Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Waziri Mwijage Atengua Uteuzi Wa Mkurugenzi Wa Wakala Wa Usajili Wa Biashara Na Leseni (BRELA)


Kesi Yamzuia Mbowe Kuhudhuria Ufunguzi wa Kampeni za Uchaguzi

0
0
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mhe. Freeman Mbowe imeelezwa kuwa atashindwa kuhudhuria ufunguzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa marudio wa Ubunge katika jimbo la Buyungu Mkoani Kigoma siku ya Jumapili kutokana na kesi iliyopo Mahakamani.

Hayo yamebainisha na Mkurugenzi wa Itifaki na Mawasiliano ya Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema  mchana baada ya Mahakama Kuu kutupilia mbali ombi la marejeo ya uendeshaji wa kesi yao.

Maombi hayo ni juu ya kesi ya kufanya mkusanyiko usiokuwa wa halali mnamo Februari 17 mwaka huu kwenye chaguzi ndogo za marudio Jimbo la Kinondoni Jijini Dar es Salaam huku wakipewa nafasi ya rufaa juu ya maamuzi hayo yaliyotolewa na Mahakama.

"Kiukweli hizi kesi zinazoendelea Mahakamani zinatuathiri sana sisi kama chama, maana hadi sasa hivi hatujui ni nani ambaye ataweza kuenda kuzindua kampeni za uchaguzi wa marudio katika jimbo la Buyungu Mkoani Kigoma siku ya Jumapili kutokana na viongozi wote wapo jijini Dar es Salaam wanafuatilia kesi zao", amesema Mrema.

Pamoja na hayo, Mrema ameendelea kwa kusema "kikawaida alipaswa aje Mwenyekiti wa chama Freeman Mbowe lakini kwa hali jinsi ilivyo hatoweza kushiriki na sasa tunamtegemea Naibu Katibu Mkuu bara John Mnyika aje mara moja kufanya ufunguzi na kurudi zake kusikiliza mwenendo wa kesi".

Wanachadema wanaoshtakiwa ni pamoja na Mwenyekiti wao Freeman Mbowe, Katibu Mkuu wa chama hicho Dkt. Vicent Mashinji, Naibu Katibu Mkuu bara John Mnyika, Naibu katibu Mkuu Zanzibar, Salim Mwalimu.

Wengine ni Mbunge wa Tarime vijijini John Heche, Mbunge Tarime mjini Esther Matiko, Mbunge wa Bunda mjini Ester Bulaya, Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa pamoja na Mbunge wa Kawe Halima Mdee.

Wote hao wanaandamwa na mashtaka 13 ikiwemo la kufanya mkusanyiko isiyokuwa na kibali kwenye chaguzi ndogo za marudio Jimbo la Kinondoni Jijini Dar es Salaam zilizofanyika Februari 17, 2018

Sheria Mpya Kudhibiti Uzito wa Magari Kuanza Mwakani

0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga, ameitaka kurugenzi ya Usalama na Mazingira katika wizara hiyo kutoa elimu kuhusu kuanza kutumika kwa sheria mpya ya udhibiti wa uzito wa magari ya jumuiya ya afrika ya Mashariki ya mwaka 2016.

Akizungumza jijini Dodoma Mhandisi Nyamhanga, amesema sheria hiyo mpya ya udhibiti wa uzito wa magari itaanza kutumia Januari Mosi, mwakani.

“Hakikisheni wadau wote wa usafirishaji hapa nchini wanapata uelewa wa kutosha kuhusu sheria mpya ya udhibiti wa uzito wa magari itakayotumika katika nchi zote za Afrika Mashariki ili kuwawezesha kudhibiti athari za uharibifu wa barabara na kuepuka adhabu zilizomo katika sheria hiyo” amesema Mhandisi Nyamhanga.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Meja Jenerali Jacob Kingu, amesema Wizara yake itashirikiana kikamilifu na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano katika kuhakikisha sheria hiyo mpya inatekelezeka kwa maslahi ya wasafirishaji na miundombinu ya barabara.

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira wa Wizara hiyo, Mhandisi Julius Chambo, amesema idara yake imejipanga kutoa elimu kwa wadau wote ili wafahamu sheria hiyo, fursa zake na adhabu zilizomo kwa watakaozidisha uzito na kuharibu barabara.

Amewataka wadau wote wa usafirishaji na watumishi katika mizani zote nchini kuielewa sheria hiyo, kuifanyia kazi na kuwa waadilifu ili kulinda miundombinu ya barabara hapa nchini na kuepuka adhabu za faini na vifungo zilizomo katika sheria hiyo.

