Nyota ya mwanadamu ni nafsi hai ya mwanadamu.
Nafsi hai ya mwanadamu ni pumzi ya Mungu aliyopuliziwa mtu baada ya kuumbwa.
Lengo la Mwenyezi Mungu lilikuwa ni kumuumba mwanadamu yaani ( MWENYE NAFSI HAI) ili amsaidie kuutawala ulimwengu na kuvitiisha vitu vyote vilivyomo ndani yake vinavyo onekana na visivyo onekana.
Ili kufanikisha lengo hili,ilimbidi Mwenyezi Mungu amuumbe kwanza mtu ( YAANI MWENYE MWILI NA NAFSI YA UDONGO ) na baada ya kumuumba mtu huyo,ndipo Mwenyezi Mungu akampulizia mtu huyo pumzi ya uhai ambayo sasa ndio ikamfanya mtu huyo kuwa Mwanadamu kamili yaani MWENYE NAFSI HAI au ALIYE PULIZIWA PUMZI YA UHAI ( PUMZI YA MUNGU)
Ndani ya pumzi hii ya uhai aliyo puliziwa mwanadamu ambayo ndio nyota ya mwanadamu, limeandikwa kusudi la Mungu juu ya maisha ya mwanadamu.
Kwa hiyo nyota ya mtu ni pumzi ya uhai ya Mwenyezi Mungu ambayo ndani yake kuna tamko rasmi juu ya maisha ya mwanadamu.
Ni tamko rasmi la Mwenyezi Mungu juu ya maisha ya mwanadamu kwa maana ya kwamba ndani ya pumzi aliyo puliziwa mwanadamu kuna neno au tamko rasmi la Mwenyezi Mungu kuhusu mambo yote aliyo yakusudia juu ya maisha ya mwanadamu huyo kuanzia siku anazaliwa hadi siku atakayo ingia kaburini.
Nyota ya mtu ni mafuta ya Mungu yaliyo pakwa kwenye nafsi ya mwanadamu. Ndani ya mafuta hayo limeandikwa kusudi la Mwenyezi Mungu juu ya maisha ya mtu huyo kuanzia siku ya kutungwa kwa mimba yake hadi siku ya kufa kwake.
Uhusiano kati ya nyota ya mwanadamu na maisha yake unafanana kwa kiasi kikubwa sana na uhusiano kati ya mbegu ya mti na mti wake.
Kwa mfano tuchukulie mbegu ya mbuyu. Mbegu ya mbuyu kwa umbo ni ndogo sana haienei hata kwenye kiganja. Lakini inatoa mti mkubwa kabisa wenye matawi, mizizi, matunda na faida lukuki kwa mwanadamu.
Katika ulimwengu wa kiroho maana yake ni kwamba ndani ya mbegu ya ubuyu, yamendikwa mambo yote hayo unayo yaona kuhusu mbuyu. Ndani ya mbegu ya ubuyu umeandikwa mti wa mbuyu, matunda ya ubuyu, ladha tamu ya ubuyu, faida za kiafya za juisi ya mbuyu, faida za kiafya za mafuta ya ubuyu, faida za kiafya za magome ya mbuyu nakadhalika nakadhalika.
Pia uhusiano baina ya nyota ya mwanadamu na maisha yake ni kama mbegu za mwanaume na maisha ya watoto wake.
Ndani ya mbegu za mwanaume ( shahawa ) kimeandikwa kila kitu kuhusu kitakachozaliwa kutoka kwenye mbegu hizo. Ukizitazama mbegu za mwanaume ni ute ute. Lakini ndani ya mbegu hizo hizo ameandikwa mtu kamili mwenye macho, masikio, pua, midomo nakadhalika.
Ila ili mtu huyo aweze kutokea ni lazima mbegu hizo zikaungane na mayai ya mwanamke. Vivyo hivyo kwa mwanadamu ndani ya nyota yake kimeandikwa kila kitu kuhusu maisha yake yatakavyo kuwa kuanzia siku atakayo zaliwa hadi siku atakayo ishi, lakini ili mambo yote hayo yatokee ni lazima yale mambo tisa yanayo unda nyota ya mwanadamu yawepo yote.
Vivyo hivyo ndani ya nafsi hai ( nyota ) ya mwanadamu, yameandikwa mambo mambo yote ambayo Mwenyezi Mungu ameyakusudia juu ya maisha ya mtu huyo hapa duniani.
Kazi ya nyota ya mwanadamu ni nini ?
Mwenyezi Mungu alivyo uumba ulimwengu aliukabidhi chini ya utawala wa viumbe wake wakuu watatu.
Kiumbe wa kwanza kupewa mamlaka ya kutawala ni Jua.Jua lilipewa mamlaka ya kuutawala mchana. Kiumbe wa pili kupewa mamlaka ya kutawala ni Mwezi. Mwezi ulipewa mamlaka ya kuutawala usiku.
Kiumbe watatu kupewa mamlaka ya utawala ulimwenguni ni mwanadamu . Na ninaposema mwanadamu namaanisha nafsi hai ya mwanadamu. Mwanadamu alipewa mamlaka ya kuutawalaulimwengu wote na vitu vyote vilivyomo ndani yake vinavyo onekana na visivyo onekana.Walaa mwanadamu hakuambiwa kuutawala mchana au usiku pekee bali yeye alipewa mamlaka ya kuutawala ulimwengu na vitu vyote vilivyomo ndani yake vinavyo tambaa juu ya ardhi, ndani ya maji na juu angani bila kujalisha ni mchana au usiku.
Kwa hiyo tumeona kuwa ulimwengu unatawaliwa kwa ushirikiano wa vitu vikuu vitatu ambavyo ni Jua,Mwezi,na Nafsi Hai ya mwanadamu. Kwa lugha nyingine tunaweza kuuita utatu mtakatifu wa utawala wa ulimwengu. Hivyo basi kazi na jukumu kuu la nyota ya mwanadamu ni kuutawala ulimwengu.
