Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Mama Kanumba: Gabo Amefanikiwa Kuziba Pengo La Kanumba

0
0
Mama mzazi wa aliyekuwa Muigizaji wa filamu maarufu zaidi Tanzania, Steven Kanumba amesema kuwa kwa sasa Watanzania wasiwe na hofu tena kwani anaamini kuna vipaji vikubwa kama alivyokuwa marehemu mtoto wake.

Akizungumza na Wasafi TV kwenye usiku wa uzinduzi wa filamu ya SUMU Mlimani City  Julai 21, 2018. Mama Kanumba amemtaja Muigizaji wa Kiume Gabo Zigamba kama ndiye msanii pekee mwenye uwezo sawa na Kanumba kwa sasa.

Akizungumzia uwezo wa Gabo Mama Kanumba amesema kuwa “Gabo anajitahidi kwa kweli, nilichogundua kwanza anajua kuuvaa uhusika kwenye filamu zake, akiwa kama mlinzi anakuwa mlinzi kweli, akiwa kichaa anakuwa kichaa kweli. Namwambia asikate tamaa kuna watu watamkatisha tamaa kila atapokaribia kuyafikia mafanikio zaidi.”

Akifananisha uwezo wa Gabo na marehemu Kanumba, Mama Kanumba amesema “ni kweli Gabo ‘anashika kijiti cha Kanumba’ anajitahidi, anauthubutu, anajaribu, anajituma na anaweza”.

Marehemu Kanumba anatajwa kuwa ni moja ya Waigizaji bora wa muda wote kuwahi kutokea kwenye tasnia ya filamu nchini Tanzania.

Watuhumiwa Watano wahukumiwa kunyongwa Hadi Kufa Kesi ya Bilionea Msuya

0
0
Mahakama Kuu ya Tanzania imewahukumu kunyongwa hadi kufa washitakiwa watano baada ya kuwatia hatiani kwa kumuua kwa makusudi mfanyabiashara wa Arusha na Mirerani, Erasto Msuya.

Waliohukumiwa adhabu hiyo ni mshitakiwa wa kwanza, Sharifu Mohamed; mshitakiwa wa tatu, Mussa Mangu; wa tano, Karim Kuhundwa; wa sita Sadick Mohamed na wa saba; Ally Mussa Majeshi.

Hukumu hiyo imetolewa leo Julai 23, 2018 na Jaji Salma Maghimbi aliyesikiliza kesi hiyo.

Pia, Mahakama imemwachia huru mshitakiwa wa pili, Shwaibu Jumanne baada ya kukosekana ushahidi dhidi yake.

Rais John Magufuli na Waziri Mkuu wa Korea Kusini, Lee Nak-Yok Watia Saini Ujenzi wa Daraja la Salender

0
0
Rais Dkt. John Magufuli amesema kuwa daraja jipya la Salenda, litakuwa ni ukurasa mpya wa kutengeneza mandhari ya jiji la Dar es salaam kutokana na muonekane wake litapomalizika kujengwa.

Rais Magufuli amesema hayo leo  wakati wa zoezi la utiaji saini kati ya wakala wa barabara  Tanzania (TANROADS) na mkandarasi aliyeshinda zabuni ya ujenzi wa daraja hilo kutoka nchini Korea.

Ujenzi wa daraja hilo eneo la Coco Beach hadi Aga Khan unatarajiwa kufanyika kwa miezi 36.

Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Patrick Mfugale amesema mradi huo umelenga kupunguza foleni jijini Dar es Salaam.

Utiaji saini ulishuhudiwa na Rais John Magufuli na Waziri Mkuu wa Korea Kusini, Lee Nak-Yok aliye nchini kwa ziara ya kiserikali.

Mfugale amesema daraja hilo litagharimu Dola milioni 126.26 za Marekani. Amesema Tanzania imechangia asilimia 17.2 na Korea Kusini asilimia 82.2.

Amesema daraja hilo litakuwa na uwezo wa kubeba tani 180 kwa wakati mmoja na magari 55,000 kwa siku moja.

Rais Magufuli Amwagiza Mweka Hazina Kuyafuta Mashirika Yasiyotoa Gawio Serikalini

0
0
Rais John Magufuli amemwagiza Msajili wa Hazina, Dk Athuman Mbuttuka kubadilisha uongozi au kufuta kampuni, wakala, taasisi na mashirika ya umma ambayo yatashindwa kutoa gawio kwa Serikali.

