Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Watanzania Kuanza Kumiliki Ardhi Juu Ya Ghorofa

$
0
0
Serikali imeandaa mpango mji mpya katika Jiji la Dar es Salaam utakaowezesha wananchi kupata hati miliki ya ardhi juu ya nyumba (ghorofani) na kuwa na haki sawa kama mmiliki wa kiwanja.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Julai 27, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, amesema lengo la mpango huo ni kuongeza upatikanaji wa maeneo kutokana na ongezeko la watu katika jiji hilo linalokadiriwa kuwa na zaidi ya watu milioni sita.

Waziri Lukuvi amesema pia katika mpango huo wananchi wenyewe ndiyo watakaopanga matumizi ya ardhi yao.

“Aidha, licha ya kupangwa kwa matumizi mapya ya ardhi hakuna mwananchi atakayevunjiwa nyumba yake badala yake mtu yeyote atakayetaka kuendeleza maeneo ya wananchi atatakiwa kukubaliana nao na kuwalipa fidia ili wahame.

“Hatua ya mwisho ya uidhinishaji wa mpango mkuu wowote kwa mujibu wa sheria ya mipango miji ya mwaka 2007 inataka wadau wakutane waipitie,” amesema.

Amesema baada ya kuidhinishwa kwa mpango huo wataipeleka kwa wananchi kwenye kata mbalimbali na kwenye vikao vya madiwani kisha Waziri wa Ardhi ataitangaza.

“Tumefanya hivi kwa sababu Dar es Salaam sasa inaendelezwa bila utaratibu, tumeandaa ‘master plan’ hii iwe dira ya upimaji na uendelezaji was jiji la Dar es Salaam,” amesema Waziri Lukuvi.

Godbless Lema Kusomewa Maelezo Ya Awali Kesi Ya Uchochezi

$
0
0
MAHAKAMA ya Wilaya ya  Arusha, imepanga kumsomea hoja za awali Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), anayekabiliwa na shitaka moja la kuamsha hisia kwa wananchi kwa njia isiyo halali, baada ya upelelezi wa kesi hiyo kukamilika.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Obadia Bwegoge, Wakili wa Jamhuri, Agness Hyera, aliiomba mahakama   kupanga tarehe ya kumsomea hoja za awali mshtakiwa huyo baada ya upelelezi wa shauri hilo namba 132 la mwaka huu  kukamilika.

Mbunge huyo anadaiwa kutenda kosa hilo alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara Oktoba 22, mwaka 2016, katika eneo la Kambi ya Fisi, Kata ya Ngarenaro ambako inadaiwa alitoa maneno yaliyochochea hisia hasi kwa jamii kwa ngazi tofauti nchini.

Katika kesi hiyo, Lema anadaiwa kutamka kuwa Rais Magufuli akiendelea na tabia ya kudhalilisha demokrasia na uongozi wa upinzani, iko siku taifa litaingia kwenye umwagaji wa damu.

Pia, Lema anadaiwa kusema Rais yeyote ambaye haheshimu mipaka ya sheria, mipaka ya katiba, ataingiza Taifa katika majanga ya umwagaji damu, watu watajaa vifua, wakiamua kulipuka  polisi  wala jeshi halitaweza kudhibiti uhalifu utakaojitokeza.

Aprili 27, mwaka huu, Lema aliachiwa huru na mahakama hiyo chini ya kifungu cha 225 (5) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai katika kesi ya uchochezi dhidi ya Rais Dk. John Magufuli aliyokuwa akikabiliwa nayo baada ya upande wa Jamhuri kushindwa kuwasilisha  ushahidi.

Hata hivyo, baada ya kuachiwa huru, alikamatwa tena na kufunguliwa kesi hiyo moja ya kuamsha hisia kwa wananchi.

Katika kesi ya awali, namba 440 ya mwaka 2016, kabla mbunge huyo hajaachiwa huru, alidaiwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika Oktoba 22, mwaka 2016, katika eneo la Kambi ya Fisi, Kata ya Ngarenaro, kwamba alitoa kauli za uchochezi dhidi ya Rais Dk. John Magufuli.

Museven Ruksa Kugombea Tena....Ni Baada ya Mahakama Uganda Kuidhinisha Sheria Ya Kikomo Cha Umri Wa Urais

$
0
0
Mahakama ya Katiba nchini Uganda leo imeidhinisha mabadiliko ya katiba yanayoondoa kikomo kwa umri wa ugombea urais nchini humo.

Uamuzi huo umetolewa leo Ijumaa Julai 27,  katika Mahakama Kuu huko Mbale na Naibu Jaji Mkuu, Alfonse Owiny-Dollo, ambaye alianza kwa kuomba radhi kwa mahakama kuchelewa kuanza katika muda uliopangwa awali.

Mahakama ilitakiwa kuyatolea maamuzi masuala makuu matatu ambayo ni kuondolewa kwa kikomo cha umri wa mgombea urais, kuongezwa muda wa kuhudumu bunge na vurugu zilizotokea bungeni mwaka jana.

Hata hivyo, mahakama imekataa kuongeza miaka ya wabunge waliotaka kusalia madarakani kwa miaka saba badala ya mitano ya sasa.

Katika uamuzi, wake Jaji Cheborion Barishaki ameeleza kwamba kuongezwa kwa muhula wa kuhudumu bunge kutoka miaka mitano hadi miaka saba itakuwa ni hatua ya kibinfasi na inakwenda kinyume na maadili ya uongozi bora

Mjadala huu ulianzia bungeni ambapo ulijadiliwa kwa siku tatu na kuleta mvutano baina ya wabunge wa nchi hiyo hadi kufikia hatua ya kupitisha muswada huo wa kuondoa ukomo wa umri wa miaka 75 kwa ugombea urais baada ya upinzani kupata kura 62.