MAMBO TISA YANAYO UNDA NYOTA YA MWANADAMU
Nyota ya mwanadamu inaundwa na mambo tisa. Yaani ndani ya pumzi ya uhai anayo puliziwa kila mwanadamu yameandikwa mambo tisa . Pamoja na mambo hayo tisa, imeandikwa stori ya maisha ya mwanadamu huyo kuanzia siku atakayo zaliwa hadi siku atakayo ingia kaburini. Mambo hayo tisa yaliyo andikwa kwenye nyota ya mwanadamu ndio yanayo saidia kuibeba stori ya maisha yake. Hili stori ya maisha ya mwanadamu iweze kudhihirika katika ulimwengu wa nyama au kwa lugha nyepesi ili mambo yote ambayo Mwenyezi Mungu ameyakusudia juu ya maisha ya mwanadamu yaweze kutokea basi ni lazima yashikiliwe na mambo haya tisa ambayo yameandikwa kwenye pumzi ya uhai ( nyota ) ambayo amepuliziwa kila mwanadamu.
NYOTA YA ADAMU ILIVYO ILIVYO CHUKULIWA NA KUMILIKIWA NA IBILISI
Ndani ya pumzi ya uhai ( nyota ) ya Adamu yaliandikwa mambo makuu tisa pamoja na stori kamili ya maisha ya Adamu na kizaz chake chote (yaani wanadamu wote ).
Adamu alipewa sharti moja na Mwenyezi Mungu kwamba asile tunda la mti ule na endapo atakula basi hakika atakufa yaani nafsi yake hai ama nyota yake ama kusudi la Mungu juu ya maisha yake litaondoka na atabaki kuwa mtu tu yani mwenye mwili na nafsi ya udongo .
Hata hivyo Adamu alienda kinyume na agano alilowekewa na Mungu na mara tu baada ya kutenda dhambi ile basi ile nafsi yake hai ikaondoka na Adamu akabaki na kujiona mtupu.
Utupu unaozungumziwa hapo sio utupu wa mwili isipokuwa ni utupu wa nafsi.
Nafsi ya Adamu ilibaki kuwa tupu. Yale mambo yote tisa yaliyoandikwa kwenye nyota yake yakayeyuka na kutoweka.
Mfano wa utupu unao zungumziwa hapa ni sawa na mwanafunzi aliye jisomea mwezi mzima kwa ajili ya mtihani halafu siku ya kufanya mtihani yale yote aliyo yasoma yanayeyuka kichwani na kumuacha akiwa mtupu kichwani asijue aandike kitu gani kwenye mtihani mwisho wa siku mwanafunzi huyu lazima atafeli tu mtihani wake.
Kwa hiyo nyota ya Adam ikachukuliwa na yeye akabaki na utupu nafsini mwake.
Utupu ni nafsi ya kwanza katika utatu mtakatifu wa shetani. Utatu mtakatifu wa shetani una undwa na nafsi kuu tatu ambazo ni Utupu, Giza na Ukiwa . kwa hivyo ndani ya nafsi ya Adamu kukabakiwa na utupu, giza na ukiwa.
Nafsi hai ya Adam ikawa imechukuliwa, na kumuacha Adamu akibaki na nafsi mfu, nafsi ya udongo yenye kuundwa na vitu vitatu yaani Utupu, Giza na Ukiwa ambayo ndani yake kinaweza kupandwa chochote kile chenye asili ya utupu, kiza na ukiwa.
IBILISI ANABADILISHA MAJIRA NA NYAKATI ILI KUMPISHANISHA MWANADAMU NA NYOTA YAKE.
Baada ya kufanikiwa kuiba na kuiweka nafsi ya mwanadamu chini ya umiliki wake, kitu cha kwanza kabisa alicho kifanya Lusifa kilikuwa ni kubadilisha majira na nyakati.
Lusifa aliamua kubadilisha majira na nyakati kwa sababu moja kuu nayo ni kumpishanisha mwanadamu na nyota yake.
Kuna uhusiano mkubwa sana kati ya nyota ya mtu na siku aliyo zaliwa. Nyota ya mtu na siku aliyozaliwa ni sawa na pande mbili za shilingi moja.
Kwa kuwa Ibilisi alibadilisha majira na nyakati basi kwa kiasi kikubwa sana alifanikiwa kumpishanisha mwanadamu na nyota yake. Watu wengi leo hii hawazijui nyota zao halisi licha ya kuzijua tarehe walizo zaliwa.
Nyota ya mtu inatambuliwa kwa kuangalia siku aliyo zaliwa na wala sio tarehe aliyo zaliwa.
Unakuta mtu anasema “ Mimi nyota yangu ni Mapacha “ ukimuuliza kwanini anajibu “ Kwa sababu nimezaliwa tarehe 15 Juni “
Lakini kiukweli kabisa kwa sisi wanajimu tulio somea na kubobea katika taaluma hii ya unajimu tunajua fika kwamba, tarehe uliyo zaliwa haiwezi kusema wewe nyota yako ni nini .
Kwanini ? Kwa sababu majira na nyakati vimebadilishwa tangu zamani. Hiyo unayo amini kuwa ndiotarehe yako ya kuzaliwa inatokana na majira nanyakati zilizo badilishwa na kubatilishwa ,wala sio tarehe yako halisi ya kuzaliwa na wala sio nyota yako halisi.
Wanajimu tunajua tukitaka kujua nyota halisi ya mtu huwa tunaulizia siku aliyo zaliwa. Nyota ya mtu inatazamwa kwa kuangalia siku aliyo zaliwa na sio tarehe aliyo zaliwa.
