Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Naibu Waziri Amtumbua Mhandisi wa Maji Halmashauri ya Korogwe

$
0
0
NAIBU Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso amemsimamisha Mhandisi wa Maji Halmashauri ya Wilaya Korogwe Mji Joseph Mcharo kwa kutumia force account kwenye mradi wa zaidi ya Milioni 700 bila ya kibali toka Wizara hiyo.

Agizo la kusimamishwa kwa Mhandisi huyo alilitoa jana wakati akikagua mradi miwili ya maji ya Mtonga ambao umetumia zaidi ya milioni 700 na msambiazi ambao umetumia zaidi ya milioni 600 ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya mkoa wa Tanga ambayo ilianza juzi wilayani Handeni.

Alisema mradi huo ulitakiwa kutumia kiasi cha shilingi Milioni 500 na wataalamu hao wakaubadilisha na kuufanya uwe wa milioni 700 ingawa bado unaendelea kusuasua jambo ambalo linaonyesha ubadhirifu wa fedha za Serikali

Akiwa kwenye mradi wa Mtonga baada ya kumalizika kuukagua alitilia mashaka na ndipo alipoamuru mhandisi huyo kumpatia maelezo ya kina kuhusiana na mradi huo lakini pia hakuridhika na maelezo hayo na kuagiza kuwa atapeleka wataalamu kutoka wizara ili kuweza kuhakiki thamani ya fedha na ubora mradi huo.
 
“Kwa kweli mimi hapa sijaridhika na utekelezaji wa mradi huu unaonekana upo chini ya kiwango na ucheleweshwaji huku wananchi wakiendelea kupata tabu hivyo nitatuma wataalamu kutoka wizarani waje kuhakiki mradi huo”Alisema

Baada ya ukaguzi wa mradi huo Naibu Waziri huyo aliambatana na viongozi mbalimbali wa halmashauri ya Korogwe mji kuelekea kwenye mradi wa Msambiazi ambako kunajengwa tenki kubwa la mradi utakaosambaza maji kwa wananchi.

Akiwa huku ndipo alipomuuliza mhandisi gharama za mradi ambapo alisema zaidi ya milioni 600 zimetumika kwa kutumia mfumo wa mkandarasi na kupelekea mradi huo kufikia kwenye hatua za mwisho jambo ambalo limeibua maswali mengi kwa Naibu Waziri na kuamua kuchukua uamuzi huo.

“Ndugu zangu haiwezekani mradi wa zaidi ya milioni 700 kutumia force account kinyume na taratibu za wizara huku mradi wa milioni 600 ukitekelezwa kupitia mkandarasi ni wazi kwamba kuna ubadhirifu unaendelea hapa na mimi sitakubali”Alisema.

Baada ya maelezo hayo Naibu Waziri aliamua kumsimamisha mkandarasi huyo kwa kigezo miradi inayotumia chini ya milioni 200 ndio inapaswa kutumia force acounti tofauti na alivyofanya mhandisi huyo huku akimdanganya kwamba anakibali kutoka wizarani.

Awali akijibu hoja za Naibu Waziri huyo Mhandisi wa Maji Halmashauri ya Korogwe Mji Joseph Mcharo alidai anakibali cha wizara kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa mtonga kutumia force acounti ndipo Naibu Waziri huyo alipoamua kupiga simu wizara kupata ufafanuzi.

Naye kwa upande wake Mkurugenzi wa Halamshauri ya Korogwe Mji Jumanne Shauri alionekana kushindwa kujibu maswali ya Naibu Waziri jambo ambalo liliibuka mabishano  baina yao kabla ya Kaimu Mkuu wa wilaya ya Korogwe Godwin Gondwe kumtaka Mkurugenzi akiri mapungufu yaliyojitokeza kwenye mradi huo.

Mradi wa Mtonga ambao Naibu Waziri Aweso aliitulia mashaka ni wa kusambaza tenki,mabomba na sehemu maalumu kwa ajili ya mtambo wa kutibia na kusafisha maji eneo la mradi husika

Waziri Kairuki Aweka Malengo Ya Uanzishwaji Soko Huria La Madini Ifikapo Desemba, 2018

$
0
0
Na Asteria Muhozya, Afisa Habari,Wizara ya Madini.
Waziri wa Madini Angellah Kairuki amesema anatamani kuona ifikapo mwezi Disemba mwaka huu, Serikali kupitia Wizara ya Madini inaanzisha Soko Huria la Madini nchini (Tanzania Mineral Exchange).

Waziri Kairuki aliyasema hayo tarehe 24 Julai, 2018, wakati wa kikao cha Menejementi ya Wizara ya Madini na Taasisi zake ambapo Wataalam kutoka Kampuni ya Tanzania Mecantile Exchange PLC  (TMC) waliwasilisha mada juu ya Elimu ya Soko la Bidhaa Tanzania.

Aidha, Waziri Kairuki aliishukuru kampuni hiyo kwa kutoa wasilisho hilo ikiwemo utaalam wao katika masuala ya soko huria la madini na kuongeza kuwa, anatamani kuona suala hilo linafanikiwa na kufanyika mapema kwa kuwa, litawezesha Watanzania kumiliki uchumi wa madini hata wale wenye kipato cha chini.

“Natamani kuona ndani ya kipindi cha miezi sita vinavyowezekana kufanyika vinaanza kufanyika. Lakini tutazingatia sheria, taratibu na utalaam kuhakikisha kwamba suala hili linafanikiwa,” alisisitiza Waziri Kairuki.

Akiwasilisha mada, Mtaalam mwelekezi kutoka kampuni hiyo, Girish Raipurie, alieleza faida za soko huria la madini kwa Tanzania, huku akisisitiza kuhusu umuhimu wa kutolewa mafunzo kwa wadau na elimu ya kutosha kuhusiana na   suala hilo.

Pia, alieleza kuhusu namna ambavyo Tanzania inaweza kujifunza kutoka kwa nchi nyingine ambazo zinafanya vizuri katika suala hilo huku akielezea mazingira wezeshi ambayo yanawezesha Tanzania kufanikiwa katika uanzishaji wa soko hilo, huku akijaribu kufananisha na mazingira ya nchini India ambayo mfumo wa soko hilo unafanya vizuri.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TMC, Godfrey Marekano, alitoa mada kuhusu Mpango wa uwekezaji katika Soko huria na pia amegusia kuhusu masuala ya kisheria na namna ambavyo Sheria ya Madini kama ilivyorekebishwa Mwaka 2017 inavyoweza kusimamia uanzishaji wa suala husika.

Naye, Naibu Waziri wa Madini Doto Biteko, alimpongeza Waziri Kairuki kwa kuanzisha wazo hilo ambalo litawezesha kuleta mageuzi katika Sekta ya Madini na kuwataka wataalam katika Wizara ya Madini na Tume ya Madini kulichukulia suala hilo kwa uzito ili utekelezaji wake uweze kufanyika kama ilivyopangwa.

“Kuna maelekezo mengi kwenye Sheria ambayo tunahitaji kuvipitia na kuyafanyia kazi. Maarifa tuliyoyapata ni makubwa. Rai yangu ni kwa wataalam kuhakikisha wanalichukulia suala hili kwa uzito mkubwa lisibaki mikononi mwa Waziri tu, alisisitiza Biteko”.

Amber Lulu Asema Hataki Tena Kupoteza Muda kwa Sababu ya Mwanaume.

$
0
0
Msanii wa muziki, Amber Lulu amedai wanaume wamemfanya aogope kuingia kwenye mahusiano ya mapenzi.

Muimbaji huyo wiki hii ameuambia mtandao wa Pro24Djs kwamba amepotezewa sana muda na wanaume ambao hawana msimamo katika mapenzi.

“Kama kutoka kimapenzi na mtu ambaye hajui thamani yako, ndio kitu ambacho huwa nakifikiria kwasababu nimepoteza sana muda,” alisema Amber Lulu. 

“Huwaga hicho kitu kinaniumiza sana,  muda ambao nilikuwa naupoteza na nguvu ambazo ningeziweka kwenye muziki wangu ningefika mbali sana,”

Aliongeza, “Ndio maana watu wanasema ni bora mtu akupende kuliko umpende, kwa sababu ukimpenda inakuwa ni shida. Vitu kama hivyo vimenipelekea kufanya vitu vya ajabu, unakuwa na watu ambae haujawataka, inakuwa kama ni hasira kwahiyo imenifanya nisitamani kumuona mwanaume yeyote katika macho yangu,”

Kumbukumbu Ya Siku Ya Mashujaa, Amani Na Uzalendo Kwa Taifa Letu

$
0
0
Na Emmanuel J. Shilatu
Leo ni Julai 25 siku ya Maadhimisho ya Mashujaa waliopambana kwa hali na mali kutetea nchi yetu ya Tanzania katika maeneo mbalimbali.

