Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Argentina Maumivu Tupu....Ni Baada ya Kupewa Kichapo cha 3-0 na Croatia

$
0
0
Kikosi cha timu ya taifa ya Argentina kimeshindwa kutamba mbele ya Croatia baada ya kukumbana na kichapo cha mabao 3-0.

Mabao ya mchezo huo wa kundi D yaliwekwa kimiani na Luca Modric, Ivan Rakitic na Ante Rebic.

Kufuatia kichapo hicho walichokipata Argentina kinawafanya wasalie na alama moja waliyoipata dhidi ya Iceland baada ya kwenda sare ya 1-1 wakiwa nafasi ya 3.

Nyota wa timu hiyo, Lionel Messi alionekana kuwa na machungu kufuatia kichapo hicho.

Messi ambaye amepewa nafasi kubwa zaidi ya kuisaidia Argentina ameshindwa kufunga bao lolote mpaka sasa katika michezo miwili ambayo timu hiyo imeshacheza.

Ufaransa Yatinga 16 Bora Kombe la Dunia....Ni Baada ya Kuitandika Peru 1-0

$
0
0
Bao pekee la Kylian Mbappe limewafanya Ufaransa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Peru katika mchezo wa kundi C kwenye michuano ya Kombe la Dunia huko Urusi.

Mbappe amefunga bao hilo akiwa na umri mdogo zaidi kwenye michuano hiyo mnamo dakika ya 34 ya kipindi cha kwanza na kudumu dakika zote za mchezo.

Mchezaji huyo anayeichezea PSG ya Ufaransa amefunga bao hilo la kwanza ikiwa ni mara yake ya kwanza kushiriki mashindano hayo akiwa na umri wa miaka 19 na miezi 6 pekee.

 
Kwa matokeo hayo, timu ya taifa ya Ufaransa imefanikiwa  moja kwa moja kuingia hatua ya 16 bora na kuiondosha Peru kwenye fainali ya kombe la dunia mwaka huu.

Ufaransa iliyopo kundi C inafikisha pointi 6 ikifatiwa na Denmark yenye pointi 4 ambayo inahitaji pointi moja ili kuungana na Ufaransa au ikiomba Peru anayeburuza mkia wa kundi hilo kwa kutovuna pointi hata moja kwenye mchezo yake miwili amfunge Australia mwenye pointi moja kwenye mchezo wa kukamilisha ratiba ya kundi hilo.

CHADEMA Kusambaza Bajeti Yao Mtandaoni....Ni Baada ya Kukataliwa Kuisoma Bungeni

$
0
0
Chadema kimetafuta mbinu mpya ya kuisambaza hotuba mbadala ya bajeti ya kambi ya upinzani bungeni kwa mwaka 2018/19.

Chadema wamesema kuanzia sasa bajeti hiyo itapatikana katika tovuti maalumu ya chama hicho.

Hatua hiyo imefikiwa ikiwa ni siku chache tangu bajeti hiyo yenye kurasa 521, kuzuiwa kusomwa ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Taarifa ya chama hicho iliyotolewa jana Juni 21 na mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Tumaini Makene inaeleza kuwa kama chama kinapinga na kulaani kwa nguvu zote uamuzi huo wa Bunge kuzuia kusomwa kwa hotuba ya bajeti mbadala, kinyume na Kanuni za Bunge.

“Wananchi wamenyimwa fursa adhimu ya kusikia namna ambavyo Chadema na Ukawa wangefanya ili kuwakwamua katika hali ngumu wanayopitia. Tutasambaza hotuba hiyo na kwa sasa tayari inapatikana katika tovuti ya chama,” alisema Makene.

 Alisema Spika Job Ndugai alipaswa kujisikia vibaya kwa sababu kambi rasmi ya upinzani bungeni chini ya uongozi wake, ililazimika kujichangisha na kutumia fedha kutoka mifuko ya wabunge wake kutafuta watu wa kuwafanyia utafiti, uchambuzi na kuandika hotuba, jambo ambalo lilipaswa kuwa sehemu ya wajibu wa Ofisi ya Bunge.

  “Tunatoa wito kwa Spika Ndugai atambue unyeti wa mamlaka ya mhimili wa Bunge, majukumu ya wabunge na Bunge lote kwa ujumla na asimamie sheria zote,” alisema.

TECNO Kuzindua TECNO Spark 2 Rasmi.