Hata hivyo, waliotaka kuondoa ukomo umri wa urais kura walipata kura 315 na wawili kutofungamana na upande wowote na kusababisha Spika wa Bunge hilo, Rebecca Kadaga kutangaza kuwa muswada huo umepitishwa baada ya kusomwa mara tatu.

Awali, umri wa mwisho kwa kugombea urais nchini humo, ulikuwa ni miaka 75. Kwa uamuzi huu wa mahakama ina maana kuwa Rais wa nchi hiyo Yoweri Kaguta Museveni atakuwa huru kugombea katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2021.

Nondo Atiwa Mbaroni Tena

$
0
0
Mwenyekiti wa Mtandao wa wanafunzi (TSNP) na Mwanafunzi wa mwaka wa tatu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Abdul Nondo amekamatwa na Jeshi la Polisi kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kuonekana katika maeneo ya chuo hicho.

Akizungumza juu ya tukio hilo Mkurugenzi wa Idara ya Habari wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania, Hellen Sisya amesema Nondo alikamatwa jana Julai 26 saa tatu usiku wakati akizungumza na wenzake, katika eneo la chuo hicho.

"Nondo alikuwa maeneo ya chuo cha UDSM pamoja na wanafunzi wengine majira ya saa tatu usiku ndipo alipokamatwa na Auxilliary polisi wa UDSM na kuchukua maelezo lakini hawakukaa naye sana wakampeleka katika kituo cha polisi hapa hapa UDSM na wakasema hawawezi kumuachia kwa usiku ule kutokana sababu za kiusalama", amesema Hellen.

Aidha, Hellen amesema kwa mujibu wa maelezo ya awali aliyopewa ni kuwa Nondo amekamatwa kwa kosa la kuingia eneo la chuo kinyume cha sheria kutokana hapo awali alishazuiliwa kuendelea kusoma chuoni hapo.

Hata hivyo, taarifa mpya jioni hii zinaarifu kuwa  Abdul Nondo tayari  ameachiliwa kwa dhamana ya Polisi huku akitakiwa siku ya Jumatatu Julai 30, 2018 kuenda kuripoti.

Mnamo Machi 26, 2018, Abdu Nondo ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wa mwaka wa tatu, alisimamishwa kuendelea na masomo yake na Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa William Anangisye baada ya kupandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa.

Nondo anakabiliwa na kesi mbili ambapo ya kwanza ni kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni kuwa yupo hatarini, akiwa katika eneo la Ubungo na kuzisambaza kwenye mtandao wa Whatsapp.

Kosa la pili likitajwa kuwa ni kutoa taarifa za uongo kwa mtumishi wa umma Mafinga wakati alipokuwa akitoa taarifa katika kituo cha polisi mjini Iringa kwa kusema kuwa alitekwa na watu wasiojulikana.

BASATA Wamzuia Diamond Kwenda Kufanya Shoo Nje Ya Nchi

$
0
0
BARAZA la  Sanaa Tanzania (BASATA) limemzuia mwanamuziki, Nassib Abdul ‘Diamond Platnumz’ kwenda kufanya shoo nje ya nchi akiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam  kwa sababu msanii huyo hakuwa na kibali.

Diamond jana  alikuwa akielekea katika visiwa vya Madagascar na Mayote ambako atatumbuiza leo (Julai 27) na kesho (Julai 28).

Meneja wa mwanamuziki huyo, Babu Tale amesema Diamond alitakiwa kuondoka jana Saa 3.00 asubuhi lakini baada ya kuzuiliwa ilibidi aondoke saa 11.00 jioni baada ya kukamilisha taratibu za kupata kibali hicho.

“Ni kweli jana msanii wangu (Diamond) alikumbana na mkono wa Basata akiwa uwanja wa ndege. Kwa kuwa tulishalipwa hela ya watu ikabidi tukishughulikie kibali haraka ili aweze kuondoka nchini,” anasema.

Hata hivyo, alilaumu Basata kwa kushindwa kuweka wazi kanuni zake ili wasanii wazijue badala ya kuwasubiri wakosee ili wawachukulie hatua.

“Ninashauri kama Basata wana chochote wanataka wasanii wakifanye wakishirikishe ili kuepusha mzozo,” anasema.

Mrema Aridhishwa na Utendaji Kazi wa Kangi Lugola....Adai kwa Kasi Hiyo Ataweza Kuvaa Viatu vyake

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Augustine Mrema amesema ameridhishwa na utendaji kazi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola huku akidai akiendelea kufanya hivyo ataweza kukivaa kiatu chake cha uwaziri wa Mambo ya Ndani enzi ya kipindi chake cha mwaka 1990.

Mrema ametoa kauli hiyo jana Julai 27, 2018 wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya chama hicho kilichopo Magomeni jijini Dar es Salaam na kusema Rais Magufuli amepata Waziri mzuri ambaye ataweza kusafisha nchi kama ataweza kuendelea na mwendo alikuwa nao sasa.

"Bila ya kuwa na kiongozi imara nchi inayumba, lakini Rais Magufuli kampata Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola anayefanya vizuri na ninaweza nikasema akiendelea hivi ataweza kuvivaa viatu vyangu kwasababu Wizara ya Mambo ya Ndani ndio kioo na taa. Uchafu wowote ambao unataka kuondoshwa kwenye nchi lazima Wizara ya Mambo ya Ndani ishughulike nao...