Mkutano wa siku moja wa wadau wa usafirishaji nchini ni sehemu ya mkakati wa Serikali kujenga uelewa wa pamoja kati yake na wadau wa usafirishaji katika kuelewa sheria hiyo na kuifanyia kazi.

Polepole Azindua Kampeni na Kumnadai Mgombea wa CCM Moshi

0
0
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amewasihi wakazi wa kata ya Mawenzi mjini Moshi, kumchagua mgombea udiwani wa CCM, Apaikunda Naburi kwa maelezo kuwa atakuwa kiunganishi sahihi kati yao na Serikali inayoongozwa na Rais John Magufuli.

Polepole ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Julai 20, 2018 katika viwanja vya kituo kikuu cha mabasi mjini Moshi, wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata hiyo, ambayo awali diwani wake, Hawa Mushi alikuwa akitokana na Chadema.

Hawa aliyechaguliwa kuwa diwani mwaka 2015 alifariki dunia mwezi uliopita na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kutangaza kufanyika kwa uchaguzi mdogo, sambamba na kata zingine 76 nchi nzima.

Polepole amesema maendeleo yanayoonekana katika mji wa Moshi yanatokana na sera nzuri za Serikali ya CCM, ambayo ndio imekuwa ikitoa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo kwa asilimia 80.

Katibu huyo amesema kitakwimu, halmashauri ya manisapaa ya Moshi ina uwezo wa kukusanya mapato ya ndani yanayofikia zaidi ya Sh5 bilioni wakati bajeti kwa mwaka mzima ni Sh46bilioni.

"Hawa wenzetu (Chadema) wanasema wao ndio wameleta haya maendeleo mnayoyaona hapa Moshi. Nataka niwaambie leo, halmashauri mapato yake ni Sh5bilioni kwa mwaka lakini bajeti nzima ni Sh46 bilioni. Mwenye macho haambiwi tazama,"amesema Polepole.

Polepole aliwaomba wakazi wa kata hiyo kumchagua Naburi akisema ndio chaguo sahihi la kuwaletea maendeleo wananchi wa Moshi, ikiwamo kuboresha huduma katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi.

Mbunge wa Siha (CCM), Dk Godwin Mollel amesema ni upotoshaji mkubwa kudai  Rais Magufuli hapendi vyama vya upinzani wakati anaendelea kutoa ruzuku ya kila mwezi kwa Chadema ambacho kinajinasibu kuwa chama kikuu cha upinzani nchini.

Dk Mollel alikuwa mbunge wa Siha kwa tiketi ya Chadema kati ya Novemba 2015 hadi Desemba 2017, kabla ya kujiuzulu na baadae kuteuliwa na CCM kugombea ubunge jimbo hilo hilo na kushinda.

Kwa mujibu wa Dk Mollel, Chadema imekuwa ikipatiwa ruzuku ya Sh337 milioni kwa mwezi kwa fedha za Serikali ya CCM hivyo si sahihi kudai Rais Magufuli hapendi upinzani.

Dk Mollel amedai pamoja na chama hicho kupokea mamilioni hayo ya fedha kwa mwezi, kimeshindwa kuzitumia kwa maendeleo ya chama hicho na ndio maana hadi leo hakina ofisi yake ya kujenga.

Katika mkutano huo, CCM kiliwatumia makada wa zamani wa Chadema waliohamia CCM, kuwashawishi wakazi wa kata ya Mawenzi, kumchagua mgombea wa CCM.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya July 21

Polepole Aipukutisha CHADEMA Jimbo la Mbowe

0
0
Viongozi wote wa Chadema Kata ya Muungano, wakiongozwa na Godliving Emmanuel Kimaro ( Baba Diana) Mwenyekiti wa Kata ya Muungano na Ibrahimu Hamis Mkindi (Mparee) Mwenezi wa Chadema Kata Muungano kutoka Wilaya ya Hai wamejivua uanachama wa Chadema na kujiunga na CCM.

Viongozi hao wamepokelewa na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Taifa Kamaradi Humphrey Polepole kwenye Mkutano wa hadhara Moshi Mjini Kata ya Mawenzi wakati akimnadi Mgombea wa Udiwani wa CCM Kata ya Mawenzi Ndg. Apaikunda Ayo Naburi.

