Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Harmonize: Siwezi Kumchagulia Diamond Mwanamke wa Kuoa...Aoe Yeyote, Kwani Utamu Ntapata Mimi?

$
0
0
Diamond Platnumz bado amezid kukamata headline mitandaoni kuhusu maisha yake  ya kimahusiano, safari hii Harmonize naye katia neno katika hayo yanayoendelea.

Harmonize amesema hawezi kumshauri Diamond Platnumz awe na nani kwa sasa kati ya Zari, Hamisa au Wema ila ataonesha ushirikiano kwa yeyote akayechaguliwa na Diamond.

“Mimi yeyote; akiniambia leo tunarudi South Africa mimi nipo pale Pictorial, akiambia kwa wakati huu tuhamie Ununio, nipo pale kwa Madam, akiambia official tunachukua Hamisa tunaweka ndani nipo, sasa jamani kwani utamu napata mimi,” Harmonize ameiambia Wasafi TV.

Awali Harmonize alisema kuwa licha ya kufanya kazi na Diamond kwa ukaribu na kusaidiana  katika mambo mbali mbali ni vigumu kwa yeye kumshauri kuhusu mahusiano yake ila watu wa karibu kutoka kwenye familia yake kama Romy Jons na Esma Platnumz wanaweza kufanya hivyo.

Wema Sepetu Atia Neno 'Ndoa' ya Diamond na Zari

$
0
0
Msanii Maarufu wa filamu za Kibongo , Wema Sepetu,  amempongeza Diamond Platnumz kwa video yake mpya ya ‘Iyena’ aliyomshirikisha Rayvanny.

Katika maudhui ya video hiyo, Diamond amecheza na mzazi mwenziye, Zarina Hassan (Zari The Boss lady),  kama wamefunga ndoa, Wema amemtaka msanii huyo kufanya kweli kama filamu hiyo inavyoonyesha.

“New Track Alert Ila kama ingekuwa Pambe ingekuwa Kweli. Just thinking out Loud, Diamond Chibudeeee Fanya kweli bwana. Inshallah mwaka huu hata mwakani. Tuje kucheza Baikoko sie, Rayvanny Kazi nzuri,” ameandika Wema kupitia ukurasa wake wa Instagram.”

Kabla ya Diamond na Zari kuwa na mahusiano yaliyowaletea watoto wawili na baadaye kutengana, mwanamuziki huyo alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Wema. 

Hata hivyo, Siku ya Wapendanao (Valentine Day) mwaka huu,  Zari alitangaza kuvunja kwa mahusiano yake na mwimbaji huyo akidai alikuwa na mtandao mkubwa wa wapenzi wengine.

Serikali Yashauriwa Kutosaini Upya Mkataba wa Songosongo Pindi Utapomalizika

$
0
0
Kamati ya Bunge iliyoundwa na Spika Job Ndugai kuchunguza mapato yatokanayo na gesi asilia imependekeza mkataba wa Songosongo usihuishwe mara utakapofikia mwisho wake mwaka 2024.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumamosi Juni 2, 2018 na mwenyekiti wa kamati hiyo, Dunstan Kitandula wakati akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo katika hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma.

Amesema kuwa mkataba huo namna ulivyo hauna faida kwa Serikali, badala yake umeegemea upande mmoja wa mwekezaji.

Kitandula amesema mkataba huo unamalizika mwaka 2024 na kwamba hadi sasa kamati yake ina amini kuwa mwekezaji alisharudisha gharama zake.

“Pamoja na hayo, tunapendekeza kuwa wahusika wote katika miradi ya gesi ikiwemo mradi kuchunguzwa na vyombo vya ulinzi na usalama ili kuona kama walikuwa na nie njema na nchi yetu au la,” amesema Kitandula.

Amesema kuwa inashangaza kuona baadhi ya watumishi walioliingiza Taifa kwenye mikataba hiyo ya utata bado wapo ndani ya Serikali wakiendelea na utumishi.

