Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Pete Za Masonic Immoring Hazina Uhusiano Wowote Na Kuabudu Masheitwani

$
0
0
Imeandikwa na: Dokta  Mungwa  Kabili -0744  000  473.
 Maneno yaliyo  zagaa   mitaani  kwamba  eti   watu  wanao vaa  pete za  Masonic  Immoring  ni  waabudu  sheitwani  hayana  ukweli  wowote.

Ikitokea mtu  maarufu  ameonekana  akiwa  amevaa  pete  hizo  basi  moja  kwa  moja  watu  wataanza kumuhusisha  na  habari  za  kuabudu  masheitwani.

Maneno  hayo  ni  uzushi  mtupu  na ambao  hauna  mashiko  yoyote katika  ulimwengu  wa kiroho.

Watu  wanao  eneza  uzushi  huo  ni  watu wenye  ufahamu  mdogo  sana  kuhusu  imani za jadi, imani  za  siri, imani za  kale  na  ulimwengu  usio  onekana  ( ulimwengu   wa  kiroho )  kwa  ujumla.

Pete  za  Masonic  Immoring  ni  pete  ambazo  zimekuwa  zikitumiwa  na  wanadamu  toka  enzi  na  enzi .

Kwa  wewe  ambae  bado  una shikilia  imani kwamba  Masonic  Immoring  ni  pete  za  kisheitwani, nakushauri  ufanye  utafiti  wako  vizuri.

Ukifanya  utafiti  wako  vizuri  utagundua  kwamba  pete  hizi  zilikuwa  zikivaliwa  hadi  na  wafalme  wenye  kuheshimika sana   katika  vitabu  vyote  vitakatifu.

Watu  wanao  dai kwamba  wavaaji  wa  pete  za  Masonic  Immoring  ni  waabudu  shetani, wana toa  hoja  dhaifu  kwamba  watu  wote  wanao  jihusisha  na  uvaaji  wa pete  za  Masonic Immoring  huwa  ni watu  wenye  mafanikio makubwa  sana  katika  maisha  ikilinganishwa  na  watu  wanao  fanya  kitu  kile  kile  kinacho  fanywa  na  watu  wenye  kuvaa pete hizo za  Masonic  Immoring.

 Kwamba  kama  ni  mwanamuziki  basi  anakuwa  juu  sana  kuliko  wana  muziki  wenzake  wanao  fanya  aina  ya  muziki  ule  ule  anao  ufanya  yeye, kama  ni  mfanya  biashara  basi  biashara  yake  inapata  mafanikio  makubwa  sana  kuliko  wafanya  biashara  wenzake  ambao  wanafanya  biashara  kama  ile  ile  anayo  ifanya . Mifano  ipo  mingi  sana.

Hata  hivyo  hoja  hii  ni dhaifu  sana  kwa  sababu  mali  na  mafanikio  vyote  vinatoka  kwa  Mungu  kwa sababu  yeye  ndio  ameumba   Dhahabu, Almasi,Fedha  na vitu  vyote  vinavyo  onekana  na  visivyo  onekana.

Ina  maana  gani  kuwapa  utukufu  masheitwani  kwa  kazi  ambayo imefanywa  na  Mungu mwenyewe. Kwani  ina  maana  Mungu  hawezi  kumfanya  mtu  awe  tajiri au  apate  mafanikio ?

SIRI  YA   PETE   MASONIC  IMMORING  NI  MOJA  TU :  Pete  za  Masonic  Immoring zimetengezwa  kwa  madini  na  vito  vinavyo  kaliwa  na  majini  wazito  wazito, wajini  wakubwa, majini watukufu na  walio  katika daraja za  juu  kabisa katika  ufalme  wa  kijini, majini  wa  kifalme.

Unapo  ivaa  pete  ya Masonic  Immoring unakuwa  umeunganisha  nyota  yako  na  nguvu ya  majini  wanao  kalia madini ,mawe na  vito  vilivyo  tumika  kutengeneza  Masonic  Immoring.

Hivyo  unapokuwa  umevaa  pete  ya  Masonic  Immoring unakuwa  umeingia  katika  agano  rasmi  la  kiroho  la  kuunganisha  nafsi/nyota  yako  na  nguvu  ya  majini  hao kwa  kuwaingiza  majini  hao  katika  mfumo  wa  nyota  yako  na  maisha  yako  kwa  ujumla.

Nyota yako  inaanza  kusafiri  kwa  kufuata  kasi  ya   mkondo  wa  nyota  za  majini  hawa  wa  kifalme kwa  sababu  tayari  nyota  yako  inakuwa  imeunganishwa  na  nyota  ya  majini  hawa na  kuwa  kitu  kimoja.

Katika  hili  la  nyota  yako  kusafiri  katika  mkondo  wa  nyota  ya  majini  hawa  watukufu  mfanano  wake  ni  rahisi  sana.  Yani  ni  kama  vile wewe  kijana  ambae  umezaliwa  na  kukulia  kijijini  kwenye  maisha  ya  tabu halafu  ghafla  ukapata  bahati  ya  kuajiriwa  na  mwanamuziki  mkubwa  anae  safari  sana  katika  nchi  mbalimbali  duniani .

Nchi  ambazo  hujawahi  kuota  kufika.  Utaanza  kusafiri  na  mwanamuziki huyo  katika  nchi  hizo.

 Kilicho  fanya  wewe  ufike  katika  nchi  hizo  ni  nyota  ya  mwanamuziki  huyo.

 Kwamba  kwa  sababu  yeye  ni  mwanamuziki mkubwa  na  anae  pata  mialiko  ya  kutumbuiza  kwenye  nchi  mbalimbali,  na  kwa  sababu  wewe  labda  umepata  kazi  ya  kuwa  mpiga  picha  wake, au  mwandishi  wake, basi  utakuwa na  wewe  unasafiri  katika  nchi  hizo  na  mwanamuziki  huyo.

Kwa  lugha  nyingine  utakuwa  una  safiria  nyota  ya  mwanamuziki  huyo.

Vivyo    kuhusu  pete  ya  Masonic  Immoring. Unapo  vaa  pete  ya  Masonic  Immoring  basi  unaanza  kusafiria  nyota  ya  majini  wanaokaa  kwenye  madini, mawe  na  vito  vilivyo  tumika  kutengeneza  Immo  Ring.

Kiuhalisia kabisa  wewe hukustahili  kusafiri  katika  nchi  hizo  lakini  umestahilishishwa  kwa  sababu  ya  agano  lako  na  mtu  anae  stahili kusafiri  katika  nchi  hizo.

