Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Kikwete, Mecky Sadick Wateuliwa Kamati Maalumu ya Kuivusha Yanga Kwenye Majanga Inayopitia

$
0
0
Klabu ya soka ya Yanga kupitia Mkutano wake Mkuu wa mwaka, uliofanyika kwenye Bwalo la Maafisa wa Jeshi la Polisi, Oysterbay, Dar es Salaam, imepitisha mabadiliko na kuteua kamati maalum kwaajili ya kuivusha timu.

Katika mkutano huo, Yanga wametangaza Bodi mpya ya wadhaamini inayoundwa na waliokuwepo awali Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala bora) George Mkuchika mke wa aliyekuwa Rais wa Zanzibar Mama Fatma Karume, Francis Kifukwe, Jaji Mstaafu John Mkwawa pamoja na Mzee Katundu.

Mkutano huo pia umeridhia kuteuliwa kwa kamati maalum ya kuivusha timu hiyo kwenye kipindi hiki cha mpito inachopitia wakati mchakato wa kuweka namna nzuri ya uendeshaji ukiendelea. Kamati hiyo yenye watu 12 itaongozwa na Mwenyekiti Tarimba Abbas na Makamu Mwenyekiti Said Mecky Sadick.

Wajumbe 10 wa kamati hiyo ni Abdallah Binkleb, Nyika Hussein, Samwel Lukumay, Mashauri Lucas, Yusuphed Mhandeni, Hamad  Islam, Makaga Yanga, Ridhiwan Kikwete, Majid Suleiman na Hussein Ndama.

Yanga imekuwa kwenye wakati mgumu kiuchumi siku za hivi karibuni kiasi cha kufikia hatua ya kutofanya vizuri pamoja na kujitoa kwenye michuano ya CECAFA KAGAME CUP 2018

Waziri Mwakyembe Awapa Neno Zito Wanachama na Wapenzi wa Yanga

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Harrison Mwakyembe amewasisitiza wanachama wa klabu ya Yanga kutoichukulia timu hiyo kimzaha na kwamba wanapotetereka msisimko wa michezo pia unakufa kwa kukosa ushindani.

Waziri Mwakyembe ameyasema hayo leo kwenye Mkutano Mkuu wa Klabu ya Yanga ambapo amewataka wanachama wa klabu hiyokufahamu kwamba klabu hiyo inahistooria kubwa ndani ya nchi ikiwepo harakati za uhuru ndani ya Tanzania.

"Yanga ikitetereka inaua msisimko, Yanga ikitetereka inaua ushidani wa timu zetu kubwa nchini pia itachangia kuzorotesha maendeleo ya mchezo wa soka sasa ni wajibu wetu sote tushirikiane kukimaliza kipindi hiki cha mpito ndani ya klabu"  Mwakyembe

Ameongeza kuwa, "Ukiondoa kuleta burudani, lakini pia dhamira yake nyingine ya kuanzishwa kwa klabu hii ilikuwa ni kuleta uzalendo wa kiafrika, Yanga imeshiriki na kuchangia kwenye harakati za uhuru, Muungano na ukombozi wa Bara la Afrika kwa ujumla"

Katika kutilia msisitizo kuhusu mshikamano katika klabu hiyo Mwakyembe amesema kuwa "Ikifungwa Yanga tunaumia wengi, ndani na nje ya nchi. Yanga ndio alama ya uhuru wa nchi hii. Naamini mkutano wa leo utafanya maamuzi yaliyo sahihi kwa mstakabali mwema wa soka la Tanzania.”

Mkuu wa Mkoa Alazimika Kutumia Helkopita Kukagua Maeneo Yalizingirwa na Maji ya Bwawa la Nyumba Mungu

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira leo Jumapili Juni 10, 2018 ametumia helikopta kuzunguka baadhi ya vijiji vya wilaya ya Same ambavyo wananchi wake zaidi ya 2500 hawana sehemu za kuishi baada ya nyumba zao kuzingirwa na maji.

Maji hayo yanadaiwa kutoka katika bwawa la Nyumba ya Mungu ambalo siku za hivi karibuni limejaa maji kupita kiasi na kusababisha kuingia katika maeneo ya makazi.

Mei 19, 2018 vijiji vya Marwa na Ruvu Darajani vilifurika maji na kusababisha watu 2500 kukosa makazi baada ya nyumba zao kujaa maji, leo Juni 20, 2018 kijiji kingine cha Ruvu Jitengeni kimezingirwa na maji na kusababisha watu 300 kuzihama nyumba zao.

Walioathiriwa na maji hayo kwa sasa wamehifadhiwa katika kambi ya za Bagamoyo na Rolesho.

Mghwira tangu saa 6 mchana leo ameanza kuzunguka na helikopta kutembelea maeneo hayo ili pamoja na mambo mengine kubaini sababu za maji hayo kuongezeka wakati maji kutoka Bwawa la Nyumba ya Mungu yameanza kupungua.

Makamu wa Rais: Hatukatazi Kuikosea Serikali lakini Tumieni Lugha Nzuri

$
0
0
SERIKALI imesema haikatii kukoselewa na mtu au kikundi chochote isipokuwa inachosisitiza ni matumizi mazuri ya lugha  wakati wa ukosoaji na sio kutumia lugha inachochea chuki na migawanyiko miomngoni mwa wananchi.

Kauli hiyo imetolewa leo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Hassan Suluhu kwenye ibada ya kuwekwa Wakfu Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania , Dayosisi ya Magharibi Kati –Tabora.

