Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Waziri Mkuu Azindua Kampeni Ya Kufufua Zao La Michikichi.....Lengo ni kumaliza tatizo la upatikanaji wa mafuta ya kula nchini

$
0
0
 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua kampeni ya kufufua zao la michikichi mkoani Kigoma na kuagiza kuanzishwa kwa kituo cha utafiti wa zao hilo katika chuo cha Maendeleo ya Jamii cha Kihinga kilichopo mkoani Kigoma kwa kuwa ndiko zao la Michikichi linalimwa kwa wingi.

Amesema Serikali imedhamiria kumaliza changamoto ya upatikanaji wa mafuta ya kula nchini kwa kuhamasisha kilimo cha zao la michikichiki kwa sababu kila mwaka Serikali hutumia zaidi ya sh. bilioni 600 kwa ajili ya kuagiza mafuta ya kula kutoka nje ya nchi.

Waziri Mkuu ameyasema hayo jana  (Jumamosi, Julai 28, 2018) wakati akizungumza na viongozi wa mkoa wa Kigoma, wadau wa zao la michikichi na wabunge wa mkoa wa Kigoma baada ya kuwasili mkoani hapa kwa ziara ya kikazi ya siku nne inayolenga kuhamasisha maendeleo na kilimo cha zao la Michikichi.

Amesema Serikali haiwezi ikaendelea kutumia fedha nyingi za kigeni kuagiza mafuta ya kula kutoka nje wakati uwezo wa kulima michikichi na kuzalisha mafuta ya mawese kwa wingi tunao, hivyo amewataka viongozi wa Serikali wabadilike na wawafuate wakulima kwenye maeneo ya vijijini na wakawasimamie na kuwashauri namna bora ya kulima zao hilo.

Aidha, ameagiza Wizara ya Kilimo ianze taratibu za kisheria za kukihamisha chuo cha Kihinga kutoka Wizara ya Elimu Sayansi ya Teknolojia kwenda wizara ya Kilimo ili shughuli za tafiti za zao la michikichi lifanyike kwa ufanisi.

Pia, ameiagiza Wizara ya Kilimo kuwahamishia mkoani Kigoma watumishi wa kituo cha utafiti wa michikichi cha Bagamoyo ifikapo mwezi Agosti, 2018 isipokuwa wale wanaohusika na utafiti wa zao la minazi tu.

Kadhalika, amewataka viongozi  wa mikoa yote inayolima michikichi waanzishe mashamba ya michikichiki ili waoneshe mfano kwa wananchi. “Serikali inataka kuona mabadiliko kwenye zao hili. Sioni umuhimu wa Taifa kuendelea kuagiza mafuta ya kula kutoka nje ya nchi wakati uwezo wa kuzalisha ndani upo,”.

Amesema Serikali inataka kuona mabadiliko ya zao hilo, hivyo amewaagiza maafisa ugani katika maeneo yote wanayolima zao hilo wakafualitie maendeleo ya zao hilo kwa ukaribu zaidi. Zao hili litasimamiwa kuanzia hatua za uandalizi wa mashamba, upatikanaji wa pembejeo na utafutaji wa masoko.

Waziri Mkuu amewataka wananchi wote wa mkoa wa Kigoma pamoja na mikoa mingine inayolima michikichi, wahakikishe wanapanda michikichi kwa wingi kuanzia kwenye makazi yao na kwenye mashamba yote wanayolima mazao mengine ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo.

“Serikali imefanya maamuzi ya kumaliza tatizo la mafuta ya kula nchini, kila mmoja lazima awajibike katika kuinua zao la michikichi ili tuweze kuzalisha mafuta ya kutosha,” amesema.

Waziri Mkuu amesema Serikali itafuatilia kwa umakini kuhakikisha zao la michikichi linalimwa kwa wingi na kuleta tija kwa wananchi na Taifa kwa ujumla. “Tutumie zao hili kama fursa ya kujikwamua na umasikini pamoja na maliza changamoto ya upatikanaji wa mafuta nchini,”.

AwaliNaibu Waziri wa Kilimo, Bw. Omary Mgumba alisema zao la mchikichiki ni muhimu katika ukuzaji wa uchumi wa nchini, hivyo ufufuaji wa zao hilo ni kichocheo cha viwanda kwa kuwa kutakuwa na uhakika wa upatikanaji wa malighafi, hivyo kuvutia wawekezaji.

Amesema kiasi kikubwa cha zao hilo hutumika katika kuzalisha mafuta ya kula, sabuni, hivyo ameshauri kiwepo chuo cha utafiti wa zao la michikichi mkoani Kigoma ili kurahisisha shughuli za uzalishaji. Mafuta yatokanayo na zao la michikichi yana mahitaji makubwa kwa kuwa bei yake ni nafuu jambo linalowezesha watu wengi wakiwemo wa hali ya chini kuyatumia.

Kwa upande,wake Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga aliishukuru Serikali kwa uamuzi wake wa kufufua zao la michikichi kwa kuwa linalenga kuinua uchumi wa Taifa.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Mke wa Waziri Mkuu Mary Majaliwa, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhadisi Hamad Masauni, Naibu Waziri wa Ujenzi, uchukuzi na Miundombinu, Mhandisi Atashasta Nditie, Naiubu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, Naibu Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI, Jpsephat Kandege, Naibu Waziri wa Kilimo Omary Mgumba.