$
0
0
Baada ya amsha amsha nyingi kuhusiana na ujio wa TECNO spark 2. kampuni ya simu ya TECNO imeitambulisha rasmi TECNO spark 2 kwa mara ya kwanza katika ukumbi wa tips jijini Dar es Salaam.
 
Katika uzinduzi huo muongeaji wa kampuni ya TECNO, Bwana Erick Mkomoye alitoa shukrani zake za dhati kwa kusema, tunayo furaha kujumuika nanyi katika uzinduzi wa simu yetu ya TECNO spark 2. TECNO spark 2 ikiwa ni muendelezo wa toleo la TECNO spark kampuni imefanya mapinduzi makubwa katika simu hii kama vile teknolojia ya face id yenye kufungua simu kupitia paji la uso, 
 
Bwana Mkomoye aliendelea, “lakini pia tumeona huu ni wakati muafaka kuitambulisha TECNO spark 2 kwajili ya wapenzi wa mpira kwani eneo lake la juu limetawaliwa na kioo chenye uwiano 18:9 na ukubwa wa nchi 6.0HD+” 
 
“TECNO spark 2 imeboreshwa kwa kupitia mfumo wa android 8.1 Oreo wenye kuzuiya uishaji wa chaji kwa haraka na kukupata ufanisi wa kasi zaidi katika simu yako” alimaliza.
 
Uzinduzi ulisindikizwa  kwa wageni waalikwa na kujishinda zawadi mbalimbali kupitia kipindi hiki cha kombe la dunia huku TECNO spark ikiwa  simu rasmi kwaajili ya wateja kungalia mechi kupitia  kioo chake kikubwa.

Aliyepigiliwa Misumari Miwili Kichwani na Bosi Wake Afariki Dunia

$
0
0
Mwanaume aliyefahamika kama Robert Muchangi aliyepigiliwa misumari miwili na bosi wake kichwani nchini Kenya amefariki jana Juni 21 katika hospitali ya taifa ya Kenyatta.

Muchangi alifariki katika hospitali ya taifa ya Kenyatta alipokuwa amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi baada ya kukumbwa na kisanga hicho mjini Meru, ambapo alitendewa unyama huo baada ya kwenda kumdai fedha walizokubaliana baada ya kumjengea nyumba Bosi wake huyo.

Familia ya Muchangi imesikitishwa na tukio hilo kwa kile walichodai kuwa Polisi wamekaa kimya, Dada wa marehemu anayejulikana kama Regina Murugi amesema kuwa tukio hilo limeleta pigo kwenye familia.

“Kaka yangu amefanyiwa unyama huu lakini kwasababu ya hali yetu duni askari hawana msaada wowote kwetu, kaka alikuwa ndio kila kitu kwakweli ametuachia mzigo mkubwa sana”, amesema Regina.

Muchangi ameacha bili ya zaidi ya Shilingi Milioni 6 za Kitanzania katika hospitali hiyo ambazo ndugu zake wanatakiwa wazilipe, ndugu zake Muchangi wamelilalamikia jeshi la Polisi nchini humo kwa kukaa kimya juu ya tukio hilo.

Muchangi ametendewa tukio hilo mnamo Juni 13, 2018 kwenye kichwa chake katika eneo la Igembe Nchini Kenya, ambapo misumari hiyo ilitoboa fuvu la kichwa chake.

Chanzo: Standard Digital

Tiba Bora ya Nguvu za Kiume, Kisukari, Ngiri, Miguu Kuvimba

$
0
0
Matatizo ya nguvu za kiume yanawaathiri watu wengi kisaikolojia hasa baada ya kujiona tofauti sana na wengine. Kawaida mwanaume anatakiwa kuwa na uume kuanzia nchi 6- 8, vinginevyo mtu huwa na matatizo. Zipo sababu nyingi zinazosababisha tatizo hilo. 

Baadhi ni upungufu wa vichocheo hivi; Homoni za getrogen ambazo mwanaume anapobalehe, vichochea hivi huchochea ukuaji wa uume.

Ngiri; Hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na hufanya tumbo kuunguruma na kujaa gesi. Sababu zingine ni korodani moja kuvimba, kupopata choo vizuri.

