Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Serikali Kuzuia Chumvi Kutoka Nje ya Nchi Kulinda Masoko ya Ndani

$
0
0
Na Zuena Msuya-Full Shangwe
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo amesema Serikali kupitia Wizara ya Madini inaangalia namna bora ya kuimarisha soko la chumvi inayozalishwa nchini yenye uwezo wa kukidhi mahitaji ya ndani na ziada, kwa kuzuia ile inayoingizwa kutoka nchi za nje.

Nyongo alisema hayo, wilayani Bagamoyo mkoani Pwani, Julai 23, 2018, baada ya kutembelea Mgodi wa kuzalisha chumvi wa kampuni ya Stanley and Sons ulioanzishwa mwaka 1948/49 uliopo katika Kijiji cha Kitame wilayani humo.

Akizungumzia uzalishaji chumvi, Nyongo alitolea mfano mgodi pekee wa Stanley kuwa, huzalisha chumvi kati ya tani 4000 hadi 6000 kwa mwaka kulingana na hali ya hewa, licha ya kuwepo migodi mingi ya uzalishaji chumvi katika baadhi ya Mikoa nchini ambapo mara nyingi wazalishaji wamekuwa wakilalamikia ukosefu wa soko la chumvi wanayozalisha.

Alitaja baadhi ya Mikoa iliyokuwa na migodi ya kuchimba na kuzalisha chumvi kuwa ni pamoja Pwani yenye zaidi ya mgozi mmoja, Kigoma katika eneo la Uvinza, Lindi pamoja na Mtwara.

” Tanzania ina migodi mingi ya kuchimba na kuzalisha chumvi bora, ya kutosha na yenye kukidhi mahitaji ya ndani na kuuza nje, hivyo ni wakati sasa, serikali kuangalia namna bora ya kulinda soko la ndani la chumvi kwa kuzuia ile inayoingizwa kutoka nje, ili wazalishaji waweze kupata soko la uhakika”, alisisitiza Nyongo.

Aidha aliwaagiza wachimbaji na wazalishaji wa chumvi nchi, kusindika chumvi hiyo katika ubora unaotakiwa na kukidhi viwango vya soko la Kimataifa kwa kuzingatia kuwa, Tanzania inazalisha chumvi iliyobora.

Sambamba na hilo, alieleza kuwa kwakuwa chumvi ni bidhaa mtambuka inayotumika kama chakula, dawa, pamoja na kuwa ni madini hivyo, aliwataka wachimbaji na wazalishaji wa chumvi, kusindika chumvi hiyo katika ujazo tofauti na kwa bei nafuu ili kila mmoja aweze kumudu gharama za kununua chumvi hiyo kwa matumizi husika ikiwemo majumbani, viwandani na hata katika mifugo.

Pia, alisema wazalishaji wakubwa wawasaidie na kuwawezesha wafanyabiashara wadogo wa chumvi ili na wao waweze kuuza na kusambaza chumvi hiyo ili iwafikie watumiaji wa aina mbalimbali kwa urahisi zaidi na kukidhi mahitaji ya walaji kwa wakati.

” Watumiaji wengi wa chumvi majumbani wananunua na kutumia iliyosindikwa katika ile mifuko midogo ya robo au nusu kilo, sasa ninyi wachimbaji na wazalishaji wa chumvi muangalie namna ya kuwafikia watumiaji wote wa chumvi hapa nchini, hii italeta tija kwa watanzania kutangaza na kutumia bidhaa zinazozalishwa nchini”, alisema Nyongo.

Nyongo aliendelea kusisitiza kuwa, Serikali inaendelea kuunga mkono juhudi za wachimbaji na wazalishaji wa chumvi nchini kwa kuweka mazingira rafiki yanayowawezesha kufanya kazi hiyo katika kiwango kikubwa na ubora unaotakiwa.

Pamoja na mambo mengine, alisema kuwa, tayari serikali imewafutia wachimbaji na wazalishaji chumvi, kodi kumi na moja ambazo zilikuwa kero kubwa kwao, na kwamba serikali inaendelea kushughulikia vikwazo vingine vinavyokwamisha shughuli zao.

Aidha alitaja baadhi ya nchi zinazonunua chumvi ya Tanzania kuwa ni pamoja na Jamuhuri ya Watu Congo, Malawi, Msumbiji,pamoja na Uganda na kusema kuwa lengo ni kufikia nchi nyingi zaidi duniani.