Ziara Ya Makamu Wa Rais Mkoani Songwe

Waziri Kigwangalla Awataka Wavamizi Maeneo Yaliyohifadhiwa Kuondoka

0
0
Na Pamela Mollel,Arusha
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla amewataka wananchi waliovamia maeneo ya hifadhi nchini, kujiandaa kuondoka ndani ya miezi mitatu kabla ya operesheni kuanza.

Akizungumza na waandishi wa habari,Julai 19  katika eneo la  hifadhi ya Jamii ya wanyamapori(WMA) ya makao, wilayani Meatu, Dk Kigwangalla alisema wavamizi wa maeneo ya hifadhi wengi wamekuwa wakijihusisha na matukio ya ujangili.

“Utakula kijiji kina ardhi kubwa, lakini wengine wanajenga hadi katika ndani ya eneo la mita 500 kutoka mpaka wa hifadhi na hao mara nyingi ndio wanaingiza mifugo hifadhini usiku na kufanya ujangili”alisema

Alisema maeneo mengi ya hifadhi na mapori ya akiba nchini yamevamia na wananchi jambo ambalo serikali haiwezi kukubali yaharibiwe ama kutumika kwa ujangili.

Waziri huyo, pia alitembelea kambi ya kitalii ya TGTS na hoteli ya  Mwiba   na kushuhudia vikosi vya kupambana na ujangili katika maeneo hayo ambavyo vipo yapo chini ya taasisi  Friedkin Conservation Fund na kueleza kuridhishwa na uwekezaji wa taasisi hiyo.

Mkurugenzi wa Mwiba Holding, Abdukaril Mohamed, alisema katika eneo la Mwiba wamewekeza sh 2.2 bilion na hivi sasa wanaendelea na shughuli za uhifadhi na utalii.

“Mheshimiwa Waziri katika eneo hili, kampuni yetu inafanya utalii wa picha na kuna hoteli,tunafanyakazi kwa amani na utulivu na vijijini vinavyotuzunguka”alisema

Mwenyekiti wa kijiji cha makao, Anthony Philip, alimweleza Waziri Dk Kigwangalla kuwa, katika eneo hilo kuna mahusiano mazuri baina ya vijiji na wawekezaji na vijiji vinapata mgao wa fedha.

Alisema kijiji cha makao kimekuwa kikipata zaidi ya sh 147 milioni kwa mwaka kutoka kwa mwekezaji na vijiji vingine sita vimekuwa vikipata zaidi ya milioni 80,000 kila mwaka”alisema.

Akiwa katika pori la akiba la Maswa,Meneja wa pori hilo, Lusato Masinde alisema pia wanauhusiano mzuri na wawekezaji ambao licha ya kulipia ada za vitalu pia wamekuwa wakitoa msaada wa huduma mbali mbali ikiwepo maji.

Hata hivyo, alisema katika pori hilo changamoto kubwa ni uvamizi wa mifugo, uchache wa watumishi na upungufu wa vitendea kazi.

Mwisho.

Taarifa kwa Umma: Barabara ya Nelson Mandela Imefungwa kwa Siku 3 tangu Jana

0
0
 Kuanzia jana  Ijumaa Julai 20, 2018 hadi Jumatatu Julai 23, 2018 watumiaji wa barabara ya Nelson Mandela jijini Dar es Salaam watakumbana na usumbufu kutokana na matengenezo yatakayoanza kufanyika katika barabara hiyo eneo la Ubungo.

Kufuatia matengenezo hayo, kuanzia  eneo la mataa ya Ubungo hadi Riverside (kama unatokea Mwenge kuelekea Buguruni), itafungwa kwa siku hizo, badala yake magari yatalazimika kupita upande wa pili wa barabara hiyo hiyo (inayotoka Buguruni kuelekea Ubungo).

Hayo yameelezwa katika taarifa iliyotolewa Julai 20, 2018 na kampuni ya CCECC inayojenga barabara za juu katika makutano ya Ubungo.

“CCECC inapenda kuwajulisha watumiaji wa barabara katika makutano ya Ubungo kuelekea Nelson Mandela (Riverside) kuwa siku ya Ijumaa Julai 20 kuanzia saa tano usiku hadi Jumatatu (Julai 23) ujenzi utakuwa unaendelea na watumiaji wa barabara hii watakuwa wanapita kama inavyoonekana kwenye mchoro huu,” imesema taarifa hiyo.

Lugola Azungumzia Suti Zake

0
0
Baada  ya suti za Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, kuwa gumzo kwenye mitandao mbalimbali, mwenyewe amefunguka na kufafanua juu ya suala hilo.
 