Alisema Serikali haina dini lakini watu wake wana dini zao hivyo itaendelea kushirikiana na viongozi wa dini ili kuhakikisha wananchi wanaendelea kutenda mema kwa ajili umoja wa nchini.

Makamu wa Rais alisema Serikali haitamvumilia mtu yoyote ambaye atataka kuwagawa Watanzania kwa misingi ya ukabili, udini na hata itikadi za kisiasa.

Aliwataka viongozi wa dini nchini kuendelea kuhubiri amani kila wakati na kusema kuwa kwa upande wa Serikali amani na usalama wa wananchi ndicho  kipaumbele chake cha kwanza na hivyo itaendelea kuhakikisha Tanzania inabaki na umoja wake.

Naye Mkuu wa Kanisa la KKKT Askofu Dkt. Fredrick Shoo alisema Kanisa linaunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano katika za kupigania haki mbalimbali za Watanzania.

Aliitaka Serikali kuwachukulia hatua wale wote ambao wanataka kulichonganisha Kanisa hilo na Serikali kwa tumia mitandao na vyombo mbalimbali kwa ajili ya maslahi yao binafsi.

Askofu Shoo alisema Kanisa litaendelea kutumia njia za kistarabu kuishauri Serikali na kama kukitokea tofauti watajadiliana na kumaliza mambo kistarabu na sio kama watu ambao wana nia mbaya wanavyochochea.

Kwa upande wa Askofu wa Kwanza wa Dayosisi ya Magharibi Kati –Tabora Askofu Dkt. Isaac Kissiri Laiser alisema Kanisa hilo lipo tayari katika kushirikiana na Serikali katika ujenzi wa Viwanda mkoani Tabora ili kuelekea katika uchumi wa kati.

Katika sherehe hizo Makamu wa Rais aliichangtia Dayosisi hiyo milioni 3 kwa ajili ya kuongezea katika azma yao ya kujenga Kituo cha Afya.

Simba SC Basi Tena...... Ndoto Zake Kucheza Na Everton Zimekufa Rasmi Baada ya Kupigwa Bao 2 Na Gor Mahia Kenya

$
0
0
Kwa  mara ya pili mfululizo, Gor Mahia ya Kenya imebeba taji la SportPesa Super Cup baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Simba SC ya Dar es Salaam, Tanzania.
 
Mashujaa wa Gor Mahia leo wameendelea kuwa wanasoka wa kimataifa wa Rwanda, Meddie Kagere na Jaqcues Tuyisenge waliofunga mabao hayo, moja kila kipindi na kurudia mafanikio ya mwaka jana mjini Dar es Salaam wakiwafunga mahasimu wao wa Kenya, AFC Leopard 2-1 na kutwaa taji hilo.
 
Kagere alianza kufunga bao zuri dakika ya sita akimalizia kazi nzuri ya George Odhiambo ‘Blackberry’ kabla ya Tuyisenge kufunga la pili akimalizia krosi ya Humphrey Mieno dakika ya 54.

Simba SC ilicheza ovyo kipindi cha kwanza na kuzidiwa kabisa na Gor Mahia, lakini kipindi cha pili ilibadilika na kutulia kujaribu kucheza soka ya maelewano, ingawa tayari wapinzani wao walikuwa wamekwishajipanga kuulinda ushindi wao.
 
Kwa ushindi huo, Gor Mahia inayofundishwa na kocha wa zamani wa Simba, Muingereza Dylan Kerr pamoja na kuzawadiwa dola za Kimarekani 30,000 lakini watakwenda kucheza na klabu ya Everton Uwanja wa Goodison Park mjini Liverpool, England.
 
Simba SC watajipatia dola za Kimarekani 10,000, Singida United waliomaliza nafasi ya tatu kwa kuifunga Kakamega Homeboyz kwa penalty 5-1 baada ya sare ya 1-1 watapatiwa dola 7, 500 na wa washindi wa nne watapewa dola 5,000.

Kariobangi Sharks ya Kenya, Yanga ya Tanzania Bara na JKU ya Zanzibar kila moja itapata dola 2,500 baada ya kutolewa hatua ya kwanza ya mashindano.

Spika Job Ndugai Awataka Viongozi Wa Dini Na Watanzania Kuhubiri Na Kudumisha Amani Na Utulivu Nchini

$
0
0
Na Benny Mwaipaja, Kondoa
SPIKA wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, amewataka watanzania kuwa na uvumilivu wa masuala ya kidini ili nchi iendelee kuwa na amani, utulivu na maendeleo.

Ndugai ametoa wito huo katika Kata ya Pahi wilayani Kondoa mkoani Dodoma, alipokuwa akizungumza wakati wa mashindano ya kuhifadhi Qur'an yaliyowashirikisha zaidi ya watoto na vijana 40 kutoka maeneo mbalimbali ya nchi.

Spika Ndugai ameeleza kuwa umoja na mshikamano uliopo hapa nchini ni matokeo ya viongozi wa dini mbalimbali hapa nchini kuendelea kuhubiri amani na utulivu na kuitaka jamii na viongozi hao kuiendeleza kazi hiyo

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameitaka jamii kuendelea kupiga vita uhalifu na kuwafichua wahalifu popote walipo ili nchi iendelee kuwa na amani.

Mratibu na Mwandaaji wa mashindano hayo, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa, Dkt. Ashatu Kijaji, amesema kuwa lengo la mashindano hayo ya kuhifadhi Qur'an Tukufu ni kuwajengea vijana maadili mema ili waweze kushiriki kikamilifu kuleta maendeleo ya taifa.
 