Mizizi 29 Power ,ndio Dawa Bora Na Imara Kwa Sasa Kwa Kutibu Na Kuponesha Tataizo La Nguvu Za Kiume Kwa Dakika 30 Tu

$
0
0
Tatizo la upungufu wa nguvu za kiume limekuwa ni janga kubwa sana kwa sasa sio vijana au wazee wanalalamiki kukimbiwa na wa wapenzi wao au ndoa kuvunjika kutokana na mwanaume kulala na mwanamke kitanda kimoja hata wiki mbili bila kushiriki tendo la ndoa na hii ndio inachangia wanawake wengi kutoka nje ya ndoa kwa nini huteseke na wakati dawa zipo ambazo zitarudisha heshima yako ya ndoa 

MIZIZI 29 POWER; ni ambayo hutibu na kurudisha virutubisho mwilini ambavyo humfanya mwanaume awe na matatizo yafatayo 1 kuwahi kukojoa kabla mke au mpenzi wake

 2. kushindwa kurudia tendo dawa, hii itakufanya kurudia tendo zaidi ya Mara tatu 

3... dawa hii inatibu uume uliolegea na kusinyaa 

4. dawa hii inatoa miungurumo ya tumbo na uchovu wakati wa kumaliza tendo 

NINI KINASABABISHA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME 1 kupiga punyeto kwa mda mrefu 
2 upungufu wa vichochoe mwilini 
3 magonjwa ya moyo, kisukari, presha, vidonda vya tumbo kiuno na mgongo 
4 utumiaji ovyo wa madawa ya kizungu 
4 usongo wa mawazo, hasira, tumbo kujaa gesi na kutopata choo.

 PATA TIBA YANGU NA NI TOFAUTI NA ULIZO WAHI KUTUMIA: 

Je una uume mfupi na mwembamba? MASHESHA MIX ni dawa ya kuboresha uume saiz upendayo asa kwa wale waliofanyiwa tohara wakiwa wadogo.. chagua saizi upendayo inch 5,6,7, adi 8 iyo ni kwa urefu na unene sentimita 2,3,4, adi 5 .dawa hizi zipo za kupaka na kunywa na hazina madhara yoyote kwa mtumiaji ,

Tunatibu kisukari,vidonda vya tumbo,ngiri, korodani iliyovimba, kupnguza kitambi, maziwa makubwa NK 

KWA TIBA NA USHAULI FIKA OFISINI KWANGU DARE S SALAAMU MBAGALA ZAKHEMU NA MIKOA YA KANDA YA ZIWA YUPO WAKALA WETU HAPO MWANZA NA KWA AMBAO HAWANA NAFASI YA KUJA OFISINI HUDUMA YETU UTALETEWA POPOTE ULIPO PIGA SIMU 0783185060 DR MAKOYE

Orodha Kamili ya Viongozi Mbalimbali Walioteuliwa Jana kuwa Wakuu wa Wilaya, Mikoa na Rais Magufuli

Wabunge Wa Kigoma Waridhishwa Na Utendaji Wa Serikali ......Waipongeza kwa kampeni ya kuhamasisha kilimo cha michikichi

$
0
0
WABUNGE wa mkoa wa Kigoma wameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli kwa kuanzisha kampeni ya kuhamasisha kilimo cha zao la michikichi kwa sababu litasaidia kuondoa umasiki kwa wananchi wa mkoa huo.

Wamesema kwa muda mrefu wamekuwa wakiiomba Serikali kulifufua zao hilo kwa kuwa ndilo zao kubwa la biashara linalotegemewa na wananchi wengi wa mkoa huo, hivyo kitendo cha kuanzisha kampeni hiyo kinaonesha dhamira ya dhati ya Serikali ya kuwakwamua wananchi.

Wakizungumza kwa jana (Jumamosi, Julai 28, 2018) wabunge hao waliahidi kushirikiana na Serikali bega kwa bega kuhakikisha kampeni ya kuhamasisha kilimo cha zao la michikichi linafanikiwa kama ilivyokusudiwa na Serikali.

Wabunge hao waliyasema hayo  baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuzindua kampeni ya kuhamasisha kilimo cha zao la michikichi katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa NSSF mkoani Kigoma. Mkutano huo ulihudhuriwa na wadau wa zao hilo.

Miongoni mwa wabunge hao ni mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe ambaye aliipongeza Serikali kwa kusikia kilio cha muda mrfu cha wananchi wa mkoa huo cha kufufuliwa kwa zao la michikichi kwa kuwa litakwenda kuchochea ukuaji wa uchumi wa wananchi wa Kigoma.

“Nakupongeza Mheshimiwa Waziri Mkuu pamoja na Serikali kwa kitendo hiki cha kufufua zao la michikichi kwani hiki ndicho kilio cha muda mrefu cha wananchi wa Kigoma kwa hatu hii naamini kuwa leo hata waliotangulia mbele ya haki watakuwa wanatabasamu huko waliko,”.

Pia mbunge huyo alitumia fursa hiyo kuwasisitiza wananchi na viongozi wa mkoa wa Kigoma kuwa ni vema wakashirikiana kwa pamoja katika kuhakikisha zao hilo linafufuliwa kwa watu kuchangamkia fursa ya kupanda michikichi kwenye mashamba yao.

Mbunge mwingine wa jimbo la Kigoma Kaskazini, Peter Serukamba alisema changamoto kubwa inayowakabili wananchi wa mkoa huo ni upatikanaji wa mbegu bora za michikichi, hivyo ameiomba Serikali kuwasaidia katika upatikanaji wa mbegu.

Kwa upande wake,Mkurugenzi Mtendaji wa Trade Mark Bw. John Luaga alisema walifanya utafiti kuhusu zao la michikichi na walibaini kuwa kuna soko kubwa la mafuta ya mawese ndani ya nchi yetu, pamoja na nchi za jirani ila uzalishaji wa mafuta hayo ndani ya nchi bado ni mdogo sana.

Alisema hali inachangiwa na kuwepo kwavikwazo vichache vinavyokwamisha ongezeko la uzalishaji wa ndani, ambavyo ni matumizi ya teknologia hafifu katika kilimo cha mchikichi, na ukamuaji  wa mafuta ya mawese.

Pia ukosefu wa miundombinu na usafiri, ukosefu wa maghala ya kukusanyia matunda ngazi ya wilaya, na badala yake mkulima mmoja mmoja anahangaika kupeleka kwa mteja hivyo kumuongezea gharama, ukubwa wa gharama za usafiri kutoka shambani mpaka sokoni.

Naye, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Josephat Faustine alisema kilimo cha zao la michikichi kina faida kubwa na kinawekezeka, hivyo wao wataanisha maeneo yote yanayofaa kuwekeza.

