Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania Yajivunia Ndege ya Emirates kutua Dar...Yasema Imeipaisha Anga la Tanzania

0
0
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imesema kutua kwa ndege ya Emirates Airbus A380-800 kumewaongezea kujiamini katika biashara ya usafiri wa anga duniani.

Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari amesema leo Aprili 27, jijini Dar es salaam kuwa Emirates walichagua uwanja wa JNIA Dar es Salaam kutokana na kuzingatiwa kwa vigezo vya kimataifa vya uwanja huo.
 
Ndege hiyo  inalotajwa kuwa moja ya ndege kubwa duniani, ilitua kwa dharura JNIA Aprili 24 kutokana na hali mbaya ya hewa Mauritius, ilikokuwa ikielekea.

 Hata hivyo ndege hiyo iliondoka Aprili 25 kwenda Mauritius.

Kamati ya Bunge yaiponda serikali kufungia nyimbo za wasanii

0
0
Kamati ya Bunge ya Huduma za Maendeleo ya Jamii imeuponda utaratibu unaotumika na Serikali wa kufungia nyimbo za wasanii, zisizoendana na maadili ya kitanzania kwa maelezo kuwa unaleta changamoto kwa wasanii.

Akiwasilisha maoni ya kamati hiyo kuhusu bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo mwaka 2018/19 kwa niaba ya mwenyekiti wake Peter Serukamba, mbunge wa Ludewa (CCM), Deogratius Ngalawa amesema vyombo vinavyohusika na usimamizi vinapaswa kuhakikisha vinatimiza majukumu yake kwa kukagua nyimbo zote za wasanii kabla hazijatoka.

“Lengo ni kuhakikisha hakuna wimbo unaotoka kama haujazingatia maadili. Kuangalia nyimbo ambazo ni za kimataifa na kuzipa kibali maalum kwa maana ya muda na mahali pa kuutumia wimbo huo kabla haujaanza kutumiwa na vyombo vya habari.

Rais Magufuli Atoa Maagizo Mazito kwa Viongozi Kondoa, Hanang

0
0
Rais John  Magufuli amewaonya viongozi wenye migogoro hususani wilayani Kondoa, kuacha kutofautiana na wakae pamoja ili kuyamaliza matatizo yao na kusisitiza pande zote zenye migogoro kuanza upya na kwamba siyo kila tatizo lazima lifikishwe kwake.

Rais Magufuli amefunguka hayo leo Ijumaa  mjini Kondoa wakati wa ufunguzi wa barabara ya Dodoma hadi Babati yenye urefu wa kilomita 251.

Amesema, Tanzania ni moja na watu wote wanahitaji maendeleo hivyo migogoro ya baadhi ya vingozi inachelewesha maendeleo ya wananchi.

"Viongozi wa Kondoa muache kugomba leo nimeona niwape meseji live muache kugombana niliwateua mimi nitawatoa mimi. Kuna wakati unakuta Hanang na Kondoa wanagombania mipaka utafikiria ni nchi jirani hilo nalo linakaa muda mrefu hata viongozi wanashindwa kulitatua hivyo ifike mahali tumalize migogoro hii" Rais Magufuli.

Ameongeza "Siyo kila mgogoro, lazima uletwe kwa rais. Nitaimaliza mingapi?  Viongozi waliopo washughulikie migogoro ya saizi yao. Tanzania ni kubwa na inachangamoto nyingi, hivyo ninyi ni viongozi mnatakiwa muelewane kwa manufaa ya wananchi wenu.  Nafahamu viongozi hampendi kuzungumzwa hadharani. Mimi nazungumzaga tu ndiyo tatizo langu. Naomba mkaniombee labda nibadilike," amesema rais Magufuli.

Msukuma Awakingia Kifua Wasanii Bungeni

0
0
Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Msukuma amesema kufungia nyimbo za wasanii nchini si jambo sahihi kwa maendeleo ya wasanii hao.