Sababu hizi na zingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba na mara kwa mara husababisha kukosa tendo ya kurudia tendo na baadae kushindwa kabisa

SILYA: Ni dawa inayozalisha homoni zxa Gestrogen na kufanya uume kukua na kuongezeka hadi nchi 6-8
 
WET POWER: Ni dawa bora ya vidonge iliyotengenezwa kwa mitishamba na matunda ambayo huongeza nguvu za kiume kuanzia miaka 15-95 na hukomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi, ina imariisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa na itakufanya uwe na hamu ya kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara mbili bila hamu kuisha na pia itakuchelewesha kufika kileleni

Pia tunatibu kisukari, presha, ngiri, miguu kuvimba na kuwaka moto

Wasiliana na Sheikh Khatib akutatulie matatizo yako. Namba zake; 0785 234 837  au 0656 551 093  au 0746473974

Makanga 3 Power; Dawa Bora Nguvu Za Kiume

$
0
0
Kutibu nguvu za kiume dakika(10) na kupona muda wa siku tatu tuu. Kuimarisha misuli ya uume uliolegea, pia ipo Dawa ya kurefusha uume mfupi inchi NNE hadi saba na kunenepesha uume mfupi sentimita NNE.

Tiba ya kudumu kutibu maumivu ya mgongo,kiuno, tumbo kuunguruma na kujaa gesi, kupata choo vizuri, na kutibu uzazi, kutibu busha bila operesheni, kisukari, presha ,miguu kuuma, uzazi, fangas sugu, vidonda vya tumbo.

Ni docta bingwa wa kutibu magonjwa sugu, kutoa ndagu za utajiri kwa kutumia Pete, kazi ,cheni, mikufu maalumu ya bahati, una kesi umedhulumiwa Mali au pesa? Zitarudi muda wa Masaa matatu tuu.

Onana na Dr shilindes shida zako zote zitakwisha, anatoa Dawa za utajiri kwa wafanyakazi, wakulima, na wafugaji, wafanyabiashara na wachimba madini kwa kutumia pete, kazi kwa yeyote anaetaka kuwa na pesa nyingi.

Pia anaboresha akili kwa wanafunzi darasani, masomo na kufaulu mitihani pia kushinda bahati nasibu yeyote.

Pia tunatoa Dawa kumrudisha Mume, mke, mpenzi, hawara, kwa muda wa SAA moja tuu, na kuomba msamaha kwa kukupigia magoti na yeyote yule, unaemtaka kimapenzi au kuoana, utampata na kumfunga asitoke nje ya ndoa daima na kutekeleza shida zako zote. Kupunguza unene, kupunguza matiti makubwa, tumbo na nyama uzembe muda wa siku sita unapata saizi uipendayo.

Kutoa makovu mwilini, chunusi, upele na mabaka, pia tunayo Dawa ya kuongeza hipsi, makalio, mguu wa bia na kupata shepu safi kwa muda wa siku saba tuu.

Wa mikoani mtapata huduma popote mlipo.
Tupo dar es salam mbagala rangi tatu.

Mawasiliano simu namba: 0784 460 348. Au 0659 103 360.

Kiboko Ya Matatizo Ya Nguvu Za Kiume,maumbile Madogo, Mvuto Wa Mapenzi ,magonjwa Sugu

$
0
0
Usikate tamaa ondoa maradhi yako, maana matatizo haya yamekua yakiasili watuwengi kisaikolojia hasa baada ya kujiona wako tofauti sana na wengine kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia (6-8) vinginevyo mtuhuyo anamapunguvu katika mwiliwake.

Kunasababu nyingi sana zinazosababisha matatizo haya, chango hushambulia never ambayo huasili misuli ya uume, Ngili :- hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kufanya tumbo kuunguluma na kujaa gesi, kolodani moja kuvimba au kuingia ndani pamoja na kutopata choo vizuli. Sababuhizi na nyingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba na marakwamara husababisha kukosa hamu ya kuludia tendo la ndoa na baadae kushindwa kabisa

MASISA 3POWER :- nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa mfumo wa vidonge, huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka 15-90 , inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii) inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa, itakufanya uludie tendo la ndoa zaidi ya mara nne (4) birahamu kuisha wara kuhisi kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya dk (20-30 )

YONINANI:- hurefusha na kunenepesha maumbile madogo ya uume uliosinyaa inchi 6-8 na unene wa sm 3-4 kwa mda mfupi sana,

SUPER MORINA :- nidawa inayotibu ama kutatua tatizo la kisukali kwawaliohangaika bila mafanikio, huondoa tatizo la kisukali na kupona kabisa, vilevile ninadawa ya magonjwa sugu km vile presha, vidondo vya tumbo, miguu kuwakamoto, muwasho mwilin, kaswende,uzazi nk.

