Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Ufaransa Yaanza Vizuri Kombe La Dunia Kwa Kuipiga 2-1 Australia

0
0
Ufaransa imefanikiwa kuibuka na ushindi wake wa kwanza katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka huu nchini Urusi  wa mabao 2-1 dhidi ya Australia.

Mabao ya mchezo huo yametiwa kimiani na Antoine Griezmann katika dakika ya 58 kwa njia ya mkwaju wa penati na la pili likitiwa kimiani na Paul Pogba .

Bao pekee la Australia liliwekwa wavuni na Mile Jedinak mnamo dakika ya 62 kwa mkwaju wa penati.

Mechi hii imekuwa ya kwanza kushuhudiwa penati mbili ndani ya dakika 90 zikipigwa kwa pande zote.
Ushindi huu wa Ufaransa unawapa alama tatu muhimu kwenye kundi C ambapo baadaye Peru na Denmark watakuwa wanacheza pia kutoka kundi hilo.

Messi akosa penalti....Argentina Yabanwa Mbavu na Iceland Kwa Sare ya Bao 1-1

0
0
Mshambuliaji Lionel Messi ameanza vibaya Kombe la Dunia baada ya kukosa penalti huku Argentina ikilazimishwa sare 1-1 na  Iceland katika mchezo wa kwanza wa Kundi D.

Messi alikosa penalti dakika 65, baada ya kipa wa Iceland, Halldorsson kuipangua.

Awali mshambuliaji Aguero aliangushwa na beki wa Iceland, Magnusson ndipo mwamuzi akatoa penalti hiyo.

Argentina ilianza mchezo huo kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la kuongoza lililofungwa na Sergio Aguero kabla ya Iceland kusawazisha kupitia Alfreo Finnbogason.

Argentina ilitawala mchezo huo, lakini kikwazo kikubwa kwao alikuwa kipa Halldorsson aliyefanya kazi kubwa kuokoa hatari zote.

Iceland iliyocheza kwa nidhamu kubwa ya kujilinda muda wote mbinu yao ilifanikiwa na kuwafanya Argentina kushindwa kupata ushindi waliotegemea.

Breaking News: Orodha ya majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha TANO, Vyuo vya Ufundi na Vyuo vya Elimu ya Kati kwa mwaka 2018

0
0
Wanafunzi 70,904 waliohitimu kidato cha nne mwaka jana wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano, vyuo vya ufundi na vya elimu ya kati kwa mwaka 2018, huku wengine 21,808 waliokuwa na sifa za kuchaguliwa wakiachwa.

==>>Orodha Yote ya Majina iko hapo chini

NB:  Server iko bize kidogo, endelea kurefresh kama itakuwa inagoma kufunguka

Kipa wa Iceland aibuka mchezaji bora

0
0
Golikipa wa timu ya taifa ya Iceland, Hannes Þór Halldórsson, amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi katika mchezo wa leo dhidi ya Argentina kwenye michuano ya Kombe la Dunia.

Halldorsson amepata tuzo hiyo baada ya kuokoa mipira mingi ya wachezaji wa Argentina ikiwemo penati ya Lionel Messi, ambayo ilionekana kumaliza furaha ya mchezaji huyo uwanjani.

Katika mchezo huo, mechi hiyo imeweza kumalizika kwa matokeo ya 1-1 na timu zote kuweza kuambulia alama moja.

Kipa huyo amemzuia Messi kujibu mapigo ya Hat-Trick aliyoyafanya Ronaldo jana dhidi ya Spain, Iceland imekuwa taifa dogo zaidi kushiriki kwenye michuano ya Kombe la dunia.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya June 17

UKAWA Wataja Vipaumbele Vitano Bajeti ya Upinzani

0
0
Kambi ya Upinzani Bungeni imetaja mambo matano ambayo ni vipaumbele kwa bajeti mbadala ya mwaka wa fedha 2018/19.

Vipaumbele hivyo ni elimu, kilimo, viwanda katika mnyororo wa thamani ya kilimo, huduma za afya, maji na uchumi.

Kiongozi wa kambi hiyo, Freeman Mbowe alisema hayo jana  Juni 16, 2018 jijini Dodoma alipozungumza na waandishi wa habari.

“Vipaumbele hivi ukivitengea fedha za kutosha mathalan hizi Sh700 bilioni za Stigler’s Geoge kwa mwaka mmoja tu, maisha ya wananchi yangekua, lakini si kwa kuweka kipaumbele katika maeneo yasiyokuwa na tija moja kwa moja kwa wananchi,” alisema.