"Jinsi Waziri Lugola alivyoanza kazi yake mimi amenitia moyo na kuwatia moyo watanzania wengi kwamba sasa tunaweza kuisafisha nchi hii. Ili lengo la Rais wetu lifikiwe la kujenga nchi yenye amani, haki pamoja na watu wanaobambikiza wenzao kesi lazima wachukuliwe hatua", alisema Mrema

Pamoja na hayo Mrema aliendelea kwa kusema "tunaye Rais Dkt. John Magufuli ambaye analeta mapinduzi makubwa katika nchi yetu, anafanya kazi kubwa sana hivyo ni lazima alindwe kwa gharama yoyote. Mimi nimekuwa kiongozi katika nchi hii sijapata kuona mfano wa Rais jasiri, mwenye uthubutu wa kufanya yale mambo ambayo yameshindikana yaliyokuwa yakitutisha sisi".

Mnamo mwaka 1990, Augustine Mrema aliteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani hadi mwaka 1994 ambapo alibadilishwa Wizara hiyo na kuhamishiwa katika Wizara ya Kazi, Maendeleo ya Vijana na Michezo.

Julai 19, 2018, Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola alibaini upotevu wa mbwa wa Polisi anayejulikana kwa jina la 'hobby' wakati alipokuwa kwenye ziara yake katika Kikosi cha Farasi na Mbwa kilichopo eneo la Bandari Jijini Dar es Salaam na kumuagiza IGP Sirro kutoa maelezo ya upotevu wa mbwa.

Pamoja na hayo, Waziri Lugola ameshamtaka IGP Simon Sirro amtafute mmiliki wa kampuni ya Lugumi popote pale alipo na kumfikisha ofisini kwake Julai 31 saa mbili asubuhi ili ajue hatma yake ikiwa ile ya kudaiwa kuwepo na ufisadi.

Mbali na hilo Waziri Lugola pia amemuagiza Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) afike ofisini kwake Julai 25 akiwa na waliopewa tenda ya kuleta mtambo wa kutengeneza vitambulisho vya taifa ili kwenda kumueleza kwani mtambo huo haujaletwa au waende na pesa walizopewa na Serikali.

Waziri Lugola tayari ameshatoa matamko mengi na sasa ikiwa ni wiki ya tatu tangu alipoapishwa, kwa mujibu wake amesema anajitahidi kufanyia kazi maagizo yote aliyopatiwa wakati anaapishwa na kama Waziri ni wajibu wake kutafuta matokeo chanya ya haraka ili Rais aweze kupumzika na kuwatumikia wananchi kwenye maendeleo

Waziri Majaliwa Akutana Na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP)

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ujio wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa  la Mpango wa  Chakula Duniani (WFP), Bw. David Beasley  hapa nchini ni fursa itakayowawezesha Watanzania kunufaika  kwa kiwango kikubwa katika kilimo, uhifadhi na uuzaji wa mazao ya chakula yanayolimwa hapa nchini.

Akizungumza baada ya kukutana na Bw. Beasley jijini Dar es Salaam jana mchana (Ijumaa, Julai 27, 2018), Waziri Mkuu amesema Tanzania inatarajiwa kuwa na ziada ya chakula  msimu wa mavuno utakapokamilika mwaka huu hivyo itahitaji sana kupata soko nje ya nchi ili iweze kuuza ziada hiyo.

“Taarifa za Wizara ya Kilimo zinaonesha kuwa mavuno ya mazao ya chakula kama mahindi, maharage na mbaazi yatafikia tani milioni 16 wakati mahitaji ya chakula kwa Watanzania kwa mwaka ni tani milioni 13, hivyo tutakuwa na ziada ya tani milioni tatu,” amesema.

Akitoa ufafanuzi, Waziri Mkuu amesema hadi kufikia Julai 2018 ambapo msimu wa mavuno bado unaoendelea, tayari nchi ina ziada ya tani milioni moja kwani taarifa za Wizara ya Kilimo zinaonyesha kuwa tayari zimekwishavunwa tani milioni 14.

Amesema hatua ya WFP kukubali kununua chakula  cha ziada kitakachozalishwa hapa nchini imewahakikishia Watanzania  kuwa mazao yao hayatakosa soko kwani utaratibu wa uuzaji na ununuzi  wa nafaka hasa mahindi unafanywa na Wizara ya Kilimo ikishirikiana na WFP.

Ili kuhakikisha usalama wa chakula kinachozalishwa nchini, Serikali inajenga maghala ya kuhifadhi nafaka kwenye mikoa minane yenye uwezo wa kuhifadhi chakula cha kutosha kwa viwango vinavyokubalika na vinavyolinda afya za walaji.

Waziri Mkuu amesema Mkurugenzi huyo, Bw. Beasley ambaye ametembelea vijiji kadhaa katika Halmashauri za Songea, Namtumbo na Madaba mkoani Ruvuma alijionea jinsi wananchi walivyopata mavuno mazuri hasa mahindi. “Amesema Serikali inahitaji kuweka mkazo mkubwa katika kujenga maghala ya kisasa ya kuhifahia nafaka ili kuepuka uharibifu wa mazao unaoweza kusababishwa uhifadhi duni wa mazao.”

Amesema akiwa mkoani Ruvuma, Bw. Beasley alitembelea maghala kadhaa ya kuhifadhia mahindi na kugundua kuwa ipo changamoto inayohitaji kutatuliwa haraka iwezekanavyo katika eneo hilo kuanzia ngazi ya wilaya.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU

Mwanamitindo Sylvester Afikishwa Mahakamani kwa kukutwa na Madawa ya Kulevya

$
0
0
Mwanamitindo wa mavazi, Wolfgang Sylvester (25) amefikishwa katika Mahakama ya Mkazi Kisutu kwa tuhuma za kusafirisha Dawa za kulevya aina ya Heroin Hydrochloride Kg. 2.49.