Pia Mkurugenzi huyo wa TADB alisema benki yao inauwezo wa kutoa mikopo ya mitaji kwa vituo vya uzalishaji mbegu za zao la michikichi na kumaliza changamoto ya upatikanaji wa mbegu, hivyo ni muhimu kwa wakala wa mbegu kuchangamkia fursa hiyo.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu alisema Serikali imedhamiria kufufua zao hilo na kwamba changamoto zinazowakabili wakulima wa zao la michikichi ikiwemoya upatikanaji wa mitaji na mikopo kwa ajili ya kununua mbegu au miche mipya zinafanyiwa kazi.

Waziri Mkuu alisema Serikali itahakikisha zao hilo linafufuliwa na kulimwa kwa wingi mkoani Kigoma pamoja na mikoa mingine inayolima michikichi nchini, ambapo amewata Maafisa Kilimo katika ngazi zote waanzishe mashamba ya michikichi.

Pia amewaagiza Wakurugenzi wa halmashauri zote nchi kuhakikisha mashamba ya wananchi yanapimwa na wahusika kupewa hati ili ziwaweze kupata dhamana ya mikopo kwenye taasisi mbalimbali za kifedha na kuwekeza kwenye kilimo.

Waziri Mkuu alisema halmashauri zinazolima michikichi viongozi wake wantakiwa kuanzisha vitalu vya miche ya zao hilo na watakaoshindwa kuanzisha vitalu hivyo pamoja na kuhamasisha kilimo cha michikichi kwenye maeneo yao wajitathimini mwenyewe.

Aliongeza kuwa kuanzia sasa mkoa huo uhakikishe miche ya michikichi inapandwa katika maeneo yote yakiwemo ya pembezoni mwa barabara, katika mashamba ya shule za msingi na sekondari, kambi ya JKT na kwenye magereza na kwenye makazi ya wananchi.

Hata hivyo Waziri Mkuu alitoa angalizo kwa wawekezaji watakaowekeza katika kilimo cha michikichi kutoanzisha migogoro na wananchi watakaowakuta katika maeneo yao na badala yake washirikiane nao vizuri kwa sababu migogoro haina tija kwao na kwa wananchi.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Rais Magufuli Ashiriki Ibada Ya Jumapili Kanisa La Mtakatifu Petro Oysterbay Jijini Dar Es Salaam

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe wakishiriki katika ibada ya Jumapili katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Julai 29, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe akipokea Sakramenti Takatifu wakati wa ibada ya Jumapili katika kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es salaam leo Julai 29, 2018 (Picha na IKULU)

Rais Magufuli Atoa Pole Kwa Mwanahabari Eric Shigongo Kwa Kufiwa Na Mama Yake Mzazi Jijini Dar Es Salaam Leo

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakitoa heshima za mwisho wakiwa na  Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Global Group Eric Shigongo ambaye amefiwa na mama yake Mzazi Bi Asteria Kahabi Kapela walipofika kuwafariji msibani Mikocheni B jijini Dar es salaam leo Julai 29, 2018.(Picha na IKULU)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa na  Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Global Group Eric Shigongo ambaye amefiwa na mama yake Mzazi Bi Asteria Kahabi Kapela walipofika kuwafariji msibani Mikocheni B jijini Dar es salaam leo Julai 29, 2018. Kushoto ni mwanafamilia Bw. Daudi Machumu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka saini kwenye kitabu cha maombolezo wakati yeye na  mkewe Mama Janeth Magufuli walipofika  msibani Mikocheni B jijini Dar es salaam leo Julai 29, 2018  kutoa   pole kwa Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya Global Group Eric Shigongo ambaye amefiwa na mama yake Mzazi Bi Asteria Kahabi Kapela

Aliyeachiwa Huru Kesi ya mauaji ya bilionea Msuya Asimulia Mambo Mazito Aliyokutana Nayo Gerezani

$
0
0
Wakati Shwaibu Jumanne akitafakari jinsi ya kuanza tena maisha uraiani, mambo mawili bado yanamtesa baada ya kukaa mahabusu kwa miaka mitano.

Jumanne, maarufu kwa jina la Mredii, ndiye pekee aliyeepuka hukumu ya kifo wakati Mahakama Kuu ilipotoa hukumu dhidi ya watu sita walioshtakiwa kwa kosa la kumuua mfanyabiashara maarufu wa Mirerani mkoani Manyara, Erasto Msuya.

Washtakiwa wenzake watano wamehukumiwa kunyongwa hadi kufa, lakini Mredii amerudi uraiani akitafakari maisha mapya baada ya kusimama kazi yake ya uchimbaji madini kwa miaka mitano.

Hata hivyo, tafakuri hiyo inakabiliwa na kumbukumbu mbaya ya tukio lake; kuanzia alipokamatwa hadi maisha ya mahabusu.

“Moja ya mambo ambayo sitakaa niyasahau ni maumivu niliyoyapata wakati nilipokamatwa,” anasema Mrediii katika mahojiano maalumu na Mwananchi baada ya kuachiwa huru.

“Kipigo nilichokipata mikononi mwa polisi kimemsababishia kilema na maumivu.”

Pamoja na kwamba hakusema bayana katika mazungumzo na Mwananchi, Mredii aliiambia mahakama wakati wa utetezi kuwa aliteswa na polisi hadi kupewa ulemavu, ikiwamo kuhasiwa.

Kutokana na kuhasiwa, Mredii alidai aliamua kumpa talaka mmoja ya wake zake, aliyemtaja kuwa ni Zuhura Hassan kwa vile alikuwa hana uwezo tena kama mwanamume. Amebakiwa na mkewe anayeitwa Adile Juma.

Akiongozwa na wakili wake Majura Magafu kutoa utetezi wake, Mredii alidai mbali na kuhasiwa, polisi walimvunja mara mbili mguu wa kushoto na mara moja mguu wa kulia.

Alisema wakati fulani walimfunga kamba na kumning’iniza kama mbuzi aliyebanikwa.

“Kwa hayo mateso niliyopata hapo kituoni nimekuwa mlemavu. Niliwekwa staili ya mbuzi anayechomwa nikiwa sina nguo,” alidai mahakamani.