Aliwaagiza wachimbaji na wazalishaji wote wa chumvi nchini kulipa mirabaha na tozo mbalimbali na kushiki katika shughuli za kijamii zilizowekwa kwa mujibu wa sheria ya madini, kwa lengo la kuongeza pato la taifa kwa manufaa ya watanzania.

Mmoja wa Wakurugenzi katika Mgodi wa Chumvi wa Kampuni ya Stanley and Sons, Richard Stanley aliiomba serikali kuboresha miundombinu ya barabara itakayorahisisha usafirishaji ya chumvi hiyo, kwa kuwa katika kipindi cha wa mvua hakuna vyombo vya usafiri vinavyoweza kufika katika eneo hilo.

Vilevile, Richard aliiomba serikali kuwapelekea huduma ya umeme katika kijiji hicho ili kupunguza gharama za uzalishaji ambapo kwa sasa hutumia mafuta mazito kuendeshea mashine za uzalishaji.

Hata hivyo, Naibu Waziri Nyongo aliwahakikisha wawekezaji hao kuwa changamoto zote zitashughulikiwa katika kipindi kifupi kijacho kwa kuwa nia ya serikali ni kuwawezesha wawekezaji wa ndani na nje waweze kufanya shughuli zao katika mazingira mazuri na rafiki ili kuunga mkono azma ya serikali ya kuwa tanzania ya viwanda kutokana na rasilimali zilizopo nchini.

Waziri Mhagama Aivunja Bodi ya NSSF

$
0
0
Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge Kazi Vijana na Ajira Jenista Mhagama ameivunja bodi ya wadhamini ya Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa kile alichodai ni kuimarisha shirika.

Waziri Jenista ametangaza kutengua uteuzi wa wajumbe wote wa bodi, wakati Akizungumza na wanahabari  leo Julai 24 2018,  jijini Dodoma ambapo amesema kuwa utaratibu wa uteuzi wa bodi mpya unafanyika.

"Kwa mujibu wa aya ya 2(1)(A) ya jedwali la Sheria ya NSSF Rais ndiye mwenye mamlaka ya uteuzi wa Mwenyekiti wa bodi hiyo, hivyo ameridhia kutenguliwa kwa uteuzi wa Mwenyekiti wa sasa wa bodi hiyo kuanzia leo," amesema Jenista.

Amesema lengo mabadiliko haya ni kuhakikisha kuwa shirika linamarishwa zaidi katika kusimamia mwenendo wa kila siku wa shirika ikiwamo kazi ya msingi ya kuongeza wanachama kukusanya michango, kulipa mafao kwa wakati na kusimamia vitega uchumi kwa uzalendo.

Utenguaji huo unakuwa ni mwendelezo wa Waziri Jenista ambaye Julai 17, 2018 alitangaza kutengua uteuzi wa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Ajira nchini (TaESA), Saneslaus Chandarua huku akitaja sababu za kumtengua mkurugenzi huyo kuwa ni pamoja na kushindwa kuunganisha watafuta kazi na waajiri, kuratibu na kuwezesha upatikanaji wa ajira ndani na nje ya nchi, kukusanya, kufanya uchambuzi na kusambaza taarifa za soko la ajira kwa wadau na umma kwa ujumla.

JWTZ Kuadhimisha Siku Ya Mashujaa Kwa Kufanya Shughuli Za Kijamii

$
0
0
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limesema kesho July 25 litatoa huduma kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii kufuatia kumbukumbu  ya siku ya Mashujaa waliopoteza uhai wakipigania Taifa.

Msemaji Mkuu wa JWTZ Makao makuu, Kanali Ramadhani Dogoli amesema kuwa Jeshi hilo (NGOME) watatoa huduma ya vipimo vya Shinikizo la Damu, Kisukari, Uchunguzi wa Kinywa na Meno ushauri nasaha na kupima VVU kwa hiari pamoja na kufanya usafi viwanja vya Mnazi mmoja ambavyo vitatumika kufanyia vipimo hivyo.

Aidha, amesema Kamandi ya Vikosi chini ya Makao Makuu vitashiriki usafi katika maeneo mbalimbali yakiwemo Hospitali ya Temeke, Zakhiem, Dar Group na masoko ya Mbagala, Temeke, Tandika.

Pia amesema vikosi hivyo vitafanya shughuli za upandaji miti katika shule ya Wailes na stendi ya mabasi ya Mbagala na Temeke.

Kwa upande wa Zanzibar Brigedia ya Nyuko watashiriki usafi katika masoko ya Mombasa, Sebuleni Majumba ya Wazee na Mwanakwerekwe.

Shughuli zote zitatembelewa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo.