Mgeni Rasmi katika Mashindano hayo, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,  Mustapher Shabaan amewapongeza vijana walioshiriki mashindano hayo na kuonesha umahili mkubwa wa kuhifadhi qoran na kuwataka waumini wa kiislamu kusoma na kukielewa kitabu hicho kitukufu kwa kuwa kimejaa elimu na maarifa mengi yatakayo wasaidia kuenenda vyema katika jamii na kupata thawabu kutoka kwa Mungu.

Trump, Kim watinga Singapore kwa Mazungumzo......, Kim awachanganya waandhishi

$
0
0
Hatimaye, Rais wa Marekani, Donald Trump na Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un wamewasili leo nchini Singapore kwa ajili ya kufanya mkutano wao wa kihistoria.

Kim alikuwa wa kwanza kutua nchini humo, takribani saa saba kabla ya Trump kutua akiwa ndani ya ndege maalumm ya Air Force One.

Mkutano kati ya viongozi wa nchi hizo utafanyika Jumanne ijayo katika hotel ya kifahari ya Sentosa, Kusini mwa Pwani ya Singapore.

Marekani imeendelea kuwa na matumaini kuwa baada ya mkutano huo, Korea Kaskazini itaanza kwa uhakika mchakato wa kuachana na mpango wake wa silaha za kinyuklia.

Aidha, kuwasili kwa Kim Jong Un uliwachanganya waandishi wa habari na wachambuzi wa maeneo mbalimbali duniani waliopo nchini  Singapore kuripoti tukio hilo la kihistoria, wasijue kwa uhakika ni ndege na gari lipi iliyombeba kiongozi huyo pamoja na hoteli aliyofikia. Hii ni tofauti na ilivyokuwa kwa Trump ambaye kuonekana kwa Air Force One angani kulijieleza.

Wakiwa makini kuripoti ujio huo, kwanza ilitua ndege ya illyushin. Hiyo ilikuwa rahisi kuitambua kwani ni ndege ya ulinzi binafsi ya Kim Jong Un yenye silaha maalum ambayo hutangulia.

Kisha ilishuka ndege ya Air China 747 ambayo humbeba rais wa China, Xi Jinping. Wanahabari wengi waliripoti moja kwa moja kuwa wanaamini Kim yuko ndani ya ndege hiyo.

Lakini ghafla ilishuka ndege nyingine ambayo ni ndege binafsi ya Kim Jong-un, dege la Ki-Soviet aina ya Ilyushin Il-62, ambayo pia walihisi ndiyo aliyokuwamo kiongozi huyo.

Gari aina na Mercedes ambayo wengi waliamini amepanda ilionekana ikishusha watu wote lakini kiongozi huyo pia hakuwemo! Bila kutarajiwa, aliwasili akiwa katika gari aina ya Mercedes-Maybach.

Singapore inakuwa nchi ya kwanza ya mbali ambayo Kim ameitembelea tangu alipoingia madarakani mwaka 2011. Safari yake ya kwanza nje ya nchi ilikuwa China na Aprili alikuwa kiongozi wa kwanza wa Korea Kaskazini kukanyaga ardhi ya Korea Kusini, alipokutana na Rais Moon Jae-in kwenye mpaka wan chi hizo.

Pacha wa Bukoba kutenganishwa Saudi Arabia

$
0
0
Serikali  ya Saudi Arabia imesema itagharamia matibabu nchini humo kutenganisha pacha walioungana, Anisia na Almesia, wenye umri wa miezi mitano, yatakayofanyika nchini Saudi Arabia.

Watoto hao walizaliwa Januari 29, wilayani Misenyi katika Kituo cha Masista cha St. Theresa Omukajunguti Kata ya Kyaka na kufikishwa Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam mapema mwezi Februari, ambako wamewekwa kwenye wodi maalumu ya jengo la watoto ya Magufuli, wakipatiwa matibabu ya awali kabla ya kupelekwa Saudia Arabia kwa matibabu.

Watoto hao wa Jonisia wameungana eneo kubwa la kifua na tumbo, lakini kila mmoja ana mfumo wake wa hewa.

Naibu Balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania, Bandar Abdullah Al – Hazani amesema kuwa watoto hao watafanyiwa upasuaji huo wa kuwatenganisha katika Hospitali ya Mfalme Abdulaziz Medical iliyopo Riyadh, mji mkuu wa Saudi Arabia, ambako kuna madaktari bingwa wa upasuaji.

Alisema mpango huo wa kufanikisha matibabu ya upasuaji wa kuwatenganisha mapacha hao, unafanywa kwa ushirikiano wa ubalozi wa Saudi Arabia nchini chini ya balozi wake Mohamed Bin Mansour, uongozi wa Hospitali ya Muhimbili na Waziri wa Mambo ya Nje, Dk Augustine Mahiga.

“Mara tu mipango na maandalizi itakapokamilika, tunatarajia watoto kuondoka kwenda Riyadh mwishoni mwa mwezi huu," alisema Al-Hazani.

Hospitali ya Mfalme Abdulaziz Medical huko Riyadh, ina uwezo mkubwa ikiwa na vifaa vya kisasa na vitanda 1,501 na ilianza shughuli zake Mei 1983.

Tangu wakati huo, imeendelea kupanuka, huku ikitoa huduma kwa idadi ya wagonjwa wanaokua kwa kasi katika maeneo yote.