Katika mahojiano maalumu na Mwananchi, Mredii alisema hakupata matibabu mazuri kutokana na kipigo hicho na kwamba kwa vile sasa yuko huru, moja ya vipaumbele vyake ni kupata matibabu sahihi ya afya yake.

Anasema jambo jingine ambalo hatalisahau ni kulazimishwa kulala saa 9:00 alasiri na kufungiwa vyumbani hata kama huna usingizi. “Wakati mwingine watu wako nje kwenye shughuli zao, lakini sisi tunalazimishwa kulala,” alisema Mredii.

“Hili jambo haliwezi kutoka kwenye akili yangu kwa haraka na litanisumbua kwa muda mrefu sana.

“Kuanzia saa 9:00 (alasiri) mtu unafungiwa ndani, unaambiwa ulale. Kwa kweli yale yalikuwa mateso makubwa kwangu. Halafu chumba kimoja tunalala watu 18 hadi 27. Kwa kweli sitakaa niyasahau maisha haya.”

Hali hiyo ndiyo inamfanya ashauri vijana na watu wengine kutojihusisha na mambo ambayo yanaweza kusababisha wapelekwee gerezani.

“Waepuke kufanya jambo lolote litakalowafanya wapelekwe gerezani kwa kuwa kule ni mahali pa kudhalilisha sana,” anasema.

“Mtu unapokuwa gerezani unakuchukuliwa kama mhalifu na unapokuwa kwenye lile karandinga watu wanaona wewe ni mhalifu na wengine wanakuita mwizi bila kujua ni kosa gani limekupeleka gerezani.

“Lipo suala la matitabu. Mtu anapewa matibabu ya kawaida bila kujali tatizo linalomkabili na ikitokea wakaamua kukupeleka Hospitali za Rufaa nje ya magereza ni kwamba mtu utakuwa umezidiwa.

“Mimi mwenyewe nimetoa matatizo yangu ikiwemo tatizo la vidonda vya tumbo, lakini sijawahi kupimwa licha ya kuomba sana nipelekwe kwenye vipimo ili kujua vidonda vimefikia hatua gani.

“Nimekuwa nikitumia dawa bila kujua (kama) ndizo zinatibu. Sasa natakiwa kwenda kwenye vipimo kwa kuwa kipindi cha miaka mitano nimekaa gerezani (vidonda vya tumbo vimekuwa sugu hasa (kwa kuwa) kule mlo ni mmoja.”

Hukumu ya Mredii na wenzake; Sharifu Mohamed, aliyekuwa mshtakiwa wa kwanza, Musa Mangu (wa tatu), Karim Kuhundwa (wa tano), Sadik Mohamed (wa sita) na Ally Mussa (wa saba), ilitolewa Julai 23 na Jaji Salma Maghimbi.

Walishtakiwa kwa mauaji ya Msuya, maarufu kwa jina la Bilionea Msuya, aliyeuawa Agosti 7, 2013 kwa kupigwa risasi eneo la Mijohoroni wilayani Hai.

Lakini wakati Jaji Maghimbi aliwapa adhabu ya kifo washtakiwa watano, alimuachia huru Mredii baada ya kutoridhika na hoja za kutaka atiwe hatiani.

Jaji Maghimbi alisema ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashitaka haukuweza kuthibitisha shitaka dhidi ya Mredii, hivyo kuamua kumuachia huru.

‘Sikuhusika kupanga wala kushiriki mauaji ya Erasto Msuya na naomba jamii inipokee” alisema Mredii katika mahojiano na Mwananchi.

Anasema uhusiano wake na baadhi ya watu umekuwa ukimtia matatizoni na vyombo vya dola.

“Mwaka 2000 niliwahi kutuhumiwa kwa kosa la mauaji porini Mirerani lakini baada ya upelelezi, nilionekana sikuhusika na kuachiliwa baada ya kukaa mahabusu miezi sita,” alisema Mredii.

“Na hii naona inaweza kusababishwa na hisia kwa kuwa hata tukio linalonikabili naona linaweza kuwa watu wanaangalia ukaribu wangu na watu kwa kuwa Mjeshi ni shemeji yangu.

“Sharifu ni mfanyabiashara ambaye nimekuwa nikimpelekea mawe na hii inaweza kuwa ndiyo iliyosababisha nikahusishwa na matatizo hayo. Lakini namshukuru Mungu na jaji.

“Hakika nilifurahi sana sana kuachiwa na naamini jaji alitumia waledi wake wa kazi kwa kuona kuwa mimi sihusiki na tukio lile, na ukweli ni kwamba mimi sihusiki.” Anasema sasa ana amani kwa kuwa yuko huru.

“Unapokuwa huru, hata kama huna chochote unakuwa na amani. Sitamani kurudi gerezani kwa sababu maisha kule ni magumu sana,” anasema Mredii mwenye watato wanne.

Chanzo: Mwananchi

Rais Magufuli amemteua pia Bibi Gift Isaya Msuya kuwa Mkuu wa Wilaya ya Uyui


Chadema yajibu mapigo, yadai Waitara ni Muongo

$
0
0
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimedai sababu kubwa ya kuondoka aliyekuwa Mbunge wa Ukonga na mwanachama wa chama hicho, Mwita Waitara ni kutokana na hofu ya kukosa Ubunge mwaka 2020 kutoka na safu yake ya viongozi kushindwa kupata nafasi.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Itifaki na Mawasiliano ya Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema ikiwa imepita siku moja tokea Mbunge huyo kutangaza hadharani kujivua uanachama wake na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM), huku kudai sababu kubwa ya yeye kuchukua maamuzi hayo ni kutokana na ugomvi wake na Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe ndani ya chama.

Sababu nyingine za Mwita Waitara kuondoka CHADEMA amedai kwamba ndani ya chama hicho hakuna ruhusa ya Mbunge kusema lolote, hakuna uchaguzi wa haki bali kuna pachika pachika pamoja na Mbowe kutotaka kushauriwa.

"Anaposema hakuna uchaguzi ndani ya chama ni muongo, jimbo la Ukonga tulifanya uchaguzi kuanzia ngazi ya chini kabisa ya misingi, tukaenda matawi, kata na hatimaye Wilaya. Mwita alikuwa amepanga safu yake ya viongozi ambayo imeshindwa na kulalamika sana kwanini safu yake ilishindwa..

