Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Bei ya petroli yashuka, mafuta ya taa yapaa

$
0
0
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), juzi  ilitangaza kushuka kwa bei ya petroli na dizeli kwa asilimia 2.7 na asilimia 3.8; na ongezeko la asilimia 0.09 kwa mafuta ya taa.

Taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Nzingagwa Mchany ilisema bei hizo mpya zitatumika Tanzania Bara kuanzia leo.

Hata hivyo, kwa watumiaji wa mafuta yanayopitia katika Bandari ya Dar es Salaam ni neema, lakini wa Bandari ya Tanga bei imeongezeka.

Mchany alisema mabadiliko hayo ya yanatokana na kushuka kwa bei ya mafuta katika soko la dunia na marekebisho ya bei yaliyofanywa na Ewura kutokana na kubadilika kwa tozo za wakala na Serikali za mitaa katika bidhaa hizo.

Ikilinganishwa na tangazo la bei ya mafuta la Aprili 4 kwa mafuta yanayopitia katika Bandari ya Dar es Salaam, bei ya petroli imepungua kwa Sh88 kwa lita (asilimia 3.8) na dizeli Sh61 kwa lita (asilimia 2.75); huku bei ya mafuta ya taa ikiongezeka kwa Sh2 kwa lita sawa na asilimia 0.09.

Tofauti na wanunuzi wa rejareja, bei ya wale wa jumla upande wa petroli imepungua kwa Sh100.91 kwa lita (asilimia 4.58), dizeli Sh73.71 kwa lita (asilimia 3.52) na mafuta ya taa Sh10.49 kwa lita sawa na asilimia 0.51.

Mafuta yanayopita Bandari ya Tanga bei kwa wanunuzi wa rejareja imeongezeka kwa asilimia 0.14 kwa petroli na asilimia 0.71 kwa dizeli.

Lakini wauzaji wa jumla bei imepungua kwa asilimia 0.46 (Sh9.8 kwa lita) kwa petroli na asilimia 0.1 (Sh1.9 kwa lita) kwa dizeli.

“Hakuna uingizaji mpya wa mafuta uliofanyika nchini kupitia Bandari ya Tanga, lakini kutokana na mabadiliko ya bei ya Ewura kuna mabadiliko ya bidhaa hizo tofauti na ilivyotangazwa Aprili 4,” alisema Mchany na kuongeza:

“Bei ya petroli itaongezeka kwa Sh3 kwa lita, huku dizeli ikiongezeka kwa Sh15 kwa lita.”

Kutokana na kupungua kwa mafuta ya taa katika Bandari ya Tanga, Ewura imewashauri watumiaji wa mikoa ya Nyanda za Juu kuchukua bidhaa hiyo katika Bandari ya Dar es Salaam kwa bei elekezi.

Taarifa ya Mchany inasisitiza kila kituo cha kuuzia mafuta kuchapisha bei kwenye mabango yanayoonekana bayana na kituo kutoa risiti za kielektroniki (EFD) kwa kila mauzo.

Familia ya kina Heche yaukataa msaada Uliotolewa na Polisi

$
0
0
Siku chache baada ya mkazi wa Tarime, Suguta Chacha kufariki dunia akiwa mikononi mwa polisi, familia yake imekataa kupokea msaada wa chakula kilichotolewa na ofisi ya kamanda wa polisi, Kanda Malumu ya Tarime/Rorya.

Chakula hicho kilitolewa na jeshi hilo kwa ajili ya shughuli za msiba wa Suguta ambaye ni ndugu wa Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche aliyefariki Aprili 27 akiwa mikononi mwa polisi.

Msaada huo wa kilo 100 za mchele, unga kilo 100, maji ya kunywa katoni 20 pamoja na sukari uliwasilishwa msibani hapo  na Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Henry Mwaibambe lakini ulikataliwa.

Alipoulizwa kuhusu suala hilo Kamanda Mwaibambe alisema: “Tuliache kwa sababu halina maana tena na tunapenda liishe salama.”

Katibu wa ukoo wa Suguta, Chacha Heche alisema familia hiyo iko tayari kupokea msaada wa Kamanda Mwaibambe kama mtu binafsi kutokana na jinsi alivyoshirikiana nao tangu mauaji hayo yatokee, lakini haitapokea msaada wa polisi kama taasisi.