Ameyasema hayo leo Julai 23, 2018 katika Ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere wakati akipokea gawio la Sh736.36 bilioni kwa mwaka 2017/18 kutoka kwa kampuni 43 kati ya 90 ambazo zinastahili kulipa gawio serikalini.

“Halipendwi shirika, inapendwa pesa tunachotaka ni gawio na si vinginevyo. Hatutaki kuwa na kitu ambacho hakishiriki kujenga uchumi wa nchi hii, nakuagiza msajili wa Hazina (Mbuttuka) hakikisha mashirika na taasisi zote zenye kutoa gawio kwa Serikali zinafanya hivyo,” amesema Rais Magufuli

Aidha ameyapongeza mashirika ambayo hayakuwahi kutoa gawio awali na mwaka huu yamejitokeza na kuchangia katika pato la Serikali yakiwemo yale ya UTT, DSE na Kadico.

Hata hivyo, ameonya kuwa bado kuna kampuni nyingi zinazalisha kiasi kidogo ikilinganishwa na kile kilichowekezwa na Serikali, hivyo kuwataka viongozi wa kampuni hizo kujitathmini.

Pia, Rais Magufuli ametoa wito kwa kampuni za Serikali kuhakikisha zinatekeleza majukumu ipasavyo ili kuondoa mianya ya rushwa na upotevu.

“Wakati mwingine tunaliwa kutokana na uzembe wa watendaji wetu, wanakaa pale wanakuwa sehemu ya kuwaumiza Watanzania badala ya kutekeleza majukumu yao. Nawaagiza wenyeviti wa bodi na watendaji wa Serikali mkalisimamie hili. Nataka kuona matrilioni na si mabilioni kama nilivyoona mwaka huu,” amesema Rais Magufuli.

Mawaziri Wakuu Wa Tanzania Na Jamhuri Ya Korea Wahutubia Kongamano La Pili La Biashara Na Uwekezaji Kati Ya Tanzania Na Korea – Jijini Dar Es Salaam

0
0
*Aalika wawekezaji kwenye viwanda vya kuongeza thamani ya mazao

*Ataka waangalie fursa za uwekezaji zilizopo kwenye sekta ya utalii

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaalika wafanyabiashara kutoka Korea Kusini waanzishe miradi ya uwekezaji kwenye sekta ya viwanda kwa kushirikiana na wawekezaji wa ndani.

Ametoa mwaliko huo leo (Jumatatu, Julai 23, 2018) akiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Korea, Lee Nak-yon wakati akifungua Kongamano la Pili la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Korea lililofanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Kongamano la kwanza lilifanyika jijini Seoul, Februari 2018.

 Amesema Serikali inahamasisha uwekezaji katika ujenzi wa viwanda vinavyotumia rasilimali za ndani ambavyo vitasaidia kuongeza thamani kwenye mazao ya kilimo, misitu, madini na bahari.

 “Tunakaribisha uwekezaji wa viwanda katika maeneo ya uanzishaji wa viwanda vya kuzalisha bidhaa za walaji (consumer goods), pamoja na viwanda vya kuunganisha bidhaa mbalimbali, yaani (assembling plants) kama vile magari, simu na majokofu,” amesema.

 Waziri Mkuu pia aliwaalika wafanyabiashara kutoka Korea waliohudhuria kongamano hilo waje kuwekeza kwenye sekta ya utalii ambako alisema kuna vivutio vya mbuga za wanyama kama Serengeti, Mlima Kilimanjaro, Olduvai Gorge na fukwe za bahari za Tanzania bara na Zanzibar.

 “Tanzania ina kilometa 1,200 za fukwe kuanzia Tanga hadi Mtwara, ziko pia fukwe za Zanzibar, ziko fukwe kwenye maziwa yetu ya Victoria, Tanganyika na Nyasa ambazo ni kivutio kingine cha utalii,” amesema.

 Amesema ili kusimamia matumizi ya fukwe hizo, Serikali inakamilisha uundaji wa Mamlaka ya Usimamizi wa Fukwe kama ilivyo ile ya Ngorongoro ambayo alisema taratibu zikikamilika, itaanza kazi hivi karibuni.

 Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa Korea Kusini, Lee Nak-yon aliwapongeza viongozi wa Serikali ya Tanzania kwa kufanikisha mageuzi ya kiuchumi hadi kuiwezesha nchi hii kuwa mojawapo ya nchi 10 duniani ambazo uchumi wake unakua kwa haraka.

 “Mapema mwaka huu, Benki ya Dunia imeitambua Tanzania na kuitangaza kuwa ni miongoni mwa nchi 10 ambazo uchumi wake unakua kwa haraka duniani. Nitumie nafasi hii kuwapongeza viongozi wa Serikali hii pamoja na wafanyabiashara na wajasiriamali wa nchi hii,” alisema.

 Alitumia fursa hiyo kuwaeleza wafanyabiashara na wenye makampuni kutoka Korea ambao wanashiriki kongamano hilo kwamba amepokea maombi kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli ambaye ameyaalika makampuni ya Kikorea yashiriki kwenye miradi mikubwa ya uwekezaji.

 “Ukiondoa mradi wa ujenzi wa daraja la Salender ambao mkataba wake umesainiwa leo, Rais Magufuli ameomba makampuni ya Kikorea yashiriki kwenye miradi mikubwa ya kiuchumi na hivi karibuni, taratibu zikikamilika, kuna kampuni moja itasaini mkataba wa kujenga meli kubwa kwenye Ziwa Victoria, na siyo huko tu, hata kwenye Ziwa Tanganyika,” alisema.

 Alieleza kuridhishwa kwake na ujenzi unaofanywa kwenye miradi ya kituo cha data cha NIDA (Kibaha) na mradi wa kuboresha huduma ya mama na mtoto katika hospitali ya Mnazi Mmoja ambayo aliitembelea jana jioni.

 Waziri Mkuu wa Korea Kusini anatarajiwa kuondoka nchini leo jioni (Julai 23, 2018).

Waziri Mkuu Wa Korea Amaliza Ziara Nchini

0
0
WAZIRI MKUU wa Jamhuri ya Korea, Lee Nak-yon amemaliza ziara yake ya kiserikali ya siku tatu hapa nchini na kusindikizwa na mwenyeji wake, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Waziri Mkuu huyo wa Korea ambaye ameondoka leo (Jumatatu, Julai 23, 2018) saa 9.14 alasiri, ameelekea Oman ambako atakuwa na ziara ya kikazi ya siku mbili. Aliwasili nchini juzi akitokea Kenya ambako pia alikuwa na ziara ya siku mbili.

 Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius  Nyerere, Waziri Mkuu wa Korea Kusini alisindikizwa pia na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dk. Augustine Mahiga, Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Eng. Stella Manyanya na viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam

 Kabla ya kuondoka alishuhudia burudani kutoka vikundi vya ngoma na matarumbeta uwanjani hapo.

 Mara baada ya mgeni wake kuondoka, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alizungumza na wasanii waliokuwepo uwanjani na kuwapongeza kwa kujitokeza kutoa burudani kila wakati wageni wanapoitembelea Tanzania.

 “Tunawashukuru sana wasanii kwa sababu mlikuja wakati wa mapokezi ya mgeni wetu na sasa mmekuja tena kumsindikiza. Mgeni wetu amefurahia sana ngoma zetu na amesema atarudi tena Tanzania.”

 “Kwa niaba ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Serikali kwa ujumla, tunatambua kuwa mnajitoa muda wenu kila mnapokuja kupokea na kusindikiza wageni ili kuweka sura nzuri ya Taifa letu wakati wa kupokea wageni wetu, tunawashukuru sana,” amesema.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, JULAI 23, 2018.

Makonda Ampongeza Rais Magufuli Kufanikisha Hatua Za Kuanza Kwa Ujenzi Wa Daraja La Salender

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Paul Makonda amempongeza Rais Dkt,John Magufuli  kwa kufanikisha zoezi la utiaji saini baina ya serikali ya Tanzania na Korea Kusini.
 
Mh. Makonda ametoa pongezi hizo kupitia andiko lake alilolitoa saa chache mara baada ya zoezi hilo kukamilika ambalo liko hapo chini.
 