Hawa walimea uzalendo mkubwa, mwili na nafsi zao walikubali kuviweka rehani kwa ajili ya Tanzania. Bado tunawakumbuka na kuwaombea kheri kutokana na kujali na kudumisha misingi ya amani.

Misingi mizuri iliyojengwa na waasisi wa Taifa, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume , imesababisha Wananchi wa Tanzania kwa muda mrefu kuishi kwa amani na utulivu, huku wakifanya mambo yao kwa uhuru bila ya kuingiliwa na mtu yeyote wa ndani ama wa nje.

Tofauti na mataifa mengine, Watanzania wako huru zaidi kwenda kokote wanakotaka na hata kuishi ama kufanya kazi au biashara bila ya bughudha yeyote endapo kanuni, taratibu na sheria za nchi zitafuatwa ama kuzingatiwa vyema. Hali hiyo ni tofauti kabisa na nchi nyingine zikiwamo zile za jirani zetu kama Kenya, Rwanda, Burundi, Kongo na hata Uganda, nchi ambazo kwa kiasi kikubwa ukabila na chokochoko za kisiasa zimetamalaki kuanzia ngazi za kijiji hadi Taifa. Hapa kwetu tumeishi kama Ndugu bila ya u-rangi, udini, ukabila wala harakati za kiitikadi na kisiasa kutugawa.

Jambo la kushangaza ni kuwa misingi hiyo ya amani na utulivu iliyogharamikiwa na Waasisi wetu, hivi sasa ipo shakani na hatarini kutoweka kwani ilishaanza kuchezewa na chokochoko za aina mpya ya siasa (kwa maana ya ukosefu wa uvumilivu na uchu wa madaraka) iliyoanza kurindima katika siku za hivi karibuni.

Tukiwa tunawakumbuka Mashujaa hao inabidi nasi tujitathmini nafasi yetu kwa Taifa letu endapo inaedana na hali ya uzalendo. Hali ilivyo sasa kiwango cha uzalendo kimeshuka sana. Mtu yupo radhi kulalamika na kudai haki pasipo kutimiza wajibu wake kwa Taifa. Wameshajiuliza, wamelifanyia nini Taifa kabla ya kudai haki?

Vijana walio wengi wameweka pembeni uzalendo wa kulipenda Taifa lao kiasi cha kufikia hatua ya kukufuru kwa maneno ya kashfa dhidi ya Taifa lao. Hali hiyo ni tofauti kabisa na mataifa mengine ambayo hatuoni wakiyakashifu mataifa yao hadharani. Hii tabia ya kujivua nguo hadharani ni kwa faida ya nani?

Hapo hapo utakuta kuna baadhi ya Watanzania wanenda nchi za kimataifa na kuanza kuikashfu nchi yao kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vya kimataifa. Laiti kama Wazee wetu waliotutangulia wangekuwa na akili mbovu kama hizi, leo hii sidhani kama tungelikuta Taifa hili likiwa salama kama lilivyo. Umejiuliza haya ya kulichafua Taifa letu unataka uache urithi gani kwa vizazi vijavyo kwa Taifa letu?

Vijana wengi wa Leo, wananyooshewa vidole kwa kutothamini tunu ya kuwa Mtanzania. Je, U-Miongoni mwao? Kwako uzalendo ni nini? Kwako amani unailindaje?

Ndugu zangu, Wapo wanaosema kuwa amani ni sawa na yai mkononi, ukilivunja hautaweza kuliunganisha kamwe; wengine wanasema kuwa amani haina bei na ikipotea haina soko la kununua. Tuitunze amani yetu na kamwe tusiizoee wala kuichoka, tuige uzalendo waliokuwa nao Mashujaa wetu ambao walihakikisha amani ya nchi wanailinda vilivyo kwa machozi, jasho na damu.
 
*Shilatu E.J*
0767488622

Kiboko Ya Matatizo Ya Nguvu Za Kiume,maumbile Madogo, Mvuto Wa Mapenzi ,magonjwa Sugu

$
0
0
Usikate tamaa ondoa maradhi yako, maana matatizo haya yamekua yakiasili watuwengi kisaikolojia hasa baada ya kujiona wako tofauti sana na wengine kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia (6-8) vinginevyo mtuhuyo anamapunguvu katika mwiliwake.

Kunasababu nyingi sana zinazosababisha matatizo haya, chango hushambulia never ambayo huasili misuli ya uume, Ngili :- hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kufanya tumbo kuunguluma na kujaa gesi, kolodani moja kuvimba au kuingia ndani pamoja na kutopata choo vizuli. Sababuhizi na nyingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba na marakwamara husababisha kukosa hamu ya kuludia tendo la ndoa na baadae kushindwa kabisa

MASISA 3POWER :- nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa mfumo wa vidonge, huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka 15-90 , inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii) inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa, itakufanya uludie tendo la ndoa zaidi ya mara nne (4) birahamu kuisha wara kuhisi kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya dk (20-30 )

YONINANI:- hurefusha na kunenepesha maumbile madogo ya uume uliosinyaa inchi 6-8 na unene wa sm 3-4 kwa mda mfupi sana,

SUPER MORINA :- nidawa inayotibu ama kutatua tatizo la kisukali kwawaliohangaika bila mafanikio, huondoa tatizo la kisukali na kupona kabisa, vilevile ninadawa ya magonjwa sugu km vile presha, vidondo vya tumbo, miguu kuwakamoto, muwasho mwilin, kaswende,uzazi nk.

LUGIMBA :- nidawa ya mvuto wa mapenzi, humtuliza mke, mme, mchumba, hawara au mtu yoyote umpendae na kumfanya akutimizie chochotekile unachokitaka kutoka kwake na kumfunga asiwe na mtu yoyote zaidi yako.

WASILIANA NA DR CHIPUPA NAPATIKANA DAR ES SALAAM KUMBUKA HUDUMAHII ITAKUFIKIA POPOTE ULIPO  0759208637 / 0785687900

Maradhi Ya Kichawi Na Tiba Zake

$
0
0
Wachawi  wana  uwezo  wa  kumsababishia  mtu maradhi  kwa  kutumia  uchawi.

Mtu  aliye tupiwa  maradhi  ya  kichawi  huanza kuonyesha  dalili  zote  za  mgonjwa  wa  maradhi  husika. 

Kama  mhusika  ametupiwa  maradhi  ya  kiharusi  basi  ataonyesha  dalili  zote  za  mgonjwa  wa  kiharusi, kama  ametupiwa  maradhi  ya  kifafa  basi  ataonyesha  dalili  zote  za  mtu mwenye  kusumbuliwa  na  maradhi  ya  kifafa  na kama  atakuwa  ametupiwa  ukichaa  basi  mtu huyo  ataonyesha  dalili  zote  za  mtu  mwenye  kichaa.

DALILI   ZA  MAGONJWA  YA  KICHAWI
Kila maradhi  ya  kichawi  yana  sifa na dalili zake     za  kipekee.

Kwa  maana  ya  kwamba  kifafa  cha  kichawi  kina  dalili  zake, kichaa  cha  kichawi  kina  dalili  zake, kiharusi  cha  kichawi  kina  dalili zake  nakadhalika  nakadhalika.

Lakini  maradhi   yote  ya  kichawi  huwa  na  sifa  moja  ya  kipekee  ambayo  kila  mwenye  kusumbuliwa  na  maradhi  ya  kichawi  huwa  nayo.

Nayo  ni  kutumia  tiba  nyingi  kwa  muda  mrefu  bila  kupata  nafuu  yoyote  ya  kudumu  pamoja  na  ugonjwa  kuto onekana  kwenye  vipimo  vya   hospitalini.

                  AINA   YA  MARADHI  YA  KICHAWI
Maradhi ya  kichawi  yamegawanyika  katika   aina  kuu  mbili  kama  ifuatavyo :

1.    AINA YA  KWANZA : MARADHI  YA  KICHAWI  YATOKANAYO NA  KULISHWA  SUMU  ZA  KICHAWI

2.    AINA  YA  PILI  :  MARADHI  YA  KUTUMWA  KWA  KUTUMIA  MAJINI  WA  KISHEITWANI

MARADHI   YATOKANAYO   NA  KULISHWA  SUMU  ZA  KICHAWI.

