Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Mbunge John Mnyika na Bulaya watolewa bungeni

$
0
0
Naibu Spika Tulia Ackson ameagiza Mbunge wa Kibamba Mhe. John Mnyika na Ester Bulaya kutolewa nje ya ukumbi wa Bunge kwa kile alichodai kutoheshimu kiti cha Spika.

Naibu Spika ametoa maamuzi hayo jioni ya leo Mei 9, 2018 katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji mwaka 2018/19 ambapo Mbunge John Mnyika alisimama akitumia kanuni ya 69(1), kutaka kuahirishwa kuhitimishwa kwa hoja ya wizara ya Maji na Umwagiliaji ili apewe nafasi ya kutoa hoja yake ya kwanini bajeti ya wizara hiyo isipitishwe na Bunge.

Mara baada ya kauli hiyo, Dk Tulia alisimama akitumia kanuni ya 69(2), kusema kama Spika atakuwa na maoni kwamba kuwasilishwa kwa hoja hiyo ni kinyume cha uendeshaji bora wa shughuli za Bunge, atakataa kuitoa ili ijadiliwe.

Hivyo kutokana na mabishano ya kinanuni hayo yaliyojiri Naibu Spika Dk Tulia Ackson aliamuru Mnyika atolewe nje kwa kutoheshimu kiti cha Spika.

Mbali na Mnyika Naibu Spika Dk. Tulia Ackson amemtoa pia ndani ya Ukumbi wa Bunge, Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya (Chadema) kwa kutoheshimu kiti cha Spika.

Ebitoke amvaa Mange Kimambi, adai siyo size yake

$
0
0
Msanii Ebitoke amefunguka na kusema kuwa katika maisha yake anamchukia sana mwanaharakati wa mitandao Mange Kimambi na kusema kuwa alimkwaza sana kuingilia maisha yake na kusababisha mashabiki wake washindwe kumuelewa kuhusu tuhuma za yeye kuiba mume wa Mama Ashura.

Ebitoke amesema hayo leo Mei 9, 2018 katika kipindi cha Kikaangoni  kinachorushwa na  EATV na kusema kuwa mwanadada huyo aliingia katika anga zake na kumchefua kabisa jambo ambalio liliongeza kumchukia.

"Kwanza yule dada Mange Kimambi mimi simpendi, sijawahi kabisaa kumkubali, sipendi mambo yake na sipendi vimtu vinavyoongea sana, yule dada aliingilia maisha yangu na kunichafulia mpaka kwa mashabiki zangu saizi wengine wanashindwa kunielewa. Mange Kimambi mimi siyo size yangu kabisaa kwanza yeye mtu mzima sasa nilishangaa kwanini yeye anaingilia maisha yangu" alisema Ebitoke.

Mbali na hilo Ebitoke aliweza kutoa ushauri wake kwa mwanaharakati huyo wa mitandaoni Mange Kimambi na kusema kuwa asifanye mambo ya kufuatilia maisha ya watu bali afanye mambo yake mengine.

Wizara Yakubali Kuunda kamati kuchunguza miradi ya maji

$
0
0
Wizara ya Maji na Umwagiliaji imeufanyia kazi ushauri wa wabunge baada ya kuunda kamati ya kuchunguza miradi ya maji inayotekelezwa tangu mwaka 2016 katika maeneo yote nchini.

Akizungumza bungeni leo Mei 9, 2018 wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge walizozitoa katika mjadala wa bajeti ya wizara hiyo mwaka 2018/19, Waziri Isack Kamwelwe amesema Profesa Tolly Mbwete wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), ndio ataongoza kamati hiyo.

Amesema hoja za wabunge kuhusu kuundwa kwa kamati hiyo ilisababisha amtume Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa Kitila Mkumbo kukutana na wafadhili ambao walikubaliana na wazo hilo.

“Hakuna mtu atayeonewa aibu, tena katika umri wangu huu siwezi kuogopa wala kumhurumia mtu lazima kila mmoja atabeba msalaba wake,” amesema Kamwelwe.

Waziri huyo amesema kesho atamkabidhi Waziri Mkuu taarifa ya kamati aliyoiunda kuchunguza miradi yote ya maji katika mkoa wa Mara ikiwa ni agizo alilopewa na Waziri Mkuu baada ya kusikia kelele za miradi hiyo.

Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege

$
0
0
Waziri wa Maliasili na Utalii Dk Hamisi Kigwangala amewataka wabunge kutokubeza juhudi zinazofanywa na Rais John Magufuli ikiwemo ununuzi wa ndege kwani ni sehemu ya kipaumbele cha nchi

“Hakuna tatizo la kununua ndege kwani zinasaidia katika sekta ya utalii, kwani kuna watu wanasema mpango huo ni wa kukurupuka, sisi tulioko katika sekta hiyo tunakereka sana kusikia kauli hizo,” amesema Kigwangala.

Amesema Tanzania ni nchi ya pili duniani kwa kuwa na vivutio vingi lakini inashangaza kuona inashindwa kuvitumia kutokana na kuwa na miundombinu mibovu ikiwemo katika shirika la ndege

Alisema nchi ya Ethiopia wamenunua ndege 10 kwa hiyo hakuna shida wala tatizo lolote kwa kununua ndege na akamuomba Rais kuendelea na mpango huo ili zinunuliwe ndege zaidi.

Ebitoke: Bikira yangu nilimpa Ben Pol

$
0
0
Msanii wa vichekesho bongo Ebitoke, ameweka wazi kuwa ahadi aliyomuahidi kumpa Ben Pol alishaitekeleza hivyo watu wasijiulize sana.

Akiongea na EATV,  Ebitoke amesema kuwa licha ya kwamba hivi sasa hayuko tena kwenye mahusiano na Ben Pol, lakini yeye ndiye alikuwa mwanaume wake wa kwanza na ndiye aliyempa zawadi ya usichana wake aliyomuahidi.

“Kama ulimuahidi mtu zawadi lazima umpe, nimeshampa Ben Pol zawadi yake”, amesema Ebitoke.

Ebitoke amesema kwamba wawili hao kwa sasa hawako pamoja lakini wanaendelea kusaidiana kwenye kazi, na sio kimapenzi tena.

Ikumbukwe kwamba baada ya Ebitoke kukiri kuwa na hisia za kimapenzi kwa Ben Pol aliweka wazi kuwa yeye bado ni msichana na usichana wake alitunza kwa ajili yake, hivyo kama angekuwa naye yuko tayari kumpa.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya May 10

Serikali Yatoa Siku Tatu Kwa Walioficha Mafuta Na Sukari......Yasisitiza kamwe haitokubali kuchezewa na wafanyabiashara wasiowaaminifu

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa siku tatu kwa wafanyabiashara na wenye viwanda vya mafuta ya kupikia na sukari nchini kuhakikisha bidhaa hizo zinaendelea kupatikana katika maeneo yote na katika bei ya kawaida.

“Natoa siku tatu kuanzia Alhamisi, Ijumaa na Jumamosi mafuta yote yaliyoko bohari yaondolewe yaendelee kusambazwa kama kawaida nchini kote ili kuondoa uhaba uliojitokeza na kamwe Serikali haitokubali kuchezewa na wafanyabiashara wasiowaaminifu,”

Ametoa agizo hilo jana jioni (Jumatano, Mei 9, 2018) Bungeni Jijini Dodoma mara baada ya Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage kutoa kauli ya Serikali kuhusu uhaba wa mafuta ya kupikia nchini.

Alisema kama uhaba wa bidhaa hiyo utaendelea, ifikapo Jumapili Serikali itaanza kufanya msako kwenye viwanda na maghala na kuchukua hatua kali kwa watakaobainika kuficha mafuta hayo.

Waziri Mkuu amesema takwimu zinathibitisha kwamba mafuta ya kupikia yaliyoingizwa nchini yanatosha, hivyo nchi haipaswi kuwa na uhaba. Amesema kwa mwezi mafuta yanayotumika nchini tani 28.9 na kila mwezi zinaingizwa tani 30,000.

“Hatuwezi kukubaliana na jambo hili kwa sababu haliko kwa bahati mbaya ni mpango uliopangwa kwani imekuwa ni kawaida kila tunapoelekea kwenye Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kunakuwa na upungufu wa bidhaa hasa sukari, hivyo Serikali haitakubali wananchi wateseke bila sababu za msingi,” alisisitiza.

Akiwasilisha kauli ya Serikali Bungeni, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Mwijage alisema vyanzo vinavyotumika kuzalishia mafuta nchini vinatosheleza mahitaji kwa asilimia 30, hivyo asilimia 70 ya mafuta huagizwa kutoka nje ya nchi.

