Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Mtendaji Mkuu wa TAA: Viwanja 50 Vya Ndege Havina Hati Miliki

$
0
0
Mamlaka  ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA), imesema viwanja vingi vya ndege vimeshindwa kupata hati miliki kutokana na wananchi kuvamia maeneo hayo na kusababisha migogoro ambayo ipo kwenye vyombo vya uamuzi.

Kauli hiyo ilitolewa juzi na Mtendaji Mkuu wa TAA, Richard Mayongela, wakati akimwelezea hali ya sekta hiyo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwele, wakati wa majumuisho ya waziri huyo mkoani Mwanza.

Alisema kati ya viwanja vyote 58,  vilivyo na hati ni vinane tu na kutokana na hali hiyo, TAA imeanza kushughulikia migogoro hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambapo hadi sasa viwanja vingine vinne vipo katika hatua ya mwisho kupewa hati miliki na kufikisha idadi ya 12 kati ya 58.

Mayongela alisema mkakati wao ni kuhakikisha viwanja vyote nchini vinakuwa na hati miliki na ikiwezekana kuwekewa uzio ili kuepusha tena migogoro ya uvamizi.

“Nitumie fursa hii kuwasilisha kwako waziri changamoto zinazotukabili TAA, kwanza tumezoea kuitwa mamlaka lakini hatujapata nguvu hiyo bali kisheria tunatambulika kama wakala, sasa kutokana na hali hiyo tunashindwa kuwa na mamlaka kamili ya maamuzi, ikiwa tutapata mamlaka hayo tutaongeza utendaji zaidi.

“Tunakuomba ukiwa unapitia nakala  ofisini kwako ukifika kwetu umalizie vipengele kadhaa ili tuwe na mamlaka kamili, jambo lingine ni masilahi kwa wafanyakazi ni madogo mno kwani muda mrefu hayajaboreshwa jambo ambalo linasababisha hata morali ya watumishi kupungua, lakini tunamshukuru Rais Dk. John Magufuli, ameonyesha dhamira ya dhati katika kuboresha miundombinu ya viwanja vya ndege.

“Lipo jambo la kuboresha baadhi ya viwanja vyetu ili kuwa vya kimataifa kwani hata ndege kubwa ya Dreamliner iliyokuja hivi karibuni inatua katika viwanja vichache kama Dar es Salaam, Kilimanjaro na Mwanza, hivyo inatubidi kuendelea kuboresha na kuwa na hadhi ya kimataifa, pale Dodoma ambapo ndio makao makuu, tunatarajia kufanya maboresho ya uwanja wa Msalato ili kuwa wa kimataifa,” alisema.

Mayongela alimwomba Waziri Kamwele kusaidia kukamilisha mradi wa ujenzi wa Uwanja wa Songwe ambao umechukuwa muda mrefu ili huduma ziweze kuendelea huku akitoa wito kwa Watanzania wote kuitunza miundombinu inayojengwa kwani fedha zinazotumika ni kodi ya Watanzania.

Pamoja na hayo pia aliainisha viwanja vingine vinavyofanyiwa ukarabati ni  uwanja wa Kigoma, Musoma, Bukoba, Shinyanga huku akisisitiza sekta ya ujenzi na uchukuzi inaendelea kuimarika.

Kuhusu changamoto, Mayongela, alizitaja baadh ikiwamo magari ya zimamoto ambayo alisema kukosekana katika baadhi ya viwanja kunasababisha kutokuwa na huduma ya ndege.

Alisema hadi sasa wana gari 10 mpya ambazo zilinunuliwa katika bajeti ya 2016/2017, 2017/2018.

Makonda aeleza mafanikio ya Serikali katika mkoa wa Dar es salaam

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amesema Serikali ya Awamu ya Tano haiungiungi mambo bali inatekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa nguvu zake zote.

Makonda alitoa akuli hiyo jana mbele ya viongozi na wanachama wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, wakati akielezea tathmini ya mafanikio ya Serikali katika utekelezaji wa ilani ya chama hicho ndani ya mkoa wake.

Alisema utekelezaji wa ilani ya CCM ndani ya utawala wa Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dk. John Magufuli, unakwenda vizuri kwa kadiri malengo yalivyopangwa.

Alisema ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam, miradi mbalimbali inaendelea kutekelezwa na mingi imekamilika ndani ya muda mfupi.

Akizungumzia ujenzi wa barabara, alisema mkoa anaouongoza una mtandao wa barabara wenye takribani kilomita za mraba 3,862.12.

Alisema mtandao huo umegawanyika katika sehemu mbili za utekelezaji ambazo ni Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) na Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (Tarura).

Alisema Tanroads wamesimamia kilomita 601 huku kilomita 3,260.91 zipo chini ya usimamizi wa halmashauri.

