Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Viongozi wa Chama cha ACT-Tanzania WAZOMEWA jukwaani baada ya kuifananisha CHADEMA na Nguruwe pori....

$
0
0
VIONGOZI wa Chama kipya cha siasa cha Alliance for Change and Transparency (ACT), juzi walijikuta wakizomewa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Mbugani, Jimbo la Nyamagani, jijini Mwanza. Mbali ya kujikuta katika wakati mgumu wa kuzomewa, baada ya mkutano huo kumalizika, viongozi hao waliondolewa chini ya ulinzi mkali wa polisi. Mkutano huo ulilenga

Sumaye akata rufaa kwa kutoridhishwa na uamuzi wa kumfungia mwaka mmoja CCM

$
0
0
Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye amekata rufaa Kamati Kuu ya CCM kupinga adhabu ya onyo kali aliyopewa na chama kutokana na madai ya kuanza kampeni za urais mapema kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu ujao.    Akizungumza na Mwananchi  mjini Dodoma jana, Sumaye alisema kwa ufupi hakuridhishwa na adhabu hiyo na kuthibitisha hilo, tayari amekata rufaa.   Hata hivyo, alisema hadi jana hakuwa

Polisi wanne wafukuzwa kazi kwa kujihusisha na vitendo vya uhalifu.......

$
0
0
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewafukuza kazi kwa fedheha askari wanne wa Jeshi la Polisi kutokana na makosa ya kujihusisha na vitendo vya uhalifu. Askari waliofukuzwa wanatoka katika vikosi mbalimbali kama ifuatavyo:   .       E.6396 CPL RAJABU MKWENDA @ UGORO wa Makao Makuu ya Polisi. ·       F.9412 PC SIMON wa Kituo cha Polisi Kati. ·       F.9414 PC ALBERNUS  KOOSA wa

Bunge maalumu la katiba lasitishwa kwa muda kutokana na vurugu zilizotokea bungeni....Nini Chanzo cha vurugu hizo??..BOFYA hapa

$
0
0
Jumatatu ya leo, Machi 17, 2014 Mwenyekiti wa Bunge la Katiba Mhe. Sammuel Sitta amelazimika kukiahirisha kikao kilichokuwa kinaendelea jioni baada ya kutokea kutoelewana bainaa ya wajumbe na wabunge wa bunge la katiba. Vurugu zilitokea pale Mhe. Sitta alipomruhusu Jaji Joseph Sinde Warioba (Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Katiba), awasilishe Rasimu ya Katiba hiyo Bungeni.  

Taarifa Muhimu kuhusu kuendelea kwa kikao cha bunge maalumu la katiba kesho Jumanne tarehe 18 March 2014 baada ya kusitishwa kutokana na Vurugu za Wajumbe

$
0
0
Baada ya kutokea vurugugu zilizosababishwa na baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalum na  kupelekea Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Katiba Jaji Joseph Warioba kutokuwasilisha rasimu ya pili ya Katiba kwa wajumbe hao, Mwenyekiti wa Bunge Maalum Mhe. Samuel Sitta aliitisha kikao cha maridhiano na baadhi ya wajumbe wanaowakilisha makundi mbalimbali yaliyopo katika Bunge hilo ili kupata

Serikali yatakiwa kukataa kuruhusu USHOGA nchini.....

$
0
0
Serikali imeombwa kufuata nyayo za serikali ya Uganda chini ya Rais Yoweri Museveni kwa kuktaa kuruhusu ushoga licha ya kuziudhi nchi za magharibi zinazokingia kifua vitendo hivyo. Ombi hilo limetolewa na Imamu wa Msikiti wa Mwembechai, Sheikh Mohammed Muhenga, alipokuwa akiwahutubia waumini kabla ya swala ya Ijumaa iliyoswaliwa msikiti hapo, jijini Dar es Salaam. Imamu Muhenga

Yatokanayo na uchaguzi wa Kalenga, Madai ya CHADEMA kuibiwa kura na Matarajio yao katika uchaguzi wa CHALINZE.....

