Wachawi wana uwezo wa kumsababishia mtu maradhi kwa kutumia uchawi.
Mtu aliye tupiwa maradhi ya kichawi huanza kuonyesha dalili zote za mgonjwa wa maradhi husika.
Kama mhusika ametupiwa maradhi ya kiharusi basi ataonyesha dalili zote za mgonjwa wa kiharusi, kama ametupiwa maradhi ya kifafa basi ataonyesha dalili zote za mtu mwenye kusumbuliwa na maradhi ya kifafa na kama atakuwa ametupiwa ukichaa basi mtu huyo ataonyesha dalili zote za mtu mwenye kichaa.
DALILI ZA MAGONJWA YA KICHAWI
Kila maradhi ya kichawi yana sifa na dalili zake za kipekee.
Kwa maana ya kwamba kifafa cha kichawi kina dalili zake, kichaa cha kichawi kina dalili zake, kiharusi cha kichawi kina dalili zake nakadhalika nakadhalika.
Lakini maradhi yote ya kichawi huwa na sifa moja ya kipekee ambayo kila mwenye kusumbuliwa na maradhi ya kichawi huwa nayo.
Nayo ni kutumia tiba nyingi kwa muda mrefu bila kupata nafuu yoyote ya kudumu pamoja na ugonjwa kuto onekana kwenye vipimo vya hospitalini.
AINA YA MARADHI YA KICHAWI
Maradhi ya kichawi yamegawanyika katika aina kuu mbili kama ifuatavyo :
1. AINA YA KWANZA : MARADHI YA KICHAWI YATOKANAYO NA KULISHWA SUMU ZA KICHAWI
2. AINA YA PILI : MARADHI YA KUTUMWA KWA KUTUMIA MAJINI WA KISHEITWANI
MARADHI YATOKANAYO NA KULISHWA SUMU ZA KICHAWI.
Wachawi wana elimu na maarifa mapana sana kuhusu miti mbalimbali ya porini ambayo inapotumiwa na wanadamu au wanyama hutengeneza sumu yenye kusababisha maradhi mbalimbali katika mwili wa mwanadamu au mnyama husika.
Mfano kuna mti mmoja wa porini. Ni mti mrefu wenye kutoa majani yenye kunukia. Mafuta ya mti huu hutumiwa na wachawi katika kuwasababishia watu maradhi ya ini.
Mafuta ya mti huo husababisha kufeli kwa ini. Kinacho fanyika mtu aliekusudiwa anakuwa anawekewa kijiko kimoja kidogo cha mafuta hayo kwenye chakula anacho tumia kwa muda wa siku saba mfululizo.
Sumu hiyo hufanya kazi kwa taratibu sana na inaweza kuchukua hata miezi sita kuanza kuonyesha dalili.
Mwisho wa siku mhusika alielishwa sumu hiyo ndio anakuwa tayari amekuwa ameshapewa maradhi ya ini.
Mara nyingi uchawi huu hufanywa na mtu wa karibu.
Kuna mti mmoja wa porini ambao wachawi wanau tumia kuwasababishia wanawake wajawazito tatizo la kuchoropoka kwa mimba.
Majani ya mti huu hupondwa pondwa na kuchemshwa na kisha kuchanganywa kwenye chakula atakacho kula mwanamke mwenye ujauzito mchanga.
Mwanamke huyo akisha kula dawa hizo za kichawi basi hazitapita siku tatu huo ujauzito utachoropoka.
Hali hii itakuwa inajirudia kila mwanamke huyo anapokuwa amebeba ujauzito kwa sababu wanao kuwa wanasimamia zoezi hilo ni watu wake wa karibu.
Ndio maana unakuta wanawake wengine amebeba mimba Zaidi ya nne na zote zinachoropoka na kumsababishia maisha magumu katika ndoa yake.
Hayo ni baadhi ya maradhi lakini karibu kila maradhi unayo yafahamu wewe wachawi wanaijua miti ya porini ambayo wakimlisha mtu basi moja kwa moja inakwenda kuathiri sehemu husika katika mwili wa mkusudiwa na kumsababishia maradhi yaliyo kusudiwa. Ipo miti inasababisha uziwi, upofu, ugumba, ukhanithi, pumu,mtoto kuchelewa kuongea, kutembea nakadhalika.