Kamati Maalumu Ya Bunge Yaibua Madudu, Mawaziri Watajwa

$
0
0
Kamati iliyoundwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai kuchunguza mwenendo wa biashara ya sekta ya gesi asilia nchini imebaini madudu katika sekta hiyo ikiwamo mikataba ya serikali na wawekezaji ilivyoliingiza hasara taifa kupitia sekta hiyo huku mfanyakazi mmoja akilipwa mamilioni.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo iliyoundwa Novemba mwaka jana, Dunstan Kitandula amesema hayo bungeni jijini Dodoma leo wakati akiwasilisha ripoti ya kamati hiyo kwa Bunge.

Katika ripoti hiyo, Kitandula amewataja mawaziri zamani wa iliyokuwa Wizara ya Nishati na Madini, Daniel Yona, Nazir Karamagi, William Ngeleja na marehemu Abdallah Kigoda kuingia mikataba hiyo, ambayo alisema imekuwa ikiliingizia hasara taifa.

“Mawaziri hao walikuwa wakisaini mikataba hiyo na makampuni ya kigeni kupitia aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Yona Kilaghani.

“Aidha, katika uchunguzi wetu, kamati ilibaini mfanyakazi mmoja wa kigeni wa Kampuni ya Payet, analipwa mshahara wa Sh milioni 96 kwa mwezi tofauti na wazawa ambao wanalipwa mshahara kidogo.

“Kutokana na hali hiyo, kamati inapendekeza vyombo vya dola vichunguze mikataba yote katika sekta ya gesi iliyoingiwa na viongozi hao ili kuona kama walikuwa na nia njema au waliiisaini kwa kujali maslahi yao,” amesema Kitandula.

Dawa Za Nguvu Za Kiume Na Kukosa Hamu Ya Tendo La Ndoa

$
0
0
Asilimia 45-80 ya wanaume wapo tofauti na wengine kwa kutowatimizia vyema wake au wapenz wao na kuwasababishia kutoka nje ya mahusiano yao. 

NINI CHANZO CHA HAYO? Kupiga punyeto,Ngiri, Vidonda vya tumbo, Korodani moja kuvimba, Msongo wa mawazo, Presha, Magonjwa ya zinaa, Kufanyiwa tohara ukiwa na umri mkubwa, Kisukari. 

DR. LUTAJA Sasa anakuletea tiba sahihi ya tatizo la Nguvu za kiume. 

NTOMBO :Hii hutibu na kuponya kabisa tatizo la Nguvu za kiume, utakuwa na uwezo wa kufanya tendo la ndoa zaidi ya mara tatu bila kuchoka na itakufanya uchelewe kafika kileleni kwa mda wa dk 20-45. Dawa hii imechanganywa na miti 18,Hata wazee wenye umri mkubwa wa zaidi ya miaka 85 wanapona kabisa okoa mahusiano yako, ndoa yako sasa. 

SUNGURURU MIX:Ndio tiba sahihi kwa wale wenye maumbile madogo hurefusha na kunenepesha uume saizi uipendayo nchi 3-8 na unene cm 2-5,dawa hii ipo katika mfumo wakupaka nakunywa na haina madhara yoyote kwa mtumiaji :Hii ni tiba tofauti kabisa nazile ambazo umekwisha wahi kutumia. 

Pia tunadawa za Kupandisha nyota , Uzazi, Pumu, Malaria sugu, miguu kuwaka moto, Kaswende, Kisonono pamoja na mvuto wa mpenzi.

 DR. LUTAJA ANAPATIKANA DAR-ES-SAALAM Simu 0713-821823 kwa wale wa mikoani huduma hii utaipata popote ulipo.

Nay Wa Mitego Ampa Ushauri Mzito Diamond Kuhusu Zari...." Acha Kupuyanga Na Hao Mapugi Machafua Nyota"

$
0
0
Msanii Nay wa Mitego ametoa neno katika ngoma mpya ya Diamond Platnumz ya ‘Iyena’ ambapoamesema hata angetupa ngoma hiyo barabarani inge – hit tu.