Mwanamitindo huyo amesomewa kosa na Wakili wa serikali Janeth Mogolo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Janeth Mtega ambapo amedai amekamatwa na dawa hizo July 22, 2018 katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Wakili wa serikali Mogolo amedai kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha 15(1)(b) cha sheria ya Dawa za kulevya namba 5 ya mwaka 2015.

Mogolo amedai kifungu hicho cha sheria kinaambatana na kifungu cha 57(1) na 60(2) cha Sheria ya makosa ya uhujumu uchumi kama ilivyorekebishwa mwaka 2016.

Wakili Mogolo amedai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, hivyo anaiomba mahakama ipange tarehe nyingine ya kuisikiliza.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Mtega amesema mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri  hilo mpaka ipate kibali maalum, hivyo mshtakiwa hapaswi kujibu lolote na mahakama hiyo haiwezi kutoa dhamana.

Hakimu Mtega ameahirishwa kesi hiyo mpaka August 9, 2018 na mshtakiwa amerudishwa rumande.

New Millenium Wachangia Sh. Milioni 4 Matibabu Ya Moyo Kwa Watoto

$
0
0
MKE wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa amewaongoza wake wa viongozi kuchangia sh. milioni nne kwa ajili ya watoto wawili wanaohitaji kufanyiwa upasuaji wa moyo.

“Kwa umoja wetu, na kwa kuguswa na uhitaji wa watoto wenye matatizo ya moyo, tuliamua tuchange fedha na zimefikia shilingi milioni nne ili tuweze kusaidia kuchangia gharama za matibabu kwa ajili ya watoto wawili,” amesema.

Ametoa kauli hiyo jana (Ijumaa, Julai 27, 2018) wakati akizungumza na baadhi ya wazazi na watumishi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili mara baada ya kuwatembelea watoto wengine waliofanyiwa upasuaji wiki hii.

Mama Majaliwa ambaye aliongozana na wake wengine wa viongozi wakiongozwa na Mwenyekiti wa New Millenium Group, Mama Mbonimpaye Mpango, alikabidhi hundi kwa wazazi wa watoto wawili ambao ni Angela Francis (2) na Sabina Mnyango (4).

Watoto hao ni miongoni mwa watoto tisa wenye umri wa miezi mitatu hadi miaka 17 ambao walipangiwa kufanyiwa upasuaji wa kufungua kifua na madaktari bingwa wa JKCI kwa kushirikiana na wenzao kutoka Shirika la Chain of Hope la Uingereza. Matibabu hayo yalianza Julai 23, mwaka huu na yanatarajiwa kukamilishwa leo.

Mama Majaliwa aliwashukuru madaktari na wauguzi wa JKCI kwa uamuzi wao wa kuwafanyia matibabu watoto hao hapa nchini kwani kwa kufanya hivyo wameokoa fedha za Serikali ambazo zingetumika kumtibu kila mtoto kama wangeamua kupelekwa nje ya nchi kwa matibabu.

Pia alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Serikali ya awamu ya tano kwa jinsi wanavyoendelea kuimarisha utoaji wa huduma kwenye sekta ya afya hasa kwa mama na mtoto.

Amesema gharama ya matibabu ya mgonjwa mmoja anapopelekwa nje ya nchi kwa siku 14, inakaribia wastani wa sh. milioni 30. “Kwa kuamua kufanya upasuaji huu hapa nchini, mmeongeza faraja kwa watoto wetu; mmewawezesha ndugu na wanafamilia kuwa karibu zaidi na mgonjwa wao tofauti na hali ambavyo ingekuwa kama upasuaji huo ungefanyika nje ya nchi,” amesema.

Mama Majaliwa amesema inakuwa vigumu kwa mzazi kutambua mtoto yupi amezaliwa na tatizo la kwenye moyo pindi tu anapozaliwa. “Takwimu zilizopo zinaonyesha kwamba katika kila watoto 100 wanaozaliwa, mtoto mmoja huwa anazaliwa akiwa na tatizo kwenye moyo wake,” amesema.

Mapema, akitoa taarifa fupi kuhusu taasisi hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Prof. Mohamed Janabi alisema wagonjwa wote waliofanyiwa upasuaji wanaendelea vizuri na watoto sita wameruhusiwa kutoka katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) na kupelekwa wodini kuendelea na matibabu.

Hii ni mara ya tatu kwa matibabu ya moyo kwa watoto kufanyika tangu Januari mwaka huu. Mara ya kwanza madaktari wa JKCI walishirikiana na wenzao kutoka Uingereza; mara ya pili ulifanyika upasuaji wa moyo bila kufungua kifua ambapo wa Save a Child’s Heart (SACH) kutoka Israel na Berlin Heart Centre ya Ujerumani walishiriki na mara ya tatu walishirikiana na taasisi ya Open Heart International (OHI) ya Australia.

Akitoa shukrani kwa niaba ya wazazi wa watoto hao, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa Watoto, Dk. Nice Majani aliwashukuru akinamama hao kwa uamuzi wao wa  kuwasaidia watoto wasio na uwezo wa kuchangia matibabu hayo.

“Tunawashukuru sana kwa msaada wenu kwa sababu kuna wazazi wengine wanashindwa kupata kama hizi kwa sababu ya gharama kubwa za matibabu. Wako Wazazi wanakabiliwa na changamoto za kulea watoto wenye matatizo ya moyo, hawawezi kufanya kazi kama watu wengine kwa sababu ya uhitaji mkubwa wa huduma kwa watoto wao,” alisema.