Wachawi  wana  elimu  na  maarifa  mapana  sana  kuhusu  miti  mbalimbali  ya  porini  ambayo inapotumiwa na  wanadamu  au  wanyama  hutengeneza  sumu  yenye  kusababisha  maradhi  mbalimbali  katika  mwili  wa  mwanadamu  au mnyama  husika.

Mfano  kuna  mti  mmoja  wa  porini. Ni mti  mrefu wenye  kutoa  majani  yenye  kunukia. Mafuta  ya  mti  huu  hutumiwa  na  wachawi  katika  kuwasababishia  watu  maradhi  ya  ini.

Mafuta  ya  mti  huo  husababisha  kufeli  kwa  ini.  Kinacho  fanyika  mtu  aliekusudiwa  anakuwa  anawekewa  kijiko  kimoja  kidogo cha  mafuta  hayo kwenye  chakula  anacho  tumia  kwa  muda  wa  siku  saba  mfululizo.

Sumu hiyo  hufanya  kazi  kwa  taratibu  sana  na  inaweza  kuchukua  hata  miezi  sita  kuanza  kuonyesha  dalili.

 Mwisho  wa  siku  mhusika  alielishwa  sumu  hiyo  ndio  anakuwa  tayari amekuwa  ameshapewa  maradhi  ya  ini.

 Mara  nyingi  uchawi  huu  hufanywa  na  mtu  wa  karibu.

Kuna mti mmoja  wa  porini  ambao wachawi  wanau  tumia  kuwasababishia  wanawake  wajawazito  tatizo  la  kuchoropoka  kwa  mimba.

Majani  ya  mti  huu  hupondwa  pondwa  na  kuchemshwa  na kisha  kuchanganywa  kwenye  chakula  atakacho  kula  mwanamke  mwenye  ujauzito  mchanga.

Mwanamke  huyo  akisha  kula  dawa  hizo  za  kichawi  basi  hazitapita  siku  tatu  huo  ujauzito  utachoropoka.

Hali  hii  itakuwa  inajirudia  kila  mwanamke  huyo  anapokuwa  amebeba  ujauzito  kwa  sababu  wanao kuwa  wanasimamia  zoezi  hilo  ni  watu  wake  wa  karibu.

Ndio  maana  unakuta  wanawake  wengine  amebeba  mimba  Zaidi ya  nne  na  zote  zinachoropoka  na  kumsababishia  maisha  magumu  katika  ndoa  yake.

Hayo  ni  baadhi  ya  maradhi  lakini  karibu  kila  maradhi  unayo yafahamu  wewe  wachawi  wanaijua  miti ya  porini  ambayo  wakimlisha  mtu  basi  moja  kwa  moja  inakwenda  kuathiri  sehemu husika  katika  mwili  wa  mkusudiwa  na  kumsababishia  maradhi  yaliyo  kusudiwa.  Ipo  miti  inasababisha  uziwi, upofu, ugumba,  ukhanithi, pumu,mtoto kuchelewa kuongea, kutembea  nakadhalika.

MARADHI   YA   KUTUMWA   KWA   KUTUMIA   MAJINI   WA  KICHAWI.
Haya  ni  maradhi  yanayo  tumwa  moja  kwa  moja  kwa  mkusudiwa  kwa  kutumia  majini  wa  kisheitwani.

Hapa  jinni  wa  kisheitwani  huamriwa  kwenda  kukaa  ndani  ya  nafsi  ya  mtu  Fulani  na  kumsababishia  maradhi  Fulani.

Mtu  aliye  tumiwa  jinni huyu wa  kisheitwani  huanza  kuonyesha  dalili  zote  za  mtu  mwenye  maradhi  yaliyo  kusudiwa.

Atakaa  na  maradhi  hayo  kwa  muda  mrefu  na  atatumia  tiba  za  kuondosha  maradhi  hayo bila  kupata  nafuu  yoyote  ya  kudumu na  mwisho  wa  siku  atakata  tamaa  kabisa  akisubiri  kifo  kimchukue .

TIBA ZA   MAGONJWA   YA   KICHAWI
Maradhi  ya  kichawi  yanaweza kutibiwa  kwa  kutumia  dua, kafara, na  miti  ya  aina  mbalimbali  kulingana  na  aina  ya  maradhi  yanayo  msumbua  mhusika.

Lakini  kabla  ya  mhusika  kutibiwa  ni  lazima ijulikane  kwanza  kama  maradhi  yanayo  msumbua  ni  ya  kawaida  ( ya kibinadamu ) ama  ya  kisheitwani  ( maradhi  ya  kichawi )

Zipo  njia  mbalimbali zinazo  tumika  kujua  kama  mgonjwa  husika  maradhi  yake  ni  ya  kibinaadamu  au  ya  kisheitwani.

 Nitazielezea  kwa  ufupi  njia  hizo.

(  Utajuaje  kama  maradhi  yanayo  kusumbua  ni maradhi  ya  kichawi )

1.    Kusoma  dalili  za mgonjwa. ( Kila  maradhi  ya  kichawi  yana  dalili  zake  maalumu  ambazo  huweza  kutumika  kama  viashiria  vya  kujua  kama  mhusika  ana sumbuliwa  na  maradhi  ya kibinadamu  au  ya  kichawi.

2.    Kusoma nyota  ya  mgonjwa  ili kujua  kama imetiwa  kiza cha maradhi

3.    Kufanya  dua  maalumu  ya  kuomba  kujua  kama  maradhi  yanayo  msumbua  mhusika  ni ya  kibinadamu  au  ya  kisheitwani. Kama  ni  maradhi  ya  kibinadamu  basi  mgonjwa huyo  atapewa  tiba  za  kawaida  ambazo  hutibu  magonjwa  ya  kibinaadamu  na  kama  ni  itajulikana  ni  maradhi  ya  kisheitwani  basi  atapewa  tiba  sahihi  kulingana  na  maradhi  yanayo  msumbua.

4.    Kumtibu  mgonjwa  kwa  kutumia tiba  maalumu  za  asili  ambazo  hutibu  na  kuondosha  kabisa  maradhi  husika.

 Katika  ulimwengu  wa  kitabibu  zipo  tiba  maalumu  za  asili  ambazo zina sifa ya  kutibu  na  kuondosha  kabisa aina  Fulani  ya  maradhi  yanayo  wasumbua  wanadamu.

 Ikitokea  tiba  hiyo  imeshindwa  kumtibu  mgonjwa  huyo basi  ni ishara  ya  moja  kwa  moja  kwamba  maradhi  yanayo  msumbua  mtu  huyo  ni  maradhi  kisheitwani.

Mfano  wa  tiba  hiyo  ni  ile  itokanayo  na  mti  wa  Mgude.

Kwa  wenyeji  wa mikoa  ya  Tanga, Pwani  na  kusini  ( Lindi  na  Mtwara ) mtakuwa  mnaujua  mti  huu  vizuri.

 Unajulikana  kwa  wengi  katika  utabibu  kama  mti  wenye  kukaliwa  na  majini  wakubwa  wa  kisheitwani  wenye  sifa  tofauti  tofauti.

Ni mti  wenye  maajabu  sana  na  unao  tumika  kufanyia kafara  nyingi  kubwa  kubwa.

Kwa  kifupi  ni  mti  unaopendwa  sana  na  majini  wabaya.  Kama  unataka  kufanya  ushirika  ama  agano  na  majini  wabaya  basi  mti  wa  mgude  utakufaa  sana.

Ukiwa  unataka  kuwa  unaona  mauza  uza  nyumbani  kwako  basi  panda  mti  huu  wa  mgude.     Mti wa Mgude unaingia  pia  katika  nyungu  ya  miti  saba  mikubwa  ya  porini na  huweza  kutumika  pia  kuwafukuza  baadhi  ya  majini  wabaya  ambao  ni  wadogo  kimamlaka  kwa  majini  wanao  kaa ndani  ya  mti  huu.