Ndio maana unakuta watu wawili wenye nyota inayo fanana ( mfano mapacha ) na wanafanya kitu kile kile kimoja lakini mmoja anakuwa tajiri sana na mwingine anabaki kuwa masikini sana, ila wote nyota yao ni mapacha. Jibu ni moja tu, wamezaliwa siku tofauti. Nyota zinafanya kazi kutokana siku na muda ulio zaliwa na sio tarehe uliyo zaliwa.
Ndio sababu watu wengi wanashindwa kufanikiwa katika mambo wanayo yafanya kwa sababu wanayafanya katika majira na nyakati batili. Na majira na nyakati ndio vitu vinavyo tawala kila kitu katika ulimwengu huu.
JINSI IBILISI ALIVYO BADILSHA MAJIRA NA NYAKATI
Majira na nyakati viliwekwa kwa ajili ya kuitumikia nyota ya mwanadamu iweze kutenda kazi na kutimiza majukumu yake kwa ufanisi. Hii ni kwa sababu mafanikio ya nyota ya mwanadamu yanategemea na siku pamoja na muda alio zaliwa. Kama alizaliwa siku ya kwanza basi nyota yake itatawaliwa na kuongozwa na majini na malaika wanao tawala na kutumia siku hiyo ya kwanza. Pia itategemea amezaliwa muda gani, katika siku hiyo, kama amezaliwa mchana basi nyota yake itatawaliwa na kuongozwa na majini wanao tawala mchana wa siku hiyo ambao wanatawala pamoja na jua na kama amezaliwa usiku basi nyota yake itaongozwa na kutawaliwa na majini wanao tawala na kuongoza usiku wa siku hiyo ambao watatawala pamoja na mwezi.
Hivyo Ibilisi alibadilisha majira na nyakati ili kumpishanisha mwanadamu na nyota yake.
1. ALIANZA KWA KUBADILISHA SIKU .
Kwa Mungu hakuna Jumatatu, wala Jumanne wala Jumatano, Alhamisi, Ijumaa, Jumamosi, wala Monday, Tuesday, Wednesday, Thursday, Friday , Saturday na Sunday.
Wala majina ya siku niliyo yataja hapo juu hayana uhusiano wowote yenyewe kwa yenyewe. Kwa maana kuwa Jumatatu sio Monday wala Tuesday sio Jumanne wala Jumapili sio Sunday . Hakuna uhusiano wowote hapo.
Mfano Jumapili sio Sunday.Sunday ni siku ya jua na Jumapili siku ya pili. Kwa hiyo hakuna uhusiano wowote hapo kati ya siku hizo mbili.
Kama nilivyo sema hapo juu kwa Mungu hakuna Jumatatu wala Monday. Ukisoma Torati vizuri hutaona sehemu yoyote ile imeandikwa “ IKAWA JUMATATU, MUNGU AKAFANYA HIVI , AU IKAWA JUMATANO MUNGU AKAFANYA VILE“ Nadhani wote tunakubaliana katika hili
Utakacho kiona ni “ IKAWA SIKU YA KWANZA , MUNGU AKAFANYA HIVI, IKAWA SIKU YA PILI, MUNGU AKAFANYA VILE …
Kwa hiyo kwa Mungu kuna kuanzia SIKU YA KWANZA hadi SIKU YA SABA. Haya ndio majina ya siku za Mungu.
1. SIKU YA KWANZA ( KWA MUNGU SIKU YA KWANZA NI SIKU AMBAYO DUNIANI INAJULIKANA KAMA JUMATANO(WEDNESDAY) HII AMBAYOWEWE UNAIJUA KAMA JUMATANO KWA MUNGU NDIO SIKU YA KWANZA )
Jina la kiroho la siku ya kwanza ni : SIKU YA NURU.
2. SIKUYA PILI ( KWA MUNGU SIKU YA PILI NI HII AMBAYO DUNIANI INAITWA ALHAMISI AU THURSDAY .. SASA KWA UTARATIBU WA HESABU ZA KIMUNGU, ALHAMISI NDIO SIKU YA PILI.. )
Jina la kiroho la siku ya pili ni : SIKU YA AKILI YA MUNGU.
3. SIKU YA TATU: (KWA MUNGU SIKU YA TATU NI HII AMBAYO DUNIANI INAJULIKANA KAMA IJUMAA AU FRIDAY SASA BASI KWA UTARATIBU WA KUHESABU SIKU WA MUNGU, SIKU AMBAYO DUNIANI INAJULIKANA KAMA SIKU YA IJUMAA AU FRIDAY NI SIKU YA TATU )
Jina la kiroho la siku ya tatu ni SIKU YA FAIDA NA THAMANI.
4. SIKU YA NNE ( KWA MUNGU SIKU YA NNE NI HII AMBAYO DUNIANI INAJULIKANA KAMA JUMAMOSI AU SATURDAY. ILA KWA UTARATIBU WA HESABU ZA MUNGU, SIKU YA JUMAMOSI NDIO SIKU YA NNE )
Jina la kiroho la siku nne ni : SIKU YA MAJIRA NA NYAKATI.
5. SIKU YA TANO (KWA MUNGU SIKU YA TANO NI HII AMBAYO HUKU DUNIANI INAJULIKANA KAMA JUMAPILI AU SUNDAY. ILA KWA MUNGU HII NI SIKU YA TANO )
Jina la kiroho la siku ya tano ni : SIKU YA KUFANYA MAMBO MAKUBWA.
6. SIKU YA SITA ( KWA MUNGU SIKU YA SITA NI HII AMBAYO DUNIANI INAJULIKANA KAMA JUMATATU AU MONDAY . SASA KATIKA UTARATIBU WA HESABU ZA KIMUNGU,SIKU YA SITA NDIO HII AMBAYO DUNIANI INAJULIKANA KAMA JUMATATU AU MONDAY )
Jina la kiroho la siku ya sita ni SIKU YA KUMILIKI NA KUTAWALA.