"Walishindwa kutokana na wapiga kura waliamua kuchagua viongozi wengine na hicho ndicho kilimfaya Mwita kuwa na hofu ya kukosa Ubunge katika chaguzi zijazo na amelalamika kwa maandishi", amesema Mrema.

Mbali na hilo, Mrema amemtaka Mwita Waitara kutoa sababu za msingi za kuondoka ndani ya chama hicho nasio kufanya siasa nyepesi za kuchafuana.

Mwita Waitara amekuwa Mbunge wa pili kutoka CHADEMA kujivua Ubunge, ambapo Mbunge wa kwanza alikuwa Dkt. Godwin Oloyce Mollel mnamo Disemba 14, 2017 alitangaza kujivua rasmi uanachama wa chama hicho na kujiunga na CCM kwa madai ya kuunga mkono utendaji ya Rais Magufuli.

Jokate Mwegelo afunguka mazito baada ya kuteuliwa na Rais Magufuli kuwa Mkuu wa Wilaya

$
0
0
Ikiwa ni siku moja imepita tangu Mwanamitindo na Mjasiriamali, Jokate Mwegelo ateuliwe na Rais Magufuli kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Hatimaye mwenyewe amefunguka jinsi alivyohaha hadi kupata nafasi hiyo.

Jokate amesema mwaka jana alitaka kukata tamaa kwenye maisha yake ya siasa kwani aliona giza mbele yake lakini hakufanya hivyo hii ni kutokana na kupokea maoni mengi kutoka kwa vijana ambao alikuwa anawashawishi kuingia kwenye siasa.

Akifunguka kuhusu Changamoto, Jokate amesema kuwa vijana wengi sio wavumilivu pale wanapopatwa na changamoto na ndio maana unakuta wanakata tamaa lakini wakati mzuri wa kuweza kujitathmini ni pale unapopatwa na changamoto.

==>Soma zaidi taarifa aliyoitoa Jokate Mwegelo kwa mashabiki wake

"Amini Mungu ni mwingi wa rehema kamwe hamtupi amtumainiye yeye!! Ahsante Mungu Wangu. Labda ni-share kitu kidogo, kuna muda mwaka jana mwishoni nilikuwa so down nilitamani kukata tamaa na kila kitu kwenye maisha nilikuwa pia sijaelewa vizuri hatma yangu kwenye siasa. Nilikuwa kwenye mkutano mkuu wa chama kuna mdada mmoja kutoka Arusha akanikimbilia na kunikumbatia kwa nguvu sana alikuwa na mama mmoja hivi walikuwa wamekuja kupiga picha namimi.

"Huyo dada mdogo hivi akasema ananipenda sana sana na mimi ndio nilimfanya aingie kwenye siasa na akagombea nafasi kupitia mkoa wa Arusha akashinda!! Nikabaki natabasamu. Ikanipa nguvu kubwa ya kupiga moyo konde na kusonga mbele. Nilifurahi kuona kuna mdada nimeweza kumhamasisha na kumpa ujasiri wa kugombea. Unaweza ukawa unapitia mitihani migumu sana kwenye maisha yako lakini inakubidi usikate tamaa saa zingine kwasababu tu ya wale wanaokutegemea, wanaokuangalia na kuvutiwa nawe na kujifunza kupitia maisha yako.

"Lakini zaidi kwasababu safari ya mafanikio ina milima na mabonde, inabidi upambane na kiukweli hakuna mafanikio yasiokuwa na changamoto. Na kuna muda changamoto ndio haswa zinatengeneza “character” zetu.
 
"Kikubwa zaidi wakati wa changamoto tukumbuke kuwa wanyenyekevu, wenye kujishusha na kumuomba Mungu aendelee kutupa imani, hekima na busara ya kusubiri wakati wake. Tukumbuke Mungu hamtupi mja wake. Nawatakia Jumapili Njema. Nawapenda Sana. Ahsanteni 🙏🏽"

Jokate kabla ya kuteuliwa jana alikuwa ni kada wa CCM ambapo kipindi cha nyuma alishawahi kuwa Kaimu Katibu wa Hamasa na Chipukizi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi  (UVCCM) .

Waziri Mkuu Asema Ukaguzi Kwenye Kizuizi Cha Uvinza Ni Endelevu.....Asema lengo ni kudhibiti uingizwaji wa silaha haramu nchini

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwaamesema ukaguzi wa watu na mizigo unaofanywa kwenye kizuizi cha Uvinza mkoani Kigoma utaendelea kufanyika ili kudhibiti wimbi la uingizwaji wa silaha haramu nchini.

“Lazima ukaguzi ufanyuke ili kujiridhisha kama watu wote wanaoingia nchini wamepita kihalali na kama hawapitishi silaha haramu na vitu vingine ambavyo haviruhusiwi kuingizwa nchini,”.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumapili, Julai 29, 2018) wakati akizungumza na wananchi wa wilaya ya Uvinza akiwa katika siku ya pili ya ziara yake ya kikazi mkoani Kigoma.

Ametoa ufafanuzi huo baada ya Mbunge wa jimbo la Kigoma Kusini, Bibi Hasna Mwilima kudai kuwa wananchi wengi wanapata usumbufu mkubwa kutokana na ukaguzi unaofanywa na Maafisa wa Uhamiaji katika kizuizi cha Uvinza.

Waziri Mkuu amesema iwapo viongozi wa mkoa huo hawatakuwa makini katika kufanya ukaguzi kwenye vizuizi watasababisha watu wengi kuingia kiholela nchini na hivyo kuathiri mipango ya Serikali ya kuwahudumia wananchi wake.

Wakati huo huo,Waziri Mkuu amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu Emanuel Maganga kufuatilia kwa umakini mwenendo wa utendaji kazi katika kizuizi cha Uvinza.

