Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Rais Magufuli: Wafadhili wanne Wamejitokeza mradi wa reli ya kisasa

$
0
0
Rais John Magufuli amesema zaidi ya wafadhili wanne wamejitokeza kutaka kufadhili mradi ujenzi wa reli ya kisasa baada ya Serikali kuanza mchakato huo peke yake.

Reli hiyo ya kisasa maarufu kama 'standard gauge' inajengwa kutoka Dar es Salaam, Morogoro hadi Dodoma.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo Mei 2, 2018 wakati akizungumza na wanafunzi na wafanyakazi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Mkwawa mkoani Iringa.

Amesema fedha zilitokana na kuwabana mafisadi ambao hivi sasa wanamchukia kutokana na msimamo wake.

"Wameshatujua sisi ni wanaume ndiyo maana wamejitokeza kutaka kufadhili mradi huu ambao wakandarasi wameshapatikana na wapo eneo la kazi," amesema Rais Magufuli.

Serikali Yasema Nondo akishinda kesi Atarejea chuoni

$
0
0
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesema mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, (UDSM) Abdul Nondo amesimamishwa masomo ili kulindwa, asipoteza sifa za kuwa mwanafunzi wa chuo hicho.

Kusimamishwa chuo kwa Nondo, kuliibua mjadala mkali wakati wa kuijadili bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wakidai hatua hiyo ni aibu kwa chuo hicho.

Akijibu hoja hiyo leo Mei 2, 2018 bungeni mjini Dodoma, Naibu Waziri wa wizara hiyo, William Ole Nasha amesema kwa kuwa Nondo ana kesi kama akishinda anarejea chuoni na sheria inamlinda badala ya kumminya asipoteze sifa.

Waziri wa Elimu Atoa Maagizo NACTE, TCU

$
0
0
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako ameagiza Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Baraza la Vyuo vya Ufundi (Nacte) kufanya mapitio upya ya nyenzo wanazotumia kukagulia ubora wa vyuo.

Profesa Ndalichako amesema vikibainika havina ubora wavifungie mara moja hata kama ni vya Serikali.

Akijibu hoja za wabunge leo Mei 2, 2018 bungeni mjini Dodoma walipojadili bajeti ya wizara yake ya mwaka 2018/19 amesema kuna baadhi ya wabunge wamelalamikia kuhusu wahitimu wa vyuo kushindwa kuandika wasifu.

“Nacte na TCU wamekuwa wakifungia vyuo vingi sana, lakini tatizo badi lipo, kwa hiyo naviagiza vyombo vya udhibiti wa elimu kufanyia mapitio upya ya nyenzo za ukaguzi ikiwemo sifa za walimu, mitihani inayotolewa na usahihishaji wao,” amesema Profesa Ndalichako.

“Iwapo watabaini havikukidhi ubora wavifungie bila kuogopa mtu yeyote hata kama vikiwa vya Serikali, vifungiwe.” ameongeza

Waziri huyo amewaagiza maofisa elimu nchini kusimamia kwa karibu ubora wa elimu katika shule zilizopo katika maeneo yao huku akidai kitendo cha kumfukuza mwalimu mkuu na kumuacha ofisa elimu wa eneo husika ni uonevu kwa sababu wao ndiyo wanapaswa kusimamia ubora wa elimu.

“Utakuta ofisa elimu ana shule tano tu lakini anashindwa kuzisimamia na Serikali haitakubali kuwa na viongozi mizigo,” amesisitiza Waziri huyo.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya May 3

Startimes Kurusha Na Kutangaza Kombe La Dunia Kwa Kiswahili

$
0
0
KAMPUNI ya Star Media (T) Ltd yenye chapa ya StarTimes imetangaza rasmi kurusha matangazo ya Kombe la Dunia Urusi mwaka 2018 Mubashara kupitia king’amuzi chake. 

StarTimes imethibitisha kuonesha michuano hiyo jana  katika hafla fupi iliyofanyika Terrace, Slipway Masaki jijini Dar es Salaam na kushirikisha waandishi wa Habari pamoja na wadau mbalimbali wa soka nchini.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Meneja Masoko wa Kampuni hiyo David Malisa alisema “Mwaka huu katika Kombe la Dunia la 21, StarTimes ni mrushaji rasmi wa michuano hiyo itakayoanza Juni 14 hadi Julai 15 nchini Urusi. Mechi zote 64 zitakazochezwa Urusi katika Kombe la Dunia zitarushwa moja kwa moja.

