Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Kombe la Dunia 2018: Uingereza Italipa kisasi leo kwa ubelgiji?

$
0
0
Na Magdalena Kashindye:
Michuano ya kombe la dunia iliyoanza Juni 14 nchini Urusi itafikia tamati kesho Jumapili, Julai 15 kwa mchezo wa fainali kati ya Ufaransa dhidi ya Croatia.

Na leo  Jumamosi, saa 11 jioni kutakuwa na mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu kati ya Uingereza na Ubelgiji.

Timu hizo zinazokutana kwa mara ya pili kwenye michuano ya mwaka huu zilikutana hatua ya makundi na Ubelgiji ilishinda mchezo huo kwa goli 1_0.

Timu hizo zinakutana baada ya kutolewa hatua ya nusu fainali Ubelgiji akifungwa na ufaransa 1_0 na uingereza akifungwa na Croatia 2_1.

Mtoto wa miaka 7 abakwa na Baba yake mzazi

$
0
0
Mtoto wa kike mwenye miaka saba amelazwa katika hospitali ya kata ya Marimanti nchini Kenya baada ya kunajisiwa na baba yake kabla ya kukimbia.

Akizungumza kutoka hospitali ambako alikuwa amempaleka msichana, mama yake alisema ni bahati mbaya kwamba baba anaweza kumfanyia binti yake kitendo kiovu namna hiyo.

Alisema mumewe alikuja nyumbani jioni na kuanza kugombana juu ya mtoto wao wa mwezi mmoja akisema kuwa hakuwa wake.

Alimwaga chakula ambacho mke wake alikuwa amemtayarishia kabla ya kumshukia kwa mateka na makofi.

“Sikuweza kuvumilia hili na nililazimika kukimbilia kwenye vichaka vya karibu. Wakati huo ambao sikuwepo alianza kuwapiga watoto wengine na kumtia unajisi msichana kabla ya kukimbilia, “ alisema Mama

Ilikuwa baada ya hayo mama wa msichana alikuja na kumpeleka hospitali. Afisa wa kliniki Bernard Mwenda ambaye alimhudumia msichana alisema uchunguzi ilithibitisha msichana alibakwa.

“Msichana alikuwa na mipasuko katika sehemu zake za siri lakini tunahitaji uchunguzi zaidi ili kujua kiwango cha majeruhi yake. Tunaweza kulazimishwa kumpeleka hospitali ya rufaa ya Chuka kwa matibabu zaidi,” alisema.

Mama wa msichana pia ana wasiwasi kuwa mumewe anaweza kurudi wakati akiwa hospitalini na kuendelea kuwatenda vibaya watoto wengine wawili walioachwa nyuma.

“Ningependelea watoto kupelekwa mahali salama na polisi au hata Wasamaria wema kwa sababu anaweza kurudi na kuwatenda vibaya wengine wawili,” alisema.

Mkurugenzi wa polisi wa Tharaka wa Kusini Walter Abondo alithibitisha tukio hilo na kuongeza kuwa harakati za kumsaka mtuhumiwa tayari zimekwisha anza.

“Hatuwezi kurudi nyuma katika kumtafuta mtuhumiwa na tutampata popote alipojificha,” alisema.

Ajali ya Gari Yaua Diwani na Dereva Huku Mkurugenzi na Wengine Wakijeruhiwa

$
0
0
Diwani wa Kata ya Manuzi, Elias Shukia na dereva wa halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Haruna Ngata wamefariki dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutoka koani Dodoma, kupasuka tairi na kupinduka mara tatu.

Taarifa za awali kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Mtaturu zinaelea kuwa ajali hiyo imetokea  eneo la Mkiwa, Wilayani Singida.

 Mtaturu amesema mkuregenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Meatu,  Fabian Manuzi; mwenyekiti wa halmashauri hiyo,  Piuz Machungwa na watu wengine wanne wamejeruhiwa katika ajali hiyo.

Amesema majeruhi wanne wamelazwa katika hospitali ya St Gasper iliyopo Itigi na wawili wamelazwa hospitali ya Puma iliyopo wilayani Ikungi.

“Chanzo tulichokiona kwenye eneo la tukio ni kupasuka kwa tairi la mbele kushoto, hata hivyo tuwasubiri polisi wafanye uchunguzi zaidi watatuambia chanzo cha ajali yenyewe,”amesema.

Kumbe mzungu wa Nisha Zilikuwa ni Kiki za Wimbo Mpya....Utazame Hapa

$
0
0
Msanii wa filamu na muziki, Nisha Bebee baada ya kuonekana na mzungu na kudai kwamba ni mpenzi wake mpya, Ijumaa hii ameachia video ya wimbo wake mpya uitwo Yeye ambapo ndani yake anaonekana mzungu huyo akicheza matendo.

Mbunge wa Tunduma (Chadema), Frank Mwakajoka Atiwa Mbaroni

$
0
0
Mbunge wa Tunduma (Chadema), Frank Mwakajoka amekamatwa na Polisi akiwa kwenye kituo kikuu cha polisi Tunduma alikokwenda kuomba ulinzi.

