Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Shahidi adai gari lililobeba wanafunzi Lucky Vicent halikuwa na kibali

$
0
0
Shahidi wa nne upande wa mashtaka katika kesi inayomkabili mmiliki wa Shule ya Lucky Vicent, Innocent Mushi pamoja na makamu mkuu wa shule hiyo, Longino Nkana jana ameieleza Mahakama ya Wilaya ya Arusha kuwa gari lililobeba wanafunzi wa shule hiyo halikuwa na kibali cha kusafirisha wanafunzi.

Shahidi huyo, Allen Mwanri (48) ambaye ni ofisa mfawidhi wa Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) alisema gari hilo lilipewa leseni ya kusafirisha abiria kutoka wilayani Arusha kuelekea Mirerani Mei 16, 2016 na kiliisha Mei 15, 2017.

Mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo, Desdery Kamugisha shahidi huyo aliieleza mahakama kwamba kwa mujibu wa kumbukumbu za ofisi, haijawahi kupokea maombi yoyote ya kubadilisha matumizi ya leseni ya gari hilo tangu kumalizika kwa leseni yake.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi leo  ambapo shahidi mwingine upande wa mashtaka atafika mahakamani hapo kuwasilisha utetezi wake.

Wanafunzi 32 wa shule hiyo, walimu wawili na dereva Mei 6, 2017 walifariki dunia kwa ajali ya basi la shule hiyo eneo la Rhotia, Karatu mkoani Arusha wakati wakielekea Karatu ambako watoto hao walipaswa kufanya mtihani wa kujipima uwezo na wale wa Shule ya Tumaini.

Wakati kesi hiyo ikiendelea baadhi ya wazazi ambao watoto wao walifariki katika ajali hiyo walikuwa nje ya mahakama hiyo.

Shamsa Ford Amjia Juu Harmonize Kwa Kuingilia Ndoa Yake

$
0
0
Msanii wa Bongo fleva kutoka label ya WCB Harmonize amepokea makavu live kutoka kwa mwanadada anayefanya vizuri kwenye tasnia ya Bongo movie Shamsa Ford baada ya kumuorodhesha mumewe Chidi Mapenzi Kwenye orodha ya Wolper.

Siku ya jana Wolper, Harmonize na Sarah walikuwa kwenye vita kali ya Kwenye mitandao ya kijamii na katika harakati hizo Harmonize alianika orodha nzima ya wanaume ambao Wolper amewahi kujivinjari nao na mmoja kati ya watu hao ni Chidi Mapenzi.

Chidi Mapenzi ni mume halali kabisa wa Shamsa Ford kwahiyo baada ya kusikia mumewe katajwa Kwenye orodha hiyo alishindwa kujizuia kwani alikuja juu na kumtaka Harmonize amkome mumewe na asimuingize Kwenye ugomvi wao.

Shamsa alienda kukomenti maneno haya Kwenye posti ya Harmonize:

"Harmonize nakuheshimu sana mdogo wangu pls nisingependa kuona jina la mume wangu Kwenye huo ujinga wenu. Chidi kwenu anaweza akawa mshkaji kwangu mimi ni mume, kulikuwa hakuna haja ya wewe kuweka jina lake wakati unajua ana maisha mengine. Tusichukuliane Poa”.

Rais Trump ajitoa katika mkataba wa nyuklia wa Iran

$
0
0
Rais Donald Trump ametangaza kujitoa katika mkataba wa kimataifa wa Nyuklia wa Iran. Ameuita mpango huo kuwa umeoza na ni kero kwa raia wote wa Marekani.

Amesema mpango huo hauwezi kuleta amani hata kama Iran ikikubaliana na kila kitu kama sehemu ya utekelezaji wa mpango huo uliosainiwa mwaka 2015 chini ya utawala wa aliyekuwa rais taifa hilo Barack Obama.

Rais wa Iran amekosoa hatua ya Marekani kujitoa na kudai kuwa haiheshimu makubaliano yake. 

Akienda kinyume na mataifa ya Ulaya yaliyofikia makubaliano hayo,Trump amesema kuwa watarejesha vikwazo vya kiuchumi vilivyoondolewa dhidi ya Iran kupitia makubaliano hayo ya mwaka 2015.

Israel na Saudi Arabia kwa pamoja wamepongeza hatua hiyo.Vikwazo vipya vinatarajiwa kuanza dhidi ya Iran ndani miezi mitatu ijayo.

Trump awali alilalamikia mkataba huo kwamba ulikuwa unaiwekea Iran vikwazo kwa muda tu na kwamba ilishindwa kusitisha mpango wake wa makombora

Mloganzila Yazindua Kitengo Cha Kuchuja Damu

$
0
0
Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, Kampasi ya Mloganzila imezindua rasmi kitengo cha huduma ya uchujaji damu (dialysis) kwa wagonjwa wa figo.