"Kwa niaba ya Wananchi wa Mkoa wa Dar es salaam napenda kumpongeza Rais wetu Mpendwa Dkt. John Magufuli kwa kufanikisha utilianaji saini Baina ya Serikali ya Tanzania na Korea Kusini kuashiria kuanza kwa ujenzi wa Daraja la Salender litakaloanzia Coco Beach hadi Agha Khan hospital kupitia bahari ya Hindi ambalo litasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo la msongamano wa magari lililokuwa likipelekea upotevu wa mabilioni ya shilingi.
 
"Rais Dkt. John Magufuli ameamua kutujengea Daraja hili la kisasa baada ya kujionea adha ya foleni inayowasumbua watumiaji wa Daraja lililopo sasa ambalo kimsingi ni finyu na haliwezi kumudu idadi kubwa ya magari yaliyopo sasa.
 
Mbali na *kupunguza foleni ujenzi wa daraja hili la kisasa litasaidia kuboresha mandhari ya Jiji letu la Dar es salaam huku wananchi tukiombwa kuendelea kutoa ushirikiano wakati wote wa ujenzi na kuendelea kuweka jiji letu safi kwani mji wetu Ndio kitovu cha biashara na uchumi wa taifa letu.
 
Ujenzi wa *Daraja la Salender utagharimu zaidi ya Shilingi Billion 250 ambapo itachukuwa muda wa miezi 36 hadi kukamilika na litakuwa na urefu wa Km 1.03 kwa upande wa baharini huku likiwa na uwezo wa kuhimili zaidi ya Tani 180 kwa wakati mmoja na magari zaidi ya 55,000 kwa siku.
HAKIKA HUU NDIO UTEKELEZAJI WA YALE ULIYOWAAHIDI WANANCHI KUPITIA ILANI YA CCM."

Mkapa Kumwakilisha Rais Magufuli Katika Hafla Ya Maadhimisho Ya Miaka 50 Ya Frelimo

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Magufuli amemteua Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa kumuwakilisha katika maadhimisho ya miaka 50 ya mkutano wa pili wa chama tawala cha Msumbiji (FRELIMO) .

Maadhimisho hayo yatafanyika tarehe 25, Julai katika jimbo la Niassa ambapo kutokana na majukumu mengine ya kitaifa Rais amemuagiza Mkapa kumuwakilisha ambaye ataongozana na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (Bara), Philip Mangula.

Kupitia taarifa iliyotolewa leo na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, imesema kuwa Mkapa na ujumbe wake wanatarajia kuondoka nchini tarehe 24 Julai, 2018 na kurejea tarehe 26 Julai, 2018.

“Rais wa Jamhuri ya Msumbiji, Mhe. Filipe Nyusi alimwalika Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kushiriki maadhimisho hayo. Kutokana na majukumu mengine ya kitaifa Mhe. Rais Magufuli hatoweza kushiriki”, imesema taarifa.

Aidha taarifa imeongeza kuwa Tanzania na Msumbiji zimeendelea kushirikiana katika masuala ya kiuchumi na biashara kwa kuzingatia ujirani na muingiliano mkubwa wa wananchi wa nchi hizi mbili, hususani katika Mikoa ya Ruvuma na Mtwara kwa upande wa Tanzania, na Majimbo ya Niassa na Cabo Delgado kwa upande wa Msumbiji.

Afisa aliyeshtakiwa kwa kumiliki magari 19 alianza kazi TRA akiwa nayo

0
0
Afisa Mchunguzi wa TRA, Tumaini Fadhir ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa Ofisa Msaidizi wa Forodha wa mamlaka hiyo, Jennifer Mushi anayekabiliwa na kesi ya kumiliki magari 19 yenye thamani ya Shilingi Milioni 197 aliajiriwa TRA na mali zake.

Afisa huyo ameyaeleza hayo wakati akiongozwa na wakili wa Jennifer, Fulgence Masawe kutoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Katika ushahidi wake, Fadhiri amedai yeye ni mchunguzi wa ndani wa TRA, huku majukumu yake ni kufanya uchunguzi wa malalamiko yote na kuhakiki mali za watumishi ili kudhibiti vitendo vya rushwa.

Fadhiri alipoulizwa na wakili Masawe kwamba anamfahamu Jennifer, alijibu kuwa anamfahamu kwa sababu aliwahi kumchunguza.