Majini  hawa  wana  sifa  moja  kuu, kwanza  huwa  hawakai  na  kitu  chochote  kichafu  kama  majini  wa  baharini, kwa  hiyo  kama  utakuwa  na  kitu  chochote  kichafu  ndani  ya  mwili  wako,uwe  umetupiwa  uchawi,  majini /mapepo wachafu/mizimu mibaya, kijicho  au  kifungo  chochote  kile  cha  kichawi ndani  ya  mwili  wako, vitu  vyote  hivyo  vitafukuzwa  ndani  ya  mwili  wako  kwa  sababu  majini  wanao  kaa  kwenye  vito,madini na mawe  yaliyo tumika  kutengeneza  Masonic  Immoring   huwa  hawakai  na  kitu  kichafu.

Majini  hawa  watafukuza  shari zote  ndani  ya  mwili  wako  na kuvuta  heri  zote katika  maisha  yako  sambamba  na  kuzuia  shari yoyote  ile iliyo elekezwa  kuja  kwenye  mwili  wako.

Majini  wanao  kaa ndani  ya  vito na  madini  yaliyo  tumika  kutengeneza  Masonic  Immoring hawapendi  uchafu  na  hawakai  na  vitu  vichafu.

Ndio  maana  basi  mtu  anae  vaa  pete  hii, huwa  haruhusiwi  kunywa  pombe  huku  pete  ikiwa  kidoleni,  au  pombe  ikiwa  mwilini.

Haruhusiwi  kufanya  zinaa  huku  akiwa  ameivaa  pete  hii  tukufu  na  haruhusiwi  kujisafisha   baada  ya  kumaliza  haja  kubwa   huku  pete  ikiwa  kidoleni  kwa  sababu  pete  hii  huvaliwa  mkono  wa  kushoto.

Ilhali  mwanamke  haruhusiwi  kuvaa  pete  hii  akiwa  kwenye  siku zake.

Na  mtu yoyote  Yule  awe  mwanamke  au  mwanaume  baada  ya  jimai  anatakiwa  kukoga  kwanza  kabla  ya  kuivaa  tena  pete  hii.

Pete  zote  za  Immoring  zina alama  kama  inavyo  onekana  hapo  juu, kwa  hiyo kwa  mtu  yoyote  Yule  atakae  hitaji  pete  ya  Masonic Immoring , kitu  cha  kwanza  anacho  takiwa  kukitazama  ni  alama ya  pete  hiyo  kama inavyo  onekana  pichani.

Na  kama  unahitaji  pete  ya  Masonic  Immoring, basi  wasiliana  na  Dokta  Mungwa  Kabili  kwa  simu  namba  0744  000  473.

Watakaohujumu Miundombinu Tanesco Kukiona

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka Watanzania kuilinda na kuitunza miundombinu ya Shirika la Umeme nchini (Tanesco), huku akiagiza mamlaka husika kuwashughulikia watakaojihusisha na uharibifu wa miundombinu hiyo.

Majaliwa ameyasema hayo jana Mei 21, alipokuwa akizindua uunganishaji wa gridi ya taifa kwa Mkoa wa Lindi na Mtwara iliyofanyika katika Kituo cha kupozea umeme cha Maumbika mkoani hapa.

“Wapo baadhi ya watu wasio na nia njema na serikali wanaharibu miundombinu kwa kung’oa vyuma na kuuza kama vyuma chakavu, hawa ni wahujumu uchumi.

“Naagiza mamlaka zinazohusika kufanya ukaguzi kila eneo linalouza au kununua chuma chakavu kubaini kama kuna miundombinu ya Tanesco na endapo mtaikuta wahusika wawajibishwe kwa mujibu wa sheria,” alisema Majaliwa.

Pamoja na mambo mengine, Waziri Majaliwa amesema kuwa mkakati uliopo sasa ni kuboresha miundombinu ya zamani na kujenga miradi mipya ya umeme ili kuzalisha umeme wa kutosha ili kuwafikia wananchi wengi.

Je Wajua Saa Zenye Moyo Kama Wa Binadamu

$
0
0
NDio najua bado kichwani mwako unajiuliza saa zenye moyo wa binadamu kivipi? basi mwandishi wa makala hii ndo kazi yangu kukupa majibu na elimu kuhusu saa zenye moyo...


Tuanzie hapa msomaji saa zenye moyo kwa lugha sahihi ya kiswahili ni saa ambazo hazitumii battery yaani kiingereza automatic watch/mechanical watches....katika ulimwengu huu wa saa basi saa hizi ndo zilikuwa za kwanza kugunduliwa saa hizi ziligunduliwa na peter henlein wa mji wa nuremberg ujerumani....wakati saa za mabattery ziligunduliwa mwaka 1955 yaani quartz watch huko japani ..... baada ya historia fupi hiyo ngoja sasa tuone uchawi wa mzungu huyu peter henlein alifanyaje saa hizi hazitumii battery tutamia lugha nyepesi kila mtu asomae makala hii aelewe na video nitaweka
 
1.SAA HIZI HUPATA NGUVU UNAPOTIKISA MKONO WAKO
chazo kikubwa cha nguvu za saa hizi huwa mtu alivaa saa hii akiwa anatembea anavyotikisa mkono basi saa hizi kama unajua wana fikia hapa wataelewa saa hii huchukua motion energy na kuifadhi nguvu hii kwenye spiringi kuu (main spring)yaani saa hii uko zako mishe mishe zako unatembea ..na yenyewe inakuwa bize inachaji jinsi unavyotisa mkono.....
 
2. INA GIA
mi ndo maana nasemaga wazungu bwana kwenye ugunduzi ni watu hatari saa hizi bwana zina mfumo wa gia ...gia hizi bwana zinafanya kazi kwa waledi wa hali ya juu yaani kubadilisha nguvu ya mtetemeko wa mkono wako na kuziifadhi kwenye spiring kuu yaaani huu sasa NDO HUITWA MOYO wa saa yaani ukizima na saa inasimama kana kwamba binadamu moyo ukizima nae anakufaaa....lakini saa hizi moyo huu wa saa ni kwamba ukitisaa tu mkono na moyo wa saa unaanza kufanya kazi ...ngoja niwekee mfano saa ya kampuni t winner ambayo nayo ni moja ya SAA AMBAYO INA MOYO
basi ndugu msomaji hii kwenye video hapo juu ni moja kati ya mfano saa nyingi ambazo hazina mabattery ..kama utakuwa ni mdadisi wa mambo utakuwa umeangalia vizuri umeona kama kitu kama cha mvirigo kinatikisika kwa spidi basi ule ndo moyo sasa wa saa
 
3.HAZIINGII MAJI
basi saa hizi bwana ili kutunza ule moyo wake yaani springi kuu usichoke kufanya kazi hizi saa bwana huwa ni rafiki na maji yaani ukupita mvuani sawa tu hazina shida .....pia saa hizi wafanyakazi hasa wa POSTA huzipenda sana koz zinaongezea muonekano hata mimi hapa kama mwandishi wa habari hii saaa ni ninayo ina skeleton mechanical watch bofya jina hapo kuiona unaweza nunua hapo pia niliko nunua mimi mwandishi wako
 