” Amefafanua mbali na kurusha tu michuano hiyo maarufu zaidi Duniani, StarTimes watarusha matangazo ya michezo yote katika lugha ya Kiswahili na hiyo ni katika jitihada za kuienzi na kuikuza   lugha ya Kiswahili lugha ambayo ni maarufu zaidi katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.

“StarTimes tutarusha matangazo ya Kombe la Dunia, mechi zote 64 katika lugha ya Kiswahili pamoja na uchambuzi utakaoambatana na mechi hizo, uchambuzi utakaofanywa na wachambuzi mahiri na tuliowazoea hapa nchini”, ameongeza David.

Sambamba na kuzindua Kombe la Dunia, StarTimes pia wametangaza ofa kwa wapenzi wa soka, ambapo wateja watakaonunua king’amuzi au Luninga zao za kidigitali kati sasa na Juni 30 watapatiwa kifurushi cha juu hadi Julai 31 mwaka huu bure.

Rais Magufuli Anatarajia Kuwa Mgeni Rasmi Tuzo Za hirikisho la Wenye Viwanda nchini (CTI) Mei 4

$
0
0
Mkurugenzi mtendaji wa Shirikisho la Wenye Viwanda nchini (CTI), Leodegar Tenga amesema baadhi ya wenye viwanda wana hofu ya kushiriki shindano la mzalishaji bora wa mwaka wakidhani wataharibu masoko yao iwapo hawatashinda.

Hata hivyo, Tenga aliwatoa hofu kwamba tuzo hizo hazina uhusiano wa moja kwa moja na ubora wa bidhaa, bali wanaangalia vigezo vingine muhimu katika uzalishaji na namna wenye viwanda wanavyoweza kujifunza kutoka kwa wenzao.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Tenga alisema katika tuzo za Rais za mzalishaji bora wa mwaka 2017 zinazotarajiwa kufanyika Mei 4, ni wenye viwanda 36 waliojitokeza kushiriki shindano hilo.

Tenga alibainisha kuwa mwitikio umeongezeka kidogo ikilinganishwa na mwaka jana, lakini akasisitiza kwamba kampuni kubwa hazitaki kushiriki kwa kuhofia kuharibu taswira iwapo hazitashinda.

“Changamoto kubwa ni hawa wazalishaji wakubwa, ukiwafuata wanakwambia hawatashiriki wakihofia kuharibu taswira za kampuni zao,” alisema Tenga na kuongeza:

“Tunajitahidi kuwaeleza kuwa mashindano hayo ni muhimu kwao na hayahusiani na ubora wa bidhaa zao hivyo wanatakiwa kushiriki kuonyesha ukuaji wa uzalishaji wao.”

Awali, mwenyekiti wa CTI, Dk Samwel Nyantare alisema kwamba tuzo hizo zitatolewa kwa sekta 17 zinazotambulika kimataifa na mwaka huu wameongeza sekta moja ya matumizi bora ya nishati.

Alizitaja baadhi ya sekta zitakazoshindaniwa kuwa ni vinywaji, ujenzi, kemikali, nishati, plastiki, fedha, mbao na samani, chuma, magari, usafirishaji, karatasi, dawa na vifaatiba, nguo na bidhaa za madini.

Naye mkurugenzi wa machapisho na mawasiliano wa CTI, Thomas Kimbunga alibainisha kuwa vigezo vilivyotumika kuwapata washindi wa kila sekta ni pamoja na utendaji wa kiuchumi, utendaji wa kiteknolojia, matumizi ya nishati, uuzaji bidhaa nje ya nchi, usalama sehemu ya kazi na kuzingatia masuala ya kijamii.

Kuhusu mshindi wa jumla, Kimbunga alisema kwamba wataangalia vigezo vingine kama mizania ya jinsia kwenye ngazi ya utawala, uhifadhi wa mazingira, uhusiano mzuri, kuzingatia viwango vya ubora na uhusiano na sekta nyingine za uchumi.

Rais Magufuli Anusa Ufisadi wa Bilioni 8 Ukumbi wa Chuo cha Mkwawa....Atoa Maagizo Mazito Kwa Vyombo vya Dola

$
0
0
Rais John Magufuli amefichua siri ya kukataa kuweka jiwe la msingi katika ukumbi wa jengo lililopo katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Mkwawa mkoani Iringa akisema limejengwa kifisadi kwa Sh 8bilioni.

Rais ameeleza hayo jana, Mei 2, 2018 wakati akizungumza na wafanyakazi na wanafunzi wa chuo hicho ikiwa ni sehemu ya ziara yake mkoani humo.

