Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Vikosi vya Simba SC na Yanga SC vyatangazwa

$
0
0
Klabu ya Simba na Yanga  leo zinakabiliana kunako dimba la Uwanja wa Taifa ambapo  tayari vikosi vya timu zote mbili vimeshatangazwa.

Yanga wao watawakosa wachezaji wao muhimu kama Amis Tambwe na Donald Ngoma ambao wote ni majeruhi huku Simba ikiwa na wachezaji wake wote muhimu ambapo mashambulizi yataongozwa na Emmanuel Okwi na John Bocco.

Klabu ya Simba inaongoza ligi kwa pointi 59 ikifuatiwa na Azam FC wenye pointi 46 na Yanga ni ya tatu kwenye msimamo kwa alama 48.

Hata hivyo Simba imecheza michezo mingi 25 huku mahasimu wao wakiwa na viporo vya mechi mbili (23).
Kikosi cha Simba SC kitakachoanza dhidi ya Yanga SC,
 1. Youthe Rostand
2. Hassani Kessy
3. Gadiel Mbaga
4. Andrew Vicent
5. Kelvin Yondani
6. Saidi Juma
7. Yusufu Mhilu
8. Papy Tshishimbi
9. Obrey Chirwa
10. Rafael Daudi
11. Ibrahim Ajibu

Benchi
– Ramadhani Kabwili
– Abdallah Shaibu
– Juma Abdul
– Juma Mahadhi
– Maka Edward
– Pius Buswita
– Emanuel Martin


Kikosi cha Simba SC kitakachoanza dhidi ya Yanga SC, mechi ya Ligi Kuu Bara
1. Aishi Manula
2. Erasto Nyoni
3. Nicholas Gyan
4. Yusufu Mlipili
5. James Kotei
6. Jonasi Mkude
7. Asante Kwasi
8. Shomari Kapombe
9. John Bocco
10. Emanuel Okwi
11. Shiza Kichuya

Kikosi cha akiba

12. Mohamed Nduda
13. Paul Bukaba
14. Said Ndemla
15. Mzamiru Yassin
16. Laudit Mavugo
17. Rashid Juma
18. Mohamed Hussein

Muleba: Watoto 2 wapoteza maisha baada ya kugongwa na Basi, wengine 20 wajeruhiwa

$
0
0
Watoto wawili wamefariki kwa kugongwa na basi lenye namba za usajili T720 EEV ambalo linafanya safari zake Bukoba kwenda Mwanza na kisha basi hilo kupinduka na kusababisha majeruhi ya watu 20 waliokuwa kwenye basi hilo.

Ajali hiyo imetoka katika Kitongoji cha Katongo kjiji cha Rulanda kata ya Rulanda Wilayani Muleba Mkoani Kagera na gali hilo likapinduka na kusababisha majeruhi ya watu watatu.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Rulanda, Evart Erenest amesema kuwa tukio hilo limetokea leo majira ya asubuhi ambapo watoto hao walikuwa wanavuka barabara wakielekea msikitini.

Amewataja watoto waliofariki ni Muhajiri Abdumajidi mwenye umri wa miaka 6 ambaye ni mkazi wa kata ya Gwanseli pamoja na Abdallah Alidi mwenye umri wa miaka 7 ambaye naye ni mkazi wa kata ya Rulanda.

Aidha abiria waliojeruhiwa wameokolewa na wenzao na wamepelekwa katika hospitali ya Rubya wilayani Muleba mkoani humo.

Hata hivyo, mashuhuda wamesema kuwa sababu kubwa ya ajali hiyo ni hali mbaya ya hewa katika eneo hilo iliyosababishwa mvua zinazoendelea kunyesha.

Rais Magufuli amlilia Abbas Kandoro

$
0
0
Rais John Magufuli ametuma salamu za rambirambi za kifo cha mkuu wa mkoa mstaafu, Abbas Kandoro akisema Taifa limepoteza mtu muhimu ambaye mchango wake hautasahaulika.

Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Gerson Msigwa aliyoitoa leo Aprili 28, 2018 amesema Rais Magufuli Kandoro alikuwa kiongozi shupavu, aliyejiamini na kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria na taratibu, aliwapenda watu aliowaongoza na alidhirisha uzalendo wa kweli.

“Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mkuu wa Mkoa mstaafu Abbas Kandoro, nawapa pole wana familia, ndugu, jamaa na marafiki wote walioguswa na msiba huu,” amesema Rais Magufuli na kuongeza:

“Tumempoteza mtu muhimu ambaye mchango wake katika utumishi kwa umma katika nyadhifa mbalimbali zikiwemo mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya na mkurugenzi wa halmashauri hautasahaulika.”

Rais Magufuli amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza kufikisha salamu hizo kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huo.

“Nimesikitishwa sana na kifo chake, nawaombea wafiwa wote wawe na moyo wa subira, uvumilivu na ustahilivu katika kipindi hiki cha majonzi na pia namuombea marehemu Abbas Kandoro apumzike mahali pema peponi, Amina,” amesema Rais Magufuli

Enzi za utumishi wake, Kandoro amehudumu mikoa ya Tabora, Arusha, Dar es Salaam, Mwanza na Mbeya.

Kandoro alifariki jana Aprili 27, 2018 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) na anatarajiwa kuzikwa kesho Aprili 29, 2018 mkoani Iringa.

Muhimbili Kupandikiza Figo Wagonjwa 200 Kwa Mwaka

$
0
0
Hospitali ya Taifa Muhimbili  (MNH) imeweka mipango ya muda mrefu na muda mfupi ili kuhakikisha huduma ya upandikizaji figo inakuwa endelevu, na imedhamiria kupandikiza figo kwa wagonjwa zaidi 200 kwa mwaka.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dare es Salaam na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Wateja wa MNH, Aminiel Aligaesha wakati akizungumza na waandishi wa habari  mara baada ya kuruhusiwa wagonjwa wawili ambao wamepandikizwa figo Aprili mwaka huu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Amesema katika  mpango wa muda mfupi, kila mwezi hospitali hiyo itapandikiza figo wagonjwa watano, hivyo kwa mwaka itakuwa imefanikiwa kupandikiza figo wagonjwa 60.

“Mipango ya muda mrefu ni kuwa na sehemu maalum ya upandikizaji figo na hivi karibuni MNH itaanza ujenzi wa jengo jipya la ghorofa saba na katika jengo hilo tutatenga sehemu maalum ya upandikizaji figo , kila siku mgonjwa mmoja atapandikizwa figo, kwa wiki tutakuwa tumepandikiza figo wagonjwa watano, kwa mwezi wagonjwa 20 na kwa mwaka tutafanikiwa kupandikiza figo wagonjwa 240,’’ amesema Aminiel.

Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Magonjwa ya Figo  Muhimbili , Dkt. Jacqueline Shoo amesema tukio hilo ni la kihisoria kwani mwaka jana  hospitali ilifanikiwa kupandikiza figo mgonjwa mmoja  na Aprili mwaka huu hospitali hiyo imepandikiza figo wagonjwa wanne kwa mfululizo.

Naye Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo MNH, Dkt. Onesmo Kisanga amesema takribani wagonjwa 800 nchini wanasubiri huduma ya upandikizaji figo na kati ya hao 50 tayari wameandaliwa.

Kwa upande wao wagonjwa waliopandikizwa figo na kuruhusiwa leo, Bi. Suzana John na Bi. Asha Athuman Kisebengo wameishukuru Hospitali ya Taifa Muhimbii  pamoja na waaalam wake kwa kuwapatia matibabu ya ubingwa wa juu ambayo awali hayakuwepo nchini.

Aliyejiuzulu udiwani Chadema, avuliwa uanachama

$
0
0
Katibu wa Chadema, Kanda ya Iringa Mjini, Suzana Mgonokulima, ametangaza kumvua uanachama  aliyekuwa diwani wa chama hicho, Kata ya Gangilonga, Dady Igogo. Igogo pia alikuwa Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa.

Katika taarifa iliyotolewa leo Aprili 28, imeelezwa kuwa Igogo amevuliwa uanachama kwa kuwa alikisaliti chama kwa kujivua nafasi ya unaibu meya na baadaye udiwani.