Akizungumza katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo waka 2018/19, Msukuma amesema wasanii nchini wanalenga soko la kimataifa, kwamba haiwezekani wapeleke video za nyimbo zao, katika soko la kimataifa, ikiwamo Marekani wakiwa wamerekodi huku wamevaa madela.

Amesema ni jambo lisiloingia akilini watu kutazama video za mwanamuziki Rihanna katika vituo mbalimbali vya televisheni, huku wahusika wakiwa wamevaa nusu utupu, huku zile za Tanzania zikifungiwa.

“Mtu kaimba wimbo mwaka mzima uliopita leo waziri unaibuka na kufungia. Huko vijijini watu wameshaipata hizo nyimbo, mnatupa taabu sana huko vijijini maana watendaji wanakamata kompyuta za watu zenye nyimbo zilizofungiwa,” amesema Msukuma.

“Msitumie muda mwingi kufungia nyimbo, tumieni muda mwingi kuwaelimisha hawa wasanii maana wanatumia muda mrefu sana kutengeneza nyimbo zao.”

Mbowe na viongozi wenzake waripoti Polisi

0
0
Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe ameripoti Kituo Kikuu cha Polisi saa nane mchana na kuondoka saa 8.20 mchana.

Vingozi wengine walioripoti ni  Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji, Mbunge wa Kawe,  Halima Mdee,  Mbunge wa Bunda Ester Bulaya ,  mbunge wa Tarime, Ester Matiko na Naibu Katibu Bara, John Mnyika.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ilitoa dhamana kwa viongozi hao Machi 27 na kuwapa sharti la kuripoti kituo kikuu kwenye ofisi ya RPC kila Ijumaa.

Viongozi ambao hawajafika mpaka sasa ni Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu na  Mbunge wa  Tarime, Vijijini, John Heche.

Viongozi hao kwa mara ya kwanza walipokea wito Februari 20, Jeshi la Polisi likiwataka kufika kituoni hapo baada ya maandamano ya Februari 16.

Ajali ya Polisi na wanajeshi yauwa Morogoro

0
0
Mwanajeshi mmoja wa JWTZ pamoja na mtoto wa Mwanajeshi mwenzake wanadaiwa kupoteza maisha katika ajali iliyohusisha gari la Polisi aina ya Basi lililogongana na gari dogo aina ya Noah iliyokuwa imebeba Wanajeshi wa JWTZ, maeneo ya Bwawani Morogoro

Inadaiwa basi hilo la Polisi lilikuwa likitokea Dodoma huku Noah hiyo iliyokuwa imebeba Wanajeshi takribani 6 pamoja na mtoto wa Wanajeshi mwezao ilikuwa ikitokea Morogoro.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo ingawa amekiri kutokuwa na taarifa za undani zaidi kwa sasa 


Zungu amtaka Mwakyembe kutaja sababu za kufungiwa wimbo wa ‘mwanaume mashine’

0
0
Mbunge wa jimbo la Ilala Mhe. Mussa Azzan Zungu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemtaka Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe aje na majibu bungeni kumweleza sababu za wimbo wa 'Mwanaume mashine' kufungiwa.

Zungu amesema hayo leo April 27, 2018 wakati akihairisha kikao cha bungeni na kumtaka waziri jioni ya leo kuja na sababu za kufungiwa wimbo huo kwa kuwa yeye anaona ni wimbo ambao hauna mapungufu kwa sababu humo ndani ya wimbo wamezungumziwa wa kina Kichuya na kina Tabwe ambao ni wachezaji wa Simba na Yanga.