LUGIMBA :- nidawa ya mvuto wa mapenzi, humtuliza mke, mme, mchumba, hawara au mtu yoyote umpendae na kumfanya akutimizie chochotekile unachokitaka kutoka kwake na kumfunga asiwe na mtu yoyote zaidi yako.

WASILIANA NA DR CHIPUPA NAPATIKANA DAR ES SALAAM KUMBUKA HUDUMAHII ITAKUFIKIA POPOTE ULIPO  0759208637 / 0785687900

Tozo daraja la Kigamboni Haitafutwa

$
0
0
Serikali imesema kuwa haitafuta tozo inayotozwa katika daraja la Kigamboni kwa kuwa fedha hizo zinatumika kulipa sehemu ya deni la mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF)

Kauli hiyo imetolewa bungeni leo Juni 22,2018 na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye ulemavu Antony Mavunde akisema kwa sasa utaratibu unaandaliwa ili wavukaji wawe na hiyari ya kulipa kwa siku, wiki au mwezi kulingana na uwezo wa mtu.

Alikuwa anajibu swali la mbunge wa Viti Maalum (Cuf) Zainab Mndolwa Amir ambaye ameomba kujua tangu kujengwa kwa daraja hilo Serikali imekusanya kiasi gani cha fedha kinachotokana na malipo kwa wanaovuka pamoja na vyombo vya moto.

Mbunge huyo pia amehoji iwapo Serikali itaweka utaratibu wa kutumia kadi maalum (smart card) kulipia kwa mwezi malipo kwa wanaovuka daraja huku akihoji ni lini wananchi wataanza kupita bure darajani hapo.

Mavunde amesema Serikali kupitia NSSF ndio wanaosimamia daraja hilo.

“Hadi kufikia Machi mwaka huu, NSSF ilishakusanya Sh 19.73bilioni tangu daraja hilo lilipoanza kutumika Mei 2016,” amesema Mavunde.

Amesema kwa sasa NSSF ipo katika hatua za mwisho za kumpata mkandarasi wa kuweka mfumo utakaotumia kadi maalum ‘Smart Card’ kwa malipo ya wanaovuka darajani hapo.

Mbowe Ashindwa Kufika Mahakamani, Kesi Yapigwa Kalenda

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeshindwa kuendelea kusikiliza kesi inayowakabili Viongozi wa CHADEMA kwa sababu Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe amefiwa na kaka yake.

Pia mahakama hiyo imeagiza mshtakiwa wa 5, Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko kuhakikisha anafika mahakamani katika tarehe ijayo kinyume na hapo atachukuliwa hatua.

Katika kesi hiyo ya kufanya maandamano washtakiwa walitarajiwa kusomewa maelezo ya awali (Ph) mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri.

Wakili wa serikali Mkuu, Faraja Nchimbi amedai kuwa kesi hiyo imeitishwa kwa ajili ya Ph, lakini mshtakiwa wa kwanza Mbowe na Matiko hawapo mahakamani.

Kutokana na hoja hiyo, Mdhamini wa Mbowe, Greyson Selastine ameiambia mahakama kuwa Mbowe amefiwa na Kaka yake wa tumbo moja na msiba umesafirishwa kwenda Moshi.

Pia mdhamini wa Matiko, Patrick John alisimama na kudai kuwa anaumwa yupo Dodoma na ameambiwa apumzike.

Hata hivyo, wakili Nchimbi alipinga taarifa ya mapumziko ya Matiko akidai nyaraka zilizowasilishwa ni batili.

Kutokana na hoja hizo, Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi June 25 ili washtakiwa wasomewe maelezo ya awali na kusikilizwa hadi June 29,2018.

Mbali na Mbowe, mwingine ni Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu na Naibu katibu Mkuu bara na Mbunge wa kibamba John Mnyika.

Pia Katibu wa chama hicho Dk.Vicenti Mashinji, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe Halima Mdee na mbunge wa bunda, Esther Bulaya.

Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 13 ikiwemo kula njama, ambapo inadaiwa  February 1 na 16, 2018, Dar es Salaam walikuĺa njama ya kutenda kosa la kufanya mkusanyiko usio halali na kukiuka tamko kutawanyika.