“Ndugu Igogo kwa muda mrefu amekuwa na mwenendo usioendana na itikadi, falsafa, madhumuni, kanuni, maadili na sera za chama,” imesema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imesema kamati tendaji ya jimbo katika kikao chake cha dharura kilichoketi Aprili 24 mwaka huu kiliadhimia Igogo avuliwe ujumbe wa kamati tendaji ya jimbo, kwa kwenda kinyume na katiba ya chama kanuni na maadili.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Igogo amevuliwa uanachama kuanzia leo Aprili 28 kama ilivyokubaliwa na wajumbe wa kamati.

Amber Lulu: Sina mpango wa mtoto kwa sasa

$
0
0
Msanii wa muziki Bongo na Video Vixen, Amber Lulu amefunguka mipango yake ya kuitwa mama.

Muimbaji huyo anayefanya vizuri na ngoma ‘Jini Kisirani’ ameiambia XXL ya Clouds FM kuwa bado anajipanga kwa ajili ya suala hilo ila kwa sasa hana mpango.

“Kwa kweli kwa sasa hivi sijatarajia bado, vitu vyangu vingi bado sijakamilisha,” amesema.

“Sio Gigy Money amepata mtoto na mimi nipate, no! unajua unapopata mtoto kuwe na maandalizi yake. Labda yeye rafiki yangu kajiandaa mtoto lazima aje kwenye mazingira mazuri,” ameongeza.

Gigy Money ambaye yupo katika mahusiano na Mtangazaji wa Choice FM, M o J alijifungua mtoto wa kike usiku wa kuamkia jana April 27, 2017 na amempa mwanae jina Mayra.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya April 29

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya Leo April 30


Rais Magufuli asema hakula nyama mwezi mmoja akiwa Iringa Sekondari ya Mkwawa.

$
0
0
Rais John Magufuli amesimulia mara ya kwanza alipopelekwa mkoani humo kusoma kwamba hakula nyama kwa mwezi mmoja baada ya kutahadharishwa na watu kuwa akifika asile kitoweo hicho.

Akihutubia wakazi wa Iringa wakati wa ufunguzi wa barabara ya Iringa-Fufu jana Aprili 29, 2018; Rais Magufuli alisema alifika Iringa kwa mara ya kwanza mwaka 1978/79 kwa ajili ya masomo katika Sekondari ya Mkwawa.

“Niliambiwa usile nyama, usile mshikaki Iringa na kweli sikula," alisema na kwamba, baada ya kukaa muda alibaini wakazi wa Iringa hasa wanaume kuwa ni wakarimu.

"Wanaume wa Iringa ni wapole sana, unamchokoza lakini anajinyonga yeye badala ya kukuadhibu wewe," aliongeza Rais Magufuli huku akishangiliwa na umati wa wananchi.

Anasema watu wa Iringa ni tofauti na wenzao wa mkoani Mara ambao ukiwachokoza utakiona cha mtema kuni.

Rais Magufuli Alivyofungua Barabara ya lami ya Iringa – Migoli – Fufu

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amefungua barabara ya lami ya Iringa – Migoli – Fufu yenye urefu wa kilometa 189 na ambayo inaunganisha Mkoa wa Iringa na Mkoa wa Dodoma.

Barabara hiyo ambayo ni sehemu ya barabara kuu ya kuanzia Cape Town nchini Afrika Kusini hadi Cairo nchini Misri (The Great North Road) imejengwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 207.457 ikiwa ni ufadhili wa benki ya maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa asilimia 65.9, Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) kwa asilimia 21.3 na Serikali ya Tanzania imetoa asilimia 12.8.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale amesema kukamilika kwa barabara hiyo kumeondoa adha iliyowakumba wananchi kwa miaka mingi ambapo safari ya Iringa – Dodoma iliyochukua siku nzima ama siku kadhaa wakati wa mvua, sasa inachukua muda wa saa 2:30.