4.UTAPATA WAPI SAA HIZI NA KWA SIFA ZIPI ILI UPATE ORIGINAL
ili upate original sifa ya kuangalia ni muda gani springi kuu ina uwezo wa kutunza chaji muda mara nyingi huwa ni masaa 48 bila kuguswa mara nyingi watu huagiza kwenye mitandao kama AMAZON wa marekani au pia POSTA kuna maduka huuza saa hizi za automatic pia kuna njia nyepesi kuna HUU mtandao wa daresalaamshop.com ambao personally nakurecommend ukanunue hawa unagiza na unaletewa ulipo TANZANIA nzima hawa majamaa huwa ni original na utalipia mzigo ukifika kitu umekiona usikose utamu wa saa hizi pia ndugu msomaji kuna link chini hapo bofya buy now kuweka order,,, mpaka siku nyingine kwenye makala zingine ASANTE
 
IMEANDIKWA NA
robnson kayaula kutoka twigaz news

Wabunge Wa CUF Wamfagilia Rais Magufuli ....Wasifu Kasi Yake Na Waziri Mkuu Ya Uletaji Maendeleo

$
0
0
WABUNGE watatu kutoka Chama cha Wananchi (CUF) mikoa ya Lindi na Mtwara wamepongeza kasi ya utendaji kazi ya Rais John Pombe Magufuli katika kutatua kero za wananchi wa mikoa hiyo.

Wabunge hao Bw. Selemani Said Bungara (Kilwa Kusini), Bw. Zuberi Mohammed Kuchauka (Liwale) na Bw. Maftaha Abdallah Nachuma (Mtwara Mjini) walitoa pongezi hizo jana, (Jumatatu, Mei 21, 2018) wakati walipopewa nafasi ya kusalimia wananchi kwenye mikutano ya hadhara ambayo Waziri Mkuu alihutubia.

Akiwa wilayani Lindi, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kuzindua kituo cha kuunganisha umeme wa gridi ya Taifa katika kijiji cha Mahumbika, aliwapa fursa wabunge wote alioambatana nao katika ziara hiyo maalum kwa ajili ya uzinduzi wa miundombinu ya nishati kwa mikoa ya Kusini.

Akizungumza na wananchi na viongozi wa taasisi mbalimbali mkoani humo waliohudhuria uzinduzi huo, Mbunge wa Kilwa Kusini, Bw. Bungara ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wabunge wanaotoka Mkoa wa Lindi alisema analishukuru Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuisimamia vizuri Serikali ya CCM.

“Faida ya demokrasia ya vyama vingi ni kwamba CCM bila CUF, CCM hakuna na CUF bila CCM, kama ambavyo hakuna Simba bila Yanga wala hakuna Yanga bila Simba. Tuwe kitu kimoja tu, Kusini kwanza, vyama baadaye!” alisisitiza.

Alitumia fursa hiyo kumpongeza Waziri Mkuu kwa juhudi zake za kuwaunganisha wabunge wa mikoa ya Kusini bila kuwabagua au kujali itikadi zao.

Naye Mbunge wa Liwale, Bw. Kuchauka alisema: “Niwapongeze wewe Waziri Mkuu pamoja na Mheshimiwa Rais Magufuli kwa yale ambayo mnayasimamia na mnaamini kwamba yataleta ukombozi kwa wananchi wa Tanzania. Lazima nikiri kwamba wakati mnazindua sera ya uchumi wa viwanda, nilikuwa siamini katika hiyo sera yenu kwa sababu niliona ni moja ya mbinu zenu za kututenga sisi watu wa mikoa ya Kusini.”

“Niliona hivyo kwa sababu nilijiuliza unawezaje kuwa na uchumi wa viwanda wakati huna nishati ya uhakika ya umeme? Sasa nimeona mwanga kwamba mikoa ya Kusini nayo inaweza kushiriki kwenye uchumi wa viwanda,” alisema huku akishangiliwa.

Alisema hivi sasa hakuna asiyeona mambo yanayotekelezwa na Serikali ya awamu ya tano kwani dunia yote imekuwa kama kijiji na lolote linalofanywa na Mhe. Rais au Waziri Mkuu hakuna asiyejua. “Lolote analolifanya Mheshimiwa Rais au wewe Waziri Mkuu Watanzania wote watalijua, hakuna asiyeliona. Hivi sasa hakuna haja ya kubishana nani kafanya nini, jambo kubwa ni kuungana na tuangalie Tanzania yetu. Vyama vyote baadaye, Kusini kwanza,” alisisitiza.

Kwa upande wake, Mbunge wa Mtwara Mjini, Bw. Maftaha alisema mwaka 2006 baada ya kuhitimu kidato cha sita, alipangiwa afanye mafunzo ya ualimu kwa vitendo katika shule ya sekondari Mingoyo, eneo la Mnazi Mmoja lakini alitafuta nyumba ya kuishi yenye umeme hakupata.

“Wakati ule nyumba zenye umeme zilikuwa hazizidi hata 10, na kulikuwa na simba na wadudu wa kila aina. Leo nafarijika kuona kwa kasi ya ajabu, ninyi viongozi tuliowapa dhamana, mnatumia rasilmali za nchi hii, mnasambaza umeme kwa wananchi wa mikoa ya Kusini, na pale Mnazi Mmoja leo hii, umeme siyo tatizo tena.”

Wabunge wengine waliofuatana na Waziri Mkuu ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti na Mbunge wa Mtwara Vijijini, Bibi Hawa Ghasia; Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, Bi. Hamida Mohammed Abdallah (Viti Maalum). Mbunge wa Nachingwea, Bw. Hassan Elias Masala, Mbunge wa Nanyamba, Bw. Abdallah Dadi Chikota.

Waziri Mkuu alizuru pia mkoa wa Mtwara na kukagua ujenzi wa bandari, ukarabati wa mabomba ya kupokelea mafuta, matenki ya kuhifadhi mafuta, kuzindua upanuzi wa kituo cha kufua umeme kwa kutumia gesi asilia na kuzungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa bandari.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Ripoti ya Ufisadi Mali za CCM Yatua kwa Rais Magufuli

$
0
0
Tume ya kuhakiki mali za Chama Cha Mapinduzi (CCM), iliyoundwa na Rais John Magufuli, imebaini madudu ukiwamo utapeli na usimamizi mbaya wa mali hizo.

Kamati hiyo iliyoundwa na Rais Magufuli kukagua mali za chama hicho, imefanya kazi hiyo kwa miezi mitano ambapo imekusanya taarifa, kuhakiki na kuchambua taarifa na nyaraka zenye maelezo kuhusu idadi, aina na hali ya mali zinazomilikiwa na kusimamiwa na chama hicho.

