Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Masogange azikwa Mbeya....Tazama Picha

$
0
0
Safari ya mwisho duniani ya aliyekuwa msaani maarufu aliyekuwa akipamba video za wanamuziki wa Bongo fleva, Agnes Gerald 'Masogange' imehitimishwa leo zaa tisa alasiri bada ya kuhifadhiwa kwenye nyumba ya milele nyumbani kwa wazazi wake Utengule – Mbalizi mkoani Mbeya.

Mamia ya waombolezaji kutoka Dar es salaam na maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya walijitokeza wakiongozwa na Mkuu wa mkoa huo, Amos Makalla.

Akitoa salamu za rambirambi kutoka serikalini, Makalla amesema hakuna mtu anayejiandaa wala aliye tayari kwa ajili ya kifo, hivyo kifo cha Masongange ni kilelezo kwamba binadamu wote hapa duniani ni wasafiri.

‘Kifo cha Masogange kitukumbushe kwamba sote tutakufa, nimefurahi namna wasanii mlivyojipanga bila kujali bifu na tofauti zenu, katika hili mmekuwa pamoja,” amesema Makalla.

“Nilikuwa nafuatilia tangu msiba huu ulipotokea, mlikuwa pamoja na kwa mshikamano na sisi Serikali tunawapa pongezi sana.”

Makalla amewapongeza wananchi kwa namna walivyojitokeza kwa wingi na hiyo inaonyesha ndio utamaduni wa Mtanzania kushirikiana katika matatizo.

Akimshukuru Makalla kwa niaba ya wasanii wenzake, mwenyekiti wa wasanii hao, Steve Nyerere amesema, “hili ni pigo kwetu wasanii. Na sisi kama wasanii tumekubaliana kiasi tulichojichanga, kiasi fulani kitatumika kumlipia ada ya mwaka mmoja mtoto wa marehemu ambaye yupo darasa la saba lakini pia kumlipia bima ya afya endelevu.”



Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya April 24

Rais Magufuli Alivyozindua tawi la NMB Kambarage lililopo Dodoma

$
0
0
Rais Dkt. John Pombe Magufuli amezindua ofisi na matawi mawili ya benki ya NMB Tanzania ambayo imepewa jina la Baba wa Taifa, NMB Kambarage lililopo jengo jipya la PSPF Dodoma Plaza lililopo mkoani Dodoma.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo, Rais Magufuli ameipongeza NMB kwa huduma bora ambazo inazitoa na kuitaka kuendelea na kasi hiyo ili kuhakikisha kila Mtanzania anatumia benki kuhifadhi fedha kwani ni sehemu salama.

“Nikiwa kama mteja na kiongozi wa serikali huwa najisikia vizuri sana kuona benki hii inazidi kufanikiwa napenda niwahakikishe serikali itaendelea kushirikiana na NMB. 

"Mkurugenzi wenu ametueleza mambo mengi ambayo mnayafanya mkiwa mmefika kila sehemu hapa nchini napenda kuwahakikishia kwamba tupo pamoja,” alisema Magufuli na kuongeza.

“Lakini Mkurugenzi kwakuwa umekubali kuchagua jina la Kambarage Nyerere yawezekana ni mbinu nzuri ya kuwavuta wateja wakaja kwa kutambua jina la Kambarage Nyerere kuwe na uwiano wa huduma zinazotolewa na vitendo vya Kambarage Nyerere, sitarajii kusikia mtu amekuja alafu akaanza kuombwa hata rushwa, wote tunajua kuwa Baba wa Taifa alikuwa mpinga rushwa.”

Awali akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Benki ya NMB, Ineke Bussemaker alisema benki hiyo kwa sasa imefika maeneo yote nchini na hivyo kurahisha upatikanaji wa huduma za kifedha na kwamba wamejipanga kuendelea kuboresha huduma kwa kushirikiana na serikali.

“Tunafungua ofisi na matawi mapya mawili katika jengo la PSPF, NMB Kambarage inalenga kuhudumia wateja wengi ikiwepo wa kawaida na wa serikali na katika kufanikisha hili tunamshukuru Mama Maria Nyerere kwa kuturuhusu kutumia jina la mme wake ambaye ni Baba wa Taifa na Rais wa kwanza Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,

“NMB imedhamiria kuhakikisha Watanzania wote wanapata huduma za kifedha, kwa kutumia matawi, ATM na Wakala kupitia njia ya kidigitali ya intaneti, apps na simu za mkononi. Kwa sasa NMB ina matawi 218 na zaidi ya ATM 800 nchi nzima,” alisema Bussemaker.

Aidha Bussemaker alisema pamoja na hilo pia wamekuwa wakitenga asilimia moja ya faida wanayopata kwa kila mwaka kwa ajili ya kusaidia jamii katika sekta ya afya, elimu na elimu ya fedha ambapo wamekuwa wakitoa misaada katika maeneo mbalimbali nchini kulingana na uhitaji uliopo.

“Tumekuwa tukitenga asilimia moja ya faida yetu baada ya kulipa kodi kwa ajili ya Kitengo cha Masuala ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR). Kwa mwaka 2017 pekee tulitumia Tsh. 1.4 bilioni ambazo tulisaida shule kwa kutoa madawati 6,000, kompyuta 300 na vifaa vya maabara,” alisema Bussemaker.

Katika hafla hiyo benki ya NMB imekabidhi msaada wa Sh. 50 milioni kwa uongozi wa mkoa wa Dodoma ambazo watazitumia katika shughuli za maendeleo. Hata hivyo Rais Magufuli ameshauri kuwa mradi ambao pesa hizo zitatumika upewe jina la NMB.

Waziri Mhagama Amtaka Msajili Wa Vyama Kuchukua Hatua Kwa Vyama Vinavyokiuka Sheria Na Miongozo Iliyopo.

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amemuagiza Msajili wa vyama vya Siasa kuchukua hatua kwa vyama vinavyokiuka sheria na miongozo ya vyama vya siasa.

Ametoa kauli hiyo jana (Aprili 23, 2018) alipokuwa akitoa maelezo ya ufafanuzi juu ya hoja za ofisi yake, zilizoainishwa katika Ripoti ya Mthibiti na Ukaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa fedha unoishia Juni 30, 2018 alipokutana na  waandishi wa habari Bungeni Dodoma.

Waziri Mhagama ameelekeza kuhakikisha vyama vyenye mapungufu upande wa hesabu zao basi wawasilishe kwa Msajili wa vyama ndani ya wiki 3 hadi 4.

“Namtaka Msajili wa Vyama achukue hatua za Kisheria pasi kusita kwa chama chochote kinachokiuka sheria ya vyama vya siasa Na. 2 ya mwaka 1992”.alisema Waziri Mhagama

Aidha amemtaka Msajili wa Vyama vya siasa nchini kuhakikisha anaweka miongozo na mpango kazi ili vyama vilivyozoea kutowasilisha hesabu zao viache mara moja kwa mujibu wa sheria.

Waziri Mhagama aliongezea kuwa taarifa ya Mthibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ilibaini mapungufu kadhaa katika uendeshaji wa vyama vya siasa ikiwemo; Upungufu katika hesabu zilizowasilishwa chini ya viwango vya Kimataifa vya uandaaji wa hesabu katika sekta za umma na baadhi ya vyama kushindwa kuwasilisha hesabu zao kwa CAG kwa ukaguzi

Pamoja na hayo alibainisha kuwepo kwa vyama vya kisiasa visivyotumia rejista ya mali za kudumu ambapo vyama vinne ikiwemo;CHADEMA, NLD,ADC na Demokrasia Makini havina Daftari la kudumu la mali zao ikiwa ni kinyume na sheria zilizopo.