7. SIKU YA SABA ( KWA MUNGU SIKU YA SABA NI HII AMBAYO DUNIANI INAJULIKANA KAMA JUMANNE AU TUESDAY. SASA BASI KWA KUFUATA HESABU ZA KIMUNGU, JUMANNE NI SIKU YA SABA )
Jina la kiroho la siku ya Jumanne ni SIKU YA KUSTAREHESHWA.
Mungu aliweka malaika na majini wakubwa wakubwa kwa ajili ya kuzitumikia siku hizi kwa manufaa ya mwanadamu.
Hivyo basi kila siku ina malaika na majini wake maalumu wanao itumikia. Ili mwanadamu aweze kunufaika na utumishi wa majini na malaika hao ni lazima awe anajua siku wanazo tawala . Kwa sababu Lusifa Alisha badilisha utaratibu huo, kwa kubadilisha majina ya siku husika na kuwapa majini wake mamlaka ya kutawala siku hizo,inakuwa vigumu sana kwa mtu kunufaika na usaidizi wa majini na malaika hao kwa sababu hawawezi kukutumikia kama haujui siku wanazo tawala.
Mungu aliumba siku saba kwa mwanadamu na kutenga siku moja kwa ajili ya kumuabudu. Vivyo hivyo kwa majini na malaika hawa. Kila majini na malaika wana siku yao maalumu ya kumuabudu na kumtukuza Mwenyezi Mungu.
Kwa mwanadamu atakae abudu katika siku moja na majini/malaika hawa basi majini na malaika hao watamtumikia na mtu huyo atapata mafanikio makubwa sana kwa kitu anacho kifanya ilimradi kiwe kinaendana na nguvu na uweza wa majini na malaika wanao tawala siku hiyo.
Mfano wa kwanza tunauona kwa wazungu.Wazungu waowalichagua kusali na kuabudu SIKU YA TANO ambayo ni SIKU YA KUFANYA MAMBO MAKUBWA. Siku hii inatawaliwa na majini na malaika wenye kufanya mambo makubwa makubwa. Kwa sababu wazungu wamechagua kuabudu katika siku hii basi majini na malaika wanao tawala siku hii kwa uwezo waliopewa na Mwenyezi Mungu, wamewatunuku wazungu uwezo wa kufanya mambo makubwa makubwa.
Ndiomaana wazungu wanasifika kwa kufanya mambo makubwa katika hii dunia. Kufanya vumbuzi na gunduzi kubwa kubwa nakadhalika. Wanabebwa na nguvu ya kiroho ya siku waliyo ichagua kuabudu.
Mfano wa pili tunauona kwa waarabu.Waarabuwao walichagua kumuabudu Mwenyezi Mungu katika SIKU YA TATU ambayo ni SIKU YA FAIDA NA THAMANI.
Ndio maana waarabu wanajulikana kote ulimwenguni kwa kufanya mambo yenye kuwaletea faida na thamani kubwa. Waarabu wanajulikana na kuheshimika kwa kufanya biashara zenye kuleta faida kubwa kubwa.
Uhitaji kwenda Qatar,Bahrain, Kuwait au U.A.E ili kuthibitisha ninacho kisema. Ubora wa waarabu katika kufanya biashara zenye kuleta faida kubwa unajulikana ulimwengu mzima.
Hakuna mwarabu anae fanya ibada sawa sawa halafu akafanya biashara na asipate faida hayupo. Kama yupo basi huyo atakuwa hafanyi biashara zake vizuri. Na ndio maana kwa waarabu mtu anaeishi maisha ya kimasikini anachukuliwa kama mtu asie fanya ibada au asie muamini Mungu.
Mtu yoyote Yule awe mwarabu,mzungu,mwafrika, mhindi au mchina akichagua kumuabudu Mwenyezi Mungu katika SIKU YA FAIDA NA THAMANI basi atakuwa ni mtu mwenye kupata faida kubwa sana hapa duniani katika kila kitu anacho kifanya. Tazama hata wafanyabiashara wengine wasio kuwa waarabu lakini wanamwabudu Mwenyezi Mungu katikia siku ya FAIDA NA THAMANI.Wote niwafanyabiashara wenye faida kubwa na wenye kumiliki vitu na mali zenye thamani kubwa kubwa.
Tazama vitu wanavyo miliki waarabuvyote ni vyenye thamani kubwa kubwa. Wazungu pamoja na kuwa na uwezo na karama ya kufanya mambo makubwa makubwa lakini hawamiliki vitu vyenye thamani kama waarabu. Wao wanacho jali ni kufanya mambo makubwa makubwa tu lakini sio kumiliki.
Ndio maana unakuta gari limetengenezwa na mzungu.Ilatazama thamani ya gari analo endesha mzungu na thamani ya gari analo endesha mwarabu utaona tofauti. Wakati mzungu akiishi kwa kujibana bana na kuendesha gari lenye thamani ndogo,mwarabu yeye atamiliki garilenye thamani kubwa kubwa kwa sababu anatembea na nguvu ya kiroho ya siku anayo abudu. SIKU YA FAIDA NA THAMANI.
Kama unataka kunufaika na utukufu na utumishi wa majini na malaika wote wanao tawala kuanzia siku ya nuru ( siku ya kwanza ) hadi siku ya kustareheshwa ( siku ya saba ) basi unatakiwa kutenga muda wa kumuabudu Mwenyezi Mungu kila siku ili unufaike na mambo yote hayo.