“Tutapokea msaada kutoka kwa yeyote mwenye mapenzi mema lakini siyo taasisi ya Jeshi la Polisi. Tayari tumechanga zaidi ya Sh5 milioni kati ya Sh8 milioni zinazohitajika kugharamia mazishi ya ndugu yetu,” alisema Heche.

Alisema familia inaheshimu na kutambua jinsi Kamanda Mwaibambe anavyoshughulikia tukio hilo na itashirikiana naye na kumkaribisha katika mazishi kama mtu binafsi na siyo kwa kofia ya polisi.

Katibu huyo wa ukoo wa Suguta, alisema marehemu atazikwa kesho baada ya ndugu kujiridhisha na hatua zilizochukuliwa na Jeshi la Polisi.

Suguta anadaiwa kufariki dunia baada ya kuchomwa visu na askari polisi, William Marwa (50).

Marwa alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Tarime juzi na kusomewa shtaka la mauaji.

Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Mwani Mrisho alisema mtuhumiwa alitenda kosa hilo Aprili 27 ambako alimuua Suguta (27) kwa kumchoma na kisu.

Tukio hilo lilitokea usiku wa siku hiyo baada ya Suguta na mmiliki wa baa kukamatwa na polisi waliokuwa doria. Hata hivyo, ndugu wa Suguta walipokwenda kumuangalia siku inayofuata waliambiwa amefariki na mwili upo mochwari.

Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi Asherehekea Birthday Yake Gerezani

$
0
0
Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu amesherehekea siku yake ya kuzaliwa akiwa gerezani huku familia yake ikiisherehekea kwa kula chakula pamoja na watoto yatima wanaolelewa katika Kituo cha Nuru, Uyole jijini Mbeya.

Sugu ambaye anafikisha umri wa miaka 46, alisherehekea siku hiyo akiwa gerezani ambako anatumikia kifungo cha miezi mitano.

Keki ya mbunge huyo ilipambwa kwa kuchorwa pingu, mnyororo na taswira ya chumba cha Magereza.

Sugu alihukumiwa kifungo cha miezi mitano baada ya kukutwa na hatia ya kutoa lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli, Februari 26.

Mwingine aliyehukumiwa kifungo hicho ni Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga ambao wote wanatumikia kifungo cha miezi mitano jela katika Gereza Kuu la Ruanda jijini hapa.

Jana, uongozi wa Hoteli ya Desderia inayomikiliwa na Sugu ulisherehekea siku hiyo pamoja na watoto yatima wa Kituo cha Nuru na kula nao chakula cha pamoja.

Hilo ni agizo la Sugu kuendelea kuwa karibu na jamii ya wakazi wa Mbeya.

Mke wa Sugu, Happiness Msonga alisema mumewe ndiye aliyeagiza siku ya kuzaliwa kwake iadhimishwe pamoja na watoto yatima kwa kula nao chakula.

“Sugu amesema anawapenda sana watoto na yupo pamoja nao licha ya kuwa yupo gerezani, lakini kiroho yupo nao daima. Ameagiza jana kwa kuwa pia ni Mei mosi, ni vyema tukashiriki sherehe hiyo na watoto yatima,” alisema.

Happiness alisema Sugu kupitia uongozi wa hoteli yake wameanzisha mpango maalumu wa kutembelea na kujumuika na vituo vya watoto yatima vilivyopo jijini Mbeya kila mwisho wa mwezi kwa kuwapelekea chakula na misaada mingine.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Yatima cha Nuru-Uyole, Jarson Fihavango alimshukuru mbunge huyo na uongozi mzima wa hoteli yake kwa kuwapelekea chakula na misaada mingine watoto wanaowalea kituoni hapo.

“Tunajua mbunge wetu alipatwa na matatizo, lakini pamoja na kwamba yupo gerezani, lakini bado anawakumbuka wananchi wake. Sisi tunashukuru sana kwa hiki alichotufanyia,” alisema Fihavango.

“Tunasema aendelee na moyo huohuo na sisi tunamuombea. Hiki alichokifanya kina baraka kubwa mbele za Mwenyezi Mungu, tunajua namna anavyoweza kumlipa.”

Wafanyabiashara wapewa 'shavu' jijini Dodoma

$
0
0
Kampuni zinazotengeneza vifaa vya ujenzi zimeshauriwa kutumia fursa ya kufanya biashara hususani katika kipindi hiki ambacho serikali inahamia Dodoma.