Mama wa pacha hao, Jonisia Jovitus (21) alisema tayari watoto wake wamechukuliwa vipimo mbalimbali na jopo la madaktari wa Hospitali ya Muhimbili na kuvituma Saudi Arabia.

"Madaktari wameniambia walishatuma vipimo Saudi Arabia na uwezekano wa watoto wangu kutenganishwa upo, naomba Mungu asaidie hili lifanikiwe… ila walichoniambia ni kuwa wanangu wakifanikiwa kutenganishwa salama watakuwa walemavu, mmoja atakuwa na mguu mmoja na mwingine ana miguu miwili, lakini huo mmoja hauna nguvu umepooza. Ninachoomba kwa sasa ni kuwaona watoto wangu wametenganishwa na kuwa salama, naomba jamii iniombee ili lifanikiwe.”- Jonisia

Uongozi wa Hospitali wa Muhimbili kupitia kwa Ofisa Uhusiano, Aminiel Eligaesha ulisema kuwa utaweka wazi kuhusu mchakato mzima wa watoto hao madaktari watakapokuwa tayari.

Awali, uongozi huo wa Muhimbili ulikuwa uzungumze na vyombo vya habari juzi, lakini waliahirisha kwa kile kilichoelezwa kuwa wahusika wamepata dharura, hivyo vyombo vya habari vitaarifiwa siku itakayoitishwa upya mkutano huo.

Credit: Habarileo

Dawa Lishe Ya Kuongeza Na Kunenepesha Mwili

$
0
0
Je  umekonda  na  kudhoofu  mwili  wako  kwa  sababu  ya  kuugua  maradhi  mbalimbali  au  kwa  sababu  ya  msongo  wa mawazo  ?

Unataka  kurejesha   mwili  na  afya  yako  katika  hali  yake  ya  awali ?  Kama  jibu  lako  ni  NDIO  basi  HII  NI HABARI  NJEMA  SANA  KWAKO.

Tunayo  DAWA  LISHE  YA  ASILI  ambayo  inasaidia  kurejesha   afya  na  mwili  wa  mtu  alie  dhoofu    kwa sababu  ya kuugua  magonjwa  na  maradhi  mbalimbali  au  kwa  sababu  ya  msongo  wa  mawazo.

Dawa  hii  ya  asili  itarejesha  afya  na  mwili  wako  ndani  ya  muda  wa  siku  thelathini.

Na  kama  wewe  ni   MWEMBAMBA   na  unataka   KUONGEZA  MWILI  na  KUNENEPA  basi  DAWA  LISHE  hii ndio  JAWABU  LAKO.  Dawa  hii  itafanya  mwili  wako  uongezeke  na  kunenepa  ndani  ya  siku  thelathini.

Ni  dawa  ya  asili  kabisa ( pure  herbal ) isiyo  na  kemikali  yoyote  ya  viwandani  na  inapatikana  kwa  gharama  utakayo weza  kuimudu.

Kupata  dawa  hii  fika  katika  duka  la  NEEMA  HERBALIST  linalo patikana  UBUNGO  jijini  DAR  ES  SALAAM nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA  jirani na  SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL   HOUSING.

Wasiliana  nasi  kwa  simu  namba    0766  53  83  84    au  0693 00 51 89.

Kwa  wateja  wasio  na  nafasi  ya  kufika  ofisini  kwetu, tunayo  huduma  ya  kuwapelekea  dawa  mahali  popote  walipo ndani  ya  jiji  la  DAR  ES  SALAAM.

Na kwa  taarifa  zaidi kuhusu  dawa  mbalimbali za  asili  pamoja   na huduma  zetu  kwa ujumla  , tutembelee  kupitia  blogu yetu:

Dawa Za Nguvu Za Kiume Na Kukosa Hamu Ya Tendo La Ndoa

$
0
0
Asilimia 45-80 ya wanaume wapo tofauti na wengine kwa kutowatimizia vyema wake au wapenz wao na kuwasababishia kutoka nje ya mahusiano yao. 

NINI CHANZO CHA HAYO? Kupiga punyeto,Ngiri, Vidonda vya tumbo, Korodani moja kuvimba, Msongo wa mawazo, Presha, Magonjwa ya zinaa, Kufanyiwa tohara ukiwa na umri mkubwa, Kisukari. 

DR. LUTAJA Sasa anakuletea tiba sahihi ya tatizo la Nguvu za kiume. 

NTOMBO :Hii hutibu na kuponya kabisa tatizo la Nguvu za kiume, utakuwa na uwezo wa kufanya tendo la ndoa zaidi ya mara tatu bila kuchoka na itakufanya uchelewe kafika kileleni kwa mda wa dk 20-45. Dawa hii imechanganywa na miti 18,Hata wazee wenye umri mkubwa wa zaidi ya miaka 85 wanapona kabisa okoa mahusiano yako, ndoa yako sasa. 

SUNGURURU MIX:Ndio tiba sahihi kwa wale wenye maumbile madogo hurefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo nchi 3-8 na unene cm 2-5,dawa hii ipo katika mfumo wakupaka nakunywa na haina madhara yoyote kwa mtumiaji :Hii ni tiba tofauti kabisa nazile ambazo umekwisha wahi kutumia. 

Pia tunadawa za Kupandisha nyota , Uzazi, Pumu, Malaria sugu, miguu kuwaka moto, Kaswende, Kisonono pamoja na mvuto wa mpenzi.