$
0
0
  Akiwa ameambatana na mkewe, Robby Mgimwa, Jumatatu ya Machi 17, 2014 Godfrey Mgimwa wa Chama cha Mapinduzi (CCM) alitangazwa mshindi wa ubunge katika uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga baada ya kuvibwaga kwa kura za kishindo vyama vingine viwili vilivyoshiriki uchaguzi huo. Katika uchaguzi huo uliofanyika Jumapili ya Machi 16, mwaka huu, Mgimwa alizoa kura 22, 962 ambazo ni sawa na asilimia

Mahakama leo kutoa uamuzi wa pingamizi la DPP dhidi ya Sheikh Ponda

$
0
0
Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, leo inatarajia kutoa uamuzi wa pingamizi la awali la Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) la kupinga maombi  ya kufanya marejeo kuhusu kuliondoa shitaka la kukaidi amri halali iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu dhidi ya Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda. DPP aliwasilisha pingamizi la awali dhidi

Usafi wa Kigali nchini Rwanda wamshawishi Rose Ndauka kuanzisha kampeni ya usafi jijini Dar

$
0
0
Msanii wa filamu Rose Ndauka ambaye ni balozi wa usafi wa kampeni ya ‘Amka na Badilika Ng’arisha Tanzania’ amesema alijisikia wivu baada ya kuona usafi wa jiji la Kigali nchini Rwanda hali ambayo imemfanya aanzishe kampeni yake ya usafi nchini. Akizungumza nasi, Rose amesema baada ya kutembelea jiji la Rwanda nakuona hali yake,aliamua aanzishe kampeni itakayoihamasisha jamii juu ya

Ombi la Sheikh Ponda latupiliwa mbali na Mahakama....Arudishwa Segerea akiwa chini ya ulinzi mkali

$
0
0
Ombi la marejeo lililowasilishwa na Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda limetupiliwa mbali na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam  leo   ilipotoa uamuzi wa pingamizi la awali lililowasilishwa na Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), akidai kuwa ombi hilo halikuwa na msingi kisheria.   Kesi hiyo iliyosikilizwa kwa saa 1 na dakika 40 ilitolewa uamuzi na Jaji

Hotuba ya mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba , Mhe. Jaji Joseph Sinde Warioba akiwasilisha Rasimu ya Katiba bungeni leo

$
0
0
Iliyowekwa hapo   chini ni hotuba ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Mhe. Jaji Joseph Sinde Warioba alipowasilisha Rasimu ya Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Bunge Maalumu la Katiba, leo Jumanne, Machi 18, 2014. << BOFYA    HAPA  KUISOMA >> Bofya  hapo  juu   Kuiosoma  au  Kuidownload

Habari kuhusu hili kanisa jipya lililofunguliwa Kigoma linalokataza watoto kwenda shule na watu kwenda hospitali kutibiwa

$
0
0
Licha ya serikali kulipiga marufuku dhehebu lililoibuka katika kijiji cha Rumashi wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma liitwalo Sabato matengenezo, mwanzilishi wa dhehebu hilo amejitokeza na kusisitiza kuendelea na imani hiyo.    Baada ya kupata taarifa za kuwepo kwa dhehebu hili ambalo linakataza watoto kwenda shule na wagonjwa kutibiwa hospitalini, Serikali ilimkamata kiongozi  wake

Baraza la Sanaa na Idara ya Uhamiaji wazungumzia biashara ya ngono inayofanywa na wasanii wanaotoka nje ya nchi

$
0
0
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), limekiri kuwepo kwa baadhi ya wasanii wa nje wanaokuja nchini kufanya kwa madai ya kufanya shughuli za Sanaa lakini hutumia vibali vyao vibaya kwa kujihusisha na biashara ya 'ngono' katika kumbi mbalimbali za starehe zinazojulikana kwa jina la 'Mujra Club'.   Hali hiyo imebainika baada ya Idara ya uhamiaji kubaini kuwa kuna baadhi ya maofisa wa