Balozi wa Japan hapa nchini Mhe. Masaharu Yoshida na Mwakilishi wa AfDB Bw. Jeremy Aguma wameipongeza Serikali ya Tanzania kwa utekelezaji mzuri wa miradi inayofadhiliwa na taasisi zao, na wameahidi kukuza zaidi ushirikiano katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo itakayosaidia kukuza uchumi wa wananchi kama inavyoelekezwa katika dira ya maendeleo ya mwaka 2025.

Wabunge wa Mkoa wa Iringa wakiongozwa na Mbunge wa Ismani na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi wamemshukuru Mhe. Rais Magufuli kwa juhudi zake zilizoyawezesha majimbo yao kupata miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa barabara, vituo vya afya na zahanati, Maji, uwanja wa ndege wa Nduli, Umeme, ruzuku ya elimu na dawa.

Akizungumza na wananchi waliojitokeza katika ufunguzi wa barabara hiyo Mhe. Rais Magufuli amewapongeza kwa kupata barabara ya uhakika na amewataka kuongeza juhudi katika uzalishaji mali hasa katika kilimo na biashara ili waweze kunufaika nayo.

Mhe. Rais Magufuli amezishukuru AfDB na JICA kwa kuendelea kuwa washirika muhimu wa maendeleo ya Tanzania, na kwa namna ya pekee amempongeza Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Patrick Mfugale kwa uchapakazi wake, ubunifu, uaminifu na uadilifu uliomwezesha kuiongoza TANROADS kwa mafanikio hasa katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara na madaraja.

Mhe. Rais Magufuli amesema pamoja na kujenga barabara hiyo, Serikali inauboresha uwanja wa ndege wa Nduli ili uweze kupokea ndege kubwa zitakazoleta watalii wengi na wafanyabiashara katika mkoa wa Iringa na maeneo mengine ya kusini mwa Tanzania ili rasilimali zilizopo katika maeneo hayo ikiwemo Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ziwanufaishe wananchi kama wanavyonufaika wananchi wa Kaskazini mwa Tanzania.

“Ruaha ni hifadhi kubwa, nataka hifadhi hii iwe kitovu cha utalii, nataka nyinyi ndugu zangu wa Iringa mnufaike na utalii katika hifadhi hii kama wanavyonufaika kule kaskazini kupitia Serengeti, watalii wakija hapa wenye hoteli watapata wateja, wenye maziwa watauza, wenye matunda watauza, wenye mahindi watauza, mtapata hela” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewataka wananchi wa Iringa kuwapuuza wanaodai Serikali inakopa sana, na kueleza kuwa fedha hizo hukopwa kwa masharti nafuu, riba ndogo na hulipwa kwa muda mrefu, na kwamba ndizo zinatumika kujenga miundombinu ya kuchochea uchumi.

Pamoja na Mke wa Rais Mhe. Mama Janeth Magufuli sherehe hizo pia zimehudhuriwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Yustino Ndugai, Mawaziri, Wabunge kutoka kamati ya bajeti na kamati ya miundombinu, Maaskofu na viongozi wa vyama vya siasa.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Iringa
29 Aprili, 2018

Tanzania yatumia Dola milioni 200 kuagiza chakula

$
0
0
Na Mahmoud Ahmad Dodoma
Imeelezwa kuwa hapa nchini TANZANIA hutumia zaidi  ya dola milioni 200 sawa na bilioni 400(Mutungi and Affognon 2013)  kuangiza chakula kutoka nje ya nchi kila mwaka hali inayosabaisha wakulima wadogo wadogo kulazimika kuuza mazao yao kwa bei ya nchini.

Hayo yalibainishwa mwishoni mwa wiki  na Afisa habari wa wakulima wadogo Tanzania Flora Mlowezi wakati wa mkutano wa wadau wa sekta ya kilimo na kamati ya bunge kilimo, mifugo na maji  uliofanyika bungeni jijini Dodoma.

Mlowezi alisema wakulima wanalazimika kuuza mazao kwa bei ya chini kwa sababu ya uwezo mdogo kwenye usimaminzi wa mazao baada ya mavuno.

Aliongeza kuwa katika Afrika Mashariki ni asilimia tano tu ambayo huwekezwa kwenye usimaminzi wa mazao baada ya mavuno na asilimia 95 hutumika katika uzalishaji.