MARADHI YA KUTUMWA KWA KUTUMIA MAJINI WA KICHAWI.
Haya ni maradhi yanayo tumwa moja kwa moja kwa mkusudiwa kwa kutumia majini wa kisheitwani.
Hapa jinni wa kisheitwani huamriwa kwenda kukaa ndani ya nafsi ya mtu Fulani na kumsababishia maradhi Fulani.
Mtu aliye tumiwa jinni huyu wa kisheitwani huanza kuonyesha dalili zote za mtu mwenye maradhi yaliyo kusudiwa.
Atakaa na maradhi hayo kwa muda mrefu na atatumia tiba za kuondosha maradhi hayo bila kupata nafuu yoyote ya kudumu na mwisho wa siku atakata tamaa kabisa akisubiri kifo kimchukue .
TIBA ZA MAGONJWA YA KICHAWI
Maradhi ya kichawi yanaweza kutibiwa kwa kutumia dua, kafara, na miti ya aina mbalimbali kulingana na aina ya maradhi yanayo msumbua mhusika.
Lakini kabla ya mhusika kutibiwa ni lazima ijulikane kwanza kama maradhi yanayo msumbua ni ya kawaida ( ya kibinadamu ) ama ya kisheitwani ( maradhi ya kichawi )
Zipo njia mbalimbali zinazo tumika kujua kama mgonjwa husika maradhi yake ni ya kibinaadamu au ya kisheitwani.
Nitazielezea kwa ufupi njia hizo.
( Utajuaje kama maradhi yanayo kusumbua ni maradhi ya kichawi )
1. Kusoma dalili za mgonjwa. ( Kila maradhi ya kichawi yana dalili zake maalumu ambazo huweza kutumika kama viashiria vya kujua kama mhusika ana sumbuliwa na maradhi ya kibinadamu au ya kichawi.
2. Kusoma nyota ya mgonjwa ili kujua kama imetiwa kiza cha maradhi
3. Kufanya dua maalumu ya kuomba kujua kama maradhi yanayo msumbua mhusika ni ya kibinadamu au ya kisheitwani. Kama ni maradhi ya kibinadamu basi mgonjwa huyo atapewa tiba za kawaida ambazo hutibu magonjwa ya kibinaadamu na kama ni itajulikana ni maradhi ya kisheitwani basi atapewa tiba sahihi kulingana na maradhi yanayo msumbua.
4. Kumtibu mgonjwa kwa kutumia tiba maalumu za asili ambazo hutibu na kuondosha kabisa maradhi husika.
Katika ulimwengu wa kitabibu zipo tiba maalumu za asili ambazo zina sifa ya kutibu na kuondosha kabisa aina Fulani ya maradhi yanayo wasumbua wanadamu.
Ikitokea tiba hiyo imeshindwa kumtibu mgonjwa huyo basi ni ishara ya moja kwa moja kwamba maradhi yanayo msumbua mtu huyo ni maradhi kisheitwani.
Mfano wa tiba hiyo ni ile itokanayo na mti wa Mgude.
Kwa wenyeji wa mikoa ya Tanga, Pwani na kusini ( Lindi na Mtwara ) mtakuwa mnaujua mti huu vizuri.
Unajulikana kwa wengi katika utabibu kama mti wenye kukaliwa na majini wakubwa wa kisheitwani wenye sifa tofauti tofauti.
Ni mti wenye maajabu sana na unao tumika kufanyia kafara nyingi kubwa kubwa.
Kwa kifupi ni mti unaopendwa sana na majini wabaya. Kama unataka kufanya ushirika ama agano na majini wabaya basi mti wa mgude utakufaa sana.
Ukiwa unataka kuwa unaona mauza uza nyumbani kwako basi panda mti huu wa mgude. Mti wa Mgude unaingia pia katika nyungu ya miti saba mikubwa ya porini na huweza kutumika pia kuwafukuza baadhi ya majini wabaya ambao ni wadogo kimamlaka kwa majini wanao kaa ndani ya mti huu.
