Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Polisi Mkoani Dodoma yakamata watu watatu waliokuwa wakiandamana na mabango kwa lengo la kulivuruga bunge maalumu la Katiba

$
0
0
WATU watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma kwa kufanya mkusanyiko usio halali huku wakiwa wamebeba mabango yanayohamasisha uvunjifu wa amani. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) David Misime alisema tukio hilo lilitokea  jana katika maeneo mawili tofauti. Aliwataja waliokamatwa katika tukio hilo ni Augustino Pancras (60), 

Tangazo la nafasi za kazi kutoka Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma lililotolewa jana tarehe 1 April 2014.....Mwisho wa maombi ni April 15

$
0
0
Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki, pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).

Wimbo Mpya:Professor Jay ft Diamond Platinumz- KIPI SIJASIKIA

$
0
0
Sikiliza wimbo mpya wa Professor Jay aka Heavy Weight MC akiwa amemshirikisha Diamond Platinumz,wimbo unaitwa Kipi Sijasikia. Wimbo umefanyika studio za Bongo Records chini ya producer P Funk Majani Usikilize hapa

IKULU yafafanua kuhusu madai ya tume ya katiba Kutupiwa virago, kupewa kiinua mgongo cha sh. milioni 200/= kwa kila mjumbe na kunyang'anywa magari

$
0
0
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Gazeti la Raia Mwema lililotoka leo, Jumanne, Aprili 2, 2014, limeandika habari zisizokuwa za kweli chini ya kichwa cha habari : “Warioba: Ikulu imetutupia virago”.    Habari hiyo inamkariri aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Mheshimiwa Jaji Joseph Warioba akidai kuwa Tume yake ilifukuzwa kazi, kwamba haikupewa muda wa kuandaa na

Wazazi 100 mkoani Ruvuma wafikishwa mahakamani kwa kosa la kusherehekea watoto wao kefeli mitihani

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Thabit Mwambungu ameiambia  FIKRA PEVU  leo Jumatano, Aprili 2, 2014 kuwa Serikali ya Mkoa huo imewafikisha mahakamani wazazi 100 kwa tuhuma za kufanya sherehe baada ya watoto wao kufeli mitihani. Pamona na wazazi/walezi hao kujitetea kuwa walikosa karo ya kuwapeleka watoto hao shule, imeelezwa pia kuwa mazingira duni ya kufundishia na kujifunza katika

Magazeti ya leo Alhamisi ya tarehe 3 April 2014

$
0
0
                             Magazeti  ya  leo  Alhamisi  ya  tarehe  3 April  2014

Mchungaji adai hajaoga tangu mwaka 2001 kwa sababu alimbiwa na Mungu asioge

$
0
0
Nadhani ulishawahi kusikia ama kushuhudia watu wa eneo Fulani ama jamii fulani wakimlazimisha kichaa kuoga kwa nguvu kwa kuwa amezidi kuwa mchafu, lakini hii ni tofauti kwa waumini wa dhehebu analolisimamia mchungaji Wale Olanguji wa Nigeria.   Mchungaji Wale wa kanisa la Divine Seed of God wa Ibadan, Oyo, Nigeria ameliambia jarida la People City la Nigeria kuwa hajawahi kuoga

Watu watano wafariki dunia katika Mapigano ya wakulima na wafugaji wa mipaka ya Shinyanga na Tabora

$
0
0
Mapigano ya kugombea ardhi kati ya wakulima na wafugaji katika eneo la mpaka kati ya wilaya za Kishapu mkoani Sninyanga na Igunga, mkoani Tabora yameua watu watano. Mapigano hayo yaliyotokea Jumapili iliyopita katika kijiji cha Magalata wilayani Kishapu na kusababisha vifo hivyo na mtu mmoja kujeruhiwa baada ya kushambuliana kwa kutumia mikuki. Waliouawa ni Peter Korongo Masolwa(72)

Jokate Mwegelo adai bado yupo single....Kazi kwenu akina kaka

$
0
0
Jokate Mwegelo yupo single ... Staa huyo mwenye vipaji lukuki alisema hayo Jumatatu hii kwenye kipindi kipya cha TV1, ‘The One Show’ anachokiendesha kwa kushirikiana na Ezden Jumanne aka The Rocker. Katika kipindi hicho cha kwanza kuoneshwa, watangazaji hao walianza kwa kuhojiana wao kwa wao kwanza na moja ya maswali aliyoulizwa Jokate ni kama yupo kwenye uhusiano wowote wa

Rais Kikwete amteua Mwandosya kuwa Mkuu wa Chuo cha MUST

$
0
0
Rais Jakaya Kikwete amemteua Profesa Mark Mwandosya kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (Must) wakati Profesa Joseph Msambichaka akiteuliwa Makamu Mkuu wa chuo hicho.    Katika uteuzi huo uliofanyika mwishoni mwa Machi mwaka huu, Rais pia amemteua Profesa Osmund Kaunde kuwa Naibu mkuu wa chuo upande wa taaluma, utafiti na ushauri, wakati Profesa Emmanuel Luoga

