Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Mwijaku Amchana Uwoya: “Irene Hana Marafiki Wa Kweli, Shamsa Ford ni Mnafiki”

$
0
0
Muigizaji wa Bongo movie maarufu kama Mwijaku amemmwagia povu zito msanii mwenzake Irene Uwoya baada ya picha yake kusambaa siku ya jana.

Siku ya jana Irene aliposti picha iliyozua utata Kwenye mitandao ya kijamii na mara moja Mwijaku alimwandikia posti nzito ambayo alimsema sana kwa vazi lile hasa kwa sababu ni mke wa mtu.

Lakini Mwijaku hakuishia hapo kwani Kwenye mahojiano aliyofanya na Millard Ayo Tv, Mwijaku alionekana akiweka wazi Kuwa marafiki zake na a Uwoya wanaomsapoti kwa picha zile ni wanafiki wakubwa kwani wanamshauri vibaya wakijua wazi kabisa picha ile siyo nzuri:

"Irene ni mtu mzima na mke wa mtu na hii ni ndoa yake ya pili kwa nini aposti picha kama ile? Nikajiuliza Marehemu Ndikumana angekuwepo wakati amemuoa angeweza kuposti kitu kama kile? Asingeweza kuposti Ndikumana alikuwa mkali ila kwa sababu mume wake Dogo Janja ni mdogo basi anamuonea.

"Halafu na marafiki wanaomzunguka Irene ni wanafiki siku akija kufa atakuwa peke yake halafu na Shamsa Ford anaenda kumwambia hivyo hivyo umependeza ishi utakavyo! Tuongee ukweli Shamsa Ford ni mnafki na anampoteza mwenzake”.

Dogo Janja ambaye ni mume wa Irene Uwoya aliweka wazi kuwa hakukerwa na picha ile zaidi alimpa sapoti mke wake....Tazama Alichoandika


Zari Achaguliwa Kuwa Jaji Wa Mashindano Ya Miss Uganda

$
0
0
Zari The Bosslady amelamba shavu lingine baada ya kutangaza siku ya jana kuwa anatarajia kwenda kuwa ajaji wa mashindano ya ulimbwende nchini Uganda.

Zari amezidi kuthibitisha kuwa yeye ni mfanyabiashara na bosi kwani amekuwa akifanya kila jitihada ya kuingiza mkwanja.

Zari anategemewa kuwa jaji mkuu wa shindano hilo litakalofanyika rasmi tarehe kumi mwezi wa nane mwaka huu katika hoteli ya Sheraton Kampala nchini Uganda.

Kupitia mtandao wa Instagram, waandaaji wa shindano hilo wamethibitisha hilo kwa kuandika,

"The Miss Uganda beauty pageant is proud to announce its first patron and judge for #Missug18 @zarithebosslady 💃💃. Miss Uganda is a celebration of beauty with a purpose to inspire young women to succeed in life.”

"We are also pleased to announce that she will also be a guest speaker at a CSR (corporate social responsibility) activity targeted to young girls organised by the #MissUgandaFoundation. The Miss Uganda pageant is happening on the 10th of August 2018”.

Zari amethibitisha habari hizo kwa kuweka posti hii Kwenye ukurasa wake wa Instagram:

Mbunge CCM Aipinga Serikali Kununua Ndege Badala ya Kuboresha Huduma za Afya, Barabara

$
0
0
Mbunge wa Ulyankulu (CCM), John Kadutu amesema ununuzi wa ndege za Bombardier uliofanywa na Serikali hauna tija kwa wananchi wa jimbo lake iwapo huduma za afya na barabara hazijaboreshwa.

Kadutu ametoa kauli hiyo jana Jumatano Juni 20, 2018 katika mjadala wa bajeti ya Serikali mwaka 2018/19 bungeni mjini Dodoma.

Alisema umebaki mwaka mmoja kabla ya nchi kuingia katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, hivyo ahadi zilizotolewa zinapaswa kutekelezwa.

“Serikali imejenga reli, inanunua ndege hebu twendeni kwa wananchi, ujue ukienda kule Ulyankulu ukauliza Bombardier hawakuelwi, barabara mbovu, afya mbovu hawakuelewi,” alisema Kadutu.