Kwa muda sasa, tangu ateuliwe kushika nafasi hiyo, Lugola amekuwa akivaa suti zenye bendera ya Tanzania kwenye mifuko hali ambayo imesababisha mijadala kwenye mitandao ya kijamii.

Akizungumza na Michuzi, Lugola alisema anazo suti nyingi za aina hiyo na ni yeye mwenyewe aliyeamua zifanane kwa mwonekano.

Baadhi ya wachangiaji kwenye mitandao ya kijamii wamekuwa wakihoji iweje Waziri avae suti moja muda mrefu wakidhani kuwa amekuwa akiirudia.

Lakini mwenyewe jana alijibu na kueleza kuwa suti hizo ambazo ameziita kuwa ni za aina yake, anazo nyingi lakini ameamua zote zifanane.

“Hata ninapobadilisha suti hizi hakuna anayeweza kujua kwa sababu zote zimefanana,” alisema.

Mwonekano wa suti hizo umefanya watu wengine kuzishangaa kutokana na mifuko ya shati kutengenezwa kwa bendera ya taifa.

PICHA: Kangi Lugola na IGP Simon Sirro wakutana uso kwa uso

0
0
Waziri wa  Mambo ya ndani ya Nchi Kangi Lugola jana amekutana na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Sirro na Maofisa wengine Wakuu wa Jeshi hilo, Makao makuu ya Polisi Dar es salaam.

Waziri Lugola amekutana na IGP Sirro kukiwa na mfululizo wa maagizo aliyoyatoa ikiwemo kumtaka IGP Sirro amwambie kama wamewashindwa majambazi kutokana na kulazimika shughuli nyingi kufungwa inapofika jioni kwa kuhofia kuvamiwa.

Jambo la pili ilikuwa ni kutaka maelezo ya alipo Mbwa maalum wa Kikosi cha Bandari ambapo mpaka  jana asubuhi ya  July 20 2018 alikuwa hajapatikana. 

Baada ya Kikao hicho, Lugola alisema kilikuwa ni cha majumuisho ya zaiara zake ambapo ametoa mwezi mmoja zaidi kwa jeshi la polisi ili waandae ripoti kuhusiana na changamoto ya mbwa wa Bandarini pamoja na mpango mkakati wa kuwawezesha wananchi kufanya kazi zao usiku walau kwa baadhi ya maeneo.

Mazishi ya Baba Mkwe Wa Kikwete Yawakutanisha Viongozi MbaliMbali Wa Vyama Tofauti

0
0
Viongozi wa ngazi mbalimbali Serikalini , viongozi wastaafu pamoja na mamia ya wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam wameshiriki katika mazishi ya mzee Rashid Mkwachu ambaye ni baba yake mzazi Mke wa Rais mstafu Jakaya Kikwete, Mama Salma Kikwete.

Mwili wa mzee Mkwachu umezikwa jana katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

Mzee Mkwachu alifikwa na umauti Julai 19 mwaka huu  na chanzo cha kifo chake kimeelezwa na Msemaji wa familia ya Kikwete,Ridhawani Kikwete kuwa mzee huyo amefariki kutokana na magonjwa ya utu uzima kwani umri wake ulikuwa zaidi ya miaka 100.

Kabla ya mwili kufikishwa makaburi ya Kisuti ibada na dua kumuombea marehemu mzee Mkwachu zilifanyika nyumbani kwa Rais mstaafu Jakaya Kikwete Msasani jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya viongozi walioshiriki kwenye maziko hayo ni Rais Mstaafu Al haji Ali Hassan Mwinyi,  Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowassa.

Akizungumza kwenye msiba huo Sheikh Mkuu wa Tanzania Muft Abuubakary Zubeiry amesema maisha ya binadamu ya kuishi kwenye ulimwengu ni mafupi sana na kwa kawaida ni kati ya miaka 63 na ikitoa zaidi ya hapo ni zawadi tu.

Amesema kuwa viumbe vyote ni vinamuda wake wa kuondoa kwenye huu ulimwengu na hakuna ambaye ataishi milele na kufafanua na kufa si kutoweka moja kwa moja bali ni utaratibu wa maisha ya kutoka kwenye ulimwengu na kwenda akhera.

Kwa upande wake Mjuukuu wa Marehemu Mzee Mkwachu ambaye pia ni Msemaji wa Familia Ridhwan Kikwete alieleza kilichokuwa kikimsumbua babu yake ni magonjwa ya utu uzima.

Ametumia nafasi hiyo kuwashukuru woye ambao wamepata nafasi kwa namna moja a nyingine kuungana nao katiki kipindi hiki ambacho cha majonzi wako.