Alifafanua kwamba, kilomita hizo kwa  Wilaya ya Ilala ni 1,213, Kinondoni 611, Temeke 552, Kigamboni 626 na Ubungo 209.

Alisema kuwapo kwa mtandao huo wa barabara kumesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza foleni za barabarani ambapo siku za nyuma takribani Sh bilioni 400 zilikuwa zinapotea kwa mwaka.

Alisema katika ujenzi wa miundombinu kuna madaraja makubwa yanajengwa na mengine yapo kwenye mkakati wa kujengwa ambayo kusudio lake ni kuweka urahisi wa mawasiliano ya imara ya usafiri ndani ya Mkoa wa Dar es Salaam.

Alisema ndani ya mkoa wake uwanja wa ndege ‘terminal three’ upo kwenye hatua ya mwisho ya kukamilishwa.

Alisema kukamilika kwa kiwanja hicho inamaanisha kuwa Mkoa wa Dar es Salaam utakuwa na viwanja vitatu ambapo kiwanja cha terminal three kitakuwa na uwezo wa kubeba watu milioni 6 kwa mwaka.

“Kukamilika kwa terminal three ina maana Tanzania kutakuwa ni njia panda ya ndege za mashirika mbalimbali duniani, hivyo maeneo ya Majumba Sita huko tunafumua na kujengwa mahoteli makubwa na hakika eneo hilo litabadilika sana,” alisema Makonda.

Alisema ujenzi wa reli ya Standard gauge unaendelea na kwa baadhi ya maeneo ndani ya mkoa wake reli hiyo itapita juu ili kupisha shughuli za wananchi.

Akizungumzia umeme, alisema kwa sasa nishati hiyo katika Mkoa wa Dar es Salaam ipo ya kutosha kiasi kwamba nishati nyingine wanaigawa kwa Mkoa wa Pwani.

Naibu Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson Kugombea Ubunge 2020

$
0
0
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson, amekiri kuwa na matarajio ya kugombea nafasi ya ubunge katika moja ya majimbo ya Mkoa wa Mbeya.

Ingawa hakutaja jimbo ambalo atagombea, watu ambao wamekuwa wakifuatilia mwenendo wake wanasema huenda akagombea Jimbo la Mbeya Mjini linaloongozwa na Mbunge wa Chadema, Joseph Mbilinyi (Sugu) au Jimbo la Rungwe linaloongozwa na Sauli Amon wa CCM kutokana na miradi mingi inayotekelezwa na taasisi yake inayofahamika kama Tulia Trust kuelekezwa katika maeneo hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana katika viwanja vilivyopo nyumbani kwake eneo la uzunguni jijini hapa, Naibu Spika huyo alisema ingawa anatambua ya kwamba dhamana ya uwakilishi ipo mikononi mwa wananchi, lakini ndani ya chama chake upo utaratibu hivyo wakati utakapofika ataamua.

“Wengi wamekuwa wakihoji kwamba je, nina nia ya kugombea? Na hata hapa kuna baadhi yenu mmeniuliza, ngoja niondoe sintofahamu hii, ni kweli nia yangu ya kugombea ubunge ipo lakini bado sijajua nitagombea wapi,” alisema.

Alisema CCM imeweka utaratibu mzuri kwa wanachama wake wenye nia ya kugombea nafasi mbalimbali na wale wanaotaka kuwawakilisha wananchi bungeni, hivyo haitakuwa busara kwake kuvunja kanuni, taratibu na sheria za chama.

Alisema kwa sasa anatekeleza majukumu ya Serikali ya kuhakikisha wananchi wa Mkoa wa Mbeya na nchi kwa ujumla wanapata maendeleo.

Kuhusu taasisi yake ya Tulia Trust, alisema imejipanga vema kuleta ukombozi wa Mtanzania kupitia sekta ya elimu.

Aidha, akizungumzia siasa zinavyokwamisha maendeleo ya Mkoa wa Mbeya, Dk. Tulia aliwaasa watendaji na wanasiasa kuondoa siasa kwenye masuala muhimu ya maendeleo na kwamba atahakikisha anawasilisha changamoto hizo kwenye vyombo husika ili hatua kwa wahusika zichukuliwe.

“Waandishi mmeeleza mengi lakini kubwa ninaloliona ni changamoto za siasa kuingizwa kwenye utendaji kazi hasa kwenye mambo muhimu ya maendeleo, hili nitalifanyia kazi na kuangalia uwezekano wa kulikomesha kwani Mbeya itajengwa na Wanambeya wenyewe,” alisema.