Alisema hapa Tanzania kuna watoto wapatao 750 ambao wako nje wakisubiri kupatiwa matibabu kama hayo lakini hawawezi kulazwa wote kwa sababu hakuna nafasi ya kutosha. “Tunatamani kujua ni wapi tutapata mtu wa kutusadia kujenga hilo jengo ili tuweze kuwahudumia watoto wengi zaidi,” alisema.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Familia Yakubali kumzika Ndugu yao aliyekufa mikononi mwa polisi

$
0
0
Ndugu wa Pascal Kanyembe (39) aliyefariki dunia akiwa chini ya ulinzi wa polisi wamekubali kuzika mwili wa mkazi huyo wa kijiji cha Rubambagwe wilayani Chato  baada ya kususia kwa siku nne.

Kanyembe alikamatwa na polisi saa 7:00 usiku wa Julai 23, 2018 na  kufariki dunia mikononi wa askari wa doria muda mfupi baada ya kufikishwa hospitali ya wilaya kwa matibabu.

Ndugu hao walisusa kuzika mwili wa ndugu yao, wakitaka kuelezwa sababu za kifo chake kwa kuwa mwili wake ulikuwa na majeraha miguuni, bega la kushoto, usoni na upande wa kushoto kichwani.

Mkuu wa wilaya ya Chato, Shaban Ntarambe  jana alisema wamefanya kikao na familia ya marehemu, wamekubaliana kuzika na Serikali itatoa jeneza.

Alisema kutokana na kifo hicho kuwa na utata  Julai 26, 2018 walikutana na familia na kufanya kikao bila kufikia muafaka na hivyo  kulazimika kufanya kikao kingine jana .

Alisema ndugu hao walikataa kuzika kwa sababu walitaka kujua nani aliyesababisha kifo cha ndugu yao.

“Tumekubali kushirikiana na ndugu na tutatoa jeneza. Muhimu ni kumhifadhi marehemu, tumewaeleza wazi kuwa kifo hakina fidia na hata wakitaka fidia ndugu yao hawezi kurudi na Serikali haijamtuma mtu kuua,” alisema.

Kanyembe atazikwa leo wilayani humo.

Serikali Yataja Sababu za Kumzuia Diamond Kwenye Nje ya Nchi Kufanya Shoo

$
0
0
Baraza la Sanaa nchini (Basata) limefafanua umuhimu wa kibali ambacho msanii Diamond alipaswa kuwa nacho kabla ya kwenda kufanya shoo nje ya nchi.

Haya yameelezwa jana Julai 27 baada ya  Diamond kuzuiwa kwa saa tisa katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere kutokana na kutokuwa  na kibali hicho alipokuwa akielekea visiwa vya Madagascar na Mayote.

Kaimu Katibu Mkuu wa Basata, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Onesmo Kayanda, amesema kibali hicho kinawasaidia kutunza kumbukumbu ya wasanii wanaokwenda nje ya nchi.

Jingine ni endapo atapatwa na tatizo lolote iwe rahisi kumsaidia na kuongeza kuwa kuna baadhi yao walishakumbwa na matatizo wakiwa nje ya nchi huku serikali ikiwa haina taarifa kama walisafiri.

Kibali hicho ambacho gharama yake ni Sh50,000, Kayanda amesema huchukua siyo zaidi ya dakika 20 kukipata isipokuwa tu  wasanii huzembea.

“Kuanzia sasa hivi tutakuwa wakali katika hilo bila kujali ukubwa wa jina la msanii, kwani ni kitu ambacho kipo kwenye sheria na ni kwa faida ya wasanii wenyewe na Diamond siyo wa kwanza kuzuiwa, wapo wengine labda kwa kuwa hawana umaarufu kama aliokuwa nao Diamond ndiyo maana haikuzungumzwa sana,” amesema.

Hata hivyo  kibali hicho baadaye kitaisaidia serikali kujua sekta ya sanaa inachangia pato la taifa kwa kiasi gani kwa wasanii kupata shoo za nje kwani katika hatua hiyo pia watapaswa kuweka na mikataba yao mezani ya mialiko kujua serikali nayo imepata nini katika suala zima la kodi.

Mapokezi ya ndege mpya ya Boeing 787-800 Dreamliner Jijini Mwanza

$
0
0
Judith Ferdinand, BMG
Wakazi wa Jiji la Mwanza na maeneo jirani wametakiwa kujitokeza kwa wingi kushuhudia mapokezi (safari ya kwanza) ya ndege mpya  na ya kisasa aina ya Boeing 787-800 Dreamliner iliyonunuliwa na serikali ili kuimarisha shirika la ndege nchini ATCL.

Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe.John Mongella alitoa rai hiyo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari, na kubainisha kwamba ndege hiyo itatua katika uwanja wa ndege wa Mwanza jumapili Julai 29, 2018 majira ya saa moja asubuhi.

Mongella alisema tayari tiketi 244 zimenunuliwa kwa ajili ya safari ya asubuhi na tiketi 158 kwa safari ya usiku hivyo wananchi pia wachangamkie fursa ya kusafiri na ndege hiyo kwa bei nafuu ambapo ina uwezo wa kubeba abiria 262 daraja la kawaida na abiria 22 daraja la biashara.

Kwa upande wake Msimamizi wa kampuni ya ATCL kituo cha Mwanza, Theonestina Ndyetabula  alisema shirika hilo limejipanga vyema na linazidi kuimarika na hivyo kuwahimiza wananchi kutumia ndege zake ikiwemo zile za Bombadier  Dash 8-Q400.