"Muda mwingine tuambizane ukweli Chuo cha Mkwawa kimeniangusha, ndio maana nilikataa kuja kuweka jiwe la msingi katika lile jengo. Siwezi kuweka jiwe la msingi katika jengo la kifisadi.

"Nikitoka hapa nitakwenda kulikagua. Nilitegemea chuo hiki kitasimamia value of money (thamani ya fedha), kwa sababu kuna wasomi lakini tofauti."

Rais Magufuli alitumia nafasi hiyo kuviagiza vyombo vya dola kuhakikisha wanawachukulia hatua wale wote waliohusika katika mchakato huo hata kama wamestaafu, watafutwe waliko.

"Mmeshindwa kusimamia ujenzi wa lile jengo halafu leo mnaniomba mabweni? Nitaanzaje kuwakubalia wakati huku mmeshindwa, siwezi. Vyombo vya dola  na wizara vifuatilie mkishindwa nitafuatilia.

Watu 225 Huambukizwa UKIMWI kila siku

$
0
0
Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kwa kushirikiana na Tume ya kuthibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) inatarajia kuzindua zoezi la upandaji wa mlima Kilimanjaro (Kilimanjaro Challenge 2018),  na kuendesha harambee ya kuchangisha fedha kwa mwaka 2018 kwa ajili ya afua za UKIMWI nchini. 

Shughuli hii inatarajiwa kufanyika tarehe 4 Mei 2018 mwaka huu katika Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro iliyopo jijini Dar es Salaam.

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Mhe. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ambapo atafanya zozezi la ugawaji wa fedha zilizokusanywa mwaka jana 2017 zilizopatikana baada ya wadau mbalimbali kupanda na  kuendesha baiskeli kwa kuzunguzuka Mlima Kilimanjaro .

Kilimanjaro Challenge against HIV & AIDS ni mfuko unaochangia juhudi za serikali  katika mapambano dhidi ya UKIMWI na kutoa elimu kwa jamii kuhusu maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI (VVU).

Kilimanjaro Challenge ni mfuko muhimu unaoshirikiana na taasisi za nje na ndani ya nchi katika kuendeleza mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI kwa jamii ya Kitanzania na Dunia kwa ujumla ili kuwapa matumaini ya kuhakikisha jamii inabaki bila kuathiriwa na VVU/UKIMWI katika miaka ijayo.

Mfuko huo pia unalenga kuisaidia Serikali kukabiliana na VVU//UKIMWI sambamba na kutoa nafasi kwa watalii wa ndani na nje kuupanda mlima Kilimanjaro.

Takwimu zilizotolewa na Tume ya Kuthibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), zimeonesha kupungua kwa maambukizi ya virusi vya UKIMWI kutoka asilimia 5.1 %  mwaka 2011/ 2012 hadi asilimia 4.7% mwaka 2016/17.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dkt. Leonard Maboko anasema, “ Mwaka wa 2016, inakadiriwa kuwa watu milioni 1.5 nchini wanaoishi na VVU na UKIMWI hadi sasa watu 225 wanapata maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa siku. 

"Ugonjwa huu umewaathiri zaidi vijana na watoto yatima zaidi. Tunahitaji kubadilisha hali hii. Lengo la kukusanya fedha ni kuweza kusaidia serikali ya Tanzania katika jitihada zake kufikia sifuri tatu. 

"Sifuri katika maambukizi mapya, sifuri ya unyanyapaa, sifuri katika vifo vitokanavyo na UKIMWI. TACAIDS kwa kushirikiana na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) na wadau wengine kwa kupitia mpango huu wa Kili Challenge tunapenda kutoa mchango na ushirikiano wetu kwa Taifa ili kutunisha mfuko utakaowezesha kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa huu. 

"Tuna matumaini ya kujenga timu imara yenye hamasa ya kupambana na janga hili. Tunatoa wito kwa makampuni na wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi, wajitokeze ili tusaidiaane kutunisha mfuko wa Kili Challenge na mwishowe kufikia malengo yetu ya kuhakikisha tunakuwa na kizazi kisicho na maambukizi ya VVU/ UKIMWI,” alisema Dkt. Leonard Maboko.

“Watoto watakaoshiriki katika zoezi la Kilimanjaro Challenge mwaka huu ni wa kiume na wa kike wenye umri kuanzia miaka 13. Watoto hao yatima kutokana na tatizo la VVU/ UKIMWI wamesaidiwa na Kituo cha kulea watoto yatima cha Moyo wa Huruma Orphanage Center kilichopo Geita.