Kamati za bunge maalumu la katiba zaendelea vyema kujadili rasimu ya katiba.....Hizi ni picha za vikao vya kamati hizo toka mjini Dodoma

$
0
0
 Mwenyekiti wa Kamati namba sita ya Bunge Maalum la Katiba Stephen Wassira(katikati) akisoma dua ya kuharisha kikao cha Kamati leo mjini Dodoma. Wengine ni Mwenyekiti wa Bunge  Maalum la Katiba Samuel Sitta(kulia) na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dkt. Maua Abeid Daftari(kushoto). Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Ismail Jussa akitoa mchango wake leo mjini Dodoma kwa Mwenyekiti wa wa Bunge

Video: Wema Sepetu Azua Timbwili Kubwa Globalpublishers Kwa Madai Ya Kuandikwa vibaya na Magazeti ya kampuni hiyo

$
0
0
Wema Abraham Sepetu amezivamia ofisi za Global Publishers zilizoko Bamaga – Mwenge, Dar es Salaam akidai kuwa ameandikwa vibaya kwenye magazeti ya kampuni hilo na kuzua tafrani.   Ni kama unaangalia filamu mpya ya Wema Sepetu ambayo huenda jina halijafahamika..lakini pigia msitari    tu  kwamba  kituko  hiki  kimetokea  kweli  kama  kinavyoonekana  katika  video  hapo  chini  kwenye

Halmashauri ya jiji yabomoa meza za machinga maeneo ya posta jijini Dar

$
0
0
      Maafande wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi leo wameendelea na bomoabomoa ya meza za wafanyabishara ndogondogo 'Wamachinga' kama walivyonaswa na kamera yetu maeneo ya Posta Mpya jijini <!-- adsense -->

CHADEMA yazidi kuchanja mbuga katika kampeni zake za lala salama jimbo la Chalinze

$
0
0
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Issa Said Mohamed akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Miono, katika mkutano wa kampeni, uliofanyika kijijini hapo. Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Miono wakiitikia kauli mbiu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ya "Peoples Power" wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika katika kijiji cha Miono. Kiongozi

Kuelekea ukingoni mwa kampeni za uchaguzi Chalinze, CCM yazidi kuzibomoa ngome za wapinzani wake

$
0
0
Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi wa CCM,Nape Nnauye sambamba na Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya Kikwete wakiyarudi magoma wakati wa Mkutano wa Kampeni za CCM uliofanyika  April 2,2014 katika Kijiji cha Lugoba,Kata ya Lugoba. Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwahutubia

Magazeti ya leo Ijumaa ya tarehe 4 April 2014.......

$
0
0
                        Magazeti  ya  leo  Ijumaa  ya  tarehe  4 April  2014.......

Jaji Warioba aijibu IKULU....Adai tume yake ilifanya kazi hadi March 18 2014, Akerwa na kitendo cha kuitwa mnafiki, ahoji wajumbe wake kutorudishwa nyumbani

$
0
0
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema waliokuwa wajumbe wa tume hiyo hawajawahi kudai malipo ya pensheni ya Sh200 milioni kama inavyodaiwa.    “Wajumbe wa Tume hawajatoa madai ya kulipwa shilingi milioni mia mbili. Hakuna mjumbe yeyote aliyetoa dai kama hilo na Serikali inajua,” alisema   Jaji Warioba katika taarifa yake kwa vyombo vya

Mama adai kuibiwa mtoto na Manesi akiwa Leba

$
0
0
Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jinala Shakila Bakari (30),mkazi wa Mbagala jijini Dar, ametoa madai mazito kuwa manesi wa hospitali moja (jina linahifadhiwa) iliyopo Mbagala wamemuiba mmoja wa watoto wake wawili aliojifungua Machi 28, mwaka huu. Akizungumza na gazeti la  Ijumaa  juzi, Shakila alisema siku ya tukio majira ya saa 6 mchana,alijifungua mtoto wake wa kwanza,lakini

TFDA yatoa matokeo ya ukaguzi wa maduka ya Vyakula jijini Dar es salaam .....Supamaketi 29 zafungwa

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) Bw.Hiiti Sillo (kulia) akitoa ufafanuzi wa maziwa yaliyokamatwa yakiwa kwenye kifungashio kisichokua na maelezo yoyote yakiuzwa kwenye maduka ya kuuzia vyakula   “Supermarkets” na Mini-Supermarkets  katika jiji la Dar es salaam.  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) Bw.Hiiti Sillo akizungumza na waandishi wa habari leo

Mkuu wa Mkoa wa Dar ampasha John Mnyika....Adai hawezi kusitisha agizo lake la pikipiki na bajaj kuingia katikati ya jiji

$
0
0
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik amesema hawezi kusitisha agizo lake la pikipiki na bajaj kuingia katikati ya jiji, kwani hana mamlaka hayo, kwani anasimamia sheria.   Alisema hayo jana Dar es Salaam wakati akizungumza na Habari leo  kuhusu ombi la Mbunge wa Ubungo, John Mnyika kutaka asitishe agizo hilo kupisha mazungumzo baina ya Serikali, wahusika wa bodaboda na bajaj na
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live


Latest Images