“Msajili wa Vyama nakuagiza kutoa maelekezo kwa kila chama cha siasa chenye usajili wa kudumu kuwa na regista ya mali zake ndani ya wiki tatu kuanzia leo kwani kukosa daftari la mali za kudumu ni kinyume na kifungu Na.14(1)(b)(ii) ya sheria ya vyama vya siasa Na.5 ya mwaka 1992.”alisisitiza Waziri.

Sambamba na hilo Waziri alimtaka Msajili wa Vyama vya siasa kuhakikisha vyama vyote  vinafuata miongozo yote ya kihasibu ili kuondokana na mapungufu ya kukosekana kwa nyaraka za malipo kama ilivyobainishwa na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ambapo alibaini vyama vitatu kati ya tisa vina nyaraka pungufu ikiwemo CHADEMA, SAU na ADC.

“Msajili wa vyama ahakikishe vyama vya siasa vinatekeleza miongozo yote kihasibu pamoja na kanuni za fedha, ambazo zinaelekeza nyaraka ziwe na viambatisho sahihi kwani ripoti ilibainisha vyama vitatu vilikuwa na malipo yenye nyaraka pungufu zenye thamani ya shilingi 735,978,559 ambapo ni kinyume na miongozo ya kihasibu na kukosa uhalali wa malipo hayo.”alisisitiza Waziri Mhagama.

Awali kifungu cha 14(1)(a) na (b)(i) cha Sheria ya Vyama vya Siasa Sura ya 258 [RE: 2015] kinaelekeza kuwa, kila chama cha siasa kinapaswa kutunza taarifa za mapato na matumizi, ikiwamo taarifa za mali zake. Vile vile, kinapaswa kuwasilisha kwa Msajili wa Vyama vya Siasa, taarifa ya hesabu zake zilizokaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), pamoja taarifa ya mali zake.

Hivyo, Kifungu hicho kinampa mamlaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kufanya ukaguzi wa hesabu za kila chama cha siasa chenye usajili wa kudumu. Katika mwaka wa fedha unaoishia tarehe 30 Juni, 2017, CAG amefanya ukaguzi wa hesabu za Vyama vya Siasa kumi ikiwemo; CCM, CHADEMA, NLD, TLP, Demokrasia Makini (MAKINI), TLP, DP, SAU, AFP, CCK na ADC kati ya vyama vya siasa kumi na tisa vyenye usajili wa kudumu. Vyama vya Siasa tisa (9) havikuwasilisha hesabu zake kwake kwa wakati kwa ajili ya ukaguzi, hivyo hakukaguliwa.

Tanzania Na Israel Kuagalia Namna Ya Kushirikiana Katika Masuala Ya Utoaji Haki

$
0
0
Tanzania na Israel zimekubaliana kwamba ,  mataifa hayo mawili yana mengi ya kujifunza baina  yao hususani katika  eneo la utoaji wa haki na usimamiaji wa sheria.

Hayo yamejiri jana ( jumatatu) wakati Mwanasheria  Mkuu wa Serikali, Dk. Adelardus Kilangi,  alipokutana na kufanya mazungumzo  na  Waziri wa Sheria wa Israel Bi. Ayalet Shaked.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika katika Jengo la   Mikutano la Kimataifa la Mwalimu Julius    Nyerere ( JNICC), viongozi hao walikubaliana kwamba kuna haja na umuhimu wa   Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa Tanzania na Mwanasheria Mkuu wa Israel kukutana  kwa lengo la  kuainisha maeneo ambayo  Ofisi hizo mbili  zinaweza kushirikiana.

“  Nadhani  tuna mengi ya  kujifunza kutoka kwenu na halikadhalika nanyi kuna maeneo ambayo   mnaweza kujifunza  kutoka kwetu. Hivyo basi, ninaamini  kwamba pale itakapowezekana,  kuna umuhimu wa mimi kukutana na  mwenzangu ili tuweze kuangalia maeneo ya kipaumbele ambayo tunaweza kubadilishana uzoefu na kupanua wigo wa ushirikiano  baina ya  nchi zetu”, akasema Dk. Kilangi.

Akayataja maeneo ambayo  anaamini Tanzania na Israel  zinaweza kushirikiana  ni  pamoja na  namna  bora  ya  kuimarisha  mifumo ya utoaji  haki na  ushauri wa kisheria wenye tija, pamoja na eneo la uwezeshwji ( capacity  building).

 Mwanasheria Mkuu , Dk. Kilangi  ambaye alifuatana na  Naibu Mwanasheria Mkuu wa  Serikali  Bw, Edson Athnas  Makallo, aliyatumia mazungumzo  kati yake na   Waziri Shaked kuelezea baadhi ya  majukumu yake anayoyatekeleza  kama  Mshauri Mkuu wa Serikali katika   masuala yote yanayohusu sheria pamoja    muundo mpya wa Ofisi  ya Mwanasheria   Mkuu ambao umehusisha kuanzishwa  kwa Wakili Mkuu wa Serikali.

Kwa upande wake,   Waziri wa Sheria wa Israel, ambaye  Tanzania inakuwa nchi yake ya kwanza kutembelea Barani Afrika, pamoja na kukubaliana na wazo la Dk. Kilangi la kuangalia uwezekano wa  Wanasheria Wakuu kukutana  katika muda utakaopangwa. Amesema kwamba, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali   ni Ofisi nyeti na yenye hadhi ya  juu kabisa   katika nchi yoyote ile ikiwamo Israel.

Akaongeza kwamba, majukumu anayoyatekeleza Mwanasheria Mkuu wa  Serikali, Dk. Adelardus Kilangi  yanashabihiana  na  anayotekeleza  Mwanasheria Mkuu wa   Israel  yakiwamo ya kuisimamia  serikali katika  masuala yote yanayohusu sheria, kuiwakilisha serikali katika mahakama za juu na mahakama za chini pamoja na kuendesha mashauri  ya jinai  hivyo wawili  hao wakipata fursa ya kukutana bila shaka watakuwa na mengi ya  kujadiliana na  kushirikiana.

Waziri wa Sheria wa Israel Ayalet Shaked anaongoza ujumbe wa  wafanyabiashara kutoka Israel ambao upo hapa nchini  kukutana na  wafanyabiashara wa  Tanzania.

Israel Yampongeza Rais Magufuli

$
0
0
Jonas Kamaleki- MAELEZO
Serikali ya Israel imempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kurejesha uhusiano unaolenga kuziimarisha nchi hizi mbili kiuchumi.

Kauli hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Sheria wa Israel, Mhe. Ayelet Shaked wakati wa Kongamano la Tano la Biashara na Uwekezaji kati ya Israel na Tanzania.

“Tunamshukuru sana Rais Magufuli kwa kufungua ubalozi wa Tanzania nchini kwetu na tunataraji kuuzindua rasmi juma lijalo”, alisema Waziri Shaked.

Ameongeza kuwa kwa zaidi ya miongo minne Tanzania na Israel hazikuwa na mahusiano ya kiuchumi wala ya kisiasa na kuongeza kuwa sasa nchi yao iko tayari kuwekeza nchini.

Waziri huyo ameeleza kuwa ni mara yake ya kwanza kufika Afrika na yuko tayari kuja na familia yake kwa ajili ya kufanya utalii Zanzibar na kwenye mbuga za wanyama za Serengeti na Ngorongoro.

Kwa upande wake, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amewakaribisha waisraeli kuwekeza nchini kwani Tanzania ni kitovu cha uwekezaji kwa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika kutokana na amani iliyopo. Pia ameitaja nchi hii kuwa ni lango la biashara kwa nchi za kiafrika zinazoizunguka.

“Israel mnakaribishwa kuwekeza hapa Tanzania kwani mazingira ya uwekezaji ni mazuri, tunayo ardhi nzuri kwa kilimo, tunayo maziwa, mito kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji, hivyo hakuna mtakachokikosa endapo mnataka kuwekeza kwenye kilimo”, alisema Waziri Mwijage.