Nay amesema kuwa licha ya kwamba ngoma hiyo ni  kali, lakini yupo na mzazi mwenzie mwenye nyota na mafanikio, Zari The Bass Lady. Amemtaka Diamond aache kupuyanga na wachafua nyota.

“Mzee Mwenzangu Diamond platnumz Hii Ngoma Iyena Ata Ungeenda Kuacha Tu Barabarani Ukajifanya Kama Umeitupa Inge Hit Tu. Licha Ya Kwamba Ngoma Kali Pia Upo Na Mkeo Original Mama Tee Mwenye Nyota Ya Hela Na Mafanikio. Sasa Wewe Endelea Kupuyanga Na Hao Mapugi Machafua Nyota. Nitaongea Na Mama Tee Yaishe Tu.Haya Fanya Muende YouTube,” ameandika Nay wa Mitego kupitia mtandao wake wa Instagram.

Taarifa za bunge kuburuza Vigogo mahakamani

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano,  Profesa Makame Mbarawa amesema watakaobainika kuhusika na madudu yaliyomo katika taarifa za kamati maalum za Bunge zilizoundwa kuchanguza masuala ya gesi asilia na uvuvi wa bahari kuu, watachukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.

“Kuna watuhumiwa wawili wametajwa, vyombo vya dola vinatakiwa kuchukua hatua kwa wale walioghushi lesini za uvuvi,” amesema Mbarawa leo Juni 2, 2018 katika hafla ya kamati hizo zilizoundwa na Spika Job Ndugai, kukabidhi taarifa zake za uchunguzi kuhusu maeneo hayo mawili iliyofanyika viwanja vya Bunge mjini Dodoma

Mbarawa ambaye amemuwakilisha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema, “Tumeyasikia mengi, Watanzania wamesikia mengi kuhusu ripoti hizi. Tutasoma ripoti hizi neno kwa neno, mstari kwa mstari na kipengele kwa kipengele. Niwahakikishe Bunge na Watanzania kwamba mapendekezo tutayatekeleza kwa haraka.”

“Kuna shida katika mikataba hasa gesi asilia. Utasikia kuna kasoro katika mikataba na Serikali ya Awamu ya Tano tumelisikia na tumejipanga na tutafanyia kazi. Kama ambavyo ripoti zimeeleza, wale ambao walihusika tutafanya uchunguzi na sheria itachukua mkono wake.”

Amesema katika sekta ya uvuvi kuna shida ya sera, kanuni ,sheria na kuahidi kuzifanyia kazi ili uvuvi uwe na maslahi kwa Taifa.

Kamati Maalumu ya Bunge ya Uvuvi Nayo Yaibua Madudu....Trilioni 5.9 Zimepigwa

$
0
0
Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya Bunge ya Uvuvi wa Bahari Kuu, Anastazia Wambura amesema Serikali imepoteza Sh5.98 trilioni kati ya mwaka 2009 hadi 2017, sawa na asilimia 14.51 ya bajeti ya mwaka wa fedha 2017/18.

Pia, amesema katika kipindi hicho Tanzania imepata hasara ya Sh3.169 trilioni kutokana na mfumo mbovu kwenye bahari kuu.

Akizungumza leo Jumamosi Juni 2, 2018 katika makabidhiano ya taarifa za kamati mbili za kuchunguza uvuvi wa bahari kuu na gesi, Wambura amesema hatua ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kusitisha utoaji wa leseni za meli za kigeni ulisababisha hasara ya Sh5.4 bilioni katika kipindi cha 2016/17.

Amesema mbali na hasara hiyo, Taifa limekuwa likipoteza Sh352 bilioni kila mwaka kutokana na kuuza samaki ghafi nje ya nchi.