Akikabidhi ripoti hiyo kwa Rais John Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM, Mwenyekiti wa Tume hiyo, Dk. Bashiru Ally, amesema tume yake pia ilibaini usimamizi mbovu wa mali za chama.

Akielezea namna tume hiyo ilivyofanya kazi, Dk. Bashiru amesema pamoja na mambo mengine, tume iliangalia vyanzo vya udhaifu wa mifumo na taratibu za usimamizi wa mali, imekusanya ushauri mbalimbali na kutoa mapendekezo ya mikakati na ushauri wa kusimamia mali za chama.

Katika ripoti hiyo, Dk. Bashiru ameeleza tume imebaini uwepo wa upotevu mkubwa wa mali za chama uliosababishwa na mikataba mibovu, ubadhirifu, wizi, usimamizi mbaya wa mali, utapeli na ukosefu wa maadili katika uendeshaji wa miradi ya chama.

“Uhakiki huo umefanyika kwa kutembelea maeneo yenye mali za chama, kuwahoji watu mbalimbali wakiwamo viongozi waliohusishwa na mali zilizokuwa zikihakikiwa, upitiaji wa nyaraka na kufuatilia uhalisia katika ofisi za mamlaka husika, kufanya uchambuzi wa taarifa na kutoa mapendekezo,” amesema.

Kwa upande wake Rais Magufuli ameipongeza tume hiyo kwa kazi kubwa iliyoifanya na amesema ripoti hiyo itawasilishwa katika vikao vya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya CCM kwa ajili ya kufanyiwa uamuzi.

“Nilipokuwa nateua tume hii, nilikuwa najua ugumu wa kazi, nilikuwa najua kuwa mtapata shida kwenda kuwahoji watu licha ya kwamba niliwapa uhuru wa kumhoji mtu yeyote na mmefanya kazi nzuri sana, kilichobaki sasa ni kuifanyia kazi” amesema Rais Magufuli.

Viongozi Wawili CHADEMA Wavuliwa Uanachama

$
0
0
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema, Patrick Ole Sosopi, ametangaza kuwafuta uanachama wanachama wawili wa chama hicho.

Waliofutwa uanachana ni pamoja na aliyekua Naibu Katibu Mkuu Bara, Getrude Ndibalema na Mwenyekiti wa Bavicha mkoa wa Kilimanjaro, Dickson Kibona.

Akizungumza jana Mei 21, katika mkutano na waandishi wa habari jijini Arusha, Ole Sosopi alisema kwamba uamuzi huo umekuja baada ya kufuata taratibu zote za kuwahoji kupitia tume iliyoundwa.

Alisema viongozi hao wamehojiwa baada ya kuwepo tuhuma za usaliti ambalo ni kosa kubwa kwenye chama hicho.

Sosopi amesema Bavicha imeridhia kuwaondoa wanachama hao baada ya kujiridhisha kwa makosa waliyoyafanya.

Bingwa Wa Magonjwa Yote Sugu Yanayosumbua Kama Vile Pumu, Vidonda Vya Tumbo, Busha, Nguvu Za Kiume, Kisukari,

$
0
0
BABU MADUHU NI BINGWA WA MAGONJWA YOTE SUGU YANAYOSUMBUA KAMA VILE PUMU, VIDONDA VYA TUMBO, BUSHA, NGUVU ZA KIUME, KISUKARI, MIVUTO YOTE, KUSAFISHA NYOTA, KURUDISHA MALI, NK.

Tatizo la upungufu ukosefu wa nguvu za kiume, maumbile madogo ya uume limekuwa kubwa kwa lika zote hapa duniani

Matatizo hayo sio mageni kigeni ni ile tiba sahihi yakutibu na kuponya haya.chanzo cha hayo matatizo ni:

KISUKARI, NGIRI,CHANGO, TUMBO KUUNGURUMA NA KUJAA GESI, KIUNO KUUMA, MAUMIVU YA MGONGO,MAGONJWA YA ZINAA, KORODANI KUVIMBANAKUUMA,VIDONDA VYA TUMBO, NK.

Tiba sahihi nabora ya tatizo la nguvu zakiume ni NYASOSE MIX, Nidawa ya vidonge asilia vilivyotengenezwa kwa kiwango bora na salama kwa ajili yakutibu mojakwamoja tatizo la nguvu za kiume maradufu

1. MKEBE NO.1 Hutibu nguvu za kiume mda mfupi sana kati ya umri wa miaka 18-85 naitakufanya uchelewe kufika kileleni kwa mda wa dk 20 hadi 40 tendo la kwanza bila kuchoka naitakufanya uwe na hamu ya kuendelea na tendo la ndoa zaidi ya mara 5 bila hamu kuisha.

MHESHA POWER
MKEBE NO 2 ni dawa ya kuboresha maumbile ya kiume kwa kunenepesha na kurefusha kwa saizi uipendayo inchi 6,7 hadi 8 kwa mda mfupi sana.dawa hizi huanza kufanya kazi kwa mda wa dk 67 ukisha tumia guarantee miaka 55 ikishakutibu.

Pia tunatibu,

KISUKARI, PRESHA, UZAZI, NGIRI, PUMU,MALARIA SUGU, VIDONDA VYA TUMBO, CHANGO AINA ZOTE, BP, BUSHA BILA UPASUAJI NK.

ITINYA,
Nidawa ya mvuto wa biashara,kazi,hupandisha cheo humfanya mfanyakazi apendwe na mwajiri wake, humvuta mme,mke,hawara,mchumba,unaemhitaji au hakutaki hatimizi ahadi zako kwa dhati utampata kwa mda wa dk 45 tu naatatulia milele nakumfunga asitoke inje ya ndoa pia ana pete za bahati ambazo zimetajilisha wengi.

SUPER POWER,
Nidawa ya yakupunguza matiti,unene tumbo,kitambi kwa akina baba,hutoa mafuta mabaya mwilini,makovu sehemu mbalimbali mwilini,chunusi sugu,minyama uzembe,michirizi mwilini,nakuongeza makalio hips,mguu wa bia nk.

BABU MADUHU ANAPATIKANA MAGOMENI MOROCCO HOTEL/KANISANI

SIMU NO 0652 102 152/0755 684 297/0788 330 105.

HUDUMA HII UNAWEZA KUIPATA/KULETEWA MAHALI POPOTE NCHINI

Makampuni Mawili Ya Mchezo Wa Ngumi Nchini Ya Kuandikiwa Barua kali Za Onyo

$
0
0
Na Anitha Jonas –WHUSM
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mheshimiwa Dkt. Harrison Mwakyembe amemwagiza Msajili wa Vyama vya Michezo nchini kuwaandikia barua ya kali ya onyo Kampuni mbili zinazoendesha Mchezo wa Ngumi za kulipwa nchini.