Waziri Mwijage amesema Tanzania iko tayari kwa uwekezaji katika kilimo, viwanda vya dawa, TEHAMA, utalii, uzalishaji wa sukari na uongezaji thamani kwenye madini, na hivyo kuwahakikishia kuwa Serikali inaunga mkono suala la uwekezaji.

Naye balozi wa Israeli kwa nchi za Tanzania , Kenya, Uganda, Malawi na Shelisheli, Mhe. Noah Gal Gendler amesema Serikali ya Rais Magufuli imeonyesha mabadiliko makubwa ya ushirikiano wa kisiasa na kiuchumi kwa muda mfupi.

“Kwa kipindi cha zaidi ya miaka 46 hakuna waziri hata mmoja kutoka Israeli amewahi kuitembelea Tanzania, lakini ndani ya wiki mbili wamefika mawaziri wawili toka nchini mwetu”, alisema Gendler.

Ameongeza kuwa katika kuimarisha sekta ya Afya, Israeli itajenga wodi za wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalum (ICU) katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dodoma, na kituo huduma kwa watoto katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.

Kongamno hili ni la tano kufanyika hapa nchini likiwa na lengo la kuonyesha fursa za uwekezaji zitakazotekelezwa baina ya wafanyabiashara wa Israeli na Tanzania. Kongamano hili ni fursa kwa sekta binafsi kuitumia vizuri ili kuongeza tija katika biashara hususan katika kilimo na uwekezaji katika ujenzi wa viwanda.

Rais Magufuli: Vikwazo ni Vingi Lakini Nitaendelea kuchapa kazi kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amesema kuwa anajua wapo watakaotumika kuleta vikwazo kwenye hatua anazopiga za kuiletea maendeleo nchi.

Ameyasema hayo jana  katika uzinduzi wa jengo la PSPF mkoani Dodoma, ambapo Rais Dkt. Magufuli alisema kwamba wapo ambao hawapendi kuona Tanzania inapiga hatua kwenye uchumi, hivyo watu watatumika na mabeberu kuleta vipingamizi na vikwazo, lakini yeye ataendelea kuchapa kazi kwa ajili ya watanzania masikini.

“Katika juhudi hizi za kuleta maendeleo wapo wengine watasaliti njiani, wapo wengine watatumika na mbinu za mabeberu, na hasa katika masuala haya ya kujenga nchi yetu, na hasa kwa sababu nchi yetu inakwenda mbele, ni lazima itawakwaza wengine, katika jukumu lolote la kazi hata kwenye familia, lazima watapatikana wa kupinga pinga kidogo, lakini kikubwa ni kunyoosha mstari kwa ajili ya kuwatumikia Watanzania masikini”, alisema Rais Dkt. Magufuli.

Sambamba na hilo, Rais Magufuli amemuhakikishia mtoto wa Baba wa Taifa Mwl. JK Nyerere, Makongoro Nyerere, kuwa nchi ipo salama na imara, na anaamini itafika ikiwa imara zaidi licha ya vikwazo vingi anavyokutana navyo.

Jacob Zuma atangaza ndoa na binti wa miaka 24

$
0
0
Aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, ameushangaza umma baada ya kuwepo na taarifa za kutarajia kuoa mke wa tano, binti mdogo mwenye umri wa miaka 24.

Taarifa hizo zimethibitishwa na binti huyo ambaye ni mke mtarajiwa wa Zuma anayejulikana kwa jina la Nonkanyinso Conco, kupitia chombo cha habari cha Times live cha nchini Afrika Kusini.

“Ndio tunaoana, hayo ndiyo naweza kusema kwa sasa, nahitaji kutoa taarifa kabla sijafanya interview (mahojiano) yoyote”, amesikika binti huyo akiuambia mtandao wa Times Live.

Habari zaidi zinasema kuwa binti huyo tayari ana mtoto mchanga aliyezaa na Jacob Zuma ambaye amezaliwa siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa ya Jacob Zuma, April 12, na tayari mahali imeshatolewa.

Jacob Zuma ambaye ana miaka 76 mpaka sasa ameshaoa mara sita, na hii itakuwa ni mara ya saba kufunga ndoa,

Tukio hilo limeonekana kuwakwaza wananchi wa Afrika Kusini na kutoa maoni yao kwenye mitandao ya kijamii, wakisema binti huyo ni mdogo sana kwa Zuma, kwani wana tofauti ya miaka 52.

Treni ya Kisasa Kuanza Novemba Mwakani

$
0
0
Serikali imesema treni inayotumia umeme inatarajiwa kuanza kutoa huduma Novemba mwakani kwa usafiri wa reli ya kati, kipande cha Dar es Salaam - Morogoro.

Vilevile, imesema mpaka sasa ujenzi wa reli hiyo kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge) umepiga hatua saba.

Utekelezaji wa mradi huo unahusisha ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza ambao sasa unaendelea kwa Dar es Salaam-Morogoro (km 205) na Morogoro-Makutupora (km 422).

Akiwasilisha bungeni mjini hapa jana hotuba yake kuhusu makadirio ya bajeti ya wizara yake kwa mwaka ujao wa fedha, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, alisema hadi sasa ujenzi wa kipande cha Dar es Salaam-Morogoro umefikia asilimia 10 na unatarajiwa kukamilika Novemba mwakani.

Akizungumzia hatua saba muhimu zilizofikiwa katika ujenzi wa reli hiyo, Prof. Mbarawa alisema hatua ya kwanza ya ujenzi wa kambi ya mkandarasi ya Dar es Salaam imekamilika kwa asilimia 99, Soga umekamilika kwa asilimia 89 na Ngerengere asilimia 67.

Alisema hatua ya upimaji wa ardhi itakakopita reli hiyo (topographical survey), umekamilika kwa asilimia 95.

Waziri huyo alisema hatua ya tatu iliyofikiwa ni njia ya kuhudumia mradi itakayotumika kupitishia watu, mitambo na vifaa vya ujenzi ambayo imekamilika kwa asilimia 83.

"Jumla ya vifaa kwa ajili ya ujenzi (mitambo na magari 755) vimeshawasili kwa ajili ya kazi. Kazi ya kusafisha eneo la mradi nayo imekamilika kwa asilimia 59.7," alisema.

Prof. Mbarawa alitaja hatua ya sita iliyofikiwa kuwa ni utafiti wa ardhi itakayobeba misingi ya madaraja pamoja na makalavati ya kuvukia watu, wanyama na baiskeli ambao umekamilika kwa asilimia 10.

Waziri huyo alisema hatua ya saba ni ujenzi wa tuta la reli ambayo imekamilika kwa asilimia 15.

Aliongeza kuwa utekelezaji wa ujenzi wa reli ya kisasa kwa sehemu ya pili inayoanzia Morogoro hadi Makutupora yenye jumla ya urefu wa kilometa 422 (km 336 njia kuu na km 86 njia za kupishana treni) unaendelea vizuri.

"Mkataba wa ujenzi kwa utaratibu sanifu na jenga, ulisainiwa Septemba mwaka jana kati ya iliyokuwa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) na kampuni ya Yapi Merkezi ya Uturuki," alisema na kusema zaidi:

"Mhandisi mshauri wa mradi huu ni muungano wa kampuni nane unaoongozwa na kampuni ya KORAIL ya Korea Kusini."

Alisema taratibu za kusaka fedha za ujenzi wa reli ya kisasa kwa maeneo ya Makutupora-Tabora (km 295), Tabora-Isaka (km 133), Isaka-Mwanza (km 250), Tabora-Uvinza-Kigoma na Kaliua-Mpanda-Karema zinaendelea.

"Nchi za China, Korea, Ujerumani, Ufaransa, India, Marekani, Nigeria, Ureno na Uingereza zimeonyesha nia ya kushiriki katika ujenzi huo," alisema.