Mzee Wa Miaka 71 Akutwa Na Nyaraka Bandia Za Serikali .....Akutwa Na Vyeti 240 Na Mihuri 159, RPC Ataka Waliochongewa Vyeti Na Mzee Huyo Kujisalimisha.

$
0
0
Na Dixon Busagaga ,Moshi
JESHI la Polisi mkoa wa Kilimanjaro linamshikilia mzee wa miaka 71 na watu wengine watatu baada ya kukutwa na Nyaraka  bandia za serikali  240 ambazo wamekua wakiziandaa kwa njia ya udanganyifu pamoja na Mihuri 159 na kuuzwa kwa bei ya Sh 20,000.

Nyaraka zilizo kamatwa ni pamoja na Vyeti vya kuzaliwa ,vyeti vya ndoa ,vyeti vya ubatizo,vyeti vya Kliniki na matamko ya vizazi na vifo pamoja na mihuri mbalimbali miongoni mwao ikionyesha ni ile inayotumika wakati wa usajili vizazi na vifo katika manispaa ya Moshi na Kitete mkoani Tabora.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishana Msaidizi wa Polisi,Hamisi Issa alisema vifaa vingine vilivyo kamatwa ni pamoja na Mashine moja ya kuandikia (Type Writer) na kifaa cha kuwekea namba huku akiwataja watuhumiwa kuwa ni pamoja na Athuman Selemani (71) anayetajwa kuwa aliwahi kuwa mtumishi wa serikali katika ofisi ya mkuu wa wilaya .

Wengine ni Justine Mziray (55) anayetajwa kuwa ni mtaalamu wa kuchonga mihuri,Sporah Daud anayetajwa kushiriki katika uandaaji wa nyaraka hizo kwa kuchapa maandishi kwa kutumia mashine maalumu (Type writer) na Costa Lyatuu  anayetajw kuwa mtaalamu wa kughushi sahihi.


 Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishana Msaidizi wa Polisi,Hamisi Issa akionesha baadhi ya mihuri iliyokutwa kwa mtuhumiwa huyo

  Mihuri iliyokuwa ikitumika

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Kamishana Msaidizi wa Polisi,Hamisi Issa akionesha baadhi ya mashine aliyokuwa akitumia mtuhumiwa huyo kutengenezea nyaraka bandia za serikali

Kesho Waziri Mkuu kuongoza zoezi la usafi Coco beach

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa kesho (Jumatano, Julai 25, 2018) anatarajiwa kushiriki zoezi za usafi eneo la Coco Beach pamoja na wananchi na watendaji mbalimbali.

Zoezi hilo ni utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa Juni 29 mwaka huu kwamba Watanzania wafanye usafi kwenye maeneo yao ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa ambayo huadhimishwa Julai 25, kila mwaka.

Kwa muhibu wa ratiba iliyotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, wananchi wanatakiwa wafike eneo hilo kuanzia saa 12:30 asubuhi ili waanze shughuli hiyo. Usafi huo utafanyika kuanzia kwenye eneo la wafanyabiashara wa mihogo kuelekea maeneo ya Police Officers’ Mess.

Juni 29 mwaka huu, wakati akitoa maelekezo kwenye hafla ya uzinduzi wa kituo cha polisi kinachohamishika, Waziri Mkuu alisema: “Rais Dkt Magufuli anawataka Watanzania wote waadhimishe siku hiyo ya kumbukumbu ya mashujaa kwa kufanya usafi katika maeneo yaliyo jirani na makazi yao pamoja na yale ambayo wamezikwa mashujaa ikiwa ni njia ya kuwaenzi.

Siku hiyo hiyo, Waziri Mkuu alitangaza kwamba Rais Magufuli ameagiza kwamba sh. milioni 308 zilizotengwa kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa, zitumike kuboresha miundombinu ya barabara jijini Dodoma.

Aliitaja miundombinu hiyo ni pamoja na taa za kuongezea magari katika barabara ya Kisasa na taa za barabarani kwenye barabara mpya ya kutoka Emmaus hadi African Dream yenye urefu wa kilomita 1.4, ambayo kwa sasa inajengwa kwa kiwango cha lami.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, JULAI 24, 2018.

Kamanda Mambosasa Azungumzia Polisi Waliohusishwa na Mauaji ya aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha NIT, Akwilina Akwilini

$
0
0
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema askari waliokamatwa wakihusishwa na kifo cha aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini wameachiwa huru.

Akwilina alifariki dunia Februari 16, 2018 baada ya kupigwa risasi kichwani akiwa kwenye daladala eneo la Mkwajuni jijini hapa, wakati polisi wakiwatawanya waandamanaji ambao ni wafuasi wa Chadema.