Ndyetabula alisema ndege za Boeing 787-800 Dreamliner pamoja na Bombadier  Dash 8-Q400 zinafanya safari zake mara nne kwa siku katika uwanja wa ndege wa Mwanza ambapo ndege ya  Dreamliner ya Mwanza – Dar kupitia Kilimanjaro ni saa 09:20 asubuhi hadi 11:40 asubuhi, Mwanza -Dar saa 20:20 hadi  21:40 usiku huku Bombadier Mwanza – Bukoba saa 11:15 asubuhi hadi 11:45 asubuhi na   Mwanza – Dar saa 13:15 mchana hadi 15:00 alasiri.

Makamu Wa Rais Kufungua Maonesho Ya Kilimo Na Sherehe Za Wakulima Nanenane Kitaifa Simiyu

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya July 28

Kalulumila:Dawa Bora ya Nguvu za Kiume na Maumbile Madogo

$
0
0
 BORA YA NGUVU ZA KIUME NA MAUMBILE MADOGO KALULUMILA.
----------------------------------------
Ni dawa pekee iliyojipatia umaarufu nchini na nje ya nchi kwa kufanya kazi mara 3, kwa wakati mmoja 1, kurefusha uume na kunenepesha saizi uipendayo kuongeza nguvu za kiume na inatibu matatizo na gerentii miaka 30. Na kuendelea haina madhara, inaimarisha mishipa ya uume iliyoregea na udhalishaji wa mbegu za kiume. 


---------NINI HUCHANGIA MATATIZO HAYA--Ngiri ni chanzo kikubwa cha matatizo haya ili kujua kwamba una ngiri ni chanzo kikubwa cha matatizo haya, ili kujua kama unangiri dalili zake ni kufika haraka kileleni wakati wa tendo la ndoa, 2)kushindwa kurudia tendo la ndoa. 3)kutoa choo kama cha mbuzi. 4)tumbo kujaa gesi na kuunguruma. 5)kukosa choo kabisa. 6)maumbile kuingia ndani na kuwa mafupi. 7) korodani moja kuvimba 8)kutosikia hamu ya tendo la ndoa na maumivu ya kiuno wakati wa tendo la ndoa. 9)maumivu ya kiuno na mgongo pia tunatibu kisukari kwa siku7, presha, busha, bila kupasuliwa na magonjwa mbalimbali. 

---------------------------------------
TUPO TEGETA KWA NDEVU KARIBU NA MACHINJIO YA NGOMBE UTAONA OFSI IMEANDIKWA KALULUMILA HERBALIST CLINIC HOSPITAL SIMU .
----------------------------------------
-0655-557-182.
-0755-557182.
-0784-557-182.
PIA UTAWEZA KULETEWA POPOTE ULIPO.
---------------------------------------
KARIBUNI SANA.
----------------------------------------

Je Umepungukiwa Nguvu Za Kiume Na Umetumia Dawa Nyingi Bila Mafanikio?

$
0
0
Hakika nawashukuru wote mliotumia hii dawa na kunipa pongezi nyingi Sana sasa offa imeisha maana nilitoa ya wiki 2 tu     na watu wengi walioitumia wamepona kabisa 

Dawa hii ni dawa ya maajabu kabisa na huwezi kuamini ila wengi walioitumia wameiamini maana kati ya watu 89 walioitumia ndani ya wiki 2 watu76 wamepona kabisa na watu 9 hawajapona na watu 4 hawajatoa majibu! 

Dawa hii ni dawa inayotibu tatizo la upungufu wa nguvu za kiume na unapona kabisa, dawa hii ni dawa ya asili,(mitishamba) utaitumia mara moja tu na hautatumia dawa ya nguvu za kiume tena 

Dawa hii inawafaa watu kuanzia miaka 18 mpaka miaka 70, zaidi ya miaka hyo haitakusaidia ....watafiti wa dawa asilia pamoja na waganga  wameikubali pia dawa hii inawafaa hata wanawake wasiopata hisia za mapenzi 

Ukitumia hii dawa unakuwa na uwezo wa kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara 3 bila hamu kuisha, inauwezo wa ajabu na tiba bora kabisa

 SOMA DALILI HIZI;  kutokuwa na hamu ya tendo la ndoa 2 .kushindwa kurudia tendo la ndoa 3. kuwahi kufika kileleni 

Dawa hii imesaidia watu wengi sana dawa hii imegunduliwa na dr kiboko mganga wa tiba za jadi kutoka mafia pia tunatibu matatizo mbalimbali kama mambo ya biashara, nyota, kesi, mapenzi, nk, pia tunahitaji WAKALA wa kupokea dawa zetu katka nchi ya KENYA, ZAMBIA, UGANDA, mikoani tunatuma kwanjia ya mabasi au fika ofisini kwangu  Mafia kisiwani  

maelezo zaidi wasiliana na DR KIBOKO 0679923297

Kiboko Ya Matatizo Ya Nguvu Za Kiume,maumbile Madogo, Mvuto Wa Mapenzi ,magonjwa Sugu

$
0
0
Usikate tamaa ondoa maradhi yako, maana matatizo haya yamekua yakiasili watuwengi kisaikolojia hasa baada ya kujiona wako tofauti sana na wengine kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia (6-8) vinginevyo mtuhuyo anamapunguvu katika mwiliwake.