"Zabuni kwa ajili ya kununua treni na mitambo itakayotumika kutoa huduma ya usafiri kwenye reli ya kisasa ilifungwa Februali, mwaka huu na tathmini inaendelea."

Jiwe la msingi la ujenzi wa sehemu ya reli hiyo liliwekwa na Rais John Magufuli, Machi 14, mwaka huu na ilielezwa kuwa unatarajiwa kukamilika Desemba 2020.

Prof. Mbarawa pia alisema serikali inatambua umuhimu wa reli ya kati iliyopo sasa kwa ajili ya kutoa huduma za mizigo na kuendelea kusafirisha mitambo na vifaa kwa ajili ya ujenzi wa reli ya kisasa inayojengwa.

Kwa kutambua umuhimu huo, alisema maandalizi ya kukarabati miundombinu ya reli ya kati kupitia Mradi wa Uboreshaji Miundombinu ya Reli (TIRP) unaogharamiwa kwa fedha za mkopo kupitia Benki ya Dunia (WB), yanaendelea.

Katika hatua nyingine, Prof. Mbarawa alisema kuwa mwaka ujao wa fedha, Shirika la Ndege (ATCL) limetengewa Sh. bilioni 495.6 kwa ajili ya kununua ndege mbili; moja aina ya Q400 yenye uwezo wa kubeba abiria 76 na ndege kubwa ya masafa marefu aina ya Boeing 787-8 (Dreamliner) yenye uwezo wa kubeba abiria 262.

Prof. Mbarawa alisema fedha hizo pia zitatumika kulipia bima, gharama za uendeshaji wa ndege (start up cost), mafunzo ya marubani, wahandisi na wahudumu na ulipaji wa madeni.

Waziri huyo pia alisema kuwa katika mwaka ujao wa fedha, serikali itaendelea kuboresha huduma zinazotolewa na Shirika la Reli (TRC), Sh. trilioni 1.506 (fedha za ndani) zikitengwa.

Akifafanua kuhusu fungu hilo, Prof. Mbarawa alisema Sh. trilioni 1.4 zitatumika kuendelea na ujenzi wa reli ya kati (Dar - Morogoro km 300 na hadi Makutupora (km 422) kwa kiwango cha Standard Gauge.

Alisema Sh. bilioni 100 zimetengwa kwa ajili ya kuanza ujenzi wa reli ya Isaka-Rusumo (km 371) kwa kushirikiana na Rwanda, Sh. bilioni tatu zimetengwa kwa ajili ya kuanza utekelezaji wa mradi ikiwa ni pamoja na kumwajiri mtaalamu atakayeandaa nyaraka na kusaidia kutafuta fedha za ujenzi wa reli ya Mtwara-Mbambabay na matawi ya Mchuchuma na Liganga.

Prof. Mbarawa pia alisema kuwa katika mwaka ujao wa fedha, Sh. bilioni 9.29 ili kutekeleza miradi ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) ambayo ni pamoja na ununuzi na usimikaji wa rada nne za kuongozea ndege za kiraia katika viwanja vya JNIA, KIA, Mwanza na Songwe.

Aliongeza kuwa serikali imetenga Sh. bilioni sita kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya sekta ya uchukuzi ikiwa ni pamoja na ununuzi wa magari ya zimamoto kwa viwanja vya ndege vya Mpanda, Shinyanga na Iringa.

Prof. Mbarawa aliliomba Bunge kuidhinisha jumla ya Sh. trilioni 4.271 ili kutekeleza majukumu yake kwa mwaka ujao wa fedha. Kati yake, Sh. trilioni 1.865 ni kwa ajili ya sekta ya ujenzi, Sh. trilioni 2.387 za sekya ya uchukuzi na Sh. bilioni 18.856 za sekta ya mawasiliano.

Kuhusu Kuchanjwa Chale Na Wachawi

$
0
0
NA. DOKTA  MUNGWA  KABILI. ….0744  000  473.
Katika  maeneo  mengi  ya  vijijini  ni  jambo  la  kawaida  sana kwa watu  kuamka na kujikuta  wakiwa  wamechanjwa  chale  sehemu  mbalimbali  mwilini na  wasijue  chale  hizo  wamechanjwa  na  nani na  kwa  sababu  gani.

Jambo hili  halitokei maeneo ya  vijijini  tu  bali hutokea  na mijini  pia.

Watu  huamka  asubuhi  na  kujipata  wakiwa  wamechanjwa  chale  bila  kujua  ni  nani  aliehusika  na  kuwachanja  chale  hizo  na  alifanya  hivyo  kwa  sababu  gani.

Katika  makala  ya  leo  tutapata  kuwafahamu  ni  akina  nani  haswa  wanao  wachanja  watu  chale  usiku  wakiwa  wamelala  na  huwa  wanafanya  hivyo  kwa  sababu  gani.

Kwanini  wachawi  huwachanja  watu  chale  usiku ?

Wachawi  huwachanja  watu  chale  kwa  sababu  mbalimbali. Baadhi  ya  sababu  hizo  ni  kama  ifuatavyo :

1.   KUSOMA  NYOTA  ZA  WAHUSIKA : Story  ya  maisha  ya kila  mtu huwa  imeandikwa  kwenye  damu  yake .

Kwa  kutumia  maarifa  ya  juu  kabisa  ya  kichawi, wachawi  wanaweza kusoma  story nzima ya  maisha  ya  mtu  kwa  kutumia  damu  yake.

Kwa lugha  nyepesi ni kwamba  katika  ulimwengu  wa  rohoni  damu  ya  mtu  ni kama  ubao  ama  kitabu  ambacho  kimeandiwa story nzima  ya maisha  ya  mtu  huyo.

Siri  na  mipango  yote  ya maisha  ya  mwanadamu  ambayo  amepangiwa  na  Mwenyezi  Mungu  imeandikwa  katika  damu  yake.

Wachawi  wakitaka  kujua  kuhusu  siri  hii  huhaha  kutafuta  damu ya mtu  ambae  wanataka  kujua  kuhusu  maisha  yake.

Hivyo  basi  wachawi  wanavyo mchanja mtu  chale, pamoja  na  mambo mengine, hufanya  hivyo  kwa lengo la  kupata damu  ambayo  wataitumia kusoma  nyota  ya  mhusika.

KAMA  AMBAVYO  WATAALAMU WA  KISAYANSI  WANAWEZA  KUJUA  MAISHA  YA  MTU  YAKOJE  KWA  KUMFANYIA  MTU  HUYO  KIPIMO  KIITWACHO  FULL BLOOD  PICTURE, BASI  VIVYO  HIVYO  WACHAWI  WANAWEZA  KUJUA  SIRI  YA  MAISHA  YA  MTU  KWA KUTUMIA  DAMU  YAKE.

NAOMBA  NIELEWEKE  VIZURI  KUHUSU  KIPIMO  CHA  FULL BLOOD  PICTURE  NA  KUJUA  MAISHA  YA  MTU.

 SIMAANISHI  KWAMBA  KWA  KUMFANYIA  MTU  FULL  BLOOD PICTURE MADKATARI  WANAWEZA  KUJUA  MAISHA  YA MTU  HUYO  YATAKUWAJE  HAPO  MBELENI  LA  HASHA.

 NINA  MAANISHA  HIVI, KIPIMO  CHA  FULL  BLOOD PICTURE  NI  KIPIMO  KINACHO ONYESHA  HALI  HALISI  YA  AFYA  YA  MWANADAMU  NA  KAMA TUJUAVYO  MAISHA  NI  AFYA  NA  AFYA  NDIO  MAISHA.