Mbunge wa Mbozi (Chadema), Pascal Haonga amesema mbali na Mwakajoka, pia Katibu wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha) Mkoa wa Songwe, Ayub Sikagonamo naye amekamatwa.

“Pia wapo baadhi ya madiwani, wanachama wa Chadema na walinzi wa chama nao wamekamatwa,” amesema.

Amesema Mwakajoka na Sikagonamo leo asubuhi  walipanga kwenda ofisi za Halmashauri ya Tunduma kwa ajili ya kuchukua fomu za wagombea wa udiwani katika kata tano, lakini ofisi hizo zilikuwa zimezingirwa na polisi.

“Kutokana na hali hiyo Mwakajoka akiwa na Sikagonamo waliona kuliko kwenda eneo hilo na kuonekana wanakwenda kufanya vurugu, waliamua kwenda kuonana na mkuu wa kituo ili awape ulinzi wa askari,” amesema Hainga.

“Ila walipofika (Mwakojoka) alielezwa kuwa jana usiku alifanya kikao na wenzake kwa lengo la kufanya maandamano hivyo anawekwa chini ya ulinzi, basi wakawekwa ndani hadi muda huu.”

Amesema hatua waliyoichukua ni kuwasiliana na uongozi wa juu wa chama hicho sambamba na kufanya taratibu za dhamana.

Haonga amesema hadi leo saa 7 mchana hakukuwa na mgombea udiwani wa Chadema aliyechukua fomu  ya kugombea kwa kile alichokiita mizengwe inayofanyika, ikiwa ni pamoja na kukamatwa lwa wagombea walioteuliwa na chama hicho kikuu cha upinzani nchini.

VIDEO: Rais Magufuli Akiwaapisha Kamshina Jenerali wa Magereza

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli, leo Julai 14, 2018 amemuapisha Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Martin Kasike. Tukio hilo limefanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Kabla ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo ambayo awali ilikuwa ikishikiliwa na Dkt. Juma Alli Malewa, ambaye amestaafu Julai 06, 2018 , Kamishina Jenerali , Kasike, alikuwa Naibu Kamishna wa Magereza.

==>Tazama hapo chini

Rais Magufuli Amwapisha kamishna Mpya wa Magereza jenerali Phaustine Kasike na Kumpa Maagizo Mazito

$
0
0
Rais John Magufuli amemtaka Kamishna Jenerali mpya wa Jeshi la Magereza,  Phaustine Kasike kuchapa kazi kumaliza changamoto zinazolikabili jeshi hilo.

Kiongozi Mkuu huyo wa nchi ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Julai 14, 2018 Ikulu jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kumuapisha kamishna huyo na Balozi Joseph Sokoine ambaye ameteuliwa kuwa naibu katibu mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

“Nakupongeza kidogo, lakini pole ndio nyingi,” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amemtaka Kasike kuhakikisha wafungwa wanafanya kazi ipasavyo, wazuie matumizi ya simu gerezani, washiriki katika shughuli za kilimo na ujenzi, wazuie kufanya biashara na kushiriki katika matukio ya wizi wakiwa gerezani.

Lugola Ampa Matumaini Rais Magufuli....Amuahidi Sasa Atapata Ahueni na Usingizi Mnono

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amemhakikishia Rais John Magufuli kuwa atapambana na ajali za barabarani na kwamba zitapungua na kwisha kabisa ndani ya muda mfupi ujao.

Siku chache zilizopita wakati wa kuwaapisha mawaziri pamoja na viongozi mbalimbali aliowateua Magufuli alisema amechoka kutoa rambirambi kutokana na mfululizo wa ajali  za barabaran hususani Mkoa wa Mbeya.

Lugola amesema hayo  leo Julai 14 wakati Rais akimuapisha Kamishna Jenerali wa Jeshi la magereza Phaustine Kasike na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais na Muungano Joseph Sokoine viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.  

“Ulivyoniapisha yapo mambo ya msingi ambayo ulinielekeza niyafanyie kazi nataka nikuhakikishie mambo hayo nimeshaanza kuyafanyia kazi, pamoja na makatibu wangu,”amesema na kuongeza kuwa:

“Ili kuonyesha kwamba tumeyapa uzito na kuanza kuyatekeleza pasipo mzaha tayari kwenye upande wa ajali tumeshaanza kuchukua hatua na nataka nikuthibitishie kwamba utapata usingizi na hata salamu za pole zitapungua na zitakwenda kwisha kabisa ndani ya muda mfupi ujao.”

Kingine alizungumzia kuhusu  mikataba ya hovyo ya kifisadi na kulidhalilisha taifa.

“Hatuwezi kuwa na tuhuma za Watanzania zisizoisha na kuleta sintofahamu,  vitendo hivi lazima vifike mwisho, hivyo nakuahidi kwa kuwa umeniamini na mimi nitafanya kazi bila kujali nafasi ya mtu wala upendeleo,”amesema.

Ubelgiji Yatwaa Nafasi Ya Tatu Kombe La Dunia Baada Ya Kuitandika England 2-0

$
0
0
Timu ya taifa ya England imepoteza mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu kwenye fainali za kombe la dunia kwa mara ya pili, baada ya leo kukubali kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa timu ya taifa ya Ubelgiji.