Sasa  basi  mti  huu  wa  Mgude  mbali  na  kuwa  na sifa  hizo  nilizo  zitaja  hapo  juu, lakini  pia  mti  huu  unatoa  tiba  mujarabu kabisa . Mti  wa  mgude  unatumika  katika  kutibu  na  kuondosha  kabisa  maradhi  yafuatayo :

1.    KIHARUSI  :   Magamba  na  majani  ya  mti  wa  mgude  huanikwa  juani  na  kukauka  kisha  husagwa  halafu  unga  unga  wake  huchemshwa  na  maji  na  kisha  kimiminika  kupewa  mtu  mwenye  maradhi  ya  kiharusi . Mgonjwa  atapona  kabisa  kiharusi  ndani  ya  siku  21.  ( KIHARUSI  KINACHO  TIBIWA  NA  TIBA  HII  YA  MTI  WA  MGUDE  NI  KIHARUSI  CHA  KAWAIDA  NA  SIO  CHA  KUROGWA.  KATIKA  ULIMWENGU  WA  KITABIBU, MGONJWA  WA  KIHARUSI  AKITUMIA  TIBA HII  HALAFU  ASIPONE  BASI  NI  ISHARA  KWAMBA  MARADHI  ALIYO  NAYO  YAMETOKANA  NA  KUROGWA.

2.    UKHANITHI :  Hapa   namzungumzia  mwanaume  ambae  hawezi  kabisa  kusimamisha  uume wake na  sio  yule  shida  ya  udhaifu  tu wa  nguvu  za  kiume. Namaanisha  asie w eza  kabisa  kusimamisha  uume  wake . Magamba  ya  mgude  huanikwa  juani  na  kusagwa  ama  kupondwa  pondwa  hadi yawe  unga  na  kisha kuchemshwa  na  mgonjwa  kupewa  kimiminika  anywe   mara  tatu  kwa  siku  asubuhi mchana  na  usiku  kwa  muda  wa  siku  saba. Asipopona  maradhi  yake  basi  hicho  kiashiria kwamba  maradhi  ya  mhusika  yanatokana  na  kurogwa kwa  hivyo  hutafutwa  tiba  ya  kubatilisha  uchawi  ulio  msababishia  mhusika  maradhi  ya  ukhanithi.

3.    MALARIA  YA  UBONGO (  ambayo  huchukuliwa  kama  ukichaa ).   Mti  wa  mgude  hutibu  na  kuondosha  kabisa  maradhi  ya  malaria  iliyo  panda  kichwani  au  malaria  ya  Ubongo. Majani  ya  mgude  huchukuliwa  na  kuanikwa  juani  kisha  kusagwa  halafu  kuchemshwa  na  maji  halafu mgonjwa  anakuwa  anapewa  kunywa  kwa  muda  wa  siku  kumi  na  nne.  Kama  maradhi  yake  ni  ya  kawaida  basi  ndani  ya  hizo  siku  kumi  na  nne  atakuwa  amepona  maradhi  yake  na  ikiwa  vinginevyo  basi  ni ishara  kwamba  maradhi yake  ni  ya  kutengenezwa  kichawi.

4.    TATIZO  LA  KUCHOROPOKA  KWA  MIMBA : Mizizi  ya  mgude  hutumika  kutibu  na  kuondosha  kabisa  tatizo  la  kuchoropoka  kwa  mimba  hata  kama  limedumu  kwa  muda  mrefu  kiasi  gani.  Mwanamke  mwenye  tatizo  la  kuchoropoa mimba  akitumia  mizizi  ya  mgude  halafu  tatizo  lake  likaendelea  kujirudia  basi  ni  ishara  ya  moja  kwa  moja  kwamba  tatizo  lake  hilo  linasababishwa  na  majini  wa  kisheitwani.

5.    Maradhi  mengine  yatibiwayo  na  mti  wa  Mgude  ni pamoja  na kichocho  na  kuhara.

MAKALA  HAYA  YAMEANDALIWA  NA  DOKTA. MUNGWA  KABILI. ANAPATIKANA  KWA  SIMU  NAMBA  0744  000  473.

Makala  haya  yanapatikana  kwa  undani  Zaidi  katika  kitabu “ MAMBO TISA  YANAYO  UNDA  NYOTA  YA  MWANADAMU : UHUSIANO  KATI  YA   NYOTA  YA  MTU  NA  MAFANIKIO  YAKE  KATIKA  MAISHA ambacho  kimeandikwa  na  Dokta. Mungwa  Kabili.


Katika  Makala  zijazo  nitakuwa  nikielezea  magonjwa  yote  ya  kichawi  kwa  kuangalia  ugonjwa  mmoja  baada  ya  mwingine. Jinsi  yanavyo  tengenezwa  na  wachawi, lengo  la  kuyatengeneza, jinsi ya  kujiikinga  nayo  na  jinsi  ya  kujitibu   kwa  mtu  ambae  tayari  ametupiwa  maradhi  hayo  ya  kichawi.

Pia  kufuatia maombi  ya  watu  wengi  ambao  wameshindwa  kupata  nakala  za kitabu  changu  MAMBO TISA  YANAYO  UNDA  NYOTA  YA  MWANADAMU…  Siku  chachae  zijazo   nitayaelezea  mambo  hayo  moja  baada  ya  jingine.

MTI  WA  MGUDE  NI  HUO  AMBAO  PICHA  YAKE  INAONEKANA  HAPO  JUU.

Kesi Ya Mbowe na Vigogo Wengine CHADEMA Kuanza Kuunguruma Julai 31

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru viongozi tisa wa Chama cha Demekrasia na Maendeleo (Chadema) katika kesi inayowakabili viongozi hao akiwamo Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe kusomewa maelezo ya awali Julai 31, mwaka huu na mashahidi kuanza kutoa ushahidi.

Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ametoa uamuzi huo leo Jumatano Julai 25, baada ya kufahamishwa kwamba maombi yaliyowasilishwa Mahakama Kuu na viongozi hao yalitupwa kwa sababu yalikosa vigezo vya kisheria na pia iliona maombi hayo yalikuwa ni batili.

Kutokana na hatua hiyo, Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi ameiomba mahakama kuipangia kesi hiyo tarehe ya usikilizwaji wa awali na baada ya hapo zipangwe tarehe mfululizo za kuanza kusikilizwa kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka.

Wakili wa upande wa utetezi Nashon Nkungu kwa niaba ya Wakili Peter Kibatala na Jeremiah aliomba kesi iahirishwe kwa muda mrefu lakini Wakili Nchimbi alipinga akidai  hoja hizo hazijawekwa katika kumbukumbu za mahakama aliomba kesi ipangiwe tarehe ya usikilizwaji wa awali  na tarehe za kesi kusikilizwa mfululizo kwa ushahidi wa mashahidi wa upande wa mashtaka.

Hakimu Mashauri baada ya kusikiliza hoja za pande zote aliipanga kesi hiyo kwa ajili ya usikilizwaji wa awali  Julai 31,mwaka huu na kuutaka upande wa utetezi iwapo watakuwa na hoja zozote kuhusiana na maombi yao ya kesi kuahirishwa muda mrefu uwasilishe.

Washtakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 13, ikiwamo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai kati ya Februari Mosi na 16, 2018, Dar es Salaam.

PICHA: Waziri Mkuu Aadhimisha Siku Ya Mashujaa Kwa Kushiriki Katika Kufanya Usafi Wa Mazingira Eneo La Coco Beach Jijini Dar

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary  wakifyeka nyasi kwenye  eneo la Coco Beach jijini Dar es salaam  wakati waliposhiriki  katika maadhimisho ya   Siku ya Mashujaa kwa kufanya usafi wa mazingira katika eneo hilo , Julai 25, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakiadhimisha  Siku ya Mashujaa kwa kufanya usafi katika eneo la Coco Beach jijini Dar es salaam Julai 25, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakipeleka uchafu kwenye gari la takataka wakati waliposhiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa kwa kufanya usafi wa mazingira kwenye eneo la Coco Beach jijini Dar es salaam Julai 25, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua  eneo la Coco Beach  baada ya kushiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa kwa kufanya usafi wa mazingira kwenye  eneo hilo Julai 25, 2018. Wapili kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kinondoni, Ally Happy. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu: Hali Ya Usafi Coco Beach Hairidhishi

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema hali ya usafi Coco Beach hairidhishi na amewataka viongozi wa Manispaa ya Kinondoni wajipange ili eneo hilo liweze kuvutia.

Ametoa kauli hiyo leo (Jumatano, Julai 25, 2018) wakati akizungumza na wananchi mara baada ya kushiriki zoezi la usafi wa eneo hilo pamoja na wananchi na watendaji mbalimbali ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa ambayo hufanyika Julai 25, kila mwaka.