"Changamoto kubwa inayotokana na janga hili ni pamoja na maelfu ya watoto yatima wanaohitaji misaada baada ya wazazi wao kufariki, wajane wasiokuwa na kipato, pamoja na wazee wanaolazimika kuwalea wajukuu walioachwa na watoto wao ambao walifariki kutokana kwa ugonjwa huo."

Waziri Mpango akiri ongezeko la umaskini Nchini licha ya utajiri wa rasilimali

$
0
0
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema licha ya utajiri wa rasilimali uliopo nchini wananchi wameendelea kuwa maskini.

Akizungumza jana Mei 2,  wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa taasisi ya utafiti wa uchumi na jamii (ESRF) Dar es salaam, Dk Mpango aliyemwakilisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitaja sababu kubwa kuwa ni kutokuwepo kwa uwiano kati ya ukuaji wa uchumi na sekta ya Kilimo.

“Tanzania ni tajiri wa rasilimali. Tunayo maziwa kama Victoria, Tanganyika, Rukwa, Nyasa na mito mingi inayotoa fursa za uvuvi na uzalisha wa umeme. Tuna utajiri wa madini kama dhahabu, almasi, Tanzanite, ruby, bati, chuma, mkaa, uranium, gesi ya asili, helium na mengineyo,” alisema Dk Mpango.

Aliongeza kuwa Tanzania ni kituo kikubwa cha utalii ikiwa na urefu wa kilometa 1,200 za fukwe za bahari, hifadhi za wanyama, huku  ikiwa nchi ya amani na utulivu isiyokuwa na machafuko ya kikabila.

“Hata hivyo, uporaji wa maliasili umesababisha maisha ya Watanzania walio wengi kuwa masikini, huku wachache wakifaidi rasilimali hizo,” alisema Dk Mpango.

Alitaja chanzo cha matatizo hayo kuwa pamoja na ukosefu wa teknolojia ambapo alitoa mfano wa wachimbaji wadogo wa madini wanaoshindwa kupata madini ya kutosha kwa kutokuwa na teknolojia.

Bill Nass na Nandy waungana Tena

$
0
0
Wiki Kadhaa baada ya Video yao ya uchi kusambaa mitandaoni, Bill Nass amefunguka kuwa tayari kuna kuna ngoma ameshafanya na Nandy muda ukifika wataachia.

Hit maker huyo wa Tagi Ubavu amesema hayo katika kipindi cha Kikaangoni cha EATV na kuongeza kuwa mrembo huyo ni rafiki yake tu kwa sasa.

“Kuna wimbo tumefanya pamoja, wimbo umefanywa chini ya S2kizzy hivyo naamini muda ukifika utatoka tu ila nachojua ni wimbo mkali, kuhusu jambo ambalo limetokea,” amesema Bill.

Rapper huyo ameongeza, “Kuhusu mimi na yeye tayari nilishaomba radhi kwa wananchi na sasa maisha ya kawaida yanaendelea, hivyo hatuna tofauti yoyote ile kwa kuwa yule ni rafiki yangu na nina iheshimu sana familia yake akiwa pamoja na mama yake kwa kuwa ni mtu ambaye amekuwa akijitoa sana kusupport kazi za mwanae.”

Waziri asema si kila mtu ana mamlaka kuagiza upimaji DNA.....Atoa Maagizo Mazito Kwa Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu

$
0
0
Serikali  imekataza Mamlaka ya Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), kuruhusu watu au taasisi zisizo na mamlaka kisheria kuwaamuru kupima sampuli za vinasaba (DNA).

Agizo hilo lilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile, katika hafla ya uzinduzi wa Bodi Tendaji ya GCLA.

Bodi hiyo ina wajumbe saba kutoka Wizara za Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto; Mambo ya Ndani ya Nchi, Katiba na Sheria na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Dk. Ndugulile ameitaka mamlaka hiyo kutoa elimu kwa jamii kuhusu majukumu ya mamlaka hiyo, ili kuepuka watu au taasisi kutoa maagizo juu kwa mamlaka hiyo kinyume cha sheria na taratibu.

“Tusiamini kila mtu anajua utaratibu. Tunaweza sasa kuja kuvumbua mambo ambayo hayapo. Si kila mtu anaweza kuamrisha Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kuchukua vipimo vya DNA, si hivyo kuna taratibu zake,” alisema.

Alisema lazima watu waelezwe taratibu zikoje, nani anawajibika kwenda kupeleka sampuli na nani ana wajibu huo kwa sababu majukumu yake ni ya kisheria.

Dk. Ndugulile alisema katika siku za karibuni suala la kupima vinasaba limezungumziwa sana hali ambayo imezua mkanganyiko kwa jamii, hivyo kuitaka mamlaka hiyo kutimiza wajibu wa kutoa elimu.