PICHA: Waziri wa Mambo ya Ndani Alivyompokea Rais Mstaafu Barack Obama Uwanja wa Ndege wa KIA

$
0
0
Rais Mstaafu wa Marekani Mhe. Barack Obama akilakiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Mahiga alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa ya Kilimanjaro (KIA) akitokea hifadhi ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara alikotalii yeye na familia yake kwa muda wa siku nane, kabla ya kuelekea Afrika Kusini kwenye maadhimisho ya miaka 100 ya Nelson Mandela

PICHA: Mtazame Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Akiwa Shambani Kwake Kijijini Msoga

$
0
0
Rais Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete akikagua shamba lake la majaribio ya kilimo cha mapapai kijijini kwake Msoga, Pwani.

Breaking News: Rais Magufuli Atengua Uteuzi wa Mkuu ya Wilaya ya Kahama

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga Fadhili Nkurlu kuanzia.

Kufuatia hatua hiyo, Rais Magufuli amemteua Anamringi Macha kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama.

Anamringi Macha ametakiwa kuripoti katika kituo chake cha kazi mara moja.

Hii ni Habari Njema Kwa Wale Wote Waliohangaika na Matatizo ya Magonjwa Sugu Yaliyokosa Tiba

$
0
0
"HII NI HABARI NJEMA KWA WALE WOTE WALIOHANGAIKA NA MATATIZO YA MAGONJWA SUGU NA YALIYOKOSA TIBA" sasa usikate tamaa tiba imepatikanika kwa DK. ABDALA MUSSA anatibu matatizo kama yafuatayo:

Nguvu za kiume, uzazi, kisukari, tezi dume, vidoda vya tumbo, mgongo kuuma, miguu kuwaka moto na mataizo uliyonayo

1/ITAGULA- ni dawa ya mkosi kuosha nyota, kumvuta mpenzi, mke, mume, kuua kesi na kupata kazi haraka kama umeomba maombi serikalini au kampuni binafisi unaitwa ndani ya siku mbili 2/

NINJIWE- ni dawa inayomaliza matatizo ya wanaume heshima ndani ya ndoa, kuwa na nguvu za kiume milele na kukomaza mbegu na kuwa na uwezo kufanya tendo la ndoa zaidi ya mara 5 bila kuchoka kama umezaraulika na kufanya tendo na kusinyaa uume dawa ipo dozi yake siku sita vidoge 12 pia kuna na unga inayokomaza uume ndani ya siku 7 unapona kabisa.

3/MPALALA- ni dawa ya kutibu busha miguu kuwaka moto, kiuno, kisukari.

4/NGEKEWA- ni dawa ya kuvuta wateja kwenye biashara yoyote kuwa na wateja wengi katika biashara na kuzuia chuma ulete. 4/LINGWATA- ni dawa ya punguza unene, mafuta tumbo, matiti, miguu, hipsi na kutengeneza shepu dawa hii ni ya unga ukitumia utaona mabadiliko baada ya siku 3.

5/DUBISHO- ni dawa zindiko la mwili, majumba, gari, biashara, mteja wangu huduma utaipata mahali popote ulipo kuna wanasaplai mahali ulipo kama huna muda wa kufika osifini mkoa wa dar-es-salaam, iringa, kanda ya ziwa wilaya ya bunda. angalizo kwa wateja usitume sms wala kubipu huduma yangu ni kuanzia saa 12 asubui hadi saa 12 jioni kwa wateja wa dar-es-salaam ofisi ipo buguruni na mbagala zakhem na kwa wale walio nje ya mkoa dawa hizi mtazipata kwa njia za mabasi. punguzo la bei kwa wateja 5 wa kisukari na nguvu za kiume

KWA MAWASILIANAO ZAIDI WASILIANA NA DK. ABDALA MUSSA KWA SIM NAMBA 0767-171773/ 0716-608959 WOTE MNAKARIBISHWA:

Waziri Mkuu Akemea Mahusiano Mabaya Ya Watumishi Kahama

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekemea mahusiano mabaya baina ya watumishi wa wilaya ya Kahama na kusema wanapaswa kubadilika mara moja.

Ametoa onyo hilo jana(Jumapili, Julai 15, 2018) wakati akizungumza na watumishi na viongozi wa Halmashauri za Wilaya za Ushetu, Msalala na Kahama Mji, wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

“Hali ya mahusiano hapa Kahama ni mbaya kuliko Kishapu na Shinyanga. Mnachapa kazi vizuri lakini tatizo kubwa kila mmoja anaenda kivyake, hakuna anayemsikiliza Mkurugenzi wa Halmashauri wala Mkuu wake wa idara,” amesema.

Waziri Mkuu ambaye yuko kwenye ziara ya siku tano ya kikazi mkoani humo, amewaeleza watumishi na viongozi hao kwamba Serikali haitavumilia kuona watumishi wa aina hiyo wanaendelea kufanya kazi.