Mara ya mwisho England kufika hatua hii ilikuwa mwaka 1990, ambapo ilipoteza katika mchezo wa kumsaka mshindi wa tatu baada ya kufungwa na Italia mabao 2-1. Hivyo leo imerudia tena historia hiyo kupitia mabao ya Thomas Meunier  na Eden Hazard.

Kwa upande wa Ubelgiji ikiwa na kizazi cha dhahabu chenye majina kama Hazard, De Bruyne, Lukaku, Kompany na Courtois wamefanikiwa kupata nafasi ya juu zaidi katika historia ya taifa hilo kwenye kombe la dunia ambayo ni kumaliza katika nafasi tatu.

Baada ya kupoteza mechi ya nusu fainali dhidi ya Croatia na leo dhidi ya Ubelgiji, England sasa imepoteza mechi mbili mfululizo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2014 ilipofungwa na Italia pamoja na Uruguay katika mechi za fainali za kombe la dunia nchini Brazil.

Mchezaji Eden Hazard wa Chelsea na Ubelgiji ameifikia rekodi ya nyota wa zamani wa taifa hilo Jan Ceulemans ya kuhusika kwenye mabao 7 katika fainali za kombe la dunia. Hazard amefunga mabao 3 na kusaidia mengine manne.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya July 15

Mwamuzi wa fainali Ufaransa Vs Croatia ajulikana, achambuliwa

$
0
0
Shirikisho la Soka Duniani (Fifa), limemtaja mwamuzi atakayechezesha mchezo wa fainali wa Kombe la Dunia, Ufaransa dhidi ya Croatia, utakaoshuhudiwa kwenye uwanja wa Luzhniki nchini Urusi, Jumapili hii.

Nestor Pitana ambaye ni raia wa Argentina mwenye uzoefu, ndiye atakayepuliza kipyenga ndani ya dimba Jumapili hii ikiwa ni mechi yake ya tano nzito kwenye Fainali za Kombe la Dunia.

Pitana mwenye umri wa miaka 43 amepata nafasi hiyo kutokana na historia yake ya kumudu mechi ngumu, akianza na mechi ya ufunguzi kati ya wenyeji Urusi na Saudi Arabia kwenye uwanja huohuo.

Anakuwa mwamuzi wa pili kutoka Argentina kuchezesha mechi kubwa zaidi kwenye ulimwengu wa Soka akimfuatia Horacio Elizondo aliyeweka rekodi mwaka 2006.

Pitana alikuwa kwenye jopo la waamuzi kwenye Fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil miaka minne iliyopita, na hii itakuwa mechi ya tano, akiwa na rekodi nzuri alipochezesha mchezo wa robo fainali kati ya Ufaransa na Uruguay.

Wadau wa soka wamemteta Pitana, wengi wakionekana kumkubali kutokana na historia yake nzuri.

    Mugabe amuahidi mpinzani mabilioni, magari kuendeshea kampeni

Mchezaji wa Croatia, Ivan Rakitic amemzungumzia Pitana akikumbuka alivyoumudu mtanange kati ya kikosi cha timu yake dhidi ya Denmark kwenye hatua ya mzunguko wa timu 16.

“Nilifurahi kusikia atakuwa mwamuzi wa fainali. Tulikuwa na bahati kumuona akichezesha mchezo kati yetu na Denmark. Sio tu kwamba tulishinda lakini alikuwa vizuri. Wasaidizi wake pia walikuwa wazuri sana,” amesema Ivan Rakitic.

Pitana atasaidiwa na waamuzi wa pembeni Hernan Maidana na Juan Pablo Belatti. Massimiliano Irrati wa Italia atasimamia upande wa uamuzi wa kutumia video, Video Assistant Referee (VAR).

Mabasi 47 Ya Kampuni ya Mohamed Trans Kupigwa Mnada Kufidia Mkopo

$
0
0
Kampuni ya Udalali ya MEM imetangaza kuyauza mabasi 47 ya Kampuni ya Mohamed Trans, baada ya mmiliki wake kushindwa kurejesha mikopo anayodaiwa.
 
Mkugenzi wa Kampuni ya MEM, Eliezer Mbwambo, alisema mabasi hayo yatanadiwa kwenye mnada wa hadhara Julai 21 na 28, mwaka huu, mkoani Shinyanga.

Alisema mbali na mabasi hayo, pia watauza viwanja na nyumba ambavyo vinamilikiwa na mfanyabiashara huyo.

“Kwa idhini tuliyopewa na Nzaro Nuhu Kachenje ambaye ni msimamizi wa Kampuni ya Mohamedi Trans Ltd, tutauza kwa mnada wa hadhara mabasi na nyumba. Mnada utafanyika sehemu nyumba na mabasi yalipo,” alisema Mbwambo.

“Mabasi 47 yako kwenye yadi ya Mohamed Trans Shinyanga na basi moja liko kwenye yadi ya MEM Mikocheni wakati kiwanja na nyumba viko kwenye kiwanja kimoja Nyegezi jijini Mwanza,” alisema.