"Mhe. Waziri jioni kwenye majibu hebu nielimishe kidogo kuhusu huu wimbo 'Mwanaume mashine' umeufungia kisa nini, maana wimbo huu unamtaja Kichuya, Msuva na Jumapili tunataka tuisikie hebu tuambieni sababu ya kuifungia ni nini" alisisitiza Zungu

CCM yakomba safu nzima ya uongozi Chadema

0
0
Mbunge wa Jimbo la Kondoa Mjini kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ediwn Sanda amesema kuwa safu ya uongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwenye jimbo hilo wamehamia CCM kutokana na kazi nzuri anazozifanya Rais Dkt. Magufuli

Ameyasema hayo leo April 27, 2018 alipopata nafasi ya kuwasalimu viongozi mbalimbali akiwemo Rais Dkt. Magufuli kwenye sherehe za ufunguzi wa barabara ya Kondoa, Babati yenye urefu wa kilomita 251

“Rais safu ya uongozi mzima ya CHADEMA imehamia CCM, Mwenyekiti wa Jimbo, Katibu wa Jimbo, na viongozi wengine kwa uchache wao, kwa kweli nashukuru sana ila tunakwenda kubomoa moja kwa moja dhana ya upinzani Kondoa kwani viongozi wao wote wamehamia CCM tayari kutokana na kazi ambazo unafanya,”amesema Sanda

Baadhi ya viongozi mbalimbali wa upinzani wamekuwa wakihama kutoka katika vyama vyao vya siasa na kujiunga na chama tawala Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kile wanachodai kuunga mkono jitihada za Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya April 28

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro Afariki Dunia

0
0
Mkuu wa mkoa mstaafu Mzee Abbas Kandoro amefariki dunia usiku wa kuamkia leo  katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jijini Dar alikolazwa kwa matibabu.

Kabla ya kifo chake aliwahi kuwa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Arusha, Singida na Mbeya na mikoa mingine.

Siku mbili zilizopita Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alimtembelea na kumpa pole Mkuu huyo wa Mkoa Mstaafu, Abbas Kandoro ambapo awali alikuwa amelazwa katika hospitali ya Benjamin Mkapa mjini Dodoma kabla ya kuhamishiwa Muhimbili Dar  ambapo umauti ndipo ulipomkuta.

Serikali: Haiwezekani Majuto Kuomba Sh 500,000

0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe amesema inaudhi kuona msanii wa filamu, Amri Athuman maarufu King Majuto anaomba msaada wa Sh 500,000 kwa ajili ya matibabu wakati kuna makampuni yalifaidika naye kwa kuingia mikataba aliyodai ya dhuluma.

Kutokana na hali hiyo, amesema serikali imechoka kusikia vilio vya wasanii wa filamu kudhulumiwa haki zao na sasa imeunda kamati maalumu ya wanasheria kukagua mikataba yote ya mashirika na makampuni waliyoingia wasanii akiwamo  King Majuto na marehemu Seteven Kanumba ‘Kanumba’.

Pia imeagiza wasanii wote ambao wanaona wameingia mikataba ya kipumbavu na makampuni au mashirika hayo wawasilishe taarifa zao kwa serikali.

Dk. Mwakyembe amesema hayo jana  Aprili 27, bungeni jijini Dodoma wakati akijibu hoja za wabunge katika kuhitimisha hotuba ya bajeti ya wizara hiyo.

“Kwa kweli dhuluma kwa wasanii ilikuwapo kubwa sana kwa kutumia ‘middle men’ (watu wa kati), watu wenye fedha wamechezea sana Watanzania wetu. Hili limeanza kubadilika tumeanza kuwa- empower (kuwezesha) wasanii wetu kwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama) wasitumie middle men.

“Kwa mfano vijana wetu wazuri kama kina Kanumba, amefariki kila mtu anajua ni milionea, hapana.. waliotajirika ni wengine. Leo hii mwanasanaa mzuri mzee majuto anaumwa, anaomba fedha, mimi nachanga kutoka mfuko kwangu,” alisema Dk. Mwakyembe.

Alisema licha ya kwamba nusu ya mabango ya biashara na matangazo ya biashara ni ya  Mzee Majuto inashangaza kuona anaomba fedha ya matibabu.

Kim Jong-un Akubali Kuondoa Silaha za Nyukilia

0
0
Mkutano wa kihistoria baina ya Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un na Rais wa Korea Kusini Moon Jae-in umeanza Ijumaa kaitka kijiji cha truce village huko Panmunjom.