Sasa basi mti huu wa Mgude mbali na kuwa na sifa hizo nilizo zitaja hapo juu, lakini pia mti huu unatoa tiba mujarabu kabisa . Mti wa mgude unatumika katika kutibu na kuondosha kabisa maradhi yafuatayo :
1. KIHARUSI : Magamba na majani ya mti wa mgude huanikwa juani na kukauka kisha husagwa halafu unga unga wake huchemshwa na maji na kisha kimiminika kupewa mtu mwenye maradhi ya kiharusi . Mgonjwa atapona kabisa kiharusi ndani ya siku 21. ( KIHARUSI KINACHO TIBIWA NA TIBA HII YA MTI WA MGUDE NI KIHARUSI CHA KAWAIDA NA SIO CHA KUROGWA. KATIKA ULIMWENGU WA KITABIBU, MGONJWA WA KIHARUSI AKITUMIA TIBA HII HALAFU ASIPONE BASI NI ISHARA KWAMBA MARADHI ALIYO NAYO YAMETOKANA NA KUROGWA.
2. UKHANITHI : Hapa namzungumzia mwanaume ambae hawezi kabisa kusimamisha uume wake na sio yule shida ya udhaifu tu wa nguvu za kiume. Namaanisha asie w eza kabisa kusimamisha uume wake . Magamba ya mgude huanikwa juani na kusagwa ama kupondwa pondwa hadi yawe unga na kisha kuchemshwa na mgonjwa kupewa kimiminika anywe mara tatu kwa siku asubuhi mchana na usiku kwa muda wa siku saba. Asipopona maradhi yake basi hicho kiashiria kwamba maradhi ya mhusika yanatokana na kurogwa kwa hivyo hutafutwa tiba ya kubatilisha uchawi ulio msababishia mhusika maradhi ya ukhanithi.
3. MALARIA YA UBONGO ( ambayo huchukuliwa kama ukichaa ). Mti wa mgude hutibu na kuondosha kabisa maradhi ya malaria iliyo panda kichwani au malaria ya Ubongo. Majani ya mgude huchukuliwa na kuanikwa juani kisha kusagwa halafu kuchemshwa na maji halafu mgonjwa anakuwa anapewa kunywa kwa muda wa siku kumi na nne. Kama maradhi yake ni ya kawaida basi ndani ya hizo siku kumi na nne atakuwa amepona maradhi yake na ikiwa vinginevyo basi ni ishara kwamba maradhi yake ni ya kutengenezwa kichawi.
4. TATIZO LA KUCHOROPOKA KWA MIMBA : Mizizi ya mgude hutumika kutibu na kuondosha kabisa tatizo la kuchoropoka kwa mimba hata kama limedumu kwa muda mrefu kiasi gani. Mwanamke mwenye tatizo la kuchoropoa mimba akitumia mizizi ya mgude halafu tatizo lake likaendelea kujirudia basi ni ishara ya moja kwa moja kwamba tatizo lake hilo linasababishwa na majini wa kisheitwani.
5. Maradhi mengine yatibiwayo na mti wa Mgude ni pamoja na kichocho na kuhara.
MAKALA HAYA YAMEANDALIWA NA DOKTA. MUNGWA KABILI. ANAPATIKANA KWA SIMU NAMBA 0744 000 473.
Makala haya yanapatikana kwa undani Zaidi katika kitabu “ MAMBO TISA YANAYO UNDA NYOTA YA MWANADAMU : UHUSIANO KATI YA NYOTA YA MTU NA MAFANIKIO YAKE KATIKA MAISHA ambacho kimeandikwa na Dokta. Mungwa Kabili.
Katika Makala zijazo nitakuwa nikielezea magonjwa yote ya kichawi kwa kuangalia ugonjwa mmoja baada ya mwingine. Jinsi yanavyo tengenezwa na wachawi, lengo la kuyatengeneza, jinsi ya kujiikinga nayo na jinsi ya kujitibu kwa mtu ambae tayari ametupiwa maradhi hayo ya kichawi.
Pia kufuatia maombi ya watu wengi ambao wameshindwa kupata nakala za kitabu changu MAMBO TISA YANAYO UNDA NYOTA YA MWANADAMU… Siku chachae zijazo nitayaelezea mambo hayo moja baada ya jingine.
MTI WA MGUDE NI HUO AMBAO PICHA YAKE INAONEKANA HAPO JUU.