Katika taarifa yake hiyo, Wambura amesema hatua ya kutokuwa na bandari ya uvuvi kumeisababishia Serikali hasara ya Sh31.2 bilioni katika kipindi cha mwaka 2009 hadi 2017.

Amesema kiuhalisia sekta ya uvuvi inaweza kutoa mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa nchi, lakini Taifa halinufaiki kutokana na changamoto walizobaini.

Trump asema mkutano na Kim Jung Un utafanyika

$
0
0
Rais wa Marekani Donald Trump Ijumaa amekutana kwa dakika 80 katika ofisi ya Oval na Jenerali ambaye amemuelezea kama ni mtu wa pili mwenye madaraka ya juu kuliko wote nchini Korea Kaskazini.

Baadae, Trump amewaambia waandishi waliokuwako White House kwamba mkutano wa Juni 12 huko Singapore kati yake na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un, utafanyika.

Lakini, Trump alikataza kuwepo baadhi ya matumaini makubwa, akisema mkutano huo ni “mwanzo “ na mazungumzo ya hapo baadae huenda yatahitajika ili kuweza kufikia makubaliano na Pyongyang juu ya kuondosha silaha zake za nyuklia.

“Sio kwamba tutakwenda katika mkutano na kusaini kitu fulani Juni 12, na wala hatukutaka iwe hivyo,” amesema. “Tutaanza kwa pamoja mchakato fulani.”

Trump aliweka wazi kuwa “hajawahi kusema kuwa hilo litafanyika katika mkutano mmoja,” lakini mchakato huo “ hatimaye utakuwa wenye mafanikio.”

Alipoulizwa na VOA iwapo Korea Kaskazini imekubali kukamilisha, uhakiki na kutositisha kuondolewa kwa silaha za nyuklia, Trump alijibu kuwa “tumezungumzia masuala mengi sana.”

Rais amemwambia Kim Yong Chol, mkuu wa zamani wa idara ya usalama katika jeshi la Korea Kaskazini, “chukua muda wako. Tunaweza kwenda haraka. Na tunaweza kwenda polepole.”

Rais ameweka wazi kuwa vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini havitaondolewa, mpaka pale nchi hiyo itakapokubali kuacha kutengeneza silaha zake za nyuklia.

Wakati mazungumzo juu ya mkutano wa Singapore yakijadiliwa, baadhi ya wafuatiliaji wa suala hili wanahisi kuwa Trump na Kim Jong Un kila moja anajua kiuhakika kile ambacho wanataka hatimaye kukifikia.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya June 3

TANZIA: Mapacha walioungana Maria na Consolata wamefariki Dunia

$
0
0
Usiku wa June 2, 2018 Mapacha wawili walioungana, Maria na Consolata wamefariki dunia ukatika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa walikokuwa wakipatiwa matibabu.

Kwa mujibu wa mkuu wa wilaya wa Iringa Richard Kasesela,  mapacha hao wamefariki wakipishana kwa takribani saa 2.

"Wamepigania sana afya zao, mida ya saa moja hivi jioni ndio nilipokea taarifa za kifo chao na kwa sababu nilikuwa mazingira ya hospitali basi nilisogea kuwaona – na ni kweli hatunao,” amesema Kasesela.

Pacha wa kwanza alifariki majira ya saa 1 usiku, huku mwenzake akifariki saa 3 usiku.

Mapacha hao wamekuwa na historia ya matatizo ya moyo. Tangu Disemba 2017 pacha hao walianza kuumwa na kulazwa hospitali ya mkoa ya Iringa.

Baadaye walihamishiwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKIC) katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, walipolazwa kwa takribani miezi miwili kwa ajili ya matibabu mpaka waliporuhusiwa kurejea tena Iringa mnamo Mei 17.

Maria na Consolata walizaliwa wilayani Makete mkoani Njombe mwaka 1996.