Kunasababu nyingi sana zinazosababisha matatizo haya, chango hushambulia never ambayo huasili misuli ya uume, Ngili :- hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kufanya tumbo kuunguluma na kujaa gesi, kolodani moja kuvimba au kuingia ndani pamoja na kutopata choo vizuli. Sababuhizi na nyingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba na marakwamara husababisha kukosa hamu ya kuludia tendo la ndoa na baadae kushindwa kabisa

MASISA 3POWER :- nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa mfumo wa vidonge, huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka 15-90 , inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii) inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa, itakufanya uludie tendo la ndoa zaidi ya mara nne (4) birahamu kuisha wara kuhisi kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya dk (20-30 )

YONINANI:- hurefusha na kunenepesha maumbile madogo ya uume uliosinyaa inchi 6-8 na unene wa sm 3-4 kwa mda mfupi sana,

SUPER MORINA :- nidawa inayotibu ama kutatua tatizo la kisukali kwawaliohangaika bila mafanikio, huondoa tatizo la kisukali na kupona kabisa, vilevile ninadawa ya magonjwa sugu km vile presha, vidondo vya tumbo, miguu kuwakamoto, muwasho mwilin, kaswende,uzazi nk.

LUGIMBA :- nidawa ya mvuto wa mapenzi, humtuliza mke, mme, mchumba, hawara au mtu yoyote umpendae na kumfanya akutimizie chochotekile unachokitaka kutoka kwake na kumfunga asiwe na mtu yoyote zaidi yako.

WASILIANA NA DR CHIPUPA NAPATIKANA DAR ES SALAAM KUMBUKA HUDUMAHII ITAKUFIKIA POPOTE ULIPO  0759208637 / 0785687900

Mizizi 29 Power ,ndio Dawa Bora Na Imara Kwa Sasa Kwa Kutibu Na Kuponesha Tataizo La Nguvu Za Kiume Kwa Dakika 30 Tu

$
0
0
Tatizo la upungufu wa nguvu za kiume limekuwa ni janga kubwa sana kwa sasa sio vijana au wazee wanalalamiki kukimbiwa na wa wapenzi wao au ndoa kuvunjika kutokana na mwanaume kulala na mwanamke kitanda kimoja hata wiki mbili bila kushiriki tendo la ndoa na hii ndio inachangia wanawake wengi kutoka nje ya ndoa kwa nini huteseke na wakati dawa zipo ambazo zitarudisha heshima yako ya ndoa 

MIZIZI 29 POWER; ni ambayo hutibu na kurudisha virutubisho mwilini ambavyo humfanya mwanaume awe na matatizo yafatayo 1 kuwahi kukojoa kabla mke au mpenzi wake

 2. kushindwa kurudia tendo dawa, hii itakufanya kurudia tendo zaidi ya Mara tatu 

3... dawa hii inatibu uume uliolegea na kusinyaa 

4. dawa hii inatoa miungurumo ya tumbo na uchovu wakati wa kumaliza tendo 

NINI KINASABABISHA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME 1 kupiga punyeto kwa mda mrefu 
2 upungufu wa vichochoe mwilini 
3 magonjwa ya moyo, kisukari, presha, vidonda vya tumbo kiuno na mgongo 
4 utumiaji ovyo wa madawa ya kizungu 
4 usongo wa mawazo, hasira, tumbo kujaa gesi na kutopata choo.

 PATA TIBA YANGU NA NI TOFAUTI NA ULIZO WAHI KUTUMIA: 

Je una uume mfupi na mwembamba? MASHESHA MIX ni dawa ya kuboresha uume saiz upendayo asa kwa wale waliofanyiwa tohara wakiwa wadogo.. chagua saizi upendayo inch 5,6,7, adi 8 iyo ni kwa urefu na unene sentimita 2,3,4, adi 5 .dawa hizi zipo za kupaka na kunywa na hazina madhara yoyote kwa mtumiaji ,

Tunatibu kisukari,vidonda vya tumbo,ngiri, korodani iliyovimba, kupnguza kitambi, maziwa makubwa NK 

KWA TIBA NA USHAULI FIKA OFISINI KWANGU DARE S SALAAMU MBAGALA ZAKHEMU NA MIKOA YA KANDA YA ZIWA YUPO WAKALA WETU HAPO MWANZA NA KWA AMBAO HAWANA NAFASI YA KUJA OFISINI HUDUMA YETU UTALETEWA POPOTE ULIPO PIGA SIMU 0783185060 DR MAKOYE

Lipumba Awataka Wapiga Kura Waiadhibu CCM kWa Kupandikiza Usaliti Ndani ya Chama Chake

$
0
0
Mwenyekiti wa CUF (anayetambuliwa na Msajili wa Vyama), Profesa Ibrahim Lipumba amewaomba wananchi wa Kata ya Nachingwea Wilaya Ruangwa mkoani Lindi, kupinga kitendo cha CCM cha kupandikiza usaliti kwenye chama chao.

Profesa Lipumba anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, ameyasema hayo jana alipokuwa akimnadi mgombea wao wa udiwani, Abubakar Safi Kondo kwenye kata hiyo.

Lipumba amesema wapiga kura wilayani Ruangwa wanatakiwa kurudisha salamu kwa CCM kwa kitendo chao cha kumshawishi diwani wao kuwasaliti na kujiunga na chama hicho ambacho kimemteua kugombea tena kwenye kata hiyo.

“Lazima tulete mabadiliko, CCM wameshindwa kutekeleza haki ya wananchi wa kusini, tupate fursa kuhakikisha hizi mbinu ambazo walizifanya za diwani wetu kutusaliti tuwarudishie salamu watu wa CCM hatukubali kusalitiwa,” alisema Lipumba.

Aidha Lipumba ameweka wazi kwamba alimkubali Rais John Magufuli kwa mpango wake wa kupambana na rushwa, lakini kitendo cha CCM kurubuni madiwani nacho ni rushwa jambo ambalo hakubaliani nalo.