Tanzania na Zambia kutumia kituo kimoja cha forodha mjini Tunduma

0
0
Tanzania na Zambia zimekubaliana kutumia kituo kimoja cha forodha kilichojengwa mjini Tunduma.

Lengo na ushirikiano huo ni kupunguza na kudhibiti msongamano wa magari  na uingizwaji wa mizigo kwa njia za magendo.

Makubaliano hayo yamefanyika jana Ijumaa Julai 20, 2018  baina ya naibu kamishna wa forodha  wa mamlaka ya mapato  Tanzania (TRA),  Qamdiyay  Akonaay na kamishina wa forodha  wa mamlaka ya mapato Zambia (ZRA),  Sydney Chibbabbuka  baada ya kukagua miundombinu ya majengo katika mpaka wa  Tunduma na Nakonde.

Akizungumzia na waandishi wa habari mjini Tunduma, Akonaay amesema wamefikia makubaliano hayo  kwa  lengo la kupunguza msongano wa magari na usimamizi wa usafirishaji wa mizigo ili kuongeza mapato  na kuthibiti njia za magendo  za kupitisha bidhaa katika mipaka ya nchi hizo.

"Kituo cha pamoja cha forodha kitaanza kufanya kazi Julai 26 mwaka huu. Wafanyakazi wa ZRA na TRA watafanya kazi katika ofisi moja. Ushirikiano huu utakuwa  chachu ya kukuza uchumi wa mapato  hususani kwa upande wa Tanzania," amesema.

Naye  Chibbabbuka amesema ushirikiano huo utakuwa na faida nyingi katika usafirishaji wa mizigo na kupunguza msongamano uliokuwepo.

Amesema nchini Zamziba tayari wamepata eneo la maegesho ya magari kutoka Tanzania, wanatarajia kuanza ujenzi wa uzio katika eneo hilo mwakani.

Serikali Yaahidi Kuweka Mazingira Bora Kwa Sekta Binafsi Nchini

0
0
Serikali imeahidi kuweka mazingira wezeshi yatakayorahisisha sekta binafsi kushiriki katika utekelezaji wa miradi ya maji.

Ahadi hiyo imetolewa jana Ijumaa Julai 20, 2018 na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji,  Jumaa Aweso wakati wa kufunga kongamano la wadau wa sekta ya maji.

Amesema kupitia kongamano hilo imeonekana kuna haja ya kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi ili kuhakikisha changamoto ya maji inapatiwa ufumbuzi.

“Tunatambua changamoto zinazoikabili sekta binafsi, tutazifanyia kazi na kuangalia namna bora ya kukabiliana nazo lengo ni kuhakikisha maji yanapatikana ya kutosha,” amesema.

Kongamano hilo la siku mbili lililenga kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi katika kuendeleza sekta ya maji nchini lililobebwa na kauli mbiu 'maji ni uchumi'.

Naye Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, mhandisi Stella Manyanya amewataka wakandarasi kuwa na taarifa za kutosha kuhusu vifaa vinavyopatikana ndani ya nchi.

Amesema hilo litapunguza kasi ya kuagiza vifaa kutoka nje ya nchi na kutoa fursa kwa wazalishaji wa ndani kuuza vifaa vyao.

"Tunapenda kuona viwanda vinavyozaliwa Tanzania vinakuwa, wale watafiti wasikimbilie kusema vifaa vya ndani havina ubora ni jukumu lao kufanya utafiti kujua ubora na nini kifanyike viwe bora,” amesema.

“Kuanzia sasa zikitolewa zabuni kubwa za miradi ya maji, wizara ya viwanda tutapita kuangalia ni vifaa gani vimetumika na vimetolewa wapi.”

Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa Kitila Mkumbo amesema Serikali itafanya kila linalowezekana kuiwezesha sekta binafsi kufanya kazi ila sio kuilea.

Akizungumza kwa niaba ya sekta binafsi, Mkurugenzi wa Huduma kwa wanachama Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Luis Akaro ameitaka Serikali kuweka mazingira wezeshi katika ufanyaji biashara unaohusisha sekta ya maji.

Amesema kufanikiwa kwa kongamano hilo ni dhahiri kuwa Serikali imedhamiria kukabiliana na changamoto ya maji.

Jipatie Dawa za Asili za Kupunguza Maziwa, Kutoa Michirizi, Kuondoa Chunusi, Kuongeza Maumbilie na Nguvu za Kiume

0
0
Katika kusherehekea miaka 15 ya kampuni ya NATURAL BEAUTY PROD tunatoa shukrani za dhati sana kwa wateja wetu wote kwa kutuunga mkono miaka yote hiyo.
 