 DR. LUTAJA ANAPATIKANA DAR-ES-SAALAM Simu 0713-821823 kwa wale wa mikoani huduma hii utaipata popote ulipo.

Mashamba yanauzwa wilaya ya kisarawe vijijini katika vijiji vya Mwaneromango, Masaki na Msanga.

$
0
0
Mashamba  yanauzwa  wilaya  ya  kisarawe  vijijini  katika  vijiji  vya  Mwaneromango, Masaki  na   Msanga.

Bei  ya  heka  moja  ni  SHILINGI  LAKI  TANO (Tshs.500,000/=)

Mashamba  yapo katika  hali  nzuri  sana. Yana  ardhi  nzuri  yenye rutuba inayo  weza  kustawisha  mazao  mbalimbali  kama  vile  mihogo, pilipili, mchicha, Chiwa, nyanya, vitunguu, mchicha  pori, spinachi, mpunga  nakadhalika au  kufugia  mifugo mbalimbali  kama  vile  bata, kuku, mbuzi, n’gombe  nakadhalika.

Pia  yapo  mashamba  na   maeneo  kwa  ajili  ya  kuotesha  miche  ya  miti  mbalimbali  na  maua  ya  aina  mbalimbali  yakiwemo  maua  pori  ( Wild Flowers )

Kwa  wanao  hitaji  kufanya  kilimo  cha  umwagiliaji, maji yanapatikana  kwa  wingi  kwa kuchimba  visima na gharama  za  uchimbaji  visima  ni  nafuu  sana.

Na  kwa  wanao  hitaji  huduma  ya  watu  wa  kusimamia  mashamba  ya  mazao  au  mifugo, huduma  hiyo  inapatikana  pia  na  kwa  gharama  nafuu.

Vile  vile  kwa  wale  wanao  hitaji  kuwa  na  makazi  ya  kuishi  katika  vijiji  nilivyo  vitaja  hapo  juu  pamoja  na  vijiji  vya  jirani,  yapo  maeneo  mengi  mazuri  ya  kujenga.

Gharama  za  ujenzi  ni  nafuu  sana  na  gharama  za  maisha  zipo  chini  pia.  Unaweza  kujenga nyumba  yako  kwa  kutumia  matofali  ya  kuchoma.

Pia   yanapatikana  maeneo  mazuri  ambayo  yanaweza  kutumika  kwa  ajili ya  kujenga  mashule, vyuo, vituo  vya  kulelea  watoto  yatima  nakadhalika.

Kwa  maelezo  zaidi, wasiliana  nasi  kwa   simu  namba: 0687319762

Diamond Athibitisha Kumnunulia Mjengo Hamisa

$
0
0
Staa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz amethibitisha tetesi zilizokuwa zinasambaa mtandaoni kuwa amemnunulia mjengo mma watoto wake Hamisa.

Baada ya Diamond kuachana na Zari na Kurudisha majeshi kwa Hamisa imekuwa ikisemekana kuwa Hamisa amehama alipokuwa anaishi na kuhamia kwenye mjengo mpya kabisa na mtoto wake Dylan na Fantasy.


Taarifa zilisambaa kuwa mjengo wenyewe ni ghorofa  ambalo ni bonge wa mjumba ambao upo maeneo ya Mbezi Beach, Bahari Beach. Diamond amethibitisha taarifa baada ya kuandika Instagram na Hamisa kujibu kwa kumshukuru kwa nyumba hiyo:

Hii sio mara ya kwanza kwa Diamond kununua Nyumba kwa ajili ya wanafamilia wake kama utakumbuka ameshawahi kumnunulia nyumba mama yake mzazi Lakini pia ameshamnunulia nyumba mzazi mwenzake Zari nchini South Africa.

Kama Dalili Hizi Unazo Upo Kwenye Hatari Ya Kuishiwa Nguvu Za Kiume Kabisa

$
0
0
Una dalili zifuatazo?
1: Kushindwa kurudia tendo la ndoa
2: Kutojisikia hamu ya tendo la ndoa
3: Maumivu ya kiuno mgongo
4: Tumbo kuunguruma na kujaa gesi
5: Uume kusinyaa, kuingia ndani na kuwa mdogo au mfupi
6: Korodani moja kuvimba

KAMA DALILI HIZI UNAZO UPO KWENYE HATARI YA KUISHIWA NGUVU ZA KIUME KABISA

Kwa matibabu tumia OZYMIX POWER-dawa bora ya nguvu za kiume ya miti shamba ambayo haina kemikali ambayo itakuwezesha kurudia tendo la ndoa zaidi ya mara tatu bila hamu kuisha.
Pia tunatoa huduma hizi:>

1.Dawa ya Kuondoa michirizi
2.Kumrudisha mwanaume aliyekuacha 
 
Tunapatikana KAWE UKWAMANI karibu na kituo cha mabasi.
KWA MAWASILIANO ZAIDI ; 0716096205 /0756726865 FIKA OFISIN AU PIGA SIMU NA UTALETEWA DAWA POPOTE ULIPO DAR ES SAALAM NA KWA MIKOANI TUNATUMA KWA NJIA YA MABASI.

TEMBELEA KATIKA BLOG YETU HAPA>>>;

PAC Kukabidhi Taarifa kuhusu bodi na menejimenti ya BOT Leo Kwa Spika Ndugai

$
0
0
Kamati ya Hesabu za Serikali na Mashirika ya Umma (PAC) leo inakabidhi kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai taarifa kuhusu bodi na menejimenti ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT)  inayotuhumiwa kutumia bima binafsi badala ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

Hatua hiyo inakuja baada ya Jumanne iliyopita, Spika Ndugai kuagiza PAC kuihoji BoT kuhusu tuhuma hizo zilizotolewa na Mbunge wa Ulanga, Gudluck Mlinga (CCM).