“Serikali haitavumilia kuona watumishi wakifanya mambo ya hovyo. Kahama ni wilaya yenye majaribu na Shinyanga nayo ni wilaya yenye majaribu makubwa. Kwa hiyo watumishi inabidi muwe makini, kuweni waangalifu msije mkaingia kichwakichwa kwenye majaribu haya.”

“Migogoro niliyoisikia ambayo iko hapa ni kwa sababu ninyi mmeingia kwenye biashara na kutake sides. Hapa Kahama, Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Wilaya hamuelewani, Mkurugenzi na wakuu wa idara hamuelewani, wakuu wa idara na wasaidizi wao nao pia hawaelewani,” alisema.

“Napenda kusisitiza kwamba ninyi ni viongozi wa umma, kwa hiyo ni lazima mzingatie itifaki za kiuongozi, mzingatie mahusiano mema mahali pa kazi. Hatupendi viongozi muwe chanzo cha matatizo hapa Kahama,” aliwaasa.

Alisema Kahama ina fursa kubwa na nzuri kwenye kilimo, madini, mifugo na biashara na akawataka viongozi wanaoletwa kwenye wilaya hiyo wawe makini. “Kiongozi ukiletwa hapa inabidi uwe na kichwa kilichotulia. Inabidi uwe mwaminifu sana ili uweze kudumu kwenye wilaya kama hii,” alisisitiza.

“Kama kiongozi ulizoea kwenda disco inabidi uache, kama ulizoea kwenda baa inabidi ununue kreti uweke ndani kwako. Kama ulizoea kushabikia mpira kwa kujichora chaki, sasa basi. Kaa sebuleni kwako, angalia mpira kwenye luninga yako, ndiyo dhamana ya uongozi hiyo,” alisema.

Aliwataka watumishi wa umma wawasaidie wananchi kuboresha utendaji wao kwenye kilimo, uvuvi na ufugaji ili kila kuleta tija kwenye kila sekta.

Hii ni Habari Njema Kwa Wale Wote Waliohangaika na Matatizo ya Magonjwa Sugu Yaliyokosa Tiba

$
0
0
"HII NI HABARI NJEMA KWA WALE WOTE WALIOHANGAIKA NA MATATIZO YA MAGONJWA SUGU NA YALIYOKOSA TIBA" sasa usikate tamaa tiba imepatikanika kwa DK. ABDALA MUSSA anatibu matatizo kama yafuatayo:

Nguvu za kiume, uzazi, kisukari, tezi dume, vidoda vya tumbo, mgongo kuuma, miguu kuwaka moto na mataizo uliyonayo

1/ITAGULA- ni dawa ya mkosi kuosha nyota, kumvuta mpenzi, mke, mume, kuua kesi na kupata kazi haraka kama umeomba maombi serikalini au kampuni binafisi unaitwa ndani ya siku mbili 2/

NINJIWE- ni dawa inayomaliza matatizo ya wanaume heshima ndani ya ndoa, kuwa na nguvu za kiume milele na kukomaza mbegu na kuwa na uwezo kufanya tendo la ndoa zaidi ya mara 5 bila kuchoka kama umezaraulika na kufanya tendo na kusinyaa uume dawa ipo dozi yake siku sita vidoge 12 pia kuna na unga inayokomaza uume ndani ya siku 7 unapona kabisa.

3/MPALALA- ni dawa ya kutibu busha miguu kuwaka moto, kiuno, kisukari.

4/NGEKEWA- ni dawa ya kuvuta wateja kwenye biashara yoyote kuwa na wateja wengi katika biashara na kuzuia chuma ulete. 4/LINGWATA- ni dawa ya punguza unene, mafuta tumbo, matiti, miguu, hipsi na kutengeneza shepu dawa hii ni ya unga ukitumia utaona mabadiliko baada ya siku 3.

5/DUBISHO- ni dawa zindiko la mwili, majumba, gari, biashara, mteja wangu huduma utaipata mahali popote ulipo kuna wanasaplai mahali ulipo kama huna muda wa kufika osifini mkoa wa dar-es-salaam, iringa, kanda ya ziwa wilaya ya bunda. angalizo kwa wateja usitume sms wala kubipu huduma yangu ni kuanzia saa 12 asubui hadi saa 12 jioni kwa wateja wa dar-es-salaam ofisi ipo buguruni na mbagala zakhem na kwa wale walio nje ya mkoa dawa hizi mtazipata kwa njia za mabasi. punguzo la bei kwa wateja 5 wa kisukari na nguvu za kiume

KWA MAWASILIANAO ZAIDI WASILIANA NA DK. ABDALA MUSSA KWA SIM NAMBA 0767-171773/ 0716-608959 WOTE MNAKARIBISHWA:

Waziri Mkuu Aongoza Harambee Ya Papo Kwa Papo Kahama.....Achangisha mifuko 2,000 ya saruji ujenzi wa uzio wa sekondari

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amechangisha mifuko 2,000 ya saruji na sh. milioni 50 kwenye harambee ya papo kwa papo kwa ajili ya ujenzi wa uzio wa sekondari ya Mwendakulima wilayani Kahama.