“Pelekeni fedha barabara ziboreshwe, Tarura (Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini) wapewe fedha. Bajeti iliyobaki ni moja ya kujadili kwa utulivu kwani akili itakuwa majimboni tu, tusaidieni ili mwaka 2020 tupete,” alisema.

Akigusia  ahadi za kampeni za uchaguzi, Kadutu alisema waliahidiwa jimbo la Ulyankulu litakuwa wilaya lakini mpaka sasa ahadi hiyo haijatekelezwa.

“Hamtaki kutupa eneo lakini mnasema ahadi za Rais zitatekelezwa, sasa hii ni ahadi ya Rais, alisema akiingia siku tatu tu tunapata wilaya,” alisema.

“Sasa imebaki mwaka mmoja tu na nusu yako mengi, mmetuahidi lami tena kilomita tatu tu lakini tunaona mambo ambayo hayako katika ilani yanatekelezwa. Tukisema…,mimi watu wa Ulyankulu wamenituma.”

Mbunge huyo amesema anashangazwa na mawaziri kutotembelea jimboni kwake huku wakionekana kupishana katika majimbo mengine jambo linalokatisha tamaa wananchi.

Rais Magufuli Ampa Shavu CAG Mstaafu,Ludovick Utouh

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Bw. Ludovick S.L Utouh kuwa Mwenyekiti wa Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali za Madini, Mafuta na Gesi Asilia (Tanzania Extractive Industries Transparency Initiative - TEITI).

Uteuzi wa Bw. Utouh unaanza tarehe 20 Juni, 2018.

Jishindie Gari la Bure Toka Japan.....Kushiriki Ni Bure Kabisa

Onyo Kwa Wanaofanyabiashara Ya Utalii Kinyume Cha Sheria

$
0
0
Hivi karibuni kumekuwepo na wimbi la watu na makampuni yanayofanya biashara ya utalii kinyume cha sheria ikiwemo kutokuwa na Leseni ya Biashara za Utalii (TTBL). Watu hao pia wamekua wakijihusisha na vitendo vya utapeli na udanganyifu kwa watalii na hivyo kusababishia usumbufu mkubwa pamoja kuharibu taswira ya sekta ya utalii na Taifa kwa ujumla.

Tunaendelea kufanya uchunguzi wa kina kuweza kuwabaini wote wanaohusika na vitendo hivyo ili waweze kuchukuliwa hatua kali za kisheria na iwe fundisho kwa wengine. Sheria ya Utalii Na. 29 ya mwaka 2008 Kifungu cha 10, 21 na 31(1-6) inamtaka mtu yeyote anayefanya biashara ya utalii kusajili na kulipa Ada ya Leseni ya Biashara ya Utalii kwa mwaka husika.

Tunasisitiza umma, watalii na wadau wa utalii kwa ujumla kufanya biashara na kampuni zilizosajiliwa na Mkurugenzi wa Utalii na kupewa leseni na Bodi ya Leseni ya Biashara za Utalii kuepuka kutapeliwa na usumbufu mwingine utakaoweza kujitokeza.

Aidha, wafanyabiashara wa utalii, wapya na wale wanaoendelea na biashara, wanajulishwa kuwa maombi ya usajili na utoaji wa leseni za biashara za utalii kwa mwaka 2018 yanaendelea kupokelewa. Ni kosa kisheria kuwasilisha taarifa za uongo na adhabu yake ni pamoja na kufutiwa leseni.

Orodha ya wakala wa biashara ya utalii waliosajiliwa na wenye leseni ya kufanya biashara ya utalii mwaka 2018 inapatikana kwenye tovuti yetu ya Wizara, www.mnrt.go.tz katika kipengele cha wadau (Stakeholders – Tour operators).

Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti yetu ya Wizara, www.mnrt.go.tz  au fika katika ofisi zetu za Makao Makuu zilizopo Mtaa wa Kilimani, Barabara ya Askari - Dodoma au Ofisi za Utalii za Kanda zilizopo Jengo la Mpingo - Dar es Salaam; New Mwanza Hotel - Mwanza; Jengo la NSSF - Iringa na TANAPA Makao Makuu - Arusha.