Akichangia bajeti ya Wizara ya Fedha, Mlinga alisema   fedha za matibabu kwa maofisa wa BoT kwa mwezi ni Sh bilioni 12, lakini wangekuwa wanatumia mfuko wa NHIF matibabu yao kwa mwezi yangekuwa Sh bilioni moja tu.

Askofu Mkuu Avunja Ukimya.....Asema KKKT Hawakukurupuka Kuandika Waraka Wao

$
0
0
Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Fredrick Onael Shoo amesema waraka uliotolewa na maaskofu wa kanisa hilo haukuwa na nia mbaya na wala hawakukurupuka kuuandika.

Askofu Dk. Shoo alitoa ufafanuzi huo jana wakati wa ibada uzinduzi wa Dayosisi ya Magharibi Kati ya kanisa hilo mjini Tabora ya kumsimika Askofu wa Dayosisi hiyo, Dk. Isaac Kissiri na msaidizi wake, Mchungaji Newton  Maganga, iliyohudhuriwa na maaskofu wote wa kanisa hilo.

Alisema kanisa linaunga mkono jitihada zote zinazofanywa na Rais Dk. John Magufuli katika kuwaletea maendeleo wananchi.

Alisema    kanisa hilo  halina ugomvi na kiongozi yeyote   wa Serikali  ya Rais Magufuli.

Kuhusu waraka uliotolewa wakati wa Sikukuu ya Pasaka   mwaka huu, alisema haukuwa wa kukurupuka na haukutolewa kwa lengo baya dhidi ya Serikali  kama    baadhi ya watu wanavyoupotosha.

“Naomba  kila mpenda amani na maendeleo ya nchi hii aelewe hivyo, waraka huu haukuwa na nia mbaya na Serikali,”alisema Dk. Shoo.

Alisema lengo la waraka huo lilikuwa ni   kufikisha ujumbe wa kanisa kwa Serikali  iweze kuutafakari na kuufanyia kazi na haukuwa na lengo jingine tofauti.

“Kama kuna sehemu tulieleweka vibaya tuko tayari kuomba radhi kwa nia njema  kudumisha ushirikiano mzuri na Serikali.

‘Namshukuru  Rais wetu Magufuli kwa kuelewa dhamira yetu, ila wapo baadhi ya watu ndani ya kanisa na nje ya kanisa wasio na nia njema wanaotaka kutuchonganisha na Serikali, watu wa namna hii wasifumbiwe macho, wana agenda binafsi’, alisema Dk. Shoo.

Alisema ndiyo maana maaskofu wote wa kanisa hilo na waumini wao wako kitu kimoja, hawana tofauti zozote.

Kiongozi huyo wa KKKT alionya  kuwa  mtu anayeendelea kushabikia mambo yanayovuruga amani ndani ya kanisa hilo anakiuka kiapo chake cha utumishi wa Mungu.

Alisema maaskofu wataendelea  kushirikiana na Serikali kudumisha amani na utulivu wa nchi na hawako tayari kuona mtu yeyote anatumia jina la kanisa hilo vibaya kwa matakwa yake binafsi   kuharibu taswira ya kanisa na Serikali.

“Hatuko tayari kuona mtu anaharibu ushirikiano wetu na Serikali kwa sababu umejengeka muda mrefu, kanisa litachukua hatua kali dhidi yake,”alisema Dk. Shoo.

Alimshukuru Rais Magufuli kukubali mwaliko wao na kumtuma Samia   kujumuika nao katika ibada na kuomba awafikishie shukrani za kanisa.

Tunatibu Na Kuponesha Kabisa Upungufu Wa Nguvu Za Kiume, Maumbile Mdogo, Busha Bila Kupasua

$
0
0
TUNATIBU NA KUPONESHA KABISA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME UUME MDOGO BUSHA BILA KUPASUA PRESHA VIDONDA VYA TUMBO : Asilimia kubwa ya wanadamu wanasumbuliwa na magonjwa mbalimbali na wapo waliohangaika sehemu mbalimbali bila mafanikio.

Mabula Clinic ni kituo cha tiba asilia kilichopo mbagara zakhemu njia kuu ya jeshini. Je unaupungufu wa nguvu za kiume au uume wako mdogo na mwembamba? 

Mapro pawer no 2 ndio tiba, kwa sasa hutibu matatizo matatu kwa pamoja 1. itakufanya uchelewe kufika kileleni dikika 15-20 kwa tendo la kwanza 2. Huimalisha misuli iliyolegea na kusinyaa hasa kwa wale walio athirika na upigaji punyeto 3. itakufanya upate hamu ya kurudia tendo zaidi ya mara tatu :Kwa nini ujione mpweke pale ukutanapo na mpenzi au mke wako kisa unawai kukojoa au unakomea bao moja tu na huku dawa zipo 

Makakanua mix ni dawa iliyochanganywa na miti shamba 9 na kuwa na uwezo wa kuongeza uume saizi upendayo inchi 5-8 kwa urefu na unene sentimita 1-5, dawa hizi hazina madhara yoyote kwa mtumiaji ata wazee wenye umri mkubwa wanapona

 Zipo dawa za mvuto wa mpenzi mme au mke kwa masaa matatu tu ,mvuto wa biashara, kutengeneza mwonekano mzuri wa mwili kwa wanawake yani shepu.