Pamoja na kutokumtaja mtu aliyetoa amri ya watu kupimwa DNA, hivi karibuni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, aliwaita watu waliodaiwa kutelekeza watoto kujitokeza.

Baadhi ya watu hao walijitokeza, lakini 90 kati ya wanaume hao, waliwakana watoto waliodaiwa kuwa wamewatelekeza na kutaka waende wakapimwe DNA katika maabara ya Mkemia Mkuu ili kumaliza utata huo.

Katika hatua nyingine, Dk. Ndugulile aliitaka taasisi hiyo kuwa na mkaguzi wa kimataifa wa ubora wa sampuli wanazopima, ili zikubalike kitaifa na kimataifa.

“Lazima muwe na mkaguzi wa kimataifa wa kuthibitisha kile mlichopima kwa sababu taasisi hii ina majukumu ya kisheria ya kuamua ukweli kuhusu sampuli iliyopimwa. Mkisema huu ni unga wa mahindi ilhali tunaona ni dawa za kulevya hatuwezi kupinga,” alisema.

Pia aliitaka mamlaka hiyo kutoa majibu kwa wakati, ili kupunguza kesi zilizopo mahakamani zinazosubiri majibu ya maabara hayo.Alisema, ili kutekeleza agizo hilo, amewataka kuandaa mikataba inayoonyesha kazi itakamilika kwa muda gani pindi wanapopokea sampuli.

“Utakumbuka kuna wakati kesi zilirundikana katika mahakama zetu hivyo mnatakiwa kufanya kazi kwa haraka na kwa wakati na muwe na mikataba inayoonyesha kazi itakamilika kwa muda gani,” alisema.

Pia aliwataka kuwatambua wale wote wanaojihusisha shughuli za kemikali nchini wakiwamo, wauzaji, wanunuzi na wanaozitumia kwa ajili ya kupunguza matukio ya uhalifu nchini.

Kadhalika aliwataka kushirikiana na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi na Mazingira (NEMC) kuthibiti majitaka katika viwanda, ili kuepusha madhara kwa watu.

“Sijawasikia mkipima maji taka yanayotiririka viwandani mmekaa kimya kama si wajibu wenu, hakikisheni mnashirikiana nao na kuchukua sampuli nyie wenyewe mpime na mtoe majibu,” alisema.

Naye Mkemia Mkuu wa Serikali, Dk. Fidelice Mafumiko, alisema GCLA inakabiliwa na uhaba wa watumishi takribani 200 na pia uchakavu wa mitambo ya kimaabara.

Dk. Mafumuko pia alisema fedha za bajeti ya serikali ya mwaka 2017/18 zilizotengwa kwa ajili ya kununua mitambo na vifaa vya maabara hiyo hazijatoka hadi sasa hali ambayo inawafanya kushindwa kutekeleza majukumu yako kikamilifu.

Naye Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Prof. Ester Jason, aliahidi kuisumbua wizara hiyo kuhusu kutekeleza majukumu ya mamlaka ikiwa ni pamoja na kutoa fedha mapema iwezekanayo.

Rais Magufuli awajibu wanaokosoa mpango wa walimu wa sekondari kupelekwa shule ya msingi

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewajibu watanzania ambao wanakosoa mpango wa serikali wa kuwapeleka walimu wa sekondari kufundisha shule ya msingi.

Rais Magufuli amesema kuwa kitendo hicho ni cha kawaida kwani hakiadhiri mishahara yao bali kinawapa muda mwingi walimu hao kufanya kazi nyingine za ziada.

“Wakati wa Nyerere walikuwa wanachukuliwa walimu wa UPE kwenda kufundisha shule za msingi. Sasa tunachukua wenye digrii. 

"Kikubwa kinachoangaliwa ni mshahara wake tu.. Kwa sababu mshahara unapimwa si kwa vile unafundisha shule ya msingi, ni kutokana na Qualification zako. 

"Tena kule ni kurahisi tu unaweza kufanya na mambo yako mengine.“alisema Rais Magufuli jana Mei 2, 2018 wakati akizungumza na wafanyakazi na wanafunzi  wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa, kilichopo mkoani Iringa.

Rais Magufuli alitolea mfano wa nchi zinazotumia Maprofesa kufundisha shule ya msingi;  “Ukienda nchi za Scandinavia utakuta maprofesa ndiyo wanafundisha chekechea, na mishahara yao ni mikubwa kuliko wanaofundisha chuo kikuu. Just mind set.”