Maj. Gen. Gaudence Milanzi
KATIBU MKUU
21 Juni, 2018

Wakurugenzi Halotel, Zantel Wahukumiwa Jela miaka 40 Au Faini Milioni 139

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imewahukumu watu sita na kampuni mbili, wakiwamo wakurugenzi watendaji wa kampuni za simu za mkononi, Le Van Dai (35) wa Halotel na Sherif El-Barary wa Zantel,kulipa faini ya Sh. milioni 139 au kwenda jela miaka 40 baada ya kukiri tuhuma za uhujumu uchumi.

Washtakiwa wote walikiri jana tuhuma zilizokuwa zinawakabili zikiwamo za kula njama, kuingiza, kufunga mitambo, matumizi ya laini za simu bila usajili wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), na kuisababishia serikali hasara ya Sh. 1,131,936,000.

Hukumu hiyo ilitolewa na mahakama hiyo chini ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi, Kevin Mhina, baada ya washtakiwa kusomewa mashtaka yao 12 na kukiri.

Upande wa Jamhuri uliongozwa na mawakili wa serikali Jacqueline Nyantori na Batilda Mushi.

Nyantori aliwataja washtakiwa wengine kuwa ni, Lei Cao maarufu kama Peter (28), Huang Yu Meng (27), Msimamizi wa Biashara wa Halotel Zanzibar, Jimmy Mosha (26), Meneja Masoko wa Halotel, Willy Ndoni (29), Kampuni ya Viettel Tanzania Ltd maarufu kama Halotel iliyoko Kinondoni na Kampuni ya Zanzibar Telecommunication PLC, maarufu kama Zantel, iliyoko Msasani, Dar es Salaam.

Alidai katika shtaka la kwanza, kati ya Januari Mosi, 2017 na Aprili 30, mwaka huu nchini Tanzania, mshtakiwa wa kwanza hadi wa sita, walikula njama ya kutenda kosa la kutumia huduma za mawasiliano kwa njia ya udanganyifu.

Katika shtaka la pili, kati ya Mei Mosi, 2017 na Aprili 30, mwaka huu, katika jengo la Spring lililoko Mbezi mshtakiwa wa kwanza hadi wa sita, kwa pamoja walifunga mitambo ya mawasiliano kwa njia ya udanganyifu na kujipatia huduma za mtandao wa Halotel na Zantel bila kibali cha TCRA .

Shtaka la tatu, nne, tano na sita, kati ya Januari Mosi na Desemba 31, 2017, Aprili 30, mwaka huu jijini Dar es Salaam, mshtakiwa wa tatu na wa nne, waliingiza nchini, waliifunga na kuendesha mitambo ya mawasiliano kwa kuunganisha na kampuni hizo za simu bila kibali cha TCRA.

Shtaka la nane, kati ya Mei Mosi, 2017 na Aprili 30, mwaka huu katika jengo la Spring City, mshtakiwa wa tatu na wa nne, walikutwa wakitumia laini za simu za mkononi zisizosajiliwa na TCRA 281,272 za Halotel na 11,920 za Zantel.

Upande huo wa Jamhuri ulidai katika shtaka la 10 kuwa kati ya Mei, 2017 na Aprili 30, mwaka huu katika matawi ya Zantel ya Dar es Salaam, mshtakiwa wa pili na wa nane walitumia kwa makusudi laini za simu 11,920 zisizokuwa na usajili wa TCRA.

Shtaka la 11 na 12, kati ya Mei Mosi, 2017 na Aprili 30, mwaka huu washtakiwa waliisababishia serikali hasara ya Sh. 1,131,936,400.

Kwa mujibu wa mashtaka yanayowakabili washtakiwa kisheria kesi hiyo washtakiwa hawakutakiwa kujibu chochote hadi upelelezi utakapokamilika itasikilizwa Mahakama Kuu Tanzania, Divisheni ya Uhujumu Uchumi au kwa kibali maalumu kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP).

Aidha washtakiwa walikiri maelezo yote ya awali.

Hakimu Mhina aliahirisha kesi hiyo saa 8:05 na kurejea saa 8:30 kuwasomea washtakiwa hukumu.

Hakimu alisema katika shtaka la kwanza na la pili, washtakiwa wanatakiwa kulipa faini ya Sh. milioni 20 au jela miaka sita na kwa kosa la tatu mpaka la sita, walipe faini ya Sh. milioni 20 au kwenda jela miaka minane.