Alitaja vingine vitakavyouzwa kuwa ni pamoja na viwanja na nyumba vilivyoko kwenye kiwanja namba 557 eneo la Ngokolo, Shinyanga.

Mmoja wa wafanyabiashara wa mabasi ambaye hakutaka jina lake litajwe  alisema biashara yao imeyumba na hali hiyo huenda itawakuta wamiliki wengi wa mabasi.

“Watu wanaweza kudhani sisi wafanyabiashara wa mabasi tunapata sana lakini hali haiko hivyo. Watu wengi wana mikopo wanashindwa kuirejesha. Ni suala la muda tu, wengi tutafika huko alikofikia mwenzetu,” alisema.

Aidha, alisema biashara hiyo ni ngumu kwa sababu mmiliki analazimika kuagiza mabasi mapya na ya kisasa kila baada ya muda ili kujihakikishia kuwa na wateja wa kudumu muda wote.

“Huyu mwenzetu mabasi yake ni yale yale ya miaka yote. Sasa watu wameshaingiza matoleo mapya mengi tu, nani atapanda Marcopolo la miaka hiyo? Hii biashara si ya kuingia kichwa kichwa unaweza kushindwa kulipa mikopo,” alisema mtoa habari huyo.

Mwakyembe Akutana na Wasanii Kujadili Changamoto ya Kanuni mpya za BASATA za mwaka 2018

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison G. Mwakyembe (Mb) jana tarehe 14 Julai, 2018 amekutana na viongozi wa Shirikisho la Muziki, Shirikisho la Sanaa za Ufundi, Shirikisho la Sanaa za Maonyesho, Shirikisho la Filamu, Chama cha Muziki wa Kizazi Kipya na Chama cha Muziki wa Dansi na wanasanaa kujadili utekelezaji wa Kanuni mpya za BASATA za mwaka 2018 uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kikao kilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa, Katibu Mtendaji wa BASATA na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu. 

Kikao hicho kilijadili masuala mbalimbali yaliyomo katika Kanuni hizo pamoja na changamoto zinazowakuta wanasanaa nchini.

Wadau walichangia hoja zao ikiwemo changamoto ya tozo ya kazi za sanaa kwa mtangazo (branding) ya shs. milioni 5 ambayo wamesema itanyima fursa za kupata kazi za matangazo.

Waziri Mwakyembe akijibu hoja hizo alisema Kanuni hizo zilipitia hatua zote ikiwemo kuwashirikisha wadau wote katika hatua za awali na kabla hazijasainiwa.

"Ninayo majina ya wanasanaa walioshirikishwa kwenye vikao vya wadau, hata hivyo wasanii wengi wamekuwa na tabia ya kutoitikia wito na baadaye huja na malalamiko baada ya maamuzi kuwa yameshafanyika", alisema Waziri Mwakyembe.

Kuhusu suala la tozo ya matangazo, Waziri Mwakyembe ameamua kuunda kamati ndogo ya wasanii ambayo itakutana na BASATA kujadili njia mbadala ya tozo hiyo.

Waziri Mwakyembe ameelezea kwamba Kanuni mpya pia zimeongeza muda wa kumbi za muziki zilizo wazi kufungwa saa 6:00 usiku kwa siku za kazi na saa 8:00 usiku kwa wikiendi na siku za sikukuu.

Akijibu kuhusu Utekelezaji wa hoja hiyo ya tozo ya matangazo, Katibu Mtendaji wa BASATA alisema tozo hiyo haizihusu asasi na kampuni za wasanii zilizosajiliwa ambazo zinaweza kujihusisha na matangazo.

Aidha, Katibu Mtendaji wa BASATA ameelezea kwamba tozo ya kumbi za maonyesho pia hiziwahusu wasanii waliosajiliwa na kampuni/asasi wanazozimiliki na kusajiliwa na BASATA.

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu amewata wanasanaa kuzingatia taratibu zilizopo wanapoandaa matangazo yao.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo alisisitiza umuhimu wa Vyama, Mashirikisho na BASATA kuwa utaratibu wa kukutana mara kwa mara na kujenga mawasiliano bora ambayo yatakuwa ni daraja katika kutatua changamoto zao mapema.

Mwakyembe Awataka wasanii kung’oa mabango yenye picha zao

$
0
0
Waziri wa Habari, Sanaa na Utamaduni, Harrison Mwakyembe amesema msanii ana haki ya kuliondoa bango la matangazo yenye picha yake, iwapo limepitiliza muda wa mkataba.

Ameyasema hayo jana Julai 14, alipozungumza na wadau wa Sanaa jijini Dar es Salaam.

Mwakyembe aliyasema hayo baada ya msanii wa muziki, (Kibonge Mwepesi) kudai kwamba kuna baadhi ya watangazaji wanaofanya kazi na wasanii huacha mabango barabarani na kupitiliza muda wa mkataba waliokubaliana.

“Utakuta msanii kaingia mkataba wa mwaka mmoja lakini bango linakaa hata miaka mitatu, huku msanii akiwa hambulii chochote,” alisema

Akilijibu hilo, Waziri Mwakayembe alisema msanii anayefanyiwa hivyo ana haki ya kuwahoji watangazaji hao na ikiwezekana hata kuyaondoa mabango.