Aprili 20, 2018 Mkurugenzi wa Mashtaka  (DPP), Biswalo Mganga alisema jalada la kesi ya Akwilina amelifunga rasmi, kubainisha kuwa Jeshi la Polisi linapotumia nguvu kuzuia maandamano au vurugu na kusababisha mauaji, haliwezi kushtakiwa.

Leo Jumanne Julai 24, 2018 wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuulizwa hatima ya askari hao, Mambosasa amesema wameachiwa, “ni kweli kuna askari tulikuwa tunawashikilia kwa ajili ya uchunguzi, upelelezi ulipomalizika imebainika hawahusiki.”

“Wale askari waliachiwa kwa maelekezo ya mwanasheria na ushahidi ulikuwa hafifu wa kuwatia hatiana.”

Wafanyakazi wawili wa TTCL mbaroni kwa kuhujumu kampuni

$
0
0
Kamanda wa Polisi Kanda maalumu ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa amesema Jeshi la polisi linawashikilia watuhumiwa wawili kwa tuhuma ya kuhujumu kampuni ya mawasiliano Tanzania ya (TTCL) na kusababisha shirika hilo kupata hasara ya shilingi milioni 46 za kitanzania.

Mambosasa ametaja watuhumiwa hao kuwa ni Kelvin Siame (25) mkazi wa Tabata Segerea ambaye ni mfanyakazi wa shirika hilo kitengo cha huduma kwa wateja na mwingine ni Lilian Hosea (36), mkazi wa Mbezi Beach ambaye alikuwa ni mhasibu wote wakiwa ni wafanyakazi wa TTCL.

”Mnamo julai 12, 2018, Jeshi la polisi kanda maalumu  lilipata taarifa kutoka kwa Afisa mpelelezi kampuni ya mawasiliano ya TTCL kuwa wafanyakazi wa shirika hilo wanajihusisha na udukuzi wa data za kampuni ya TTCL kutoka Taasisi za Serikali zinazotumia mtandao huo na taasisi hizo ni UDSM, TASAF, NSSF, NHC na TRA”. amesema Mambosasa.

Ameongezea kuwa Taasisi hizo zilikuwa zikinunua data toka kampuni ya TTCL kwa ajili ya matumizi ya kila siku, lakini watumiwa hao wamekuwa wakiiba data hizo na kuwauzia watumiaji binafsi kwa manufaa yao binafsi na kusababisha shirika kupata hasara kubwa ya fedha.

Mara baada ya watuhumiwa hao kutiwa mbaroni na kufanyiwa mahojiano ya kina walikiri kuhusika na uhujumu huo kwa kuuza data kinyume na sheria.

Aidha taratibu zinafanyika ili watuhumiwa hao waweze kufikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kuwa umekamilika.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya July 25


Je Umepungukiwa Nguvu Za Kiume Na Umetumia Dawa Nyingi Bila Mafanikio?

$
0
0
Hakika nawashukuru wote mliotumia hii dawa na kunipa pongezi nyingi Sana sasa offa imeisha maana nilitoa ya wiki 2 tu     na watu wengi walioitumia wamepona kabisa 

Dawa hii ni dawa ya maajabu kabisa na huwezi kuamini ila wengi walioitumia wameiamini maana kati ya watu 89 walioitumia ndani ya wiki 2 watu76 wamepona kabisa na watu 9 hawajapona na watu 4 hawajatoa majibu! 

Dawa hii ni dawa inayotibu tatizo la upungufu wa nguvu za kiume na unapona kabisa, dawa hii ni dawa ya asili,(mitishamba) utaitumia mara moja tu na hautatumia dawa ya nguvu za kiume tena 

Dawa hii inawafaa watu kuanzia miaka 18 mpaka miaka 70, zaidi ya miaka hyo haitakusaidia ....watafiti wa dawa asilia pamoja na waganga  wameikubali pia dawa hii inawafaa hata wanawake wasiopata hisia za mapenzi 

Ukitumia hii dawa unakuwa na uwezo wa kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara 3 bila hamu kuisha, inauwezo wa ajabu na tiba bora kabisa

 SOMA DALILI HIZI;  kutokuwa na hamu ya tendo la ndoa 2 .kushindwa kurudia tendo la ndoa 3. kuwahi kufika kileleni 