Kwa kosa la saba mpaka la 10, aliamuru walipe faini ya Sh. milioni 22 au kwenda jela miaka 12 na kwa kosa la 11 na la 12, walipe faini Sh. milioni 20 au kwenda jela miaka 14.

Pia mahakama hiyo ilisema washtakiwa walipe fidia ya zaidi ya Sh. bilioni moja wanayodaiwa kuisababishia serikali hasara na mali zote ikiwamo mitambo na kadi za simu wanazodaiwa kukutwa navyo, washtakiwa viteketezwe.

Pia hakimu aliuamuru upande wa Jamhuri uwarejeshee washtakiwa hati zao za kusafiria, vibali vya kuishi nchini na leseni za biashara.

Vigogo hao walilipa faini kuepuka kifungo, kasoro washtakiwa Lei Cao na Huang Meng ambao walipelekwa gerezani.

Kiboko Ya Matatizo Ya Nguvu Za Kiume,maumbile Madogo, Mvuto Wa Mapenzi ,magonjwa Sugu

$
0
0
Usikate tamaa ondoa maradhi yako, maana matatizo haya yamekua yakiasili watuwengi kisaikolojia hasa baada ya kujiona wako tofauti sana na wengine kawaida mwanaume anatakiwa awe na uume kuanzia (6-8) vinginevyo mtuhuyo anamapunguvu katika mwiliwake.

Kunasababu nyingi sana zinazosababisha matatizo haya, chango hushambulia never ambayo huasili misuli ya uume, Ngili :- hii huleta maumivu ya tumbo chini ya kitovu na kufanya tumbo kuunguluma na kujaa gesi, kolodani moja kuvimba au kuingia ndani pamoja na kutopata choo vizuli. Sababuhizi na nyingine hufanya uume kulegea na kusinyaa na kuwa mfupi na mwembamba na marakwamara husababisha kukosa hamu ya kuludia tendo la ndoa na baadae kushindwa kabisa

MASISA 3POWER :- nidawa ya mitishamba iliyotengenezwa kwa mfumo wa vidonge, huongeza nguvu za kiume maradufu kuanzia umri wa miaka 15-90 , inakomaza mbegu zisizo na viini vya uzazi (manii) inaimalisha mishipa iliyolegea wakati wa tendo la ndoa, itakufanya uludie tendo la ndoa zaidi ya mara nne (4) birahamu kuisha wara kuhisi kuchoka na itakufanya uchelewe kufika kileleni zaidi ya dk (20-30 )

YONINANI:- hurefusha na kunenepesha maumbile madogo ya uume uliosinyaa inchi 6-8 na unene wa sm 3-4 kwa mda mfupi sana,

SUPER MORINA :- nidawa inayotibu ama kutatua tatizo la kisukali kwawaliohangaika bila mafanikio, huondoa tatizo la kisukali na kupona kabisa, vilevile ninadawa ya magonjwa sugu km vile presha, vidondo vya tumbo, miguu kuwakamoto, muwasho mwilin, kaswende,uzazi nk.

LUGIMBA :- nidawa ya mvuto wa mapenzi, humtuliza mke, mme, mchumba, hawara au mtu yoyote umpendae na kumfanya akutimizie chochotekile unachokitaka kutoka kwake na kumfunga asiwe na mtu yoyote zaidi yako.

WASILIANA NA DR CHIPUPA NAPATIKANA DAR ES SALAAM KUMBUKA HUDUMAHII ITAKUFIKIA POPOTE ULIPO  0759208637 / 0785687900

TTCL yaipa Serikali gawio la Bilioni 1.5

$
0
0
 Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), limetoa gawio la Sh1.5bilioni kwa Serikali, fedha zilizotokana na faida ya Sh28.5 bilioni ya shirika hilo kwa mwaka jana. Shirika hilo lilipata faida ya Sh29.2 bilioni kabla ya kukatwa kodi.

Akizungumza leo Juni 21 mbele ya Rais John Magufuli wakati wa hafla ya kupokea gawio hilo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Waziri Kindamba amesema faida hiyo inatokana na mabadiliko makubwa yaliyoanza kuonekana kupitia uongozi wa awamu ya tano.