“Miezi mitatu ya mwanzo kwa mwaka huu kuanzia Januari wastani wa mafuta yaliyoingizwa ni tani 30,210.71 kwa mwezi na jumla ya akiba ya mafuta yaliyopo nchini ni wastani wa tani 68, 902, hivyo hakuna upungufu,” alisema.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Muimbaji Wa Injili Nchini Kenya Aliyedaiwa Kubeba Mimba Ya Harmonize Afunguka

$
0
0
Siku mbili hizi kuna stori zilienea Kwenye mitandao ya kijamii  zilizosema kuwa Msanii wa Bongo fleva kutoka WCB Harmonize amempachika mimba mwanadada ambaye ni msanii wa nyimbo za Injili kutoka Kenya.

Msanii huyo anayejulikana kama Veronica Wanja ‘Nicah The Queen’ amekataa tuhuma hizo na kudai kuwa hazina ukweli wowote, awali Nicah alikuwa katika mahusiano na mchekeshaji Dr. Ofweneke’s.

Tetesi hizi zimekuja mara baada ya wasanii hawa kuonekana pamoja mara kwa mara hali iliyozua minong’ono.

Kwenye Interview aliyofanya na gazeti moja nchini humo Veronica alisisitiza kuwa yeye sio mjamzito na hapendi kuongelea sana hayo mambo kwa sababu yeye ni Msanii wa injili hivyo si vema kuongelea.


Ebitoke: Shilole Sio Msanii Bali ni Mama Ntiliye

$
0
0
Mchekeshaji maarufu kutoka Timamu Tv, Ebitoke ameibuka na kumtolea povu zito Shilole huku akidai kuwa hamuelewi kama ni msanii au mama ntiliye maana hajui kazi yake hata moja.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Kikaangoni cha East Africa Tv, Shabiki mmoja alimtaka ataje wimbo mmoja wa Shilole na kuuimba ndipo aliposema hajui wimbo wake hata mmoja kwani hajui kama ni msanii au ni mama ntiliye:

"Labda unitajie nyimbo zake mimi sijui kazi zake mimi najuaga  yeye ni mpishi tu ila hapa Kwenye nyimbo mtanisamehe kwa kweli sizijui nyimbo zake…..Nisiwe muongo naongea ukweli wala sio kiki kama mlivyozoea mambo ya kiki siku hizi nimeacha”.

Shilole mbali ya kuwa msanii wa Bongo fleva Lakini pia ni mfanyabiashara ambaye anamiliki mgahawa wake unaoitwa Shishi Food ambapo anauza vyakula mbali mbali.

Wema Sepetu Alamba Dili Nono Na Tatu Mzuka

$
0
0
Muigizaji wa Bongo movie Wema Sepetu ameendelea kuwa na mwezi mzuri kwani siku chache baada ya kupata ubalozi wa Kombe la Dunia na Star Times siku ya jana Wema alilamba dili nono na Tatu Mzuka.

Siku ya jana Kampuni ya The Network ambayo inahusika na kuendesha Michezo ya namba ya Tatu mzuka, imetangaza kuingia kwenye ushirikiano wa kibiashara na Wema.

Akizungumza Kwenye mkutano na waandishi wa habari, mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa Tatu Mzima Sebastian Maganga, alisema ushirikiano wao na Wema ni mpango mkakati wa Tatu Mzuka wa kufanya kazi bega kwa bega na Watanzania ili kuboresha maisha yao.

"Kusudi kubwa la Tatu Mzuka kuingia makubaliano na Wema, ina lengo la kutaka kusambaza fursa kwa watu wengi kadri iwezekanavyo ili kuboresha maisha yao ya kila siku”.

Lakini pia Wema aliyepata shavu hilo alifunguka na kusema:

"Nina hamu kubwa ya kuanza kuwashirikisha bidhaa hii mashabiki zangu wote na Watanzania kwa ujumla wao ili waweze kujitengenezea fursa nyingi za kuboresha maisha yao  kupitia kwangu."

Amber Lulu Apata Dili la Kutangaza Kondomu

$
0
0
Video vixen na msanii wa Bongo movie nchini Amber Lulu amekwaa dili refu la kutangaza kondomu za kiume.