Pia aliulizwa kama anafamu idadi ya mali za Jennifer na thamani yake , Tumaini alijibu anafahamu.

Pia aliulizwa Jennifer alianza kazi lini TRA, alijibu kuwa tangu mwaka 2010, lakini awali aliajiriwa katika sekta binafsi.

Pia alipoulizwa kama Jennifer aliajiriwa TRA akiwa na mali zake, Fadhir alijibu ndio.

Pia alipoulizwa ametumia mfumo gani kubaini idadi ya magari ya Jennifer, amedai kuwa alitumia mfumo wa usajili wa magari lakini hajawahi kuyaona kwa macho.

Naye wakili wa serikali Peter Vitalis alimuuliza Fadhiri ni mali gani ambazo Jennifer anamiliki, amedai kuwa ni zaidi ya magari 10 na waliyabaini kwa sababu alishindwa kuorodhesha vitu hivyo.

Baada ya kutolewa ushahidi huo, Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi August 16,2018.

Mushi anakabiliwa na kosa la kumiliki magari 19 ambayo anadaiwa aliyaingiza nchini kutokea Japan yakiwa na thamani ya shilingi Milioni 197,601, 207.

Lema awaomba wakazi Arusha Kuipiga chini CCM na Kuchagua CHADEMA

0
0
Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amewataka wakazi wa Arusha, kuonesha hasira zao za kuwa na maisha magumu kwa kuwachagua wagombea wa udiwani wa Chadema.

Akizungumza jana katika uzinduzi wa kampeni katika Kata ya Daraja Mbili, Lema alisema Chadema inaingia katika uchaguzi mdogo ili kuonyesha majaribu ambayo Taifa linapita kwa sasa licha ya hofu kutawala . 

"Katika uchaguzi huu, hatupambani na (Prosper) Msofe (mgombea wa udiwani wa CCM) ambaye alikuwa diwani wetu na tulipambana na damu kumwagika ili awe diwani lakini amejiuzulu na kujiunga na CCM, sisi tunapambana kwa ajili ya maisha ya Watanzania," alisema Lema

Alisema hivi sasa hali ya maisha ni ngumu, biashara nyingi zimefungwa, migodi imefungwa na maisha ni magumu na hakuna sehemu ya kuonyesha hasira hizo zaidi ya kutowapigia kura CCM.

"Hivi sasa akina dada warembo wanakunywa konyagi ukiwauliza vipi wanasema eti wanapunguza mafuta mwilini, lakini hapana, tatizo hali ni ngumu ya maisha," alisema

Hata hivyo, alisema tatizo kubwa la Watanzania ni woga, hawataki kusimama na kutetea ukweli jambo ambalo madhara yake yataendelea kuwa makubwa.

Aliwaomba wakazi wa Kata ya Daraja Mbili, kumpigia kura mgombea wa Chadema, Masudi Sungwa ili aendelee kuwasaidia kutatua kero zao.

Kwa upande wake,  Masudi Sungwa aliomba kura kwa wakazi wa kata hiyo na kueleza kero zao atazishughulikia vyema akishirikiana na baraza la madiwani wa Jiji la Arusha ambalo linaongozwa na Chadema.

Taarifa kwa Umma Toka LHRC Kuhusu Matukio ya Ukiukwaji wa Haki za Kiraia na Kisiasa

Kangi Lugola Amsweka Askari Mahabusu Arusha Kwa Kushindwa Kujibu Maswali Yake

0
0
Askari Polisi mmoja wa Kituo cha Utalii na Diplomasia Mjini Arusha, leo amejikuta akizindua mahabusu ya kituo hicho kwa kuwekwa mahabusu kwa agizo la Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola.

Kituo hicho kilizinduliwa na Rais John Magufuli mapema mwaka huu ambapo tangu wakati huo hakijawahi kupokea mahabusu yeyote.

Waziri Lugola, ametoa agizo hilo leo Jumatatu, Julai 23 alipotembelea kituo hicho cha kisasa, ambapo akiwa hapo alimuhoji baadhi ya mambo kadhaa ambayo askari huyo alishindwa kuyajibu kwa ufasaha.

“Nimeingia kwenye chumba cha mashtaka, nikamkuta askari nikamuuliza vitabu muhimu kwenye chumba hicho akabaki ameduwaa, nikamuagiza RPC (Kamanda wa Polisi) amuweke ndani. Lakini baadaye nikaamuru atolewe kwani yawezekana askari huyo hana elimu ya masuala ya utalii,” amesema.