Tunatibu ngiri, miguu, mgongo na kiuno kuumwa, kupunguza kitambi minyama uzembe matiti na mwili mkubwa 

Tiba na ushauli muone Dr Mabula au piga simu no 0743362017.Huduma zangu utazipata popote ulipo kama uwezi kufika ofisini

BAWACHA Wamtaka Mwigulu Nchemba Ajiuzulu

$
0
0
Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha) limelaani vikali kitendo cha udhalilishaji kilichofanywa na Jeshi la Polisi dhidi ya Amina Mapunda aliyejifungua kituo cha polisi bila msaada wowote baada ya kuwekwa mahabusu kwa muda mrefu ilhali akiwa mjamzito.

Vilevile, baraza hilo limemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Mwigulu Nchemba kujiuzulu nafasi yake kutokana na mfululizo wa matukio ya polisi kunyanyasa wananchi.

Mbali na Mwigulu, Bawacha imetaka pia naibu wa Mwigulu, Hamad Yussuf Masauni na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro kuachia nafasi zao pia.

Amina (26), mkazi wa Kiswanya, Kijiji cha Mgundeni, Tarafa ya Mang'ula wilayani Kilombero mkoani Morogoro, alijifungua nje ya kituo cha polisi Mang'ula muda mfupi baada ya kutolewa mahabusu baada ya kulalama kwa muda mrefu kuumwa uchungu wiki iliyopita.

Kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Masauni, mama huyo alikamatwa na polisi kutokana na tuhuma za mumewe kuuziwa vitu vya wizi vilivyokutwa ndani ya nyumba yao.

Wakati serikali ikiendelea na uchunguzi dhidi ya askari waliohusika na mkasa huo, uongozi wa Bawacha umesema kitendo cha mwanamke huyo kujifungulia nje ya kituo cha polisi bila msaada wowote "ni cha kinyama" na kinatoa picha mbaya kwa Jeshi la Polisi kwamba linafanya kazi yake bila kuzingatia weledi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa jana, Katibu Mkuu wa Bawacha Taifa, Grace Tendega, alisema baraza hilo linalaani kitendo hicho na viongozi ndani ya Jeshi la Polisi wanatakiwa kujipima na kujitafakari kama kweli wanatosha.

Alisema kitendo cha jeshi hilo kusababisha mwanamke huyo kujifungua kwenye mchanga hakimdhalilishi yeye peke yake, bali kinawadhalilisha kina mama wengi wa Kitanzania na ni ukiukwaji wa haki za binadamu.

"Hapa unaweza kujiuliza mama anahusikaje na wizi wa mume wake? Hata kama kweli waliona kuna vifaa vya wizi, kwanini hawakuchukua vifaa hivyo kama ushahidi?" Alihoji.

Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) pia, Tendega alisema zaidi: "Lakini inashangaza hao polisi hawakuona kama huyo mama ni mjamzito au hawajui mtu ambaye ni mjamzito? Haya ni mambo ya ajabu sana kwa Jeshi la Polisi."

Alisema kitendo hicho ni kibaya na kuna kila sababu ya viongozi wa Jeshi la Polisi kuanzia ngazi ya Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kilombero, Mkuu wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Mkuu wa Jeshi la Polisi Taifa (IGP) pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na naibu wake kujitafakari na kujipima kama kweli wanastahili kuendelea na kazi.

Alisema matukio ya aina hiyo yamekuwa yakijirudia mara kwa mara na Jeshi la Polisi limekuwa likikaa bila kuonyesha juhudi yoyote ya kuwachukulia hatua wanaohusika na ukiukwaji huo wa haki za binadamu kwa kuwatesa wananchi au kuwafanyia vitendo vya unyanyasaji.

Tendega alisema pamoja na kuwapo kwa vitisho mbalimbali, Chadema na Bawacha hawatanyamaza na badala yake watapaza sauti kwa ajili ya kuwatetea wanyonge na kudai haki bila kuwa na uoga.

Deni La Taifa Kufanyiwa Uhakiki Mwakani

$
0
0
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji amesema mwaka ujao wa fedha, Tanzania itafanyiwa tathimini kuhusu deni la taifa.

Dk. Kijaji ametoa kauli hiyo bungeni leo wakati akijibu swali la Mbunge wa Mtambile, Masoud Abdalah Salim (CUF) ambaye alihoji ni lini deni la taifa litafanyiwa uhakiki ili kuwe na hali nzuri ya uchumi.

“Mnaendelea kukopa na deni halifanyiwi uhakiki ni lini sasa mtafanya mkakati huu wa uhakiki kwa haraka,”amehoji.

Akijibu swali hilo, Dk. Kijaji amesema Serikali haijawahi kuacha kulipa deni hata mwezi mmoja ndiyo maana Tanzania bado inaaminiwa.

“Mikopo yote tunayokopa tunapeleka kwenye maendeleo ya kiuchumi na bado tunasisitiza kuwa deni letu ni himilivu.

“Kuhusu uhakiki wa deni letu katika mwaka ujao wa fedha itafanyiwa tathimini,”amesema.

Naye Mbunge wa Viti Maalumu, Sophia Mwakagenda amehoji ni lini Serikali italeta sheria bungeni ya mikopo ili inapokopa wabunge wafahamu.

Akijibu hilo, Dk. Kijaji amesema: ” Serikali tunapokopa tunafuata sheria na katiba na imeendelea kusimamia deni la taifa kwa kuzingatia sheria ya mikopo,”.