“Tuliahidi kutoa gawio la Sh1 bilioni, lakini baada ya bodi ya shirika kukaa ikaamua kuongeza gawio hilo baada biashara kwenda vizuri,”amesema.

Kindamba amesema katika juhudi za kuimarisha shirika hilo, wameanza kutekeleza maagizo ya Serikali baada ya kupunguza safari za nje kwa waendaji wake na kufuta mikataba mibovu isiyokuwa na manufaa kwa shirika hilo.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Mwenyekiti wa Bodi ya TTTCL, Omar Nundu huku Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akishiriki kwa njia ya teknolojia ya mawasiliano ya video moja kwa moja kutoka Dodoma.

Rais Magufuli Awataka TTCL Wasibweteke

$
0
0
Rais John Magufuli amelitaka Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kutobweteka baada ya kupata mafanikio makubwa.

Amesema kama TTCL itajiona imefanikiwa na kuendelea kubweteka, itajikuta ikitoka katika reli na kupoteza mafanikio yake.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Juni 21 wakati akipokea gawio la Sh1.5 bilioni kutoka shirika hilo.

 “Nawapongezeni sana kwa mafanikio haya mliyopata katika kipindi cha miaka miwili, hongereni sana. Lakini hata hivyo itakuwa ni jambo la aibu sana kama mafanikio mliyopata yakawafia mikononi,” amesema.

Rais amesema pamoja na mafanikio hayo pia waangalie namna ya kuendelea kuboresha huduma na kuangalia njia nyingine za kujiongezea kipato.

“Pia angalieni uwezekano wa kupunguza gharama ili muendelee kupata wateja zaidi,” amesema.

Viwanja vya makazi Vinauzwa Bunju na Mapinga Kwa Bei Nzuri

$
0
0
Viwanja vya makazi: Bunju na Mapinga
Viwanja vipo Kimele, ni km 3 kutoka main road.
 
Vipo viwanja size zote kwa bei tofauti: mil 2 for 10/20, mil 4 for 20/20, mil 6 for 20/30, mil 8 for 20/40, mil 12 for 30/40, mil 16 for 40/40 na mil 24 for 40/60. 

Ruksa kulipa kwa awamu. Hakuna dalali, mpigie mhusika: 0757489709

Rais Magufuli Atamani Wafanyakazi TTCL Waongezewe Mishahara Kwa Kazi Nzuri Wanayofanya

$
0
0
Kutokana na faida waliyoipata mwaka 2017 hadi kutoa gawio la Sh1.5 bilioni kwa Serikali, Rais John Magufuli amesema wafanyakazi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) wana haki ya kuongezewa mishahara.

Akizungumza leo Juni 21 wakati wa hafla ya Serikali kupokea gawio hilo kutoka TTCL, Rais amesema hata kama hajapandisha mishahara kwa watumishi wote wa Serikali lakini shirika hilo limeonyesha jinsi linavyotanguliza masilahi ya Taifa mbele.

“Tangu shirika hili lianzishwe mwaka 1993 halijawahi kutoa gawio. Uchapakazi wenu unaonekana. Ingawa sijaongeza mishahara kwa watumishi lakini ninyi ayayaya,” amesema Magufuli.

Serikali imepokea gawio kutoka shirika hilo ukiwa ni mwaka mmoja tangu lilipobadilishwa kutoka kuwa kampuni na kuanza kujiendesha kwa faida.

Rais ameyataka mashirika ya umma kujiendesha kwa faida na kutoa gawio huku akiyasisitiza kujiendesha kwa ufanisi.

Amesema mwaka 2005 kulikuwa na mashirika 92, lakini ni manne yaliyotoa gawio la Sh130.868 bilioni.

Baadaye yaliongezeka mashirika 24 yaliyotoa gawio la Sh149.3 bilioni mwaka 2006 na mwaka 2007 mashirika 38 yaliipa Serikali Sh677 bilioni.

Nafasi za Masomo Shule ya Lake Tanganyika.....Ewe Mzazi, Mpeleke Mtoto Akapate Elimu Bora, kwa Ada Nafuu Kabisa

$
0
0
Tangazo Shule ya sekondari Lake Tanganyika iliyopo kijiji cha Mkigo,wilaya ya Kigoma Vijijini mkoa wa Kigoma inawatangazia watu wote nafasi za masomo kwa kidato cha kwanza na cha tatu.