Walihitimu darasa la saba katika shule ya msingi Ikonda, kisha wakajiunga na shule ya Maria Consolata iliyopo Kilolo mkoani Iringa ambapo walihitimu kidato cha nne.

Baada ya hapo, walijiunga na shule ya Sekondari ya Udzungwa wilani Kilolo walipohitimu kidato cha sita, ikifuatiwa na Chuo Kikuu cha Katoliki cha Ruaha (Rucu) walipokuwa wakisomea fani ya ualimu.

Rais Magufuli Kafanya Uteuzi wa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania

Rais Magufuli Awalilia Mapacha Walioungana Maria na Consolata

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa familia, Masista wa Maria Consolata na wote walioguswa na kifo cha mabinti mapacha walioungana Maria na Consolata Mwakikuti waliofariki dunia jana jioni katika hospitali ya Mkoa wa Iringa.

Mhe. Rais Magufuli aliwatembelea Maria na Consolata walipokuwa wakipata matibabu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Jijini Dar es salaam tarehe 06 Januari, 2018.

Pamoja na kuwapa pole, Maria na Consolata waliongoza sala ya kuliombea Taifa na Viongozi wake.

Mhe. Rais Magufuli anasema anatambua kuwa Maria na Consolata walikuwa na ndoto kubwa ya kuja kulitumikia Taifa baada ya kumaliza Chuo Kikuu cha Masista wa Consolata Ruaha (RUCO) walikokuwa wakiendelea na masomo yao, lakini haikuwa hivyo.

Amewaombea Mwenyezi Mungu aziweke roho zao mahali pema peponi, Amina.

Operesheni Polisi Yanasa 35, Silaha 5 Mikoa Ya Kusini

$
0
0
Na. Jeshi la Polisi.
Jeshi la Polisi nchini limefanikiwa kukamata Silaha mbalimbali na watuhumiwa 35 katika Oparesheni Maalum inayoendelea katika Ukanda wa mikoa ya  Kusini unaojumuisha mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma.

Akizungumza mkoani katika eneo la Kilambo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji mkoani Mtwara, Mkuu wa Operesheni Maalum za Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi Liberatus Sabas alisema kati ya watuhumiwa 35, wawili wamekabidhiwa Idara ya Uhamiaji kwa hatua zaidi, 16 wapo chini ya Upelelezi na 17 wapo chini ya uangalizi wa Polisi (Police Supervisee).

Sabas amezitaja Silaha zilizokamatwa kuwa ni pamoja na SMG mbili, Rifle mbili na Gobore moja ambapo amebainisha kuwa ufuatiliaji bado unaendelea ili kuwabaini wafadhili wa uhalifu hapa nchini.

“Kama nilivyosema kipindi kilichopita kuwa Operesheni hii ni endelevu na matokeo ndio kama haya hivyo hata wale waliokimbilia nchi jirani ya Msumbiji hawapo salama kwa kuwa hata kule operesheni zinaendelea na tunashirikiana na Jeshi la Polisi la nchi hiyo kuhakikisha kuwa wote wanakamatwa“. Alisema Sabas.

Aidha Kamanda Sabas amewataka wakazi wa mwambao wa mto Ruvuma kuendelea kutoa taarifa mapema mara tu waonapo watu wanaowatilia mashaka katika maeneo yao kwa kuwa uzoefu umeonyesha kuwa baadhi ya watuhumiwa wamekuwa wakitumia vipenyo vya mto huo na kufanya uhalifu kati ya nchi yetu na Msumbiji.

Pia amesema Operesheni hiyo inashirikisha vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama hivyo ametoa wito kwa raia wema kuendelea kutoa taarifa za siri ili kuendeleza amani na usalama hapa nchini.

Kufuatia mafanikio hayo, baadhi ya Wananchi katika mkoa wa Mtwara wamelipongeza Jeshi la Polisi kwa kazi kubwa inayofanya ya kuhakikisha kuwa wahalifu wanaosumbua wananchi wanakamatwa na kufikishwa mahakamani.