Mwezi Februari mwaka huu serikali kupitia Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma ilitangaza kuwa baadhi ya walimu wa masomo ya sanaa kutoka shule za sekondari watapelekwa shule za msingi ili kukidhi mahitaji.

Rais Magufuli atoa agizo kwa Halmashauri zote nchini

$
0
0
Halmashauri nchini zimetakiwa kuhakikisha zinaanzisha mifuko ya dawa na vifaa tiba ili kurahisisha upatikanaji wa huduma katika Hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati katika maeneo yao.

Agizo hilo limetolewa jana, Mei 2 na Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika hafla ya kuweka jiwe la msingi la Hospitali ya Wilaya ya Kilolo, mkoani Iringa.

Rais Magufuli alisema kuwa kuanzishwa kwa mifuko hiyo kutasaidia upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwa urahisi kwakuwa halmashauri zitakuwa na uwezo wa kununua moja kwa moja kupitia fedha zitakazotokana na mifuko hiyo.

“Natumia fursa hii kuziagiza Halmashauri zote nchini kuanzisha mifuko ya dawa na vifaa tiba (Drug Funds), hili isaidie katika kurahisha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika maeneo yenu”, alisisitiza Rais Dkt. Magufuli.

Aliongeza kuwa katika kutambua umuhimu wa upatikanaji wa dawa na vifaa tiba Serikali imetenga Sh.50 Bilioni katika bajeti yake ya mwaka wa fedha 2018/19.

Kwani kusoma ni kujua Kiingereza? – Rais Magufuli ahoji

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli amehoji wanafunzi wa chuo cha Mkwawa iwapo  kujua kusoma ni kujua Kiingereza.

Rais Magufuli ameyasema hayo jana , Mei 2 wakati akizungumza na wanafunzi pamoja na wafanyakazi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa, kilichopo mkoani Iringa wakati akitoa ufafanuzi wa shule za private na shule za Sekondari.

''Eti mtu amemaliza form four halafu hajui kuandika barua ya Kingereza, kwani kusoma ni kujua Kingereza!? Warusi wanajua Kingereza!? Kwani Wachina wanajua Kingereza !? Mbona wanatengeneza silaha za kila aina" !?

Aidha Rais Magufuli amesema kuwa “Shule za private wanafunzi wake wanachujwa, wakifika form 2 kuingia form 3 wanawachuja tena. Wanabaki na ile cream ili waonekane wanaongoza. Serikali inayowapenda wananchi wake haiwezi ikafanya hivyo.”

==>>Msikilize hapo chini

Rais Dkt Magufuli Ahani Msiba Wa Mkuu Wa Mkoa Mstaafu Marehemu Mzee Abbas Kandoro Mjini Iringa Leo

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka saini kwenye kitabu cha maombolezo wakati yeye na mkewe Mama Janeth Magufuli walipokwenda kuhani msiba wa Mkuu wa Mkoa Mstaafu Marehemu Mzee Abbas Kandoro eneo la Ihema nje kidogo ya mji wa Iringa leo Alhamisi Mei 3, 2018.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakitoa pole kwa wafiwa walipokwenda kuhani msiba wa Mkuu wa Mkoa Mstaafu Marehemu Mzee Abbas Kandoro eneo la Ihema nje kidogo ya mji wa Iringa leo Alhamisi Mei 3, 2018.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakitambulishwa kwa watoto wa marehemu walipokwenda kuhani msiba wa Mkuu wa Mkoa Mstaafu Marehemu Mzee Abbas Kandoro eneo la Ihema nje kidogo ya mji wa Iringa leo Alhamisi Mei 3, 2018.

Upelelezi Kesi Kigogo Wa TPA Anayedaiwa Kujilimbikiza Mali Za Bilioni 1.4/- Bado Haujakamilika, Apata Dhamana

$
0
0
 MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu ,imeelezwa upelelezi wa kesi ya kujilimbikizia mali zenye thamani ya Sh.bilioni 1.4  zisizolingana na kipato chake halali inayomkabili Meneja wa Fedha wa Mamlaka ya Bandari Tanzania,(TPA), Prosper Kimaro bado haujakamilika.

Taatifa hiyo imeelezwa leo mahakamani hapo na Wakili wa Serikali  Vitalis Peter mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba ambapo  kesi hiyo ilikuja kwa kutajwa.

Kutokana na taarifa hiyo, kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 5 mwaka huu na kuutaka upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi. Mshtakiwa huyo anashtakiwa  chini ya kifungu cha 27 (1)(4) cha sheria ya kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007.