2. KUBADILISHA SIKU
Kwa utaratibu mpya wa kuhesabu siku ulio wekwa na Lusifa siku mpya inaanza saa sita usiku na kuisha saa sita mchana. ( Kama imekuchanganya hii tazama mambo ya A.M na P.M )
Ikifika saa saba mchana ni siku nyingine hiyo.Huu ni utaratibu uliopotoshwa kutoka katika utaratibu ulio wekwa na Mwenyezi Mungu kwa lengo la kumpoteza mwanadamu.
Kuanza na kumalizika kwa siku ni vitu muhimu sana katika ulimwengu wa kiroho. Ukitaka kujua hili tazama mawio na machweo ya jua,tazama ndege wa porini nyimbo wanazo imba nyakati za asubuhi na sauti wanazo toa nyakati za usiku.
3. KUBADILISHA MIEZI.
Kwa utaratibu wa Mwenyezi Mungu,mwaka mmoja unamiezi kumi na miwili. Lakini kwa utaratibu uliowekwa na Lusifa,mwaka mmoja una miezi kumi na tatu. Ila kwa kutumia maarifa yake amevuruga vuruga siku na masaa na kufanya ionekane kana kwamba mwaka mmoja una miezi kumi na miwili.
Ndio maana ninasema watu wengi hawajui tarehe zao halisi za kuzaliwa wala nyota zao halisi,jambo linalo waweka mbali na mafanikio yao ya kinyota.
Hiyo tarehe unayo amini umezaliwa sio tarehe yako halisi katika ulimwengu wa kiroho. Tarehe yako ya kuzaliwa ina umuhimu mkubwa sana katika ulimwengu wa kiroho. Hii ndio inayo tumika kujua umezaliwa siku gani na nyota yako inatawaliwa ama kutumikiwa na majini/malaika wepi. Hii ndio sababu yetu sisi wanajimu kutumia siku na siku tarehe ya mtu kuzaliwa.
Mwezi mmoja una wiki nne na kila wiki ina siku 7. Kwa hiyo mwezi mmoja unapaswa kuwa na siku 28. Hizo siku 30 au 31 zimetoka wapi ? Tarehe 29,30, na 31 zimetoka wapi ?
Ukipiga hesabu kwa utaratibu uliowekwa na Lusifa utagundua kuwa mwaka mmoja una miezi kumi na tatu ( 13 )
Chukua 365 gawanya kwa 28 unapata 13 . Kwa wenye ufahamu wa kiroho mnajua kuwa namba 13 ni namba ya Lusifa.
Kwa utaratibu wa Mungu,mwaka mmoja kwa wanadamu unapaswa kuwa na siku 336 ambazo ni sawa sawa na 3 + 3 + 6 = 12
Ndio sababu madaktari hospitalini huwa hawahesabu miezi ya mtoto kukaa tumboni. Wao huwa wanahesabu wiki.Kama wewe ni mama ambae umewahi kujifungua mtoto au ni nesi unaefanya kazi hospitalini utakuwa shahidi yangu katika hilo.
Kwa hivyo basi kwa utaratibu huu wa kubadilisha majira na nyakati,watu wengi wanazaliwa wakiwa watupu, wakiwa na wenye kukabiliwa na kiza kuu katika maisha yao ya hapa duniani kwa sababu maisha ya duniani yanaongozwa na nyota na wao wanazaliwa wakiwa hawazijui nyota zao.
Ili kurejesha umiliki wa nyota ya mwanadamu kwa wamiliki wake halisi, Mwenyezi Mungu alishusha Torati kupitia Mussa ambako ndani yake aliweka Amri zake Kumi.
MAMBO YANAYO UA NA KUCHAFUA NYOTA YA MWANADAMU.
Yapo mambo mengi sana yanayo changia kuharibika, kuzimika au kufa kabisa kwa nyota ya mwanadamu. Baadhi ya mambo hayo ni pamoja na uzinzi, tendo la kujamiiana, na kurogwa na wachawi . Na uchawi wa kuharibu, kuzima na kuua nyota upo wa aina nyingi sana. Unaweza kutupiwa majini, kulishwa uchawi, kutegwa urukwe uchawi, kupakwa uchawi au kuchanjiwa uchawi wa kuharibu na kuua nyota yako.
Uchawi wa kuchanja upo wa aina kuu mbili. Aina ya kwanza unachanjwa chale ambazo huwezi kuziona kwa macho ya kawaida na aina ya pili, unachanjwa chale ambazo unaweza kuziona. Hapa unaamka asubuhi au alfajiri na kujikuta umechanjwa chale. Watu wengi wanao chanjwa chale zisizo onekana huwa wanakuwa hawajijui kama wamechanjwa ila kinacho onekana huwa ni matokeo ya kilicho kusudiwa na wachawi .
Unapo chanjwa chale zenye kuonekana maana yake ni kwamba wachawi wamekusudia uone na ujue kwamba wanakufuatilia. Hawa fanyi hivi kwa kukosea bali wanafanya hivi kwa sababu maalumu kabisa ambayo utaifahamu hapo baadae.
Kila aina ya chale huwa ina maana yake . Katika kutafsiri maana ya chale za kichawi huwa tunatazama mambo makuu yafuatayo : Kwanza ni alama ya chale husika, pili ni sehemu ya mwili ambako chale imechanjwa na tatu ni siku ambayo chale imechanjwa.
JINSI YA KURUDISHA NYOTA ILIYO IBWA
Unaweza kurudisha nyota yako kwa kufanya mambo makuu mawili kama ifuatavyo :
MOSI : KUFANYA AGANO NA MAJINI WA KISHEITWANI
Unaweza kurejesha nyota yako kwa kufanya agano la kuunganisha nafsi yako na majini wa kisheitwani. Hawa ni majini wakubwa sana na wana uwezo mkubwa sana wa kurejesha nyota yako na kukufanya kuwa vile unavyo taka kuwa .