Waziri Mkuu ameendesha zoezi hilo jana (Jumapili, Julai 15, 2018) wakati akizungumza na walimu na wanafunzi wa sekondari ya Mwendakulima, wilayani Kahama mkoani Shinyanga ambako alienda kupokea mabweni mawili ya wasichana.

Ujenzi wa mabweni hayo yenye uwezo wa kulaza wanafunzi 126, umegharimu sh. milioni 560 na umefadhiliwa na kampuni kuchimba madini ya ACACIA kupitia fedha za Corporate Social Responsibility. Mabweni ya awali yaliteketea kwa moto.

Waziri Mkuu ameendesha harambee hiyo baada ya kuombwa na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mwendakulima, Bi. Neema Mfunya. Kwa wastani, mfuko mmoja wa saruji unagharimu sh. 16,500.

Katika harambee hiyo, Waziri Mkuu alichangaia mifuko 500 ya saruji, huku kampuni ya ACACIA ikichangia mifuko 400 kutoka kwa watumishi wake. MNEC wa Simiyu, Bw. Emmanuel Nsangali aliahidi kuchangia mifuko 200.

Ahadi nyingine zilizotolewa na Naibu Mawaziri, wabunge, na wakuu wa taasisi waliombatana na Waziri Mkuu kwenye ziara yake zilikuwa ni za mifuko 50 hadi 100.

Shule ya sekondari ya Mwendakulima ina wanafunzi 336 wa kidato cha tano na cha sita. Lakini kwenye kidato cha kwanza hadi cha nne, shule hiyo ina wanafunzi 771 ambao kati yao, wavulana ni 423 na wasichana ni 348.

Ufaransa Bingwa Mpya Kombe La Dunia 2018

$
0
0
Hatimaye kiama cha michuano ya Kombe la Dunia Urusi kimefikia mwisho jana kwa timu ya taifa ya Ufaransa kuweza kutwaa Kombe hilo kwa kuifunga Croatia mabao 4-2.

Mabao ya Ufaransa yaliwekwa kimiani na Mario Mandzukic aliyejifunga, Antoine Griezmann aliyefunga kwa njia ya penati pamoja, Paul Pobga pamoja na Kylian Mpabbe.

Wakati huo mabao ya Croatia yalipachikwa kimiani na Ivan Perisic pamoja na Mario Mandzukic aliyesahihisha makosa yake kwa kuifungia timu yake bao la pili.

Ubingwa huo kwa Ufaransa unakuwa wa pili baada ya kuutwaa pia katika mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 1998 nchini kwao.

Kocha wa timu hiyo, Didier Deschamps amekuwa miongoni mwa makocha watatu kutwaa ubingwa huo kama mchezaji na Kocha baada ya Mbrazil Mario Zagallo na Mjerumani Franz Beckenbauer.

Vilevile Ufaransa imekuwa timu ya kwanza kufunga mabao manne katika fainali hizo tangu Brazil iifunge Italia 4-1 mwaka 1970.

Mtaalam na Bingwa wa Magonjwa Yote Sugu Yaliyoshindikana Kama Vile Pumu, Vidonda vya Tumbo, Bush's, Nguvu za Kiume

$
0
0
MTALAAM NA BINGWA WA MAGONJWA YOTE SUGU NAYALIYOSHINDIKANA KAMA VILE PUMU, VIDONDA VYA TUMBO, BUSHA, NGUVU ZA KIUME, KISUKARI,MIVUTO YOTE, KUSAFISHA NYOTA, KURUDISHA MALI, NK.

Tatizo la upungufu ukosefu wa nguvu za kiume, maumbile madogo ya uume limekuwa kubwa kwa lika zote hapa duniani

Matatizo hayo sio mageni kigeni ni ile tiba sahihi yakutibu na kuponya haya.chanzo cha hayo matatizo ni:KISUKARI, NGIRI,CHANGO, TUMBO KUUNGURUMA NA KUJAA GESI, KIUNO KUUMA, MAUMIVU YA MGONGO,MAGONJWA YA ZINAA, KORODANI KUVIMBANAKUUMA,VIDONDA VYA TUMBO, NK.