"Moja ya sababu ya kuzibana kampuni zinazofanya matangazo na wasanii ni kutokana na kuwanyonya kwa muda mrefu wasanii wetu,” alisema.

Aliongeza: “Hili nimeliona kwa Msanii Mzee Majuto, ambapo yeye kuna moja ya tangazo limekaa miaka mitano barabarani lakini kaambulia Sh5 milioni jambo ambalo halikubaliki.”

Alifafanua kuwa wasanii wanapaswa kuelewa kuwa kanuni za tozo mbalimbali zilizopitishwa hivi karibuni ni katika kuwafanya wafaidike na kazi zao na aliwashangaa wale wanaozipinga.

"Nina uhakika hakuna kampuni kubwa zinashindwa kulipa Sh5 milioni, nashangaa nyie mnavyowatetea wakati wao hata mmoja mpaka sasa hivi hakuna aliyenijia kulalamika," alisema Mwakyembe.

Polepole Ajibu Mapigo ya CHADEMA

$
0
0
Chama cha Mapinduzi (CCM), kimesema hakina wasiwasi wa aina yoyote na Tume ya Uchaguzi (NEC) katika uchaguzi mdogo wa marudio wa Ubunge katika Jimbo la Buyungu mkoani Kigoma huku kikidai waoitilia shaka tume hiyo wao ndio wenye matatizo.

Hayo yamelezwa na Katibu Mwenezi wa chama hicho, Humphrey Polepole baada ya kupita takribani siku tatu tokea Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutoa kauli yake iliyokuwa ikiitaka NEC kuendesha uchaguzi huo kwa uhuru na haki kuwa kuna baadhi ya vitu wamevibaini vikiendeshwa ndivyo sivyo.

"Sisi hatuna mashaka yoyote na Tume ya Uchaguzi (NEC) na kama tungekuwa nayo basi tungeshayaeleza mahali husika ila ukiona mtu anajitokeza barabarani na kusema kuna changamoto bila ya kuzipeleka sehemu husika basi ujue yeye ndiyo mwenye changamoto nasio Tume", amesema Polepole.

Pamoja na hayo, Polepole ameendelea kwa kusema "Chama cha Mapinduzi kimejiwekea rekodi ya kushughulika na shida za watu na kutatua kero za wananchi wa Tanzania na hili limefanyika vizuri sana chini ya serikali ya CCM inayoongozwa na ndugu John Magufuli. Tumekuwa hatuna mzaha, masihara na watu wanaocheza na rasilimali za umma, wanaonyanyasa wananchi, wasiowajibika na kushughulika na shida za watu na kwa rekodi ambayo tumeshajiwekea mpaka sasa hivi tutaenda kupanda ushindi mkubwa wa kishindo kwasababu ya kazi ile nzuri ambayo tumekwisha ifanya hadi sasa hivi".

Uchaguzi huo mdogo wa marudio umepangwa kufanyika Agosti 12 mwaka huuu baada ya kuwepo wazi Jimbo la Buyungu Mkoani Kigoma kufuatia Mbunge Kasuku Bilago kufariki dunia mwanzoni mwa mwezi Mei mwaka huu pamoja na madiwani wa maeneo mbalimbali kuyaacha majimbo yao na kujiunga CCM kwa lengo la kumuunga mkono Rais Magufuli.

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) wazungumiza kauli ya Rais Magufuli kuhusu wafungwa

$
0
0
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) umesema kauli ya Rais John Magufuli aliyoitoa jana, akitaka wafungwa kutumikishwa wakiwa gerezani,   inakiuka Katiba ya nchi na haki za binadamu.

Kiongozi mkuu huyo wa nchi alitoa kauli hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam katika hafla fupi ya kumuapisha Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Phaustine Kasike na Balozi Joseph Sokoine ambaye ameteuliwa kuwa naibu katibu mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

Rais Magufuli alimtaka Kasike kuhakikisha wafungwa wanafanya kazi ipasavyo, wazuie matumizi ya simu gerezani, washiriki katika shughuli za kilimo na ujenzi, wazuie kufanya biashara na kushiriki katika matukio ya wizi wakiwa gerezani na wazuie kujamiiana.

“Unakuta hata maaskari na watumishi hawana nyumba za kukaa na wafungwa wapo tena wa bure kabisa ambao unaweza kuwaambia wafyatue matofali na teke ukawapiga. Askari huna pa kulala na wafungwa wapo, lakini unawatafutia Bajeti ya Serikali,” alisema Rais Magufuli.

Akizungumza na gazeti la Mwananchi leo Jumapili Julai 15, 2018 mkurugenzi wa mtandao huo, Onesmo Ole Ngurumwa amesema, “mfungwa ana haki ya kula na kuishi na wakati mwingine anaweza kufanya shughuli akiwa gerezani ambazo zitamuingia kipato na hizo fedha akatunziwa na kupewa siku akitoka gerezani ili zimsaidie,”

“Mgungwa anapaswa kupata haki zake za msingi na haimaanishi mtu akiwa mfungwa apigwe, anyanyaswe na kufanya hivyo ni kwenda kinyume na haki za binadamu. Mfungwa hapaswi kupigwa na hakuna sehemu yoyote inasema apigwe na kunyanyaswa.”