Mheshimiwa Mwakyembe ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari kwa ajili ya kutoa taarifa ya kazi inayoendelea kufanyika na Kamati aliyoiunda kwa ajili ya kuunda Katiba itakayosimamia Mchezo wa Ngumi nchini ambapo anatarajia kufanya kikao kikubwa cha wadau wake mwezi Juni mwaka huu.

“Nimemwagiza Msajili wa Vyama vya Michezo kutoka Baraza la Michezo la Taifa Tanzania ifikapo kesho kuwaandikia barua kali ya onyo Kampuni mbili zinazoendesha mchezo wa ngumi za kulipwa nchini ambazo ni Tanzania Proffesional Boxing Organization (TPBO) na Pugilistic Syndicate of Tanzania (PST) kutoka na viongozi wake  kuingilia shughuli za Kamati ya kuboresha Katiba ya Ngumi niliyoiunda pamoja na kukashifu na kudharau maagizo ya serikali”,alisema Dkt.Mwakyembe.

Akiendelea kuzungumza katika mkutano huu Mheshimiwa Mwakyembe aliongeza kuwa  kama viongozi wa kampuni hizo za TPBO na PST wataendelea kukashifu na utaratibu unaotumika sasa,amempa Mamlaka Msajili wa Vyama vya Michezo kuwafutia kabisa usajili kwani serikali haitavumilia kuona mchezo wa boxing unaendeshwa bila kuzingatia utaratibu.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Kamati ya kuunda Katiba ya kusimamia mchezo wa ngumi nchini Bw.Emmanuel Salehe alieleza kuwa kazi ya kuandaa Katiba hiyo imekuwa na changamoto nyingi ikiwemo baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo kuleta mvurugano mpaka kufika uamuzi ya kuwapunguza wajumbe sita.

“Kumekuwepo na changamoto nyingi ikiwemo baadhi ya wadau wa mchezo wa ngumi za kulipwa kutoa maneno ya kashfa kwa Kamati pamoja na kudharau utekelezaji wa baadhi ya majukumu waliyopewa kama ya kutoa vibali kwa mabondia wanaokwenda katika mapambano nje ya nchi,”Bw.Salehe.

Pamoja na hayo Waziri huyo mwenye dhamana na Michezo alihitimisha kwa kusema kuanzia sasa ni lazma mabondia wote wanaokwenda nje ya nchi katika mapambano ya ngumi kupata kibali kinachotolewa BMT kwa kuzingatia ushauri unaotolewa na kamati hiyo ya mpito na kwa upande wa uhamiaji atawaeleza hilo ili kuhakikisha mabondia wanaokwenda nje ya nchini wanakwenda kuiwakilisha nchi vizuri na siyo kuuza mchezo.

Waziri Mkuu: Shida ya Umeme Mikoa ya Kusini Imekwisha

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema shida ya umeme iliyokuwa inaikabili mikoa ya Lindi na Mtwara hivi sasa imekwisha.

"Kuunganishwa kwa mikoa ya Lindi na Mtwara kwenye gridi ya Taifa, kumeondoa tatizo la umeme lililokuwa likiikabili mikoa hii, na mitambo ya jenerata iliyokuwepo, itabakia kuwa ya akiba endapo dharura yoyote itatokea," alisema.

Ametoa kauli hiyo jana jioni (Jumatatu, Mei 21, 2018) wakati akizungumza na wakazi wa mji wa Mtwara kwenye viwanja vya bandarini mjini humo.

Alisema pengo lililokuwepo la kukatikakatika kwa umeme, limezibwa kwa kupata umeme wa kutoka Somanga hadi Lindi. “Umeme huu umeanzia kituo chetu cha Mbagala, umekuja Mkuranga, Muhoro, Lindi na hatimaye umefika pale Mahumbika. Na mchana wakati nikiwa Mahumbika, niliwasha kwa kompyuta kuashiria umeme wa gridi kuingia mikoa yetu ya Lindi na Mtwara,” alisema.

Akiwa Mtwara mjini, Waziri Mkuu alikagua na kisha kuzindua mradi wa upanuzi wa kituo cha kufua umeme wa gesi asilia wenye uwezo wa kuzalisha megawati nne.

Kabla ya kuzindua mradi huo, alipita bandarini kukagua ukarabati wa mitambo ya kupokelea mafuta ya dizeli na petroli ambako alielezwa kuwa kampuni mbili za GM na OILCOM zimeanza ukarabati na kwamba mwezi ujao, bandari hiyo itaanza kupokea meli za kubeba mafuta.

“Bandari ya Mtwara hivi sasa itaanza kupokea meli kubwa za mafuta, jambo ambalo halijafanyika tangu mwaka 2014. Mwezi ujao, wakati wowote, wataanza kupakua mafuta. Kwa hiyo mji utaanza kuchangamka.”

“Kuanza kupakuliwa kwa mafuta katika bandari hii, kutasaidia kushusha bei ya mafuta kwenye mikoa hii na pia kiasi kitakachobakia, tutakipeleka nchi za jirani za Msumbiji na Malawi,” alisema.

Alisema matengenezo hayo yakikamilika yatafanya bandari za Dar es Salaam, Mtwara na Tanga zote ziwe na uwezo wa kupokea mafuta. Pia aliitaka Mamlaka ya Bandari (TPA) iondoe urasimu na Mkurugenzi Mkuu wake awatumie vizuri watendaji waliopo chini yake.

Mapema, walipopewa nafasi ya kusalimia wananchi, wabunge wa Chama cha Wananchi (CUF) walitumia fursa hiyo kuelezea kufurahishwa kwao na hatua za maendeleo zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano.

Kwa upande wake, Mbunge wa Kilwa Kusini, Bw. Selemani Said Bungara alisema aliamua kutoka Chama cha Mapinduzi kwa sababu aliamini kwamba mtu hawezi kusukuma gari akiwa ndani, ni lazima atoke.

“Tumetoka ndani ya gari ya gari na sasa tunalisukuma na linakwenda kwa kasi. Hebu angalia, ndani ya miaka miwili tu, mambo yanavyokwenda kwa kasi. Kama tungebakia ndani, gari lingeenda?” alihoji.

Hoja yake ilijibiwa na Mbunge wa Nanyamba, Bw. Abdallah Dadi Chikota ambaye alisema gari analolizungumzia mbunge huyo liko imara na wala halihitaji kusukumwa. “Gari letu halihitaji kusukumwa hata kidogo, liko imara, matairi yako imara, na dereva wetu yuko makini. Tena gari letu hata muda wake wa service haujafika,” alisema na kuamsha shangwe kwa wananchi waliokuwa wakimsikiliza Waziri Mkuu.

Naye Bw. Zuberi Mohammed Kuchauka (Liwale) aliwataka wananchi wa mikoa ya Kusini wachangamkie fursa zinazopatikana kutokana na maendeleo yanayofanywa na Serikali ya awamu ya tano. “Kusini hivi sasa imeamka na imetoka gizani, sasa wananchi tuchangamkie fursa,” alisema.