Kim Jong-un alivuka eneo la mpakani lisilokuwa na harakati za kijeshi ambalo limeyagawanya mataifa hayo mawili kwa zaidi ya miaka 60.

Hatimaye viongozi hao kutoka upande wa utawala wa kikomunisti (kaskazini) na upande wa utawala wa kidemokrasia (kusini) walikaribiana kabla ya kutangaza azma yao ya kuondoa silaha za nyuklia na kuendeleza amani.

“Leo, Mwenyikiti Kim Jong Un na mimi tumethibitisha ile azma yetu ya kufikia hali ya kutokuwepo silaha za nyuklia katika eneo la rasi ya Korea katika hatua ya kuondosha kabisa silaha za nyuklia ikiwa ni lengo letu la pamoja,” amesema Rais Moon Jae katika sherehe za kutangaza makubaliano ambayo wameyaita tamko la Panmunjom.

Kiongozi wa Korea Kaskazini kwa upande wake amesema kuwa amekubaliana na Tangazo hilo la pamoja na mikataba iliyotangulia baina ya nchi hizo mbili bila ya kufafanua au kuthibitisha matokeo ya makubaliano hayo ya kuondosha vitisho vya programu ya silaha za nyuklia za nchi hiyo

“Tumeamua kufungua awamu hii ya kuboresha mahusiano na maendeleo kwa kutekeleza kikamilifu Tangazo la Kaskazini- Kusini na mikataba yote iliyotangulia ambayo ilikubalika.,” amesema Kim.

Chanjo Ya Saratani Ya Shingo Ya Kizazi Haizuii Ukimwi wala Magonjwa Mengine ya Zinaa

0
0
Serikali imesemachanjo ya saratani ya shingo ya uzazi haizuii magonjwa ya kuambukiza yanayotokana na ngono zembe kama vile Ukimwi, kaswende na kisonono.

Kauli hiyo imetolewa jana bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndungulile wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Faharia Khamis Shomari.

Mbunge huyo alitaka kujua iwapo chanjo hiyo ya saratani inazuia magonjwa yatokanayo na ngono zembe kwa sababu vijana wanaanza kujihusisha na vitendo katika umri mdogo.

Akijibu swali hilo Dk. Ndungulile amesema serikali imezindua chanjo dhidi ya saratani ya shingo ya uzazi  kwa kuanza na na mabinti wenye umri wa miaka 14.

“Baada ya hapo watafuata wa miaka tisa hadi 13. Aidha tafiti zimeonesha kuwa vijana wadogo wanajihusisha na ngono zembe hivyo niwaonye mabinti kuwa chanjo ya saratani ya shingo ya uzazi  haitawakinga dhidi ya magonjwa mengine ya kuambukiza kama ukimwi,  kaswende na kisonono,” alisema.

Aidha, ametoa rai kwa wabunge na wananchi wote kuwa chanjo hiyo ni salama na lengo la serikali ni kuhakikisha Taifa linaondokana  na tatizo la saratani ya shingo ya kizazi.

Gigy Money ajifungua Mtoto wa Kike

0
0
Msanii wa muziki wa bongo fleva nchini  Gift Stanford maarufu kama Gigy Money, amefanikiwa kujifungua salama mtoto wa kike na kumpatia jina la Myra.

Gigy Money anatoka kimapenzi na mtangazaji wa Choice FM, Mo J ambaye pia ni baba mzazi wa mtoto huyo aliyezaliwa jana.

Gigy na Mo J kabla ya kuzaliwa kwa mtoto huyo walikuwa wakijiita Baba Candy na Mama Candy ila mara baada ya kuzaliwa kwa mtoto huyo wamesema hawatatumia tena jina hilo na tayari wamempa mtoto wao jina la Myra.