Dawa hii imesaidia watu wengi sana dawa hii imegunduliwa na dr kiboko mganga wa tiba za jadi kutoka mafia pia tunatibu matatizo mbalimbali kama mambo ya biashara, nyota, kesi, mapenzi, nk, pia tunahitaji WAKALA wa kupokea dawa zetu katka nchi ya KENYA, ZAMBIA, UGANDA, mikoani tunatuma kwanjia ya mabasi au fika ofisini kwangu  Mafia kisiwani  

maelezo zaidi wasiliana na DR KIBOKO 0679923297

Mambosasa: Fateni Sheria, Mkikamatwa na Trafiki Sitaki Mnipigie Simu

$
0
0
Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi (SACP), Lazaro Mambosasa amewataka watumiaji wa vyombo vya moto kutompigia simu pindi wakamatwapo na askari wa barabarani kwa kuwa yeye ndio amewaagiza kufanya kazi hiyo.

Kamanda Mambosasa ametoa kauli hiyo jana Julai 24, 2018 wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam na kutaka kila mmoja ambaye anatumia chombo cha moto kufuata sheria zilizowekwa ili kusudi kuepukana na ajali zisizokuwa na ulazima ambazo zinapelekea vifo, ulemavu na utegemezi kwenye familia.

"Ninaomba nisipigiwe simu juu ya kwamba umekamatwa kwa kosa la usalama barabarani bali unipigie tu pale unahisi umeonewa. Kwa kuwa wengi wao wanaopigia simu wametenda makosa ninaomba nisipigiwe kwasababu mimi ndio nawatuma wawakamate", alisema Kamanda Mambosasa.

Pamoja na hayo, Kamanda Mambosasa amliendelea kwa kusema; "Jeshi la Polisi tunaendelea kuhimiza watu kufuata sheria za usalama barabarani, makosa haya yanafanya watu walalamike kwamba wanakamatwa sana lakini cha ajabu watu wanaendelea kutenda makosa sana. Bodaboda bado ni tatizo tunawashuhudia kwenye vivuko 'zebra cross' lakini hata matumizi ya barabara ya mwendokasi wanavamia na kufanya wanavyotaka".

Kauli hiyo ya Mambosasa imekuja baada ya kuwepo kwa madereva wa vyombo hivyo kufanya makosa ya barabarani kwa makusudi kwa kujua yupo mtetezi wao ambaye ataweza kuwasaidia mara wanapokuwa wamesimamishwa na kukamatwa barabarani.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam kupitia Kikosi chake  cha Usalama barabarani kuanzia Juni 01 hadi Juni 3 mwaka huu  wamefanikiwa kukamata jumla ya magari 42,488 na pikipiki 1,941 kutokana na makosa 73 ya usalama barabarani na kuingizia mapato Jeshi la Polisi takribani shilingi Bilioni 2.15 kama tozo zitokanazo na madereva kukiuka sheria za usalama barabarani.

TFF yaipa Simba siku 75 ifanye uchaguzi Mkuu

$
0
0
Rais wa shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia, ameitaka klabu ya simba kufanya uchaguzi wao ndani ya siku 75.
 
Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya shirikisho hilo, alisema kwamba kamati ya Uchaguzi ya TFF, wamemfikishia taarifa kwamba Simba wanatakiwa kufanya uchaguzi wao mkuu.
 
"Kawaida huwa ni 60 na ndivyo ninavyojua mimi, lakini Kamati ya Uchaguzi imewapa siku 75 nazani siku 15 ni za maandalizi, wanatakiwa wafanye uchaguzi wao mzima ili kupata viongozi wao," alisema.
 
Mabingwa wa Ligi Kuu Bara, Simba wapo nchini Uturuki wakiendelea na mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu Bara.
 
Simba imefikia katika hoteli ya The Green Park Kartepe Resort and Spa iliyopo katika jiji wa Istanbul Uturuki na watakuwa hapo kwa muda wa siku 16 na watarudi nchini Agosti 5 siku tatu kabla ya siku ya Simba (Simba Day).
 
Kocha msaidizi wa Simba, Mrundi Masoud Djuma alisema hali ya hewa, viwanja na mahala walipofikia ni sehemu sahihi ya kufanya maandalizi ambayo wataitumia vizuri kama walivyopanga.
 
Djuma alisema mazingira ya hoteli waliyofikia ni nzuri, viwanja vinakizi kufanya mazoezi magumu na mepesi au programu yoyote ambayo benchi la ufundi tutakuwa tunahitaji kufanya kulingana na mahitaji yetu ya siku.