Waziri Mkuu amesema iwapo atabaini kuwepo kwa Maafisa wa kizuizi hicho wanaojiashishughulisha  na vitendo vya rushwa pamoja na kuwasumbua wananchi na abiria wanaopita kizuizini hapo awachukulie mara moja.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Waziri Mkuu: Gereza La Kwitanga Kuwa Kituo Kikuu Cha Michikichi

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imeliteua Gereza la Kwitanga lililopo wilayani Kigoma kuwa kituo kikuu cha uzalishaji wa zao la michikichi nchini.

Hivyo ameuagiza uongozi wa gereza hilo waongeze nguvu katika uzalishaji wa michikichi kwa kupanua mashamba na kuongeza askari wenye ujuzi wa kilimo cha michikichi na kupanda miche mipya ya michikichi na kukata ya zamani.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumapili, Julai 29, 2018) wakati alipotembelea gereza hilo akiwa katika siku ya pili ya ziara yake ya kikazi yenye lengo la kufufua zao la michikichi mkoani Kigoma.

Amesema Serikali imedhamiria kwa dhati kufufua kilimo cha zao la michikichi mkoani Kigoma, hivyo kila mwananchi lazima awe na shamba la michikichi.

Katia hatua nyingine, Waziri Mkuu ameuagiza Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kigoma Bw. Sabas Matolo kuhakikisha Gereza la Kwitanga linawezeshwa kwa kuwa na zana bora na za kisasa za kilimo yakiwemo matrekta na vifaa vya kuvunia ili waweze kuongeza uzalishaji wa mafuta.

Pia, Waziri Mkuu amemuagiza Bw. Matolo awahamishe askari  ambao ni wataalamu wa kilimo wenye ujuzi wa zao la michikichi kutoka kwenye Magereza mengine mkoani Kigoma  na kuwahamishia katika gereza la Kwitanga ili kuimarisha uzalishaji.

Awali, Mkuu wa gereza hilo Bw. Majuto Masila alisema ili kilimo cha michikichi na uzalishaji wa mafuta uweze kuwa na tija, wanahitaji wafungwa wasiopungua 300 wawepo kila siku gerezani hapo ili kumudu shughuli za shamba hilo. Kwa sasa kuna wafungwa 112.

"Uzalishaji wa mafuta kwa miaka mitatu mfululizo gerezani Kwitanga ni kama ifuatavyo mwaka 2015/2016 tulizalisha lita 16,094, mwaka 2016/2017 lita 12,674, na mwaka 2017/2018 tulizalisha lita 16,000,"  alisema.

Alisema mafuta yanayozalishwa gerezani hapo yanatumika katika kulisha wafungwa wa gereza hilo la Kwitanga, Bangwe, Kasulu, na Kibondo. Ziada ya mafuta hutumika kulisha wafungwa magereza ya mikoa ya Kagera, Mwanza, Shinyanga, Singida, Dodoma, Morogoro na Tabora.

Baada ya kutoka katika Gereza la Kwitanga, Waziri Mkuu alitembea shamba darasa na eneo la kuzalisha miche ya michikichi la Seed Change katika eneo la Mungonya na kuziagiza halmashauri zote zinazolima michikichi mkoani Kigoma kwenda kununua mbegu kwenye shamba hilo.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Serikali Kutaifisha Mali Za Kampuni Ya Tanzam 2000 Zilizopo Ndani Ya Pori La Akiba Moyowosi Baada Ya Ilani Ya Siku 7

$
0
0
Na Hamza Temba-Geita
..........................................................
Kampuni ya uchimbaji madini ya Tanzam 2000 iliyokuwa ikifanya utafiti wa madini ya dhahabu katika eneo la Luahika ndani ya Pori la Akiba Moyowosi/Kigosi imetakiwa kuondoa vifaa na mitambo yake katika eneo la hilo ndani ya siku saba kwa amri ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla.

Dk. Kigwangalla ameiagiza Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA kutoa ilani ya siku saba kwa kampuni hiyo iondoe vifaa na mitambo yake katika eneo hilo na endapo muda huo utapita bila kufanya hivyo mali hizo zitataifishwa na kuwa mali ya Serikali kwa kuwa wao ni wavamizi kwa mujibu wa sheria.

Waziri Kigwangalla ametoa agizo hilo juzi alipotembelea pori hilo katika wilaya ya Bukombe mkoani Geita ambapo alihitimisha ziara yake ya siku 25 aliyoipa jina la Pori Kwa Pori kwa ajili ya kukagua shughuli za uhifadhi nchini na kutatua changomoto zake.

Alisema uwepo wa vifaa na mitambo ya muwekezaji huyo ndani ya hifadhi hiyo imekuwa kishawishi kikubwa kwa wachimbaji wadogo wa madini kuvamia maeneo hayo wakiamini kuwa eneo hilo lina dhahabu na kwamba bado linaruhusiwa kwa shughuli za uchimbaji.

Awali Meneja wa Pori hilo, Benjamin Kijika alisema kampuni hiyo ilipewa kibali na Wizara ya Malisili na Utalii kwa ajili ya kufanya utafiti wa madini ya dhahabu katika eneo hilo kwa mwaka 2005 hadi 2010 na kuongezewa muda hadi 2012.Alisema wakati kibali hicho kinatolewa Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009 ambayo inazuia tafiti kama hizo na shughuli nyingine za kibinaadamu kwenye maeneo ya hifadhi ilikua bado haijatoka.

Alisema baada ya hapo wizara haikutoa tena kibali kwa kampuni hiyo licha ya wizara ya madini kuipa kibali cha kuchimba dhahabu katika eneo hilo mwaka 2013. Aliongeza kuwa kwa nyakati tofauti Wizara ya Maliasili imeitaka kampuni hiyo iondoe mali zake zote ndani ya eneo hilo, agizo ambalo bado halijatekelezwa mpaka sasa.

Kwa upande wake aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Josephat Paulo Maganga alisema atasimamia utekelezaji agizo hilo la Waziri Kigwangalla ili eneo hilo liendelee kuhifadhiwa kwa mujibu wa sheria.

Alisema hifadhi hiyo inakabiliwa na changamoto kubwa ya uvamizi wa mara kwa mara wa wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu hususan katika eneo la Kigosi Kaskazini na hivyo kupelekea uharibu mkubwa wa mazingira katika hifadhi hiyo.