TUNATOA OFFA YA WIKI NZIMA KWA WATEJA WETU UKINUNUA BIDHAA UTAPATA PUNGUZO LA 20%. KWA WATEJA WA MIKOANI UTATUMIWA BURE.

Ni bidhaa salama kabisa zilizotengenezwa kwa mimea na matunda pia zina matokeo mazuri na kwa haraka zaidi.

🥑🍇🍋🍓🍒🌱🍇🍇
👇👇👇👇
1.HANDSOME UP ORIGINAL_ Inaongeza uume kwa size uipendayo na kuimarisha misuli (wiki 2) @220,000/=
2.SHARK POWER GELY_ Inaongeza uume inch 6 (wiki 4) @150,000/=
3VigRX CREAM_ Inaongeza uume inch 7.5 hadi 8 (wiki 2-3) @180,000/=
4.Vidonge maalum vya kuongeza nguvu na hamu ya tendo hata kwa wenye kisukari na BP @140,000/=
5. MAXMAN 2-Hii ni vidonge vinavyoongeza nguvu za kiume pamoja na uume @210,000/=
6.VIGA SPRAY OG_ Inaongeza uwezo ktk tendo na kuchelewesha kufika kileleni @140,000/
7.BOTCHO MULT PLUS_Hii ni dawa ya kunywa ya kuongeza ( Hips mapaja na makalio) inapatikana kwa @160,000/=
8.BOTCHO CREAM HOLOGRAM_ Hii ni yakupaka ya kuongeza (HIPS na MAKALIO) @150,000/=
9.LEG BOOSTER_Ni dawa ya kuongeza miguu (CHUPA YA BIA) @140,000/=
10.BODY BOOSTER_ Hii ni yakuongeza mwili pamoja na hamu ya kula vizuri @140,000/=
11.YODI PILLS--- Hii ni dawa ya vidonge ya kuongeza (hips mapaja na makalio) inapatikana kwa @160,000/= N.K

NB:Hakikisha unapata risiti yenye muhuri halisi wa NATURAL BEAUTY PROD ili kuthibitisha ubora wa bidhaa zetu.
Wasiliana nasi Popote ulipo duniani kwa no÷

(+255) 659618585
au
0759029968
Follow us instagram-
GOOGLE
YOU TUBE
@natural_beauty_prod
@natural_beauty_prod
@natural_beauty_prod
@natural_beauty_prod < WELCOME ALL>

Mtaalam na Bingwa wa Magonjwa Yote Sugu Yaliyoshindikana Kama Vile Pumu, Vidonda vya Tumbo, Bush's, Nguvu za Kiume

0
0
MTALAAM NA BINGWA WA MAGONJWA YOTE SUGU NAYALIYOSHINDIKANA KAMA VILE PUMU, VIDONDA VYA TUMBO, BUSHA, NGUVU ZA KIUME, KISUKARI,MIVUTO YOTE, KUSAFISHA NYOTA, KURUDISHA MALI, NK.

Tatizo la upungufu ukosefu wa nguvu za kiume, maumbile madogo ya uume limekuwa kubwa kwa lika zote hapa duniani

Matatizo hayo sio mageni kigeni ni ile tiba sahihi yakutibu na kuponya haya.chanzo cha hayo matatizo ni:KISUKARI, NGIRI,CHANGO, TUMBO KUUNGURUMA NA KUJAA GESI, KIUNO KUUMA, MAUMIVU YA MGONGO,MAGONJWA YA ZINAA, KORODANI KUVIMBANAKUUMA,VIDONDA VYA TUMBO, NK.

Tiba sahihi nabora ya tatizo la nguvu zakiume ni 3Power,;Nidawa ya vidonge asilia vilivyotengenezwa kwa kiwango bora na salama kwa ajili yakutibu mojakwamoja tatizo la nguvu za kiume maradufu

1,hutibu nguvu za kiume mda mfupi sana kati ya umri wa miaka 18-85 naitakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dk 20 hadi 40 tendo lakwanza bila kuchoka naitakufanya uwe nahamu yakuendelea na tendo la ndoa zaidi ya mara 5 bila hamu kuisha.

FINA Power: Nidawa yakuboresha maumbile ya kiume kwa kunenepesha na kurefusha kwa saizi uipendayo inchi 6,7 hadi 8 kwa mda mfupi sana.dawa hizi huanza kufanya kazi kwa mda wa dk 67 ukisha tumia guarantee miaka 55 ikishakutibu.