KWA  KUFANYA  FULL  BLOOD  PICTURE  MADAKTARI  WANAWEZA  KUBAINI  KAMA MHUSIKA  ANA VIRUSI  VYA  UKIMWI, KISUKARI, PRESHA,SHINIKIZO   LA  DAMU, LEHEMU MWILINI  NAKADHALIKA.

WANAWEZA  KUJUA  KAMA  MTU  NI  MGONJWA  AU  ANA  AFYA  NJEMA.

NA KWA  KUJUA  KAMA  MTU  NI  MZIMA  BUKHERI  WA  AFYA  AU  ANASUMBULIWA  NA  MARADHI  MAZITO  NDANI  YA MWILI  WAKE  NI  SAWA  NA  KUJUA  KUHUSU  MAISHA  YAKE  KWA  SABABU  MAISHA  YA  MTU  NI  AFYA  NA  AFYA  NDIO  MAISHA  YA  MTU. UKIACHILIA  MIPANGO  YA MUNGU NA SHARI  ZA WACHAWI, AFYA  YA MTU NDIO INAYO AMUA UMRI WA MTU KUISHI.  UHAI  WA  MTU  UPO  KWENYE  DAMU  YAKE.

Vivyo  hivyo  basi  wachawi  wanapo taka  kujua  siri  za  maisha  ya  mtu  hufanya  hivyo  kwa kutumia  damu  yake. Hii ni  kwa  sababu  maisha  ya  kila  mwanadamu  yameandikwa  kwenye  damu  yake. Siri  zote  kuhusu  maisha  ya  kila  mtu  zimefichwa  kwenye  damu  yake.

2.   KUIBA  NYOTA  : Hii  ni  sababu  nyingine  kwanini  wachawi  huwachanja  watu  usiku  wakiwa  wamelala. Hufanya  hivyo kwa  lengo  la  kuiba  nyota  zao.  Suala  la  kuiba  nyota  huja  baada  ya kusoma  nyota  ya  mhusika  kupitia  damu  yake na  kuona  inafaa  kuchukuliwa  kwa  matumizi  mbalimbali  kama  vile  biashara, mali nakadhalika.

3.   KUPIMA KINGA  YA  MTU : Kama  nilivyo  eleza  hapo  juu  kuwa ndani  ya  damu  ya  mtu  ndimo  kumefichwa  kila  kitu  kuhusu mtu  huyo.

Kila  siri  inayo  muhusu  mwanadamu, imeandikwa  ndani  ya  damu  yake .

Wachawi  wanapo  taka  kupima mtu  fulani  ana  kinga  kubwa  kiasi  gani hufanya  hivyo  kwa kusoma  damu  yake  au  vitu  vya  mtu  huyo  ambavyo  vimetokana  na  msukumo  wa  damu  kama  vile  manii n.k.

Kumbuka  kuwa  kinga  yoyote  ile  ya  mtu  huwa  inakaa  kwenye  damu  yake. Dawa  anazo  chanjwa  mtu  kwa  ajili  ya  kinga, dawa  anazo  kula  ama  kunywa  mtu  kwa  ajili  ya kinga  huwa  zinaenda  kukaa  kwenye  damu yake.

Sasa  basi katika  uchawi  njia  ya  juu  kabisa  ya  kujua  kinga  ya  mtu  ikoje  ni  kusoma  damu  yake.

Hivyo basi   wachawi  wanapo mchanja  mtu  chale, pamoja  na  mambo mengine, hufanya  hivyo  kwa  lengo  la  kupima  kinga  ya  mtu  huyo..

Na  lengo  la  kutaka  kujua  kinga  ya  mtu  ni kujua  mtu  huyo  kinga  yake  ina  nguvu  kiasi  gani  na  wakisha  jua  nguvu  ya  kinga  ya  mtu  huyo  kitakacho  fuatia  baada  ya  hapo  ni  kutuma  uchawi  wa  kuteketeza  kwanza  kinga kisha  ili  wapate  urahisi  au  mwanya  wa  kutupa  uchawi  wao  kwa  mtu  waliemkusudia.

4.    KUPANDA  MAPANDO  YA  KICHAWI :  Inaeleweka  vyema  kwa  wengi  kuwa  mwanadamu  aliumbwa  kwa udongo.

Wachawi wana amini  sana   katika  jambo  hili. Wao  hawaishii  tu  kuamini  kuwa  mwanadamu  aliumbwa  kwa  udongo bali  wanaenda mbele  zaidi  na  kumtreat  mwanadamu  kama udongo  kabisa.

Na  katika  kudhihirisha  hilo  kwa  vitendo, wachawi  wanaweza  kuutumia  mwili  wa  mwanadamu  kupanda  mapando  yao  mbalimbali.  Wachawi  wanaweza  kuutumia  mwili  wa  mwanadamu  ( ambao  ni  udongo) kama  shamba  la kupanda  mapando  yao.

 Mapando  yao  yanaweza  kuwa  kwa  faida  yao  wao  kama  wachawi  huku  mtu  huyo  wakimtumia  kama  shamba  tu  au  yanaweza  kuwa  kwa  ajili  ya  mtu  huyo  ili  baadae aje  ayavune katika  maisha  yake  halisi.

Ndani  ya  mwili  wa  mwanadamu  inaweza  kupandwa  roho  ya  mauti  ambayo  itakuwa  inakua  kadri  mwanadamu  anavyo  kuwa  na  anaweza  “ kula  matunda” ya  roho  hiyo  hata  baada  ya  miaka  ishirini. Inaweza  kupandwa  roho  ya  kukataliwa, roho  ya  umasikini, ufukara  nakadhalika.

Kwa  hiyo chale  hizo  zaweza kuwa  ishara  kwamba  wachawi  walikuwa  wanalima  kwenye  mwili  wako  na  kupanda  mapando  yao  ya kichawi  kupitia    damu yao.

5.   KUFUGIA  MAJINI  WACHAFU : Wachawi  wanaweza  kuutumia  mwili  wa  mtu  kama  banda  la  kufugia  majini  wachafu  ambao  watakuwa  wanawachukuwa  kuwatumia  kila  watakapo  wahitaji.,Majini  hao  wachafu  wanaweza  kukaribishwa  kwenye  mwili  wa  mtu  kupitia  chale hizo  za  kichawi.  Chale hizo  hutumika  kama  Antenna  za  kuwavuta  majini wachafu  ndani  ya  mwili  wa  mtu  walie mkusudia.

6.   KUMPAKA  MTU  NUKSI NA  MIKOSI: Kama  nilivyo  sema  hapo  awali  kuwa  story  ya  maisha  ya  kila  mtu  huwa  imeandikwa  kwenye  damu  yake.

Kuna  kanuni  moja  kubwa  sana  katika  ulimwengu  wa  rohoni  ambayo  inasema  chochote  utakacho  kiunganisha  na  damu  ya  mtu  basi  kinamezwa  na  kuwa  sehemu  ya  damu  ya  mtu  huyo  na  kitu  hicho  kikisha  kuwa  sehemu  ya  damu  ya  maisha  ya  mtu  huyo  basi  kinakuwa  sehemu  ya  maisha  ya  mtu  huyo  na  kikisha  kuwa  sehemu  ya  maisha  ya  mtu  huyo  basi  kitaanza  kujidhihirisha  chenyewe  katika  maisha  ya  mtu  huyo.

  Hii  ni  kwa  sababu  damu  ndio  nishati  inayo endesha  maisha  ya  mtu. Nishati  hii  ndio  inayo  amua  kila  kitu  katika  maisha ya  mwanadamu.

Wachawi  kwa  kulitambua  hilo, huwa  wanafanya  uchawi  maalumu  wa  kuunganisha  damu  ya  mtu  na  vitu  vibaya ili  vitu  hivyo  vibaya  na  vichafu  vikafanyike  kuwa  sehemu  ya  damu  ya  mtu  huyo  na  hivyo  kuharibu  utaratibu  mzima  wa  maisha  ya  mtu  huyo.