Ushauri huo ulitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi wakati alipokuwa akizungumzia juu ya maandalizi ya maonyesho kwa kampuni zinazotengeneza vifaa vya ujenzi na samani za ndani pamoja na wadau wa sekta ya ujenzi.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa amezitaka kampuni hizo kutumia fursa ya ujio wa makao makuu kwa kujitambua, ili mashirika, taasisi na watu binafsi wanaojenga Dodoma wafahamu ni bidhaa gani bora kwa ajili ya ujenzi.

Maonyesho hayo yanafahamika kama Dodoma Builders Expo 2018, na alisisitiza kwamba fursa hiyo ni kubwa na wafanyabiashara wa vifaa vya ujenzi waitumie kuonyesha bidhaa bora.

Kunambi alisema ni kosa kulifananisha jiji la Dodoma na mikoa mingine nchini kwani linatakiwa kufananishwa na Jiji la Nairobi Kenya na Pretoria Afrika ya Kusini.

Kwa upande wake mratibu wa maonyesho hayo, Victor Simon alisema katika Jiji la Dodoma kuna vibarua na mafundi ambao wote wanachangamoto zinazofanana.

Mratibu huyo aliwataka makandarasi wa jiji hilo kuwatumia mafundi na vibarua wa Dodoma, na kuacha tabia ya kutumia wale wa kutoka maeneo mengine.

Alisema maonyesho hayo pia yanalenga kuwatambulisha na kuwaibua mafundi na vibarua na wanatarajia kuongeza ujuzi na kukuza vipato. 

Kanisa lapiga marufuku uvaaji wa Shela za harusi

$
0
0
Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Arusha, limewapiga marufuku wanawake wajawazito kuvaa shela wakati wa kufunga ndoa kwa madai vazi hilo ni alama ya ubikira kwa mwanamke na sio vinginevyo.

Hayo yamesemwa na Paroko Msaidizi wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Theresa, Padre Festus Mangwangi  wakati akiweka mkazo juu ya tamko lililotolewa na Askofu Mkuu wa Jimbo hilo Isaack Amani, wakati akiadhimisha misa ya shukrani iliyofanyika Jumapili iliyopita, baada ya kuteuliwa kwake na Baba Mtakatifu Francis kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo hilo. 

Kabla ya uteuzi huo uliotangazwa Desemba 27 mwaka 2017, Askofu Mkuu Amani alikuwa Askofu wa Jimbo la Moshi na kusema haitakiwi kwa mwanamke yeyote ambaye anajijua ni mjamzito kuvaa shela kipindi anafunga ndoa kwa kuwa vazi hilo linavaliwa na mwanamke asiyemjua mwanaume (bikra).

Aidha, Padre Festus Mangwangi amewataka wazazi kuwafundisha watoto wao wa kike kutunza miili yao na kuishi maisha ya kimaadili hadi watakapopata wenza wa kufunga nao ndoa na hapo ndipo alama ya shela itakapoonekana umuhimu wake.

"Tamko la Askofu Mkuu linatekelezwa kwa kuwaeleza maharusi watarajiwa wanapokwenda kupata mafundisho ya ndoa kwa katekista na baadaye padre, kuwa kama ni wajawazito basi wasivae shela na hata wale wanaowajua wanaume pia wanashauriwa wasivae", amesema Padre Festus.

Pamoja na hayo, Padre Festus ameendelea kwa kusema "wanaojitambua kuwa si bikira, hawavai shela, lakini wako wanaojificha na kuvaa shela, hii inakuwa sawa na kudanganya".

Kwa upande mwingine, Padre Festus amesema endapo atatokea mtu akadanganya na kuvaa shela wakati tayari anamjua mwanaume au kuwa mjamzito basi atakuwa anafanya utovu wa nidhamu.

Harmonize Atoa Sababu ya Kutompa Mkono Alikiba.

$
0
0
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva kutoka label ya WCB, Harmonize amefunguka sababu ya kutompa mkono Alikiba walipokutana katika msiba wa Agness Gerald ‘Masogange’.

Muimbaji huyo anayefanya vizuri na ngoma ‘Kwa Ngwaru’ ameiambia The Playlist ya Times FM kuwa mambo yote yanayozungumzwa si ya kweli, bali walisalimiana ila si kwa kushikana mikono.

“Unajua asilimia kubwa ya watu wanaozungumza hawakuwa pale, unajua unapomzungumzia Alikiba ni mtu ambaye amefanya muziki wetu upate heshima kwa namna moja au nyingine, kama msanii namheshimu siwezi nikakutana na mtu halafu nisimsalimie, sio kweli,” amesema na kuongeza:

“Kilichofanyika ni kwamba Diamond kamsalimia kwa mkono, wamesamiliana kwa mkono. Mimi nimekuja nimezunguka nikaona kwa kuwa Diamond kamsalimia kwa mkono, kamgeuzia kiganja, mimi nikamsalimia kwa sauti tu, tukakaa pale tukaendelea.” .