Pia tunatibu,KISUKARI, PRESHA, UZAZI, NGIRI, PUMU,MALARIA SUGU, VIDONDA VYA TUMBO, CHANGO AINA ZOTE, BP, BUSHA BILA UPASUAJI NK.

ISHOSHA,Nidawa ya mvuto wa biashara,kazi,hupandisha cheo humfanya mfanyakazi apendwe na mwajiri wake,humvuta mme,mke,hawara,mchumba,unaemhitaji au hakutaki hatimizi ahadi zako kwa dhati utampata kwa mda wa dk 45 tu naatatulia milele nakumfunga asitoke inje ya ndoa.

SHEPU EXRA,Nidawa ya yakupunguza matiti,unene tumbo,kitambi kwa akina baba,hutoa mafuta mabaya mwilini,makovu sehemu mbalimbali mwilini,chunusi sugu,minyama uzembe,michirizi mwilini,nakuongeza makalio hips,mguu wa bia nk.

HUDUMA HIZI NANYINGINE NYINGI MTALAAM BINGWA DR SHEIKH OMARY
Anapatikana dar magomeni moroco hotel
SIMU NO 0767 14 53 57/0629 03 45 50.

NAKAMA NAFASI YAKUFIKA OFISINI HAIPO UTALETEWA HAPO ULIPO.

Tiba Bora ya Tatizo Sugu la Nguvu za Kiume

0
0
OFA! Je umepungukiwa nguvu za kiume na umetumia dawa bila mafanikio? Sasa utapona kwa sh 15000 tu .Ofa ni kwa watu kumi wakwanza kila siku .Ofa hii itadumu ndani ya wiki 2 baada ya hapo bei itakuwa nyingine na kama hujapona tunakurudishia hela yako !

Dawa hii ni dawa ya maajabu, huwezi kuamini Ila wengi wameiamini,inatibu tatizo la upungufu wa nguvu za kiume na utapewa garantee ya mwezi mmoja 

Dawa hii inapatikana hapo hapo ulipo nyumbani kwako na tutakupatia maelezo ya namna ya kuiandaa wewe mwenyewe na baada ya kuiandaa utakunywa Mara moja tu,na hautatumia dawa yoyote ya nguvu za kiume 

Dawa hii inawafaaa watu kuanzia miaka 18 mpaka miaka 70 zaidi ya miaka hyo haitakusaidia 

Ni dawa ya asilia, haina madhara yoyote,watafiti na waganga wameikubali pia hii dawa inawafaa hata wanawake wasiopata hisia za mapenzi

Pia tunaweza kukutumia dawa popote ulipo lakini s kwa bei ya ofa, ukiitumia dawa hii unakuwa na uwezo wa kurudia tendo la ndoa zaidi ya Mara 3 bila hamu kuisha na itakufanya uwe na uwezo wa kufanya tendo la ndoa muda wowote 

Imesaidia watu zaidi ya 148 ndani ya mwaka mmoja tangu igunduliwe  na Dr kiboko mganga wa tiba za jadi toka kisiwani mafia 

Pia tunatibu magonjwa mbalimbali, kurudisha mpenzi aliye kuacha,biashara iliyoyumba, nk 

OMBI LANGU; kwanza naomba radhi kwa watu wanaofika kwenye ofisi yangu na kuchelewa kupata huduma kutokana na foleni ya watu wengi kuja pia pongezi nyingi nimepata kutokana na mafanikio makubwa wanayoyapata baada ya kutumia hii dawa ombi langu naomba upige cm nikuelekeze hii dawa hapohapo kuepuka usumbufu na kuokoa mda wako asante

Maelezo zaidi ; Dr kiboko-  0679923297

Kwanini Baadhi ya Wanaume Wana Maumbile Mafupi na Upungufu wa Nguvu za Kiume? Suluhisho Hili Hapa

0
0
KWANINI BAADHI YA WANAUME WANA MAUMBILE MAFUPI NA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME... DR SITTA NDO SULULISHO LAKO

Tatiza, hili limekuwa likiwaathiri watu wengi sana kisaikolojia hasa baadhi yao kujiona wako tofauti na wanaume wengine. Kwa kawaida, mwanaume anatakiwa awe na uume, usiopungua nchi 6-7au-8 ,vinginevyo mtu huyo anamatatizo.

Zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo hilo... baadhi ni  upungufu wa vichocheo vya, HORMONES ZA CETROGEN .