Naye Mbunge wa Nachingwea, Bw. Hassan Elias Masala, alitumia fursa hiyo kuomba barabara ya kutoka Nachingwea iwekewe lami ili wakazi wake waweze kutumia fursa ya kusafirisha korosho zao hadi kwenye bandari ya Mtwara.

Naye Bw. Maftaha Abdallah Nachuma (Mtwara Mjini) pia aliomba barabara ya kutoka Mtwara hadi Mingoyo ikamilishwe matengenezo yake kwani kwa hali ya sasa siyo rahisi kusafirisha mizigo. Pia aliomba apelekewe umeme maeneo ya Mbawalachini na Mkunjanguo. “Maendeleo hayana chama, kabila wala itikadi,” alisema.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Tanzania Yapigiwa Mfano Matumizi Bora Ya Fedha Za Maendeleo Za Benki Ya Maendeleo Ya Afrika-AfDB

$
0
0
Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imeitaja Tanzania kuwa moja ya nchi za Afrika zenye matumizi bora ya fedha zinazofadhiliwa na Benki hiyo kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya miundombinu ya barabara na nishati.

Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika anayesimamia nchi 7 za Kanda ya Afrika Mashariki, Dkt. Nyamajeje Weggoro wakati  wa kikao  cha Magavana wa nchi za Afrika kwenye Mkutano wa  mwaka wa Benki ya AfDB unaoendelea Mjini Busan, Jamhuri ya Korea ya Kusini.

Dkt. Nyamajeje alisema kuwa changamoto nyingi zinazotokea katika kutekeleza miradi ya maendeleo kwa nchi  za Afrika zinatokana na  ukosefu wa  wataalamu wa fani mbalimbali, jambo linalosababisha miradi mingi  kutomalizika kwa wakati  hata hivyo Benki ya AfDB inaendelea kuangalia ni jinsi gani inaweza kusaidia kutatua matatizo hayo na kuleta maendeleo chanya kwa nchi za Afrika.

Akizungumza katika Mkutano huo kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Amina Khamis Shaaban, alisema kuwa Serikali ya Tanzania imesawasilisha barua kwa uongozi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, ili iweze kusaidia katika ujenzi wa  Uwanja wa ndege ya Msalato Jijini Dodoma na Uwanja wa ndege wa Zanzibar,  aidha miradi hiyo ikiridhiwa na kutekelezwa  itakua kichocheo kikubwa cha kukuza uchumi wa Viwanda nchini Tanzania.

Tanzania ni wadau wakubwa  katika Benki ya AfDB hivyo inanufaika na mikopo nafuu inayotumika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kama vile ujenzi wa Barabara  za kiwango cha Lami hususani mkoa wa Tabora na pia miradi ya  Nishati  ya umeme na maji maeneo mbalimbali nchini.

Babu Tale Atiwa Mbaroni

$
0
0
Mkurugenzi wa Kampuni ya Tip Top Connection ya jijini Dar es Salaam,  Hamis Taletale maarufu Babu Tale, ametiwa  mbaroni na kufikishwa mahakamani na Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam kwa amri ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es  Salaam.

Babu Tale amekamatwa kufuatia amri iliyotolewa Februari 16, 2018 na Naibu Msajili wa Mahakama  Kuu Kanda Maalum, Wilbard Mashauri iliyoelekeza kukamatwa mtuhumiwa huyo na ndugu yake, Idd Taletale.

Amri hiyo pia, ilielekeza watakapokamatwa wapelekwe Gereza la Ukonga wakiwa wafungwa wa kesi ya madai, hadi hapo mahakama hiyo itakapotoa maelekezo mengine.

Hata hivyo, Babu Tale hakuweza kupatikana na ndipo mahakama hiyo ikatoa amri nyingine kama hiyo Aprili 4 mwaka huu. Tangu hapo wamekuwa wakitafutwa bila mafanikio hadi jana alipokamatwa.

Mahakama hiyo iliwaamuru kumlipa Mhadhiri wa Dini ya Kiislamu, Sheikh Hashim Mbonde kiasi cha Sh250 milioni, baada ya kupatikana na makosa ya ukiukwaji wa haki za hakimiliki kwa kutumia masomo yake kibiashara bila ridhaa yake kinyume cha Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki.

Baada ya kutiwa mbaroni leo alifikishwa mahakamani saa tisa alasiri  kwa ajili ya hatua zaidi. Hata hivyo,  Naibu Msajili wa Mahakama hiyo, aliyetoa amri ya kumkamata hakuwepo.  Kufuatia kutokuwepo kwa msajili huyo Taletale amerudishwa mahabusu Kituo Kikuu cha Polisi hadi kesho asubuhi atakapopelekwa tena mahakamani hapo kwa hatua zaidi.

Hukumu hiyo iliyomwamuru Babu Tale na nduguye kulipa kiasi hicho cha fedha,  ilitolewa na Jaji Agustine Shangwa, Februari 18,2016  katika kesi ya madai namba 185 ya mwaka 2013, iliyofunguliwa na Sheikh Mbonde kutokana akiwalalamikia ndugu hao kutumia mahubiri yake kibiashara bila ridhaa yake.

John Heche Aiwakia Serikali Uwekaji Vigingi Vijijini

$
0
0
Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche (Chadema), ameionya serikali kama haitasitisha uwekaji wa vigingi katika maeneo ya vijiji vinavyopakana na hifadhi inaweza kusababisha machafuko wilayani Tarime.

Heche ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma leo Mei 22, alipokuwa akichangia bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka wa fedha 2018/19.

Kwa mujibu wa Heche uwekaji huo wa vigingi unawekwa katika vijiji vinavyotambuliwa kisheria tangu enzi za utawala wa Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

“Aidha, ukamataji wa mifugo inayodaiwa kuingia katika hifadhi za taifa, utaratibu huo haukubaliki kwa kuwa baadhi ya mifugo inakamatwa na kuingizwa katika hifadhi hizo na watumishi wa TANAPA na kisha kutozwa faini kubwa zisizoweza kulipika kwa haraka,” amesema Heche.

Mtanzania Ateuliwa Naibu Katibu Mkuu Umoja wa Mataifa Mazingira

$
0
0
Na.Mwandishi Wetu-MAELEZO.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw.Antonio Guterres ametangaza uteuzi wa Bi.Joyce Msuya kutoka Tanzania kuwa naibu katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa anayeshughulikia program ya mazingira yenye makao makuu yake Nairobi nchini Kenya.

Kwa mujibu wa taarifa ya Umoja wa mataifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari leo tarehe 22 Mei, Bi Msuya anachukua nafasi hiyo kutoka kwa Bw.Ibrahim Thiaw wa Mauritania aliyemaliza muda wake ambaye katibu Mkuu wa umoja wa mataifa amemuelezea kuwa na utumishi uliotukuka katika kipindi chake cha uongozi.