Amesema kauli kwamba mfungwa apigwe, afanye kazi na kugeuzwa kitega uchumi inashtua na ni kinyume na Katiba na haki za binadamu.

Kwanini Baadhi ya Wanaume Wana Maumbile Mafupi na Upungufu wa Nguvu za Kiume? Suluhisho Hili Hapa

$
0
0
KWANINI BAADHI YA WANAUME WANA MAUMBILE MAFUPI NA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME... DR SITTA NDO SULULISHO LAKO

Tatiza, hili limekuwa likiwaathiri watu wengi sana kisaikolojia hasa baadhi yao kujiona wako tofauti na wanaume wengine. Kwa kawaida, mwanaume anatakiwa awe na uume, usiopungua nchi 6-7au-8 ,vinginevyo mtu huyo anamatatizo.

Zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo hilo... baadhi ni  upungufu wa vichocheo vya, HORMONES ZA CETROGEN .

SUPER MIZIZI, ni dawa inayozalisha HORMONES ZA CETROGEN,na kufanya, uume kukuwa na kuongzeka sazi utakayo na kuzibua mrija iliyosinyaa,

NSHOLA; ni dawa bora, ya kurudisha nguvu za kiume kwa kutibu kabisa  tatizo hilo na kukupa  hamu ya  kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara nne 4 bila kuchoka 

Pia  kuna dawa za kutibu presha ya kupanda na kushuka, kisukari , kuondoa mafuta  mwilini na maumivu ya mgogo kiuno, matazo, ya hedhi kwa wanawake, hedhi zisizokuwa na mpangilio.

NKANYA; ni dawa ya mvuto wa kimapenzi ,mchumba mpenzi aliyekuacha, mke, mme atakurudia .

NKOMA; Ni dawa kuongeza HIPS na mguu wa bia kwa wadada ,

NGAKAMA ,ni dawa ya kutibu miguu kufa ganzi na kuwaka moto, huduma zetu ,zipo ,vizuri, popote pale dawa utaletewa! 

DR SITTA, amebobea kwa tiba asilia 

Kwa DAR ANAPATIKANA MBAGALA ZAKHEM, SONGEA BOMBAMBILI, SHINYANGA- KAHAMA MJINI, 

KWA MAELEZO ZAIDI  PIGA SIMU; 0763172670/ 0715172670,/

WOTE  MNAKARIBISHWA... KAMA, UTAKUWA NA TATIZO, UTAHUDUMIWA,

Kiboko Ya Matatizo Ya Nguvu Za Kiume,maumbile Madogo, Mvuto Wa Mapenzi ,magonjwa Sugu

$
0
0
Usikate tamaa ondoa maradhi yako, maana matatizo haya yamekua yakiasili watuwengi kisaikolojia hasa baada ya kujiona wako tofauti sana na wengine kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia (6-8) vinginevyo mtuhuyo anamapunguvu katika mwiliwake.

Kunasababu nyingi sana zinazosababisha matatizo haya, chango hushambulia never ambayo huasili misuli ya uume, Ngili :- hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kufanya tumbo kuunguluma na kujaa gesi, kolodani moja kuvimba au kuingia ndani pamoja na kutopata choo vizuli. Sababuhizi na nyingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba na marakwamara husababisha kukosa hamu ya kuludia tendo la ndoa na baadae kushindwa kabisa

MASISA 3POWER :- nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa mfumo wa vidonge, huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka 15-90 , inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii) inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa, itakufanya uludie tendo la ndoa zaidi ya mara nne (4) birahamu kuisha wara kuhisi kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya dk (20-30 )

YONINANI:- hurefusha na kunenepesha maumbile madogo ya uume uliosinyaa inchi 6-8 na unene wa sm 3-4 kwa mda mfupi sana,

SUPER MORINA :- nidawa inayotibu ama kutatua tatizo la kisukali kwawaliohangaika bila mafanikio, huondoa tatizo la kisukali na kupona kabisa, vilevile ninadawa ya magonjwa sugu km vile presha, vidondo vya tumbo, miguu kuwakamoto, muwasho mwilin, kaswende,uzazi nk.

LUGIMBA :- nidawa ya mvuto wa mapenzi, humtuliza mke, mme, mchumba, hawara au mtu yoyote umpendae na kumfanya akutimizie chochotekile unachokitaka kutoka kwake na kumfunga asiwe na mtu yoyote zaidi yako.

