Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Waziri Mkuu aongoza mamia ya wananchi wa Mkoa wa Dodoma kuuaga mwili wa aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mara, marehemu John Gabriel Tupa

0
0
  Viongozi Dini wakiongoza ibada ya kuuaga mwili wa Marehemu John Gabriel Tupa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara na hapo awali aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma,aliefariki ghafa siku kadhaa zilizopita. Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akitoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu John Gabriel Tupa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara na hapo awali aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma,

Rais Kikwete apokea ripoti ya mahesabu ya Serikali toka kwa mkaguzi mkuu wa Serikali Ikulu jijini Dar

0
0
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Ripoti ya Mwaka kutoka kwa Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Bw. Ludovick Utouh Ikulu jijini Dar es salaam leo. Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akisikiliza muhtasari toka kwa Mthibiti na Mkaguzi Mkuuwa Hesabu za Serikali Bw. Ludovick Utouh kabla ya kupokea Ripoti ya mwaka Ikulu jijini Dar es salaam leo.    Rais Dkt

Yaliyojiri Bungeni Dodoma Ijumaa ya leo ya tarehe 28 Machi 2014 kuhusu Maamuzi ya kura ya WAZI au ya SIRI

0
0
  Wapendwa  wasomaji, kama Mwenyekiti wa Bunge Maalum, Sammuel Sitta alivyotangaza jana wakati akiahirisha kikao cha jioni, kwamba, kazi kubwa ya leo ni kufanya maamuzi juu ya vifungu vya 37 na 38 vya Kanuni za Bunge Maalum ambavyo vinahusu jinsi ya kufanya maamuzi. Mjadala hapa ambao umeteka hisia za wananchi wengi ndani na nje ya Bunge ni juu ya Kura ya Siri au ya Wazi.  Hakika

Wawili wafariki dunia, Saba wajeruhiwa na wanne hawajulikani walipo baada ya ajali ya treni ya mizigo Gulwe mkoani Dodoma

0
0
Wafanyakazi walioajiriwa na shirika la Reli Tanzania (TRL) wakitoa mchanga kwenye kichwa cha treni ya mizigo kilichopata ajali usiku wa kuamkia katika stesheni ya Gulwe, Wilaya ya Mpwampwa. Katika ajali hiyo watu wawili wamefariki dunia na wengine saba kujeruhiwa na kulazwa katika hospital ya Benjamin Mkapa Wilayani Mpwampwa. Sehemu ya mabehewa ya mafuta na ngano ambayo

Bunge Maalum la Katiba lapitisha azimio la kura ya mseto....Kura ya SIRI na ya WAZI itatumika kwa pamoja katika kuendesha bunge hilo

0
0
  Na Magreth Kinabo, Dodoma Hatimaye baada ya mvutano wa baadhi wa wajumbe wa Bunge la  Maalum la Katiba kuhusu upigaji wa kura ya siri na ya wazi kuendelea  leo  Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge Maalum, Mhe . Pandu Ameir Kificho amewasilisha  azimio la mapendekezo ya  ya upigaji kura wa wazi na siri  kutumika kwa pamoja katika kaununi ya 37 na 38, ambalo

Picha: Madhara yaliyosababishwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha jijini Dar....Barabara hazipitiki

0
0
  Mvua zilizoanza kunyesha juzi usiku na kuendelea jana  jijini Dar es Salaam zimesababisha adha katika makazi ya watu hasa wanaoishi katika maeneo ya mabondeni na watumiaji wa barabara kutokana na miti kuanguka na kuziba njia huku maji yakijaa barabarani na kusababisha ugumu kwa vyombo vya moto kupita....           <!-- adsense -->

Aunt Ezekiel achizika na busu la MBWA......

0
0
  Diva wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel ameonekana kuchizika na busu la mbwa baada ya kunaswa akiwa amewabeba mbwa wawili na kufurahia mmoja wapo alipombusu. Tukio hilo lilitokea juzikati nyumbani kwa Wema Sepetu, Kijitonyama, jijini Dar. Alipoulizwa furaha aliyokuwa nayo baada ya kubusiwa na mbwa huyo, Aunt alisema: “Haipimiki. Natamani na mimi kuwafuga  wawe  wananibusu  kila  siku.”

Mwanamke ashitakiwa kwa kumuua mwanae wa miaka 4 baada ya kuhisi ni SHOGA .... ujumbe wa Facebook wammaliza

0
0
Mwanamke aliyetajwa kwa jina la Jessica Dutro, anakabiriwa na kesi ya mauaji huko Washington Marekani baada ya kutuhumiwa kuwa alimpiga mwanae wa miaka 4 hadi kumuua baada ya kuhisi kuwa atakuwa ‘shoga’.   Waendesha mashitaka walidai kuwa August 14, 2012 mama huyo aliwapiga vibaya watoto wake watatu, lakini kipigo kilikuwa kikali zaidi kwa mwanae aitwae Zachary Dutro- Boggess ambaye

Magazeti ya leo Jumapili ya tarehe 30 March 2014

0
0
                  Magazeti  ya  leo   Jumapili  ya  tarehe  30  March  2014 <!-- adsense -->

CCM yaendelea na mbio zake katika kampeni za uchaguzi mdogo Chalinze

0
0
Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Hondogo,Kata ya Mandera wakati wa muendelezo wa Mikutano yake ya Kampeni za kuomba ridhaa ya kuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Machi 29,2014. Mbunge wa Jimbo la Kisarawe,Suleiman Jaffo akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Mandera Kibaoni wakati

Makamu wa Rais Dr. Bilal aongoza mazishi ya aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mara, marehemu John Gabriel Tupa mkoani Morogoro