Tiba sahihi nabora ya tatizo la nguvu zakiume ni 3Power,;Nidawa ya vidonge asilia vilivyotengenezwa kwa kiwango bora na salama kwa ajili yakutibu mojakwamoja tatizo la nguvu za kiume maradufu

1,hutibu nguvu za kiume mda mfupi sana kati ya umri wa miaka 18-85 naitakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dk 20 hadi 40 tendo lakwanza bila kuchoka naitakufanya uwe nahamu yakuendelea na tendo la ndoa zaidi ya mara 5 bila hamu kuisha.

FINA Power: Nidawa yakuboresha maumbile ya kiume kwa kunenepesha na kurefusha kwa saizi uipendayo inchi 6,7 hadi 8 kwa mda mfupi sana.dawa hizi huanza kufanya kazi kwa mda wa dk 67 ukisha tumia guarantee miaka 55 ikishakutibu.

Pia tunatibu,KISUKARI, PRESHA, UZAZI, NGIRI, PUMU,MALARIA SUGU, VIDONDA VYA TUMBO, CHANGO AINA ZOTE, BP, BUSHA BILA UPASUAJI NK.

ISHOSHA,Nidawa ya mvuto wa biashara,kazi,hupandisha cheo humfanya mfanyakazi apendwe na mwajiri wake,humvuta mme,mke,hawara,mchumba,unaemhitaji au hakutaki hatimizi ahadi zako kwa dhati utampata kwa mda wa dk 45 tu naatatulia milele nakumfunga asitoke inje ya ndoa.

SHEPU EXRA,Nidawa ya yakupunguza matiti,unene tumbo,kitambi kwa akina baba,hutoa mafuta mabaya mwilini,makovu sehemu mbalimbali mwilini,chunusi sugu,minyama uzembe,michirizi mwilini,nakuongeza makalio hips,mguu wa bia nk.

HUDUMA HIZI NANYINGINE NYINGI MTALAAM BINGWA DR SHEIKH OMARY
Anapatikana dar magomeni moroco hotel
SIMU NO 0767 14 53 57/0629 03 45 50.

NAKAMA NAFASI YAKUFIKA OFISINI HAIPO UTALETEWA HAPO ULIPO.

PICHA: Ufaransa walivyosherehekea Ubingwa wao wa pili wa World Cup 2018

$
0
0
Ufaransa walivyosherehekea Ubingwa wao wa pili wa World Cup 2018

Harry Kane abeba tuzo ya mfungaji bora Kombe la Dunia 2018

$
0
0
Nahodha wa England, Harry Kane ameibuka mfungaji bora wa michuano ya mwaka huu ya Kombe la Dunia, baada ya kutupia mabao sita wavuni.

Yakiwa ni mashindano yake ya kwanza, Straika wa Tottenham, ameingia katika rekodi kwa kuwa mchezaji wa pili wa England kuwahi kutwaa tuzo hiyo, baada ya Gary Lineker, aliyeitwaa mwaka 1986, alipotupia mabao sita wavuni. 

Kane alifunga mabao mawili zaidi ya Romelu Lukaku, Kylian Mbappe, Denis Cheryshev, Cristiano Ronaldo na Antoine Griezmann.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24, alifunga mabao matatu tu kwa njia ya kawaida huku mengine matatu yakiwa ni penalti. 

England walimalizA katika nafasi ya nne, baada ya kupigwa 2-0 na Ubelgiji kwa mabao ya Thomas Muernier na Eden Hazard.

Tiba Bora ya Tatizo Sugu la Nguvu za Kiume

$
0
0
OFA! Je umepungukiwa nguvu za kiume na umetumia dawa bila mafanikio? Sasa utapona kwa sh 15000 tu .Ofa ni kwa watu kumi wakwanza kila siku .Ofa hii itadumu ndani ya wiki 2 baada ya hapo bei itakuwa nyingine na kama hujapona tunakurudishia hela yako !

Dawa hii ni dawa ya maajabu, huwezi kuamini Ila wengi wameiamini,inatibu tatizo la upungufu wa nguvu za kiume na utapewa garantee ya mwezi mmoja 

Dawa hii inapatikana hapo hapo ulipo nyumbani kwako na tutakupatia maelezo ya namna ya kuiandaa wewe mwenyewe na baada ya kuiandaa utakunywa Mara moja tu,na hautatumia dawa yoyote ya nguvu za kiume 

Dawa hii inawafaaa watu kuanzia miaka 18 mpaka miaka 70 zaidi ya miaka hyo haitakusaidia 

Ni dawa ya asilia, haina madhara yoyote,watafiti na waganga wameikubali pia hii dawa inawafaa hata wanawake wasiopata hisia za mapenzi

Pia tunaweza kukutumia dawa popote ulipo lakini s kwa bei ya ofa, ukiitumia dawa hii unakuwa na uwezo wa kurudia tendo la ndoa zaidi ya Mara 3 bila hamu kuisha na itakufanya uwe na uwezo wa kufanya tendo la ndoa muda wowote 