Amesema kama kituo hicho hakijawahi kuweka mahabusu mtu, basi askari huyo amekuwa wa kwanza kukifungua kwa kukaa mahabusu,” amesema Waziri Lugola.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya July 24

Muonekano wa Mpya wa Elizabeth Michael (Lulu)

0
0
Ni miezi mitatu imepita tokea muigizaji na staa wa filamu nchini Elizabeth Michael “Lulu” aachiwe huru na kubadilishiwa adhabu yake na Mahakama Kuu ya Tanzania na kwa sasa anatumikia kifungo cha nje.

Katika mitandao ya kijamii picha ya muonekano mpya wa Elizabeth Michael imekuwa gumzo  alipohudhuria tamasha la “Awe” liloandaliwa na muimbaji wa nyimbo za Gospel Paul Clement siku ya Jumapili July 22,2018.

Picha hiyo imesambaa sana katika mitandao ya kijamii ikiwa imepostiwa na watu mbalimbali lakini kwa upande wa instagram account ya Lulu mwenyewe bado hajapost picha yoyote mpya toka October 22 2017.

Rosa Ree : Hakuna Mwanaume Mwenye Uwezo wa Kunihonga

0
0
Mwanadada anaefanya vizuri katika kiwanda cha muziki kwa upande wa rap ,Rosa ree amefunguka na kusema kuwa katika maisha aliyoishi mpaka kufikia sasa hivi haona kama kuna mwanaume anaeweza kumhonga hela nyingi za yee kuridhika nazo .

Mwanadada huyo ambae amekuwa akionekana na muonekano wa kiume kila siku na imekuwa ikisemekana kuwa hana mwanaume katika maisha yake ya kimahusiano anasema kuwa haoni kama mwanaume anaweza kumpa hela yoyote inayoweza kumridhisha.

Pia rosa ree anasema kuwa huwa hawaelewi sana wanaume wanapokuja na kumhonga kwa sababu anakuwa haelewi kama  ndio wanaonga au wanajaribu ....” mimi sihongeki , kwahio hata mtu akinionga huwa nashindwa kuelewa ni kwamba ananihonga au ananijaribu.”

Mbunge Avuliwa Udiwani Kwa Kutohudhuria Vikao

0
0
Mkurugenzi wa Jiji la Tanga, Daudi Mayeji ametangaza Kata ya Ngamiani Kusini kuwa wazi  kutokana na Diwani wake ambaye pia ni Mbunge wa Tanga Mjini, Mussa Mbaruku (CUF), kutohudhuria vikao zaidi ya sita vya Baraza la Madiwani.

Mayeji amesema mbunge huyo amepoteza sifa kwa mujibu wa Sheria ya Mamlaka za Majiji.

“Sheria ya Serikali za Mitaa, Mamlaka ya Majiji Sura ya 228, kifungu cha 30B ndiyo imemuondoa, ni kwa mujibu wa sheria,” amesema Mayeji.

Mbaruku aligombea nafasi hizo za ubunge na udiwani katika chaguzi Mkuu mwaka 2015, kupitia Chama cha Wananchi (CUF) na kushinda zote.

JUKATA Wataja Vikwazo 9 Uchaguzi 2020

0
0
Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata) limeitaka Serikali kufanya marekebisho ya sheria na Katiba ya nchi yanayoendana na mahitaji ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Julai 23, 2018 jijini Dar es Salaam, mwenyekiti wa Jukata, Hebron Mwakagenda alitaja maeneo tisa yanayohitaji mabadiliko ili kuhakikisha uchaguzi huo unakuwa huru na wenye haki.

“Kutokana na kwamba serikali ya awamu hii imetamka kuwa mchakato wa katiba mpya sio kipaumbele chake, na kimesalia kipindi kifupi kufika mwaka wa uchaguzi tukiwa kama jukwaa la katiba tunashauri mabadiliko yafanyike haraka”. alisema Mwakagenda.