Rais Magufuli Kuzindua Programu Ya Kuendeleza Sekta Ya Kilimo Awamu Ya Pili (ASDP II)

$
0
0
Na Mathias Canal-WK, Dar es salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa programu ya kuendeleza sekta ya kilimo awamu ya pili (ASDP II) tarehe 4 June 2018.

Katika dhifa hiyo inayotarajiwa kuanzia Saa 2.00 asubuhi katika jengo la Mikutano la kimataifa la Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaam, Rais Magufuli ataambatana na wageni wengine wa kitaifa na kimataifa akiwemo makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa, Mkuu wa Mkoa wa Dara es salaam Mhe Paul Makonda, Mawaziri wa sekta za kilimo pamoja na wadau wote wa sekta ya hiyo.

Taarifa ya uzinduzi wa Programu hiyo ya kuendeleza sekta ya kilimo nchini imetolewa jana 1 June 2018 na waziri wa kilimo Mhe Dkt. Charles Tizeba wakati akizungumza na waandishi wa habari katika jengo la Mikutano la kimataifa la Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaam.

Dkt Tizeba alisema, Wizara za kisekta zikijumuisha Wizara ya Kilimo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa-TAMISEMI, Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji, Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Wizara ya Maji na Umwagiliaji  ndizo zenye jukumu la kuhakikisha ASDP II inakuwa na mafanikio makubwa nchini na kuwa mkombozi wa wananchi katika kilimo.

Alisema kuwa ASDP II itatekelezwa katika mikoa na wilaya zote kwa kuzingatia mazao ya kipaumbele kufuatana na ikolojia ya kilimo ya kanda kwa miaka kumi (10) kwa vipindi viwili vya miaka mitano mitano ambapo kipindi cha kwanza kitaanza 2018/19 hadi 2023/24.

Katika hatua nyingine Dkt Tizeba ametaja lengo la Programu hiyo kuwa ni kuleta mageuzi katika sekta ya kilimo ili kuongeza uzalishaji na tija  katika kilimo, mifugo na uvuvi; kuongeza pato la wakulima, wafugaji na wavuvi; kuongeza pato la Taifa na kuwa na uhakika wa usalama wa chakula na lishe.

Aidha, Programu hii itatekeleza sera mbalimbali kama vile Sera ya Kilimo ya Taifa, Sera ya Mifugo ya Taifa, Sera ya Uvuvi, Sera ya Masoko ya Mazao ya Kilimo, Sera ya Umwagiliaji ya Taifa, Sera ya Usalama wa Chakula na Lishe, Sera ya Ugatuaji Madaraka, Sera ya Maendeleo ya Ushirika na Sera ya Mashirikiano kati ya Sekta za Umma na Sekta Binafsi.

Katika hatua nyingine Mhe Dkt Tizeba ameuarifu umma wa watanzania kuwa endapo mpango huo utatekelezwa kama ilivyopangwa hadi kufikia mwaka 2022 Tanzania itakuwa katika uchumi wa kati.

Katika utekelezaji wa ASDP II washiriki ni wadau wa sekta ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Ushirika, Wizara, Taasisi za Serikali na zisizo za Serikali, Washirika wa Maendeleo, Sekta Binafsi na wananchi wote.

MWISHO.

Kigwangalla Ashiriki Mazishi Ya Mama Yake Mzazi Hussein Bashe Wilayani Nzega

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Nzega Vijijini, Dkt. Hamisi Kigwangalla akimfariji mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe kufuatia kifo cha mama yake mzazi aliyezikwa jana wilayani Nzega. Kulia ni mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye. Wabunge mbalimbali wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiongozwa na Abdallah Bulembo walishiriki msiba huo pamoja na viongozi mbalimbali wa vyama na Serikali.

 Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Nzega Vijijini, Dkt. Hamisi Kigwangalla (kulia) akimfariji mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe kufuatia kifo cha mama yake aliyezikwa jana wilayani Nzega. Kulia ni mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye na mbunge wa Kigoma Vijijini, Peter Selukamba. Wabunge mbalimbali wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiongozwa na Abdallah Bulembo walishiriki msiba huo pamoja na viongozi mbalimbali wa vyama na Serikali.
 Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Nzega Vijijini, Dkt. Hamisi Kigwangalla akitoa salamu za rambirambi katika msiba wa mama yake mzazi mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe aliyezikwa leo wilayani Nzega.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni (wa tatu kulia), Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Nzega Vijijini, Hamisi Kigwangalla (wa sita nyuma kutoka kulia), Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (wa nne kulia), viongozi wengine wa chama na Serikali na wananchi mbalimbali wakiwemo wa wilaya ya Nzega wakishiriki kusalia jeneza lenye mwili wa mama yake mzazi Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (haonekani pichani) muda mfupi kabla ya kupelekwa makaburini kwa ajili ya maziko wilayani Nzega jana.
 Jeneza lenye mwili wa mama yake mzazi Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (haonekani pichani) likiondolewa kwenye eneo la makaburi kupisha mwili huo kuhifadhiwa kwenye nyumba yake ya milelel (kaburini) wilayani Nzega jana.
Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (kulia), Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Nzega Vijijini, Dkt. Hamisi Kigwangalla (mbele yake kulia) na viongozi wengine wa vyama na Serikali na wananchi mbalimbali wakiwemo wa Jimbo la Nzega wakishiriki kumzika mama yake mzazi, Hussein Bashe katika makaburi wilayani humo jana.

Tundu Lissu Kufanyiwa Upasuaji Mwingine Kesho

$
0
0
Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu kesho Juni 4, 2018 atafanyiwa upasuaji wa 21 wa kuunga goti la mguu wake wa kulia huku akiwataka Watanzania kumuombea.

Upasuaji huo ni mwendelezo wa upasuaji ambao amekuwa akifanyiwa katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya alikokuwa amelazwa baada ya kushambuliwa kwa risasi akiwa katika makazi yake mjini Dodoma Septemba 7, 2017.

Alipatiwa huduma za awali katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

Lissu ameeleza hayo leo Jumapili Juni 3, 2018 kupitia taarifa aliyoitoa katika ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Instagram, akiambatanisha na picha yake akiwa amelala wodini kando ya mkewe, Alicia.

“Hello  wapendwa wangu. Ninaamini wengi wenu, kama sio wote, mnafahamu kwamba Jumatatu Juni 4 nitafanyiwa operesheni ya mwisho kwenye mguu wa kulia,” amesema.

“Ni operesheni kubwa inayotazamiwa kuchukua takriban saa nane kwa taarifa nilizopewa tangu mwanzoni mwa wiki hii. Hivyo madaktari wangu wametumia muda mrefu kidogo kuniandaa kwa ajili ya Jumatatu.”

Ameongeza, “Napenda niwajulishe kwamba ninajisikia vizuri kiafya na baada ya kuwa kitandani tangu  Aprili 11 (2018) nilipofanyiwa operesheni ya pili, sasa niko tayari kwa ajili ya hii ya mwisho. Madaktari wangu wako vizuri. Nina imani watafanya kazi nzuri ya kitabibu.”

Lissu alishawashukuru wote waliomsaidia tangu aliposhambuliwa kwa risasi hadi sasa na kuwataka wazidi kumuombea.

“Bado safari ni ndefu lakini ninaweza kusema nimeanza kuona mwanga katika hili tanuru refu. Nimesema mara nyingi kwamba ninaona fahari na faraja kwamba Watanzania wenzangu na wasio Watanzania wamenitibu na wanaendelea kunitibu. Najua mtaniponya kwa nguvu za Mola wetu na kwa upendo na ukarimu wenu. Nawaombeni msichoke. Nawashukuruni sana,” amesema.