Aunty Ezekiel: Mchango wa Moze Kwangu ni Zaidi ya Pesa

$
0
0
MSANII nyota wa filamu nchini, Aunty Ezekiel, amesema changamoto alizokutana nazo kwenye chumba cha kujifungulia ndio sababu ya kutunga na kuandaa filamu ya 'Mama' ambayo itazinduliwa Mei 13, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Slaam jana, Aunty Ezekiel, alisema  ameamua kuandaa filamu hiyo ili kuonyesha thamani ya mama na amepanga kuizindua kwenye Ukumbi wa Mlimani City.

Alisema lengo la filamu hiyo ni kuwafanya watu na jamii kwa ujumla kuona thamani ya mama na kuwaheshimu.

“Wakati nasubiri kujifungua nikiwa kwenye kile chumba nilipitia magumu ambayo najua mama yangu aliyapitia na baada ya hapo ndipo nikajua thamani ya mama, nilifikiria nimpatie zawadi gani, lakini nikaona ni bora nitengeneze filamu ili nionyeshe thamani ya mama,” alisema

Aidha, alisema mama mara zote amekuwa na mchango mkubwa katika jamii huku akipambana zaidi na familia ikilinganishwa na kina baba.

“Naweza nikasema mama ni muhimu kuliko baba na sisi tumekuwa haturudishi upendo kwa mama zetu kuhusiana na yale waliyotutendea, nikiwa kama msanii nimeona nije na kitu ambacho kitawarudishia thamani yao,” alisema.

Alisema katika movie hiyo ambayo ameifanyia katika Kijiji cha Kisarawe mkoani Pwani, ameshirikiana na mtoto wake (Cookie) na hakutaka kumshirikisha mumewe (Mose Iobo) kwa kuwa fani yake ni mnenguaji.

“Katika kazi zetu hatuingiliani hata siku moja hawezi kuniambia leo nikawe mnenguaji, hilo siliwezi na mimi siwezi nikamuambia aje kwenye movie kwa sababu hawezi ila kwa msaada ananipatia yaani ana msaada mkubwa sana kwangu zaidi hata ya pesa,” alisema.
.

Wabunge waibana Serikali bungeni kuhusu nyongeza ya mishahara

$
0
0
Siku moja baada ya Rais John Magufuli kuahidi kupandisha  mishahara ya watumishi baada ya uchumi kutengamaa, wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Sixtus Mapunda(Mbinga Mjini) na Musa Sima (Singida Mjini), wameitaka serikali kueleza ni lini mishahara hiyo itapanda.

Wabunge hao wamehoji hayo leo Mei 2, bungeni jijini Dodoma baada ya kuomba muongozo kwa mwenyekiti wa Bunge Andrew Chenge kuhusu majibu ya Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji kuhusu mipango ya serikali kupunguza umaskini.

Mapunda amesema katika swali namba 166 lililoulizwa na Mbunge wa Kasulu Mjini, Daniel Nsanzugwanko, majibu ya serikali katika ujumla wake yalijikita kwenye kuondoa umaskini wa kipato na kwa kuwa umaskini wa kipato una uhusiano moja kwa moja na ongezeko la mishahara ya watumishi wa serikali wa kada zote.

“Kwa kuwa jana rais alisema kuwa ongezeko la mishahara pamoja na mambo mengine litazingatia hali halisi ya uchumi  uwezo wa serikali kulipa na mahitaji halisi ya serikali, na kwa kuwa rais ameshaji-commit kuwa kutakuwa na ongezeko la mishahara litakalozingatia mahitaji ya msingi, serikali inatoa kauli gani, lini ni mishahara hiyo itapanda maana hili suala ni kama lipo hewani na limeacha sitofahamu nyingi kwa wananchi,” alihoji Mapunda.

Kwa upande wake Musa Sima naye aliomba mwongozo na kueleza kuwa Dk. Kijaji anatoa majibu kuhusu miongoni mwa hatua za kuondoa umaskini Tanzania hakuweza kuonesha nyongeza ya mishahara kwa watumishi.