Amber Lulu amefunguka kuhusu Dili hilo nono alilolipata huku akiweka wazi kuwa limeweza kumpatia mpunga mrefu:

"Nimepata mpunga mrefu nimshukuru Mungu, ni hatua moja ambayo nimepiga, so inabidi tushukuru Mungu wote”.

Baada ya kupata dili hilo Amber Lulu aliweka Habari hiyo njema na kuandika kupitia ukurasa wake wa Instagram:

Hii ni habari njema kwa Amber Lulu ambaye tayari anafanya vizuri na ngoma yake ya ‘Jini Kisirani’.

Mbowe Atua Mbeya Kuongoza mapokezi ya Sugu anayetoka jela

$
0
0
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, mbunge wa Viti Maalumu, Sophia Mwakagenda na viongozi wengine wa chama hicho wamefika Gereza Kuu la Ruanda mkoani Mbeya kuwapokea Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi 'Sugu' na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga.

Viongozi hao wamefika gerezani leo Mei 10, 2018 saa 12:45 asubuhi na kuingia ndani ya uzio wa gereza ambako askari wamewaondoa. Mbowe na wenzake wametii amri hiyo.

Wengine waliofika gerezani ni Meya wa Jiji la Mbeya, Mchungaji David Mwashilindi na madiwani.

Askari wamefika gereza kuu kuimarisha ulinzi wakiwa na magari mawili, moja limeingia ndani na lingine lipo nje.

Sugu na Masonga walitiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miezi mitano jela Februari 26 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya kwa kutoa lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli kwenye mkutano wa hadhara walioufanya Desemba 30 mwaka jana eneo la Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.

Wawili hao wameshatumikia adhabu hiyo kwa siku 73 ikiwa ni zaidi ya robo ya kifungo chao.

BREAKING: Sugu na Masonga Waachiwa Huru

$
0
0
Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa Chadema Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga wameachiwa huru kutoka Gereza la Ruanda Jijini Mbeya walikokuwa wakitumikia kifungo cha miezi mitano baada ya kukutwa na hatia ya uchochezi.

Wawili hao wamepokelewa uraiani leo Mei 10, 2018 asubuhi na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, na viongozi wengine waandamizi wa chama hicho waliosafiri hadi Mbeya kwa ajili ya mapokezi hayo.

Sugu na Masonga walitiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miezi mitano jela Februari 26 mwaka huu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya kwa kutoa lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli kwenye mkutano wa hadhara walioufanya Desemba 30 mwaka jana eneo la Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.

Wawili hao wameshatumikia adhabu hiyo kwa siku 73 ikiwa ni zaidi ya robo ya kifungo chao.

Mbowe: Tutakata Rufaa hata kama Sugu ameachiwa Huru

$
0
0
Kufuatia  kuachiwa huru kwa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi na Katibu wa Chadema Nyanda ya Juu Kusini, Emmanuel Masonga kutoka Gereza la Ruanda, Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, amesema bado hawajafahamu ni taratibu gani zimetumika kuwaachia huru wakati  kifungo chao kilikuwa bado.

“Katika mazingira ya kawaida, siku yao ya kifungo walichokuwa wamepewa kilikuwa kinaishia Juni 5, mwaka huu, lakini ghafla wakapewa taarifa kwamba wataachiwa leo. Hatuna hakika sana ni taratibu gani zimetumika kufupisha kifungo chao kwa sababu jambo hilo halijawekwa wazi.

“Tangu wamewekwa gerezani ni takribani miezi mitatu, mawakili wetu walifanya jitihada za kuhakikisha rufaa yao katika mazingira ya dharura inasikilizwa, lakini haikuwahi kupata jaji wala kusikilizwa kwa sababu kila jaji aliyepangiwa kesi hiyo alionekana ana udhuru,”alisema Mbowe.

Aidha, amesema wao wanaamini kesi hiyo haikuwa ya haki kwa sababu watuhumiwa walinyimwa dhamana mwanzoni, na kutokana na mazingira ya kesi yenyewe hawakutakiwa kupewa kifungo. 

Pia amedai kwamba wataendelea na rufaa yao ili kuweka rekodi sawa na kudhihirisha kwamba Sugu na Masonga hawakuwa na makosa.

Sugu na Masonga walitiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miezi mitano jela Februari 26 mwaka huu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya kwa kutoa lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli kwenye mkutano wa hadhara walioufanya Desemba 30 mwaka jana eneo la Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.