Kitengo hicho kimezinduliwa jana  Mei 8 na Makatibu Wakuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mpoki Ulisubisya na wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Leonard Akwilapo.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Dk. Ulisubisya alisema kitengo hicho kimewekwa jumla ya mashine 12 na kwamba kitakuwa na uwezo wa kuhudumia zaidi ya wagonjwa 10,000 kwa mwaka wakiwamo wasio na maambukizi na wenye maambukizi.

“Kitengo hiki kinachoongozwa na madaktari bingwa wazoefu na wauguzi wenye ari, kitakuwa kituo-darasa cha tiba makini kwa wagonjwa wote, vile vile kituo hiki kitatoa mafunzo endelevu kwa madaktari wajao na kitakuwa chachu ya tafiti zenye kutoa miongozo ya matibabu na kuboresha sera za matibabu ya wagonjwa ya figo nchini,” alisema.

Naye, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk. Leonard Akwilapo amesema kwa kipindi cha miezi sita hadi sasa tangu kuzinduliwa kwa MAMC tayari jumla ya wanafunzi 350 wamepokea mafunzo mbalimbali ya udaktari na udaktari bingwa.

Israel Yasema Itamuua Rais Assad wa Syria

$
0
0
Mmoja  wa mawaziri walio katika Kamati ya Usalama ya Baraza la Mawaziri Israel amesema wanaweza kuupindua utawala wa Rais, Bashar al Assad na kumuua iwapo Iran itatumia ardhi ya Syria kuishambulia Israel.

Waziri huyo wa Nishati, Yuval Steinitz amenukuliwa na mtandao wa habari wa Israel, Ynet akisema Israel haijajiingiza katika vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria hadi sasa.

Lakini alionya iwapo Rais Assad ataendelea kuiruhusu Iran kuendesha shughuli zake katika ardhi ya nchi hiyo Israel itammaliza na kuundoa madarakani utawala wake.

Kadhalika Waziri huyo ameendelea kueleza ikiwa Rais Assad atairuhusu Iran kuigeuza Syria kambi ya kijeshi dhidi ya Israel anapaswa kufahamu huo utakuwa mwisho wake.

Israel na Iran zimekuwa zikishambuliana katika vita maneno kuhusu Syria tangu Februari mwaka huu 

Aprili 9 mwaka huu shambulio la anga liliua askari sita wa kikosi cha makomando cha Revolutionary Guards cha Iran kambini nchini Syria.

Tehran iliilaumu Israel na kuapa kulipa kisasi, kauli iliyojibiwa na Israeli kuwa itafanya mashambuilizi makubwa dhidi ya miliki za Iran nchini Syria.

Pia Waziri Steinitz alionekana kugusia kuwa kauli yake haiakisi sera ya Serikali ya Israeli, akisema: ‘Sizungumzii kuwapo mkakati wowote kumhusu.”

Hakukuwa na mwitikio wa haraka kutoka ofisi ya Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu wala Wizara ya Ulinzi Israel kuhusu kauli hiyo nzito.

Iran, wanamgambo wa Lebanon, Hezbollah na Urusi zimekuwa zikiimarisha usaidizi wao kwa Damascus dhidi ya uasi wa miaka saba nchini Syria.

Lakini Israel inahofia uwapo wa maadui wake Iran na Hezbollah utatengeneza jeshi nchini humo litakalotishia usalama wake.

Uingereza, Ufaransa, Ujerumani Zasikitishwa Na Maamuzi ya Trump Kujiondoa Mkataba wa Nyuklia wa Iran

$
0
0
Hatua ya Rais Donald Trump wa Marekani, ya kutangaza kwamba nchi hiyo inajiondoa kwenye mkataba wa kimataifa wa mpango wa kuizuia Iran kutengeneza silaha za nuklia, JCPOA, imepokelewa kwa hisia kinzani na wabunge wa Marekani na viongozi mbalimbali ulimwenguni kote.

Wabunge wengi wa chama cha Demokratik wameikosoa huku Warepublikan wakiisifu kama hatua ifaayo.

Speaker wa bunge, Paul Ryan, ambaye ni Mrepublikan, aliutaja mkataba huo kuwa ulikuwa na hitilafu kubwa.

Lakini kiongozi wa wachache kwenye bunge hilo, Nancy Pelosi alimshutumu Trump na kusema kwamba katika uamuzi wake, rais huyo hakutilia maanani ukweli kwamba mkataba huo ulikuwa unafanya kazi kama ulivyokusudiwa.

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, kupitia ujumbe wa Twitter aklisema kuwa nchi yake, Ujerumani na Uingereza "zimesikitishwa mno na hatua hiyo ya Trump."

Mapema Jumanne, Macron alisema kuwa Ufaransa itaendelea kuunga mkono mikakati ambayo itaimarisha usalama katika eneo hilo.