“Sasa nimpongeze rais kwa hotuba yake ya Mei mosi, lakini ni vizuri kama Bunge tukahitaji kusikia kauli ya serikali kwa ajili ya watumishi ni lini sasa serikali itahakikisha itapandisha mishahara ya watumishi hawa kama hatua mojawapo ya kuondoa umasikini?,” aliuliza Sima.

Akijibu miongozo hiyo, Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge aliitaka serikali kujipatia nafasi nzuri nzuri ya kujielezea na kuwapa matumaini wananchi.

“Kwa kuwa ni swali ambalo linahusu na maslahi ya wafanyakazi wa Watanzania, ndiyo maana limelengwa na Mapunda na Sima, nadhani serikali mnaweza kupata nafasi nzuri ya kujielezea na kuwapa matumaini wananchi.

“Ni lini, hayo ni maswali sasa tunaiachia serikali hadi hali ya uchumi itakaporuhusu, tufanye haya makubwa yatakayowezesha kukuza uchumi wetu kwa haraka siri ya maendeleo ni hiyo tu, tufanye kazi kwa bidii tukuze uchumi, lakini serikali nadhani kwa wakati muafaka wanaweza kulitolea maelezo,” amesema Chenge.

Ajira 10,140 za walimu wa shule za msingi kutolewa Juni

$
0
0
Serikali imesema Juni 30, 2018 inatarajia kutoa ajira 10,140 za walimu wa shule za msingi nchini.

Hayo yamesemwa leo Mei 2, 2018 Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Tamisemi, Joseph Kakunda wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Ludewa (CCM), Deogratius Ngalawa.

Katika swali lake, Ngalawa alitaka kupata majibu ya Serikali kuhusu  upungufu wa walimu 500 wa shule za msingi na jinsi litavyoshughulikiwa.

Akijibu swali hilo, Kakunda amesema; "Tunaendelea na mchakato kwa kushirikiana na Baraza la Mitihani la Taifa kwa kupitia vyeti vya vya walimu na tunategemea ifikapo Juni 30 kuwaajiri."

Serikali Yasema Bungeni Hakuna Njaa Nchini

$
0
0
Serikali imesema inapata tabu kukiri kuwa kuna hali ya njaa nchini kwa kuwa mvua zimenyesha za kutosha mwaka huu.

Kauli hiyo imetolewa leo Mei 2, bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji wakati akijibu swali la Mbunge wa viti maalumu (CCM), Khadija Nasri Ally.

Mbunge huyo alitaka kujua kauli ya serikali kuhusu hali ya njaa na umaskini nchini.

Alisema ripoti za Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na Taasisi ya utafiti (REPOA), zimebainisha kuwa hali ya njaa na umaskini imeongezeka mwaka huu ikilinganishwa na miaka iliyopita.

Akijibu swali hilo Dk. Kijaji amesema hali ya njaa nchini haipo kwani mvua za kutosha zimenyesha na wananchi wana amani kwani hakuna uhaba wa chakula.

“Napata tabu kusema kusema hali ya njaa imeongezeka ndani ya mwaka 2018 wakati mfumuko wa bei za bidhaa zinazochangia upatikanaji wa chakula nchini kwa mwezi Machi mwaka huu ulikuwa asilimia 3.9 pekee.

“Hii ni dalili kuwa hali ya njaa nchini haipo labda mbunge ametumia takwimu za miaka iliyopita mwaka 2016/17 ,” amesema.

Waziri Mwakyembe afanya uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu nchini

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amemteua Prof. Frowin Paul Nyoni kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu nchini Tanzania pamoja na wajumbe wapya sita wa bodi hiyo.

Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa na Wizara hiyo na kusema uteuzi huo umeanza kufanya kazi rasmi Aprili 18, 2018 na wataitumikia bodi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu.

Kwa taarifa kamili soma hapa chini..

Ushahidi Kesi Ofisa TRA Anayedaiwa Kumiliki Magari 19 Ya Thamani Ya Milioni 197.6 Kusikilizwa Mfululizo

$
0
0
Ushahidi  dhidi ya kesi inayomkabili Ofisa Msaidizi wa Forodha wa (TRA), Jennifer Mushi anayedaiwa kumiliki magari 19 yenye thamani ya Sh.milioni 197.6 yasiyolingana na kipato chake unatarajia kusikilizwa kwa siku mbili mfululizo.

Hayo yameelezwa leo Mei 2 mwaka huu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya Mwendesha Mashtaka wa Jamhuri, Inspekta Hamis kueleza kuwa shauri hilo limeitishwa kwa ajili ya kusikilizwa.