Tatizo La Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Na Maumbile Madogo

$
0
0
Tatizo La Upungufu Wa Nguvu Za Kiume Na Maumbile Madogo Ya Uume Limekuwa Kubwa Kwa Lika Zote Hapa Kwetu Na Duniani Kote. Tatizo Si Tatizo Bali Ni Iletiba Sahihi Ya Matatizo Haya Chanzo Chake Na Visababisho Vyake.

DALILI;mwili kuchoka, maumivu ya mgongo na kiuno, kutopata choo vizuri hata ukipata choo kinakuwa kigumu au gololi kama mavi ya mbuzi. misuli ya uume kulegea na kusinyaa hata uume kulegea na kushindwa kufika kileleni. miguu kuuma na kuwaka moto.

 TIBA YAKE; 4mix ni dawa pekee inayoweza kutibu matatizo hayo inarudisha nguvu za kiume mara dufu na kufanya urudie tendo la mara tatu bila kuchoka. 

LUKUBA 3 pump; ni dawa inayorefusha na kunenepesha uume hadi inchi 7 hadi 9 na kunenepesha kwa CM 2 na kukupa umbile la uhakika. ITUMIE TIBA HII KUOKOA NDOA YAKO NA KUOKOA KUKIMBIWA NA UMPENDAYE,

 ISABILO; Ni dawa itoayo mafanikio na utajili kwa watu walioshindwa kufanikiwa kimaisha, 

MWITE; Ni dawa ya mvuto kumvuta umpendaye na kumrudisha aliyembali na atakutimizia ahadi zote awe mwanamke au mwanaume. 

LUTA CD; Ni dawa inayotibu magonywa nyemelezi yanayopunguza kinga za mwili na kusababisha mwili kuzoofu na inaondoa miwasho na kuondoa kemikali na taka zinazozagaa mwilini. 

KISUKARI; Tunayo dawa ya DAYON inayotibu na kuzalisha insulin kwa wingi na kumfanya mwenye tatizo hili kupona kabisa ugonjwa wa kisukari, kwani husababisha misuli ya mwili kutokufanya kazi vizuri

MPIGIE DR DAGOTIMAN NDIYE SULUHISHO LA MATATIZO YAKO 0754372325/  0658920640
 
HUDUMA HII INAWEZA KULETWA POPOTE ULIPO OFISI ZETU ZIPO MBAGALA ZAKHEM DAR ES SALAAM.

Spika Ndugai Akerwa na Gawio Kiduchu la Benki ya NBC Kwa Serikali

$
0
0
Sika wa Bunge, Job Ndugai, ameitaka Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kutoa maelezo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji (PIC) kuhusu kiasi kidogo cha gawio wanachokitoa kwa Serikali. Kwa mwaka 2016-2017 ilitoa Sh bilioni 1.2.

Kauli hiyo aliitoa mjini hapa jana wakati akifungua semina kwa wajumbe wa PIC na baadhi ya wajumbe wa kamati nyingine ikiwamo bajeti, uongozi wa NBC na Ofisi ya Msajili wa Hazina.

Pamoja na mambo mengine, Ndugai alisema kwa hisa ya asilimia 30 ambazo Serikali inazo kwa benki hiyo, gawio hilo ni kidogo sana na linatia shaka.

“Hisa zenu hazitofautiani sana na za Serikali zilizopo Benki ya NMB, lakini wenzenu wamekuwa wakitoa gawio kubwa kuliko ninyi, hapa mna kazi kubwa ya kuishawishi kamati ili iweze kukubaliana na majibu yenu juu ya kiasi hicho cha gawio.

“Inadhihirisha wazi kwamba hakuna urafiki na wananchi kutokana na kutokuwa karibu nao kwa kushindwa kufungua matawi wala kutoa mikopo kwa wananchi kama zinavyofanya NMB na CRDB,” alisema.

Aliutaka uongozi huo wa NBC kulitafakari hilo na kulifanyia kazi ili benki hiyo iwe karibu na wananchi.

“PIC imepewa jukumu la kuangalia mashirika yote na kuona utendaji kazi wao kwa sababu kuna takribani mashirika 272 ambayo ni muhimu na itasaidia Serikali kujua nini kinaendelea kabla ya kuingia mikataba na kuondoa malalamiko ambayo yamekuwepo,” alisema.

Awali, Mwenyekiti wa Kamati ya PIC, Raphael Chegeni, aliitaka NBC kuacha kulala na kuanza kufanya kazi kwa ufanisi na Serikali.

Kuhusu agizo hilo la Spika, Chegeni alimwomba kwa kuwa Bunge linaendelea, awape nafasi ili wakutane na taasisi hizo.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa NBC, Theobald Sabi, alisema watapata nafasi ya kuzungumza na kamati kuwaeleza juu ya mwenendo wa benki, mafanikio na changamoto mbalimbali ambazo inazipitia.

Kuhusu gawio, alisema hivi sasa wanasonga mbele wakiendelea kuikuza benki hiyo na mwaka 2000 ilikuwa na jumla ya mtaji wa Sh bilioni 326, lakini sasa mtaji ni Sh trilioni moja.

Alisema hayo ni mafanikio na watajitahidi kusonga mbele na mwaka 2017 walilipa gawio kwa Serikali Sh bilioni 1.2 na wanategemea wamiliki wa benki watafanya uamuzi juu ya ulipaji wa gawio miaka ijayo.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images