Majinihawa wa kisheitwani wanafanya kazi chini ya Ibilisi na ndio waliopewa jukumu la kutawala siku saba za Juma baada ya Ibilisi kuiba nyota ya mwanadamu kupitia Adamu.
Ni majini walio katika daraja kuu kabisa katika ufalme wa kisheitwani . Ni majini wa kifalme wenye nyota ( nafsi hai ) kubwa.
Watakacho kifanya majini hawa ni kuunganisha nyota yako na nyota zao. Kwa hiyo unakuwa unatembelea nyota zao. Inakuwa sio wewe ila ni wao.
Utapata mafanikio makubwa sana na ulimwengu utastaajabishwa kwa mafanikio yako lakini kiuhalisia yanakuwa sio mafanikio yako. Utamiliki kila kitu utakacho kitaka duniani lakini vyote vitakuwa si vyako bali vyao.
Ili kuunganisha nafsi ( nyota ) yako na nafsi ( nyota ) zao majini hawa watahitaji kafara ya damu ya mnyama au kafara kubwa.
Watu wengi wanao onekana kuwa na nyota kubwa wapo katika kundi hili. Wanasafiria nyota za majini hawa wa kisheitwani. Nyota zao zinasafiri katika mkondo wa nyota za majini hawa wa kisheitwani.
Ukiona mtu yoyote Yule,nyota yake ipo juu lakini anafanya mambo ambayo hayaendani na mafundisho ya Mwenyezi Mungu basi maanayake ni kwamba anatumia nyota za majini hawa wa kisheitwani
Hata wale wanaosema mambo yao yamebadilika na kuwa mazuri baada ya kufanya mapenzi na mwanamke Fulani, ni kwamba nyota ya mwanamke huyo inakuwa inakaliwa na majini hawa wa kisheitwani ambao nguvu yao ni kubwa sana sema wapo upande wa adui.
Kuunganisha nyota ya mtu na majini hawawa kisheitwani hufanyika kwa kafara ya damu ya mnyama au kafara kubwa pamoja na maagano mengine makubwa makubwa.
Baadhi ya majini walio katika kundi hili hukalia madini na mawe au vito ambavyo hutumika kutengeneza pete maalumu za kijini. Mtu atakae vaa pete hizo basi anakuwa ameunganisha nafsi yake na nafsi ya majini hao kupitia pete hizo.
Njia za kumuunganisha mwanadamu na majini hawa wa kisheitwani zipo nyingi sana nyingine nitazielezea kwenye kitabu.
Njia ya Pili : KUTUMIA MITI NA MIMEA INAYO KALIWA NA KUTAWALIWA NA MAJINI NA MALAIKA WANAO TAWALA SIKU SABA ZA WIKI.
Unaweza kurejesha nyota yako mwenyewe kwa kutumia miti na mimea inayokaliwa na majini na malaika wanao tawala siku saba za Juma.
Unacho takiwa kufanya ni kwanza ufahamu ulizaliwa siku gani na muda gani. ( ULIZALIWA USIKU AU MCHANA )
Ukisha fahamu siku na muda ulio zaliwa kitakacho fuata sasa utatakiwa kufahamu ni majini na malaikawepi wanatawala siku na muda ulio zaliwa.
Na ukisha fahamu ni majini na malaika wepi wanao tawala siku na muda uliozaliwa, unatakiwa kufahamu miti na mimea ambayo inakaliwa na majini na malaika hao.
Ukisha fahamu kuhusu miti na mimea inayo kaliwa na majini na malaika hao, unatakiwa ufahamu kuhusu dua unayo takiwa kufanya ili kuunganisha nguvu ama nyota ya majini wanao kalia miti au mimea hiyo na nyota yako.
Kinacho fanyika hapo ni kuwaamuru / kuwaomba majini na malaika hao watukufu kuhamisha makazi yao kutoka kwenye miti wanayo ikalia na kuhamishia kwenye nafsi yako ili kuunganisha nyota yako na nyota zao. Na utakapo fanikiwa kufanya jambo hili basi nyota yako itarejeshwa na stori ya maisha yako iliyo andikwa kwenye nyota yako na Mwenyezi Mungu itatimia.
Kumbuka kuwa Mwenyezi Mungu alimpa mwanadamu mamlaka ya kuvitiisha vitu vyote vilivyomo ndani yake vinavyo onekana na visivyo onekana. Na moja kati ya vitu hivyo ni pamoja na mimea na miti inakaliwa na majini na malaika. Majini na malaika wanao ishi ndani ya mimea na miti hiyo bado wanamtambua mwanadamu kama bosi wao au kama mtawala wao wanae paswa kumtumikia. Ukiijua mimea na miti inayo endana na siku na muda ulio zaliwa halafu ukajua kufanya dua ya kuwaombaau kuwaamuru majini na malaika hao kuunganisha nguvu yao na nguvu ya nyota yako basi nyota yako itarejea na kuwa juu kama Mwenyezi Mungu alivyo kusudia.
Ndani ya mbegu za miti na mimea yote unayo ijua kimeandikwa kila kitu kuhusu maisha ya mwanadamu na mafanikio yake. Unacho takiwa kufahamu ni kujua ni mimea ipi inaendana na nyota yako na ndani ya mimea hiyo kimeandikwa kitu gani kuhusu maisha yako.
Hata hivyo ipo mimea ambayo ndani yake yameandikwa mambo yanayo kinzana na nyota ya mwanadamu. Mimea hii haipaswi kutumiwa na mwanadamu kwa namna yoyote ile. Mfano wa miti na mimea iliyo katika kundi hili ni ule mti uliokuwa katika bustani ya Eden ambao Mwenyezi Mungu alimzuia Adam kutumia matunda yake.