Hata hivyo, Inspekta Hamis amedai kuwa hana taarifa za kutosha kuhusu usikilizwaji wa shauri hilo kwani lipo chini ya Mawakili wa Takukuru na hawapo mahakamani.Kutokana na taarifa hiyo Hakimu Shaidi ameahirisha kesi hiyo hadi Mei 28 na 29, 2018, kwa ajili ya kuanza kusikilizwa mfululizo.

Katika kesi hiyo, mshtakiwa anadaiwa kati ya Machi 21, 2016 na Juni 30, mwaka 2016 maeneo tofauti jijini Dar es Salaam, mshtakiwa akiwa mfanyakazi wa TRA  alikutwa akimiliki mali zisizolingana na kipato chake, kinyume na sheria.Inadaiwa pia, alikutwa akimiliki magari 19, yakiwemo Toyota Ra4,Toyota dyna truck, Toyota viz, Suzuki carry, Toyota Ipsum na mengineyo ambayo yote yote yana thamani ya milioni.197,601,207

Pia anadaiwa, kati ya Machi 21, 2012 na Machi 30, 2016 maeneo ya Dar es salaam akiwa mwajiriwa wa TRA aliishi maisha ya kipato cha juu (kifahari) yenye thamani ya Sh.milioni 333.2 tofauti na kipato chake.

Msekwa Apongeza Utendaji wa Rais Magufuli

$
0
0
Jonas Kamaleki-MAELEZO
Spika wa Bunge mstaafu, Mhe. Pius Msekwa amesema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli anafanya kazi vizuri katika kuiletea nchi maendeleo hasa kwa kulinda na kusimamia rasilimali .

Msekwa alisema hayo jana katika mahojiano na shirika moja la utangazaji la kimataifa yaliyofanyika Ukerewe, mkoani Mwanza.

"Mwenye macho haambiwi tazama, yanayofanywa na Rais Magufuli yanaonekana wazi hata yanatoka kwenye vyombo vya habari badala ya kubaki kwenye kumbukumbu za serikali", alisema Msekwa.

Kuhusu demokrasia nchini, Msekwa amesema kuwa hali ya demokrasia nchini inaridhisha kwani viongozi muda wao wa kukaa madarakani ukiisha wanaondoka. Wanaominya demokrasia ni wale wanaong'ang'ania madarakani baada ya kipindi chao kuisha, jambo ambalo kwa Serikali ya Tanzania halipo. Tangu Serikali ya Awamu ya Tano imeingia madarakani mambo mengi yamebadilika na kuwa bora zaidi. Mfano, nidhamu ya watumishi na uwajibikaji serikalini imeongezeka na hivyo ukiritimba na urasimu umepungua.

Huduma za Afya zimeboreshwa kwa kujenga na kukarabati hospitali, zahanati na vituo vya afya. Hii pia ni pamoja na upatikanaji wa dawa hospitalini kupitia bohari ya dawa ya serikali (MSD). 

Kwa kujali afya za Watanzania, Serikali imeongeza bajeti ya dawa kutoka bilioni 39 hadi bilioni 268, jambo ambalo limefafanya upatikanaji wa dawa kuongezeka.

Rais Magufuli: “Mniombee nisijekuwa na kiburi”

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewaomba Watanzania wamuombee asije akabadilika na kuwa na kiburi.

Akizungumza wilayani Kilolo mkoani Iringa katika uwanja wa Luganga, Leo Mei 2 wakati wa uwekaji wa Jiwe la msingi amesema kuwa wamuombee asije akasahau pia ni wapi alikotoka.

“Niwaombe ndugu zangu mniombee, nisije kusahahu nilikotoka, ili niitumikie Tanzania kwa mafanikio makubwa, hata siku nikitoka duniani nikaenda huko, nikaishi kwa furaha kwa sababu niliwatumikia Watanzania wenzangu kwa upendo na mafanikio mazuri,” amesema Rais Magufuli.

“Nataka kuwahakikishia wananchi wa Kilolo, Iringa na Watanzania kwa ujumla sitawaangusha mimi siku zote nitakuwa mtumishi wenu ninajua kuongoza Kiutumishi. Naomba mniombee nisije nikabadilika nisiwe na kiburi.“ Amesema Magufuli.