Katika hotuba iliyosubiriwa na wengi, RaisTrump alitangaza Jumanne kwamba ameamua kuiondoa Marekani kutoka mkataba wa kimataifa juu ya mpango wa kuizuia Iran kutengeneza silaha za nuklia, JCPOA.

Akizungumzia kutoka Ikulu, Trump alisema ataiwekea tena Iran vikwazo vikali vya kiuchumi vilivyondolewa wakati wa kufikiwa mkataba huo na mataifa mengine matano yenye nguvu duniani pamoja na Iran mwaka 2015.

Washirika wa Ulaya hasa Ufaransa, Uingereza na Ujerumani, wamekuwa wakijaribu kumshawishi kiongozi huyo kutochukua hatua hiyo ambayo wanasema ndio njia pekee ya kusimamia na kufuatilia harakati za nuklia za Iran.

Kabla ya hatua hiyo ya Trump, Iran ilikuwa imeeleza kwamba haingekubali kujadiliana tena juu ya mkataba mwengine na Marekani, na kwamba kwa kujiiondoa, Marekani ingekuwa inakiuka mkataba uliopo na kwamba itaendelea na mipango yake.

Wizara ya fedha ya Marekani ilitoa taarifa Jumanne kuwataka Wamarekani wote walioanza uhusiano na Iran chini na makubaliano hayo, kuanza kusitisha kazi zao.

Mbunge CCM Adai Kugawana Miradi ‘kimjomba Mjomba’ Kumewakosesha Maji Wananchi

$
0
0
Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ali Mohamed Kessy amesema anao ushahidi wa baadhi ya viongozi wakubwa waliomilikishwa miradi ya maji katika Mkoa wa Rukwa namna wanavyomshawishi ili asizungumze kuhusu ubadhirifu uliopo katika miradi hiyo.

Aidha, alisema kutokana na wakandarasi kupewa miradi kimjomba mjomba imesababisha wananchi wa Nkasi kukosa maji na kipindi cha masika huchimba maji kwenye madimbwi kama panya.

Kessy ametoa kauli hiyo jana Mei 8, bungeni jijini Dodoma wakati akichangia bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji ambapo pamoja na mambo mengine amesema viongozi hao wanapewa zabuni za miradi hiyo kiujanja ujanja.

“Awamu ya nne mkandarasi alipewa mabilioni ya fedha, miaka kadhaa sasa bwawa halina maji, wizara inaibiwa hela… na viongozi wakubwa ndiyo wenye miradi, kwa ushahidi wananitafuta ili nizungumze nao nawakatalia, eti mbunge nyamaza, ili waibe zaidi?” alisema.

Pamoja na mambo mengine, alisema katika mkoa huo kumejitokeza ujambazi kwa wakandarasi wa miradi ya maji katika baadhi ya vijiji vya Nkasi ambao hata Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Isack Kamwelwe na Naibu wake, Juma Aweso waliona namna serikali inavyoibiwa fedha.

“Mradi wa Kamwala, mkandarasi ameingia mkataba wa Sh bilioni 7.7 wakati uwezo mdogo, anao uwezo wa kutekeleza miradi ya thamani ya Sh 750 lakini akapewa kijomba mjomba.

“Maelezo bodi ya usajili wa wakandarasi yalieleza kuwa mkandarasi huyu hana sifa, Baraza la Madiwani Nkasi lilimkatalia lakini akapewa kimjomba mjomba,” alisema.

TMA yatabiri ujio wa mvua kubwa kwa siku tano

$
0
0
Mvua kubwa yatarajiwa kunyesha katika mikoa ya Dar es salaam, Tanga, Pwani na Visiwa vya Unguja na Pemba.

Utabiri huo umetolewa na Mamlaka ya Utabiri wa Hali ya Hewa Nchini (TMA), ambao umeeleza kuwa kiwango hicho cha mvua kilitarajiwa kuanza jana usiku.

Kwa mujibu wa utabiri huo kiwango cha mvua hiyo kitaendelea kwa siku tano hasa wanaoishi mabondeni, wametakiwa kuchukua tahadhari.

TMA imeeleza kwamba athari zinazoweza kutokea ni mafuriko ambayo yatasababisha msongamano wa magari na watu hali itakayochelewesha usafiri na usafishwaji maeneno ya mjini.

Aidha kwa siku ya jana asubuhi kulikuwa na wingu zito lililoashirijia ujio wa mvua kubwa, lakini haikunyesha mvua hiyo kama ilivyotarajiwa huku asubuhi ya leo majira ya saa kumi na mbili asubuhi katika baadhi ya maeneo jijini Dar es salaam imenyesha mvua ambayo imedumu kwa kipindi kifupi.