Mbowe alikosoa bajeti ya Serikali ya mwaka 2018/19 ya Sh32.5 trilioni iliyowasilishwa bungeni Juni 14, 2018 akisema haitekelezeki.

Kiongozi huyo ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema, amlisema Serikali imekuwa haizingatii sheria ya fedha na kinachotengwa sicho kinachotolewa na hasa fedha za maendeleo

Kocha wa Nigeria aeleza sababu za Kutandikwa Bao 2-0 Na Croatia Jana Usiku

0
0
Kocha ya kikosi cha timu ya taifa ya Nigeria, Gernot Rohr amesema kuwa makosa mengi waliyoyafanya katika mechi dhidi ya Croatia ni chanzo kikuu cha kipigo cha 2- 0 walichopokea.

Kikosi hicho maarufu kama ‘Super Eagles’ kilipokea kipigo hicho jana katika uwanja wa Kaliningrad nchini Urusi ambapo mchezaji wake Oghenekaro Etebo alijifunga na pia kupokea kipigo cha mkwaju wa penati uliopachikwa na Luka Modric.

“Tunafahamu kuwa tulifanya makosa mengi sana ambayo yalikuwa muhimu; na iko wazi kuwa tunatakiwa kuhakikisha tunayafanyia kazi ili twende mbele,” alisema kocha huyo.
 
Aliongeza kuwa kipigo hicho kimewavunja moyo wachezaji na kwamba wanapaswa kufanya kazi kiuweledi zaidi watakapokutana na vigogo wengine Argentina na Iceland.

“Tulijipanga vizuri na iko wazi kuwa mbinu zetu hazikuwa mbaya. Lakini tunatakiwa kuhakikisha tunazingatia weledi zaidi kabla ya michezo inayofuata,” aliongeza.

Aidha, kocha huyo ambaye amekiri kuwa kupoteza mchezo huo wa jana kunafanya kazi waliyoianza kuwa ngumu zaidi, alisema kuwa kiwango cha soka kilichooneshwa na nahodha wa timu hiyo Mikel Obi kilikuwa cha kuridhisha sawa na kiwango kilichooneshwa na safu ya ulinzi.

Messi aeleza machungu aliyoyapata kwa kukosa penati

0
0
Mshambuliaji wa kutegemewa wa kikosi cha timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi amesema kuwa imemuuma sana kukosa penati iliyosababisha kutoka sare ya 1-1 na Iceland kwenye mechi ya makundi ya fainali za Kombe la Dunia.

Mkwaju wa penati wa Messi ambao ulivuta lenzi za macho ya wengi uliishia mikononi mwa mlinda mlango Hannes Halldorsson na kuzima matumaini ya Argentina kujitwalia alama tatu muhimu.

Messi anatazamwa akisaka kuifikia rekodi ya mshindani wake Cristiano Ronaldo ambaye alifanikiwa kupata ‘hat-trick’ kwenye mechi nzito kati ya Ureno na Uhispania, Ijumaa iliyopita.

“Kwa kawaida inauma sana kukosa penati. Kama wangefungua zaidi tungeweza kupata nafasi zaidi,” alisema Messi.

“Tuna uchungu wa kushindwa kuzipata alama tatu ambazo tulistahili. Kuanza na ushindi ni muhimu wakati wote, sasa tunatakiwa kuanza kufikiria kuhusu Croatia. Tutajaribu kulipita hili haraka,” aliongeza.

Alisema kuwa mbinu ya Iceland ilikuwa ngumu kwa upande wake kwakuwa wahakutaka kucheza sana bali walijikita katika kuziba lango lao.

Croatia ambayo inasubiri kukutana na Argentina pamoja na Iceland, jana ilijitwalia alama 3 muhimu baada ya kuifunga Nigeria 2-0.

Magoli ya Croatia lilitokana na Oghenekaro Etebo kwa kujifunga (dakika ya 32) na Luca Modri (dakika ya 71) kwa mkwaju wa penati.

TCRA yafafanua Kuhusu Watumiaji wa Facebook, Twitter, Instagram Kutakiwa Kujisajili

0
0
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema mtumiaji mmoja mmoja wa mitandao ya Facebook, Instagram na Twitter hatakiwi kujisajili.