Wawili hao wameshatumikia adhabu hiyo kwa siku 73 ikiwa ni zaidi ya robo ya kifungo chao.

Sugu Azungumza Baada ya Kuachiwa Kutoka Gerezani

$
0
0
Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ambaye ameachiwa huru leo Mei 10, 2018 kutoka katika Gereza la Ruanda jijini Mbeya alikokuwa amefungwa na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga, amefunguka na kuweka wazi kilichojiri.

Amesema hakuwa anafahamu iwapo angeachiwa huru leo hadi polisi walipomfuata na kumwambia ajiandae. Amedai mapaka sasa hafahamu imekuwaje hadi akaachiwa kwani ilijulikana ataachiwa Juni 5, ambapo kifungo chake kingekamilika.

“Watu wote walitarajia ningetoka jela mwezi Juni, lakini ghafla jana niliambiwa nijiandae kwamba kesho asubuhi (leo) natakiwa niachiwe huru, nilipotoka nje nikakuta askari wengi, nikaelekezwa kuingia kwenye gari la RCO mimi na mwenzangu Masonga, tukasindikizwa na maofisa magereza watano hadi nyumbani na kutukabidhi kwa familia.

“Watu wanauliza, imekuwaje? Lakini mimi ninawaambia sijui, kwa sababu haikuwa kazi yangu kufanya hesabu za magereza, hiyo ni kazi ya magereza, kwa sababu mimi ninachoamini sikutakiwa kuwa magereza in the first place, utumishi uko palepale kwa level ileile, tulikuwa na exposure sasa hivi tumeongeza experience,” amesema Sugu.

Sugu na Masonga walitiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miezi mitano jela Februari 26 mwaka huu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya kwa kutoa lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli kwenye mkutano wa hadhara walioufanya Desemba 30 mwaka jana eneo la Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.

Wameshatumikia adhabu hiyo kwa siku 73 ikiwa ni zaidi ya robo ya kifungo chao.

Magereza: Sugu Ametoka kwa msamaha wa Rais

$
0
0
Jeshi la Magereza limesema mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu Sugu ametoka kwa msamaha wa Rais John Magufuli alioutoa kwa wafungwa katika maadhimisho ya miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Aprili 26, 2018.

Ofisa habari wa jeshi hilo, Mrakibu Msaidizi wa Magereza, Lucas Mboje amesema katika maadhimisho hayo,  Rais Magufuli alitoa msamaha kwa wafungwa 3,319, kati yao wafungwa 585 waliachiliwa huru Aprili 26, 2018.

“Wafungwa 2,734 walibakia gerezani akiwemo Sugu kumalizia sehemu ya kifungo kilichobakia baada ya kupewa msamaha huo na Rais Magufuli,” amesema.

Ninogeshe ya Nandy Yamfunika Ommy Dimpoz

$
0
0
Msanii wa muziki wa Bongo fleva Nandy ambaye sasa anafanya vyema na wimbo wake 'Ninogeshe' amemshusha chini katika mtandao wa Youtube msanii Ommy Dimpoz ambaye naye anafanya vyema na wimbo wake wa 'Yanje'.

Nandy sasa kwa upande wa Tanzania video yake imeshika nafasi ya kwanza katika mtandao huo wa YouTube na kumshusha Ommy Dimpoz ambaye alikuwa ana trend na kushika nafasi hiyo ya kwanza toka Mei 2, 2018 na sasa kushika nafasi ya tatu chini ya Nandy.

Hata hivyo mapokeo ya video hiyo ya Nandy yamekuwa ni makubwa sana kwani video yake ndani ya siku sita toka ilipotoka Mei 3, 2018 imeshafikisha watazamaji zaidi ya Laki saba huku wengine wengi wakisema kuwa kupitia wimbo wake huo mpya na video yake hiyo imewafanya wasahau ujinga wake aliofanya wiki kadhaa zilizopita baada ya video yake akiwa faragha na Bill Nas kusambaaa kwenye mitandao ya kijamii.

Zitazame hapa video za wakali hawa ambao sasa wanafanya vyema na nyimbo zao


Dogo Janja achora Tattoo ya Irene Uwoya kwenye kwapa

$
0
0
Kama mwezi tangu umepita Irene Uwoya alipoamuakuchora tatoo ya mume wake dogo janja kwa kuandika jina la Abdul ambalo ndio jina halisi la msanii huyo, mwanamuziki huyo nae ameamua kumjibu mke wake kwa kuchora tatoo  kwenye kwapa.