SUPER MIZIZI, ni dawa inayozalisha HORMONES ZA CETROGEN,na kufanya, uume kukuwa na kuongzeka sazi utakayo na kuzibua mrija iliyosinyaa,

NSHOLA; ni dawa bora, ya kurudisha nguvu za kiume kwa kutibu kabisa  tatizo hilo na kukupa  hamu ya  kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara nne 4 bila kuchoka 

Pia  kuna dawa za kutibu presha ya kupanda na kushuka, kisukari , kuondoa mafuta  mwilini na maumivu ya mgogo kiuno, matazo, ya hedhi kwa wanawake, hedhi zisizokuwa na mpangilio.

NKANYA; ni dawa ya mvuto wa kimapenzi ,mchumba mpenzi aliyekuacha, mke, mme atakurudia .

NKOMA; Ni dawa kuongeza HIPS na mguu wa bia kwa wadada ,

NGAKAMA ,ni dawa ya kutibu miguu kufa ganzi na kuwaka moto, huduma zetu ,zipo ,vizuri, popote pale dawa utaletewa! 

DR SITTA, amebobea kwa tiba asilia 

Kwa DAR ANAPATIKANA MBAGALA ZAKHEM, SONGEA BOMBAMBILI, SHINYANGA- KAHAMA MJINI, 

KWA MAELEZO ZAIDI  PIGA SIMU; 0763172670/ 0715172670,/

WOTE  MNAKARIBISHWA... KAMA, UTAKUWA NA TATIZO, UTAHUDUMIWA,

Waziri mwakyembe atofautiana na TFF ongezeko la wachezaji 10 wa kigeni badala ya 7.

0
0
Na Magdalena Kashindye
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amesema hakubaliani na uamuzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wa kuongeza idadi ya wachezaji wa kigeni kufikia 10 kwenye vilabu vya soka nchini na  ameliagiza Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kuwahoji TFF kuhusu msingi wa uamuzi huo na kutaka utaratibu wa awali uendelee.

Akihojiwa na wanahabari wilayani Kyela ambako ana ziara ya kikazi katika jimbo lake la uchaguzi, Dk. Mwakyembe amesema alitegemea TFF kupunguza idadi ya wachezaji wa kigeni kutoka 7 hadi watano au chini yake na  si vinginevyo.

"Hili ni suala la ki-sera linalodai ushirikishwaji mpana wa wadau ikiwemo Serikali na vyombo vyake, si la TFF peke yake kuamua", amesema mwakyembe

Utaratibu uliokuwepo awali ni wa klabu kusajili wachezaji wa kigeni wasiozidi saba na kati ya hao watano tu kuweza kuchezeshwa katika mchezo moja.

Lakini kwa mabadiliko yaliyotangazwa wiki iliyopita na TFF, timu inaweza kuwasajili na kuwatumia wachezaji wote 10 kutoka nje katika mchezo moja, hatua ambayo Dk. Mwakyembe amesema itaua vipaji vya ndani kwa maslahi finyu ya vilabu vikubwa vyenye ukwasi.

"Binafsi sioni hoja yoyote yenye mashiko kuhalalisha ongezeko hilo la wachezaji wa kigeni nchini. Ninachokiona hapa ni kuwapunguzia fursa vijana wa Kitanzania uzoefu kuchezea klabu kubwa nchini na hivyo kuinyima Timu ya Taifa vipaji vipya vya Kitanzania vinavyotokana na michuano mikali ya Ligi Kuu", amesisitiza. amesema mwakyembe.

Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten akanusha kujihuzulu yanga

0
0
Na Magdalena Kashindye
Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amekanusha taarifa zinazosambaa kuwa amejiuzulu nafasi yake.

Ten ambaye alikuwa nje ya ofisi kwa wiki kadhaa kutokana na kuugua maradhi yaliyosababisha akalazwa, amesema yeye bado ni mwajiriwa wa Yanga.

"Bado tupo mapambano yanaendelea "-Ten ameandika kwenye akaunti yake ya instagram

Baadhi ya vyombo vya habari vimeripoti kuwa Ten amejiuzulu nafasi yake baada ya kuenea taarifa za kujiuzulu kwa Katibu Mkuu, Charles Mkwassa.

Taarifa hizo zimebainisha kuwa Ten amejiondoa Yanga sababu kuu ikielezwa kukosa ushirikiano kutoka kwa baadhi ya viongozi wa mabingwa hao wa Kihistoria Tanzania Bara.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images