‘’Thamani ya upotevu kwenye nafaka kwa mwaka ni zaidi ya dola milioni nne sawa na bilioni nane (Rockeffer foundation)’’alisema.

Alifafanua kuwa zaidi ya asilimia 70 ya wanawake wa Tanzania wanahusika katika uzalishaji wa mahitaji ya chakula pia sera ya Taifa ya kilimo ya mwaka 2013 imesema zaidi ya asilimia 90.4 ya wanawake wa Tanzania wanajihusisha na shughuli za kilimo na kutimiza lengo namba mbili la ajenda ya malenho endelevu (2030).

‘’Wengi wao ni wakulima wadogo ambao hawana uwezo wa kuendesha shughuli za kilimo kwa ufasaha kutokana na changamoto mbalimbali kama upatikanaji wa pembejeo kwa wakati na kwa bei nafuu, ukosefu wa taarifa, mitaji na kufikiwa na huduma za ugani pamoja na uhakika wa ardhi,’’alisema Mlowezi.

Naye msemaji wa shirika lisilo la kiserikali la Action Aid Joram Wimmo alisema katika bidhaa ya maziwa bado upo uwezekano wa kuzalisha zaidi kutokana na hivi sasa kuwa katika kiwango cha chini.

Alisema hivi sasa kuna  viwanda 75 vya maziwa vyenye uwezo wa kusindika lita 672,000 kwa siku , uwezo wa sasa kwa siku ni lita 155,450 sawa na asilimia 23.3 kwa siku.

‘’Maziwa yanayozalishwa ni wastani wa lita bilioni 2.2 kwa mwaka, kati ya hayo ni asilimia 10 tu ndiyo yanayoingia katika mfumo rasmi  wa soko kutokana na kiasi kidogo kinachosindikwa nchini bado tunatumia kiasi cha Sh. bilioni 23.6 kuagiza maziwa nje ya nchi kwa mwaka,’’ alisema Wimmo.

Wimmo aliiomba serikali kutenga fedha ya kutosha ili kuboresha huduma za ugani na pembejeo ,serikali kutekeleza miongozo kwa kuzingatia ikama ya kila kijiji kwa kila watu 600 awepo afisa ugani mmoja au zaidi.

Mara baada ya kupokea taarifa hiyo wabunge wa kamati ya kilimo, mifugo na maji akiwemo mwenyekiti wa kamati hiyo Christine Ishengoma alisema wameipokea taarifa hiyo na kuahidi kuifanyia kazi na kuishawishi serikali kuongeza bajeti ili kuweza kutatua changamoto hizo.

Lengo la mkutano huo ni kuwasilisha mapendekezo ya wakulima kwa kamati ya kilimo, mifugo na maji ili waishauri Serikali kutwenga bajeti yakutosha ili kuwepo na uboreshwaji wa miundombinu kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji.

Polisi anayedaiwa kumuua mdogo wa Heche Afikishwa Mahakamani

$
0
0
Askari polisi E. 1156 William Marwa amefikishwa mbele ya Mahakama ya Hakimu mkazi wilaya ya Tarime, akikabiliwa na shtaka la mauaji ya Saguta Chacha ambaye ni mdogo wa Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche.

Mshtakiwa huyo amesomewa kesi ya mauaji namba, PI 76/2018 mbele ya Hakimu A.R. Kahimba leo Aprili 30.

Askari huyo anayedaiwa kutenda kosa hilo Aprili 27 hakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo.

Mahakama Yatoa Amri Hans Pope Wa Simba Kukamatwa

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Jumatatu imetoa amri ya Mwenyekiti wa Kamati ya  Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe na Franklin Lauwo wakamatwe na wafikishwe mahakamani hapo kuunganishwa katika kesi  ya utakatishaji fedha inayomkabili rais wa timu hiyo, Evans Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’.
 
Aveva na Kaburu wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha fedha  kiasi cha dola 300,000 za Kimarekani.
 
Amri hiyo imetolewa na hakimu mkazi mkuu wa mahakama hiyo, Thomas Simba baada ya wakili  Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini  (TAKUKURU), Leonard Swai kubadilisha hati ya mashtaka na kuwaongeza watuhumiwa hao.
 