Waziri Mkuu Awaonya Viongozi wa Vyama vya Siasa

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwaamewataka viongozi wa vyama vya siasa wajitahidi kuwa makini na namna wanavyoendesha vyama vyao kwa sababu wananchi wanaowaongoza ni wa vyama vyote.

Pia amewaasa viongozi wa Baraza la Vyama vya Siasa waendelee kushikamana ili waweze kulifikisha Taifa mahali ambapo Watanzania wanapatarajia ikiwa ni pamoja na kupunguza umaskini.

Ameyasema hayo leo (Ijumaa, Aprili 27, 2018) wakati akizungumza na Kamati ya Uongozi ya Baraza la Vyama vya Siasa katika ukumbi wa mikutano wa Waziri Mkuu ulioko Mlimwa jijini Dodoma.

“Viongozi wa vyama vya siasa wanatakiwa wajitahidi kuwa makini na namna ambavyo wanaendesha siasa katika vyama vyao, wananchi wanaowaongoza ni wa vyama vyote hivyo tupeleke ujumbe ambao utawaongoza kujileta maendeleo.”

Waziri Mkuu amesema kuwa mazungumzo yaliyofanyika leo baina ya Serikali na viongozi hao yameonesha nia ya pamoja ya kuendeleza ushirikiano. Pia amesema wana wajibu wa kuendeleza historia nzuri kwani siasa ni moja ya nyenzo zinazochochea  maendeleo.

Akijibu ombi la viongozi hao kuhusu changamoto ya upatikanaji wa fedha za kuendesha shughuli za baraza hilo ikiwemo mikutano, Waziri Mkuu ameahidi kuwa Serikali  itafanyia kazi maombi hayo ili waweze kutimiza majukumu yao kama ilivyokusudiwa.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Makonda Mgeni Rasmi Simba Vs Yanga Jumapili April 29

0
0
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Paul Makonda atakua mgeni rasmi wa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara utakaowakutanisha Simba na Yanga utakaochezwa Jumapili Aprili 29,2018 Uwanja wa Taifa Dar Es Salaam.

Ndugu Makonda atawaongoza maelfu ya mashabiki wa mpira wa miguu watakaojitokeza kweye Uwanja wa Taifa kushuhudia mchezo huo namba 178 utakaoanza saa 10 jioni.

Tayari tiketi za mchezo huo zinaendelea kuuzwa ambapo VIP A ni shilingi 30,000,VIP B na C 20,000 na Mzunguko(Jukwaa la rangi ya Chungwa,Kijani na Bluu) 7,000.

Tiketi zinapatikana kupitia Selcom.

Katika mchezo huo Simba wanaingia uwanjani wakiwa wanaongoza ligi baada ya kujikusanyia pointi 59 ikicheza michezo 25 wakati Yanga wana pointi 48 wakiwa nafasi ya pili baada ya kucheza michezo 23.

Familia 208 za watoto waliotelekezwa na baba zao, zaanza kupata huduma

0
0
Zaidi ya familia 208 za watoto waliotelekezwa na baba zao, zimepatanishwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Paul Makonda.

Hayo yamebainishwa jana Aprili 27 na Makonda wakati akitoa majumuisho ya zoezi la kuwasikiliza wanawake waliotelekezwa na wenza wao wakiwa na watoto.

Kadhalika Makonda, hakuacha kuwashukuru waandishi wa habari kwa kufanya kazi kubwa katika kuhabarisha umma kuhusu kampeni yake.

“Kwanza niwashukuru waandishi wa habari kwa kazi nzuri mliyofanya, lakini pia niwashukuru wote walionitukana kwa kuanzisha zoezi hili wakiwamo wabunge,"alisema.

Alisema zoezi hilo limefanikiwa kwani  familia 208 zimeanza kupata huduma kutoka kwa baba zao.

Kadhalika amesema, kati ya watu 17,000 waliofika ofisini kwake, 90 wamefanikiwa kupimwa uhalali wa baba kwa mtoto ( DNA) na watoto 2971 wakifanikiwa kupata  bima ya afya.