Rais Magufuli: Baridi imeletwa na Mungu tuwajibike kujikinga na UKIMWI

$
0
0
Rais Magufuli  Leo May 2, 2018 ameweka jiwe la msingi katika ujenzi wa hospital ya Kilolo ambapo amewataka watu wa mikoa ya Njombe na Iringa kuchukua tahadhari juu ya gonjwa la UKIMWI sababu mikoa hiyo ndio inayoongoza nchini.

“Mkoa wa Iringa na Njombe ina maambukizi mengi ya UKIMWI, Iringa una 11.2% na Njombe ni 11.6%. Inawezekana sababu ya msingi ni baridi lakini sina uhakika. Ni lazima tuwajibike katika kujikinga na UKIMWI,” amesema Rais Magufuli.

“Kwahiyo Iringa ni ya pili Njombe ni ya kwanza kwa maambukizi ya Ukimwi nilipofika hapa Kilolo inaonekana shida kubwa hapa ni baridi na kwasababu inaletwa na Mwenyezi Mungu inabidi tujikinge na kuchukua tahadhari zote kwa gonjwa hili.”Amesema Rais Magufuli

Abaka Mtoto Kwa Ahadi Ya Kumpa Andazi

$
0
0
Jeshi  la  Polisi mkoani Shinyanga  linamshikilia Amos Meshack (36), mfanyabiashara wa udongo wa pemba, kwa tuhuma za kubaka mtoto wa umri wa miaka tisa, mwanafunzi wa darasa la pili katika Shule ya Msingi Ndala A Manispaa ya Shinyanga.

Tukio hilo lilitokea juzi  mchana nyumbani kwa mtuhumiwa huyo, Kata ya Ndala.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Simon Haule alisema chanzo cha tukio hilo ni tamaa za  mwili.

Alisema mbinu iliyotumika ni mtuhumiwa kumwita mtoto kwa ahadi ya kumpatia Sh 200 kwa ajili ya kununulia maandazi.

“Kutokana na ahadi hiyo, mtoto aliingia katika nyumba au kibanda ambacho mtuhumiwa hukitumia kufanyia biashara ndogo ndogo za kufinyanga na kutengeneza udongo wa pemba, alimkamata na kumbaka akimsisitiza asieleze chochote kwa mtu yeyote.

“Hata hivyo, mama mzazi wa mtoto aligundua tukio la kubakwa kwa mwanaye  baada ya kumuona akiwa hana furaha na kuamua kumdadisi,” alisema.

Alisema aligundua mwanae  amebakwa baada ya kuona nguo zake za ndani  zikiwa zimefichwa nyuma ya kitanda, huku akionekana mnyonge.

Alisema baada ya kumhoji  mwanae alidai alibakwa na baba Amani ambaye ni Meshack, na kuwa huo ndiyo mchezo wake wa kila siku.

Alisema wakati akianza uchafu huo, alikuwa akimpatia pipi na safari hii alimnunulia maandazi kisha kumvutia ofisini kwake na kumbaka tena.

“Alipelekwa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga kupimwa  na majibu ya daktari yalivyotoka ilibainika amebakwa…mchezo huo amekuwa akifanyiwa kila mara na siyo mara moja,”alisema.

Kamanda Haule  alisema wanamshikilia mtuhumiwa na baada ya uchunguzi   kukamilishwa atafikishwa mahakamani.

Bunge Laibana Serikali Kutekeleza Agizo La Spika Kuhusu Rea

$
0
0
Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge ameitaka Serikali kutekeleza agizo la Spika wa Bunge, Job Ndugai kuhusu kusuasua kwa miradi ya Wakala wa Umeme Vijijini (REA).

Chenge ametoa kauli hiyo leo Mei 2, bungeni jijini Dodoma baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu ambapo wabunge wengi walisimama ili kuuliza maswali ya nyongeza zaidi katika maswali yanayohusu Wizara ya Nishati.

Amesema serikali inapaswa kufuatilia maelekezo ya Spika kwa kuwa lipo tatizo.

“Juzi Spika alielekeza lakini angalieni wabunge waliosimama humu kuna tatizo! Nadhani serikali ifuatilie maelekezo ya Spika, lipo tatizo haiwezekani.. angalieni, suala la letter of credit (barua ya mikopo) ndiyo linasemwa na wakandarasi wote hazijafunguliwa,  letter of credit ni tatizo,” amesema.

Chenge alitoa maelekezo hayo baada ya Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu kujibu swali la Mbunge wa Morogoro Mashariki Kusini (CCM), Omar Mgumba aliyetaka kujua serikali ina mkakati gani wa kuvipatia umeme vijiji vilivyorukwa na miradi wa REA III.