Hufanya  hivyo  kwa  kuwatia watu  nuksi.Nuksi  hiyo  inaweza  kuingizwa  kwenye mfumo  wa  maisha  ya  mtu  kwa  njia nyingi   sana, kubwa  kuliko  zote  ni  njia  hiyo  ya  kuwachanja  chale  na  kuwapaka nuksi.

Nuksi  sio  neo  tu  kama  baadhi  ya  watu  wanavyo  lichukuliwa. Sio  neno  wala  msemo.

Ni uchawi  kabisa  ambao  nguvu  yake  hubeba  maudhui  ya  jina  lake. Zipo  nuksi za  aina  nyingi  sana.

 Moja  wapo  kati  ya  nuksi  hizo  ni  nuksi  inayo  tengenezwa  kwa  vitu  mbalimbali  kama  vile : Mavi  ya  mtu  fresh ambayo  alijisaidia  akiwa  porini, mavi  ya  nyani, mavi ya sokwe, mavi ya  chatu, mavi ya kenge, uchafu  wa  kwenye  majalala  saba ( Wakati  uchafu  huu  unachukuliwa  hufanyika  tambiko  maalumu  la  kichawi  linalo  husisha  kafara  ya  mnyama  au  ndege, ambayo  hulenga  katika  kuwaamsha  majini  wachafu  walio  lala  katika majalala  hayo  kuingia  ndani  ya  uchafu  huo), kipande  cha  mti kilicho  okotwa  ndani ya  kaburi wakati  kaburi  linachimbwa, utumbo  wa  kuku, maji yaliyo tumika kuoshea  maiti, uchafu  wa  mochwari, shahidi  la  kaburi, dawa  moja  ya  kiarabu  ifananayo  na  lami  na yenye  kutoa  harufu  mbaya  sana , uchafu  wa chooni pamoja na  madawa  mengine  ya  kichawi  ambayo  ninayahifadhi  hapa)

Vitu  vyote  hivyo vinapikwa  kwa  pamoja  kwa  kutumia  dawa  ya  paka  mweusi.

Vinakaangwa  hadi  kuwa  majivu  halafu  mhusika  anaenda  kupakwa  kichawi  usiku.

Wakati  mwingine  zoezi  la  kumpaka  mtu  nuksi  huweza  kuendana  na  zoezi  la  kumpaka  damu  mbichi  ya  mnyama  mmoja  apendwae  sana na  wachawi…

Damu  hii  hunuizwa  kutamka  mambo yatakayo  enda  kubatilisha mambo  yote  mazuri  yaliyo  andikwa  kwenye  damu  ya  mhusika.

Damu  ya  mnyama  huyu  huenda  kufuta  kila  kitu  kizuri  kilicho andikwa  kwenye  damu  ya  mtu  aliekusudiwa  na badala  yake yenyewe  ndio hukaa na  kuweka  tamko  jipya  juu  ya  maisha  ya  mtu  aliekusudiwa.

Matokeo  yake  mtu  huyo  huanza  kuandamwa  na nuksi  mabalaa  na  mikosi .
 
Makala  haya  yameandaliwa  na  Dokta. Mungwa  Kabili  ambae  anapatikana  kwa  SIMU  NAMBA  : 0744  000  473.

Rais Magufuli Abaini Mchezo Mchafu NMB.......Ashangazwa Gawio Kufanana Miaka Mitatu Mfululizo

$
0
0
Na: Lilian Lundo – MAELEZO, Dodoma.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli ameiagiza Bodi ya National Microfinance Bank (NMB) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo kuangali kiasi cha gawiwo kinachotolewa na benki hiyo, kutokana na kiasi hicho kutoongeza ndani ya miaka mitatu mfululizo.

Rais Magufuli ameyasema hayo jana Mjini Dodoma wakati alipokuwa akifungua jengo jipya la Mfuko wa Pensheni wa Watumishi wa Umma (PSPF) pamoja na tawi jipya la NMB Kambarage lililoko katika jengo hilo.

“Kuna mambo mazuri mengi yaliyofanywa na NMB lakini tunahitaji uhakiki wa gawiwo linalotolewa kwa Serikali, kutokana na gawiwo hilo kutopanda kwa miaka mitatu mfululizo tangu mwaka 2014/2015 mpaka mwaka 2016/2017 ambapo benki hiyo imekuwa ikitoa shilingi Bilioni 16.525 kama gawiwo la hisa ya asilimia 32 iliyonayo katika Benki hiyo,” alisema Rais Magufuli.

Ameendelea kwa kusema, ni matumaini yake kuwa kiasi hicho cha fedha kitapanda kwa mwaka 2017/2018 kutokana na benki hiyo kutengeneza faida kila mwaka.  

Aidha, Rais Magufuli ameipongeza benki ya NMB kwa kuwa na matawi mpaka vijijini pamoja na kutoa ajira kwa zaidi ya Watanzania 3000 na kutoa misaada ya kijamii ikiwemo madawati 600, kompyuta 300 kwa shule za Sekondari na vitanda vya wagonjwa.

Vilevile Rais Magufuli ameupongeza mfuko wa PSPF kwa kuona fursa ya Serikali kuhamia Dodoma na kujenga jengo ambalo limeboresha na kupendezesha mandhari ya Dodoma ambapo pia ujenzi huo umetoa ajira kwa Watanzania takribani 250.

Pia amesema, mfuko huo umekuwa ukitoa mikopo kwa wanachama wake pamoja na kuwekeza katika ujenzi wa viwanda mbalimbali ikiwa ni pamoja na kiwanda cha cha Sukari Kagera, kiwanda cha nguo na turubai vilivyopo mkoani Morogoro.

Wakati huo huo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge amesema Rais Magufuli kupitia TAMISEMI ametoa shilingi bilioni 70 kwa ajili ya ujenzi mbalimbali wa miundombinu mkoani Dodoma.

Dkt. Mahenge ametaja miundombinu hiyo kuwa ni pamoja na ujenzi wa stendi mpya ya kisasa yenye uwezo wa kuingia mabasi makubwa 250, magari madogo 600 pamoja na bajaji na bodaboda 300 kwa wakati mmoja.

Aidha, Dkt Mahenge ameitaja miundombinu mingine ambayo ni ujenzi wa soko la kisasa, sehemu ya kupaki malori, miundombinu ya majitaka, maeneo ya kupumzikia pamoja na kuboresha miundombinu ili kuondoa msongamano wa magari.

kwa upande wake, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji ameutaja mfuko wa PSPF kuwa ndio mfuko wa kwanza kuwekeza katika vitega uchumi Makao Makuu ya Nchi ukiondoa mfuko wa LAPF ambao Makao Makuu yake yapo Mkoani Dodoma.

Jengo la PSPF ni moja ya majengo marefu yaliyoko mkoani Dodoma ambapo ina jumla ya ghorofa 11 pamoja na eneo la maegesho ya magari 161 ambapo mpaka sasa jengo hilo limeshapata wapangaji kwa asilimia 100.

Mbunge CHADEMA Ahoji Bungeni sababu za ripoti za CAG kutokuwa na taarifa za Tanroads Shirika la Ndege (ATCL)

$
0
0
Mbunge wa Momba, David Silinde (Chadema), amehoji bungeni kuhusu taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kutokuwa na taarifa za Shirika la Ndege (ATCL) na Wakala wa Barabara (Tanroads).

Akichangia bungeni jana mjadala wa makadirio ya bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka ujao wa fedha, mbunge huyo ambaye pia ni Naibu Waziri Kivuli wa Fedha na Mipango, alisema hakutarajia kuona ripoti ya CAG ya mwaka 2016/17 ikikosa taarifa za taasisi hizo muhimu katika kipindi hiki ambacho zinatengewa fedha nyingi.