WASILIANA NA DR CHIPUPA NAPATIKANA DAR ES SALAAM KUMBUKA HUDUMAHII ITAKUFIKIA POPOTE ULIPO  0759208637 / 0785687900

Mizizi 29 Power ,ndio Dawa Bora Na Imara Kwa Sasa Kwa Kutibu Na Kuponesha Tataizo La Nguvu Za Kiume Kwa Dakika 30 Tu

$
0
0
Tatizo la upungufu wa nguvu za kiume limekuwa ni janga kubwa sana kwa sasa sio vijana au wazee wanalalamiki kukimbiwa na wa wapenzi wao au ndoa kuvunjika kutokana na mwanaume kulala na mwanamke kitanda kimoja hata wiki mbili bila kushiriki tendo la ndoa na hii ndio inachangia wanawake wengi kutoka nje ya ndoa kwa nini huteseke na wakati dawa zipo ambazo zitarudisha heshima yako ya ndoa 

MIZIZI 29 POWER; ni ambayo hutibu na kurudisha virutubisho mwilini ambavyo humfanya mwanaume awe na matatizo yafatayo 1 kuwahi kukojoa kabla mke au mpenzi wake

 2. kushindwa kurudia tendo dawa, hii itakufanya kurudia tendo zaidi ya Mara tatu 

3... dawa hii inatibu uume uliolegea na kusinyaa 

4. dawa hii inatoa miungurumo ya tumbo na uchovu wakati wa kumaliza tendo 

NINI KINASABABISHA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME 1 kupiga punyeto kwa mda mrefu 
2 upungufu wa vichochoe mwilini 
3 magonjwa ya moyo, kisukari, presha, vidonda vya tumbo kiuno na mgongo 
4 utumiaji ovyo wa madawa ya kizungu 
4 usongo wa mawazo, hasira, tumbo kujaa gesi na kutopata choo.

 PATA TIBA YANGU NA NI TOFAUTI NA ULIZO WAHI KUTUMIA: 

Je una uume mfupi na mwembamba? MASHESHA MIX ni dawa ya kuboresha uume saiz upendayo asa kwa wale waliofanyiwa tohara wakiwa wadogo.. chagua saizi upendayo inch 5,6,7, adi 8 iyo ni kwa urefu na unene sentimita 2,3,4, adi 5 .dawa hizi zipo za kupaka na kunywa na hazina madhara yoyote kwa mtumiaji ,

Tunatibu kisukari,vidonda vya tumbo,ngiri, korodani iliyovimba, kupnguza kitambi, maziwa makubwa NK 

KWA TIBA NA USHAULI FIKA OFISINI KWANGU DARE S SALAAMU MBAGALA ZAKHEMU NA MIKOA YA KANDA YA ZIWA YUPO WAKALA WETU HAPO MWANZA NA KWA AMBAO HAWANA NAFASI YA KUJA OFISINI HUDUMA YETU UTALETEWA POPOTE ULIPO PIGA SIMU 0783185060 DR MAKOYE

Maagizo 10 Aliyopewa Mkuu wa Mpya wa Jeshi laagereza na Rais Magufuli

$
0
0
Rais  Dk. John Magufuli, amempa maagizo 10 Kamishna Jenerali mpya wa Magereza, Phaustine Kasike, huku akimwonya kuwa asipochukua hatua atamchukia.

Maagizo hayo aliyatoa jana Ikulu, Dar es Salaam, wakati akiwaapisha Kamishna Jenerali Kasike na Balozi Joseph Sokoine ambaye anakuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira.

Kamishna Jenerali Kasike ametakiwa kushughulikia promosheni za askari wa jeshi hilo, kuhakikisha mashine ya ukaguzi inafungwa, wafungwa wanajilisha wenyewe, wanafanya kazi ikiwamo ujenzi, kufanya ufugaji na kujenga nyumba za askari.

Pia alimtaka kuhakikisha mfungwa hafanyi mambo asiyotakiwa kama simu, bangi, kujamiiana lakini pia mfungwa kuhukumiwa kisha anakutwa na hatia nje ya gereza.

Akifafanua agizo moja baada ya jingine, Rais Dk. Magufuli ambaye alianza kwa kutoa pole nyingi kwa Kamishna Jenerali Kasike kuliko pongezi, alisema askari wako nyuma katika kupandishwa vyeo.

“Naanza kwa kukupongeza na kukupa pole. Mategemeo yangu nataka yakawe makubwa ya kuleta mabadiliko magerezani. Sio siri Jeshi la Magereza na maaskari wenyewe wamekaa kama wameachwa hivi, hata katika promosheni zao imekuwa ni tatizo.

“Wakati nampromoti Kamishna Jenerali aliyestaafu, palikuwa na makamishna wawili tu, si kwamba hawana sifa, waliachwa aidha kwa makusudi au kuhofia waliojuu,” alisema Rais Magufuli.

Alisema hadi Kamishna Kasike anashika kijiti hicho mtangulizi wake alikuwa ameanza kutekeleza agizo la Rais na kufanikiwa kuwapandisha Makamishna na Manaibu Kamishna zaidi ya 10, hivyo aendeleze hilo hadi kwa askari wa chini waliokaa muda mrefu.

Mbali na hilo, Rais Dk. Magufuli alirudia kauli yake aliyopata kuizungumza siku za nyuma kwamba ni jambo la aibu kwa nchi kulisha wafungwa kwa kuwa mashamba yapo.

Alisema wafungwa wanapaswa kufanya kazi na si kuomba msaada wa tofali wala chakula.

“Maeneo ya Magereza ni mengi, ukienda Mbeya eneo linalolimwa ni robo tu. Kila mwaka kuna maombi ya bajeti kulisha wafungwa, kufungwa maana yake ni ukamenyeke kwa kazi,” alisema Rais Magufuli.