Kalulumila:Dawa Bora ya Nguvu za Kiume na Maumbile Madogo

$
0
0
 BORA YA NGUVU ZA KIUME NA MAUMBILE MADOGO KALULUMILA.
----------------------------------------
Ni dawa pekee iliyojipatia umaarufu nchini na nje ya nchi kwa kufanya kazi mara 3, kwa wakati mmoja 1, kurefusha uume na kunenepesha saizi uipendayo kuongeza nguvu za kiume na inatibu matatizo na gerentii miaka 30. Na kuendelea haina madhara, inaimarisha mishipa ya uume iliyoregea na udhalishaji wa mbegu za kiume. 


---------NINI HUCHANGIA MATATIZO HAYA--Ngiri ni chanzo kikubwa cha matatizo haya ili kujua kwamba una ngiri ni chanzo kikubwa cha matatizo haya, ili kujua kama unangiri dalili zake ni kufika haraka kileleni wakati wa tendo la ndoa, 2)kushindwa kurudia tendo la ndoa. 3)kutoa choo kama cha mbuzi. 4)tumbo kujaa gesi na kuunguruma. 5)kukosa choo kabisa. 6)maumbile kuingia ndani na kuwa mafupi. 7) korodani moja kuvimba 8)kutosikia hamu ya tendo la ndoa na maumivu ya kiuno wakati wa tendo la ndoa. 9)maumivu ya kiuno na mgongo pia tunatibu kisukari kwa siku7, presha, busha, bila kupasuliwa na magonjwa mbalimbali. 

---------------------------------------
TUPO TEGETA KWA NDEVU KARIBU NA MACHINJIO YA NGOMBE UTAONA OFSI IMEANDIKWA KALULUMILA HERBALIST CLINIC HOSPITAL SIMU .
----------------------------------------
-0655-557-182.
-0755-557182.
-0784-557-182.
PIA UTAWEZA KULETEWA POPOTE ULIPO.
---------------------------------------
KARIBUNI SANA.
----------------------------------------

Uongozi Yanga Waweka Hadharani Viingilio Vya Mchezo Dhidi Ya Gor Mahia

$
0
0
Uongozi wa klabu Yanga umetangaza viingilio vya mchezo wa mkondo wa pili dhidi ya Gor Mahia FC utakaopigwa Uwanja wa Taifa, Julai 29 2018.

Kueleka mchezo huo wa Kombe la Shirikisho Afrika, Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, amesema kuwa kiingilio cha chini kabisa kitakuwa ni shilingi 3000 pekee ambacho ni kwa jukwaa la mzunguko.

Katika jukwaa la VIP A kiingilio kitakuwa ni Tshs 10,000 huku VIP B na C kikiwa ni 7,000 pekee.

Yanga inaenda kucheza mchezo huo ikiwa inashika mkia kunako kundi D ikiwa na alama moja pekee iliyoipata baada ya suluhu tasa dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda katika mechi iliyopigwa Uwanja wa Taifa Dar.

Yanga inakutana na Gor Mahia ambayo iliwapa kichapo cha maana kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza jijini Nairobi kwenye Uwanja wa Moi Kasarani wa jumla ya mabao 4-0.

Yanga yafanya uteuzi mrithi wa Clement Sanga

$
0
0
Mara baada ya aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Young Africans, Clement Sanga  kujiuzulu, Kamati ya Utendaji kwa kushirikiana na Bodi ya Wadhamini wamefanya kikao cha dharula na kumteua kiongozi mwingine atakayeshikilia nafasi hiyo iliyoachwa wazi.

Katika taarifa iliyotolewa jana na Afisa habari Yanga, Dismas Ten amesema Kamati ya Utendaji pamoja na Bodi ya Udhamini imemteua Omary Kaya kuwa Kaimu Katibu Mkuu kwa kipindi hiki cha mpito ili kuweza kurudisha utendaji wa kazi na shughuli za kila siku kwenye klabu.

Aidha amesema zipo nafasi kadhaa ambazo zipo wazi, Kamati ya Utendaji na Bodi ya Udhamini inaendelea kushughulikia taratibu husika za nafasi hizo na muda mfupi ujao itawekwa wazi nani atashika nafasi hizo.

Kamishna Jenerali Jeshi La Magereza Afanya Mabadiliko Ya Kiungozi Kwa Wakuu Wa Mikoa Na Vituo

$
0
0
Kamishna Jenerali wa Jeshi  la Magereza nchini, Phaustine Martin Kasike (pichani)  amefanya mabadiliko madogo ya kiuongozi kwa Wakuu wa Magereza wa Mikoa na Vituo vingine vya Magereza nchini.