Mwendokasi kuhamishiwa stendi ya mabasi Ubungo

$
0
0
Halmashauri ya jiji la Dar es salaam ipo kwenye majadiliano ya kuhamisha kituo cha Mabasi yaendayo haraka Udart kilichopo jangwani na kuhamishia  kituo cha Mabasi yaendayo Mikoani Ubungo (UBT).

Hatua hiyo ni kutokana na eneo hilo la jangwani kukumbwa na mafuriko ya mara kwa mara hali inayosababisha kuharibika kwa magari hayo.

Kufuatia kikao cha kawaida kilichofanyika jana cha  Madiwani, Meya wa jiji la Dar es salaam, Isaya  Mwita amesema uamuzi huo umefikiwa kunusuru magari hayo yasiendelee kuharika.

Menejimenti ya kampuni ya UDART na viongozi wa jiji wapo kwenye majadiliano kuhusu suala hilo waweze kufikia mwafaka.

”kwa sasa tupo kwenye majadiliano kwa ajili ya  kuhamisha kituo cha mabasi yaendeyo kasi UDART cha Jangwani tuweze kukipeleka Ubungo kwa sababu eneo la jangwani limekuwa likikumbwa na mafuriko ya mara kwa mara mvua inapomyesha" alisema Mwita.

Alisema suala hilo linaendelea  kufanyiwa kazi na Halmashauri ya jiji hilo ipo kwenye mchakato wa kupanua Mto Msimbazi uweze kuwa na nafasi kubwa ya kusafirisha maji hadi baharini.

Kufuatia mvua zilizokuwa zinaendelea kunyesha jijini Dar es salaam, Jangwani ni moja ya eneo ambalo mara kwa mara limekuwa likikumbwa na mafuriko na kupelekea safari za mabasi ya mwendokasi kuhairishwa

Aidha kufuatia mvua zilizonyesha siku tatu zilizopita zimepelekea mabasi 29 kati 140 kuharibika na na kufanya baadhi ya wafanyakazi kupewa likizo mpaka marekebisho yatakapokamilika.

Lusinde adai serikali imeshindwa kudhibiti matumizi ya fedha

$
0
0
Mbunge wa Mtera kwa tiketi ya (CCM), Livingstone Lusinde amefunguka na kuiponda serikali kuwa inashindwa kusimamia mambo yake vizuri jambo ambalo linapelekea matumizi ya fedha kuwa makubwa huku miradi ikikwama.

Lusinde amesema hayo leo bungeni wakati akichangia hoja katika bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji na kusema kuwa serikali imekuwa ikishindwa kusimamia vizuri matumizi ya fedha jambo ambalo linazidi kuturudisha nyuma kimaendeleo.

"Waziri akinisikiliza vizuri anaweza kuona namna ambavyo serikali wakati mwingine inashindwa kusimamia matumizi mazuri ya fedha kwani ikisimamia vizuri fedha thamani ya fedha itaonekana na tutapata maji mengi na kwa uhakika 

"Kwa mfano watu wa WFP wametupa milioni mia saba tisini na tisa kwenye jimbo la Mtera, kwa fedha hizo hizo tumepata matenki makubwa ya lita laki nane matatu, tumepata visima kumi na nane, tumepata mashamba heka mia tatu kwa ajili ya umwagiliaji, tumepata visima kumi na mbili vilivyofungwa solar Power kwa ajili ya wananchi kupata maji hebu angalia matumizi haya ya fedha hizi yameleta vitu vikubwa ambavyo wananchi wananufaika lakini ukija kwenye serikali hakuna kitu"

"Kwenye serikali inatolewa bilioni moja pale Kwayungu kwa ajili ya kujenga bwawa la umwagiliaji mpaka sasa bwawa halijakamilika, hakuna miundombinu na bilioni imeliwa 

"Kwa hiyo unaweza kuona matumizi mabaya kwenye miradi ya maji kwa upande wa serikali ndiyo yanatuletea matatizo makubwa... hawa wametoa milioni 800 wametengeneza mambo ambayo ni maajabu kabisa.

" Mhe Waziri na Katibu Mkuu piteni muone namna ambavyo pesa ikisimamiwa hata ikiwa kidogo inaweza kufanya vitu vikubwa watu saizi wanapata maji ya kunywa, wanamwagilia na maisha yao yapo safi" alisisitiza Lusinde

Steve Nyerere: Michango ya Masogange haipewi familia

$
0
0
Msanii wa filamu bongo ambaye pia ni mchekeshaji maarufu Steve Nyerere, amefunguka juu ya tuhuma za kutofikisha fedha za michango zilizobaki kwenye msiba wa Agness Masogange, na kusema kuwa pesa hizo haziwezi kupewa familia.