Waziri Mkuu ambaye aliambatana na mke wake, Mary Majaliwa, alishiriki zoezi hilo kwa kufyeka nyasi, kuzoa takataka na kupanda miti kwenye ufukwe huo. Zoezi hilo limefanyika kuanzia kwenye eneo la wafanyabiashara wa mihogo kuelekea Police Officers’ Mess.

“Eneo hili nimelitembelea, bado haliridhishi kwa usafi. Nimeenda kwenye fukwe pale na kukuta takataka nyingi zimelundikwa mahali pamoja. Ni vema Manispaa ya Kinondoni na Mamlaka zote zinazosimamia usafi ziwaratibu wanaotoa huduma na wanaopata huduma ili    kuendeleza usafi wa maeneo haya nchini kote,” amesema.

Amesema Manispaa ya Kinondoni haina budi kuratibu eneo hilo kwa kupanga eneo la maegesho, la watu kupumzikia, la huduma za chakula na kuongeza kupanda miti ili wananchi waone ni maeneo mazuri yanayovutia.

“Muandae shughuli za burudani zitakazofanyika kila Jumamosi na Jumapili. Karibisheni watu wa kuleta michezo ya baharini kama vile viboti na vibaiskeli vya majini, wekeni bembea ili fukwe ivutie zaidi. Wazazi wataleta watoto wao kwenye michezo wakati wao wakikaa pembeni na kupumzika,” amesema.

Amesema vibanda vilivyoko kwenye ufukwe huo havipendezi na ikibidi waangalie uwezekano wa kuweka makontena ili kuongeza mvuto. “Vibanda hivi havileti picha nzuri sana, hivyo mnaweza kuweka makontena kutoka Pepsi au Coca-Cola ili kuleta muonekano sawia.”

“Jambo hilo linaweza kuwa ni chanzo cha mapato kwa Manispaa hii. Uongozi wa Manispaa tengenezeni haya wakati mkisubiri andiko lenu lipitishwe na muweze kupata fedha za kuboresha ufukwe huu,” amesema.

Alisema eneo jingine linalopaswa kuangaliwa katika ufukwe huo ni kuimarishwa kwa ulinzi ili watu wanaokwenda kupata huduma wasihofie usalama wao.

Waziri Mkuu amesema usafi siyo uishie kufanyika tarehe 25 tu, na akawataka watendaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kwenye fukwe zote. “Hii ni changamoto kwenye Mamlaka ya Halmashauri ya Kinondoni, lakini pia Ilala, Temeke, Bagamoyo hadi Tanga, zinapaswa aihakikishe hizi fukwe ziwe safi,” amesema.

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na wananchi hao, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Bw. Ally Hapi alisema mbali ya wananchi wa kawaida, walikuwepo pia askari polisi 100 na wanajeshi 150 ambao walishiriki zoezi hilo la usafi.

Alisema Manispaa ya Kinondoni wameanza kutekeleza maelekezo ya Waziri Mkuu juu ya uboreshaji wa fukwe ya Coco kwa kuandika andiko maalum na kulipeleka Ofisi ya Rais – TAMISEMI. “Manispaa kupitia miradi ya kimkakati, tumeandaa andiko la kuomba sh. bilioni 11 za kutengeneza na kuboresha ufukwe wa Coco, na tumeshalipeleka TAMISEMI na mazungumzo yanaendelea,” alisema.

Juni 29 mwaka huu, wakati akitoa maelekezo kwenye hafla ya uzinduzi wa kituo cha polisi kinachohamishika, Waziri Mkuu alisema: “Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli anawataka Watanzania wote waadhimishe siku hiyo ya kumbukumbu ya mashujaa kwa kufanya usafi katika maeneo yaliyo jirani na makazi yao pamoja na yale ambayo wamezikwa mashujaa ikiwa ni njia ya kuwaenzi.

Siku hiyo hiyo, Waziri Mkuu alitangaza kwamba Rais Magufuli ameagiza kwamba sh. milioni 308 zilizotengwa kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa, zitumike kuboresha miundombinu ya barabara jijini Dodoma.

Aliitaja miundombinu hiyo ni pamoja na taa za kuongezea magari kwenye makutano ya barabara ya Kisasa na barabara kuu ya Dodoma Dar es Salaam na kuweka taa za barabarani kwenye barabara mpya ya mchepuko kutoka Emmaus hadi African Dream iliyojengwa ili kupunguza msongamano wa magari yanayoingia kutoka barabara kuu ya Dar es Salaam.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Ombi la Kamanda Mambosasa Kwa Rais Magufuli

$
0
0
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam SACP, Lazaro Mambosasa amemuomba Rais Dkt. John Magufuli kutenga Wilaya ya kipolisi Chanika na Mbweni jijini humo ili kurahisisha shughuli za kiusalama na huduma kwa wananchi wa maeneo hayo.

Akizungumza katika kongamano la usalama katika jimbo la Ukonga, mapema leo Julai 25, 2018 Mambosasa amesema uhitaji wa Wilaya hizo za kipolisi ni muhimu kwani maeneo hayo yanahitaji kuongezewa askari polisi hadi kufikia 100 lakini kutokana na kuwa hakuna Wilaya ya kipolisi ni ngumu kuongezewa askari hao.

“Jambo hili la kukosekana kwa wilaya za kipolisi katika maeneo haya linapelekea shughuli za kiusalama kushindikana huku wananchi wakikosa huduma za kipolisi ngazi ya wilaya na kulazimika kusafiri mwendo mrefu kutafuta huduma hizo”, amesema Mambosasa.

Aidha, SACP Mambosasa amewaagiza makamanda wote kusimamia kikamilifu vikundi vya ulinzi shirikishi katika maeneo yao kwani vikundi hivyo vinasaidia kupunguza upungufu wa askari polisi, huku akihimiza kero zote za kata zitatuliwe ngazi ya kata kuliko kuwaacha wananchi kuwa na kero nyingi.

Takwimu za matukio ya uhalifu kutoka jeshi la polisi zinaonyesha kuwa katika maeneo hayo kuanzia mwezi Januari, mwaka 2018 kuna matukio ya uhalifu 990 huku ubakaji ya kiwa 89, matukio ya wizi wa pikipiki 154.

CHADEMA Wadai Kushitushwa na Kauli ya "CCM Itatawala Milele"

$
0
0
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kauli kuwa hadi ifikapo mwaka 2020 upinzani hautakuwepo na ile ya CCM itatawala milele, zinazidi kuwapatia mashaka.

Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa CHADEMA , Benson Kigaila amesema kauli hizo na yale yanayojiri katika uchaguzi mdogo, vinawapa shaka kuwa kuna mpango usio wa heri.

“Tumepata nyaraka inayosambaa kwenye mitandao ina nembo ya Tume (ya Taifa ya Uchaguzi) na CCM wanaitumia kujitapa kushinda kata 30. Tunashindwa kuelewa kwa nini hatujapewa vyama inazunguka mitandaoni,”

Akizungumzia juu ya namna wanavyodhulumiwa  Kigaila amesema kwamba “Kata za Halmashauri ya Iringa Mjini pia wagombea wameondolewa kwa uonevu,”.

Hata hivyo kauli hii ya Bw. Kigaila inakuja ikiwa tangu siku moja ipite tangu Mwenyekiti wa UVCCM, Kheri Jame kusema kwamba CCM imejiandaa kupima ‘mitambo’ yake katika uchaguzi huo mdogo ili kuhakikisha inakifuta CHADEMA katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Katika kampeni hizo, James alisema kwamba “Nataka kuwaambia kwa namna mitambo yetu ilivyofungwa hakuna mgombea wa upinzani ambaye atashinda, na mwaka 2020 CHADEMA watabaki labda ya majimbo mawili tu kusini moja na kaskazini moja,”

Alisema katika kuhakikisha kazi zinafanyika vizuri, wabunge wa upinzani wataporomoka wote mwaka 2020 na CCM itakaa yenyewe ili kupitisha mambo ya maendeleo kwa Watanzania.

 Hata hivyo kauli Mwenyekiti wa UVCCM haijapishana na ya Mwenyekiti wa Chama hicho Rais John Magufuli  kwamba chama hicho kitatawala milele

“CCM ni chama tawala na kitaendelea kutawala milele na milele. Kwa wanaohangaika watapata tabu sana siku zote, siku hakuna mbadala ni CCM hadi milele. Wanachama wa CCM tembeeni kifua mbele tumeamua kuleta Tanzania mpya inayowapigania wananchi  hasa wanyonge ili waweze kushiriki katika maendeleo,”  alisema Dk. Magufuli.