Wanadaiwa kuwa February 16,2018 katika barabara ya Kawawa Kinondoni Mkwajuni washtakiwa hao wakiwa na wenzao 12 ambao hawapo mahakamani walikiuka tamko la kuwataka kutawanyika la Afisa wa polisi SSP, Gerald Ngiichi kwa kugoma kutawanyika na kupelekea uvunjifu wa amani.

Inadaiwa kugoma huko kulipeĺekea hofu na hatimaye kusababisha kifo cha Akwilina Akwiline na majeruhi kwa askari wawili ambao ni  H.7856 PC Fikiri na E.6976 CPL Rahim Msangi.

Katibu Mkuu NECTA Ashambuliwa na Wananchi

$
0
0
Katibu mtendaji wa Baraza la Mitihani (Necta), Dk Charles Msonde ameshambuliwa na kujeruhiwa na wananchi baada ya gari alilokuwa amepanda kugonga pikipiki na kusababisha kifo cha dereva.

Tukio hilo lilitokea juzi saa kumi jioni katika Kijiji cha Inala, Kata ya Ndevelwa katika Manispaa ya Tabora.

Dk Msonde amesema anaendelea vizuri na kwamba ajali ilitokea akiwa katika utekelezaji wa majukumu yake ya kazi.

“Ninaendelea vizuri. Haya maumivu ninayoyasikia yanatokana na kipigo kutoka kwa wananchi waliotuvamia baada ya ajali ile kutokea,” alisema Dk Msonde.

Hata hivyo, katibu mtendaji huyo hakuwa tayari kueleza kwa kina chanzo cha ajali na namna walivyoshambuliwa. “Naomba itoshe kusema ninaendelea vizuri.”

Ofisa habari wa Necta, John Nchimbi alisema Dk Msonde aliruhusiwa kutoka katika Hospitali ya Mkoa wa Tabora ya Kidete jana alikokuwa akipatiwa matibabu.

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Tabora, Nestory Didi alisema gari alilopanda Dk Msonde lilimgonga Mzee Salum (23) alipokuwa akikata kona kuingia nyumbani kwake.

Alisema kutokana na ajali hiyo wananchi walifanya vurugu ndipo dereva alipokimbia na kumwacha Dk Msonde.

Didi alisema Dk Msonde alitibiwa na kuruhusiwa na hakuwa na madhara makubwa mwilini kama baadhi ya watu wanavyodai.

Kamanda huyo aliwataka wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi na badala yake waache sheria ichukue mkondo wake.

Chanzo: Mwananchi

Dkt Tizeba Atoa Siku 4 Wakulima Wa Mkonge Mkoani Tanga Kulipwa Fedha Zao

$
0
0
Na Mathias Canal-WK, Tanga
Wakulima wa Mkonge Mkoani Tanga wamempongeza Waziri wa Kilimo Mhe Dkt. Charles Tizeba kupitia agizo lake alilolitoa kwa Kampuni ya Katani Limited kuhusu kulipa madeni ya wakulima ndani ya siku nne kuanzia 21 Juni 2018 hadi 26 Juni 2018 Kwa madeni ya muda mrefu ya wakulima wa zao hilo jambo lililopelekea kupunguza ufanisi na tija ya Kilimo Kwa wakulima hao.

Dkt Tizeba ametoa agizo hilo jana 21 Juni 2018 akiwa kwenye mkutano na wadau wa Kilimo cha Mkonge cha mkataba (SISO) unaotekelezwa kwenye mashamba matano ya Hale, Magunga, Magoma, Mwelya na Ngombezi yaliyo chini ya miliki ya Bodi ya Mkonge Tanzania.

Katika Mkutano huu uliofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Tanga na kuhudhuriwa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe Martin Shigela sambamba na Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe Godwin Gondwe, Msajili wa Hazina, Mtendaji wa BRELA, Muwakilishi wa mwanasheria Mkuu wa serikali, Mkurugenzi wa Bodi ya Mkonge na wataalamu wengine; Waziri wa Kilimo Mhe Tizeba ametoa agizo hilo Kwa Uongozi wa mfumo wa Kilimo cha wakulima wadogo wa kilimo cha Mkonge cha mkataba (SISO), Kampuni ya Katani ltd ambayo ndio mnunuzi pekee wa Mkonge wa mkulima na Bodi ya Mkonge Tanzania.