Moto Wateketeza Maduka Lamadi Mkoani Simiyu

$
0
0
Na Hezbon Mahaulane
 Moto ambao unadaiwa chanzo chake ni mfanyabiashara mmoja kusahau kuzima pasi ya umme na kushika moto, umesababisha hasara kubwa baada ya kusambaa na kuteketeza vitu mbalimbali kwenye maduka sita katika mji wa lamadi uliopo wilaya ya busega, mkoani simiyu.

Moto huo ambao ulizuka majira ya saa mbili kasorobo usiku wa kuamkia juni 03, chanzo chake kinadaiwa ni mfanyabiashara mmoja kusahau kuzima pasi ya umme ndani ya duka na kushika moto, na hivyo kusambaa na kuunguza vitu mbalimbali, ambapo maduka sita yameteketea.

John balale ni mmoja wa mashuhuda wa tukio hili, anasema jeshi la polisi  kituo cha lamadi, zima moto na wananchi  walishirikiana kuuzima moto huo lakini changamoto ikawa ni vifaa duni.

Mkuu wa mkoa wa simiyu anthony mtaka, amefika katika eneo la tukio na kujionea athari za moto huo, na kuwataka  wahanga kuwa na subira  ,wakati tathimini ya mali iliyoteketea ikifanyika, huku akiwapongeza juhudi za wananchi wa lamadi kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama katika kuuzima.

Kamanda wa  jeshi la zimamoto na ukoaji mkoa wa simiyu gerevas fungamali, akizungumzia tukio hilo, anasema elimu ya zima moto na uokozi itaendelea kutolewa kwa wananchi ili kujikinga na majanga, huku diwani wa kata ya lamadi laurent bija, akiwataka wananchi kujiandaa kujikinga na majanga yanapotokea.


Merkel: Umoja wa Ulaya haupaswi kuwa Umoja wa madeni

$
0
0
Na Hezbon Mahaulane
 Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amempongeza waziri mkuu mpya wa Italia Giuseppe Conte. Hata hivyo ameonekana kupuuza wito ya Italia kutaka Umoja wa Ulaya kuisamehe madeni yake

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel alifanya mazungumzo na waziri mkuu mpya wa Italia Giuseppe Conte Jumamosi na kumkaribisha mjini Berlin kwa mazungumzo zaidi kuhusu mustakabali wa uhusiano wa nchi zao.
 
Kwenye tarifa, ofisi ya kansela imesema Merkel alimpongeza Conte kwa kuwa waziri mkuu. Taarifa hiyo imeongeza kuwa, Merkel na Conte walizungumza kwa njia ya simu, walitilia msisitizo umuhimu wa kuendeleza ushirikiano wa pande zote mbili.
 
Conte ambaye ni profesa wa shera asiyejulikana sana, amekuwa kimya tangu alipoapishwa . Lakini alitangaza kwenye ukurasa wake wa Facebook kuwa, kando na Merkel pia alizungumza na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron siku ya Jumamosi.
 
Amesema atakutana na viongozi hao katika mkutano wa kilele wa G7 utakaofanyika Canada, ambapo pia atazungumzia masilahi ya raia wa Italia.

Kutinyu Atambulishwa Rasmi Azam FC

$
0
0
Na Hezbon Mahaulane
Uongozi wa klabu ya Azam FC umeamua kumtambulisha rasmi aliyekuwa mchezaji wa Singida United, Tafadzwa Kutinyu katika kikosi chao.
 
Kutinyu ameingia mkataba wa miaka miwili na Azam ambapo ataingia kambini kuanzia Julai 3 2018 kuanza rasmi maandalizi ya msimu ujao wa ligi zitakazoanza kuchezwa.
 
Mzimbabwe huyo alijunga na Singida United akitokea klabu ya Chicken Inn inayoshiriki ligi kuu Zimbambwe. 

Kutinyu amesaini Azam, usajili unaoelezwa umegharimu kiasi cha dola 2 0,000 kwa Singida kumuachia.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images