Katika uchaguzi mdogo unaoendelea CHADEMA wamekuwa wakilalamika kuchezewa rafu na wapinzani wao huku wakieleza kwamba dola, pamoja na Tume ya uchaguzi imekuwa ikiwapendelea wenzao.

Mizizi 29 Power ,ndio Dawa Bora Na Imara Kwa Sasa Kwa Kutibu Na Kuponesha Tataizo La Nguvu Za Kiume Kwa Dakika 30 Tu

$
0
0
Tatizo la upungufu wa nguvu za kiume limekuwa ni janga kubwa sana kwa sasa sio vijana au wazee wanalalamiki kukimbiwa na wa wapenzi wao au ndoa kuvunjika kutokana na mwanaume kulala na mwanamke kitanda kimoja hata wiki mbili bila kushiriki tendo la ndoa na hii ndio inachangia wanawake wengi kutoka nje ya ndoa kwa nini huteseke na wakati dawa zipo ambazo zitarudisha heshima yako ya ndoa 

MIZIZI 29 POWER; ni ambayo hutibu na kurudisha virutubisho mwilini ambavyo humfanya mwanaume awe na matatizo yafatayo 1 kuwahi kukojoa kabla mke au mpenzi wake

 2. kushindwa kurudia tendo dawa, hii itakufanya kurudia tendo zaidi ya Mara tatu 

3... dawa hii inatibu uume uliolegea na kusinyaa 

4. dawa hii inatoa miungurumo ya tumbo na uchovu wakati wa kumaliza tendo 

NINI KINASABABISHA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME 1 kupiga punyeto kwa mda mrefu 
2 upungufu wa vichochoe mwilini 
3 magonjwa ya moyo, kisukari, presha, vidonda vya tumbo kiuno na mgongo 
4 utumiaji ovyo wa madawa ya kizungu 
4 usongo wa mawazo, hasira, tumbo kujaa gesi na kutopata choo.

 PATA TIBA YANGU NA NI TOFAUTI NA ULIZO WAHI KUTUMIA: 

Je una uume mfupi na mwembamba? MASHESHA MIX ni dawa ya kuboresha uume saiz upendayo asa kwa wale waliofanyiwa tohara wakiwa wadogo.. chagua saizi upendayo inch 5,6,7, adi 8 iyo ni kwa urefu na unene sentimita 2,3,4, adi 5 .dawa hizi zipo za kupaka na kunywa na hazina madhara yoyote kwa mtumiaji ,

Tunatibu kisukari,vidonda vya tumbo,ngiri, korodani iliyovimba, kupnguza kitambi, maziwa makubwa NK 

KWA TIBA NA USHAULI FIKA OFISINI KWANGU DARE S SALAAMU MBAGALA ZAKHEMU NA MIKOA YA KANDA YA ZIWA YUPO WAKALA WETU HAPO MWANZA NA KWA AMBAO HAWANA NAFASI YA KUJA OFISINI HUDUMA YETU UTALETEWA POPOTE ULIPO PIGA SIMU 0783185060 DR MAKOYE

Kamati Ya Bunge Ya Miundombinu Yaipongeza TTCL Kwa Kujenga Mazingira Rafiki Kwenye Minara Ya Simu Nchini

$
0
0
Kamati ya Bunge ya Miundombinu imelipongeza Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kwa kujenga mazingira rafiki ya uwepo wa choo na kibanda cha mlinzi kwenye minara ya simu iliyojengwa na Shirika hilo maeneo mbali mbali nchini kote

Hayo yameelezwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Hawa Mchafu wakati wa ziara ya Kamati hiyo ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano kwenye kijiji cha Mbatamila kilichopo kwenye kata ya Nampungu wilayani Tunduru mkoani Ruvuma

Mhe. Mchafu amesema kuwa tumeshuhudia kuwa Shirika letu la kizalendo la TTCL pekee ndilo ambalo limejenga miundombinu rafiki ya choo na kibanda kwenye minara yao yote waliyojenga kwenye maeneo mbali mbali nchi nzima kwa ajili ya mlinzi anayelinda minara ya mawasiliano tofauti na kampuni nyingine za mawasiliano ambapo zote kwa pamoja zimepatiwa ruzuku na Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) ya kujenga minara hiyo kwenye maeneo yasiyo na mvuto wa kibiashara

“Hongereni mmepata mawasiliano ya mnara wa TTCL ambapo wamejenga miundombinu rafiki ya choo na kibanda cha mlinzi cha kupumzikia hivyo mnara utalindwa muda wote, kutakuwa hamna maambukizi ya magonjwa kwa kukosa choo”, amesema Mhe. Mchafu. Ameipongeza TTCL kwa kuwa wamejenga mnara ambao unatoa mawasiliano muda wote kwa kuwa kuna nishati ya jenereta kubwa ya kisasa.

Naye Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye ameipongeza TTCL kwa kujenga minara ya mawasiliano yenye mazingira rafiki kwenye minara yao yote iliyopo maeneo mbali mbali nchi nzima. Nditiye ameongeza kuwa Tunduru ni Wilaya pekee ambapo TTCL ina jumla ya minara 14 na kupitia UCSAF itaongeza minara mingine mitatu kwenye vijiji ambavyo vina mawasiliano hafifu kwa kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa wananchi wanawasiliana. Ameongeza kuwa Serikali inajenga meli na reli ya kisasa hivyo wahakikishe kuwa muda wote wananchi wanawasiliana wakiwa safarini.

Pia, ameiagiza Mamlaka ya   Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuhakikisha kuwa kampuni za simu zinatoa huduma ya mawasiliano kwa wananchi ya kupiga simu, vifurushi na ujumbe kuendana na gharama ya vocha iliyowekwa ambapo ni tofauti na TTCL ambao hawana ujaja ujanja wa kuwaibia wananchi.

Akithibitisha kuhusu upatikanaji wa mawasiliano mbele ya Kamati hiyo, mwananchi wa kijiji cha Mabatamila kilichopo kwenye kata ya Nampungu iliyopo wilayani Tunduru mkoani Ruvuma Bwana Kassim Zuberi amesema kuwa wanaipongeza TTCL kwa kutoa mawasiliano kwa gharama nafuu zaidi ukilinganisha na kampuni nyingine za mawasiliano. “Tunaiomba TTCL watufungulie huduma za 4G ili tuweze kupata mawasiliano ya intaneti”, amesema Zuberi.

Mwendeshaji wa UCSAF Mhandisi Albert Richard amesema kuwa UCSAF imetoa shilingi milioni 460 kwa TTCL ili iweze kujenga mnara huo ambapo wananchi wanapata mawasiliano. Pia, ameongeza kuwa tayari UCSAF kupitia ruzuku inayotoa tayari minara 14 imejengwa kwenye Wilaya hiyo na kwenye zabuni ijayo itaongeza minara mitatu ili wananchi waweze kuwasiliana muda wote.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Mhe. Christina Mndeme akizungumza na wajumbe wa Kamati hiyo walipofika ofisini kwake wakati wa ziara yao ya kukagua upatikanaji wa mawasiliano mkoani humo, Mhe. Mndeme ameishukuru Serikali kwa kujenga minara 14 kwenye Wilaya ya Tunduru. Amesema kuwa mawasiliano ni kichocheo cha ukuaji wa uchumi kwa kuwa wanapokea watalii wengi ambao wanachangia pato la taifa. “Niwaombe watoa huduma watoe huduma ya intaneti kwa kuwa ni kikwazo kwa wawekezaji mkoani kwetu ambapo wanataka wapate mawasiliano wakati wote,”amesema Mndeme. Ameongeza kuwa mawasiliano yatasaidia miamala ya kifedha ambapo inakuwa rahisi kwa wananchi kuwasiliana.

Pia, amefafanua kuwa watoa huduma za mawasiliano wanaojenga minara waangalie jiografia ya mkoa wa Ruvuma kwa kuwa una milima, misitu ni mingi sana, hifadhi, mabonde, ziwa Nyasa na iko mpakani mwa nchi ambapo maeneo hayo yanakuwa na changamoto za mawasiliano na baadhi ya maeneo ya Chiwindi na Chimati wananchi hawapati mawasiliano. Amesema kuwa mawasiliano yanahitajika wakati wote hasa maeneo ya mipakani kwa kuwa mawasiliano ni muhimu katika kuimarisha ulinzi na usalama wa wananchi na taifa kwa ujumla.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

CHADEMA Wapangua Tuhuma za Kuhusika na Mauaji ya Akwilina Akwiline

$
0
0
Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), limesema kauli ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa ya kukihusisha Chadema na mauaji ya mwanafunzi Akwilina Akwiline, inalenga kukiwekea chama hicho vikwazo kwenye uchaguzi mdogo wa Agosti 12.