"Sina mpango wa kuolewa na mwanaume wa kibongo, lazima niolewe nje ya nchi"....Jackline Wolper

$
0
0
Star mkubwa wa filamu nchini Jacqueline Wolper ameibuka na kudai kuwa, atafanya kila njia ili aolewe na mwanaume wa nje ya nchi na siyo Wabongo ambao hawathamini mastaa.   Akizungumza na Uwazi, Wolper alisema, amefikia uamuzi huo kwa sababu ana uchungu moyoni unaotokana na dhana waliyonayo wanaume wa Kitanzania juu yao, wakiamini kuwa ni wahuni tu hivyo kuwashusha thamani.   “

Snura Majanga anaswa kwa Sangoma ( Mganga wa Jadi ) akiwa amebebeshwa vibuyu ......

$
0
0
Msanii  mkongwe  nchini  maarufu  kwa  jina  la   Snura  Mushi  au  Snura  Majanga  amenaswa  live  akiwa  kwa  sangoma ( mganga  wa  jadi )  akisafisha  nyota  yake  kwa  lengo  la  kujiongezea  mashabiki...... Tazama  ushuhuda  wa  picha  hapo  chini....   <!-- adsense -->

Shilole afungua mgahawa, unaitwa "CHUNA BUZI"

$
0
0
  Star wa filamu na muziki nchini Shilole anatarajia kufungua mgahawa wake wa chakula utakaoitwa "Chuna Buzi " ambao utakuwa maeneo ya Mwananyamala.... Akizungumza kwenye 255 ya XXL, Clouds FM,Shilole amesema ameamua kufungua mgahawa kwakuwa ana taaluma ya Hotel Management na pia mama yake alikuwa mama Ntilie. “Mgahawa wangu ambao natarajia kuufungua hivi karibuni utakuwa naeneo ya

Huddah Monroe akana kutoka kimapenzi na Colonel Mustafa, adai alitafuta ‘kiki’ kupitia jina lake

$
0
0
Mwezi uliopita aliyekuwa mwakilishi wa Kenya kwenye BBA, Huddah Monroe na Colonel Mustafa walitangaza uhusiano wao wa kimapenzi kwenye kipindi cha ‘Kiti Moto’cha KTN. Hata hivyo, Huddah ameibuka na kusema interview hiyo ilikuwa imepangwa. Kwenye interview hiyo, wawili hao walidai kuwa wanapendena na wanaweza kufunga ndoa.  Hata hivyo kwenye mahojiano na mtandao wa Ghafla, Huddah

Picha tatu za muonekano wa Wema Sepetu akiwa amenyoa UPARA, na akiwa bila Make-Up

$
0
0
Huu  ni  muonekano  mpya  wa  msanii  Wema  Sepetu  akiwa  kanyoa  upara  na  akiwa  bila  make  up....   <!-- adsense -->

Madereva wa daladala mkoani Morogoro wagoma kuingia barabarani....Chanzo cha mgomo ni kukamatwa hovyo na matrafiki

$
0
0
Madereva wa daladala Manispaa ya Morogoro wamegoma asubuhi hii wakidai kukamatwa hovyo na matrafiki na hakuna daladala linalofanya safari yoyote katika manispaa hiyo.   Madereva hao wanadai wameamua kugoma kutokana na kamatakamata ya askari wa usalama barabarani, ambapo wamesema daladala moja kwa siku linaweza kukamatwa hadi mara nne na wakihoji wanaambiwa ni makosa tofauti.  

Habari kuhusu watu wanne waliouawa na wananchi wenye hasira kali mkoani Mwanza wakituhumiwa kuiba Ng'ombe

$
0
0
WATU wanne wameuawa mkoani Mwanza kwa tuhuma za wizi wa ng’ombe Katika eneo la Igwambiti kata ya Buhongwa Wilaya ya Nyamagana. Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Valentino Mlowola amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana  majira ya  saa 11 alfajiri ambapo wananchi walipata taarifa ya kuwepo kwa  wizi wa ng’ombe katika kitongoji cha Mtende.  
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images