Swai alidai kuwa  amewatafuta washitakiwa hao toka machi tatu mwaka huu  bila mafanikio na kuomba hati ya kuwakamata washitakiwa hao ambao hawakuepo mahakamani.

Waziri Mkuu Afungua Kikao Cha Mawaziri, Wakuu Wa Taasisi

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akifungua Kikao cha Kazi cha Mawaziri, Naibu Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Taasisi na Viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, kilichofanyika kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma Aprili 29, 2018.

Picha na Ofisi ya Waziri Mku

CHADEMA wakanusha habari ya Tundu Lissu kuwasili muda wowote

$
0
0
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kimekanusha taarifa zinazoendelea mitandaoni kuhusu uwezekano wa kurejea nchini kwa Mwanasheria Mkuu wa Chama hicho, Tundu Lissu kutokea Ubelgiji alipokuwa akipatiwa matibabu tangu mapema Januari mwaka huu.

Kupitia kwa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano CHADEMA, Ndg. Tumaini Makene amesema kwamba kupitia mitandaoni mapema leo kumekuwa na taarifa za kwamba Lissu anatarajiwa kurejea nyumbani Tanzania wakati wowote kuanzia juzi, kwamba amemaliza matibabu yake kitu ambacho sicho cha kweli na kimezua taharuki.

Katika taarifa yake Ndg. Makene amesema kwamba Mwanasheria huyo ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki, hajazungumza na mwandishi wa habari yeyote juu ya kurejea kwake nyumbani kwa sababu zilizo wazi kabisa kuwa bado hajapona na anatarajiwa kufanyiwa upasuaji mwingine mwisho wiki hii au wiki ijayo.

Hata hivyo chama hicho kimetoa wito kwa na wanachama na Watanzania wote wenye mapenzi mema kutokana na kuguswa na uzito wa masahibu yaliyompata Lissu wameendelea kuguswa na kufuatilia kwa ukaribu maendeleo ya matibabu na hali ya afya yake kupuuza taarifa hizo.

Tundu Lissu yupo nchini Ubelgiji akipatiwa awamu ya tatu ya matibabu baada ya kumaliza matibabu nchini Kenya mwezi Januari ambapo alikuwepo huko kwa takribani miezi minne ambapo alikuwa akiuguza majeraha ya risasi.

Mbunge huyo machachari alipigwa risasi zilizokadiriwa 37 nje ya makazi yake huko Jijini Dodoma majira ya saa 7 mchana na watu wasiojulikana wakati alipokuwa akitoka kwenye majukumu yake ya kibunge.

PWANI: Watatu Wafariki Dunia Na 530 Wakutwa Na Dalili Za Saratani Ya Mlango Wa Kizazi

$
0
0
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
JUMLA ya akinamama 20,815 waliofanyiwa uchunguzi wa saratani ya mlango wa shingo ya kizazi mkoani Pwani katika kipindi cha miaka mitatu kati yao 530 walikutwa na dalili za awali za saratani hiyo,ambapo watatu walifariki.
 
Aidha kati ya akinamama hao waliofanyiwa uchunguzi akinamama 412 walitibiwa matibabu na  115 walipata rufaa ya kwenda Oceanroad na hospitali ya Taifa ya Muhimbili  kwa matibabu zaidi.
 
Akitoa takwimu hizo ,wakati wa uzinduzi wa zoezi la chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa shingo ya kizazi kwa watoto wenye umri wa miaka 14 ,kimkoa yaliyofanyika kituo cha afya mkoani,Kibaha,mganga mkuu wa Mkoa wa Pwani ,Yudas Ndungile alisema , ipo changamoto ya kutojua idadi ya vifo kamili kwa kuwa wengi hupata rufaa.
 
Pamoja na hayo ,alisema ipo haja ya kuona ukubwa wa tatizo hilo kwa kuangalia afya mapema na watoto wa mashuleni kupata chanjo.
 
Ndungile alisema jumla ya watoto wa kike 18,823 waliopo shule na nje ya shule mkoani hapo watapatiwa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi mwaka huu.
 