Miti hii inakaliwa na majini wa kisheitwani. Ndani ya mbegu za miti hii yameandikwa na kunenwa mambo yaliyo kinyume na mafanikio ya nyota ya mwanadamu.
Wachawi wana elimu kubwa sana kuhusu miti hii. Ni miti hii hii ndio ambayo wachawi wanaitumia kutengeneza magonjwa na maradhi mbalimbali ya kichawi ili kuwatesa wanadamu.
Kwa kutumia elimu kuhusu miti hiyo wachawi wanaweza kutengeneza kila aina ya ugonjwa na kumsababishia mtu ugonjwa huo.
Wachawi hushirikiana na majini wanao kalia miti hii kuwaroga na kuwatesa wanadamu kwa kuwasababishia matatizo mbalimbali ya kimaisha kama vile nuksi, mabalaa na mikosi pamoja na magonjwa ya kichawi kama vile kiharusi (kupooza), ugumba, uziwi, ukichaa, kifafa na hata nguvu za kiume.
Kwa mfano katika kutengeneza maradhi ya nguvu za kiume wachawi huwa wanatumia majini wa kisheitwani watatu ambao wanaishi kwenye mitatu tofauti ya porini. Majini hawa watatu wa kisheitwani wanapo tumwa kwa mwanaume alie kusudiwa, huelekezwa kwenda kukaa kwenye sehemu tatu katika mwili wa mwanadamu. Majini hawa wa kisheitwani wakisha weka makazi hayo kwenye sehemu hizo kuu tatu ndani ya mwili wa mwanadamu humsababishia mwanadamu huyo maradhi ya nguvu za kiume na hufanya hivyo kwa kutengeneza sababu za kumuhalalishia mtu huyo maradhi ya nguvu za kiume.
Kwa ufupi wachawi wana maarifa makubwa sana juu ya miti yenye kukaliwa na masheitwani wabaya na namna inavyo tumika kuwatesa wanadamu.
Unacho takiwa kufanya ni kuifahamu miti inayo kaliwa na majini na malaika wazuri ambayo itakusaidia kujilinda, kujikinga na kupambana dhidi ya shari hii ya wachawi.
Miti hii ipo mingi sana na utapata kuifahamu miti yote pamoja na shari zote za kichawi itakayo kukinga nazo.
Kwa mfano Kuna mti mmoja (jina lake linahifadhiwa ) unapatikana porini, mti huo ukikomaa, urefu wake hauzidi wa mtoto wa miaka saba, una magamba kwa mbali na rangi yake ni nyeupe
Mti huu ukikauka ukausaga unga wake huwa mweupe kama kama mti wenyewe.
Ukichukua unga wa mti huu halafu ukajipaka usoni unakuwa na uwezo wa kuwaona wachawi.
Ukijipaka unga wa mti huu usoni halafu ukatembea mtaani wakati wa mchana, unaweza kuona mambo yote yanayofanyika katika siri kubwa kama vile wachawi wakiwa wanawanga au wanafanya shughuli zao wakiwa uchi.
Dawa hii itakupa pia uwezo wa kuwaona misukule.
Vilevile mti huu una uwezo wa kukimbiza nyoka mfano ukiwa na kipande cha mti huu mfukoni halafu ukawa unatembea, kama mbele yako kuna nyoka atakimbia kabla hujafika.
Hata ukikaa mahali kama kuna nyoka hawezi kukaa hapo, atakimbia tu.
JIANDAE KUSOMA KITABU CHANGU KINACHOITWA “ MAMBO TISA YANAYO UNDA NYOTA YA MWANADAMU NA UHUSIANO KATI YA NYOTA YA MTU NA MAFANIKIO YAKE KATIKA MAISHA “
Kitabu hiki kitatoka hivi karibuni na utafahamishwa kitakapo kuwa mtaani.
Ndani ya kitabu hiki utapata kuyafahamu kwa kina mambo yote yaliyo elezewa kwenye makala haya.
Pamoja na mambo mengine mengi, ndani ya kitabu hiki cha kipekee kabisa, utapata kufahamu kuhusu mambo yafuatayo :
1. MAMBO TISA YANAYO UNDA NYOTA YA MTU.
2. MITI YOTE INAYO TAWALA SIKU ZOTE SABA ZA JUMA KUANZIA SIKU NURU ( SIKU YA KWANZA ) HADI SIKU YA KUSTAREHESHWA (SIKU YA SABA ). UTAPATA KUFAHAMU NI MITI GANI HUTAWALA USIKU NA MITI GANI HUTAWALA MCHANA KATIKA SIKU HIZO SABA ZA JUMA.
3. MAJINI NA MALAIKA WANAO TAWALA SIKU ZOTE SABA ZA JUMA KUANZIA SIKU YA NURU ( SIKU YA KWANZA ) HADI SIKU YA KUSTAREHESHWA ( SIKU YA SABA )
4. MAJINI NA MALAIKA WANAO TAWALA KILA MTI NA KILA MMEA KATIKA KILA SIKU YA JUMA KUANZIA SIKU YA KWANZA HADI SIKU YA SABA.
5. DUA ZIPI ZA KUOMBA KATIKA KILA SIKU YA JUMA KUANZIA SIKU YA KWANZA HADI SIKU YA SABA.
6. DUA ZA KUOMBA ILI KUUNGANISHA NYOTA YAKO NA NYOTA ZA MAJINI NA MALAIKA WANAO TAWALA KATIKA KILA SIKU KUPITIA MIMEA WANAYO IKALIA.