Mabadiliko hayo ni pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma, Naibu Kamishna wa Magereza(DCP), Julius Sang’udi amehamishiwa Makao Makuu ya Magereza kuwa Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Wafungwa na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Singida Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza(SACP), Salum Hussein.

Aliyekuwa Mkuu wa Gereza Mtego wa Simba, Kamishna Msaidizi wa Magereza(ACP), Msepwa Omary amehamishiwa Magereza Mkoa wa Singida kuwa Kaimu Mkuu wa Magereza mkoa huo na nafasi yake inakaimiwa na Mrakibu wa Magereza, Muta Tibalinda.

Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga, Naibu Kamishna wa Magereza (DCP), John Masunga amehamishiwa Makao Makuu ya Magereza kuwa Mkuu wa Kitengo cha Viwanda vya Jeshi la Magereza, na nafasi yake imekaimishwa kwa aliyekuwa Mnadhimu wa Magereza Mkoani Tanga, Kamishna Msaidizi wa Magereza(ACP), Emmanuel Lwinga.

Wengine ni aliyekuwa Boharia Mkuu wa Magereza, Naibu Kamishna wa Magereza (DCP), Afwilile Mwakijungu amehamishiwa Makao Makuu ya Magereza kuwa Mdhibiti Mkuu wa Shirika la Magereza na nafasi yake inachukuliwa na aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mara, Kamishna Msaidizi wa Magereza(ACP), Goleha Masunzu. Pia aliyekuwa Afisa Mwandamizi sehemu ya Utawala Magereza Mkoani Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Magereza (ACP), Benezeth Bisibe anakwenda kuwa Kaimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mara.

Aliyekuwa Naibu Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCTA), anayeshughulikia Taaluma, Utafiti na Ushauri, Kamishna Msaidizi wa Magereza(ACP), Joel Matani anakuwa Mkuu wa chuo hicho na nafasi yake inachukuliwa na Mrakibu Mwandamizi wa Magereza (SSP), Wilington Kahumuza ambaye alikuwa Naibu Mkuu wa Chuo hicho akishughulikia Manunuzi, Fedha na Utawala na nafasi yake inachukuliwa na Mrakibu Mwandamizi wa Magereza(SSP), Ahmad Seleman.

Wakati huo huo, Kamishna Jenerali wa Magereza amemteua Mrakibu wa Magereza (SP), Amina Kavirondo kuwa Msemaji Mkuu wa Jeshi la Magereza. Mabadiliko haya yanalenga kuboresha utendaji kazi ndani ya Jeshi la Magereza ili kuongeza ufanisi.

Imesainiwa na;
Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Lucas Mboje – Ofisa Habari,
Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,
DAR ES SALAAM,


Makamu Wa Rais Awaonya Watanzania Kutokufuru Uumbaji wa Mwenyezi Mungu

$
0
0
Na Daniel Mwambene, Afisa Habari Ileje
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan   amewaonya Watanzania kutokufuru uumbaji wa Mwenyezi Mungu kwa kuharibu mazingira ili kuendelea kulinda ikolojia.

Akizungumza na wananchi wa wilaya ya Ileje mkoani Songwe katika kijiji cha Sange mara baada ya kuzindua shamba la miti la Iyondo-Mswima katika eneo la Katengele Mhe. Suluhu alisema kuwa kuharibu mazingira ni kumkufuru Mungu.

“Kuharibu alichokileta Mungu kiwafae wanadamu huku mkiwa mnaenda misikitini na makanisani ni kumkufuru yeye”alisema kiongozi huyo. 

Alisikitishwa na shughuli za binadamu katika baadhi ya maeneo aliyoyapitia ndani ya wilaya ya Ileje ambako kilimo kinaendeshwa kando ya mito bila kujali sheria zinazolinda mito.

Mhe.Suluhu alisema kuwa iwapo sheria hizo hazitazingatiwa iko hatari ya milima mingi kubaki vipara kwani kinachofanyika si ukataji miti kwa malengo ya kutunza akiba bali ni unyoaji wa miti. 

Aliongeza kuwa kamwe kilimo kisiwe kisingizio cha kuharibu mazingira kwakuwa uharibifu wa mtu mmoja huleta madhara kwa wengi.

Awali kabla ya mkutano huo,Makamu wa Rais alizindua shamba la miti ambalo linaongeza idadi ya mashamba ya serikali huku likitarajiwa kutumia mamilioni ya pesa ambayo matokeo yake yataongeza ukubwa wa jina la Ileje kitaifa na kimataifa.