Alielezea, tayari wameshapokea chanjo na wataanza kuzitoa katika vituo mbalimbali vya huduma.
 
Ndungile aliitoa shaka jamii kuwa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi ni salama ,haina madhara na haiathiri uwezo wa binti kupata watoto hapo baadae
 
” Serikali imethibitisha usalama wa umadhubuti wa chanjo ya kukinga saratani ya mlango wa kizazi ndiyo maana imeiongeza kwenye mpango wa Taifa wa chanjo ili iweze kusaidia kudhibiti tatizo hilo kwa akinamama”:
 
Ndungile alieleza mwaka 2018 chanjo itatolewa kwa wasichana waliofikisha umri wa miaka 14 na ili kupata kinga kamili walengwa watahitaji kupatiwa dozi mbili.
 
Alisisitiza chanjo hiyo huwakinga wasichana wasipate saratani ya mlango wa kizazi pindi wawapo watu wazima wakiwa na familia zao.
 
“Nchini Tanzania saratani ya mlango wa kizazi ni ya kwanza kwa vifo ikifuatiwa na saratani ya matiti ” Saratani hizi mbili kwa pamoja husababisha zaidi ya asilimia 50 ya vifo vyote vya wakinamama vitokanavyo na saratani”alibainisha Ndungile.
 
Kwa upande wake ,Mganga mkuu wa halmashauri ya Mji wa Kibaha ,Dkt.Tulitweni Mwinuka alisema ,wamezindua chanjo hiyo kwa wasichana wenye umri wa miaka 14.
 
Alielezea ,kiwilaya wamezindua chanjo hiyo kwa wasichana 100 kituoni hapo na wanatarajia kufanikisha na kuleta matokeo kutokana na chanjo hiyo .
 
Akizindua zoezi hilo ,kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Pwani,mkuu wa wilaya ya Kibaha Assumpter Mshama aliwataka wanafunzi wa kike kuacha kujiiingiza kwenye vitendo vya ngono mapema ili kujiepusha kuingia kwenye hatari ya kupata magonjwa ya zinaa,ukimwi na hata saratani ya mlango wa kizazi.
 
Alisema moja ya sababu zinazosababisha saratani hiyo ni kuwa na wanaume wengi ,kuvuta sigara ,wenye mitala, na kuanza mapema kufanya ngono.
 
“Acheni kujiingiza kwenye mapenzi mapema ni hatari katika maisha yenu, ukivua sketi ,na mwanaume akavua suruali jua kuna hatari ya kuhatarisha maisha yako kwa magonjwa yanayosababishwa kutokana na ngono”
 
“Jizuieni hadi hapo mtakapoolewa ,msikimbilie ngono za haraka,mtapata saratani”: alisisitiza Mshama.
 
Mshama aliwahimiza wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao wa kike wenye umri wa miaka 14 kupata chanjo hiyo kwani haina madhara.

NIDA Yafafanua Tangazo La Ajira Mtandaoni

Mbunge Alalamika Kuminywa na Kiti Bungeni

$
0
0
Katika hatua isiyo ya kawaida leo Bungeni Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini ametoa mwongozo akitaka viti vya bungeni kukarabatiwa kwa kuwa viti hivyo ni vibovu na vinawapa shida wabunge.

Salasini ameyasema hayo kwenye kipindi cha Maswali na majibu huku mwongozo wake ukiitaka serikali itoe majibu ni lini viti hivyo vitakarabatiwa ili kuwaondolea adha wabunge wakati wa vikao.

''Mh. Spika viti hivi tunavyokalia havipo kwenye hali nzuri kabisa, vimechakaa na havifanyiwi marekebisho na leo kiti changu kimenifinya makalio. Je ni lini vitafanyiwa ukarabati ?,'' amesema Selasini.

Baada ya kuomba muongozo huo Spika wa Bunge Mh. Job Ngudai amesema kuwa suala hilo limepokelewa na litatolewa ufafanuzi.

Mfanyabiashara Atiwa Mbaroni Mwanza Kwa Mauaji

$
0
0
Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza linamshikilia mfanyabiashara wa samaki aliyefahamika kwa jina la Nicholas Light (25) kwa tuhuma za kumuua mpenzi wake kwa kumnyonga hadi kufa wilayani Nyamagana.