Akizungumza na wanahabari jana, Kamanda Mambosasa alisema askari waliokuwa wanashikiliwa na polisi wakihusishwa na kifo cha mwanafunzi wa chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) waliachiwa huru baada ya ushahidi kuwa hafifu.

Mambosasa alinukuliwa akisema, badala yake waliohusika ni Chadema waliohamasishaji maandamano yale ya kisiasa yaliyofanyika Februari 16, siku moja kabla ya uchaguzi wa Jimbo la Kinondoni.

Akwilina alipigwa risasi kichwani akiwa kwenye daladala wakati viongozi na wanachama wa Chadema wakiandamana kwenda Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kinondoni.

Akizungumza na wanahabari leo Julai 25, Mwenyekiti wa Bavicha Patrick Ole Sosopi amesema kauli ya Mambosasa inalenga kuwaaminisha wananchi kuwa shughuli za Chadema ni hatari na sio salama kwa watu kuhudhuria.

"DPP (Mkurugenzi wa mashtaka) alishafunga jalada la kesi ya Akwilina, lakini Mambosasa ameliibua upya tena wakati ambao tunaelekea katika uchaguzi ili kuonyesha kuwa maandamano yanasababisha mauaji. Propaganda kama hizi alitakiwa kuzifanya Polepole (Katibu Mwenezi wa CCM) na sio mtendaji wa chombo cha dola," amesema Ole Sosopi.

Amesema hata leo yakiitishwa maandamano ya nchi nzima kama polisi hawatumii nguvu kuyazuia, hayawezi kusababisha mauaji kwa kuwa mtu hafi kwa kuandamana bali kwa kusababishiwa kifo hivyo polisi wafanye uchunguzi wa kutosha.

"Anasema viongozi wa Chadema waliokuwepo pale walikuwa na silaha, kama wao ndiyo walihusika waseme ni silaha ya nani iliyotumika kwani kuna maganda yaliyookotwa? Hivyo uchunguzi ukifanyika mhusika atabainika lakini katika mkutano ule polisi ndiyo waliokuwa na silaha za kivita," amesema Ole Sosopi.

Pia wametoa wito kwa wanafunzi wote nchi nzima na wazazi kulilia damu ya Akwilina mpaka pale haki itakapotendeka, lakini pia wao wataandika barua kwa balozi zote hapa nchini kuzitaarifu kuhusu hali ya ukandamizaji wa haki za binadamu ili wachukue tahadhari wawapo hapa.

Msemaji Mkuu Wa Serikali Aelezea Miradi Ya Maendeleo Inayotekelezwa

$
0
0
YALIYOJIRI WAKATI WA MKUTANO WA MKURUGENZI IDARA YA HABARI/ MSEMAJI MKUU WA SERIKALI NA WAANDISHI WA HABARI LEO TAREHE 25 JULAI, 2018 JIJINI DODOMA

#Mkutano huu ni mwendelezo wa mikutano ya kila mwezi kati ya Msemaji Mkuu wa Serikali na wanahabari kwa lengo la kutoa mrejesho kwa umma kuhusu utekelezaji wa ahadi za Serikali.

#Nawapongeza na kuwashukuru wanahabari kwa ushirikiano mkubwa waliutoa kwa Serikali katika mwaka wa fedha 2017/2018 katika kusaidia kuhabarisha umma masuala mbalimbali ya utekelezaji wa shughuli za Serikali.

#Kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Habari na. 12, 2016 vyombo vya habari vinapaswa ,kutekeleza kazi zao kwa mujibu wa maadili ya kiwango cha juu.

# Niwakumbushe wamiliki wa magazeti kuhuisha leseni zao mwaka huu kuanzia mwezi Agosti.

# Hata hivyo tunashuhudia kuwepo kwa badhi ya vitendo vya ukiukwaji wa maadili ya taaluma hivyo pale Serikali itakapochukua hatua tusilaumiane.

*Hali ya Uchumi wa Taifa*
#Hadi kufika Machi 2017, Pato la Taifa lilikua kwa wastani wa asilimia 7.1 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 7.0 kwa mwaka 2016.

#Ukuaji huu ulitokana na utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo na kuimarika kwa shughuli mbalimbali za kiuchumi.

*Makusanyo ya Kodi Yaongezeka*
# Katika Mwaka wa Fedha 2017/2018 Serikali kupitia TRA ilifanikisha kukusanya jumla ya Shilingi Trilioni 15.5 kuanzia Julai 2017 hadi Juni 2018 ikilinganishwa na Shilingi Trilioni 14.4 ambazo zilikusanywa katika kipindi kama hicho kwa mwaka wa Fedha 2016/2017, kiasi hiki ni sawa na ukuaji wa asilimia 7.5.

#Kwa niaba ya Serikali niwapongeze watendaji wote waliosimamia hili na wananchi waliolipa kodi na tuendelee na mshikamano huu huu.

# Ninyi kama Wanahabari, tunaomba mtumie kalamu zenu na kamera zenu kufichua wale wote wanaokwepa kodi na pia kutangaza mashujaa wa kulipa kodi nchini.

*Makampuni Yaanza Kulipa Gawio na Mapato kwa Serikali*
# Kutokana na utendaji makini wa Rais Magufuli na Serikali ya Awamu ya Tano kwa ujumla hata mashirika ambayo yalikuwa hayatoi gawio kwa Serikali sasa yanatoa.

#Zaidi ya TZS Bilioni 700 zimekusanywa kama gawio na mgawo wa asilimia 15 kutoka taasisi na mashirika ya umma na binafsi 43 na taarifa za sasa ni kuwa fedha hizo zitaongezeka hadi zaidi ya bilioni 800 ikiwa ni baada ya taasisi nyingine kuhamasika na hii ni ongezeko la asilimia zaidi ya 500.

*Utekelezaji Katika Sekta Muhimu kwa Wananchi*
# Serikali imetimiza ndoto ya kuendelea kulifufua Shirika la Ndege kwa kuleta Boeing 787 Dreamliner, Ndege nyingine 2 za C Series zinakuja Novemba na Boeing nyingine 1 itawasili Januari 2020.

# Tangu ujio wa ndege hizi abiria wa ATCL wameongezeka hadi kufikia 107,207 katika mwaka 2016/2017 kutoka 49,174 mwaka 2015/2016 hii ni sawa na ongezeko la asilimia 118.

#Mwaka 2017, Serikali iliendelea kutekeleza miradi ya maji vijijini kupitia programu ya kuendeleza sekta ya maji kwa lengo la kuongeza kiwango cha upatikanaji wa maji vijijini na zaidi ya miradi 366 inaendelea kutekelezwa nchi nzima.

# Katika mwaka 2017 barabara kuu, barabara za mikoa na barabara za wilaya kwa kiwango za lami na changarawe zilikuwa na urefu wa kilometa 32,170 ikilinganishwa na kilometa 30,265 kwa mwaka 2016 sawa na ogezeko la asilimia 6.3.

#Serikali pia iliunda wakala maalumu wa kusimamia barabara za vijijini na miji midogo TARURA ambapo wameshaanza kazi na inasogeza zaidi huduma vijijini.

#Serikali inaendelea kukamilisha miradi mbalimbali ya umeme nchini, ambapo Kinyerezi 1- extension tayari mitambo imeanza kufungwa ili kuzalisha megawati 185.

Mradi wa Kinyerezi II nao wa megawati 240 mawanda yameongezeka na sasa utazalisha megawati 280 na tayari megawati 208 zimeshaingizwa katika gridi.

# Mradi ujao ni mradi mkubwa wa kihistoria, Mradi wa Stiglers wa megawati 2,100 na utekelezaji wake utaanza mwaka huu wa fedha.

# Serikali imeendelea kutekeleza agizo la kuhamia Dodoma ambapo takribani watumishi 6,400 wameshahamia.

Kwa ujumla yako mengi yanayotekelezwa na Serikali kwa kasi na tutaendelea kuyatolea ufafanuz katika vikao vijavyo.