Alisema taarifa za fedha za taasisi hizo zilipaswa kuwamo kwenye ripoti ya CAG ili wahoji kama wanavyofanya sasa kuhusu kutoonekana kwa matumizi ya Sh. trilioni 1.51.

Silinde ambaye alihoji ni sababu za ripoti za CAG kutokuwa na taarifa za Tanroads ili wabunge waangalie barabara za Tanzania kama zinaendana na thamani ya fedha inayotolewa.

“Sisi kama wabunge tunatakiwa kuhoji kwanini katika ripoti ya CAG huwa hakuna Tanroads, tunatakiwa kuhoji; je, barabara inayojengwa inalingana na 'value for money' (thamani ya fedha)?” alisema Silinde.

Mbunge CHADEMA Aishangaa Serikali Kununua Ndege Mpya

$
0
0
Mbunge wa Viti Maluum (Chadema), Lucy Magereli amesema uamuzi wa Rais John Magufuli kununua ndege hauwezi kuwa sababu ya kulifufua Shirika la Ndege Tanzania (ATCL).

Akizungumza katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano mwaka 2018/19, mbunge huyo amesema kuliko kununua ndege hizo, Serikali ingekodisha ndege na kuanza kujipanga taratibu kuliboresha shirika hilo.

“Nani aliyemshauri Rais kununua ndege? Tungeweza kuifufua ATCL kwa ndege za kukodi, hatuhitaji ndege kubwa. Hivi tunawezaje kushindana na mashirika makubwa ya ndege duniani ambayo yapo muda mrefu na yamejiimarisha,” amesema.

“Suala si kuhitaji ndege, suala tumezipata kwa utaratibu upi. Tuna ndege wakati viwanja vya ndege vya ndani havifai kwa matumizi yetu. Leo mtalii akitua Dar es Salaam akitaka kwenda maeneo mengine atafika kwa shida.”

Mbunge huyo alihoji sababu za Serikali kununua ndege kubwa wakati haijaimarisha miundombinu, vikiwemo viwanja vya ndege, “ndege tunazonunua ni mzigo kwa nchi hii, zinahitaji matengenezo, tutayaweza?”

“Kesho na keshokutwa Bunge litakaa tena na kusema tumetumia fedha nyingi kuifufua ATCL na kuliingiza Taifa katika matatizo. Nawaambieni tutakaa hapa kujadili tena jambo hili.”

“Tumetumia fedha nyingi kukomboa ndege zetu zilizozuiwa Canada je hizo fedha Bunge gani limezipitisha?” Amehoji.

Rais Magufuli Ampongeza Mizengo Pinda.....Ataka Viongozi Wengine Wastaafu Waige Mfano Wake

$
0
0
Rais John Magufuli jana alimmwagia sifa Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Pinda kwa kumwelezea ni kiongozi mkimya na asiyependa kuzungumza ovyo ovyo.

Rais Magufuli alisema Pinda, maarufu kama Mtoto wa Mkulima, ni kiongozi anayefaa kuigwa na viongozi wengine, na kwamba hata yeye siku akistaafu atamfuata ili kujifunza.

Aliyasema hayo jana mjini Dodoma wakati akifungua Tawi la Benki ya NMB la Kambarage na Jengo la Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF).

“Mzee Pinda anaishi maisha ya kawaida sana, hapigi kelele, hazungumzi chochote, Mzee Pinda ‘you are too special’ (wewe ni mtu wa kipeke),” alisema Rais Magufuli.

“Watu watakukumbuka (Pinda) kwa ukarimu wako, wewe ni mtu wa kawaida sana. Sasa hivi hatujui thamani yako lakini ipo siku tutaijua.

“Ndiyo maana bado unaonekana kijana, hujipi ‘pressure’ (hofu), unaamini kile unachofanya, na mimi nikistaafu nitakuja kuchukua ‘course’ (mafunzo) kwako.”

Sifa kwa Pinda zinakuja miezi saba tangu alipokosoa viongozi wastaafu wa "maeneo mengine" wanaosemasema kila wakati kuhusu uendeshaji wa serikali.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Septemba 11, mwaka jana Rais Magufuli alitoa mfano wa majaji wastaafu ambao alisema ni tofauti na wastaafu wengine na kwamba huenda kujua sheria ndiko kunakowasaidia kutokuwa waropokaji.

Rais Magufuli alisema hayo wakati wa kumuapisha Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma.

“Nawashuruku majaji wakuu wastaafu, Barnabas Samatta na Augustino Ramadhani, walifanya kazi kubwa ya kujenga misingi ya mahakama nchini," alisema.

“Bahati nzuri majaji hawa ni waadilifu sana huwezi kumsikia Jaji (Mkuu mstaafu Othman) Chande, (Barnabas) Samatta, Augustino (Ramadhani), (Damian) Lubuva au majaji walioko hapa... ukiangalia wastaafu wa maeneo mengine hawachoki kusema, wanawashwawashwa.

“Ndiyo maana nawapongeza sana mahakama...Ni safi mno, nina uhakika wanapotaka kutoa ‘advice’ (ushauri) yoyote (wowote) lazima wanakushirikisha (Jaji Mkuu); ndiyo faida ya kujua sheria.

“Sisi wengine huku ambao hatujajua sheria mahali popote, chochote unaweza ukazungumza.”

Waziri Mkuu: Nimeridhishwa Na Maadhalizi Ya Sherehe Za Muungano

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na maandalizi ya sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yanayoendelea katika Uwanja wa Jamuhuri mjini Dodoma.

Ameyasema hayo leo (Jumanne, Aprili 24, 2018) mara baada ya kukagua maandalizi hayo yanayofanyika kwenye Uwanja wa Jamuhuri mjini Dodoma, ambapo amesema maandalizi yanaendelea vizuri.

Waziri Mkuu amejionea maonesho mbalimbali yakiwemo ya kikundi cha halaiki  ambacho kinaundwa na wanafunzi 2,000 kutoka Manispaa ya Dodoma pamoja na maonyesho ya kujihami na maadui yaliyooneshwa na Jeshi la Magereza.

“Nimeridhika na kazi ambayo mmeifanya, nawaruhusu muendelee kushirikiana katika kukamilisha maeneo ambayo yamesalia na kuanzia kesho tujiandae kuwapokea wageni kutoka maeneo mbalimbali.”

Alhamisi Aprili 26, 2018 Watanzania wanatarajia kuadhimisha miaka 54 ya Muungano tangu Tanganyika ilipoungana na Zanzibar, chini ya waasisi wake Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Aman Karume.


Maxcom yatoa ufafanuzi utata tiketi za mabasi ya mwendokasi

Bilioni 256 Kutumika Kujenga Kiwanda Cha Kemikali Mlandiz

$
0
0
SERIKALI imezindua mradi mkubwa wa ujenzi wa kiwanda cha kemikali za kutengeneza dawa za kusafishia maji kitakachogharimu sh. Bilioni 256.
 
Uzinduzi huo umefanyika eneo la Mlandizi  Msufini mkoani Pwani jana na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage kwa niaba ya Makamu wa Rais, Samiah Suluhu Hassan.
 
Mwijage alisema mradi huo ukikamilika utasaidia serikali kuokoa kiasi cha  fedha kilochokuwa kikitumika kununua dawa hiyo nje za nchi.
 
” Mradi huo ni wa tatu kwa ukubwa Afrika   na kwa sasa tunatarajia kuzindua viwanda vingine tisa vilivyo na viwango. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

 Na ili kuhakikisha adhma ya  viwanda inafanikiwa nitatoa  eneo langu kwa ajili  kujenga jumba   la utamaduni  wa viwanda, ” alisema.
 
Mwijage aliwataka Watanzania kujenga uthubutu wa kuwekeza kwenye viwanda ili kuchochea  mageuzi ya kiuchumi.
 