Hayo yameelezwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Naibu Kamishna wa Polisi, Ahmed Msangi wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari hii leo Aprili 30, 2018 na kumtaja mwanamke anayedaiwa kuuliwa na mfanyabiashara huyo kuwa ni Victoria Swai (26) ambaye alikuwa akifanya kazi katika kampuni inayohusika na masuala ya anga. 

Kamanda Msangi amesema chanzo cha mauaji hayo inasemekana kuwa ni wivu wa kimapenzi ambapo inadaiwa mtuhumiwa alikuwa akimtuhumu marehemu kuwa anamsaliti kimapenzi, jambo ambalo lilisababisha kuzua ugomvi kati yao na kupelekea Nicholas kumnyonga mwanamke huyo kwa kumkaba shingo akiwa ofisini kwake na baadae kukosa pumzi hadi kufariki dunia.

Aidha, Kamanda Msangi amesema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa Bugando kwa ajili ya uchunguzi na pindi uchunguzi utakapokamilika utakabidhiwa kwa ndugu wa marehemu ili waweze kufanya mazishi.

Kwa upande mwingine, Kamanda Msangi amewapa pole ndugu na familia kwa msiba walioupata pamoja na kutoa wito kwa wakazi wa jiji la mkoa wa Mwanza hususani vijana kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi pindi wanapokuwa kwenye migogoro.

Wizara Ya Afya Yazindua Mfumo Wa Tehama Kwa Vituo Vya Kutolea Huduma Za Afya Nchini

$
0
0
Na: Lilian Lundo – MAELEZO, Dodoma.
Wizara wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  imezindua mfumo mpya wa TEHAMA kwa vituo vya kutolea huduma za afya ikiwa na lengo la kuboresha utoaji wa huduma za afya katika  vituo vyote hapa nchini.

Uzinduzi huo umefanywa na Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile leo, Jijini Dodoma ambapo pia alizindua kanuni za sheria ya uongozi wa hospitali za watu binafsi, mwongozo wa viwango vya msingi kwa vituo vya kutolea huduma za afya nchini pamoja uzinduzi wa bodi mpya ya ushauri wa hospitali za watu binafsi.

“Nina uhakika maombi ya usajili wa vituo vya afya sasa yataenda kwa haraka. Waombaji watajaza fomu na kulipia hukohuko walipo bila kufika ofisini  na vile vile watakuwa na uwezo wa kutumia mfumo kwa kutumia simu zao,” alisema Dkt. Ndugulile.

Amesema Sekta ya Afya ni miongoni mwa sekta muhimu katika Serikali ya Awamu ya Tano ambapo sekta hiyo ni ya tatu kwa kupata  bajeti kubwa. Aidha  kwa mwaka huu wa  fedha jumla ya vituo vya afya 208 vimeboreshwa kwa ajili ya kutoa huduma ya dharura ya mama na mtoto.

Dkt. Ndugulile amesema ndani ya bajeti hii vituo vya afya 67 vitajengwa nchini pamoja na hospitali za rufaa kwa mikoa ambayo haina hospitali za rufaa.

Wakati huo huo, Waziri Ndugulile ameutaka Mfuko wa Taifa wa Bima wa Afya (NHIF) kufanya majukumu iliyopewa ikiwa ni pamoja kusajili vituo vyenye uwezo wa kutoa huduma kutokana na vigezo vilivyowekwa na mfuko huo na kuziachia mamlaka  nyingine majukumu yake ya kukagua vituo hivyo kama vile mikataba ya kazi ya wafanyakazi wa vituo husika.

Aidha ameutaka mfuko huo kutafakari juu ya masharti yaliyowekwa katika kusajili vituo ambapo kituo hakiwezi kusajiliwa mpaka kiwe katika uangalizi na mfuko huo kwa miaka isiyopungua mitano.

Naye, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Otilia Gowele amesema kanuni mpya za sheria ya uongozi wa hospitali za watu binafsi zitasaidia kusogeza huduma kwa wananchi pia hospitali hizo kutoa huduma kulingana na mahitaji ya sasa.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images