Shule ina walimu wa kutosha wenye ari na uzoefu kufundisha masomo ya sanaa na sayansi.

Ada zetu ni nafuu sana ambazo ni laki saba kwa mwaka (700000)na michango ya laki na hamsini(150000). Ada inalipwa mara nne kwa mwaka yaani (175000) kwa kila awamu.

Kwa mawasiliano tumia nambari 0769697667,0763091810,0745907094,au fika shuleni kwa maelezo zaid.

Lake Tanganyika, the World of Champion....Ewe mzazi/mlezi mlete mwanao apate elimu bora

Seth aruhusiwa Kuongea na Mkewe Mahakamani

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeruhusu Mmiliki wa Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL, Harbinder Seth  kuongea na mke wake mahakamani baada ya kutokumuona kwa muda wa miezi mitatu.

Ruhusa hiyo imetolewa leo June 21 na Hakimu Mkuu Mkazi, Huruma Shaidi baada ya upande wa mashtaka kuwasilisha ombi hilo kufuatia kutokuwa na kibali cha kumuona mumewe huyo gerezani.

Kabla ya kutolewa kwa ruhusa hiyo, wakili wa utetezi, John Chuma aliomba mshtakiwa aweze kuonana na mkewe ambaye hajaweza kumuona kwa kipindi cha miezi 3 sababu kipindi chote hicho alikuwa amefiwa na mama mkwe wake( mama wa mkewe).

“Mheshimia tunaomba mshtakiwa namba moja (Sethi) aweze kuongea na mke wake ikiwezekana hata kumkumbatia ili aweze kumpa pole ya kufiwa na mama yake kwa sababu bado hajapata kibali cha kuruhusiwa kwenda kumuona gerezani”

Akijibu ombi hilo Wakili wa serikali kutoka TAKUKURU, Leornad Swai, alidai, ” kwa sababu ni ombi anaomba kusalimiana na mkewe hapa mahakamani sina pingamizi lakini kwa magereza kuna taratibu zake na mkewe alizivuruga yeye mwenyewe”

Kufuatia majibu hayo, Hakimu Shahidi aliruhusu mshtakiwa kuongea na mkewe mahakamani hapo chini ya uangalizi wa askari magereza.

Kesi hiyo ambayo leo ilikuja kwa ajili ya kutajwa, upelelezi bado haujakamilika, imeahirishwa hadi July 5, mwaka huu.

Mbali na Seth mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ni James Rugemalira ambao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka kumi na mawili ya uhujumu uchumi ,utakatishaji fedha  na kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya shilingi bilioni mia tatu.

Rais Magufuli: “Kuna vilaza wanaajiriwa nawaona tu”

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ameinyooshea kidole wizara ya kazi na ajira kuwa kuna watu wameajiriwa lakini wanafanya kazi chini ya kiwango jambo ambalo hapendezwi nalo.

Rais ametoa kauli hiyo mapema leo wakati akipokea gawio la Serikali kutoka Shirika la Simu Tanzania (TTCL) , ambapo amesema kuwa suala hilo ameliona na amewaachia wabunge walitazame kwa mapana.

“Wizara ya Kazi kuna matatizo matatizo huko, nimeshayaona, nimeanza kuyafuatilia, kuna wengine vilaza kabisa lakini wanaletwa huko kuja kufanya kazi, hili nitalishughulikia, nalichomekea tu ili wabunge walitazame”, amesema Rais Magufuli.

Wizara hiyo ambayo iko chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) inaongozwa na Waziri Jenista Mhagama, pamoja na Naibu wake Anthony Mavunde.

Papa Francis Amteua Askofu Mkuu Ruwaichi Kumrithi Kadinali Pengo

$
0
0
Baba  Mtakatifu Francis amemteua Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mwanza Yuda Thaddeus Ruwaichi kuwa mrithi mtarajiwa wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, ambalo limekuwa linaongozwa na Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo. 

Kwa uteuzi huu, Askofu Mkuu Ruwaichi anakuwa Askofu Mkuu Mwandamizi Mwenye Haki ya Kurithi Jimbo Kuu la Dar es Salaam.