Mwakagenda alitaja maeneo yanayohitaji mabadiliko ya katiba zaidi kuwa ni, uhuru kamili wa tume ya taifa ya uchaguzi na tume ya uchaguzi ya Zanzibar,kuungana kwa vyama vya siasa, uwakilishi wa uwiano wa 50/50,mgombea binafsi aruhusiwe kwenye uchaguzi mkuu, na matokeo ya Rais yahojiwe mahakamani,Tume ya Uchaguzi kusimamia uchaguzi zote na kurejesha ushindi wa rais kwa kura nyingi.
"Kama tunahitaji uchaguzi wa amani, mabadiliko hayo ni muhimu sana ili kuingia kwenye uchaguzi kwa amani, "alisema Mwakagenda.

Historia ya kuandikwa kwa Katiba Mpya ilianza Desemba mwaka 2011 wakati Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akilihutubia taifa na baadaye aliwateua wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyokuwa ikiongozwa na Jaji Joseph Warioba, ambayo ilianza kazi yake Mei 3, mwaka 2012.

Tume hiyo ilikusanya maoni ya wananchi nchi nzima na kuandaa Rasimu ya kwanza ya Katiba iliyotolewa Juni 4, 2013 kabla ya kutoa Rasimu ya pili ya katiba hiyo iliyoendelea kujadiliwa bungeni, huku wabunge wa upinzani wakisusia vikao hivyo ndipo lilipoibuka jina UKAWA (Umoja wa Katiba ya Wananchi), Tume ya Mabadiliko ya Katiba ilitakiwa kumaliza kazi ya kuandaa rasimu ya pili, lakini haikufanikiwa kukamilisha mpaka awamu ya Rais Kikwete ilipomalizika.

Makamu wa Rais Atishia Kulivunja Baraza la Madiwani Tunduma

0
0
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan amesema Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Tunduma mkoani Songwe linastahili kuvunjwa kutokana na kutofanya vikao vyake kwa muda wa miezi tisa kinyume na tataribu na kanuni zake.

Alisema hayo jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Shule ya Msingi Mwaka mjini Tunduma wilayani Momba mkoani Songwe kuwa mgogoro uliojitokeza hadi baraza kutofanyika kwa muda mrefu unatokana na ukiukwaji wa kanuni na sheria uliofanywa na baraza hilo.

 Alisema kwa mujibu wa sheria iwapo baraza la madiwani lisipokutana katika kipindi cha miezi mitatu linastahili kuvunjwa na kwamba atawasiliana na Waziri wa Tamisemi, Seleman Jafo ili kuona nini cha kufanya.

Makamu wa Rais alitumia nafasi hiyo kusisitiza umuhimu wa kufuata sheria na kuachana na matumizi mabaya ya madaraka kwa kuingiza maslahi binafsi.

Kuhusu wafanyabiashara waliohamia Zambia, alisema hakuna nchi yoyote ambayo haikusanyi kodi na kwa kuwa wao wameonyesha kukaidi sheria na hawataki kulipa kodi wabaki huko huko (Zambia) ambako kodi hazikusanywi.

 "Tangu nimeingia mji wa Tunduma nimeona biashara nyingi sana na hivyo kuondoka kwa hao wametoa fursa nzuri kuwapisha wengine wenye uzalendo wa kulipa kodi ambazo ndiyo fedha zinazowaletea maendeleo" Alisema Samia

Kauli hiyo ilikuja baada ya Mbunge wa Tunduma  (Chadema), Frank Mwakajoka kudai halmashauri hiyo hakuna demokrasia kufuatia baraza la madiwani kuzuiwa kufanya vikao kwa miezi tisa kutokana na kutoelewana kwa Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Ally Mwafongo na Mkuu wa Wilaya ya Momba, Jumaa Irando.

Alisema mgogoro ulianza baada Mwafongo kutangaza kuondoa ushirikiano na Irando kwa madai ya mkuu huyo wa wilaya alikuwa anaingilia mipango ya halmashauri, lakini baadae naye Irando akatumia mamlaka yake kuzuia madiwani hao kutofanya vikao vyote vya baraza hilo.

Pia aliwaagiza watumishi wote kuanzia maofisa watendaji wa mitaa, kata na halamshauri kutopokea maelezo au maagizo yoyote kutoka kwa madiwani hao.