0
0
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiaga mwili wa aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Mara Marehemu John Gabriel Tupa, baada ya mazishi yake yaliyofanyika  jana  Machi 29-2014 Wilayani Kilosa  Mkoani Morogoro.  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiweka shada la maua kwenye kaburi la aliyekuwa mkuu wa

Watanzania wenzetu wazuia KUCHOMWA MOTO kwa mpendwa wetu Augustino Michael Lukindo aliyefariki Wisconsin, Marekani

0
0
Watanzania wenzetu  wamezuia kuchomwa moto kwa mpendwa wetu  Augustino Michael Lukindo aliyefariki dunia  jijini Madison, jimboni Wisconsin nchini Marekani  jumapili ya March 16, 2014.  Wameomba msaada kwa Watanzania wengine waishio Marekani na kokote pale Duniani kujitahidi kadri tuwezavyo tuweze kumstiri Mtanzania mwenzetu .Gharama za mazishi ni $6,000 ....   jina la AC ni

Ajali MBAYA yaua wanawake 12 mkoani Kilimanjaro waliokuwa wakienda msibani....Majina yao yatajwa, Saba wajeruhiwa

0
0
Waombolezaji 12 waliokuwa njiani kuhani msiba wa mtoto aliyepoteza maisha baada ya kusombwa na mafuriko, wamefariki dunia na wengine saba wamejeruhiwa, baada ya gari lao kugongwa na malori mawili kwa wakati mmoja. Abiria hao walikuwa wanasafiri na gari dogo aina ya Toyota Pick Up namba T 170 AKZ kwenda kuhani msiba uliotokea katika kijiji cha Kongei kilichoko Hedaru mkoani

Lulu Michael ABUGI Instagram baada ya kuweka picha hii.....Mashabiki wamtandika Matusi, wadai AMEJIDHALILISHA....

0
0
Muda  mfupi   jana  baada ya Lulu  Michael   kuposti mwonekano wa mbele wa jarida la VIBE utakavyo  kuwa, huku  ukiwa  umepambwa  na  picha  yake  ya  nusu  uchi, watu wengi walianza kumshambulia kwa  maneno  machafu  kwamba  ameiga  pozi la Rihana alilotumia katika Jarida GQ mwaka jana. Wengi wamelalamika na kusema kuwa  Lulu  amejishusha sana na  amechafua  sifa ya gazeti hilo kwa

INASITIKISHA.....Watu wengine 21 wafariki dunia katika ajali mbaya iliyohusisha magari manne mkoani Pwani

0
0
Watu 21 wamefariki dunia katika ajali mbaya iliyotokea jana saa mbili usiku katika Wilaya ya Rufiji, mkoani Pwani ikihusisha magari 4  na wengine 11 kujeruhiwa. Akizungumzia tukio hilo kwa njia ya simu jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, ACP Ulrich Matei, alisema ajali hiyo imetokea katika Barabara Kuu ya Dar es Salaam-Lindi, eneo la Ikwiriri, wilayani humo. Awali ajali hiyo

Magazeti ya leo Jumatatu ya tarehe 31 March 2014

0
0
                Magazeti  ya  leo  Jumatatu  ya  tarehe  31  March  2014 <!-- adsense -->

"Mimi na Gardner tumefikia hatua ya kuishi kama DADA na KAKA"....Lady Jayde

0
0
Staa wa  kike  katika  muziki  wa  bongo, Judith Wambura a.k.a Lady Jaydeee au Jide amefunguka kuwa yeye na mumewe, Gardner Habash ‘Kapteini’ kwa sasa wanaishi kama kaka na dada hivyo kuibua swali kivipi?  Akizungumza na  gazeti  la  Ijumaa Wikienda katika mahojiano maalum yaliyofanyika kwenye mgahawa wa staa huyo wa Nyumbani Lounge uliopo Ada Estate, Kinondoni jijini Dar mwishoni mwa

Snura wa Majanga asimulia jinsi KIUNO chake kilivyomponza na kusababisha KTMA wamteme

0
0
Baada ya kutolewa video yake ya Nimevurugwa kwenye tuzo za KTMA  2013/2014,  Snura amefunguka  kuhusu  kile ambacho kilionekana kusababisha video yake kufungiwa na kutolewa kwenye mashindao ya Kilimanjaro Tanzania Music Awards  kwa  kudai  kuwa  kiuno  chake  ndo  tatizo  hivyo  katika  video  yake  mpya  hakutakuwa  na  mauno  ya  mitego!: "Snura mpya ataonekana kwenye video ya

Njia 64 za daladala jijini Dar zitasitishwa kutokana na kuanza kwa Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka Dar es Salaam (DART)

0
0
NJIA 64 za magari ya daladala jijini Dar es Salaam zitakoma kutumika kutokana na kuanza kwa Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka Dar es Salaam (DART).   Kwa kuanzia matayarisho ya kupisha mradi huo, Wakala wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (DART) umetaka wamiliki wote wa mabasi ya daladala yanayopita katika Barabara ya Morogoro au kukatiza katika njia hiyo, kufika katika ofisi

TANAPA yakanusha taarifa zinazodai kuwa Hifadhi ya Taifa ya Katavi imeuzwa

0
0
SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA), limekanusha taarifa zinazodai Hifadhi ya Taifa ya Katavi ipo kwenye mpango wa kukabidhiwa kwa wawekezaji kutoka nchini Afrika Kusini.   Habari hiyo iliandikwa Machi 25 mwaka huu na gazeti moja linalotoka mara moja kwa wiki ikiwa na kichwa cha habari kinachosema, "Nyalandu 'auza' Hifadhi”.   Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TANAPA kupitia Idara
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images