Taarifa iliyotolewa Juni 16 na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, James Kilaba imesema taarifa hizo ni za uongo kwa kuwa mtumiaji mmoja wa mitandao ya kijamii hahitaji kusajiliwa na TCRA.

Taarifa hiyo imesema kanuni zinawataka watumiaji wa mitandao kuwajibika kwa maudhui watakayopakia kwenye mitandao hiyo.

Hata hivyo taarifa hiyo imesema wamiliki wote walio na leseni za utangazaji wanaotumia mitambo iliyosimikiwa ardhini (terrestrial) endapo watapenda kutumia mitandao ya kijamii (facebook, instagram na twitter) kurusha maudhui yao kwa lengo la kujisajili, lazima wajisajili kwanza TCRA.

Kilaba amesema mamlaka hiyo itaendelea kuchukua hatua za kisheria dhidi ya watu wanaoeneza uongo huo.

Kivuko cha MV Mwanza Chafanyiwa Majaribio Kwa Mara ya Kwanza

0
0
Kivuko kipya cha MV Mwanza kimeingia majini leo kwa mara ya kwanza kwa ajili ya majaribio, baada ya ujenzi wake kukamilika.

 Kivuko hicho kitafanya safari kati ya Kigongo na Busisi na kinatarajiwa kubeba abiria zaidi ya 1,000 na magari madogo 36.

Pia, kitawasafirisha abiria wa mikoa ya Mwanza kuelekea Geita, Kagera, Kigoma na nchi za Rwanda, Burundi na Congo.

Akizungumza wakati wa kushusha kivuko hicho kwenye maji, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Vivuko wa Wakala wa Umeme na Ufundi (Temesa), Kokombe King’ombe amesema kivuko hicho kimetengezwa kisasa na kitakuwa na uwezo kwenda kwa kasi zaidi ikilinganishwa na vingine vitatu vilivyopo sasa.

Kivuko hicho kilianza kujengwa Juni 2016 na Kampuni ya Songoro Marine ya wazawa wa jijini Mwanza kwa gharama ya Sh8.9 bilioni.

“Kuwa na vivuko vingi katika kivuko cha Bususi ni tija kubwa, mbali na kuimarisha huduma lakini pia itatusaidia hata sisi kuvifanyia matengenezo bora vinapoharibika bila kuathiri shughuli za usafirishaji,” amesema King’ombe

Mkurugenzi Mtendaji wa Songoro Marine, Salehe Songoro amesema kivuko hicho kimekamilika kujengwa ila kitakuwa kwenye majaribio kwa kipindi cha wiki tatu.

“Kuanzia Julai mwaka huu ndipo kitaanza kufanya kazi ya kuvusha abiria kutoka Kingongo wilayani Misungwi kwenda Busisi wilayani Sengerema,”amesema.

Ajali Ya Basi Yaua Watano Geita

0
0
Watu watano wamefariki dunia na wengine 36 kujeruhiwa baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutoka Mwanza kwenda Bukoba kupinduka.

Akizungumza leo Juni 17, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo amesema ajali hiyo iliyohusisha basi la King Msukuma na gari ndogo aina ya Harrier ilitokea jana asubuhi eneo la Kasamwa wilayani Geita.

Mabasi ya King Msukuma yanamilikiwa na mbunge wa Geita vijijini, (CCM) Joseph Kasheku maarufu kwa jina la Msukuma.

Kaimu Mganga Mfawidhi Hospitali ya Mkoa wa Geita, Dk Mazoea Fimbo amesema maiti za watu watano, wanawake wanne na mtoto anayekadiriwa kuwa na umri wa miezi sita zimepokelewa na kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti hospitalini hapo.

"Majeruhi watatu wamehamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza kwa matibabu zaidi kutokana na hali zao kuwa mbaya na kuhitaji huduma Maalum," amesema Dk Fimbo.

Akizungumzia ajali hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel amesema kwa mujibu wa maelezo ya mashuhuda, ajali hiyo ilitokea baada ya basi kukosa mwelekeo na kulifuata gari dogo upande wa kulia wa barabara na kuligonga ubavuni kabla ya magari yote mawili kupinduka.

Agizo La Waziri Jafo Kwa Wakuu Wa Mikoa Wote Nchini Ndani Ya Siku 60

0
0
 Angela Msimbira OR-TAMISEMI
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo ametoa muda wa miezi miwili kwa Wakuu wa Mikoa wote nchini kuanza kusimamia ujenzi wa miundombinu ya shule katika Mikoa yao.

 Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake leo, Mhe. Jafo amesema miundombunu hiyo itahusisha ujenzi wa vyumba vya Madarasa 478 na mabweni 269 ambapo kila bweni moja litachukua wanafunzi 80.

 Mhe. Jafo alisema kuwa ni wajibu wa kila Mkuu wa Mkoa kusimamia kusimamia kwa dhati kazi ya ujenzi wa miundombinu ya Madarasa na Mabweni na kuhakikisha kuwa fedha zinazotolewa na Serikali zinaendana na majengo yatakayojengwa kama walivyokuwa wakifanya katika miradi ya afya na Elimu.

Aliendelea kusema kuwa Serikali imeweza kuchagua shule 119 ambazo orodha itatolewa wakuu wa Mikoa hiyo wahakikishe wanasimamia kwa haraka zoezi la kubaini maeneo ya yatakapojengwa madarasa na mabweni, pia kusimamia uteuzi wa Kamati za Ujenzi na kuanza mchakato wa kuwatafuta wajenzi wa majengo hayo.

 Alisema kuwa Serikali itatoa fedha kukamilisha haraka ujenzi wa miundombinu ya mabweni 269 na madarasa 478 kwa ajili ya wanafunzi kujiunga na Kidato cha Tano kwa kipindi hiki na kuagiza fedha hizo zikasimamiwe kwa weledi.

 Mhe Jafo alisema ujenzi wa miundombinu hiyo utatumika kwa njia ya “Force Accont” utaratibu unaotumika katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na ambao umetuika katika ujenzi wa shule na vituo vya afya Nchini.

 Aliwaagiza Wakuu wa Mikoa wote ambao Halmashauri zao kazi ya Ujenzi wa Miundombinu ya Shule inaenda kufanyika kusimamia kwa nguvu mchakato wa kutafuta mafundi wa ujenzi wa majengo na kuhakikisha wanapatikana haraka ili kazi ianze mara moja baada ya kubainisha maeneo.

 Aliwataka Wakuu wa Mikoa kuhakikisha wamekamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa na mabweni ifikapo tarehe 30/8/2018 ili kuhakikisha wanafunzi walio na sifa ya kujiunga na kidato cha Tano watapata fursa ya kujiunga na kidato cha tano.

 Wakati huohuo aliwaagiza Wakurugenzi ambao watasuasua katika utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu ya madarasa na mabwebi pamoja na miradi mingine hatasita kuwachukulia hatua na kuwataka watakapopata fedha wahakikishe kazi hiyo inakamilika mapema.

 “Niwatake Wakurugenzi ambao wanatabia ya kusuasua utekelezaji wa mradi mbalimbali kuacha mara moja na katika jambo hili sihitaji masiahara hata kidogo, Mamlaka za Serikali za Mitaa itakapo pokea fedha ihakikishe inakamilisha ujenzi huo haraka.” Alisema Jafo

 Aliendelea kusema kuwa Serikali haiwezi kukubali kuona watoto wa maskini wanakosa nafasi ya kujiunga na kidato cha Tano wakati wanasifa, hivyo amewataka nawata Wakuu wa Mikoa kusimamia kazi hiyo haraka kwa lengo la watanzania kuweza kupata fursa ya elimu katika nchi yao.

 Aidha alisema Serikali imetenga shilingi bilioni 29 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ikiwemo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ili kuhakikisha vijana wa Tanzania wanapata Elimu.

Davido Ampandisha Diamond Kwenye Show Ya Clouds

0
0
Na Amini Nyaungo-Fullshangwe
Muimbaji kutokea Nigeria Davido alifanya show katika Ukumbiwa Next Door Arena ulipo Dar es Salaam ambapo aliambata na wasanii wanao fanya muziki wa bongofleva ambao ni Ruby, Nandy, The Mafik, Aslay na wegine.

Lakini Moja ya Jambo ambalo halikutegemewa na mashabiki ni kumuona msanii Diamond Platnumz akipanda kwenye stage moja na Davido tena waki-perform wimbo wa Number one Remix, wimbo ambao Diamond aliwai kumshiirikisha Davido kipindi cha Nyuma.

Ikumbukwe kuwa Kumekuwa na mgogoro wa chini kwa chini baina ya Diamond na uongozi wa Clouds Media, huku mashabiki wa muziki nchini wakiachwa na sintofahamu. Ngoma za msanii huyo maarufu barani Afrika ni kama zimepigwa marufuku kusikika ndani ya redio ama kuonekana katika televisheni inayomilikiwa na Clouds Media.