Sambamba na agizo hilo pia Mhe Waziri ameiagiza Bodi ya Mkonge Tanzania kupitia upya mikataba yote iliyopo Kwa kushirikisha Bodi yenyewe, Kampuni ya Katani na wadau wa zao hilo haraka iwezekanavyo ili kurekebisha makosa yaliyopo.

Aidha, ameitaka Bodi hiyo ya Mkonge Tanzania kuitisha kikao na wadau wote wa zao hilo ili kupitia upya utaratibu wa makato ya mgawanyo wa mapato katika kusindika zao la Mkonge.

Mhe Dkt Tizeba aliongeza kuwa hati za miliki ya mashamba zitapaswa kutolewa Kwa wahusika Mara baada ya kujiridhisha na mchakato utakapokamilika huku akiwataka wakulima kulipa malimbikizo ya kodi ya ardhi.

Waziri wa Kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba amemaliza ziara ya siku moja ya kikazi mkoani Tanga huku akimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe Martin Shigela Kwa umakini na uwajibikaji katika kusimamia sekta ya Kilimo hususani zao la Mkonge mkoani humo.

MWISHO.

Mwanamke Auawa Manyara, Chanzo Cha Kifo Bado Hakijafahamika, Mmoja Ashikiliwa Na Polisi

$
0
0
Na. Vero Ignatus , Manyara.
Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jila la Josephine Peter (51)mkazi wa Mrara kata ya Mamire wilayani Babati  ameuawa na watu wasiofahamika  huku shingo yake ikikatwa na kitu chenye ncha kali.

Akizungumza jana june 21 Kamanda wa polisi  mkoani Manyara  Augustino Senga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, amesema mwanamke huyo alifariki dunia juni 19 saa 4 usiku akiwa nyumbani kwake  na mtu mmoja anashikiliwa na jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi kutokana na mauaji hayo.

Kamanda amesema kuwa hadi sasa chanzo cha mauaji hayo hakijafahamika kwani mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi nakubainika  kuwa hajabakwa kama watu wanavyozusha  bali jeshi la polisi unaendelea na upelelezi wa tukio hilo la mauaji amesema kuwa ukikamilika taarifa kamili itatolewa

Mwili wa marehemu huyo umehifadhiwa kwenye hospitali ya mji wa Babati (Mrara)

Majibu ya Naibu Waziri Kilimo Dr. Mwanjelwa Kuhusu Kauli ya Mzigo Mzito Mpe Mnyamwezi

$
0
0
Mbunge wa Tabora Kaskazini (CCM) Almas Maige amesema umefika wakati sasa ambapo ule usemi wa mzigo mzito kumpa Mnyamwezi uachwe.

Akizungumza kabla ya kuuliza swali la nyongeza, Mbunge huyo alisema kuwa kituo cha wanyama kazi cha Puge kina mfanyakazi mmoja tu ambapo hawezi kufanya kazi zote peke yake.

“Suala la mzigo mzito tumpe Mnyamwez tuache, wapunguze wabebe wenye mzigo,” amesema Maige akiitaka serikali kukisaidia kituo hicho.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Kilimo, Dr. Mary Mwanjelwa alikiri kuwa ni kweli kituo hicho kina mtumishi mmoja lakini akaongeza kuwa wizara hiyo haihusiki.

Alisema kuwa tayari wizara ya kilimo ilihamishia vituo vyote vya aina hiyo nchini kwenye halmashauri za wilaya.

Alizitaka halmashauri hizo kuvipa kipaumbele vituo hivyo kwa lengo la kusaidia wananchi wa maeneo husika.

Kwa upande wake Mbunge wa Lupa Victor Mwambalaswa (CCM) alitaka serikali kugawa eneo la kituo cha utafiti cha Nkena kwa wananchi.

Alisema kuwa kituo hicho kina eneo la hekari 500 ambazo zinaweza kugawiwa kwa wanakijiji kwa ajili ya kilimo.

Aidha Mbunge huyo alimtaka Naibu Waziri kutembelea jimbo la Lupa na kuwaeleza wapiga kura umuhimu wa tafiti.

Akijibu swali hilo Naibu waziri Mwanjelwa alisema kuwa kituo hicho kinatumia eneo hilo kwa ajili ya utafiti wa zao la tumbaku.

Alisema kuwa hata hivyo bado eneo hilo halitoshi na itakuwa vigumu kwa serikali kuligawa.Mbali ya Lupa alisema kuwa  eneo hilo pia linatumiwa na watalaam wa chuo cha utafiti wa kilimo cha Uyole kilichopo jijini Mbeya.