Kimaro anadaiwa kumiliki nyumba zenye thamani ya Sh.1,178,370,334,  na magari  yenye thamani Sh 307,364,678.20, zisizolingana na kipato chake ambapo anadaiwa ametenda kosa hilo kati ya mwaka 2012 na 2016.

Alidai mshtakiwa  akiwa maeneo ya Temeke  na mtumishi wa umma wa TPA kama Meneja wa Fedha, amekutwa akimiliki mali zisizolingana na kipato chake halali cha zamani na  cha sasa.

Mali hizo ni nyumba mbili  zilizopo mtaa wa Uwazi Temeke zenye thamani ya Sh.milioni 124.2,  kiwanja kilichopo Yombo Vituka chenye thamani ya Sh.milioni 12.9 . Nyumba   mbili  zilizopo Temeke zenye thamani ya Sh.milioni 63.5, nyumba tatu zilizopo Temeke zenye thamani ya Sh.milioni  159.

 Nyumba nyingine tatu zenye thamani ya Sh.milioni  170.1,  nyumba nyingine moja yenye thamani ya Sh.milioni   71.3.kiwanja  kilichopo Temeke chenye thamani ya Sh.milioni  35.Pia kiwanja chenye thamani ya Sh.milioni 25 na amejenga nyumba tatu ambazo zinathamani ya Sh.milioni  159 pamoja na  nyumba nyingine moja yenye thamani ya Sh.milioni 106.Nyumba zenye thamani ya Sh.milioni  214,  nyumba  nne eneo la Viziwaziwa Kibaha Mjini zenye thamani ya Sh.milioni 199.7 na nyumba nyingine iliyopo Kilimahewa Tandika yenye thamani ya Sh.milioni 70.

Imedaiwa mahakamani hapo kuwa pia anamiliki magari aina ya Toyota Land cruise lenye thamani ya Sh.milioni 180.1,  Mitsubishi lenye thamani ya Sh.milioni 38.4,  Massey Ferguson lenye thamani ya Sh.milioni  24 na Trailer lenye thamani ya Sh.milioni  4.5.

Mengine ni  Toyota Harrier yenye thamani ya Sh.milioni  35.8,  Trailer lenye thamani ya Sh.milioni 4.8,  na Massey Ferguson lenye lenye thamani ya Sh.milioni 19.1.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, mshtakiwa  huyo alikana shtaka  na yupo nje kwa dhamana. Hiyo ni baada ya kukamilisha masharti ya  kuwa na wadhamini wawili ambao kila mdhamini  awasilishe hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya Sh.milioni 200.

Pia alimtaka mshtakiwa huyo  asitoke nje ya mkoa wa Dar es Salaam bila ya kuwa na kibali cha mahakama na mshtakiwa awasilishe hati zake za kisafiria mahakamani.

Mbunge wa Ulanga (CCM), Goodluck Mlinga Alitaka Jeshi la Polisi Kutumia Nguvu

$
0
0
Mbunge wa Ulanga (CCM), Goodluck Mlinga amemtaka Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro kutumia nguvu alizonazo kwa watu wanaotumia mitandao ya kijamii vibaya kwa kuwatukana viongozi.

Akichangia bajeti ya Wizara ya Mambo ya ndani kwa 2018/19, Mlinga amesema; “Matusi mitandaoni yamejaa, hajulikani Rais ni nani, kiongozi ni nani, kuna akaunti nyingi zinatukana, IGP (Sirro) tumekuwekea nyota mabegani tumia nguvu zako.”

Mlinga licha ya kupongeza utendaji wa polisi, amedai asilimia 85 ya huduma inayotolewa na jeshi hilo inahusisha rushwa ingawa anasema askari wa kike hawamo kwenye kundi hilo.

“Kesi ya kuku inakuwa ya ng’ombe, kesi ya kutusi inakuwa ya kuua kwa maneno, lakini niwapongeze wanawake katika hili hawamo,” amesema Mlinga huku akishangiliwa.

Amesema matukio ya kamatakamata yanayofanywa na Trafiki: “Ni janga la Taifa, wanaitwa wana mapato Dar es Salaam huko wanaitwa Tigo. Bodaboda ndiyo kabisa usiseme, ukienda katika vituo vya polisi, pikipiki ni nyingi.”

Naye mbunge wa Mlimba (Chadema), Susan Kiwanga amesema; “Kazi ya polisi si kunipangia cha kusema katika mkutano. Kama unaona nakosea subiri niongee nikimaliza  ukiona nimekosea nikamate.”