Inasemekana kuwa uteuzi huu maana yake huenda mchakato wa kustaafu kwa  Kardinali Pengo umekamilika, hasa kutokana na matakwa ya kisheria kuhusu umri, na kwa sababu ya afya yake kutetereka.

Kabla ya kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Kardinali Pengo naye aliteuliwa kuwa askofu Mkuu Mwandamizi Mwenye Haki ya Kurithi tarehe 22 Januari 1990. Aliteuliwa kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam tarehe 22 Julai 1992 baada ya kustaafu kwa Mwadhama Laurean Kardinali Rugambwa.

Kabla ya uteuzi huu, Askofu Mkuu Ruwaichi alikuwa ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mwanza tangu tarehe Novemba 10, 2010.  Kwa uteuzi huu wa leo, Askofu Mkuu Ruwaichi amepitia katika mikono ya wateuzi watatu – Papa Yohanne Paulo II, Papa Benedicto XVI, na Papa Francis.

Askofu Mkuu Ruwaichi alizaliwa tarehe 30 Januari 1954, Mulo, Kilema, Jimbo Katoliki la Moshi. Alipadirishwa  tarehe 25 Novemba 1981, akapewa daraja la uaskofu tarehe 9 Februari 1999. Baba Mtakatifu Yohane Paulo II alipomteua kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Mbulu, na akawekewa wakfu tarehe 16 Mei 1999.

Tarehe 15 Januari 2005, Baba Mtakatifu Yohane Paulo II akamteua kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Dodoma na kusimikwa rasmi tarehe 19 Februari 2005. Tarehe 10 Novemba 2010, Baba Mtakatifu Mstaafu Benedikto XVI akamteua kuwa Askofu mkuu wa Jimbo Kuu la Mwanza, akasimikwa rasmi tarehe 9 Januari 2011. 

Denmark yalazimishwa sare ya bao 1 – 1 na Australia kombe la dunia nchni Urusi

$
0
0
Michuano ya Kombe la Dunia 2018 imeendelea tena leo kwa timu ya taifa ya Denmark kucheza mchezo wake wa pili wa hatua ya makundi dhidi ya timu ya taifa ya Australia.

Mchezo wa Denmark ulikuwa na mvuto zaidi kwa upande wa Tanzania, hii inatokana na uwepo wa staa wa Denmark mwenye asili ya Tanzania Yussuf  Yurary Poulsen ambaye mchezo uliopita aliipatia ushindi Denmark dhidi ya Peru wa goli 1-0.
 
Denmark leo wakicheza mchezo wao wa pili wameambulia sare ya kufungana goli 1-1, goli la Denmark lilipatikana dakika ya 7 kupitia kwa staa wao Christian Eriksen lakini Australia walisawazisha goli hilo dakika ya 38 kwa mkwaju wa penati baada ya Yussuf Poulsen kushika mpira katika eneo la hatari.

Poulsen baada ya kushika katika eneo la hatari na kusababisha penati alioneshwa kadi ya njano ikiwa hiyo ni kadi yake ya pili katika World Cup 2018 na amesababisha penati kwa mara ya pili, Yussuf anakuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya World Cup kusababisha penati nyingi (2) katika msimu mmoja toka 1966.

Sare hiyo sasa inawaweka pazuri Denmark kwa kufikisha point nne na wanahitaji point moja tu mchezo ujao dhidi ya Ufaransa ili wafuzu hatua ya 16 bora au kama ikitokea bahati mbaya wakapoteza, basi watahitaji kuomba Peru amfunge Australia mechi ya mwisho huku Ufaransa leo afanikiwe kumfunge Peru.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa ya June 22

Waziri Mkuu: Serikali Kuongeza Wataalamu Wa Afya

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itaongeza idadi ya wataalamu wa afya nchini watakaodahiliwa katika vyuo vya afya vya Serikali na binafsi katika programu za Uuguzi na Ukunga, Sayansi Shirikishi za Afya na wahudumu Afya ya Jamii.

Waziri Mkuu ameyasema hayo jana  (Alhamisi, Juni 21, 2018) wakati akizindua majengo ya Taasisi ya Elimu ya Afya Mvumi, yaliyojengwa kwa ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa Kupambana na UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria.

