanafanya mambo ya hovyo kwa kuajiri vikongwe kufanya kazi za ulinzi, utamkuta kikongwe kavaa sare ukimuuliza anasema mimi ni mfanyakazi wa kampuni fulani, hii haikubaliki hata kidogo, kwasababu kwa umri ule hawawezi kupambana na wahaarifu, na kwa umri ule muda wote usinzia na baadhi yao unyang’anywa silaha,” alisema Lugola.

Pia lugola alisema kitendo cha baadhi ya makampuni hayo kulipa mishahara midogo, au kutowalipa kabisa wafanyakazi hao, hiyo hali inasababisha uhalifu kwasababu wafanyakazi hao hawataridhika na kipato duni hivyo uweza wakashirikiana na wahalifu au wenyewe kushiriki matukio hayo.

“Nataka makampuni haya yajirekebishe na yasipojirekebisha ndani ya mwezi mmoja ambapo tunataka kuyaakiki makampuni haya, wasije wakamlaumu waziri wa mambo ya ndani ya nchi ambapo yapo baadhi ya makampuni tutaondoa tulichoridhia ili wasifanye kazi katika nchi hii,” alisema Lugola.

Aidha, Lugola aliwataka askari polisi nchini wahakikishe wanafanya kazi kwa weledi na endapo askari atawaonea wananchi kwa kuwabambikizia kesi, kuwaomba rushwa, ameapa katika uongozi wake atahakikisha anawaondoa.

Pia Lugola aliwataka madereva wa magari yakiwemo mabasi pamoja na bodaboda kua makini kwa kufuata sheria za barabarani kwa kuwa, Rais John Magufuli wakati anamuapisha aiongoze wizara hiyo, alisema amechoshwa na ajali zinazotokea nchini ambazo zinamfanya atoe rambirambi kila siku, hivyo yeye kama Waziri husika, hatakubali kuona madereva wanafanya uzembe barabarani.

Katika mkutano huo ulioandaliwa na ofisi ya mkuu wa wilaya, ulihudhuriwa na viongozi wa wilaya hiyo pamoja na mamia ya wananchi wa Bunda ambapo baadhi ya wananchi walipewa nafasi ya kumuuliza maswali Waziri huyo. Hata hivyo, Waziri Lugola aliyajibu maswali hayo ambapo baadhi ya maswali yalililalamikia Jeshi la Polisi Bunda, baadhi ya askari  wanawanyanyasa wananchi, Lugola aliyajibu maswali yote katika mkutano huo.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live


Latest Images