Akitoa taarifa Mkuu wa Wilaya ya Ileje Ndugu Joseph Mkude alisema kuwa wananchi wake ambao kwa asili ni wachapa kazi wamekuwa wakiitikia maagizo ya serikali vizuri ingawa wameonekana kufanya vibaya kwa kujiingiza katika imani za waganga wa jadi wajulikanao kama rambaramba. 

Viongozi wengine wa wilaya hiyo wakiwemo machifu,wachungaji na vyama vya siasa ngazi ya mkoa wa Songwe waliiomba serikali kuendelea kutatua kero ya miundo mbinu ya barabra ili kuwaongezea kasi ya maendeleo wananchi ambao kwa sasa wanashuhudia ujenzi wa barabara ya Mpemba-Momba hadi Isongole-Ileje kwa kiwango cha lami.

Dar es Salaam na Pwani Kukosa Maji Leo

$
0
0
Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASCO) linawaarifu wateja wake wote kuwa kutakuwa katizo la maji kwa siku ya  leo Jumatano , Julai 25, 2018 kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 2 usiku.

Taarifa kutoka shirika hilo zinadai kuwa sababu ya katizo hilo ni kupisha matengenezo ya transfoma katika mtambo.


Polisi Mkoani Mbeya Wanamshikilia Mtu Mmoja Kwa Tuhuma Za Ujangili

$
0
0
Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya limefanikiwa kumkamata mtu mmoja anayetuhumiwa kwa ujangili akiwa na nyara za serikali. 

Mtuhumiwa huyo aliyetambulika kwa jina la Edson Mwakalenga (43) Mkazi wa Lualaje Wilayani Chunya, alikamatwa Julai 20 mwaka huu akiwa na Pembe  mbili za Ndovu, Mkia wa Tandala na Gobole pamoja na kipande cha ngozi ya Tandala. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei (pichani) amethibisha kutokea kwa tukio hilo.

DC Hapi Amtumbua Mwanasheria wa Manispaa ya Kinondoni

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ali Hapi amemsimamisha kazi mwanasheria wa manispaa ya Kinondoni, Anord Kinyaiya.

Kinyaiya amesimamishwa kazi jana Jumanne Julai 24, 2018 kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwakumbatia watu wanaolalamikiwa na wananchi.

Hapi amechukua uamuzi huo baada ya wananchi kutoa kero zao katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kinondoni Shamba, wakiwemo wafanyakazi 13 wa kampuni ya kuzoa taka ya Total West Solution walioeleza jinsi wanavyozungushwa kulipwa kiasi cha Sh15milioni wanazodai.

Mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo,  Ridhiwan Hussen amesema waliwasilisha malalamiko yao kwa mkuu huyo wa wilaya na kutakiwa kwenda kwa mwanasheria huyo ili wapitie madeni wanayoidai kampuni hiyo.

Amedai walipofika kwa Kinyaiya aliwazungusha na kuwatamkia wazi kuwa Hapi hana mamlaka ya kushughulikia suala lao.

“Binafsi ninadai mshahara wa miezi 11, watu wote 13 tunadai Sh15milioni,  hata tunapokwenda ofisini kwa mwanasheria, meneja wa kampuni nae hatokei na wamekuwa na utaratibu wa kuwasiliana wao wenyewe, kwa kweli inatupa shaka sana,” alisema Hussein.

Alisema anashangazwa na Kinyaiya kuwapendelea  wenye fedha badala ya wananchi wanyonge wanaodai haki yao.

“Ninakusimamisha kazi na sitaki kukuona katika ofisi yangu. Ninataka wakuchunguze hayo mambo unayolalamikiwa na ikibainika utachukuliwa hatua za kisheria,” alisema Hapi.

“Polisi mkamateni huyu meneja popote atakapokuwepo na awekwe ndani kwa saa 48 na baadaye achukuliwe hatua za kisheria ili awalipe vijana hawa mishahara yao.”

CHADEMA Kukata Rufaa Kamati ya Taifa ya maadili

$
0
0
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinajipanga kuwasilisha malalamiko yake katika kamati ya Taifa ya maadili kutokana na kutoridhishwa na  sababu za kuondolewa kwa baadhi ya wagombea wao.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Jumanne Julai 24, 2018 mkurugenzi wa uchaguzi wa Chadema, Reginald Munisi alisema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeshindwa kutoa sababu za kuondolewa kwa wagombea wa chama hicho katika kata tano za mjini Tunduma na kata ya Gangilonga manispaa ya Iringa.

“Tutapeleka malalamiko yetu katika chombo hicho na tusipopata msaada tutakwenda kamati ya maadili ya rufaa kabla ya kwenda mahakamani,” alisema.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images