Mara kadhaa, msanii huyo amekuwa akisikika akitoa vijembe dhidi ya redio na televisheni hiyo maarufu nchini.

Ukiuliza urafiki wao umeisha vipi hakuna anayejibu sawa sawa, ndio maana Edwini Senzaba amesema mambo ya ‘Ngoswe muachie Ngoswe’.

Mchongo uko hivi, Davido alikuwa na show hapo ambapo imeandaliwa na Uongozi wa Clouds.

Diamond alifanya show huko Dar Live na baada ya kumaliza aliondoka haraka na kwenda Next Door na kuruka na Davido kwenye ‘My Number One Remix’ huku shangwe likiwa kubwa kwa mashabiki waliojazana hapo.

Baada ya kumaliza show hiyo ya kama dakika 8 hivi, Diamond alisikika akisema kuwa “Nimekuja kumpasupport rafiki yangu tukutane Wasafi Festival,” amesema.

Baada ya maneno hayo alitoka jukwaani na kuondoka akiwaacha watu wakipiga shangwe kubwa sana.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya June 18

Jipatie Tiba ya Asili ya Ngiri, Vidonda vya Tumbo,Kisukari na Nguvu za Kiume

0
0
Super nzoka IKEMEKO TRDITONAL clinic Ni dawa ya Asili ya vidonge iliyotengenezwa kwa techknojia ya kisasa na ubora wa hali ya juu 

Huongeza nguvu za kiume maradufu hata kwa wale wasiojiweza kabisa kufanya tendo la ndoa na wapo abao hata wakifanya hushindwa kutoa maji maji maji ambayo ndani yake kuna mbegu za kiume zinazotakitakiwa kurutubisha yai

Dawa hii huboresha na tunatibu nakumaliza matatizo haya kwa muda mfupi tu na haina madhara kwa mtumiaji yeyote hata wa umri wa miaka 80 na kuendelea.... inaongeza hamu, urijali kwa wanaoshindwa kuendelea na tendo la ndoa.

Huanza kufanya kazi baada ya dakika 60 tu na kufanya uchelewe kufika kileleni dakika 20 kwa tendo la kwanza itakuwa unauhakika wa kurudia tendo la ndoa zaidi ya Mara tatu bila kuhisi kuchoka 

SILYA; inakuza uume uliosinyaa kurefusha umbile dogo urefu inchi (6-9)na unene wa cm 4 za upenyo kwa wenye kasoro za kimaumbile na walioathiriwa na kupiga punyeto pamoja na matatizo ya kiafya

Tiba hii ni ya kudumu.Pia tunatibu ngiri ya kupanda na kushuka,tumbo kuuguruma chini ya kitovu ,kaswende kisukari ,maumivu ya mgongo, kiuno, kutopata choo vizuri na uvimbe kupitia njia ya mkojo, presha, vidonda vya tumbo

Wasiliana Nasi kwa namba;  0716343218,0789289945. TUNAPATIKANA MBAGALA ZAKIEM STENDI ya musanga

Stend, Simba Zatinga Nusu Fainali Uhai CUP.

0
0
Na, Magdalena Kashindye.
Timu ya stend United ya mkoani shinyanga na timu ya simba zimefanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali ya mchuano ya vijana wa timu B za ligi kuu Tanzania bara walio chini ya umri wa miaka 20.

Stend imeingia hatua ya nusu fainali kwa kuifunga timu ya Ndanda ya mtwara kwa goli 1_0 na simba imeingia hatua ya nusu fainali kwa kuifunga timu ya Tanzania prisons ya Mbeya kwa penati 5_4 mara baada ya kutoka sare ndani ya dakika 90 na mshindi kupatikana kwa mikwaju  ya penati.

Nusu fainali zitachezwa kesho, Azam FC ikimenyana na Stand United na Simba SC wakimenyana na Mtibwa Sugar, wakati fainali itakuwa Juni 21.

Mexico Yaanza Vizuri Kombe La Dunia.... Yawatandika Mabingwa Watetezi Ujerumani 1-0

0
0
Na  Magdalena  Kashindye.
Bingwa mtetezi wa kombe la dunia timu ya Ujerumani imeanza vibaya kutetea kombe lake kwa kukubali kipigo cha goli 1_0 kutoka kwa Mexico.