Naibu Waziri huyo alisema mafaili yote ya wakandarasi yameshakusanywa na utaratibu wa kufungua barua hizo za mikopo unaendelea sasa.

Magufuli asema hategemei mtoto wake kupata mkopo elimu ya juu

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema katika utoaji wa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu, kuna vigezo muhimu ambavyo huzingatiwa ikiwa  ni pamoja na kuangalia hali ya familia ya muombaji.

Rais Magufuli amesema hayo leo Mei 02, alipokua akihutubia wanafunzi na uongozi wa Chuo Kikuu cha Mkwawa mkoani Iringa na kuongeza kuwa kwa familia ambazo zinauwezo hasa viongozi hawana sifa za kupata mkopo hata ingekua ni mtoto wake.

“Hiki sio kitu kidogo, kwa mwaka unatoa bilioni 427, kwa nchi masikini kama Tanzania na unapotoa mkopo ni lazima pawepo na utaratibu na taratibu hizo zinaendeshwa na watu, na ndiyo maana mtoto wangu mimi hawezi kupata mkopo, mtoto wa( William) Lukuvi,  mtoto wa Profesa haitaji kupata mkopo, mtoto wa mkuu wa mkoa hatakiwi kupata mkopo” alisema Rais Magufuli

Rais Magufuli amedai kwamba wanafunzi wa elimu wa juu wanaonufaika na mkopo kwa sasa ni zaidi ya 130,000 ambapo serikali imetoa bilioni 427.

Sambamba na hilo Rais Magufuli amekiri serikali kukumbwa na changamoto ya kubaini wanafunzi hewa  wa elimu ya juu zaidi ya 3500 katika orodha ya wanufaika na mikopo.

Katibu Mwenezi CCM Apigwa Risasi na 'Watu Wasiojulikana'

$
0
0
Aliyewahi kuwa Katibu Mwenezi, CCM Wilaya ya Sumbawanga Mkoani Rukwa Ndg. Benedict Chapewa ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando amesema kuwa Bw. Chapewa alivamiwa na kundi la watu wasiojulikana wakati akiwa anakunywa pombe katika moja ya baa anayomiliki kijijini hapo.

Kamanda Kyando amesema kuwa Chapewa ambaye ni Mtendaji wa Kata ya Mwandui iliyopo mwambao wa bonde la ziwa Rukwa alimiminiwa risasi na watu hao kwa kutumia bunduki aina ya gobore kisha kumkata kata na mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake.

Hata hivyo amesema kwamba baada ya wauaji kutekeleza adhima yao waliondoka kuelekea kusikojulikana na hawakuchukua kitu chochote kutoka kwa marehemu wala katika baa hiyo.

Kamanda Kyando amesema uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo unaendelea kufanyika na watuhumiwa wanasakwa popote walipo ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.


James Mbatia aungana na Mkapa ........“Tupo kwenye janga, tunaangamia”

$
0
0
Mbunge wa Vunjo James Mbatia ambaye ni mdau mkubwa wa elimu amesema kwamba  umefika wakati wa kukubali kuwa hali ya elimu ya Tanzania ni janga hivyo mjadala ufanyike kama walivyoshauri marais wastaafu.

Mbunge huyo ameyasema hayo bungeni wakati  akichangia hoja katika bajeti ya wizara ya elimu, iliyowasilishwa Bungeni na waziri mwenye dhamana, Pro. Joyce Ndalichako.

"Mzee Mkapa amesema kwamba elimu yetu tunahitaji mjadala wa kitaifa. Mzee Kikwete naye ametamka . Sasa nani mwingine atamke zaidi mpaka tuhakikishe kwamba tunaangamia elimu yetu?" Mbatia.

Ameongeza "Mh. Mwenyekiti niseme 'The way Foward' tukubali elimu yetu tupo kwenye janga ni maafa na ukiwa na maafa naomba tusiwe na tofauti za kiitikadi huku ndani. Tusimame  sote kwa pamoja na Mh. Waziri yote tunayoyasema naomba uyachukulie very positive kwa ajili ya kujenga Taifa letu, Wizara yetu pamoja na kujenga watoto wetu na kizazi chetu".

Hata hivyo Wabunge wanatarajiwa kujadili na kuipitisha bajeti ya wizara ya elimu sayansi na teknolojia ya zaidi ya shilingi trilioni 1.4 kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images