Mbunge aomba radhi tukio la kuwachoma mabinti sindano

$
0
0
Mbunge wa Ulanga (CCM) Goodluck Mlinga amewaomba radhi Watanzania kwa tukio alilolifanya la 'kujigeuza daktari.'

Mlinga amesema aliitwa kuhudhuria uzinduzi wa chanjo na wala yeye si mtaalamu wa afya.

"Kitaalamu mimi ni mtawala si daktari, nilifanya nilivyoelekezwa na sikufahamu madhara yake wanasema kitabibu huruhusiwi kushika hata sindano," amesema Mlinga na kuongeza:

"Kuomba msamaha si woga, sisi tulioendelea nasema kunradhi."

 Mlinga amesema hayo baada ya picha yake kuzagaa katika mitandao ya kijamii ikimuonesha anamdunga sindano binti wakati wa uzinduzi wa chanjo ya kuzuia saratani ya shingo ya kizazi kwa wasichana jimboni mwake.

 Waziri wa Afya Ummy Mwalimu alizungumzia suala hilo bungeni na kusema ingawa viongozi hao hawakuwachoma sindano lakini ni makosa kushika hata sindano.

Ofisa Utumishi Asimamishwa Kwa Kukaidi Kuwarudisha Watumishi Waliokuwa na vyeti vya Darasa la 7

$
0
0
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bumbuli, wilayani Lushoto mkoani Tanga, Peter Nyalali, amemsimamisha kazi Kaimu Ofisa Utumishi wa halmasahauri hiyo Protas Dibogo kwa kosa la kukaidi kuwarudisha kazini watendaji wa vijiji 41 licha ya serikali kuagiza warejeshwe.

Nyalali ametoa kauli hiyo wakati wa kikao chake na watumishi wa halmashauri hiyo ambapo pamoja na mambo mengine amesisitiza watendaji hao kwenda kufanya kazi kwa bidii kwenye maeneo yao mara tu watakaporejea kazini.

Hivi karibuni serikali iliagiza kurudishwa kazini kwa watumishi wote walioajiriwa kuanzia Mei Mosi, mwaka 2004, ambapo mara baada ya kauli hiyo Nyalali alimwagiza Dibogo kuwarudisha kazini watendaji hao 41 wa vijiji.

Pamoja na kutolewa agizo hilo Kaimu Ofisa huyo Utumishi anadaiwa kutotekeleza agizo hilo jambo lililomlazimu mkurugenzi kumsimamisha kazi.

Nao baadhi ya watumishi waliokuwa wamesimamishwa kazi kwa miezi minane walitoa shukrani zao kwa serikali na kuahidi kuendelea kuwa wachapakazi.

Mei 2, mwaka 2004 serikali iliwaajiri watumishi waliokuwa wakijitolea katika maeneo mbalimbali nchini na baadaye kutoa kibali cha kuajiri watumishi wapya wenye elimu ya darasa la saba huku ikiwataka kujiendeleza wawapo kazini.

Ole Nasha: Wabunge, Wahadhiri Acheni Ukware Waacheni Wanafunzi Wasome

$
0
0
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha ametoa wito kwa wabunge kutojihusisha na vitendo vya kingono na wafunzi wa vyuo vikuu na wawaache wasome.

Pia ametoa rai kwa wanafunzi na wananchi kwa ujumla kutoa taarifa kwa mamlaka husika pindi wanapopata taarifa za walimu na wahadhiri wa vyuo vikuu kuwafelisha wanafunzi kwa kutaka rushwa ya ngono.

Kauli hiyo ya OleNasha imekuja baada ya Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga (CCM) kusema kuwa baadhi ya wahadhiri wanajifanya ni vidume vya mbegu katika kuwafelisha wanafunzi hao.

Aidha, Naibu Waziri huyo amesema serikali imelipokea suala hilo na haina uvumilivu kwa vitendo hivyo.

“Pia mwanafunzi hadi ahesabike kuwa amefeli haitokani na mtazamo wa mwalimu mmoja tu, kuna taratibu zimeweka kupitia ‘marks’ (alama) ambazo amepata kutokana na kazi zake ili kuamua amefaulu au amefeli. Hata kama ilitokea mwalimu mmoja amefanya vitendo hivi, hii haiwezi ikaathiri ufaulu kwa vitendo hivi.

“Vyuo vikuu ikiwamo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), vina taratibu maalumu ya kushughulikia masuala haya ya unyanyasaji wa kijinsia lakini wanafunzi wengi hawatumii msaada huu. Tunawasihi kama watapata matatizo kama haya waende kwa mshauri wa wanafunzi (dean of student),” amesema.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live


Latest Images