Steve Nyerere amesema kwamba pesa hizo ambazo zimetajwa kuwa milioni mbili zimekusudiwa kumsaidia mtoto wa marehemu Sania, atakapoanza kidato cha kwanza hapo mwakani,

Steve Nyerere ameendelea kwa kusema kwamba familia ya Agness inapaswa kushukuru kwa mchango wao walioutoa kumzika ndugu yao, na sio kuanza kuulizia masuala ya pesa, kwani pesa hizo si kwa ajili yao bali ni kwa ajili ya mtoto.

Mchungaji Msigwa, Naibu Spika 'Wavurugana' Bungeni

$
0
0
Mvutano umeibuka bungeni kati ya mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson.

Mvutano huo umeibuka leo Mei 9, 2018 baada ya Mchungaji Msigwa kutakiwa kufuta maneno aliyoyazungumza kuhusu utendaji wa Rais John Magufuli  katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji mwaka 2018/19.

Mbunge huyo alianza kuzungumzia kero za maji majimboni, kueleza jinsi wabunge wengi wanavyolalamikia jambo hilo na kubainisha kuwa kama ni suala la uwajibikaji wa Serikali, inapaswa kuundwa tume.

Huku akitolea mfano kukosekana kwa maji ni sawa na wananchi kula uchafu, wakiwemo watalii na huenda wote wakapata ugonjwa wa kipindupindu, Mchungaji Msigwa aliingia katika mvutano huo baada ya kudai kuwa tatizo la maji ili litatuliwe ni mpaka Rais John Magufuli apige simu kwa Katibu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji.

“Yaani tatizo la maji hadi Rais apige simu kwa katibu wa wizara, aunganishwe na mtendaji wa kijiji, hii inaoyesha mfumo umekwama,” amesema.

Amesema katibu huyo wa wizara amejikita mitandaoni kujibizana na maaskofu badala ya kutafuta ufumbuzi wa maji.

Wakati akiendelea kuchangia, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama alisimama na kusema kwa mujibu wa kanuni ya 64, mbunge hatozungumzia utendaji wa Rais ndani ya Bunge.

“Madaraka aliyopewa Rais ni ya kikatiba, anaweza kusimamia jambo lolote, kwa utaratibu wowote anaoona unafaa kwa muktadha wa Watanzania. Na kanuni zinatufunza tusizungumzie mienendo ya Rais,” amesema Mhagama.

“Tukiacha liendelee kama anavyofanya Mchungaji Msigwa si sawa na tunavunja Katiba, ninaomba aheshimu kanuni ya 64 (1)(e) ya Bunge na kama itakupendeza Naibu Spika hayo anayozungumza afute.”

Baada ya maelezo hayo, Naibu Spika alisimama na kumtaka Mchungaji Msigwa kufuta maneno hayo.

Hata hivyo, Mchungaji Msigwa amesema hajui afute maneno gani jambo ambalo lilimnyanyua tena Dk Tulia, “kama hujui ufute yapi, futa mchango wako wote uliochangia na uanze moja.”

Agizo hilo lilipingwa na Mchungaji Msigwa na kuendelea kuchangia kitendo ambacho Dk Tulia hakukubaliana nacho na kumtaka aketi huku akimuita mbunge mwingine kuendelea na mjadala wa bajeti ya wizara hiyo.

Mwanasayansi kuuliwa na sindano ya sumu kesho

$
0
0
Mwanasayansi aliyesafiri kutoka Australia mpaka Uswiss David Goodall,  kwa ajili ya kuukatisha uhai wake kesho inatarajiwa kuwa ndiyo siku ya kuhitimisha maisha yake ya duniani baada ya madaktari kuchomeka sindano ya sumu katika mshipa.

Kesho, madaktari wanatarajiwa kuweka sindano iliyojazwa dawa ya sodium pentobarbital katika mshipa wa Mwanasayansi huyo mkongwe duniani na kumuacha aisukume mwenyewe kwenda mwilini mwake.

Goodall amelazimika kusafiri kutoka Australia mpaka Basel, Uswisi kukifuata kifo baada ya sheria za kwao kutomruhusu kufanya hivyo.

Akihojiwa na shirika la utangazaji la Marekani CNN, Goodall amesema maisha yake hayana thamani tena ndio maana ameamua kuomba kujiua akiamini hadithi yake itakuwa mfano na kuhamasisha uamuzi kama huo kwa wengine waliochoka kuishi.

Katika mahojiano Goodall amenukuliwa akisema "Natamani ningekuwa na uwezo wa kutembea mashambani na kuona vitu vinavyonizunguka. 

"Katika umri huu naamka asubuhi, nakunywa chai. Nasubiri mchana nile halafu sina cha kufanya tena. Maisha ya aina hii ya kazi gani?

Goodall aliyezaliwa katika Jiji la London Aprili 1914, anatarajia kufa akiwa na miaka 104 ambapo ameweka wazi kuwa maisha yake yalisimama miaka 10 iliyopita baada ya kupoteza uoni na uwezo wa kutembea na alitamani kama kifo kingemchukua katika miaka hiyo.