Alisema ili kukabiliana na changamoto hiyo pori hilo limeanzisha kambi mbili za ulinzi katika eneo hilo kwa ajili ya kudhibiti uharibifu huo ambapo mpaka sasa kesi 24 zenye wachimbaji haramu 52 zimeshafikishwa mahakamani huku kukiwa na vielelezo kadhaa ambavyo ni pamoja na baiskeli 102, viroba vya mchanga unaosadikika kuwa na madini ya dhahabu na vifaa vya uchimbaji.

Pori la Akiba Moyowosi/Kigosi ni muunganiko wa mapori mawili yenye ukubwa wa kilometa za mraba 21,060. Pori la Moyowosi lipo katika wilaya za Kibondo na Kakonko (Kigoma) na Pori la Kigosi katika wilaya ya Biharamulo (Kagera), Bukombe na Mbogwe (Geita), Kahama (Shinyanga) na Kaliua (Tabora).

Pori hili lina umuhimu mkubwa kiikolojia na kiuchumi kwakuwa pia ni ardhi oevu ambayo ni chanzo kikubwa cha maji ya ziwa Nyamagoma na Sagara ambayo huingiza maji mto Malagarasi na hatimaye ziwa Tanganyika, maji hayo hutumika kwa matumizi mbalimbali ya majumbani na kilimo. Pia hifadhi hiyo ni makazi muhimu ya wanyamapori adimu kama Nzohe ambao huliingizia Taifa fedha za kigeni.

Habari Zilizopo Katika Magazewti ya Leo Jumatatu ya July 30

Mugabe amtosa Mnangangwa, asema kura yake anaipeleka upinzani

$
0
0
Rais wa zamani wa Zimbabwe, Robert Mugabe amesema hamuungi mkono mrithi wake Rais wa sasa Emmerson Mnangagwa ndani ya chama tawala Zanu PF, kwa kile alichodai kuondolewa kwa nguvu madarakani na chama alichokianzisha.
 
Mzee Mugabe mwenye umri wa miaka 94, ametoa kauli hiyo jana wakati wa mkutano wake na wanahabari Jijini Harare,  ambapo taifa hilo la kusini mwa Afrika linafanya uchaguzi mkuu leo

Mugabe amesisitiza kuwa, hawezi kuwapigia kura watu waliomtesa na kwamba kura yake atampigia mmoja kati ya wagombea wengine 22 wanaowania nafasi ya urais.

"Namtakia kila kheri kiongozi wa chama cha upinzani cha Vuguvugu la Mageuzi ya Kidemokrasia, MDC, Nelson Chamisa katika uchaguzi wa leo . Kijana huyu ndio anaonekana kufanya vizuri na ndiye mgombea anayefaa", amesema Mugabe.

Zaidi ya raia milioni tano wa Zimbabwe wanajiandaa kumchagua Rais kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 38 bila Mugabe madarakani.

Je Umepungukiwa Nguvu Za Kiume Na Umetumia Dawa Nyingi Bila Mafanikio?

$
0
0
Hakika nawashukuru wote mliotumia hii dawa na kunipa pongezi nyingi Sana sasa offa imeisha maana nilitoa ya wiki 2 tu     na watu wengi walioitumia wamepona kabisa 

Dawa hii ni dawa ya maajabu kabisa na huwezi kuamini ila wengi walioitumia wameiamini maana kati ya watu 89 walioitumia ndani ya wiki 2 watu76 wamepona kabisa na watu 9 hawajapona na watu 4 hawajatoa majibu! 

Dawa hii ni dawa inayotibu tatizo la upungufu wa nguvu za kiume na unapona kabisa, dawa hii ni dawa ya asili,(mitishamba) utaitumia mara moja tu na hautatumia dawa ya nguvu za kiume tena 

Dawa hii inawafaa watu kuanzia miaka 18 mpaka miaka 70, zaidi ya miaka hyo haitakusaidia ....watafiti wa dawa asilia pamoja na waganga  wameikubali pia dawa hii inawafaa hata wanawake wasiopata hisia za mapenzi 

Ukitumia hii dawa unakuwa na uwezo wa kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara 3 bila hamu kuisha, inauwezo wa ajabu na tiba bora kabisa

 SOMA DALILI HIZI;  kutokuwa na hamu ya tendo la ndoa 2 .kushindwa kurudia tendo la ndoa 3. kuwahi kufika kileleni 

Dawa hii imesaidia watu wengi sana dawa hii imegunduliwa na dr kiboko mganga wa tiba za jadi kutoka mafia pia tunatibu matatizo mbalimbali kama mambo ya biashara, nyota, kesi, mapenzi, nk, pia tunahitaji WAKALA wa kupokea dawa zetu katka nchi ya KENYA, ZAMBIA, UGANDA, mikoani tunatuma kwanjia ya mabasi au fika ofisini kwangu  Mafia kisiwani  

maelezo zaidi wasiliana na DR KIBOKO 0679923297

Waziri Mkuu: Michikichi Ni Zao Kuu La Sita La Biashara Nchini

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imelitangaza zao la michikichi kuwa zao kuu la sita la biashara linalotarajiwa kuinua uchumi Taifa.

Awali, kulikuwa na mazao makuu matato ya biashara nchini ambayo ni korosho, tumbaku, pamba, kahawa na chai, ambayo yanategemewa na Taifa kukuza uchumi.

Waziri Mkuu aliyasema hayo jana (Jumapili, Julai 29, 2018) wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Mwakizega wilayani uvinza mkoani kigoma.

Alisema baada ya Serikali kupata mafanikio katika mazao ya korosho, tumbaku, pamba, kahawa na chai, sasa imeamua kufufua zao la michikichi mkoani Kigoma ili lianze kuzalishwa kwa wingi na kuongeza pato la serikali.

“Tulianza na mazao matano, baada ya wakulima wake kupata faida sasa tumehamia  katika mazao mengine likiwemo la michikichi,” alisema.

Waziri Mkuu aliongeza kuwa Serikali imeamua kulipa kipaumbele zao hilo kwa lengo la kumaliza tatizo la upatikanaji wa mafuta ya kula nchini.