Bi.Joyce Msuya amekua akifanya kazi kama mshauri wa makamu wa rais wa benki ya dunia anayeshughulikia nchi za Asia Mashariki pamoja na ukanda wa Pasifiki tangu mwaka 2017, makao makuu ya benki ya Dunia Washington D.C Marekani.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bi.Msuya atatumia muzoefu wake wa miaka 20 katika benki ya Dunia, pamoja na uzoefu wake katika masuala ya maendeleo ya kimataifa katika kazi yake mpya na anaimani kuwa ataleta mabadiliko makubwa katika umoja wa mataifa.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo Bi.Msuya amewahi kufanya kazi kama mwakilishi maalum wa benki ya Dunia na mkuu wa kundi la benki ya dunia nchini Korea ya kusini,pamoja na mratibu wa taasisi ya benki ya dunia katika Asia Mashariki na ukanda wa Pasifiki ofisi iliyoko China, na ameahi kuwa na nafasi mbalimbali za juu katika benki ya dunia na washirika wake.

Aidha taarifa hiyo imefafanua kuwa Bi.Joyce Msuya ana Shahada ya uzamili ya Maikrobailojia na kinga kutoka Chuo Kikuu cha Ottawa, Canada pamoja na shahada ya Baiokemia kutoka Chuo Kikuu cha Strathclyde,Scotland.

Programu ya umoja wa mataifa ya mazingira ni mpango wa kidunia wa mazingira unaolenga kutoa mwelekeo katika uongozi na usimamizi wa mazingira, na kuwashauri wadau na nchi wanachama kwa ujumla njia sahihi za kutunza na kuhifadhi mazingira kwa manufaa ya vizazi vijavyo. Programu ya umoja wa mataifa ya mazingira inafanya kazi na serikali,mashirika na asasi za kimataifa duniani kote.

Spika Ndugai aunga mkono usitishwaji wa kuweka mipaka (vigingi)

$
0
0
Spika wa Bunge, Job Ndugai amekubaliana na ushauri wa Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira wa kusitisha uwekaji wa mipaka (vigingi) katika mipaka ya hifadhi.

Ndugai ametoa kauli hiyo leo jioni Mei 22, 2018 wakati Bunge lilipokaa kama kamati kupitisha vifungu vya bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii ya mwaka 2018/19.

Alikuwa akijibu hoja ya Mbunge wa Serengeti (Chadema), Ryoba Chacha aliyebainisha kuwa uwekaji wa mipaka  haushirikishi wananchi.

“Ushauri uliotolewa na kamati naona ni mzuri tu, kabla ya kuweka vigingi mshauriane kwanza na kukubaliana. Lakini hili sijui la kuweka vigingi halafu baadaye uje usogeze sidhani kama ni sawa, Tanapa (Hifadhi za Taifa Tanzania) hili linawezekana kweli," amesema.

Baada ya kauli hiyo, wabunge walishangilia huku wale wa upinzani baadhi yao wakisimama kabisa kumuunga mkono.

Akihitimisha hoja yake, Chacha amesema: "Naungana na wewe mheshimiwa spika."

Watu 7 wafariki Sumbawanga kwa Kipindupindu.... 44 walazwa hospitalini

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule amethibitisha kufariki kwa wagonjwa saba wa kipindupindu katika Wilaya ya Sumbawanga huku wagonjwa wengine 44 wakibaki wodini kuendelea kupatiwa matibabu na wagonjwa 115 wakiruhusiwa kurudi nyumbani.

Akizingumzia tukio hilo Dkt. Haule amesema kuwa ugonjwa huo umelipuka Mei 6, 2018 katika Kijiji cha Mayenje, kata ya Milepa katika bonde la Ziwa Rukwa na kusambaa katika maeneo mengine ya Wilaya na hatimaye kupatikana kwa wagonjwa wawili katika hospitali ya rufaa ya mkoa.

"Sasa hivi katika bonde la ziwa Rukwa kuna shughuli za uvunaji wa mpunga na hivyo watu wengi hutokea huku juu kwenda bondeni kutafuta vibarua vya kuvuna mpunga kwenye maeneo hayo yaliyoathirika na kipindupindu, maji yanayotumika huko ni machafu kutoka katika madimbwi na mito. Nawaomba viongozi wa dini watoe tahadhari kwa waumini hasa katika maeneo yale yalioathirika zaidi", amesema Dkt. Haule.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya May 23

Sababu Zilizofanya 'Makontena ya RC Paul Makonda' Yakose Masamaha wa Kodi

$
0
0
Kitendo cha nyaraka za makontena 20 yenye samani yaliyo katika hatari ya kupigwa mnada na Mamlaka ya Mapato (TRA) mwezi ujao kuwa na jina la mtu binafsi Paul Makonda,ni moja ya sababu zilizomkwamisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kusamehewa ushuru wa forodha na kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kama alivyoomba, imefahamika.

Kwa mujibu wa barua ya Waziri wa Fedha na Mipango, Philip Mpango kwa 'RC' Makonda ya Machi 24, mwaka huu kwa mujibu wa sheria, shehena hiyo ya samani haistahili kupata msamaha wa ushuru wa forodha au bidhaa na kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwa sababu kadhaa ikiwamo kuonekana kuwa mali ya mtu binafsi.

Makonda aliiandikia wizara barua Januari 3, mwaka huu akiomba msamaha wa kodi kwenye samani za shule za Mkoa wa Dar es Salaam zenye thamani ya "takribani" Sh. bilioni 1.4 ambazo alidai ni msaada kutoka kwa wananchi wapenda maendeleo waishio Marekani.

Ombi hilo hata hivyo limekataliwa na Waziri Mpango kwa kuzingatia Sheria ya Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya mwaka 2004 na Sheria ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ya mwaka 2014.

Barua ya Dk. Mpango inasema kwa mujibu wa Sheria ya VAT, msamaha kwa taasisi za Serikali ni kwa shughuli zisizo za kibiashara, "kwa masharti kwamba usiwepo uwezekano wa shughuli kama hiyo kutolewa na taasisi isiyo ya kiserikali".

Kwa mujibu wa barua hiyo ya Wizara ya Fedha, samani kama hizo zinaweza kutolewa na taasisi isiyo ya kiserikali au mtu binafsi hivyo kuwa nje ya eneo la msamaha.

Aidha, Makonda amekataliwa msamaha wa kodi kwa kuwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa siyo asasi ya kiraia au taasisi ya kidini, barua hiyo inasema na kufafanua:

"Magazeti ya Serikali namba 205 na 206 ya mwaka 2016 yanatoa misamaha ya ushuru wa forodha na wa bidhaa kwa asasi za kiraia na taasisi za dini kwa vifaa vitakavyotumika kwa ajili ya kuendeleza, kuanzisha au kukarabati miradi inayolenga elimu, usambazaji maji, huduma za afya na miundombinu."