Serikali yafunguka suala la elimu bure Kidato cha Tano na Sita

$
0
0
Serikali ya awamu ya tano kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesema haina mpango wowote kwa sasa kutoa elimu bure kwa ngazi ya kidato cha tano na sita nchini bali wamejipanga katika kuboresha miundombinu pamoja na kutoa elimu iliyo kuwa bora.

Kauli hiyo imetolewa leo Mei 09, 2018 na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. William Ole-Nasha Bungeni Jijini Dodoma kwenye kikao cha 25 mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge Edwin Mgante Sanda aliyetaka kujua ni lini serikali itatekeleza suala la elimu bure kwa kidato cha tano na sita ambalo ni kundi pekee lililobaki kugharamiwa na serikali.

"Serikali imeweka kipaumbele cha kuhakikisha fursa sawa ya kutoa elimu kwa ngazi ya awali 'msingi na sekondari' kwa sababu hii ndio ngazi ya elimu ambayo humpatia muhusika stadi za msingi ambazo ataweza kukabiriana na mazingira yake. Dhana ya elimu bila malipo inazingatia uendeshaji wa shule bila ya ada wala michango ya aina yeyote ya lazima kutoka kwa wazazi au walezi", amesema Ole-Nasha.

Pamoja na hayo, Ole-Nasha ameendelea kwa kusema "kwa sasa serikali haijaandaa mpango wa elimu bure 'bila malipo' kwa ngazi ya kidato cha tano na sita bali inaelekeza jitihada zake za kuboresha miundombinu na ubora wa elimu kwa ngazi zote za elimu nchini ikiwemo elimu ya kidato cha tano na sita".

Kwa upande mwingine, Naibu Waziri Ole-Nasha amesema mpango wa elimu bila ya malipo nchini kutoka shule ya msingi hadi sekondari umeweza kuonesha mafanikio makubwa katika sekta ya elimu tangu ulipoanza mwaka 2016.

Mbunge CHADEMA Ahoji MAFISADI Kuhamishwa Vituo vya Kazi Badala ya Kutumbuliwa

$
0
0
Mbunge wa Tarime Mjini (Chadema) Esther Matiko amesema Serikali imeshindwa kuchukua hatua kwa watendaji ambao miradi wanayoisimamia imegubikwa na ufisadi na badala yake imekuwa ikiwahamishia maeneo mengine.

Akichangia katika bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji kwa mwaka 2018/19, Matiko amesema kuwa kuna mradi wa Geita ambao ulitumia Sh 6.6 bilioni lakini umeshindwa kutoa maji.

“Ufisadi umekithiri katika miradi ya maji nchini hata hizo fedha kidogo zinazoenda katika miradi ya maji bado zinaliwa. Serikali imekuwa ikisema inapambana na ufisadi lakini hatuoni hatua zikichukuliwa kwa wanaokula fedha za miradi ya maji matokeo yake huyu mtendaji wa Geita mlimchukua mkamhamishia wizarani,”amesema.

Amesema anaungana na wabunge wenzake waliotaka kuundwa kwa kamati ya Bunge ya kuchunguza miradi ya maji kama ilivyokuwa katika maeneo mengine yaliyowahi kuchunguzwa na kamati za Bunge.

“Asilimia tano ya watu ndio wanatumia ndege. Hivi kipaumbele ni ndege ama maji ambayo yanatumiwa na watu asilimia 100?”Amehoji.

Amesema maji ni uchumi, kwamba viwanda haviwezi kujengwa bila kuwa na maji, “ukiwezesha Watanzania kuwa na maji, mambo mengine yatafanikiwa yenyewe.”

Nkamia Adai Kwenye Miradi ya Maji Kuna Ufisadi Kushinda wa Makinikia

$
0
0
Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia (CCM), ameliomba Bunge kuunda tume maalumu kuchunguza miradi ya maji nchi nzima kwa kuwa kuna ubadhirifu zaidi ya uliokuwa kwenye mchanga wa dhahabu (makinikia).

Pia amesema baadhi ya miradi ya maji katika jimbo la Chemba amepewa Ofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) hali inayothibitisha namna gani kulivyo na ubadhirifu.

Nkamia ametoa kauli hiyo leo bungeni jijini Dodoma wakati akichangia majadala wa hotuba ya bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji na kuongeza kuwa licha ya kutoa maombi mwaka jana kuhusu kuundwa kwa tume hiyo sasa anarejea kuliomba Bunge litekeleze ombi lake kwa kuwa hatua alizoanza kuchukua na Rais John Magufuli dhidi ya ubadhirifu huo wa miradi hazitoshi.

“Tusimuachie rais peke yake, Bunge lina nafasi kama mhimili na wakati tume inaundwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ijiandae kupanua magereza. Miradi mingi kwa sisi wabunge tuliotoka vijijini imekuwa ‘dili’ tu.