Alisema kwa mwaka Serikali inatumia zaidi ya sh. bilioni 600 kuagiza mafuta ya kula nje ya nchi, hivyo ufufuaji zao hilo utaliwezesha Taifa kuzalisha mafuta ya kutosha.

Waziri Mkuu aliwaagiza wananchi wa mkoa wa Kigoma kuandaa mashamba ya kupanda michikichi wakati Serikali ikipanga namna ya kuwasambazia mbegu.

Pia aliwaagiza wananchi wote wapande michikichi mbele ya nyumba zao kama mapambo ambayo baada ya miaka mitatu itageuka na kuwa chanzo cha mapato.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu alitembelea na kukagua shamba jipya la michikichi la kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) 821 KJ Bulombora.

Akiwa katika shamba hilo jipya lenye ukubwa wa ekari 34, Waziri Mkuu alipata fursa ya kupanda mche wa mchikichi kwa lengo la kuhamasisha kilimo cha zao hilo.

Alisema Serikali itahakikisha inafuatilia kwa ukaribu kilimo cha zao hilo kuanzia hatua za awali za utayarishaji wa shamba hadi upatikanaji wa pembejeo.

Kadhalika,Waziri Mkuu aliwaagiza wazazi kuwakatia vijana wao maeneo kwa ajili ya kilimo cha michikichi, jambo litakalowakwamua kiuchumi badala ya kuwa tegemezi.

Pia aliwashauri vijana hao na wakulima wengine wajiunge katika vikundi vitakavyowawezesha kupata mikopo na kuendeleza mashamba yao ya michikichi.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Mwanamke Mjamzito Aliwa na Mamba Akiogelea Ziwa Tanganyika

$
0
0
Mkazi  wa Kijiji cha Msamba, Kata ya Ninde, wilayani hapa Magreth Ndasi (18), ameuawa kwa kuliwa na mamba wakati akiogelea katika Ziwa Tanganyika.
 
Akizungumzia tukio hilo, kaka wa marehemu Joseph Ndasi, alisema tukio hilo lilitokea Ijumaa iliyopita (Julai 27) majira ya saa 12:30 jioni baada ya Magreth aliyekuwa pia ni mjamzito kwenda kuoga katika ziwa hilo.

Alisema alipofika katika ziwa hilo aliingia ndani ya maji na kuanza kuoga ndipo alipovamiwa na mamba huyo ambaye alimkamata mguu na kuondoka naye kuelekea katika kina kirefu cha maji.

“Wakati alipokuwa anavutwa na mamba huyo alipiga mayowe ya kuomba msaada ndipo walipojitokeza wananchi kutaka kumsaidia,” alisema.

Alisema baada ya mamba huyo kuona kundi la watu likiwa linaingia ndani ya maji, alimzamisha Magreth na kumkalia juu huku akifoka kuwatisha watu waliokwenda kumuokoa.

Aidha, wananchi walioshuhudia tukio hilo, walisema watu wenye silaha za jadi walipofika karibu na mamba huyo ili kumshambulia, alimwachia mwanamke huyo ambaye tayari alikuwa ameshakufa na kukimbia.

Kamanda wa Polisi mkoani Rukwa, George Kyando, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kutoa wito kwa wananchi kuacha kwenda kuogelea ziwani hasa nyakati za jioni.

Sumaye Alilia Demokrasia.....Asema Chaguzi Ndogo Zinagharimu Pesa Nyingi za Maendeleo

$
0
0
Waziri  Mkuu mstaafu, Fedrick Sumaye, ameweka kile alichokieleza njama za kufuta upinzani nchini na kutahadharisha kuwa kufanya hivyo ni kuondoa sauti, uhuru wa watu na kwamba jambo hilo ni hatari kwa mustakabali wa taifa.

Sumaye ambaye ni Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho, alieleza hayo wakati akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni za uchaguzi wa marudio wa udiwani Kata ya Makorola jijini Tanga.

Alisema kufuta upinzani ni kukataa demokrasia, hivyo kuwafanya watu wakose mahali pa kusemea kero zao, jambo alilolifananisha na bomu ambalo alidai linaweza kuleta madhara makubwa litakapo kuja kulipuka.

Aliwataka Watanzania watambue kuwa kufutika upinzani nchini ni kusababisha mapambano na kuondoa amani iliyopo kwa kuwa kushindana kwa vyama ndiyo nguzo ya amani.

“Watanzania msishabikie kuua upinzani maana yake mnashabikia kuua demokrasia na kuondoa sauti za watu, maendeleo na uhuru wa watu kuongea matatizo yao,” alisema Sumaye.

Alisema sababu ya kufanyika chaguzi ndogo kila mara ni dalili za kukosekana kwa demokrasia ya kweli na kwamba mabilioni ya fedha yanayotumika kwenye uchaguzi huo yangetumika kuondoa kero mbalimbali za kijamii.

Alieleza athari nyingine ya kuua upinzani ni kuzalisha vibaraka wengi na kudumaza maendeleo na kuvishauri vyombo vya dola kutoingilia masuala ya uchaguzi huo badala yake kazi hiyo iachwe kwenye ushindani wa vyama vya siasa.

Alimwombea kura mgombea wa kata hiyo anayeungwa mkono na Ukawa, Zainab Ashiraf, ambaye alisema kumchagua kuwa diwani pamoja na mambo mengine, ni kukataa ukandamizwaji wa demokrasia nchini.

Mkutano huo uliofunguliwa na Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi Wilaya ya Tanga, Richard Abel, ulihudhuriwa na vyama vinavyounda Ukawa ambao ni mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Tanga, Rashid Jumbe na Jonatha Bahweje ambaye ni katibu wa Chadema Mkoa Tanga.

Wengine waliohudhuria na kupewa nafasi ya kuzungumza ni Mkurugenzi wa Habari na Uenezi CUF, Amour Abal-hasan; Kamishna wa NCCR- Mageuzi, Ramadhan Manyeko na Mbunge Viti Maalum Chadema, Yosephar Komba.

Rais Magufuli Atuma Salamu za Rambirambi Kifo cha Sheikh Fereji

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images