Viti, meza na mbao za darasani vinavyodaiwa kuwamo katika mzigo wa Makonda vinaonekana kuangukia nje ya jedwali hilo.

Mbali na majibu kwa Makonda, nakala ya barua ya Waziri Dk. Mpango imepelekwa pia Ofisi ya Rais, Waziri Mkuu, Tamisemi, Wizara ya Fedha na TRA.

Alipoulizwa jana kwa njia ya simu kama Makonda alipokea barua hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma wa Wizara ya Fedha na Mipango, Benny Mwipaja hakuweza kuthibitisha.

Lakini alionyesha kushangazwa kwake kusikia "barua iliyonakiliwa kwa Waziri Mkuu ipo mitandaoni?"

Mwanzoni mwa wiki iliyopita TRA ilitangaza kusudio la kupiga mnada kontena 20 za Makonda ikiwa atashindwa kuzilipia ushuru na kuzichukua ndani ya siku 30 zitakazomalizika katikati ya mwezi ujao.

Katika tangazo hilo, Kamishna wa Idara ya Kodi ya Ushuru wa Forodha na Bidhaa, alitoa siku 30 kwa wamiliki wa mali mbalimbali zilizopo katika ghala la TRA kwenda kuzichukua la sivyo baada ya muda huo zitapigwa mnada kwa mujibu wa sheria na utaratibu wa ushuru wa forodha.

Credit: Nipashe

Kamanda wa Polisi aliyewaonya wanaume kukohoa azungumzia kuhamishwa kwake ghafla baada ya kauli hiyo

$
0
0
Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mjini Magharibi Visiwani Zanzibar, Hassan Nassir Ali, amefunguka juu ya uhamisho wake aliopewa siku chache baada ya kuwaonya wanaume juu ya tabia zao zisizofaa kwenye jamii.

Kamanda Hassan amesema kwamba uhamisho wake ni wa kawaida na wala haujatokana na kauli alizotoa, ambazo zilizua gumzo kwenye mitandao ya kijamii.

Akiendelea kutolea ufafanuzi suala hilo Kamanda Hassan amesema kwamba kauli hiyo aliitoa na alikuwa anamaanisha, lakini haijaleta mtafaruku wowote kwenye jamii kama ambavyo inasemekana, na hata walipoijadili kwenye Baraza la Wawakilishi Zanzibar ilikuwa ni utani.

“IGP amesema mwenyewe amefanya uhamisho na uteuzi huu ili kuimarisha safu yake kiutendaji, mimi ningekuwa nimesema nimewakwaza watu sio kweli, hata wale waliosema katika Baraza la Uwakilishi ilikuwa ni kwa utani, ni uhamisho wa kawaida kabisa, wala sio chuki”, amesema Kamanda Hassan.

Kamanda Hassan ameendelea kwa kuwataka wananchi wa Kaskazini Pemba ambako amehamishiwa kufuata sheria bila shuruti kwani kazi iko pale pale.

“Nitaendelea kufanya kazi yangu vizuri nitaendelea kusimamia sheria vizuri, kazi iko pale pale bado mimi ni Kamanda wa polisi nitasimamia sheria za nchi, wala sio jambo langu hili wala mie sio mzee wa vikohozi, mimi nimetoa mifano, hivyo kazi iko pale pale”, amesema Kamanda Hassan.

Kamanda huyo ambaye metokea visiwani Zanzibar wiki iliyopita aliibua mzozo kwenye mitandao baada ya kuwaonya wanaume wenye tabia ya kukohoa pindi waonapo wanawake wenye maumbile makubwa, akisema hilo ni kosa kisheria ambalo linatambulika kama shambulio la aibu.

Sugu alitetea Jeshi la Magereza Bungeni

$
0
0
Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi 'Sugu' amelitetea Jeshi la Magereza mbele ya  Bunge  kuwa jeshi hilo lina matatizo makubwa ya kiusafiri jambo ambalo linapelekea wafungwa kupelekwa Mahakamani kwa miguu kitendo ambacho kina hatarisha usalama wa mfungwa na askari kiujumla.

Kauli hiyo ya Sugu imetolewa jana  Mei 22, 2018 Bungeni Jijini Dodoma kwenye kikao cha 34 mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati wa kipindi cha maswali na majibu kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

"Pamoja na matatizo waliyokuwa nayo Jeshi la Polisi katika masuala ya vyombo vya usafiri lakini niwahakikishie Jeshi la Magereza lina hali mbaya sana, hawana magari sio tu magari mabovu hawana magari kabisa, kiasi kwamba wanafikia hatua ya kuwapeleka wafungwa ambao wanakesi Mahamani kwa miguu huku wakiwa wamewafunga pingu. Hii ni mbaya sana kwa usalama wa askari magereza pamoja na wale watuhumiwa ambao wamefungwa pingu", alisema Sugu.

Pamoja na hayo, Sugu aliendelea kwa kusema "mtu anatuhumiwa ujambazi halafu anapitishwa mtaani kwa miguu wananchi wanamuona, wanaweza wakamvamia na kumshambulia pamoja na kuhatarisha maisha ya mfungwa".

Kutokana na ushauri huo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba akampongeza Mhe. Sugu kwa kusema "nimpongeze Mhe. Sugu kwa kuuliza swali kwa experience, na niseme kwamba yeye ni mshauri mzuri. Tutalizingatia hilo ili tuweke mgao kwenye upande wa Jeshi la Magereza ili kuepuka na tahadhari aliyosema".

Maofisa Watatu Kituo cha Uwekezaji cha nchini ( TIC ) Wafariki kwa Ajali

$
0
0
Maofisa watatu wa Kituo cha Uwekezaji cha nchini  (Tanzania Investment Center (TIC) wamefariki dunia katika  ajali ya gari usiku wa kuamkia jana Mei 22, 2018 maeneo ya Chalinze wakiwa njiani kuelekea jijini Dodoma.

Waliofariki ni Saidi Amiri Moshi (Kaimu Mkurugenzi wa Research zamani Corporate Affairs), Zacharia Kingu (Kaimu Mkurugenzi wa Corporate Affairs zamani Investment Promotion) na Martin Masalu (Meneja Research).

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Jonathan Shana amesema ajali hiyo imehusisha gari ya serikali STK 5923 aina ya Toyota land cruiser lililongana na Scania T620 AQV ambaye dereva wake alihama kwenye njia yake na kusababisha ajali hiyo.

Waliopata majeraha ni wawili Godfrey Kilolo (Meneja wa Sheria) na dereva wa gari hilo aliyejulikana kwa jina moja tu la Priscus.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images