“Kwa mfano pale Chemba kuna miradi mitatu, mmoja wapo amepewa Ofisa wa Takukuru, mimi nimekutana naye ‘site’ ndiye mkandarasi aliyepewa mradi. Kule Kiremba kuu mradi huo nao umechezewa tu halafu humu ndani tunaonekana hovyo,” amesema.

Bunge: Si Lazima Kutoa Video Za Wabunge

$
0
0
Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson amesema Kitengo cha Habari cha Bunge hakilazimishwi kutoa taarifa za video za wabunge zinazorekodiwa wakati wakichangia mijadala mbalimbali ndani ya Bunge hilo.

Dk. Tulia ametoa kauli hiyo leo Mei 9, wakati akijibu mwongozo wa Mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali (Chadema), aliyehoji nani anayetoa amri kwa kitengo hicho kukata kwa asilimia 90 maelezo ya video za wabunge wanaochangia mijadala mbalimbali bungeni.

Lijualikali amesema licha ya kwamba wabunge wanaongozwa kwa kanuni kuzungumza na hakuna amri ya kufuta kauli unayozungumza bungeni hadi mwisho inashangaza kuona kwenye vipande vya video wananyimwa au inakatawa.

“Unapewa ‘hansard’ iliyokamilika, lakini cha ajabu watu hao wa hansard tunapoenda kuomba video zetu ambazo tumeongea humu bungeni, zinakuwa zimekatwa kwa asilimia 90 hawa wanaokata hotuba zetu wanakata kwa amri ya nani, wakati mbunge nimeongea na kiti kimeniruhusu niongee hadi nimemaliza, anayekata, anakata kwa amri ipi na kwa maelekezo ya nani, naomba mwongozo,” amesema.

Akijibu mwongozo huo, Dk. Tulia alisema taarifa rasmi za Bunge huchapwa na mbunge kukabidhiwa, lakini utaratibu wa bunge kutoa clip za wabunge  hiyo hutegemea utashi wa kitengo cha habari.

“Kwa hiyo kuna wakati wanaweza wasikupe na hawalazimiki kufanya hivyo, kwa hiyo kama kuna jambo lolote ambalo umeenda kuomba na hawajakamilisha waambie unaomba muda wako wa dakika 10 kama labda wamekupa dakika mbili badala ya 10 waambie unahitaji zote.

“Sasa inategemea ninyi mmetumia utaratibu upi kuzipata hizo taarifa lakini taarifa rasmi za Bunge ni zile zilizoandikwa na si hizi tunazozungumza. Huo ndiyo utaratibu tulio nao,” amesema.

Bunge Laikomalia Serikali Kodi Ya Tende

$
0
0
Bunge limeendelea kuibana Serikali itekeleze agizo la kuondoa kodi kwenye tende ili kuwawezesha waumini wa dini ya kiislamu kupata bidhaa hiyo kwa urahisi katika kipindi cha mfungo wa Ramadhani.

Kauli hiyo imetolewa leo bungeni jijini Dodoma na Naibu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson wakati akitolea ufafanuzi mwongozo ulioombwa na Mbunge wa Mchinga (CUF), Hamidu Bobali.

Bobali aliliomba Bunge kujadili hoja hiyo kwa muda wa dakika 30 kwa kuwa licha ya wabunge kadhaa akiwamo Mbunge wa Ubungo, Saed Kubene (Chadema) na Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM), kuiomba serikali iondoe kodi kwenye tenda katika vikao vilivyopita, bado serikali haijatekeleza.

Amesema tende katika nchi za Kenya, Zanzibar na Msumbiji zimefutiwa kodi lakini inashangaza kwa upande wa Tanzania bado haijafutiwa kodi.

“Sasa mwezi wa Ramadhani unaanza wiki ijayo na makontena yapo kwenye meli bandarini ambayo yametolewa kwa msaada wa mali za wakfu, watu wanajichangisha mali za wakfu zinaletwa na wao wanatafuta thawabu. Sasa naliomba Bunge walau nusu saa, kwa sababu jambo hili linaiaibisha Tanzania,” amesema.

Akitolea ufafanuzi huo Dk. Tulia alisema kwa kuwa jambo hilo limeshazungumzwa na utaratibu wake upo kisheria, serikali haina wajibu wa kutekeleza.

“Nadhani serikali ifanyie kazi jambo hili ione namna bora ya kushughulikia, kama ambavyo Bobali ametaja mifano ya huko kwingine sijasoma sheria zao.

“Lakini sheria tunatunga wabunge, ila watekelezaji serikali, upande wa watekelezaji muangalie namna ya kushughulikia jambo hili ili mwezi wa Ramadhani unapokuja wenzetu wenye imani ya kiislamu  waweze kupata hizo huduma ambazo zipo kiutaratibu,” amesema.