Imesaidia watu zaidi ya 148 ndani ya mwaka mmoja tangu igunduliwe  na Dr kiboko mganga wa tiba za jadi toka kisiwani mafia 

Pia tunatibu magonjwa mbalimbali, kurudisha mpenzi aliye kuacha,biashara iliyoyumba, nk 

OMBI LANGU; kwanza naomba radhi kwa watu wanaofika kwenye ofisi yangu na kuchelewa kupata huduma kutokana na foleni ya watu wengi kuja pia pongezi nyingi nimepata kutokana na mafanikio makubwa wanayoyapata baada ya kutumia hii dawa ombi langu naomba upige cm nikuelekeze hii dawa hapohapo kuepuka usumbufu na kuokoa mda wako asante

Maelezo zaidi ; Dr kiboko-  0679923297

Kylian Mbappe ashinda tuzo ya mchezaji bora Chipukizi Kombe la Dunia 2018.

$
0
0
Kiungo wa Ufaransa na Paris Saint-Germain, Kylian Mbappe, ametangazwa kuwa ndiye mshindi wa tuzo ya mchezaji bora chipukizi katika fainali Kombe la Dunia 2018 iliyofanyika jana.

Licha ya kuvunja rekodi nne kwenye michuano hii, ikiwa ni pamoja tuzo ya mchezaji mwenye umri mdogo kuwahi kucheza kombe la dunia, rekodi ya kinda aliyewahi kufunga mabao mawili kwenye Kombe la Dunia, rekodi ya kinda aliyefunga kwenye mechi ya fainali na rekodi ya kutwaa kombe, Mbappe ndiye mchezaji bora wa mashindano haya.

Mbappe amekuwa mchezaji wa pili wa Ufaransa kuwahi kushinda tuzo hiyo, baada ya Paul Pogba aliyeshinda tuzo hiyo miaka minne iliyopita. Tuzo hiyo inaweza ikashindwa na mchezaji aliyezaliwa na baada ya Januari mosi.

Kigezo kingine kinachotumiwa kupata mshindi wa tuzo hiyo ni ufundi uwanjani, kasi, utundu udambwidambwi, mchango kikosini na uungwana mchezoni, kwa mujibu wa kamati ya ufundi ya FIFA. 

Mbappe amefunga mabao manne kwenye michuano hii, ikiwemo bao la nne, katika ushindi walioupata kwenye fainali dhidi ya Croatia.

Thibaut Courtois Ashinda Tuzo ya kipa bora wa Dunia -World Cup 2018

$
0
0
Kipa wa Chelsea na Ubelgiji ameondoka nchini Russia akiwa shujaa na mfalme, licha ya timu yake kushindwa kuingia mechi ya fainali, baada ya kutawazwa kipa bora wa michuano hiyo, iliyomalizika rasmi jana.

Kipa huyo, amekuwa na kiwango bora katika michuano ambapo katika mechi ya kwanza, aliiongoza Ubelgiji kuisulubu Panama 3-0, huku wakiitungua England mara mbili (1-0, 2-0), huku akimzuia mchezaji bora wa mashindano hayo, Harry Kane.

Courtois anayewindwa na Real Madrid, aliwabwaga kipa wa Ufaransa, Hugo Lloris na Kipa wa Croatia, Danijel Subasic. Baada ya kutangazwa mshindi wa tuzo hiyo, Courtois aliandika maneno haya kwenye ukurasa wake wa mtandao wa twitter:

 "Moja ya mafanikio makubwa kabisa katika maisha ya mchezaji ni kutambuliwa na kupewa tuzo, nimefarijika kushinda tuzo ya kipa bora. Ahsanteni sana."

Makipa wengine ambao waliwahi kushinda tuzo hii, ni Kipa wa Ujerumani Manuel Neuer, aliyeishinda mwaka 2014. Wengine ni Iker Casillas, Gianluigi Buffon, Oliver Kahn, Fabien Barthez, na Michel Preud'homme.

Dawa Za Nguvu Za Kiume Na Kukosa Hamu Ya Tendo La Ndoa

$
0
0
Asilimia 45-80 ya wanaume wapo tofauti na wengine kwa kutowatimizia vyema wake au wapenz wao na kuwasababishia kutoka nje ya mahusiano yao. 

NINI CHANZO CHA HAYO? Kupiga punyeto,Ngiri, Vidonda vya tumbo, Korodani moja kuvimba, Msongo wa mawazo, Presha, Magonjwa ya zinaa, Kufanyiwa tohara ukiwa na umri mkubwa, Kisukari. 