Alisema si sahihi watumishi wa magereza kukosa nyumba za kuishi na kuomba fedha serikalini wakati wafungwa wanaweza kufyatua tofali na kuzichoma.

Mbali na hilo, Rais Dk. Magufuli, alisema hataki kuona mtu akipangiwa majukumu kutokana na kufahamiana na mtu fulani.

“Sitaki niyasikie yale ya Mbeya, mfungwa amehukumiwa kufungwa ni jambazi halafu baadaye anashikwa akishirikiana kuwinda tembo porini na anakamatiwa huko wakati huku amehukumiwa kufungwa, sitaki nisikie mfungwa aliyeacha familia yake kule nyumbani anakuja mke wake gerezani, anakaribishwa na askari wa magereza akafanye yule mfungwa mambo ambayo hakutakiwa kuyafanya akiwa gerezani,” alisema Rais Magufuli.

Alisema hataki kusikia wafungwa wakiwasiliana na familia au jamaa zao kupitia simu ambazo zimejaa magerezani na kusababisha kuwa kitu cha kawaida.

Katika hilo, Rais alikwenda mbali na kusema kuwa jambo hilo linafanyika hata katika magereza ya Dar es Salaam ambako wapo wanaopiga simu hadi nje ya nchi wakiwa gerezani.

“Sitaki kwenye magereza wafungwa wakapate nguvu ya kuvuta bangi na saa nyingine kujamiiana, kwa sababu hawafanyishwi kazi za kutosha. Sitaki mfungwa akafungwe, baadaye akiwa huko akaanze kufuga mbuzi na ng’ombe anapeleka hadi mnadani, anakuwa tajiri hata kuliko askari. Nina mifano ya kila gereza,” alisema Rais Magufuli.

Akisisitiza Rais Magufuli alisema: “Nakupongeza kidogo, pole ndio nyingi. Najua wapo maaskari watakaochukia kwa hatua utakazochukua na usipozichukua mimi utanichukia, nataka magereza ikafanye kazi askari wafaidike.”

Rais Magufuli pia alisema haoni sababu ya Jeshi la Magereza kukosa vitendea kazi kama trekta wakati Jeshi la Kujenga Taifa liliwahi kukopesha vitu hivyo.

Changamoto nyingine aliyotakiwa kuishughulikia ni fedha alizotoa kiasi cha takribani Sh bilioni 10 ili kukamilisha ujenzi wa nyumba za maaskari katika eneo ya Ukonga ambazo hazijakamilika.

“Kama malori yamepungua, nitayatoa mengine yaliyokuwa ya polisi, nitawapa ninyi. Serikali ni moja, fedha ni za wananchi, kaeni mjadili namna mtakavyogawana. Ni wizara moja. Nataka Jeshi la Magereza likawe mfano,” alisema Rais Magufuli.

Alimtaka Kamishna huyo kupanga vizuri safu yake ikiwamo kushirikiana na makamishna wenzake katika kufanya kazi ili kupata mwelekeo.

“Kuna watu wana rekodi nzuri, mfano Mwakijungu alipelekwa Makete kila mtu alikuwa akipakataa, akapelekwa Iringa akafanya vizuri, mtu wa operesheni kama huyo mnampeleka akawe store keeper? (mtunza stoo), sina hakika kama wamepangwa vizuri. Sikufundishi kazi,” alisema Rais Magufuli.

Ili kukabiliana na tatizo la kupitisha simu kwa wafungwa, Rais Magufuli alishauri kifungwe kifaa cha utambuzi ili kuwabaini wahusika.

Zaidi alimtaka Kamishna huyo kutembelea magereza pamoja na kukutana na majeshi mengine nchini ili kupata mikakati ya kujiimarisha.

Awali Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, ambaye alianza kwa kumwamkia Rais Magufuli kwa kusema; “Shikamoo Mheshimiwa Rais,” alisema mambo ambayo alimwagiza wakati akimwapisha alikwishaanza kuyafanyia kazi likiwamo suala la ajali za barabarani pamoja na mikataba.

Alisema baada ya kuingia kuongoza Wizara hiyo aliitisha mkutano na wakuu wa vyombo vilivyo chini yake kujitafakari huku akitoa siku 21 kila chombo kuwasilisha kwake taarifa ya mwelekeo.

“Zimebaki siku saba, hakika tutachukuwa hatua bila kutazama usoni,” alisema Lugola.

Alisema kwa sasa wanaelekea kufanya mikakati ya maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao utafanyika mwakani ili kuweka hali ya utulivu na usalama.

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano, January Makamba, akizungumza katika hafla hiyo alisema walipata maelekezo ya Rais kuhusu ucheleweshaji wa vyeti vya tathmini ya athari kwa mazingira kwenye ujenzi wa viwanda.

“Wiki mbili zijazo nitasaini kanuni mpya za kufanya tathmini ya athari kwa mazingira ambazo zitawezesha ndani ya siku tatu tangu mtu atakapoleta ombi la kujenga kiwanda tutakuwa tumetazama na tutatoa ruhusa ya awali ili aanze kujenga halafu mchakato mwingine uendelee,” alisema January.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images