Tanzania yaanza majaribio dawa kinga ya Ukimwi

$
0
0
Serikali imesema tayari nchi imeanza rasmi majaribio ya dawa kinga mpya inayozuia maambukizi ya virusi vya Ukimwi (PrEP), huku ikikanusha kuwapo kwa dawa inayotibu ugonjwa huo.

Dawa kinga hiyo mpya  ina uwezo wa kuzuia maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) ikiwa mtumiaji atameza kila siku kwa muda wa siku saba kabla hajashiriki tendo la kujamiiana, ataendelea kumeza kwa kipindi chote atakachokuwa katika hatari ya kuambukizwa.

Hayo yamesemwa leo Mei 9, 2018 mjini Dodoma na naibu waziri wa Afya, Dk Faustine Ndugulile wakati  wa uzinduzi wa mpango wa nne wa VVU na Ukimwi katika sekta ya afya (HSHSP IV 2017-2022) sambamba na maadhimisho  ya miaka 30 ya Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi.

Amesema taarifa kwamba nchi inazindua tiba dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi, si sahihi kwani Tanzania haijapata tiba hiyo.

"Kinachoendelea tumezindua dawa kinga, kuna dawa ambayo tunataka tuielekeze katika makundi ambayo tunayaona yapo kwenye hatari ya kuambukizwa virusi vya Ukimwi, watapatiwa kwa lengo la kuwakinga wasipate,” amesema Dk Ndugulile na kuongeza:

“ila sio suluhisho na tuseme vilevile kwamba hatujapata tiba ya virusi vya Ukimwi na utaratibu huu wa dawa kinga, ndiyo inaanza majaribio sasa  na haijaanza kupatikana.”

Dawa hizo mpya zenye uwezo wa kukinga maambukizi dhidi ya VVU kwa asilimia 99, zilizoanza kutumika katika baadhi ya nchi za Kusini mwa Afrika, zinakuja wakati ukanda huo ukiongoza duniani kwa kuwa na asilimia 50 ya waathirika wote duniani.

Utafiti uliofanywa na mwanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha London, Dk Sheena McCormack umeonyesha kuwa PrEP inazuia maambukizi ya Ukimwi kwa kuua virusi baada ya kufanyiwa majaribio na kundi la wapenzi wa jinsia moja, ambao wamo katika hatari zaidi ya maambukizi.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetambua kwamba dawa hiyo ya tembe inaweza kupunguza maambukizi kwa kiwango kikubwa.

aziri Mkuu Majaliwa atoa siku tatu kwa wafanyabiashara kusambaza mafuta ya kula nchini

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa siku tatu kwa kampuni za mafuta ya kula nchini kuingiza bidhaa hiyo sokoni na kuonya kuwa baada ya muda huo kupita, Serikali itapita viwandani na katika bohari za mafuta kufanya tathmini.

Majaliwa ametoa kauli hiyo leo jioni Mei 9, 2018 bungeni mjini Dodoma alipokuwa akijibu agizo la Spika wa Bunge, Job Ndugai ambaye jana aliitaka Serikali kutoa majibu kuhusu madai ya kupanda kwa bei ya mafuta baada ya baadhi ya wabunge kuhoji jambo hilo na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage kutoa majibu ambayo hayakumridhisha.

“Serikali tunatoa siku tatu kuanzia kesho kwa mafuta yote yaliyoko katika bohari kuu ambayo tunajua yapo ili Watanzania wasihangaike kununua kwa bei ya juu, mafuta yaliyoko bandarini yanaendelea na taratibu zake,”amesema Majaliwa.

Amesema Serikali itaendelea kuzungumza na wafanyabiashara walio na mafuta bandarini kuondoa mafuta yao ili yaweze kusambaa sokoni ili watu wapate mafuta.

“Kuanzia Jumapili tutalazimika kuingia viwandani na kuhakiki kama mafuta yapo ama hayapo,”amesema.

Awali, Mwijage amesema mahitaji ya mafuta nchini ni kati ya tani 400,000 hadi 450,000 na kwamba vyanzo vya mafuta nchini vinatosheleza asilimia 30 ya mahitaji huku asilimia 70 ikiagizwa kutoka nje ya nchi.

Amesema mafuta yanayoagizwa kutoka nje ya nchi ni yaliyosafishwa na yale ambayo hayajasafishwa.

Amesema mwaka jana kampuni binafsi ambazo ndizo zinazoingiza mafuta kwa ajili ya kusafisha katika viwanda vilivyoko nchini, yaliingiza tani 344,369.5 ikiwa ni wastani wa tani 28,697 kwa mwezi.

Amesema Januari hadi Machi, 2018 kiasi kilichoagizwa cha mafuta kutoka nje ya nchi ni tani 30,210.71 na kwamba kwenye hifadhi kuna tani 68, 902 za mafuta.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images