7. UHUSIANO KATI YA NYOTA YAKO ( NYOTA YA SIKU ULIYOZALIWA ) NA MAFANIKIO KATIKA MAISHA YAKO.
8. UTAFAHAMU KUJUA NAMNA YA KUSOMA NYOTA YAKO MWENYEWE KWA KUTAZAMA SIKU ULIYO ZALIWA.
9. UTAZIJUA TABIA ,SIFA NA NGUVU HALISI YA NYOTA YAKO HALISI AMBAYO INAJULIKANA KWA KUTAZAMA SIKU ULIYO ZALIWA.
10. JINSI UZINZI NAKUJAMIIANA VINAVYO WEZA KUSABABISHA KUHARIBU, KUZIMA AU KUUA NYOTA YAKO NA JINSI YA KUJIEPUSHA.
11. JINSI TENDO LA NDOA LINAVYO WEZA KUTUMIKA KUPANDISHA NYOTA YAKO.
12. MBINU ZOTE WANAZO TUMIA WACHAWI KATIKA KUHARIBU NA KUZIMA NYOTA ZA WATU.
13. JINSI YA KUSOMA NA KUTAFSIRI CHALE ZA WACHAWI NA NAMNA YA KUJIKINGA NA KUJIEPUSHA NA MADHARA YAKE.
14. SEHEMU TATU NDANI YA MWILI WA MWANADAMU AMBAZO HUWEKWA MAJINI WA KISHEITWANI KWA AJILI YA KUWAHALALISHIA WANAUME MARADHI YA NGUVU ZA KIUME
15. MAABARA ZA KICHAWI : JINSI WACHAWI WANAVYO TENGENEZA MAGONJWA MBALIMBALI YA KICHAWI KUANZIA KIHARUSI, KIFAFA, UCHIZI, UZIWI, UGOMBA, UKOJOZI, UKHANITHI NAKADHALIKA.
16. MITI NA MIMEA MBALIMBALI INAYO TUMIWA NA WACHAWI KUWATESA WATU, JINSI WANAVYO ITUMIA NA JINSI UNAVYO WEZA KUJIKINGA NA SHARI HIYO.
17. MITI MBALIMBALI INAYO TIBU NA KUPONYESHA MARADHI YOOTE YANAYO MSUMBUA MWANADAMU KAMA VILE : UDHAIFU KATIKA NGUVU ZA KIUME, KIFAFA, KIHARUS,I, KUPANDISHA CD 4, KISUKARI, VIDONDA VYA TUMBO, BAWAZIRI, UGUMBA NAKADHALIKA.
18. MITI MAALUMU YA KITABIBU INAYO PATIKANA KATIKA KILA WILAYA YA TANZANIA BARA NA VISIWANI : Katika utabibu wa jadi, karibu katika kila wilaya ya Tanzania bara na visiwani inasifika kwa kutoa dawa moja yenye uwezo wa kutibu kwa ufasaha na usahihi kabisa maradhi Fulani yanayo mkabili mwanadamu. Mfano katika wilaya ya kisarawe kuna kijiji kimoja ambako unapatikana mme mmoja unaoota kwa kutambaa chini. Mmea huo ni tabia ya uhakika na sahihi kabisa kwa watu wanao taka kupandisha CD4. Mmea huo unapandisha CD4 kwa namna ya kipekee sana. Katika tafiti zangu za kitabibu mmea huu kwa Tanzania bara nimeuona katika kijiji hicho tu na huko visiwani Zanzibar kwenye msitu mmoja unao patikana katika kisiwa cha Tumbatu.
Pia huko wilayani Handeni Tanga kuna mti mmoja ambao mimi ninautambua kama mti pekee wenye uwezo mkubwa sana wa kuwasadia watu wanao taka kupungua mwili. Mti huu unapukutisha mwili kwa kasi ya ajabu sana. Kwa umbo mti huu ni mwembamba sana na wachawi walikuwa wanautumia kuwasababishia watu maradhi ya kukonda sana na kuwafanya waonekane kama waathirika wa Ukimwi kwa kuwanywesha kimiminika cha mti huu kupita kikomo bila mhusika kujua. Mmea huu unatumika mara mbili tu kwa wiki mbili tu. Yaani unaanza siku ya kwanza unachemsha unakunywa robo glasi, halafu baada ya wiki moja unatumia tena robo glasi. Utapungua sana mwili.
Katika ulimwengu wa kitabibu tuna imani moja, kwamba unapotaka kutumia mmea au mti Fulani kwa ajili ya tiba maana yake ni kwamba unakuwa unakula kile ambacho mmea au mti huo unakila. Ndio maana huwezi kuwa mwembamba kwa kutumia mti ambao sio mwembamba. Mti unakupa kile unachokila wenyewe.
19. UCHAWI NA ULOZI UNAO SIFIKA KUTOKA KATIKA KILA KONA YA TANZANIA NA NCHI JIRANI PAMOJA NA NAMNA YA KUJIKINGA NAO.
20. UCHAWI NA ULOZI WA MAPENZI WA AINA ZOTE, JINSI UNAVYO TENGENEZWA, MADHARA YAKE , JINSI UNAVYO WEZA KUMZINDUA MTU ALIE LISHWA AU KUTUPIWA UCHAWI NA ULOZI WA MAPENZI.
21. PETE MBALIMBALI ZA KIJINI NA MATUMIZI YAKE . FAIDA NA HASARA ZAKE.
22. UTAJIRI WA KUKU KUDONOA MCHELE
23. MISUKULE WA KILA AINA NA JINSI YA KUJIZUIA USICHUKULIWE MSUKULE.
PAMOJA NA MAMBO MENGINE MENGI AMBAYO NITAYABAINISHA .
Makala haya yameandaliwa na DOKTA. MUNGWA KABILI. ANAPATIKANA KWA SIMU NAMBA 0744 000 473.
KUPATA UPDATES KUHUSU KITABU HIKI, TEMBELEA KILA SIKU :
www.mungwakabhili.blogspot.com
PIA UNAWEZA KUNIPATA KWENYE MTANDAO WA FACEBOOK KUPITIA :www.facebook.com/MungwaKabhili