DR. LUTAJA Sasa anakuletea tiba sahihi ya tatizo la Nguvu za kiume. 

NTOMBO :Hii hutibu na kuponya kabisa tatizo la Nguvu za kiume, utakuwa na uwezo wa kufanya tendo la ndoa zaidi ya mara tatu bila kuchoka na itakufanya uchelewe kafika kileleni kwa mda wa dk 20-45. Dawa hii imechanganywa na miti 18,Hata wazee wenye umri mkubwa wa zaidi ya miaka 85 wanapona kabisa okoa mahusiano yako, ndoa yako sasa. 

SUNGURURU MIX:Ndio tiba sahihi kwa wale wenye maumbile madogo hurefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo nchi 3-8 na unene cm 2-5,dawa hii ipo katika mfumo wakupaka nakunywa na haina madhara yoyote kwa mtumiaji :Hii ni tiba tofauti kabisa nazile ambazo umekwisha wahi kutumia. 

Pia tunadawa za Kupandisha nyota , Uzazi, Pumu, Malaria sugu, miguu kuwaka moto, Kaswende, Kisonono pamoja na mvuto wa mpenzi.

 DR. LUTAJA ANAPATIKANA DAR-ES-SAALAM Simu 0713-821823 kwa wale wa mikoani huduma hii utaipata popote ulipo.

Luca Modric ndio mchezaji bora wa Kombe la Dunia 2018

$
0
0
Kiungo  na Nahodha wa Timu ya Taifa ya Croatia, Luka Modric ameibuka mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 na kupewa Mpira wa Dhahabu wakati timu yake ikipoteza mchezo wao wa fainali kwa kukubali kichapo cha bao 4-2 kutoka kwa Ufaransa huko Urusi.

Modric ambaye amemaliza mashindano akiwa na mabao mawili, ameisaidia timu yake kutinga fainali ikiwa ni mara ya kwanza kwa timu hiyo kufikia hatua hiyio kubwa ya kihistoria.

Modric amewashukuru mashabiki wa Croatia na wachezaji wenzake kwa sapoti kubwa waliowapa hadi kufikia fainali licha ya kufungwa.

Mbelgiji, Eden Hazard amekuwa mchezaji Bora wa Pili na kutunukiwa mpira wa Silver, na Mfaransa, Antoine Griezmann ameibuka mchezaji Bora wa Tatu na kupewa mpira wa shaba.

Wachezaji wengine ambao wamewahi kubeba tuzo hiyo ni pamoja na Lionel Messi, Zinedine Zidane, Ronaldo de Lima, Davor Suker, Diego Maradona na Paolo Rossi. 

Tuzo hii, inamuweka Modric katika nafasi nzuri ya kushinda tuzo ya mwaka huu ya Ballon d'Or.

Tundu Lissu Awaasa Wafuasi CHADEMA....."Hatuna wa Kumlilia, Ni Lazima Tupambane Wenyewe"

$
0
0
Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA), Tundu Lissu amewataka wanachama na viongozi wa chama hicho kutumia vizuri fursa ya uchaguzi mdogo wa marudio uliopangwa kufanyika Agosti 12 mwaka huu kwa kupambana kiakili ili waweze kushinda chaguzi hiyo.

Lissu ametoa kauli hiyo jana Julai 15, 2018 kupitia ukurasa wake maalum wa kijamii na kusema uchaguzi huo wa marudio katika Jimbo la Buyungu Mkoani Kigoma na kata 77 Tanzania Bara ni fursa kwao kuendelea kupigania haki za wananchi na utawala bora.

"Hakuna uchaguzi mdogo, kila uchaguzi ni muhimu katika mazingira halisi ya sasa ya kisiasa. Uchaguzi wa marudio wowote ule una kuwa na ugumu wa kipekee, tutafanyiwa na tayari tunafanyiwa kila aina ya fujo na CCM na mawakala wake kwenye Tume ya Uchaguzi na vyombo vya dola", amesema Lissu.

Pamoja na hayo, Lissu ameendelea kwa kusema "wajibu wetu ni kupambana kwa akili na maarifa ya hali ya juu ili kuzishinda fujo hizo na kushinda chaguzi hizo. Najua ni kazi ngumu, haijawahi kuwa rahisi mahali popote. Hatuna mjomba au shangazi wa kutufanyia kazi hii, au wa kumlilia baadaye tusipoifanya vizuri. Ni jukumu letu pekee".

Kauli hiyo ya Tundu Lissu imekuja yakiwa yamepita masaa machache tangu dirisha la kuanza kupiga kampeni kufunguliwa kwa kuomba ridhaa ya wananchi katika maeneo ambayo yatakuwa yana uchaguzi nchini Tanzania ifikapo Agosti 12 mwaka 2018.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images