"Tumeunda tume ya watu 15 watakaofuatilia kwa kina matatizo ya kiutawala katika kushughulikia masuala  yanayohusu jamii kwani imeonekana kuna shida kubwa kwa watu wanaoshughulika na ustawi wa jamii," alisema.

Kanuni mpya kudhibiti matusi na Picha za Uchi mitandaoni

0
0
Serikali imesema kanuni mpya za maudhui kwenye mitandao, runinga na redio zimetungwa kwa lengo la kudhibiti usambazaji wa kauli chafu, matusi, picha za utupu na zenye maudhui yasiyofaa kwa watoto.

Kanuni hizo zimetungwa ikiwa ni utekelezaji wa Sheria ya Mawasiliano ya Kiektroniki na Posta ya Mwaka 2010.

Pia imesema itaendelea kuhamasisha utengenezaji na uzalishaji wa maudhui ya ndani yanayozingatia maadili, mila na desturi za Mtanzania huku ikikiri kuwapo kwa mmomonyoko wa maadili kunakoongezeka siku hadi siku, hivyo imejipanga kukabiliana na changamoto hiyo.

Akiwasilisha bungeni mjini hapa jana hotuba ya makadirio ya bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Waziri wa wizara hiyo, Dk. Harrison Mwakyembe, alisema kanuni hizo zinamtaka kila mtumiaji wa mitandao awe na namba ya siri ili 'wajanja' wasitumie kirahisi chombo chake cha mawasiliano kutenda matendo yanayokwenda kinyume cha sheria.

Alisema kanuni hizo pia zinaweka muda maalumu kwa picha mgando na nyongevu za filamu au muziki wenye maneno yasiyofaa kwa watoto kuonyeshwa kwenye runinga.

"Tuliweka muda huo maalumu kuanzia saa 4:00 usiku hadi saa 11:30 asubuhi, lakini wadau wamekuwa wakali, wanadai picha na nyimbo hizo zirushwe kuanzia saa 6:00 usiku wakati watoto wamelala na mwisho saa 11:00 asubuhi, kabla watoto hawajaamka," alisema Dk. Mwakyembe.

Aliongeza kuwa kanuni hizo zinataka madaraja yawekwe kwa kila filamu, video, wimbo au albamu kutoka ndani au nje ya nchi ndipo kazi hizo zitumike kwenye vyombo vya utangazaji.

"Msingi wa kanuni hizi ni kuhakikisha teknolojia inatutumikia badala ya kututumikisha na kuvuruga mustakabali wa maadili ya taifa letu. Ni kanuni zilizozingatia mazingira yetu halisi kama kila Watanzania," alisema.

Dk. Mwakyembe alisema, mmomonyoko wa maadili ya Kitanzania unaoongezeka siku hadi siku, ni miongoni mwa changamoto zinazoikabili wizara yake.

Alisema wanaendelea kutoa elimu kupitia vyombo vya habari na kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kuzingatia maadili, mila na desturi za Kitanzania.

Ili kutekeleza majukumu yake kwa mwaka ujao wa fedha, Dk. Mwakyembe aliliomba Bunge kuidhinisha bajeti ya Sh. bilioni 33.3. Kati yake, Sh. bilioni 12.2 ni mishahara, Sh. bilioni 9.3 kwa ajili ya matumizi mengine na Sh. bilioni 8.7 za utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Rais Magufuli: Hakuna Chakula cha Bure Kitakachogawiwa Mwaka Huu

0
0
Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, amewapa ujumbe mzito watanzania kupitia wakazi wa kondoa mkoani Dodoma akiwataka wazitumie vizuri mvua zinazonyesha na kuhakikisha wanajihusisha na kilimo kisawa sawa ili kuepukana na njaa.

Magufuli aliwataka wananchi kuzitumia vizuri mvua zinazoendelea kunyesha badala ya kuziona kero kwao huku akisema,hakuna mtu yeyote atakayepewa msaada wa chakula msimu huu.