4Mkurugenzi wa Kiwanda  hicho,  Justine  Lumbert , alimwakikishia Rais Dk.John Magufuli kuwa anacho kikosi  mahiri nchini  kwa ajili ya jenzi wa viwanda kwa mkoa wa Pwani.
 
Alisema mradi  huo wa dawa ni mkubwa barani Afrika  hivyo  utaisaidia nchi kutengeneza aina  ya dawa ya Chlorine itakakayotumika kusafisha maji.
 
” Utengenezaji wa dawa hiyo hutumia chumvi,  sasa hakuna chumvi yoyote itakayouzwa nje ya nchi hadi mahitaji ya kiwanda hicho yatakapojitosheleza kwa sababu bidhaa zitakazotengenezwa zitakuwa na soko  la asilimia 20 ndani ya nchi na 80 nje ya nchi,” alisema.
 
Mkurugenzi huyo ujenzi wa mradi huo utagharimu kiasi cha sh.  Bilioni 256 kwa eneo la hekari nane na utakamilika  ndani ya miezi 23.
 
” Tunaiomba serikali kuweka sheria na kanuni stahiki zitakazosaidia kulinda bidhaa  na malighafi  ya chumvi itakayotumiwa na mradi huu,” alisema.
 
Lumbert  alitaja faida za mradi huo, utasaidia  kuingizia taifa fedha za kigeni, kuokoa fedha za kununulia dawa nje, kuokoa gharama za  matumizi ya kusafisha maji nchini na kuongeza ajira rasmi  kwa vijana takribani 700.
 
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Isack  Kamwelwe, alimuagiza  Mkurugezi wa  Mamlaka ya  Maji  Safi na Maji taka  Dar es Salaam (DAWASCO), Mhandisi  Cyprian  Luhemeja, ndani ya siku tatu anakutana na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi  Evarist Ndikilo kwa  ajili ya ujenzi wa pipa kubwa la maji eneo la Mlandizi ili kuhakikisha yanapatikana eneo hilo kwa urahisi.
 
” Kwa Wizara yangu itabadilisha muundo wa ununuzi kwani tutakuwa tukinunua  ununuzi wa pamoja kuanzia  Julai mwaka huu  sasa wizara yangu haitakwenda kununua sawa ya kusafisha maji nje wakati itakuwa ikipatikana  nchini,” alisema.
 
Kamwele alizitaja aina ya upungufu uliokuwepo katika wizara yake kuwa ni utengenezaji wa  mabomba ya chuma cha pua na dawa ya kusafisha maji kwa haraka  iliyo na uwezo wa kuzamisha  vumbi na matope kwa haraka.
 
Naye Mhandisi  Ndikilo alisema mradi wa kiwanda hicho  ni wa tofauti Afrika Mashariki  kwa sababu  Afrika   kinapatikana   nchi ya Misri na  Nigeria.
 
” Wawekezaji tambueni ya kuwa mkoa wa Pwani  uko salama  kwa hiyo msipigiwe kelele na mitandao ya kijamii.
“Kiwanda hicho kinahitaji tani 2500 ya chumvi  kwa  mwezi kwa hiyo wazalishaji changamkieni fursa hiyo  kwa sababu hakuna chumvi itakayochukuluwa nje ya nchi,” alisema.

Waziri Ummy apiga marufuku kuuza dawa za malaria

$
0
0
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeendelea na msisitizo wa vituo vya Afya, Zahanati na Hospitali za serikali kuacha tabia ya kuuza dawa za kutibu malaria nchini na endapo mtoa huduma ataenda kinyume na hilo atachukuliwa hatua stahiki dhidi yake.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati alipotembelea Zahanati ya Mwandiga iliyopo wilayani Kigoma Mkoa wa Kigoma katika akiwa anangalia hali ya matibabu dhidi ya malaria wilayani humo kuelekea kilele cha siku ya Malaria Duniani.

"Nawaagiza waganga wakuu wa Mikoa na Wilaya kuweka matangazo yanayooonyesha kipimo cha haraka cha Malaria, dawa za kutibu Malaria ya mseto na sindano ya kutibu malaria kali ni bure kwenye kila zahanati, kituo cha afya na hospitali ya serikali", amesema Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy amewataka waganga wakuu wa vituo ngazi za zahanati na waganga wakuu wa wilaya waweke namba zao za simu kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini ili kuwasaidia Watanzania kutoa malalamiko yao pindi wanapopatiwa huduma ambazo za hazikidhi viwango ili kubendelea kuboresha huduma za afya nchini.

Waziri Ummy amesema kuwa katika kujikinga na Malaria wananchi wanatakiwa kutumia vyandarua vyenye dawa, kusafisha mazingira na kuondoa mazalia ya mbu waenezao ugonjwa huo kwani kinga ni bora kuliko tiba.

Sambamba na hilo Waziri Ummy ametoa vyandarua vyenye dawa ya kukinga dhidi ya Malaria katika kijiji cha Mwandiga ili kuendelea na juhudi za kutokomeza Malaria nchini katika kuelekea siku ya Malaria Duniani.

Watu Saba Arusha wakamatwa kwa kuhamasisha maandamano

$
0
0
Watu saba akiwamo mwanamke mmoja wanashikiliwa na Polisi mkoani Arusha kwa tuhuma za kuhamasisha maandamano kupitia mitandao ya kijamii.

Kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha, Yusuph Ilembo amewaambia wanahabari leo Aprili 25 kuwa watu hao wamekamatwa kutokana na sababu za kuhamasisha maandamano Aprili 26 mwaka huu.

Ilembo amesema watuhumiwa hao wamekuwa wakihamasishana kwa kutumia mitandao ya kijamii ikiwamo ya Telegram na WhatsApp.

Amesema watu hao wamekamatwa kupitia vitengo vya intelijensia baada ya kuwekewa mitego mbalimbali na kufanikiwa kuwakamata.

Amesema miongoni mwa watuhumiwa hao baadhi yao wapo vyuo vikuu, mitaani na maeneo mengine.

Ilembo ameongeza kuwa watuhumiwa hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani muda wowote, huku wakiendelea kuwatafuta wengine kwa njia mbalimbali.

"Nasisitiza hakuna maandamano Aprili 26, atakayeandamana atavuna alichopanda kwa kuwa Serikali haijaribiwi," amesema Ilembo.

Ndege Kubwa Zaidi ya Emirates Iliyobeba Abiria 475 Yatua kwa Dharura Dar

$
0
0
 Ndege ya kampuni ya Emirates iliyokuwa ikielekea Mauritius ikiwa na abiria 475 wakitokea Dubai, imetua jijini Dar es Salaam leo kwa dharura kutokana na hali mbaya ya hewa nchini humo.

Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege Tanzania, Kamishna msaidizi, Matanga Mbushi amethibitishia taarifa hizo akisema ndege hiyo ya Emirates, aina ya Airbus 380, EK701, ilishindwa kutua mara tatu nchini Mauritius kutokana na mvua kali iliyokuwa ikinyesha.

“Hiyo ndege ilikuwa ikielekea Mauritius, sasa hali ya hewa imekuwa mbaya ikashindwa kutua. Rubani alijaribu kutua mara tatu lakini akashindwa ndipo akaamua kuja Dar es Salaam kutua kwa dharura,” alisema Mbushi.

Amesema ndege hiyo ilikuwa na abiria 475 na wote wamepangiwa hoteli ili kusubiri taarifa za hali ya hewa ikiwa nzuri waendelee na safari.

“Kesho kama hali itakuwa nzuri wataondoka,” amesema Mbushi.

Ndege hiyo ni ya Shirika la Emirates la Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE). Ni kampuni tanzu ya Emirates Group, ambayo inamilikiwa na Shirika la Uwekezaji la Serikali ya Dubai.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images