Ujerumani ilifungwa goli 1_0 na Mexico dakika ya 35 ya mchezo kwa mpira uliopigwa na mchezaji Hirving  Lozano na kuingia wavuni moja kwa moja.

Mexico inavunja rekodi aliyokuwa ikishikiliwa na Algeria kwa kumfunga mjerumani kwenye mchezo wa kwanza mwaka 1982 rekodi iliyodumu miaka 36

Makanga 3 Power; Dawa Bora Nguvu Za Kiume

0
0
Kutibu nguvu za kiume dakika(10) na kupona muda wa siku tatu tuu. Kuimarisha misuli ya uume uliolegea, pia ipo Dawa ya kurefusha uume mfupi inchi NNE hadi saba na kunenepesha uume mfupi sentimita NNE.

Tiba ya kudumu kutibu maumivu ya mgongo,kiuno, tumbo kuunguruma na kujaa gesi, kupata choo vizuri, na kutibu uzazi, kutibu busha bila operesheni, kisukari, presha ,miguu kuuma, uzazi, fangas sugu, vidonda vya tumbo.

Ni docta bingwa wa kutibu magonjwa sugu, kutoa ndagu za utajiri kwa kutumia Pete, kazi ,cheni, mikufu maalumu ya bahati, una kesi umedhulumiwa Mali au pesa? Zitarudi muda wa Masaa matatu tuu.

Onana na Dr shilindes shida zako zote zitakwisha, anatoa Dawa za utajiri kwa wafanyakazi, wakulima, na wafugaji, wafanyabiashara na wachimba madini kwa kutumia pete, kazi kwa yeyote anaetaka kuwa na pesa nyingi.

Pia anaboresha akili kwa wanafunzi darasani, masomo na kufaulu mitihani pia kushinda bahati nasibu yeyote.

Pia tunatoa Dawa kumrudisha Mume, mke, mpenzi, hawara, kwa muda wa SAA moja tuu, na kuomba msamaha kwa kukupigia magoti na yeyote yule, unaemtaka kimapenzi au kuoana, utampata na kumfunga asitoke nje ya ndoa daima na kutekeleza shida zako zote. Kupunguza unene, kupunguza matiti makubwa, tumbo na nyama uzembe muda wa siku sita unapata saizi uipendayo.

Kutoa makovu mwilini, chunusi, upele na mabaka, pia tunayo Dawa ya kuongeza hipsi, makalio, mguu wa bia na kupata shepu safi kwa muda wa siku saba tuu.

Wa mikoani mtapata huduma popote mlipo.
Tupo dar es salam mbagala rangi tatu.

Mawasiliano simu namba: 0784 460 348. Au 0659 103 360.

Kombe la Dunia: Serbia Yang'aa Kwa Costa Rica

0
0
Na Magdalena Kashindye
Goli pekee la nahodha wa Serbia, Aleksandar Kalarov limetosha kuipa timu yake pointi tatu muhimu  dhidi ya Costa Rica.

Kalavor aliiandikia timu yake goli la kwanza na la ushindi dakika ya 35 kwa mpira wa adhabu nje kidogo na eneo la kumi na nane na mpira kuzama moja kwa moja vyavuni.

Mchezo huu wa kundi E ulichezwa jana saa tisa mchana katika uwanja wa Samora Arena

Brazil Nayo Yabanwa Mbavu ya Sare 1-1 na Switzerland Kombe la Dunia

0
0
Na Magdalena Kashindye
Brazil jana ilishindwa kufurukuta mbele ya Switzerland na kulazimishwa sare ya 1_1 katika mchuano ya kombe la dunia inayoendelea nchini urusi .

Brazil ilikuwa ya kwanza kuliona lango la Switzerland dakika ya 19 ya mchezo kupitia kwa nyota wake aliyeng'aa katika mchezo huu Phillippe Countinho na hadi wanaenda mapumnziko Brazil akiwa kifua mbele.

Kipindi cha pili dakika ya 50 Steven Zubery aliisawazishia timu yake kwa goli Safi la kichwa na hadi mwamuzi anapuliza kipenga cha mwisho Brazil 1_1 Switzerland.

Kwa matokeo  hayo,  Brazil inaongeza idadi ya vigogo wa soka duniani kuanza vibaya .

Kati ya vigogo Sita waliocheza ni Ufaransa pekee ndiye aliyefanikiwa kushinda wakati Ujerumani akipoteza na Argentina, Brazil, Ureno na Hispania zikiambulia sare na kuleta taswira mpya ya ushindani mwaka huu.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images