Alisema yapo baadhi ya maeneo wananchi hawalimi lakini baadaye wataanza kulia njaa na kuomba chakula.

“Hivi mvua inanyesha namna   hii baadaye uje useme una  njaa ,na hii nawaeleza watanzania wote kuanzia Kongwa mpaka Chato,hakuna atakayepewa msaada wa chakula.”alisema Magufuli.

Akieleza zaidi alisema,wananchi wanaoishi kando kando mwa barabara  wanapaswa kuitumiwa katika kukuza Uchumi ili wanufaike na kuwataka wananchi kulima kwa bidii huku akisema,bila kufanya hivyo barabara hiyo haitawasaidia

Amewasifia wanawake wanaoishi kandokando mwa barabara katika mikoa ambayo tayari wanaitumia nafasi hiyo kama fursa na kuwataka wote wanaojidekeza kusubiri serikali kuwahudumia hasa vipindi vya njaa kwamba hawatafanikiwa.

Wanafunzi watoroka wakidai kukwepa viboko

0
0
Wanafunzi wanne kati ya watano wa Shule ya Msingi Ndolage, Kata ya Kamachumu, Kagera wamekamatwa wakidaiwa kutoroka shule na kwenda kutafuta kazi za ndani mjini Bukoba.

Wanafunzi hao wenye miaka 11 hadi 14 walitoroka Aprili 25 wakiwa na sare za shule.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Ndolage, Frederick Byarugaba alisema wanafunzi hao (majina tunayahifadhi) walitoka nyumbani kwao Kitongoji cha Buganda B, Kamachumu na walipata usafiri wa kuelekea Bukoba Mjini.

“Baada ya taarifa hizo kusambaa kuwa wanafunzi wametoroka, uongozi wa shule ulitoa taarifa kwa Jeshi la Polisi, Kituo cha Kamachumu, Muleba,” alisema Byarugaba.

Alisema watoto hao walionekana kwa mara ya kwanza, Manispaa ya Bukoba wakitembea pamoja na baadhi ya watu wakiwamo abiria waliwakamata na kutoa taarifa polisi na kwa uongozi wa shule.

“Walikuwa na utoro wa rejareja na mara kadhaa wamekuwa wakikanywa kuhusu tabia mbaya ya utoro, hivyo baada ya wazazi kutoa taarifa ya kutoonekana nyumbani tulianza kusambaza ujumbe wa kuwatafuta,” alisema Byarugaba.

Mmoja wa walezi wa watoto hao, Christopher Kalumuna alisema kuwa baada ya mwalimu wa zamu kudai hawakuonekana shuleni hapo alisambaza taarifa kwenye miji midogo ya Kemondo, Kyetema na Bukoba Mjini hadi kwenye vituo vya magari ili kubaini kama wanaweza kusafiri.

“Huyu ni mtoto wa marehemu kaka yangu (jina tunalihifadhi) na mama yake naye ni marehemu, alikuwa akinifanyia kazi za nyumbani baada ya kutoka shule,” alisema Kalumuna.

Akizungumza kuhusu kilichowafanya kutoroka, mtoto huyo alisema walirubuniwa na mwenzao, ambaye aliiwambia kuwa shuleni kumeandaliwa adhabu ya watoto watoro hivyo watoroke kuepuka viboko au nyaya za umeme.

“Tuliogopa adhabu na ni kweli tumekuwa watoro kila mara na tunachelewa shule. Tulipoondoka tulilala kichakani bila kula huko Kemondo na tulitembea kwa miguu.

“Baada ya kufika Bukoba mjini kiongozi wetu (mwanafunzi mwenzao) alitutoroka na tuliokotwa baada ya kuanza kulia, ndipo tukamweleza aliyetuokota akatupandisha kwenye gari hadi Kamachumu,” alisema mtoto huyo.

Kamanda wa Polisi mkoani Kagera, Agustino Olomi alithibitisha kupokea taarifa za watoto hao.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images