Mwakajoka aliongeza kutokana na mahusiano mabaya baina ya Serikali ya wilaya na halmashauri na wafanyabiashara kudaiwa kodi kwa vitisho wafanyabiashara zaidi ya 2,000 wamehamia nchi jirani ya Zambia.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa Songwe, Chiku Galawa alisema mkoa umejipanga kuhudumia wananchi ambao wako tayari kushirikiana na Serikali kwa kulipa kodi ambayo ndiyo inayotumika kuwaletea maendeleo na kuwa walioondoka wasirudi na ikiwezekana eneo hilo litawekewa uzio ili wasirudi tena.

Jalada La Kesi Dhidi Ya Mke Wa Bilionea Msuya Liko Mkononi Mwa DPP

0
0
Upande wa mashtaka katika kesi ya mauaji inayomkabili mke wa bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita (41), umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa jalada la kesi lipo mikononi kwa  kwa mkurugenzi wa mashtaka (DPP).

Wakili mwandamizi wa Serikali, Patrick Mwita ameeleza hayo jan Jumatatu Julai 23, 2018 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, wakati shauri hilo lilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Mbali na Mrita, mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ya mauaji namba 5 ya mwaka 2017 ni mfanyabiashara Revocatus Muyela (40)  ambapo wote wanakabiliwa na shtaka mmoja la mauaji ya dada yake Erasto Msuya, Aneth Msuya.

"Shauri lilikuja kwa ajili ya kutajwa na jalada la kesi kwa sasa lipo mikononi mwa DPP bado tunalifuatilia "alidai Mwita.

Kufuatia taarifa hiyo, Hakimu Simba amewataka upande wa mashtaka kulifuatilia jalada hilo ambalo mwanzoni walidai liko ofisini kwa DPP na sasa liko mikononi mwake.

Wakili wa utetezi Peter Kibatala alikubaliana na upande wa mashtaka na kuiomba mahakama hiyo kupanga tarehe nyingine fupi.

 Hakimu Simba ameahirisha  kesi hiyo hadi Julai 30, 2018 itakapotajwa tena.

Februari 23, 2017, washitakiwa hao waliachiwa huru na mahakama hiyo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Godfrey Mwambapa na kisha wakakamatwa tena na baadaye kusomewa upya shtaka moja la mauaji.

Washtakiwa wanadaiwa kumuua kwa makusudi Aneth tukio linalodaiwa kutokea Mei 25, 2016 maeneo ya Kibada Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Waziri Jafo: Serikali Ya Magufuli “Sio ya walimila Dole”.

0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi) Selemani Jafo jana alitembelea halmashauri ya wilaya ya Kibaha kufanya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

 Katika Ziara hiyo, Waziri Jafo amefanikiwa kutembelea kituo cha afya Mlandizi, ukarabati wa sekondari ya wasichana ya Ruvu, pamoja na uboreshaji wa Kituo cha afya cha Magindu ambapo zaidi ya sh. bilioni 1.9 zimeshatolewa na serikali kufanikisha miradi hiyo.

 Akizungumza na wananchi wa Magindu waziri Jafo aliwaambia wananchi hao kwamba serikali inayoongozwa na Rais John Magufuli ni serikali ya vitendo sio ya kuahidi bila kutekeleza na kwamba kwa kizaramo “Sio ya walimila Dole”.

 Jafo alitumia neno hilo la Lugha ya kizaramo kwa wakazi hao wa magindu ambao wengi wao ni wazaramo ili kuleta msisitizo.

 Waziri Jafo amempongeza Mbunge wa Jimbo la Kibaha vijijini Hamood Abuu Jumaa kwa kazi kubwa anayoifanya ya kiwaletea wananchi wa kibaha vijijini maendeleo ya kweli.

 Aidha, waziri Jafo amewapongeza viongozi wa Kibaha vijijini kwa usimamizi mzuri wa ukarabati wa shule ya Ruvu kwani kwasasa imekuwa shule ya kuvutia kutokana na usimamizi mzuri wa fedha za serikali.

Hata hivyo katika ziara hiyo, Jafo ametoa mwezi mmoja agizo la kuwekwa majokofu jengo la kuhifadhia maiti katika kituo cha afya mlandizi lililojengwa tangu mwaka 2015 ili  wananchi waweze kupata huduma hiyo.

 Nao, wananchi wa Magindu wamemshukuru mbunge wao kwa kuwapigania mpaka wamepatiwa fedha hizo za maendeleo.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live


Latest Images