Amesema Serikali ya Awamu ya Tano, inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, itaendelea kushirikiana na wadau wote kuboresha vyuo vya mafunzo ya afya kwa kufanya upanuzi, ujenzi wa majengo na ukarabati.

Waziri Mkuu amesema ukarabati na upanuzi utafanyika katika vyuo vya uuguzi vya Nachingwea, Kibondo, Kagemu, Kondoa, Same na Kiomboi na vyuo vya Mafunzo ya Maafisa Afya vya Bombo (Tanga), Mpwapwa na Ngudu (Mwanza) na Chuo cha Maafisa Tabibu cha Kibaha na Chuo cha Maabara Singida.

Amesema lengo la Serikali ni kuongeza idadi ya wataalamu wa fani mbalimbali wenye uadilifu na weledi wa kustahili pamoja na  kusimamia ubora wa mafunzo ya kada za afya zisizo katika kiwango cha shahada. 
 
Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali itaongezaidadi ya udahili wa wanafunzi watakaosomea utaalamu wa kibingwa katika fani mbalimbali na kuajiri watumishi wa kada za afya katika vituo vya kutolea huduma za afya nchini kwa kuzingatia maeneo yenye uhaba mkubwa wa watumishi hususan maeneo ya vijijini.

Amesema Serikali itaendelea itasimamiana kuratibu uandaaji wa wataalamu wa sekta mbalimbali ikiwemo ya afya kutoka vyuoni ili waendelee kuwa nguzo muhimu ya utoaji huduma za afya kwa wananchi.

Pia, Waziri Mkuu amewasihi wakufunzi wote nchini watekeleze majukumu yao kwa weledi na Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali itaendelea kuhakikisha uwepo wa mazingira bora ya kufundishia na kujifunzia.

“Vilevile, nitumie hadhara hii kutoa rai kwa wanafunzi wote nchini wasome kwa bidii na kuhakikisha wanahitimu vyema masomo yao ili waweze kutimiza malengo yao binafsi sambamba na kuleta tija na ufanisi kwa Taifa letu muda wote na popote pale watakapokuwa wakitekeleza majukumu yao,”.

Awali, Mkurugenzi wa Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii (CSSC), Bw. Peter Maduki alisema mradi huo ambao ulisimamiwa na CSSC ulianza Aprili 2015 na ulitarajiwa kukamilika Mei 2016. “Kutokana na changamoto mbalimbali mradi ulikamilika Machi 2018,”.

Alisema mradi huo ambao umegharimu sh. bilioni 5.2 kati yake sh. bilioni 4.4 zilitumika katika upanuzi, ukarabati wa majengo na ujenzi wa majengo mapya ya kulala wanafunzi mawili, jengo la utawala na sh. milioni 864.4 zilitumika kununulia vifaa vya kufundishia.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Bibi Ummy Mwalimu, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.Binilith Mahenge, Mwakilishi wa Global Fund, Bi. Martha Setembo, Mkurugenzi wa Tume ya Kikristo ya Huduma za Jamii Bw. Peter Maduki na Mbunge wa Mtera Bw.  Livingstone Lusinde na Viongozi wa Dini.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Mtibwa Sugar U-20,Mabingwa Wapya Kombe La Uhai Cup 2018

$
0
0
Timu ya Mtibwa Sugar wamefanikiwa kuipoka Simba ubingwa wa michuano ya Vijana wa Timu za Ligi Kuu Bara chini ya Umri wa MIaka 20 (Uhai CUP – Under 20) baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Stand United.

Stand wamechukua taji hilo ambalo lilikuwa linatetewa na aliyekuwa bingwa mtetezi, Simba SC ya jijini Dar es Salaam.

Mtibwa wamefanikiwa kutwaa kombe hilo kwa mara ya kwanza tangu kuazishwa kwake kupitia udhamini wa Maji ya kunywa ya Uhai.

Singida nao baada ya kupoteza wanakuwa wanaambulia nafasi ya pili kwenye mashindano hayo yaliyokuwa yanatimua vumbi kwenye Uwanja wa Chuo kikuu jijini Dodoma (UDOM).
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live


Latest Images