Upande wa chama cha CUF unaomuunga mkono, Prof. Lipumba unashiriki uchaguzi uliotangazwa na Tume ya Taifa uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Agosti 12, huku upande unaomuunga mkono Katibu Mkuu Maliim Seif ukiwa na msimamo wa kutoshiriki kwa madai ya kwamba kwa sasa wanashughulikia migogoro inayoendelea ndani ya chama.

Lukuvi Apiga ‘stop’ Nyumba Kuwekewa X.....Ni zile ambazo hazijarasimishwa

$
0
0
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wiliam Lukuvi, amepiga marufuku uwekaji wa alama ya ‘X’ kwenye makazi ya wananchi waliojenga katika maeneo ambayo hayajarasimishwa kote nchini.

Alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa wadau wa ardhi waliokutana kujadili mpango mji wa miaka 20 wa Jiji la Dar es Salaam.

Alisisitiza kuwa hakuna mwananchi atakayevunjiwa nyumba yake kwa sababu amejenga katika eneo ambalo halijarasimishwa, kwa sababu Serikali imewapa fursa ya kurasimisha maeneo hayo.

Pia alizipiga marufuku kampuni zinazojihusisha na urasimishaji wa maeneo kuwachangisha fedha wananchi kutokana na kubaini kuwapo kwa kasoro kadhaa wakati wa zoezi hilo maeneo ya jijini Dar es Salaam.

“Zoezi hili tulilianza tukaona lina kasoro, Dar es Salaam kuna watu walianza kutoza wananchi Sh 500,000 hadi Sh 400,000 ili kupima kiwanja kimoja cha maskini aliyejenga kwenye eneo lisilo rasmi.

“Lakini baada ya kuchunguza nimegundua gharama halisi hazizidi Sh 250,000, kwa hiyo nimetoa agizo kwamba katika urasmishaji wowote hapa Tanzania, mwananchi asichangie zaidi ya Sh 250,000 ili kupimiwa kiwanja chake hiyo ni gharama ya juu.

“Kampuni hizi zishindane kwa sababu tenda zitatangazwa na wilaya ili kila mtu anayetaka kupata kazi lazima atoe bei isiyozidi Sh 250,000 na iwe marufuku kwa kampuni kuchangisha fedha za wananchi katika sehemu ambayo inarasimishwa.

“Dar es Salaam yako makampuni matatu yamechukua fedha, wananchi wamechangisha kwenye akaunti zao na wametoroka hawakufanya kazi, hawa tunawakamata.

Alisema wakati wa urasimishaji wa ardhi katika maeneo mbalimbali wananchi wenyewe watafungua akaunti zao za mitaa ambazo watazisimamia.

Aliwaonya viongozi wa mitaa kujihusisha na fedha hizo na kwamba, malipo yatafanyika baada ya kazi hiyo kuthibitishwa na maofisa wa wilaya.

Alisema gharama zitakazotumika kurasimisha zitakapokubaliwa ndipo wananchi watatoa fedha kuzilipa kampuni zitakazopewa kazi hiyo.

“Najua watendaji na wapimaji wa Serikali ni wachache, ndiyo maana tumeweza kusajili kampuni nyingi za upimaji, kwa hiyo ni marufuku kwa kampuni binafsi kwenda kuomba kazi huko mitaani, lazima waanzie wilayani na isimamiwe na wilaya. Na iwe kiungo kati ya wale warasimishwaji na warasmishaji.

“Narudia, ni marufuku kwa kampuni kuchukua fedha za wananchi na kuingiza kwenye akaunti zao. Lakini iwe tena ni marufuku kwa madiwani na wenyeviti wa mitaa kwa sababu baadhi yao wamekuwa wanachukua fedha kwa makampuni wakidanganya kuwa wao ndio wanatoa kazi za urasimishaji na upimaji.

“Matokeo yake wanataka kuhongwa fedha na gharama hizo zinaingia kwenye gharama za watu wanaotaka kurasimishiwa. Kazi hazitatolewa na mwenyekiti wa mtaa wala diwani, zitatolewa wilayani kwa hiyo kampuni zisiende kwenye mitaa kuhonga madiwani au wenyeviti wa mitaa ili wapate kazi ya urasimishaji,” alisema.

Waziri Lukuvi aliwataka watendaji wote wa ardhi wa wilaya zote nchini kuhakikisha wanasimamia zoezi la urasimishwaji na uhamasishaji na kwamba, migogoro yoyote itakayotokea watawajibika.

“Isitokee mtu tena akaweka X kwenye nyumba za wananchi kama ilivyojitokeza Babati jana (juzi), katika maeneo ambayo watu wamejenga kiholela isipokuwa kwa watu waliojenga kwenye maeneo yaliyo kwenye hifadhi zilizopo kwa mujibu wa sheria, kama vile hifadhi ya barabara, hifadhi ya misitu iliyosajiliwa au iliyotangazwa kwenye gazeti la Serikali,” alisema Waziri Lukuvi.

Waziri Lukuvi alizitaka wilaya zote kuhakikisha zinaainisha maeneo yote ambayo hayajarasimishwa ili kupanga utaratibu wa zoezi hilo ili wananchi wapate barabara, hati miliki za maeneo hayo kulingana na nyumba walizozijenga.

“Barabara watazipata kwa kukubaliana wenyewe ni nani achangie ardhi yake ili barabara iweze kupita na kila mwananchi atachanga fedha kuhakikisha nyumba yake inapimwa kwa gharama zake,” alisema Lukuvi.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images