*Imeandaliwa na Idara ya Habari- MAELEZO*

==>>Zaidi, Soma Jarida zima hapo chini

Makubaliano Sita Ya Chadema, ACT Uchaguzi Buyungu

$
0
0
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na ACT-Wazalendo, wameingia makubaliano sita katika uchaguzi mdogo wa wa ubunge wa Jimbo la Buyungu na kata 77, unaotarajiwa kufanyika Agosti 12, mwaka huu.

Makubaliano hayo yamefanyika baada ya mazungumzo na mashauriano ya viongozi wa pande zote mbili za vyama hivyo.

Katika makubaliano hayo vyama hivyo vimekubaliana kuwa ACT Wazalendo kitaiachia Chadema Jimbo la Buyungu na kushiriki kwenye kampeni na Chadema kitaiachia ACT Wazalendo Kata ya Gehandu (Hanang) na kushiriki kwenye kampeni.

Aidha, makubaliano mengine ni kwamba  Chadema kitaiunga mkono ACT Wazalendo kwenye kata ambazo ACT pekee kimegombea huku ACT Wazalendo kikiiunga mkono Chadema kwenye kata ambazo Chadema pekee kimegombea.

Makubaliano ya tano ni kwamba wagombea wa vyama vyote kwenye kata zilizosalia wataruhusiwa kuendelea na kampeni na sita ni ACT Wazalendo na Chadema vitashirikiana kukabiliana na hujuma kwenye kampeni, upigaji kura na utangazaji wa matokeo.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya July 16

Ufafanuzi wa TTCL Kuhusu Watumishi Wake Wawili Waliokamatwa na Jeshi la Polisi kwa Uhalifu

Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza atembelea Benki Kuu, JWTZ NA TAKUKURU

$
0
0
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania,  Prof. Florens Luoga amelipongeza Jeshi la Magereza kwa kuendelea kutoa mchango wake katika kudumisha hali ya ulinzi na usalama nchini kupitia majukumu yake ya uhifadhi salama wa wafungwa na utoaji wa huduma za urekebishaji kwani Amani na Usalama ni msingi wa maendeleo katika nchi yoyote duniani.
 
Prof. Luoga amesema hayo wakati wa mazungumzo katika ziara ya Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Phaustine Kasike alipotembelea Benki Kuu ya Tanzania ikiwa ni mwendelezo wa ziara zake  za kujitambulisha kwa viongozi mbalimbali wa kitaifa tangu ateulie kuwa Mkuu wa Jeshi hilo Julai13, 2018.
 
Aidha, Profesa Luoga amelishauri Jeshi la Magereza kuongeza ubunifu katika miradi ya uzalishaji mali kwa kufanya utafiti utakaoongeza ubora  wa bidhaa mbalimbali zinazozalishwa ili kuendana na mahitaji ya soko la ndani na hata nje ya nchi kwa kuwa taasisi kama magereza inaaminika.
 
“Jambo kubwa ni kubadili mtazamo na namna ya kufikiri kwa kusoma alama za nyakati na mabadiliko ya ulimwengu, kila kitu kinawezekana”. Amesisitiza Prof. Luoga.
 
Prof. Luoga ameahidi kuwa Benki Kuu ya Tanzania ipo tayari kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Magereza hasa katika ushauri wa kitaalam pale itakapohitajika kufanya hivyo ili kufikia malengo mahususi.
 
Ameongeza kuwa Taasisi anayoiongoza italipa ushirikiano Jeshi la Magereza kwa kuliunganisha na wadau mbalimbali watakaofanya kazi na Jeshi hilo kufanikisha majukumu yake pale fursa za kufanya hivyo zitakapojitokeza.
 
Wakati huo huo, Kamishna Jenerali Kasike amekutana na Uongozi wa juu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU)  ulioongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo Valentino Mlowola. 
 
Mkurugenzi Mlowola amemhakikishia Kamishna Kasike ushirikiano wa dhati kwa kuwa vyombo hivyo viwili ni miongoni mwa taasisi  zinazosimamia utekelezaji wa sheria nchini hivyo ukaribu wao katika utendaji hauepukiki.
 
“Msingi wa amani katika nchi umewekezwa katika vyombo vyetu, kwahiyo ushirikiano ni muhimu sana”. Amesema Mlowola.
 
Kamishna Jenerali Kasike yuko katika ziara ya kujitambulisha kwa viongozi mbalimbali wa kitaifa ikiwa pia ni sehemu ya kuelezea majukumu ya msingi ya Jeshi la Magereza ambayo ni pamoja na uhifadhi salama wa wahalifu na utoaji wa huduma za urekebishaji kwa wafungwa ili wawe raia wema pindi wamalizapo vifungo vyao.
 Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akisalimiana na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Flolens Luoga alipotembelea Benki Kuu ya  Tanzania katika ziara yake ya kujitambulisha kwa Viongozi waandamizi Serikalini  jana Julai 25, 2018, jijini Dar es Salaam.
 Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akiteta jambo na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Flolens Luoga(kulia) alipotembelea Benki Kuu ya Tanzania kwa lengo la kujitambulisha jana Julai 25, 2018.
 Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike akiwa na Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Luteni Jenerali Yakubu Hassan Mohamed alipomtembelea Ofsini kwake jana Julai 25, 2018 jijini Dar es Salaam. 
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU nchini, Valentino Mlowola akimkabidhi nembo ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike kama inavyoonekana katika picha alipotembelea Taasisi hiyo jana  Julai 25, 2018

Lugola Aibua Ufisadi wa Kutisha NIDA.......Aipa Siku 14 Kampuni ya Iris Ijieleze, Pia Bosi wa Zamani NIDA Katakiwa Kuripoti Ofisi Kwake

$
0
0
Na Felix Mwagara, MOHA
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola ameipa wiki mbili Kampuni ya Kimataifa ya Iris Corporation Berhard impe majibu ya kuwa italeta mtambo wa kutengeneza kadi ghafi au Dola za Marekani Milioni 14 sawa na zaidi ya shilingi bilioni 32 za Tanzania. 

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dodoma jana, mara baada ya kumaliza kikao na Menejimenti ya Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) pamoja na viongozi wa Kampuni hiyo, Waziri Lugola alisema kampuni hiyo haiwezi ikacheza na fedha za Watanzania ambao ni za walipa kodi.

Lugola aliongeza kua lazima fedha hizo au mtambo huo upatikane kwa kuwa Serikali ya Awamu ya Tano haitakubaliana na mchezo mchafu wa aina yoyote, na pia yeye kama Waziri wa Wizara hiyo anaendelea kutekeleza maagizo ya Rais Dkt John Magufuli.

“Tumezungumza nao na tumekubaliana nao kwamba tuwape wiki mbili ili bodi ya kampuni hiyo ikakae ifanye maamuzi ya aidha waturudishie fedha zetu au walete mtambo, lakini sisi kama nchi huu mtambo muhimu sana, bado tuna uhitaji, sisi tungependa baada ya hiyo wiki mbili wafanye maamuzi ya kutuletea mtambo,” alisema Lugola.

Aidha, Waziri Lugola amewataka wamiliki wa kampuni zilizolipwa kifisadi fedha za Mradi wa mtambo wa NIDA kujisalimisha jijini Dodoma Agosti 3 mwaka huu wakiwa na mtambo huo vinginevyo warejeshe fedha zilizotumika.

Pia Lugola ametoa agizo kwa aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dickson Maimu na Mfanyabiashara Jack Gotham kufika ofisini kwake Agosti 3 saa 3:00 asubuhi ili kutoa maelezo yanayojitosheleza yatakayomsaidia kutoa maamuzi sahihi kuhusiana na ufisadi wa fedha zaidi ya bilioni 32 za mtambo huo ambao hadi sasa haujafika nchini.

Lugola aliyataja kampuni hayo kuwa Gotham International ambayo imelipwa kifisadi shilingi 2,848,878,659.75, Iris Corporation Berhard ambayo imelipwa kifisadi 22,919,414,169,84, Gwiholoto Impex inayodaiwa shilingi 946,406,989,00, Sykes Travel Agent 5,979,600,00, Dk Shija Paul Rimoy 27,000,000,00, Aste Insurance 1,206,619.93, na Kampuni ya BMTL 569,192,090,00.

Hata hivyo, Waziri Lugola aliwataka Watanzania kutowahusisha viongozi wa sasa wa NIDA na ufisadi huo kwa kuwa hawahusiki hata kidogo, matukio yote ya ufisadi yamefanywa na watangulizi wao na viongozi waliopo sasa wameletwa kuiongoza Mamlaka hiyo kwa ajili ya kuboresha utendaji wa NIDA.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images