Rais Magufuli Afanya Uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Yohana Luhunga Budeba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (Tanzania Agricultural Research Institute – TARI).

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Dkt. Budeba umeanza June 20, 2018.

Nigeria Yawa Timu Ya Pili Kupata Alama Tatu Kutoka Afrika....Ni Baada ya Kuitandaika Iceland Bao 2-0

$
0
0
Dakika 90 za mchezo wa kundi D umemalizika kwa Nigeria kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Iceland.

Mechi hiyo imekuwa ya pili kwa timu kutoka Afrika kupata ushindi baada ya Senegal kuitwanga Poland 2-1 katika mchezo wa kundi H.

Mabao yote ya Nigeria yamewekwa kimiani na Ahmed Mussa katika dakika za 49 na 75.

Ushindi huo sasa unawaweka pazuri Nigeria na kuwapa imani Argentina kuwa wanaweza kufuzu hatua ya 16 bora kwani kufuzu kwa Argentina na Nigeria kutatokana na timu zote mbili kupata ushindi zitakapo kutana June 26 ila Nigeria hata sare inamvusha hatua inayofuata.

Croatia tayari amefuzu hatua ya 16 kutokana na kupata ushindi mechi mbili na kuwa na point 6, wakati Nigeria wao wapo nafasi ya pili kwa kuwa na point tatu, Iceland nafasi ya tatu kwa kuwa na point moja sawa na Argentina walio nafasi ya nne kwa kutofautiana magoli ya kufungwa.

Mzee Majuto Awasili Kutokea India, Afikishwa Muhimbili

$
0
0
Muigizaji nguli nchini Tanzania, Amri Athuman maarufu kama Mzee Majuto amewasili nchini na kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Ny.0erere jijini Dar es Salaam akitokea nchini India alikokuwa amekwenda kwa ajili ya matibabu.

Mzee Majuto amewasili Airport leo Juni 22, 2018 majira saa 10 jioni na kupelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo atakua hapo kwa muda ili kukutana na wataalam kwa ajili ya uangalizi kukamilisha matibabu yake.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya June 23

Brazil Yajiweka Pazuri kuelekea 16 bora Kombe la Dunia ....Ni Baada ya Kuichapa Costa Rica 2-0

$
0
0
Na, magdalena kashindye
Mabao mawili yaliyofungwa na Philippe Countinho na Neymar Jr katika muda wa majeruhi yameipa Brazil ushindi wa 2-0 dhidi ya Costa Rica.

Countinho alifunga goli lake la pili katika michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea nchini Urusi katika dakika ya ya kwanza ya nyongeza huku mwamuzi akikaribia kupuliza kipenga chake kuashiria kumalizika kwa mechi hiyo,

Neymar aliihakikishia Brazil ushindi kwa kupachika bao katika dakika ya saba ya nyongeza.

Mchezo huo ambao ulipigwa jana jioni, umempa nafasi Neymar Jr ya kufikisha mabao 56 ya kuifungia timu yake ya taifa na kumfanya sasa awe mchezaji wa 3 kufunga mabao mengi zaidi akitanguliwa na Ronaldo De Lima mwenye mabao 62 na Pele 77.

Kwa upande wa Coutinho bao la jana limekuwa la pili kwake kwenye Fainali za mwaka huu likitanguliwa na lile alilofunga kwenye mechi ya kwanza dhidi ya Switzerland ambapo walitoka sare ya 1-1.

Uswizi Yaitandika Serbia 2-1 Dakika za Majeruhi

$
0
0
Switzerland imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Serbia katika mchezo wa kundi E

Mabao ya mchezo huo yalifungwa na Mitrovic mnamo dakika ya 5 tu ya mchezo kwa upande wa Serbia huku la Switzerland likiwekwa kimiani na Granit Xhaka mnamo dakika ya 52 kabla ya Xherdan Shaqiri kuongeza msumari wa mwisho dakika ya 90 ya mchezo

Xhaka ambaye hivi karibuni amesaini mkataba wa muda mrefu kuitumikia Arsenal ameweka rekodi ya kupiga jumla ya pasi 71 ambazo hazijapigwa na mchezaji yoyote wa Urusi katika michuano hiyo tangu 1996.

Matokeo hayo yanaifanya Uswizi kuwa pointi sawa na Brazil katika kundi E lakini ikishika namba 2 kutokana na idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images