Kuchora tattoo inaweza isiwe ishu, stori ni eneo ambalo tattoo yenyewe imechorwa si kawaida. Kupitia Instagram Dogo Janja ameweka picha hiyo na kuandika; I made this infinity Promise for you @ireneuwoya8 #NoMoreDrama🌹.

Dogo Janja na Irene Uwoya waliripotiwa kufunga ndoa November 25, 2017, hata hivyo ni vigumu kutaja tarehe kamili kutokana na namna walivyoliweka suala hilo hasa kwa upande wa vyombo vya habari na mitandao.

Waziri Mkuu: Tumeanza kutafuta muwekezaji mwingine mradi wa mabasi yaendayo haraka (Udart).

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema ili kupunguza tatizo la usafiri jijini Dar es Salaam, Serikali itawashirikisha Chama cha Wamiliki wa Daladala (UWADAR) ili kuwa miongoni mwa watoa huduma katika mradi wa mabasi yaendayo haraka (Udart).

Akizungumza bungeni leo Mei 10,  Waziri Mkuu amesema wako wawekezaji wa ndani na nje wakiwamo Uwadar wenye uwezo wa kutoa huduma muhimu na Serikali inaendelea kuondoa changamoto zilizopo sasa na kupata mwekezaji mwingine atakayeingia magari na kuufanya usafiri huo kutoa huduma kwa ufanisi.

 Akijibu swali la Mbunge wa Kinondoni(CCM) Maulid Mtulia, Majaliwa, amesema:

“Ni kweli tuna mradi wa usafirishaji wa Udart, muungano wa Uda na Dart, Serikali inajua miundombinu yetu hasa pale makao makuu ya mabasi (Jangwani), mgogoro wa undeshaji, sehemu yoyote kunapokuwa na muungano wa taasisi mbili kunakuwa na changamoto.”

Katika swali la msingi, Mtulia alitaka kujua mikakati ya Serikali kutatua mgogoro ulipo baina ya kampuni ya Udart na Maxmalipo jijini Dar es Salaam ili kurahisisha usafiri kwa wakazi wa jiji hilo, Majaliwa amesema wanalifanyia kazi.

“Tunaingia awamu ya pili, tunaingia na mdau mwingine ili kuwa na ushindani zaidi,” amesema Majaliwa na kusisitiza kwamba ukiwa na mwendeshaji mmoja akipata tatizo mwingine anaendelea.

 Waziri Mkuu amesema iwapo itabainika mwendeshaji wa sasa akawa na matatizo  basi ataondolewa.

Mhandisi aliyetajwa na Rais Magufuli Chuo cha Mkwawa asomewa mashtaka na kunyimwa dhamana

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi, Iringa, imemnyima dhamana Mkurugenzi wa Kampuni ya MNM, Engineering Service Ltd, Mhandisi Godwin Mshana, kwa tuhuma za kujenga ukumbi wa Chuo Kikuu Mkwawa, (MUCE) chini ya kiwango.

Mshana alifikishwa leo Mei 10, Mahakamani hapo na kusomewa mashtaka matatu mbele ya Hakimu Mkazi wa Mkoa, Iringa, David Ngunyale.

Wakili wa Serikali, Blandina Mnyamba amemsomea mashtaka Mshana na kusema kuwa alitenda makosa hayo kati ya 2010 na 2012.

 Amesomewa mashtaka ya kughushi nyaraka za serikali, kujipatia fedha Sh 3 bilioni kinyume na utaratibu na shtaka la tatu ni kuhujumu uchumi katika matumizi ya Sh 2bilioni.

Dhamana ya Mshana imezuiwa na kesi hiyo itasikilizwa tena Mei 22 mwaka huu.

 Mei 2 mwaka huu, akiwa katika ziara Chuo Kikuu cha Muce, Iringa, Rais Magufuli aliagiza uchunguzi ufanyike katika ujenzi wa ukumbi wa mikutano wa chuo hicho, uliogharimu Sh 8 bilioni.

Pia, Rais Magufuli  aliagiza, aliyekuwa Mkuu wa chuo hicho, Profesa Philemon Mushi naye ahojiwe kuhusiana na ujenzi huo.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images